ADA (Niloge)

book cover og

Utangulizi

Hivi umeshawai kuangukia kwenye penzi la mtu ambaye umjui kabisa, Yaani unamjua Jina tu na sura yake lakini haujui chochote kile kuhusu yeye ?

Huyu ni Mimi sasa 😂🙌 nimeangukia kwenye penzi ya huyu Binti ambaye ana matatizo ya kusikia, Muite ada, siijui ni Ada ya kitu gani lakini anaitwa Ada, msichana Fulani hivi, anajua kupenda na kujali, ni msichana ambaye anauwezo wa kumfanya mwanaume yeyote Yule aka fall in love na yeye Walahi huyu msichana anapendeka.

Ada ana kuja kuniingiza kwenye msongo wa mawazo baada ya kupotea kwenye mazingira ya kutatiza na kusababisha kubadilisha mfumo wangu wa maisha.

JE ADA ATARUDII KWENYE MAISHA YANGU ?
JE NI SABABU IPO ILIYOMFANYA ADA KUPOTEA GAFLA ?

ADA (niloge)

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 01

ANZA NAYO…..

Waliosemaga mapenzi ni upofu hawakuwai kukosea jamani, unaweza ukawa unatumia hadi miwani lakini ukipenda kweli kweli, Walahi lazıma uwe kipofu.

Naitwa MAHIL Mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wanne, katika watoto hao Bwana Mimi ndio Mtoto wa kiume.

Naweza kusema Kuwa kwenye familia yangu nilikuwa kama almasi hivi, nilipendwa sana na wazazi wangu lakini pia nilipendwa na ndugu zangu, kwetu sikuwa last born kwenye familia yangu lakini kila mtu alinitreate mimi kama last born kwakuwa Mimi tu ndio nilikuwa mwanaume.

Yaani ilifikia hatua hadi Mdogo wangu wa mwisho ananiita Mimi Mdogo wake.

Kitu ambacho najivunia kwenye maisha yangu ni Kuwa na hii familia, ni familia yenye upendo sana, familia yangu ilibarikiwa Kuwa na wasomi lakini pia na Pesa chafu, ukiniuliza Mimi kuhusu shida shida ninayoijua ni ya mahusiano tu lakini sio maisha magumu au Pesa.

Ila familia yangu ilikuwa na shida moja tu, sio Mimi wapi dada zangu ambao walikuwa tayali kuama Nyumbani, Yaani wote tulikuwa ni watu wazima na tumefikia Umri wa kuoa na kuolewa lakini sote utatukuta Nyumbani kwetu utazani ni familia ya mzee kikala wa kombolela.

KWa upande wangu Naomba nikubali Kuwa Mimi ni mzee wa gusa achia twende, Yaani Mimi nikimuona demu akanivutia uwa namtongoza tu, halafu siku Mbili Tatu napiga mzigo nikitoka hapo namuachia Pesa ya kutosha na penzi linakuwa limeisha.

Kwenye maisha yangu pia uwa napenda sana maisha ya uswazi na Mungu alinibariki Rafiki mmoja hivi wa uswazi, Mimi uwa namuita Mwarabu koko maana daaaah 😂🙌.

Ikiwa ni siku ya weekend, siku ambayo siendi kazini, nilishika njia na kwenda Nyumbani kwa Rafiki yangu mwarabu koko, Mimi Bwana ni mtu wa sifa sana, Mara nyingi uwa Natembelea ile gari nzuri nzuri ya pale Nyumbani ili Kuchanganya watoto Wazuri tu waweze kunipa mizigo nisepe zangu.

Hapo Mtaani kwa kina mwarabu koko nishakula wadada zaidi ya sita na sijali Wala nini na nikiwamisi nawapigia tunamalizana na kila mtu anaendelea na mishe zake.

Anyway tuendelee jamani, Kama kawaida nilifika kwa Rafiki yangu na kukaa Ndani kwake tukicheza magame tu ya kushindana uku tukipata miguu ya kuku ya uswahilini.

Majila ya jioni, ulikuwa ni muda wangu wa kuondoka, Mimi na mwarabu koko tulitoka nje kwaajili ya kuondoka, lakini kwenye kibaraza chao tuliweza kukutana na Mdada mmoja mrembo sana, Ninaposema Kuwa ni mrembo muwe mnanielewa jamani ni mrembo mpaka nikajikuta nikimtazama Mara Mbili Mbili.

“Mambo Mtoto mzuri ??”

Nilimsalimia.

Mwarabu koko aliniangalia kisha akanimbia.

“Uwe na huruma Broh kaaah upitwiiiiiii “

Hapo sikuwa nimemuelewa kabisa, lakini kwa msichana huyo hakuwa ameitikia salamu yangu zaidi alikuwa bize akiendelea na mapishi yake.

“Koko huyu ni Mgeni wenu au ??”

“Ahahah Broh kaaaahh tutakuzika na kilo Mbili me nakuambia ukweli, Yaani usione mwanamke Mbele yako tayali unataka kupita nae “


“Aaah umeanza na wewe, unajua sijawai kuona dada mrembo Kama Yule, lakini pia ni Ana kiburi sana Hajaitikia salamu yangu “

“Ndio maana nimekuwambia kuwa na huruma Broh, mahil unatakiwa kujifunza kuheshimu wanawake, ata hivyo Yule ni mpangaji wetu Mpya wameamia juzi tu yeye na Mama yake na sababu ya yeye kutokuitikia salamu yako ni kWa Kuwa yeye ni KIZIWI”

Hapo kwanza nilishtuka sana, Yaani Mdada mrembo kiasi kile anawezaje Kuwa KIZIWI jamani, Walahi nilishindwa kuamini na kWa Kuwa Mimi Mshipa wangu wa fahamu ulishakatika nilishuka kwenye Gari na kurudi kwa Yule dada.

“Mrembo “

Nilimuita kwa sauti ya utulivu sana..

Msichana Yule Hakugeuka wala kushtuka.

Kijana wenu sikukata tamaa nilimshika ili kuweza kumshtua.

“Dada nakusalimia muda Mrefu sana lakini umenikaushia”

Nilimlalamikia.

“Aaah, Sawa lakini hapa Wala awauzi hizo barafu, labda huulizie Nyumba ya jilani maana me pia ni mgeni”

Nyieeeh Kama zambi nahisi nilipata Kubwa sana maana nilijikuta nikicheka kutokana na anavyoongea kwa nguvu sana lakini pia majibu yake na mazungumzo yangu ni vitu 12 tofauti……

JE HUYU TÜMLE AU TUMUONEE HURUMA ??

ADA (niloge)

MTUNZI: PATRIA DAMAS

SEHEMU YA: 02

SONGA NAYO……

🤎🤍🤎🤍🤎🤍🤎🤍

Walahi nilijikuta nikicheka sana. Mwisho nikamwambia.

“Sister mi nakusalimia tu ni Rafiki wa Mwarabu koko naitwa Mahil “

Wakati huo ata Mimi Nilizungumza kWa sauti ya juu sana 😂🙌 Yaani imagine na Mimi nilikuwa nafosi ili aweze kusikia ni kitu gani nazungumza.

Msichana hiyo aliniangalia kisha akajibu.

“Aaaaaash hapo sasa ndio nimekuelewa, kumbe unatafuta chumba ? Aah umu Ndani hakuna sisi wenyewe ndio tumeamia na mama yangu na ndio tumemaliza kule nyumba kote kumejaa”

“Mweeeh we kweli bure”

Nilizungumza kWa hasira na kuondoka zangu.

Nilitoka nje nikiwa Nina hasira sana utazani nilifosiwa kwenda kuzungumza nae.

“Huyu msichana wenu ni mshenzi sana, Yaani ni anafanya makusudi au nta za uchafu zimejaa masikioni mwake ??”

Nilimuuliza mwarabu koko.

“Ahahhaha relax Broh relax 😂🙌 huyo ndio Ada Bwana, sikuwai kuelewa kabisa Kuwa yeye ni Kiziwi au masikio yake yanapokea Maneno tofauti “

“Yaani mtu namsalimia halafu ananiambia habari za mabarafu me mabarafu ya nini na kifua iki ??”

Yaani nilijikuta nikipata hasira sana, akili yangu ilikataa kabisa kuelewa Kuwa dada Yule ni kiziwii.

Basi tuliendelea kumdiskasi Mdada wa watu uku safari ya kuelekea Nyumbani ikianza, siku hiyo Mimi na mshikaji wangu tulienda Nyumbani na alikuwa akilala kabisa.


Nyumbani kwetu mwarabu walimzoea sana Yaani walimzoea utazani ni Mtoto wao, mwarabu anaweza akaja Nyumbani kwetu muda wowote ule anaotaka yeye na asipate shida yoyote anapokelewa Kama kawaida.

“Sema Ada ni mrembo sana “

Nilimwambia mwarabu koko, muda huo Mimi na yeye tulikuwa chumbani tu tukicheza ma game kama kawaida yetu.

“Huna lolote Broh hapo unataka kumuandalia mazingira ya kumkamata ndege tu umle umeletelekeze Kama hao wengine”

Mwarabu Walahi ananijua sana, na katika vitu alivyoongea hakuna ata Kimoja cha uongo, Yaani hapo nilikuwa namuandaa mwarabu ikiwezekana aende akazungumze na Ada ili niweze kumpata.

Ila Bwana kwenye ukweli iwe ukweli tu huyu Binti ni mrembo sana, Kuanzia usoni mpaka Umbo yaani unaweza ukasema Kuwa ni Kama Mungu alimpendelea sana Yaani Mdada mrembo hatari.

“Zungumza nae Basi we si umemzoea kidogo ??”

Nilimwambia mwarabu.

“Ebu niache mie, unajua pale mtaani ushaniletea shida na madada wote uliopita nao, Yaani kila mtu ananilaumu kwa kuwaunganisha. Na wewe halafu Leo hii unataka Uniletee shida na mpangaji Mpya “

Safari hii Bwana mshikaji wangu akagoma kabisa kunifanyia Jambo langu, Yaani alikaza zaidi ya kukaza.

“Nitampata tu “

Nikaanza kujiongelesha kimoyomoyo tu.

*******

Siku zilisonga uku niliendelea kumfatilia ada nyieeeh huyu dada ni mgumu Walahi, nilifanya kila njia kila kitu ili niweze kumpata lakini alikuwa ni msichana Mwenye misimamo ya aina yake.

Kwenye kumzoea nilishamzoea na mpaka nikawa najua jinsi ya kuzungumza nae, Yaani ukitaka kuzungumza na Ada ni lazima muangaliane ili aweze kuangalia movement za mdomo wako lakini pia Kama unaweza kutumia ishara hii Una rahisisha zaidi.

Kitu ambacho nilishindwa kukuelewa kWa ada ni hii ya kumuongelesha kitu halafu asipokuangalia anakujibu kitu kingine kabisa, nilikuwa najiuliza ni anasikia Maneno tofauti ? Au Anahisi Kuwa ameongeleshwa na Anajibu anavyojisikia.

Siku moja nikiwa Ndani chumbani kwa mwarabu, muda huo mwarabu hakuwepo nyumbaani alikuwa ameenda kwenye mishe zake kwani yeye ni mtu wa mishen town, nilitumia muda huo kumuita ada chumbani kWa mwarabu na kwakuwa tulishazoeana Ada hakuogopa ata kidogo akaja.

“Ulikuwa unafanya nini??”

Nilimuuliza uku tukiangaliana maana kwenye upande wa ishara bado kabisa sikuwa nazijua ishara zao.

“Napika “

Alijibu Ada kwa sauti ya juu sana, daaah hii nayo inanikata sana, kWa wakati huo sikutaka mtu yeyote ajue Kuwa Nipo chumbani na Ada.

“Unaweza kuongea taratibu ?”

Nilimuuliza maana mtu anapayuka utazani anaongea na mtu wa nje kumbe ni tumekaa kwenye kochi moja.

“Unasema ? Kuongea taratibu Mbona naweza halafu Mimi siwezagi kuzungumza kwa sauti ya juu sana si unasikia sauti yangu inatoka kwa mbali sana “

Eeeeeh Yaani ni Kama sauti ndio ilikuwa inaongezwaaa hivi 😂🙌 halafu Mwenyewe ni anaona anaongea Kama ananong’oneza.

“Sasa Ada achana na ili Mamaa Angu, hivi bado Ujafikilia jibu langu ? Au utaki kuamini Kuwa nakupenda sana ??”

Hapo Ada akaanza kuona aibu na kuinamia chini akaanza kukunja kuja kijora chake alichokuwa amevaa.

“Nikubalie nikuoneshe maana halisi ya husband material


Bwana Bwana hapa Nilizungumza pasi na kuangaliana maana yeye alikuwa ameinamia chini hivyo hakuwa ameelewa Nimeongea nini na Kama kawaida akajibu.

“Aaaah kumbe sasa me siwezi Kuwa mchepuko kwakweli, me Mwenyewe Mamaa yangu alinizaa na mume wa mtu nikawa Mtoto wa nje ya ndoa, we baki na mke wako tu “

“Aaaah we nawe ni dishi Walahi, Yaani unayumba muda wowote pasi na kujali kuna upepo au hakuna upepo “

Nilizungumza nikiamini kuwa hajaelewa kwani hakuwa akiniangalia.

“Huyu sasa ni kumla kinguvu tu “

Nilijiambia kimoyo moyo.

Nilisogea mpaka kwenye sabufa la mshikaji wangu na kuliwasha kWa sauti ya juu kabisa, nikasogea mlangoni na kufunga mlango kisha nikamsogelea Ada.

“Chagua unipe kwa utulivu au tushindane nguvu ??”

Nilimwambia na wakati huo tulikuwa tukiangaliana.

“Kukupa nini ??”

Akaniuliza.

Nikaona huyu ananiletea mambo ya utoto tu kudadeki zake, nilimvuta Karibu yangu kabisa na kuanza kukisi nae kWa kumfosi.

KWa wakati huo sikuwa nikiogopa Wala nini zaidi nilisikiliza msukumo wa mwili wangu.

“Aaaaah, niachie “

Alipiga Kelele Ada.

KWa muda huo Bwana sauti ya Ada iliisha Ndani tu kwani mziki ulikuwa mkubwa sana.

Nikiwa naendelea kumlazimisha ada, gafla nikasikia sauti ya zungu dirishani.

“Oyaaah fungua mlango Basi “

Haraka nika……

ITAENDELE….
ADA (niloge)

MTUNZI: PATRIA DAMAS

SEHEMU YA: 03

SONGA NAYO……

🤎🤍🤎🤍🤎🤍🤎🤍

Daaaah Yaani mwarabu kaja kuharibu kila kitu Yaani nilikuwa nakula Mzigo wa Ada maana ni Kama alitulia hivi.

Haraka nikamuachia na kumwambia.

“Ila wewe muoga sana nilikuwa nilikutania tu Rafiki yangu”

Baada ya hapo nikajiweka Sawa na ada akajiweka sana nikazima mziki na kufungua mlango, kitendo cha kufungua tu mlango Ada akatoka nje kwa kasi ya 5G ni Kama hakuwa anaamini kama Ametoka salama.

“Wewe ulimuingiza huyu Ndani ?!”

Mwarabu aliniuliza baada ya kuingia Ndani.

“Aaaah tulikuwa tunapiga story za hapa na pale si unajua Tena “

Nilijibu uku nikijichekesha tu.

“Story wapi wewe ulikuwa unataka kumla Mtoto wa watu, story gani Mnapiga uku umewasha mziki mkubwa kiasi hiko ? Broh najua hauna nia njema yoyote ile na huyu Binti Ebu Muache, at least angalia hali yake au mama yake, wanaishi maisha magumu sana “

Alizungumza mwarabu koko kwa sauti ya huzuni sana, kuna kitu niliona Kuwa akipo Sawa hivyo nikamuuliza.

“Kwani wanaishi maisha gani ??”

“Magumu Yaani magumu, hivi ushangai kila siku ni wanakula mboga za majani ? Tazama mavazi ya Ada, ni kila siku Vijora na anarudia rudia, tazama jinsi ambavyo vimepauka na bado anashare na mama yake, iko hivi Ada Anamtegemea mama yake kwa kila kitu, sio kwamba Ada ataki kufanya kazi lakini hiyo hali yake ndio inamfanya watu kutokumpa kazi na ukizingatia yeye sio msomi, kWahiyo hapo ni mama yake aangaike na tenga la mboga juani ndio wapate chochote kitu”

“Lakini Ada anaweza akamsaidia mama yake kuuza mboga “

Nilimwambia uku nikiwa sijafikilia kabisa.

“Kama tu sisi watu wake tuliomzoea tunapata nae shida kwenye mawasiliano itakuwaje watu ambao awajamzoea Unafikili biashara itaenda ? Tuachene na hayo Broh me ni mshikaji wako nakuomba sana achana na Ada Kama auna plan nae yoyote ile ya maisha “

Daaaah kuna Namna nilijisikia vibaya sana na ukizingatia na kitendo ambacho nilitaka kumfanyia Walahi nafsi ilinisuta sana.

“Lakini sikuwa na nia mbaya yoyote ile kuhusu yeye “

Nilijitetea.

“Mi nakujua Broh endelea kuangaika na hawa wadangaji wazoefu Ada muache kaama Alivyo “

Basi nikaamua kubadilisha mada pale na kuzungumza mambo yetu mengine, kuna Namna mwarabu ni Kama alibadilisha akili yangu hivi, nilitaka kupita tu na Ada lakini niliona Kuwa naitajika kunisaidia chochote kitu ikiwa Kama ni sehemu ya msamaha kWa kile ambacho nilitaka kumfanyia.

*******

Week moja ilipita nikiwa sijaenda kabisa Nyumbani kWa Kina mwarabu, siku hiyo niliamka mapema na kuingia zangu kazini na Majila ya jioni nikafunga safari na kwenda kwa kina mwarabu, siku hiyo sikuwa nimeenda mikono mitupu nilienda na baadhi ya zawadi kwaajili ya Ada na Mamaa yake.

Nilikuwa nimewanunulia kiroba cha , Unga, mchele, maharage na sukari .

Katika siku zote sikuwai kukutana na mama Ada lakini siku hiyo ndio nilimkuta ada akiwa amekaa nje na Mamaa yake na sura ya mama Ada haikuwa ngeni kabisa machoni mwanga ni vile tu sikumbuki niliwai kumuona wapi.

“Za hapa, shikamoo mama “

Niliwasalimia kWa heshima Sanaa.

“Eeeeh wewe si Mahil wewe au nimekufananisha ??”

Mama Ada aliniuliza na alionesha Kuwa ananifahamu Sana.

“Ni Mimi mama”

Nilijibu uku nikijaribu kuvuta kumbukumbu niliwai kumuona wapi.

“Ni wazi Kuwa umenisahau “

Alizungumza mama huyo.

“Ni kweli mama sina kumbukumbu nzuri kuhusu wewe”

“Nilikuwa ni mpishi wa shuleni kwenu kipindi kile mlivyokuwa kidato cha Tatu Sijui cha nne sikumbuki vizuri lakini nakumbuka sura yako na Jina lako maana ulikuwa na vituko sana. “

Daaaah nyie huyu maana ana kumbukumbu sana walaahi, Yaani katika Wapishi wa shuleni huyu mama nilikuwa nikimpenda sana, kwanza alikuwa ananiwekea chakula kWa Kunijazia kwakuwa tu nilimzoea sana, nakumbuka Mara ya mwisho alifukuzwa kazi baada ya kusingiziiwa Kuwa anaibaga chakula na kupeleka Nyumbani kwake.

Basi tuliongea Mengi sana mwisho nikawakabizi vitu ambavyo niliwapelekea.

“Asante sana aiseeeh Kijana wangu, lakini hivi ulikuwa unatuletea sisi kweli ??”

Mama Ada aliniuliza.

“Ndio mama, Ada ni Rafiki yangu sana na nikaona nimsapoti tu unajua sisi ni binadamu na ata hivyo nimefurahi sana kujua Kuwa wewe ndio mama wa Ada, hivi huyu ndio alikuwa Anakufanya unaniita mkwe au kuna Mtoto mwingine??”

Nilimuuliza maana huyu mama kipindi cha nyuma alikuwa akiniita mkwe.

“Ahahhahah nddio huyo huyo sasa hivi amekuwa Mdada “

Muda huo Ada alikuwa amechangamka na kuingiza vitu Ndani nisije nikaghaili bure.. 😆😂

“Asante sana Mahil “

Ada alinishukuru baada ya kumaliza kuingiza vitu Ndani.

“Tuko pamoja sana Rafiki yangu, mchumba wangu wa utotoni “

Nilimwambia.

Bwana Bwana kwakuwa Ada hakuwa ameniangalia wakati nazungumza haraka akajibu.

“Kumbe mke wako amejifungua? Hongereni sana lakini Mbona watoto wanne ni wengi sana “

😂🙌 ila huyu msichana Mbona ananitafutia dhambi mwenzenu ? Yaani anataka nianze kumcheka mbele ya mama yake ili mimi nionekane Kuwa ni Kijana wa hovyo.

Mama Ada akamvuta Mtoto wake kwa nguvu sana na kumfanya akae chini bila kupenda kisha akamwambia.

“Hajakuambia Kuwa mke wake amejufungua amesema Kuwa Tuko pamoja mchumba wake wa utotoni, we Sijui ukoje wewe”

Mama Ada alimaliza kumuelezea Mtoto wake na akamtuliza na Mbao mmoja me nikabaki kuwaangalia tu wakibishana.

Ila Ada na mama yake wanaelewana vizuri kabisa Yaani wanazungumza kWa Maneno lakini pia kwa ishara.

Naweza nikasema Kuwa huu ndio ulikuwa mwanzo mzuri sana wa Mimi kumzoea mrembo Ada, tulijikuta tukianza Kuwa watu wa Karibu sana..

Mambo yakaanza kwenye simu Bwana, tulikuwa tunachati mpaka Saa 8 usiku yote ni kupiga umbea tu wa hapana pale.

Baada ya muda Ada akanikubalia lile ombi langu la mahusiano, Jambo baya ni kwamba alinikubalia kipindi ambacho sikuwa nikimuitaji Tena, alinijibu kipindi ambacho nilikuwa nikumuonea huruma sana yeye na mama yake.

Yaani iko hivi mimi sijawai ku fall in love na mwanamke yeyote Yule Yaani Mimi ni mzee wa gusa aachia twende, kwakuwa sikutaka kumvunja moyo nikajifanya Kuwa nimefurahi sana na mahusiano kuanza Rasmi.

Ada ni mwanamke anayejali sana Walahi, muda mwingi aliniuliza Kama nimechoka, amuda mwingine aliniuliza Kama nimekula, muda mwingi alihakikisha Kuwa Nina Furaha.

KWa upande wangu hayo mambo yalinikela sana Tena sana ni vile tu sikuweza kumwambia.

Siku moja nikiwa nimelala chumbani kWa mwarabu koko, nilishtuka sana baada ya kuhisi kama kuna mtu hivi yupo Karibu yangu, ile kufungua macho tu ni uso kWa uso na Ada ambaye alikuwa amelala pembeni yangu akiniangalia.

“Aaaah umenishtua sana umeingia Saa ngapi ??”

Nilimuuliza tukiwa tunaangaliana hivyo alielewa swali langu.

“Muda sio mrefu, nimekuletea chakula upate kula mpenzi wangu “
Uwiiiiiih huyu sasa kuongea taratibu ajui halafu ndio kakazana kuniita mpenzi na sikuwa nataka watu wajue Kuwa Mimi nina mahusiano na Ada.

“Asante unaweza kwenda “

Nilimjibu kavu kavu Wala sikumchekea.

“Jamani nataka kukuangalia ukila chakula changu Nimekupikia wewe tu “

Eeeh hivi mambo ya mahusiano ndio yako hivi uwiiiiih Sijui Kama nitakuja kuoa Mimi Mbona naboweka nikiona Kuwa mtu ni ananijali sana au mimi ndio Nina matatizo.

Ada hakuwa na baya jamani, aliweka chakula vizuri na kuanza kunilisha Kama Mtoto wake vile, alinilisha kWa utulivu uku akinikisi kisi.

“We unataka nikupitie mwenzio nipate dhambi “

Nilizungumza Kimoyo moyo.

Yaani mambo mazuri nilikuwa nikiyataka sana sema ni vile tu nilikuwa nikimuonea huruma.

Huyu nae bwna ni Kama alikuwa na upwiru hivi maana alikuwa anafanya vituko ambavyo viliweza kabisa kwenye kiunipandisha midadi ya mwili wangu.

Niliinuka chap na kwenda kuwasha mziki kWa sauti ya juu sana na kufunga mlango Kama kawaida kisha tukaingia mzigoni.

Polepole Mimi na Ada tukaanza kuama ulimwengu, shida ya Ada ni sauti 😂🙌 Yaani sauti yake ni iko juu muda wote kitu cha kushukuru ni ile sauti ya mziki tu ambayo niliiweka.

Baada ya muda tukaanza kuingia kwenye mechi Rasmi naa hapo ndipo nikagundua Kuwa Mimi ndio mwanaume wa kwanza kabisa kwa Ada.

Ada alihisi maumivu makali sana ambayo alishindwa kuvumilia haraka nikamziba mdomo na Mimi nikaendelea na shughuli yangu maana ni ameyataka Mwenyewe.

Muda huo huo mlango ukagongwa na uligongwa kWa sauti ya juu Sana Mimi ndio nilisikia hivyo nika……

ITAENDELEA…..

ADA (niloge)

MTUNZI: PATRIA DAMAS

SEHEMU YA: 04

SONGA NAYO……

🤎🤍🤎🤍🤎🤍🤎


Nilisimamisha zoezi langu na kumuoneshea Ada Ishara ya kukaa kimya, nikajiweka Sawa na kufungua mlango na kujifanya Kuwa nilikuwa nimelala.


“Eeeeh pole baba weeh Nimekusumbua “

Alizungumza mama Ada ambaye alikuwa Amesimama mlangoni kwa wakati huo.

“Bila samahani mama hivi umeanza kugonga muda mrefu eeeh ? Maana nililala nimesikia hodi kwa mbali sana “

Nilijielezea uku nikiwa na wasiwasi wa hali ya juu.

“Hapana Mwanangu, namtafuta Ada Sijui ata ameenda wapi “

“Aaah alikuwepo nina Uhakika Kuwa hajaenda mbali ulikuwa na shida nae sana “

“Hapana baba, nilitaka kumuaga tu, akija Mwambie Kuwa nimeenda kufuata mboga kule chini mashambani “

“Hakuna shida mama “

Basi mama Ada akaondoka na Mimi nikarudi Ndani chapu na kufunga mlango.

“Nani huyo ??”

Ada aliniuliza.

“Nani Nani kitu gani mama ako huyo, Yaani Leo ulikuwa unaniingiza matatizoni “

Nilijikuta nikimfokea maana yeye ndio alijileta kwangu.

Ada alikasilika na kuvaa mavazi yake na haraka akaondoka.

“Utajua Mwenyewe Bwana, mtu unaonewa huruma halafu unaleta mambo ya mapenzi hapa “

Nilianza kulalamika.

Niliona ni Kama Ada ameharibu siku yangu hivi, nilivaa mavazi yangu na kuondoka zangu Nyumbani kwetu.

Siku hiyo sikutaka kukaa Nyumbani kizembe, Majila ya usiku nilitoka zangu na kwenda club, Walahi nilikuwa sijatoka muda mrefu snaa hivyo siku hiyo Niliinjoy sana na sikuacha kuchukua demu wa kunituliza kWa usiku huo.

Siku hiyo mambo yalikuwa tofauti sana kWa upande wangu, Yaani Nipo na mwanamke mwingine lakini akili yangu ilibaki ikimkumbuka Ada, na hii ilinifanya nishindwe kufanya chochote kile na mwanamke ambaye nilimlipa kWa siku hiyo.

“Vaa uwende “

Nilimwambia msichana huyo uku nikimpatia Pesa zake.

Week nzima ilipita uku akili yangu ikimfikilia Ada, sasa Sijui uku ndio ku fall in love au ni kitu gani maana nilifikia hatua ya kutabasamu peke yangu kila nilipokuwa nikifikilia moment nzuri ambazo nilipitia na Ada.

KWa kipindi iko, mawasiliano kati yangu na Ada Yalikata kabisa, Ada hakuwa akinitumia sms Kama ambavyo alinizoesha, lakini pia ata nilipomtumia sms zangu hakujibu na hii iliniuma sana.

Siku moja nikiwa chumbani kwangu, dada yangu mkubwa akaja chumbani kwangu na kuniambia.

“Baba anatuita sote sebuleni”

“Eeeh huyu mzee nae anataka nini usiku huu ??”

Nilimuuliza dada Angu.

“Ebu inukaga twende uku labda anataka kugawa urithi utajuaje ??”

Ila dada yangu jamani 😂🙌 sasa mambo ya urithi yanekujaje wakati mzee wetu bado ako na nguvu za kutosha.

Nilibaki nikijivuta vuta dada yangu akanishika mkono na kunivuta kWa nguvu sana na haraka tukafika sebuleni.

“Eeeeh ni nini kunivutia Mwanangu kama hivyo ??”

Mama yangu alimuuliza dada yangu baada ya kuniona Kuwa ananivuta sana.

“Alikuwa ataki kutoka”

Baada ya muda familia nzima tulikuwa tumejumuika mezani na baba akafungua mazungumzo Ka kuuliza.

“Mnataka umu Ndani niwafukuze au ??”

Hapo kwanza watoto Kama watoto tukaangaliana kisha dada mkubwa akauliza.

“Kivipi baba ??”

Baba alituangalia kWa muda kisha akaendelea.

“Hivi Mnaona ni Sawa kuendelea Kuwa umu Ndani eeeh ? Umri unaenda watoto wangu, Mimi katika umri wenu tayali nilikuwa Nina Nyumbani kwangu lakini pia Nina mke “

“Aaaah baba umeanza mambo yako “

Dada yangu wa pili ambaye ndio nafanana nae hadi tabia akaanza kulalamika.

“Tena wewe ndio usiongee kabisa, maisha unayoyaishi sasa, ikifika miaka mitano mbele utakuwa na majuto Makubwa sana, Mungu amewabariki sana watoto wangu , mnawazazi ambao wanawajali sana, ikiachana na sisi Mungu amewabariki kazi nzuri sana lakini ni kaama Mungu hizi baraka alitoa kWa watu ambao sio sahihi kabisa “

Nyie baba alilalamika sana na ukija kuangalia kila kitu kilikuwa kina ukweli mtupu, Yaani sisi ni watu wazima Tuna kazi nzuri lakini maisha yetu uwiiiiiiih 😂🙌 ni huzuni kubwa, Yaani sisi ni watu wa kusubiili ugali wa kengere Nyumbani halafu Pesa zetu tunafanyia mambo ya hovyo.

“Me tayali ninamchumba baba muda ukifika nitamleta “

Nyieeeeh si nikajikuta nikilopoka na muda huo akili yangu ilimuwazia Ada.

Familia yangu ilifurahi sana na kila mtu akabaki kunipongeza na kusisitiza kumpeleka mpenzi wangu Nyumbani.

Baada ya muda kikao kiliisha naa kila mtu akarudi chumbani kwake.

“Sasa ndio nimefanya nini mimi jaamani “

Nilianza kujilaumu kutokana na iliopokaji wangu.

Siku ziliendelea kwenda na Nyumbani kila mtu akawa anamuilizia mchumba wangu, kila mtu akawa anauliza ni siku gani nitaenda kumtambulisha mchumba Angu.

********

Ikiwa ni siku ya weekend, nilifunga safari na kwenda Nyumbani kWa kina Ada, nilifika na kupaki gari na muda huo Ada alikuwa amekaa nje na aliponiona tu akanyannyuka na kuingia Ndani.

“Ada, Ada, ada “

Nilimuita mfululizo ili aweze kusimama lakini ilishindikana kwani hakuwa akinisikia.

Nilibaki nikishangaa tu na kujiuliza kuna kitu gani nimemkosea Ada maana ni amechukia sana tangu siku ile tulipokutana kimwili.

“Yaani nilikuwa najiandaa Nije kwenu “

Alizungumza mwarabu koko baada ya mimi kuingia chumbani kwake.

“Daaaah Nina shida na Ada “

Nilizungumza.

“Alikuwa hapo nje muda sio mrefu”

Alijibu mwarabu uku aakishuka kitandani kwajili ya kwenda kumuita Ada, lakini kabla hajatoka nje nikazungumza.

“Nataka kumuoa Ada “
Hapo kwanza Mshikaji wangu akarudi nyuma na kuangua kicheko cha hali ya juu, baada ya muda akanyanyua mkono wake na kuanza kupika joto la mwili wangu.

“Broh niko serious ujue “

Nilimwambia kWa sauti ya kumaanisha kabisa.

KWa wakati huo sikuwa nikitania ata kidogo, moyo wangu na akili yangu ni muda wote vinamuwaza Ada, Yaani unamfikilia mtu mpaka unahisi kichwa kinapata moto.

“Mbona Kama uko serious kweli hivi “ Alizungumza mwarabu na kukaa mbele yangu.

“Najua ujanizoea hivi lakini ninachozungumza nakimaanisha, nampenda sana Ada Tena sana, mwarabu najua uwezi kuamini lakini ukweli ni kwamba Ada anatembea na hisia zangu zote kWa sasa na kubwa kuliko nimewaambia wazazi wangu kuhusu Ada “

Mwarabu alishtuka na kuinuka mzima mzima na kuanza kuzunguka uku na uku kisha akakaa na kuniambia.

“How ? Yaani wazazi wako umewaambia nini kuhusu ada, Walahi unanivuruga”

“Achana na hivyo, Jambo kubwa ni kwamba Ada ataki kabisa kuzungumza na Mimi na hali hii imetokea tangu siku ile ambayo nilikutana kimwili na Ada”

“Eeeeeeeh 😳😳”

Mwarabu alishtuka sana na kubaki akiwa amenitolea macho maana hakuwa anajua Kama Mimi na Ada tulishavunja amri ya Sita.

Nilichukua muda wangu na kumuelezea kila kitu ambacho kilitokea siku ile.

“Ada ameumia baada yakukuonesha kila aina ya upendo halafu ukamuoneshea dharau lakini kila kitu kitakuwa powa, Kama uko serious me nakuunga mkono Kaka mkubwa “

Tulizungumza Mengi na mwisho mwarabu akanisaidiia na nikaweza kuzungumza na Ada na nikapata msamaha kutoka kwa babe wangu KIZIWI.

Siku zilisonga na penzi langu na Ada lilikuwa likiziidi kunoga tu na hapa ndio nilielewa maana halisi ya mapenzi, nilielewa maana halisi ya kupendana.

Hatimaye siku ya kumpeleka Ada Nyumbani iliwadia na sikusita kumpeleka, siku hiyo nilihakikisha Kuwa Ada wangu anapendeza sana na katika suala la kupendeza ni 1000/10 Yaani my wangu aliwaka sana.

Mimi na Ada tulifika Nyumbani na tulipokelewa na baba yangu mkubwa ambaye ndio alisimama nje kwaajili ya kumpokea mkwe.

Kitendo cha Ada kumuona tu baba yagu mkubwa, Ada alishtuka sana na kwa uwoga na wasiwasi wa hali ya juu akanikumbatia.

Lakini pia kWa upande wa Ba mkubwa alishtuka sana na kubaki akitetemeka kWa kiasi chake.

JE KUNA NINI KATI YA HAWA WATU WAWILI ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO…..
ADA (niloge)

MTUNZI: PATRIA DAMAS

SEHEMU YA: 05

SONGA NAYO……

🤎🤍🤎🤍🤎🤍🤎🤍

Niliogopa sana maana Ada hakuonesha Kuwa Sawa kabisa naa alinikumbatia kwa nguvu sana.

“Ada, ada “

Nilimshtua ili kutaka kumuuliza.

Baada ya muda Ada alitulia na nikapata kumuuliza.

“Shida nini lakini ??”

“Aaaah hakuna shida lakini najikuta napata wasiwasi sana ni Mara yangu ya kwanza Nyumbani kwenu na Nipo Mwenyewe “

Hapo nilimuelewa ba mkubwa akatukaribisha kisha Mimi na Ada tukaingia Ndani.

Aaaah kitendo cha familia yangu kumuona Ada kilifuraji sana na kila mtu akakubali Kuwa Ada ni mrembo Yaani kila idala
Iko vizuri.

“Shikamooni “

Alisalimia Ada kWa sauti yake ya juu Kama kawaida yake, hapo familia yangu yote ikagundua Shida ya Ada.

Kitu ambacho nampendea Ada ni msikilizaji mzuri sana, ninaposema Kuwa ni msikilizaji mzuri sana ni Namaanisha Kuwa ni Mtulivu na alikuwa makini sana kwenye kuangalia midomo ya watu ili kuweza kwenda Sawa nao ili asiweze kujibu kinyume na kilichoilizwa.

“Binti wewe Una elimu gani ?”

Mama yangu alimuuliza Ada na wakati huo mama hakuwa ameangaliana na Ada Na shida ikaanzia hapo.

“Aaaah hapana sijawai kuolewa na mwanaume mwingine huyu ndio wa kwanza “

Ada akajibu kinyume kabisa na alivyoulizwa kila mtu akacheka isipokuwa baba yangu na dada yangu mkubwa ambao walikuwa makini sana kwenye kumtazama Ada.

Kitendo cha familia yangu kumcheka Ada kilimkosesha Ada amani na kumfanya awe Mpole sana na safari hii Akashindwa kabisa kuwaangalia usoni na hali hii ndio Adui mkubwa Sana kwa Ada kwani asipokuangalia awezi kujua unazungumza nini.

“Kilichowachekesha ni nini ??”

Niliwauliza ndugu zangu kWa hasira mno.

“Kwamba tusicheke au ? Mahil Ebu Kuwa serious Mwanangu huyo mkwe yuko wapi ??”

Mama yangu aliuliza na alionesha wazi Kuwa hakuwa amevutiwa na Ada, na sio kuvutiwa yaaani hii shida ya Ada ndio ilikuwa ni sababu kuu.

“Huyu ndiye mwanamke wangu ndio Ada ambaye nilikuwa Niliwaambia, nakumbuka Niliwaambia Kuwa mwanamke wangu Ana shida kidogo na hii ni ndio shida yake”

Nilizungumza kwa hisia ya hali ya juu sana.

“Me sioni kama kuna tatizo, mimi Kama WiFi mkubwa nampistisha WiFi yangu Sijui baba zangu mbasemaje “

Hapo haraka baba yangu mkubwa akadakia.

“Upande wangu ni big no, Yaani Mahil Mwanangu ujaona wanawake wengine zaidi ya huyu ? Usinielewe vibaya au labda kuna kitu kimekushawishi kWa huyu Binti, familia yake Ina Pesa nyingi kuliko sisi ??”


Eeeeh Mbona ni majanga Yaani ni wazi Kuwa Ada wangu anakataliwa kweupe kabis kitu ambacho nashukuru ni kwamba Ada hakuwa akisikia Wala kuelewa kile walichokuwa wakizungumza kwani alikuwa akiangalia chini tu.


“Inatosha sasa aaah, Ada ni chaguo la Mahil na tunatakiwa kumuunga mkono Kijana wetu kWa hatua kubwa Aliyochukua kWa sasa lakini sio kuweka vipingamizi “

Baba yangu Alizungumza kiume na aliamua kusimama Kama baba wa familia.

“Mahil Mimi ndio mama yako na mimi ndio najua uchungu wako, na. Kama Mimi ni mama yako Basi tambua Kuwa huu mkosi siutaki tena Ndani kwangu “

Daaaah 🥹 Nyumbani kwetu Leo kumewaka moto sababu ni Ada, na sababu kuu ya Ada kukatakiwa ni hii tatizo lake lakini pia kwakuwa sio msomi wala hawana Pesa.

Nilitumia kila njia kuhakikisha Kuwa Ada aelewi ni mambo gani yalikuwa yakiendelea kwa wakati huo.

Baada muda familia nzima tukajumuika kwenye meza ya chakula na baada ya kila Mimi na Ada tukaaga na kuondoka, muda huo ndugu zangu walibaki wakiwa wamechukia sana isipokuwa baba tu na dada yangu mkubwa.

Sikumrudisha ada Nyumbani kwao zaidi Nilimchukua na kumpeleka hotelini ili aweze ata kupumzika.

“Familia yako ni wachangamfu sana “

Alizungumza Ada uku akiniangalia kwenye Kioo ambacho kilikuwa Ndani ya chumba iko cha hotel.

“KWa Mara ya kwanza namshukuru Mungu kwa kukufanya wewe Kuwa kiziwi maana Maneno ya Leo yangeuvunja moyo wako “

Nilizungumza kimoyokoyo uku nikimkumbatia Ada wangu kWa Nyuma.

Baada ya hapo nikamshika mikono yake na kusogea nae mpaka kwenye kitanda na kWa utulivu nikazungumza.

“Ada nakupenda sana mpenzi wangu, nakupenda kuliko chochote kile, mwanzo sikuwa najua maana halisi ya upendo lakini wewe ndio umekuwa maana Halisi ya upendo kwenye maisha yangu, Naomba usimame na Mimi kwenye kila hatua, simama na Mimi kwenye kila kitu Nina imani tutafikia Lengo “

Hapo Nilizungumza uku machozi yakinilenga Lenga kwani niliku nikikumbuka Maneno machafu ambayo mama yangu Alizungumza juu ya Ada..

Siku hiyo Mimi na Ada tulilala pamoja hotelin na ilikuwa ni siku yetu ya pili ya mechi, siku hii mechi ilikuwa Kali sana kwani ilikuwa ni mechi ya kuinjoy na sio ya maumivu Kama ile ya kwanza.

Niliamka asubuhi na mkumkuta Ada ameshaamka na amekaa tu kitandani na alionekana Kuwa mi mtu mwennye mawazo sana.

“Uko Sawa ??”

Nilimuuliza baada ya kwenda mbele yake.

“Sio sana “
Alijibu Ada.

“Shida nini ??”

“Namuwazia mama ada, Sijui Kama ataweza Kuwa Mwenyewe mama yangu, unajua katika maisha yangu sikuwai kukaa mbali na mama yangu, naweza nikasema Kuwa Leo ndio Mara yangu ya kwanza kabisa Mimi kulala mbali na Mamaa yangu na amenitumia ujumbe huu “

Hapo nilichukua simu ya Ada na kusoma ujumbe wa mama yake ambaye ulisomeka hivi.

“Usiku wangu umekuwa mzito sana pasi na uwepo wako Ada wangu, kesho usichelewe kurudi nitakuandalia chakula chako pendwa, unisimulie familia yako Mpya umeionaje “

Daaah hii hali kama umelelewa na Mamaa tu ndio utaielewa sana, nikanyuka na kumkumbatia Ada wangu na nikamruhusu kulia kwenye bega langu.

Muda huo huo Mimi na ada tukajiandaa na kuanza kwenda Nyumbani lakini tukiwa njiani niliweza kupokea simu kutoka kWa mwarabu koko.

“Uko wapi Broh ??”

Mwarabu aliniuliza baada ya Mimi kupokea simu.

“Niko njiani NAKUJA uko niko na Ada”

“Eeeh sasa sikia, angalia Namna ya kuzuungumza na Ada muweke Sawa kisha ndio uje nae mama yake amefariki asubuhi hii “

Kwanza nika…..

UWIIIIIIIIH MATATIZO NI MATATIZO JAMANI ADA WANGU.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote