Follow Channel

EVAN (kaka mpishi) 💙

book cover og

Utangulizi

EVAN (kaka mpishi) 💙
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 01

www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

Ila nyie maisha ya chuo yanaitaji moyo sana kwakweli Yaani sana aswaah Aswa ukiwa hauna hela, maisha ya chuo yamejawa na ushawishi mwingi sana ambao Mara nyingi upoteza sana ma Binti na wakati mwingine ata vijana wa kiume.

Niite ZANELE ingawa wengi wamezoea kuniita ZAN ikiwa ni kifupi cha zanele, Mimi nimezaliwa
Mkoani kigoma uko sehemu Fulani hivi Wanapaita kasuru.

Me ni mrembo Tena mrembo aswaah, kwanza ni mna nywele Ndefu na nyingi sana, ikirudi upande mwingine Mimi weusi niliukataa kwakweli hivyo nilikuwa na Karangi kangu Kazuri tu, Ka rangi Fulani hivi ambapo Kama napata matunzo mazuri Basi nang’aa sana.

Maisha yangu yote Nimekulia Kigoma uko, Yaani kila kitu nimefanya kigoma sijui kusoma na kila kitu.

Kwa kudra za Mwenyezi Mungu nikafanikiwa kumaliza kidato cha Sita na niliweza kupata chuo dar es salama, mimi Bwana niliamua kusomea biashara na nilienda kusoma chuo cha ustawi wa Jamii kilichopo dar es salama Bamaga.

Kwakuwa dar es salama mimi ni mgeni, wazazi wangu walinilipia hostel ambayo ipo Ndani umo umo kWa chuo na maisha ya chuo yanasonga, ukiachana na bum wazazi wangu wanajitadi sana kuhakikisha Kuwa napata Pesa kWa wakati na hii walikuwa wakifanya ili tu kuniepusha na tamaa za hapa na pale si unajua Tena.

Anyway kWa sasa Nina miezi miwili hapa chuoni na nimeshazoea mazingira Mimi sio mgeni Tena jamani, kitu ambacho kinaweza kukufanya kujua Kuwa Mimi ni muha ni rafudhi yangu tu maana najua kukaza Maneno jamani 😂 kuna muda mpaka naona aibu.

KWa kipindi iko room mate wangu ndio walikuwa marafiki zangu aswaah aswaah, kwenye chumba chumba chetu tulikuwa wasichana watatu na tulipendana sana zaidi ya sana kwakweli.

Ikiwa ni siku ya jumatatu Majila ya jioni nikiwa nimetoka kuoga, akaja shoga yangu Joyce, huyu ni mmoja kati ya room mate wangu wawili, Joyce alikuja kwa bashasha nakuniuliza.

“Hivi leo ulitoka uko nje shoga Angu ? “

Nikamuangalia na kumjibu, Sijatoka si unajua Nipo kwenye mfungo Kwahiyo sikuwa na sababu ya kwenda nje maana nafataga chakula tu kuna nini kwani ??”

“Eeeh kuna mgahawa Mpya shoga Angu halafu mpishi ni mwanaume wewe, likaka lizuri ilo jamani unabaki unamuangalia mara Mbili Mbili”

Ila Joyce na Wakaka wazuri uwiiiih, Yaani shoga Angu huyu anapenda sana Wakaka wazuri lakini mpaka awe na hela Ila ukiwa mzuri halafu hauna hela Wala ana Muda na wewe anabaki kusifia pembeni tu.

“Na Cecy yuko wapi kwani ??”

Nilimuuliza Joyce maana nje akitoka akiwa na Cecy halafu Ndani Karudi Mwenyewe.

“Nimemuacha nje uko ameniambia Nije kukuita tukale pale pale”

“Hakuna shida wacha Basi nisali kidogo then nakuja “

“Eeeeh wewe Tena mama mchungaji haya me natangulia utatupigia simu tukuambie tulipo “


“Hakuna shida”

Basi ZANELE wa watu nikavaa pale kisha nikaanza kusali, mpaka namaliza kusali muda wa kufungulia ulikuwa umeshafika hivyo nikatoka nje na kwenda kuungana na wenzangu.

Moja kWa moja nikiwa na shoga zangu tukaenda kwenye mgahawa Mpya, nyieeeeeeh huyu kaka jamani 🥹 sijawai kumtamani mwanaume lakini huyu kaweza halafu kaweza Tena nyie 🥹 nilijikuta nikiganda na kumuangalia kwa kurudia rudiia.

Muda huo mkaka wa watu alikuwa bize kukaribisha wateja ambao walikuwa wakiingia ikiwemo na sisi.

“Karibuni sana jamani, karibuni mkae”

Nyieeeeh hivi hizi ndio hisia au umalaya tu Mbona nimeanza kumuwazia mbali mkaka wa watu, uwiiiih mfungo wangu Unaharibika sasa.

“Zan, zan “

Cey aliniita mfululizo lakini sikuweza ata kumsikia nilikuwa nikimuangalia tu kaka mpishi.

“We ZANELE “

Hapo Niliitwa kwa sauti ya juu kabisa lakini pia nilishikwa Na bega ndio nikashtuka la sivyo 😂🙌 nisingestuka.
“Mwenzetu vipi ??”

Cecy aliniuliza.

“Aaah, eeeh, am aaaah, amna kitu, kwani kipindi kimeanza ??”

Nilijikuta nikiuliza vitu ambavyo ata Mimi sivielewi kwakweli 😂🙌 mtu Nipo mgahawani na naulizia Mambo ya vipindi hii ni nini my zangu mniwai kabla sijapotea.

“Makubwa Leo, swaumu Kali Sana au ? “

Joyce aliniuliza.

“Amna “

“Sasa amna nini na wewe, Yaani mkaka wa watu anakutajia vyakula vilivyopo mwenzetu umeganda una smile tu Kama Chizi kaona ndugu zake”

“Aaah kuna chakula
Gani kwani ??”

Niliuliza maana sikuwa nimesikia ata kitu kimoja wakati anataja.

“Eeeeh mashokolo mageni mwaya, kaka Angu huyu njaa imemzidia yuko kwenye mfungo mvumilie tu”

Cecy alimwambia mkaka huyo ambaye aliishia kutabasamu tu.

“Aaah kuna chapati na maharage, kuna tambi namayai, wali nyama na mahaarage na ugali na Mbona saba”

Eeeeeh napotea sasa mwenzenu, hii base yake ya sauti ndio inanimaliza Mtoto wa mwenzenu uwiiiih si Nimekuja kusoma Mimi.

Basi tukaagiza chakula tulichoitaji na mkaka wa watu akaenda kutuhudumia kwani alikuwa Mwenyewe na hakuwa na msadizi.

Tukiwa bize tunasubili chakula Joyce akaniuliza.

“We mwenzetu vipi jamani Mbona kama hauko Sawa umepatwa na nini ??”

Kabla sijajibu Cecy akadakia.

“Amepatwa na nini kuhusu nini nawe, hivi kusoma ujui ata Picha uoni kweli, muangalie macho yake anavyomtazama huyo mpishi, naona shoga anataka kula chakula na mpishi “

Ila katika marafiki zangu Cecy ni mwendo kasi, Yaani Cecy akili yake anaijua Mwenyewe 😂🙌 ni shwaaaah Wala anaga muda wa kufikilia Mara Mbili.

KWa aibu nikazungumza.

“Cecy ni nini lakini eeeh, me niko na mawazo yangu tu Wala siko
Uko unakowazia wewe “

“Thubutu yako Unafikili wote ni watoto wa kigoma eti ? Shoga Angu me Mtoto wa mjini najua A mpaka Z, Sawa wewe ni mamma mchungaji dini imekukaa lakini pia wewe ni binadamu hisia Zipo shoga yangu na Leo nimeziona usifanye watu watoto wadogo hapa “

Eeeeh Cecy sio mtu wa kubishana nae kabisa maana anaweza akakutia aibu kabisa, Yaani muda huo ananichamba hivyo sio kwamba ni sisi tu ndio tulikuwepo hapana, kulikuwa na wasichana wengine ambao nao walikuja kula na walikuwa tayali wameshahudumiwa.

Baada ya muda chakula Chetu kikaletwa na tukaanza kula.

“Sijui yeye amekula mwaya maana. Anaonekana amechoka sana “

Nilijiuliza kimoyomoyo uku nikimuangalia mkaka wa watu ambaye alikuwa bize na kusafisha vyombo.

Hakuna siku nilikula polepole Kama siku hii jamani, Yaani unakula chakula akiishi ni unagusa gusa tu mpaka wenzangu wakabaki wakinishangaa na kunicheka.

Hatimaye tulimaliza kula na pasi na kutalajia, nikajikuta nikisimama na kuanza kukusanya vyombo vya watu wote ambao walikuwa wamemaliza kula.

“Makubwa Leo disko Kaingia muha Leo 😂🙌 we mwenzetu hivyo vyombo unapeleka wapi jamani ??”

Joyce aliniuliza, uwiiiiih hapo ndio Kama akili zangu zikarudi nikajikuta nikiuliza kWa sauti.

“Kwani ni Mimi ndio nimekusanya ??”

“Hapana ni mizimu ya Nyumbani kwenu , Ebu weka chini tulipe tuondoke uko “

Basi nikaweka vyombo chini na kumlipa kisha nikaondoka.

Tukiwa njiani kuelekea hostel, nilikuwa nikiongea kimoyomoyo lakini gafla nikajikuta Nilizungumza kWa sauti.

“Ila anatilia huruma sana anachoka mwaya “

Joyce na Cecy wakajigeuki na kuniuliza.

“Unaongea kuhusu nini kwani ?”
Hapo ndi nikashtuka Kuwa Nilizungumza kWa sauti, nikajibalaguza kWa kujichekesha na kusema.

“Naimba Bwana “

“Hapo Sawa, Ila twendeni mbele turudi nyuma Evan ni mzuri sana, Yaani yooooh bonge la handsome “

Alizungumza Cecy na Mimi haraka nikamuuliza.

“Evan ndio Nani Tena ? Kuna mada ilinipita nini ??”

“Eeeh leo ma mtumishi Sijui umepatwa na nini, Evan si ni Yule mkaka mpishi jamani, yani kwani ujaona kibao chake kimeandikwa EVAN DELICIOUS FOOD “

“Ata sikuAngalia kabisa”

“Ndio hivyo anaitwa Evan, anafaa kWa matumizi ila anaonekana kabisa hana Pesa Yule kaka jamani “

Alizungumza Joyce Mpenda Pesa.

Nikajikuta nikidakia
“Mapenzi sio Pesa “

Uwiiiiiih, iko hivi, Mimi ni mtu ambaye uwa sichangiagi mada ikiwa masuala ya wanaume Sijui mahusiano lakini hii ya Leo Kali my zangu naombeni mniombee.

NAKUJA……


EVAN (kaka mpishi) 💙
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 02

www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

Wenzangu walinishangaa sana maana mimi sio mtu wa kuchangia hizo mada, naweza kusema Kuwa Nimekuwa tofauti sana na jamii ya wasichana wa sasa hivi, Yaani Mimi ndio maana walikuwa wakiniita mama mchungaji 😂🙌.

Kwa pamoja tukarudi hostel na kubaki kusubilia muda wa kuingia darasani maana tulikuwa na kipindi cha mwisho ambacho ni Saa Mbili kamili usiku.

Hatimaye Saa Mbili ikafika na sote tukaelekea darasani.

Naomba Nikubali Kuwa katika siku ambazo sikuelewa lecture alikuwa akifundisha kitu gani Basi ni siku hii Walahi, Yaani kuna muda nilikuwa naona Kama lecture anapiga makelele, nilijitaidi sana kutuliza akili yangu ili kuweza kumuelewa lakini kaka mpishi ndio alikuwa akitawala kwenye ubongo wangu na moyo pia.

Baada ya muda nikanyanyuka na kutoka nje na moja kwa moja nikaenda chooni na kunawa usoni na kuamini Kuwa nitakuwa Sawa, nilivyotoka chooni BADALA ya kwenda darasani nikashika njia ya kwenda getini na mwisho kabisa nikatoka nje ya chuo na safari yangu ikaishia kwa kaka mpishi.

“Oooooh pole chakula kimeisha “

Alizungumza kaka mpishi baada ya kuniona kwani aliamini Kuwa nilifata chakula .

ZANELE Mimi nikatabasamu na kuzungumza.

“Ooooh nimechelewa”

Ila Mimi jamani si nilishakula lakini, Ila ukija kwenye ukweli sikuwa nimefata chakula Ila moyo wangu ulitamani sana kumuona kaka mpishi kWa Mara nyingine.

“Kesho nitapika cha kutosha maana Leo nilikuwa najaribu jaribu maana ni siku ya kwanza “

“Usijali lakini Hongera zako chakula chako kina Radha nzuri sana”

“Ooooh Asante sana”

Alijibu mkaka uyu uku akiendelea kuweka vitu vizuri ni wazi Kuwa alikuwa akijiandaa kufunga.

Macho yangu hayakutulia ata kidogo, nilibaki nikimuangalia tu mkaka wa watu.

“Nitakuja kuambiwa mchawi bure sasa nafanya nini hapa “

Nilijiuliza kimoyomoyo.

Akili na kila kitu kilinishawishi kuondoka lakini miguu yangu Ulikataa kabisa kunyanyuka na macho yangu hayakuchoka kumtazama mkaka huyo ambaye alijua kunikamata kWa siku ya kwanza kabisa.

My zangu Mimi sikuwai kuwa na mahusiano ata kidogo, Yaani Mimi ata mambo ya mchumba mchumba yalinipitaga kutokana na kusimamiwa sana na wazazi wangu, lakini pia nilishika sana dini na Mafunzo ya wazazi wangu, Ila huyu mkaka sasa ndio anataka kunibadilisha ZANELE wa watu sielewi kabisa, hivi hii ndio love at first sight au ni tamaa tu ??.

“Uko Mwenyewe ??”

Nilimuuliza mkaka huyo, kwanza mkaka wa watu alionesha kushtuka kisha akaacha Alichokuwa akifanya na kuniangalia na kunijibu.

“Kama unavyoniona na nimechoka sana naitaji kumalizana na kila kitu nikapate kupumzika “

Sauti yake ilionesha wazi Kuwa Amechukizwa na swali langu, lakini pia kuna Namna alianza kupata wasiwasi maana anijui halafu Nipo namuuliza iliza tu maswali yasiyokuwa na msingi.

Kuna muda na mimi nikajishtukia Kuwa namshobokea mno hivyo nikamuaga.

“Haya usiku Mwema wacha nikatafute chakula”

Niliondoka nikiwa na aibu ya hali ya juu, moja kWa Moja nikarudi tu hostel maana ata ningeenda darasani ningetoka patupu tu.

Majila ya Saa nne niliweza kusikia wenzangu wakiwa Wanaarudi kutoka darasani chap nikashuka kitandani na kupiga goti chini na kufanya Kuwa nilikuwa nikisali, kWa Mara ya nyingine Tena nafanya kitu cha kijinga mwenzenu.

Baada ya Kama dakika 10 hivi nikafungua macho yangu na kukuta Cecy na Joyce wananiangalia niangalia sana ni wazi Kuwa walikuwa wakisubili nimalize kusali.

“Ma mchungaji Leo vipi kwani ??”

Cecy aliniuliza.

“Kuna nini kwani ?”

Na Mimi nikauliza ingawa nilikuwa najua ni kitu gani anazungumzia.

“Hauko Sawa ma mchungaji Bwana, Yaani tangu Tumeenda kula tumerudi, halafu ili la kuondoka darasani ndio limenishangaza zaidi me nilizani Kuwa unaenda uwani na kurudi”

“Ooooh ni kweli siko Sawa Ila sio sana Bwana, nahisi mwili wangu Kuwa mzito sana ni Kama homa inaninyemelea hivi “

Niliwadanganya, daaahh kWa Mara nyingine nafanya kitu ambacho sijawai kufanya Mwenzenu 🥹 kwani nimepatwa na nini Mimi.

Sisi three dadaz tulikuwa tumejiwekea ratiba ya kusoma kila siku usiku lakini siku hii sikusoma kabisa kwa kisingizio cha Kuwa Naumwa.

********

Siku iliyofuata asubuhi na mapema niliamka na kuanza kuweka vitu Sawa nikasali pale kwani nilikuwa naendelea na mfungo wangu.

Baada ya kuweka kila kitu Sawa nikatoka moja moja mpaka kwenye mgahawa wa Evan, muda huo marafiki zangu walikuwa wametoka Mara moja.

“Karibu “

Evan alinikaribisha baada ya kuniona kwenye mgahawa wake.

“Asante, aaaah sijaja kwaajili ya chakula hivyo usinikaribishe sana Bwana 😂, Nimekuja kukusaidia tu vikazi kazi “

Kwnza Evan alishangaa na kuniuliza.

“Umekuja kunisaidia ??”

“Ndio kwani kuna ubaya ??”

“Ubaya upo Tena mkubwa tu, sikujui unijui halafu unataka tu kunisaidia how ?, ata hivyo Sina Pesa ya kulipia msaidizi “

“Nakusaidia bure tu, tangu Jana Nimeona ni kiasi gani unaangaika peke yako ndio maana Leo Nimekuja kukusaidia kwa muda huu ambao Sina kipindi darasani”

“Asante “

Alijibu na kuendelea na kazi yake, nilibaki nikishangaa uku nisijue ile Asante ni amekubali au ni kitu gani, kwakuwa kWa muda huo nilikuwa na ki here here sana nikamuuliza.

“Naweza kukusaidia kazi gani ??”

Kwa wakati huo kila mtu ambaye alikuwa akipata chakula alikuwa akiniangalia Mimi jinsi ambavyo najizalilisha kWa kaka mpishi 😂🙌 ila hii inawezekanaje jamani Mbona ni aibu kubwa lakini Nipo tu.

“Msichana siitaji msaidizi mie “

Hapo kaka mpishi Alijibu kwa hasira sana na sauti ya juu, Walahi nilipata aibu kubwa sana, Sijui ata nguvu nilitoka wapi lakini niliondoka kwa kukimbia hii naitwa hakuna kugeuka nyuma 😂🙌.

Nilifika chumbani na kukuta Rafiki zangu wakiwa wamesharudi.

“Ulikuwa unakimbizwa au ??”

Cecy aliniuliza maana nilikuwa nikihema haraka haraka lakini pia jasho lilikuwa likinitililika sana.

“Nimezalilika mwenzenu “

Nilizungumza maana niliona ni mambo yameanza kunielemea.

“Umeanguka mbele za watu au ??”

Joyce aliniuliza uku akikaa vizuri kunisikiliza.

“Bora ningeanguka, unajua sijawai kujihisi hivi ninavyojihisi sasa lakini nahisi nampenda sana Evan, Namaanisha huy kaka mpishi “

“Makubwa haya, weeeeh ma mtumishi wewe 😀 akhaaaaah hii nayo Kali, wewe unawajua Wakaka wazuri vizuri wewe ? 😀 kabla sijakujaji nikuulize umeenda kimtongoza au ?”

“Hapana”

Basi nikajikuta nikiwaelezea kila kitu, nilianza kuwaelezea tangu usiku nilivyotoka darasani na kumfata mpaka Leo hii nilipoenda kumsaidia kazi.

Rafiki zangu Wakaniangalia kisha wakacheka kWa pamoja.

“Eeeeeeeh mama mchungaji in love “

KWa hasira nikajikuta niki……

ITAENDELEA



EVAN (kaka mpishi) 💙
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 03

www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

Nilijikuta nikijitupia chini na kuangua kilio maana yoooh 😂🙌 mtu nimetoka zangu uko nimezalilika vya kutosha halafu unarudi kWa wenzio unawaelezea wanaanza kukucheka, kilio changu Wala akikuwashtua Rafiki zangu zaidi waliongeza sauti ya kunicheka.

Mwisho nikanyanyuka na kuwauliza.

“Kwahiyo amnibembelezi ??”

Wakacheka Tena kisha Cecy akanisogelea na Kujikumbatia na kuniambia.

“Lia, toa machungu yako yote halafu tukae chini tuanze kuzuungumza lugha moja maana uwezi kutuelewa kWa sasa “


Basi nililia sana nikiwa nimemkumbatia Cecy wangu, Ila huu ni ujinga jamani, sasa nalia nini, nikatoa kwa Cecy na kuzungumza.

“Ila Mimi ni mpuuzi ujue “

Joyce akadakia.

“Jipige na kakibao ata Ka moja kwanza 😂🙌, nilitaka kushangaa mama mchungaji anaangukiaje kwenye penzi la mpishi kwa mfano”

Ila sisi daaah, kWa pamoja tukakaa chini na Cecy akazungumza.

“Ata hivyo ma mchungaji uanze kubadilika Bwana “

Nikamuangalia na kumuuliza.

“Kubadilika nini ??”

“Muonekano tu, tabia yako Baki nayo hiyo hiyo maana sisi tumekupenda na utulivu wako na kila kitu, lakini uache kujichukulia powa shoga Angu, hizo nywele zako kila siku Unabana Kama jumong Walahi sijawai kupenda, mavazi yako Walahi sipendagi watu wanavyokusemaga”

Hapo nilijikuta nikipata huzuni maana watu wamekuwa wakiniseme sana juu ya mavazi yangu, Wakaka wengi unicheka lakini uwa napotezea.

KWa sauti ya huzuni nikawauliza.

“Sasa nitafanyaje ? Ukweli haupingiki Kuwa Mimi ni mashamba kwenye kila kitu”

“Ilo tuachie sisi bff Sawa, Kama ambavyo tulisema Kuwa sisi ni familia Basi tutafanya kwa uwezo wetu “

Nyieeeh Kama marafiki tu Basi nimepata, Yaani sisi ni watu ambao tuko serious sana na urafiki wetu ingawaje tumetofautiana tabia.

Majila ya Saa 8 mchana hekaheka za kujiandaa zilishia nafasi kwani tulikuwa na kipindi Saa 9.

KWa upande wangu Mimi ni Binti Mwenye aibu sana sana, wenzangu uwa Wanaoga kWa pamoja kabisa lakini Mimi sasa 😂🙌 siwezi ata kuvaa mbele Yao, Mara nyingi wamekuwa wakitoka nje na kuniacha Nivae.

Basi baada ya wenzangu kuoga na Mimi nikaingia bafuni na kuoga , nilipotoka Joyce akaniambia.

“Kaa kwanza nikubabe nywele then utavaa “

Nyieeeeh 🥰 hawa watu waananifanya Mimi kama last born wao hivi, Yaani Wananidekeza hatari, ata hivyo Mimi ndio Mdogo kwenye kikundi.

Basi nikakaa chini na Joyce akaanza kunitengeneza nywele zangu, kWa Mara ya kwanza Walahi nilivutiwa na muonekano Mpya wa nywele zangu nyie, ukizingatia Kuwa Nina nywele Ndefu sana Basi weeeh 😻.

“We Joyce wewe umejulia wapi haya mambo ?”

Nilimuuliza.

“Upande wa urembo na nywele Mimi niko powa sana, mama yangu anamiliki saloon na Nimekuwa nikimsaidia tangu utoto wangu “

“Asante bff “

KWa pamoja Cecy na Joyce wakatoka nje na kuniacha nivae sasa, kWa upande wangu nguo pia ni wao waliniandalia na zilikuwa Mpya kabisa, Rafiki zangu wanajua kabisa Kuwa sijawai kuvaa nguo fupi Wala Suruali hivyo waliniwekea mavazi ambayo Mimi niliyazoea lakini yalikuwa ni ya kisasa zaidi, nyieeeeh nilipendeza sana mpaka nikawa siamini kama ni Mimi ndio Nina muonekano mzuri kiasi iko.

Nilitoka nje nikiwa na tabasamu la kutosha.

“Weeeh ma mchungaji weeeh, aaah shoga Angu uwa unaficha mambo Mengi Walahi, umependeza babe “

Cecy alinisifia baada ya Mimi kutoka nje.

Joyce akadakia

“na hii shape sasa uwiiiih 🥰 ma mchungaji mitano Tena”

Basi tukashika njia na kwenda darasani nyieeeh, kwa Mara ya kwanza niliona Kuwa watu wananiangalia sana sana, Yaani hii sio kwa wanaume Wala wanawake yaani kila mtu alikuwa akiniangalia.

“Umependeza “

Mmoja kati ya wasichana wa darasani alinisifia ni wazi Kuwa alishindwa kujizuia.

“Thanks “

Aghaaaaah nimejibu kWa kingereza 😀ila mchawi ni hii rafudhi ya kigoma 😂.

Hatimaye lecture ikaanza pale na ilipoisha nikawai kwenda hostel kwajili ya kusali kwani muda wa kufungulia ulikuwa umewadia.

Nilisali na nilipomaliza nikaungana na Rafiki zangu na safari ya kwenda kupata chakula ikaanza, tulipokaribia kwenye Kibanda cha kaka mpishi nikasimama na Kuwaambia.

“Nendeni tu mie Pesa yangu hii hapa mtaniletea chakula Ndani “

KWa pamoja Wakaniuliza.

“Kisa nini ??”

“Naona aibu aiseeeh Sijui mkaka wa watu namuangaliaje jamani “

“Basi tubadilishe sehemu ya kula tu kwani ni peke yake ndio anauza chakula au “

Kama kawaida mzee wa kukurupuka akaja na majibu, Yaani hapa namuongelea Joyce.

Nikajifikilia mwisho nikakubali tu kwenda kwa kaka mpishi maana ujinga wangu mimi usimkoseshe Pesa mkaka wa watu.

“Au Basi twendeni “

Walahi nilijikaza sana ingawa nilikuwa na wasiwasi Sana.

Tulifika na Kama kawaida mkaka Yule akatukaribisha, safari hii Bwana ni kaka mpishi ndio alikuwa ananiangalia mimi mara Mbili Mbili 😀 Yaani kuna Namna alikuwa anashindwa kuamini Kama ndio Mimi.

KWa upande wangu nilikuwa serious sana kwakuwa naijua menu nikamwambia na kutulia nikisubili anihudumie.

Siku hii Bwana Mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumaliza kula, sikutaka kuendelea kukaa hapo nikanyanyuka na kuwaambia wenzangu.

“Mtanikuta hostel Basi “

“Powa “

Huyo nikatoka na kuondoka pasi na kugeuka nyuma nikaondoka.

İle nafika kwenye mlango mkubwa wa hostel nikakutana na wasichana Wapatao watatu, ambao nilipotaka Kuwapita mmoja akaniuliza.

“We muha, Cecy yuko wapi ??”

😂🙌 Ila watu ni wakorofi jamani kwani Muha ni Jina langu au ? Kwakuwa mimi sio mtu wa ukorofi nikasimama na kuuliza.

“Mnashida nae gani ??”

Mmoja kati ya wasichana hao akaniuliza.

“Na wewe ni chawa wake au? Umeulizwa swali jibu swali na sio kuuliza maswali Binti Sawa? Cecy yuko wapi??”

Nikaona hawa nao ni wanataka kunizoea nikajibu.

“Sijui “

“Eeeeh nyie muoneni huyu muha ananijibu mimi kwa dharau, Binti unanijua au unataka kunizoea ??”

Kabla sijajibu Cecy na Joyce wakafika na wote wakamsogelea Cecy na wakamuuliza.

“Wewe ndio unajilengesha kwa kaka mpishi si ndio ??”

Kaulizwa Cecy lakini Mimi uku presha ni inapanda 😂🙌.

NAKUJA MY ZANGU.


EVAN (kaka mpishi) 💙
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 04

www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

Miguu yangu ilianza kutetemeka kwa wasiwasi maana najua kabisa hawa watu ni wananitafuta Mimi na sio Cecy maana Cecy hana muda wowote ule na kaka Mpishi.

Cecy ni msichana Fulani hivi ambaye anampokea mtu kutokana na jinsi alivyokuja.

KWa sauti ya ukali Cecy akawauliza.

“Mnaniuliza au mnanipa taarifa??”

“Oooooh naona kiburi kimekujaa Binti, we unamjua Evan vizuri wewe ? Anyway usije ukamjua jua sana mwanaume wangu Sawa ? Evan ni wa kwangu na atabaki Kuwa wangu tu hapa nyie wengine wote mnaliwa, mnachezewa halafu mnaachwa “

Kwanza nilishtuka na kushangaa, yani huyu Evan ndio kwanza Ana siku ya pili tangu aanze kuuza chakula sana hizi tayali ako na mwanamke ? 😂😂 dunia yetu hii Mbona mambo yanaenda kasi sana.

“We nawe Nitokee hapo, Yaani huyu huyu Mnuka moshi ndio Anakufanya unipigie Kelele, msichana sikujui, unijui usinipande kichwani Sawa ? Hao waliokuelekeza kwangu hawakukueleza ni mtu wa aina gani unamfata kawaulize vizuri “

Alijibu Cecy muda huo Cecy alikuwa ameshachukia vya kutosha, kWa situation hiyo nikaona hawa watu wanaweza wakapigana halafu Msala ukawa mkubwa, nikamsogelea Cecy na kumshika mkono moja kWa moja nikampekea chumbani.

“Ma mchungaji nae ungeniacha niwaoneshe mimi ni mtu wa aina gani maana wanakuja kichwa kichwa tu”

Muda huo huo Joyce akaingia na kusema.

“Wameshaondoka”

Nikashusha pumzi Ndefu na kukaa kitandani nikazungumza.

“Ni wazi Kuwa wananitafuta Mimi “

“Ma mchungaji tuliaga nawe haya mambo tuachie sisi “

Alizungumza Cecy, kisha joy akazungumza.

“Hakuna cha kutuachia sisi, ZANELE umeona sehemu unayotaka kuingia ? Umeona mwanaume ambaye wewe unamtaka ? Kama Umependa kweli hizi drama utatakiwa kuzimudu, sisi Leo tupo kesho hatupo lazima ujue kujitetea “

Sikuwa ata na cha kuzungumza maana haya mambo sio mambo yangu kabisa nilibaki nikipumua tu Kama sina akili nzuri.

********

Siku zilikimbia sana na hatimaye week Mbili zilikatiza uku nikiwa bize sana, Walahi nilizidi kupendeza kila siku na Kuwa mtu wa tofauti, Walahi niling’aa.

Sawa moyo wangu ulimpenda sana kaka mpishi lakini niliamua kukaa mbali nae ili kujiepushia aibu za hapa na pale, lakini ukiachana na hivyo kaka mpishi hakuonesha Kuwa interested na Mimi ata kidogo hivyo niliona ni vyema nikaishi maisha yangu.

Ukiachana na kaka mpishi sasa, nikaanza kupata usumbufu kutoka kwa Wakaka wengine, Yaani wale waliokuwa wakinicheka sasa
Hivi kila siku wananiomba Namba lakini sikuwa na muda nao.

Niliacha kabisa kwenda kula kWa kaka mpishi, sio kwamba nilikuwa Siri chakula chake hapana, nilikuwa nakula lakini ndio kwa kuletewa na Rafiki zangu.

Ikiwa ni siku ya ijumaa, siku hiyo nilikuwa nikiumwa sana, nilikuwa nikipata maumivu makali sana ya tumbo jamani, Sijui Kama mnanielewa lakini tumbo lilikuwa likiniuma sana, ilikuwa kulala shida, kukaa shida na ta kusimama shida.

Rafiki zangu waliangaika sana, mwisho walipata wasiwasi zaidi na kuamua kunipeleka hospital ambapo nikajulikana Kuwa na typhoid, baada ya matibabu nikupatiwa dawa kisha tukarudi chuoni.

“Utakula nini ??”

Cecy aliniuliza maana Giza lilishaingia kWa wakaati huo na tunatakiwa kula chakula cha usiku.

“Nafikili ndizi tu “

Nilijibu ingawa sikuwa Nikijisikia kula ata kidogo ingawa nilikuwa Nina njaa Sana.

“Nafikili pia tungepata na uji wa moto labda ungesaidia kutuliza maumivu ya tumbo “

Alizungumza Joyce.

Cecy akashika njia na kwenda kufata chakula kisha Joyce akabaki na Mimi hawakuweza kuniacha Mwenyewe.

Ila nyieeeh Mimi nimepata marafiki Walahi Tena, kWa dunia yetu hii ukipata marafiki Kama hawa lazima ufurahi.

Baada ya Kama nusu Saa hivi Cecy alirudi akiwa na mfuko ameweka zagazaga za kutosha.

“Leo minyoo lazima ishtuke “

Alizungumza Cecy pale tu alipoingia Ndani, mgonjwa Mimi vishina vya umbea ni Kama vilianza kuota Ndani yangu nikajikuta nikiuliza.

“Kwanini minyoo ishtuke ??”

“Matunda dada matunda, umu Ndani Mara ya mwisho lini kula matunda ? Kwa upande wangu sikumbuki labda nyie wenzangu mwaya”

“Nani nawe amekula matunda, Ila Binti subili kwanza we umepata wapi matunda hayo ??”

Cecy akaweka vitu chini na kuanza kucheza uku akijiimbia Mwenyewe, Mimi na joyce tulibaki tukimshangaa tu maana mtu ako na mood moja nzuri sana .

“We nawe si useme jamani “

Joyce alishindwa kabisa uvumilia akajikuta akimfosi cecy kuzungumza.

“Haya jamani nasema nasema, kwanza salamu nyingi sana za pole kwako mgonjwa, mgonjwa Kama mgonjwa umeambiwa ugua pole na Utakuwa Sawa “

Nilikuwa nimejilaza lakini nikanyanyuka na kukaa wima kisha kWa shauku nikauliza.

“Hizo salamu kutoka kwa nani ??”

“Nani mwingine zaidi ya Evan A.K.A kaka mpishi “

Nyieeeeh kwanza moyo wangu ukalipuka kwa furaha sana kusikia Kuwa kaka mpishi ndio ameniambia Pole, nilijikuta nikianza kublash kWa aibu si mnajua Tena mambo ya ma love love.

“Mkaka wa watu ajaishia hapo, akaniaachia banda akaenda kununua matunda kwaajili yako dada”

Nyieeeh nilijikuta nikidakia.

“Weeeeh unasema kweli ??”

Cecy akanituliza.

“Kaa kwa kutulia Binti sijamaliza yani ndio kwanza naanza, mkaka wa watu ameweza halafu ameweza Tena, ma mchungaji Mungu wako makali ujue ooooh Sijui umemtupia maombi gani kaka wa watu lakini Amechanganyikiwa kusikia unaumwa kiasi iko “

Nyieeeeh hizi habari Mbona kama zinaniponya hivi 😂 Mbona Kama maumivu ya tumbo yanakata hivi au basiiiii my zangu am in love 🥰 .

“Mkaka wa watu kakupikia uji huu, and guess what??”

Joyce akadakia chap.

“What ??”

“Ajachukua ata Mia ya Pesa ya chakula Pesa zote hizi hapa, kasema kwa niaba ya mgonjwa lakini pia na sisi Wauguzi “

Hapo Joyce akapiga sarakasi moja Matata na kusema.

“Shem kama shem, Shem tunae na tunatamba nae “

Muda huo huo huo simu yangu ikaita na Namba ilikuwa ni ngeni chap nikapokea.

“Hellow “

Nilizungumza baada ya kupokea simu.

“Hello ZANELE, Evan hapa Unaendeleaje ??”

Majilaniiiiiiiiiiih itaneni itaneni amenipigia ukuuuu 😂💃💃 eeeeh my zangu mjiandae kudadeki zenu.

Kusikia Jina lake nika……

NAKUJA MY ZANGU….


EVAN (kaka mpishi) 💙
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 05

www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

Kwanza kWa Wenger’in la hali ya juu nikaweka simu chini na kubaki nikiwa nimetoa macho na kuachia Mdomo Kama Nimeona kitu cha ajabu hivi, Joyce na Cecy akaniangalia na kuniuliza.

“Nani kwani ??”

“Evan…”

Nilijibu haraka haraka, Cecy akasogelea simu na kuichukua kisha akaweka loudspeaker na kuniambia.

“Ongea wewe “

Walahi nilikuwa na furaha mpaka nikawa nashindwa kuongea Cecy akaamua kumdanganya tu.

“Subili kidogo anatapika”

Kitendo cha kaka mpishi kusikia Kuwa natapika kWa wasiwasi akauliza, yuko Sawa kweli ? Kama anaumwa sana tumuwaishe Tena hospital.

Nyieeeehe 🥰👌 majilani kazi mnanielewa mnamuona kaka mpishi anavyonijali lakini, hapo shoga yenu mbichwa ukawa juu juu ni Kama ulikuwa unataka kuchomoka kwa misifa.

“Hapana hapana atakuwa Sawa usijali “
Cecy Alijibu ili kutuliza wasiwasi ya kaka mpishi.

“Cecy acha zako ujue Kama yuko serious sana tumuwaishe tu hospital “

“Yuko Sawa usijali “

Nikaona mkaka wa watu ni Kama presha Inampanda hivi, hivyo nikaamua kumjibu.

“Evan niko Sawa ni tumbo tu limetibuka”

“Ooooh thanks God”

Alijibu Evan na kushusha pumzi Ndefu sana ni wazi Kuwa alijisikia afadhali baada ya kusikia Kuwa naendelea vizuri.

“Jikaze ule mama Sawa, na Utakuwa Sawa ZANELE uwe na usiku Mwema “
Alizungumza Evan kisha akakata simu.

Mimi na shoga zangu wote tukabaki tukiangaliana tu na tusiamini kitu ambacho kimetokea Joyce akaniuliza.

“We mbwa wewe, ujatuma Jina la kaka wa watu kwa bibi yako uko kigoma kweli ??”

Hapo tulijikuta wote tukianza kucheka, Walahi mgonjwa nilipona kabisa, nilisogeza chakula na kWa pamoja tukaanza kula.

Baada ya kumaliza kula, Joyce akanyanyanyuka na kwenda kuoga.

“We Joyce wewe tangu lini usiku ukaoga Mara Mbili jamani “

Nilimuuliza maana sio kawaida kabisa kuoga Mara Mbili muda wa usiku.

Joyce akiwa bafuni akanijibu.

“Ma mchungaji ushaanza Kuwa mmbea abu niache mwenzio “

Baada ya muda Joyce akajianda na kutuambia Kuwa anatoka na boyfriend wake na atarudi siku ijayo.

“Take care babe ukiona mambo ndivyo sivyo piga simu kitengo cha uokoaji tuko kazini”

Alizungumza Cecy.

Ila nyieeeh huyu Cecy ni a akiamini Walahi, kuna muda ata Mimi na muogopa maana weeeh ni habari nyingine huyu msichana, kitu ambacho nampendea Cecy ni msichana Fulani hivi Mwenye upendo, anajali sana, lakini pia anasikiliza pale anaposhauriwa.

*******

Siku Tatu zilipita na hatimaye mgonjwa wenu nikapona kabisa, baada ya kukaa muda mrefu pasi na kwenda kwenye Banda la Evan hatimaye baada ya kupona nikaongozana na Rafiki yangu tukaenda.

“Ooooh karibuni sana jamani “


Evan alitukaribisha kwa furaha sana kuliko siku zote ambaazo Nimekuwa nikimuona.

“Asante Unaendeleaje ??”

Joyce alimuuliza Evan uku akionesha ishara ya kutaka kumu hug, Ila Joyce jamani 😂🙌 my zangu Kama marafiki zangu uwezi Kuwamudu, hawa wangu nakupa siku moja tu unawarudisha.

Evan wa watu Wala hakuwa na chaguo zaidi akamkumbatia tu kaama ambavyo Joyce alitaka.

“Wewe ndio nini sasa ??”

Cecy alimuuliza Joyce ni Kama hakupendezwa na kitendo cha Joyce, lakini pia alimuuliza kWa sauti ya chini ambayo tulisikia sisi tu.

“We nawe tulia kwanza Unafikili me Chizi au, nimemkumbatia makusudi kWa sababu nimemuona Yule mpuuzi aliyekuja kututambia Kuwa Evan ni mtu wake”

Hapo Cecy akaanza kuangalia uku na uku na kweli kwa mbali tuliweza kumuona msichana Yule ambaye alikuja siku ile kumfanyia fujo Cecy .

“Aaah my wangu umeniangusha nawe, Yaani hapo ungemkisi kabisa, uwiiiih Kwanini sikumuona huyu msichana wakati naingia jamani “


Ila Cecy Anapenda ugomvi kuliko kula.

Evan wa watu alikuwa amesimama tu akisubili tukuagize mwisho akauliza.

“Girls amtakula Leo au ??”

“Tunakula bwa usilete utani na msosi wewe”

Baada ya muda tuliletewa chakula na kuanza kula, Kama kawaida nikawa wa kwanza kumaliza maana Mimi nakulaga Kama bado Nipo kigoma kwenye ugali wa mafungu 😂🙌 Namaanisha wa ugali wa familia Bwana.

Nilipomaliza nikanyanyuka haraka kaka mpishi akaniuliza.

“Unaondoka ??”

Nikatabasamu na kujibu.

“Hapana nakusanya vyombo nikusaidie kusafisha”

KWa siku hii Bwana Kama mpishi hakuchukia na Wala hakunikataza zaidi akaniacha nifanye kitu ambacho nilikuwa nikitaka.

KWa upande wa Joyce na cecy, walimaliza kula kisha Wakaaga baba kuondoka na kuniacha Mimi nikiendelea kumsaidia Evan wangu.

Ila nyieeeh watu huyu kaka nampenda sio utani Walahi, na Kama atachelewa kuniambia hisia zake juu yangu Basi Mimi niko tayali kumwambia siwezi kuendelea kuvumilia.

“Mitihani mnaanza lini ??”

Evan aliniuliza.

“Kesho kutwa Yaani mapuziko kesho tu kesho kutwa tunaingia kwenye chumba cha mtihani”

Evan akanisogelea na kunipokonya dodoki niliyokuwa nikioshea vyombo kisha akazungumza.

“Ni muda wa kusoma huu sio wa kuosha vyombo vya Evan Sawa “

Nyieeeh huyu kaka Mbona anazidi kunichanganya mwenzenu, kwanza kitendo cha yeye kusogea Karibu yangu ni Kama alikuja kupushi mapigo yangu ya moyo hivi, mapigo yangu ya moyo yalikimbia kuliko kawaida.

KWa sauti ya utulivu nikamwambia.

“Namalizia tu hivi then naenda kujisomea “

“Hapana hapana, ZANELE usicheze na elimu yako mama Sawa, Evan utamsaidia sana tu lakini kwa sasa hivi go and study kipenzi Sawa “

Majilaniiiii nimeitwa kipenzi uku nazimia sasa maana yoooh Mbona Kama niko dunia ambayo sijawai kuishi hivi.

KWa utulivu Evan akanisafisha mapovu yaliyokuwa kwenye mikono yangu na kunitoa nje ya Banda lake.

“Zanele soma sana mama Angu Sawa “

“Sawa “
Nilijibu kw utulivu kisha nikaaga na kuondoka.

Nikiwa njiani kuelekea hostel, msichana Yule ambaye alimfata cecy siku ile, gafla tu akaja mbele yangu na Kuniambia.

“Kumbe ni wewe mama mchungaji “
Kabla Sijafanya chochote kile nikachezea kibao kimoja tu kutoka kwa Msichana huyo.

Nika…..

MBONA VITA YANGU YA MAPENZI IMEANZA MAPEMA KABLA PENZI ALIJAANZA 😂🙌 HAYA NGOJA TUONE.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote