Frank ni mwanaume tajiri ambae sumbuliwa sana na maradhi ambayo anaamini hana muda mrefu wa kuishi hivyo anaamua kukata tamaa ya kuowa anaamua kuishi mwenyewe.
Kuna siku alitoka safari dereva wake alienda kumpokea Frank akataka kwenda kazini badala ya nyumbani huko kazini anakutana na mfanya usafi mgeni mwana dada mcheshi , mrembo na mwenye mvuto(vivian ).Frank alitokea kuvutiwa nae lakini hakutaka kuweka wazi hisia zake. Siku moja usiku Frank anakutana na vivian anahudumia watu bar kitendo kile kilimshitua sana Frank , alimfuata lakini vivian hakutaka kuongea nae pale aliomba waongee kesho sababu alikuwa bize kuhudumia wateja.
Kesho yake wanakutana ofisini wanaongea Frank anamuongeza mshahara na kutaka aache kazi ya bar.
Siku zinaenda wanatokana na kufanya wafanyakazi wengine kushangaa maana ceo alikuwa zieleki.
Siku moja Frank anaomba vivian amtembelee nyumbani kwake vivian akakubali.
Alipoenda Frank anatoa ombi la kuzaliwa mtoto lakini kwa mkataba wa kulipana. Vivian vanashituka sana lakini kwa dau alilotajiwa anakubali.
Vivian anabeba mimba na kuishi kwenye nyumba ya Frank.
Madam Caroline shangazi yake Frank anafika lakini anachukiwa anapomuona vivian akiwa mjamzito.
Shangazi yake Frank anakuwa mkali sana na mwenye chuku kwa vivian .
Vivian anakuja kupata taarifa kuwa kuna wenzake wawili wamefariki na mimba zao na wengine mimba zilitoka sababu shangazi yake Frank hataki Frank awe na mtoto (mrithi) pia maradhi ya Frank chanzo ni shangazi yake.
Je vivian atafanya nini kujiokoa yeye na mimba yake ya mkataba naatafanya chochote kumsaidia baba ya mtoto wake kumsaidia ili ajue adui yake ni shangazi yake na binamu yake Jacob?
CEO NA MIMBA YA MKATABA 1
MTUNZI SMILE SHINE
Frank ni mwanaume wa makamo mwenye umri wa miaka 39, ni mtu ambae ana miliki mali nyingi pamoja na makampuni makubwa ila shida na tatizo lake hakuwa anataka kabisa kusikia swala la kuowa wala kuanzisha familia kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua alinikazia tamaa na kuona hawezi kuwa na familia japo kuna muda alitamani kupata mrithi wa mali zake.
Frank alikuwa anasumbuliwa yasiyoelezeka mara mifupa yake kushika, mara figo kufeli na moyo kuwa mkubwa mara kwa mara alikuwa akienda nje kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Siku moja alikuwa anatoka safarini mfanyakazi wake akaenda kumpokea uwanja wa ndege .
" Habari boss , pole na safari.
Alisalimia Daniel huku akipokea mzigo na kwenda kupakia kwenye gari.
" Asante.
Daniel aliwasha gari kwaajili ya kuanza safari ya kuelekea nyumbani lakini Frank akamwambia.
"Daniel naomba unipeleke kwanza ofisini .
" Boss lakini umetoka safari unatakiwa kupumzika kwanza.
" Unanipangia nini cha kufanya ?
" Hapana nilikuwa natoa ushauri tu.
" Fuata ninachotaka.
" Sawa.
Dereva akiitii wakaenda mpaka kwenye kampuni yake ya Dala's entertainment.
Alipofika wafanyakazi wote walisimama na kumsalimia kwa heshima . Aliingia kwenye lifti na kuelekea ghorofa ya 3 ilipo ofisi yake akiwa karibia na ofisi yake alimuona binti mrembo akifanya usafi. Yule binti hajua kama ceo kafika na anataka kuingia ofisini kwake.
" Kaka issa leo nitakusikamisha mpaka nitakapomaliza kusafisha maana umezidi sana kuwahi unanikuta bado nafanya usafi.
Frank aliendelea kusimama akiwa anasubiri kupishwa na yule binti aliendelea kufanya usafi bila kuangalia nyuma yupo nani.
Mara Issa alifika akakuta boss , ceo wa kampuni kasimama na binti vivian yupo Bize anafanya usafi.
Issa alitembea kwa kasi ili amshitue apishe ceo lakini frank alimzuia kwa kumshika mkono wakasimama wote wakawa wanamuangalia mpaka alipomaliza akageuka huku akisema
" Angalau leo umeheshimu nilichokwambia unaweza kuingia.
Vivian alipomuona mwanaume mrefu , mwenye sura ya kuvutia , nywele zake zilikuwa zimenyolewa mtindo wa kupendeza zilizompa mvuto zaidi amevalia suti nadhifu na kiatu chake cheusi kunachongaa aligundua huyo ndio ceo wa kampuni mr Frank .
Watu hawa hawakuwa wanafahamiana kwani wakati binti vivian anaanza kazi pale kwenye kampuni mr frank hakuwepo ila alikuwa anasikia tu story zake.
Vivian alisogea pembeni akasalimia kwa heshima huku akiinamisha kichwa chake chini.
Mr Frank aliitikia salamu kisha akapita na kuingia ofisini kwake na Issa akamfuata nyuma.
Mr Frank alikaa kwenye kiti chake na kuangalia vitu vyake kwenye pc alipomaliza alivua koti lake la suti Issa akampokea na kuhifadhi vizuri, Frank alikunja mikono ya shati lake lenye mikono mirefu.
" Huyu binti ni mgeni ?
" Ndio
" Ana muda gani?
" Huu ni mwezi wa pili sasa tangia ameanza kazi hapa.
" Nahitaji kahawa naomba uniagizie.
" Sawa.
Issa alitoka ofisini na kwenda kuagiza kahawa kwaajili ya boss kisha akarudi ofisini.
Baada ya muda vivian aliingia ofisini akiwa na chupa ndogo iliyojaa kahawa na vikombe.
Alitengwa mezani na kuuliza.
" Samahani boss naweza kumimina kahawa kwenye kikombe?
" Sawa mimina.
Alimimina alipomaliza
kumkaribisha.
" Boss karibu kahawa.
" Asante.
Vivian aliondoka akiwa kabeba trei, Frank alimuangalia kisha akasema
" Sijawa kuona muhudumu muungwana hivi.
Issa alishangaa mr Frank hajawahi kumsifia mtu kirahisi namna ile ila kwa vivian alimsifia kwa jambo dogo tu la kumkaribisha kahawa.
" Uungwana, mcheshi ni kawaida yake.
Ilipita kama wiki moja majira ya jioni Frank aliamua kutoka na kwenda kutembea katikati ya mji ili kupunguza mawazo . Alienda kwenye club moja na kwenda kukaa sehemu ya VIP wakiwa na dereva wake wanapata vinywaji huku wakisindikizwa na burudani ya muziki laini
Mara Frank alimuona mtu kama vivian akihudumia, alihisi kama vile macho yake yanamdanganya alizidi kuangalia kwa makini , mwishowe alijihakikishia kuwa yule ni vivian mfanya usafi wa kwenye kampuni yake, taratibu alinyanyuka na kumfuata kwenye meza aliyokuwa anahudumia akasimama kwa nyuma
Vivian alipogeuka akamuona Frank alishituka sana.
" Boss...
" Vivian unafanya nini?
Vivian alinyamaza kwanza , Frank walimshika mkono na kumvutia pembeni ili wakaongee vizuri
" Boss hapa nipo kazini .
" Kazi gani hii?
" Ni kazi kama kazi nyingine boss wangu.
" Inamaana ile unayofanya kwenye kampuni yangu sio kazi au haikutoshelezi?
" Boss Naomba majibu ya maswali yako niyajubu kesho.
Vivian akikatisha maongezi baada ya watu kuwa wanasumbua wanahitaji huduma mpaka kuna wengine walianza kuongea maneno yaliyokosa heshima kwa boss wake.
" Oya muache huyo dem atuhusumie kama kumnunua utanunua badae .
Frank alimuacha aendelee na kazi lakini hakufurahishwa kabisa na ile kazi.
Kesho yake Frank alipofika kazini kitu cha kwanza alitaka kuonana na vivian ili ajibu maswali yake.
Vivian aliingia ofisini kwa boss kwa kujiamini. Alisalimia na kukaa .
" Vivian unaweza kuniambia kwanini unafanya kazi night club ikiwa na hapa una fanya kazi au mshahara wangu haukutoshelezi?
CEO NA MIMBA YA MKATABA 2
MTUNZI SMILE SHINE
Vivian aliinama kwa muda kama vile alikuwa anatafakari jibu la kumjibu boss wake.
" Swali langu ni gumu? Frank aliuliza kwa sauti ya juu kidogo.
" Hapana .
" Kwahiyo ni kiburi ndio maana umenyamaza?
" Hapana .
" Ila?
" Boss napitia kwenye maisha magumu sana hapa mjini sina baba, sina mama wala ndugu yoyote nipo mimi kama mimi sina wa kumlilia shida wala wa kukimbilia ninapopatwa na matatizo , mambo yangu yote najisimamia mwenyewe, pesa inayopata hapa hainitoshelezi inanibidi nifanye kazi nyingine mbali na hii ili kuweka mambo yangu sawa. Na muda wangu mwingine ni usiku ndio maana nimeamua kufanya kazi kwenye night club . Sifanyi kwa kupenda ila ni shida ndio zinanisukuma kufanya hivyo.
Frank alimuangalia huku akiwa anamuonea huruma kutokana na maelezo aliyojiekezea kisha akashusha pumzi wakati huo vivian alikuwa akimuangalia ili kusikia tamko la boss maana alishaambiwa huyo mtu huwa hapendi ujinga na huwa hakawii kutoa maamuzi magumu.
" Mshahara wako hapa huwa unapokea kiasi gani?
"Laki 3
" Kwahiyo nikikuongeza mshahara mara mbili ya unaopokea utaachwa kufanya kazi sehemu nyingine?
" Ndio boss nitaacha.
" Basi kuanzia leo mshahara wako umepanda na kama kutakuwa na tatizo lolote basi nipigie simu uniekezee.
Frank alichukua kadi yenye namba zake za simu akampatia.
" Asante sana boss nashukuru sana.
" Unaweza kwenda.
Vivian alitoka ofisini kwa boss akiwa na furaha siku hiyo alitaniana na kuongea na kila aliyemuona alifanya usafi akiwa na tabasamu usoni huku akiimba nyimbo za kumshukuru MUNGU.
Siku zilienda maisha yaliendelea kuwa mazuri na kwa kiasi fulani maisha yalianza kubadilika kwa upande wa vivian , alihamia kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mwanzo nyumba ya miti iliyokuwa na matobo ya kutosha ambayo alijitahidi kuziba na matambara akaamua kwenye chumba chenye muonekano mzuri pia chenye usalama.
BAADA YA MIEZI 6.
Siku moja akiwa anafanya usafi akasikia baadhi ya wafanyakazi wakiongea kuhusu Frank.
" Nasikia hali ya boss Frank sio nzuri na amelazwa kwenye hospitali ya St thomas.
" Mmmh mbona mimi nilisikia kasafiri yupo nje ya nchi?
" Watu wanaficha tu ukweli ndio huo.
" Masikini.
Zile taarifa zilimuhuzunisha sana vivian .
" Kumbe anaumwa ndio maana leo siku ya tatu sijamuona kazini, sasa kwanini wafiche kama ni mgonjwa?
Akiwa anajiuliza hayo maswali mara alipita Issa.
" Wewe acha kusimama maliza kazi.
Vivian alishituka akamuangalia
" Samahani kaka Issa naomba kukuuliza swali.
" Eheee uliza.
" Ni kweli kuwa boss Frank ni mgonjwa na yupo hospitali?
" Wewe umepata wapi hizo habari?
" Naomba unipe jibu tafadhali.
" Ni kweli yupo hospitali amelazwa alizidiwa juzi usiku akiwa nyumbani kwake.
" Maskini hizi habari zimenihuzunisha sana.
" Badae twende tukamuone.
" Mmmh naogopa.
" Unaogopa nini?
" Inaonekana hataki watu wajue juu ya ugonjwa wake sasa akiniona huko si itatua maswali au atakasirika.
Issa alitabasamu alafu akasema.
" Wala hawezi ni watu wanamuogopa.
" Basi sawa ukienda uniambie twende pamoja.
" Sawa.
Baada ya kukubaliana vivian aliendelea na kazi yake na Issa alienda kufanya kazi zake.
Ulipo karibia muda wa kwenda hospitali Issa alimfuata vivian.
" Tunaweza kwenda sasa.
" Sawa nipe dakika mbili nikachukua mkoba wangu.
" Sawa.
Vivian alienda kuchukua mkoba baada ya sekunde kadhaa alirudi wakaondoka na kwenda hospitali ya St thomas.
Waliingia kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Frank, vivian alishangaa na kuongea kwa sauti ya chini akimwambia Issa
" Sijawahi kuona wodi ya namna hii ?
" Kwanini?
" Mbona kizuri hivi yani kuna mpaka mauwa , kusafi, kinanukua vizuri sio harufu za dawa.
" Ukiwa na pesa hakuna kinachoshindikana kila kitu kizuri utapata.
" Hapo kweli kabisa.
Wakasogea mpaka kitandani walimkuta Frank akiwa kupitiwa na usingizi lakini baada ya muda alifungua macho na kuwaona wakiwa wamesimama pembeni yake. Akitoa tabasamu huku akiwaangalia kwa macho yaliyokuwa yamekosa nguvu alafu akaongeza kwa sauti ya chini akisema
"Issa, vivian mmekuja kuniona.
" Ndio boss pole"
" Asante.
Walikaa kwa mgonjwa kwa muda wa dakika kumi baada ya hapo wakaaga
" Boss sisi tunaenda tutakuja tena wakati mwingine kukuona.
" Sawa asanteni sana.
Issa na vivian akipiga hatua kuelekea mlangoni mara Frank akaita.
" Vivian.
" Abeee boss
" Naomba usichoke kuja kumuangalia
" Sawa boss tutakuja kesho.
Wakiwa wanatoka nje ya jengo la hospitali Issa asema.
" Nyota yako ipo juu sana.
" Kwanini?
" Frank sio mtu wa kuzoeana na mtu kirahisi hivyo hasa watoto wa kike lakini kwako naona mnaelewana sana .
" Basi nyota yangu na yake zimeendana .
" Labda lakini nimeona ajabu pale alipokwania uwe unaenda kumuangalia au kuna kitu kipo kati yenu?
Vivian alimuangalia Issa alafu akacheka.
" Nitakuwa na kitu gani na boss mimi na unajua yule mtu alivyo bandidu tabasamu lake nimeliona leo tena kwa mbali sijui huyo mke wake anaishi nae vipi hapo ndani.
" Frank hana mke.
Alijibu Issa na vivian alimkazia macho kwa muda.
" Sijamuelewa hana mke kumuacha au hana mke ametangulia mbele za haki?
" Hajawahi kuowa.
" Acha basi masihara.
" Huo ndio ukweli labda afanye maamuzi ya kuowa leo au kesho lakini huko nyuma hajawahi kuishi na mwanamke kabisa.
CEO NA MIMBA YA MKATABA 3
MTUNZI SMILE SHINE
kila siku vivian alikuwa anaenda hospitali kumuangalia CEO wao na kumuhudumia mambo madogo madogo kama kumpa chakula kumfuta jasho na mengineyo.
Siku waliporuhusiwa vivian alienda nae mpaka nyumbani kwake.
Nyumba yake ilikuwa ni kama vile jumba la kifalme kulikuwa na wafanyakazi karibia kumi kila mmoja alikuwa na kazi yake. Walipo shuka tu kwenye gari wafanyakazi wote walijipanga mstari kwaajili ya kumpokea boss wao . Dereva alimsaidia kumshika mkono wakaingia ndani huku vivian wakiwa anawafuata nyuma huku akiangalia maandhari ya mazingira yavyokuwa yalivutia na kupendeza.
Walifika ndani na kuangaliwa chakula. Vyakula vilipamba meza kama vile kulikuwa kuna sherehe kila mtu alikula alichotaka tena mpaka atosheke.
Baada ya kupata chakula vivian alishukuru na kuomba ruhusa ili aweze kuondoka.
" Kwakuwa muda umeenda acha nikuruhusu pia asante sana kwa huduma zilizokuwa ukinipatia .
" Usijali boss.
" Basi acha dereva akupeleke.
" Sawa.
Vivian waliondoka na dereva na Frank alienda mchumbani kujipumzisha.
Siku zilizidi kwenda Frank na vivian walikuwa ni watu wanaopatana japokuwa hawakuwa na ukaribu sana ila kuna wakati walikuwa wakiongea mawili matatu kuhusu maisha basi tofauti na wafanyakazi wengine walikuwa wakiongea maswala ya kikazi basi na wengine hawajawahi kabisa kuongea nae.
Siku moja Frank akiwa ofisini kwake alitembelewa na mwanadada ulimbwende Anne ambae aliwahi kushinda kwenye shindano la urembo na kuchukua taji huko miaka mitatu nyuma.
Anne na Frank waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini walikuja kuachana baada ya Anne kutoa mimba ya Frank akidai kuwa umri wa kuzaa kwake ulikuwa bado hakutaka kuzeeka mapema , Frank alishikwa na hasira na kuamua kuachana nae tangia siku waliyoachana hawakuwahi kuonana ndio siku hiyo Anne alienda kumtembelea.
" Karibu sana Anne.
" Asante, unaendeleaje?
" Naendelea vizuri.
" Nilipata habari kuwa unaumwa.
" Nipo sawa sasa.
" Ni jambo la kushukuru Mungu.
Baada ya kujuliana hali wote walikaa kimnya kwa sekunde kadhaa.
" Aaah utatumia kinywaji gani?
" Nipo sawa na kilichokuleta ni kuwa nimekumiss sana
Anne aliongea kwa Madaha huku akimuangalia kwa jicho la mahaba. Frank alimuangalia alafu akasema
" Asante.
Anne hakuridhika na asante ya Frank alinyanyuka akamfuata na kuzunguka nyuma yake na kumshika mabegani kisha akainama kidogo saizi ya sikio na kusema.
" Baba tusahau yaliyopita tuendelee penzi letu kipindi kile usichana ulikuwa unanisumbua.
Frank aligeuka kumuangalia alafu akasema.
" Kwahiyo umemaliza mambo yako, umehangaika mpaka umetosheka.....
" Mmmmmh isifike huko kilichotokea tukisahau sasa nipo tayari kukuzalia hata ukitaka watoto sita nitazaa.
Frank aliachia tabasamu lililofanya uso wake uwe na nuru. Anne alivyoona lile tabasamu akajua mambo yameisha alizunguka na kukaa mapajani kwake na kupeleka midomo yake karibu na midomo ya Frank na kutaka kumbusu lakini kabla hajafanya hivyo mlango ulifunguliwa na vivian akaingia.
Anne alimuangalia huku akiwa kakunja uso pia vivian alishituka kwani alikuwa anajua Frank hayupo ofisini.
" Wewe hiyo ni adabu ya wapi unaingia ofisini kwa ceo kama unaingia chumbani kwako?
" Nisamehe madam. Alijibu vivian huku akiwa kusimamisha kichwa chini na mikononi kwake alibeba trei ya kahawa .
Vivian alitaka kutoka lakini Frank akamzuia .
" Vivian lete kahawa. Anne naomba uende.
" Niende wapi baby?
" Mimi na wewe tulishamalizana siku nyingi na siwezi kurudiana na wewe.
" Frank kwahiyo umeamua kujidhalilisha mbele ya huyu mfanyakazi wako.
Vivian alitengwa kahawa haraka haraka alafu akatoka na kuwaacha na marumbano yao.
" Anne naongea kistaarabu sana naomba utoke kabla sijafika njia nyingine kukutoa hapa .
" Frank.....
" Sitaki kusikia chochote kutoka kwako njia nyeupe pita nenda . Frank aliongea kwa ukali ikabidi Anne abebe pochi yake na kuondoka kwa hasira.
Baada ya Anne kutoka Frank alipiga simu kwa vivian na kumtaka aende ofisini kwake.
Baada ya dakika chache vivian alifika kwenye ofisi ya ceo na kusimama mbele ya meza ya Frank.
" Karibu ukae.
Vivian alijaa kwenye kiti na kusikiliza wito.
" Vivian naomba unisamehe kwa kile kilichotokea.
" Nisamehe mimi boss sikujua kama ulikuwa ofisini ndio maana sikuona haja ya kubisha hodi.
" Usijali na wala usijisikie vibaya kwa kilichotokea.
" Mimi nipo sawa boss.
" Sawa yangu yalikuwa hayo tu.
" Sawa boss. Alijibu vivian kisha akasimama kwaajili ya kutaka kutoka. Lakini kabla haujatoka Frank alimuita vivian alisimama na kugeuka kusikiliza alichoitiwa.
" Jioni ya leo unaweza kufika nyumbani kwangu?
: CEO NA MIMBA YA MKATABA 4
MTUNZI SMILE SHINE
Vivian alitulia kwa muda bila kujibu swali na Frank alikuwa akimuangalia akisubiri jibu kutoka kwake.
" Vipi ni swala ambalo haliwezekani?
" Sawa nitakuja.
" Shukran kwa kukubali ombi langu , ukiwa tayari utanipigia simu ilinimtume dereva aje akuchukue.
" Sawa boss.
Vivian alitoka pale ofisini kwa Frank akiwa anaongea mwenyewe
" Boss anataka niende kwake kutakuwa kuna nini? Au anataka tupate pamoja chakula cha jioni nyumbani kwake kwasababu ya yule mwanamke waliokuwa wanakiss kanifokea sasa anahisi kuwa nimejisikia vibaya?
Alafu kwanini alikasirika baada ya yule mwanamke kunifokea ?
Lakini hayo hayanihusu ya ngoswe acha nimuachie ngoswe.
Jioni ilipofika vivian akijiandaa akiwa anamalizia kujiandaa simu yake iliita Frank alikuwa anapiga. Vivian alipokea.
" Vipi vivian?
" Safi.
" Dereva anaweza kuja au bado haujapanga kutoka muda huu?
" Nimeshajiandaa anaweza kuja tu.
" Ok atakuwa hapo baada ya dakika chache.
" Sawa.
Vivian alimaliza kujiandaa akatoka nje akawa anamsubiri dereva aende kumchukua .
Baada ya dakika kama 20 kupita dereva alifika nyumbani kwa vivian na akamchukua na kuelekea kwenye nyumba ya boss wao mr Frank.
Alipofika nyumbani kwa Frank alipokelewa na mfanyakazi na kukaribishwa ndani. Vivian alitaka kuishia sebleni kama siku zote anapokuwa anaenda pale lakini yule mfanyakazi akamwambia.
" Nifuate tafadhali.
Vivian alimfuata wanapandisha ngazi na kwenda mpaka juu ghorofani wakaingia kwenye chumba kimoja kuta zake zilikuwa za vioo pia kulikuwa kuna mlango mkubwa wa kioo ukiwa huko juu ulikuwa unaona jinsi mji ilivyo na bahari kifupi kilikuwa na muonekano mzuri pia hali ya hewa ilikuwa safi sana.
Frank alikuwa kajilaza kwenye kiti kilichokuwa na muundo kama kitanda flani huku akiwa na grass ya kinywaji pembeni .
Frank alipomuona vivian alinyanyuka na kumkaribisha.
" Oooh vivian karibu.
" Asante.
" Karibu ukae.
Vivian alienda kukaa kwenye kiti kilichokuwa mbele yake.
Baada ya kukaa mfanyakazi alisogea alipokuwa kakaa vivian na kumuuliza.
" Samahani utatumia kinywaji gani? Au utataka chakula gani?
Vivian alitoa na hi hakujua aagize nini wakati huo Frank alikuwa akimuangalia ikabidi aseme .
"Nipatie maji tafadhali.
Frank alimuangalia alafu akauliza
"Maji? Kwanini maji ?
" Nayo yanafaa huwa napenda sana kunywa maji.
" Kuwa huru kuagiza unachotaka wewe ni mgeni wangu.
" Hicho nilichoagiza kina nitisha sana boss.
" Jenister hebu lete wine na juice bila kusahau hayo maji. Frank aliamua aagize na vinywaji vingine ilivaje kujichagualia kitakacho mtaa.
" Sawa boss.
Jenister alijibu alafu akaondoka kwenda kuchukua.
Kama kawaida hakukuwa na story walitulia kimnya huku vivian akiwa anaangalia mazingira ya nje.
Vivian aliamua kuvunja ukimya kwa kusema
" Hii sehemu ni nzuri sana upepo wa bahari inafika mpaka huku.
" Ndio mimi huwa napenda sana kupumzika huku hata nikiwa na msongo wa mawazo huku ndio tiba yangu.
"Kweli huku kunafanya mtu ujisikie vizuri .
Baada ya muda vinywaji na kuku wa kuchomwa vililetwa wakawa wanakula kimnya kimnya huku vivian wakiwa anabonyeza simu yake .
Frank alikuwa akimuangalia vivian kwa kuibia na kuonekana kuwa ana jambo anataka kuongea lakini ni kama alikuwa anasita kuongea.
Badae aliona ni upumbavu kukaa kimnya bila kusema kile alichotaka kusema.
" Vivian kuna jambo nataka tuongee .
" Sawa boss.
" Vivian......
" Abeeeee
Frank aliishia kuita jina la vivian na vivian alikuwa makini kusikiliza.
" Vivian kuna kazi nataka kufanya na wewe nitakulipa pesa yoyote utakachotaka ikiwa utakubali kunifanyia hiyo kazi. Hiyo kazi sio lazima ni hiyari yako kufanya au kuacha.
" Ni kazi gani boss?
" Nataka kuzaa na wewe, unizalie mtoto .
CEO NA MIMBA YA MKATABA 5
MTUNZI SMILE SHINE
Vivian macho yalimtoka alikuwa kashika kipande cha nyama ya kuku alirudisha kwenye sahani , wote waliangaliana bila kupepesa macho.
" Ikiwa utakubali tutaandikishiana mkataba ninachohitaji ni mtoto tu.
Vivian walishusha pumzi hili swala lilikuwa zito kwake kwanza hakutegemea kama Frank angemtamkia neno kubwa kiasi hicho.
" Lilikuwa ni ombi tu kama haitawezekana basi.
" Boss naomba unipe muda wa siku mbili nitskupatia jibu kwa sasa siwezi kusema chochote.
" Sawa.
Swala la Frank kuomba kuzaa nae ilijirudia kichwani kwake alikaa pale akiwa hana amani tena .
" Boss naweza kwenda sasa.
" Sawa karibu tena.
Vivian alishuka chini akamkuta dereva yupo nje wanapiga stori za mpira na mlinzi.
" Dereva nataka kuondoka.
" Sawa dada vivz ngoja nikupeleke.
Wakati vivian akasogea karibu na gari ili apande aliangalia juu wakitaka macho na Frank kwani nae alisimama akawa anawaangalia huku chini.vivian alipanda kwenye gari wakaondoka.
Akili ya vivian iliwaua mbali sana hasa alipokuwa anakumbuka kauli ya Frank.
" Hivi huyu baba kawaza nini mpaka aniambie kuwa anataka kuzaa na mimi na anachotaka ni mtoto tu.
Mmmh huu mbona ni mtihani mkubwa sana kwangu hili swala natakiwa nikalifikirie nyumbani kwa kina.
Vivian alizubaa kwa mawazo mpaka dereva aliposhituka kwa kuuliza
" Mbona upo mbali sana una waza nini?
" Aaah hamna .
" Lakini uko mbali sana na sio kawaida yako sijazowea kukuona ukiwa mkimnya hivyo uchangamfu wako uko wapi?
" Siku hazilingani kaka yangu.
" Ni kweli ila kwako imezidi inaonekana kuna jambo lina kusumbua.
" Tuachane na hayo.
Kweli waliachana na hayo maswala wakaendelea na story nyingine mpaka vivian alipofika nyumbani kwake.
Huko nyumbani kwake ndio alipata uwanja mzuri wa kuwaza na kuwatia lakini bado hakupata jibu la kwanini Frank alimtaka yeye azae nae.
Kulipokucha asubuhi alitulia kitandani kisha akisema
" Mimi nina shida zangu kibao na kama atanilipa pesa nzuri kuna haja gani ,a kukataa hii ofa acha nizae niweke maisha yangu sawa hapa nikisema anilipe millioni 50 si nitafunga biashara na kuachana na kazi za kuajiriwa.
Vivian alipitisha kukubali kuzaa.
Alipofika kazini alienda kuonana na Frank kwaajili ya kumpatia jibu lake.
" Habari za asubuhi boss.
" Salama vivian upo salama wewe.
" MUNGU ni mwema nipo salama. Boss nimekuja kukupa jibu la lile swala tuliloongea jana usiku.
" Eheeeee umeamua nini?
" Nitafanya.
" Una uhakika maamuzi yako ni sahihi?
" Ndio boss.
" Sawa unataka nikulipe kiasi gani?
" Milioni 50. Vivian alitamka hiyo hela huku macho yakiwa makavu mwenyewe aliona kataka hela nyingi sana lakini kwa upande wa Frank alicheka kidogo.
" Unasema milion 50 hizo zitakutosha?
" Zitakutosha sana boss.
" Basi sawa mimi nitakuongeza 50 iwe million 100.
Vivian alijikuta anacheka hiyo hela ilikuwa ni hela kubwa sana kwake.
" Sawa boss nitafanya.
" Najua una maswali mengi sana juu ya hili ombi langu .
" Ni kweli kwanini umetaka mtoto wa mkataba na sio kuowa mke mkaanzisha familia?
"Kwenye maisha yangu siwezi kuowa.
Vivian aliposikia hivyo akili yake ilifikiria huenda Frank akawa na tatizo la nguvu za kiume.
" Mimi sina umri mrefu wa kuishi hivyo nahitaji mrithi wangu.
" Unamaana gani kusema hivyo boss?
" Mwili wangu ni dhaifu una maradhi yasiyojulikana muda wangu wa kuishi kwenye hii dunia unahesabika na nilipogundua kuwa nina huo ugonjwa nilikata tamaa ya kuanzisha familia. Kwasababu sikutaka kumuacha mke kwenye wakati mgumu lakini kwa sasa nataka angalau mtoto ambae atanirithi hata ndugu zangu wakimuona wawe wanakumbuka kama kulikuwa kuna mtu kama mimi kwenye hii dunia. Frank alimaliza kuongea kisha akaachia tabasamu lakini halikuwa tabasamu lenye furaha bali lilikuwa la kuficha maumivu
Vivian alijikuta anamuonea huruma mpaka machozi yalimtoka akageuka pembeni akavuta machozi.
Frank alifungua droo na kutoa karatasi na kumpatia .
" Huu ndio mkataba wetu unatakiwa kusaini hapo, pia unatakiwa kunipa namba za account yako kwajili ya kujiingizia hizo pesa baada ya wewe kubeba ujauzito.
" Sawa.
Vivian alipitia ule mkataba alafu akasaini na kuirudisha kwa Frank.
" Unatakiwa kuacha kazi hapa ofisini pia utahamia nyumbani kwangu.
" Kwanini iwe hivyo boss?
" Hivyo ndivyo inatakiwa. Na kesho tutaenda hospitali kwajili ya kupata vipimo vyako na kupata vitamins kwaajili ya kuandaa mji wa mimba.
" Sawa.
Kesho yake walienda hospitali wakifanyiwa uchunguzi kila kitu kilikuwa sawa na vivian alipewa vitamin na vidonge vingine kwaajili ya kuandaa mji wa mimba . Jioni vivian akaamua nyumbani kwa Frank alipo fika alimkuta Frank yupo nje akiwa anamsubiri.
Vijakazi walimpokea mizigo yake na kuingiza ndani. Baada ya hapo aliita wafanyakazi wote waliokuwepo na kutoa utambulisho.
" Huyu ni vivian wangoje mnajua wengine hamumfahamu kuanzia sasa ataishi hapa ndani mnatakiwa kumuhudumia vizuri .
" Sawa boss, karibu miss vivian.
" Asante.
Baada ya kukaribishwa vivian na Frank waliingia ndani.
" Jenista anafaa chakula kwaajili yetu. Alisema Frank na Jenista Alitii agizo akaenda jikoni kuandaa.
" Vivian nifuate nikakuonyeshe chumba chako cha kulala.
Vivian na Frank walipandisha juu kwaajili ya vivian kukijua chumba chake ambacho atakuwa analala na kufanyia mambo yake yote.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote