Follow Channel

Honeymoon In London

book cover og

Utangulizi

MIMBA YA LAZIMA...

Baada ya benedicto kwenda fungate na mke wake ughaubun, mke wake anahadaika na nchi za watu, anaacha kumjali mume wake na benedicto anakuwa mtu mwenye mawazo Sana mpaka anapokutana na bibie annasia ambae alimpenda kutokana na ukarimu wake na namna anavyoongea kwa busara..
Benedicto anajikuta anaacha kabisa kumfikiria mke wake na kushughulikq na annasia , hisia zinamsumbua benedicto na kujikuta anamuingilia annasia bila ridhaa yake na kumpa ujauzito ambao ulimpa nguvu benedicto ya kufuatilia talaka ya ndoa yake ya muda mfupi ili amuoe mama kijacho wake...
Unajua Nini kilitokea usikose simulizi hii ya honeymoon in London

HONEYMOON IN LONDON 1
HUSQER BALTAZAR

Ndoa kubwa ilufungwa nchini Kenya kwenye kanisa kuu la kipentecost na baada ya hapo maharusi walienda ukumbini kwaajili ya kusherehekea siku yao adhimu, na harusi hii ilikuwa ni harusi ya watu wawili ambao walikuwa wanatoka kwenye familia mbili maarufu sana nchini hapo, ambapo mwanaume ambae alikuwa anafahamika kwa jina la benedicto marcus ambae alikuwa ni kijana wa kipekee kwenye familia ambayo ina miliki sheli zote kubwa nchini hapo na pia walikuwa wanamashamba makubwa sana ya mahindi na alizeti na kupelekea kufungua kampuni kubwa ya mazao ambayo walikuwa wanaiuzia serikali na mwanamke ambae anafahamika kwa jina la Marry Michael ambae alikuwa anatoka familia tajiri iliosimamia miradi mikubwa ya barabara na maji nchin hapo…

Baada ya ndoa kulikuwa na kumbi tatu za kufurahia ndoa yao, kwamba kuna kumbi ambayo walikuwa wanakaa watu wenye hadi ya juu sana, na kumbi ya pili walikuwa wanakaa watu wa maisha ya kati na kumbi ya tatu ambayo walikuwa wananchi wenye kipato cha chini, na hawakuaandaa kumbi hizi kwa ajili ya kumtenga mtu, ila walifanya hivyo kwa sababu walitaka watu wakae na waburudike pamoja na watu ambao wanaendana nao ustaarabu lakin katika kumbi zote kulikuwa na chakula na vinywaji vya kutosha na watu walikula na kusaza, na kama ambae alitaka kuleta familia yake nae aliruhusiwa…

Baada ya sherehe kubwa basi walikodi hotel mtandaoni ambayo ilikuwa haipo nchini kwao, walitamani kubadilisha mazingira na kukodi hotel jijini London , ilikuwa ni hotel ya kifahari sana na wkapanga kukaa jijini London kwa angalau mwezi mmoja, na usiku huo huo wakaenda kukata ticket na safari yao ikaanza usiku huo huo…

Safari ilikuwa ndefu nay a kuchosha lakini huduma kabambe za ndege waliopanda angalau iliwapunguzia mzigo wa safari na kuhisi unafuu kwenye safari yao…

Walipofika jijini London moja kwa moja walifikia kwenye hotel ambayo waliikodi mtandaoni na walishatoa maagizo kuwa chumba kiandaliwe kwa ajili ya maharusi, na ndivyo ilivyokuwa….
Ila mary ni kama alizuzuka na ukilinganisha hakuwahi kufika ulaya, hivyo kuna namna mji wa watu ukampagawisha, ilikuwa ni siku ya fungate ila hakutaka kulala na mume wake, alitaka usiku huo huo atembezwe sehemu mbali mbali za starehe za mji huo, akidai hawezi kulala bila kufika, kitu ambacho kilimshangaza na ,kumchukiza sana benedicto, alijua wanakuja kukaa pamoja na kufurahia fungate yao, ila mambo yalibadilika na kuwa tofauti kabisa na namna alivyofikiria…
Kwa kuwa mkewe alikuwa na shauku kubwa hakutaka kubishana nae, alikubali ila hakupenda, akajua labda ni ushamba wa kufika ughaibuni, akatoka nae ila wakati wanatoka pia alishangaa sana, maana mke wake alivaa nguo za ajabu sana, ikabidi amuulie kwa mshangao na kusema “ mke wangu ndio unatoka hivyo?…
“ kwani kuna shida gani, huku ni ulaya na sio Kenya bana, unataka nionekane mshamba kwa kuvaa manguo makubwa makubwa na wakati hata wewe mwenyewe un ajua kuwa mimi ni mtoto wa mjini, na hakuna kitu hata kimoja ambacho sijawah kufanya na hata haya mavazi niliyoyavaa umeshawah kuniona mara kadhaa nikivaa, sasa tatizo liko wapi…

“ hapana mke wangu hauwezi kutoka nje hivyo, kumbuka ulikuwa unavaa hivyo ila ulikuwa unavaa ndani ukiwa na mimi na sio kutoka nayo nje kama unavyofanya sasa hivi, akaanza kulalamika benedicto na kutaka kumzuia mke wake asiondoke mpaka abadilishge alichokivaa…

Ila mary hata hakujali akampiga kikumbo mume wake kisha akaondoka zake, akiwa amevaa kitop ambacho lilikuwa kinaonesha tumbo lake na sehemu kubwa ya maziwa wake, na sketi fupi nyeusi ambayo ilimbana vizuri maumbile yake na iliishia kwenye mapaja yake , na viatu vyake virefu pamoja na kapochi flani hivi cha kichokozi…

Benedicto alikasirika sana na kiukweli hakutaka kabisa kuongozana na mkewe akiwa kwenye mavazi kama yale, akaenda chumban na kujitupa, chumba cha fungate kikageuka na kuwa chumba cha mawazo, yale mapambo na vinywaji havikuwa na maana tena kwa benedicto kwa maana asingeweza kufuraha chochote kile akiwa mwenyewe na wakati ilikuwa ni siku maalumu kwake na mkewe…

Alijaribu kumpigia simu mke wake mara kadhaa maana aliona sio salama sana kuwa nje pekee yake usiku kama ule ila simu yake hata haikupokelewa kabisa, ilikuwa inaita mpaka inakata bila majibu yoyote yale, alishikwa na hasira na kutamani kwenda kumfdata mke wake, ila hata hakujua kuwa anaenda kumpata wapi kwa wakati ule, alishindwa kulala kabisa na kitu pekee ambacho alikuwa anaweza kukifanya ni kupiga simu mfululizo na kutuma sms akiamini kuna wakati simu yake itapokelewa na sms zake zitajibiwa, ila haikuwa hivyo…

Mlango unakuja kugongwa saa mbili asubuh, akaamka kichovu akijua ni muhudumu ila alipoenda kufungua mlango akakutana na mke wake akiwa amelewa njwi, marry akapitiliza moja kwa moja mpaka kitandani na kujitupa kisha hazikupita dakika nyingi akapitiwa na usingizi…

Benedicto alikuwa na hasira sana, alitamani kumuuliza maswali mengi sana, alitaka kujua alikuwa wapi usiku wote na kwanini alikuwa amelewa kiasi kile, alishangazwa sana na tabia mpya za mke wake maana kuanzia anamfahamu hakuwah kumuona hata kwa bahati mbaya akishika chupa ya pombe, ila hakujua kuwa mke wake alianza kunywa lini…

Alipoangalia simu yake akakutana na packet za kondom pamoja na boksi la sigara, alishikwa na hasira sana na kuona kuwa akiendelea kukaa pale anaweza kuandikiwa kesi ya mauwaji bila yeye kutaka, hivyo akatoka nje akiwa na lengo la kupata hewa safi tu hata kidogo…

Ila hata nje ya hotel hakukuwa sehemu rafiki sana kwake, maana alikuwa amelelewa kwenye maadili ya kiafrica sasa swala la kukuta mwanamke akiwa amevaa kisidiria na kichupi lilikuwa kama mateso kwenye macho yake, akaamuwa kutoka kabisa nje ya ile hotel, na akiwa anatembea tembea akakutana na bango kubwa likiwa limeandikwa “ WELCOME TPO AFRICAN TASTE” kwa mawazo yake akajua labda ni chakula, ila alipoingia akashangaa anakutana na watu weusi kama yeye na wazungu wa chache sana, na kulikuwa kuna karioki, ambayo ilikuwa inaongozwa na mwadada mmoja ambae alikuwa anaonekana fika ni mtanzania kwa namna aliovyokuwa anaongea Kiswahili fasaha sana kwenye nyimbo yake ambayo alikuwa akiimba wakati huo…

Alikuwa anaimba nyimbo moja ya mwanamuziki recho ilikuwa inaitwa upepo..
Benedico alikuwa anaisikiliza kwa makini sana, na sauti tamu ya binti huyu ni kama alianza kutuliza hasira zake, na kuuhisin upepo wa sauti yake unapuliza kwenye moyo wake na kumpa amani ambayo hakutegemea kabisa kama angeweza kuipata kwa wakati ule, akiwa anawaza mara akashangaa kimya kinatawala na alipomuangalia Yule bint ambaye alikuwa anaimba hakumuona, akajikuta anatoka nje kumtafuta, maana alihisi angalau anaweza kumpa kampani kwa kipindi ambacho mke wake anamchemsha kichwa na alipotoka nje, akamkuta Yule binti ameketi nyuma kabisa ya jengo lile akiwa analia…

Akasogea mpaka alipo kisha akamuuliza “ unalia nini mrembo?...
Yule bint alishtuka sana kisha akainua uso wake na kusema “ kumbe unajua Kiswahili?...
“ ndio najua ila sio sana, maana nimetokea nchini Kenya na wewe umetokea wap[i?..
“ arusha Tanzania , akajibu Yule bint..
“ umekuja london kwa sababu gani? Akauliza benedicto na Yule bint akaangalia chini kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ nasomea engeniaring in irrigation nilipata mdhamini wa kunisomesha ndio maana nimefika huku, na wewe kilicho kuleta huku ni kitu gani?, akauliza Yule bint..
“ nimekuja kwa ajili ya fungate, maana nimefunga ndoa siku chache nyuma nikaona fungate yangu nije kuilia huku, akasema benedicto na Yule bint akatabasamu kwa ishara ya kumuelewa..
“ naitwa annasia, akasema yul;e bint baada ya kuona haulizwi jina..
“ ohhh mimi naitwa benedicto, akasema benedicto na mazungumzo yao yakaanzia hapo, na benedicto alikuwa anajihisi amani sana akiongea na annasia kuliko kukaa na mke wake…

JE NI IPI HATMA YA HONEYMOON YA LONDON NA BENEDICTO NA MKEWE MARRY, NA HUYU ANASSIA HUYU UNAHISI KITU GANI KITAKUJA BAADAE, ACHIA MAONI YAKO TUBURUDIKE…


HONEYMOON IN LONDON 2
HUSQER BALTAZAR

Basi wakapiga soga sana, mpaka mchana ukafika na benedicto akaomba kumnunulia anassia chakula cha mchana na annasia hakuwa na sababu ya kukataa kabisa, basi wakakubaliana kwenda sehemu ambayo wangeweza kupata chakula cha mchana pamoja…
Walifika na kuagiza vya kuagiza na wakaanza kula taratibu huku wakiwa wanaendelea kusomana na kujuana, na mwisho wakabadilishana namba za simu, na benedicto hakuwa anaonesha kabisa kama anataka Annasia aondoke eneo lile, ila nduo hivyo hakuwa na la kufanya…

Sasa benedicto akaenda moja kwa moja mpaka kwenye chumba ambacho alikuwa amekaa mke wake kwa ajili ya fungate, akamkuta anaoga, akapitiliza zake kitandani na kumtumia sms anassia inayosema “ umeshafika chuo..
“ ndio nimefika, vipi mkeo anaendelea je? Akauliza annasia swali ambalo benedict aliona kama ni swali bay asana kwake, ni kama alihisi alijichanganya kumuambia annasia kuwa yupo kwenye fungate, alihisi kama hakustahili kufanya hivyo na hakujua ni kwanini anajisikia tofauti sana na vimaumivu kwa mbali mara baada ya annasia kumuulizia mke wake marry…
Kwakuwa alikuwa anataka kuendelea kuwasiliana nae, basi akajibu kuwa “ ametoka kwenda kunyoosha nyoosha miguu, vipi wewe unaendelea je lakini?...
“nipo sawa, akajibu annasia na story za hapa na pale zikawa zinaendelea kama kawaida….
Mke wa benedicto alioga kisha akaagiza chakula bila kujali kuwa mume wake alikuwa anamuhitaji au laa, na baada ya kumaliza kula aliaga na kusema kuwa kuna sehemu ya muhimu sana anataka kwenda, ikabidi benedicto akae kimya tu maana hakuwa na lakufanya, ila wakati huo aliutumia kuwasiliana na annasia, alikuwa anajihisi mpweke sana, alitaman annasia asiwe na kazi nyingine yoyote ile zaidi ya kuwa karibu nae na kuwasiliana nae tu…

Maisha yakawa yanazidi kuendelea kama kawaida, na mke wa benedicto nin kama ulaya kulimchanganya sana na kusahau jukumu lake kama mke na kilichompeleka huko, akawa ni mtu wa party kila siku, kazi kubwa alikuwa anaifanya ni kubadilisha kumbi za starehe pekee, na hakujali kabisa kuhusu haki zake kwa mume wake na jukumu lake kama mke…

Benedicto alikuwa kimya kwa sababu ni kama alipata faraja kutoka kwa anassia na kukaa kwake London sio kwa sababu ya mke wake ila ilikuwa ni sababu ya annasia, kuna muda alikuwa anataman kuwa angekutana na annasia kabla ya mke wake , alimuona kama mtu sahihi zaidi kwake kuliko hata mke wake, basi walikaa London kwa wiki tatu, siku moja mke wa benedicto hakurudi kabisa pale hotelini, bedicto akajaribu kumpigia ila simu ilipokelewa na mwanaume ambae alikuwa ameonekana kama amelewa sana na kwa sauti ya kilevi akasema “ umeipigia nyama yangu, yaan leo nataka niitie mpaka asubuh, naomba usitusumbiue kama utamtaka wewe utakuja kumchukua baada yangu, kisha akakata simu…

Benedicto akajidharau sana kwa kupiga simu, sijui kwanini hakujua kuwa mwanamke ambae alimuoa ni mshamba kwanza wa maisha na asiejiheshimu, maana haiwezekani kwenda London ndio kumchanganye kiasi chote hicho licha ya kuwa na mahusiano kwa karibu miaka miwili…

Muda wa kurudi nchini Kenya ukafika, ila mke wa benedicto hakutaka akadai kuwa anahitaji talaka maana hawezi kuwa na mwanaume ambae anambana sana kama ambavyo mume wake anafanya, benedicto hata hakubvishana nae, akaenda kumuaga anaassia maana ndio alikuwa kama familia yake na mtu wake wa karibu na kumuacha mkewe London maana kuna muda alikuwa anajilaumu sana kuwa amejichanganya sana kuoa na hakustahili kabisa kufanya hivyo…..

Basi benedicto akarudi nchini Kenya na kumuacha mke wake, ila mawasiliano yake na annasia yakawa yanaendelea kama kawaida, na akajikuta anaumia hata annasia aklienda sehemu bila kumuaga, akajikuta hana raha kabisa kama annasia asi[pomtafuta kila aapopata nafasi, aitamani awe soli au nyayo ya kiatu cha annasia kwa sababu alitamani ajue kila anapoenda…

Benedicto alisahau kabisa kama ameoa na kujiona kama kijana ambae ndio anamfukuzia mwanamke kwa ajili ya kumuoa, na familia zao hazikujua kuwa hakurudi na mke wake, maana kwanza wanakaa mbali nao, na kingine benedicto ni mtu ambae yupo busy sana, hivyo hata suala la kukutana nae kila wakati halikuwa rahisi..

Annasia alikuwa anamaliza mwaka wa mwisho London, na ukaribu wao na benedicto ukawa unazidi kupamba moto, iola wakati wote huo annasia alikuwa anamchukulia kama mume wa mtu hivyo alijiheshimu na kumuona benedicto kama kaka yake tu, na hakutaka jambo lingine lolote lile liendelee kati yao, jambo ambalo halikuwa sawa kwa benedicto maana alishindwa kuuficvha wivu wake kwa annasia, alikuwa akimuhoji maswali mengi sana kuhusu siku yake, na kama akisikia sauti ya tofauti karibu na annasia alikuwa analalamika kana kwamba mke wake kipenzi amemsaliti…

Basi muda wa kukaa London kwa annasia ukaisha na akarudi zake nchini Tanzania ambapo ndipo alipokuwa anaishi kuanzia mwanzo, annasia ni binti ambae ametoka kwenye familia yenye maisha ya kawaida sana, kwa maana hawakuwa na kipato na kwenye ukoo wake yeye ndio alikuwa anaonekana kama msomi wa familia…

Kutokana na ugumu wa maisha aliporudi akaanza kutafuta kazi, ila kama tiunavyojua sio rahisi sana kutafuta kazi maana kwenye nchi yetu wasomi ni wengi sana, na akawa kila changamoto ambayo anaipitia anamshiriksha benedicto, na benedicto alikuwa anamsaidia kwa moyo wake wote, kitu ambacho annasia alikiona kama ni msaada wa kawaida kwa marafiki kumbe ni msaada unaotokana na mapenzi makubwa sana ya benedicto kwake…..

Baada ya malalamiko mengi ya annasia kuhusu kutopata kazi, benedicto akaamua afungue kampuni nchini Tanzania ili amuajiri kipenzi cha moyo wake, na kisha akamtumia fomu ya maombi kuwa akaombe kazi, na ni kama annasia alishakata tamaa ila benedicfto akamsisitiza sana akaombe kazi, mwisho akakubali na kwenda kuomba kazi kwenye kampuni ambayo inahusika na umwagiliaji wa kisasa na uuzaji wa nafaka na mazao mengine ya chakula tu, na alipofanya usaili annasia akashangaa amedpita na siku hio hio akateuliwa kama mkaguzi mkuu wa kampuni kwenye miradi yote ambayo inahusiana na kilimo na mauzo yake kwenye kampuni kitu ambacho kilimfurahisha sana annasia, bila kujua kuwa hakufaulu kwakuwa anajua sana ila ni kwakuwa benedicto alikuwa anataka kuwa karibu yake na hatamani kumuona annateseka…

Baada ya usaili na kukabidhiwa majukum kwa siku ya kwanza, annasia wakati ambapo alikuwa anarudi nyumban alimpigia benedicto na kumuelea furaha yake ya kupata kazi mpya na namna ambavyo anamshukuru Mungu na kumshukuru yeye kwa kumpa moyo na nguvu mpaka akafanikiwa kupata kazi..

Furaha ya annasia ilimpa amani sana benedicto, na kwa namna ambavyo alikuwa anaongea kwa bashasha kubwa na utulivu wa hali ya juu benedicto akajuikuta hatamani annasia akate simu maana kuna namna sauti yake tamu ilikuwa inamburudisha na kumsisimua sana, na kupelekea mpaka mwili wake kupata msisimko wa ajabu na kuyainua maumbile yake na akajikuta anatamani sana annasia angekuwa anaongea akiwa karibu yake na ikiwezekana amburudishe kitu ambacho hakikuwa kina wenzekana maana yeye ndio alikuwa anahisia za mapenzi pekee na sio annasia….

ITAENDELEA…….


HONEYMOON IN LONDON 3
HUSQER BALTAZAR

Basi maisha ya kawaida yakawa yanaendelea kwa annasia, na benedicto akaweka watu wa kiumfuatilia, maana hakutaka kusikia kuwa annasia anakuwa na mwanaume mwingine yoyote yulke zaidi yake, na kuna muda annasia alikuwa anaonekana kama yuko busy sana na kazi, mpaka akawa anakosa muda wa kuon ghea na benedico kitu ambacho benedicto hakuwa anakipenda kabisa, na kuomba apunguziwe majukumu, maana hata kama anatakiwa kufanya kazi kiasi gani ila hatakiwi kuacha kuongea nae, maana yeye ndio faraja yake…

Maisha yakawa yanaendelea na ndoto za benedicto za kummiliki annasia zikawa zinakuwa siku baada ya asiku, na kutamani hata akafanya mchakato wa talaka, maana kuanzia amefika Kenya, mke wake hakuwah kumtafuta hata kwa bahati mbaya, n nafasi yake ilizbwa na annasia mpaka benedicto hakuona tatizo au labda kupungukiwa kokote kule kwa mke wake kuwa mbali nae na kutomtafuta…

Annasia alipewa nyumba na kampuni ambay0 ilikuwa n9 karibu na ofisini, na alipewa kwa makusudi kabisa maana uvumilivu wa kusubiri kwa benedicto uliisha kabisa, na akawa anatafuta namna ya kukaa karibu na annasia, maana kama mwanaume basi amevumilia sana, na sio rahisi kabisa kwake…

Huku ambapo benedicto anawazaz mbinu za kummiliki na annasia anaanza kuzoeana na kijana mmoja ambae walikutana kwenye semina ya kilimo ambae alikuwa ni meneja kwenye kampuni ya asas inayohusiana na kuuza maziwa, na kuanza kuwa marafiki, na kama tunavyojua kila ambacho annasia anakifanya basin i lazima benedocto akijue, na ndio hivyo ilivyokuwa, akapewa taarifa na watu wake kuwa annasia ameshaanza kuwa karibu na mwanaume flani hivi, kitu ambacho kilimuumiza sana benedicto na kupanga kwenda nchini Tanzania akaishi na annasia wake maana aliona kama akizidi kuchelewa chelewa huenda akaja kupata mwana sio wake siku moja……

Siku moja akampigia simu annasia na kumuambia kuwa anakuja kumsalimia, na annasia hakuwa anabisha kabisa, akakubaliana nae, kuwa aje tu, bila kujua kuwa benedicvto anataka kuja kukaa nae nyumban kwake pamoja na kumzuia kila mwanaume anaejaribu kumsogelea annasia basi akae mbali na mwanamke wake, hapo annasia hajui na hajawah kuhisi kuwa benedicto anampenda, maana alimchukulia kama mume wa mtu na akawa anamuheshimu sana kuliko kawaida…

Majukumu ya benedicto nchini Kenya hayakumruhusu kuondoka mapema kama ambavyo alifikiria na badala yake akatakiwa kukabidhi kila kitu kwa angalau mwezi mzima, jambo ambalo lilikuwa linamuwazisha sana benedicto kwa sababu ukaribu wa annasia pamoja na meneja wa asas bwana kelvin lymo ulikuwa unazidi, kitu ambacho kilikuwa kinampa mashaka makubwa sana benedictona kuhisi huenda tonge lake anaweza kupokonywa muda wowote ule na kusahau kuwa hakuwa amempa talaka mke wake…….

Kazi kwa upande wa benedicto hazikuwa zinaenda kabisa, kwa sababu alikuwa anaambiwa kuwa annasia anazidisha mzoea na wakati alikuwa ameshajihesabia kuwa annasia ni wake, tena wa kwake pekee yake, alifanya harakati za kuja Tanzania haraka iwezekanavyo ili asiendelee kupoteza na muda, na hatimae aje kuambulia mwana sio wake tena…

ITAENDELEA….


HONEYMOON IN LONDON 4
HUSQER BALTAZAR

Siku moja akampigia simu kisha akamuambia kuwa atafika nchini Tanzania siku moja mbele, na hakuwa na mwenyeji wala hana pa kufikia na kumuomba anassia kama ana nyumba kubwa basi afikie kwake, kwa kuwa hajawah kufika Tanzania na hajui hata anaanzia wapi…

Annasia akakubali maana kwa kipindi chote ambacho alikuwa amemfahamu benedicto hakuwah hata mara moja kumshushia heshima na alikuwa anaonekana kama mwanaume anaejiheshimu sana, hivyo hakuwa na mashaka nae kabisa bila kujua huo ulikuwa ni mtego huo…

Kweli baada ya siku mbili benedicto alifika nchini Tanzania na annasia ndio alienda kumpikera uwanja wa ndege, a siku hio aliomba kabisa ruhusa kuwa hatoweza kufika kazini, na aliruhusiwa kirahisi sana, bila kujua huyo ambae alikuwa anamfanyia kazi alikuwa ndio huyo benedicto ambae yeye anamchukulia kama rafiki wa kawaida, na hata hio nyumba ya kampuni ambayo alikuwa anaishi kila kitu anacho miliki kilikuwa kinatoka kwa benedicto, akijua ni msaada tu wa kawaida kumbe mwamba alishakufa akaoza na akasahau kabisa hata kuhusu ndoa yake ya mchongo, na alikuwa hana hata muda wa kumfuatilia mke wake, na moyo pamoja na akili yake ilishaamini kuwa hakustahili kuoa, ila alistahili kwenda London tu, na ndio maana alienda London kukutana na annasia, na alishawah kuona siku moja video za mke wake kwenye moja ya tovuti za michezo ya watu wazima, kwa maana alienda kwenye London sio kwa sababu ya fungate ila alikuwa na mambo yake mengine, ila cha ajabu hata moyo haukumuuma kabisa benedicto na alijiona kama anastahili kuwa na annasia zaidi kuliko mwanamke mwenye tamaa kama marry mke wake…

Alipofika nchini Tanzania na kupokelewa na annasia, annasia alimchukua moja kwa moja na kumpeleka nyumbani kwake, kisha akampa chumba chake, kwa sababu nyumba ambayo alipewa na kampuni ilikuwa na kila kitu, alitakiwa kuja tu na nguo zake, kisha akamtaka benedicto aoge kisha yeye alienda jikoni na kuanza kuandaa chakula….

Harufu ya pilau ilizizima nyumba nzima, bila shaka ukifika pale utajua kabisa lile pilau lazima litakuwa limepikwa kwa ustadi mkubwa sana, ustadi ambao sio wa kawaida, na harufu ya hilo pilau likamtoa kabisa benedicto chumban na kuja kushuhudia upishi maridadi wa mwanamke mtiifu mwenye heshima na huruma, na mwenye uzuri wa kipekee annastazia…….

“Nilikuwa bafuni bana ila nimeshindwa kuvumilia harufu, chakula bado hakijaiva tu, maana kwa harufu ilivyo tamu mpaka nimejikuta njaa inaniuma sana, akasema benedicto akiwa anaelekea jikoni…

“ chakula tayari, nipo hapa naandaa matunda na juice, unawezaukatangulia kwenye meza ya chakula nakuletea mgeni, annasia alisema kwa sauti tamu inayoonesha unyenyekevu wa hali ya juu…
Benedicto hakutaka annasia atenge chakula pekee yake mezani, akaanza kumsaidia kupakua, kisha akapeleka mezani, na akaja akawa anataka annasia akakae tu nay eye atenge, maana hakuamin kama mwanamke anaempenda anapaswa kuteseka kwa namna yoyote ile…

“ hapana bana wewe ni mgeni, ungekaa nikakuandalia, ila ukishazoea kukaa hapa, nitakuacha ufanye unachokitaka, hata ukitaka nikuachie jiko nitakuachia, na hata kama utataka uoshe vyombo basi sitakuzuia…
“ mimi sio mgeni kwako, labda niwe mgeni kwenye nyumba yako tu, naomba ukakae nitakuja kukutengea chakula mimi, akazidi kusisitiza benedicto, na annasia akakataa, maana hakuona kama ni sawa kwa mgeni wake kuanza kujitengea chakula pekee yake na yeye yupo, ila katika yale mabishano kuna muda annasia akadondosha kijiko, wote wakashuka chini kukiokota wakajikuta wanagongana vichwa, kisha wakajikuta wanaangaliana, na kitendo hicho kiulimpa msisimko wa ajabu benedicto na taratibu aka…

ITAENDELEA ………….


HONEYMOON IN LONDON 5
HUSQER BALTAZAR

Mapigo ya moyo wa benedicto yakaanza kwenda kwa kasi ya ajabu, akajikuta anapata msisimko wa hali ya juu, alikuwa anatamani azngalau hata aonje lips za annasia walau kidogo, joto la pumzi za annasia zikaanza kumpandisha hisia, na akajikuta anapoteza uvumilivu na kulegeza jicho kisha akawa akawa anajisogeza taratibu kwa ajili ya kubadilishana mate, ila ni kama annasia alishtuka akainuka haraka hatraka na kusema “ samahan kaka, twende tukale…

Benedicto alishusha pumzi kisha akaitikia kwa sauti ya unyonge na kusema “ sawa…
Waliongozana kwa pamoja mpaka kwenye meza ya chakula, kisha kila mmoja alikuwa kimya, maana annasia aliyahisi mapigo ya moyo ya benedicto na kuhisi labda alipata hisia juu yake, ila hakuwa na uhakika, akajikuta anaona aibu, na benedicto akajikuta anawaza ule ukaribu na joto la pumzi ya annasia na kujikuta muda wote akili yake imehama kwenye akili ya kawaida na kuanza kuwaza ngono tu, kitu ambacho hata hakikuwa kwenye akili ya annasia…

Walikula huku wakiwa kimya mpaka kila mmoja alipomaliza kula, ila benedicto alikuwa anakula kwa tabu, na mara zote alikuwa anamkata annasia jicho la pembeni lenye matamanio ya hali ya juu…
“ kaka kama hautajali naomba sana ukapumzike maana najua ni lazima utakuwa umechoka kwa safari, akasema annasia na benedicto akamuangalia kwa sekunde kadhaa na alivyokuwa anamtamani, ile sauti yake ikamfanya aanze kumvua nguo kwenye akili yake na kuhisi anafanya nae yale mambo yetu, akawa kama ameduwaa hivi, ikabidi annasia aseme tena, “ kaka kama hautajali naomba ukapumzike, ndipo benedicto kama akashtuka, akamuangalia vizuri kisha akasema “ sawa hakuna tatizo usiku mwema mrembo kisha akaanza kuongoza kwenye chumba ambacho aliambiwa ndio atakuwa analala…

Annasia aliingia jikoni na kuanza kuosha vyombo maana huwa hapendi kulala na vyombo vichafu kisha akaenda zake kulala, ila akili ya benedicto ilikataa kabisa kutulia, alikuwa anawaza kumbangua mtoto wa watu tu, kila ambapo alijigeuza aliona ule ukaribu wa annasia nay eye, alianza kuhisi anassia anambusu na hata kumtamanisha kwa ajili ya tendo, kila akifunga macho sura ya annasia ndio ilikuwa inatembea kwenye kichwa na akili yake, akaona kama hapati utulivu kabisa yaan, akaamka na kwenda jikoni, ila alipofika lile eneo ambapo wote walishuka chini kwa ajili ya kuokota kijiko, akaanza kuwaza ule ukaribu wao wa wakati ule, akajikuta maumbile yake yanasimama imara sana, yakiwa yamesisimka vya kutosha kwa ajili ya tendo…

Akaona hawez tena kuvumilia, mwanamke mwenyewe anampenda kama nini, kwa nini ajitese, taratibu akaanza kuusogelea mlango wa chjumba ambacho alikuwa amelala annasia, alipofika karibu akapokelewa na sauti tamu ya kicheko kutoka kwa annasia, alianza kupata wivu na kuhisi labda kuna mwanaume yupo nae ndani, ila aliposogea karibu ndipo alipogundua kuwa hakuwa na mwanaume ila alikuwa anaongea na simu, na kwa namna ambavyo alikuwa anaongea ni wazi kabisa alikuwa anaongea na mtu ambae alikuwa anampenda…

Roho ikaanza kumuuma benedicto, akaanza kujilaumu kwa sababu ya kuchelewa chelewa kwake, kwa namna ambavyo alikuwa anasikia wivu mkubwa sana, akataka kufanya kitu ili annasia aache kuongea na simu maana aliona kama alikuwa anajitesa, ila kabla hajafanya chochote akasikia annasia anasema “ na wewe pia, nakupenda sana mume wangu…

Benedicto aliachia msonyo na kwa unyonge akaanza kwenda chumban kwake, alishindwa kulala na kujikuta moyo unamuuma balaa, alijiona kama mwanaume ambzae hana bahati kabisa, maana mwanamke ambae alikuwa anampenda kwa mara ya kwanza jiji la London likamchanganya, akaja kumpenda annasia, akawa anavuta vuta muda na mwisho wa siku anashangaa anaangukia mikononi mwa mwanaume mwingine…

ITAENDELEA…


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote