KIJAKAZI BADALA YA MKE WANGU

book cover og

Utangulizi

NILIVYOMCHAGUA KIJAKAZI BADALA YA MKE WANGU

Waswahili usema kosea kila kitu lakini usikosee kuoa Walahi, nilikuja kuelewa akili hii baada ya kuja kumuoa ISHA mwanamke ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote.

Isha alijua kunipeleka puta alijua kunifanya nichizike.

Kitu cha kushukuru ni kwamba sisi ni wa Islam hivyo taraka aina mambo Mengi sana ila kama tungekuwa ni wakristo basi ningefia kwenye mikono ya Isha.

JE UNATAKA KUJUA ISHA ALINIFANNYA NINI TUKUTANE NDANI NDANI UKU….

NILIVYOMCHAGUA KIJAKAZI BADALA YA MKE WANGU

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 01

www.tupohapa.com

ANZA NAYO…….

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Ni asubuhi ya siku ya jumatatu, Ndani ya Jumba kubwa kiasi lakini ni jumba la kifahari lililojaa vitu kadhaa vya thamani kubwa.

Anaonekana mwanaume pande la mtu akitoka bafuni kuoga, uku akijifuta futa maji anasogelea kitanda na kumuamsha mke wake kWa kumtikisa na kumuita.


“Babe, babe, nimechelewa sana ujue na haujanyoosha nguo zangu “

Mwanamke huyo kwa uchovu wa hali ya juu, anafungua macho yake na kumuangalia mume wake na kisha anazungumza.

“Aaah babe nimechoka sana , hapa nilipo Nina hangover ya kutosha ujue “

“Are you serious right now?, babe nachelewa kazini lakini pia nachelewesha watoto Shuleni, amka uninyooshee hizi nguo please”

“Mwambie jamila akunyooshee Mimi Nalala”

Anajibu mwanamke huyo kisha anavuta Shuka na kujifunika mpaka usoni mwake.

“Hivi huyu jamila atafanya kazi ngapi umu Ndani ? Ametoka kuangaika kuwaandaa watoto, usafi wa nyumba nzima, Saa hizi anaandaa chakula vya watoto vya shule Ebu amka jamani “

“Aaah Bwana eeeh sitaki Kelele nimechoka mie “

Anajibu mwanamke huyo kwa hasira sana na kumfanya mwanaume wake kuchukia.

Mwanaume huyo anasogelea kabati na kuchukua nguo zake na kwenda kuzinyoosha.

Baada ya muda mwanaume huyo anaonekana akiwa ameshavaa na yuko tayali kuondoka.

“Thanks to you, Leo naondoka pasi na kupata kifungua kinywa”

Mwanaume huyo analalamika uku akitoka nje ya chumba iko.

Baada ya mwanaume kuondoka, mwanamke huyo anainuka na kurudia Maneno ya mume wake.

“Thanks to you Leo naondoka pasi na kupata kifungua kinywa”

Kisha Anacheka na kuendelea kuzungumza.

“Mwili wote huo bado unataka kula, baba bure ili “

Upande wa nje anaonekana mwanaume huyo akiwa na watoto wake waliovalia nguo za shule tayali kwaajili ya kuondoka.

SONGA NAYO….

Hiyo Bwana ndio hali halisi ya Nyumbani kwangu, niite Razack, watu wengi wamezoea kuniita mtu mkubwa kutokana na Kuwa mnene, yaaah Sawa Mimi ni menene lakini sio Mzigo, ni mtu ambaye najituma sana, nafanya kazi asubuhi Na mchana, na juhudi zangu zimeweza kubadilisha Jina la mtu mkubwa mpaka kuitwa Tajiri.

Hiyo uliyoiona hapo juu ni hali halisi ya ndoa yangu, oooh unajiuliza Kama Nimeona ? Yaaah Nimeona, I have two kids ambao ni mapacha na kwa sasa wako darasa la pili, Yaani ni bado wadogo, ni watoto ambao wanaitaji sana uangalizi wa wazazi.

Mimi Bwana kwenye kuoa nilikosea , Yaani niliangukia pia 😂🙌 imagine na huu mwili wangu halafu niangukie pua.

Nisiwe muongo, kipindi naangalia mwanamke wa kuoa Mimi niliangalia nyashi na uzuri na kweli nilipata mwanamke mzuri sana nyashi ipo ya kutosha Yaani.

Shida ambavyo mke wangu anayo ni uvivu na sio mvivu Yaani ni mtu ambaye apendi kabisa kujituma, Mke wangu nakumbuka nilikutana nae hotelin ambapo yeye alikuwa Kama muhudumu, kitendo cha Mimi tu kumuoa na kujua Kuwa anaishi Na Tajiri akaamua kuacha kazi na kuponda mali tu utazani Alizitafuta yeye.

Nyumbani kwangu kila kitu kinafanywa na KIJAKAZI wangu ambaye ni jamila, nyie huyu dada anaapepo yake mbinguni, jamila ndio anajua watoto wamekula nini, watoto wanalala Saa ngapi, watoto wanaenda shule na kurudi Saa ngapi, kwa Kifupi jamila alibabe majukumu ya mke wangu.

Nikiwa kazini na ni Majila ya mchana, niliweza kupokea simu kutoka kwa mke wangu.

“Yes babe”

Nilizungumza baada ya kupokea simu.

“Babe Mbona ujatuma hiyo Pesa mpaka sasa hivi jamani eeeh, Yaani nachelewa ujue Rafiki zangu wananisubilia “

Alizungumza mke wangu, hakutaka kujua nimeshindaje Wala nini, kuna muda uwa naona kabisa Kuwa mwanamke wangu ni zaidi ya chumba ulete.

Nilimsikiliza tu kisha nikakata na mwisho nikazima simu kabisa maana ananichannganya tu.

Baada ya Kama robo Saa hivi, Rafiki yangu ambaye niliku nafanya nae kazi ofisi moja alikuja na kuniambia.

“Upatikani Broh shemeji anakupigia sana Sijui kuna shida Nyumbani “

Nilimuangalia tu Rafiki yangu na kumjibu.

“Achana nae huyo “

Hapo Rafiki yangu alivuta kiti na kukaa kisha akaniuliza.

“Kwani bado hamjayamaliza ??”

“Tuyamalize wapi Broh, kiufupi Isha Amegoma kabisa kubadilika, wazee na viongozi wote wa dini wameshazungumza nae lakini amegoma, hapo ni anataka Pesa tu kWa sababu anataka awatoe shoga zake out “

“Lakini si Anapesa zake na yeye ?”

“Account yake kwa sasa hivi inasoma Kama WASAFI FM Yaani kapukuta yote na Mimi Walahi simuwekei Tena Pesa, aingie mjini aanze kazi nimeshachoka mie “

“Daaah kweli changamoto, pole sana ndugu yangu “

Huyu Rafiki yangu ndio mtu wangu wa Karibu sana na anajua takribani maisha yangu yote, anajua changamoto na kila kitu.

Baada ya muda niliwasha simu na kumpigia mke wangu na kumuuliza.

“Umeshaenda kufata watoto shuleni “

Nilimuuliza kwani muda wa watoto kutoka ulikuwa umeshafika, Mimi na mke wangu tuliwekeana utaratibu Kuwa Mimi nitakuwa naondoka nao asubuhi halafu mama Yao anawafuata mchana.

“KWa hiyo Saa hizi ndio unawasha simu si ndio ? Saa hizi ndio unajiongelesha ? Watoto wako utawafutaa Mwenyewe “

Alijibu Isha kisha akakata simu .

“Huyu mpuuzi nini “

Nilifoka.

Nilimpigia mke wangu simu mfululizo lakini hakupokea, hii ilinipa wasiwasi sana hivyo nilinyanyuka chapu na Kuwai shuleni kwaajili ya watoto wangu, na kweli niliwakuta wakishangaa shangaa tu uku watoto wengine wakiwa wameshondoka.

“Poleni daddy amechelewa “

Niliwaambia.

Niliwachukua na kwenda nao Nyumbani, Ila nafika tu kwanza nikakutana na Wakaka Kama wanne hivi wakiwa pamoja na mke wangu, na muda huo walikuwa wakiizungula gari yangu ambayo ni G WAGON.

“Nini kinaendelea hapa ??”

Niliuliza kwa jazba sana.

“Babe relax tupo kwenye biashara, unajua account yangu aina Pesa so nikaona niuze ata gari moja, nilipost hii range lakini naona baada ya kufika wamaipenda hii “

Alijibu mke wangu Tena pasi na Kuwa na wasiwasi wa aina yoyote ile nika……

ITAENDELEA….
NILIVYOMCHAGUA KIJAKAZI BADALA YA MKE WANGU

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 02

www.tupohapa.com

SONGA NAYO………

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Nikamgeukia mke wangu na kumfokea.

“Ingia Ndani “

“Lakini babe”

“Nimesema ingia Ndani, na nyie poteeni hapa haraka, kama kweli mnataka gari nendeni sehemu husika ya kuuza magari na sio Nyumbani kwangu”

Wakaka hao Wala hawakupoteza muda haraka wakaondoka.

“Sasa ndio nini babe kunizalilisha Kama hivyo, eeeh, ndio nini ? Hii ni week sasa nakuomba Pesa unipatii, hapa nilipo Nina madeni kila kona lakini Wala utaki kunisaidia wewe ni mwanaume wa aina gani lakini “

Nilichofanya ni kumshika mke wangu mkono na kwenda nae chumbani, kWa hasira nilimsukumia kitandani na kumuuliza.

“Nini unakosa umu Ndani ? “

Hapo hakuwa na majibu zaidi aliniangalia utazani anataka kunimeza vile.

“Kila kitu umu Ndani unapata, ukija kwenye kavazi kila style inayotoka nakununulia Mke wangu, account yako nilikuwa nakuwekea Pesa kila mwezi ni kipi unafanyia hizo Pesa ? Ukuwai ata kuwanunulia watoto wako ice cream Yaani hela zako ni hela zako, am sorry tu say this lakini mke wangu Una roho mbaya sana, Isha Una roho mbaya”

“Razack ni Mimi ndio unaniongelesha hivyo au ??”

Isha aliniuliza maana hakuwa anaamini kama kuna siku naweza nikawa mkali kiasi iko, Mimi ni mtu ambaye Mara nyingi uwa nakaa kimya pasi na kuzungumza kitu.

“Unafikili nakuogopa au ? Ukweli ni kwamba nakupenda sana lakini siwezi kuendelea kuvumilia huu ujinga ambao unanifanyia Sawa ? Kwanza nikuulize hiyo gari unayotaka kuuza ulichangia bei gani ? Ni kiasi gani ulichangia kwenye hiyo gari “

“KWa hiyo razack unataka kusema Kuwa mali zako sio zangu ??”

Ila huyu mwanamke Walahi ni pasua kichwa.

“Ni mali zangu, tangu Nimekuoa ni kitu gani umewai kuleta ? Nimekuvumilia for ten years Isha lakini inatosha sasa”

“Waoooooh “

Isha aliishia kusema hivyo tu na kuangua kilio, nilibaki nikimshangaa tu.

Muda huo huo simu ya mke wangu iliita na nilipoangalia Namba inayopiga iliseviwa utamu wangu, eeeeeeeh wanawake jamani 😂🙌 haya Nimeoa mimi lakini kumbe utamu uko nje.

“Pokea hiyo simu”

Nilimwambia.

“Huyu ni ndugu yake jamila nahisi anashida ya jamila”

Mke wangu aliamua kujitetea .

“Sawa ni ndugu wa jamila lakini ni utamu wako wewe si ndio ? Haya pokelea simu utamu wako mama “

Mke wangu aliogopa sana kupokea simu na hapo akatupia simu pembeni na kuniambia.

“You know babe, nimekumisii sana, Leo nataka nikupe style zote”

Hii Bwana ni moja kati ya trick ambazo Mara nyingi mke wangu uwa anazitumia katika kunipumbaza na Mara nyingi uwa nanasa kwenye mitego yake.

“Hizo style mpelekee utamu wako na nauli nitakupa maana najua hauna ata Mia”

Nilijibu na kutoka nje nikiwa na hasira sana.

“Jamila, jamila”

Nilitoka nje na kuanza kumuita jamila kWa sauti ya ya ukali utazani yeye ndio amenikosea.

“Watoto wamekula ??

Nilimuuliza..

“Hapana kaka ratiba Yao ni kwamba wanarudi wanaoga kisha wanalala kidogo wakiamka ndio wanakula “

“Ooooh Sawa”

Walahi jamila ni bonge la mama yaan, hii ratiba ni yeye ndio amewatengenezea watoto wangu na wameshaizoea.

“Me natoka nitarudi usiku sana”

********

Siku ziliendelea kwenda uku Nyumba yangu ikizidi kuwaka moto, niliacha kumpa mke wangu Pesa baada ya kugundua Kuwa Anatabia ya kununua wanaume kwaajili ya kulala nao.

Ila maisha ya ndoa ni Machungu
Sana Kama utapata mwanamke Kama wangu, Yaani Mimi nikiomba unyumba kWa mke wangu amachokifanya ni kujilaza na kuniambia.

“Maliza kazi yako me nilale”

Na mke wangu akisema hivyo ujue umekula kwako Yaani anakususia utazani umelala na robot, Ila siku yeye ndio akikuitaji Walahi unainjoy.

Ikiwa ni Majila ya asubuhi najiandaa kwaajili ya kwenda kazini , nikiwa navaa nilishangaa sana kuona Kuwa hakukuwa ata na boxer moja kwenye droo yangu ya boxer.

“Isha, Isha, boxer zangu ziko wapi ??”

“Kwenye chumba cha pasi kule “

Alijibu uku akiendelea kuchezea simu yake.

Nilitoka moja kWa moja mpaka kwenye chumba cha pasi na sikukuta ata boxer moja haraka nikarudi chumbani.

“Hakuna boxer kule “

Nilimwambia.

“Usumbufu tu “

Muda huo huo akaanza kumuita jamila.

“Jamila, we jamila, jamilaaaaaaaaaah “

Baada ya muda mfupi jamila alifika na kusimama nje ya chumba chetu.

“Abeeeh dada”

“Ebeeeh dada na uko nje Ebu ingia”

Hapo ndio niliamini Kuwa mke wangu Hayuko vizuri kichwani, Yaani Mdada wa kazi aingie chumbani kwetu na wakati huo Mimi nilikuwa nimevaa taulo tu.

“Abeeeh dada “

Jamila aliitika kwa Mara ya pili baada ya kuingia chumbani.

“Boxer za kaka ziko wapi ? “

Eeeeeh 😳 Walahi macho yalinitoka Yaani nguo zangu za Ndani anaulizwa dada wa kazi.

“Zipo kwenye tenga la nguo chafu”

“Jamila toka nje “

Nilimwambia.

“Atoke nje kwaajili ya nini? We jamila Jana si umefua wewe au ? Inakiwaje boxer bado chafu ??”

“Lakini dada nilishakuambia Kuwa siwezi kufua nguo zenu za Ndani “

Hapo Mke wangu alinyanyuka kWa hasira na kutaka kumpiga jamila lakini haraka nikamdaka na kumwambia jamila atoke nje kisha nika……

NAKUJA MY JAMANI HUYU MWANAMKE NI MIKOSI

NILIVYOMCHAGUA KIJAKAZI BADALA YA MKE WANGU

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 03

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Jamila alivyotoka tu nje nilimgeuza mke wangu kwa hasira sana na kumuwasha kibao kimoja cha mwana ukome.

Tangu nimemuoa huyu mwanamke sikuwai kunyanyua mkono wangu na kumpiga, tangu nimemuoa Isha sikuwai kabisa kumpiga lakini Leo ameniuzi sana.

“Huu mchezo wa jamila kunifulia nguo za Ndani umeanza lini ??”

Nilimuuliza isha.

“Kwahiyo ulitaka Nani afue ? Umu Ndani jamila ni Nani Kama sio dada wa kazi tu, kufua ni jukumu lake “

“Kwahiyo ndio anifulie nguo za Ndani ? Isha umekuwa je weee jamani eeeh, Mbona mwanzo ukuwa hivyo eeeh, Mbona haujiheshimu Kama Mke ? “

Muda huo mke wangu alinyanyuka na kuanza kuchukua nguo zake kwenye kabati na kuweka kwenye begi lake.

“Nimechoka sana haya maisha ya manyanyaso, Yaani wewe razack ni wa kunipiga Mimi ? Wewe ni wa kunifokea ? Walahi siwezi, naondoka na taraka yangu naitaka”

Weeeh kwa jinsi Ninavyompenda mke wangu halafu yuko serious kutaka kuondoka, haraka nikamuwai na kumkumbatia kwa nguvu sana na kumwambia.

“Nisamehe mama Angu eeeh, nisamehe mke wangu mrembo, ni bahati mbaya sikuwai kukusudia kukupiga ata siku moja ni shetani tu amenipitia nisamehe mke wangu “

Nyieeeh mwanaume Mimi na mwili wangu mkubwa wote nikajikuta nikiangua kilio mbele ya mke wangu nikiitaji msamaha wake, nyieeeeh Walahi Isha amejua Kunikamata.

“Razack unipendi ata kidogo kWa sasa, haunijali kama mke wako nimechoka mimi “

Hapo mke wangu aliangua kilo cha hali ya juu na kuna Namna niliona ni Kama Mimi ndio nimekosea, ila wanawake 😂🙌 Yaani Mimi ndio naona ni mkosefu khaaaah.

Zoezi la kulia liliisha kabisa na kugeuka uwanja wa mahaba, muda huo nilisahau kabisa kwamba nilikuwa najiandaa kwaajili ya kwenda kazini lakini pia kuwapeleka watoto shuleni.

Mimi na mke kWa asubuhi hiyo tuliingia mchezoni na mchezo ulikuwa mkali sana na ukizungatia ndio kwanza tumetoka kuombana msamaha..

“Nakupenda mume wangu “

Isha aliniambia kWa sauti nyororo kabisa ya kumtoa nyoka pangoni, Muda huo alikuwa amelala juu ya tumbo langu , bora tu niseme tumbo maana nikisema kifua nitawadanganya na huu unene wangu 😂🙌.

“Nakupenda Isha wangu, Naomba tusahau kila kitu “

“Me nimekusamehe mpenzi wangu, babe lakini unajua account yangu Haina kitu ??”

Isha aliniambia.

Ila Isha anajua kucheza na akili yangu, kwa wakati huo na hivi ndio nilitoka kuelewa utamu Wala sikuwa na muda wa kuuliza Mara Mbili Mbili nilichofanya ni kumuwekea tu Pesa kwenye account yake.

“Thanks babe I love you”

Isha Alijibu akiwa Amefurahi sana na kiss akanipatia.

Hapo hapo akainuka na kwenda Bafuni na kuanza kuoga, baada ya muda akaatoka na kuanza kutafuta nguo, alitafuta nguo kWa muda kisha akaanza kuita.

“Jamila, jamila, we jamila weeweeeeh “

Ila mke Wangu kWa Kelele tu yuko vizuri Walahi.

“Jamila wa nini jamani??”

Nilimuuliza.

“Kuna nguo yangu haipo hapa na ndio nataka kuivaa Saa hizi “

“Kwani unatoka ??”

Nilimuuliza.

“Yes babe lakini sichelewi kurudi”

Imagine ata kuagwa siagwi mpaka nimuulize Yaani.

Mke wangu akatoka nje na baada ya muda akarudi akiwa na hasira sana na kulalamika.

“Huyu mfanyakazi wako kichaa Sijui ameenda wapi”

Nilivuta simu yangu na kumpigia simu jamila na hakuchelewa akapokea.

“Abeeeh kaka “

“Uko wapi ??”

Na Mimi nikajikuta Nilimuuliza kwa. Hasira sana.

“Niko njiani narudi niliwapeleka watoto shuleni “

Uwiiiiiiiiiiiih Yaani hapo ndio nikashtuka Kuwa nilikuwa natakiwa kuwapeleka watoto shuleni daaaa 🥹 katika siku ambazo nimefeli Kama baba Basi ni Leo.

“Aaah Sawa usichelewe Kurudi”

Nilijibu kWa upole.

“Ameenda wapi ??”

Isha aliniuliza.

“Amepeleka watoto shule baada ya kuona Kuwa nachelewa”

“Sema huyu msichana ana kiherehere sana, asubuhi hii anawaangaisha watoto wangu na mibajaji kwani angesubili ata kesho si wangeenda “

Ila Shukran ya punda siku zote ni mateke Walahi, Yaani baada ya kumshukuru jamila ndio kwanza mke wangu anaanza kumlaumu na kumsema.

“Sasa me hii nguo Nani ataninyooshe “

Mke wangu alijilalamisha nilibaki nikimtazama tu, Yaani nilikuwa nikimuangalia utazani sio yeye aliyetoka kuigiza kuwa mke Mwema baada ya muda mfupi tu.

Basi Mwenyewe akajinyooshe nguo zake na wakati anataka tu na jamila nae akawasili Nyumbani.

“Watoto wangu umewapeleka na usafiri gani ??”

Isha alimuuliza jamila kWa hasira sana.

“Nilikodi bajaji dada “

“Hela umetoa wapi ?”

“Ni Pesa zangu za akiba ambazo uwa naweka “

Hapo mke wangu alimsogelea jamila na kumvuta sikio na kumwambia.

“Mwanzo mwisho Leo kuwapakia watoto wangu usafiri wako wa kijinga, wazazi wao Tuna magari kibao hapa Nyumbani halafu weeeh, Tena koma zaa wako ndio uwatese kama hivyo “

Aaaah Isha ni pasua kichwa, alimfokea snaa jamila kisha akamwambia.

“Muandalie mume wangu chai Leo yupo atoki, hakikisha anapata huduma nzuri nitarudi baadae “

“Sawa dada “

Alijibu jamila lakini kwa sauti ya kutaka kulia, kitendo cha mke wangu kutoka tu jamila akakaa kwenye kochi na kuanza kulia.

Hali hiyo Niliniumiza sana na ukizungatia jamila hakuwa na kosa lolote lile haraka nikamsogelea na kumkumbatia uku nikimtuliza.

“Ni hasira tu zile Sawa , msamahe sana “

Nilimwambia.

Ila na Mimi Sijui nini jamani Yaani kumkumbatia tu jamila Razack akasimama….

NAKUJA JAAMANI 😂🙌
NILIVYOMCHAGUA KIJAKAZI BADALA YA MKE WANGU

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 04

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Ni Kama jamila alihisi kitu haraka akasogea pembeni naa kwa sauti ya wasiwasi akaniuliza.

“Utakunywa cha na nini kaka ??”

“Am, aaaah, you”

Ata Sijui kigugumizi kilitokea wapi lakini nilijikuta nikishindwa kabisa kujibu swali dogo kabisa ambalo jamila aliniuliza.

“Au mikate na mayai ??”

Jamila akaniuliza Tena.

“Yaaah, yaaaah hayo hayo “

Nilijibu uku nikiondoka kwakweli.

Majila ya mchana nikiwa nimekaa zangu sebuleni nafanya kazi zangu za hapa na pale, jamila alikuja na kukaa pembeni yangu kisha kwa utulivu akazungumza.

“Kaka naweza nikazungumza na wewe ??”

Nilimuangalia kisha nikaweka miwani yangu vizuri na kumjibu.

“Bila Shaka”

“Samahaani lakini Kama nitakuwa nakosea lakini ni kwaajili ya watoto, Kiukweli malumbano yenu kila siku wewe na dada uwa yanawatesa sana watoto”

Hapo kwanza nilishangaa na kujiuliza hivi ni kweli sauti inafika mpaka uku chini jamani.

“Aswa kulwa, amekuwa akikosa usingizi Mara kWa Mara, anaweweseka sana na wakati mwingine kulia Majila ya usiku “

Kuna muda niliona ni Kama huyu jamila anadanganya hivi, maana yeye na watoto wangu wanalala vyumba viwili tofauti sasa amejuaje yote hayo, nilimtazama kwa muda na kumuuliza.

“Umejuaje Kama wanaweweseka usiku ??”

“KWa sababu nalala nao chumbani kwangu, kulwa amekuwa ni mtu wa kupata Homa za usiku na nakumbuka niliwai kumwambia dada kuhusu ili lakini hakufanyia kazi yoyote ile, week ile ambayo ulisafiri, kulwa aliumwa sana usiku na dad aliishia kumpa panaadol tu na hii ilinitisha sana, homa ilikuwa Kali lakini dada hakuweza kuchukulia maanani “

Eeeh hii sasa ni Mpya Walahi Tena, Yaani mpaka Mtoto wangu anazidiwa lakini Sijui kitu chochote.

“Dada ulivyomwambia alisema je kuhusu kumpeleka Mtoto hospital??”

“Alisema Kuwa bima zao zimeisha muda na wewe ukirudi ndio utalipia, kWa upande wangu niliona sio Sawa nilichukua tu Pesa yangu na kumpeleka hospital”

“Are you serious??”

Nilimuuliza kwa mshangao wa hali ya juu.

“Kaka siongei kwa ubaya lakini Naomba sana muwe makini na watoto, wao bado ni wadogo sana na wanawaitaji sana ninyi wazazi wao, Leo mimi Nipo nawaangalia Itakuwaje nikiondoka ? Hii siongelei kwaajili ya dada tu Naongea pia na wewe, Mara ya mwisho lini wewe kukaa na watoto wako na kufanya home work ??”

Daaaah swali ni dogo sana lakini ni zito sana kWa upande wangu, nilibaki nikimuangalia tu jamila ambaye alikuwa serious sana kWa wakati huo.

“Kuna muda najiuliza mmeniamini kiasi gani mpaka kuniachia majukumu Makubwa hivi kwenye Nyumba yenu lakini pia kWa watoto, sasa hivi matukio ni Mengi snaa duniani, Leo Nipo Mimi naishi nao vizuri vipi akija mwingine na kuwazuru hawa watoto ?? Halafu Mungu amewabariki sana ammewajaalia watoto ambao ni waelewa sana, watoto ambao ukiwafundisha kitu wanakushika muda wote na hawafanyi kinyume”

Aiseeeeeh huyu jamila imekuwa je mpaka amekuwa mfanyakazi wa Ndani jamani eeeh ? Mbona anazungumza vizuri kiasi hiki, Yaani jamila anazungumza Kama mama yangu, jamila anazungumza Kama mtu Mzima ambaye Ana busara sana.

“Yangu ni hayo tu, muda umeenda sana wacha nikawafuate watoto maana naona uko bize na dada nimempigia simu hajapokea “

Alizungumza jamila na kunyanyuka na kuelekea chumbani kwake, muda huo niliganda tu nikimshangaa jamila ambaye alijua kunishangaza kWa wakati huo.

“Ni huyu huyu jamila anayesema shule aliishia darasa la pili au ??”

Nilijiuliza kWa sauti kabisa maana jamila alijua kunishangaza.

“Me niko tayali, chakula nimekuwekea pale Kama utasikia njaa “

Jamila aliniambia uku akiondoka.

“Eeeh, jamila subili “

Nilimwambia nae akasimama.

“Wacha twende wote “

Basi nilinyanyuka na kuchukua funguo za gari na kWa pamoja Mimi na jamila tukaanza safari ya kwenda shuleni na kuchukua watoto.

Kwakweli jamila anajua ratiba vizuri Ila kufika tu na watoto nao walikuwa wakitoka, kWa Mara ya kwanza nilishuhudia upendo wa Dhati uliopo kati ya jamila na watoto zangu, wote walitoka moja kWa moja na kumkumbatia jamila na kuniacha Mimi nikishangaa shangaa Kama mtu baki vile .

“Shikamoo baba “

Walinisalimia baada ya wao kumaliza kumkumbatiana na jamila.

“Marahaba amjambo ??”

Niliwauliza kwa kujichekesha sana.

Moja kWa moja tulipanda gari na kurudi Nyumbani, Nyumbani pia ndio nilishangaa kabisa, watoto wangu walifika na kubadili sale zao za shule wenyewe, wakaenda sehemu ya kufua na kufua, alipomaliza wakaoga na kumuaga jamila na kwenda kulala.

Yale matendo yalinishangaza sana, Yaani watoto wa darasa la pili wanawezaje kujifulia nguo zao wenyewe.

Nilinyanyuka mtu mzima mimi na kwenda kuangalia nguo walizofua Kama zimetakata weeeeeh sio
Tu kutakata jamani ziling’aa vizuri sana.

Moja kWa moja nikamfata jamila na kumuuliza.

“Tangu lini wameanza kujifulia wenyewe ??”

Hapo Jamila aliogopa sana, kWa haraka akarudi nyuma na kuzungumza.

“Ni miezi minne sasa, lakini nakuaidi Kaka awatajifulia tena”


Jamila aliogopa Akihisi uwenda mimi nimechukia, lakini ukweli ni kwamba nilifurahi sana, Yaani nilifurahi kuliko kawaida.

“Ubarikiwe jamila “

Mke wangu Bwana alikuja kurudi Majila ya Saa 8 usiku na alikuwa amelewa sana, Yaani kalewa mpaka akawa ananiona mimi kama shoga yake vile na kuanza kulopoka hovyo.

“Unajua nini shoga Angu, kesho Tena pale pale na namtaka Kijana Yule Yule, Kijana anajua kupeleka moto Yule, kuna muda nilikuwa naona mpaka ile laki 5 niliyompa ni ndogo kWa kazi kubwa ambayo alinifanyia “

Daaah nilijisikia vibaya sana, Yaani Mimi nimetoa Pesa halafu kaenda kupewa Kijana mwingine uko nje kwaajili tu ya kuchapa uno.

Nilichukia sana na haraka nikatoka nje.

Nilitoka nje kabisa ya Nyumba Ila nilishtuka sana kumkuta jamila akiwa amesimama pembeni ya gari yangu na alikuwa amebeba Mtoto mgongoni.

Nika…..

ITAENDELEA…….

NILIVYOMCHAGUA KIJAKAZI BADALA YA MKE WANGU

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 05

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Nikamsogelea haraka sana na kumuuliza.

“Mnafanya nini usiku wote huu hapa nje ??”

“Nambembeleza kulwa hatulie”

Alijibu jamila uku akinesanesa kwaajili ya kumtuliza Mtoto wa mgongoni.

“Analia nini ??”

“Kama kawaida ni mwendo wa kuweweseka na mwisho kilio, Ila sasa hivi ametulia nasubili apate kulala tuingie Ndani “

Daaaah huyu dada jamani 🥺 Anastahili kuongezewa mshahara, yaani kumbe sisi tunalalaga tu halafu yeye ndio anaangaika kiasi iki na watoto.

“Ebu mlete “

Nilimwambia na kumpokea Mtoto, woiiiiiih huyu Mtoto ni Mzito na hivi amelegea kwaajili ya usingizi ndio kabisa .

“Usiwe unambeba atakuumiza mgongo huyu, hii week kwanza tutakuwa tukilala nao sisi upata kupumzika Sawa ??”

“Sawa kaka “

*******

Siku iliyofuata niliamka asubuhi na mapema na kuanza kufanya usafi wa Nyumba, niliganda yiye haya kwaajili ya kumsaidia jamila ambaye alikuwa akiangaika na kila aina ya majukumu ya pale Nyumbani uku akikosa usingizi kwaajili ya kuangalia watoto.

Baada ya kumaliza kila kitu, nilijianda ana kwenda kazini uku Nilimwambia jamila Kuwa watoto nitawafuata Mwenyewe maana ni Kama mama Yao amesahau majukumu yake.

Yaani mke wangu anasalimiana na watoto wake kama watu baki kisha anaendelea na mishe zake pasi na kujali watoto Wanahali gani.

Nikiwa ofisini, niliweza kumsimulia kila kitu Rafiki yangu.

“Ni jamila huyu huyu ambaye ulikuwa unasema Kuwa hatoweza kazi za Nyumbani ??”

Rafiki yangu aliniuliza.

“Huyo huyo Yaani, sasa hivi amekuwa zaidi ya mama, jamani ni mwanamke na nusu anajua kila aina ya majukumu”

“Broh make her happy, simchukii shemeji yangu lakini mkwe mkweli tu bora impoteze shemeji na sio kumpoteza jamila, hakikisha jamila aachi kazi mtateseka sana “

Hapo nilicheka sana kisha nikazungumza.

“Jamila ni mwanamke Bwana, itafikia kipindi ni yeye ataitajika Kuwa na familia yake, ataitajika Kuwa mke wa mtu na hatimaye mama Kwahiyo Kama muda utafika Basi Sitakuwa na budi Bali kumuacha aende “

“Yaaah ni kweli “

Mimi na Rafiki yangu tuliongea Mengi sana kisha tukaendelea na shughuli zetu.

********

Maisha yaliendelea kusoma kwakweli na jamila aliendelea Kuwa dada bora sana kwenye familia yangu.

KWa upande wa mke wangu ndio alizidisha kula starehe Yaani mke wangu alizidisha kasi kwenye kuzurula uko nje na kubadilisha wanaume Kama hana akili nzuri.

Simu moja Bwana Mtoto wangu mmoja alipata ugonjwa wa gafla sana ambapo alikuwa akitapika na kuharisha mfululizo.

Jamila Kama kawaida akabeba majukumu na kuwaisha Mtoto wangu hospital, hali ya Mtoto haikuwa nzuri hivyo baada ya vipimo akapatiwa kitanda Yaani walilazwa.

Muda huo Mimi nilikuwa kazini a taarifa nilipata baada ya jamila kunipigia simu na sikupoteza muda nikafika eneo husika.

“Umekuwaje ??”

Nilimuuliza jamila baada ya Mimi kufika hospital.

“Ata sifahamu kaka, ni gafla sana, lakini daktari amesema Kuwa ni mchafuko wa tumbo tu na ata Kuwa Sawa”

“Mchafuko wa tumbo na mtu ametundikiwa na kadripu kabisa “

Nilizungumza kWa jazba sana maana jamila anafanya Kama kitu cha kawaida hivi.

“Dripu ni kwakuwa alipoteza maji Mengi sana kwa muda ambao alikuwa akitapika na kubarisha”

Basi nilishusha jazba na kuanza kumtafuta mke wangu, nilimpigia simu mfululizo lakini hakupokea simu.

Baada ya muda mrefu kupita nilijaribu Tena kumpigia na safari hii alipokea lakini alionekana Kuwa kwenye Kelele nyingi sana.

“Babe nitakupigia baadae, Nipo kwenye birthday party ya Yule shoga yangu mariamu nitakupigia babe “

Alizungumza mke wangu haraka haraka kisha akakata simu.

Walahi nakuwaga na hasira lakini siku hii ndio nilipata hasira zaidi, nilijaribu kumpigia simu mke waangu Tena na Tena lakini hakupokea, mwisho nilimtumia ujumbe wa kumuelezea hali halisi ya Mtoto wake.

*******

Siku iliyifuata, Majila ya Saa 6 mchana, Mtoto wangu alikuwa Sawa kabisa na tukaruhusiwa kwaajili ya kurudi Nyumbani.

Tulifika Nyumbani na kuwaacha watoto watulie kisha Mimi na jamila tukaingia jikoni na kuandaa chakula.

KWa wakati huo Bwana Mimi na jamila tulishazoeana sana sana, jamila hakuwa akiniogopa Tena, alikuwa na uwezo wa kupiga story na Mimi kwa kujiachia sana pasi na kuniogopa, muda huo Mimi jikoni nilikuwa nikimenya Nyanya na jamila alikuwa bize akitengeneeza juice.

“Hivi Jamila yale maharage uwa unatuwekea nini wenzio ? Yaani matamu nawaonaga wakiwa kulwa Wanavyojilamba ?”

“Hahaha hakuna chochote mule zaidi ya hii peanut butter “

Alijibu jamila ukiendelea na kazi zake.

Muda huo huo akaingia mke wangu akijifanyakuwa amechanganyikiwa.

“Where is my babe? Is she fine ?”

Isha aliuliza uku akijiliza.

Nilimuangalia jamila kisha nikamshika mkono mke wangu na moja kWa moja safari ya kumpeleka chumbani ikaanza, nilifika na kumsukuma kwa nguvu sana na kumfanya aanguke kama Mzigo.

“Ulikuwa wapi ??”


Nilimuuliza.

“Babe I can explain, unajua “

Isha alianza kunipangilia Kama kawaida yake lakini safari hii sikumpa nafasi nyie nilikanyaga huyu mwanamke, nilimpiga utazani nilikuwa Nikipigana na Twaa kiduku, sikujali sauti yake ya kilio, sikujali maumivu ambayo alikuwa akisikia.

Kuna muda nilikuwa naona ni Kama aukii hivi, haraka nikasogelea mkanda wangu wa suruali na kuanza kumtandika nao Walahi nilipiga mpaka sauti yake ya kulia akabaki akinguruma tu.

“Nitakuja nikuuwe Mimi unaniletea upuuzi, tangu Jana nakuambia Mtoto amelazwa unanifudia Leo hii Tena Saa sana mchana na unataka kuniletea drama ? “

Hapo nilichukia taulo yangu na. Kuanza kufuta jasho ambalo lilinitilikika sana utazani maji.

“Rudia Tena halafu uone Kama sijakuzika mzima kunguni wa kike wewe, weeeh hivi kwakuwa sikunyagi kitu unaniona Mimi Kama kolo si ndio ? Ukirudia safari hii nakutengua uti wa mgongo uwe kilema, unafanya mzaa halafu unajua mama? Kuitwa mama sio kwenda leba tu mpuuzi weee “

Nilifoka na mwisho nikamuuliza na teke moja tu.

Walahi nilikuwa na hasira sana haraka nikatoka nje maana niliona kabisa huyu mwanamke naweza nikamuua

Wakati huo nilishamchakaza vya kutosha ni Damu tu zilikuwa zikimtililika kutoka puani.

Kufika sebuleni niliwakuta watoto wangu wamemkumbaatia jamila na walikuwa wakilia tu. hapo niliamini Maneno ya jamila aliposema kwua watoto wa ateşkes sana kutokana na malumbaano yetu.

“Nani anataka ice cream??”

Niliwauliza ili tu Kuwa Paris mood nzuri lakini ilishindikana na wakabaki wakiwa wamekumbatia tu jamila.

Siku hiyo Bwana Isha hakutoka nje ata Mara moja alinaki chumbani tu maana ile mi mnundu niliyompa sio ya kutoka nayo nje 😂🙌.

Majila ya Saa 4 usiku jamila akiwa Anosha vyombo akiw amevali nguo ya kulaalia, Walahi nilijikuta nikimuangalia sana na niligundua ni kiasi gani ameumbika, Sawa mke wangu ako na nyashi kubwa lakini aka ka mwili ka jamila ni mama lako hot sana.

Sikuwai kumuona jamila akiwa kwenye mavazi hayo na hiyo ndio ilikuwa Mara yangu ya kwanza, muda wote huo nilikuwa nikimuangalia jamila lakini jamila akiwa amejua Kama kuna mtu akamuangalia.

“Ooooh kaka”

Jamila aliniita kWa mshtuko baada ya kuniona.

Mwili wangu ulishindwa kabisa kuvumilia mihemko yangu na pasi na kufikilia nikamsogelea jamila na kumkumbatia kwa nguvu sana na kuanza kumpapasa

je nini kitafuta ? TUKUTANE sehemu inayo.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote