RIWAYA: BOX LA NINJA
MTUNZI: MAULID KIFUMBE (MR ROY)
Sehemu Ya 1
Uso wake ulitawaliwa na furaha, hakuwa na mawazo yakuutesa ubongo wake nakuufanya ufukute. Mchecheto wa raha ulilanda kwenye nafsi yake. Kwenye ngome ya masikio yake zilipenya sauti safi zilizotoka kiumaridadi, japo sauti zile zilikuwa za kiume, ila kwa jinsi maneno yalivyotamkwa yalivutia mnoo!. Naam! Maneno yale yalitamkwa kwakuimbwa juu ya mdundo, uliopikwa kisawa sawa na mpishi mashuhuri aliyetambulika kwa jina la Geniusjini X66. Mpishi wa mdundo ule, ndio huyo huyo aliyesikika akianzisha mashairi, kama kawaida yake yeye huwaga anaanza kutambaa kwenye beat kwakingereza kisha anafatia kwa kiswahili. Nafasi yake ilitamatika, ikaingia nafasi ya kijana mwenye melody tamu. Jina lake lilifanana na kile alichokuwa anakifanya juu ya Beat zote alizoziimbia. Anaitwa Jay Melody, wimbo ulikwenda kwa jina la Far Away alioshirikishwa. Wimbo huu ulio imbwa kiustadi wa hali ya juu, ulikuwa unapenya kwenye ngome ya masikio ya kijana aliyekuwa ndani ya gari akiwa ameshikilia usukani, akiliongoza gari lile kwenye ile barabara ya lami. Magari mengi hayakuwa yanapita mahala pale, hata watu pia hawakuonekana wakipita sana.
Burudani ile ilimkolea kwenye ubongo wake kisawa sawa, alikuwa anaendesha huku akifatisha maneno ya wimbo ule, huku akitikisa kichwa kuonesha wimbo ule ulitembea na hisia zake. Wakati aliokuwa nao kwenye mahusiano yake, ulifanya wimbo ule aurudie mara mbili mbili. Wimbo ule ulifanya umakini wake wakuangalia mbele upungue, alifikia hatua yakuimba huku akiwa ameyafumba macho yake. Mshtuko mkubwa ulimvaa! Ni baada yakufumbua macho yake, na mbele akaona mtu amelala katikati ya barabara. Alifunga breki upesi, gari ikaseleleka, kabla yakumfikia mtu yule, ikasimama. Alishusha pumzi ndefu! Macho aliyakodoa kama mjusi kabanwa na mlango, hakuamini kama hajamgonga. Alifungua mlango wa gari, kisha akashuka, nakusogea alipolala mtu yule.
Kwa mavazi aliyovalia mtu yule, ilionesha dhahiri shahiri alikuwa ni jinsia ya kike, alilala kifudifudi, uso wake akiuwelekeza chini ya lami. Mwili wake ulivalia vazi la gauni.
"Wewe binti wewee! Amka! Utoke barabani." Sauti yake ilitoka ikimtaka mdada yule amke. Ujasiri ulikuwa mbali naye, alihofia kumsogelea zaidi, alitamani kuinama na kumgusa ili amtikise tikise, ila alisita kufanya jambo hilo. Kwa sekunde kadhaa mawazo yalilindima kwenye kichwa chake, akifikiria cha kutenda. Ilifika tamati ya mafikirio yake, aliona bora amtikise. Akalifanyia kazi wazo lile, akamtikisa mara kadhaa, huku akitamka maneno yale aliyoyatamka mwanzo. Alimgeuza uso wake na kiwili wili, alishtuka! Ni baada yakumtazama usoni. Pamoja na mavazi aliyovalia, lakini alikuwa anasura ya kiume, alikuwa mzima wa afya kabisa. Mtu yule alimkodolea macho kijana yule, hali iliyomfanya yule kijana aanze kurudi nyuma upesi, yule mtu aliyekuwa amelala pale chini, akajiinua taratibu. Yule kijana akataka kukimbilia kwenye gari, mara akapigwa teke lililomsukuma mpaka kwenye gari lake. Akajibamiza, eneo teke ilipotoka, ilionesha aliyempiga ni mtu mwingine tofauti na yule aliyekuwa amelala pale chini.
Yule kijana alikuwa ameumia kwenye paji la uso, ni baada yakujibamiza kwenye gari. Akageuka na kutazama mtu aliyemlamba teke lile. Hakuweza kujua ni nani kwakuwa mbele ya macho yake walionekana vijana watatu waliovalia kisela tu. Ila sura zao zilitoa majibu yake, walionekana ni watu wabaya, maana hata miili yao ilionesha ni watu wenye kufanya mazoezi sana. Yule mtu aliyejifanya mwanamke, akaungana na wale watatu, wakawa wanne. Wakaanza kumsogelea yule kijana, alikuwa anatetemeka isivyo kawaida. Alitaka kufungua mlango wa gari aingie, ila nguvu hakuwa nazo, kutetemeka ndio kulimuondolea nguvu zote. Alipiga magoti chini nakuanza kuomba wasimdhuru.
"Jamani niacheni niende! Kama mnataka pesa ingieni kwenye gari mchukue, ila niachieni uhai wangu." Aliinua mikono juu akiomba, huku machozi yakidondoka chini. Alikuwa analia.
"Hatuna shida na hela zako! Sisi tunataka uhai wako." Alisema jamaa mmoja kati ya wale wanne, huku wakiwa wamemfikia, yule kijana akiwa chini ya miguu yao akiwaomba msamaha. Waliona kama anawapigia kelele, mmoja akapiga teke, ila kimasihara tu, yule kijana akaikwepa. Yeye mwenyewe hakuamini kama ameweza kukwepa. Yule jamaa aliyepiga teke, baada yakuona teke lake limekwepwa, alikasirika! Akarusha lingine kwa hasira. Nalo akalikwepa huku akiinuka na kusimama, uso wake ulionesha bado anaogopa maana alikuwa analia. Wengine wawili wakarusha ngumi kwa pamoja. Zote akazikwepa, hakuacha kulia aliendelea kulia huku akionesha kutetemeka.
Wale jamaa walishangaa! Wakawa wanapiga mapigo kwa pamoja. Ila kilicho washtua na kuwashangaza zaidi! Ni baada yakuona mtu yule akijibinua na kuruka sarakasi, nakutua nyuma yao. Waligeuka upesi huku macho yao wakiyakodoa kama kipofu aliyeona. Yule kijana aliwaoneshea ishara ya mikono akiwaita wamsogelee, hakusitisha zoezi lake la kulia, aliendelea kulia. Huku akitetemeka kama kawaida. Walimsogelea nakuanza kupiga mapigo mfululizo, mtu yule hakuwa wa kawaida kama walivyomchukulia. Alikuwa mwepesi zaidi ya karatasi, aliinama chini ikapita ngumi nzito juu yake. Kisha akainuka, akaruka, teke lililotumwa likapita chini, miguu yake akairudisha chini akasimama akajibinua ubavu ubavu, ngumi iliyotumwa ikapita na hewa. Aliyakwepa mapigo yote, hakika alijaliwa kipaji cha kuigiza, jinsi alivyokuwa anatetemeka na kulia, unaweza nadhani alikuwa analia kweli. Ndani ya nafsi yake hakuwa anatetemeka wala kulia, alikuwa anafuraha kubwa kupata changamoto ile. Alibadilisha muonekano wa sura yake na mwili wake, akaanza kutabasamu. Kama sio yeye aliyekuwa analia sekunde kadhaa nyuma, na machozi yalikuwa yanatoka kweli kweli, ila wakati huu yalikuwa yamekata. Alijua kuutendea haki unafki.
Tabasam lililobeba mengi, lilishamiri kwenye mashavu yake. Aliona imetosha kuwaendekeza, aliona awape somo kidogo yakutokuzoea zoea watu. Kila aliyesogea alipokea kisago cha mwana ukome. Ulitanda ule msemo wa vunja mifupa kama meno iko. Ilisikika milio ya mifupa ikilia, aliwavunja vunja kama anavunja kuni. Sekunde kadhaa alikuwa ameshawalaza wote wanne pale chini, kila mmoja akishika kiungo alichoumia, ilisikika milio ya kuugulia maumivu. Yule kijana akawavutia pembeni ya barabara, akawatelekeza kando ya barabara. Kisha akaenda kuzama ndani ya gari, ule wimbo wa Far away uliendelea kupiga, maana aliuseti ujirudie rudie. Aliachia tabasam mwanana, akaongeza sauti ya mziki, akawasha gari nakuiondoa mahala pale.
Mataili ya gari yaliendelea kuikanyaga lami, hadi mwisho wa lami ile, sasa yakaanza kuikanyaga barabara yenye vumbi. Barabara ile ya vumbi haikukanyagwa sana kama ile ya lami. Mwisho wa safari ile ulifika, baada yakupiga honi, zilipita sekunde kadhaa geti likafunguliwa, gari likazama ndani. Nakuipaki gari kando ya geti, yule kijana akashuka.
"Waoooooh baby, nimekumisi" Ilisikika sauti tam, iliyotoka kwa umaridadi. Mkumbato ndio uliowagandisha pale kwa sekunde kadhaa.
"Mmmh! Masaa kadhaa tu haya umeshanimisi?"
"Handsome Boy wangu! Kwa jinsi navyokupenda! Hayo masaa kadhaa, mi naona kama siku kadhaa." alisema yule binti, akiwa bado amemkumbatia.
"Mmmh! Twende sasa ndani." Alisema yule kijana, akimshika mkono mahabuba wake. Wakapiga hatua mpaka ndani, wakakaa kwenye sofa, walimwagiana mabusu, wakazama ndani ya hisia nzito.
Upande mwingine. Mtu huyu alijaliwa sura yenye upole, sura yake ilimfanya aonekane ni mtu mwenye roho nzuri sana. Kule mtaani alipokuwa anaishi, hawakujua kazi yake maalum anayoifanya walimuona ni mtu wa mtaani tu akipata kazi yoyote anafanya ili maisha yazidi kusonga, kumbe sivyo. Watu wengi wanabalikiwa vipaji, vya aina mbali mbali. Kati ya hao watu waliobalikiwa vipaji, naye alikuwa mmoja wao. Ila kipaji alichokuwa nacho yeye nicha tofauti na walio wengi. Sura yake ya upole ilikuwa tofauti na uhalisia wa roho yake. Alipenda kuona wengine wanalia, wanaumia na kufariki. Hakuwa na chembe ya huruma kama sura yake ilivyoonesha. Alipenda kufumba jicho moja, nakuliacha lingine likiona. Alipenda mikono yake ishike kitu cha moto, bunduki! Naam! Bunduki aliihusudi kupita maelezo, mchezo wakuchezea bastola na bunduki aliupenda sana.
Wakati huu alikuwa anafanya mchezo aupendao, alikuwa anacheza na roho ya mtu aliyekuwa anamuona kwenye bunduki aliyokuwa ameishikilia. Mtu yule aliyekuwa anaonekana kwenye bunduki yake, alikuwa na walinzi hodari wapatao sita, waliokuwa wamemzunguka. Alikuwa kwenye uzinduzi wa kiwanda, alikuwa anasogea kwenye utepe kwaajili yakukata na kufungua kiwanda kile. Alipewa mkasi na kusogea kukata, ni kama alivyokuwa anakata, alikuwa anajikata mwenyewe. Maana damu ziliruka nakutapakaa mkononi mwake na damu zingine zikaenda kutua kwenye nyuso za watu waliokuwa karibu yake. Zilipenya risasi mbili kwenye paji la uso wake, aliganda kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kwenda chini. Walinzi wakamuwahi na kumdaka....
USIBANDUKE.
RIWAYA: BOX LA NINJA
MTUNZI: MAULID KIFUMBE (MR ROY)
Sehemu Ya 2
SONGAA NAYO.
"Deal Done! Mi ndio Triple X, Mzee wakucheza na roho za watu" Alisema huku akilifunga dirisha, nakuibusu silaha yake, akaiweka sawa na kuirudishia vizuri kwenye begi, akalivaa lile begi nakuanza kuzipiga hatua za kutoka ndani ya chumba kile bila wasi wasi wowote. Akafungua mlango, mara mbele akaona vijana wanne wakiwa wametanda kwenye mlango. Wakamsukumia ndani ya kile chumba na kuufunga mlango kwa ndani.
Upande mwingine, alionekana jamaa mmoja akiwa amebeba mzigo ambao ulikuwa ni mzito, hakutaka kuubeba mzigo ule ila alijikuta tu anaubeba. Ni kama mzigo ule ulinata kwenye kichwa chake, kila alivyojaribu kuushusha alishindwa. Kusimama alishindwa, hata alipokaa pia alishindwa kuvumilia. Hakuwa na chagua lingine zaidi yakutafakari jinsi yakuushusha mzigo ule. Alikaa kwenye kiti huku mzigo ukiwa kichwani mwake, kila alichofikiria aliona hakifai, mzigo ule ulimtesa mnoo!.
Naam! Ulikuwa ni mzigo wa mawazo ndio uliokuwa unakichemsha kichwa chake, kichwa kilitiririsha jasho. Alitoa, alizidisha aligawanya lakini bado hakupata jibu la swali lake. Akapata wazo lakuufanya mzigo ule wa mawazo usiwe mzito sana. Alibofya simu yake kisha akaipigia namba aliyotaka kuipigia.
"Mmefanikisha nilicho waagiza?" Alizungumza mtu yule, akajibiwa upande wa pili.
"Ndio mkuu! Kazi wameenda kuimalizia" Ilisikika sauti upande wa pili ikijibu kauli yake. Alikata simu kisha akaiweka pembeni kwenye meza. Wakati huu alijihisi tofauti na awali, amani kidogo ilitawala kwenye nafsi yake. Akapata wazo! Alishangaa kupata wazo lile, maana mwanzo hakulipata. Alijiona kama fala, maana alitumia mda mwingi kuwaza wakati kulikuwa na sehemu yakumpatia majibu yale. Alikumbuka kitu, alichowahi kukisikia kwa mtu. "Huwezi kuwaza mawazo mazuri ukiwa umepaniki, maamuzi mengi mabaya yanafanyika ukiwa na hasira. Ukitulia ukatatua swali lako kwa utaratibu bila kupaniki ni rahisi kupata jibu lako. Hata hivyo ukiwa na furaha nirahisi zaidi kutatua hayo maswali, ufikirii sana majibu yanajijaza tu." Ni maneno aliyowahi kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mtu wake wa karibu.
Aliinuka upesi, akaishika simu yake, nakusogea mlangoni, akashika kitasa akafungua mlango na kutoka kwenye chumba kile. Miguu yake aliirusha rusha haraka haraka, alizipiga hatua mpaka kwenye moja ya chumba. Akafungua mlango nakuzama ndani ya kile chumba. Alipokelewa na bonge la tusi. Naye akamjibu.
"Nimekuacha mdomo wazi ili upumue vizuri, lakini naona unapoelekea maneno yako yatakuponza." Alisema mtu yule akikaa kwenye kiti cha pembeni na kitanda.
"Lucas! Nishakwambia mi sikutaki sihitaji kuishi na wewe. Niache na maisha yangu." Ilisikika sauti ya binti ikilalama. Alikuwa amefungwa kamba mikononi, mikono ikiwa nyuma ya mgongo, alifungwa pia na miguuni. Alikuwa amekaa kitandani.
"Hahahaha! Nimekuleta hapa sio kwa sababu nakupenda! Upendo wangu kwako ushaenda na maji, nimekuleta hapa ili nipate majibu tayokuwa najiuliza. Na pia nilipe kisasi changu, nyie wote inatakiwa niwauwe. Taanza na wewe kisha wengine watafata." Lucas alisema kauli hiyo akiwa na anatoa bastola kwenye kiuno na kuifuta futa kwakitambaa alichokuwa ameshikilia.
Upande wa pili, ndani ya chumba, Triple X mawazo yake yalikuwa tofauti na wale vijana. Aliwaza ni watu wamekuja kumkamata, bila kulemba mwaandiko aliruka teke kadhaa zilizotoka kiumaridadi, zikatua kwenye shavu za wale vijana. Hakutaka kupoteza mda aliwarushia ngumi zenye ujazo mzito, alikuwa mwepesi mnoo! Hawakuweza kupangua pigo lake hata moja. Ngumi walizopigwa zilitua kwenye nyuso zao, hawakuona kwa sekunde kadhaa.
"Xhaka Xavi!!.." Ilisikika sauti ya kijana mmoja kati ya wale aliowapiga, akitaja jina hilo. Aliganda kwa sekunde kadhaa Triple X, ni baada yakusikia anaitwa jina lile. Alisita kuendelea kuwachabanga. Alizama kwenye tafakuri nzito, akiwaza wale ni nani hadi wanamjua majina yake. Hakukumbuka kama kuna mtu yeyote ndani ya jiji hilo, anayejua majina yake halisi! Hali hiyo ndio ilimfanya asitishe zoezi la kupambana na kuwaangalia vizuri.
"Nyie ni wakina nani? Na mmenijuaje?." Triple X aliuliza swali huku akizidi kuwakodolea macho kama atamjua hata mmoja. Aliwaona lakini hakuwatazama, umakini ulikuwa mbali naye kidogo.
"Alex Sinio." Alisema yule jamaa aliyemuita jina lake halisi. Alitaja jina lililomshtua Triple X, akabaki anamuangalia kwa mshangao! Akazipiga hatua za kurudi nyuma taratibu.
"Hapana! Usitie shaka yoyote, sipo hapa kwa nia mbaya. Nimekuja kufanya kazi na wewe! Nimeona kazi bora ambayo umeifanya, lakini usijiulize nimejuaje, jua tu ninapenda kazi zako. Nahitaji tuungane tufanye kazi kwa pamoja." Alisema yule jamaa akimtazama Triple akisubiria jibu lake. Zilipita sekunde kadhaa! Triple X hakusema chochote, alimuangalia tu. Mlango wa chumba kile ulisikika unagongwa kwa fujo! Hali iliyowashtua wote!. Mawazo yao yaligongana kwa pamoja, kila mtu alihisi ni askari wanaomsaka mtu aliyemuuwa muheshimiwa.
"Juu ya jengo hili kuna ndege inatusubiria, tumekuja kukuchukua, tukafanye kazi kwa pamoja. Hamna mda wakupoteza, vaeni mask tutoke nje." Alisema yule jamaa akichomoa bastola yake na kuvaa mask na wengine wakafanya vile vile. Triple X ndio hakufatisha vyote, alivaa tu mask, hakuchomoa bastola japo alikuwa nayo. Upesi yule jamaa akasogea mlangoni na kufungua mlango, bila kusita kwa sekunde yoyote, akatoka anamimina risasi mfululizo. Na wengine wakatoka wanamimina, sekunde kadhaa waliwalaza chini askari kadhaa na wahudumu waliokuja nao. Walivaa mask kwa sababu walijua tu camera lazima ziwepo. Wakatoka nduki maeneo yale wakienda kwa umakini wakiangalia nyuma na mbele, Triple X aliwafata nyuma bila kujishughulisha na chochote. Walipandisha ng'azi, wakatokea juu ya jengo. Kulikuwa na Helikopta, wakafika wanazama ndani, mda si mrefu helikopta ikaanza kuinuka na kuondoka eneo lile.
Ndani ya chumba, Mr Lucas alionekana akiwa ameshikilia bastola akifuta futa huku akiendelea kumtazama binti yule, aliyempenda sana.
"Lucas! Nimekwambia sikutaki!. Niachie niende nimechokaaa!." Alizidi kulalama binti yule akipalang'anya pale kitandani.
"Hahahaaa! Yani siku mbili tu zakuwepo hapa zimekuchosha? Hahahaha! Tulia ugonjwa ukuingie. Na leo na bonge la ugonjwa utakuumiza mnoo! Takupa huo ugonjwa kama hautoyajibu maswali tayokuuliza. Na swali moja! Hivi Sam amekuaje na nguvu hadi yakuwavunja vunja vijana wangu? Maana nakumbuka tuliwahi kumpiga sana na hakuweza kufanya chochote" Lucas aliuliza swali lile, akitegemea kutuliwa mzigo ule wa mawazo aliokuwa ameubeba kichwani mwake. Hilo ndio swali lililokuwa linauchemsha ubongo wake mda wote.
"Hahahaha! Ameshaanza kukupa presha et eeeh! Hahahaha! Kama swali ni hilo nakujibu. Sam bwana alikuwa hivyo hivyo sema hakutaka kujionesha kwa sababu hapendi ugomvi ila kwa ulichokifanya umeviamsha vilivyo lala, umemchokoza pakubwa sana na utaona makucha yake. Unataka maelezo mengine yaziada? Au yametosha?" Alihoji Binti yule akiongea kwa nyodo.
"Kama kuna maelezo mengine yoyote unaweza kuendelea." Alizungumza Lucas akijiseti sawa.
"Sina maelezo mengine zaidi ya hayo." Alisema binti yule.
"Sasa nimeshajua tawauwaje wote, maana mmejigawa gawa. Na wewe ndio chanzo cha yote haya."
"Heeeeh! Kumbe bado unawaza kuuwa? Kwakosa gani hadi utake kuwauwa? Kama kukupiga risasi, Rey alikuwa anajihami ili usimdhuru ndiomaana hakukuuwa. We shetani mkubwa." Alisema binti yule akiwa ameyakodoa macho, akimtazama Lucas, alimuona kama binadamu wa ajabu mnoo! Binadamu mwenye roho mbaya.
"Oooh! Recho! Nataka nikwambie kitu, mzazi wako mmoja nilihusika kumuuwa kipindi hicho, japo nilikuwa mdogo na nilikuwa bado sijajua kama niliyemuuwa kipindi kile ni mzazi wenu ila hivi karibuni ndio nimejua. Bado nyie tu kuwauwa, sipendi mzaha mimi, ni dharau kubwa mwili wangu kuguswa na risasi, ni lazima niwafyeke wote pamoja na mtu na mtu wake. Hahahahaaa!!." Lucas alicheka.
"Lucas unasemaje?.. Uliuwa nini? Shetani mkubwa wewe nikitoka hapa nahakikisha nakuuwa, Aaaaaaah." Alisema aking'aka kwa hasira huku machozi yakimtoka.
"Kosa la kwanza nilifanya mimi, ila kosa la pili umefanya wewe na sipendi kufanyiwa kosa lolote hata kama nimekuanza mimi. Yani unanikimbia tena na pesa zangu? Halafu nakufata huko, wifi yako anajifanya kunipiga risasi? Aisee! Lazima mlipe kwa hicho." Alisema Mr Lucas akiinuka na kumlengeshea bastola binti yule aliyeitwa Recho, akafyatua risasi...
USIBANDUKE.
RIWAYA: BOX LA NINJA
MTUNZI: MAULID KIFUMBE (MR ROY)
Sehemu Ya 3
SONGA NAYO.
Mida ya asubuhi, yalionekana mataili ya gari yakiikanyaga lami, kwa mwendo wa mdedeso. Ndani gari ulisikika mziki wa aina ya bongo fleva, aliyekuwa ndani ya gari alihusudu sana aina hii ya mziki, ulimkonga roho yake vilivyo. Jana yake alipita kwenye hiyo Barabara akiwa anapiga wimbo mwingine tofauti na huu, japo kwenye mziki huu muhusika alikuwepo. Wimbo uliitwa 'Nakupenda' Msanii alikwenda kwa jina la Jay Melody.
Wakati huu safari yake ilikuwa ndefu kidogo, aliichepuka njia aliyoipita jana yake, akapita kwenye njia nyingine ya vumbi. Wakati huu aliseti wimbo usijirudie rudie. Kwenye list ya Ngoma zile hakukuwa na nyimbo za kizungu wala amapiano, ilikuwa ni Bongo Fleva Pure, ndio mziki alioukubali.
Safari yake ilienda mpaka kwenye msitu mkubwa, gari ilizidi kupenya kwenye njia iliyokuwa inazama msituni zaidi. Ulifika ukomo wa gari kuendelea kusonga mbele, akaizima gari na kushuka. Aliruka sarakasi kadhaa, alipotulia akaonekana na muonekano mwingine kabisa. Muonekano wa kininja, Aliruka juu kwenye moja ya mti, kwa kasi ya ajabu akahama kwenye mti ule akahamia kwenye mti mwingine, alikuwa mwepesi zaidi ya nyani.
Alizidi kuhama kwenye miti ile akisonga mbele, kwa mbele akaona mji uliojengwa kwa mzunguko na kuacha kati kati mbuga, kama nyumba za kichina. Alishuka chini, na kusogea mbele taratibu kwa umakini mkubwa. Aliwaona walinzi, wakiwa wametanda kila eneo, ila yeye alikuwa mjuzi zaidi ya wale wote walinzi. Alikuwa anapita karibu yao bila kuonekana, alipita kwa nyuma nyuma, mpaka kwenye moja ya dirisha, akalifungua na kuzama kwenye moja ya chumba. Akatua chini, haukusikika mshindo wa kutua kwake, alikuwa mwepesi mnoo. Mbele alimuona mtu amekaa kwakuikalia miguu yake, kama vile anaswali, au anafanya meditesheni.
Bila kusubiri akazipiga hatua akamsogelea, akaruka teke ili amtwange ya kichwa. Ila mtu yule aliinama chini teke likapita juu, akarusha teke lingine la chini chini, yule mtu akaruka kwa juu, teke llikapita chini. Akatoa silaha aina ya Star, akazirusha kwa yule mtu, yule mtu alipiga sarakasi akazikwepa zote. Ile ninja anashangaa! Akapokea teke la shavuni, likamyumbisha, kidogo adondokee chini. Akasimama imara, akazipanga ngumi ulipigwa mkono wa maana, ilisikika milio ya mifupa ikigongana. Ninja pembeni aliona panga akachomoa, kisha akamsogelea yule mtu, alirusha panga kwa ustadi mkubwa ila yule mtu alikwepa vyema alikuwa mjuzi haswa. Naye aliona panga pembeni ila hakutaka kuutumia, aliendelea kukwepa huku akipenyeza pigo kadhaa kwenye mwili wa yule ninja pamoja na kutumia mkono tu ila alikuwa moto wakuotea mbali, ninja alianza kuzidiwa.
Mara ghafla! Wakazama ndani ninja sita, wote walishtuka! Yule mtu na yule ninja. Wakasogeleana na kupanga mstari mmoja. Wale ninja wakawarushia silaha mfululizo, ila wakazikwepa kwa kasi. Wakawasogelea huku wakizidi kurusha zile silaha aina ya Star. Kosa walilofanya nikuwasogelea, walitembezewa kipigo cha mbwa koko. Sekunde kadhaa walikuwa chini wakiugulia maumivu, wengine wakafariki, akabakia mmoja tu anapumua na waliacha kumuuwa kwa makusudi. Yule mtu aliyekula chumvi nyingi, alimsogelea na kumfunua usoni.
"Nyie ni kwani nani na mnataka nini?" Alitupa swali kwa yule ninja.
"Hauna haja yakutujua ila jua tu, tunataka ramani na funguo" Alisema yule ninja akiwa hoi.
"Ramani na funguo! Nyie mmejuaje?" Alihoji mtu yule, lakini yule ninja alifariki.
"Sam! Hii kazi siifanyi tena." Alisema yule mtu akimsogelea ninja aliyemuita kwa jina la Sam.
"Kwanini Master Chen?" Alihoji yule ninja akijifunua usoni.
"Hebu sogea umuone huyu mtu." Alisema Master Chen na Sam akasogea mbele kumtazama mtu yule.
"Kama vile sura inakuja kuja, ila sikumbuki nilimuonea wapi." Alisema Sam akizipiga hatua za kurudi nyuma hadi aliposimama Master Chen.
"Ulimuona hapa hapa! Ila aliondoka bado hajaiva vizuri."
"Oooh! Sasa nimemkumbuka! Na vipi mbona amesema Ramani na funguo! Kuna nini?" Alihoji Sam akimtazama Master Chen, mzee mwenye asili ya kichina, pamoja na umri wake kwenda lakini bado alikuwa ni moto wa kuotea mbali.
"Usiwe na haraka utajua tu, ila naona kuna hatari kubwa inakuja mbele, inanifanya nisiamini mtu na niachane na hii kazi." Alisema Master Chen akiwa amevalia mavazi ya kichina.
"Sioni kama ni jambo jema kuacha." Alisema Sam.
"Katika wote waliokulia kwenye mikono yangu, ni wewe tu ndio uko upande wangu. Nawezaje kukuza watu wanaotaka kuniuwa baadae?." Alisema Master Chen akizipiga hatua zakuzunguka kwenye chumba kile.
"Nimekuelewa Master, vipi hawa vijana unao wakuza utasitisha zoezi hilo." Alihoji Sam.
"Kuna wengine nakula hela za wazazi wao, inabidi tu hawa wawe wa mwisho. Mi kinachoniumiza na kunikatisha tamaa ni kuona watu ambao hawalipi hela, ambao nawaokota na kuwasaidia tu, ndio wanakuwa watu wabaya, wanaingia kwenye makundi makubwa ya kiharifu kama huyu kijana. Bado inanipa hofu kwa hawa wengine ndiomaana nataka nisitishe zoezi hili." Alisema Master Chen.
"Kwa jinsi ulivyoelezea nimekuelewa vyema, ni sawa pia ukifanya maamuzi hayo."
"Naona leo umekuja kunisalimia." Alisema Master Chen akikaa alipokuwa amekaa mwanzo, na Sam akamfata na kukaa pembeni yake.
"Nafikiri miezi mitatu sasa imepita, toka mara ya mwisho kuonana. Tuanzie hapa kwanza, we ulikuwa ushanijua? Na kama ulikuwa ushanijua, ulinijuaje? Maana walipoingia wale ukawa upande wangu badala yakunijumlisha kama adui."
"Wakati dirisha linafunguliwa, nikawa tayari kwa lolote, ila ulipotua chini nikajua ni wewe. Nilijua kwa jinsi ulivyotua na harufu yako. Nimekulea tuko ukiwa mdogo, naachaje kukujua?. Naona kiwango kinapungua sijui ndio umelegezwa na mapenzi au ndio haufanyi mazoezi." Alihoji Master Chen.
"Kweli kuna kipindi, nilikuwa sifanyi mazoezi ila Kwa Sasa nafanya sana."
"Sawa, kuna kitu nataka nikwambie, hiki kitu ni maisha yako mwenyewe, ni siri nzito sana." Alisema Master Chen kisha akakaa kimya kwa sekunde kadhaa. Sam Alipatwa na shauku yakujua siri ile.
Upande mwingine, alionekana mzee wa makamo, akizipiga hatua za taratibu bila wasi wasi, mikono yake aliishikanisha kwa nyuma. Alipita kwenye njia ya vumbi, mawazo yaliyokuwa yamejazana kwenye kichwa chake hayakumfanya kuifikiria sana safari ile, ufahamu wakujua wapi anaenda ulikuwepo. Ila umakini wa safari ile ulikuwa kando na yeye. Alizidi kuirusha rusha miguu yake, kama mtu aliyejikatia tamaa ya maisha. Hata muonekano wake pia ulionekana vile, alikuwa kama mtu mwenye shida mnoo na pesa, maana nguo alizovalia zilikuwa shagala bagala.
Macho yake aliyatazamisha chini, aliuona mchanga, ila hakuwa na umakini nao. Alishtuka! Ni baada yakuona kitu kinafumuka kutoka chini ya ardhi, likaruka vumbi. Alijua amechelewa kuweka umakini, aliona kitu cha kumsaidia kwa sekunde zile ni kufumba macho huku akirudi nyuma. Kwa asilimia kadhaa wazo lile lilibeba uhai wake, kama mchanga ule ungemuingia machoni, shughuri yake ingekuwa pevu, wezekana ingeishia pale.
Katikati ya lile vumbi, akahisi mlio wa kitu kikija kwa kasi, akainama chini, akasikia kikipita juu. Mara akasikia kama vitu vingine vinakuja, akafumbua macho kidogo, akaona silaha za kininja zikija kwa kasi mnoo. Umakini wote akauweka pale, alizikwepa upesi upesi. Alikuwa mwepesi tofauti na muonekano wake wakukimbilia uzeeni. Vumbi lilikuwa limepungua, akayafumbua macho vyema. Aliona mbele yake maninja sita wakiwa wamesimama kwa mstari, kila mmoja alikuwa anarusha silaha. Uwezo wake wakukwepa ndio uliomuweka hai hadi mda ule, silaha zile zilikuwa na sumu, ikikuchoma moja tu, kupona ni ngum. Alilijua swala lile ndiomaana alikuwa makini kuzikwepa. Wale maninja sita walimsogelea, na, kuanza kumshambulia kwa teke na ngumi, hawakumjua vizuri na hata kama waliambiwa kuhusu yeye, walipewa nusu maelezo.
USIBANDUKE.
RIWAYAA: BOX LA NINJA
MTUNZI: MAULID KIFUMBE (MR ROY)
Sehemu Ya 4
SONGA NAYO.
Kwanza tabasam lilishamili kwenye shavu lake, maana moyo wake ulidunda kwa furaha ya kukutana na mchezo aupendao. Aliumisi sana mchezo ule mtam kama asali. Alikuwa anaucheza kila siku, lakini haukuwa wa mashindano yakuondoa uhai kama huu aliokutana nao safari hii. Alisimama wima bila kimuhe muhe cha aina yoyote. Wale ninja walimzunguka, wakamuweka mtu kati. Mikwala ilishika nafasi yake, walirusha kitu kama bom pembeni, ukatanda moshi eneo lile lote. Njia ile haikuwa na watu kabisa! Na haikuwa kawaida, huwenda waliona balaa lile wakashindwa kupita njia ile.
Mbwembwe za kininja ziliendelea, huku wakirusha teke za kila aina. Hadi mda huo mzee yule hakuwa amejibu pigo lolote, aliendelea kukwepa mapigo yao. Fikra zilimpeleka kama vile yuko shambani anatafuta kuni, kuni zingine zilikuwa ngum kukatika. Alipiga kifuti akavunja mkono wa mtu, akamshika mwingine maeneo ya shingoni, akamvunja. Ulisikika mlio wa mfupa ukilia, alimkwida mwingine akampiga kichwa, ulisikika mlio 'Paaaah!!." Aliyumba, akashindikizwa na ngumi ya shingo, akadondoka chini. Na malaika mtoa roho akafanya kazi yake, iliyomleta duniani. Mwingine akamtwanga teke kwa sarakasi ya kinyume nyume.
Mzee alishika ndevu zake, akazitachi tachi kidogo, kisha akaruka teke iliyotua kwenye uso wa ninja mwingine, kabla hajafika chini, akamtandika lingine. Mmoja aliyebakia akataka kutumia mpango wa kininja, ili kutoweka. Yeye ndio alikuwa mwalim wa zile kazi, alimzimisha upesi, akamtwanga na ngumi ya shavuni, ikamtupa chini na kulala chali. Mzee akamsogelea taratibu, akainua mguu wake na kumuwekea shingoni.
"Nyie ni wakina nani na mnataka nini kwangu?" Alihoji Mzee.
"Mzee Tich! Haina haja yakutufahamu, ila tunataka Ramani na funguo." Alisema yule ninja kisha akaiaga dunia nzuri yenye watu wenye roho mbaya.
"Ramani na funguo!.. Ndio nini sasa au wamekosea mlengwa sio mimi? Hapana ni mimi maana ameniita jina langu! Kama ni mimi hizo habari za Ramani na funguo mi zajulia wapi?" Mzee Tich alizama kwenye dimbwi la mawazo ghafla, alijikuta anadumbukia mazima maana muokozi mwenyewe alikuwa ameshafariki. Aliduwazwa na kauli ya ninja yule.
Aliutoa mguu kwenye shingo ya yule ninja, kisha akazipiga hatua za taratibu kuendelea na safari yake.
*********
"Ndio huyu unayemuaminia! Anaiweza hii kazi kweli?" Ndani ya mjengo ilisikika sauti ikitoka na mwangwi, sababu sauti hii kutoka hivi nikutokana na jumba lile kutokuwa na vitu ndani, kulikuwa patupu. Walisimama wanaume wawili mstari mmoja, akasimama mbele yao mwanaume mwingine. Alikuwa kama mwalimu anavyowakaguwa wanafunzi wake. Bwana yule baada yakuwazunguka na kuwauliza swali lile, alirudi mbele akamtazama mtu aliyemuuliza swali, ajibu.
"Kiongozi! Huyu bwana ametoka kufanya mauwaji ya waziri jana tu. Ameshafanya kazi nyingi mnoo za hatari hata mbunge aliyefariki hivi juzi juzi, yeye ndio aliyemuuwa." Alieleza mtu yule.
"Hilo ndio swali nililokuhoji?" Aliuliza akimkazia macho.
"Namuamini! Na kazi hii anaiweza vyema." Alijibu.
"Alex Sinio! Huyu mtu anaitwa nani?" Alihoji bwana yule akiendelea kuweka umakini wakumuangalia na kumsikiliza.
"Anaitwa Triple X!.."
"Basi!. Inatosha. Nielezee jina lake hasilia." Alihoji akiendelea kumtazama mtu aliyemleta.
"Mr Lucas! Umeniita hapa kufanya kazi au kujuana majina? Kwanini usiniulize mwenyewe? Kama hakuna cha maana sioni haja yakuendelea kukaa hapa." Alisema Triple X, Akizipiga hatua zakuelekea mlangoni. Mr Lucas akamshika mkono.
"Hujui nilichokuwa nakilenga. Shika hii picha! Huyu ndio unatakiwa kumuuwa." Alisema Mr Lucas, akimkabidhi picha Triple X.
Triple X baada yakuipokea ile picha, alionesha kushtuka kidogo! Alihisi aliona vibaya, akakaza macho kuitazama vyema ile picha.
"Mbona unashangaa unamfaham?" Alihoji Mr Lucas, badala yakujibiwa naye akaulizwa swali.
"Huyu ndio natakiwa kumuuwa?" Aliuliza swali la kipuuzi kweli.
"Kwani we ni mbovu wa masikio? Wakati nakupa picha nimesemaje?" Mr Lucas alimuhoji.
"Haina haja ya picha, namfahamu vyema. Nachohitaji niongezewe malipo na mahali anapopatikana kwa sasa." Alisema Triple X akitaka kuzipiga hatua za kuondoka mahala pale.
"Tulia! Unaenda wapi wakati bado naongea? Sikia hiyo hela ambayo utapewa inatosha sana, maana huyu kijana uwezo wake ni mdogo sio mkubwa kiasi chakuongezewa hela." Alisema Mr Lucas akimtazama Triple X.
"Kama uwezo wake ni mdogo, basi sawa kazi mtaifanya wenyewe!" Alisema Triple X akielekea mlangoni, akafungua mlango akatoka.
"Mkuu! Mbona umemuacha aende? Unajua kumpata ni ngum na hatuna namba zake, muongezee tu hizo pesa." Alisema Alex Sinio akishangaa maamuzi ya mkuu wake.
"Muache aende, kwanza anakiburi sana anataka kunipanda kichwani, hatuwezani, hii kazi mtaifanya wenyewe haina haja yakukodi mtu. Mkimaliza kunywa chai jikusanyeni muende mkamtoe duniani." Alisema Mr Lucas akizipiga hatua za kuelekea kwenye moja ya chumba.
"Sawa mkuu." Alijibu Alex Sinio.
Mr Lucas akiwa ameshika kitasa ili akazame ndani, akakumbuka kitu, akamtazama Alex Sinio.
"Mkamuwekee chai na yule kidem jau. Maana tokea jana nilipompasha ukweli na kumtishia kumpiga risasi, hajala chochote." Alisema Mr Lucas akizama ndani, na Alex Sinio akatii agizo lile.
*********
Mkao waliokaa, kama vile chakula kiko mbele yao, wanajiandaa kwaajili yakuishibisha minyoo iliyoko tumboni. Tatizo utulivu wa nafsi ulitoweka ghafla, shauku kubwa ilitanda ndani ya nafsi. Alitakiwa kutulia, lakini ukimya ule ulimuondolea hali hiyo, alitamani kuuliza swali, na uvumilivu ulimshinda maana ukimya ulienda kwa dakika mbili, kwake aliona ni mda mrefu kwa shauku iliyojengeka ndani ya nafsi yake.
"Siri gani hiyo unataka kuniambia Master?" Sam alimuuliza swali Master Chen.
"Unajua sasa hivi siamini mtu yeyote zaidi yako muhusika? Basi staki asikie mwingine. Tuliza kichwa chako na nafsi yako, fumba macho, usijifanye kusahau mtindo huu, fanya kama nilivyokufundisha, toa tamanio lilioko moyoni mwako, ipe nafasi nafsi yako itulie hapo ndio utanisikia nikiongea. Nilikuwa nishaanza kuongea ila nilijua hujasikia chochote kutokana na kimuhe muhe ulichonacho." Alisema Master Chen na Sam akaelewa sasa, taratibu akatuliza hali aliyokuwa nayo, sasa nafsi ikatawaliwa na utulivu wa hali ya juu. Utulivu ambao uliwezesha kusikia kitu chochote kinachocheza mule ndani, kwa hali ile hata mdudu iliwezekana kumsikia akitembea ndani mule. Master Chen alianza kuongea kama vile anatikisa mdomo tu hasemi chochote, ila Sam alimsikia vyema kama vile anatoa sauti. Alielezea mwanzo mpaka mwisho, kisha wakatoka kwenye hali ile. Sam alishtuka! Baada yakutoka kwenye hali ile na kukumbuka ile story aliyoambiwa na Master Chen, ile story ilimuuma mnoo! Alijikuta anatokwa na machozi bila kutarajia.
"Pole! Najua inauma ila vumilia usiwaze sana." Alisema Master Chen na Sam akaipokea pole ile kwakitikisa kichwa.
"Naweza kuondoka sasa." Alisema Sam.
"Huu mkao usiutoe, utendee haki." Alisema Master Chen mara mlango ukagongwa, akaruhusiwa kuingia, na kijana mmoja akaingia na chakula pamoja na chai akaiweka pale mbele yao kisha akaondoka na kuufunga mlango.
"Haya utendee haki mkao huo, nadhani unakumbuka kula kwakutumia hizi fito zakikwetu china."
"Siwezi kusahau" Alisema Sam na wakaanza kula. Walipo maliza, akaaga na kuondoka.
Nyumbani kwa Sam, uliibuka ugeni ambao haukutarajiwa, ugeni wa ghafla. Nje ya nyumba walitanda watu kadhaa. Mke wa Sam alikuwa ndani, alikuwa anasikia mlango unagongwa, wazo lake lilimtuma ni mme wake Sam, lakini alikumbuka Sam alienda na gari, angesikia honi. Na kingine haukugongwa mlango wa getini, uligongwa mlango wa nyumba, wakati anakumbuka alilifunga geti, aliwaza mtu yule alipitaje getini? Alisita kwenda kufungua.
"Fungua mlango sisi ni mafundi" Ilisikika sauti ikitamka kauli ile. Mke wa Sam akashusha pumzi ndefu, akakumbuka kuna fundi alimuita. Akaenda kufungua mlango.
Baada yakufungua alishtuka! Alirudi nyuma akinyoosha mikono juu baada yakunyoshewa bastola na mtu aliyekuwa anagonga. Walizama ndani wanaume watatu. Mke wa Sam alionekana kuogopa, mwili wote ulikuwa unatetemeka, alidondoka chini kwa uoga, alipiga magoti huku akiomba asiuwawe.
"Mrembo! Sio mbaya ukinijua jina langu, naitwa Alex Sinio, tunamuhitaji mmeo. Kama hayupo tuambie ameenda wapi, sivyo tunakubaka wote kisha tunakuuwa atakuta maiti hapa inatoa dam." Alisema Alex Sinio akimkazia macho mke wa Sam ambaye alikuwa anatetemeka isivyo kawaida, alikiona kifo mbele yake...
USIBANDUKE.
RIWAYA: BOX LA NINJA
MTUNZI: MAULID KIFUMBE (MR ROY)
Sehemu Ya 5
SONGA NAYO.
Vitisho viliendelea, wote walizikoki bastola zao, wakimtaka aseme mme wake alipo. Ila mke wa Sam akafumba macho, huku akiwa umeinua mikono juu mwendo wa mateke. Alikuwa amevaa kagauni kakujiachia maana alikuwa ndani mwenyewe, hata taiti aliyoivaa kwa ndani ilikuwa fupi sana, ilifunikwa na kagauni kalikoishia mapajani, umbo lake lilivutia sana. Baada yakuona hasemi chochote amefumba tu macho akilia, Alex Sinio alimtazama kwenye mapaja yale meupe na umbo lake, akapatwa na matamanio, akampa bastola mwenzake. Yeye akainama alipopigia magoti na kuanza kuyapapasa yale mapaja malaini. Alimsukuma pale kwenye malu malu, mke wa Sam akalala chali, hali iliyompelekea kupandwa na mizuka zaidi baada yakuona mlalo ule aliolala. Mke wa Sam alikuwa bado amefumba macho akisikilizia anachofanyiwa huku machozi yakimbubujika. Alex Sinio akaanza kufungua mkanda wa suruali yake huku akikapandisha juu kagauni ka mke wa Sam, na wenzake wakaziweka bastola pembeni na kuanza kufungua mikanda ya suruali zao. Walijua akishatoka Alex Sinio wataingia wao, ndio kosa kubwa walilolifanya.
Huu ndio wakati uliosubiriwa kwa hamu na mke wa Sam. Alisikia mikono ya Alex Sinio ikitalii mapaja yake, alikuwa amefumba macho lakini alikuwa anaona kwa mbali, alishuhudia walivyoweka bastola zao pembeni. Ndio wakati aliokuwa akiusubiria.
Alirusha teke za upesi upesi, akiwa amelala vile vile chali, teke moja ikatua kwenye familia ya Alex Sinio na nyingine ikatua vyema kwenye kidevu chake. Wakati wale wenzake wanasogea kuzichukua bastola, Mke wa Sam aliiweka mikono yake kwa chini, nyuma ya shingo, akajibinua na kuinuka upesi. Akaruka sarakasi juu juu miguu akiitanua, akawatwanga teke za vichwani, wote wakaenda kujibamiza kwenye ukuta. Hakutaka kulembesha mwandiko aliwafata na kuachia teke za mfululizo staili ya Van Damme ya kinyume nyume. Aliwatepetesha kisawa sawa, akamrudia Alex Sinio aliyekuwa pale chini ameshikilia sehem ya familia yake, akiugulia maumivu.
Mke wa Sam alimkwida shingo, akamuinua juu juu kisha akamtwanga kichwa kitakatifu, akamuachia. Alex Sinio alihisi wadudu wanalilia kichwani mwake, alihisi kizungu zungu aliyumba yumba, akashindikizwa na ngumi ya shavu, akadondokea kwenye sofa zilizokuwa pale pembeni. Alikuwa hoi hajielewi, hata kuona aliona mawenge mawenge. Baada ya dakika moja ndio akaanza kuona ona japo sio sana, alimuona Mke wa Sam akiwa amesimama mbele yake, akisubiria aone vizuri. Baada ya mda aliona vyema japo alikuwa hoi sana.
"Naitwa Rey Lii nakili sura hii, popote utakapoiona kaa nayo mbali. Staki mnirudishe nilipotoka, mnaweza kuinuka na kuondoka." Alisema Rey Lii. Alex Sinio kusikia kauli ile, akajiinua hivyo hivyo kibishi akatembea anayumba yumba. Na wenzake wakainuka wakiwa hoi, wakaondoka ndani mule, hawakuamini kutoka wazima, hata bastola zao walizisahau.
Rey Lii aliufunga mlango kisha akaenda chumbani, akaichukua simu yake na kuipigia namba iliyoandikwa mme wangu.
Wakati huo Sam alikuwa ndani ya gari akiendesha, ndani ya gari kama kawaida ulisikika mziki wa bongo fleva, alikuwa na mawazo rundo, aliamini mziki ule utampa faraja, ndio ulimpa faraja lakini haikuwa sana, bado alikuwa anawaza sana kuhusu maneno aliyoambiwa na Master Chen. Alijiuliza maswali mfululizo na alijua kabisa hakuna wakumjibu maswali yale hata kule alipotoka kwa Master Chen asingeweza kujibiwa, ndiomaana hakutaka kuuliza. Fikra zilimpeleka mbali mpaka akawa anajisahau kama anaendesha gari. Alishtuka! Ni baada yakuhisi kuna kitu kinamtekenya mfukoni, akatoka kwenye chumba kile cha mawazo, akarudi sehemu mwili ulipo. Alisikia mlio wa simu, ilimaanisha ilikuwa inaita. Mkono wa kulia ukiwa umeshikilia usukani wa gari, mkono wa kushoto akaushughulisha kuifanya kazi yakuichukua simu kutoka mfukoni. Tabasam lilishamili mashavuni baada yakuona namba ya mpigaji.
"Hello my wife!" Aliongea baada yakuipokea simu na kuipeleka sikioni.
"I miss you My King" Ilisikika sauti tam na laini ikitamka maneno hayo.
"Mmmh! Saivi tu umenimisi jamani?"
"Masaa matatu kwangu ni mwezi, na pia kuna kitu kimechangia nikumisi." Aliongea Rey kwa sauti ya mideko.
"Kitu gani? Penzi langu au?" Alisema Sam akiendelea kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu.
"Kugawa mkong'oto pamoja, kama kipindi kile."
"Mmh! Usiniambie kuna mtu umempa mkong'oto?" Sam aliongea akitabasamu.
"Kuna panya watatu walikuja hapa et wanamuulizia paka dume, et wanataka wamuuwe. Nikawaambie nipo mimi paka jike mdili na mimi kwanza, mkinimaliza ndio mtamfata huyo dume. Mawazo yao wakafikiri wataniweza, wamepokea kipondo mpaka wamekimbia." Alisema Rey kwa njia ya utani.
"Hahahaha!. Tatizo hawajui mke wangu nilikutolea wapi ndiomaana wanakuchukulia poa sana. Mi nahisi ni yule yule uliyempiga risasi ndio anatusakama. Nahisi pia hata mdogo wangu Recho atakuwa kwenye hatari maana hata namba zake hazipatikani." Alizungumza Sam akiwa amepatwa na wasi wasi.
"Ila kweli maana na mimi nishamtafuta simpati sema nilisahau kukuuliza." Alisema Rey.
"Sawa kuwa makini sana." Alisema Sam
"Usijali mume wangu nadhani unanijua vyema, ondoa hofu. Haya niambie unaenda wapi sasa hivi?"
"Nimetoka kwa Master wangu hapa ndio naelekea kazini sasa."
"Oooh sawa, halafu nataka nimuone huyo Master wako maana unamuongeleaga sana halafu hata sijawahi kumuona"
"Sawa usijali takuletaga siku moja umuone, ila naomba unikatie simu, boss wangu Mr Donald ananipigia nahisi kwa sababu hanioni kazini." Alisema Sam na mke wake akakata sim. Akaipokea simu ya boss wake Mr Donald.
"Sam uko ofisini?" Ilisikika sauti nzito ikihoji.
"Hapana boss! Sipo ofisini nilipata dharula kidogo, ila sasa ndio naelekea."
"Basi usiende huko njoo hapa kwangu kuna sehemu nataka twende."
"Sawa boss, dakika kadhaa tu takuwa nishafika." Alisema Sam, na simu ikakatwa, akaongeza spidi ya gari.
************
Zilisikika sauti nyingi, zikiongea kwa pamoja na kwa neno moja. Ungesema zilikuwa zinaimba wimbo, lakini hakukuwa na vina kwenye maneno yale wala mdundo. Kwakukadiria sauti zile zilikuwa zinatoka kwenye vinywa vya watu wanaozidi mia mbili. Sauti ya mtu mmoja ilisikika ikichengana na zile zingine, ya kwake ilianza kutamka neno fupi tu. Na wale wengine walilitamka lile neno vile vile kwa pamoja. Ilikuwa katikati ya mji, ulionekana uwanja mkubwa na watu wale walionekana wakisimama katikati, wakiwa wamejipanga mistali uliyonyooka. Yule mmoja alisimama mbele yao, aliinua mguu juu na wengine walifatiliza alichofanya yeye. Wote walivalia tshet nyeupe na chini walivalia suruali nyepesi yenye rangi ya weusi. Walielekezwa staili ya mapigano na wao walifatiliza staili zile.
Karibu na mlango juu ya ng'azi, alionekana Mzee mmoja aliyeonekana kula chumvi kwa kiasi frani, kwakumtazama alikuwa na miaka hamsini na kitu. Alivalia nguo nyeusi iliyokaa kama gauni ilishuka mpaka chini, mikono yake aliiweka nyuma akitazama staili zile za mapigano. Nyuma yake alikuja mtu akasikika akiongea.
"Master Keti! Hakuna aliyerudi hata mmoja."
"Gasi! Inamaana vijana kumi na mbili wote hamna hata mmoja aliyerudi kuleta ripoti?" Alihoji Master Keti.
"Ndio mkuu! Nahisi wameuwawa wote, maana wale watu sio wa mchezo mchezo."
"Sikupingi maana wewe ndio uliyelifufua hili swala na wewe ndio unawafahamu vyema, maana mi nilikuwa nishasahau kabisa maana nilishindwa wapi pakuanzia na pakumalizia. Ila naimani hii kazi tutaifanikisha kabla ya hali yetu kiuchumi haijashuka sana." Alisema Master Keti.
"Sawa mkuu ripoti ndio hiyo mi naenda"
"Subiri! Triple X tokea jana hajaonekana hapa! Atakuwa wapi?" Alihoji Master Keti.
"Sijajua kwakweli ila kazi uliyompa aliifanya vyema kabisa."
"Sawa, kuna kazi mbili zakufanya hapa, moja imekuja yakumuuwa mfanyabiashara, na nyingine ni yangu binafsi kuna mfanyabiashara mwingine ananiumiza kichwa sana ananisumbua, nimemtafuta kwa miaka mingi, leo nimejua anapoishi, nataka auwewe. Huyu utaenda kumuuwa wewe sasa hivi, na huyo mfanyabiashara mwingine, ataenda kumuuwa Triple X, akirudi." Alisema Master Keti akimpa picha ya huyo mfanyabiashara na Gasi akaipokea.
"Anaitwa Mr Donald, ukishindwa kwa jina basi ndio utatumia kwa picha, maelezo haya hapa." Alisema Master Keti akimpa picha na karatasi. Master Keti alitazama mbele. Wote macho yao waliyaelekeza kuangalia mbele kwa mshangao! Ni baada yakumuona mtu waliyetoka kumuongelea...
USIBANDUKE.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote