Follow Channel

BREAKING HELITHA

book cover og

Utangulizi

Helitha analia kwa sauti ya chini,anajikunja kama mtu anaeumia sijui sababu ni nini lakn mungu wangu naomba isije kuwa ni hicho nachofikiria haiwezekani
“Hapana,” nanung’unika kwa hasira, nikikataa kuamini kile kinachonijia kichwani.
Lakini linaingia.
Linaenea kama saruji kwenye kila nafasi ndani yangu—na kunifanya nigande pale pale. Nimezama ndani yake, lakini sasa nimesimama tuli kabisa, nikiangalia maumivu yanavyoupinda uso wake wa malaika.
“fuck! Wewe ni—”
Neno hilo linakufa kwenye ulimi wangu. Halina maana. Halina uhalisia.
“Niangalie.”
Ninakumbatia mashavu yake, vidole vyangu vikifuta machozi yaliyoanza kupenyeza.
“Vuta pumzi. Ndani... nje... polepole, mrembo.”
Lakini hafanyi hivyo.
kucha zake zinazidi kuchimba zaidi ndani ya ngozi yangu. Inauma, lakini sioni hilo. Maumivu hayo hayafiki. Akili yangu imevamiwa na kitu kimoja tu:
Alikuwa bikira.
Na mimi—mimi ndiye niliyemvunjia. Bila hata kujua. Bila hata kujali.
“Niambie ni ukubwa wangu. Niambie nilikuwa mkubwa mno,” ninang’ona, nikijaribu kushikilia wazo hilo kama mkombozi. Lakini najua ukweli si huo. “Helitha… kwa nini hukuniambia?”
Ninapapasa nywele zake kwa upole, nikimfariji wakati moyo wangu wenyewe umejifunga kwa hatia.
“Ulipaswa kuniambia... kwamba hujawahi kufanya mapenzi.”
“Sikujua,” ananong’ona kwa shida, kila neno likitoka na pumzi nzito.
“Nilidhani niliwahi. Samahani.”
Songa nayo….

SURA YA 1-HELITHA
Ninapofumbua macho kwa shida, mwanga mkali wa unayachoma hadi kichwa kinaniuma kama kuna kisu kinachochoma ndani yake. Najaribu kufunika macho yangu, lakini mikono haiinuki — ni mizito na ganzi.
Kila pumzi ninayovuta inahisi kama vile navuta vipande vya kioo. Harufu ya dawa za hospitali inanidunga puani na kunipa mshtuko wa baridi mgongoni. Midundo ya mashine na sauti ya kiyoyozi vinafanana na muziki wa huzuni unaopigwa kwenye fidla iliyovunjika.
Niko katika hali ya kuchanganyikiwa, akili imejaa ukungu kana kwamba bado nimelala au nimeamka kutoka usingizi mzito wa mateso.
Hatimaye, ninagundua: nipo hospitalini.
Maswali yanajitokeza kichwani mwangu kama vikaragosi vinavyoruka kutoka kwenye kisanduku:
Kwa nini? Nini kilitokea? Mimi ni nani?
Lakini sina majibu. Sifahamu chochote. Hata jina langu mwenyewe limemezwa na shimo jeusi lililo katikati ya ubongo wangu.
Mungu wangu... jina langu ni nani?
Majibu yatakuja.
Lazima nitulie.
Shit.
Moyo wangu unaanza kupiga kwa kasi, mashine inayopima mapigo ya moyo sasa inalingana na hofu yangu inavyopanda. Kadri sauti inavyopiga haraka, ndivyo hofu yangu inavyo ongezeka.
“Helitha.”
Sauti ya baba yangu inakatiza kelele zote akilini mwangu kama kisu kinachokataa siagi.
Pumzi inatoka mapafuni kwa mshtuko wa ahueni. Helitha.
Ndiyo jina langu. Helitha Joseph Vaughn.
Mlango wa hospitali unafunguka kwa sauti ya kusogea, ukikata mvumo masikioni na kupunguza midundo ya mashine. Mapazia yanatikisika, na hatua nzito za viatu vya kijeshi vinagonga sakafu kwa mtindo ule ule wa zamani… ni sauti ninayoifahamu.
“ni sawa sunshine upo sawa,” anasema kwa upole. “Upo salama. Jaribu kutulia, sawa? Upo salama, nakuahidi.”
“Baba?” sauti yangu inatoka kwa shida, koo likiwa limekauka kana kwamba limetengenezwa kwa tambi zilizochemshwa mno.
“Nipo hapa,” ananijibu, akibana mkono wangu zaidi. Sauti yake imejaa hisia, iko nzito na yenye maumivu yaliyofichwa.
“Uko hospitalini, lakini uko salama.”
“Nini...” ninasema kwa tabu, nikipambana kuzungumza. Najaribu kuinuka kwa mikono yote miwili, lakini mwili wangu ni mzito mno.
“Nini kilitokea?”
Baba anakimbia kunisaidia. Anapanga mito nyuma yangu kwa upole, akiniinua polepole.
“Polepole. Usijilazimishe. Mwili wako lazima una maumivu,” anasema kwa sauti yenye majonzi. Macho yake yanang’aa kwa machozi ambayo hajayatoa bado. “Ulipata ajali ya gari.”
“Ajali?” narudia kwa mshangao, nikipiga uso wa mshangao. Kichwa changu kinazunguka, kikitafuta kumbukumbu. Lakini bado hakuna kitu. Isipokuwa jina langu… na sasa Baba. Najua mimi ni nani. Najua yeye ni nani. Lakini hiyo ajali...
“Si... siwezi kukumbuka,” nasema kwa sauti dhaifu.
“Usijali, sunshine,” anasema kwa upole, kisha ananiachia mkono na kuvuta kiti karibu na kitanda.
“Usijitese na kumbukumbu kwa sasa. Daktari alisema ni kawaida kuchanganyikiwa unapoamka. Gari lako lililipuka tairi na ukatoka barabarani.”
“Ulishuka bondeni. Gari lilipinduka mara tatu kabla ya kugonga mti.”
Ninaangalia mwili wangu chini ya shuka jeupe na gauni la hospitali. Siwezi kutambua ni wapi niliumia au kama kuna kiungo kilikosekana.
Lakini kila sehemu inauma.
Ninachezesha vidole vya miguu, na kwa mshangao, vyote vinahama. Shukrani kwa Mungu—viungo vyote vipo. Hiyo ni mwanzo mzuri.
“Ni mbaya kiasi gani?” nauliza kwa sauti ya kupoa.
“Pangeweza kuwa mbaya zaidi,” Baba anasema kwa pumzi nzito. Macho yake ya samawati sasa hayana machozi, na tabasamu la pembeni linatokea taratibu.
“Uliwahi kuwa jasiri. Na bado upo hivyo. Utaweza tu. Maumivu kidogo tu na kovu moja kubwa zaidi ya yale ya zamani.”
Anagusa sehemu ya bega langu.
“Tawi la mti liliingia kupitia dirishani... likakuchoma moja kwa moja hadi kwenye kiti.”
Sikumbuki ajali, lakini najua kitu kimoja—Baba yangu, Joseph Vaughn, hawezi kusema uongo. Wazazi wengine, hasa mama, wangeniambia “pumzika tu, usijali,” lakini si yeye.
Ninavuta pumzi ya haraka, nikigundua kitu muhimu—ninaweza kukumbuka mambo.
Si mambo ya hivi karibuni, wala ajali yenyewe, lakini kumbukumbu za zamani zinajirudia taratibu.
“Mbavu tatu zimevunjika,” Baba ananiambia huku tena akikamata mkono wangu kwa upole.
“Ulipata mtikisiko wa kichwa, kuvuja damu ndani, na kushonwa nyuzi ishirini na tisa.”
Anapumua kwa nguvu, pumzi nzito kama mashine. “Ulinitisha sana, sunshine. Nilijiona nipo nusu kaburini kwa hofu. Lakini utapona. Nakuahidi.”
Ninakubali kwa kichwa, macho yangu yakichunguza chumba. “Mama yuko wapi?”
“Mama?” anarudia kwa mshangao, uso wake ukionyesha hali ya kushangaa, kisha sura isiyoeleweka inachukua nafasi.
“Unamaanisha nini, sunshine? Mama yako...”
Anafanya sauti ya kama kucheka kwa mashaka, isiyo na maana, kisha akafumba macho kwa sekunde na kujikuna usoni kwa mkono mzito.
“Ni lazima nimwite daktari. Sitachelewa.”
“Hapana! Tafadhali usiondoke,” nasema kwa ghafla, nikinyosha mkono kumzuia.
“Siwezi chelewa, Matthews yuko nje tu. Atakuwa hapa kukuangalia.”
Anatoka nje ya chumba huku akitabasamu kwa juhudi, lakini tabasamu hilo
Baba alisema hatachelewa, lakini saa inasonga… inagonga… inagonga tena, na bado nipo peke yangu, nikiwa nimezungukwa na mashine za hospitali.
Mapigo ya moyo wangu yanapanda kadri Baba anavyoendelea kutokuonekana.
Anafanya nini huko nje kwa muda wote huu?

Endeleaa..

SURA YA 2; SHAWN

“Ni kuhusu Aalyiah,” sauti ya Romano inasema kwa ukali kupitia simu, bila hisia zozote. “tukutane cicero.”
Kisha akakata. Kama kawaida yake—ni mtu wa maneno machache.
Lakini maneno hayo machache yanatosha kufanya moyo wangu udunde kwa nguvu, damu kuchemka, misuli kukaza hadi kuuma.
Ninashikilia dawati kwa mikono yote miwili, kichwa chini, nikivuta pumzi ndefu na nzito.
Dada yangu wa miaka kumi na minane—Aalyiah—ndiye mtu wa pekee duniani ambaye nahisi kitu cha kweli kwake. Macho yake mazuri, sura yake isiyo na doa inajitokeza akilini, nikijaribu kuzuia hofu isichukue nafasi.
Romano asingeweza kuwa mtulivu hivi kama jambo baya sana lingekuwa limetokea.
Aalyiah ni kipenzi chake pia. Tunda la jicho lake. Mpango wake mkamilifu na mke wake marehemu. Mtoto pekee aliyemtaka kwa kweli. Mtoto ambaye angeutoa uhai wake kwa ajili yake.
Mimi? Mimi ni matokeo ya tamaa ya haraka tu.
Romano hakujua hata kuwa aliniacha duniani hadi nilipofikisha miaka kumi na moja—mama yangu alipokufa.
Aliniachia shangazi yangu, alimlipa kunilea, na hakuonekana tena hadi nilipotimiza miaka kumi na sita. Ilikuwa siku hiyo alipogonga mlango na kuniambia ni wakati wa “kujifunza sheria za mchezo.”
Nilitaka kumtemea mate usoni.
Lakini alikuja na zawadi... muuaji wa mama yangu.
Romano alinipeleka nje, akafungua buti la gari—na pale ndani alikuwa Francis Sawyer—mnyama aliyempiga mama yangu hadi kufa.
Akasema ni wangu. Ni juu yangu nifanye naye nitakacho.
Na nilifanya.
Katika ghala chakavu pembezoni mwa Cosa notra, nilitumia masaa kumi na mawili chini ya macho makali ya Romano, nikimtesa yule mwanaume aliyemuua mama yangu. Nilimwangalia akifa kwa mateso makali—na nilifurahia. Niliifurahia sauti ya kilio chake, na zaidi, nilifurahia kuridhika kwa uso wa Romano.
Miaka minane iliyopita, alinituma Chicago kufanya kazi chini ya Dante Carrow, akinitumia kama silaha yake ya siri—nje ya rada ya polisi.
Mlango wa ofisi yangu unafunguka kwa kelele. Hatua nyepesi za Broadway zinaingia.
“Uko sawa, Boss?” anauliza.
“Romano amepiga simu,” najibu haraka nikikaa sawa kwenye kiti.
Broadway ni mmoja wa watu wachache ninaowaamini kabisa. Ni mmoja wa watu saba tu hapa Chicago wanaojua kuwa jina langu halisi si Beckett kama jina la ukoo wa mama, bali ni Willard.
Ni siri ya ndani kabisa. Romano alitaka iwe hivyo—alitabiri kuwa kutokuwa wazi kuhusu uhusiano wetu kungekuja kuwa faida siku moja.
Na kweli, mara kadhaa imetusaidia.
“Unaonekana kama umeona mzimu, Shawn,” Broadway anasema akinitazama kwa makini ninaponyakua funguo za gari kutoka mezani.
“Alinitajia tu Aalyiah,” namwambia. “Wewe utabaki hapa. Hakikisha kila kitu kinaendelea vizuri. Nipatie ripoti kila jioni… na usiharibu.”
Anatikisa kichwa kwa utii, uso wake ukionyesha uzito wa jambo hili.
Nikiwa na simu sikioni, natoka ofisini nikishuka kwa lifti binafsi hadi eneo la chini la maegesho.
“Najua,” Dante anajibu mara simu inapoingia. “Romano alinishirikisha kabla hajakupigia.”
“Basi labda unajua zaidi yangu,” nashusha pumzi kwa huzuni, nikihisi hofu ikitembea nyuma ya shingo yangu. “Nitakupatia taarifa nikiweza.”
Anatoa sauti ya kukubaliana upande wa pili wa simu.
Nimefanya kazi na huyu jamaa kwa miaka minane sasa, kwa hiyo namtathmini kichwani kwa urahisi—akiwa ndani ya Delta, ameketi kwenye stoo ya VIP, macho yake ya kijani yaliyokomaa yakimfuatilia mke wake, ingawa ana walinzi wakubwa wanaomfuata kama mbwa wa doria.
“Jihadhari,” Dante ananambia kabla hajakata simu. Hajawahi kuwa na imani na baba yangu.
“Daima nipo makini,” najinong’oneza, kisha nainua simu na kuitupa kwenye kiti cha abiria.
Ninavuta mafuta kwa nguvu, tairi zikilia ardhini huku nikiliondoa gari langu kwa kasi kutoka kwenye maegesho ya chini.
Endeleaa…

SURA YA 3- HELITHA

Saa nzima inapita kabla muuguzi mmoja kuingia chumbani kwangu, akiwa na tabasamu la upole usoni. Lakini haligusi macho yake. Ni tabasamu lakulazimisha—huruma ya mazoea.
Hata hivyo, uwepo wake unanizuia nisipate mshutuko kamili wa hofu. Machozi yanazidi kunigubika, yakiongeza hali ya kutokuwa na msaada. Mimi si mtu dhaifu kwa kawaida.
“Baba yangu yuko wapi?” nauliza kwa sauti ndogo, nikiminya kona ya shuka kwa vidole, nikikunja pembeni kama mkunjo wa kipaza sauti.
“Yuko na daktari wako. Hawatachelewa,” anajibu kwa upole. “Unahitaji kitu chochote, mpenzi?”
“Dawa ya maumivu, tafadhali. Kichwa changu kinanifanya nihisi kama kinapasuliwa.”
“Ah, bila shaka. Ngoja...” Anakata maneno, akichungulia clipboard iliyo chini ya kitanda changu.
Anapindua kurasa chache, akipitia maandishi yaliyopo, kisha gafla anatoa simu yake na kuanza kupiga picha rekodi zangu za matibabu.
Ninakunja macho kwa mshangao...
“Nahitaji kuviweka kwenye mfumo,” anasema.
“Ah... sawa.”
Ninajaribu kujiegemeza zaidi kwenye mto lakini maumivu ya bega lililoteguka yanachoma ghafla, yanifanya niache haraka.
“Kitufe cha kumuita muuguzi kiko wapi? Sijaweza kukipata.”
Anazunguka kitandani, akitabasamu tena kistaarabu, kisha anakichukua kitufe kutoka sakafuni.
“Lazima kilianguka ulipokuwa ukijigeuza.”
Anaangalia viwango vyangu vya afya kwa haraka, kisha anavuta chuma cha dripu karibu na kuanza kufanyia marekebisho, kabla hajaniwekea mito vizuri mgongoni.
Lakini... Baba yangu alifanya vizuri zaidi.
“Maumivu yatapotea hivi karibuni,” anasema kwa sauti nyembamba kama mpira wa bubble gum. “Pumzika tu.”
Macho yangu yanaanza kuogelea. Kichwa kinaning’inia kulia na kushoto, najaribu kumtazama muuguzi kwa ukali, nikijaribu kupambana na usingizi unaoninyemelea kwa kasi kama wimbi.
Kope zinashuka, mikono yangu inaachana na shuka, mkunjo niliokuwa nikiushikilia ukifunguka...
Siwezi hata kuinua kidole kimoja.
“Nini...?” ninabembeleza kusema, lakini sentensi inakatika, ikitumbukia kwenye shimo lile lile ambako kumbukumbu zangu zimezama.
Ninapumua kwa ahueni, nikitambua maumivu yamepotea.
Dawa wanazonipachika kwenye mishipa zinafanya miujiza. Hivi sasa naweza hata kukimbia—lazima iwe morphine.
“Unajisikiaje, Helitha?” anauliza huku akisoma clipboard mikononi.
“Unakumbuka uko wapi?”
“Hospitalini,” najibu kwa sauti ya ukavu, koo langu bado limekaushwa na usingizi mwingi.
Ninatazama dirishani—ni usiku sasa… haikuwa hivi wakati yule muuguzi alikuja kunipa dawa.
Ninatazama saa ukutani: masaa matatu yamepita.
“Vizuri sana.” Anatikisa kichwa mara mbili, anageuza ukurasa, kisha ananiangalia.
“Mimi ni Daktari Phillips. Mimi ni mtaalamu wa mishipa na nimekuwa nikikuhudumia tangu ulivopata ajali.”
Lakini hiyo haionekani kuwa sahihi.
“Nadhani tairi yangu ililipuka,” nasema kwa mkazo.
“Hatuna uhakika kwa sasa, sunshine,” Baba anakatisha haraka, macho yakimtazama Daktari kwa ukali.
“Kuna uwezekano wa mambo mawili. Uchunguzi bado unaendelea, kwa hiyo huenda ilikuwa tairi, au mnyama. Lakini sababu si muhimu kwa sasa.”
Si muhimu kwake.
Kwangu ni muhimu kujua kama mimi ndiye nilisababisha ajali au la.
“Ni lazima iwe tairi,” nasisitiza. Siwezi kuamini niko hapa kwa sababu nimesahau ushauri wa Baba.
Daktari anafunga clipboard yake na kuiweka pembeni.
“Nina maswali machache,” anasema. “Baba yako alisema huwezi kukumbuka ajali. Unaweza kuniambia jambo la mwisho unalokumbuka?”
“Um... nakumbuka nilipoondoka chuoni. Mvua ilikuwa inanyesha nilipoingia ndani ya gari,” nasema huku nikikaza macho, nikitafuta undani.
“Simu yangu ililia. Sikumbuki nani alinipigia, lakini nilisimama kando ya barabara kupokea, halafu… halafu…”
“Usijitie shinikizo, Helitha,” Daktari Phillips anasema kwa sauti ya upole.
“Ulipata kichwa kugongwa vibaya sana. Kulikuwa na uvimbe mkubwa karibu na ubongo wako.”
“Uvimbaji umepungua sasa,” Daktari Phillips anasema, “lakini bado haujaisha kabisa. Huenda ukawa na kizunguzungu, kuchanganyikiwa, na maumivu kwa siku chache. Unapona vizuri, lakini usijilazimishe, sawa?”
Anangoja niitikise kichwa kabla hajamalizia:
“Unaweza kuniambia ni siku gani ya wiki leo?”
Nikikumbuka jinsi alivyosema “tangu ajali,” naangalia kucha zangu, nikitathmini urefu wake.
Ni ishara pekee ya muda iliyopita ninayo.
“Siwezi kusema kwa uhakika. Kucha zangu ni ndefu kuliko kawaida. Nadhani nimekuwa hapa kwa muda mrefu.”
“Una akili,” anasema daktari, akinitupia tabasamu lililobana.
“Ulikuwa kwenye koma kwa siku tisa. Sasa, niambie jina lako kamili na umri wako.”
“Helitha Joseph Vaughn. Nina miaka kumi na minane.”
Baba anavuta pumzi kali ghafla, kisha anakandamiza sauti ya maumivu kooni, macho yamefungwa kwa nguvu. Damu yangu inaganda ninapomwangalia akiuma mdomo wa chini kwa nguvu.
“Kuna nini?” nauliza kwa wasiwasi, moyo wangu ukianza kudunda kwa kasi.
“Helitha,” Daktari ananigeukia tena, na mistari miwili inaonekana kwenye paji lake. Baba anainama, akizika uso wake mikononi mwake.
“Ni mwezi gani sasa?”
“Nini? Kwa nini? Kuna nini kinatokea?”
“Disemba,” najibu kwa haraka, sauti yangu ikiwa na mkwaruzo wa hofu. “Krismasi iko karibu.”
Daktari anakohoa, macho yake yakizunguka kati yangu na Baba.
“Samahani, Helitha. Huo si ukweli. Sasa ni mwisho wa mwezi wa Agosti. Si Disemba.”
Agosti? Vipi tena—
“Si... sielewi,” nasema kwa kigugumizi, sauti ikitetemeka.
“Agosti?”
Anatikisa kichwa kwa uthibitisho, nami nabaki nikiwa nimeganda. Siwezi hata kupepesa macho.
“Lakini... ulisema nilikuwa nimezimia kwa siku tisa, si miezi minane!”
Ninasema kwa mshangao, nikitetemeka.
“Naamini umepata upotevu mkubwa wa kumbukumbu kutokana na jeraha la kichwa,” ananieleza kwa utulivu.
“Inaonekana umepoteza karibu miaka miwili ya kumbukumbu. Helitha, wewe si mtoto wa miaka kumi na minane. Sasa una miaka ishirini.”
Kama radi iliyonigonga moyoni, ninashtuka kwa undani zaidi ya maumivu ya mwili.
“Ungetakiwa kuanza mwaka wako wa tatu chou wiki hii.”
Endeleaa…


SURA YA 4; SHAWN

Safari ya Cicero kutoka Chicago ni ya takribani masaa matano kwa gari. Nikiwa nimechukua mapumziko mawili kwa ajii ya kununua kahawa, nawasili katika nyumba salama saa kumi kasorobo alfajiri.
Kutoka kelele za klabu hadi muziki mzito wa rock kwenye gari, kisha ukimya mrefu na utulivu mzito wa asubuhi ya mapema. Anga ni jeusi, nyota ziko chache—lakini najua hali hiyo haitadumu.
Ninafungua mlango wa gari kwa nguvu. Misuli yangu inakaza kwa uchovu wa safari ndefu. Najinyoosha kushoto na kulia, huku mgongo wangu ukitoa mlio wa kuridhisha
Mlango wa mbele unafunguliwa kabla hata ya nusu dakika.
Apollo, mtu wa karibu zaidi wa Romano, anatoka nje akiwa amenyooka, akitikisa kichwa kidogo kwa ishara. Uso wake haueleweki.
Haangalii macho yangu.
Hilo ni ishara mbaya.
“Anakusubiri,” anasema, akinyosha mkono kuomba funguo za gari.
Ninajua utaratibu. alfajiri karibu kuingia, na mwanga wa jua ukichomoza, utaangaza vichaka vinavyochipuka kwenye nyufa za njia ya gari… na Corvette yangu nyekundu mpya ya kifahari itavutia macho ya watu mtaani.
Naanza kutembea kuelekea sebuleni kana kwamba napita juu ya karatasi ya tissue.
Ninajaribu kupuuza hofu inayozidi, pamoja na harufu ya hewa mbovu iliyochanganyika na vumbi na kuoza.
Ninapogeuka kushoto, napita sehemu ambayo zulia linabadilika kutoka kijani kilichochakaa hadi pinki chafu.
Na pale, mbele ya mahali pa moto, Romano—baba yangu—anakaa kwenye kiti chake.
Koti lake refu la kahawia limewekwa nyuma ya kiti, na kofia yake ipo kichwani kama kawaida.
Mwili wangu unarejea katika hali ya hatari. Adrenalini inachafua kila kitu, ikichana kabisa tumaini ambalo hata sikuwa nalo kwa kweli. Ndani kabisa, nilijua nitasikia majibu haya, lakini… Dante alisema kweli.
Tumaini hufa mwisho.
“Vipi?” ninasema kwa meno yaliyojifunga, wakati dunia yangu inaanza kuanguka taratibu.
Majibu haya yasiyo ya maneno kutoka kwake yanakata matumaini yangu.
Hicho kipande kidogo cha huruma nilichojifunza kutoka kwa Dante... kimeondolewa kabisa.
“Alijiua,” Romano anajibu kwa ukali, akinywa pombe yake kana kwamba hakusema jambo la kusikitisha.
Alijiua.
Alijiua.
Alijiua.
Kadri neno hilo linavyorindima akilini mwangu, linazidi kupoteza maana.
Nimewahi kupitia giza, lakini kufikiria kujiua hakujawahi kuwa chaguo kwangu.
Ninapigwa butwaa.
Sikuwepo kwa Aalyiah alipoitaji msaada.
Sikuweza kumzuia kuanguka kwenye shimo hilo la matatizo yasiyoeleweka.
Kila kitu kinaweza kurekebishwa.
Tungelipata njia kama angenipigia simu.
Nilipaswa kuwa pale.
“Kaa.” Romano anaamuru, akionyesha kiti cha mkono kilicho mbele yake.
Kisha anagonga glasi yake dhidi ya ile iliyo tupu, pembeni ya chupa ya pombe iliyojaa karibu yote.
“Kunywa.”
Hii siyo ombi.
Hii ni amri. Ni amri, na najua vizuri sana kuwa si jambo la kubishana.
Licha ya miaka ambayo hakujua kuwa mimi ni wake, miaka niliyotumia nikiishi na shangazi, na hata ile niliyofanya kazi chini ya Dante—Romano Willard hunitia hofu ambayo haifutiki.
“Nilisema, kaa,” anasisitiza kwa sauti kalii.
Ninatii. Kwa miguu inayotetemeka, ninavuka sebule na kuketi kwenye kiti chenye rangi ya njano iliyofifia.
Kwa kimya, najitahidi kuzuia huzuni inayonichana rohoni ninapomimina pombe kwenye glasi ya kioo hadi ikafurika.
Mikono yangu inatetemeka kiasi kwamba pombe inamwagika kwenye suruali yangu ya jeans.
Shit. Moyo wangu umesambaratika vipande, na vipande hivyo vinakuwa kama vipande vidogo vya kioo vinavyopenyeza kwenye mapafu yangu.
Ninapiga funda kubwa.
pombe inachoma koo langu, inapooza ulimi—lakini haipoozi maumivu.
Dada yangu mdogo.
Amefariki.
Hayupo tena.
Kujiua.
“Kwa nini?” nauliza kwa sauti iliyokauka. “Lini? Kulitokea nini?”
Romano ananitazama kwa macho ya baridi, ya kuhesabu. Yupo tulivu. Tulivu kupita kiasi—hata kwake.
Si hisia ambazo mtu aliyepoteza binti yake anatarajiwa kuwa nazo.
Kuna huzuni machoni mwake, lakini ni ya kulegea. Tayari imechakatwa. Tayari imekubaliwa.
“Karibu wiki mbili zilizopita.”
Ninaruka kwa ghafla kutoka kwenye kiti. “Wiki mbili?!”
“Ameshakufa kwa wiki mbili nzima na unaniambia sasa hivi tu?!”
Ninazunguka kumkabili, sura yangu ya giza — inayofanana kabisa na yake — ikiwa wazi. Huzuni yangu imegeuka kuwa hasira kali.
“Anza kuongea sasa hivi!”
“Shawn.” Sauti ya Apollo yavunja ukimya. Ni tulivu, thabiti, lakini bunduki iliyoelekezwa kati ya macho yangu inanieleza vingine — hayupo mtulivu kama sauti yake inavyodai.
“Iweke chini, mwanangu.”
Ninakunja uso, nikichanganyikiwa kabisa. Kwanini—?
“Je, aliwahi kukuambia kuhusu mpenzi wake?” Romano anauliza kwa sauti ya kuchunguza, macho yake yakiwa makini.
“Mpenzi? Alikuwa na mpenzi? Alikuwa mtoto bado, Romano! Kwa nini—”
“Nitalichukulia hilo kama jibu la hapana,” anakata kauli, akiniruka kama kwamba hasira zangu ni upepo tu.
“Hakuwa mtoto, Shawn. Alikuwa na miaka kumi na nane.”
Miaka kumi na nane siyo umri wa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi — siyo bila kuniambia kwanza, ili nimchunguze huyo jamaa sawasawa.
Ningeenda Columbus, nikamchukue kidogo tukae bar, kisha nimtishie kumkata nyeti zake kama hatampenda na kumheshimu Aalyiah kama malaika aliyekuwa.
“Alex alikuwa askari wa siri.”
Romano anatupa bomu lingine bila huruma.
Anakaribia kuniua kwa mshtuko usiku huu.
“Alikuwa...?” Ninaliona neno hilo. Sijashangazwa kwamba Alex hayupo tena.
Romano bila shaka alimtundika juu chini, akamchanachana tumbo, na akaangalia utumbo wake ukijikunja nje taratibu, huku akinywa whisky kwa raha.
“Askari wa serikali...” ninasema kwa hasira, nikimkazia macho.
“Kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, mbona haikugundulika tangu alipoanza kumkaribia Aalyiah?”
Romano alikaza meno yake, hasira zikimjaa. Hakufurahishwa na ukweli kuwa ulinzi wake ulishindwa, na bado anaumia kwamba nina ujasiri wa kuibua dosari zake.
“Vaughn ndiye aliyemchagua kwa mkono wake, bila kibali wala taarifa.”
Anasema kwa mkazo.
Vaughn, afisa ambaye sidhani kama ni wa kuvunja kanuni, ndiye kiongozi wa uchunguzi dhidi ya Romano.
Kwa mwaka mmoja sasa, amekuwa akikusanya ushahidi kidogo kidogo, na kuleta matatizo makubwa kuliko timu nzima ya wachunguzi waliomtangulia.
Ushahidi mwingi ni wa kudhania, lakini Romano si mtu wa tahadhari.
Badala ya kutulia wakati Vaughn alipopewa kesi yake na kuhamia ceciro, alianza kupanua biashara yake hata zaidi — chini ya pua ya mchunguzi huyo.
Si hatua ya busara.
Romano anamjua Vaughn vizuri, lakini anamdharau kila mara.
Mwaka jana, aliniambia kuwa wana historia ndefu.
Nadhani aliwahi kumuua mwenza wa Vaughn wakati Romano alikuwa na biashara kule Florida.
“Tulimkagua Alex kwa undani, lakini tulikosa.”
Romano anakiri kwa mara ya nadra kabisa.
“Hakuna rekodi yoyote ya kuwa alikuwa askari. Ama Vaughn alifuta kila kitu, au hakuwa askari kabisa.”
Anang’aa nyekundu kwa aibu — si kawaida kwake kukubali kosa.
“Hilo ni kosa langu,” anasema kwa meno yaliyokakamaa.
Na kosa hilo limemgharimu binti yake.
Dada yangu.
Mtu ambaye ningekufa kwa ajili yake bila kusita.
“Niambie kilichotokea,” namsihi, nikibana ngumi zangu.
“Alex alikuwa na mwanamke mwingine. Sijui Aalyiah alijuaje, lakini moyo wake uligawanyika. Alimpenda huyo mbwa.**”
Romano anakunywa, akiendelea,
“Siku moja tu, maisha mawili na miaka miwili ya kumbukumbu ilipotea.”
Anasimulia:
Aalyiah aliacha ujumbe mfupi sana. Sentensi mbili tu:
“Yeye ni askari, Daddy. Hanipendi… anampenda yeye.”
Romano aliagiza Alex na yule mwanamke wake wakamatwe wakiwa hai, ili ajue ni habari gani walikusanya, waliwapa nani, na ni kesi ipi walikuwa wakijenga.
Lakini Babyface — jitu la misuli lisilo na ubongo — alifanya makosa.
“Alikuwa anawafuatilia,” Romano asema.
“Walikuwa wanatoroka. Babyface alisema aliwasukuma kidogo, lakini...”
Apollo ananipatia picha.
Gari jeupe, lililoharibika vibaya.
Limeviringika, likajikunja kuzunguka mti.
Dereva hakupona.
Baada ya kumimina pombe ya pili na kukubali polepole ukweli mgumu, Shawn anaendelea kuchimba ukweli kutoka kwa baba yake, Romano.
“Ni nani alikuwa anaendesha?”
“Alex. Alikufa papo hapo.”
Alex, mpenzi wa Aalyiah, na pia askari wa siri aliyekuwa amejificha kama mpenzi wa kawaida, alikufa kwenye ajali ya gari baada ya kufuatwa kimakosa na watu wa Romano.
Lakini msichana aliyekuwa naye hakufa.
“Ilikuwa karibu sana, lakini alinusurika.”
“Jina lake ni Helitha.”
Picha ya msichana huyo imewekwa mikononi mwa Shawn—macho yake ya buluu kama chuma, nywele za rangi ya strawberry-blond, sura ya upole yenye kuvutia. Lakini huyu si msichana wa kawaida.
Romano anasema kwa sauti ya kupinda:
“Huyo ni binti pekee wa Joseph Vaughn.”
Endeleaa…


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote