IN THE NAME OF LOVE

book cover og

Utangulizi

IN THE NAME OF LOVE❤️1

MTUNZI SMILE SHINE
Emily binti mchangamfu na mwenye akili sana ni binti wanye umri wa miaka 20 tu.
kwenye familia yao wapo wawili yeye na kaka yake Nathan ambae ana miaka 37 kwa sasa.
Nathan na Emily walikuwa wanapendana sana , Nathan alikuwa kumfuatilia sana mdogo wake na kumlinda asijiingize kwenye mambo ya anasa alijitahidi kumpatia kila anachostahili kupata .

Nathan hakuwa kaka yake Emily wakuzaliwa , Emily Alilelewa na wazazi wa nathan tangu nilipokuwa na miaka 4 baada ya kuokotwa na Nathan akiwa anazunguka mitaani.
Nathan alimchukua na kwenda nae nyumbani kwao, wazazi wa Nathan walienda polisi kutoa taarifa lakini mzazi wa mtoto hakupatikana basi wazazi wa Nathan walianza kufuata taratibu wakamchukua Emily na kuishi nae kama mtoto wao wa kumzaa.

Emily alipofikisha miaka sita wazazi wa Nathan walifariki kwenye ajali mbaya ya gari walipokuwa wanatoka kwenye msiba wa mama yake mzazi na baba yake Nathan, hilo lilikuwa pigo kubwa sana kwa Ethan na Emily .

Kwakuwa Nathan alikuwa mkubwa anaejitambua ilibidi achukue jukumu la kumlea mdogo wake na kumsimamia kwa kila kitu pia alikuwa anasimamia miradi waliyoacha wazazi wao na huo ndio ulikuwa wasia wa wazazi wao kuwa Emily ni jukumu la Nathan hivyo lolote likitokea Nathan achukue jukumu la kumlea Emily.



Miaka ilienda Emily aliendelea na masomo mpaka kufikia chuo kikuu na Nathan alisimamia vizuri sana miradi maana alitambua kama angefanya uzembe au kosa lolote basi angeharibu maisha yake pamoja na mdogo wake Emily.
Hasa alipokuwa anaona watoto wakike wakizurula mitaani na wengine kufanya kazi haramu na kujiuza akili yake ilihama na kumfikiria mdogo wake. Na alikuwa akimsihi sana kuwa makini na vishawishi , makundi mabaya na marafiki wasio faa ili kufikia malengo yake.

Siku moja asubuhi Emily aliamka kutoka usingizini akaangalia saa ilikuwa ni saa moja asubuhi.
" Ooooh nimechelewa kuamka siku kaka Nathan atakuwa haja ondoka.
Alinyanyuka kitandani akakimbia mpaka sebleni alimkuta Nathan ndio anajiandaa kwaajili ya kuondoka.
" Morning bro.
" Morning how are you?
" Am fine ,Kaka Nathan usisahau Leo ni siku yangu muhimu ee.
Nathan alimuangalia alafu akasema
" Muhimu kivipi?
" Inamaana umesahau?
" Mmmmm.... Nathan aliangalia juu huku akiwa kashika kidevu chake akijaribu kukumbuka ni kitu gani hicho muhimu.
" Nikumbushe tafadhali.
"Inamaana umesahau?
" Nina mambo mengi sana mdogo wangu . Nikumbushe basi.
" Leo ni siku ya kumbukizi yangu ya kuzaliwa.
" Oooh my God, nilisahau kipenzi .
" Basi nahitaji zawadi na usikose kunitoa out ukitoka kazini"aliongea Emily kwa kudeka huku akiwa kashika mkono wa kaka yake
"Shaka ondoa little one nimeshakuahidi kukutoa out na zawadi kedekede Wacha niwahi job kwanza "alijibu Nathan huku akiwa anamvuta mashavu mdogo wake
"Okay kaka take care na usisahau"
" Usijali kipenzi changu wewe niandae nikija tunatoka.
" Sawa.
Nathan aliondoka na Emily alirudi chumbani kwake akiwa na furaha maana kaka yake hakuwahi kuahidi jambo bila kutimiza .

Mida ya jioni Emily alikuwa kasha kuandaa akawa anamsubiri Nathan arudi kutoka kazini ili watoke.
Emily alimsubiri sana kaka yake lakini hakutokea mpaka ikafanya apate wasiwasi.
" Hii sio kawaida Nathan atakuwa kapatwa na shida gani?
Emily alimpigia sana lakini hakupokelewa simu yake
"Jamani kaka Nathan naona anataka kuniharibia siku huyu Sasa namfuata hukohuko ofisini kwake.
Emily alichukua viatu na pochi yake ndogo pamoja na simu yake akaondoka na kuelekea ofisini kwa Nathan.

Alipofika alienda moja kwa Moja alienda kwenye ofisi ya kaka yake. Aligonga mlango lakini hakuitikiwa alitaka kufungua lakini akasita alirudi kwa secretary .
" Samahani Salome hivi kaka Nathan yupo Ofisini kwake?
" Ndio yupo lakini alisema hataki kusumbuliwa na mtu yoyote.
" Kuna tatizo?
" Inaonekana hivyo maana hayupo sawa.
Emily aliamua kwenda ofisini kwa Nathan akafungua mlango bila kubisha hodi.
Emily alishangaa baada ya kuona vitu vikiwa vimezagaa chini hakukuwa na mpangilio mzuri kama inavyokuwa siku zote.
"Kaka umefanya Nini mbona vitu vimezagaa namna hii?"
Aliuliza Emily huku akiwa anaokota baadhi ya mafile na kuweka mezani alafu akasogea karibu na kaka yake lakini nathan alikuwa kajiinamia. Emily aliendelea kuuliza

"Bro kuna tatizo? Umeomba na mtu?
Nathan alinyanyua kichwa chake akamuangalia Emily huku macho yake wakiwa mekundu, vifungo vya shati vikiwa vimefungiwa na tai ilikuwa imeleezwa.
" Kaka unajua unanitisha hiyo hali sio kawaida niambie umepatwa na tatizo gani?
Ethan alisimama akashusha pumzi ndefu alafu akasema
"Mark amenichezea mchezo mchafu, Emily Ile project aliyoleta ilikuwa fake hivyo tumepoteza Kila kitu Hadi pesa za watu". aliongea Nathan Kisha akamshika mdogo wake mabegani
"Nisikilize kwa makini Emily muda wowote naweza kukamatwa na polisi kwa hili,likitokea lolote jitahidi usijihusishe na hili ni Bora ukaenda mbali sawa? Aliongea Nathan kama mtu alikata tamaa na kuamua liwalo na liwe atawajibika kwa kile kilichotokea.
" Unafikiri naweza kukaa mbali na hili? Kama ikipambana kwaajili yangu basi na mimi nitapambana kwaajili yako kaka .
Aliongea Emily akiwa anajiamini. Na Nathan alimuangalia usoni.
" Tunatakiwa tuondoke hapa , twende nyumbani ukapumzike.

IN THE NAME OF LOVE ❤️ 2
MTUNZI SMILE SHINE
Nathan alikubaliana na Emily walirudi nyumbani kwaajili ya kupumzika lakini akili ya Nathan haikuwa sawa alikwisha usiku kucha akizunguka chumbani kwake huku akifikiria atakapokutana na marck atafanya nini.

Hatimae kulikucha Nathan alikuwa wakwanza kutoka sebleni akiwa kashika grass ya mvinyo anakunywa.
Emily alienda kumuangalia chumbani kwake lakini hakumkuta akatoka mpaka sebleni akamkuta akiwa kashika grass anakunywa mvinyo.
" Kaka Nathan unakunywa pombe asubuhi yote hii? Alisema Emily huku akiwa anataka kumnyang'anya ile grass lakini Nathan akawahi kuikwepesha.
" Emily kwa sasa hii ndio faraja yangu niache ninywe mpaka nitosheke.
" Kwahiyo mimi sifai kuwa mfariji wako?
" Unafaa lakini huyu ndio msaidizi wako.

Nathan alikataa katakata kuachia grass aliendelea kunywa na Emily alishindwa kumzuia.
Nathan alikumywa mpaka akawa chakari na kulala chini.

Ilipofika majira ya saa kumi jioni kimvua kilikuwa kinaonyesha , Nathan aliamka na kwenda kuoga baada ya kuoga alitoka kwaajili ya kupata supu aliyokuwa imeandaliwa na Emily.
Alikunywa ile supu huku Emily akiwa kakaa pembeni akimuangalia kwa huruma huku akiwaza juu ya kutatua hilo tatizo kwani halikuwa swala dogo .
Mara walisikia mlango unagongwa Emily akaenda kufungua.
Baada ya kufungua Emily alishituka alipoona wanaume wawili mmoja akiwa kavalia sare za polisi.
" Habari.
" Salama.
" Tumemkuta mr Nathan?
Emily aligeuka nyuma kumuangalia Nathan ambae alikuwa anaangalia mlangoni.
" Kuna tatizo lolote? Emily aliuliza
" Sisi sio watu wabaya naitwa afande Tino. Na mwenzangu anaitwa afande Enock. Alijitambulisha yule polisi ambae alikuwa kavalia kiraia.

Wakiwa bado wanatambulishana Nathan alifika mlangoni.
" Habari mr Nathan.
" Salama.
" Mr Nathan kuanzia sasa upo chini ya ulinzi kwa shutuma za dhulma na ulaghai, dhamana ipo wazi pia una nafasi ya kutafuta mwanasheria wako.
Nathan hakuwa na alijitetea alinyoosha mikono na kufungwa pingu.
" Afande....
" Kwa maelezo zaidi fika kituoni dhamana ya ndugu yako ipo wazi.
Wale polisi walimchukua Nathan na kuondoka nae wakamuacha Emily akiwaangalia huku machozi yakimtoka.

Emily alikumbuka kuna mtu ambae ataweza kumsaidia .
" Lazima niende kwa Raphael anaweza kunisaidia hili.
Emily aliondoka Muda uleule huku mvua inanyesha alienda nyumbani kwa Raphael.
Alipofika getini alikutana na mlinzi.
" Habari.
" Salama, nikusaidie nini?
" Naomba kuonana na Raphael.
Yule mlinzi alimuangalia Emily kama vile anamkagua alafu akauliza
" Una miadi nae?
" Nilijua ofisini ndio kuna kuwa na miadi kumbe hata nyumbani?
" Ndio kila mtu huwa na utaratibu wake wa maisha.
" Ok sina miadi nae lakini nataka kuonana nae nina jambo la dharura.
" Ni ngumu sana kumuona nenda urudi kesho.
" Wewe kaka hivi hunionei huruma hivi nilivyo nimelowana na mvua unajua nini kimenikuta? Nionee huruma hata kidogo.
Yule mlinzi alimuonea huruma .
" Subiri nikaongee nae kwanza nimwambie ni nani anataka kuonana nae?
" Emily Sagamba.

Mlinzi aliingia ndani akamkuta Daphael anafanya kazi zake kwenye laptop yake.
" Samahani boss.
" Mmmmm
" Kuna msichana yupo hapo nje anaitwa emili Sagamba anataka kukuona amesema anaa dharula.
" Kwani hujui ratiba za hapa? Kamwambia sihitaji mgeni kwa sasa kuna mambo yangu muhimu nafanya kama anashinda arudi kesho.
Raphael aliendelea kufanya kazi zake, mlinzi alitoka na kwenda kumpa jibu Emily.
kuwa boss wake amekataa kuonana nae
"Ahaa basi Mimi nitakaa hapa Hadi atakapokubali siwezi kuondoka"Emily alisimama muda mrefu hali ya hewa nayo ilizidi kuwa mbaya ilionyesha mvua kubwa lakini hakujali aliendelea kusimama kwenye mvua huku anaangalia dirisha la chumba cha juu katika nyumba ya Raphael.
Muda huo Raphael nae alikuwa kasimama dirishani akimuangalia
" Huyu Binti mjinga Sana anataka kunifia nyumbani kwangu"alitoa simu mkononi na kumpigia mlinzi
"Hebu muingize ndani huyo mtu asije akaniangukia hapo"
"Sawa boss"
" Dada boss kakubali ukaonane nae.
Emily alifurahi, alichukuliwa na mlinzi na kupelekwa Hadi katika sitting room ya jumba la Raphael
"Naona familia ya sagamba mmekuwa ombaomba Sasa,bint mrembo unasimama kwenye mvua kwaajili ya kutaka msaada tu"
Aliongea Raphael huku anamchunguza vizuri Emily
"Nahitaji msaada wako"alijibu Emily kwa sauti y kutetemeka.

Raphael alicheka kwa dharau " utanipa ujira gani nikikupa msaada wangu?

IN THE NAME OF LOVE ❤️3

MTUNZI SMILE SHINE
Emily alikumbuka miezi kama minne nyuma kuna siku alikutana na Raphael club, Raphael alikuwa akimsumbua acheze nae na kumtumia kama madada wa wasiojiheshimu lakini Emily alikataa na kumtolea maneno makali na kumkashifu kuwa hana utu anataka kutumia pesa zake kwaajili ya kudhalilisha wanawake.
Kwakuwa alikuwa na shida siku hiyo ilimbidi akubali kuwa chombo cha starehe kwa Raphael.

"Nitakupa ulichokuwa unataka sikuile klabu"
Alijibu Emily huku akianza kuvua koti alilokuwa amevaa na kubaki a kigauni kilichoonesha sehemu kubwa ya mwili wake.
Taratibu alimsogelea Raphael na kuanza kumpiga mabusu.
Raphael alimpokea na kuanza kumkiss mfurulizo lakini ghafla Emily alianza kupata woga
" Hivi ndo unavyoreact wakati unahitaji msaada?"
"Sorry Raphael sijawahi kufanya haya mambo."

"Kama unahitaji msaada unatakiwakuonesha ushirikiano"alimjibu Raphael bila hata kukwepesha macho.ilibidi Emily amsogelee Tena na kuanza zoezi upya la kumkiss Raphael japo alifanya kwa woga.
Raphael alisogea nyuma akamuangalia alafu akasema
" Emily huna unachojua kwenye hii Dunia ya mapenzi na siwezi kufanya chochote Sababu naona kamaunajiuza kwangu naomba uondoke".
" Basi naomba unisaidie niweze kumtoa kaka yangu.
" Sina msaada na wewe naomba uondoke.

Raphael alimfukuza Emily,lakini aliumia sana moyoni kwani ni miaka mingi amekuwa akimpenda Emily na hakutaka wafanye kitendo kile kwa Sababu zisizokuwa za kiupendo baina Yao.
"Emily I wish ungejua kuwa Mimi ndo niliekuokota siku ulivyochukuliwa na wazazi wa Nathan na sio Nathan ..upendo unaomuonesha ulikuwa uwe wangu" aliwaza Raphael akiwa kashika Chen ambayo alibaki nayo siku ambayo alimsaidia Emily wakiwa wadogo..

Baada ya kufukuzwa na Raphael Emily aliondoka kinyonge huku akiwa anageuka nyuma kuangalia jumba la Raphael.

Emily alikuwa bize kutafuta namna ya kumsaidia kaka yake Nathan aweze kupata dhamana,akiwa kwenye harakati za kutafuta msaada alikutana na Joseph.
"Emily mrembo wangu " aliongea Joseph ambae ni ex wa Emily huku alimzuia Emily asipite yani alikuwa kama anataka kumkumbatia, Emily alisimama akamuangalia kwa hasira na kusema
"Hebu nipishe sitaki mabishano na wewe sipo kwenye mood hiyo"alifoka Emily
"Hahaha una huzuni ya kukamatwa kaka yako?
Emily yalizidi kukasirishwa na kicheko cha joseph.
" Sitaki mzaha kwenye hili hebu pisha barabarani.

" Tulia basi Mimi nitakusaidia ukinipa ninachokitaka maana ulinibania sana kipindi tunadate"aliongea Joseph huku anamvutia Emily upande wake.
" Joseph kaa mbali na mimi sitaki hata uniguse.
Ghafla alishtukia kapigwa ngumi yupo chini
"Unaanzaje kushika wanawake kumdhalilisha mwanamke kwaajili ya shida zake tena mbele ya hadhara hivi?
Ilikuwa ni sauti nzito ya Raphael.
Emily alibaki anashangaa na kujiuliza huyu mtu kafika saa ngapi na amekuja kumtetea wakati alimfukuza kwake na kusema hawezi kumsaidia.
" Emily shida ndio zinakifanya ujidhalilishe kwa kila mwanaume? umekuja kwa huyu mshenzi wako wa zamani atakusaidia nini wakati ananuka njaa?"alifoka Raphael
"Wewe si ulinifukuza kwako? Kwanza usinifuate Ninapokwenda, ninayofanya hayaakuhusu" alijibu Emily huku anamuangalia Raphael usoni
"Kwani umemaliza shida zako mpaka uwe jeuri hivyo?
" Hata kama sijapata siwezi kunyenyekea na kujiuliza ikiwa nina nafasi ya kupambana. Na sijui umefuata nini hapa.
"Nimekuja huku kukufuata wewe nimekubali kumsaidia kaka yako kwa sharti 1 tu".
" Wewe mshenzi unafikiri hizo hela za makampuni ya baba yako unaweza kumchukua mwanamke wangu nataka kukueleza kuwa huyu Emily ni mwanamke wangu tulipishana kauli kidogo ila hatukuachana hizo tamaa zako peleka kule ,nitasimamia kesi ya shemeji yangu.
Aliongea Joseph kwa kujiamini huku akiwa kamkodolea macho Raphael.
" Wewe kapuku funga mdomo wako na uondoke hapa.
" Joseph naomba utupishe tunataka kuongea mambo ya maana. Alisema Emily.
"Emily huyo sio mwanaume atakusababishia maumivu zaidi ya niliyokupa mimi.
" Ondoka wewe fala. Alisema Raphael
" Sawa naondoka lakini sitaruhusu muwe pamoja.
Joseph alipoondoka Emily akauliza kwa shauku kubwa ya kutaka kujua hilo sharti
" Sharti Gani?
"Kuwa mwanamke wangu, na najua wewe ni mtu mzima unaelewa namaanisha nini na kwanzia Leo huruhusiwi kumpa mwanaume yoyote mkono Wala kumkiss au kumkumbatia hiyo ni kwa wanaume wote hata kaka yako isipokuwa Mimi tu".
" Hata kaka yangu Nathan?
" Ndio nina maana yangu kusema hivyo.

Kwakuwa Emily alikuwa na shida hakuona haja ya kuendelea kuhoji alikubali.
" Nimekubali, ila naomba uwe ni uhusiano wa Siri kaka Nathan asijue kwasababu hawezi kukubali mimi kuwa na wewe . alijibu Emily
" chukua Namba yangu hiyo muda wowote nikikupigia basi haraka sana upokee, messege zangu ujibu kwa wakati na ninapokuhitaji uwepo au ufike haraka sana." Aliongea Raphael na kupanda gari lake akaondoka

Muda wote huo Joseph alikuwa kasimama pembeni kidogo anawaangalia aliogopa kumfanyia fujo Raphael Sababu alikuwa kawazidi Kila kitu , ana jeuri ya pesa na anaweza kufanya lolote hivyo hawezi kushindana nae.
" Huyu Emily anajifanya mjanja kudate na Mr Raphael Sasa ngoja nimkomoe.

Joseph alitoa simu yake akapiga simu kwao na kuwaelezea kuwa anataka kuoa.
" Hallow baba.
" Ndio kijana wangu.
" Nina jambo langu naomba ulifanyiwa kazi haraka sana iwezekanavyo .
" Jambo gani hilo?
" Baba wasiliana na baba mdogo wa Nathan Mr sagamba nataka nikampose Binti yao Emily .
IN THE NAME OF LOVE ❤️ 4

MTUNZI SMILE SHINE

Baba yake joseph alifurahishwa na uamuzi wa mtoto wake.
" Safi sana kijana wangu nimefurahishwa na uamuzi wako hata nyumba unayotaka kuingia ni nyumba sahihi sana kwako.
" Asante baba , naomba ufanye hivyo bila kuchelewa .
" Sawa kijana wangu.
Baada ya baba yake Joseph kukata simu alimpigia baba yake mdogo na Nathan na kumueleza nia yao.

Kesho yake Emily aliitwa kwa baba yake mdogo alipofika akamkuta Joseph na washenga wake.
"Emily ujio huu ni kwaajili yako unatakiwa kuolewa na Joseph"aliongea baba mdogo, Emily alimuangalia Joseph huku akiwa kakunja uso.

" Baba mdogo Siwezi kuolewa na mwanaume alietaka kunibaka na wote mnafahamu kuwa Joseph sio mtu mzuri . alilalamika Emily
"Hatuwezi kuona damu yetu inapotelea jela wakati solution ipo ,utake usitake utaolewa na Joseph" baba mdogo wa Nathan aliongea kwa kufoka.
" Joseph sio njia pekee tunayoitegemea......
" Yeye ndio njia pekee tunayoitegemea yupo tayari kumuwekea dhamana kaka yako na kufanya kesi iishe.
"Kama Emily Hataki nimuoe basi nasikitika kusema kuwa sitaweza kumsaidia Nathan na mnajua kabisa Mimi ndo mtu pekee ninaeweza kuwasaidia kwa Sasa lasivyo ataozea jela" Joseph aliozea kwa nyodo.
Watu wote walimkazania Emily aolewe na Joseph ikiwemo mke wa baba yake mdogo na Binti yao Linda.
Walitumia kigezo cha kumsaidia kumsaidia Nathan kama Sababu ya kumshawishi kuolewa na joseph
" Kama Emily atakubali basi leo nataka kuondoka na mke wangu mtarajiwa " . alisema Joseph huku akisimama na kuanza kumvuta Emily waondoke.
Emily aliomba msaada lakini hakuna aliehangaika nae Sababu wote walionyesha kumjali zaidi Nathan.
" Baba mdogo, mama nisaidieni mimi sitaki kuolewa na jose huyu sio mwanaume sahihi kwangu tafadhali nisaidieni.

Wakati akiendelea kuvutwa na kutolewa nje mara alikuja Raphael na bodyguard wake,
" Hebu muache mara moja. Raphael aliamuru
" Mmmh huna mamlaka ya kujizuia huyu ni mwanamke wangu nimeshafanya taratibu za kuposa.
" Nimesema muachie.
Raphael aliongea kwa mara ya pili lakini Joseph aligoma kumuachia.
Raphael alimpiga Joseph teke Moja tutakatifu akaanguka chini Washenga wakasogea nyuma.
" Kijana kwanini unafanya fujo nyumbani kwangu?
Alisema baba mdogo
" Mzee kaa mbali na hilo maana sitaki laana za wazee.
Raphael alimfuata Emily
"Emily uko sawa" aliuliza Raphael
Emily alijibu kwa kutingisha kichwa akiashiria kuwa yupo sawa.
"Joseph nimekuonya sana juu ya kumfuatilia na kumsumbua Emily Sasa naona unataka kuvuka mipaka"
"Emily lazima aolewe na Mimi Ili aweze kuokoa maisha ya kaka yake"alijibu Joseph
"Wewe kama nani kwenye huu mji? Nathan tayari ameshaachiwa kupitia dhamana yangu na kwa uchunguzi uliofanyika inaonekana kampuni yenu inahusika kwahiki kilichotokea,hivyo cha kukushauri kwa Sasa nenda kapambanie kampuni yenu" Raphael alimwambia Joseph.

Baada ya Joseph kuambiwa hivyo alitoa simu haraka haraka na kupiga polisi
" Hallow, habari afande yunis
" Salama.
"Vipi Nathan yupo wapi?
Sauti ya upande wa pili ilimjulisha kuwa Nathan kaachiwa huru kwa dhamana ya Raphael ,
Joseph alitoka mbio bila kuaga na kuelekea kwenye kampuni Yao.
Baba mdogo wa Nathan na familia yake waliona aibu na kuanza kujichekesha
"Tunashkuru sana Mr Raphael kwa kutusaidia katika hili,hatukuwa na namna nyingine ya kufanya kumuokoa Nathan"aliongea mama Yao mdogo.
" Karibu ndani kijana, mke wangu nenda kaandae vinywaji vijana wanywe.
" Hapana hatuhitaji chochote.
" Basi karibu ndani.
" Naomba mtuposhe nataka kuongea na Emily.
Watu wote waliondoka wakamuacha Raphael na Emily wakiwa wamesimama
"Vipi umeumia sana?inaonekana Joseph kakupiga"
"Hapana si sana Wacha nikapake dawa kwenye hii michubuko". alijibu Emily na kunyanyuka kuelekea chumbani kwake, Raphael alimfuata nyuma nae akaingia chumbani
"Heee raph umefuata Nini huku ?watu wakikuona haitaleta picha nzuri."
Raphael alitabasamu "nimependa ulivyoniita,pia usisahau kuwa wewe ni mwanamke wangu popote pale ulipo na mimi nitakuwepo" . aliongea huku akianza kumpapasa na kumkiss
"Raphael niache bwana kaka Nathan atafika hapa Sasa hivi"
Raphael hakumsikiliza aliendelea kumkiss mfululizo akiwa kambananisha ukutani.nje ya chumba cha Emily walisikia mtu anapandisha ngazi kuelekea chumbani kwa Emily
"Itakuwa ni kaka Nathan huyo"aliongea Emily kwa wasiwasi
Raphael alimuachia na Emily akifanya kutandika kitanda, mlango ulipofunguliwa Nathan aliwakuta Emily yupo bize anatandika kitanda na Raphael kasimama pembeni yake..
Emily alipomuona alimkimbilia Nathan na kumkumbatia
" pole sana kaka karibu tena nyumbani"Emily alikuwa anaongea huku anatabasamu muda wote
"Asante sana "alijibu nathan
Baada ya kuvunja kumbatio akaenda kumkumbatia Raphael
"Asante sana kwa msaada wako Raphael"
"Usijali unakaribishwa"Raphael alijibu tu kifupi
"Twendeni tukapate chakula cha mchana pamoja nilikuja huku kwaajili ya Hiyo"alisema Nathan...

Walitoka na kwenda kupata chakula cha mchana pamoja huku wakiongea mawili matatu baada ya kumaliza Raphael aliaga na kuondoka

" Kwakuwa umefanikiwa kutoka mnaonaje tunaandaa sherehe kidogo? Alisema baba mdogo.
" Tulikuwa tunataka kurudi nyumbani nikapumzike labda tufanye kesho.
" Sawa sio mbaya tutafanya maandalizi hiyo kesho.
Emily na Nathan waliondoka na kurudi nyumbani kwao

Family ya Nathan waliandaa sherehe ya kumpongeza Nathan kwa ushindi ,walialika watu wenye hadhi zao.kila mtu kwenye sherehe alimsifia Nathan na kubwa zaidi ni wao kusaidiwa na tajiri mtoto Raphael.
Nathan na rafiki yake Jackson walikuwa wamekaa sehemu Moja na Raphael lakini Raphael alikuwa kalala kwenye kochi.
"Vipi huyu jamaa mbona analala " aliuliza jack
"Huyu sehemu kama hizi yeye ndo anapata usingizi mnono "alijibu Nathan

"VP mbona Simuoni Emily"
" atakuwa anamalizia kujiandaa si unajua mambo ya wanawake kujiremba ili kuonekana wa tofauti kidogo" Nathan alimjibu Jackson
Baada ya muda mfupi aliingia Emily ukumbini akiwa kavalia Gani jeupe na Vito vya rubi,Kila mtu alimtolea macho hata Raphael alikurupuka alipokuwa amelala kutokana na minong'ono ya watu. Alimuangalia moja kwa moja huku akiwa anatabasamu
Nathan alimfuata Emily na kumshika kichwa",umependeza sana my little one"
"Ooh jamani Asante sana kaka "Emily aliachia tabasamu ambalo Raphael aliliona vizuri na kumfanya azidi kupata wivu maana hakutaka mwanaume yoyote amguse Emily. Na ukizingatia anajua Nathan na Emily sio ndugu wa damu .

Raphael alivizia muda ambao Emily alikuwa peke yake na kumfuata.
" Raphael hapa kuna watu naomba uwe na heshima hata kidogo tafadhali usije ukafanya chochote cha ajabu"
"Mimi sipo hivyo unavyofikilia lakini ninahaki pia kwa mpenzi wangu "alijiu Raphael na kumvuta Emily akamkumbatia.watu wote walibaki Wana waangalia
"Unafanya Nini wewe? Kila mtu anatuangalia " Emily Alimsukuma Raphael
" Acha kuringa basi mrembo Mimi nataka tu kucheza na wewe kwani hilo pia ni kosa ?
Raphael alimshika mkono Emily Hadi katikati ya ukumbi na kwenda kufungulia mziki.
kila mtu aliwaangalia wao
Walicheza kimahaba Raphael alikuwa anampapasa Emily mgongoni
Nathan aliliona Hilo na hakufurahia akakumbuka siku Moja alikutana na Joseph akamwambia amchunge sungura wake kuna mtu atampora.
Alipata wivu kwani hata yeye anampenda Emily kama mwanamke na sio kama mdogo wake ila kuna sehemu ilimbana akashindwa kuweka wazi hisia zake.

IN THE NAME OF LOVE❤️ 5

MTUNZI SMILE SHINE
" hakuna anayejua hisia zangu kwa Emily na nikuonyeshe kuchukizwa na kwenda pale kufanya fujo watu hawatanielewa.
Nathan alijaribu kuficha hisia zake lakini moyoni alikuwa anaumia.

Wakati party inaendelea Linda mtoto wa baba yake mdogo Nathan alikuwa anawaangalia sana Emily na Raphael ni wazi hakupendezwa na ukaribu wao.
alichukua glass mbili za mvinyo na kuweka dawa kwenye vinywaji alafu akamuomba muhudumu apeleke grass moja kwa Joseph na nyingine na kwa Emily.
Joseph alipokea na kuendelea kunywa maana kabla ya hapo alikuwa anakunywa kwa hasira alipowaona Emily na Raphael wanacheza pamoja .
Baada ya muda Joseph alijihisi vibaya akakaa chini , lakini kadri muda ulivyokuwa unaenda alizidi kulegea alipelekwa Moja kwa Moja chumbani na muhudumu wa hoteli inapofanyika sherehe.

Emily alipolelekewa glass alipokea na kutaka kuanza kunywa mara Raphael akamdaka mkono kwasababu alimuona Linda alivyokuwa anamkabidhi muhudumu ile grass pia alimuona Linda alivyokuwa anajificha ficha .
" Vipi mbona umenizuia nisinywe?
" Nahisi kuna kitu hakipo sawa.
Emily akicheka
" Unacheka nini?
" Nyie watu wenye pesa zenu huwa anaishi kwa mashaka sana.
" Una uhakika hakuna mtu mwenye ubaya na wewe kwenye hili eneo?
" Siamini kama nina maadui wakubwa wa kuweza kunidhuru labda kunikomoa tu.
" Basi kunywa.
Emily alikunywa ule mvinyo lakini alihisi kitu baada ya kumuona Linda anamuangalia sana akakumbuka kile alichokiongea Raphael muda mfupi uliopita, Emily aliweka grass mezani akatoka nje kwaajili ya kwenda kujitapisha mvinyo aliokuwa kinywa. Alifika sehemu alisimama na kugeuka nyuma akamuona Linda anamfuatilia.
" Hapa lazima kuna jambo , kuna kitu Linda amefanya nataka kujua kafanya nini.
alajifanya hayuko sawa alikaa chini mara Linda alifika.
" Wewe mbona umekaaahapa kuna tatizo?
Emily hakujibu alizidi kujilegeza, Linda aliachia tabasamu na kusema
" Kwisha kazi.
Alimpigia simu rafiki yake na kumuomba atoke nje haraka kwaajili ya kumpa msaada kwani hakutaka Nathan wala Raphael waone lile tukio .


Baada ya sekunde chache rafiki yake alitoka .
" Mpango wangu umefanikiwa Emily anaenda kudhalilika nisaidie tumbebe tumpeleke chumbani.
" Sawa.
Walimbebelea na kumpeleka kwenye chumba alichokuwa amelala Joseph na kumtupia kitandani kisha wakawa weka vizuri ili waonekane walikubaliana kwenda kufanya .
" Diana hili limeisha Emily atachukuwa na kila mtu yani Nathan hatataka kumsikia na Raphael atachukua kupita maelezo na mimi ndio nitakuwa pembeni ya Raphael.
" Sawa shoga yangu twende ikamilishe mpango kabla hawajaamka.
" Unafikiri wataamka saizi hawa.
Wakati wanatoka Emily alinyanyuka pale kitandani.
" Kumbe ndio akili zako finyu kiasi hicho?
Linda na furaha walishituka.
" Wewe mpuuzi inamaana hukunywa si ndio?
"Sijawahi kukukisea wala kukifanyia baya hivyo siwezi kuumbuka na nitaenda kukushitaki kwa hili maana nina uthibitisho.
Diana alivyosikia hivyo alitoka nje.
" Mimi Simo humo malizabebi nyie ndugu.
Diana aliondoka akawaacha.
" Wewe mtoto wa kuokotwa huna hadhi ya kuwa kwenye familia yetu wala kuwa karibu na Raphael .
Emily alishikwa na hasira alinyanyua chupa ya mauwa na kumpiga Linda kichwani .
Linda alipoteza fahamu Emily akampandisha kitandani na kumsogeza karibu kabisa na Joseph kisha akatoka na kufunga vizuri.

Wakati anahangaika kujitapisha ule mvinyo
Ghafla akaanza kuhisi joto.
Alitaka kwenda kutafuta maji ghafla aligonga a na Raphael.
" Emily mara hii umelewa?"aliuliza Raphael
"Nisaidie Raphael nimepewa dawa na Linda nahisi joto "
Dawa aliyokuwa amepewa ilikuwa inamfanya Emily awe na hisia kali.
" Nilikwambia ukawa mbishi.
" Nisaidie tafadhali.
Raphael alimbeba hadi kwenye chumba chake cha kupumzikia katika hiyo hoteli.
" nisaidie tafadhali" Emily aliongea kwa kulalamika
,"Unajua natakiwa kukusaidia vipi?"aliuliza Raphael
"Ndio wewe nisaidie tafadhali naumia"
"Kwanza niangalie vizuri unajua mimi ni nani?"
"Wewe ni Raphael bwana nisaidie"Emily alizidi kulalamika Raphael hakuwa na jinsi Ilibidi amtimizie Emily kile anachotaka Ili aweze kukaa sawa.walianza kukiss na hatimae wakazama dimbwini.
Baada ya muda Emily alikaa sawa akabaki kuona aibu,alitaka kuondoka Raphael akamzuia
"Unaenda wapi? Unanikimbia baada ya kunitumia?"
Emily aliangalia chini kwa aibu.
" Umeona sasa na hautaki kuniangalia hata usoni , husemi hata neno asante?
" Samahani haikuwa dhamira yangu kufanya hivi.
" Unamaana gani kusema hivyo ? Unamaana mimi ndio nilitaka ?
" Naomba tusahau yaliyopita.
Emily alivaa nguo zake haraka alafu akatoka chumbani.

Wakati huo Nathan alimtafuta sana Emily lakini hakumuona kabisa .
" Mbona siwaoni wote wawili atakuwa kaondoka na Raphael ?
Aliendelea kutafuta wakati anatoka nje ya ukumbi alimuona Emily.
"Ulikuwa wapi?
" Nilikuwa naitafuta Linda.
" Kaenda wapi?
" Sijui ila nimeambiwa alitoka na Joseph waliongozana kuelekea kwenye vyumba vyao hoteli.
" Unasemaje Emily?
" Ndio hivyo.
" Kwanini Joseph afanye hivyo? Nataka kuhakikisha.
Alisema Nathan kisha anaelekea mapokezi na kuulizia kama kuna mtu amechukua chumba anajulikana kwa kina la Joseph.
Ilionekana kweli Joseph kachukue chumba , Nathan alitaka aonyeshe chumba ili akashuhudie.
Mchezo ambao alikuwa kausuka Linda ukamgeukia badala ya watu kumfumania Emily wakamkuta yeye ndoyupo na Joseph.

Familia ilikusanyika
"Bamdogo hii ni aibu na Ili kuficha hii aibu nashauri Bora tu Linda aolewe na Joseph"alisema Emily.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote