GIANA (My choice) 🥰
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA : 01
ANZA NAYO........
"Sema we msichana uwaga unajizima sana data me nakuambia kweli, yaani maelezo yote yale niliyokupatia asubuhi saa hizi nakuja ujafanya kazi yangu si ndio ? Yaani unaachaje nguo zangu zikiwa chafu namna Ile ? " Nilimfokea Giana ambaye ni dada wetu wa kazi ambaye hatujawai kuelewana tangu siku anaingia nyumbani.
"Chris ukirudigi kwenye kazi zako unachokiwazaga ni kuwai tu kurudi nyumbani ili uweze kugombana na Giana si ndio ? "Giana alinijibu kama kawaida yake, yaani uwaga aniogopi ata kidogo.
Giana ni kama msichana mwenyeshida sana, sio mimi tu ambaye atuelewani adi mdogo wangu wa kike ambaye anasoma chuo awakuwai kupatana na Giana, kila siku mama yetu anasikia tu kelele zetu.
"Nimekuambiaje tabia za kunijibu ? Yaani unanijibu unavyotaka unaongea na mimi kama unaongea na kidogo yako unachokifutaga kamasi uko nyumbani kwenu " nilimfokea nikiwa nimechukia sana.
"Haya nini shida tena ndani kwangu ? Mwenyewe natoka kazini ili nikifika nyumbani nitulize akili, halafu nakutana na kelele za watu wawili wakubwa kabisa wenye akili za watoto wa chekechea " alizungumza mama baada ya kuja jikoni akiwa amebeba pochi yake yaani na yeye ndo alikuwa ametoka kazini.
"Mama tubadilishie mdada walahi tena, huyu mimi nitakuja kumpiga mpaka achanganyikiwe halafu mimi nipate kesi " nilijibu.
"Kwahiyo ndo umekuja kugombana nae jikoni ? Chris una shida gani mtoto wangu ? Maana kila siku uko na sababu mpya juu ya huyu binti wa watu."
"Mama unajua kabisa kuwa kesho nasafiri, nimemwambia kuwa anifulie nguo zangu maana nguo ninazozipenda zote ni chafu, narudi saa 9 hii kuna nguo amefua ata kidogo" nililalamika.
"Ahaha nikajua ni mambo ya maana kumbe ni nguo tu ,m Chris nimeshasema umu ndani kila mtu atajifulia mwenyewe, naitaji kumpunguzia majukumu Giana, ukizingatia ninyi ni watu wazima, kila mtu umu ndani atafua mwenyewe nimemaliza " alizungumza mama kusha akaondoka.
"Aaah mama sio kweli, unanionea mama, yaani nafuaje ? Me naenda kazini asubuhi narudi mda huu kweli mama nachoka sana, Giana yupo tu nyumbani mama sio fair kabisa " nililalamika.
Mama wala akusikiliza malalamishi yangu aliongeza mwendo na kuwai chumbani kwake uku akisema kuwa haitaji usumbufu anapumzika.
Ginna alinicheka sana yaani huyu msichana kuna siku nitampiga na kumgeuza supu subili aone.
SONGA NAYO........
Niite Chris mtoto wa kwanza kabisa kwenye familia ya watoto wawili kwa mama yetu, lakini kwa baba tulikuwa wanne uku mimi nikiendelea kuwa mtoto wa kwanza.
Baba na mama yetu ni watu walioachana miaka kadhaa nyuma, lakini niseme kuwa ni watu wa tofauti sana, waliendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kwenye kampuni ambayo walifungua pamoja kipindi ambacho walikuwa wakiishi pamoja.
Baba yangu baada ya kuachana na mama apifanikiwa kupata watoto wawili ambao wote ni wakike, hivyo mimi tu ndo wakiume.
Baba na mama wameachana sawa, lakini ni watu wanaheshimiana sana, mama yangu hakuwa na shida ata kidogo.
Haikuishia tu baba kuoa nje lakini pia mke wa baba alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni hiyo hiyo na alikuwa ni rafiki wa mama wa enzi hizo can you imagine.
Mwanzo mama alikuwa na hasira Sana na shoga yake lakini mwisho alikubaliana na hali halisi na kufanya maisha kuendelea na hakimfukuza rafiki yake kazi.
Kwa upande wangu mimi ni drama boy, kwanza napenda kumpelekesha mtu tu bila sababu, ukiachana na kila kitu bado mimi ni mtu ninayejali sana.
Baada ya kugombana sana na Giana na kukosa wa kunitetea nilishika njia na kurudi chumbani kwangu.
Nikiwa na hasira kama zote nilichukua tenga langu la nguo chafu na kutoka nalo nje ili nikafue Maana nilikuaa nikisafiri kikazi.
Nilikuwa nafanya kazi tofauti kabisa na kampuni yetu, kiukweli sikuwai kumpenda mke wa baba, na sijui mama aliwezaje kukaa nae.
Nakumbuka kipindi nakua rafiki wa mama nilikuwa nikimpenda sana, yaani yeye ndio alikuwa mtu wangu wa karibu nilimuonaga kama mama yangu mwingine.
Alikuja kufuta upendo wangu kwake baada tu ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na baba yangu na Ata wakafunga ndoa.
Najijua ufuaji wangu uwa nafua na kujimwagia maji sana, hivyo nilitoka nje na kwenda kufua kwenye eneo la maua maua, yaani kwenye bustani ya maua ambayo mama aliipenda sana na alikuwa akikataza kufulia hapo ila mimi sasa.
Nilifua kwa hasira sana, nikiwa naendelea kufua mdogo wangu grace alikuja akiwa ndio kwanza ametoka masomoni, alifika na kuanza kucheka.
"Unacheka nini.??" Nilimuuliza.
"Aaah naona unafua mwenyewe baba, baada ya mikwala yote ile uliyompatia Giana asubuhi lakini bado saa hii unafua mwenyewe, huyu msichana na kinyo sio kama wale uliokuwa unawaonea " alizungumza mdogo wangu uku akicheka.
"Si mama amemtetea, yaani Leo nilikuwa naenda kuharibu Ile yake kama tikiti "
"Yaani mama karudi na weee unafua hapo ? Eeh we unataka vita na mama Chris nakuona kabisa akuuh grace mimi nijiondokee" alizungumza grace na kuondoka.
Nilimaliza kufua na kuweka sawa mazingira yale, nikarudi ndani na kwenda kuandaa vitu vingine, maana safari ilikuwa kama ya week mbili.
Nikiwa bize napanga zangu vitu vyangu muhimu kwenye begi, alikuja mdogo qangu grace akiwa amekasilika mno.
"Kaka walahi sasa hivi Giana nitampiga sasa " alizungumza grace.
"Amefanyaje ?? " nilimuuliza.
"Eti anasema kuwa ajatengeneza juice, yaani hii siku ya tatu mfululizo tunakula chakula bila juice huyu msichana ananichosha sasa, nilitaka kwenda kumwambia mama akanizuia na kuniambia kuwa mama amesema ataki usumbufu "
"Kwahiyo alivyokuambia hivyo ? Na wewe ukaacha kwenda kumwambia mama ? My wangu nenda kamwambie " nilimsapuza makusudi ingawa nilikuwa najua nini kitamkuta.
Baada ya kumpa moyo grace na kumfanya kujiona kuwa anaweza akaenda kuongea na mama, aliondoka kwa kujiamini akiwa na uhakika kuwa anafanikiwa jambo lake.
Nilitoka chumbani kwangu na kwenda sebuleni ili niweze kusikia yeye na mama watafikia wapi.
"Grace toka nje " niliweza kusikia sauti ya mama akimfokea grace.
"Lakini mama tunakulaje kila siku kama wadudu jamani, kishushio ni maji kweli jamani me nimechoka sasa " alizungumza grace.
"Nilivyokutuma juzi kwenda kununua matunda si ulikataa ? Endelew kukataa binti sawa ? Pambaneni na hali zenu, tena nisione pua yako mbele yangu tokaa...."
Weeeh nilibaki nikicheka sana, maana nakumbuka kabisa, grace alitumwa na mama sokoni kununua matunda aka Kataa na mama akasema kuwa atatunyoosha, hivyo basi na kazi ndo umeanza.
**
Siku iliyofuata niliamka mapema Sana na kujiandaa kwaajili ya kusafiri kikazi na nilikuwa nina ndege ya asubuhi Sana.
Kusikia ndege msije mkajua naenda nchi za wenyewe oooh 😂🙌🏿 naenda zangu tu mwanza mwaya.
Niwaambie kitu, kampuni jinayofanya nayo kazi ni kubwa tu tena sana, na inafanya kazi na watu wa nje kabisa lakini sasa kunituma mimi kuwakilisha nje awawezi, boss wangu anasemage Mimi ni kichwa maji 😂.
Nikiwa nawai kutoka nje, kwani dereva wa bolt alishafika, Giana aliniita kwa sauti kubwa sana na kuja karibu yangu kwa mwendo wa kukimbia kwani nilishafika getini.
"Umesahau Bible yako, lakini pia hii saa, uliiacha bafuni " alizunguma Giana.
"Bafuni kwangu ulienda kufanya nini ??" Nilimuuliza kwa hasira.
"Achaga kuwa na hasira, kumbuka unasafiri na safari yako inaitaji sana amani, ata hivyo nilienda kukufanyia usafi maana najua ukupata muda wa kufanya usafi " alizungumza.
Kwa namna moja au nyingine, niliona, giana ni msichana anayejali sana ni vile tu kichwa chake mara nyingi kinakuwaga 🔥.
"Asante sana " nilimshukuru.
"Uwe na safari njema na kazi njema " alizungumza kisha akageuka nyuma na kuanza kurudi ndani, nilijikuta nikibaki nikishangaa kingongingo chake.
Moja kwa Moja nikatoka nje na kuondoka kwa kutumia usafiri wa bolt ikiwa ni safari ya kuelekea airport.
Nikiwa njiani mama yangu alinipigia simu na kunitakia safari njema maana hatukuweza kuonana.
Kingine kuhusu familia yetu, tunapendana sana, lakini kila mtu na mambo yake, yaani tunaweza kukaa siku nzima tusionane, mtu ambaye tulikuwa tunamuona ni Giana tu maana huyu ndo kila kona ya nyumba yupo.
HUU NI MWANZO TU.......
ITAENDELEA.....
GIANA (My choice) 🥰
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 02
SONGA NAYO.....
Zilipita siku mbili na hatimaye nilifanikiwa kumaliza majukumu yangu yaliyonipeleka mwanza, na hatimaye niliweza kurudi nyumbani.
Ikiwa ni siku ya weekend nilirudi nyumbani Na nilichoka sana, yaani safari nzima nilikuwa nawaza tu kufika nyumbani lakini pia kulala sana, maana sikuweza kupumzika kutokana na majukumu niliyopata uko.
Jambo zuri ni kwamba, kazi niliweza kumtumia boss kupitia mtandao na ilikuwa powa nikapatiwa kalikizo ka week moja tu
Sema kwa safari hii Chris mimi kazi ya ifisi nilijua kuifanya bwana nilifanya kazi nzuri sana mpaka boss mwenyewe akawa aamini kama ni mimi.
Nilifika nyumbani na kumkuta Giana akiwa peke yake nyumba nzima.
"Karibu sana pole na uchovu " Giana alinikaribisha.
"Asante " niliitika na kuanza kuitilia.
"Mama, mama, we mama grace " niliita mfululizo na Giana alikuwa akiniangalia mwisho akaniambia.
"Utapiga kelele mpaka kesho hakuna mtu, wote wametoka "
"Wanatokaje na niliwaambia kuwa narudi na nina zawadi zao jamani " nilijikuta tu nikilalamika.
"Chris bwana, unavyolalamika utazani walipoenda uko awarudi tena, au labda hizo zawadi zitapotea " alizungumza Giana.
"Oooh uko sawa, wacha nimapumzike,.please kusiwe na usumbufu kabisa nimechoka mno " nilimwambia.
Moja kwa Moja nikaenda chumbani kwangu, walahi chumba kilikuwa kizuri sana sana, yaani Giana alijua kukiweka sawa kwenye kipindi iki ambacho nilisafiri hakukuwa ata na vumbi.
Kwakuwa nilichoka mno nilichofanya ni kuvua viatu kisha nikapanda kutandani, sikuchukia ata dakika 10 usingizi ukanichukua, nililala kama mzigo na nilikoloma kama trekta.
Nilikuja kustuka ikiwa ni usiku ilikuwa kama majila ya saa 2 hivi hapo sasa ni minyoo tu ndo ilikuwa ikipigana tumboni kwangu.
Niliinuka chapu na kutoka nje, sema giana anajua majukumu yake, nilikuta meza ya chakula ushapendeza, yaani tayali chakula kiko mezani.
Sikuwa ata na mtu wa kumsubili kwa Mara ya kwanza nilipakua chakula na kukaa kwenye meza hiyo ya chakula.
Niseme kuwa mimi na mdogi wangu grace, tuliacha kukaa kwenye meza ya chakula tangu siku baba alipoondoka na kwenda kwenye familia yake.
Mama yetu amekuwa mtu wa kupiga kelele na kutusihi sana kuhusu kukaa kwenye meza ya chakula lakini alishindwa na yeye akajikuta askichukua chakula na kwenda kulia chumbani.
Hii hali ilimtesa sana Giana ambaye alipata kibarua cha kuwa anafata vyombo kwenye vyumba vyetu.
Yaani akisema asahau na sisi ndo tukishashiba inakuwa imeisha, kwa upande wangu naweka zangu uvunguni na akuna kitu utanifanya.
Nikowa naendelea kula alikuja Giana akiwa ameshavalia mavazi yake ya kulalia, mavazi fulani hivi daaah nilijikuta nikimuangalia vizuri sana.
"Unawaza nini ??" Aliniuliza Giana baada ya kuona kuwa nimeganda tu.
"Ooooh hapana sina, hivi hawa bado awajarudi??" Niliuliza.
"Bado, lakini pia waliniaga na kuniambia kuwa watachelewa kurudi"
"Hii familia sasa " nililalamika.
Giana akapita zake kushoto na kwenda jikoni kuendelea na shughuli zake.
Niliongia jikoni na kumkuta Giana akijaribu kusafisha fliji ambalo lilikuwa limenwagikia juice.
Niwaambie tu mimi ndiye niliyemwaga juice ndani ya fliji, ila kwakuwa uvivu ni jadi yangu nilifunga fliji pasi na kusafisha.
"Ulitaka hii juice iendelee kusambaa kwenye fliji sio ??" Giana aliniuliza, na huyu ndo giana ninayemjua mimi.
"Mambo madogo unayafanya yanakuwa big dear sana, acha zako giana " nilimwambia.
"Chris unachukulia kawaida sana hizi kazi za nyumbani si ndio ? Ungejaribu ata kunionea huruma basi "
"Umeanza yaani umeanza, unatafutaga maneno tu ili uweze kubishana na Chris sio, nikuambie kuwa sijajiandaa binti" nilimwambia na kuweka vyombo vyangu vichafu kwenye sink
"Ni kwamba utaki kuambiwa ukweli tu, sasa unachafuaje sehemu na kuacha kama ilivyo ? Weeeh muds wote kila kitu uambiwe kama mtoto mdogo kweli ".
"Eeeeh nyumbani kwangu kumewaka tena si ndio ??" Ilikuwa ni sauti ya mama ambaye ndio kwanza alikuwa amerudi.
"Si huyu Giana sijui anajikuta nani, ananifokea itazani ananimudu sana, kumwaga tu juice kidogo analalamika kama kitu gani " nilianza kujielezea.
"Unajua nini, Chris na grace mnaonaga shughuli za nyumbani ni za kawaida sana, sasa naanza na wewe week hii ambayi hakuna auendi kazini shughuli zote ni zako, Giana itapumzika binti yangu "
"Sawa tu kwani kuna shida gani, yaani vikazi hivi ndo vanishinde " nilikubali mwenyewe nikiamini kuwa ni kazi za kawaida sana.
"Saa 2 kamili kesho asubuhi chai iwe tayali kwenye meza ya chakula " alizungumza mama.
"Limeisha ilo, yaani kesho ndo utajua huyu Giana uwa anajilegeza tu "
"Sawa, eeeh nambie mtoto wangu za utokako ??"
Mama aliniuliza uku akinisogelea na kunikumbatia kijana wake, maana tangu nimerudi atukuwa tumeonana.
Niliingia chumbani kwangu na kuchukua zawadi nikampatia mama yangu, usiku uliingia sana kila mtu akaingia chumbani kwake, mimi sikuwa ata na usingizi kutokana na kulala sana musa niliorudi.
Nilivuta simu yangu na kumpigia baby wangu, niwaibie siri, nadate na binti wa boss wangu, katoto fulami hivi pisi ya kwenda.
Mimi na baby wangu tunapendana sana, na yeye ndo aliniunganisha kazi iwa baba yake.
"Hi baby " nilizungumza baada ya yeye kupokea simu.
Tulipiga story pale furaha kama zote, mwisho tuligaba na kulala.
ITAENDELEA........
GIANA (My choice) 🥰
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 03
SONGA NAYO.......
Asubuhi na mapema niliamka na kuanza shughuli zangu ambazo nilimuaidi mama kuwa nitafanya.
Nilianza na kifuta vumbi, nikadeki, yaani nilifanya shughuli zote za nyumbani niliandaa kifungua kinywa kabisa na niliwai sana kumaliza.
Sawa nilimaliza kazi zote lakini kuchoka sasa, kwanza maumivu ya mgongo jamani uwiiiih nilihisi kama mifupa ya mgongo inataka kuchomoka hivi.
Ukikaa chini na kuinuka unaona kama kiuno sio chako 😂🙌🏿 nyieeeeh ila sikuacha ubishi, niliona uwenda labda naumwa tu lakini sio kwaajili ya kazi.
Nilipata kifungua kinywa kisha nikarudi zangu ndani maana niliamka mapema Sana hivyo nilikuwa na usingizi lakini pia nilichoka sana sana.
Sikukumbuka ata kuoga, kiuno kilibaki kikinichoma Choma tu, nilichofanya ni kujitupia kitandani AC nikaweka ya kitosha ili nipigwe na baridi manaa ni kama joto lilikuwa Kali sana.
Majila ya saa 6 nilikuja kushtuka baada ya kuamshwa na Giana.
"We nawe nini ? Tangu lini unaniamsha ??" Niliamka tu na kuanza kumfokea.
"Umelala ukiwa unamuoga Giana au ? Maana aiwezekani kuamka na kuamka tu unaanza kumfokea giana wa watu, eeeh imekuwaje ?? " Giana alinijibu.
Kwakweli nilijistukia maana alikuja tu kuniamsha, nikawa mpole na kumuuliza.
"Umeniamshia nini ??"
"Mama anakuita "
Giana ameshazoea kumuita mama yetu, mama na ndio utaratibu wa mama yetu yaani mama binti wa kazi akija lazima amwambie niite mama.
"Nakuja " nilijibu na giana akatoka nje.
Niliinuka kwa uchovu sana, yaani mwili mzima unaniuma, nyieeeeh mnaochukulua uangalifu kwa kazi za nyumbani niwape maua yenu.
Moja kwa Moja nikaingia bafuni kwani sikuwa nimeoga tangu nilipoamka.
Baada ya kumaliza kuoga nikatoka na kwenda kumsikiliza mama, nilifika na kumkuta mama akiwa sebuleni kavimba hatari kwakuwa nilichelewa kuitikia wito wake.
"Shikamoo mama " nilimsalimia.
"Marahaba, unalala baba unataka chakula cha mchana tule saa ngapi ??" Mama aliniuliza.
Nikiangalia saa ilikuwa ni saa 7 kasoro.
"Napika sasa hivi mama usijali, naivisha soon niamini mimi"
Mama alibaki akiniangali tu nimavyojiongelesha, nilishika njia na kwenda jikoni, nikaroa mchele na kuwek kwenye ungo, ile nafungua fliji tu, hakukuwa ata na mboga ya aina yoyote ata nyanya amna.
Nilichoka kwakweli, na hii niliona asubuhi nikasema nitaenda kununua au nitamtuma giana ila nilipoenda kulala ndo nikasahau kila kitu 🥹.
Nilitoka nje chap nikawai chumbani kwangu nikachukua pesa ili kuwai sokoni, yaani muda huo natililikwa na jasho tu, unaweza ukasema kuwa nilimwagiwa maji.
Nikaona nikichukua gari hapa nitachelewa, mpaka kufika sokoni kutafuta sehemu ya paki hapa na hapa, nikawai kuchukua boda tu na kweli nilifanya haraka haraka.
Mpaka saa tisa kasoro chakula tayali kilikuwa mezani, sawa chakula kiko mezani lakini mimi niko Hoi, mtu akiniona anaweza akasema Labda naumwa au nimezidiwa kumnee ni kazi tu za nyumbani.
"Hivi mama grace yuko wapi ??" Nilimuuliza mama.
"Ajaliaga kwani ? Wameenda zanzibar na rafiki zake tangu jana "
"Sema mama grace unamuachia sana oooh uwe unamkataza vitu vingine " nilimwambia.
"Mmmh wewe tena, unajua Chris ujawai kueleweka, si ni wewe ndio uliniambiaga nimpe uhuru ? Leo tena unaniambia kingine nifanye kipi ? Halafu uwende kwa baba yako kule "
"Nikafanye nini ? " niliuliza kwa jazba.
"Yaani unasahau mpaka siku ya muhimu ya baba yako, si ni siku yake ya kuzaliwa na mama yenu ameandaa ka party kidogo " alizungumza mama.
Yaani mama sijui sio binadamu wa kawaida yaani yeye anachukulia powa kila kitu.
"Sitaenda " nilijibu na kwakuwa nilishamaliza kula nikainuka na sahani yangu na kupeleka jikoni.
Nikiwa nimesimama kwenye sehemu ya kuoshea vyombo, giana alikuja na kunishika kwenye bega na kusema.
"Hasira yako usiipe nafasi na ukasahau siku nzuri ya baba, yako achana na kila kitu weka hasira pembeni na yafanye maisha yako kuwa na furaha" alizungumza Giana kwa utaratibu sana niligeuka na kumuangalia.
"Ujawai kupitia kitu kama iki giana na uwezi kuelewa, mama yangu anajikaza tu ila kwa mimi namchukia sana yule mwanamke na baba pia"
"Nimepitia kitu kama iko, Chris mimi niliacha kusoma nikiwa darasa la 5 hii yote ni kwaajili ya baba kututelekeza na kwenda kuanza familia Mpya, na sisi hatukuwa na pesa kama ninyi, baba akujali kuhusu sisi na kwakuwa mimi ndo nilikuwa mkubwa nikaacha shule na kuanz kufanya kazi za ndani mpaka sasa unavyoniona " alizungumza Giana na alionesha kuumia sana akageukia pembeni.
"Bado Mungu akaona haitoshi akanipa jaribu la msamaha, baba yangu aliugua sana na familia yake mpya kumtelekeza mimi na mama yangu tukamchukua na kumuuguza na ndio akafia kwenye mikono yetu, baada ya baba kufariki ndugu wa baba lawama zote ni juu yetu sijui unanielewa " alilalamika giana.
Daaah kwa namna moja au nyingine nilimuonea huruma Sana sana, kuna nilianza ata kujilaumu kwanini uwa namfokea mtu mwenye maumivu makali.
"Basi sawa, nitaenda lakini nitaenda na wewe " nilimwambia.
"Mmmh mama awezi kukubali " alijibu giana.
Nilitoka na kwenda sebuleni ambapo mama alikuwa amekaa akiangalia taarifa ya habari.
"Naenda mama, lakini kitaenda na giana kama kutakuwa hakuna kazi ya kumuhusu " nilimwambia mama.
"Kikubwa ni wewe kwenda tu " alijibu mama.
Ni wazi kuwa mama alikubali, nikarudi jikoni na kumwambia Giana kuwa mama amekubali.
Tukajiandaa siku hiyo Giana alipendeza sana, tangu afike sikuwai kumuona akivaa suruali lakini kwa siku hiyo alivaa na ilimpendeza sana.
"Unajiwekaga kama mzee kumbe una mavazi ya kukupendeza " nilimwambia tukiwa ndani ya gari.
Giana alicheka na kujiangalia tu Kisha akajibu.
"Aaah nilinunuaga tu hii Moja, nyumbani kwetu mama anakataza sana hata mavazi kwakweli.
"Mmmh, jua tu mavazi yamekupendeza, unaweza ukavaa tu kwani mama yako anakuona uku '
Story kati yangu na Giana zilinoga sana, niliona ni msichana fulani hivi simple sana na ni rahisi kuishi nae.
Tulifika kwa baba, na baba alifurahi sana kuniona yaani akufikilia kabisa kama nitafika maana anajua kabisa nina chuki kubwa dhidi yao.
"Waooooh jamani Chris wangu " ilikuwa ni sauti ya mke wa baba, alikuja na kutaka kunikumbatia nilitaka kukataa lakini giana alinipatia ishara hivyo nikamkumbatia.
"Karibuni Sana sana, yaani tulikuwa tunaangalia uku na uku Kama utakuja, maana mama yenu amesema kuwa grace hayupo dar " alijiongelesha mama yetu wa kambo.
Kiukweli sikuweza kushindana na hasira zangu, nilishindwa kuvumila nilichofanya ni kumpa baba zawadi zake na kuaga kwq kusema kuwa kuna sehemu natakiwa kuwai.
Niliingia kwenye gari nikiwa na hasira sana giana hakuwa mbali alifanya kazi nzuri kabisa ya kunituliza.
Sijui giana alikuwa ananitaka 😂🙌🏿 maana ananibembeleza kama ananipapasa hivi, anasahau mimi ni mwanaume lijali oooh.
Sijui nini kilinikuta gafla nilijikuta nikimvuya Giana vizuri kabisa na kuanzs kumkisi ajabu akunisukuma akatulia ahahaha alikuwa ananitamani huyu sio bure......
NAKUJA.....
GIANA (My choice) �
SEHEMU YA: 04
Tulikisi kwa muda kama wa dakika tano hivi, ndipo akashtuka na kujitoa karibu yangu kwa aibu akashuka kwenye gari na kwenda kusimama akiwa anaangalia nje.
Nilijikuta nikitabasamu tu, kiukweli mimi napenda sana wanawake wenye drama na hii aliyofanya Giana ni drama ambayo imenivutia sana.
Nilishuka polepole na kwenda kumuangalia alikuwa anafanya, nilipomsogea mbele yake haraka akafumba Macho yake eti madai anaona aibu.
"Kwahiyo hautaondoka na mimi ??"
Nilimuuliza baada ya kuona kuwa
ananikwepa sana.
"Yaaah nitapanda daladala " alijibu.
"Ouk tutaonana nyumbani" nilimjibu kisha nikaeuka ili kurudi kwenye gari.
"Tutaenda wote lakini nitakaa nyuma
"alizungumza. Nilicheka tu.
Kwa pamoja tukapanda gari uku yeye akikaa nyuma, bado sio tu kukaa nyuma alinilaza ili nisiweze kuangalia sura yake kwa kutumia kioo cha pale juu.
"Giana " nilimuita.
"Usiniongeleshe bwana " akanijibu kwa kunifokea.
"Khaaah Giana nipo serious ujue, wewe ni mama kijacho au ? Maana tabia zao zote naziona kwako" nilimuuliza makusudi.
Hapo aliinuka haraka na kunijibu.
"Ushindwe na ulegee, yaani saa hizi nikawe mama kwa maisha gani ? Eeeh tena shindwa "
"Khaaah ila weeh umezidi sasa kosa langu nini ? Me si nasema ukweli, na bado unaendelea kunihakikishia kuwa wewe kweli ni mama kujacho " niliendelea kuchokoza ili asijilaze na aongee na mimi.
"Nishushe " akanifokea .
"Gari yangu aisimami kama unaweza vunja kioo halafu ruka " nilimwambia uku nikicheka.
Kwa kweli kwa muda huo Giana alikuwa akinichekesha sana sana, hayo macho yake na mdomo alivyokuwa akiutunisha na kuupishisha nilicheka mno.
"Unacheka nini ? Chris unajua wewe ni milifi sana ningekuwa na nguvu ningekupiga mpaka ushangae ni vile tu sina nguvu "
"Aaah itakuwaje kama nitakuachia unipige utakavyo "
"Nitahakikisha nyumbani kwenu wanaweka matulubai "
Eeeh nilishtuka kwakweli na gafla nikasimamisha gari na kumuuliza. "Kwamba utaniua ??" Kabla ajanijibu nilishtushwa na sauti ya oni ya gari zilizokuwa nyuma yangu maana nilisimama bila sababu maalumu.
Niliwasha gari na kuanza kuondoka kwa mwendo wa polepole, muda huo giana alikuwa akicheka mpaka anakauka niliwaza huyu anacheka nini sasa.
"Ujanja mwingi na unaogopa kufa mbwa wewe, sio kwa kushtuka uko " alizungumza giana uku akiendekea kunucheka.
"Unajua wewe sio mzima" nilimwambia
"Hongera wewe uliyemzima " alinijibu.
Tuliingia mahali tukala ice cream, na kununua vitu vingine kwaajili ya kwenda navyo nyumbani kwakweli niliinjoy sana siku hiyo.
Tulifika nyumbani uso kwa uso na demu wangu, mwenyewe alikuwa bize alipiga story na mama aliponiona tu akainuka na
kunikimbilia akanikumbatia.
Shida ya Briana bwana uzungu mwingi, aangalii yuko wapi tuko na nani anachojisikia tu anafanya, alinikisi mdomoni walahi nikiona aibu kwani mama yangu alikuwepo.
"Nilikumisi sana, muda wote nilikuwa naangalia mlangoni kwamba utakuja saa ngap "
alizungumza briana ambaye ni mpenzi wangu.
"Kwani mama akukuambia kuwa nimeenda wapi ??" Nilimuuliza.
"Ameniambia na ndio maana nikawa
nakusubilia kipenzi, ndo ulitoka na huyu kijakazi wenu "
Walahi Briana ajui kabisa kuchunga mdomo wake analopokaga tu, analojisikia kuzungumza yeye linamtoka tu.
Mama yangu ni mtu mzima na anajielewa sana alichoganya ni kunyanyuka na kwenda chumbani kwake.
"Leo nitalala hapa ujue " alizungumza Briana.
Nilishangaa maana hakuwa kulala ata siku moja a mara nyingi uwa anasema kuwa baba yake ni mkali mno awezi kulala nje tena kwa mwanaume ambaye bado awajatambulishana majumbani kwao.
Kwa upande wangu, nyumbani kwetu nilimtambulisha Briana kama mchumba wangu, na mama alimpokea.
Kwa upande wa baba yake anajuaga tu kuwa nimesoma na Briana na Ni marafiki tu wa karibu sana.
Nimekuwa nikimuomba tupige hatua lakini amesisitiza kusema kuwa muda bado na nisiwe na haraka.
Nilimshika mkono na moja kwa moja tukaenda chumbani muda huo, Giana alisimama tu sebuleni akishangaa shangaa.
Mwaya Giana wa watu amerudi na mimi akiwa na furaha sala lakini amefika nyumbani amepooza tena.
"Una uhakika kuwa utalala hapa na baba yako Atoleta shida ??" Nilimuuliza.
"Yaah awezi kuleta shida niamini mimi " alijibu Briana uku akijitupia kitandani.
Nilisogelea kabati na kuaanza kubadili nguo na kuvaa mavazi yangu ya kushindia nyumbani, mimi nikiwa nyumbani ni mtu wa vipensi, yaani vipensi mwanzo mwisho.
"Niko jikoni hapo " nilimwambia Briana.
"Jikoni ? Yaani unaenda jikoni na kuniacha mimi hapa ? "
"Ndio maana nimekuaga sasa unaweza kunifata au kunisubili "
"Unaenda kufanya nini ??" Aliniuliza.
"Aaah unazingia Briana we jana si nilikuambia kuwa week yote hii kazi nafanya mimi kupika na kila kitu "
"Utanikuta uku, nacheza zangu game "
Nilishuka zangu chini na kwenda kuanza kupika, nilikutana na Giana akianza kuandaa andaa viungo nikamuuliza.
"Mbona unafanya kazi sio yako ??"
"Nikajua utatumia muda kuwa na mgeni ndio maana nikaona nisaidie, na nimemwambia mama pia, so usijali " alijibu Giana lakini hakuweza ata kuniangalia usoni.
"Usijali nitafanya majukumu yangu.
Kiukweli ofa yake niliipenda sana na
nilitamani kupumzika, lakini moyo tu
ulinisukuma kuwa natakiwa kufanya kazi.
Lakini ndani ya siku hiyo moja niliweza kujua ni jinsi gani kazi za nyumbani ni ngumu na zinachosha ni kazi ndogondogo sawa lakini mmmh.
"Kwahiyo unataka kupika mwenyewe ??" Giana aliniuliza.
"Nafikili kama tutasaidiana itapendeza zaidi" nilijikuta nikiinjoy sana uwepo wa Giana.
Tukaanza kupika kwa pamoja pale, story za hapa na pale zikiwa zinaendelea.
"Hivi Giana ni aibu gani umewai kuipata shuleni na hautakuja kusahau ??" Nilimuuliza.
"Mmmmh, we nawe na maswali yako aaah aibu yangu walahi ni kujikojolea darasani tena mbele ya darasa" alijibu.
"Ebu subili kwanza, yaani ilikuwaje ??" Nilimuuliza.
"Halafu nilikuwa darasa la Tano, yaani darasa ambalo niliacha shule, ilikuwa ni muda wa somo la English, sasa bwana mwalimu ameandika mambo yake
unaoni akataka tujaze, darasa Zima nikawa wa kwanza kuchaguliwa, muda huo kitu ambacho naelewa shuleni ni what is your name ��sijui
kama unanielewa, so nilisogea mbele kwa wasiwasi, nikakosa cha kujibu nikaanza
kuzomewa, na kujikojolea hapo hapo na mizomeo ikaongezeka � "
Kwa pamoja mimi na Giana tulicheka sana sana yaani daaah.
"Imagine unapelekwa nyumbani na wanafunzi wenzio wakiwa wanakuimbia kikojozi, eeeh kikojozi eeeh " alizungumza giana akiwa ameshika kichwa na alikuwa akipiga piga kwenye bakuli.
Na mimi sijui nilipatwa na nini nikavuta mwiko na kuanza kupiga kwenye sufulia na kwa pamoja tukawa tunaimba kikojozi ��.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote