Follow Channel

CEO’S ANGEL

book cover og

Utangulizi

CEO’S ANGEL 1
Penzi la CEO playboy na SECRETARY wake
HUSQER BALTAZAR
Kuna baadhi ya watu wakikupenda hauwezi kukataa wala kubisha zaidi ya kufata wanachokitaka, kutokana na nguvu, pesa na madaraka waliyo nayo…
Hayo ndiyo yalionikuta mimi, naitwa lola, ni binti wa kipekee kwenye familia yangu ila wazaz wangu wana maisha ya chini kwa maana hawana uwezo, ni hawa watanzania wa kawaida, sasa mwaka 2015 nilipata mpenzi, alikuwa ananipenda sana na alikuwa tayar kufanya chochote kile kwa ajili yangu, nilikuwa namuonea huruma sana kwenye mapambano yake, maana alikuwa anahudumia familia ytake pamoja na mimi, hivyo nikamuomba anitafutie kazi ya kufanya….
Basi akanambia kwenye kampuni ambayo anafanya kazi wanatafuta secretary , na kwakuwa mimi nilisomea usecretary akasema atatafuta namna ya kuniunganisha, nikafurahi sana, maana alikuwa anapambana sana kunihudumia na alikuwa anahudumia familia yake, alikuwa anamdogo wake anasoma chuo na hakuwa anamkopo, pesa zote alikuwa anatoa yeye, na mdogo wake mwingine wa kike ambae alikuwa kidato cha nne, pamoja na mama yake ambae alikuwa anafanya kazi sokoni tu, na mbaya zaidi walikuwa wanakaa kwenye nyumba ya kupanga na kodi alikuwa analipa yeye, hivyo akawa hata hawez kujifanyia jambo lolote lile kwa ajili yake, nikataman sana kumsaidia majukumu…

Basi siku ya siku ikafika, akanambia kazini kwao kuna usaili, akaenda kunitafutia nguo nzuri, ili na mimi niwe na muonekano mzuri, nikakubali pale kisha akaniaga maana hatukuwa tunakaa sehemu moja …

Kesho yake ikafika na akaja kunifata, tukapanda zetu daladala mpaka kwenye kampuni ya SOAL kampany, ambayo ilikuwa inahusika na usafi wa majumbani pamoja na kilimo cha mazao ya chakula…
Kabla sijaingia kwenye usaili akanambia kuwa boss wao ni Malaya sana hivyo niwe makini, nikamuelewa, na tulikuwa wasailiwa watano, na mimi ndio wa kwanza kwenda kwenye usaili, wakati naingia tukapokelewa na sauti za miguno, kana kwamba kuna watu walikuwa wanafanya mapenzi, nikaingia mpaka ndani, nikakuta kweli huyo boss amempakata mwanamke na sijui hata wanafanya nini…

Nilishangaa sana, na sio siri nilimuona kama mchafu sana, maana anaweza vipi kuleta wanawake ofisini kwake hali ya kuwa anajua kuwa siku hio alikuwa anatakiwa kufanyia watu usaili?…
Nikakohoa kidogo ili wajue nilikuw pale, kweli akashtuka na akamsimamisha Yule mwanamke ambae alikuwa nae, ila aliponiona nikashangaa anamfukuza Yule mwanamke kisha akaanza kuweka kila kitu sawa kwenye ofisi yake, akaniangalia kwa sekunde kadhaa na kusema “ samahan sana sikujua kama ulikuwa umeshaingia…

“ usijali boss, tunaweza kuanza usaiili, nikaongea kwa unyenyekevu mkubwa, maana niliona kama mambo ya watu hayawezi kunihusu mimi, basi akaanza usaili wake , ila alikuwa ananiangalia sana mpaka nikawa naona aibu, nikashangaa maswali hayaishi anataka kuniuliuza maswali mapya kila saa, sikujali sana, maana nilihisi huenda ndio kawaida yake kuwa hivyo alivyo endapo anapotaka kufanya usaili…

“ulisema unaitwa nani?” akauliza..
“ naitwa lola, nikajibu kwa kujiamini, akatabasamu kisha akasema “ umeshapata kazi lola, na unaanza kufanya kazi sasa hivi kama secretary wangu, nikatabasamu kisha nikamuambia “ asante sana boss..
“ owww tafadhali naomba usiniite boss, unaweza ukaniita Nabili, na kama nilazima uniite jina ambalo linaanza na boo, basi niite my boo, kisha akatabasamu na mimi nikatabasamu kisha akanambia “ ukitoka waambie hao wengine kuwa waondoke maana nimeshapata ninae mtaka, wao hawana umuhimu tena…

“ samahan boss, nikasema ila kabla sijamalizia kusema akadakia na kusema “ sio boss ni boo…
“ owww am sorry, ila naomba kama hautajali uende ukawaambie pekee yako, au utafute mfanyakazi mzoefu ndio umpe hio kazi ambayo unataka..
Basi huyo boss akachukua simu yake kisha akapiga sehemu na baada ya sekunde chache ikaanza kuita, na ikapokelewa, kiukweli sikusikia upande wa pili, ila nilimsikia anasema “ amani njoo watimue hawa waliokuja kufanya usaili maana nimeshampata wangu…

Sikujua kwanini kasema ameshampata wake, ila hakutaka niondoke mpaka alipokuja huyo amani alikuwa ni msaidizi wake, akawaambia wale wadada wengine waondoke, na baada ya kuondoka akaingia ndani kisha akasema “ boss wameshaondoka..

“ naomba umpe huyu majukum yake, ila hakikisha meza na kiti chake unakiweka pale, akasema na hio sehemu ambayo alitaka kiwekwe kiti na meza yangu kulikuwa na kioo kikubwa, ambacho mtu akiwa ndani ya ofisi anaona waliokuwa nje, ila waliokuwa nje, hawakuwa wanaona yanayoendelea ndani, nikashangaa Yule msaidizi wake anatabasamu kisha kwa sauti ya upole akasema “ naomba unifate miss…

Sikuwa na hiyana zaidi ya kumfata, kweli akaniwekea kiti na meza na laptop yangu ya kufanyia kazi, na kunielekeza namna ya kufanya kazi, basi nikaanza kufanya majukum yangu, kumbe kule ndani Yule boss ameacha kufanya kazi zake akawa ananiangalia, na kwakuwa mimi sikuwa namuona nikawa naendelea na majukum yake bila kujua kitu chochote kile…

Basi nikakaa wee imefika kama saa nane mchana nikashangaa simu ambayo ipo mezani inaita, nikapokea, alikuwa ni boss akawa anataka niende ofisini kwake, sikubisha maana ndio kazi ambayo ilinipeleka pale, nikaenda ofisini akawa ananiangalia kwa dakika kadhaa, alikuwa ananiangalia kwa jicho la kunitamani kabisa, nilimuelewa, nikajua ndio huo umalaya wake unamsumbua tu hana lolote lile…

“ samahan boss umeniita, ni jambo gani naweza kukusaidia? Ikabidi nimuulize..
Akatabasamu kisha akasema “ inawezekana kazi ambayo unaitakiwa kuifanya ni kusimama mbele yangu na mimi ni kutazame, kwani kikubwa si nina kulipa mshahara kwa kazi unayoifanya, au unasema je..
Nikakaa kimya, maana sikujua hata natakiwa kumjibu nini….
“ nasikia njaa sana, unaonaje kama ukienda kuleta chakula..
“ sawa boss naomba pesa nikakuletea, basi kweli akatoa elfu hamsini, kisha akanambia “ nenda pale nje waambie nataka biryani kuku, na wewe utachukua chakula unachotaka mrembo, kisha uje navyo vyote huku ofisini, akasema…

Sikutaka kubisha nikatoka na kwenda kununua hicho chakula ambacho anataka, ila wakati natoka nikakutana na mpenzi wangu ameri, maana nay eye alikuwa anafanya kazi sehemu hio hio, ila tulikuwa vitengo tofauti, aliponiona tu akanikumbatia kisha akanambia “ mbona haujanijibu kama umepata kazi au laa…

“ nilishindwa kukujibu maana nimefanyiwa usaili na wakati huo huo nikaanza kazi, asante sana Amer wangu, hakika ww ni zaidi ya mwanaume kwenye maisha yangu, nikasema na amer akatabasamu kisha akasema “ siku zote nipo kwa ajili yako lola…

Kumbe bana, boss nabil alinifata akawa ananiangalia, akaniona na amer hapo kumbe ameshanielewa vibaya sana, ila mimi namchukulia kama Malaya tu na mwanaume mwenye tamaa hivyo sikuwa namtilia maanani kabisa kumbe mtu kafa kaoza kwangu..

Basi nikaenda na ameri kwenye sehemu ya chakula, tukanunua chakula huku tunapiga story na kucheka, akanambia yeye atakula pale pale, mimi niendelee na majukum yangu, basi nikabeba vyakula vyangu kisha nikaenda mpaka ofisin kwa boss nabili, kitendo cha mimi kuingia tu nikashangaa anafunga mlango na kitasa, kisha akanipokea kile chakula ambacho nilikuwa nimekibeba na kukiweka mezani, kisha akazima taa, maana pale ofisini bila kuwasha taa hauoni, kutokana na namna jengo lilivyo kaa, hivyo akizima taa ya ofisini kwake hata kama kutakuwa ni mchana ila kuna kuwa na kagiza flani hivi…

Kisha akanisogelea na kunambia “ hivyi lola unanichukulia je mimi?...
NAKUJA……


CEO’ ANGEL 2
Penzi la playboy ceo na secretary wake…
HUSQER BALTAZAR
Mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda kasi, maana sikujua hata alikuwa anataka kufanya nini, kwa sauti ya uoga wa hali ya juu nikauliza “ nimefanya nini boss na unataka kufanya nini…

Nikashangaa ameshusha pumzi kisha akasema “ samahani lola, samahani sana kisha akawasha taa na kusema “ kama hautajali naomba ukae pale ule hapa hapa ofisini kwangu…
Nilikuwa natetemeka balaaa, hivyo hata nguvu za kukataa sikuwa nazo kabisa, nikakaa nakuanza kula sikuwa hata nakula kwa raha, ila kwakuwa nilichukua chips kuku nan i chakula ambacho na kipenda sana, hivyo sikuacha hata tomato, akawa nay eye anakula huku ananiangalia, nimlipomaliza kula nimamuomba vyombo niondoe, akatabasamu kisha akanambia “ sawa…

Nikasogea kwenye meza yake kisha nikachukua vyombo ambavyo vilikuwa mezani kisha nikasema “ samahani kama hautajali unaweza kuwa mke wangu?...
“ nani mimi!, nikauliza kwa mshangao..
“ ndio wewe, naomba uwe mke wangu lola, akaendelea kusema..
“ hapana boss, kwanza ndio nimeanza kazi leo, hata kama nisingekuwa na mahusiano nisingeweza kukubali kuolewa haraka hivyo, na pili nina mahusiano yangu na nampenda sana mwanaume wangu na la mwisho siwez kuwa na mwanaume asiejiheshimu hata kidogo kwenye maisha yangu kisha nikawa nataka kuondoka…

nikashangaa amesimama kisha akanishika mkono na kusema “ nakupenda lola…
nilimuona kama mwenda wazimu maana sikuamin kama mtu anaweza kunipenda ghafla vile, nikajua umalaya wake unamsumbua tu hana lolote..
nikashangaa anapiga magoti kisha akaniangalia na kusema “ nisamehe sana lola, nakuapia kwa jina la mungu, hautakaa uone hata kwa bahati mbaya tena kile ulichokiona leo, najua ni ghafla sana mimi kusema hivi ila niamini nimekupenda sana kuanzia nakuona najikuta nashindwa hata kufanya kazi nakuangalia wewe, nikubalie basi nakuahidi sitakusumbua ila nataka tu niwe na amani ya moyo kuwa wewe ni wangu pekee yangu…


“ siwez kuwa na mwanuame Malaya mimi na kama kazi yako ndio sababu yaw ewe kuanza kunisumbua basi naacha kazi, kisha nikatoka zangu nje…
Alidhani utani nikatoka na kwenda kukaa kwenye ofisi yangu kisha nikaanza kuandika barua ya kuacha kazi, yaan siku hio hio ambayo nimeanza kazi, nimeshatongozwa na boss na nimeacha kazi…
Nilipomaliza kuandika barua nikampelekea, alishtuka, nadhani alijua natania bana, nilipoweka mezani nikamuangalia kisha nikasema “ samahani sana kwa kila kitu, na nashkuru kwa ukarimu mdogo ulionionesha, najua wewe ni muhuni sana, hivyo umenitamani na unaweza kumtamani mwanamke mwingine yoyote yale, hivyo katafute mwanamke wa aina yako, maana sio kila mtu ambae anapenda wetu wenye pesa au wenye madaraka, naomba niondoke…

Alikuwa kimya hajanijibu kitu, nilipotoka nje nikamkuta mchumba wangu ananisubiri nje, sikutaka kumuambia kuwa nimeshaacha kazi, maana nilihisi huenda anaweza akajisikia vibaya, hivyo tukarudi zetu nyumban, akanifikisha nyumbani kisha akanikiss kwenye paji la uso kisha akaondoka zake…

Nilijiona kama nina mkosi, au nuksi flani hivi, maana haiwezekani niwe imetafuta kazi kwa shida alafu niache siku hio hio, ila nikawa najiambia kuwa thamani yangu ni kitu cha msingi zaidi kuliko hata kazi, pesa na madaraka…

Basi nikalala zangu, asubuh mwanaume wangu amer akaja kunipitia, nilishaamka, hivyo nikajiandaa kinafki, maana sikutaka ajue kama nimeacha siku hio hio , tukafika mpaka kazini, Amer akaingia zake ndani, mimi nikawa narudi zangu nyumban, ila kabla sijaondoka nikamuona boss nabil na Yule msaidizi wake, Yule msaidizi akaniita…

Mwanzo sikutaka kumsikiliza, ila akasisitiza sana ikabidi nikubali kwenda, boss hakuwa na manenio mengi ila aliniambia kuwa “ sitakaa nikusumbue, na hautakaa unione kama mwanaume asie na heshima tena, naomba sana urudi kazin, wewe ni mwanamke mchacharikaji sana, na una stahili kuwa na boss atakae kuheshimu, nakuomba sana urudi kazini…

Sikutaka kubishana nae, sasa kama amenihakikishia kuwa atakuwa na nidhamu sikuwa na sababu za kukataa kurudi kazini maana maisha yangu yenyewe ni magumu sana, basi nikarudi kazini na majukum yangu ya kikazi yakaanza kama kawaida, ni kweli alikuwa na heshima sana, hakuwah kunisumbua tena kivyovyote vile, alinifanya niipende sana kazi yangu, maana alikuwa ananiheshimu na baada ya mwezi wa kwanza akaniongezea na mshahara…

Na mwanaume wangu nay eye akaongezewa mshahara, sasa maisha yetu kidogo yakawa na uangalau flani hivi…
Ila sasa kuna vitu sikuwa navielewa kabisa, siku moja asubuh nimeenda kazini nikakutana na saa nzuri sana mezani na ujumbe ulikuwa umeandikwa kuwa “ nakupenda sana lola, na nakuahidi kukutunza siku zote za maisha yangu, natumani utaipenda zawad yangu…

Nikawa naangalia pemben kumuona alietuma, ila sikuona kitu, sasa akili yangu ikawa inaniambia kuwa mwanaume wangu ndio ambae amenitumia, nikatabasamu na kuiweka ile saa kwenye pochi kwanza, kumbe alieleta ile saa alikuwa ni nabil, akawa ananiangalia kupitia kioo cha ofisi yake, na alipoona nimefurahia zawad ambayo amenipa nay eye akatabasamu na kujiambia “ nimetulia kwa ajili yako, na nitahakikisha nakupata lola…

Basi nikaendelea zangu na majukum yangu, mchana nikawa na rafiki yangu mmoja nikamwambia nina hamu na pilau kuku kinyama, mwisho wa mwezi huo lazima nitafute sehemu niende nikale, Yule dada alikuwa anitwa amina..

“ wenzako wanakula pilau mpaka walikinai, alafu kuna sisi ambao mpaka tule pilau ni lazima mwisho wa mwezi ila maisha haya, akadakia amina nikajikuta naanza kucheka, maana ni kweli hio hela ya kula vizuri kila siku naitoa wapi mtoto wa maskini mimi…

Kumbe bana nabil alikuwa maeneo yale na alikuwa anasikia kila ambacho nilikuwa nasema, nikiwa nimekaa zangu, na siku hio nilipanga kupiga pasi ndefu, mara wakawa wanaingia wahudumu pale kazini wakiwa wamevalia kama wapishi, wakaanza kumpa kila mfanyakazi chakula, waligawa kwa kampuni nzima, nikapewa na mimi, ilikuwa ni pilau kuku, yaan sikuamini, amina akanifata na kusema “ wewe una mungu, yaan una waza kitu na unakipata muda mchache baadae, sasa hivi nikiwa na shida nitakuwa nakuambia wewe uniwazie…

Nikajikuta naanza kucheka, sasa kumbe baada ya mimi kusema nina hamu na pilau kuku boss nabil akaagiza kila ,mfanyakazi apewe ya kwake, maana huwa anatamani kunipa kila ninachotaka, ila ndio hakuwa anajua namna ya kunipa, maana alikuwa anaogopa sana kunikera, sasa aliponiona nimekaa nakula akawa anajisikia vizuri sana …

Maisha yakawa yanaendelea kama kawaida, siku moja Amer akaniambia amepewa nafasi ya kwenda kusoma Russia kwenye maswala ya uzamili, na kampuni itaendelea kumlipa mshahara wake licha ya kuwa atakuwa anasomeshwa na kampuni..

Nilihisi kama ndoto, nikaona angalau ndoto zetu zinaanza kutimia, basi siku ya siku ikafiuka na Amer akaanza safari, kumbe hata hio safari ilikuwa ni mpango tu wa nabil kumuweka Amer mbali na mimi, bila ya sisi kujua kabisa…

Basi kuanzia Amer anafika huko mawasiliano yakawa yatabu sana, maana kila wakati alikuwa analalamika masomo ni magumu, ila pia kuna majukumu mengine ya kikazi ambayo alikuwa analazimika kuyafanya, hivyo ilikuwa inaweza kupita hata siku tatu hatujawasiliana, baadae ikawa inapita wiki, na muda ulivyokuwa unazidi kwenda ikawa inapita mpaka mwezi mzima tunakosa muda wa kuwasiliana, na nikiuliza ananiambia kuwa yuko busy sana, mpaka nikaanza kujisikia vibaya sana, na kiukweli nikajikuta nakuwa mpweke sana, na nadhani hii ndio ilikuwa dhamira ya nabil…

Siku moja nikiwa natoka kazini mvua ikaanza kunyesha, nikajikunyata na kuanza kutembea, ila kabla sijatoka nikashangaa gari linasimama pemben yangu kisha nikamuona nabil ndani ya gari akanambia kuwa “ naweza kukusogeza nyumbani kwako..

Sikubisha maana alionekana kama amebadilika kwa muda mrefu sana, alionekana kama amekuwa mtu mwingine kabisa, na mimi nikajikuta namuamini, na kweli alijitahidi akanipeleka mpaka nyumban, ila wakati nataka kushuka mvua ikazidi kuwa kubwa, nabil akavua koti lake akanipa nivae, kisha aklachukua mwamvuli na kuomba kunipeleka mpaka kwneye mlango wa nyumba yangu, nikakubali, basi tumefika mlangoni nikavua koti lake nikampa kisha nikamshkuru…

“ hivi ndio namna huwa unamshukuru mtu aliekusaidia, unaonaje kama nikiingia ndani tusubiri mpaka mvua iishe ndio nitafute namna ya kuondoka, maana hizi mvua kubwa zinaletaga mafuriko, sina uhakika kama barabara hazijaharibika..

Sikuwa na sababu ya kukataa kumuingiza ndani, ila nikiwa na imani kuwa mvua ikikata basi ataondoka zake kumbe alikuwa na malengo yake bana…
NAKUJA………………..


CEO’S ANGEL 3
Penzi ceo playboy na secretary wake
HUSQER BALTAZAR
Ile mvua ilikuwana kusudi sana jamani, maana mpaka saa saba haikuwa imeisha, nilikaa na mgeni sebleni mpaka saa saba, nikajikuta nimepitiwa na usingizi, kumbe ndicho ambacho alikuwa anataka, nikalala akawa amekaa pemben yangu ananiangalia tu, sasa kama mnavyojua ukiwa karibu na mtu ambae unampenda, kuna namna hisia zinapanda ndivyo ilivyokuwa kwa nabil…
Nikahisi naanza kupapaswa mwili wangu, nilishtuka sana nikakurupuka kutoka usingizini, nikamuona boss nabil ananiangalia akiwa amelegeza jicho balaa, akaniangalia na kusema “ lola mamaa nakupenda sana nashindwa kabisa, nashindwa mimi ni mwanaume na nimekamilika, samahani sana ila nimevumilia muda mrefu bila kuwa na mwanamke kwa sababu yako lola, nilikuwa natamani unione kama mwanaume bora sana kwenye maisha yako, please mamaa kidogo tu….

Sasa mimi nilikuwa nina mawenge ya usingizi, nikajikuta nasema “ amer umerudi, aisee niliwekwa bussu moja matata, mkapa mwili wangu ukalegea ila sikuwah kufabnya hivyo kabla maana amer alikuwa ananiheshimu sana na aliniahidi kuwa hata kaa aniguse mpaka tufunge ndoa, na niridhike mwenyewe, mara nikashika mkono wa mtu, nilishasahau kuwa nilikuja na boss wangu nyumban ndio nikakurupuka, na kusema “ unafanya nini wewe…

Nabil akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ nimeshindwa kuondoka lola…
“ mvua imeisha boss, naomba uwapigie wafanyakazi wako waje kukuchukua maana sioni kama ni sawa wewe kulala nyumban kwangu kwa wakati huu, ukiangalia mimi ni mtoto wa kike na wewe ni mtoto wa kiume…..

Akashusha pumzi kisha akawa ananiangalia, niliona namna mtalimbo wake ulivyokuwa umetuna ila sikumjali kabisa, maana nilikuwa nampenda amer wangu, na katika moyo wangu hakukuwahi kutokea mwanaume ambae ameushika moyo wangu kama ameri…

Alikuwa kama anataka kusema jambo, ila akasita na kusema “ naomba nilale kwa usiku wa leo tu lola…
“ hapana siwezi kulala na wewe hapa, naomba uondoke, nikajibu na hakuwa na namna zaidi ya kuondoka nyumbani kwangu, maana sikuwa nataka kuendelea kukaa nae pale…

Basi akaondoka bila kusema neno lolote lile, na mimi hata sikumjali, nikashika simu yangu kuangalia kama amer amenipigia, au hata kunitumia sms, au kujibu jumbe fupi ambazo nilimtumia, ila haikuwa hivyo, nikakunja sura kisha nikajiegemeza kitandani mpaka ambapo nilipitiwa na usingizi…

Nimekuja kuamshwa na majogoo ya asubuh ambayo yalikuwa yakiwika, nikakurupuka na kujiandaa kisha nikakimbia kazini, sikuw nimechelewa, ila nilikuwa na wasiwasi tu, maana hata nilipokuwa natoka nyumban sikuangalia saa…

Wakati nafika kwenye geti la kuingilia kazini nikasikia naitwa, na nikageuka nyuma kuangalia ni nani ambae alikuwa ananiita, ndio nikakutana na sura ya boss wangu, akaomba nikamsaidie baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa kwenye gari, kweli nikaenda mpaka alipo kisha akanikabidhi fail moja na kunitaka nilibebe, sasa wakati ambapo alikuwa ananipa, akanishika mkono, sijui kama ni makusudi au ni bahati mbaya, nikashangaa ameshusha pumzi kisha kama akatulia akiwa ananiangalia….

“ bosso upo sawa? Ikabidi niulize, na ndio kama nilimkurupuka akasema “ ndio nipo sawa, embu twende ndani…

Siku bisha basi tukaanza kuandamana pamoja mpaka ofisini na mimi nikaenda kuweka ninavyotakiwa kuweka ofisini kwake kisha nikatoka kuendelea na majukumu yangu…

Sasa huku kwa nabil kumbe kazi hazifanyiki, akawa ananiangalia kwenye kile kioo ambacho kinatenganisha mimi nilipo nay eye alipo, kisha akawa anapata hisia kali kabisa, akaanza kuhisi kama nimeenda pale ofisin kwake, kisha nikaanza kumpapasa sehemu mbali mbali za mwili wake, akawa anaguna guna, na mwisho akaanza kuvuta picha kuwa anafanya mapenzi na mimi, mimi hapo sina habari, sasa nikawa natakiwa kwenda kumpa taarifa za kikao a,mbacho kilikuwa kinafanyika dakika kumi na tano mbele, nimefika ofisini kwake, nikashangaa namkuta mtu kafumba macho kisha akaanza kusema “ ahhhh lola tamu, ashhhhh tamu ahhhh…
ITAENDELEA…


CEO’S ANGEL 4
PENZI LA PLAYBOY CEO NA SECRETARY WAKE
HUSQER BALTAZAR

Ikabidi nijikohoze, aiseee alishtuka kisha akaniangalia na kusema “ owww lola umekuja…
“ kwani kuna shida boss? Nikamuuliza…
“ hamna, hamna sina shida yoyote, ehee niambie naweza kukusaidia nini lola?..
“ hapana sijaja hapa kwa sababu nataka msaada wako, ila nimekuja hapa kuku taarifu kuwa utakuwa na kikao dakika chache mbele,kama dakika kumi na tano kutoka sasa hivi nikasema…
Akashusha pumzi kisha akanambia “ unaonaje kama tukiongozana wote kwenye huo mkutano, maana natamani ujifunze vitu vingi kuhusu hii kampuni, maana siku ambazo sitakuwepo majukum ya hapa yasikushangaze, kiukweli sikubisha, kwa kuwa niliona kama ni majukum yangu ya kikazi, hivyo nikamuambia kuwa muda ukifika nitakuja kumkubusha, incase akisahau…

Basi nikatoka na kwenda kuendelea na majukum yangu, ila lile jina lola ambalo nabil amelitamka wakati anavuta mahisia yake, ni langu au ni kwamba sijasikia vizur, nikawa najiuliza…

Nilijiuliza maswali mengi bila hata majibu, nikaona niache kuwaza ujinga na nipambane na yanayonihusu…

Basi muda ukafika ambapo tulipaswa kwenda kwenye kikao, ile naenda ofisin kwa nabil namkuta mlangon kana kwamba alikuwa amekaa hapo muda mrefu akiwa ananitazama, nikatabasamu kisha nikamuambia “ boss tunaweza kwenda, kisha nikaanza kuongoza njia…

Kilikuwa ni kikao cha uwekezaji, ambapo kampuni moja ilitaka kuwekeza kiasi kadhaa cha fedha kwenye kampuni yetu, na alikuwa kijana mmoja ambae alikuwa anaonekana kama ajazidi miaka 35 na wazee wawili, Yule kijana akawa ananiangalia, nikaona kabisa nabil amekosa kabisa utulivu, akawa anakunywa maji kwa hasira, kana kwamba ajawah kuyanywa maji kuanzia amezaliwa, na siku hio ndio amekutana na maji….

Akaanza kupoteza umakini kwenye kujibu maswali, maan macho yake kila wakati yalikuwa yananiangalia mm na huyo kijana mtanashart ambae amekuja kuwekeza, nikaanza mimi kumjibia maana alishaanza kujibu vitu visivyoeleweka, na kwa sababu ya kukuza jina kampuni nikawa najibu mimi, yaan kitendo cha kikao kuisha tu, akanishika mkono kwa hasira akaanza kunikokota kwamba alihisi nitachelewa kutoka pale kwenye sehemu ya mkutano, hivyo akaona bora anitoe yeye…
“vipi boss uko sawa? Ikabidi nimuulize mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa mkutano…
Akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha hakunijibu akaondoka zake…

Nikajiuliza pale shida ni nini, ila sikutaka kuchosha akili yangu, kwanza akili yenyewe sina, huo muda wa kuichosha si bora nihangaike na mambo mengine…

Basi nikawa nimekaa naendelea na majukumu yangu mara nabil akanifata kisha akasema “ samahani lola, tunaweza kwenda kupata chakula cha mchana pamoja?...
“ hapana kuna kazi namalizia kufanya boss, unaweza ukaenda mwenyewe tu kama hautojali, nikajibu, maana sio kweli kama nilikuwa na kazi, ila sikutaka kuongozana nae, maana kuna muda nahisi kama ananitaka hivi, na mimi nina amer wangu….
“ hivi huyu mwanamke anajikutaga nani? Kila anachoambiwa hataki, na kitu pekee anachokitaka ni kuchekeana chekeana na wanaume tu, akawa anawaza nabil huku akiwa anatoka nje kwa ajili ya kwenda mgahawani kupata chakula cha mchana, na hakuwa anajua kama anaongea kwa nguvu, kiasi kwamba watu wakawa wanamshangaa boss wao anaongea mwenyewe, mpaka msadizi wake alipomshtua, ndio akaacha kuwaza kwa sauti…

Ila shida ya nabil kila akikaa pekee yake, anawaza kunivua nguo na kufanya nae mapenzi, maana hisia zake ndio zilikuwa zinamtuma huko…..
ITAENDELEA……………..


CEO’ ANGEL 5
Penzi la playboy CEO na secretary wake
HUSQER BALTAZAR
Basi nabil akaenda kula lakin akili yake haikuwa inatulia, kila akitaka kula akawa anawaza huenda nilikuwa nachekeana na wanaume, basi akachukua chips kuku na juice na chakula chake akabeba kisha akaja nacho mpaka nilipo…

Nilikuwa namalizia kuhifadhi nyaraka flani hivi kwenye laptop yangu, nikashangaa kipasel kinawekwa mezani mwangu, kisha nikasikia sauti ya boss wangu nabil ikasema “ kuna muda wa kazi na muda wa kula mrembo, naomba uache kila kitu na ule maana afya yako ni bora zaidi….

“ owww asante sana boss, nikasema kisha nikazima laptop yangu kisha nikaanza kula na nabil akakaa pemben yake akiwa na chakula chake, akawa ananiangalia sana, mwisho nikaona niseme maana sipendi kuangaliwa bila mpango maalumu…
“ alafu boss siku hizi sikuoni kabisa na wale wanawake wako, maana wakati nafika kila mtu alikuwa anakuongelea wew, nikasema, nikiamin maneno na hadhith zangu huenda zikapunguza namna ambavyo nabil alikuwa ananiangalia…
Nabil akacheka kisha akasema “ mwanaume ukimuona ni Malaya sana na huenda anadhalilisha sana wanawake, jua hajapata mwanamke ambae atamchanganya na kumfanya asifikirie wanawake wengine wote zaidi yake, kipindi kile nilikuwa sijui maana halisi ya upendo ila sasa hivi nimependa sasa, maana sitamani mwanamke ambae nina mpenda anichukulie kwa namna yoyote ile tofauti, natamani anione kama mwanaume bora kuliko wanaume wote kwenye maisha yangu, natamani anione kama mm ni wathamani kuliko kitu chochote kile, ndio maana nimeacha kila kitu kwa ajili yake…

“ owww huyo mwanamke atakuwa ni mwanamke mwenye bahati sana, maana sio rahisi mwanaume mwenye pesa, muonekano mzuri na ambae yupo romantic kama wewe, yaan vigezo vyote vya mwanaume bora unazo na kumpenda mwanamke mmoja na kuacha kila kitu kwa ajili yake………………

Nabil akacheka kidogo kisha akaangalia chini kwa sekunde kadhaa na kusema “ vipi kama huyo mwanamke unamfahamu, una kipi cha kumshauri..
“ nitamuambia kuwa boss wangu kipenzi kaacha kila kitu kwa ajili yako, hivyo hakikisha unampenda, unamueshimu na kumtii, maana kumpata mwanaume anaekupenda kwa dhati siku hizi ni kazi sana, nikasema…

Nabil akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akashusha pumzi na kuangalia chini kwa kama dakika mbili, akawa kama anatabasamu kwa mbali, kisha akainua uso wake na kusema “ hivi lola ni sifa gani kuu huwa unaangalia kwa mwanaume na hizo sifa zikasababisha umpende…
“ sifa kama za mwanaume wangu, nikajibu…
Nabil akacheka kwa dharau kisha ni kama akawa anajipooza na kusema “ kwani mwanaume wako anasifa gani?...
“ mwanaume wangu kwanza ni mtu wa mungu sana, kila wakati huwa tunasali pamoja na kuomba huwa tunaomba pamoja, na hio ndio dua ya kwanza ambayo nilikuwa naomba kila siku nipate mwanaume wa aina hio, na pili ni mwanaume mpambanaji sana , yaan kuna muda anakosa kabisa ila unaona kabisa jitihada zake kwenye kutafuta, na mwisho ni mwanaume ambae kila nikiwa nae anahakikisha kuwa nina furaha, huwa anapambana sana kuweka tabasamu kwenye uso wangu, na kiukweli kwenye maisha yangu yote nadhan amer ndio mwanaume wa kwnza na wa mwisho kwangu na kwneye maisha yangu yote kwa ujumla….

Nabil hata hakunijibu akasimama na kuanza kuondoka bila kusema kitu, nilishangaa maana alikuwa anaonekana kama amekasirika sana, ila hata hicho kisirani chake sikutaka kukijali nikaendelea na kazi zangu kama kawaida…
ITAENDELEA …..


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote