Amina alimkuta kwa mara ya kwanza Feisal, kijana aliyeonekana kama kichaa kutokana na muonekano wake mchafu, bila kujua kuwa ni bilionea mwenye mtaa wake. Walipokutana tena kwenye mgahawa wa mama yake mkubwa, Feisal alivutiwa na supu aliyoandaa Amina na akaanza kumuita "Amina Mama," jina lililomfuata kila mahali. Alimpa kazi kama mpishi wake wa kasri na mapenzi yakaanza kuchipua hadi kufikia usiku mmoja wa kushangaza ambapo Amina aligundua kuwa Feisal alikuwa bado bikra—jambo lililomalizika kwa tukio la kuchekesha na la kusisimua. Hadithi hii ni ya kuchekesha, ya kimapenzi, na yenye mafundisho.
SIMULIZI: AMINA MAMA
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 01
ENDELEA........
"Ananibakaaaa.... jamani msaada nabakwa mie bikira yangu inaenda hivyooo jamani msaada nabakwa!" Haka kasauti kalinikata stimu ya kuendelea kuzagamua Sponsa langu lililo lala kama gogo kisa na maana huwa ananipa pesa.
Unajua sisi hapa ndio Askari, Wanasheria na Hakimu wa mtaa wa Igogo B. Kama nitasema nilale kweli basi mtu anayeomba msaada atabakwa kweli, nadhani mnajua namna Wabakaji wanavyo kuwaga na uchu uliopitliza.
Nilichukua kimtandio changu chepesi, sikuwa nimevaa chochote kwa ndani, sinaga aibu mie.
Niliinama uvunguni ni kabeba sululu, nilimuona Sponsa wangu akikodoa macho.
"Unaenda wapi na hicho kimtandio, kwani hujioni kama umbile lake lipo hadharani!" Alifoka.
"Mwanaume huna aibu eti eeh, huko nje kuna mtu anaomba msaada unawezaje ku relax namna hiyo!... usiniambie wewe ndio mdhamini wa hao Vibaka huko nje, acha kuniuliza maswali ya ajabu tena....naenda kutoa msaada!"
"Mimi umeniita mdhamini wa vibaka!" Sponsa wangu aliongea kwa hasira.
Sikutaka kuhangaika naye tayari Washikaji waliniita tukatoe msaada.
Nilitoka nje, wao pia walikuwa wamevaa tu boksa....hakuna aliyekuwa na muda wa kumchungulia mtu mwingine.
Kisauti cha bi Dada kilituongoza mpaka eneo la tukio.
Watu kishazi walikuwa wamejaa, niliwasihi wazime tochi zao kwa sababu kuna watu walikuwa uchi kabisa.
"Dada Amina, naomba unisaidie katika hili. Huyu mwanamke nimempa afu tano yangu kwa makubaliano ya kula mzigo, na yeye ndio kapendekeza hii site. Tumefika hapa ananigeuka kweli hii ni haki" Mshikaji anaye tuhumiwa aliongea.
"Eeenhe na wewe mrembo ongea tukusikie kabla hatujaamua tunaua au tunasamehe" Niliongea.
"Ni kweli kanipa hiyo afu tano kwa makubaliano ya kula mzigo, lakini hakuniambia kama umbile lake ni kubwa namna hiyo.... Dada Amina kitu kimepinda mie ni bikira sitaweza kumudu, anipe siku tatu tu nitafute afu tano yake" Mrembo aliongea huku akilia.
Nilimchungulia Mkaka anaye tuhumiwa, kweli umbile lake lilikuwa linatisha.
"Oyaaa sikilizeni nyie waji.....nga, mmetutoa kwenye starehe zetu watu tulikuwa tunakula na kuliwa. Tumefanya kama uungwana tu kuja kuwasaidi. Sikiliza braza fanya kuweka kichwa tu. Endapo huyu mtu atapiga kelele tena za kuomba msaada siye tutakuja kuupunguza huo mzigo au siyo washikaji" Niliuliza.
"Upo sahihi Dada Amina" Wana waliitikia.
Tuliwaacha waendelee kubakana kwa sharti la kuingiza kichwa.
Nilirudi kumuangalia Sponsa wangu, jamaa hili liliondoka tayari.
Nilichungulia kwenye droo nione kama kaniachia pesa, nilisikia hasira baada ya kukutana na pakiti la condom.
Nilijitupa kitandani ni kalala, nilikuwa nimechoka sana.
Kulivyo pambazuka asubuhi niliingia mtaani kabla ya kuoga kwanza.
Nilihitaji kununua mafuta ya usoni, mwenzenu huwa napaka zangu baby care tu.
Hii ndio inaniweka mjini ukiniona unaweza kusema ni katoto fulani hivi.
Nilifika dukani kwa Mangi ni kachukua mzigo, siku ya leo sikuwa na hofu yoyote ile kwa sababu sikuwa naenda kukopa nilikuwa naenda kulipa.
Baada ya kumalizwa kuhudumiwa, nilianza safari ya kurudi nyumbani.
Bahati mbaya niliparamiana na Kaka mmoja hivi aliyeonekana kama kichaa kutokana na namna alivyo vaa.
Mafuta yangu yalienda kule yakakanyagwa na gari lililokuwa kwenye mwendo. Niliyashuhudia yakipasuka, nilimtazama huyo mkaka nione kama ana roho ya utu....nilitaka nione kama hata atanipa pole kwa kudondoka cha ajabu aliendelea na safari yake.
"Weee braza njoo unisaidie kunyanyuka" Nilipaza sauti.
Duh! Mwanaume huyu aliendelea na safari yake....niliokota kipande cha ndizi kilichokuwa chini, nilikirusha kikagonga mgongo wake.
Alifunga breki, alinigeukia kwa macho makubwa.
Alinirudia kwa kasi ya ajabu, mweee Mnyakyusa mie nilipata presha.......
ITAENDELEA........
SIMULIZI: AMINA MAMA
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 02
ENDELEA......
Kila ni kikukumbu ka Mimi ni semaji la mtaa wa Igogo B nilikaza macho.
"Kwanini umenichafua shati langu ...." Mwanaume huyu aliuliza huku akipambana kujichungulia mgongoni.
"Sababu yako wewe mafuta yangu yamekanyagwa na gari....kuwa mwema kwa kunirudishia 1000 langu nataka kwenda kuoga" Niliongea.
Nilishangaa tu Mwanaume huyu akinisogelea taratibu. Sikutaka kukimbia nilitaka kuona ni kitu gani atafanya.
Wacha nicheke kwanza, sijui ni kichaa au nini alinitishia kisu.
"Acha kuniletea usumbufu wa akili asubuhi hii, nitakutoboa visu ufe kabla ya siku zako mjinga wewe" Mwanaume huyu aliongea kisha akaondoka.
Nilitaka kumfuata kwa nyuma lakini nilisita, mtaa wetu una vichaa wengi sikuwa tayari kufa kisa buku.. kwa kuwa sikuwa na hela nyingine nilirudi zangu nyumbani kuoga.
Sikupaka chochote usoni, ile nataka kukaa kwenye TV Mamkubwa wangu alinipigia simu.
"Njoo unisaidie mwanangu nalemewa na kazi wasaidizi wangu wote wamefiwa....nina uhakika wamenichoka" Mamkubwa aliongea kwa kubembeleza.
Kanilea huyu kama nitampuuzia kuna hatari ya kulaaniwa.Nilivaa kijora changu kisha nikasepa.
Mamkubwa hakuwa amefanya chochote, kwa kuwa si mwepesi katika swala zima la upishi, nilimuacha afanye usafi kisha Mimi ni kakaa jikoni kuandaa chai, supu pamoja na vitafunwa vingine.
"Upishi wako ni mzuri sana, nitawasikiliza Wateja wee endelea kupika tu" Mamkubwa aliniambia.
Niliachia tabasamu nikijua sitapewa hata mia ni bahili sana kwenye swala zima la pesa. Nikishakula tu basi yanakuwa ni malipo tosha.
"Wewe ndio umepika hii supu!" Sauti ya Mwanaume iliyojaa hasira ilipenya mpaka jikoni nilikokuwa.
Aunt yangu si muongeaji sana kama nitazubaa anawezwa kuwekwa makofi kabisa....nilitembea kwa haraka mpaka sehemu walipokuwa Wateja.
Nilishangaa baada ya kumuona yule jamaa aliyenitishia kisu muda mchache uliopita. Huenda hili jitu lina kichaa, kwa namna macho yake yalivyokuwa na ukali unaweza teteleka.
"Mimi ndio nimekupa supu kwani kuna nini" Niliuliza nikiwa najiamini, Amina mie siye mtu wa kuonesha uoga mbele za watu. Mara nyingi hofu yangu huwa inajificha ndani kwa ndani.
"Umepika vizuri sana, nitaagiza bodyguard wangu akuletee zawadi. Unastahili kufanya kazi kwenye hoteli kubwa. Ahsante sana nimefurahia breakfast...." Mwanaume huyu naye mchukulia kama kichaa aliongea.
Nilijikuta nikicheka kimtindo hasa alipo zungumzia kuhusu bodyguard, ni kama alikuwa anajikweza hivi....kwangu mie nilimchukulia poa sana.
"Nitashukuru kwa zawadi, karibu sana kwenye mgahawa wetu" Niliongea.
Mwanaume huyu nisiye mfahamu jina alilipia bill kisha akaondoka.
"Inaonekana unakutana na vichaa wengi sana kila siku pole...." Nilimuambia Mamkubwa kisha nikaenda kuandaa chakula cha mchana.
Nikiwa bize na kata kata nyama, Mamkubwa alinifuata .
"Twende ukapokee zawadi yako....,najua huwezi kuamini lakini huyo jamaa ni CEO katika hotel ya Burj Al" Mamkubwa aliongea
Sikutaka kuamini maneno yake, nilihitaji kuwaona kwanza waleta zawadi.
Nilitembea kwa haraka kwenda nje........
ITAENDELEA........
SIMULIZI: AMINA MAMA
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 03
ENDELEA.......
Nilikodoa macho kwa namna bodyguard na Mfanyakazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Secretary Lui walivyokuwa wamependeza.
Nilipatiwa kiboksi kidogo, nilikichukua kwa pupa kwa sababu nilikuwa na shauku ya kujua kina nini.
Mate yalinidondoka baada ya kukutana na saa nzuri sana.
"Imetengenezwa kwa dhahabu tupu.... ahsante kwa kumfurahisha CEO wetu. Tutafurahi kama utakuja kuomba kazi katika hoteli yetu" Secretary Lui.
"Sikuwahi kufikiria kama upishi wangu unaweza kuleta changamoto chanya kwenye akili za watu. Ahsanteni kwa zawadi nitalifikiria hili kwa upana zaidi" Niliongea.
Watu hawa wanaonekana kuwa na haraka sana, waliondoka.
Mamkubwa alikuja kushangaa zawadi niliyopatiwa.
"Ni supu tu umepika umepatiwa saa ya dhahabu vipi kama ukimshika kidevu chake si utapatiwa gari la dhahabu tupu" Mamkubwa aliongea, nilijikuta ni kicheka kuna namna akili yake inakuwaga mbovu kabisa.
"Una uhakika huyo jamaa akili zake zipo sawa?...ujue alinishikia kisu asubuhi kweupe".
"Kuwa CEO wa hoteli kubwa kama Burj Al si mchezo. Huenda kuna mengi yanaendelea kichwani mwake. Mara ya kwanza kukutana naye nilihisi ni muokota makopo kuna namna anakuwa hovyo sana si rahisi kumuita Boss".
"Sasa kwanini anakuja kula kwenye mgahawa kama huu, nina uhakika vyakula vinavyo pikwa kwenye hoteli yake vina ubora mkubwa kuliko hata hivi vya kwenye sufuria zilizotoboka".
"Amina weee japo sijasomea mapishi lakini kitu pekee anacho angalia mlaji wa aina yoyote yule ni ladha....".
"Ladha?....".
"Ndiyo, kuna namna moyo wangu unaniambia huu ndio wakati wako wa kufanikiwa" Mamkubwa aliongea kisha akaingia ndani, sikuelewa maana ya maneno yake.
Kazi ya mgahawa inachosha hatari, Mamkubwa alifunga mgahawa wake saa nne kamili usiku.
Nilifika nyumbani nikiwa nimechoka sana, sikuwa na ratiba ya kuoga nililala hivyo hivyo.
Simu yangu ilianza kuita, niliichungulia kwa jicho moja. Ilikuwa ni namba mpya sikuwa tayari kuanza kujieleza.
Mpigaji alionekana kuwa mkorofi sana, niliamua kuizima simu kisha ni kalala.
Kulivyo pambazuka asubuhi niliitwa kwenda kuamua ndoa ya jirani yangu.....kuna namna naaminika sana katika mtaa wa Igogo B, kuna muda najionaga kama hakimu hivi. Hata bila kunawa uso wenye kesi walionekana kunivumilia tu.
Nilitumia masaa 4 kutatua kesi ya Wanandoa, niliachia tabasamu baada ya kuona nimeeleweka.
Nilirudi nyumbani kwangu nikiwa na njaa, hakuna kesi ngumu kama kumfundisha Mwanaume kuandaa mke wake kabla ya tendo la ndoa.
Niliogopa baada ya kumuona Secretary Lui pamoja na bodyguard wa CEO wa hotel ya Burj Al.
"Nimekupigia sana simu usiku wa jana kwanini hukupokea" Secretary Lui aliongea.
"Nilikuwa nimechoka sana sikusikia muito wa simu, kwanini mko hapa" Niliuliza.
"Boss wetu anahitaji kupata breakfast nzuri kama ya jana naomba twende nyumbani kwake ukamuandalie, siku ya leo anaingia kazini mchana naomba tuwahi" Secretary Lui aliongea.
Nilijikuta ni kikodoa macho kwa sababu watu hawa walikuwa kama wananiamrisha hivi na si kuniomba.
Nilishtukia tu na bebelewa juu juu na hili jitu linalojiita bodyguard Spark.
Nilitupiwa kwenye gari kisha safari ikaanza.
Dakika 25 hazikupita tulifika katika nyumba ya CEO wa Burj Al hoteli.
Nyumba yake ilikuwa na hadhi ya kasiri, nilipogeuka mkono wangu wa kushoto niliona kibao kimeandikwa "Mtaa wa Feisal" kuna watu wanapesa hadi mitaa inaitwa majina yao.
Nilikaza moyo wangu, tukaingia kwa pamoja....moyo wangu ulilipuka baada ya kuona simba, twiga, swala na chui wakiwa wamefungiwa katika mabanda tofauti.
Sikuelewa hii ni nyumba au sehemu ya utalii.
Mkojo kidogo ulipita kama masihala hivi baada ya Simba kuunguruma.
"Sura yako ni ngeni machoni kwake ndio maana kaunguruma" Bodyguard Spark aliongea.
"Tusi likanitoka kimya kimya !" Nilijisemea ndani ya moyo wangu.
Ile napiga hatua, nilishtukia tu mpira umenigonga kichwani.
Niliangalia mbele nimuone mtu aliyenifanyia hivi, nilikutana macho na CEO wa hoteli ya Burj Al.
Hakuonesha kujali, jamaa hili lina kiburi na eti nimeletwa hapa kuandaa breakfast.
Nikiwa bado na hasira nilishtukia na pondwa na ndizi mgongoni, niligeuka nyuma kwa haraka nione mtu anayenifanyia hivi.
Nilishangaa baada ya kukutana na sokwe tena likinizomea.
"Hahahaaaahaha!" Feisal alicheka alionekana kufurahi
Nilishikwa na hasira niliokota ndizi iliyokuwa chini nikairusha ikagonga paji la uso wake.
ITAENDELEA......
SIMULIZI: AMINA MAMA
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 04
ENDELEA......
Bodyguard Spark alitaka kunipiga teke kwa kumponda na ndizi Boss wake.
"Usisahau kama yuko hapa kuandaa breakfast ya Feisal, ukimvuruga utamlisha makalio yako" Secretary Lui aliongea kwa sauti ya chini.
Bodyguard Spark ndio kupata akili alichukua mpira akamrushia Feisal, walianza kucheza kisha kisha Mimi na Secretary Lui tuliingia ndani.
Aisee nilijikuta ni kikodoa macho, kila sehemu niliyotazama ilikuwa ni nzuri sana.
"Karibu Madame, hili ndio jiko kuwa huru..." Secretary Lui aliongea.
"Siwezi kuwa huru ni kama nahisi kila kitu hapa kinaniangalia.... naomba unisimamie mpaka nitakapo maliza kupika" Niliongea.
"Usiwe na shaka, usisahau kama utalipwa hivyo pika kwa ustadi wa hali ya juu" Secretary Lui aliongea.
Baada ya kusikia malipo nilizima kabisa simu yangu ni kaanza kupika.
Nikiwa napika huwa napenda kumfikiria sana Sultana wa kwenye Master of snacks 🥙 namna ya upishi wake huwa ni wa kipekee sana hata kama huna hamu ya kula ni lazima ule.
Secretary Lui alikuwa bega kwa bega na Mimi mpaka nilipomaliza, inaonekana wanamjali sana Boss wao.
Niliweka supu pamoja na chapati mezani, Feisal (Boss mwenyewe) alikaa akaanza kula.
Mie tena nilikaa zangu kwenye kiti nikiwa nasubiria amalize kula nipatiwe malipo yangu.
"Bodyguard Sparkkkkkk!" Feisal aliita kwa sauti ya juu, nilijikuta nikiogopa ndani ya moyo wangu japo Mimi si mtu wa kushtuka ila hili lisauti lilinishtua.
"Yes CEO...." Spark aliongea baada ya kuja kama mshale.
"Nimefurahishwa na hii breakfast....hakika nimefurahi sana" Fiesal aliongea.
Ee bhana ee kwanini asiniambie hizi shukurani Mimi anamuambia Spark, nilijikuta nikicheka ndani ya moyo wangu.
"Kwahiyo tunampa zawadi gani...." Spark alijiongelesha huku akijichekesha.
"Kesho nina kikao na Wapishi wote katika hoteli yangu....tutamfanya kuwa Msemaji mkuu, pia nitampatia milioni 75 kwa kunifurahisha" Feisal aliongea.
Nilijikuta nikishtuka niliposikia milioni 75, nilitaka nimtajie akaunti namba yangu lakini kwa kuwa wanazungumza kana kwamba Mimi sipo nilivunga pia.
Baada ya Feisal kumaliza kula alisepa hata bila kuniambia ahsante.
Nicheke mie, yaani Secretary Lui ndio kuja kunishukuru kwa niaba ya Boss wake.
"Nipatie akaunti namba yako nitakuingizia milioni 75, pia kesho nitakuja kukuchukua nyumbani kwako saa mbili kamili. Kutakuwa na kikao hotelini kwetu, Feisal kaona unafaa kuwa Msemaji mkuu"
Sikuwa na sababu ya kukataa, nimekuwa semaji la mtaa wa Igogo B kwenye kesi mbalimbali sishindwi kuwa main speaker kwenye kikao cha Wapishi wote kwenye hoteli ya Burj Al.
Nilimpatia Akaunti yangu kisha nikamsihi anisaidie kuondoka mahali hapa. Sikuwa tayari kufanyiwa fujo na Sokwe .
Secretary Lui ni mtu mstaarabu sana kama angekuwa ni Mwanamke basi ningesema yeye ni Mama mjengo kwenye nyumba hii na Bodyguard Spark angekuwa ni Shangazi sababu ya muonekano wake wa kijeuri lakini huyu Feisal angekuwa ni Mwanamke mwenye kisirani cha mimba.
Ile tunakaribia kufika getini, tulisubirishwa kwanza. Bodyguard Spark alikuja kwa kukimbia.
"Feisal anauliza unaitwa nani" Spark aliongea.
"Naitwa Amina...." Niliongea.
Spark alishika simu akarudisha mrejesho, sijui ilikuaje lakini alinipatia simu ni zungumze.
Nilichukua simu nikaweka sikioni mwangu.
"Amina...." Feisal aliniita
Sauti yake ilikuwa imetulia sana kama wale Watangazaji habari wa Kimataifa.
"Abeee...." Niliitika.
"Nimefurahi kulifahamu jina lako Amina....uwe na siku njema" Feisal aliongea kisha akakata simu.
Bodyguard Spark aliichukua simu yake, mie na Secretary Lui tuliendelea na safari ile nataka kufunguliwa geti, nililetewa simu tena na Spark
"Amina...." Feisal aliita.
"Abeee ....." Niliitika, cha ajabu upande wa pili ulikaa kimya
Nilitaka kumrudishia simu Spark lakini aligoma alinisisitiza niendelee kuweka simu sikioni.
Dakika kama 20 hivi zilitembea bila Feisal kuongea.
"Amina...." Aliniita tena.
"Abeee...." Niliitika
"Nitafurahi kama kesho utafika hotelini kwangu" Feisal aliongea kisha akakata simu.
Sikuwa tayari kupatiwa simu tena, kitendo cha Mlinzi tu kunifungulia geti niliondoka kwa kukimbia......
"Amina simama....." Niligeuka nyuma nikamshudia Bodyguard Spark akija kwa kukimbia huku mkononi akiwa ameshika simu🤣🤣🤣🤣🤣.........
ITAENDELEA........
SIMULIZI : AMINA MAMA
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 05
ENDELEA.......
Nilisimama kujua ni kitu gani nataka kuambiwa
"Amina..." Feisal aliita.
"Amina Mimi hapa niambie hicho kitu ulicho shindwa kuongea nikiwa nyumbani kwako...." Niliongea.
"Tofauti nakupika ni kitu gani kingine unaweza kufanya kwa usahihi mkubwa..." Feisal aliuliza.
"Tafuta muda kwa ajili yangu tutazungumza kuhusu hili...." Niliongea nikataka kurudisha simu.
Bodyguard Spark alinipa ishara ya kujibu swali nililoulizwa na si kukwepa.
"Nipo vizuri sana katika swala zima la kutatua migogoro, ukija mtaani kwetu nafahamika kama hakimu asiye na cheti. Pia nipo vizuri sana katika swala zima la sita kwa sita. Ikitokea nimekuonyesha ni lazima utanitafuta usiku na mchana. Kitumbua changu hakina tofauti na madawa ya kulevya" Niliongea.
Feisal aliachia kicheko kikubwa, inaonekana maneno yangu yalimfurahisha sana.
"Sawa, uwe na siku njema...." Aliongea kisha akakata simu.
"Sitarajii unifuate tena... nitakapo tega mgongo sitageuka nyuma" Nilimuambia Body guard Spark.
Hili jitu sijui lina kichaa au nini lilinibusu shavuni.
"Ahsante kwa kumfanya CEO wangu achangamke namna hii..." Spark aliongea kisha akaondoka.
Niliondoka pia, furaha yangu iliongezeka maradufu baada ya ujumbe wa shilingi milioni 75 kuingia kwenye simu yangu kutoka Burj Al hoteli.
Nilifika nyumbani kwangu nikiwa na furaha kubwa kupita maelezo, nilishangaa baada ya kukuta Sponsa wangu akikusanya vitu vyake alivyowahi kuninulia.
Sikutaka kuumia moyo, tena kwa uzuri kabisa nilimuitia bajaji imsaidie kubeba.
"Nenda tu, hata kama usingeniacha leo kesho ningekuacha. Nataka niwe kwenye mahusiano yanayoeleweka kuanzia sasa hivyo pita kule na Mimi nipite kule" Niliongea.
Hili Sponsa ni jeuri sana, liliondoka bila kuniuliza chochote.
Niliachia sonyo kwa sababu kila gemu Mimi ndio nilikuwa mfungaji mwanzo mwisho sioni hasara kumpoteza.
Sikutaka kupumzika hata kidogo, niliingia ndani nikabadili nguo zangu. Nilihitaji kwenda saluni kutengeneza nywele yangu.
Tangu nizaliwe sijawahi kuingia katika hoteli ya Burj Al.
Sikuona shida kutumia laki mbili kutengenezwa tu kichwani.
Mimi ni mjuzi wa kupangilia nguo, nilitafuta pamba zinazoendana na mandhari ya Hoteli. Si kila nguo inafaa kila mahali. Ili nionekane wa kipekee nilihitaji kufikiria vazi litakalo nifanya wa kishua.
Muda ulikimbia aisee, kulivyo pambazuka asubuhi tu Secretary Lui akiwa na gari la Burj Al hoteli alifika kunichukua.
Nilimshuhudia akiachia tabasamu bila shaka nilikuwa nimependeza kwa kiwango kikubwa.
Ingawa hakuongea chochote, kwa pamoja tulipanda gari.
Nilijikuta ni kitetemeka hasa nikifikiria eti leo naingia katika hoteli ya Burj Al.
"Relax, hii hoteli haina tofauti na migahawa midogo ya huko nje" Secretary Lui alinitia moyo.
Nilijikuta nikicheka kwa sababu alikuwa ananitia moyo kimtindo.
Kwa pamoja tuliingia kwenye hotel ya Burj Al baada ya kufika.
Watu wote walinigeukia, pengine ni kwa sababu nimependeza sana au ni kwa sababu nimeongozana na Secretary Lui.
Sina kawaida ya kushangaa mtu mwenye jinsia kama yangu lakini Mwanamke aliyekuwa ana zungumza na Feisal alikuwa ni mrembo mfano wa katuni ya kishua.
"Huyo ni Mwanasheria wa Feisal, jina lake anaitwa Carolina. Amekaa sana uzunguni si mtu wa kupenda kuongea sana hivyo jitahidi kumpuuzia usioneshe shobo sana" Secretary Lui aliongea.
"Oh Amina...." Feisal aliita kwa sauti kubwa baada ya kuniona.
Watu wote walinigeukia, nilijikuta nikishtuka.... macho ya watu yanatisha aisee.
"Mimi hapa Feisal..." Niliongea kwa sauti kubwa pia, si kwa sababu nilikuwa najiamini hapana, sikuwa tayari kudondoka kwa sababu ya macho ya watu
Feisal alipiga hatua mpaka akanifikia sehemu niliyokuwa. Nilishangaa tu kanikumbatia.
Macho yangu yalikutana na ya Carolina, alinionesha tabasamu pana kana kwamba sisi ni marafiki.
Nilijikuta ni kimkodolea macho kwa namna alivyokuwa anavutia, uzuri wake ulipitiliza kiasi nilifumba macho.
"Amina...." Sauti ya Feisal ilinishtua ndio ni kafumbua macho.
"Amina jina lako zuri sana, si ajabu CEO wetu ana changanyikiwa...." Carolina aliongea.
"Hahahaaaaa...." Feisal aliachia kicheko kikubwa huku akinigonga gonga begani. Watu wote walianza kucheka, inaonekana ni sheria CEO akicheka na Wafanyakazi wake ni lazima wacheke. Nilianza kucheka pia.......
ITAENDELEA...... ..
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote