CAPTAIN SILVER (Nakupenda Leo Hata Kesho) 💕💕
By Miss Hamida
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Mfano ukifungiwa chumba kimoja na mtu unae mchukia sana kwa dakika kumi utatoboa kweli??
Hapa namzungumzia Jolene, dada mdangaji ambae anategemea pesa za wanaume ili apate kuishi vizuri. Siku moja anaalikwa na Mr Kimaro ambae ni danga lake la muda mrefu, amsindikize Zanzibar alipokua anaenda kikazi tena kwa meli.
Mr Kimaro anakodisha meli iliyokua chini ya Captain Silver! Huyu ni Jamaa aliekua anateswa na usaliti wa mkewe. Kwenye meli Silver anakutana na Jolene na anatokea kumchukia sana sababu ya udangaji wake.
Lakini wakati wakiwa safarini unatokea uzembe na kusababisha meli waliyokua wamepanda kuzama. Kwa bahati nzuri wote wanapona ila sasa Joline na Silver wana kwama katika kisiwa kwa miezi sita, tena wakiwa wawili tu!
Ndani ya hio miezi sita ni visa na visanga vinatokea lakini mwisho wa siku wanajifunza kupendana kuliko hata walivyo tarajia!
Unataka kujua kitaendelea nini baada ya hapo?? 😜
SONGA NAYO…………..
SEHEMU YA : KWANZA
Ni asubui flanii iviii Jolene alikua akirudi nyumbani baada ya kukesha bar usiku mzima akiwahudumia wateja.
Alichoka mno hata tembea yake ilibadilika. Alipofika kwenye chumba alichokua ana ishi, alifungua mlango na moja kwa moja akaenda kujitupa kwenye godoro lililo kua chini.
Ile anaishilia usingizini tu, simu ikaanza kuita. Alikerekwa sana na kujikuta anatukana pasipo sababu.
“Mbona tunasumbuana jamani? Kwaiyo mtu asipumzike??” Alilalamika lakini hakuacha kupeleka mkono kwenye pochi na kutoa simu yake.
Alie kua anampigia ni Mr Kimaro, danga lake la siku nyingi ambalo linamhongaga pesa za kutosha. Usingizi na uchovu Ukamuisha, akapokea haraka na kupeleka simu sikioni.
“Mr Kimarooooo! Nilikua nakuwaza jamani nikasema umenisusa hatari”
“Jojo jojo! Jojo baby! Jojo chocolate! Jojo tamu tamu! We binti unajua kucheza na hisia zangu! Wallah umeni changanya” Mr Kimaro alimwaga sifa nyingi hadi Jolene akafurai
“Sio kama unani pamba tu Mr Kimaro”
“Nikupambe wapi mrembo?? Upo juu kama mlima kilimanjaro! Kweli mambo unayaweza”
“Ndo ivo sasa ukinisifia umwage na pesa pia, ama hujui ilo?”
“Usihofu! Kuhusu swala la pesa hapa ndo kisima kisicho kauka Jojo!”
“Enhee Mr Kimaro, simu yako ya asubui asubui kunani? Ama ndo umemiss mambo!”
“Unajua nini Jolene, nina safari ya kikazi kesho kutwa! Naenda Zanzibar na nitakaa huko mwezi mzima! Unaonaje tukaenda wote? Ili tukiwa huko unipe raha za kutosha! Usijali kuhusu pesa hapa ndo mahala pake”
“No! Mr Kimaro nataka kujua utanipa kiasi gani maana nitaharibu ratiba zangu za mwezi mzima kwaajili yako ujue”
“Milioni 5! Ama haikutoshi?”
Jolene aliposikia kile kiasi alicho tajiwa akazidi kuongeza matabasamu.
“Basiiiiii, tutaenda Mr Kimaro hata usihofu! Si kesho kutwa?”
“Ndio ni kesho kutwa! Ila tutaondoka jioni, tukutane ferry maana tunaenda na meli private”
“Sawa Mr Kimaro usiwe na hofu”
Baada ya simu kukatwa Jolene aliruka kwa furaha. Na ili Mr Kimaro kumuonyesha kwamba alikua serious, akamtumia laki 7 kwaajili ya maandalizi tena dakika zile zile.
Jolene akazidi kuchanganyikiwa zaidi, anapenda pesa mno kushinda kula. Alichokifanya ni kutuma kiasi kidogo kwa mama yake kijijini.
Kiasi kingine kilicho bakia akaenda kununua viwalo vipya vya kuendea Zanzibar tena siku ile ile. Mbele ya pesa mbona uchovu unaisha.
Tukiachana na Jolene, twende nje kidogo ya mji! Na huku ni maeneo ambayo wanaishi matajiri wenye pesa zao mjini.
Katika jumba moja la pesa nyingi alionekana Silver pamoja na mkewe Camilla wakirejea nyumbani toka kwenye honeymoon yao walioifanya kwa siku tatu tu.
Na yote nikwa sababu Camilla alidai kuwa hawezi kupoteza siku saba kufurai ikiwa ana wagonjwa hospitali wanao subiri kutibiwa na yeye.
Silver hakua na shida alikubali kufanya mkewe alicho kitaka sababu alikua akimpenda mno. Basi walipofika nyumbani cha kwanza Camilla aliingia bafuni akaoga kisha akabadili nguo zake ili aweze kutoka
“Unaenda wapi?” Silver alimuuliza akimuangalia namna alivyo pendeza
“Hospitali!”
“Tumerudi mda sio mrefu kwanini tusipumzike?”
“No! Sababu ya kurudi ni ili mimi niende kazini! Acha niende baby kuna wagonjwa wengi wanani subiri”
Silver hata kama angepinga isinge fanya Camilla abadili mawazo yake.
“Sawa! Kazi njema”
“Oooh asante baby your the best” Camilla alimsogelea Silver akambusu shavuni kisha akatoka mbio mbio na kuondoka.
Kweli alienda mpaka hospitali, alipofika huko alipokelewa vizuri na madaktari wenzake huku wakizidi kumpongeza kwa kuolewa. Miongoni mwa madaktari alikuwepo Dokta Marcus!
Basi Camilla alipomuona Marcus akatabasamu zaidi, alimkonyeza na kuelekea ofisini kwake. Naweza sema ule mkonyezo ulimpagawisha Marcus kwani na yeye alimfuata Camilla nyuma nyuma hadi ofisini.
Alipoingia tu alimvamia Camilla na kuanza kumshushia mvua ya mabusu tena kwa pupa kama fisi alie ona mfupa.
“Marcus subiri kwanza bhana” Camilla akamzuia
“Nisubiri nini wakati nime kumiss?? Siku tatu zilikua nzito kwangu, alafu pia nina maumivu ya kushuhudia unaolewa na mwanaume mwingine”
“Najua baby ndo maana nimefupisha honeymoon yetu kwaajili yako. Nikikaa na Silver naona kero tu! Wewe ndo unaejua kunigusa penyewe”
“Sasa tunasubiri nini?? Nipe tamu yangu”
“Nooo! Subiri! Hapa ni ofisini ujue! Tukikutwa je?”
“Hakuna atakae tukuta! Tunafanya chap chap alafu acha uoga uoga Camilla”
“Hakuna shida”
Wakaanza kushikana shikana pale na mabusu ya kutosha. Upande wa Silver hakua na habari kama mkewe yupo kwenye mahaba mazito na Daktari mwenzake na ndio sababu kubwa ya kufupisha honeymoon yao.
Yeye alishinda nyumbani maana hakuweza kwenda kazini sababu alikua kwenye likizo fupi ya harusi. Alicho kifanya ni kuingia jikoni ili kuandaa chakula kwaajili ya mkewe.
“Atakua kachoka sana, na sidhani kama atapata mda wa kula! Acha nipike kisha nimpelekee chakula”
Silver akazama jikoni na kuanza kukarangiza masotojo kwaajili ya Camilla. Alipomaliza alikipaki chakula kwenye kontena na kukitia kwenye mfuko.
Kisha na yeye akaoga na kujiandaa vizuri ndipo akaelekea hospitali. Alipofika, nae akawa anapongezwa na baadhi ya watu waliokua wakimjua.
Alipokea pongezi baada ya pale akapiga hatua kuelekea ofisini kwa mkewe. Alipokua anakaribia mlangoni alisikia vilio kwa mbali na miguno ya ajabu.
Mwanzoni alidhani pengine ni mgojwa anapatiwa matibabu ila kadri alivyo zidi kusogea ndipo aligundua kuwa vile vilio vilikua vya mkewe.
Mapigo ya moyo yakamuenda kasi sana hadi kupelekea jasho kutoka. Alihisi pengine mkewe alikua akimsaliti na mwanaume mwingine kule ndani ila hakutaka kuamini.
Ili kujiaminisha zaidi, alifungua mlango taratibu na kuchungulia ndani. Alichokiona kilimuumiza sana moyo! Akahisi kupagawa mno.
Alitamani awavamie Marcus na Camilla pale mezani ila akashindwa. Akafunga mlango na kuondoka taratibu huku akilengwa na machozi.
Nakuja………..
SEHEMU YA : PILI
Alipiga hatua haraka haraka kutaka kuondoka ila hakufika mbali akasikia akiitwa. Alifosi tabasamu usoni na kumgeukia aliye muita.
Alikua ni Zulfa ambae ni rafiki mkubwa wa Camilla.
“Shem!! Vipi?”
“Safi”
“Mbona hapa sasa ivi?? Kwani honeymoon imeisha?”
“Yeah”
Zulfa akashangaa Silver anamjibu kifupi wakati hajawai mjibu vile ata siku moja.
“Uko sawa shem?”
“Ndio”
“Mhhh! Basi nafurai kukuona”
“Mimi pia” Silver hakutaka mambo mengi, aligeuka na kuondoka.
Huku nyuma Zulfa alikwenda kwenye ofisi ya Camilla. Alipofika akakutana na Marcus mlangoni akiwa anatoka.
Walisalimiana kisha Marcus akaondoka zake na Zulfa akaingia ndani.
“Wewe! Umerudi hata kuniambia? Mimi niwa kusikia habari toka kwa watu kweli?”
“Jamani, nimefika tu hata sijapata nafasi ya kuja ofisini kwako! Vipi lakini? Vipi hali yako?”
“Nzuri tu! Sijui wewe? Mbona umefupisha honeymoon yako?”
Camilla akashindwa kujibu akabaki akitabasamu kwa aibu. Moja kwa moja Zulfa akawa amepata jibu lake.
“Sababu ya Marcus sio?? Camilla seriously??”
“Nini sasa? Usinilaumu bhana unajua ni jinsi gani najihisi juu yake”
“Mungu wangu Camilla, wewe ni mke wa mtu! Angekua anakupenda sana asingekubali kuona unaolewa na mwanaume mwingine, angekuoa mwenyewe”
“Mimi sijali sana kuhusu ndoa, kikubwa tunapendana na icho nicha muhimu”
“Come one Camilla, huyu mwanaume hakupendi hata kidogo, anakutumia tu! Ama umesahau jinsi alivyokua anakunyanyasa?? Umetoa mimba ngapi kwaajili yake? Na mwisho wa siku ukaolewa na mwanaume mwingine mbele yake na hakufanya kitu?!”
“Stop! Hiyo ni zamani, Marcus kabadilika”
“Kwaiyo ndo mlikua mnafanya uchafu wenu huku ndani?? Mngefumwa je?”
“Hakuna alietufuma”
“Kabla sijasahau nimekutana na Silver, alikua tofauti sana! Yani hakua kawaida kabisa, ni kama kuna jambo ameona!…….. usikute aliwaona??”
Camilla akatoa macho na kuanza kutetemeka. Aliogopa mno hali iliyofanya apaniki
“Sidhani”
“No! Yawezekana kawaona ndo maana alikua akinijibu vibaya kiasi kile”
“Hapana bhana, angetuona unadhani hapa ndani pangekalika?? Pangefanywa ulingo mdogo wa ngumi. Au katuona??? Mungu wangu”
Camilla alitoa simu kwenye pochi na kumpigia Silver. Simu iliita tu pasipo kupokelewa. Akazidi kupatwa na kichaa.
“Kama katuona nimekwishwa mimi Zulfa” Camilla alitoa machozi
“Tena kama kawaona itakua afadhali maana nimechoshwa na hizi dhambi zenu zisizokua na maana”
“Usisema ivyo Zulfa, nakuja sasa ivi, ngoja niende nyumbani”
Camilla alibeba pochi yake na kutoka mbio mbio akielekea nyumbani. Alipofika hakukuta mtu yoyote, palitulia tuli.
“Sasa atakua wapi? Eeeh Mungu asije tu akawa ametuona” alijaribu kupiga simu yake bado haikupokelewa.
Silver alikua kaegesha gari lake pembezoni mwa barabarani akisononeka. Simu za mkewe aliziona
Na hakutaka kabisa kupokea.
Mwanaume chozi likamshuka kwa machungu aliyokua nayo moyoni. Alie toa ule msemo wa mke anauma kweli hakua amekosea.
Machungu yake yanazidi yale maumivu unayo yahisi baada ya kutia chumvi kwenye kidonda. Maumivu yake ni extra unatamani hata utoe moyo na kuurarua rarua.
Basi Akiwa kwenye gari Silver alimpigia rafiki yake wa karibu ambae pia wanafanya kazi sehemu moja.
“Broooo! Naona unajilia vyako tu huko honeymoon! Wanandoa mnaraha sana”
“No Davis tumerudi leo!”
“Kwanini? Ina maana siku tatu zinawatosha?” Davis alishangaa
“Tuachane na hayo, vipi naweza kupata safari??”
“Mhhh safari tena Bro?? Ama umesahau upo likizo”
“Najua, sio lazima hata ziwe za ofisini! Mimi nataka nipate kitu cha kuniweka busy maana nahisi nikikaa na Camilla naweza kumnyonga”
“Duuuh! Bro kuna nini? Niambie shida nini??”
“Kwa sasa kukuambia itakua ngumu, kama hakuna safari basi poa”
“No! Subiri kwanza, kuna Mzee hapa anaitwa Kimaro anataka kwenda Zanzibar na meli ya Private. Alitafuta Captain amekosa ndo akawa kanicheki mimi! Ila sema nini Bro, utaenda wewe badala yangu! Analipa vizuri, dollar 2000 kwenda na kurudi”
“Sijali sana kuhusu hela! Safari yenyewe ni lini?”
“Kesho jioni”
“Nitafika on time usiwaze”
“Daah poa mwanangu, nitakutumia detail zote kwenye whatsapp mda sio mrefu! Alafu ukikaa sawa usisahau kunicheki nipo tayari kukusikiliza”
“Thanks Bro”
Silver alikata simu kisha akawasha gari kuelekea nyumbani. Alipofika alikuta Camilla anamsubiri kwa hamu. Hata hakumsemesha, alikwenda moja kwa moja chumbani na kuanza kupaki nguo zake kwenye sanduku.
“Unaenda wapi Mume wangu”
“Nina safari kesho”
“Mbona ghafla? Si upo likizo”
“Kama unavyo penda kazi yako na mimi pia napenda kazi yangu”
“Mhhh! Sawa kama unaenda safari, alafu Zulfa alinambia ulikuja kuniona, sasa mbona hukuja ofisini?” Camilla aliuliza kimtego ili kutaka kujua kama Silver aliwaona au laah!
“Kabla sijafika nilipokea simu ya kazini na huko ndipo nilipo kuwepo”
Camilla kusikia vile kidogo akapumua. Hakujua Ni kiasi gani Silver alikua na hasira nae, angekua ni mwanaume mwenye hasira za karibu Camilla angeshakula kipigo na talaka juu.
Basi zile habari za Silver kusafiri Camilla alimjulisha Marcus, na wakapanga kabisa namna ya kuzitumia zile siku chache za uhuru vizuri.
Wakachati kwa mda mrefu mpaka Camilla akaishia usingizini. Alipolala Silver aliamka, akachukua simu ya mkewe na kuanza kuikagua.
Alikutana na vitu vingi vya ajabu ambavyo hakuvijua hapo kabla. Mpaka anamaliza kukagua simu ya Camilla, jamaa alikua na hasira kiasi cha kutamani kumnyonga Camilla akiwa amelala.
Nakuja………..
SEHEMU YA : TATU
Basi siku iliyofuata ndo ilikua ni siku ya safari. Jolene alikua tayari kusafiri na Danga lake Mr Kimaro, nae Captain Silver alikua tayari kuendesha chombo mpaka Zanzibar.
Wa kwanza kufika kwenye meli alikua ni Silver. Alivaa uniform zake nyeupe zenye mistari meusi akapendeza hatari.
Alipofika akakuta tayari msaidizi wake alishafika ambae angesaidiana nae kuendesha meli. Alafu sasa meli yenye ilikua kubwa kama nyumba.
Ndani palikua na vyumba vinne vya kulala, sebule, dinning area, jiko pamoja na ukumbi wa starehe. Pia kulikua na wafanyakazi wa tano akiwemo na mpishi.
Kwaiyo wafanyakazi watano, Captain na msaidizi wake pamoja na Jolene na Mr kimaro jumla walikua watu Tisa.
Haya, baada ya lisaa kupita akafika sasa Jolene akiwa na sanduku lake mkononi. Alikua kajipodoa siku hiyo na kupendeza kwaajili ya Mr Kimaro.
Alipofika kwenye ile meli alishangaa mno sababu mbali ya kupanda pantoni, hakuwai kupanda meli kubwa kiasi kile hapo kabla.
Kama kawaida yake akatoa simu kwenye pochi na kuanza kujipiga picha. Akazunguka kila mahali na mwishoni akapanda kabisa juu ya meli ili apate picha nzuri zaidi.
Akiwa ana hangaika kupiga picha Silver alikua akimuona kupitia kioo. Jinsi Jolene alivyokua amevaa Silver alikua na uhakika kua anadanga.
Taratibu alimfuata hadi alipokua anapiga picha na kusimama pembeni yake.
“Hili sio eneo la picha” aliongea kwa ukali na kufanya Jolene aogope
“Kuna ubaya gani mimi kupiga picha?”
“Ukiambiwa kitu mara moja elewa ama masikio yako mabovu??” Mara hii akafoka mpaka Jolene akashindwa kuelewa shida yake ni gani.
“Sawa yaishee” alimsonya akaondoka zake kurudi upande wa chini. Bahati nzuri nae Mr Kimaro akawa amefika ivyo walipo onana wakakumbatiana.
“Umenisubiri mda mrefu Jojo wangu??”
“Hapana, mimi mwenyewe nimefika mda sio mrefu”
“Unayaonaje madhari ya hapa? Umepapenda??”
“Ndio pazuri kweli ila sijampenda Captain wako! Ananiangalia utadhani nimeiba mkewe”
Mr Kimaro kusikia vile akacheka kweli
“Ooh pole! Itabidi uvumilie maana kwa dakika hizi chache siwezi kupata Captain mwingine, alafu nimesikia sifa zake nyingi kuwa ni fundi wa kuendesha vyombo vikubwa kama hivi”
“We msifie tu ila sijampenda kabisa” Jolene alivuta mdomo na kumfanya Mr Kimaro afurai zaidi.
Wakiwa wanaongea akafika Silver na kumsalimia Mr Kimaro.
“Naitwa Captain Silver nitakua muongoza safari yenu hadi Zanzibar! Sitakua mwenyewe bali nitasaidiana na mwenzangu”
“Safi sana kijana, nimesikia sifa nyingi sana kuhusu wewe! Natumaini hutaniangusha”
“Ondoa shaka kuhusu ilo, utafika salama salmini”
“Haya, na mimi sitakua mwenyewe! Nitakua na tamu yangu hapa! Ukipenda umuite Jojo”
Mr Kimaro alimtambulisha Jolene kwa Silver lakini Silver hakuonekana kabisa kumfuraia Jolene. Tabia ya Jolene kudanga kwa wazee walio mzidi umri ni sawa na Tabia ya mkewe kumsaliti na mwanaume mwingine. Aliwachanganya kwenye kundi moja la wanawake wa hovyo.
“Ok basi mzee acha nirudi kwenye eneo langu”
“Sawa Captain tunakutegemea”
Silver aliondoka na kumfanya Jolene abinue mdomo na kumgeukia Mr Kimaro
“Daddy unaona alivyokua anani tazama?? Tena kwa dharau ya hali ya juu! Mimi sipendi kabisa” alideka
“Tulia mtoto mzuri, Captain asikupe presha kabisa! Ukiwa na mimi hakuna chochote kitakacho haribika”
“Nakuamini tu wewe Daddy siamini mtu yoyote yule” Jolene aliinama kidogo na kumbusu Mr Kimaro shavuni
“We mtoto weeee! Unanipagawisha ujue! Kweli sijafanya makosa kuongozana na wewe kwenye hii safari! Haya twende ukanikande kande nipate kumpuzika”
“Hakuna shida Daddy! Baby akeee, Odogwu mwenyewee”
Jolene alimpamba Mr Kimaro kwa majina matamu huku wakiongozana kuelekea chumbani. Huko Jolene alikua na kazi kubwa ya kumkanda yule mzee mpaka akaishia usingizini.
Masaa mawili mazima hali ya bahari ilikua shwari kabisa mpaka mtu unajisahau kama upo ndani ya meli. Ulipofika mda wa kula tayari mpishi alishaandaa chakula mezani ivyo Jolene akamuamsha Mr Kimaro na kwenda nae mezani kula.
Mr Kimaro alipofika mezani alimuita Captain Silver ili wapate chakula kwa pamoja! Mwanzoni alikataa lakini baada ya Kimaro kuhimiza sana Silver akaamua kwenda.
Alipakua chakula kidogo na kwenda kukaa mbali kidogo na akina Jolene. Uwepo wa Silver pale mezani ulikua ukimtisha sana Jolene.
Kila alipo inua jicho tu alikutana na macho ya Silver yaliyojaa hasira. Hakujua ni kipi alicho mfanya mpaka amchukie kiasi kile ila hakujali sana sababu alikua pale kwaajili ya Mr Kimaro tu na sio vinginevyo.
Basi wakawa kimya kula chakula huku kila mtu akiinamia sahani yake. Ni mara chache sana ilisikika sauti ya Jolene alipokua akimlisha Mr Tarimo. Mara ghafla kikasikika kishindo kikali kilicho fanya meli ianze kuyumba yumba.
Captain Silver alinyanyuka spidi spidi kuelekea kwenye chumba chake cha mitambo na kugundua kuwa meli iligonga mwamba. Yani ni Vile vile kama ilivyokua kwenye movie ya Titanic. Walio itazama nahisi wana elewa.
“Ulikua unafanya nini hujaona mwamba?” Alimfokea msaidizi wake kwa hasira
“Nilipitiwa kidogo na usingizi”
“Ona sasa tunaenda kuzama” Silver akajaribu kila aliloweza ikashindikana. Tayari upande mmoja ulishaanza kuingia maji.
Akatuma signal ya kuomba msaada toka kwa meli nyingine ama boti zilizokua kariibu ila hakupata jibu.
Huku upande wa pili tayari watu walianza kupaniki hasa Jolene, alijuta kabisaa kwanini alikubali kusafiri na Mr Kimaro! Ni bora angejilalia zake nyumbani na kula matembele yake ya chumvi. Na hivi ambavyo hakua najua kuogelea, weee mbona alikiona kifo chake kinabisha hodi.
“We Captain unataka kutuua?? Umesema tutafika salama nini hiki???”
Mr Kimaro alipaniki na kwenda kumkwida Silver.
“Mzee hatuku uona mwamba! Msaidizi wangu mwenyewe hakua muangalifu kwaiyo badala ya kulaumiana, ni bora kutafuta njia ya kujiokoa kwenye hili”
“Njia gani, tunakufa Jamani! Nina mke na watoto nyumbani” alilalamika sana Mr Kimaro huku jasho likimtoka
“Kila mtu achukue boya! Haraka haraka hali inakua mbaya” alisema Silver ndipo wote wakakimbilia walipo hifadhi maboya.
Maboya yenyewe yalikua matano na wao walikua tisa. Kwaiyo ni lazima wengine wangekosa na wengine wangepata. Na Jolene alikua mmoja kati ya waliokosa boya.
“Kuna wengine wamekosa, tutashea boya moja wawili wawili! Ni ngumu sana ila hatuna namna”
Silver aliposema vile watu wakachukuana wawili wawili. Jolene akajisogeza kwa Kimaro sababu ndo mtu pekee aliekua anamjua. Cha ajabu yule baba akamsukuma Jolene pembeni eti hataki kabisa kushea boya lake.
Jolene mwenyewe akastaajabu na kupigwa na butwaa. Yani yule mzee alikua tayari kabisa amuache afe ili ajiokoe nafsi yake.
“Kimaro?” Jolene alimuita kwa sauti ya upole
“Katafute sehemu nyingine!” Alikataa tena kwa ukali.
“Jamani! Wapi niende zaidi ya kwako?”
“Umeona kifo ndo unadhani mimi niwa maana? Unadhani sijui kama wewe ni kupe uliefuata pesa zangu?? Binti pambana na hali yako” Mzee akabadilika kuwa shetani pale pale.
“Kimaro bhana acha masihara! Kweli unataka kuniacha nife? Kumbuka nimekuja huku kwaajili yako”
“Toka hapa mnafki mmoja mkubwa wewe! Umekuja kwaajili yangu ama umekuja sababu nilikuahidi milioni 5?”
“Kimaro bhana usiwe ivo” Jolene alimsogelea Kimaro huku akitokwa na machozi sababu hakua tayari kufa.
“Tokaa nakuambia! Kwanini usiende kwa Captain, yeye pia hana mtu! Kwani lazima ushee na mimi”
Jolene alipoangalia kweli alimuona Silver yupo mwenyewe. Akashindwa amfuateje ikiwa Silver alimuonyesha chuki zisizo na sababu.
Akabaki amesimama akiwa amejikunyata huku akilia. Silver kuona vile akamfuata na kumshika mkono, japo alikua akimchukia ila hakua tayari kuona anakufa ikiwa ana uwezo wa kumsaidia.
“Tutashea la kwangu”
“Asante” Jolene alishukuru na kufuta machozi yake.
Basi Muda huo meli ilikua inazidi kuzama taratibu ilibakisha eneo dogo ambalo ndilo eneo walilokua wamesimama.
“Aya rukeni! Fanya haraka hatuna muda wa kupoteza”
Watu wakamsikiliza Silver na kuanza kuruka, wakaruka wote mpaka Kimaro akaruka, kisha Jolene na Silver wakaruka wa mwisho.
Nakuja………..
SEHEMU YA : NNE
“Tuogelee tusogee mbele kidogo” Silver alimwambia Jolene
“Siwe…zi…. Kuogelea” Jolene alitetemeka sababu maji yalikua ya baridi vibaya mno.
Silver hakujibu badala yake alipambana kuogelea ili waweze kusogea. Kaka wa watu alikua anajitahidi mno kuokoa maisha yao. Jolene angekua anaweza kuongelea kidogo angemsaidia.
Alipambana weee mwishoni akashindwa kabisa. Spidi ikapungua na kubaki wakiwa wamesimama pale pale kati kati ya bahari.
Kwa mbali Mr Kimaro na wengine walikua wakiogelea kutafuta msaada. Wakasahau kabisa
Kama kuna watu wamewaacha nyuma.
“tuna…kufa! Kweli tunakufa” alisema Jolene akilia
“Hatufi”
“Hakuna msaada wowote…! Tumekwama katikati ya bahari! Mungu ikiwa utanisaidia basi nakuahidi nitaacha kabisa kudanga na kuuza bar! Nitatafuta kazi nyingine ya kumsaidia mama”
Silver alimuangalia Jolene alivyokua ana ongea kwa hisia. Yeye kwake alikua tayari kufa maana mtu pekee aliekua na umuhimu kwake alimuumiza vibaya mno.
“naskia baridi sana…! Baridi”
Jolene akamsogelea Silver na kumkumbatia kwa nguvu huku Silver hakua akijali maana alikua na uhakika kuwa wanaenda kufa.
Basi upande wa Mr Kimaro walikua bize kuogelea. Walichoka mno ila hawakukata tamaa. Mpishi alipogeuka nyuma hakumuona Captain wala Jolene, akageuka haraka kuwaambia wenzake.
“jamani simuoni yule Captain wala yule binti!”
“Watakua wamezama! Ama wamemezwa na samaki”
“Turudi tukawaangalie, yawezekana wamenasa mahali jamani” kidogo yule mpishi alikua na huruma na utu
“Kama unarudi rudi wewe! Acha sisi tutafute msaada wa kuokoa nafsi zetu” alisema Kimaro huku akizidi kuogelea kuelekea mbele. Hakujali kabisa kuhusu habari za Jolene wala Captain.
“Mzee kasema kweli, tuendeleeni jamani” walikubaliana kuendelea na safari na sio kuwarudia wenzao.
Basi walipofika mbele kidogo wakaona boti ikija kwa kasi sana hasa upande walipo. Wakafurai na kuona msaada umefika.
“Jamani tupooo hapaaaa! Msaaada jamani msaadaa” wakapiga kelele kwa pamoja na kwa bahati nzuri lile boti liliwaona.
Ilikua ni timu ya uokoaji ambayo ilifika baada ya kupata signal ya msaada iliyo tumwa na Captain Silver mda ambao Meli ilianza kuzama.
Wakasaidiwa pale, wakapewa mablanketi ya kujikinga na baridi pamoja na makoti.
“Mlikua wangapi ndani ya meli?”
“Tulikua Tisa, wenzetu wawili hatuwaoni!” Alijibu Mpishi
“Basi nionyeshe eneo mlilo pitia ili twende tukawasaidie”
Boti iligeuzwa kwaajili ya kwenda kutoa msaada kwa Silver pamoja na Joline. Walipita kulekule ambapo Kimaro na wenzake walipita hadi wakafika eneo ambalo meli ilizama na wasione mtu.
Wale waokoaji wakamulika na tochi zao zenye mwanga mkali kwenye lile eneo kwa mda mrefu bila mafanikio.
“Watakua wamezama hao” alisema Mzee Kimaro bila ya huruma
“Kama wamezama inabidi tukawatafute!”
“Usiku huu??? Tuondokeni jamani turudi kesho” alisema Kimaro
“Kwakua hakuna alie na jereha kati yenu! Basi hamtapungukiwa na chochote ikiwa mkisubiri wakati tukiwa tafuta wenzenu! Ama mnataka wafe?”
Kimaro akaona aibu na kunyamaza kimya. Basi wale waokoaji wakavaa nguo zao maalumu na kupiga mbizi kuwasaka.
Hawakwenda mbali, walizunguka eneo lile lile na kwenda chini zaidi ya bahari na bado hawakuwaona. Mwishoni walikata tamaa kabisa na kugeuza boti kurudi nchi kavu kwaajili ya msaada zaidi.
Upande wa Camilla alikua akiandaa chakula cha jioni kwaajili yake na Marcus. Hakuona kabisa aibu ya kumleta mchepuko wake kwenye nyumba yake na mumewe.
Sasa kwanini aone aibu ikiwa Haikua mara yake ya kwanza kumleta Marcus kule ndani??? Alifanya vile mara nyingi na Silver hakuwai kumshtukia.
Haya…. Alipomaliza kuandaa chakula nae akajiandaa ili baada ya Marcus kula chakula basi apate kula chakula kingine cha nyongeza.
Baada ya kuwa tayari nae Marcus akawa amefika, tena kabeba ua kubwa na chupa ya wine mkononi. Hayo ndo mambo ayapendayo Camilla.
Alipomfungulia mlango akamkumbatia kwa mabusu mengi mpaka ya shingo.
“Unanukia vizuri! Unanipandisha midadi ujue” alisema Marcus
“Wacha weee!”
“Nakuhitaji sana Camilla! Nimekua nikikuwaza usiku kucha”
“Hunizidi mimi ila kwanza nataka upate chakula kizuri nilicho kiandaa ili upate nguvu ya kunigeuza utakavyo! Ama unasemaje??”
“Ilo limepita”
“Basi karibu ndani”
Marcus akaingia utadhani ni kwake vile. Akajitawala kama baba mwenye nyumba. Kabla ya kula akaenda chumbani anapolala Silver na Camilla akafungua kabati na kutoa taulo la Silver.
Alivua nguo zote na kujifunga lile taulo! Bila hata ya aibu akaenda kukaa nalo mezani akila chakula alicho kinunua mwanaume mwenzake.
“Unajua kupika sana”
“Ndio! Mdigo kwa mapishi??? Aisee hapa ndo mahala pake”
“Wacha weee! Ndo maana nakupenda”
“Subiri kwanza…” Camilla alisimama na kwenda kuwasha Tv kisha akaweka chaneli ya habari
“Tv ya nini my dear??”
“Napenda sana habari, hata sijui kwanini” aliongea huku akirudi mezani kula. Alikaa pembeni ya Marcus na kuanza kulishana nae kwa mahaba.
Wakiwa pale mezani, habari iliyokua inaonyeshwa kwenye Tv ni habari iliyohusiana na meli kuzama. Camilla alipoiona akajikuta ghafla tu anamkumbuka mume wake Silver.
“mbona kama umepoteza mudi ghafla??” Marcus alimuuliza
“Amna ni vile nimejikuta namkumbuka Silver”
“Kwaiyo nimekuja hapa ili tu enjoy ama kwaajili ya wewe kumkumbuka mumeo?”
“No! Sio ivyo usikasirike bhana! Kama jinsi ambavyo wewe una umuhimu kwenye maisha yangu ndivyo ivyo ilivyo kwa Silver. Ila wewe umezidi umuhimu zaidi kwa maana nakupenda sana”
“Icho ndicho nachotaka kusikia na sio hizo habari za mumeo”
“Kwaiyo ushapata wivu?”
“Ndio kwanini nisipate wivu……! Subiri kwanza……Camilla ile sio picha ya mumeo??” Marcus alinyoosha kidole na kumfanya Camilla arudishe macho yake kwenye Tv.
Kweli picha ya Silver ilikua imetawala kwenye screen yake. Camilla akazidi kuogopa zaidi hasa alipogundua kua mume wake alikua kwenye ajali mbaya ya meli. Na kibaya zaidi hakua amepatikana hadi mda huo.
“Mungu wangu! Mungu wangu” alisimama haraka
“Tulia Camilla”
“Nooo! Umesikia kabisa akisema amepata ajali!! Mpaka sasa ivi hajapatikana!! Uwiii!!” Akaanza kulia
“Kinacho kuliza hapo ni kipi??”
“Unataka nisilie wakati Ni mume wangu??”
“Hata kama lakini si umesema humpendi?? Hata kama amekufa”
“Ivi kweli swala deep kama hili unataka nisilie?? Alafu huu sio muda sahihi wa wewe kuleta wivu wako wa kijinga! Na nikuambie tu, Silver hajafa”
Camilla akakasirishwa sana na Marcus. Alichukua simu yake na kutafuta namba za Davis. Kabla hajazipiga tayari Davis akawa amempigia.
“Hellow shem, umesikia habari?” Alipokea haraka haraka
“Ndio nimezipata mda sana! Nimeshafika hadi huku ferry kujua utaratibu! Wamesema mpaka kesho ndo wataanza process za uokoaji maana kwa sasa ni usiku sana hawawezi kupata chochote. Kwaiyo pumzika na ondoa hofu! Kesho fika mapema sana ili kujua kitakacho endelea”
“Asante sana Shem kwa taarifa! Mimi sidhani kama nitapata usingizi”
“Naamini hakuna lolote baya lililo mkuta Silver, usijali huko alipo atakua sawa”
“Hakuna shida Shem! Tutaonana kesho”
Camilla alikata simu na kukaa kwenye kochi. Marcus akamsogelea na kumtuliza japo hakua akipenda namna ambavyo Camilla alikua akipata hofu juu ya Silver.
SEHEMU YA: TANO
Siku iliyofuata asubui na mapema Camilla aliamka kwaajili ya kuelekea Ferry ambapo shughuli zote za uokoaji zingeanzia pale.
“Twende wote” alisema Marcus
“Hapana! Sidhani kama ni vizuri tukienda pamoja, alafu watu watani hoji sana kuhusu wewe”
“Kwaiyo hautaki kabisa tuonekane pamoja?”
“Marcus una nini lakini? Sio kila kitu nicha kuonea wivu ama kuchukia! Nakuambia ivyo sababu nae Zulfa atakuja”
“Okay! We nenda” bado aliendelea kuvuta mdomo.
Camilla hakujali, alimsogelea akambusu kisha akaondoka kuelekea Ferry. Alipofika alikuta tayari Davis na Zulfa wameshafika na wao.
Pia watu wa uokoaji walikua tayari kwaajili ya kwenda kuwatafuta.
“Ni Silver pekee ndo hajapatikana?” Camilla alimuuliza Davis
“Aaah wamesema wapo wawili na walikua wanashea boya kama walivyo fanya wengine! Ni Silver na dada mmoja ivii wamesema anaitwa Jolene sema picha yake wameikosa”
Camilla aliposikia vile akaanza kuingiwa na kawivu! Mbali ya kumsaliti mumewe hakutaka kabisa Silver awe karibu ya mwanamke yoyote yule.
“Uyo Jolene ni nani kwani?”
“Alikua ni abiria! Hakuna mtu anajua taarifa zake”
“Kwaiyo akipatikana huyo dada na Silver nae atakua amepatikana?”
“Ndio!”
“Basi hakuna shida acha tuendelee kusubiri”
Waliendelea kusubiri huku zoezi la uokoaji likiendelea. Walipita kila kona na kila mahali ili kuwatafuta akina Silver!
Wapiga mbizi nao walikua makini kweli. Walipo choka walipokezana huku wakipumulia oksijeni kusudi waweze kuzama chini kabisa ya bahari.
Walianza asubui saa mbili mpaka saa nane mchana hawakuona chochote au kupata chochote cha kuwasaidia kujua ni wapi walipokuwa.
Ilipofika saa kumi kamili zoezi la uokoaji likafungwa kwaajili ya siku iliyofuata. Davis hakutaka kukubali kabisa, alitafuta wavuvi kadhaa, akakodi boti kisha akaenda nao kutafuta.
Walipita sehemu ambazo walihisi wale waokoaji hawakupita ila na wao hawakupata chochote. Hadi saa tatu ya usiku mambo yalikua mabaya bado.
Wale wavuvi aliokua nao walilalamika sana kuchoka ivyo ikabidi Davis ahairishe uokoaji na kurudi ferry.
“Imekuaje? Umempata?” Aliuliza Camilla baada ya Davis kushuka toka kwenye boti
“Hapana”
“Mungu wangu”
“Usijali shem kesho nayo ni siku tutaendelea tena!”
“Kadri masaa yanavyo zidi kusogea ndivyo napata wasiwasi! Uko alipo Silver wangu sijui yupo katika hali gani”
“Tulia! Kila kitu kitakwenda sawaa, mimi naona turudi nyumbani tukampuzike kwaajili ya kukusanya nguvu za kesho”
“Hakuna shida”
Camilla aligeuka na kuondoka kurudi nyumbani mwenyewe kwani Zulfa aliondoka toka mchana. Huko nyumbani kwake Marcus alikuwepo. Alikuta kasha mpikia chakula na kumuandalia maji ya kuoga.
“Heee bado hujaondoka?”
“Niondoke wakati bado upo kwenye matatizo??”
“Umejuaje sijala?? Daah nimechoka sana” Camilla alivua viatu na kuingia ndani
“Vipi mmepata chochote?”
“Hakuna tulicho kipata”
Marcus kusikia vile akatabasamu kidogo bila Camilla kumuona.
“Mna hakika kabisa mmetafuta jinsi inavyo takiwa?”
“Marcus, wale waokoaji wametafuta karibia masaa nane, bado Davis nae akaenda kutafuta masaa matatu mazima ila hakuna kitu!”
“Mmhhh! Yawezekana labda wamezama”
“Wangekua wamezama miili yao ingepatikana kwa haraka zaidi! Mimi najua wapo hai ndo maana inakua ngumu kuwapata”
“Au pengine wamepelekwa na maji mbali ya mnavyo tegemea”
“Mbona kama unanikatisha tamaa! Nategemea unipe moyo ila mwenzangu naona kabisa lengo lako ni kunihuzunisha”
“Umeelewa vibaya my dear! Fanya hivii… kaoge kwanza kisha uje mezani tule! Baada ya hapo upumzike kwaajili ya kesho ama unasemaje?”
“Aya..” Camilla akaelekea chumbani kwaajili ya kwenda kuoga.
Basi kama ambavyo Marcus alisema, kweli Jolene na Silver walipelekwa na maji toka pale walipokua na kwenda mbali zaidi kwenye kisiwa kimojaa iviii kilichokua kimejitenga chenyewe.
Uzuri ni kwamba wote walikua salama salimini, na vile vile walivyokua wamekumbatiana ndivyo walivyo jikuta baada ya fahamu zao kuwarudia.
Silver alipoona Jolene yupo kifuani kwake akamsukuma na kusimama haraka. Mwili haukua na nguvu kabisa sababu hawakua wamekula na walishinda kwenye maji mda mrefu.
“Tupo hai…. Tupo hai” Jolene alifurai, nae akasimama huku akitazama kulia na kushoto, akashangaa kuona msitu wenye miti mingi mirefu. Hapakua na nyumba wala mtu yoyote zaidi yake yeye na Silver.
Aliporudisha macho yake upande wa kulia akaona bahari kubwa isiyo kua na mwisho. Sehemu waliyokua nika kisiwa kadogo kalichokua kamejitenga katikati ya bahari.
Jolene akaogopa mno sababu pia palitisha sana
“Hapa ni wapi?? Hapa ni wapi?”
Silver hakumjibu, yeye mwenyewe hakujua pale ni wapi ila alichojua ni kwamba walikua kwenye kisiwa.
“Mbona hujibu?? Eeeh hapa ni wapi??”
“Kisiwani”
“Kisiwa kipi? Mbona hakuna watu?? Hakuna hata nyumba jamani”
“Ni Mara chache kwa kisiwa kukaliwa na watu”
“Kwaiyo tunatokaje?? Mimi sitaki kubaki huku panatisha sana”
Silver hakutaka kupoteza mda wake kumjibu, alipiga hatua taratibu ili kuangalia kama lile eneo lina usalama kwao na pia kutafuta msaada kama ingewezekana.
“Unaenda wapi? Wee Captain unaenda wapi??”
“Kaa hapo nakuja”
“Akuuuu! Uniache peke yangu?? Hapana, tunaenda wote” Jolene alikimbia haraka haraka alipomfikia Silver akamshika mkono.
“Kama unataka kwenda na mimi usini shike! Kila mtu atembee kivyake”
“Mhhhh sawa”
Akamuachia mkono wake na kuendelea kutembea huku macho yao yakiangaza huku na kule. Waliingia ndani kabisa ya ule msitu, palitulia tuliii, ni sauti za ndege ndizo zilizokua zinasikika kwa mbali.
Alafu sasa ardhi ilikua imeloa vya kutosha sababu kwenye kile kisiwa mvua hunyesha kila wakati. Walizidi kutembea huku Jolene akigeuka nyuma kila dakika sababu ya uoga aliokua nao.
Walipofika mbele kidogo Jolene akaona kama jani linacheza lenyewe akahisi kuchanganyikiwa. Alikimbia spidi na kwenda kumkumbatia Silver kwa nyuma.
Jinsi alivyo mkumbatia, hata Silver mwenyewe akahisi msisimko wa ajabu kwenye mwili wake! Mara ya mwisho kwa yeye kuhisi vile ni siku ambayo alishikwa na Camilla. Akadhani labda ni njaa ndo iliyokua inamsumbua
“Nini??” Alitoa mikono ya Jolene haraka
“Pale! Palee…. Kuna jani linacheza cheza lenyewe” aliogopa kweli mpaka akawa anatetemeka🤣.
Silver akageuka taratibu kuangalia sehemu ambapo jani linacheza cheza lenyewe ndipo akaona kuna ndege. Akajikuta tu anatabasamu 🤣
“Ni ndege”
“Ni ndege??? Uuuuuu!” kidogo Jolene akapumua
“Kama huwezi kwenda na mimi rudi kule baharini”
“Sitaki, najua ukipata msaada huko utaondoka uniache! Akuu apa tunaenda wote! Mguu wako mguu wangu”
“Ok!”
“Nishike basi mkono, au niruhusu nishike wako! Mimi naogopa kutembea mwenyewe”
Silver alimuangalia sana Jolene asipate kummaliza.
“Lakini kulala na wababa wakubwa wenye umri sawa na babu zako huogopi sio??”
Maneno ya Silver yalimkera Jolene. Akajihisi vibaya mno maana Silver alikua anamlaumu tu pasipo kujua ni sababu gani ilimpelekea afanye vile anavyo fanya.
“Usimlaumu sana mtu usie mjua maana katika hii dunia hakuna alie mkamilifu. Mbona mimi sijakulaumu wewe kwa kua mzembe mpaka tukapata ajali?? Nimenyamaza kimya kama hakuna chochote kilicho tokea!… hata siendi tena narudi nilipo toka”
Jolene aligeuka na kurudi baharini, alitembea haraka tena kwa hasira hata asitizame chini. Hakufika mbali, aliteleza akadondoka na kukalia mguu.
Maumivu aliyo yasikia yakamfanya aanze kulia.
“Umeona hasira zako?” Alisema Silver akimsogelea
“Usinishike niache”
Silver hakumsikiliza, aliinama kidogo akambeba kwenye mikono yake na kurudi nae baharini. Basi Jolene akiwa mikononi mwa Silver ndo akapata nafasi ya kumchunguza vizuri.
Alimuangalia sana hata asichoke sababu ni kijana flanii bomba mno. Silver akagundua Kua Jolene alikua akimchunguza, akamuambia
“Unani chunguza sana! Bakisha na baadae”
Jolene akahisi aibu vibaya mno, akavuta mdomo na kutazama pembeni.
We unahisi ni kipi kitatokea baina ya Silver na Jolene kwenye kile kisiwa??
Nakuja………….
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote