CEO WOMAN NA PENZI LA DEREVA DALADALA
Ni simulizi inayomuhusu binti Lilly
Lilly Marcel ni msichana wa miaka 24 ,mrembo na mchapakazi
Miaka mingi iliyopita baba yake Lilly Mr Marcel na mama yake Rita waliishi kwa furaha sana pamoja na mtoto wao Lilly , walimpatia kila kitu na kumthamini mtoto wao wa pekee
Mr Marcel alimiliki kampuni moja kubwa iliitwa MAC
Lilly aliishi maisha ya kupata kila alichokitaka kwa wakati
Lakini familia yao yenye furaha haikudumu kwa muda mrefu
Miaka 11 iliyopita mama yake bi Rita aliaga dunia kwa ugonjwa wa kansa
Haukupita hata mwezi baba yake Mr Marcel alioa mwanamke mwingine ambae alikuwa na watoto wawili John na johar
Maisha ya Lilly yalibadilika sana ni kama baba yake hakumjali tena kama zamani aliangalia familia ya mama wa kambo
Kila alichokifanya au kupewa johari dada yake wa kambo alikitaka pia
Alifikia hatua ya kumchukua mpenzi wa Lilly ili kumkomoa
Baada ya lilly kutokuwa sawa Mr Marcel alimpeleka marekani .
Miaka mitano baadae Lilly alirudi Tanzania na baba yake Mr Marcel aliamua kumpa cheo Cha CEO kwenye kampuni yake baada ya kuona John Hana muelekeo na hawezi kuiendesha kampuni
Siku moja Lilly akiwa njiani gari lake liliharibika aliamua kupanda daladala kwa mara ya kwanza
Ndipo alikutana na kijana victor ambaye ni dereva wa daladala
Kukutana kwao hakukuwa kwa kheri hata kidogo
Lilly na konda walibishana sana , victor alienda kutetea ugomvi
iikapelekea Lilly kumchukia victor
Victor alikuwa ni kijana mpole na mpambanaji kila mtu alimjua hata rafiki wa lilly aliyeitwa Angle alimfahamu pia
Siku moja Angle alimuhadithia Lilly historia ya maisha ya victor
Lilly alitokea kumunea sana huruma victor alimuajiri kama dereva wake wa binafsi
Bila kujua kadri siku zilivyozidi kwenda Lilly alijikuta anavutiiwa sana na victor walianza kuwa marafiki uliopelelea kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi
Lakini baadhi ya watu walimdhihaki na kumdharau binti tajiri kumpenda mwanaume Kapusi asie na kitu . Je baba yake atakubali huo uhusiano wao?
CEO WOMAN NA PENZI LA DEREVA DALADALA
MTUNZI SMILE SHINE
SEHEMU : 1
Katika familia ya Mr Marcel na bi Rita walibahatika kupata mtoto mmoja wakike waliyempa jina la lilly , kila mtu alimuonea wivu Rita kwani mumewe Mr Marcel alikuwa tajiri na alikuwa akimpenda sana , ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu kwani bi Rita mama wa Lilly aliaga dunia kwa maradhi ya kansa akimuacha binti yake lilly akiwa na miaka 13 tu.
" Tumeshamaliza msiba Sasa itakuwaje kuhusu Lilly?"
Aliuliza shangazi yake lilly bi Eva
" Sijui kama nimekuelewa au laa lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa naweza kumlea vizuri tu binti yangu sitaki msaada kutoka kwa mtu yoyote " alisema Mr Marcel
"Mmh mimi nakujua vizuri kaka yangu ndomana nilikuwa nakushauri uoe ili lily apate malezi Bora muda wote upo busy na kazi utamuangalia saa ngapi mtoto au utawaachia wafanyakazi" alisema Eva
"Eva naomba unyamaze huoni hata aibu ndo kwanza tumemaliza msiba unataka nikaoe mwanamke mwingine” alifoka Marcel kisha alinyanyuka na kuingia ndani "
“Utaoa tu nakwambia utake usitake na mwanamke wa kuoa tumeshakuchagulia " Eva aliondoka
"Daddy Ina maana mama ndo hayupo tena ?" Lilly alikuwa haamini amini kile kinachoendelea
"Ndio hatunae tena ngoja akapumzike ameteseka sana , nakuhakikishia nitakupa upendo wa hali ya juu na zaidi ya ule tuliokupa zamani mimi na mama yako " alisema Mr Marcel
" Asante sana Dady na mimi nakuahidi wewe na mama yangu aliyetangulia kuwa nitakuwa binti mzuri na mwenye mafanikio makubwa " alisema lilly huku anatabasamu
"Najivunia sana kuwa na binti kama wewe hata mama yako huko aliko atakuwa anajivunia sana kuwa na binti kama wewe " Mr Marcel alimkumbatia binti yake lilly ,
Baada ya week moja kupita lilly alirudi shuleni , ilikuwa ni shule ya bweni alikaa huko kwa miezi mitatu bila kurudi nyumbani.
Aliwasiliana tu na baba yake kupitia simu na Muda wa likizo ulipofika Lilly alirudi nyumbani alishangaa kukuta mazingira yapo tofauti na alimkuta mwanamke mmoja alionekana kama mama mwenye nyumba maana aliwafokea wafanyakazi na kuwatuma atakavyo
"Shikamoo Dady" Lilly alimsalimia baba yake Mr Marcel na kumpuuzia yule mwanamke.
"Marahaba , Lilly mbona upo hapa kwani ni kipindi Cha likizo ?" Mr Marcel alimuuliza binti yake lilly
"Daddy kweli umesahau kila kitu nadhani nilikwambia Leo ni siku yetu ya kufunga shule " lilly aliongea kwa kudeka kwa baba yake
“Oh samahani kipenzi changu unajua mambo mengi nilisahau kabisa" Mr Marcel aliongea huku anakuna kichwa chake
"Na huyu mwanamke ni nani naona anafokea wafanyakazi bila mpangilio wowote ?" Lilly aliamua kumuuliza baba yake, Mr Marcel alimuangalia yule mwanamke aliyekaa pembeni yake kisha akamgeukia lilly na hata kabla hajaongea chochote waliingia watoto wawili wakike na wakiume walionekana kama mapacha
" Shkamoo baba , shkamoo mama" walisalimia wale watoto walikuwa wakubwa kidogo kwa Lilly
"Marahaba watoto wangu wazuri vipi maendeleo yenu ya shule ?" yule mwanamke alienda kuwa kumbatia wale watoto
“Yako vizuri Leo tunaanza likizo yetu tunataka kwenda kwa babu " walisema wale watoto
Lilly alibaki kumkazia macho baba akiwa anasubiri jibu la swali lake kwa hamu
"Lilly huyu anaitwa bi Rhoda ni mama yako wa kufikia na Hawa wawili ni kaka yako na dada yako John na johari" Mr Marcel alitoa utambulisho
“wow kumbe wewe ndo mdogo wetu karibu sana nyumbani " John alimkaribisha lilly , kwa upande wa johari alimuangalia Lilly kwa dharau kisha aliondoka
"Hii haipo sawa kabisa Dady ni miezi michache imepita tangia mama atuache imekuwaje tayari unafamilia tena unaishi kwa furaha kama hakuna chochote kilichotokea , vipi kuhusu mimi ?" lilly aliongea kwa uchungu huku machozi yanamtoka kwenye macho yake mazuri
"Lilly wewe ni binti yangu lakini hauruhusiwi kuvuka mipaka yako unawezaje kumfundisha baba yako nini Cha kufanya ondoka nenda chumbani kwako haraka " mr Marcel alifoka
"Okay nitaondoka mbele ya macho yako naona siku hizi sina thamani tena kwako " lilly alikimbilia chumbani alifungua mlango lakini hakuingia alibaki amesimama mlangoni
"Wewe kwanini upo chumbani kwangu ?" Lilly alimuuliza johari aliyekuwa busy kupaka rangi kucha zake
"Oh masikini baba yako hakukwambia hiki ni chumba changu unaweza kwenda kutumia chumba kingine utakachokipenda " Johari aliongea kwa dharau akapiga teke begi la lilly likaanguka chini ,lilly alijikuta mwili wote unaishiwa na nguvu
"Mume wangu huyu binti yako mbona kama tutashindwana siku ya kwanza tu kurudi ananiita mimi mwanamke kashindwa hata kusema shangazi kama hawezi kuita mama " bi Rhoda alilalamika kwa Mr Marcel
"Aaah usijali mke wangu si unajua mwanzo alikuwa mwenyewe alikuwa ana deka sana lakini saizi anawenzie itabidi ajifunze na akubali kila alichokikuta " alisema Mr Marcel
Muda huo huo lilly alishuka akiwa analia
" Vipi mbona unalia ?" Mr Marcel alimuuliza binti yake lilly
"Daddy kwanini chumba alichonitengenezea mama yangu anakitumia yule msichana nataka atoke kwenye chumba changu Sasa ivi " lilly aliongea huku analia
"Kuwa na adabu binti yule si ni dada yako kwanini umnyang’anye chumba? vyumba vingine kwani havipo" bi Rhoda alimfokea lilly mbele ya baba na baba yake hakufanya chochote.
Kwanzia siku hiyo maisha ya lilly yalikuwa ya kunyanyasika na baba yake alihisi kama lilly ni muongo na hakuna ukweli wowote.
"Daddy laptop yangu imeharibika naomba uninunulie nyingine" lilly alimwambia baba yake
"Sawa nitakununulia " Mr Marcel alikubali muda sio mrefu Johari nae alienda kumuomba Mr Marcel baba yake wa kufikia amnunulie laptop pia
"Baba laptop yangu haiwaki sijui shida ni nini naomba uninunulia nyingine " Johari alimwambia Mr Marcel
"Sawa usijali , Leo jioni nitarudi na laptop mpya kwaajili yako"
Mr Marcel alimnunulia laptop Johari na kumuacha Lilly mpaka alimkumbusha kwa mara nyingine. Maisha ya Johar yalikuwa ya kushindana na lilly atakachokitaka au kupata lilly na yeye pia anataka akipate pia
Baada ya miaka mitano kupita lilly akiwa na miaka kumi na nane alikutana na kijana mmoja aliyeitwa Amir walianzisha mahusiano. Baada ya johari kulijua Hilo alitamani sana siku moja aje kumpata Amir kama njia ya kumkomoa lilly.
"Wanajikuta wanapendana sana subiri nitafanya kila njia ili nimpate huyu mapenzi wako " Johar aliongea huku anacheka kisha alienda kwa baba yao Mr Marcel
"Baba nilikuta hiki kikaratasi kwenye begi la lilly… " Johar alimpatia kile kikaratasi Mr Marcel ilikuwa ni barua ya mapenzi
"Umezikuta wapi umesema ?" Mr Marcel aliuliza kwa ukali
"Sasa ndo unamuulizaje kwa ukali hivyo , mtoto amekuletea barua anasema kazikuta chumbani kwa lilly wa kufokewa hapa ni lilly na sio Johar wangu " alisema bi Rhoda
"Kaniitie lilly mwambie afike hapa haraka " Mr Marcel alikasirika sana...
"Wewe kizuu baba yako anakuita huko" johari alimwambia lilly
"Nakuja na ukome kuniita kizuu kama mimi kizuu basi wewe ni ndondocha mana kila siku repoti zikija wa pili kutoka mwisho Bora hata John anajitahidi kuliko wewe " lilly alimzomea johari kisha alimpita na kwenda sebleni
"Daddy nimesikia unanita .." lilly hata hakukaa sawa alikaribiswa na Kofi zito la kwenye shavu na kuanguka mpaka chini
"Daddy nimefanya nini, mbona unanipiga ?" Lilly alishika shavu lake huku analia
"Huu ndo ujinga unaoufanya si ndio ama kweli mtoto wa kike anachukua tabia za mama yake " bi Rhoda alimtupia lilly zile barua pale chini
"Usimuingize mama yangu kwenye makosa yangu " lilly alimkata jicho bi Rhoda
"Naona umekubali makosa yako Sasa kwanzia leo sitaki kukuona nyumbani kwangu " alifoka Mr Marcel
"Sasa nitaenda wapi daddy?" Lilly alipiga magoti mbele ya baba yake, Bi Rhoda na johari walifurahi kusikia hivyo
"Kusanya nguo zako usisahau na passport unaenda marekani utasomea huko sitaki kusumbuliwa kichwa changu kina mambo mengi sana ya kufanya " Mr Marcel alinyanyuka na kuelekea chumbani kwake
"Mama Sasa mbona kama anaenda tena marekani ku enjoy maisha na mimi sikupanga iwe hivyo " johari alimwambia mama yake mbele ya lilly Wala hakuona haya
"Usijali kipenzi kila kitu kina muda wake " bi Rhoda alimshika mkono johari wakaondoka walimuacha lilly pale chini analia kwa uchungu akijikuta anamkumbuka sana mama yake .
"Mama umeniacha mkiwa sina pa kukimbilia ni Bora ungenichukua na mimi tukaenda wote " lilly alilia kwa uchungu hadi wafanyakazi walimuonea huruma lakini hawakuwa na Chochote Cha kumsaidia.
CEO WOMAN NA PENZI LA DEREVA DALADALA
SEHEMU: 2
TULIPOISHIA………
"Usijali kipenzi kila kitu kina muda wake " bi Rhoda alimsihi
"Mama umeniacha mkiwa sina pa kukimbilia ni Bora ungenichukua na mimi tukaenda wote " lilly alilia kwa uchungu hadi wafanyakazi walimuonea huruma lakini hawakuwa na Chochote Cha kumsaidia
TUENDELEE……..
"Lilly nakuomba uwe shupavu kwaajili ya mama yako unajua mama yako ameshawahi kuniambia kampuni anayosimamia baba yako nusu ni Mali yake kwahiyo pambana huko unakoenda usichukulie kama adhabu chukulia kama ni fursa kasome sana ili uje kuwa msimamizi wa Mali na kampuni ya baba yako " hayo yalikuwa ni maneno ya bi zawadi ambae ni mfanyakazi kwenye Hilo jumba
"Nimekuelewa bi zawadi nitafanya kila niwezalo nije kuwa mrithi wa Mali zote nitahakikisha hawapati hata kijiko "
Lilly alifuta machozi akasimama na kwenda chumbani kwake, alipaki baadhi ya nguo atakazo zihitaji alichukua na passport yake hakusahau kumuaga mapenzi wake Amir na walipanga kuoana pale tu lilly atakapomaliza masomo yake nchini marekani na kurudi Tanzania.
Haikuwa utani Mr Marcel alimpeleka lilly uwanja wa ndege na kumkatia ticket kisha Lilly Alisubiri ndege yake na baada ya hapo aliondoka kwenye ardhi ya Tanzania.
Miaka mi 5 baadae anaonekana binti mrembo sana akitoka uwanja wa ndege , alikuwa rangi ya chocolate , mrefu , ana kishepu flani hivi Cha uchokozi na kila mara alitabasamu na hii ilifanya dimpos zake ziweze kuo nekena na kumfanya kuwa mrembo zaidi
"Tax ..." Aliita lilly
"Nakuja dada" yule dereva tax alimpokea lilly mabegi yake na kuyaweka kwenye Buti
"Unaelekea wapi ?" Aliuliza dereva tax
"Naelekea mtaa A “. Lilly alijibu huku yupo busy kuchati na rafiki zake aliowaacha nchini marekani.
Baada ya kama lisaa limoja walifika nje ya jumba la Mr Marcel, Yule dereva alishusha mizigo ya lilly kwenye Buti
"Dada tumefika "
"Oh Asante sana kaka hii hapa pesa yako" lilly alishuka kwenye gari na walikuja wafanyakazi kumpokea
"Karibu sana lilly umekuwa mdada mkubwa na mrembo pia " wafanyakazi walimsifia lilly.
“Asanteni hata nyie pia mmebadilika sana "lilly aliwakumbatia
"Ingia ndani ukamsalimie baba yako " lilly aligeuka nyuma akakutana na sura ya bibi zawadi
" bibi shikamoo " lilly alienda kumkumbatia kwa nguvu .
"Marahaba umekuwa binti mkubwa Sasa naimani umeacha kulia Lia ?" Aliuliza bi zawadi
"Yeah nimekuwa Sasa siwezi kuumizwa na Chochote tena naweza kujiongoza mwenyewe na nimekuwa imara zaidi ya chuma , asante kwako bibi zawadi kila kitu nilichukulia kama fursa mpaka nimefika hapa " lilly alijibu huku anatabasamu
"Vizuri sana nimefurahi sana kusikia hivyo ingia ndani Sasa"
Lilly aliingia ndani alikuta watu wapo dining room wanakula chakula Cha mchana aliona watu sita alisogea karibu akasalimia
"Shikamoo , habari zenu "
"Marahaba kipenzi kwanini hukumwambia baba kama unarudi Leo aje kukupokea " mr Marcel alimuuliza lilly huku anatabasamu ni wazi alimkumbuka sana binti yake ambae kwa wakati huo alikuwa kopi ya mama yake bi Rita kabisa.
Lilly hakujibu chochote macho yalikuwa kwa Amir , alishangaa kwanini Amir Yuko pale na anakula chakula Cha pamoja na familia yake . Johari kuona vile alitabasamu kisha akasimama na kusema
"Karibu sana mdogo wangu lilly , na acha nifanye utambulisho kidogo huyu ni shemeji yako anaitwa Amir na yule pale aliyekaa pembeni ya John anaitwa Anita ni wifi yako kwa John " Johari aliongea vile makusudi ili kujua lilly atafanya nini Muda huo Amir alikuwa anaona aibu kwa alichokifanya
"Wow hongereni na nimefurahi sana sana tena sana siku zote furaha yenu ni furaha yangu pia nashukuru kukufahamu shem Amir na wifi yangu pale Anita " lilly alitabasamu kisha akaondoka alijikaza lakini moyoni aliumia mno
"Najua unanionea wivu na unataka kumrudisha kwako Amir lakini nakuhakikishia hauwezi kumpata tena hata ufanye nini siwezi kukuacha uwe na furaha lilly " johari alijiongelea mwenyewe
"Hiki ni nini kinachoendelea mpaka week iliyopita nilikuwa nawasiliana vizuri tu na Amir na Wala hakuniambia chochote ina maana wameanza mahusiano week hii au mimi ndo sielewi kinachoendelea hapa na nimefanywa mjinga "
Lilly alikaa chini alitamani kulia maana alimpenda sana Amir na alikataa wanaume wengi wenye pesa zao huko marekani kwa kujua anampenzi Tanzania kumbe hakuwa na wake tena.
"Hapana lilly hutakiwi kulia hao watu wote hawastahili machozi yako kila kitu nitakiweka kwenye mstrari "
Lilly aliingia bafuni na baada ya hapo alivalia gauni lake zuri lililoishia magotini akatoka alikutana USO kwa USO na Amir nje ya chumba chake .
"Shem vipi mbona kwenye milango ya watu au umekichanganya chumba changu na Cha mpenzi wako johari?"
Lilly alimuuliza Amir akiwa mkavu kama hakuna chochote kilichomuumiza
"Nataka kuongea na wewe lilly " Amir alitaka kuushika mkono wa lilly , lilly alimsukuma
"Sina Cha kuongea na wewe Amir tena naomba ujiheshimu wewe ni shemeji yangu kwa Sasa na kingine naomba uniache niishi kwa amani sitaki kero ya aina yoyote ile " lilly alimpiga kikumbo Amir akaondoka. Alielekea jikoni huko alimkuta bi Rhoda na mtoto wake johari
"Oh mungu wangu kila Kona nakutana na kero sitamani tena kuishi kwenye hii nyumba " lilly alijiongelea mwenyewe, alisogea kwenye fridge akachukua juice na kumimina kwenye glass
"Lilly mimi na shemeji yako Amir tunatarajia kupata mtoto na nafurahi sana Amir ni mume mzuri na atakuwa baba Bora kwa mtoto wetu " johari aliongea huku anashika tumbo lake
"Kumbe wameoana kabisa?”
"Lilly hukumsikia mwenzio alichokwambia " bi Rhoda alimshtua lilly aliyekuwa mbali kimawazo "
“Oh jamani sijui nawaza nini , hongera sana johari mara zote huwa unakipata unachokitaka ila kuwa makini sio kila king'aacho ni dhahabu” lilly alitabasamu kisha akaondoka
"Mama umemuona ee mimi simtaki kwenye hii nyumba kwanini tusimwambie baba amfukuzie mbali asije akaniibia mume wangu" alilalamika johari
"Usijali mwanangu muda ukifika ataondoka tu kwenye hii nyumba tena akiwa mweupee hatoondoka na kitu chochote " alisema bi Rhoda Na johari akatabasamu
Usiku wakiwa wanakula chakula Cha usiku kama familia lilly aliamua kuvunja ukimya
"Daddy nimeshamaliza degree yangu ya biashara natamani kwenda kufanya kazi kwenye kampuni yetu ili niweze kupata uzoefi zaidi " aliongea lilly huku anamuangalia baba yake aliyekuwa mbele yake
"Hata mimi nilitaka kumwambia hivyo hivyo sema umeniwahi tu, Sasa Cha kufanya mwezi ujao utaanza kufanya kazi kwenye kampuni yetu kwa Sasa pumzika na uyazoee mazingira ya Tanzania " alisema Mr Marcel huku anatabasamu
"Asante sana Dady lakini mimi sina haja ya kupumzika au kuyazoea mazingira hapa ndipo nilipozaliwa napafahamu vizuri sana" alisema lilly
Bi Rhoda na binti yake johari walibaki kubinua midomo hawakupenda kabisa kile kitendo Cha lilly kukubaliwa kirahisi kwenda kufanya kazi kwenye kampuni.
"Fanya upendavyo ukitaka kuanza kazi jumatatu ni sawa tu " alisema Mr Marcel
" Asante sana daddy , kesho nitatoka kidogo nataka kwenda kwa rafiki yangu Angel nimemmiss sana na baada ya hapo nitapita madukani kufanya shopping sina nguo za kuvaa kazini " lilly aliongea kwa furaha na Muda wote Amir alikuwa anamuangalia lilly
"Hongera sana lilly Sasa tutakuwa tunaonana ofisini na nyumbani natumai hii itasaidia tuzoeane zaidi " alisema John
" hata mimi nimefurahi sana, asanteni kwa chakula " lilly alisimama akaondoka, alienda chumbani kwake kitu Cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu rafiki yake Angel
"Dear kesho utakuwa free ?" Lilly alimuuliza Angel
"Mie tena na wewe shoga angu nambie tu unataka nikupeleke uka enjoy wapi mana najua umepamiss sana Tanzania " alisema Angel na yeye pia alionekana kuwa na furaha sana kurudi kwa rafiki yake lilly Tanzania
"Tunaweza kwenda kokote utakapo pendekeza wewe lakini sitaki kuchelewa kurudi nyumbani na upatikane muda wa kwenda shopping " aliongea lilly kwa mapozi akiwa amejilaza kitandani hakujua kama mlangoni kulikuwa Kuna mtu amesimama
"Hilo tu limeisha shoga ufanye tu utoke huko kwenu mapemaa na uje unichukue nyumbani si unamjua bi mkubwa alivyo" alisema Angel
"Usijali shoga kesho saa tatu nipo hapo kwenu si mnaishi pale pale nisije nikaja kichwa kichwa kumbe mmeshahama "
"Tuende wapi shoga weee tupo pale pale , tena ngoja nimpange bi mkubwa mapemaaa ukija tu tunaondoka "
"Sawa dear uwe na usiku mwema usisahau kumpa salamu zangu bi Yolanda" Lilly aliagana na rafiki yake Angel akakata simu alishtuka sana baada ya kumuona Amir amesimama mlangoni .
"Wewe unafanya nini chumbani kwangu ? Nani kakupa ruksa ya kuingia Humu mana sijasikia hata ukibisha hodi " Lilly alisimama na kusogea pale mlangoni
"Nataka kuongea na wewe lilly kuna vitu vingi nimekukosea lakini nilikuwa na sababu ya kufanya hivyo" Amir alitaka kushika mikono ya lilly ila Lilly alimkwepa
"Usinifanye nicheke Amir ila usijali kila kitu hutokea kwa sababu na mimi ni mtu poa sana nimeshakusamehe kwa kunipotezea muda wangu na kingine toka kwenye chumba changu na tuishi humu ndani kama hatujawahi kujuana hapo kabla utakuwa umenisaidia sana " lilly alifungua mlango na kumuonyesha Amir njia kwa mkono wake atoke nje.
Je Nini kitaendelea???
CEO WOMAN NA PENZI LA DEREVA DALADALA
MTUNZI SMILE SHINE
SEHEMU :3
TULIPOISHIA……….
"Usinifanye nicheke Amir ila usijali kila kitu hutokea kwa sababu na mimi ni mtu poa sana nimeshakusamehe kwa kunipotezea muda wangu na kingine toka kwenye chumba changu na tuishi humu ndani kama hatujawahi kujuana hapo kabla utakuwa umenisaidia sana " lilly alifungua mlango na kumuonyesha Amir njia kwa mkono wake atoke nje
TUENDELEE……..
"Lilly mimi .." kabla Amir hajamaliza kusema alichotaka kusema lilly alifungua mlango tena na funguo kabisa ....
"Mijitu mingine heshima sifuri kabisa mfyuu " lilly alipanda kitandani akalala.
Kesho yake asubuhi Lilly alijiandaa kwaajili ya kutoka kama alivyomwambia baba yake. Alipendeza sana maana alivalia kigauni chake kifupi na turaba twake simple alishuka sitting room akamkuta bi Rhoda hakumjali aliendelea na safari zake
"Shkamoo lilly " bi Rhoda alimsalimia lilly kwa kejeri
"Oops kwa bahati mbaya hua siitikiagi hiyo salamu hata kwa mtoto mdogo ningependelea kama ungenisalimia habari za asubuhi miss lilly itakuwa poa sana" lilly aliongea huku yupo busy kuweka nywele zake vizuri
"Mfyuu tamba unavyotamba lakini humu ndani unakaa kwa idhini yangu na huruma yangu siku nikitaka tu uondoke utaondoka tu" alisema bi Rhoda kwa matambo
"Kweli ee , basi Fanya utakavyo mimi Wala siitaki hiyo huruma yako upoo" lilly alimuangalia bi Rhoda juu hadi chini kisha aliondoka zake.
"Safari njema uendako" bi Rhoda aliangalia Pini aliyoishika mkononi kisha alitabasamu
Lilly alipandaa kwenye gari aliyokabidhiwa na baba yake kisha aliondoka Hakufika mbali sana taili iliisha upepo
"Kimetokea nini na Jana nililikagua lilikuwa sawa tu halikuwa na tatizo lolote " lilly alishuka kwenye gari hakujua afanye nini aliangalia saa yake aliyovalia mkononi
"Muda umeenda ngoja nichukue usafiri mwingine ,lakini swali ni kwamba naupata wapi usafiri mwingine?" lilly alienda kwenye duka la kaka mmoja
"Habari yako kaka " lilly alimsalimia yule kaka
"Salama tu dada karibu”
"Samahani kaka angu nataka kuuliza kwa maeneo ya hapa karibu wapi naweza kupata tax au bodaboda ?" Lilly alimuuliza yule kaka
"Aaah dada angu usafiri wa tax na bodaboda utatembea sana vituo vyao vipo mbele uko sio karibu ila Kuna kituo Cha daladala hapo mbele hata sio mbali " alisema yule kaka
"Asante sana kaka "
Lilly alitembea mwendo mrefu kidogo alikuta daladala tena ilikuwa ikielekea mitaa anayoishi rafiki yake Angel
"Dada unaenda ?" Aliuliza konda, Lilly alijifikilia akaona Bora apande tu daladala
"Naenda subiri " lilly alisogea kwenye daladala kwa bahati nzuri upande wa kukaa abilia ulikuwa umejaa
"Dada njoo ukae hapa mbele " yule konda alimfungulia Lilly mlango akapanda hakuwa na muda na mtu yoyote alikuwa busy anachati na Angel Kuna muda Amir alimtumia message
"Lilly mpenzi wangu nataka kuweka mambo sawa tumalize tofauti zetu, niambie uko wapi nije tuongee vizuri "
Lilly alikasirika sana hakujua amjibu vipi Amir, akiwa anatafakali Cha kumjibu Amir alisikia sauti ikimuuliza
"Dada unashuka wapi ?" Aliuliza dereva
"Ninakoshuka wewe kunakuhusu nini au mnadhani siwajui madereva na makonda mlivyo kazi zenu kutongoza kutwa kucha, isipite sketi mnayo " Lilly aliongea moja kwa moja kwa hasira
"Oya wewe demu hutujui hatukujui gari imefika kituo Cha mwisho haukushuka Wala nauli hujatoa usiulizwe wewe umekuwa nani mtoto wa raisi au ?" yule konda alikuja juu
"Beka punguza jazba , dada toa tu nauli uondoke " alisema yule dereva kwa upole
"Victor , mademu wengine sio wa kuwalegezea unajua katudharau sana sisi, hii ni kazi kama kazi nyingine tunapambana kuzitunza familia zetu iweje yeye atudharau?" beka alitaka kumpiga lilly ilibidi victor aende kumzuia
"Muache anipige , nipige ....Yani niguse hata ukucha kama hautaenda kusota jela maisha yako yote " Lilly alimtishia yule konda
"Dada nimekwambia toa nauli uondoke usitake kujaza watu hapa" Victor hakuongea kwa upole tena ilimbidi afoke mana aliona lilly haelewi kile anachomwambia
"Natoa kwani nimekwambia nilipanda Bure " Lilly alifungua pochi yake akatoa noti ya shilingi elfu kumi akampatia yule konda
"Sina chenji hapa ipo elfu tano tu” beka alimwambia victor
"Dada chukua tu pesa yako hatuna chenchi " alisema victor huku anampatia ile pesa lilly
"Sikupanda Bure na sipendagi kupewa msaada mimi sio ombaomba , kwanza mnaonekana hamna kitu so keep the chench" lilly alimtupia victor ile noti usoni kisha akaondoka
"Wewe demu acha mambo yako ya kimama kwani sisi umeambiwa ndo ombaomba tungetaka kuomba ungetukuta barabarani uko tumekaa chini na vibakuli " Beka alikuwa anamfuata lilly victor akamzuia
"Achana nae usipoteze nguvu zako Bure twende tukachukue abiria" victor alimshika bega beka kama kumtuliza
"Daah ila kaniharibia siku kabisa " beka aliendelea kulalamika wakati huo lilly alikuwa amefika mbali na alikaribia kabisa kufika nyumbani kwa kina Angle.
Victor William ni kijana wa miaka 27 mrefu , rangi yake maji ya kunde ni handsome ila maisha ndo yalimfubaza Anaishi yeye na wadogo zake wawili wote wa kiume Vicente mwenye miaka 17 na Justin mwenye miaka 15 yeye, ndo mama na yeye ndo baba wadogo zake wana mtegemea kwa kila kitu.
"Hodi humu ndani " lilly alipiga hodi nje ya nyumba ya kina Angel
"Wow karibu shoga angu nimekumiss... kidogo nikusahau mana umekuwa mzunguu " Angel alimkumbatia lilly
"Hata wewe pia umebadilika sana yani tofauti na nilivyokuacha na kwenye picha ulizonitumia " alisema lilly na Angel alivunja kumbato
"Kwahiyo unataka kuniambia mimi mbaya tofauti na kwenye picha " Angel aliongea huku amenuna
"Hapana kipenzi namaanisha you are so so beautiful kuliko hata kwenye hizo picha " lilly alimsifia Angel
" Kweli ?" Angel aliuliza huku anatabasamu
"Yeah nasema kweli " lilly na Angel walishikana mikono wakaingia ndani
"Mama njoo umuone mgeni wetu" Angel alimuita mama yake bi yoranda
"Nani tena au ni lilly ameshafika ?" Bi yoranda alienda sebleni akamkuta lilly amekaa kwenye kochi
"Shkamoo shangazi " lilly alimsalimia bi yoranda
"Mwali wangu uyoo , marahaba mwaya njoo umkumbatie shangazi " Lilly alinyanyuka akaenda kumkumbatia bi yoranda
"Za hapa shangazi ?" Lilly alimuuliza bi yoranda
"Salama tu tunashukuru tangu utuache wazima inapita mitihani midogo midogo mara pameuma hapa mara hapa lakini tunashukuru Mungu wazima , vipi masomo yako umemaliza salama ?" Bi yoranda alimuuliza Lilly
"Ndiyo shangazi na hapa ndo nimerudi kabisa sina ninapoenda tenaa ,kazi nitafanyia hapa hapa kama nitaolewa pia ni hapa hapa”
"Sema nitaolewa hapa hapa sio kama nitaolewa Ina maana hujiamini na ulivyo mzuri Masha Allah Yani ningekuwa na mtoto wa kiume ningekupaga tu uwe mka mwana wangu " bi yoranda alimtania lilly
"Hahaha hata mimi natamani ingekuwa hivyo " lilly alimkumbatia tena bi yoranda
"Sasa mama sisi ndo tunataka tutoke tunaenda kuzunguka kidogo nimuonyeshe mazingira na baada ya hapo tunaenda madukani" Angel alimwambia mama yake
"Sawa nyie nendeni lakini mjue kurudi mapema hasa hasa wewe Angel unajua kutoka tu hujui kurudi kwenu usije ukamchelewesha mtoto wa watu kurudi kwao " Bi yoranda aliongea huku amemnyooshea kidole Angel
"Sawa mama tutawahi " alijibu Angel
"Kunyweni kwanza chai kabla ya kuondoka mana kwa ninavyomjua Angle anavyojua kuzurula utaanguka na njaa" bi yoranda aliondoka na kuelekea jikoni
"Hahaha shangazi huwa haishiwi vituko jamani " Lilly alibaki kucheka
"Na kuchamba sijui ndo anazeeka vibaya , shoga ngoja nitenge chai tunywe tuchape rapa " Angel alitenga chai wakanywa na baada ya hapo waliaga wakaondoka
"Enhee kidogo nisahau shoga , unajua wakati nakuja huku gari langu liliniharibikia njiani " alisema lilly
"Weee pole kipenzi kwahiyo ukafanyaje ?"
"Si nikajishaua kupanda daladala yaliyonikuta si madogo shoga angu nimezozana na dereva na konda wake ila nimewakomesha siku nyingine watapunguza kushobokea watu wasio wajua "
"Pambeeee hayo ndo ninayo yapenda sasa natamani ningekuwepo , Sasa gari yako itakuwaje ?" Angel alimuuliza lilly
"Yani hapa ndo nawaza nipate fundi akalitengemeze lakini sina fundi yeyote ninaye mfahamu" alilalamika Lilly "
Hilo tu mbona limeisha ngoja nikupe namba umpigie huyu kaka ni fundi mzuri na nimuaminifu sana
"Angel alitoa simu yake akaitafuta hiyo namba”
Je nini kitaendelea???
CEO WOMAN NA PENZI LA DEREVA DALADALA
MTUNZI SMILE SHINE
SEHEMU : 4
TULIPOISHIA……
"Yani hapa ndo nawaza nipate fundi akalitengemeze lakini sina fundi yeyote ninaye mfahamu" alilalamika Lilly
"Hilo tu mbona limeisha ngoja nikupe namba umpigie huyu kaka ni fundi mzuri na nimuaminifu sana " Angel alitoa simu yake akaitafuta hiyo namba
TUENDELEE……
"Bora unipe shoga angu"
Anglel alimtajia zile namba Lilly aliziandika kwenye simu yake kisha akaipiga ile namba iliita mara ya kwanza ikakata
"Hapokei " lilly aliitoa simu yake sikioni
"Mpigie tena huwa Hana kazi moja huenda anaendesha daladala saizi "
Lilly alifanya kama alivyoambiwa na Angel aliipiga tena ile namba mara hii ilipokelewa haraka sana
"Hallo .." ilikuwa ni sauti nzito ya kiume
"Habari yako " alisalimia Lilly
"Salama tu, nikusaidie nini ?" Aliuliza yule mwanaume
"Samahani sana kaka angu nilikuwa Nina uhitaji wa fundi haraka sana kama una nafasi naomba uje huku magogoni " Lilly alimwambia yule kaka
"Sawa nakuja Sasa ivi sipo mbali sana "
"Sawa nakusubiri " lilly alikata simu
"Si umeona atafika hapa dakika sifuri nyingi njoo tukae hapa tumsubiri " Angel na Lilly walienda kukaa kwenye kibaraza Cha duka moja.
"Oya beka mshtue Chris mwambie aje anishikie mpaka mchana Kuna kazi nimepata ya haraka " alisema Victor huku anaendesha gari likielekea magogoni
"Poa ngoja nimcheki " beka alimpigia Chris na alikubali kwenda kumshikia victor kama kawaida yao.
Gari ilifika kituo Cha mwisho victor alivua sare zake za udereva daladala akavaa nguo zake nyingine akachukua na kibegi chake Cha vifaa vya kutengenezea .
"Oya beka badae " victor alimuaga beka
"Sawa kaka "
"Enhee mkaka mwenyewe yule pale "
Angel alimnyooshea kidole victor aliyekuwa amesimama anaangaza angaza huku na huku kama atamuona aliyempigia simu
"Willy ..."
Angel alimuita victor Mtaani alijulikana kwa jina la baba yake William walimfupisha na kumuita willy
"Malaika kumbe ni wewe " victor aliwasogelea huku anatabasamu lakini tabasamu lake lilififia baada ya kumuona Lilly
"Ndiyo ni mimi lakini ambae anataka fundi ni rafiki yangu huyu apa anaitwa .." kabla Angel hajataja jina la lilly Lilly alimkatisha
"Angel sikujua una urafiki na watu wa hovyo na wa Hali ya chini namna hii, siwezi kumkabidhi gari yangu mtu kama huyu vipi kama akiiba spare za gari " Lilly alimuangalia victor kwa dharau juu hadi chini
"Lilly umekuwaje huyu ni mtu poa tu Hana shida yoyote watu kibao wanamuamini " Angel alijaribu kumuelewesha lilly lakini Lilly alikataa kata kata kumuamini Victor
"Malaika usitumie nguvu nyingi kumuaminisha kitu asichotaka kukiamini acha mimi niende nikaendelee na kazi zangu nyingine " victor alitaka kuondoka Angel akamzuia
"Kwasababu amekupotezea muda wako kuja hapa itabidi tu ukalitengeneze na atakulipa ,na wewe lilly kama humuamini Willy basi twende nae "
Lilly alikubali wazo la Angel walienda na victor mpaka maeneo ya mbuyuni victor alianza kutoa taili kisha aliweka taili jingine lililokuwa kwenye Buti la gari
"Nimemaliza kazi yako " alisema victor
"Wow upo vizuri dakika kumi tu umeshamaliza unataka nikulipe kiasi gani ?" Lilly alimuuliza victor
"Elfu ishirini ndo bei " aliongea victor huku anajifuta jasho na shati lake, Lilly alimuangalia kwa kinyaa
"Ananuka jasho hivi Hawa watu wanaishije jamani " lilly alijisemea mwenyewe, alifungua pochi yake akatoa noti za elfu kumi 5 na kumpatia victor
"Mbona nyingi ?" Aliuliza victor
"Utakata nauli na nyingine utanunua hata maji ya kunywa" alisema lilly
"Pokea tu Willy usikatae " Angel alimwambia victor
"Hapana siwezi kupokea pesa ambayo sijaifanyia kazi "victor alitoa elfu kumi tu nyingine akamrudishia lilly
"Mbona umechukua elfu kumi tu ?" Aliuliza lilly
"Hii nikichanganya na ile uliyonitupia kwenye daladala inakuwa elfu ishirini " victor alichukua vifaa vyake akaondoka
" Kwahiyo unataka kuniambia dereva uliye kwaruzana nae ni willy?" Aliuliza Angel
"Yeah ndo huyu huyu Wala sijamfananisha " alisema lilly
" Mbona hanaga mambo ayo kaka wa watu wanaume wote wangekuwa ma gentleman kama willy haki ya mungu kusinge kuwa Kuna wanawake wanaolizwa na mapenzi " alisema Angel huku ameshika kifua chake upande wake wa kushoto
"basi achana na Derick kaolewe na huyo dereva daladala" lilly alimtania Angel
"Tuachane na hayo niambie tunaanza wapi tunaishia wapi"
Lilly na Angel walipanda kwenye gari na safari ilianza walizunguka sehemu mbalimbali za ku enjoy na mwisho walienda madukani kufanya shopping . Jioni lilly alirudi nyumbani kwao akiwa na mifuko mingi sana ya nguo na viatu
“Lilly ndo unarudi saizi ?" Bi Rhoda aliongea kwa sauti kubwa ili Mr Marcel asikie
"Huyu mchawi anashida gani tangu lini akajali natoka na kuingia saa ngapi ?" Lilly alijiuliza mwenyewe
"Lilly njoo huku baba anataka kuongea na wewe " John alimuita lilly
" Nakuja Dady " lilly alimpita bi Rhoda na Johari huku anatabasamu kwa kejeri
"Mama kwani huyu tunamlea Lea wa nini hapa ?si tummalize kama ulivyommaliza mama yake" johari aliongea kwa sauti ya chini sana
" Chunga mdomo wako johari unataka kutoa Siri , huyu tutammaliza taratibu wewe subiri na uone " bi Rhoda alikumbuka alivyomchoma bi Rita mama wa Lilly sindano ya sumu
"Subiri Lilly siku sio nyingi utaungana na mama yako " bi Rhoda alicheka sana
"Daddy nipo hapa nakusikiliza " Lily alimwambia baba yake aliyekuwa busy kupitia baadhi ya mafile
"Oh kumbe umeshafika ,Umenunua kila kitu ulichokuwa unakihitaji ?" Aliuliza Mr Marcel
" Yes daddy nimenunua vitu vingi sana na nime enjoy sana sikujua kama Tanzania inasehemu nyingi sana za kuvutiwa " aliongea lilly huku anatabasamu
" Tunajivunia Tanzania yetu kipindi Cha rikizo utaenda kutembelea mbuga za wanyama ukitaka " alisema Mr Marcel
"Wow thanks Daddy .." lilly alifurahi sana na alijitahidi kuongea kwa sauti kubwa ili bi Rhoda na johari wasikie
"Tukiachana na hayo kesho unatakiwa kufika kwenye kampuni tuna kikao na washirika wetu na kutakuwa na uchaguzi kidogo " alisema Mr Marcel
"Okay daddy kitu kizuri ni kuwa muda wote nipo tayari kufanya kazi "
"Vizuri sana wewe kweli umefuata nyayo zangu , nenda ukapumzike kesho mapema sana tunatakiwa kuondoka hapa "
Lilly aliondoka akaenda chumbani kwake alitoa nguo alizo nunua alianza kuchagua ni ipi atavaa kesho kwenye kikao
Je Nini kitaendelea?
CEO WOMAN NA PENZI LA DEREVA DALADALA
MTUNZI SMILE SHINE
SEHEMU : 5
TULIPOISHIA…….
Lilly aliondoka akaenda chumbani kwake alitoa nguo alizo nunua alianza kuchagua ni ipi atavaa kesho kwenye kikao
TUENDELEE……
"Hii hapa ipo vizuri nitavaa hii kesho " lilly alikuwa na furaha sana alitamani usiku upite haraka
Kesho yake asubuhi lilly alijiandaa kisha alishuka sitting room
"Wow umependeza sana wifi " Anita alimsifia lilly
" Asante sana wifi , John Yuko wapi nataka kuongozana nae " lilly alimuuliza Anita
"Ametoka Sasa hivi , muangalie hapo packing "
Lily alitoka akamkuta John anapanda kwenye gari
"John naomba tuongozane " alisema lilly
"Sawa panda kwenye gari basi tuwahi " John alimfungulia Lilly mlango wa gari
"Hapana nitatoka na gari yangu wewe uwe tu mbele yangu mana nahisi nimesahau MAC Iko pande gani " alisema Lilly MAC ni jina la kampuni ya Mr Marcel
"Haha kumbe unaogopa kupoteza sawa basi nitakuwa mbele yako " John alipanda kwenye gari lake na Lilly pia alipanda kwenye gari lake
Mida ya saa mbili Lilly , baba yake Mr Marcel , John na washirika wengine walikuwa wapo kwenye chumba Cha mkutano
"Nimeitisha hicho kikao kwa madhumuni ya kutaka kumteua CEO mpya wa hii kampuni " alisema mr Marcel
"Huyo CEO mpya utamteua kwa vigezo gani ?" Aliuliza mzee mmoja
"Uchapakazi , nidhamu , mtu mwenye hekma na anayeweza kujitoa kwa maendeleo ya kampuni bila kujali kitu chochote " alisema Mr Marcel
"Mara zote huwa unafanya uamuzi mzuri tunakusikiliza ni yupi tutakayeweza kumuamini na kumkabidhi kampuni " alisema mmzee mwingine
" Tusicheleweshe muda nitataja tu jina lake hakuna haja ya kizungushana CEO mpya wa MAC ni Lilly Marcel "alisema Mr Marcel Kuna baadhi ya watu walifurahi na Kuna wengine hawakufurahia ule uteuzi
"Mr Marcel cheo Cha u CEO kinataka mtu mzoefu inakuwaje unamteua binti yako Lilly ambae ndo kwanza ametoka masomoni na Hana uzoefu wowote na kwanini sio John ambae tunajua utendaji wake wa kazi” aliuliza mzee Mateo
"Swali zuri sana , Mr Mateo kila kitu huwa kinatokea kwa sababu maalum , kumkabidhi kampuni John ni sawa sawa na kuiweka kampuni rehani miezi miwili iliyopita John ameisababishia kampuni hasara ya milioni 78 je mtu kama huyo tunaweza kumkabidhi kampuni ? Kama hamumuamini Lilly basi tumpe miezi mitatu tuone ufanyaji kazi wake katika kiti Cha u CEO " alisema Mr Marcel kwa msisitizo
John alikuwa amenuna kweli kweli alitamani siku moja aje kuwa CEO wa MAC lakini kwa bahati mbaya aliikosa hiyo nafasi kwa tabia yake ya kucheza kamali na kufanya anasa kwa kutumia pesa ya kampuni
"Hongera sana Lilly " John alimpa hongera lilly lakini haikutoka moyoni
"Asante sana John natumai utaniongoza vyema kwani wewe umeshafanya kazi hapa na mambo mengi unayajua" Lilly aliongea huku anatabasamu kama kawaida yake lakini kichwani alijiwazia
"Lilly huwezi kumuamini yeyote "
"Mimi ni nani nisimsaidie mdogo wangu , kwa Hilo Wala usijali tutasaidina majukumu " John aliongea huku anajichekesha
"Miss Lilly njoo huku nikukabidhi ofisi yako " Mr Marcel alimuita Lilly
"Nakuja Mr Marcel “ Lilly aliitikia kwa heshima kisha alienda
"Hii ndo ofisi yako kwanzia leo natarajia mengi kutoka kwako usiniangushe " alisema Mr Marcel
" Nakupa ahadi yangu Mr Marcel nitasimama imara na kuiongoza vizuri kampuni wewe mwenyewe utafurahi“ aliongea Lilly kwa adabu kama anaongea na boss wake
"Vizuri sana "
Mr Marcel alitoka akamucha Lilly pale ofisini Kumbe John alikuwa anawaangalia kwa mbali kutokana na ofisi ya CEO kuwa imezungukwa na vioo aliwaona vyema kabisa.
"Lilly nilitamani kuishi na wewe kama mdogo wangu lakini umekuja kuwa mpinzani wangu sitokuacha ushinde kamwe ,MAC ni Mali yangu lazima mimi ndo niwe CEO na sio wewe "
John alijiongelea mwenyewe Lilly alianza kufanya kazi kwa bidii sana hakuwa Lele mama kabisa ndani ya miezi mitatu kampuni ilipanda chati na mafanikio yalianza kuonekana Mr Marcel aliitisha kikao Cha mwisho
"Nadhani kila mwenye macho haambiwe tazama , ndani ya miezi mitatu kampuni imepiga hatuna kubwa sana na imerudi kwenye chati kama zamani na kama tulivyokubaliana natangaza rasmi kiti changu Cha u CEO namkabidhi Lilly ..”
Baada ya muda wa kazi Lilly alirudi nyumbani Amir ndo mtu pekee aliyempokea kwa tabasamu lakini wengine wote walikuwa wamenuna
"Wewe binti huna shukurani hata kidogo John amekuwa akiteseka kuisimamia kampuni lakini umekuja na kumpora bahati yake " alisema bi Rhoda
"Sio hivyo tu mama nahisi atakuwa mchawi kabisa alivyokuwa marekeni kila kitu kilikuwa kinaenda sawa ona Sasa alivyorudi kila kitu kimeharibika " alisema johari
"Hivi mnajisikia mnachokiongea kweli ?hata kwa bahati mbaya hamuwezi kuwa warithi wa hii kampuni ni jasho la mama yangu na baba yangu sijui mnakielewa hiki kitu na kama mlikuwa hamjui ngojeni niwaambie, hii kampuni asilimia 50 ni jasho la mama yangu nastahili kupewa hii nafasi " Lilly alipitiliza chumbani kwake hakutaka kuendelea kuzozana nao
"Daddy nataka kuongea na wewe " Lilly alienda maktaba ya pale nyumbani
"Okay kaa hapo na uniambie unataka nini binti yangu " Mr Marcel aliweka kitabu pembeni
"Nimenunua nyumba nataka kuhamia huko kwanza ni karibu na kazini " alisema lilly Mr Marcel alimuangalia Lilly kwa makini
“ No daddy nimenunua kwa pesa zangu sikuchukua pesa ya kampuni " Lilly alijitetea
“Hahaha najua huwezi kufanya hivyo najiuliza kwanini unataka kuhama hapa nyumbani ,lakini wewe ni mtu mzima una uamuzi wako siwezi kukukatalia "
"Asante sana daddy, nitahamia nyumbani kwangu weekend hii " Lilly alifurahi sana Weekend kama alivyo mwambia baba yake alichukua mabegi yake na kuhami nyumbani kwake kulikuwa Kuna kila kitu ndani
"Sasa najihisi kama mtu , ngoja nimtafute shoga angu " Lilly alimpigia Anglel
"Nambie shoga kidawa umeshahamia makazi mapya ?" Angel alimuuliza Lilly
"Yeah , Yani nahisi naweza kuishi kwa amani Sasa kuliko kuishi kwenye ile nyumba muda wote nilihisi hatari" Lilly alijilaza kitandani
"Kwanini Sasa , ulikuwa unawaogopa ?"
"Bora wote lakini Amir alizidi kunisumbua Yani nilijikuta namuogopa yeye ndo sababu kubwa ya mimi kuhama pale"
"Duuh pole shoga angu na hapo pia uwe makini kuishi mwenyewe sio kitu rahisi " alisema Angel
"Mimi nimeshazoea sio kama wewe kila siku kudeka kwa bi yoranda , kwahiyo tutatoka Leo?" Lilly alimuuliza Angle
"Kutoka lazima shoga angu tunatakiwa kusherekea ushindi wako " alisema Angel.
Jioni Lilly na Angel walitoka pamoja walienda club moja maarufu waliagiza vinywaji na kuanza kunywa
“Angel yule sio yule kaka mnamuita willy sijui" Lilly alimuonyesha Angel
"Hee una macho shoga angu ndo yeye kabisa hata hujakosea "
"Sikutegemea kumuona hapa kabisaa " alisema Lilly
"Yule kaka ana historia ya kusikitisha sana anaishi na wadogo zake wawili wote wanasoma yeye ndo baba yeye ndo mama na ukizingatia hakumaliza hata elimu yake ya sekondari kwahiyo ndo kama unavyomuona kila kazi anafanya sijui hata anapumzikaga saa ngapi ?" Angel alimsikitikia sana victor
"Kumbe Kuna watu wana maisha magumu hivyo , pole yake kama Kuna maisha mengine baada ya haya atazaliwa akiwa tajiri tena mwenyewe ni handsome hatari "
Lilly alimuangalia sana victor aliyekuwa akihudumia vinywaji
"Mmh umeanza ...umeshaanza kulewa eti ee si ni wewe ulimsemaga vibaya wewe ?"
Lilly alibaki kucheka Cheka tu pombe ilikuwa imeanza kupanda kichwani
"Mambo zenu " alikuwa ni mpenzi wa Angel, Derick
"Poa , shem karibu " Lilly alimkaribisha Derick
" Asante shemu , ngoja nimuibe huyu mara moja atarudi Sasa ivi " alisema derick
" Hakuna shida shem huyo ni wa kwako " alisema Lilly Derick alimshika mkono Angel wakaondoka
Lilly alikunywa sana na masaa yalizidi kukatika na Angel hakurudi. Watu wote walianza kuondoka Lilly alibaki peke yake alikuwa amelewa sana
"Lilly twende nikupeleke nyumbani " Amir alitaka kumnyanyua Lilly , Lilly aliusukuma mkono wake
" Sitaki niachie wewe vipi ?" Lilly aliongea kwa sauti ya kilevi Victor alitamani kumpuuzia lakini hakuona kama ni busara kufanya hivyo
"Kaka Kuna nini mbona kama unamlazimisha na yeye ameshakwambia hataki ?" Victor alimuuliza Amir
"Oya fuata yanayo kuhusu huyu ni mpenzi wangu" Amir alitaka kumshika mkono Lilly
" Usinishike wewe kaka vipi ,sikia willy mimi huyu kaka simjui kabisa " lilly alienda kujificha nyuma ya victor
" Umesikia alichokisema , naomba uondoke kabla sijakufanya kitu mbaya " alisema victor.
Je nini nitaendelea??
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote