IN LOVE WITH MY ENEMY
( Moyo ni yuda)
πΎ01
HUSQER BALTAZAR
Lilikuwa ni kosa kubwa kwangu kuamini Binadamu pekee ndio wanatengeneza usaliti..... sikuwahi kuchunguza kuhusu moyo wangu na ndio sababu niliuamini kupita kiasi.
Wakati ubongo wangu ukinikumbusha kulipa kisasi kwa Muuaji.... moyo wangu ulinisaliti nikajikuta nampenda adui mkubwa wa familia yangu.
Kama utani vile lakini iliibuka vita kubwa ndani ya mwili wangu, Ubongo na Moyo vilishikiana silaha kuamua hatma yangu, sijui ni nani atashinda katika vita hii.
Karibu unisome πΎ
Jijini Deos kila ukoo unasifika kwa kumiliki watu wenye vitu vya thamani. Wakati ukoo huu ukisifika kuwa na watu wanaolijua soko la biashara, ukoo mwingine ulisifika kuwa na watoto wenye mionekano mizuri. Mwingine ulisifika kumiliki watu wanaojua maana halisi ya elimu wanapokuwa darasani.
Jina langu naitwa Kalyani....nimetokea katika ukoo unasifika kuwa na Madaktari bingwa.
Sifa hii imetupa hadhi ya kufanya kazi katika hospitali kubwa.
Ilikuwa ni kawaida kwa mgonjwa kutoa pesa nyingi ilimradi tu ahudumiwe na Mimi au mtu yoyote aliyetokea katika ukoo wa Burak.
Nilijivunia sana kuona wagonjwa wananiamini katika Mimi kupita kiasi.... nilijikuta hata ni kisahau kuimarisha mahusiano yangu hivyo kuachika kila baada ya miezi mitatu lilikuwa ni jambo la kawaida kwangu wala halikunipa maradhi ya moyo
Siku moja nikiwa natoka kazini nilipokea simu kutoka kwa mtu nisiyemfahamu. Aliomba kuonana na Mimi, nilikuwa nimechoka sana lakini kwa kuwa alihitaji msaada wangu sikuona shida kuvumilia.
Nilielekea katika hoteli ya Lakshmi kutokana na maelekezo niliyopatia, nilishtuka kidogo baada ya kumuona mtoto mwenye umri kati ya miaka kumi hivi akinipungia mkono.
Niliachia tabasamu baada ya kugundua kajaliwa sauti ya ujazo fulani kana kwamba ni Mwanamke mwenye miaka 28
"Jina lako lina zungumzwa sana masikioni mwa watu kuliko hata ukoo wa Burak na hii ndio sababu imenifanya ni kupigie simu" Binti mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Kaur aliongea
"Naweza kusikia sababu iliyokufanya unipigie simu" Nilienda moja kwa moja kwenye lengo
"Mama yangu yupo kitanda huu ni mwezi wa nne sasa.... naweza mfananisha na mfu kwa sababu hajiwezi kwa lolote, Madaktari wengi wamejaribu kadri ya uwezo wao lakini imekuwa ni ngumu kumponya" Kaur aliongea
"Naweza kumuona Mama yako siku ya kesho?.." Nilimuuliza
Baada ya kuelewana nilielekea nyumbani kupumzika.
Siku iliyofuatia sikwenda hospitali badala yake niliekea nyumbani kwao Kaur.
Nilipokelewa vizuri na hata nilipewa heshima kutokana na utendaji wangu wa kazi mzuri.
"Mama yako yupo hapa kitandani sababu ya maumivu....moyo wake umevunjika sana sababu ya mapenzi, itakuwa ngumu kwangu kumsaidia kama sitasikia hadithi iliyopelekea moyo wake uvuje damu" Niliongea
"Inasemekana alimfuma Baba yangu akiwa na mwanamke mwingine..... mshtuko alioupata ndio umemfanya alale hapo" Kaur aliongea
"Baba yako alizungumza maneno gani baada ya kufumwa?'' Niliuliza
"Ni aibu kusema lakini alidai hawakuwa wanafanya ngono kujifurahisha isipokuwa alikuwa anatolewa sumu na Daktari bingwa kutoka katika ukoo wa Burak" Kaur aliongea
"Kaur, ngozi pia hubadilika kutokana na vipodozi tunavyopaka....kama Mama yako angelijua hili sidhani kama angeshtuka kiasi hicho, ni kweli kuna sumu hutolewa kwa njia hiyo na mara nyingi huacha madhara kwa mtu anaye ruhusu iingie mwilini mwake" Niliongea kisha ni kanyoosha mkono wangu taratibu kuzipima pumzi za mgonjwa....nilishtuka ndani ya moyo wangu baada ya kugundua tayari ameshapoteza maisha.
Sikutaka kupaniki, badala yake nilianza kumfanyia vipimo..... niliamini hakuna mwanamke katika ulimwengu huu anaweza kuwa nusu mfu kwa miezi minne sababu ya mapenzi.
Nilijikuta nikiogopa zaidi baada ya kugundua sumu ndio imemuua Mama yake na si maumivu ya mapenzi.
"Naweza kujua nani huwa anaingia chumbani kwa Mama yako mara mara...." Nilijikuta ni kiuliza
"Pekee yangu ndio huwa naingia humu....nilimzuia Baba yangu kutia miguu yake sababu ya upuuzi aliomtendea Mama yangu" Kaur aliongea
"Mama yako kapoteza maisha masaa sita yaliyopita....sumu ndio imemuua na si maumivu. Kwa kuwa wewe ndio unaingia humu mara kwa mara utakuwa na kazi ya kuwaeleza Polisi" Niliongea
Kaur aliachia tabasamu ni kama alikuwa ana fahamu kile kinacho endelea
"Watu wote huko nje wanajua upo hapa ndani kumtibu Mama yangu....kifo chake kitahesibika kama uzembe wako na si sumu kama ulivyosema" Kaur aliongea
Sikuonesha kupaniki....nilimtazama kwa sababu nilihitaji kusikia akiongea zaidi.
"Mama yangu alimfuma Baba yangu akiwa na mwanamke anaye sadikika katokea katika ukoo wa Burak, namaanisha ukoo wako wewe..... hivyo siyo mbaya kama Baba yangu akijua umemuua mke wake ili ndugu yako awe Mama yangu wa kambo" Kaur aliongea
Nilijikuta ni kitabasamu kwa maneno yake ya kitoto, lakini baada ya Polisi kufika niligundua hatanii
"Can Demir kasema Daktari aachiwe.....punguza utoto kwenye mambo ya wakubwa" Mmoja wa Polisi alizungumza
"Baba yangu Mimi karuhusu huyu mbwa aachiwe pamoja na kwamba kahusika na kifo cha Mama?" Kaur aliuliza
Polisi alitikisa kichwa kuashiria ndiyo, sikutaka kujua nini kinaendelea niliondoka.
Ilikuwa wiki, ikawa mwezi hatimaye mwaka mmoja ulipita bila kusikia chochote kutoka kwa Kaur.
Siku moja Mimi na watu wa ukoo wangu tukiwa tuna furahia mafanikio yetu, tulishangazwa na uvamizi wa ghafla.
Risasi zilikuwa zinapenya kwenye miili ya ndugu zangu kama utani hivi.....
Nilipata shauku ya kumjua mtu anayetoa amri risasi ziachiwe bila huruma.
Pamoja na kwamba risasi mbili zilipenya tumboni kwangu lakini sikujizuia kumtazama kwa umakini sikuweza kumuona vizuri sababu ya giza
"Kabla sijafa naomba kusikia kwanini upo hapa kutumaliza....." Nilipaza sauti nikijua fika atanisogelea
Na kweli ilikuwa hivyo.....alisogea karibu yangu akiwa hana hata chembe ya hofu usoni mwake
Macho yangu na yake yalikutana..... japo nilikuwa katika mvurugiko mkubwa lakini moyo wangu ulilipuka, alikuwa ni kijana mzuri anayestahili kuwa Malaika na si shetani.
Nilinyoosha mikono yangu taratibu nishike miguu lakini alinikanyaga kwa nguvu zake zote. Nilinyanyua kichwa changu ni kamtazama kwa mara nyingine
Itaendelea π₯
IN LOVE WITH MY ENEMY
(moyo ni yuda)
πΎ02
MTUNZI; HUSQER BALTAZAR
Endelea πΎ
"Kama si wewe kuingia chumbani kwa mke wangu sidhani kama angepoteza maisha....hukuwa na haja ya kumpa sumu kulinda dhambi niliyowahi kuitenda na ndugu yenu. Mimi si mtu wa kusamehe makosa, kama ulihisi nimekusamehe ulikosea kwa kipindi chote hicho nilikuwa nafikiria adhabu ya kukupatia.....jina langu naitwa Can Demir hakikisha unalikumbuka utakapokuwa kuzimu" Can Demir aliongea kisha akaniongezea risasi
Nilitamani kumuambia binti yake ndio mhusika wa kifo cha mkewe lakini sikuwa na nguvu hiyo.
Nilishuhudia moto ukiwaka kwenye miili ya ndugu zangu..... nilikata tamaa ya kuishi. Sikumbuki kitu gani kilitokea lakini nilikuja kushtuka nikiwa kitandani..... nilihitaji kujua hapa ni mahali gani, wakati nashuka kitandani nilishtuka sana baada ya macho yangu kutua kwenye kioo.
Sura yangu ilibadilika.....sikuwa Kalyani ninayejijua. Nilijikuta nikipiga kelele.....mlango ulifunguliwa kwa kasi niligeuka kwa hasira nimuone mtu aliyebadilisha sura yangu bila ruhusa yangu
"Denis....." Niliita kwa mshangao
"Nisamehe kwa kubadilisha sura yako bila ruhusa yako..... kwa namna ulivyokuwa umeharibika sikuwa na njia nyingine" Denis aliongea kisha akanikumbatia
Sikuamini masikio yangu aliponiambia ni miezi mitatu imepita nikiwa kitandani.
"Vipi kuhusu watu wa ukoo wangu, usiniambie hakuna hata mmoja aliyesaidika tofauti na Mimi" Niliuliza
"Nisamehe kusema, lakini pekee yako ndio umesalia. Pengine ni kwa sababu wakati wako wa kufa ulikuwa hujafika bado.....sijui ni kitu gani utafanya lakini kwa sasa hakutakuwa na mashujaa wa Burak katika hospitali zote kubwa ndani ya Jiji la Odes" Denis aliongea
"Ahsante kwa msaada wako lakini kuanzia sasa na kuendelea nitajisimamia mwenyewe......" Niliongea
"Ni kama unataka kukaa mbali na Mimi tena" Denis aliongea
Kwa namna nilivyokuwa nahisi uchungu mkali ndani ya moyo wangu sikuwa na muda wa kuongea wala muda kumshukuru kwa wema alionifanyia, mapenzi hayakuwa na maana yoyote kwangu hivyo niliondoka..... nilihitaji kumuua Can Demir, nilihitaji kumtia kilema Kaur kwa kunitengenezea mazingira magumu.
Nilielekea moja kwa moja nyumbani kwa Can Demir, nilishangaa baada ya kukutana na foleni la watu kana kwamba wapo kuomba msaada.
Nilijiunga pia kwenye foleni bila kujua lina husiana na nini.
Dakika zilizidi kutembea bila foleni kufanyiwa kazi.
Nikiwa katika kukata tamaa, macho yalinitoka baada ya kumuona Kaur akija usawa wetu kwa mwendo wa madaha,
"Nafurahi kuona nyie wote mko hapa kujaza nafasi 20 nilizozitangaza...... mtihani wangu utakuwa rahisi sana hivyo msiogope" Kaur aliongea huku akiachia tabasamu
Nilijikuta ni kimuangalia kwa namna alivyokuwa amependeza kuliko watu wazima...kitu kingine kilichonifanya ni tabasamu ni kwa namna alivyokuwa ana zungumza kwa kujiamini kupita kiasi
"Ndani ya Nyumba yetu kuna mawe madogo meupe mfano wa theluji. Watu 20 wa mwanzo watakaoweza kuniletea ndio watakuwa wafanyakazi wa hii nyumba....." Kaur aliongea kisha akapuliza kipenga
Wote kwa pamoja tulifukuzana kuingia ndani....ni wazi watu wote walitamani kuwa Wafanyakazi ndani ya jengo hili lakini shauku yangu Mimi ilikuwa ni kulipa kisasi na si kingine. Ili niweze kufikia malengo yangu ni lazima niwe Mfanyakazi ndani ya hii nyumba.... sikutaka kukumbuka kuhusu taaluma yangu ya Udaktari.
Nilifanikiwa kupata jiwe dogo jeupe mfano wa theluji.
Sikutaka kufikiria mara mbili nilikimbia haraka mpaka sehemu aliyokuwa Kaur
"Ulikuwa mtu wa mwisho kwenye foleni lakini umekuwa wa kwanza kuleta kitu nilichowaagiza.....hongera umepita katika usahili huu" Kaur aliongea kisha akanipigia makofi kimtindo
Zoezi lilikamilika baada ya watu 20 kupatikana
"Kama mnavyoona jiwe hilo halina doa jeusi hata kidogo.... natarajia nyie wote mtakuwa wasafi kama jiwe hilo. Nyumba hii haina tofauti na hadithi ya kufikirika hivyo kila mtakachoona au kusikia hakikisheni kinadumu vifuani mwenu na si kuvitangaza huko nje.... karibuni" Kaur aliongea kisha akaongoza njia
Kwa pamoja tulimfuata kwa nyuma.....tukiwa katika kutembea nilishtukia mpira una gonga kichwa changu.
Watu wote tuligeuka kujua mpira umetokea wapi.
Mapigo ya moyo wangu yalisimama kwa muda baada ya kumuona Can Demir.
Ni mzuri wa sura kuliko Wanaume wote niliowahi kuwaona lakini nina uhakika ni Mwanaume pekee anayeongoza kuwa na roho mbaya Jijini Odes
"Can Demir.... kuna haja ya kutengeneza mpira wenye macho" Kaur alimuambia Baba yake
Watu wote walicheka sababu ya maneno yake, niliuokota mpira kisha nikamrushia Can Demir kwa nguvu zote kitendo cha kuudaka tu alidondoka chini pengine ni kwa sababu nilitumia nguvu yangu yote niliyojaliwa
Watu wote walinigeukia, bila shaka walitarajia nitaomba msamaha lakini sikufanya hivyo.
"Inaonekana una kula sana chips kuliko ugali.....pole kwa hilo" Kaur alimwambia Baba yake kisha akatupa amri tuendelee na safari.....
Baada ya kukaa kwenye viti alianza kutuangalia kwa umakini mkubwa mmoja baada ya mwingine
"Kuanzia sasa utakuwa Chief maid wa Wafanyakazi wote.....kabla hujaja hapa nina uhakika ulikuwa na matarajio ya kuwa Mfanyakazi wa kawaida au Kiongozi wao. Sitakufundisha kuhusu majukumu yako..... naomba ufanye kazi kwenye mazingira ya bila kusimamiwa" Kaur aliniambia
Watu wote walinigeukia, ni kama walikuwa hawaamini naweza kuwa Chief maid
"Jina langu naitwa Kalyani..... kuanzia sasa mtafanya kile nitakachowaagiza, sitaogopa kutoa adhabu kwa mtu yoyote atakaye nenda kinyume na amri yangu...." Niliongea kwa kujiamini
"Mimi pamoja na Baba yangu tutahudumiwa na wewe.....hakikisha haufanyi makosa" Kaur alinikumbusha kisha akaondoka
Kwa kuwa kila mtu alikuwa anaielewa sababu iliyomleta hapa haikuwa ngumu kuanza majukumu bila kusimamiwa.
Nilielekea bustanini kuhakikisha mazingira yapo vizuri .....wakati narudi nilikutana na Can Demir bila shaka alikuwa anaelekea bustanini
Nilitaka kuendelea na safari yangu lakini alinizuia kwa kunitegea mguu....kama si kujishikiza kwenye mti basi ningedondoka, nilimgeukia kwa macho yaliyojaa hasira
Itaendelea π₯
IN LOVE WITH MY ENEMY
(Moyo ni yuda)
πΎ 03
MTUNZI; HUSQER BALTAZAR
Endelea πΎ
Can Demir alinisogelea kwa ukaribu zaidi akitaka kujua sababu ya kumuangalia kwa macho makali.
Ilinilazimu kuachia tabasamu la uongo kumaanisha nipo sawa
"Chumbani kwangu hapafai..... hakikisha unaweka mazingira vizuri kwa sababu bado sijao. Nimesikia wewe ndio Chief maid hivyo kuwa makini kwa kila kitu. Chumba changu hakina tofauti na yai, kosa moja dogo litasababisha kipasuke" Can Demir aliongea
"Kazi yangu ni kufanya usafi tu na kuondoka, chochote nitakachoona kitakuwa ni siri yangu na si ya jamii, nadhani ndio ulitaka kusema hivi" Niliongea
Can Demir alinirushia kitambaa chake kikafunika uso wangu
"Hivyo ndivyo unapaswa kuwa pindi utakapo kutana na kitu cha kushangaza chumbani kwangu..." Aliongea kisha akaondoka
Nilielekea chumbani kwake kuweka mazingira sawa, nilijikuta ni kitabasamu kwa sababu kulikuwa kumepangwa vizuri sikuelewa maana ya yeye kuniambia kuna hitaji usafi.
Taratibu nilisogea kwenye kioo kikubwa kilichokuwa ukutani. Nilijiangalia kwa umakini mkubwa.....nilimshukuru Denis kwa kuniwekea sura mpya.
Ghafla kitasa cha mlangoni kilinyongwa, sikuwa tayari kukamatika nilivunga nasafisha kioo...... Can Demir aliingia akiwa kashika chupa ya maji
"Nisaidie kuvua nataka kuoga" Kauli hii ilinishtua sana
Sikutaka kupaniki hata kidogo....ni kawaida wa watu Matajiri kujifananisha na Wafalme katika ulimwengu huu.
Nilisogea taratibu mpaka ni kamfikia.....
nilimfungulia vifungo vya shati lake kisha nikamvulisha nikiwa nimemkazia macho.
Ile nataka kufungua zipu ya suruali yake alinizuia.
"Nilikuwa napima kiwango cha utiifu wako kwangu....sasa nimeelewa kwanini Kaur ameona unafaa kuwa Chief Maid wa hii nyumba, nina uhakika aliuona utiifu wako na hii ndio sababu akakuchagua. Mimi ni mtu wa kujali sana biashara zangu kuliko hata msiba wa mtu wangu wa karibu, kwa kipindi nitakachokuwa mbali naamini utamsaidia Kaur......" Can Demir aliongea
Nilitikisa kichwa kuashiria nimeelewa, nilitega mgongo niondoke lakini alinizuia.
"Nimepewa mualiko wa kutoa semina fupi kwa wajasiriamali wapya..... hakikisha unafikiria nitavaa nguo gani pindi nitakapotoka bafuni" Can Demir aliongea kisha akaelekea bafuni
Nilifungua kabati lake la nguo.... sikuwa mzuri sana kwenye upande wa mavazi, ili niweze kuwasogeza watu hawa karibu na kulipa kisasi changu kwa uhakika ni lazima nifurahishe mioyo yao.
Nilimchagulia suti niliyoona inafaa kwa upande wangu.
Niliiwekea kitandani kwake kisha ni kaondoka, siyo pekee yake tu anahitaji huduma yangu nilielekea kwa Kaur
Niliachia tabasamu baada ya kumkuta anafatilia mijadala ya uchumi kupitia runinga.
Nilitaka kuongea lakini alinipa ishara ya kukaa kimya.
Niliendelea kusimama mpaka kipindi kilipoisha
"Wanaongea hivyo kwa sababu wamezaliwa katika familia zilizokwisha jipata kwenye swala zima la kifedha....ni us*nge wa hali ya juu kuongelea neno akiba kwa mtu anayeshika shilingi elfu moja kwa siku.....tuachane na hao wapuuzi niambie kwanini uko hapa" Kaur aliniuliza
Kwa umri wake alipaswa kuangalia cartoon za Tom and Jerry na si kufuatilia hoja nzito namna hiyo kuhusu uchumi....nilijikuta ni kiachia tabasamu na hata ni kasahau sababu iliyonileta kwake.
"Usiwe na shaka siku ya leo nitakula nje ya nyumba hii..... nitafurahi kama utamsindikiza Can Demir. Ndiyo ni semina tu anaenda kutoa lakini uwepo wako naamini utamzuia kuingiza ratiba nyingine......sifurahii kuona yupo single mpaka sasa na ndio sababu nitakula nje siku ya leo" Kaur aliongea
"Una maanisha unataka kumtafutia Baba yako mke?" Niliuliza
"Yes, pindi atakapooa kwa mara ya pili moyo wangu utapunguza kumhofia" Kaur aliongea kisha akanipa ishara niondoke
Nilienda kukaa sebuleni kumsubiria Can Demir...... kitendo cha kuona amevaa nguo nyingine tofauti na nilizo mchagulia niligundua hajafurahishwa na uchaguzi wangu
"Kutokana na maelezo ya Kaur natakiwa kuambatana na wewe...." Niliongea
Can Demir hakujibu chochote badala yake alinirushia briefcase.
Ilinilazimu niendeshe gari lake kwa sababu alidai yeye ni boss.
Tukiwa katikati ya safari niliijiwa na wazo la kutengeneza ajali ya makusudi tufe wote.
Yes, hii ndio ilikuwa njia pekee ya kujeruhi moyo wa Kaur.....kama atasikia habari kuhusu kifo cha Baba yake nina uhakika ataanza kuishi kama mtoto na si mtu mzima.
Mbele yetu kulikuwa na gari kubwa la mizigo....sikuona sababu ya kulikwepa pamoja na kwamba lilikuwa jukumu langu kupisha
Ghafla mikono ya Can Demir ilishika usukani.....ilisalia kidogo tu nitengeneze ajali lakini kwa sababu yake ilishindikana
"Wee k*ma kuwa makini, unapokuwa barabarani hakikisha unafuta kumbukumbu zote mbaya zilizojaa kichwani mwako. Hakuna dhambi inayo sumbua moyo wangu kama kuua bahati mbaya...... ni heri niue kwa kukusudia na si kama ulivyotaka kufanya wewe" Can Demir alinifokea
Nilishikwa na hasira, maneno yake yalikuwa magumu mfano wa jiwe....bila kufikiria mara mbili nilimtia kibao cha uso.
Can Demir alijishika shavu lake kisha akanisogelea tukawa pua na mdomo, nilimtazama macho yake, nilijikuta nikiona kama yanawaka moto bila shaka hasira yake ilikuwa inamwagikia....nilidondokea kifuani sababu ya hofu.
Ghafla nilihisi mkono wake umeshika kichwa changu.... sikuelewa amenihurumia au anataka kuninyonga. Mapigo ya moyo yalidunda zaidi
Itaendelea π₯
IN LOVE WITH MY ENEMY
04 πΎ
MTUNZI; HUSQER BALTAZAR
Endelea πΎ
Can Demir alinikumbatia pia...alinipa pole kwa hofu iliyo ni zonga.
"Nikawaida kuona vitu vya ajabu hasa unapokuwa umeshika usukani.... nisamehe kwa kukufokea" Can Demir aliongea
Nilimuomba msamaha pia kwa kumtia kibao, nilijitetea niliona mzuka akipita. Aliachia tabasamu bila shaka aligundua ni uongo
Nilishika usukani tena tutaendelea na safari
Tulifika katika hotel ya Lakshmi, tulikuwa tunaenda ghorofa ya nane hivyo itulazimu kupanda lifti.
Tukiwa ndani ya lifti Can Demir alitoa marashi kwenye koti lake akajipaka mikononi.
Ni mtu nadhifu sana.....ni wazi kabisa uchafu kwake ni sawa na maradhi.
"Hakikisha una kaa mbali na Mimi, sitaki kila mtu ajue tumeongozana.....siku nyingine ukiambatana na Mimi jaribu kuwa mwanamke na si kuvaa vibaya namna hiyo mithili ya Mwanaume" Can Demir alinichamba kisha akasepa
Nilitoka kwenye lifti pia ni kaelekea kwenye ukumbi..... watu wengi walikuwa maeneo haya. Nilikaa siti ya nyuma kabisa
Japo mtu huyu ni adui yangu mkubwa lakini nilijikuta ni kitekewa na sauti yake.
Si Mimi tu hata Mabinti wengine walionekana kuchanganyikiwa kwa namna alivyokuwa anaongea.
Sikuwa tayari kuvutiwa na sauti yake, niliondoka ni kaenda kumsubiria kwenye gari.
Nikiwa mahali hapa nilifanikiwa kumuona Denis akiwa na msichana mwingine.....kwa namna walivyokuwa wanashika shikana niligundua wana mahusiano.
Moyo wangu ulipata amani kuona Denis kapata mtu wa kumfariji....muda wowote naweza kufa nikiwa katika harakati za kulipa kisasi hivyo itapendeza kama yeye atakuwa mbali na Mimi.
Nilimsubiria Can Demir zaidi ya masaa manne ndipo akarejea.
"Hukuwa na haja ya kukaa kwenye gari....fungua mlango tukapate chakula" Can Demir aliongea
Kwa pamoja tulikaa VIP room, chakula kililetwa baada ya kufanya uchaguzi. Linapokuja swala la kula huwa na sahau kila kitu..... nilianza kula kama nafukuzwa
"Nilitarajia baada ya kupata sura mpya ungeendelea na maisha yako....badala yake umekuja nyumbani kwangu kuishi kama Chief maid, naweza kuona kisasi kwenye macho yako.....nikupe pole kwa sababu hauwezi kumdhulu Kaur wala mtu yoyote wa malangoni kwangu. Sikuwa na mpango wa kukuacha hai....Babu yako aliniomba ni kuache uishi kwa sababu aliamini huwezi kufanya kitu chochote zaidi ya kutibu wagonjwa" Can Demir aliongea
Nilijikuta ni kishtuka sababu ya maneno yake
"Nilipoteza pesa nyingi kuhakikisha una miliki hiyo sura...... sitarajii uniletee visa vya ajabu, naomba usisahau kama unaishi kwa sababu nimeruhusu uishi...." Can Demir aliongea
Hasira zisizo na kipimo zilinijaa ghafla.....nilichukua glasi iliyokuwa na juisi ni kammwagia, sikuishia hapo nilishika umma ni kataka kumtoboa macho lakini alinikamata mkono wangu kwa nguvu
"Unataka kulipa kisasi? nitakupa hiyo nafasi.... hakikisha unatimiza nia yako ndani ya mwezi mmoja, endapo utashindwa nitakuua" Can Demir aliongea
Nilimtemea mate kwa upuuzi aliokuwa ana zungumza, ghafla taa zilizima. Wote kwa pamoja tuligeukia mlangoni
Itaendelea π₯
IN LOVE WITH MY ENEMY
πΎ 05
MTUNZI; HUSQER BALTAZAR
Endelea πΎ
"Samahani taa zitazimwa kwa dakika 10 kwa sababu ya hitilafu iliyojitokeza" Sauti ya Mhudumu ilisikika
"Samahani pekee haitoshi..... nitafurahi kama mtatupatia fidia kwa kutuweka gizani" Can Demir aliongea
"Kuwa na amani, ni kawaida yetu kufanya fidia pale huduma zetu zinapo kuwa chini ya ubora tuliokusudia" Mhudumu aliongea kisha akaondoka
Niliutoa mkono wangu kutoka kwa Can Demir.....kwa kuwa simu yangu ilikuwa na chaji ya kutosha niliwasha tochi ili tupate mwangu.
"Bila shaka unaamini nimeumaliza ukoo wako wote sababu ya ujinga wa Kaur.... naelewa binti yangu ni kichaa na ndio sababu niliwapigia simu Polisi wakuachie" Can Demir aliongea
"Naomba kusikia sababu iliyopelekea ufanye tukio la kijinga namna hiyo..." Niliongea
"Sijui ni lini na saa ngapi lakini nilikuja kushtuka ndani ya mwili wangu kuna sumu inaishi..... Madaktari pekee wenye kuweza kunisaidia walikuwa ni wa ukoo wako. Binamu yako alipendekeza sumu itolewa kwa njia ya tendo la ndoa.....sikuwa tayari kumsaliti mke wangu na wala sikuwa tayari kumuua" Can Demir aliongea
Niliendelea kumsikiliza....moyo wangu ulihitaji kusikia sababu mpya iliyopelekea ukoo wangu wote upotee kwa usiku mmoja ukiachana na uongo wa Kaur
"Nilijikuta ni kishiriki tendo la ndoa na binamu yako kama sehemu ya tiba.....mke wangu alinifuma nikiwa na mwanamke mwingine. Hata kama ningemueleza mara 1000 kuwa kila ilikuwa ni sehemu ya tiba asingeamini...." Can Demir aliongea
"Sitaki kusikia historia yako....ongea kwa ufupi kwanini uliuangamiza ukoo wangu wote" Nilifoka
"Sumu iliyoingia mwilini mwangu ilitoka kwa Binamu yako..... lengo lake lilikuwa ni kumuua mke wangu kwa presha. Na yeye ndio alimtumia ujumbe mfupi aje kushuhudia namna navyotibiwa. Mke wangu alikaa miezi minne kitandani sababu ya Binamu yako. Kaur aliamua kumpatia sumu Mama yake kwa sababu Madaktari bingwa wa ukoo wako walithibitisha hawezi kupona......hivyo kuanzia sasa na kuendelea naomba ukumbuke akilini kuwa niliumaliza ukoo wako wote kwa sababu ya ujinga wa Binamu yako" Can Demir aliongea
"Ulipaswa kumalizana na Binamu yangu na si ukoo wangu wote..... sababu zako ni za kitoto nitahakikisha na lipa kisasi kufidia roho za ndugu zangu zilizopotea bila hatia" Niliongea
"Na ndio sababu nimekupa mwezi mmoja.... usisahau kama watu wa Burak mlikuwa na uwezo wa kumtibu mke wangu lakini kwa sababu ya Binamu yako kusingizia nimembaka hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kuokoa maisha ya mke wangu.....nilikuacha uishi si kwa sababu tu Babu yako aliniomba ni kwa sababu pekee yako tu ndo hukuwa unajua kuhusu upuuzi wa Binamu yako" Can Demir aliongea
Kabla sijaongea chochote umeme ulirudi..... mazungumzo yetu yaliishia hapa.
Nilisimama nikiwa bado na hasira, nilipiga hatua niondoke lakini bahati mbaya nilijikwaa.... kabla sijaangukia pua au mdomo Can Demir alinidaka....tulidumu kutazamana huku kila mmoja akiwa amekunja uso wake.
Can Demir alisogeza mdomo wake karibu na lips zangu, mapigo ya moyo yalienda juu nisiamini kichaa huyu anataka kunibusu.....sijui ni pepo gani lilinivaa lakini nilifumba macho kuonesha nipo tayari pia. Lengo langu lilikuwa ni kumng'ata ulimi afe.
Itaendelea π₯
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote