ESME (just a maid ) 💃🥂
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 01
www.tupoahapa.com
ANZA NAYO…
Ikiwa ni Majila ya jioni, Ndani ya jumba kubwa la kifahari, jumba ambalo lilijawa na vitu vingi vya thamani, Ndani ya jumba ili ukiingia mtu mlala hoi Kama Mimi Lazima Uhisi Kuwa unachafua Nyumba ya watu😂.
Ndani ya Nyumba hiyo anaonekana mwana mama wa makamo, akiwa amevalia mavazi ya kisasa sana lakini Pia yenye thamani ya Pesa nyingi, mwana mama huyo kichwani alikuwa na na nywele ya bei ya juu kabisa.
KWa hasira mwanamke huyo akaita.
“Jace, Jace, we Jace wewe “
Mama huyo anaita Mara Tatu mfululizo kisha baada ya muda anakuja Kijana Fulani hivi mtanashati kuliko kawaida, mkaka ambaye Kama wadada wakimuona lazima waombe mbegu maana kaka yuko hot.
“Umekuwa bubu sasa hivi ??”
Mwana mama huyo anamuuliza Kijana huyo.
“Hapana mama lakini umeniita kwa Kelele sana ujue “
Alizungumza mkaka huyo uku akitabasamu pasi na kujua Kuwa mama yake alikuwa na hasira sana na yeye.
“Umemfanya nini Esme ??”
Mwana mama huyo alimuuliza Kijana huyo aliyejulikana Kama Jace.
“Sijamfanya kitu mama”
“Jace nakuuliza kWa Mara nyingine umemfanya nini Esme ? “
“Mama sijamfanya kitu Kwanini utaki kuamini ??”
“Kwahiyo Esme sasa hivi amekuwa Kama chizi, Eşme amekuwa kama Mtoto kwamba akijisikia kulia tu Analia muda wowote si ndio ? Achana na kulia zile alama za vidole kwenye mashavu yake ni nini ??”
Jace anashindwa kumuangalia mama yake na kubaki akiangalia chini tu ikionesha wazi Kuwa yeye ndio amempiga huyo Esme ambaye ata sisi hatumjui.
“Kwanini umempiga ??”
Mama huyo alimuuliza Kijana wake.
“Mama nimeshakushtakia Mara kadhaa Kuwa Esme amekuwa jeuri sana kwangu, mama Esme sasa
Hivi nikimtuma aendi, usafi chumbani kwangu ana mwezi sasa ataki kufanya, lakini Leo asubuhi before sijaenda chuo nilimuachia nguo zangu aweze kunifulia lakini mama nimerudi nimezikuta zikiwa vilevile, so nimempiga lakini sio sana “
Mama mama huyo anamsogelea Kijana wake na kuanza kumvuta mashavu yake na kumuuliza.
“Ni wewe ndio unamlipa Eşme umu Ndani ?? “
“Hapana mama”
“Mara ya mwisho nilikuammbiaje ??”
“Shughuli zangu nifanye Mwenyewe “
“Good kumbe kumbukumbu unazo vizuri kabisa, so kabla Sijakupokonya gari na Kuanza kwenda chuoni kwa daladala, sasa hivi INGIA chumbani kWa Esme na ukamuombe msamaha “
KWa mwendo wa taratibu Kijana huyo anaonekana akisogelea chumba cha Esme.
SONGA NAYO SASA……
Niite ESME Nina miaka 24 Binti wa kwanza kwenye familia ya watoto wawili, ukiachana na mimi Kuwa Mtoto wa kwanza lakini pia nina damu group O you can imagine how nakuwa na hasira za haraka .
Mimi ni mtu ambaye sitaki matani kabisa ikija upande wa serious, Mimi ni Binti ambaye sivumilii dharau na Nina misimamo yangu muzuri sana na ninajua kujisimamia, Ila kuna mtu mmoja tu ndio ananiweza na kunionea sana 🥹.
Kutokana na Kuwa na ugumu wa maisha kwennye familia yetu, familia ambayo inasimamiwa na baba tu pasi na Kuwa na mama, kwani mama yetu alifariki Mdogo wangu akiwa Mdogo sana hivyo kwa upande wangu nikalazimika Kuwa mama kwaajili ya Mdogo wangu japo nilikuwa Mdogo pia.
Eşme mimi nilifanikiwa kupata kazi kwenye familia ya kutajiri sana hapa mjini, familia ambayo Pesa kwao sio shida kabisa.
Familia hii ilibarikiwa watoto watatu ambapo wawili ni wa kike na wa mwisho ni wa kiume ambaye anajulikana Kama Jace.
Ndugu wa Jace ni kila mtu Ana Makazi yake uko, hivyo Nyumbani kwao yupo tu baba, mama na huyu Mtoto wao Jace.
Familia hii ni familia yenye upendo sana, ni familia ambayo Inajali utu wa mtu, ni familia ambayo inajua utu ni nini.
Hii imekuwa tofauti kwa Jace kwani Jace ni Kijana kwennye dharau, majivuno lakini pia unaweza kuongezea na roho mbaya maana yooooh huyu Kijana ananionesha kila aina ya rangi umu Ndani kwao.
Kuna muda nawaza ata kuachana kazi lakini nikifikilia na hali ya nyumani kwetu Nashindwa kabisa kufanya maamuzi magumu najikuta nikiendelea kuvumilia manyanyaso kutoka wa Jace.
Ikiwa ni siku ya jumanne, kila mtu akiwa ameenda kwenye majukumu yake, Nyumbani nilibaki Mimi tu, nilifanya shughuli zangu zote kisha nikaandaa chakula cha mchana ambacho ni Mimi na Jace tu ambaye Mara nyingi uwa Anawai sana kurudi kutoka chuoni kwao.
Nikiwa zangu chumbani, niliweza kusikia sauti ya jace ikiniita kWa ukali sana na ndio kwanza alikuwa Amefila Nyumbani.
“Limesharudi sasa”
Nilinung’unika kisha nikanyanyuka na kwenda sebuleni ambapo alikuwepo Jace.
“Hivi umepika Tena hii mitambi na hayo maini kwani hakuna chakula kingine ??”
Jace aliniuliza.
“Ndani hakuna kitu na madam amesema Kuwa manunuzi yatafanyika kesho kWa Leo kilike kilichokuwepo “
Nilijibu na Kugeuka nyuma uku nikitaka kuondoka, Jace akaniuliza.
“Aliyekuambia uondoke ni Nani ??”
Nikageuka nyuma na kumuangalia tu Kama Ana neno azungumze Nami nikajipumzishe maana nimechoka sana.
“Kwahiyo Jana ulifurahi sana mimi kukuomba msamaha ??”
Jace aliniuliza.
Ila huyu kaka jamani ni anapendaga ukorofi na na Mimi na sio kitu kingine, kulikuwa na haja gani ya kurudisha mada za nyuma.
“Jace mambo hayo yameshapita lakini pia sio Mimi niliyekuambia uniombe msamaha”
Kabla Jace ajajibu kitu simu yake iliita na haraka akapokea na kuzungumza.
“Yes babe ndio nimefika home hapa najiandaa chap nakuja “
Baada ya hapo Jace akanioneshea ishara ya Ngumi na kuondoka chumbani kwake.
KWa upande wangu nikaamua kutoka nje tu na kwenda kupiga story na kaka mlinzi ambaye nilimzoea sana sana na alikuwa ni Mcheshi sana.
Tukiwa bize Tunapiga story na kaka mlinzi, tulikuwa tukicheka sana muda huo huo sauti ya Jace ikasikika.
“Juma fungua geti chapu na wewe Eşme njoo hapa “
Basi nikanyanyuka nilipokuwa nimekaa na kusogea Karibu na gari yake kwaajili ya kumsikiliza.
“Pale unafanya nini ??”
Nilimuangalia kWa muda kisha nikamuuliza.
“Kwani wewe uliona nikiwa nafanya nini ??”
“INGIA Ndani sasa hivi halafu nikirudi utanieleza Kama na huyu unampa Utamu wangu Walahi nakung’oa shingo”
Nika………
ITAENDELEA…..
ESME (just a maid ) 💃🥂
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 02
www.tupoahapa.com
SONGA NAYO…
Iko hivi my zangu, wakati naanza kazi hapa, mbwa mimi nikaangukia kwenye uongo na ukweli wa huyu Kijana Yaani Jace na tukawa wapenzi na ndugu yenu nikazama kweli kweli mpaka nikawa namuita mume.
Lakini gafla tu Jace akabadilika na Kuwa mtu wa tofauti sana, Jace alihakikisha Kuwa ananiumiza kila iiitwapo Leo na sijawai kujua kosa langu ni nini, ninachojua ni Kwamba aliniambia Mimi sio Type yake na awezi Kuwa na future na Mtoto wa kimasikini kama mimi 🥹.
Sasa hivi Jace ako na mwanamke wake mrembo sana na wanaendana kwani Binti nae Nyumbani kwao Pesa ipo.
KWa upande wangu nimebaki kunyanyasika tu na kutumika kingono na huyu Kijana pale tu anaponiitaji, kitu kingine Jace apendi kuniona na mwanaume
Mwingine na Mara nyingi uwa ananipeleka mpaka sokoni .
Anyway tuendelee.
Basi Jace akapanda kwenye gari yake na kuondoka uku akisisitiza niweze kuingia Ndani.
“Ila kama umu Ndani boss Angekuwa ni Jace Walahi tungemlamba mpaka miguu “
Alizungumza Juma uku akifunga geti.
Nikacheka na kumjibu.
“Aaaah mwenye Pesa sio mwenzio Bwana tukomae tupate za kwetu na sisi “
“Sawa lakini huyu Kijana ana roho mbaya sana, Yaani yuko tofauti na wazazi wake lakini pia wale dada zake Yaani huyu Sijui Alizaliwa kwenye Giza “
Walahi Juma ni mtu Mwenye Maneno sana nilijikuta nikicheka tu maana doooh Sijui Maneno yake anatoaga wapi.
“Juma Niache mwenzio sitaki kucheka”
“Cheka tu ndugu yangu sasa hivi maisha mafupi sana, Yaani Mimi ndio maana nikipata nafasi ya kuinjoy uwa nainjoy sana Sina muda wa kupoteza.
Basi tulipiga story kadhaa kisha nikarudi zangu Ndani.
******
Siku iliyofuata Bwana, ilikuwa ni siku ya kwenda kununua zaga zaga za Ndani maana kulikuwa hakuna kitu chochote kile Yaani kila kitu kilikuwa kimeisha.
Nikajiandaa zangu kisha Mimi na Jace tukaanza safari ya kwenda sokoni.
Tukiwa kwenye gari, kila mtu alikuwa kimya, mimi nilikuwa nikiangalia mazingira ya nje na Jace alifocus na kuendesha gari; gafla tu from no where Jace akaanza gubu lake.
“Hivi Kwanini Jana usiku nakupigia ujapokea ata simu yangu moja ??”
Nikiwa naendelea kuangalia nje nikajibu.
“Nilikuwa nimelala”
“Umelala wapi wakati nilikuwa nakuona online, Eşme umeanza kunizoea sasa hivi si ndio ??”
“Jace usiku Kama ule ulikuwa unataka kuzungumza nini na Mimi ? Ni muda wa kupumzika so nilikuwa nimepumzika”
KWa hasira Jace akapaki gari pembeni na kufoka.
“Hivi unanipandishia sauti Mimi si ndio ? Esma ni mwezi sasa unanikwepa sana, nikikuomba penzi utaki kunipa unataka niendelee kutumia nguvu si ndio ??”
Hapo nikajikaza na kumuuliza.
“Kwani happy akupi ? Si Jana ulikuwa nae takribani siku nzima “
My zangu happy ni mwanamke wa Jace.
“Happy ni mke wangu Sawa, Yule sio mtu wa kutumika hivyo she’s my everything Sawa, sasa hapa tukirudi unanipa haki yangu “
“Jichanganye Leo uone kama Sijambembea hayo ma Nanii yako “
Nilizungumza kimoyomoyo.
Kiukweli nilishachoka kutumika na huyu Kijana hivyo niliamua kujisimamia Mwenyewe, Yaani huyo happy ndio anamuona Kuwa ndio mwanamke halafu Mimi ni Chambo chake cha starehe Walahi Ataona upande wangu wa pili.
Basi akawasha gari na safari ikaendelea.
Tulifika sokoni na kuanza kununua kila kitu tukizunguka uku na uku.
“Weeeh Esme weeeeh unananichanganya mwana wa mwanamke mwenzio “
Alizungumza mkaka ambaye anatubebeaga mizigo kwaajili ya kumpeleka kwenye gari.
Huyu mkaka jamani ni amenizoea sana na Mara nyingi uwa ananitania kama hivyo na anajuaga Mimi na Jace ni kaka na dada na Mara nyingi uwa anamuita Jace shemeji pasi na kujua Kuwa mwenzie uwa Anachukia sana.
Tulifanya manunuzi pale kisha hao tukafunga safari na kurudi Nyumbani.
“Tunaweka vitu chap tunaingia chumbani Nina hali mbaya sana “
Alizungumza Jace uku akitelemesha mizigo kwenye gari haraka haraka.
İle kufungua mlango wa kuingia Ndani tu uso kWa uso na mama yake mzazi.
KWa upande wangu nikashusha pumzi Ndefu sana nakushukuru Mungu maana ni Kama aliniokoa kwenye mikono ya Jace.
“Oooh mama Leo mapema “
Jace akaanza kujiongelesha.
Mama huyo akamuangalia Kijana wake kisha akamuuliza.
“Kwani ujapenda Mimi kuwai kurudi jamani ? Ata hivyo Leo ni siku ya kuzaliwa kwa baba yako so Lazima tufanye kitu “
Hapo Jace alishtuka sana na kusema.
“Uwezi aminI nimesahau mama ata kumuwishi sijamuwishi”
“Na usije ukamuwishi tuje kumfanyia surprise”
Majila ya Saa 2 usiku, baba mjengo alirudi na kukuta Nyumba ikiwa imechangamka sana, lakini pia watoto zake wote watatu walikuwepo, lakini pia na mkwe yake nae alikuwepo Yaani mume wa Mtoto wake wa kwanza.
KWa furaha familia hiyo ikaanza kumuimbia baba yao na kumpatia zawadi.
KWa upande wangu nilijikuta nikilia tu maana maisha yetu sisi ni kukimbizana na Pesa tu sijawai ata kumnunualia baba yangu cake kwenye siku yake ya kuzaliwa, na sio baba tu ata Mimi sijawai kukata cake maisha yangu yote, hivyo kitendo iki kilinifannya nilie sana.
Muda huo huo zilisikika hon za kutosha nje mama jace akazungumza.
“WiFi yangu huyo hatimaye Amefika “
Kila mtu akatoka nje mbio mbio na Mimi sikutaka kupitwa nikaenda nje 😂🙌.
Nyieeeh Kuna watu wanaishi luxurylife jamani, hii ndinga aliyokuja nayo huyu Wifi sio ya michezo, wakakumbatiana pale kisha mwanamke huyo mgeni akasema.
“I have a surprise “
Kisha akafungua gari na akashuka mkaka Fulani hivi hot kuliko hiyo hot yenyewe, Walahi huyu mkaka ni mzuri kuliko huo uzuri wenyewe kila mtu akapiga Kelele kWa kutaja jina la mkaka huyo …
“SKYLER “
Kwa upande wangu nilibaki nikimshangaa na kushindwa ata kufunga mdomo, Jace akanisogelea na kuniambia.
“Kunakoelekea Utakula mbu”
😂🙌😂 Ila kweli jamani..
NAKUJA MY ZANGU.
ESME (just a maid ) 💃🥂
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 03
www.tupoahapa.com
SONGA NAYO…
Basi mwaya Eşme mimi nikafunga mdomo wangu na kusogea Karibu kwaajili ya kupokea mizigo Yao ambayo walikuja nayo.
Huyo Kijana waliyekuja nae jamani Kwanza muda wote ni ako na tabasamu panda usoni mwake nyie na hii ndio ilimfanya azidi Kuwa handsome.
KWa pamoja wakaingia Ndani kisha Mimi na Juma tukaanza kuingiza mizigo Ndani.
Baada ya kuingiza mizigo Ndani moja kwa moja nikaenda kwenye vyumba vya wageni na kuanza kuweka vizuri ili wageni hao Kama watakuwa Wanalala Basi walale kwenye sehemu nzuri lakini safi .
Ila kwa ile mi begi ambayo wamekuja nayo hawa watu sio wa kuondoka Leo wale kesho.
“Eşme, Esme”
Mama Jace aliniita baada ya kuona Kuwa Sipo eneo ambalo kila mtu alikuwepo.
“Abeeh “
Niliitika baada ya kufika.
“Unafanya nini uko jamani na sote tuko hapa “
“Nilikuwa naweka mazingira safi kwenye vyumba vya wageni “
“Ooooh Sawa si umemaliza lakini ??”
“Ndio “
Basi mama Yule akaamua kufanya Utambulisho kidogo kwani Mimi sikuwa nikiwajua wageni hao waliofika.
“WiFi huyu ni dada yetu Mpya ako na six months tangu aje hapa anaitwa EŞME , Eşme, huyu ni WiFi yangu Yaani ni dad wa baba yenu huyu, na huyu ni kijaana wake anaitwa SKYLER”
KWa sauti ya aibu uku Nikiangalia chini nikajibu.
“Nashukuru Kuwafahamu na karibuni sana”
SKYLER akazungumza.
“Esme ni maana halisi ya black si beauty “
Mama Jace akatabasamu na kujibu.
“You can say that again Eşme ni mrembo sana “
Mie sasa mbichwa umekuwa mkubwa Kama kichwa cha fuso 😂🙌, muda huo nilikuwa natamani ata kumuuliza Jace Kama anazisikia hizi sifa ninazopatiwa.
KWa pamoja tukaungana kwenye meza ya chakula, na siku hiyo ata Juma tulikuwa nae maana Mara nyingi amekuwa akila uko uko nje.
Muda wote huo skyler amekuwa ni mtu wa kuniangalia sana mpaka nikawa naona aibu jamani.
Mimi ni mtu ambaye napenda sana kula Yaani kwenye mambo ya misosi uwa sijivungi ata kidogo lakini Sijui hiyo nilikuwa wa kwanza kunyanyuka mezani tena nikiwa sijamaliza chakula nilichopakua hii yote ni kwajili ya aibu tu.
Baada ya muda kila
Mtu alimaliza kula na Mimi nikaanza kusafisha meza, kitu cha ajabu na cha kushangaza Skyler akanyanyuka na kuanza kunisaiiida kupeleka vitu jikoni.
“Sky baba ungepumzike tu Eşme atafanya “
Mama Jace alimwambia sky, lakini mama sky akadakia.
“Wacha amsaidie “
Muda huo huo Jace nae akanyanyuka na kuanza kusaidia, kitendo iki kilimshtua kila
Mtu Yaani 😂🙌 Jace ni Yule mtu ambaye anaweza akala na sahani yake asiitoe akasubili mimi Nije kutoa hivyo hii ya Leo ni gafla sana na lilimshangaza kila
Mtu.
“Una ngozi nzuri sana kwakweli “
Alizungumza sky, muda huo Mimi na yeye tulikuwa jikoni akitaka kunisaidia kuosha na vyombo kabisa.
Muda huo huo Jace akaja na kuzungumza..
“Sky unaitwa sebuleni “
Sky akaondoka nikabaki na Jace sasa.
“Chizi huyu ujue “
Jace Alizungumza nikageuka na kumuuliza.
“Unaongea kuhusu nini ??”
“Naongea kuhusu SKYLER ni Chizi, Yaani mwezi mchanga huyu, mwaka mzima alikuwa uko milembe ndio Ametoka baada ya hali yake kuimalika Kwahiyo usimuamini “
Ila jace jamani, sasa ananiambia yote haya mimi ya nini lakini, nikamjibu kWa kiufupi tu.
“Sawa “
“Sio tu Sawa Kaa nae mbali atakuja kukuzulu bure maana vikimpanda weeeh ni kasheshe kubwa”
“Sawa Jace “
“We Sema Sawa, kwanza acha kunchekea Chelsea hivyo maana nakuona tu”
Walahi nilijikuta nikaingua kicheko cha hali ya juu.
“Nakuchekesha si ndio ??”
Jace aliniuliza.
“Jace shida yako nini lakini Naomba Niache nifanye shughuli zangu nimechoka sana naitaji kupumzika pia”
Muda huo huo sky akaingia jikoni na kuzungumza.
“Haya niikusaidie kusuuuza vyombo sasa si ndio “
“Nikatabasamu na kutukisa kichwa ishara ya kukubali “
Gafla Jace akadakia.
“Sky unaweza kwenda kuoga na upate kupumzika ni Mimi ndio uwa namsaidia Eşme kusafisha vyombo “
Nyieeeh nilijikuta Nikiachia Mdomo maana Jace anajua kunionesha viola Walahi, eti mimi ndio uwa namsaidiaga tangu lini Leo ndio ukawa Mara ya pili, nilibaki nikimuangalia tu.
Pasi na kujivunga Jace akasogelea sink la vyombo na kuanza kuweka vizuri kwajili ya kunisaidia Mimi.
Sky hakuwa sababu ya kuendelea kubaki pale jikoni zaidi Akatoka nje na kwenda kwenye chumba chake ambacho alitakiwa kushare na Jace.
Tukiwa Tunaenda Lea kusafisha vyombo Jace akazungumza.
“Kwahiyo hapa umefurahi kuona nachezea maji ya mapovu usiku huu ??”
Nikamgeukia na kWa sauti ya kuchoshwa na mambo yake nikamjibu .
“Jace unaweza kwenda sijakuita hapa “
Jace akaishia kuniangalia tu mwisho huyo akaondoka zake na kuniacha nikiangaika peke yangu na vyombo.
******
Siku iliyofuata Kama kawaida jamani, niliamka na kuendelea kufanya shughuli zangu za pale za kila siku, siku hiyo Bwana nilikuwa. Nikisumbuliwa sana na tumbo, Yaani tumbo la kikubwa jamani.
KWa sababu hiyo, nilijikuta nikiwa nafanya kazi kWa uvivu sana uku nikiugulia tumbo langu.
KWa uwezo wa Mungu nikajitadii na kumaliza kazi zangu zote na mwisho nikaandaa kifungua kinywa cha familia nzima kwani siku hiyo kila mtu alikuwepo Nyumbani.
KWa pamoja familia ikaungana kwenye meza ya chakula nikiwemo na Mimi jamani hii familia haikuwa ikinitenga ata kidogo.
Kalma kawaida nilikuwa wa kwanza kumaliza chakula lakini pia tumbo lilikuwa likiniuma sana hivyo niliitaji kutoka kwenye eneo ilo.
Nilinyanyuka na kutembea hatua kadhaa tu, lakini gafla nikashtuka mtu akinikumbatia kWa Nyumba Tena kWa nguvu sana, na kwa muonekano wa mikono alikuwa ni mwanaume.
JE NI NANI AMENIKUMBATIA ? NA. KWANINI AMENIKUMBATIA ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO…..
ESME (just a maid ) 💃🥂
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 04
www.tupoahapa.com
SONGA NAYO…
Aliyenikumbatia jamani hakuwa mwingine Bali ni Skyler na kwa sauti ya chini sana akazungumza Karibu na sikio langu.
“Umechafuka sana nyuma so songa nikusaidie kufika chumbani kwako”
Walahi niliona aibu Sana imagine mbele ya familia nzima unachafuka kweli jamani.
Basi hivyo hivyo sky akiwa amenikumbatia nikaongoza kwenda chumbani kwangu na nilipofika tu nikamkabizi sky vyombo vyangu ambavyo nilikuwa nimeshika mkononi kisha akaondoka.
KWa upande wangu niliingia bafuni chapu, kwanza nikafua nguo yangu haraka kisha nikaoga na kujiweka Sawa, muda huo huo boss wangu akaja Yaani mama mzazi wa Jace na kuniuliza.
“Uko Sawa ??”
“Hapana maana, tumbo linanisumbua sana leo “
“Pole sana, nakuja “
Akazungumza hivyo kisha akaondoka.
Baada ya muda mama huyo akarudi akiwa na kikombe chenye maji moto yakiwa na baadhi ya viungo ambavyo vilifanya maji hayo kunukia sana lakini pia Kuwa na rangi ya tofauti sana.
“Kunywa hii ikiwa ya moto hivyo hivyo kisha ulale “
Basi nilipokea na mwana mama huyo akaondoka.
Kwakweli Sijui ata haya maji yalikuwa namchanganyiko gani lakini yalikuwa na ukakasi sana Tena sana, Walahi nilibaki nikinywa uku nimekunja sura.
KWa Namna moja au nyingine maji hayo yaliweza kunisaidi sana na maumivu ya tumbo yakaanza kupungua polepole na nikaweza kupata usingizi.
Walahi nilillaa sana mwenzenu, Yaani nililala usingizi mzito sana zaidi ya sana na hii yote ni kwaajili ya uchovu wa kazi za umu Ndani maana hii Nyumba kazi Zipo za kutosha na vile hakuna mtu ananisaidiaga ndio kabisa.
Nilikuja Kuamshwa na boss wangu Yaani mama Jace.
“Unajisikiaje ??”
Mama Jace aliniuliza baada ya kuniamsha.
“Vizuri kabisa maumivu yameisha “
“Mungu Mwema, haya jiweke Sawa uje ule uku “
Hapo jicho lilinitokana na kWa jazba nikavuta simu yangu na kuangalia Saa kwa mshtuko wa hali ya juu nikasema.
“Uwiiiiiiih Saa 9 kasoro “
Mama Jace akacheka na kuniambia.
“Fanya haraka”
Basi haraka nikanyanyuka na kuingia bafuni kwangu kwani chumbani changu pia kulikuwa na Choo chake, Yaani umu Ndani kila chumba Kina Choo Yaani ni raha tupu.
Baada ya muda nikawa niko tayali na nikaenda kuungana na kila
Mtu kwennye chakula, safari hii nilikuwa Sawa kabisa hivyo ata vyombo vya mchana niliweza kuosha.
Kwakuwa kila kitu kilikuwa powa nikatoka nje na kwenda kukaa na Juma maana huyu ndio Rafiki yangu Mara nyingi ndio mtu ambaye napiga nae story ingawaje Jace uwa apendi sana.
“Hivi huyu ndugu wa Jace ni mazungu au ??”
Juma aliniuliza, Nami nikamuuliza.
“Unamuongelea Nani sky au ??”
“Achana na huyo sky nawe Naongele huyu mgeni amekuja Jana, huyu mzuri kuliko ata huyo mwanamke”
Nikageuka na kujibu.
“Sasa si ndio sky huyo jamani”
“Majina ya watu wenye hela hayo “
“Acha mambo yako Bwana, Mbona ni Jina Kama majina mengine tu”
“Weeeeh Eşme usinichuze mwenzio, we tangu lini umekutana na Mtoto anaitwa Juma halafu ni Mtoto wa Tajiri? 😂🙌 Eşme staki mwenzio oooh, Sema tuache utani, huyu SIKAILA manyi sikai Sijui Nani Nani ashukuru ule mwili na kile kidali kikubwa na sauti nzito la sivyo eeeh Angekuwa Kama mwanamke kabisa”
Muda huo huo tukamuoka sky akitoka nje na safari yake ikaishia tulipokaa Mimi na Juma.
Kabla sky ajakaa muda huo huo akaja Jace akiwa na kibunda cha karata kisha akazungumza.
“Tuchezeni jamani “
Mimi na Juma tukaangaliana na mwisho tukaishia kuguna tu maana Jace sio mtu wa kuzungumza na sisi tena ameleta na karata kabisa, aaah hivi ni vioja kwakweli.
Basi kWa pamoja tukaanza kucheza pale na kwa Mara ya kwanza Leo ndio nimemuona Jace akiwa na mood nzuri sana, Yaani mood ile ya kumuona kila mtu ni Sawa maana Mara nyingi uwa anajiona yeye ndio yeye.
Tulicheza sana na mwisho Mimi nikanyanyuka na kuingia Ndani, moja kWa moja nikaenda chumbani kwangu na kuoga, nikajiweka Sawa kisha nikanyoosha njia na kwenda zangu jikoni kwani muda wa kuandaa chakula cha jioni ulifika.
Nikiwa bize naandaa chakula, boss wangu wa kike, Yaani mama jace, alikuja na kuniambia.
“Sikuwa Nimekuambia, sky tutakuwa nae hapa kwa sasa mpaka pale atakapojisikia kuondoka “
Nikajibu.
“Sawa madam “
“Haya naona mnainjoy uwepo wake, sky ni Kijana Mwenye upendo sana hakikisheni anakuwa na amani hapa maana
Uko alikotoka amelelewa
KWa upendo sana”
“Kwahiyo ni kweli alikuwa milembe ?”
Nilijiuliza tu kimoyomoyo sikuweza kuuliza kWa sauti.
*******
Hatimaye week Tatu zilipita tangu mama sky aondoke pale Nyumbani na kumuacha Kijana wake, Walahi huyu sky ni zaidi ya mwanaume, ni Kijana ambaye anaupendo wa hali ya juu.
Lakini pia sky hakuwa mtu wa kushinda Nyumbani kwani alikuwa akifanya kazi Sijui kwenye kampuni gani uko mi Sijui, Mara nyingi amekuwa akitoka pale Nyumbani asubuhi na kurudi jioni na Mara nyingi amekuwa akiniletea zawadi ndogo ndogo.
Ikiwa ni siku ya jumatano, siku hiyo Jace alirudi Nyumbani akiwa na Rafiki zake lakini pia na mwanamke wake ambaye alijulikana Kama happy.
KWa bashasha nikawapokea na kuwaandalia juice na biscuits, kisha nikamuita Jace jikoni na kumuuliza.
“Niwaandalie nini ??”
Jace akaniangalia kisha akazungumza.
“Kumbe muda mwingine unakuwaga na akili eeeh, nikajua utapika unachokitaka wewe”
“Niambie mtakula nini ili niwaandalie “
Basi Jace akaniambia pale kisha nikawaandalia chakula na kwenda Kuwatengea mezani , mmoja kati ya marafiki wa Jace akazungumza.
“Da mzuri ungana na sisi mezani “
Kabla sijajibu Jace akadakia.
“Ameshakula hiki ni kwajili yetu si ndio house helper ?”
Siku zote Jace amekuwa akiniita Jina langu lakini Leo hii ananiita Mdada wa kazi kweli jamani 🥹 Sijui ata huyu kaka nilimkoseaga nini maana sio kWa hii Chuki Walahi.
Sikuwa na neno la kuzungumza zaidi nikaanza kwenda chumbani kwangu, muda huo huo sky akaingia na kwa furaha na haraka sana akazungumza.
“Eşme jiandae tunatoka Mara moja “
Nikageuka na kumuangalia maana ni Kama sijamuelewa hivi Jace akadakia.
“Unaenda nae wapi ? Ata hivyo mama ajawai kumruhusu Eşme kutoka umu Ndani muda Kama huu “
Sky akamsogelea Jace kisha akamshika bega na kWa utulivu akazungumza.
“Antie anajua Nilimwambia tangu juzi Kuwa Leo nitatoka na Eşme na sasa hivi nimetoka kuwasiliana nae wako njiani wanarudi so kila kitu kiko Sawa “
Nyieeeeh nilifurahi sana haraka nikakimbilia chumbani kwangu na kwenda kujiandaa si mnajua Tena mambo ya mitoko.
Moja kWa moja nikaingia bafuni na kuoga, ile natoka tu bafuni nikakutana na Jace akiwa amekaa kitandani kwangu kisha akaniuliza.
“Hivi wewe ujuagi kusema hapana ??”
Nilimuangalia na kumwambia.
“Naomba unipishe nivae”
Jace akanyanyuka na kunisogelea akiwa na hasira sana kisha akanivuta taulo yangu na kunifanya nibaki mtupu kisha akaniuliza.
“Kipi sikijui kwenye huu mwili wa starehe ??”
Ila Jace Ana dharau jamani Kwahiyo mwili wangu ni wa starehe 🥹💔, nilijikuta nikiangalia chini uku nikitamani kulia, Yaani Jace alinijengea mazingira ya kunifanya Nijione Kuwa sina thamani kabisa.
Muda huo huo mlango wangu uligonjwa na sauti ya Sky ikasikika.
“Eşme samahani njoo uchukue nguo ya kuvaa”
Jace akaniangalia na kuniambia kWa sauti ya chini sana.
“Mwambie siendi”
KWa upande wa sky baada ya kuona Kuwa Nipo kimya akafungua mlango na kuingia, sky alishtuka sana baada ya kukuta nikiwa mtupu kabisa lakini pia taulo yangu ipo mikononi Mwa Jace.
Sky aka……
IKI NI KISANGA MY ZANGU MNIOMBEE.
ESME (just a maid ) 💃🥂
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 05
www.tupoahapa.com
SONGA NAYO…
Sky akaweka nguo aliyokuja nayo kitandani kwangu kisha akamsogelea Jace ambaye alikuwa na wasiwasi sana kWa wakati huo, polepole sky akachukua taulo na kunipatia kisha akamrudia Jace na kumwambia.
“Potea”
KWa haraka Jace akatoka nje, Walahi sikuwai kumuona Jace akiwa na wasiwasi kiasi iko lakini Leo hii Nimeona hadi akitetemeka kabisa.
KWa upande wangu nilijikuta nikilia tu maana sio kWa aibu hii lakini pia niliwaza sky atanichukuliaje.
“Samahani nimeingia chumbani kwako bila ruhusa “
Alizungumza sky.
KWa upande wangu sikuweza ata kujibu Yaani maneno yaligoma kabisa kutoka kwenye kinywa changu.
“Niligonga mlango kwa muda lakini ukujibu hivyo niliwaza Kuwa Utakuwa bafuni hivyo nikaona sio mbaya Kama nikaingia na kukuwekea hii nguo tu am so sorry Eşme”
“Ni Sawa “
Nilijibu kwa sauti ya chini sana.
“Vaa then nywele tutaenda kutengeneza kwenye saloon ya karibuni “
“Sawa “
Basi sky akatoka nje na kuniacha nikiwa Mwenyewe.
Nikashusha Pumzi Ndefu sana kukaa chini maana sio kwa mzaliliko huu, kwa Jace Sawa ameshazoea kuona mwili wangu Ila sky jamani uwiiiih na vile Tunaheshimiana sana ndio kabisa.
Basi nikavaa pale Walahi Gauni ilinipendeza sana Tena sana na ukizingatia na ki shape changu kidogo cha uchokozi ndio kabisa nikajikuta nikijiangalia tu kwenye kioo.
Upande wa viatu sasa ni huzuni tupu 😂🙌 Gauni zuri refu lakini viatu ni hizi mosimo 😂 Gauni liliitaji sana viatu virefu lakini ndio hivyo Tena 😀 Sina viatu virefu na ukiachana Kuwa sina viatu virefu pia Sijui ata jinsi ya kutembelea hivyo viatu 😂👌.
Baada ya muda nilitoka nje uku nikishikilia Gauni yangu ambayo ilikuwa ikubuluza chini.
Nilifika sebuleni na kukutana na madam ambaye Sijui alirudi Saa ngapi kutoka Kazini, lakini pia sky na Jace pia wallikuwepo, kWa upande wa Rafiki zake Jace kwakweli Sijui ata waliondoka saa ngapi maana sikuwakuta pale sebuleni.
“Niko tayali “
Nilizungumza uku nikitabasamu maana najua kabisa nimependeza.
“Hizo nywele vipi ??”
Madam aliniuliza.
“Aaaah usijali auntie, tutapita saloon ataweka Sawa maana tuna muda kidogo “
Alijibu sky.
“Haya party njema wanangu, sky Kuwa makini na Eşmea ajazoea hayo mambo ujue “
“Hakuna shida auntie “
Nikamgeukia madam na kumuaga kisha sky akashika Gauni yangu na Kunisaidia kutoka nje uku Jace akitushangaa tu.
Moja kWa moja tukapanda kwenye ndinga moja Kali sana, ndinga ambayo sky aliachiwa na mama yake.
“Tunaenda wapi kwani ??”
Nilimuuliza sky tukiwa kwenye gari.
“Tulia mama au unahisi naenda kukuchuna ngozi uku ??”
Nikacheka na kujibu.
“Hapana jamani nilitaka tu kujua si unajua Tena”
“Usijali Tunaenda kuinjoy tu”
“Sawa”
Moja kWa moja tukaingia saloon nikatengeneza nywele kutokana na maelezo ambayo alitoa sky na kweli nilipendeza gafla sky akazungumza.
“Tunaomba na simple make up, lazima mrembo wangu aonekane wa tofauti Leo “
Nikabaki nikitabasamu tu na kuna Namna Fulani nilijiona special sio Kama nikiwa na Jace.
Baada ya muda Walahi nilibadilika na Kuwa mrembo zaidi, muda wote huo sky alikuwa akinitazama na Kutasamu, Walahi kumbe Mimi ni mrembo ni vile tu Sina matunzo.
Sky akalipia ghalama zote kisha Mimi na yeye tukaondoka, tukiwa njiani kuelekea sehemu husika, muda huo Giza lilishaingia ilikuwa Kama Saa moja moja hivi, sky akaniuliza.
“Unaweza Kuwa girlfriend wangu kwa Leo tu ?”
Ka moyo kwanza kakafanya paaah kisha nikamuuliza.
“Unamaanisha nini ?”
“Ouk iko hivi, uku tunakoenda ni kuna party kubwa sana ni ya marafiki zangu ambao nilisomaga nao chuo, sisi uwa Tuna utaratibu ule wa kukutana kila mwaka na Kuwa na party fupi tu kwaajili ya kudumisha ukaribu wetu na ilo tumeweza kwakweli, shida iliyokuwepo ni kwamba, nilikuwa na girlfriend lakini tumeachana na amweshavikwa Pete na mtu mwingine, sio kwamba bado nampenda hapana maana ameniumiza sana, kitu nataka ni kwamba asinichukulie kinyonge “
Nikacheka na kumuuliza.
“Kwahiyo unaona aibu akikuona Kuwa hauna mwanamke ??”
“Yaaaah ata hivyo nitapooza sana sana maan uku kila mtu na wake Yaani, na sijawai kusherehekea hii siku nikiwa Mwenyewe, so please nakuomba sana snaa be my girl kwa Leo tu na Ukitaka nikulipe nitakulipa “
Nikatabasamu na kujibu.
“Usijali wewe ni Rafiki yangu na marafiki ni kawaida kusaidiana nitakusaidia, Ila hakikisha unanilinda nisije nikapigwa chupa Mtoto wa baba EŞME “
Sky akaniangalia na kuniuliza.
“Kwanini Mtoto wa baba Eşme na sio Mtoto wa mama Eşme au ndio Mtoto wa kike na baba yake 😀”
“Sasa je “
Nilijibu tu lakini kuna Namna niliumia rest in peace mama 😭💔.
Hatimaye tukafika eneo husika nyie kwenye hotel uwiiiiih mambo ya kudhalilika uku sijawai kufika kwenye sehemu Kama hizi 😂 mniombee maana kila kitu ni jipya kwangu.
Tukashuka na sky akasogea Karibu yangu na kuweka mkono wake akitaka na Mimi nimshike, Ila Bwana ni Kama mwalimu wangu bubu halafu somo İMLA, sikuelewa kabisa nikabaki nikimtumbulia macho.
“Nishike Bwana your my babe now “
Sky aliniambia na hapo ndio nikaelewa na tukashikana na kuanza kuingia Ndani.
“Sky nishike kwanguvu Mbona Kama nataka kuanguka”
Nilimwambia sky kWa sauti ya chini sana nisije nikatia aibu.
“Eşme please usinichekeshe Sawa, sasa uanguke kisa nini “
“Miguu inatetemeka lakini pia nahisi nateleza mwenzio na hivi viatu”
Sky akasimama na pasi na kuzungumza kitu akanibeba Kama watu wanavyobeba wapenzi wao, nyieeeeeh kumbe Watu wanaopendana ndio wanakuwaga hivi au ni ushamba unanisumbua ??
Moja kWa moja tukapanda lift kwani ukumbi ulikuwa juu uko, muda wote nilikuwa nikimtizama sky tu usoni nyie huyu kaka mzuri jamani uwiiiiih, Mungu nipe huyu sitamchiti 😂👌.
Hatimaye tukafika sehemu husika na kipaza sauti kikasikika.
“Anayeingia sasa ni SKYLER the big boss”
Uwiiiiiih huu moyo Sijui unataka kuchomoka mwaya maana sio kWa kudunda uku, muda huo macho ya watu wote yalikuwa kwetu, lakini pia sky bado alikuwa amenibeba nikamwambia.
“Nishushe”
“Tulia wewe “
Alijibu sky kisha akanikiss kwenye paji la uso.
“Sky nitazimia ujue “
Nilimwambia.
Sikuwai kujua Kuwa sky ni mtu wa misifa baada ya kumwambia hivyo akanikiss mdomoni kabisa, nyieee nilijikuta nikifulukuta Kama samaki aliyetolewa kwenye maji na pasi na kutalajia nikaanguka chini Kama Mzigo.
NAZALILIKA MWENZENU HUYU KAKA AMESHINDWA KUNISHIKA KWA NGUVU 😂👌
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote