Friends With Benefits

book cover og

Utangulizi

SASA SIJUI ITAKUWAJE..
baada ya kupitia mateso makubwa ya ndoa yangu, kuwa na mwanaume ambae alikuwa ananinyanyasa sana, kwa mara ya kwanza nilikutana na kijana ambae alinitetea kwa mume wangu na kumfanya mume wangu aniogope mpaka akubali kunipa talaka...
Kutokana na mateso niliyopitia nikakataa kabisa kuwa kwenye mahusiano, mpaka nilipokutana na faby, kijana ambae alinisaidia kumuadabisha ex wangu, nae pia hakutaka kuwa kwenye mahusiano hivyo akaniomba niwe mshirika mwenzake kwenye tendo, lakin tukawekeana na viapo kuwa hatutakaa tuwe kwenye mahusiano wala kuwa na hisia kati yetu, lakin mambo yanakuja kwenda ndivyo sivyo baada ya mimi kuhisi naanza kumpenda faby..
Anakubali kuniacha lakin ni kwa maneno tu, ila kila akinikuta na mwnaaume alikuwa analeta vurugu sana na kunirudisha nyumban, alikuwa anaonekana kama kachanganyikiwa sana na mimi na ananipenda kupita kias..
Ila hakuwa anataka kunioa na wala hakutaka niwe karibu na mwanaume mwingine yoyote yule zaidi yake, unadhan ni ipi hatma ya penzi hili...
Usikose simulizi hii tamu ya kusisimua ya FRIENDS WITH BENEFITS
(No fillings, no relationship just sex)

FRIENDS WITH BENEFITS 1
(no fillings,no relationship, just s*x)
HUSQER BALTAZAR
Maisha bana ni fumbo kubwa mno, unaweza ukawa unajiona kama mtu ambae una laana, au mtu ambae dunia imekutenga sana, au mtu ambae umejaa maovu mno, ila mungu akakuletea mtu ambae atakupenda licha ya mapungufu mengi uliokuwa nayo…

Martha ndio jina ambalo nilipewa na wazaz wangu, nilishi kwenye ndoa kwa miaka mitatu ila ndoa haikuwah kuwa riski maana mwanaume ambae alinioa alikuwa ni Malaya na mlevi ,kupindukia, yote niliyavumia maana nilishajiaminisha kuwa hakuna mwanaume ambae hasaliti na ndoa zote zinachangamotyo hivyo nikaamua kuvumilia changamoto yangu, mpaka siku moja mume wangu alipotaka kumuingilia kwa nguvu mtoto wa dada yangu ambae alikuja kunitembea kipindi cha likizo na alikuwa na miaka 15 tu, hapo niliona kama amenidhalilisha mpaka mwisho, nikaona ndoa sio rizki tena, nikaamua kuondoka na Yule mtoto na kudai talaka yangu….

Mume wangu mwanzo akaanza kunichafua kwa watu kuwa nilikuwa Malaya sana, ila nilichagua kukaa kimya kwa maana sikutaka kuendelea kutoleana maneno maana kwanza nilikuwa na mtoto mdogo wa kike, hivyo sikuytaka kujibizana nae…

Siku moja nikiwa zangu nimetoka out, hapo ni baada ya kupewa talaka, nikaona nijipongeze maana maisha ya ndoa hayakuwa mchezo, sijui Yule mume wangu tulieachana alitoka wapi akaanza kunitolea maneno ya ajabu na hapo alikuwa amelewa mno, akaanza kunambia, “ mwanamke una mikosi sana wewe, yaan namshukuru mungu sana kwa kuachana na wewe , maana kuanzia tumeachana nimenawiri sijui ni mwanaume gani anaweza kukoa mwanamke kama wewe, yaan unanuka na una mikosi sana, yaan mwanaume akiokuoa wewe najisaidia kwa mafungu mpaka dar bila kupumzika…

Nilijisikia vibaya sana, ghafla nikasikia sauti nyuma yangu ikisema “ anza sasa hivi kujisaidia mafungu, maana ameshapata mwanaume anaempenda kuliko kawaida, yaan yupo tayar kufanya lolote lile kwaajili yake…

Ilikuwa ni sauti ngeni kabisa masikioni mwangu, sikuwah kuisikia kabla , ex mume wangu ni kama akawa ajasikia vizuri akabaki katoa macho ambayo yalikuwa yanamuonesha vyema kuwa alikuwa amelewa sana, kisha akasema “ yaan wewe ndio umempenda huyu Malaya, ama kweli kila kichaa na jalala lake..

Nikashangaa Yule mwanaume akaenda kumkwida ex wangu kisha akamuweka ngumi moja mpaka akaangiuka chini kisha akamnyanyua na kusema “ nisije kusikia ukimuita mke wangu tena Malaya nitakupoteza, kisha akanisogelea na kunikiss kwenye lips zangu, yaan wakati wote huo nilikuwa nimeduwaa tu sijui nifanye nini, sio siri nilijisikia vizur sana Yule mwanaume aliponisaidia, na ex wangu akatoka nduki kama sio yeye ambae alikuwa ananidhalilisha dakika chache zilizopita…

Nilitaman kujua Yule mwanaume ni nani, na kwanini amekuja kunitetea kiasi kile, na kwanini aje kunitetea na wakati hata hanijui hata kidogo, so nikamsogelea na kumuambia “ nashkuru sana kaka yangu kwa kunisaidia, nikampa mkono kwa ishara yak um shukuru, ila badala yake alitoa sigara mfukoni mwake kisha akaiweka mdomo na kuanza kuondoka bila kusema neno…

Na hata nilipojaribu kumuita hata hakugeuka, nilishangaa huyu ni nani, na kwanini amenisaidia ila hataki hata kuongea na mimi, nikaona ni sawa tu, nikamshukuru pale kimoyo moyo kisha nikaendelea zangu kula, na nilipomaliza nikaondoka zangu kurudi sehemu ambayo nilikuwa nimepangisha…

Sasa wakati nataka kulala Yule mwanaume akaanza kunipigia simu, Yule ex wangu, nikawa sitaki kupokea kabisa, maana nilijua hakuna kitu ambacho anaweza kukifanya zaidi ya kunitukana na kiukweli nilikuwa nimeshachoshwa na matusi yake, yaan kila siku ni tusi jipya mpaka nachoka…
NAKUJA……………


FRIENDS WITH BENEFITS 2
(no fillings, no releatin ship just s*x)
HUSQER BALTAZAR

Basi ex wangu Alipiga simu karibu mara nne, na sio kawaida yake, ila sikupokea hata mara moja, maana sikutaka kutukanwa mimi, mara nikashangaa sms inaingia kwenye simu yangu ikiwa inatoka kwa ex wangu, ikawa inasema “ martha mamaa naomba nisamehe sana naomba nisaidie tu kwa kupokea simu yangu, hata kama nilikuwa nakutukana kiasi gani ila bado mm ni baba wa mtoto wetu, hivyo naomba hata kwa hilo upokee simu yangu, unavyokuwa haupokei simu haujui unaniweka kwenye wakati gani mamaaa, nilishangaa nimeanza lini kuitwa mamaaa, kwa namna alivyokuwa ametuma ile sms ni dhahiri niligundua kuna kitu hakipo sawa kabisa, basi nilipomaliza kusoma ule ujumbe kweli simu yangu mara simu ikaanza kuita na sikusita kupokea….

“ naomba unisamehe sana, na naomba nikiri kuwa nikija kukudhalilisha tena jambo lolote lile linikute, sityakaa kukudhalilisha wala kukutukana na hata ikitokea nimekuona barabaran nitakupisha anagalau tu nisije kukutana na wewe, naomba nisamehe sana martha na sio siri najuta sana kwa kukukosea…

Nilibaki nimekaa kimya, maana kuanzia namfahamu huyu mwanaume sijawah kumsikia akiongea kistaarabu zaidi yah ii siku, nikahisi labda kuna kitu hakipo sawa, ila sikujali kabisa maana sion siri amenitesa sana huyu mwanaume hivyo hata akiwa kwenye hatar kwangu ni sawa tu….

Basi baada ya kumaliza kuomba msamaha akakata simu, na mimi nikaingia zangu bafuni kwaajili ya kuoga, nikaoga, hapo mtoto wangu nimemuacha kwetu nimeona mimi nije kujitafuta kidogo, maana kukaa na mtoto mdogo na wakati hata haujajipata kidogo ni changamoto…

Nikamaliza kuoga nikapanda zangu kitandani, sasa huwa nina kawaida ya kusali kabla ya kulala, sasa wakati namaliza kusali ili nilale zangu mara nikasikia mlango unagongwa, nilishtuka sana maana ilikuwa kama saa tano usiku hivi…

Kwa wasiwasi na uoga mkubwa nikazima taa na kuchungulia ni nani, nikashangaa nakutana na sura ya Yule kijana ambae alimpiga biti ex wangu, na alijua kuwa namchungulia , kwa wasiwasi na uoga mkubwa nikamfungulia mlango, nikashangaa anapitiliza mojan kwa mloja mpaka kitandani kwangu, maana nilikuwa na chumba kimoja, na kulikuwa na kochi, sijui hata kwa nini hakutaka kukaa kwenye kochi na badala yake akaenda kukaa moja kwa moja kitandani…..

“ samahan kaka yangu mbona umekuja nyumban kwangu usiku? Na umepajuaje,? Ikabidi niulize, maana sehemu ambayo tulikutana mpaka nyumban kwangu kidogo kuna kaumbali flani hivi, sasa mwamba amefikaje kirahisi hivyo….

Akaniangalia kisha akacheka na kusema “ ingekuwa nina mpango wa kuoa ningekuoa, ila kwa kuwa sijawh kuwaza kuoa basi itabidi unilipe kwa wema niliokufanyia martha…

Baada ya kusema hivyo akaanza kufungua vifungo vya shart lake, hofu ikaanza kuniingia na kuamini kuwa naenda kubakwa sasa, nikaanza kurudi nyuma ila hata hakunizuia, akavua zake sharty na viatu kisha akachukua blanket langu na kulala zake kwenye kochi kimya kimya…

Nilikuwa naogopa sana, maana kwanza sikuwa namjua na pili analalaje chumban kwangu, nadhan aliuhisi uoga wangu, akaasema “ mimi sio kijana mpuuzi, kama ningekuwa nakutaka kimwili wala hio nguvu ya kunizuia usingekuwa nayo, ila nakuheshimu sana, hivyo siwez kukulazimisha jambo lolote lile, embu acha uoga na upande kitandani ulale…..

Ingawa nilimsikia ila sikuwa namuamin kabisa, nikaingia kabatin na kutoa shuka lingine kisha nikapanda kitandani na wasiwasi wa hali ya juu, nilipata usingizi kwa shida sana ila mwishoni hatimae nikalala…
NAKUJA……


FRIENDS WITH BENEFITS 3
(no fillings, no relationship, just s*x)
HUSQER BALTAZAR
Nimekuja kuamshwa na sauti ya jiko langu la gesi, nilikurupuka maana nilishasahau kuwa nililala na mtu nyumba moja, nikakurupuka na kufungua macho nikamkuta Yule mwanaume anamalizia kupika chai, alichemsha mayai na mkate na chai…

Akaweka chai kwenye chupa kisha akajimiminia na kaunza kunywa, nikawa kimya kwanza namsoma, basi nikaamka na kuanza kuvaa vizuri kisha nikaenda kupiga mswaki na kuoga, nilienda na nguo zangu bafuni maana sikuwa namuamin kabisa yaan, sikuwa naamin kama anaweza asinifanye kitu…

Nimetoka nikakuta ameshakunywa chai na vyombo vyake alivyonywea chai kavisuuza na amekaa zake kwenye kochi anachezea zake simu, nikaenda na mimi kuchukua chai nikanywa, sikuwa naosha vyombo hapo hapo, ila ukikaa na mwanaume msafi lazima na wewe uwe msafi tu, hivyo nikajibaraguza kuosha vyombo baada ya kunywa chai…

Nimemaliza na mimi nikaanza kupanga ndani kisha nikapanda zangu kitandani na mimi nikawa busy na simu yangu, mara nikashangaa mwamba kajamba, nikakausha sikutaka kumuuliza, mara nikasikia anasema ‘ uliza tu kuwa kaka kwanini umejamba, nilikuwa nakulipizia kwa kunijambia usiku kucha, mwanamk sijui huwa unaendaga kwenye mashindano ya kujamba, maana ulikuwa unayashusha kwa mstari nikasema usinitanie lazima na mimi nilipize…

Nikajikuta naanza kucheka, maana nilidhani nimekutana na kauzu kumbe mtu wa kawaida tu, nikajikuta na mimi naropoka kuwa “ nilikuwa nakuonea aibu hapa penyewe nilikuwa najibana, nikaliachia la nguvu, aiseee mwamba alicheka kisha akasema “ nilijua tu nikapika mayai, lazima utayapumua, kitu inanuka kama nini…

“ kwamba wewe ulivyojamba ndio haijanuka? Nikauliza…
“ weee ushuzi wangu unapafyumu huwa haunuki unanukia, akasema nikajikuta naanza kucheka…
Ingawa nilikuwa namuona kama kauzu sana ila sio kweli kama alikuwa hivyo, alikuwa mcheshi sana, kiasi kwamba sikutegemea kama ndio Yule kauzu ambae nilikutana nae jana yake, ambae hata kucheka alikuwa anaona dhambi…

Ndani ya masaa machache tulikuwa tumezoeana sana kana kwamba tulijuana muda mrefu sana, ila nilikuwa naogopa hata kumuuliza jina lake, kila nikitaka kumuuliza nafsi yangiu inasita, na ni kama alikuwa ameshaweza kuisoma akili yangu, akanambia “ usione haya kuniuliza jina bwana, naona unajiuma uma weee mwisho uje ujiumize nianze kulia, najua unataka kuniuliza jina, naitwa lugemarera sokojakalaumishomwamba fatamba, hilo ni jina langu na baba yangu anaitwa mwakijambekifopo mwanakalugulunga shayambayogo zimbwane, ila kama unaweza usikumbuke hayo majina unaweza kuniita tu mume wangu…….

“ aaa weee, kama kweli ni majina yako embu yarudie, majina gani hayo kama mzizi wa dawa ya kifurukobe, nikasema aiseee alicheka sana kisha akasema jina pekee ambalo naweza kurudi ni mume wangu, maana kikwetu kurudia rudia jina ambalo umepewa na ukoo ni laana, akasema tukajikuta tunaanza kucheka…

Nikaona hapa nimepata mwenda wazimu mwenzangu..
Mchana sasa ukafika, akaniangalia kisha akasema unataka tupike nini?...
“ siwez kupika mimi mpaka uniambie jina lako, nikajibu..
“ ndio maana niliambiwa wanawake sio waelewa kabisa, nimekuambia naitwa mume wangu, akajibu..
“ kama wewe unaitwa mume wangu na baba yako jina lake la kawaida ni nani? Nikamuuliza swali lingine la mtego nikijaribu kama anaweza kunambia jina lake halisi..
Akasimama kisha akachukua remote na kuifanya kama kipaza sauti kisha akasimama juu ya meza na kuanza kusema “ ladies and gentralman, nashkurun sana kwa kufika hapa, labda nianze kwa kujitambulisha majina yangu kamili, nikianza kwa kusema naitwa mume wangu nakupenda, nashkuru sana kwa kunisikiliza…
NAKUJA…………


FRIENDS WITH BENEFITS 4
(no fillings, no relationship just s*x)
HUSQER BALTAZAR

Nikaona hapa sasa nimepata mental kabisa, yaan nikajua kabisa kuwa hataki kunambia jina lake na hilo sikutaka kuliona kama tatizo kabisa kwangu, ikabidi nijifanye kama nimekubaliana nae tu, kuwa anaitwa mume wangu…
Nikamuangalia kwa sekunde kadhaa kisha nikasema “ haya mume wangu nambie tupike nini mchana?...

Akaniangalia nay eye kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kucheka, alicheka sana mpaka na mimi nikaanza kucheka kisha akasema “ nilishasahau kama naitwa mume wangu kwa hio nikawa kama nimepigwa na bumbuwazi, si unajua wenzako tumeshazoea kuitwa majina yetu ya kimila, sasa ni hivi mke wangu, leo nina hamu ya kula ugali na nyama choma, embu vaa ujianda twende sehemu tukale akasema…

“ wewe umesema unaitwa mume wangu ndio maana nikakuita hivyo , ila mimi siitwi mke wanmgu naitwa martha naomba uwe unaniita jina langu please…

Akaniangalia kisha akasema “ kinyume cha mume ni nini?..
Nikakaa kimya, nikajifanya kama nimejinunisha, akacheka kisha akasema “ acha kujifanya umekasirika na wakati wewe mwenyewe unajua kinyume cha mume ni mke, sasa unataka mimi tu ndio uniite mume alafu mimi nisikuite mke, labda uniue…

“ lakin si nimekuuliza jina lako haujanambia, ila mimi nimekuambia kuwa naitwa martha, nikasema…
“ utachagua kuwa uniite jina langu la ukoo au uniite mume wangu, mimi sina majina mengine ninayo yakumbuka katika kumbukumbu zangu, haya jiandae utanikuta nje mke wangu, kisha huyo akatoka zake nje kunisubiri…

Nilikuwa kwenye mashangao, maana ni kama ndoto tu, yaan kwanza sikujua huyu mwanaume ni nani na kwanini aje kwenye maisha yangu, na kwa nini anipe furaha na najikuta namuamin sana tena ndani ya muda mchache sana, nikaona niachane na mawazo na nijiandae ila nikawa najiambia kuwa nisijiachie sana kisije kikaniramba bure…

Basi nikaingia kabatin na kutoa gauni lango moja la solo, huwa napenda sana kulivaa nikiwa na mitoko ya kawaida, lilikuwa lina mauwa makubwa ya maroon na lenyewe lilikuwa jeupe, Kisha nikafunga zangu lemba langu uchwara na vislippers vyangu na kipochi changu cha kubebea nyama zikibaki, kisha nikajipulizia manukato yangu na kujipaka kawanja cha kichokozi kidogo kwenye macho yangu ya duara makubwa kiasi, watu wengi huwa wananisifia sana kuwa nina macho mazuri sana, na kwenda kunyonga kitasa cha mlango kisha nikatoka, aliponiona tu ni kama alipigwa na bumbuwazi akawa ananishangaa, nilikuwa nimevaa kikawaida sana, ila ni kama alikuwa amevutiwa sana na muonekano wangu…

Akanisogelea na kusema “ siku nyingine usiwe unaniangalia hivyo ukiwa umepaka wanja, nitakuteka shauri zako…

Nikajikuta natabasamu tu, basi tukachukua toyo maana sikuwa na gari na wala yeye hakuwa na gari, hivyo kila mtu akalipa toyo yake, na kweli baada ya dakika chache tukafika kwenye restaurant moja inasifika kwa kuchoma nyama ambapo wanapaita nyama choma center, tukashuka kisha akalipa wale madereva toyo kisha akanishikla mkono, nikashangaa na kumuuliza kwa sauti ya chini kuwa “ mimi sio mpenzi wako, kwanini unanishika kama sisi ni wapenzi, unataka kunizibia rizki nini…

Nikashangaa mwamba kabadilika, akanigeukia macho yakiwa mekundu mpaka nikajikuta naogopa, kisha akashusha pumzi na kusema kwa sauti ya chini, “ kiss me please …
NAKUJA


FRIENDS WITH BENEFITS 5
(no fillings, no relationship, just s*x)
HUSQER BALTAZAR
Nilishangaa sana anamaanisha nini, maana hatukuwah kuwa na mahusiano hata ya kusingiziwa, sasa anataka nimkiss kivipi yaan, maana sikuwa na muelewa kabisa, akawa amenikazia macho kana kwamba anasubiri hilo busu, nikaonaisiwe tabu nikasogea na kumkiss kwenye mashavu yake, ila ni9 kama hakuwa anataka, ikabidi nimkiss kwenye lips tu ili kumaliza utata, maana huwa sijawah kupenda heka heka hjata mara moja kwenye maisha yangu…

Basi bana baada ya pale tukakaa sehemu na kuanza kula sasa, ila wakati wote alikuwa ananiangalia sana, yuaan tena alikuwa ananiangalia kwa macho fkani hivi, nikawa najiambia ehee mwamba mbona kama amenitamani, ila nikasema nikaushe, maana sikutaka mambo yawe mengi kwa maana hata kama anajifanya ni mstaarabu ila nimeshawah kuona ubabe wake mara kadhaa, na najua ni mbabe sana, hivyo sikuwa nataka kabisa anilete ubabe wake…

Tumemaliza kula tukaanza kurudi nyumban, siku hio nilimuona kama usiku wake ulikuwa mgumu sana, maana kila wakati nikishtuka alikuwa amekaa amejiinamia kwenye kochi nikawa najifanya kama sijamuona vile, basi hali iliendelea mpaka asubuh, na wakati naamka nikakuta amenisaidia kufanya kazi zote za pale nyumban, na amepika chai yake na chapati za maji….

Basi nikaamka na kujiandaa na baada ya hapo nikaanza kunywa chai, baada bya kumaliza nikachukua vyombo na kwenda kuanza kuosha, ila ni kama alikuwa amenifata nilipo, maana nI kama alikuwa anataka kuzungumza na mimi…

Kweli nilipotulia akaniita na kusema martha mamaaa, ikabisi na mimi nitulie nimsikilize anataka kusema nini,nikaitikia abee…
“martha mamaa nina maongezi na wewe na naomba usinichukulie tofauti, ninachotaka ni tuwe tunasaidiana tu kwenye baadhi ya mambo na kama utaona kama sio kitu sahihi unaweza ukakataa kabisa na nitakuelewa tu, maana nitakuwa na uhakika ni maamuzi yako….

“ eheee nieleze nakusikiliza, akajibu martha kwa sauti ya kujiamin kabisa…
“naomba tufanye kitu kimoja, kinaitwa friends with benefits, akasema kwa sauti ya kujiamin kabisa huku akiwa amemkazia macho martha…
“ friends with benefits?, ndio nini, akauliza martha na yeye, kana kwamba hakuwah kusikia neno kama hilo hata mara moja kwenye maisha yake…

“ yaan tunakuwa ni maragfiki wa kusaidiana kwenye kila kitu, ila no fillings, no relation ship just sex, yaan hatutakiwi kupendana kabisa ila tunasaidiana kuondoleana upwiru, akasema Yule kijana..

“ kwanza kabla ya yote embu niambie jina lako, maana nimeshachoka kukuita wewe kila siku, akasema martha…
“ niite fabiano, akajibu Yule kijana na martha akadakia, “ ohhhhh kaka faby..
“ ndio utajua kama ni kaka ama kakaaa, maana ninavyojua makaka na madada hawakulani, akaendelea kusema fabiano…
“ kwani nimekubali ombi lako mpaka unipangie, mimi ninachojua wewe ni kaka faby hayo mengine labda kama utakuwa umeyasema wewe, akaendelea kusema martha…

“ ila martha kwa namna ambavyo nazijua akili zako najua kabisa hautakubali na wakati unajua kabisa kuwa hautaki kuwa na mwanaume, yaan mimi sitakuzuia wala hata sitakaa nikuonee wivu kwenye maisha yetu yote, tunakuwa kama sex partners tu, na hata ikitokea baadae ukapata mtu wako na mkapendana mimi sitokuwa na shida kabisa , akaendelea kusema faby…

“ sawa nimekubali, akasema martha akashangaa mwamba amemrukia kisha akamkumbatia na kupitisha ulimi kwenye sikio lake bila martha kutegemea, alishtuka na akajikuta amepata msisimko wa ajabu kisha akasema “ nakusubiri ukubali akijua ameshamvuruga bint wa watu na kutoka zake nje….
NAKUJA…………..


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote