NAMNA SHILLING MIA ILIVYONIPA MUME DAKTAR
Jamila alikuwa kwenye majukum yake ya kila siku ya kuuza karanga, ndipo gari Kali linasimama mbele yake na kufungua vioo na kutaka kununua karanga,jamila alisogea na kumpa pakti moja ya karanga na yule kijana akatoa shilling elfu kumi na wakat alinunua karanga ya Mia..
Jamila akaomba apitishiwe pesa yake maana hakuwa na chenchi lakin Deni la Mia la Jamila ndilo lilitengeneza ukaribu wa Jamila na DAKTAR maarufu wa upasuaji kwenye hospital ya St Peter, anaefahamika kwa jina la criss, unajua Nini kilitokea usikose muendelezo wa simulizi hii
BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI 01
MTUNZI;
"Karanga ya shilingi mia halafu unanipa elfu kumi! siwezi kupata hiyo chenji" Rose aliongea kwa sauti ya kukwaruza kidogo
"Waombe chenji majirani zako, kwani nyie huwa hamsaidiani" Chris aliongea, ni wazi kabisa alitaka kumsumbua binti huyu mwenye asili ya Wahindi weusi.
"Hakuna mtu anaweza toa chenji kwahiyo pesa yako, nenda utanipitishia" Jamila aliongea huku akimrudishia pesa yake
Chris aliachia tabasamu ndani ya moyo wake.
"Nisaidie namba yako ili iwe rahisi kwangu kukupata"
"Sina simu, kuwa na amani nipo hapa masaa 24 ikitokea umenikosa mpe jirani yangu hapa "
"Sawa usijali Mrembo" Chris aliongea kisha akaondoa gari lake
Jamila na wenzake walijikuta wakicheka kwa jinsi Mwanaume huyu alivyo bahili
"Ni njia yake akiwa anaenda kazini nina uhakika atalipa....huu ni mwaka wa pili namuonaga akipita hapa" Jamila aliongea
Upande wa Chris akiwa ndani ya gari lake, aliihifadhi karanga ndani ya koti lake.
Moyo wake ulienda mbio kidogo baada ya kugundua bado dakika 3 tu kikao kianze.
Bila yeye hakuna kitu kinawezekana, hivyo uwepo wake ni muhimu kuliko kitu chochote.
Jopo la Madaktari wote lilikuwa linamsikilizia yeye.
Kitasa cha mlango kinanyongwa taratibu, na madaktar wote wanaachia tabasamu baada ya kumuona Daktari Chris ambae ni maarufu Kama bingwa wa kucheza na operasheni zote sugu zilizo shindikana kwa watu wengine
Kwa criss Ni kawaida yake kuvaa miwani anapotaka kuona maandishi katika laptop yake, ila siku ya leo ilikuwa ni kichekesho badala ya kutoa miwani avae anajikuta anatoa karanga.
Dorin (daktari bingwa wa mifupa anaachia tabasamu kuna namna anamkubali sana Chris anaamini ukaribu wao utazaa matunda siku za karibuni, na kusahau kwamba unaweza upanga lako na Mungu akakupangia unalostahili.......
"Si unipatie hiyo karanga" Dorin ana muambia docta criss baada ya kikao kuisha
"Aisee, nimeitoa mbali sana na hata hivyo haijalipiwa siwezi kukupatia badala yake nitakununulia chai, hapo vipi" Chris aliuliza
Dorin aliachia tabasamu kumaanisha hapo poa..........
Na kweli baada ya kusubiri muda kidogo hatimae muda wa kupata kifungua kinywa unafika na Kama alivyoahidi criss anaenda na dorin mpaka mgahawan na kumnunulia chai na kitafunwa anachokitaka Kama ahadi aliyo ahidi......
Upande wa Jamila biashara yake ilienda vizuri sana. Na baada ya kumaliza mauzo alirudi anapoishi na huwa anaishi na mdogo wake kwenye nyumba moja ya kawaida na kwa muonekano wanaishi watu wenye Hali ya chinu sana, sasa Akiwa katulia chumbani kwake alimpatia mdogo wake kopo amsaidie kuhesabu pesa na kufunga mahesabu.
"Shilingi 100 haipo....vipi ulikula wewe karanga" Mdogo wake aliuliza
Jamila ndio kushtuka, maana kikawaida huwa wanaanza kuhesabu pacti za karanga na wanakuwa wanajua wanatakiwa kupata sh ngapi kila siku..
Ndipo Jamila alikumbuka kuwa Kuna mteja mmoja hakumlipa pesa ya karanga lakini baada ya kuukumbuka ustaarabu wa sura ya Chris hakuwa na shaka kuhusu deni lake na kuamin atamlipa tu...
Kulivyo pambazuka asubuhi, aliwahi kukaa barabarani. Japo biashara yake ni ndogo lakini huwa ana nidhamu nayo sana maana ndio biashara pekee ambayo anaitegemea kwa ajili ya kuendesha maisha yake na mdogo wake..
Asubuh kulipopambazuka Kama kawaida jamila alienda kibaruani ila Anashangaa baada ya gari la Chris kumpita shwaaaaa tena siku ya leo hata dirisha la gari halikuwa limefunguliwa kabisa ..
"Huyu mbwa anataka kunitapeli au anawaza nini ....." Jamila aliongea kwa sauti ya hasira kidogo
"Ni Daktari Maarufu sana katika hospital ya St. Peter kama vipi mfuate pale anaitwa Chris" Jirani yake alimuambia
"Yakipita masaa sita hajatokea nitaenda kumdhalilisha nadhani hanijui vizuri" jamila aliongea
Aliendelea kuangalia masaa katika simu yake mbovu, kitendo cha masaa sita tu kuisha bila Chris kutokea kilimvuruga.
Wakati anatembea haraka haraka kuelekea hospital ya St. Peter kudai deni lake, Chris alijiandaa vilivyo kuingia kwenye chumba cha operation
Bila kujua huku nyuma Jamila anajiandaa kuja hospital kudai Deni lake Tena kwa vurugu ikitokea hatomlipa
Itaendelea π₯
BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI 02
MTUNZI; LIZY MICA
Hospitali ya St. Peter ilikuwa kubwa sana, Jamila alianza kugeuza macho yake huku na kule. Bahati mbaya aliparamiana na Dorin (Daktari bingwa wa mifupa na rafiki wa Chris)
"Samahani naweza kumuona Daktari Chris..." Aliuliza
Dorin alimuangalia kwa kumkadiria kwanza kisha akaangalia saa yake ya mkononi.
"Si rahisi kumpata....kwa masaa yote nane yaliyosalia atakuwa bize sana. Sijui una shida gani na yeye lakini ningeshauri kama utaweza basi ungekuja kesho, uwe na mchana mwema" Dorin aliongea kisha akaondoka, haraka haraka akionekana Kama alikuwa Ni mtu alikuwa na ratiba ngumu Sana...
Jamila hakutaka kukata tamaa, alikaa kwenye benchi akamsubiria Chris.
Masaa yalizidi kwenda, hakuwa na shaka kuhusu usalama wa karanga zake. Watu anaofanya nao biashara katika eneo moja ni watu wema sana.
Operation alizokuwa ana shughulika nazo Chris siku hio zilikuwa ngumu sana. Huwezi kuamini kila alipohisi kuchoka alifikiria kuhusu karanga ya Jamila alikuwa mpaka yeye anajishanga maana sio kawaida yake kuwaza Wala kufikiria kitu Cha shilling Mia tu kila wakato, na Kuna namna kila akifikiria kuhusu Jamila na karanga yake alipata Hari na nguvu ya kufanya kazi zaidi.....
Basi Kama tunavyojua hakuna marefu yasio na ncha, na criss pia Anafanikiwa kumaliza Operation zote tatu.
"Nilitarajia utakuwa umeondoka tayari...." Aliongea kwa mshangao criss baada ya kumuona Dorin anamsubiria
"Pole na hongera kwa kumaliza kazi hii ngumu....nina uhakika siku ya leo kijasho kimekutoka" Dorin aliongea huku akimpatia maji ya kunywa
"Mara nyingi huwa unaweza kuyasoma mawazo yangu kuliko watu wengine, ni kweli kijasho kimenitoka" Chris aliongea huku akiachia tabasamu jepesi kwenye uso wake....
Dorin alimpiga piga kwenye bega kumaanisha wapo pamoja.
Wakati wanashuka kwenye ngazi waelekee nyumbani, alishangaa baada ya kumuona Jamila akijinyoosha viungo vyake. Ni wazi kabisa alikuwa amechoka.
Japo kulikuwa na ka umbali lakini macho yao yalikutana...
Ndipo Chris alishtuka kuwa anadaiwa shilingi mia.
"Ah huyo binti alikuwa ana kutafuta, siamini kama amekaa hapa kukusubiria....ni vyema ukimsikiliza" Dorin aliongea kisha akaendelea na safari bila mashaka yoyote yale kwa Jamila maana alikuwa havutii Sana kutokana na ufubavu wa ngozi yake na kupauka kwa nguo zake...
Chris alimsogelea Jamila akiwa kachoka kupita kiasi
"Nisamehe, nilitingwa sana leo... isingekuwa rahisi kupata muda wa kukupitishia malipo"
"Wala usijali..,nipe changu nisepe" Jamila aliongea huku akijitahidi kuzizuia hasira zake
Chris alijikagua mifukoni mwake kama kumfurahisha tu Jamila lakini ukweli kutoka moyoni hakuwa na pesa ya sarafu mfukoni mwake
"Shika hii pesa utakata deni lako, itakayo bakia tumia....nisipofanya hivi tutasumbuana" Chris aliongea na kutoa noti ya shilling elfu 10
"Nadhani hata jana ungefanya hivyo tu, ni uongo mkubwa Daktari kama wewe kumiliki sarafu tena ya shilingi mia mfukoni mwako" Jamila alimchana
"Ulisema hauna simu hii ni nini...." Chris aliongea huku akitaka kuichukua simu ya Jamila
Jamila hakuwa tayari kumshikisha kasimu kake kabovu criss alikarudisha kwenye mfuko wa suruali yake.
Criss alijua fika kuwa Jamila hapendi kasimu kake kaonekane "Naomba nikupe lifti..." Chris alijipendekeza
Jamila alijikuta akikumbuka namna gari la Chris lilivyopita asubuhi kwa kasi ya ajabu. Hofu ilimuingia akawaza vipi kama Mwanaume huyu atampitilizisha kusikojulikana....
"Ahsante nitatembea kwa miguu...." Jamila aliongea akitaka kuondoka.
Pamoja na Chris kuwa mtu wa watu lakini ana udhaifu mmoja akitaka kitu huwa ametaka.
Alijikuta akimshika mkono Jamila kwa nguvu, amri ilikuwa ni moja tu kupanda gari na si kutembea
Itaendelea π₯
BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI 03
HUSQER BALTAZAR
"Mbona kama uninilazimisha?...kuna ulazima wa Mimi kupanda gari yako" Jamila aliuliza akiwa kakunja sura yake
"Sa... samahani kwa kukushika mkono kwa nguvu namna hii, lakini kuna dalili ya mvua nahofia utalowana" Chris alijiongelesha
Jamila alishika simu yake akampigia rafiki yake wanayeuza genge moja
"Napanda gari la Daktari Chris wa hospitali ya St. Peter lolote baya likitokea juu yangu naomba utawasaidia Polisi...." Jamila aliongea kisha akakata simu
Daktari Chris hakuamini kama anaonekana Kibaka kwa mrembo huyu.
Kwa pamoja waliingia ndani ya gari
"Naomba usifunge dirisha la gari, nahitaji kuvuta hewa....pia punguza mziki ili ikitokea nimepiga kelele basi sauti yangu isikike vizuri huko nje...."
"Ni kama unahofia naweza kukufanyia kitu kibaya, naomba usinifikirie hivyo" Chris aliongea
"Binadamu hawatabiriki, kubadilika ni gusa unate..." Jamila aliongea
Chris alijikuta akimuangalia badala ya kuwekeza akili yake kwenye kuendesha gari. Anakuja kushtuka kafika nyumbani kwake....mvua nayo ilikuwa imepamba moto balaa
"Ni makusudi kabisa, kwanini umeshindwa kunishushia pale Kijiweni..." Jamila alilalamika
"Nisamehe, lakini hata ningefanya hivyo ungelowana...." Chris aliongea
Jamila alikosa neno la kuongea, kuna namna aliwaza mbali
"Hivi ikitokea huyu mbwa anataka kunibaka nikasema nipige kelele kuna mtu atanisikia kweli!" Jamila aliwaza mbali
Lakini kuna namna alijifariji, muonekano wa sura ya Chris ulikuwa wa kipole hivyo alipata amani ya moyo.
"Sina uhakika kama hii mvua itakata hivi karibuni, kuliko ukae hapo umejiinamia ingia jikoni upike, kuna chumba pale kwa ajili ya Wageni unaweza pumzika pia" Chris aliongea
"Kwahiyo unataka nipike na kulala hapa!...muda huo wewe unakuwa wapi!" Jamila aliuliza kwa hofu
"Mbona una hofu machoni kwako au una Malaria!" Chris aliuliza huku akimshika kwenye paji la uso
Jamila alishtuka zaidi,mkono wa Chris ulikuwa kama una mtekenya hivi na si kumpima
"Kuwa na amani, pika kisha ule mwenyewe mie naenda kulala....siku ya leo nimechoka sana" Chris aliongea
Jamila hakuamini macho yake baada ya kukabidhiwa jiko....
Alikuwa na hamu sana ya kupika pilau, anaachia tabasamu baada ya kuona nyama kwenye friji.
Alijikuta akihisi ni mchana ilihali ilikuwa ni usiku....alifungulia mziki kwenye kisimu chake kibovu kisha akaanza kulitendea haki jungu la pilau.
Nyumba nzima ilitapakaa harufu ya pilau....
Saa sita kamili juu ya alama alipata kupumzika baada ya kuivisha.
"Nitaonekana mlafi kama nitamaliza hili jungu lote pekee yangu...nitampelekea pia" Jamila alijisemea kisha akajaza pilau kwenye sahani
Alitembea kwa tahadhari kidogo mpaka alipofika chumbani kwa Chris, alitengeneza sauti kisha akagonga
Baada ya kuona kama hafunguliwi aliupush mlango kidogo.... tobaaaaa! sahani ya pilau ilidondoka kule. Alijikuta akipiga kelele baada ya kukutana na fuvu la binadamu likiwa limevalishwa koti jeupe
Chris anashtuka usingizini baada ya kusikia kelele.
Jamila ndio kuchanganyikiwa zaidi baada ya kumshuhudia Chris akiwa kavaa boksa tu huku umbile lake limepinda kule kama mshale wa kinjikitile ngwale
Itaendelea π₯
BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI 04
HUSQER BALTAZAR
"Simamaaa hapo hapo, kwanini unaishi na jitu la ajabu hivi chumbani kwako!..." Jamila aliongea huku akizidisha kujibana kwenye kona
Chris ndio kushangaa, kumbe kelele zote hizi ni kwa sababu ya fuvu la plastic lililopo chumba kwake
Alinyoosha mkono akamnyanyua Jamila.....hakuamini kabisa baada ya kulishuhudia kojo.
"Mvua imekata naomba niondoke siwezi kuendelea kukaa hapa, mdogo wangu ni muoga hawezi kulala pekee yake" Jamila aliongea akiwa kafumba macho hakuwa tayari kuangalia boksa ya Chris
"Nitakupeleka nyumbani, ni hatari kwako kutembea usiku..." Chris aliongea
"Saa sita siyo usiku wa kutisha wala usihangaike nitaenda mwenyewe" Jamila aliongea akataka kuondoka
Lakini Chris alimtuliza kwa kumshika mkono......
"Nitakupeleka nyumbani nisubirie nivae...."
"Sa...sa..sawa..." Jamila aliongea huku akijikagua hakuamini kama kajikojolea lakini pamoja na presha lote hili alikumbuka kuhusu pilau.
Aliangalia chombo chenye ukubwa wa kujaza pilau lote akaweka.
"Utaonekana kichaa ukienda na nguo yenye harufu ya mkojo....vaa nguo zangu" Chris aliongea kisha akampatia nguo
Jamila alichekelea ndani ya moyo wake, japo ni nguo za kiume lakini zilikuwa ni za gharama.
Kwa pamoja waliingia kwenye gari,
"Hizi nguo niachie tu ingawa hujasema lakini zimenitoa" Jamila alijiongelesha
"Sikuwa na ratiba ya kuziomba tena....." Chris aliongea huku akimrekebishia tisheti
Macho yao yaligongana, kuna namna wote wawili walipata mshtuko.
Chris aliendesha gari baada ya kupatiwa maelekezo na Jamila
Wanafika nyumbani baada ya dakika 25 kupita
"Ahsante kwa kunifikisha nyumbani salama... " Jamila aliongea kisha akaelekea ndani baada ya mlango kufunguliwa.
Hakuwa akikumbuka kuhusu pilau.
Chris aliondoa gari pia, hakujua kama siti ya nyuma kulikuwa na pilau lililosahauliwa na Jamila.
"Kuwa na amani, shilingi mia niliyokuwa nadai nimelipwa..." Jamila alijitetea kwa mdogo wake
"Hizi nguo ni kama za Mwanaume hivi, na kwanini umeletwa na gari hapa..." Ali aliuliza, japo ana miaka 7 lakini kuna namna huwa ana mchunga Dada yake
Jamila alivunga haelewi, alisikia hasira ndani ya moyo wake baada ya kukumbuka kuhusu pilau alilolisahau kwenye gari. Alishika simu ampigie Chris bahati mbaya hakuwa na namba yake
Ali anaamua kukaa kimya baada ya kuona Dada yake ni kama hamsikii hivi.
Kulivyo pambazuka asubuhi, Jamila aliwahi kupeleka biashara yake barabarani. Muda wote macho yake yalikuwa barabarani, alikuwa na shauku ya kuonana na Chris ikiwezekana achukue kiporo chake cha pilau.
Baada ya nusu saa hivi gari la Chris lilisimama, alisogea kwa haraka dirishani.
"Kuna chakula nilisahau kukichukua jana......" Jamila aliongea huku akitengeneza uso wa tabasamu
"Nimekitupa kwa sababu kimeharibika.....nitakupitia jioni baada ya kazi twende nyumbani kwangu, kuna kitu nataka ni kuambie.... naomba utanisubiria hapa" Chris aliongea huku akimpatia pesa
Jamila alijikuta akitetemeka mikono, Chris aliitambua hofu yake alisogeza mkono akamuwekea kwenye mfuko wa tisheti yake.
"Tutaonana baadae Mama yangu...." Chris aliongea kisha akaondoa gari
Jamila aliishia kushika mashavu yake, hasa akikumbuka namna alivyoitwa Mama.
Wakati anageuka hivi alishtuka moyo wake baada ya kukutana macho na Ali (mdogo wake) anayependa kumfuatilia kila hatua
Itaendelea π₯
BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI 05
HUSQER BALTAZAR
Hakuwa tayari kujieleza alivuta benchi lake akakaa
"Kuwa makini na Wanaume hasa hawa wenye magari wanakuwaga Wahuni sana" Ali aliongea kisha akaondoka
Kuna namna Jamila alijisikia aibu kufumwa na mdogo wake akiwa kasimamishwa na Mwanaume.
Lakini alijipiga kifua kwa kujifanya hajui nini kimetokea.
Chris anafika kazini kwake kwa wakati, siku ya leo hakuwa na majukumu mengi hivyo alipata muda wa kuzungumza na Dorin (Daktari bingwa wa mifupa)
"Ni kitu gani kizuri unaweza kumuambia msichana unayehitaji muwe kwenye mahusiano" Chris aliuliza na kumfanya Dorin apaliwe mate
"Unataka kusema una msichana moyoni mwako!...." Dorin aliuliza akiwa na shauku ya kujua
"Kuna kasichana kadogo dogo hivi kameyakamata macho yangu...."
"Unamtaka kwa ajili ya mahusiano ya muda mrefu au unataka kupita tu...."
"Ningekuwa nataka kupita naye si ningetoa pesa tu wala nisingeumiza kufikiria ni jambo gani nimuambie...." Chris aliongea
"Kama unaweza kufanya operation bila kusaidiwa, nina uhakika unaweza kuzungumza hisia zako pia bila kusaidiwa. Nina kazi nyingi za kufanya naomba tuzungumze baadae" Dorin aliongea kisha akaondoka
Chris anashindwa kuelewa kwanini rafiki yake kabadilika ghafla.
Hakutaka kumfikiria sana, alianza kupiga mahesabu ni kitu gani atazungumza pindi atakapo kutana na Jamila.
Upande wa Jamila pia presha ilipanda na kushuka, alijiuliza na kujijibu maswali ambayo hakujua yanatoka wapi.
Aliogopa sana kutumia pesa alizopatiwa na Chris kabla ya kusikia ni kitu gani ataenda kuambiwa.
Mida ya jioni Chris akiwa anatoka kazini alipita, bahati nzuri karanga zake zilikuwa zimeisha zote.
"Naenda na huyo jamaa nyumbani kwake, endapo nitapotea katika mazingira ya kutatanisha usihangaike mripoti moja kwa moja Polisi" Jamila aliongea
"Kama huna imani naye acha kwenda kwanini ujipeleke sehemu ambayo huna uhakika wa kuishi" Rafiki yake aliongea
Jamila alimkonyeza jicho kimtindo kisha akaelekea kwenye gari la Chris.
Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanasikika puuh puuh puuh, sikio la Chris liliweza kuyasikia vyema kabisa.
Alimshika mkono akamtaka ashushe presha.
Baada ya kufika nyumbani, Chris aliingia jikoni akaandaa chakula.
Muda wote Jamila aliendelea kubashiri vitu ambavyo ataambiwa
Baada ya chakula kuiva, Chris alimkaribisha. Kwa pamoja walianza kula
"Kwanini usiniambie hilo jambo ulilokuwa unataka kuniambia....nakosa uvumilivu" Jamila alivunja ukimya
"Nilitaka ni kuulize haupati usumbufu unapokuwa kwenye eneo lako la kazi.... namaanisha watu wa ushuru hawakusumbui" Chris alijikuta akiongea kitu ambacho hakuwa amepanga
Jamila alishusha pumzi kisha akagonga meza kwa hasira
"Kuhusu suala la ushuru mbona ni kitu cha kawaida sana, yaani kweli umeniita hapa kuniuliza kitu kama hiki!" Jamila aliongea akionekana kukasirika
Chris aliachia tabasamu kisha akajikuna kichwa chake
"Nakupenda, naomba tuwe kwenye mahusiano...." Alienda moja kwa moja kwenye lengo
Jamila ndio kuchanganyikiwa zaidi, alijikuta akijibu text ya juzi aliyotumiwa na rafiki yake.
Chris alihamia kwenye kochi alilokaa Jamila. Alihitaji kupata jibu la uhakika hivyo alikishika kisimu chake akakiweka mezani.
"Nimesema nakupenda...."
"Niache nipo kwenye siku za hatari..." Jamila aliongea vitu vingine kabisa.
Alielewa endapo atatoa jibu linalo eleweka ni lazima mzigo upigwe kama kawaida ya wabongo
"Ni vizuri kuwa kwenye siku za hatari....hongera kwa hilo" Chris aliongea kisha akajisogeza zaidi kwa Jamila
"Utamwaga nje please...." Jamila alionesha udhaifu wake mapema ni wazi kabisa alikuwa na hamu ya kuliwa na si kingine
Chris alinyoosha mkono wake akamshika paja, walijikuta wakibadilishana mate. Wakiwa wamenogewa kabisa kushikana shikana mlango uligongwa
Itaendelea π₯
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote