ALINIACHA KWASABABU SIZAI
Zayana ndio Jina langu, mwanamke ambaye nilikuwa na ndoto nyingi sana na kubwa kwennye maisha yangu.
Furaha yangu iliongezeka baada ya kuolewa na mwanaume wa ndoto zangu, mwanaume ambaye nimekuwa nikifunga na kusali ili aweze Kuwa mume wangu wa halali.
Huyu mwanaume Bwana mahusiano yetu yalianzia chuo, Yaani tulikuwa tukipendana sana na mwisho tukafanikiwa kufunga ndoa ya halali.
Ndoa. Yangu ilikuwa ni ya furaha sana, kila mtu aliitamani ndoa yangu na kuvutiwa nayo, nilikuwa ni mwanamke kwenye furaha kupita maelezo.
Kisanga kulianza baada ya ndoa yang kutimiza miaka 8 pasi na kupata Mtoto weeeh moto niliuona kwakweli ? Hivi ushawau kuchambwa na WiFi yako ambaye umempita miaka kibao kwenye kuzaliwa? Hivi ushawai kutendewa unyama mbele ya michepuko ya mume wako ?
Kama bado Kaa Nami soma kisa iki mwanzo mwisho…..
ALINIACHA KWASABABU SIZAI
SEHEMU YA: 01
MTUNZI: PATRIGIA DAMAS
www.tupohapa.com
ANZA NAYO …….
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Niite Zayana, mrembo wa miaka 33, najiita mrembo kwasababu, Mimi nikisimama na Binti wa mwaka wa 2000 mpaka 20005 anaweza yeye akaambiwa shikamoo halafu Mimi nikaambiwa mambo, inshot niko vizuri Kuanzia muonekano na kila kitu.
Zayana Mimi niliolewa lakini pia nikaachia sababu kuu ikiwa ni kuto kuzaa, nakumbuka niliolewa nikiwa na miaka 24 na nikadumu kwenye ndoa yangu Ndani ya miaka 8 pasi na kuwa na Mtoto ata Mmoja.
Hii kitu ilikuwa ikiniuma sana lakini nilijikaza kuhakikisha Kuwa nakuwa imara kwenye ndoa yangu, nakumbuka niliwai kumwambia mume wangu azae nje ya ndoa ili mladi tu apate kuitwa baba lakini pia nilifeli, anyway ongozana na Mimi kujua Mkasa huu ambao Nitakuanzia Kuanzia kwenye ndoa yangu ya kwanza mpaka hii ya pili inayonifanya nijione niko peponi.
*******
Ni siku ya weekend Kama kawaida, siku Kama hizi Mara nyingi uwa napokea sana wageni Nyumbani kwangu, muda mwingine ni ndugu wa mume wangu, muda mwingine ni marafiki wa mume wangu.
Najua unajiuliza Kwanini ni ndugu wa mume wangu tu na Rafiki wa mume wangu na sio ndugu zangu Wala Rafiki zangu, iko hivi, tangu nimeolewa na mwanaume huyo amenikataza vitu vingi sana, yaaah mimi ni Msomi lakini alinikataza kufanya kazi na baba yangu mzazi amekuwa akisapoti hivyo kwani alimfanyia mama yangu hivyo.
Mume wangu aliniweka mbali na marafiki lakini pia hakuwai kuruhusu ndugu zangu kuja kunitembelea.
Siku hiyo Bwana tulitembelewa na marafiki wa mume wangu ambao walikuja na wake zao lakini pia na watoto wao, hii kitu uwa inaniumaga sana na uwa namuoneaga huruma sana mume wangu ambaye anaitaji sana kuitwa baba lakini sikuwa na uwezo wa kumpatia Mtoto.
Nikiwa chumbani najiweka Sawa ili Nikaungane na wageni, gafla mume wangu akaingia chumbani na kWa jazba akaniuliza.
“Unavalia hivyo unakwenda wapi ??”
Niligeuka na kumuangalia mume wanngu kisha nikajibu kwa utulivu.
“Abbas Bwana, najiweka Sawa tu nije kuungana Nanyi kwenye chakula maana nimeshamaliza majukumu yangu yote”
“Unajumuika na sisi kwenye nini Yaani ? Zayana hivi kichwa chako kiko vizuri eeeh, tazama wenzio walivyopendeza na watoto wao ? Tazama Rafiki zangu wanavyocheza na watoto wao, Ila Mimi na wewe tuko hapa tunajiangalia kwenye vioo tu na kupaka hizo make up zako “
“Jamani, Kwahiyo kwakuwa Sina Mtoto ndio sitakiwi küpendeza au? Abbas Mbona Kama umekuwa mwiba kwenye maisha yangu kWa sasa, wewe ndio ulikuwa ukinipa moyo kila siku Kuwa kuna siku na sisi tutapata wa kwetu lakini kwa sasa mambo yamebadilika kabisa “
“Ebu Kaa kimya, sikia hakuna kutoka nje Sawa, uko nje wote Nitawaambia Kuwa haujisikii vizuri na umelala”
Aaah nguvu ziliniiishia kwakweli kWa utulivu wa hali ya juu nikavua mavazi yangu mazuri ambayo nilikuwa nimevaa na kusogea kitandani.
“Ikiwezekana lala kabisa maana utatoka nje baada ya wao kuondoka”
Alizungumza mume wangu na kutoka nje na kuniacha nikishangaa shangaa tu na Kuamini kitu ambacho ananifanyia.
Kiufupi mume wangu amebadilika sana, Abbas alikuwa ni mwanaume ambaye Anajalia sana, ni mwanaume ambaye alikuwa akinipa bega lake nipate kufutia machozi lakini sasa hivi yeye ndiye ananiliza.
Nikiwa chumbani kwangu najililia tu Mwenyewe, gafla nikasikia sauti ya mtu akiniita.
“Mrs Abbas, mrs Abbas “
“Abeeeeh “
Niliitika na kwenda kufungua mlango, alikuwa ni mmoja kati ya wageni na alikuwa ni mmoja kati ya mke wa Rafiki wa mume wangu.
“Ooooh mama zai “
Nilimuita baada ya kumuona.
“Nimeshangaa Abbas alivyosema haujisikii vizuri wakati muda mfupi tu ulikuwa Sawa kule jikoni ukiandaa chakula”
Alizungumza mwanamke huyo akionesha kujali sana kuhusu Mimi.
“Aaaahh si unajua Tena mwili wa binadamu ndugu yangu, Yaani nilikuwa navaa gafla tu tumbo limeanza Kunikata kwa nguvu sana mpaka nimeogopa mwenzio “
Niliamua kudanganga uku nikificha maumivu makali yaliyomo Ndani ya moyo wangu.
KWa pamoja mimi na msichana huyo tukaingia Ndani na kuanza kupiga story za hapa na pale.
“Hivi wewe na Abbas mmeshaenda hospital kwajili ya vipimo vikubwa ??”
Mama zai aliniuliza ni Kama alikuwa akinidadisi hivi.
“Yaaaah, yaaah tumeenda “
Nilijibu uku nikiwa Sina Uhakika na majibu yangu.
“Sijui Kama unanielewa Zayana, Naongelea kuhusu suala la ninyi kupata Mtoto, hii hali naona inaamuumiza sana Abbas na Mara nyingi uwa anazungumza na mume wangu”
“Tumeenda hospital na kila mtu yuko Sawa, Nafikili ni wakati wa Mungu tu ndio unasubiliwa kWa sasa”
“Mungu Awafanyie wepesi mwaya, maana ndoa ni Mtoto na Nyumba yoyote ile furaha kubwa ni kuwa na watoto “
Alizungumza hivyo na kuondoka nje hapo ni kama ndio alikuja kutonesha kidonda kikubwa sana kilichopo Ndani yangu nilijikuta nikilia sana.
Majila ya usiku, kila mtu aliondoka na kutuacha Mimi na mume wangu.
“Mume wangu “
Nilimuita Abbas.
“Niite Abbas tu inatosha, haya mambo ya mume wangu ni kuwekeana Giza tu kwenye maisha “
Kheeeeeeh 🙄😩 nyieeeh Mbona hamkuniambia Kuwa itafika hatua sitaruhusiwa kumuita mume wangu mume ? Eeeh hii Kali ya mwaka jamani.
“Sawa, aaah nili….”
Kabla sijamaliza kauli yangu Abbas akanikatisha na kuniambia.
“Kesho mama atakuja Sijui atafika Saa ngapi lakini hakikisha unamuandalia chakula anachokitaka yeye “
“Sawa, aaah nilikuwa….”
Kabla sijamaliza Tena kuzungumza Abbas akanikatisha kwa Mara nyingine.
“Aaah zima taa nataka kulala nimechoka sana”
“Lakini Abbas nataka tuzungumze suala ambalo ni muhimu sana”
Nilizungumza kWa utulivu sana.
Abbas akageuka na kuniuliza.
“Una mimba ??”
“Hapana “
“Haya hakuna cha muhimu hapo, na usinipigie Kelele “
Aaaaah nilishindwa kabisa kuzungumza hivyo nikapanda kitandani na kulala.
*******
Siku iliyofuata Majila ya Saa 7 mchana mama mkwe aliwasili Nyumbani,
Mama mkwe hakuwa peke yake Bwana alikuwa ameongozana na msichaana Fulani ambaye sikuwai kumuona kabla, alikuwa amejazia hatari, nyamaanyama Kama zote zilikuwa zikitikisika tu mwilini mwake.
“Binti yangu Karibu sana”
Mama yangu mkwe alimkaribisha msichana huyo na kuniangalia Mimi kwa dharau.
“Shikamoo mama, Karibuni “
Nilimsalimia na kuwakaribisha, mama mkwe akajibu.
“Hizo shikamoo zingekuwa mali Saa hizi ungekuwa umeniletea wajukuu, sasa wewe na Mimi tuna tofauti gani ? Mimi sizai kwakuwa umri umeenda na wewe je ? Au umeanzia kwennye uzee mwenzetu ??”
Eeeh Kama ni Picha jamani ndio kwanza linaanza Yaani mama mkwe ni kaama amekuja kwaajili yangu 🥹.
NAKUJA MY ZANGU KAMA
NI PICHA ILI NDIO KWANZA LINAANZA 🥹
ALINIACHA KWASABABU SIZAI
SEHEMU YA: 02
MTUNZI: PATRIGIA DAMAS
www.tupohapa.com
SONGA NAYO….
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Niliona kabisa hapa ni Kama disko Kaingia Mmasai, nikachukua mizigo Yao na kupeleka kwenye chumba cha wageni kisha nikarudi sebuleni.
“Begi la mke mwenzio Nina imani umepeleka chumbani kwenu na sio kWa wageni “
Alizungumza mama mkwe uku akimuanngalia msichana ambaye alikuja nae.
“Mke mwenzangu!!”
Nilijikuta nikiuliza kWa mshangao wa hali ya juu maana huyu mama mkwe anajua kunivuluga kwakweli.
“Nini ujasikia hapo ? Nimemleta mke wa Mtoto wangu, huyu ndio atatuzalia warithi wa Mali zote hizi, sio wewe umekuwa hapa kazi kujaza Choo cha mwanangu tu”
“Mama Mimi siwezi kukataa mke wa pili kwaajili ya mume wangu, maandiko ya dini yetu yanasema Kuwa mume anaweza kuoa mke wa kwanza mpaka wa nne kikubwa aweze kuwatimizia Mahitaji Yao muhimu, lakini pia Nafikili kuna utaratibu wa mke kuingia kWa mume na sio Kama hivi mama yangu, wewe unaijua dini hivyo hapa unakosea “
Nilizungumza kWa utulivu ingawa je moyo ulikuwa ukiniuma sana, mimi Bwana nilimruhusu mume wangu kuoa mke wa pili ili apate mwanamke wa kumzalia
Mtoto kwani kwangu ilionekana kushindikana kabisa hivyo niliamini akipata mwanamke mwingine Atapata Mtoto.
Lakini pia mke huyo nilitaka aje kWa taratibu za dini na sio Kama hivi anavyofanya mama mkwe wangu ambaye alipanga Kunikimoa kabisa.
Baada ya kumwaga Maneno yangu, nilishika njia na kwenda jikoni kuendelea na kazi yangu ya mapishi.
Majila ya jioni, mume wangu Abbas akarudi na kumkuta mama yake akiwa na mgeni ambaye ata yenye hakuwa akimjua.
“Umeoa bila kunishirikisha ??”
Nilimuuliza mume wangu muda huo Mimi na yeye tulikuwa chumbani.
“Kuoa ??”
Abbas aliniuliza kwa mshtuko mno akionesha kutokujua kitu.
“Si ndio, Abbas kumbuka Kuwa Una baraka zangu zote za kupata mke wa pili, lakini sio kWa style hiinuliyonifanyia, umeoa pasi na kuniambia na Mke wako umemleta Nyumbani kWa utaratibu ambao ata Mimi siujui “
“Zayana nimechoka sana aiseeeh na hizo habari unazonipa ni Mpya kabisa”
Kabla sijafanya kumwambia Abbas kuhusu mama yake na taarifa za mke wa pili gafla mama mkwe akaingia chumbani kwetu Tena pasi na kupiga Hodi.
“Mama ni nini jamani Mbona gafla chumbani kwangu ??”
“Ni chumbani kwako pia na Mimi ni mama yako, nakujua A to Z “
“Lakini Nipo na mke wangu mama, iki ni chumba cha Mtoto wako na Mkwe yako “
“Tangu muanze kutumia iki chumba na huyu mgumba wako ni matunda gani mmevuna, iki chumba akina maana kabisa ni Sawa na jikoni tu au store ambapo kila mtu Anaingia na hakuna faida yoyote ile”
Nilibaki nikimshangaa mama mkwe yangu ambaye hakuwa akijiheshimu ata kidogo.
Mama mkwe akaniangalia usoni kisha akaniambia.
“Toka nje Nina maongezi muhimu sana na Mtoto wangu “
Niligeuka na kumuangalia mume wangu ambaye pia akanipatia İShara Kuwa nifanye Kama mama yake anavyotaka.
Nilitoka zangu kWa utulivu na kwenda kukaa sebuleni alipokuwa amekaa Mdada huyo a ambaye alikuwa Mtulivu sana.
Baada ya muda mume wangu na mama yake wakatoka nje wakiwa wanazozana sana.
“Mama mi najua Kama unaniombea mema lakini haya mambo ya kuleteana mke kiolela olela kama hivi hapana na mambo ya kuongeza mke mama sio ya Mchezo ujue “
“Abbas me simaanishi Kuwa uongeze mke Sawa ? Ninachotaka huyu mgumba, huyu ambaye ajui kama raha ya Kuwa mwanamke ni kuitwa mama aondoke na umchukue huyu, mwanangu mpaka lini utakaa ukimvumilia huyu mwanamke ? Unataka kuja kuitwa babu na Mtoto wako Mwenyewe au ??”
“Siko tayali kwa sasa mama please, Maamuzi nitafanya Mwenyewe, lakini pia siwezi kuishi na mtu ambaye Simjui kabisa kabisa “
Mume wangu akamgeukia msichana Yule na kumwambia.
“Binti Asante kwa kushiriki, Asante kWa kuja Kama ambavyo mlikubaliana na mama yangu lakini Mimi siko tayali kuongeza mke wa pili “
Mwanamke huyo kWa Ghadhabu ya hali ya juu Akanyanyuka na kufoka.
“Msiwe mnaniita kwenye dili zenu ambazo Azieleweki mbwa nyie “
Eeeeeh mama mkwe amemletea Mtoto wake kisanga, Yaani mtu ana nguvu ya Kuwaita watu mbwa.
“We nawe kanipe mabegi yangu niondoke “
Mwanamke huyo akanifokea kwani Mimi ndio nikipeleka mabegi yake Ndani, kwa haraka nikaenda chumbani na kuchukua mabegi yake na kuja kumkabizi.
“Halafu mniite Tena muone, pusi wa blue nyie “
Kisha huyo akaondoka zake.
“Kwenda mwana kwenda uko,
Mtu Mwenyewe minyama njinja nginja kama una undugu na tembo “
😂🙌 Ila kumuelewa mama
Mkwe yangu ni kazi sana jamani, Yaani yeye ndio amemleta halafu Saa hizi anamsema utazani alikuwa ajamuona vile.
“Na wewe unashangaa Shangaa nini hapa toka “
Eeeh mama mkwe akaamishia hasira kwangu ata Sijui kosa langu nini lakini nimefokewa 😂🙌 Mbona kazi ipo .
“Mama usije ukarudia haya mambo Sawa, ne ni mtu mzima mama yangu na Ninajua nini nafanya, Mimi ni mtu mzima na Ninajua nini nataka”
Mama mkwe akaona kama Mtoto wake anamchanganya hivi, kWa hasira Akanyanyua Pochi yake na kuondoka pasi na kuaga maana eeeh mambo yamekuwa mambo.
******
Majila ya usiku, nilishindwa kulala kabisa, mwili wangu ulikuwa hot sana, Yaani hot kuliko kawaida maana Nina miezi mitatu Mimi na mume wangu Tunalala Kama mtu na dada yake vile.
“Babe, mume wangu, Abbas”
Nilimuita mume wangu majina yake yote apendayo lakini Wala akuniitika mwisho niliamua kumtikisa na kumfanya kuamka akiwa na hasira sana.
“Nini na wewe ? Kusumbuana usiku wote huu “
“Mume wangu nimekumisi sana, nashindwa kulala kabisa Naomba ata kimoja tu “
“Kuomba nini Roho yangu au ?? “
“Jamani Abbas ni Maneno gani hayo mume wangu, mimi ni mke wako lakini umu Ndani sasa hivi tunaishi Kama baba na Mtoto wake au dada na kaka yake “
“Zayana nimechoka sana Naomba nilale “
Aaah kWa upande wangu hali ilikuwa ni tete sana hivyo nikajikuta nikianza kulia na kulalamika.
“Sasa ndio mambo gani haya, umenioa lakini haki yangu utaki kunipa Unafikili me nitaishi vipi ? Abbas unajua kabisa siwezi kutoka nje ya ndoa yangu nakupenda sana”
Abbas Akanyanyuka kWa hasira kabisa na kunifokea.
“Zayana nitakuja kukuchapa mabao ya mwana ukome halafu uje kunichukia Sawa ? Hivi kuna Faida gani ya mimi na wewe kufanya hivyo, Una kazi ya kuchosha mwili wangu tu na hakuna faida ninayopata, sikiliza, unaweza ukatoka nje ya ndoa it’s okay kwa upande wangu, lakini siko tayali kujichosha kwako wewe “
Kisha Abbas akanishika mkono na moja kwa moja akanipeleka kwenye chumba cha wageni.
“Kuanzia Leo iki ndio chumba chako “
Eeeeeh hii ya Leo Kali jamani, Yaani nimeanza na kutolewa nje kabisa, Yaani Leo hii Mimi naambiwa nikalale kwenye chumba cha wageni kWa sababu tu sizai 😩 ila hizi ndoa zina mambo Mengi sana.
“Abbas uko serious ? “
Nilimuuliza mume wangu kWa utulivu wa hali ya juu.
“Nilichokisema nakimaanisha, Fanya maisha yako nifanye ya kwangu Zayana Sawa ? Nimekuchoka sana “
Nilibaki nikijililia tu na Abbas akatoka na kwenda chumbani ambapo tulikuwa tunalala mimi na yeye.
*******
Asubuhi na mapema niliamka na kuendelea na shughuli za usafi lakini pia kumuandalia mume wangu kifungua kinywa Kama ilivyo kawaida yetu.
Nikiwa bize napanga meza ya chakula, Abbas akatoka chumbani kwake akiwa ameshavaa mavazi yake ya kazini na akanipita Kama anioni.
“Mume wangu “
Nilimuita Abbas, akageuka na kuniangalia pasi na kuitika kWa sauti.
“Chai iko tayali mume Mbona kama ndio unaondoka hivyo ??”
“Sina shida na chai yako “
Alijibu Abbas na kuondoka na kuniacha nikimuangalia.
Majila
Ya usiku nilikaa sana nikisubili mume wangu ambaye uwa anawai sana kurudi lakini Leo hii mpaka Saa 6 usiku ajarudi lakini pia simu Apokei kabisa.
Baada ya muda niliweza kusikia honi ya gari ya mume wangu haraka nikaenda kumfungulia, nilishtuka sana baada ya kumuona Abbas akiwa amelewa sana na Abbas hakuwai kunywa pombe.
NAKUJA MY ZANGU.
ALINIACHA KWASABABU SIZAI
SEHEMU YA: 03
MTUNZI: PATRIGIA DAMAS
www.tupohapa.com
SONGA NAYO….
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Haraka nikamuwai mume wangu ambaye aalitaka kuanguka lakini nikaishiwa nguvu baada ya kumuona mwanamke mwingine akishuka kwenye gari ya mume Wangu, kwa kumuangalia tu mwanamke huyo niligundua Kuwa ni wale wa dada wa kusimama barabarani hivi.
“Sorry Nani wenzangu ??”
Nilimuuliza mwanamke huyo, na wakati huo Abbas alikuwa tayali yupo chini 😂😂 yaania meshaanguka pombe sio chai.
Mwanamke huyo kwa dharau akanipandisha naa kunishusha kisha akanijibu.
“Nipo kazini dada usiiingilie kazi yangu, wewe Kama ni house girl Mimi Nipo kwaajili ya jumpa raha “
Eeeeeh 🥹 mume wangu Amefikia uku sasa, Yaani Anapata na nguvu ya kununua mwanamke na kumleta Ndani uwiiiiih.
“Poin of correction dada Mimi mke wake na sio dada wa kazi, so ningekuomba utoke Nyumbani kwangu “
“Utajua mwenyew uwe, mke uwe Nani Nani me ninachojali Nipo kazini, na kuhusu kuondoka sahau , Yaani siwezi kuondoka bila kulipwa”
“Mlikubaliana kiasi gani ??”
Nilimuuliza nikiwa n hasira sana.
“50k usiku kucha “
Alijibu msichana huyo kisha nikampapasa mume wangu na kutoa kiasi cha elfu 50 na kumpatia msichana huyo.
“Mwanzo mwisho na mwanzo Leo kukanyaga kwenye hii Nyumba “
Nikamfokea msichana huyo ambaye hakuonesha Kujali ata kidogo, Yaani alikuwa bize na kujipepea na Pesa ambazo nilimpatia.
Baada ya muda msichana huyo akaondoka na kuniacha Mimi nikiangaika na mume wangu, Walahi Abbas alikuwa Mzigo sana, nilijitaidi na kumkokosa mpaka sebuleni, nilishindwa kabisa kumpeleka chumbani hivyo tukajikuta tukilala sebuleni sikuweza kumuacha mume wangu peke yake.
*******
Kwakuwa Mimi ni mtu ambaye nimeshazoe kulala mapema hivyo nilijikuta nikichelewa sana kuamka kwani usiku nilichelewa kulala, siku hiyo mume wangu ndio alikuwa mtu wa kwanza kuamka hivyo akaamka na kumuamsha.
“Imekuwaje nimepata sebuleni ??”
Mume wangu aliniuliza akiwa na hasira sana.
“Za asubuhi kwanza mume wangu ?”
Nilimsalimia.
“Sina shida na salamu yako, niambie imekuwa je nimelala sebuleni eeeh, hivi Zayana Una shida gani wewe eeeh, Yaani umeona kitikunizalia aitosho kWa sasa umeamua unilaze sebuleni si ndio ? Haya makini yako ndio yamekuwambia hivyo au ??”
“Abbas kama ni gubu ili la sasa
Hivi ni pro max mume wangu, hivi ulitegemea me nikubebe peke yangu nikupeleke chumbani kwako ? Ulitegemea Mimi peke yangu ningeweza kweli eeeh, kwanza hizi tabia za ulevi umeanza lini ? Abbas mume wangu unaweza AFYA yako lehani ujue “
Hapo kidogo ndio Kama akili Ikaanza kumla Sawa, polepole akainamisha sura yake chini na kuondoka pasi na kuzuungumza kitu.
Abbas akaingia chumbani na kujiandaa kisha akaondoka pasi na kunywa chai yangu Wala kuniaga.
Maisha ya Nyumba yangu yalibadilika sana, Sijui nisemeje lakini yalibadilika na Kuwa mabaya sana, Abbas akawa Yule mlevi wa kipindukia, Abbas akabadilika kabisa na kuanza kumpigia ikiwa hakuwai kunipiga uko nyuma.
Kiukweli mambo yalikuwa magumu sana, kWa upande wa familia ya kina Abbas hakuna mtu anataka kunisikiliza na ukiwauliza ni kwakuwa Mimi sizai.
Kwakuwa nilikuwa nikitaka kuinusuru ndoa yangu, nilifunga safari na kwenda Nyumbani kwetu ili niweze kupata masada.
Nilifika Nyumbani na kumkuta mama na baba yangu na hawa ndio watu ambayo nilikuwa nikiwaitaji sana, mama na baba yangu ni watu ambao wamedumu muda mrefu sana kwenye ndoa Yao hivyo niliamini Kuwa wao ndio watanisaidia kwenye kila kitu.
“Mama, baba, ndoa yangu imekuwa ni zaidi ya moto, kila siku tukio jipya, kila siku Abbas anarudia akiwa amelewa, uwezi amini mimi na Abbas kWa sasa tunalala vyumba viwili tufauti Kana kwamba ni watu ambao hatujuani “
Nilielezea uku nikilia kwani mambo yalikuwa sio mambo kWa upande wangu.
Baba yangu aliniangalia kwa muda kisha akaniuliza.
“Kabla ya kuja hapa ni sehemu gani nyingine ulienda kupata ushauri ??”
“Nimeanzia hapa baba Angu, kWa wakwe zangu kule najua siwezi kupata msaada kwani kWa sasa hawataki ata kunisikia, 🥹🥹 kWa sasa Sina masada mwingine zaidi yenu wazazi wangu”
“Hivi Zayana unajua Kama mume wako alikuwa hapa Jana ??”
Baba aliniuliza na kunifanya nishtuke sana.
“Alikuwa hapa ??”
“Unashangaa nini ? Mume wako alikuwa hapa Jana na ametuambia uchafu wako wote, kwakweli Zayana unatuvua nguo wazazi wako, Zayana unatukatisha tamaa wazazi wako, sisi hatukukulea hivyo Kwanini lakini eeeh, Kwanini unataka tuonekane sisi ni wajinga tumeshindwa kukufunza maadili ??”
Yoooooooh Abbas ameniweza kwakweli, Yaani ameshaniwai kabisa, makosa ni yake lakini Amewai kuja kujitilisha huruma kWa wazazi wangu.
Wazazi wangu walishindwa kabisa kunielewa na wote Wakamuamini Abbas na sio Mimi.
KWa unyonge wa hali ya juu, nikanyanyua kila kilichokuwa changu na kurudi Nyumbani kwangu, nilifika na kumkuta Abbas akiwa sebuleni Ana kunywa, Yaani sasa kokote pale anajelewea.
“Eeeh mapokezi yamekuwaje uko ??”
Abbas aliniuliza uku akicheka sana, lakini Nilijiuliza Abbas amejuaje kama mimi naenda Nyumbani.
“We need to talk Abbas”
“Hahaha uongee na Naani ? Zayana kitu usichokijua ni kwamba Mimi nakujua kuliko wewe unavyojijua, Naomba niweke iki kitu Sawa, ugomvi wangu Mimi na wewe utaishia umu umu Ndani, lakini ukipanga kuutoa nje Basi nitahakikisha Kuwa Jina lako kina chafu Ka before ujafanya kitu chochote kile”
“Kitu unachotakiwa kuelewa mume wangu ni kwamba, Mimi sijawai Kuwa na mawazo mabaya juu yetu, nilienda Nyumbani ili watusaidie kurudisha ndoa yetu kwenye mstari na sio kitu kingine “
“Nitokee hapa, mwanzo mwisho Leo kuongelea ndoa yetu na watu wa nje. Sasa jichanganye “
Abbas akanyanyuka na kuondoka kabisa pale Nyumbani.
Siku hiyo Abbas Alichelewa sana kurudi na alirudi akiwa na wanawake wawili ambao wamejazia sana nika…..
ITAENDELEA.
ALINIACHA KWASABABU SIZAI
SEHEMU YA: 04
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
www.tupohapa.com
SONGA NAYO….
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Nikasogea na Kuwauliza.
“Na nyie ni kina Naani ??”
Mmoja kati ya wanawake wale aliniangalia kWa Dharau sana na kWa sauti ya kejeli Ndani yake akazungumza.
“Oooooh kumbe wewe ndio mgumba mjaza Choo ??”
Daaaah nimeanza kutangazwa hadi nje ya Nyumba uko Walahi, hivi kweli nastahili haya jamani ? Ni kweli kusemwa Kama hivi nastahili Mimi 🥹 aaah Abbas anajua kunivua nguo, Yaani mume wangu amebadilika kuliko kawaida.
KWa uchungu na maumivu makali sana, nikatoka eneo ilo na kwenda kujifungia kwenye chumba cha wageni ambapo sasa hivi ndio kumekuwa chumbani kwangu.
Nilifika chumbani na kujikuta nikilia sana, sikuwai kufikilia Kuwa kuna siku moja ndoa yangu inawezekana ikawa ndioo sehemu kubwa ya maumivu yangu.
Sik huyo sikuweza kulala kabisa, nilibaki nikisikilizia Kelele za mahaba kati ya Abbas na Wanawake zake wawili aliokuja nao, Walahi kiatu ni changu lakini kwa sasa akijitoshi, Sijui Kama kimekuwa kikubwa au kidogo maana daaah ni more than pain.
Asubuhi nilishindwa ata kutoka nje nilibaki tu chumbani nikitafakari mwisho wa ndoa yangu ni nini, nilibaki nikilia na Mungu Nikimuuliza iki ni kitu gani, Nilimuuliza Mungu ni kweli haya ndio maisha ambayo umeyaandaa kwaajili yangu 🥹.
Nikiwa bize naendelea kulia na Mungu wangu, gafla mlango wangu ukuanza kugongwa kWa Fujo sana na Abbas ndio alikuwa kigonga, kWa utulivu nikasogea na kwenda kufungua mlango.
“Unalala mpaka sasa hivi Una raha gani ??”
Abbas aliniuliza kWa hasira sana. Kiukweli nilishindwa kabisa kujibu zaidi nilibaki nilimuangalia tu Abbas.
“Toa madela yako mawili na uwape wenzio wavae “
Alizungumza Abbas akitaka Mimi nichukue nguo zangu na Kuwapatia wanawake zake waweze kuvaa .
“Lakini abb….”
Kabla sijamaliza kauli yangu Abbas akanifokea.
“Nimesema toa nguo wape wenzio wavae, kisha uje kutuandalia kifungua kinywa Saa hizi “
Basi mwaya mume ndio ameshasema Mimi ni Nani Nipinge na ukizingatia Mimi bado Nipo chini yake.
Niliwapatia mavazi yangu wakavaa kisha nikawaandalia kifungua kinywa, baada ya hapo nikaoga na kumuaga mume wangu.
“Naenda sokoni kuongezea baadhi ya vitu vilivyoisha”
“Pesa inatosha ??”
Abbas aliniuliza.
“Ndio “
Yaani Abbas mapungufu yake ni sehemu nyingine tu lakini kwenye kuhudumia yuko vizuri sana na hata hayo mambo mengine ni kwakuwa tu anataka Mtoto na anakosa.
Nilifunga safari Moja kWa moja nikaenda hospital maana nilishindwa kabisa kuamini Kuwa Nina shida kwenye uzazi wangu, Nimekuwa Nilimwambia Abbas kuhusu kuja hospital lakini hajawai kabisa kukubali hivyo ni bora niangalie AFYA yangu Mwenyewe.
Basi nilifika hospital na kuonana na specialist wa wanawake na kumuelezea shida yangu mwisho, nikafanya vipimo vyote.
Nikiwa bize naendelea kusubili majibu, simu yangu ilikuwa ikiita sana na Abbas ndio alikuwa akipiga, haraka nikarudi kWa dokta na kumwambia.
“Naomba nikuachie Namba yangu tu kisha utanitumia majibu kWa simu maana Nina dharula”
Dokta Yule akanipatia business card yake Nami nikaondoka.
Nilifika Nyumbani nikakutana na gubu la Abbas ambaye alikuwa akitaka kuonekana mwanaume mbele ya wanawake zake.
“Nakupigia simu upokei maana yake nini ??”
Abbas aliniuliza uku akiminya mkono wangu.
“Jamani unaniumiza ujue Abbas, Kwanini unanifanyia hivi eeeh, simu nimeacha Ndani ningewezaje kupokea jamani “
Aaah siku hiyo nilipigwa sana mbele ya wanawake hao, Abbas hakuishia tu kunipiga na kundhalilisha akanidhalilisha maana alinifanyia mbele ya wanawake hao, Abbas hakujali Kuwa Mimi ni mke wake, Wala hakujali Kuwa pale kuna watu na ni sebuleni, alichodai ni haki yake ya ndoa na akatimiza haja zake mbele ya watu wale.
Baada ya kipigo na kuzalilishwa, nikalazimika kuingia jikoni nakuwaandalia chakula cha mchana.
Baada ya chakula cha mchana wanawake hao wakavaa mavazi Yao na kuondoka, lakini walionekana kuumizwa sana na matendo ya mume wangu.
Majila ya jioni, niliweza kupokea majibu yangu ya hospital na nilikuwa Sawa kabisa Yaani Mimi nilikuwa Sina shida yoyote ile na hapo nikaona ni bora pia mume wangu akaenda kupima ili kujua shida ni nini.
“Abbas Naomba tuongee”
“Wewe Tena ? Hivi Zayana ujui ata kusoma alama za nyakati wewe mwanamke? Hivi uwezi kuona Kuwa Sina ata hamu ya kukutazama ??”
“Unaweza ukafunga macho yako ili usiweze kunitazama Abbas, kwanza kabisa nachukizwa sana na hizi tabia zako ulizozianzisha ? Hivi Abbas ujionei huruma wewe ? Eeeh Mimi pia mkeo unionei huruma ? Unataka tufe kwa magonjwa eti ?”
“Zayana Zayana chunga mdomo wako Sawa ? Tena Kaa kimya wewe kasuku usiyekuwa na Faida, katika kitu natujia kwenye maisha yangu Basi ni kukuoa wewe, Yaani najuta zaidi ya kujuta 🥹 unajua nilibabaika na huu urembo wako lakini kumbe ni urembo wa kasha tu na thamani yako ni ya smart kitochi “
Uwiiiiiih sio kWa haya matusi jamani khaaah, Nashindwa kuelewa hii ni tabia ya Abbas alikuwa akiificha na sasa hivi ameamua kunyoosha makucha au ni kitu gani 🥹.
“Abbas kama unanichukia kiasi iko ni bora ukanipatia taraka tu ili kila mtu akaendele na maisha yake”
“Uko serious au ? You know what Zayana, Ninauwezo wa kukupatia taraka ata muda huu, Tena sio taraka yako tu Nakupa mpaka taraka ya ukoo wako wote, Kiukweli sina hisia zozote na wewe”
“Nipatie taraka yangu sasa “
Nilijibu uku nikilia kWa uchungu mno maana Maneno ya Abbas yalikuwa makali sana kWa upande wangu.
“Siku ambayo nitakupatia taraka kale kazee kako Sijui baba yako Nina Uhakika katakufa na presha, na Kama unataka Kuwai kumtanguliza uko mbele me niko tayali kukupa taraka “
Nilijikuta nikilia kwa uchungu sana Walahi, Yaani Abbas anatumia hali ya baba yangu kunitishia 🥹.
Abbas Akanyanyuka zake na kuondoka Kana kwamba hakuwa akizungumza na mtu.
*******
Siku moja Nilihisi maumivu makali sana ya tumbo, haraka nikajiandaa na kuwai kwenda hospital na nikakutana na dokta Yule Yule, nilimuelezea shida yangu na akanipima na nikaonekana Kuwa Nina UTI Kali sana, daaaah hii nimeletewa na mume wangu kabisa Tena ni siku ile ambayo alilala na wanawake zake halafu akaja kulala na Mimi.
“Zayana ni Kama hauko sawa shida nini ??”
Daktari Joel aliniuliza.
Kwakuwa moyo wangu haukuwa Sawa, nilijikuta nikaangua kilio cha hali ya juu, mwisho nikamsimulia dokta Joel Kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yangu.
“Zayana ni vizuri sana kutunza ndoa yako, lakini sizani Kama ni Sawa kuendelea kubaki kwenye toxic marriage Kama hiyo, tazama unahatarisha maisha yako ? Tazama AFYA yako inayumba, me Nafikili ungeachana na hiyo ndoa huyo sio mume, ni Sawa utazalilika kwenye familia na ndugu na jamaa na marafiki lakini ni bora kuliko kurudishwa Nyumbani kwenu ukiwa kwenye jeneza “
Walahi me nampenda sana Abbas wangu nilijikuta nikiona kama dokta Joel ana changanya akili yangu tu kwa hasira pasi na kuchukua dawa nikaondoka zangu.
Nilirudi Nyumbani na maisha yaliendelea Kuzidi Kuwa magumu Walahi, nilikonda kuliko kawaida, 🥹 nilijaribu kuomba ushauri kWa watu wangu kadhaa na kila mtu akajishauri kuachana na Abbas, upande wa familia yangu ndio kabisa nilikosa utetezi kwani baba aliona Kuwa Mimi ndio mkosefu.
KWa upande wa dokta Joel, aliendelea kujenga ukaribu na Mimi uku akinishauri mammbo Mengi sana, kuna muda ulifika niliona dokta Joel ndio kama Rafiki yanngu hivi Yaani siku ikipita pasi na kuzungumza nae Basi nachanganyikiwa.
Jamani dokta Joel sio Kijana ooooh ni mtu Kama wa miaka 50 na kidogo Sema alikuwa na muonekano mzuri sana na ni mtu wa gym.
Siku moja Majila ya usiku nikiwa chumbani kwangu nachati na dokta Joel gafla nikasikia sauti za watu wakiimba sebuleni, Walahi niliogopa sana maana nakumbuka kWa wakati huo Nyumbani nilikuwa peke yangu.
JE NI KINA NANI WANAIMBA KWA USIKU HUO ? NA NDANI WALIINGIAJE ?? TUKUTANE SEHEMU IJAYO…..
ALINIACHA KWASABABU SIZAI
SEHEMU YA: 05
MTUNZI: PATRIGIA DAMAS
www.tupohapa.com
SONGA NAYO….
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Kwa wasiwasi nikasimama na kusogelea mlango wangu na hapo nikaweza kusikia vizuri nyimbo Yao ambayo walikuwa wakiimba hivi.
“Walisema aolewi Mbona kaolewa, walisema aolewi Mbona kaolewa. Walisema ampati Mbona kampata walisema ampati Mbona kampta “
Eeeh hapo nilijua kabisa drama Mpya imeanza Nyumbani kwangu, haraka nikatoka nje na kukutana na ndugu wa Abbas na Abbas Mwenyewe na watu wengine ambao sikuwa nikiwafahamu.
Abbas wangu alikuwa vizuri kabisa kwenye mavazi ya harusi, Yaani kiufupi Abbas wangu ameoa na ameleta mwanamke Nyumbani pasi na kunishirikisha kitu chochote kile, Yaani hapa ndio naona Kuwa sipendwi ata kidogo , Yaani Abbas anipendi kabisa kabisa.
Nilibaki nikiwaangalia tu uku machozi yakinitoka, lakini muda mwingine nilijiambia bora ameoa anaweza akatulia na kuachana na tabia za kiuni ambazo amezianzisha.
Mama mkwe akanisogelea nilipokuwa nimesimama na kuniambia..
“Kaandae chumba cha mke mwenzio vizuri kabisa Leo ni siku ya kutafuta mjukuu”
Ila huyu mama jamani 😂🙌 khaaah hivi wakwe wote ndio wako hivi au huyu wangu tu ako na shida kidogo.
KWa unyonge nikashika njia na kwenda kwenye chumba ambacho nilikuwa Nikitumia na mume wangu na kuanza kuweka vizuri, nilihakikisha Kuwa kinaonekana vizuri kisha nikatoka nje na kwenda kumwambia mama mkwe Kuwa chumba kiko tayali.
Wageni waaalikwa na watu wengine wakaondoka wakabaki Wifi zangu na mkwe.
“Umeona chombo ya kaka yangu ? Mtoto mbichiiiiiiiih sio wewe ajuza, ila Sijui kaka yangu aliona nini kwako Walahi “
Alizungumza WiFi yangu Mdogo ambaye ndio kwanza yupo kidato cha Sita Yaani ata ubwaubwa wa shingo bado haujamtoka Saa hizi ananinyooshea kidomodomo chake.
Nilibaki nikiwangalia tu Wanavyojinanga na wakati huo nilikuwa nikimuelezea dokta hali halisi ya Nyumbani kwangu, dokta Joel Aliishia kunipa pole tu maana ni ameshanishauri sana tu lakini sielewi.
*******
Siku ziliendelea kwenda uku maisha yangu yakizidi kudolola, lakini kWa upande wa mke mwenzangu Walahi alijua kula raha, yaani huyu Binti alipatiwa kila Alichokuwa akiitaji, halafu ni Kama Alijazwa sumu dhidi yangu maana daaah.
“Zayana “
Aliniita msichana huyo ambaye kWa haraka haraka nilikuwa nampita Kama miaka Saba hivi maana hakupishana sana na Wifi yangu wa mwisho.
“Nambie Amina “
Nilimjibu kWa utulivu kabisa uku nikiendelea kupika kwani tulikuwa jikoni.
“Hivi Kwanini utaki kuzaa ? Ndio unaogopa kuzeeka au ??”
Nilimgeukia na kumuangalia sana mwisho nikamuuliza.
“Ni Nani amekuambia Maneno Kama hayo ? “
“Shida ya uswahili sasa, Yaani unaulizwa Swali badala ya kujibu swali na wewe unaweka swali, Sema ni Sawa Ila nakuambiaje utamkosa mume huyu ooooh, kwanza hakuna kitu kinaniuma sana kama kuonekana Kuwa Nina mke mwenza”
“Amına we ni Binti Mdogo sana na ndoa yako bado ni changa sana, Nafikili itapendeza sana kama Utakuwa bize na ndoa yako na kumuomba Mungu akutunzie ndoa yako, kuhusu Mimi Nafikili ni Mimi na Mungu wangu kwa sasa “
“Mmmmmh unavyoongea Kama sio wewe unayetoa mimba asubuhi mchana na usiku 😂🙌 Ila shoga Angu weeeh noma kama ulikuwa utaki kuzaa Kwanini uliolewa sasa”
Eeeh huyu Mtoto jamani , Yaani anazungumza utazani Ana Uhakika na mambo Anayoongea, angejua ni kiasi gani naitamani hiyo mimba Wala asingeniambia mambo Kama haya 🥹.
“Kila la kheri Amina “
Nilimwambia na kuendelea na kazi yangu maana kuendelea kumsikiliza huyu Binti ni kujiumiza mimi Mwenyewe.
Majila ya usiku Kama kawaida Abbas akarudi, lakini siku hizi Bwana Abbas ametulia sana Yaani mavituko yake yote ameacha na amekuwa Mtulivu sana.
“Mke wangu, laaaziziiiii”
Abbas alimuita Amina kWa bashasha sana mimi nikabaki nikishangaa tu maana umu Ndani kWa sasa mimi ni Zayana tu sikumbuki ata Mara ya mwisho kuitwa mke ilikuwa ni lini.
Kwa Furaha wawili hawa wakakumbatiana na kabusu Kama yote,
Mpenzi Mtazamaji nikabaki nikitazama kila tukio 😂 ni huzuni kwakweli.
“Zayana niletee maji ya kunywa yasiwe bardii sana “
Abbas aliniagiza lakini Amina akadakia.
“Babe ni Mimi ndio natakiwa kukuhudumia, dada Zayana ameshaakuhudumia sana
Ni muda wake kupumzika”
Yaani Amina utazani ni Mwema kweli kumbe ni kishetani kenye miguu mmoja.
Tukiwa kwenye meza ya chakula,
Nilikuwa bize sana na chakula changu uku Abbas na Amina wakilishana tu, Yaani walifanya kila kitu kuhakikisha Kuwa Naumia moyo.
Amina ndio alikuwa mtu wa kwanza kumaliza kula
Hivyo akanyanyuka na kuanza kutoa vitu lakini Abbas akamzuia.
“Minah babe, Kaandae uwanja wetu vizuri kabisa tuje kuongezea miguu ya Mtoto huyu pata potea atasafisha vyombo”
Khaaaaah Leo hii Mimi ni wa kuitwa pata potea kweli 🥹 hivi ni kitu gani nimewakosea hawa watu, wait kwanza nimesikia kuongezea mguu wa Mtoto kwamba ni tayali amina Ana mimba au ? Na Kama kweli anayo Mbona imekuwa haraka sana au mimi Nina shida kweli halafu dokta amenificha tu, kWa shauku nikauliza.
“Kwani Amina ni mjamzito??”
Abbas akaniangalia kWa dharau kisha akazungumza.
“Ooooh kumbe sikukuambia ? Yaaah Amina ni mjamzito, sio Kama wewe years uko hapa hakuna kitu umeleta mwenzio mwezi tu kitu kimejibu “
KWa sauti ya utulivu Amina akadakia.
“Mume wangu sio Maneno mazuri kwa dada Zayana jamani, ata hivyo ni Mungu ndio amepanga iwe hivyo, inaweza ikawa Mungu amenitumia Mimi kufungua njia tu then zamu ya Zayana iko Karibu”
“Mke wangu Kaandae nilichokuambia huyu unayemetetea ata sio mtu Mwema “
Basi Amina akaondoka na kuniacha Mimi na Abbas.
“Hongera Karibu unakuwa baba “
Nilimpongeza Abbas uku Nikinyanyuka na vyombo vyangu.
“Hongera Sijui nini nini, kajifungie chumbani kwako ulie uko mwanamke umekosa Bahati wewe “
Jamani sasa hapo Mimi kosa langu ni nini jamani kumsifia au ?.
********
Siku iliyofuata, Kama kawaida nikawa wa kwanza Kuamka na kufanya shughuli zote za Nyumbani, kWa upande wa Abbas na Amina walikuwa wakipeana cha asubuhi na sauti za juu kabisa ili tu Niweze kusikia, Ila ni Kama ata awainjoy maana ni kila kitu wanafanya kwaajili ya kunirusha roho Mimi 😂.
Baada ya muda abbas akatoka nje akiwa Ameshajiandaa kwaajili ya kwenda kazini, akiwa anataka kuondoka akaniaambia.
“Amina amepumzika , akiamka utamuandalia chakula ambacho atakitaka yeye “
Kisha Abbas akaondoka , hakutaka kujua naendeleaje au nimeamkaje.
Siku hiyo Bwana, Nyumbani nikamuulika Rafiki wa mume wangu huyu Bwana nakumbuka yeye ndio alikuja na mshenga pale Nyumbani kwetu, Muda ambao shemeji yangu alikuja, Amina hakuwepo Nyumbani hivyo tukapata muda mzuri wa kuzungumza.
“Unajua shemeji, haya mambo nilisimuliwa na Yule mama zai,
Walahi nilishindwa kuamini kabisa, nikabaki nikchunguza Mwenyewe, nikaanza kuamini baada ya Abbas kuoa mke wa pili pasi na kutushirikisha sisi Rafiki zake, lakini pia Leo wewe ndio unanifungua masikio zaidi Kiukweli Abbas amebadilika mno”
Alizungumza shemeji yangu baada ya Mimi kumaliza kumuelezea hali halisi ya ndoa yangu .
“Kiukweli hii Nyumba imekuwa Inawaka moto muda wote Sina amani ata kidogo, me naitaji amani Naomba nisaidie kuongea na mume wangu, weee ndio Msaada wangu wa mwisho “
Basi tukazungumza Mengi snaa mwisho tukapata chakula na shemeji yangu akaaga na kutaka kuondoka, ile anatoka tu nje akapishana na Amina ambaye ndio alikuwa anarudi, walitazamana kwa muda kisha Amina akaingia Ndani.
“Wewe huyu ndio mke wa Abbas ??”
Shemeji yangu aliniuliza baada ya sote kutoka nje ya geti.
“Ndio, ndio Amina huyo”
“Aaaah Broh anapigwa huyu 😂🙌 Yaani huyu wakati NAKUJA uku nimemuacha magetoni kwa Yule mshikaji wangu ambaye anaanza mambo ya u producer Tena kanitambulisha Kuwa ni mtu wake”
Eeeeh nika…..
ITAENDELEA….
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote