Follow Channel

DEMIR (Mwizi Wa Moyo Wangu)

book cover og

Utangulizi

Aisee mapenzi ya kweli yapo my wangu so usijikatie tamaa kuona kila leo unakutana na wahalifu wanaokuja na kuuiba moyo wako kisha kwenda kuuburuza kwenye michanga ,na kuurarua.

Mwisho wanautelekeza kati kati ya bara bara boda boda wanau kanyaga na kuua kabisa 😁, masikini mtoto wawatu unabaki kuona mapenzi kama usongo🥺.

Haya kaa nikupe story yangu uone nilivyo kutana na mwizi wangu ,mwizi wa kipekee alie iba moyo wangu na kwenda kuutunza mahali safi na salama sio kama huyo mhalifu wako alieutelekeza moyo wako kati Sinza kwenye mataa.

Na ukishamaliza kusoma embu amka kung'uta mavumbi ukaoge uvae vizuri na urudi sokoni sawa my wangu ☺️.

DEMIR ( mwizi wa moyo wangu🥰)
SEHEMU YA 01
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com

Ikiwa ni saa tisa kasoro usiku ,nilikuwa nimekaa kitandani huku nikiangalia sketi yangu ya mwanamke nyonga na blauzi ya vuta domo kwenye kifua ☺️ huku nikitamani mda uende niweze kuivaa🥲.

Dakika zilisogea nikiwa bado nimekotoa macho , akili ilinambia we boya lala ila moyo unasema lala uone utakavyo achwa na gari sijui utapaa kufika huko uendako .😕

Nikaona moyo una point acha nisubirie kama vip nitalala nikiwa tayari kwenye gari😊, jamani kesho yake nilikuwa na safari ya kwenda dar.

Safari hii ilininyima usingizi maana ilikuwa mara yangu ya kwanza kusafiri nje ya mkoa wangu( Kigoma ) hivyo nilishindwa kulala nikihofia nitaachwa na gari.😌

Mda ulienda ilipofika saa kumi na moja kasoro haraka nikashuka kitandani na kwenda seblen nikachukua ndoo yenye maji na kwenda kuoga .

Sikuogopa kuwa bado hakujakucha ila akili yote ilikuwa kwenye safari☺️, basi nilioga na kujisugua vizuri kabisa ,na ninaweza kusema toka nimeanza kujiogesha basi leo ndo nimeoga .😁

Ila siku zingine naona nilikuwa najimwagia tu , maana nikitoka hapo ukanikagua uchafu utakao kuta mwenyewe utanirudisha bafuni ila leo aaah nimeoga bwana .☺️

Basi baada ya kuhakikisha nimeng'aa cheusi mie nikatoka ,hapo natembea kwa kunyata mchanga usije kunigusa😌, sasa ile nimefika karibia na mlango nikashtuka kuona kitu kimekaa .

Kutokana na kuwa na giza bado ilinifanya nisijue ni kitu gani, hilo yowe nililopiga alooh hadi ndege walio kuwa wamelala waliamka na kukikimbia kuokoa maisha yao 😅

Niligeuka haraka yebo/malapa nikazivulia kule mbio hadi chooni nikajificha kwenye pembe maana choo hakikuwa na mlango zaidi kulikuwa na gunia lililochnwa kati kati na kuwekwa kama pazia huku likishikiliwa mawe.

(Nisisikie mtu anatia neno kwenye hili , mkiache choo chetu🥲)

Basi bwana kelele yangu iliwaamsha baba ,mama pamoja na kaka wakatoka ndani mbio na kuja nje ,baba akaniita , kusikia sauti ya baba nikatoka huku nikiogopa .😢


Sasa baba akawa ananiuliza kuna nini mbona nimepiga kelele mama na kaka wakawa bize kunichamba eti nafanya nini nje wakati ni usiku bado .🙄

"Mnaweza kuacha ujinga wenu nikajua nini kimemkuta mtoto maana mnaropokwa tu" alionga baba baada ya kuona hamna usikilizano.

Mama kwa sauti ya juu akamjibu " tuache ujinga gani yeye saizi usiku anafanya nini nje we komwe siuna ndoo yako ya kujisaidia haja ndogo haya huku nje umefuata nini?"

Mama alivyo sema hivyo nilimkata jicho nikatamani nimwambie nilikuwa na wanga( maana wanaona kabisa nimetoka kuoga halafu bado anauliza eti nafanya nini nje 🙄),ila nikajiambia nifunge mdomo maana kama ninge thubutu kuongea hivyo.

Ninge kanyagwa mguu wa shingo shwaaa kifo hiki naenda kuzimu 😬,hivyo nikakaa kimya baba hakutaka tuendelee kubaki nje tukaingia ndani na moja kwa moja akaenda zake kulala.

Sasa mama yangu mimi cha mdomo hakutaka liishe akanifuata nyuma hadi chumbani, na kuniuliza " nimekuuliza nje huku jibu mh nambie ulikuwa unafanya nini?"

"Jamani mama kwani huoni kama nimetoka kuoga "

"Kuoga saizi ,kwanza tangia lini mbwa wewe ukaoga asubuhi tena bila kusemwa ,unaniona sina akili si ndio?"

"Jamani mama sasa mbona unataka kuzua vitu ambavyo havipo ,ina maana ulitegemea nitasafiri bila kuoga ?"
"Shida sio kuoga ,utakuwa na ujinga wako ilienda kuufanya na ili tusikugundue ukajifanya unaoga , we hizo janja janja zako nazijua nilishafanya zaidi yako ."

"🙄sa kama ulikuwa unafanya si wewe unataka kusema kila mtu anafanya ulicho kuwa unafanya wewe ?, mtu unaongea hadi mishipa ya shingo inakusimama kisa unahisi watu wote wako kama wewe.

Ila sikulaumi naona ufupi ukizidi inakuwa tatizo la taifa , kamdomo hadi watu tunaishi bila amani 😏"

Niliongea kwa sauti ya chini nikijua hatanisikia nikasahau huyu kiumbe anamasikio kama sumaku😬, kitu kilicho nikuta ni historia ambayo inabidi iwekwe kwenye kumbu kumbu za matukio ya taifa 😢😔


ITAENDELEA

DEMIR (mwizi wa moyo wangu 🥰)
SEHEMU YA 02
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO...........

Nilipondwa nusu nife 😩, baba na kaka walikuja kunigombelezea ila haikusaidia kitu maana tulikuwa chumbani na alikuwa amefunga mlango.

Naweza kusema siku unilimuona mtoa roho macho kwa macho maana yoooh sio kwa kipigo kile , nilipondwa nikapondeka na hakujali kama nilikuwa na safari😔
Kitu alijali ni kunisurubu tu 😮‍💨 alivyo maliza kutoa hasira zake akaondoka na kuniacha nikiugulia kwa maumivu😩, mwili karibia wote ulikuwa unauma na nashukuru Mungu rangi yangu ni nyeusi.

Maana kama ningekuwa mweupe naona alama za kuvilia damu zingekuwa wazi wazu, lakini Mungu alinipa rangi nyeusi 😊

Basi nililia hadi nikapitwa na usingizi nikalala , dakika zilisogea ikapita lisaa na nusu akaja kuniamsha kwakunitia mkofi😪

Niliamka kwa kukurupuka akanambia " umelala hadi mda huu hilo gari linakufuata hapa mjinga wewe?"

(😥eeeh kumbe bado nina safari?) Niliwaza na kumjibu " Mama mi naona nisiende leo, ona nilivyo vimba nikienda huko watu siwatani angalia sana "

"Embu amka huko wakuangalie Kwa kipi ulicho nacho haswa, au umekuwa mnyama wa taifa ?"

"Ila ma.......!"

"Wewe amka mama nini mimi mwenyewe nina mama yangu , amka haraka nasema "

Kinyonge niliamka na kutaka kuchukua nguo nivae akanishika mkono na kusema " unataka kuchukua nini!, Hizi nguo zinazobana ndo unataka uvae?"

"Jamani mama sasa hii nguo inabana wapi?"

"Wewe acha ujinga hii nguo inabana wapi kwamba sijakuona jana wakati unajipima?,sikia hakuna kuvaa hizo nguo huko hauendi kuonesha makalio yako unaenda kufanya kazi"

Aliongea na kufungua shangazi kaja langu akaanza kupekua pekuea mwisho akaacha na kutoka chumbani, dakika mbili akarudi akiwa ameshika gauni mkononi.

"Shika vaa hili "

"Jamani mama ndo nivae nguo yako ?"

"Wewe vaa unataka uvae hiyo minguo yako kwani umeambiwa huko kuna maonyesho ya shape au ?"

"Hata kama lakini hii siwezi kuvaa"

"Kwa hiyo unataka kwenda uchi maana hakuna namna yoyote utakayo fanya kubadilisha maamuzi yangu"

Nilimuangalia kwa hasira sana , kinyonge nikavaa lile gauni lake na kujiangalia nikawa kama vile vinyago vya kwenye mashamba ya mpunga😕

Mama aliniangalia vizuri na kusema " hapa ndo umevaa sasa ,halafu hii nguo ulinishonea vibaya yaani nguo inayo kutosha wewe ndo unashona iwe yangu "

Sikutaka kuongea maana ningesema niongee lilelilo kwenye akili yangu safari hii angenipiga aniue kabisa 😮‍💨.

Basi baada ya kuvaa nilichukua shangazi kaja langu nikatoka nje na kukuta tayari baba ameshatoa piki piki nje ,nikapanda na mama akapanda nyuma yangu.

Nilivuta mdomo na kutamani kumwambia ashuke ili kaka apande ila nikabaki kukaa kimya, haya safari ya kutoka nyumbani kuelekea kasulu mjini ikaanza .

Sasa karibia njia yote mama anaongea tu oh tumechelewa mara vile mara hivi ,nilikuwa napata hasira natamani hata kumjibu, maana yeye ndo kasababisha haya yote kama asinge nipiga ninge lala sangap 😏

Safari iliendelea na kwa bahati nzuri tukawahi gari na sio kwamba tulifika ndani ya mda husika no ila bahati yetu ni kwamba gari lilichelewa kuondoka.

Basi tulishuka na kumpa konda mzigo wangu akaweka kwenye buti ,kwa huzuni nikamuaga baba na kutaka kuondoka bila hata kumuaga mama akaniita na kusema.

"Ina maana mimi sio wa kuagwa si ndio"

Sikutaka kuongea mengi nikamwambia tu " bye mama ubaki salama "

"Nitakuwa salama ndio ,sasa mpumbavu wewe nenda huko ukalale wala usifanye kazi sawa ? Ukirudishwa huku jambo ni hili moja kuolewa "

"Sawa" nilijibu na kuingia kwenye gari bila hata kuangalia nyuma , jamani mahusiano yangu mimi na mama yangu hayajawahi kuwa sawa hata siku moja.

Yani sisi ni watu wa kugombana na kununiana kila iitwapo leo , na nisiwe muongo kwa namna ambavyo huwa tunaishi kuna mda natamani kumuuliza hivi wewe ni mama yangu Kweli?

Maana kwa mambo anayo nifanyiaga huwa ananifanya nijihisi huenda sio mama yangu mzazi ,ila ndo mama yangu sina mwingine zaidi yake.😔

Safari ya kutoka Kasulu kwenda dar ikaanza bwana , dakika za mwanzon ilikuwa raha sana nikawa bize kuangalia namna miti inavyo kimbia 😊.

Ila baada ya saa moja nilianza kuona kila aina ya rangi ,aisee mwili ulibadilika tumbo likavurugika ikawa ni mwendo wa kurudisha chenji .😩

Ile kanga niliyo jifunika kuficha manundu ya kipigo nilicho pewa na mama haikukaa tena , watu wakabaki kunishangaa huku wakijiuliza kulikoni nimevimba uso vile .😢

Safari ilikuwa ngumu mnoo kiasi cha kujutia kwanini nimepanda bus maana niliona kama nakufa 😩, huwezi amini nilitoka kigoma hadi dar bila kula chochote.

Hata maji sikuthubutu kunywa nikawa nimekaa kinyonge huku mwili ukiwa vibaya sana 😪, lakini Mungu ni mwema nilifika salama .

Tukashuka wakuondoka wakaondoka mimi nikabaki nimekaa kumsubiri mwenyeji wangu, hapo sina simu wala nini. 😪


ITAENDELEA
DEMIR ( mwizi wa moyo wangu)
SEHEMU YA 03
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com

SINGA NAYO..............
Nilikaa stend yakapita masaa mawili ba nusu nikaona konda wa gari nililio panda anakuja akiwa ameongozana na mkaka mmoja hivi mrefu amevaa nyeupe juu hadi chini.

Walivyo fika yule konda akamwambia ndo huyu, mh nikatoa macho kulikoni aseme ndo huyu hawa wanataka kuniuza nini? 🤔.

Basi kaka yule baada ya kuambiwa kuwa ndo mimi akaniuliza " we ndo Niffer"

"Hapana siitwi Niffer naitwa Shenifa "

"🙄Sasa kuna utofauti gani, embu amka beba furushi lako kisha nifuate "

"Nikufuate kwani we nani?🤨"

"Oya sina mda wa kupoteza nitakuacha hapa oho " mkaka huyo baada ya kusema hivyo konda akanambia .

"We cheusi amka basi mbona umekaa kama umefika ?"

"Ukitaka nikae kama nimefikiwa? Me siendi kokote kwanza huyu si mwenyeji wangu "

"Sio mwenyeji wako kivp wakati yuko hapa kukupokea wewe"

"Yuko hapa kunipokea mimi kwani mimi ndo Niffer?"

"Sasa kumbe wewe ni nani?"

"Shenifa "

"Sasa Shenifa na Niffer vinatofautiana nini embu amka acha ufala "

" Eeeh kaka usinifokee , nimesha sema siendi kwasababu anaemtaja sio mimi "

Mabishano yalipamba moto , mwisho nikawambia moja tu " nyie wakaka sikieni mimi hapa nitakuja kuchukuliwa na rafiki yangu sio huyu"

Yule kaka aliekuja kunipokea akasema " sikia huyo rafiki yako ndo kanituma nije kukuchukua maana anakazi kwa hiyo kama unagoma niambie nisepe zangu"

"Rafiki yangu ndo kakutuma, haya huyo rafiki yangu anaitwa nani?"

"Malaika ndo jina lake"

"Su naona sio mimi, mimi sina rafiki wala ndugu anaeitwa Malaika wala kwenye ukoo wetu hajawahi kutokea mtu mwenye jina hilo "

Yule kaka alichukia akataka kunichukua kwa nguvu weeeh thubutu yake nani wakuchukuliwa kama gunia la mahindi mabovu 🤨, niling'ata nusu nitoke na nyama.

Watu walijaa na kila mmoja anawa anauliza kuna nini kuna nini, kwa hasira akataka kuondoka mbaba mmoja akasema hakuna kuondoka mpaka useme kwanini unataka kumchukua ile hali si wewe unatakiwa kuja kumchukua?.

Yule kaka alikuwa na hasira sana wala hakutaka kujieleza ila kutokana na hasira za watu waliokuwa pale ilimbidi awe mpole na aongee kwa utulivu.

Maana kila mtu alihisi huenda anataka kuniteka , basi akaambiwa kama ni kweli ampigie huyo mtu.

Nikasema hakuna nioneshwe namba kwanza maana kama anania mbaya na mimi hashindwi kumpanga mtu mwingine.

Kweli akaonesha namba, bahati mbaya namba alio onesha yeye sio ile niliyo nayo, nikasema hapana hii namba sio ya rafiki yangu.

Akaulizwa huyo mtu aliekutuma hana namba nyingine akasema hana , konda akasema basi ipigwe ile ninayo jua mimi akipokea akasema ni yeye inshu iishe .

Hapo nikasema sawa , na kutaja namba ( niliikalili kichwani) ikapigwa Mungu saidia ikaita akapokea, na kuulizwa kama kamtuma huyo mkaka akasema ndio.

Hadi kufikia hapo sikuwa na neno, nikabeba shangazi kaja langu na kumfuata nyuma.

Kaka yule alitembea kwa mwendo mkali , ukichanganya na urefu wake ndo kabisaa nikajikuta na kimbia ili tuweze kwenda sawa nisije kupotea bure.

Basi tukafika kwenye gari bila hata kufungua mlango akaingia na kuniacha nimesimama nisielewe hata namna ya kufungua mlango.🥺

Baada ya yeye kuingia na mimi kubaki nimesimama alishusha kioo na kusema kwa hasira" binti ingia haraka niondoke zangu "

"Samahani sijui kufungua mlango"

"Hahahah hujui kufungua mlango ,na uko wote huo hujui kufungua mlango wa gari ila zipu za washamba wezio zenyewe unafungua "

"Sio za washamba wenzangu tu hadi za baba yako naweza kufungua😏"(shenzi kabisa yaani kama sijui kitu nisiseme eti zipi za washamba wenzako zenyewe unaweza kufungua 🤧 zipu na mlango wa gari vinaingilianaje 😒)

Bwana wee kijana kujibiwa hivyo akajifanya kapanick " umesemaje wewe cheusi nitakupasua umvunjia heshima baba yangu?"

Niliwaza kumjibu hovyo nikaona eeh ngoja nitulize komwe nisije nikaachwa hapa, Kwanza nina njaa kali 🥱.

Basi kinyonge nikakaa kimya huku nikimuangalia , alipata hasira akasema "sishuki na sikufungulii nione utasimama hapo hadi mda gani fala wewe"

"Fala mwenyewe 🙍‍♀️"

"Umesemaje wewe?"

"Nimesema fala mwenyewe 😏"

"Halafu nitakufumua we binti unajifanya kichaa lione lilivyo jaa manundu kama jizi, sura baya "

Sikutaka kumjibu tena nikaweka shangazi kaja langu vizuri na kukaa ,maana nguvu za kusimama na jua lilivyo kali sina kwakweli.

Sasa bwana kichogo( ngoja nimuite hivyo maana anakichogo utafikili ndugu yake madenge) basi alivyo olivyoona nimekaa akashuka kwa hasira na kufungua mlango.

Nikataka kuingia akasema " embu subiri kaa huko mbele nisije kuonekana dereva wako "
Bila kuongea neno nikataka kukaa akanizuia na kunitaka niweke nguo zangu siti za nyuma , nikaweka na kukaa kisha akaingia na kuondoka kwa mwendo mkali.

Njia nzima hakuna alie ongea na mwenzake , mda wote alikuwa amekuja ndita kwa hasira hadi tunafika .


ITAENDELEA
DEMIR ( Mwizi wa moyo wangu🥰)
SEHEMU YA 04
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com

SONGA NAYO...............
Tulifika akashuka na kuondoka akiniacha kwenye gari ila alivyo fika mbele akarudi na kufungua huku akiniangalia kwa hasira.

Nilivyo mkorofi nilimzomea 😝na kushuka tukafuatana na kuingia ndani, jamani eneo hili lilikuwa zuri kila mahari palivutia mnoo ila sikutaka kuonekana mshamba kwa kushangaa .

Nikawa natembea macho mbele 😊 bwana kichogo alivyo mchokozi akageuka na kunambia

" Nakuona unavyo kaza fuvu na kujitaidi usigeuke ili usionekene mshamba 😁 we geuka tu maana hata usipo geuka haibadili kuwa wewe ni mshamba ."

Nilimuangalia kwa macho ya hasira moyoni nikajiambia( nipe mda mbwa wewe mbona utabweka ).

Basi tukaingia ndani ,mmh huko uvumilivu ukinishinda bwana nikajikuta nageuza shingo kuangalia huku na huko , bwan kichogo akacheka na kusema .

" Kuku wa shamba atabaki kuwa kuku wa shamba tu ona akavyo pepesa vimacho kama kachawi 😆"

Bado nilichagua kukaa kimya , akamuita Malaika na kumwambia " njoo umchukue mshamba wako asije kupiga kelele maana naona anashangaa kulikoni anajiona kila mahali😆"

Baada ya kusema hivyo Malaika alitoka jikoni mbio na kuja sebleni, nikabaki mdomo wazi 😮, baada ya kumuona rafiki yangu Ambae mimi namjua kwa jina la Kashindi.

Kashindi au Malaika alikuwa mweupe pekee kitu ambacho kilinishangaza sana ,maana toka tunakua huyu binti hakuwahi kuwa mweupe .

Wala kwenye familia yake hakuna mtu mweupe ,sasa hii rangi ameitoa wapi , na nina vyo jua mimi hata mtu akitumia caloright anakuwa na rangi zisizo pungua tatu.

Ila cha ajabu Kashindi anarangi moja tu ,nilishangaa sana 😦, basi Kashindi baada ya kunifikia nilitegemea ataniwao kwa furaha ila aligeuka huku na huko huku akionesha uoga na kusema.

"Wewe ndo umekujaje hivi sasa?"

"Nimekuja hivi ukimaanisha nini ?"

"Mungu wangu bora nikemleta Siwema yeye kidogo anajielewa , yaani unakuja umevaa kama mbibi kweli Niffer "

"Alafu kumbe wewe ndo umebadilisha jina langu, kwanza achana na mimi niambie mbona umekuwa m......."

Kabla sijamaliza ilisikika sauti ya mwana mama akimuita Kashindi kutokea nyuma yetu, wote tulieuka kumuangalia .

Macho yangu yalitua kwenye mapaja yaliyokuwa wazi kisha nikapandisha macho kuamuangalia usoni, alikuwa ni mama flani amekaa kimjini mjini sana.

Muonekano wake mavazi yake vyote vilionesha anamaisha safi sana , sasa mimi na ushamba wangu nilimuangalia na kutamani kuchungua kitenge nimfunge .

Maana niliona nikama yuko uchi 🧐, basi Kashindi aliitika mama yule akatusogelea akiwa na uso wa mshangao sana ?.

Alivyo tufikia akaniangalia na kumuuliza Kashindi " Malaika huyu ndo mwana mitindo ulie sema ?"

"Ndio madam ni huyu !"

"Mungu wangu Malaika wewe jamani !!" Aliongea huku akiniangalia juu na chini na mda huo huo wakaja binti wawili na kuungana na mwana mama huyo kunishangaa.

Mmoja wa wale mabinti akamuuliza Kashindi( Malaika )

"Malaika usinambie huyu ndo mwana mitindo uliesema anakuja leo?"

"Ndio ndo huyu" Malaika kujibu vile wakaangua vicheko vikali nikabaki nashangaa kwani kuna shida gani ?maana so kwakucheka huko.😒

Baada ya kicheko kuisha mama yule akamwambia Kashindi (Malaika )," kwa hiyo ndugu yangu wewe ulisikia maongezi ya watu na kuyarukia ,na ulivyo kosa haya ukasema una mtu wako anae jua sana kuhusu mitindo .

Lakini kimuangalia huyu mtu wako hafai hata kuwa house girl, na sijui kama unafikilia Demir atasema nini mara tu atakapo aona hii shida"


" lakin madam ni kweli anaweza sana ndo maana nilichagua kumleta hapa"

"Embu tunondolee ujinga wako hapa, mtu amevaa kama chizi ndo unasema mwana mitindo , kwanza ngoja "

Alinigeukia na kuniuliza " mh unaitwa nani na umetokea wapi?" Nilivyo ulizwa hivyo nilimuangalia Malaika akawa kama ana jaribu kuniambia kitu ila sikumuelewa.

Mama yule kuona niko kimya akaniuliza tena " wewe nakuuliza unaitwa nani na unatokea wapi?"

"Naitwa Shenifa natokea Nyumbigwa "

"Nyumbigwa ndo wapi iko ?"

"Kasulu "

"Hiyo kasulu ni mkoa au kitongoji?"

"Wilaya iliyo ndani ya mkoa wa Kigoma "

"Tobaa mwisho wa reli, haya unajua nini kuhusu fashion "

"Mmmmmm!😶"

"Mmmh nini nakuuliza unajua nini kuhusu fashion?"

Nilitoa macho nisielewe nijibu nini maana hata fashion yenyewe sikujua ni kitu gani, basi walivyoona niko kimya binti yule alie ongea mwanzo akasema.

"Ila mama unajua kupoteza mda na wewe , we mtu unaona alivyo vaa vyenyewe havieleweki halafu unakazana kumuuliza mambo ya fashion "

"Aaah acha nimuulize usikute tuna msema bure "

"Aa wapi hamna kitu hapa , yaani huyu katoka bushi ndani ndani huko ndo unataka akujibu "

Mama yule alimnyamanzisha binti na kuridia kuniuliza swali lile lile bado nikawa kimya , kuona hivyo akamwambia Malaika.

"Malaika naomba usinitafutie matatizo sawa ,mchukue ndugu yako kampandishe gari arudi alikotoka "

"Lakini madam saizi mda umeenda nilikuwa naomba walau alale kwa leo tu kisha anaondoka "

"Alale wapi ,hivi ukimuangalia unaona ana hadhi ya kulala huku ndani mfyuu embu acha ujinga na uniondolee matatizo hapa"

"Madam tafadhali sana naomba ..!"

"Wewe sitaki kumuona hapa, hivi unafikili Demir akimkuta tutasema au unataka nigombezwe kama mtoto mdogo?.

We fanya nilicho kwambia mpatie nauli aondoke haraka sana "

Mama yule aliongea na kutaka kuondoka , bwana kichogo akamuita na kusema.

" Mama mpe walau nafasi apumzike kwa leo tu kisha ataondoka kesho ,maana ametoka mbali sana bila shaka amechoka mno"

"Hivi nyie hamnielewi eeh nimesemaje aondoke leo leo , kama maetoka mbali atajua mwenyewe"

"Tafadhali sana mama muonee huruma , amekaa njiani zaizi ya masaa 20 sasa huoni kama kumrudisha saizi itakuwa sio utu"

" Sio utu ndio ila mimi kuja kugombezwa na Demir ndo utu?"

" Hapana sijasema akae ninacho omba mimi alale kisha ataondoka kesho hata hivyo Demir hawezi kurudi kesho na wewe unajua hilo"

Mama yule alitaka kukataa ila bwana kichogo akamuomba sana mwisho akakubali na kuondoka.

Na baada ya mama yake Bwana kichogo kuondoka na wengine pia wakaondoka nikabaki mimi na bwana kichogo.

Ambae baada ya kuona wote wamaondoka alinisogelea na kunambia " kesho nitakupeleka stend na nikwambie tu nitakacho kufanya kitakulizs zaidi ya hiki"

Aliongea na kushika machozi yaliyo kuwa yakitiririka mashavuni mwangu na kunicheka kwa dharau sana😢.


ITAENDELEA
DEMIR (Mwizi wa moyo wangu)

SEHEMU YA 05

MTUNZI RITHA STORIES

https://www.tupohapa.com

SONGA NAYO............

Mda huo huo Malaika alitoka jikon akashika shangazi kaja langu na kunambia nimfuate ,bila kuongea neno nikamfuata .

Kufika chumbani alirusha shangazi kaja kitandani kwa hasira na kunigeukia , nilishtuka maana aliniangalia kwa macho makalo sana .

Kwa sauti iliyojaa hasira akaniuliza " ndo umefanya nini sasa ?"
" nimefanya nini kwani?"

"Umefanya nini kwamba huoni ulicho fanya ?, Shenifa nikuunganisha huku ili uje utengeneze maisha yako ila umekuja kuniharibia .

We ni wakuja umevaa kama kibibi kichawi kweli ona linguo ulilovaa lilivyo baya , cheki minywele ulishindwa hata kusuka yebo yebo za elfu tano kweli?.

Kama haukuwa tayari kuja siunge sema kuliko kuja kuniabisha namna hii?"

Malaika aliongea kwa hasira sana , nikainua macho yangu na kujiangalia kwenye kioo kilichokuwa mbele yangu , kweli sikuwa nimependeza ila kwanini wanitolee maneno makali vile kama vile nimetenda dhambi.😔

Kwakweli nilijiskia vibaya sana na kushindwa kuzuia machozi 😭, Malaika baada ya kuona nalia akaendelea kunisemesha .

"Ona watu mlivyo kosa shukrani hapo unalia ukimaanisha nakunyanyasa ,kwanza nikuulize hiyo minundu usoni umepata ajali au uliiba chakula cha mtu kwenye gari ndo ukapigwa "

" Malaika! Nisamehe kama nimekuja tofauti na ulivyo taka ila tafadhali angalia maneno yako mimi sio mwizi"

"Unaona maneno yote niliyo ongea umesikia moja tu !, sasa sikia sina mda wa kupoteza wala siwezi kukaa nikiona maisha yangu niliyo tumia nguvu kuyajenga yakiharibika kisa upumbavu wako.

Kesho asubuhi na mapema utarudi nyumbani wala sisubiri watoe nauli nitatoa hata pesa yangu urudi tu maana ushakuwa mkosi"

Aliongea na kutaka kuondoka ila alivyo fika mlangoni akageuka na kusema " usitoke nje ya chumba hiki nadhani umenielewa"

Sikumjibu akaondoka nikarudi kujiangalia kwenye kioo na kufuta machozi😓, kisha nikakaa chini nisije kuchafua kitanda cha watu.😔

Akili ilizama kwenye dimbwi zito la mawaza , nikawaza namna nitavyo enda kusemwa na mama maana hatanielewa kama nimerudishwa kwasababu hawaja nipenda yeye moja kwa moja atajua nimefanya kosa.😔

Lakini sawa nitarudi maana sina sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kurudi nyumbani😪

Basi mda ulienda hapo njaa inanitafuna vibaya mno, kumbuka njia nzima nilikuwa na rudisha chenji na sijala chochote hivyo njaa niliyo kuwa nayo nikali.🥱

Kinyonge nilijilaza chini huku mikono yangu ikiwa tumboni , na macho yangu yalifunikwa na machozi.

Nisiwe muongo nilichukia na kujuta kwanini nimekuja dar , kichwani nikatamani iwe ndoto niamke lakini haikuwa hivyo yote yalikuwa kweli 😩💔

Msaa mawili yalipita bila Malaika kuja , njaa ilizidi kuwa kali nikasema hapana nitakufa, taratibu nikajiinua na kutoka nje ya chumba lengo niende jikon ambako yuko Malaika .

Bahati mbaya nyumba ilikuwa kubwa na sikukumbuka tulipopita hadi kufika chumbani, nilicho kifanya nikatembea kufuata koldo bila kujua niendako sio

Nikitembea na kujikuta nasimama baada ya kuona sielewi ,nikaona nirudi nikapite sehemu nyingine ,sasa kabla sijageuka ili kuondoka mlango wa chumba jirani ukafunguliwa.

Akatoka mama kichogo, alooh kitendo cha kuniona pale alianza kubwata na kunitamkia maneno makali vibaya mnoo😢.
Niliomba msamaha lakini haikusaidia akaendelea kunitukana na kuniita mwizi 😥, matusi yote niliyaacha yaende ila kuitwa mwizi kuliniumiza mno.😩💔

Malaika na wengine walikuja ikabidi Malaika aniombee msamaha na kunitaka nirudi chumbani, mama kichogo akasema.

"Unampeleka wapi?"

"Nampeleka chumbani "

"Ili akachore mazingira aje atuibie si ndio?, embu mpeleke nje kwenye nyumba ya mlinzi huko ndiko atakaa hadi kesho.

Na naomba sana ikifika kesho aondoke mapema sana ,staki niamke nimkute akiwepo mnanielewa?"

"Sawa madam" alijibu na kutaka kunishika ili anipeleke nje kwa mlinzi kama alivyo ambiwa , nimzuia na kumgeukia mama kichogo na kusema.

"Samahani mama ,naomba unisamehe sana kwakukukwaza ,lakini naomba nitengue kauli moja kati ya zote ulizo tamka .

Mimi sio mwizi wala sitakaa niwe mwizi, ila naomba ombi moja tu naombeni nauli nirudi kwetu, najua mda huu siwezi kupata gari ila niko radhi kulala stend kuliko kulala hapa nikakunyima amani"

"Ooooh waooo kumbe we ni jeuri eeh, yaani uko hapa kimakosa ila bado unafungua bakuri lako kunijibu mimi ?, eti naomba nauli 🤧.

Sasa sikia hakuna baba yako wala mama yako hapa, hivyo swala la kupewa nauli ni mapenzi yangu kwani umefanya kazi gani hadi upewe hiyo hela lione sura "

Nilitaka kuongea ila Malaika aliniwahi na linitoa kwa nguvu hadi nje na kuniachia kwa kunisukuma moja kwa moja nikaenda chini.

"Hivi una shida gani mpuuzi wewe si ilikwambia usitoke nje ya chumba haya ulikuwa unafanya nini kwenye vyumba vya watu?"

Nilimuangalia usoni Malaika nikajiuliza huyu ni rafiki yangu kweli au nimebadilishiwa mbona mara zote alikuwa na huruma sana na mimi ,ila leo ananisukuma kama mzigo bila kujali nitaanguka au kuumia.
Kwa sauti ya upole nikamwambia " Nisamehe sana ila sikuwa na lengo la kwenda kule me nilitaka kuja uliko ili nikuombe chakula maana nasikia njaa sana "

"Unasikia njaa kwanj ungevumulia hadi nikamaliza kazi zangu unge kufa ? Haya umesha kasirisha watu unafaraha sasa ?"

"Nisamehe rafiki yangu ni njaa tu, sijala chochote toka jana na nimesafiri na tapika njia nzima "

"We simshamba wa magari utaachaje kutapika 😒, embu amka nenda kakae kwa mlinzi na ole wako utoke tena"

"Sawa naomba basi chochote cha kitafuna kama hamna naomba hata maji"

"We amka hapo bwana, chakula chakula kwenu kipo ?"

Kauli yake ilinipa hasira nikatamani kumjibu ila nikaona nikae kimya kwani sina mda wa kukaa hapa , kinyonge nikainuka na kuanza kupiga hatua kuelekea anakokaa mlinzi .

Mara ikasikika honi nje ya geti, haraka mlinzi akainuka na kufungua geti, kwa hatua za haraka haraka nikaenda kukaa na gari likaingia na kwenda kupark.

Baada ya kupark akashuka dereva na kuzunguka upande wa pili akafungua mlango , kishaa akashuka mwana mama alikuwa ndani ya mavazi nadhifu sana .

Mama yule baada ya kushuka alipiga hatua kidogo na kumsalimia mlinzi kwa sauti ya furaha, mlinzi alijibu salama na kwenda kusaidizana na dereva kubeba mabegi ( bila shaka ametoka safari).

Basi mnyonge mie nikaendelea kujikunyata huku macho yote yakiwa kwenye mti mkubwa wa machungwa 😔, mara nikasikia hatua za mtu akija nilipo .

Haraka niligeuka na kukutana macho kwa macho na mama yule alieshuka kwenye gari sekunde kadhaa zilipita.

Haraka niliinuka na kumsalimia kwa heshima huku nikiinamisha kichwa chini, mama yule aliitikia salamu yangu kwa uchangamfu na kuuliza.

"Binti mzuri mbona umekaa juani?"

Kauli yake ilinifanya nikainua uso kumuangalia , alikuwa anatabasamu pana usoni .

Basi kwa uoga nikajibu .

"Aaaa nime.....!" Kabla sijamaliza kuongea ilisikika sauti ya mama kichogo akiita dada huku anamkimbilia .

Alimfikia wakakumbatiana kwa upendo sana , baada ya salamu mama kichogo akataka kumshika dada yake huyo ili waende ndani ila mama yule aligoma na kuuliza.

"Huyu binti mbona yuko hapa na jua lote hili?"

Mama kichogo alivyo ulizwa hivyo alipata kigugumizi na kushindwa kujibu, akaja yule binti ambae toka nimefika hakuwa ameongea akasema .

"Mama huyu ndo binti alie letwa na Malaika kwaajili ya kazi ya kaka "

Mama yule alivyo ambiwa hivyo alinigeukia na kuuliza " Okay so kwanini yuko nje ?"

Mama kichogo alitaka kujibu ila binti yule aliwahi na kusema " aunt kamfukuza na kusema ni mwizi so anatakiwa kulala kwenye nyumba ya mlinzi na ikifika kesho aondoke kwao"

Maneno ya binti yule yalimfanya mama yake akachukia na kumgeukia dada yake kwa hasira akamuuliza " hiki anachosema Alina ni kweli?"

" Aaaam ni kweli ila nimefanya hivyo kwasababu hana sifa tulizo hitaji ndio maana anatakiwa kuondoka"

"Hana sifa mlizo hitaji sawa na sifa za ubinadamu pia hana hadi mumuweke binti wawatu nje kwenye jua hili ona alivyo dhaifu.

Hivi mnatoa wapi roho mbaya namna hii , kweli mtu ametoka nyumbani kwao anafika sehemu nakufanyiwa haya ? Kwakweli mmenikwaza sana ."

Aliongea akionesha kuchukia sana ,kwa upendo akanishika mkono na kunambia " nisamehe sana mwanangu na pole pia , naomba twende ndani ukapumzike "

"Hapana mama niko sawa hapa ,ila kama hutojali tafadhali naomba nauli nirudi nyumbani "

"Sawa utaenda ila hadi aliekutaka aje ndo utaondoka , kwasasa twende ndani ukapumzike "

Nilitaka kukataa ila nikaona niache ubishi nisije kuninywa nauli, basi alinishika mkono tukaongozana kuelekea ndani.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote