KIND LOVE ❤️(Mapenzi na ahadi)

book cover og

Utangulizi

KIND LOVE ❤️(Mapenzi na ahadi)
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 01

www.tupohapa.com

ANZA NAYO...........

Babe nipost, kwani me si mali yako?, una muogopa nani ai wewe, Baby nichumu, mwaaaaaah, kwani me si mali yako, unamuofia nani, au weweh

Achaneni na nyimbo za watu, hivi hali yako ya mahusiano ikoje kwa sasa, usinijibu, ji jibu mwenyewe, halafu kama mahusiano yako hayaeleweki jipige kifua halafu sema one day yes.

Love, love, love, nimekuita mara tatu, woiiiih, kwanini unatutesa sisi watu wengine na kufanya watu wengine wainjoy?, yaani kuna sisi hapa kutwa nzima ni vilio tu, halafu kuna watu mahusiano yao ni raha kwenda mbele.

Leo nimewaletea kisa hiki kipya kinachokwenda kwa jina la KIND LOVE ukisikia hivi unaelewa nini? Wacha nikueleze maana halisi ya kind love kwa siku ya leo.

Ikiwa ni kwenye jumba kubwa, jumba la kitajiri, ndani ya chumba kimoja ambacho ukiangalia unajua kabisa iki chumba ni cha wanawake maana kilipangwa vizuri na mapambo yake yalikuwa ni ya kike.

Ndani ya chumba iko, kitandani wanaonekana mabinti watatu wakiwa wamelala, naweza kusema kuwa mabinti hawa ni walalavi sana, kwa jinsi ambavyo walikuwa wamelala ukiwaona lazima uvunje mbavu kwa kucheka.

Mmoja kati ya wasichana hao, anakurupuka usingizini na kupiga kelele moja matata na kuwafanya wenzie kuamka kwa mshtuko wa hali ya juu.

Msichana huyo aliyeshtuka anashika kifua chake na kupima mapigo ya moyo kisha anaanza kukemea.

"Kwa jina la Yesu, eeeh Mungu niepushe na hiki kikombe, Mungu kumbuka mimi ni binti yako ambaye Nasali sana lakini pia natoa sadaka ipasavyo, eeh Mungu nijibu maombi yangu "

Msichana huyo alimaliza kukemea na kutelemka kitandani, muda wote huo wenzie walikuwa wameganda tu wakimshanga, mmoja kati ya wasichana hao alivunja ukimya na kumuuliza.

"Kilichokufanya upige kelele kama umeona kitu cha ajabu ni nini??"

Msichana mwingine akadakia.

"Umetushtua mno, ni ndoto ya aina gani tena ??"

Msichana ambaye alipiga kelele alisimama na kuwaangalia mwenzie kwa muda kisha akawaambia.

"Kwanza kabisa saa hizi ni saa 3 asuhuhi kumbukeni kuwa mzee Mengi anaenda kutunyoosha vilivyo, ukiachana na hivyo walahi nimeota ndoto mbaya sana leo, sijawai kuota ndoto kama hii"

Wasichana wale walitoa macho na kwa pamoja wakamuuliza.

"Ndoto gani ??"

"Nimeota naolewa"

Jibu la msichana huyo liliwafanya wenzie wacheke sana mwisho walitoka kitandani na kuingia bafuni na kujiweka mwili Safi kisha wakajongea sebuleni.

Ooooh poleni kumbe sikutoa utambulisho, iko hivi, Mzee Mengi, ni mzee ambaye amebarikiwa maokoto ya kwenda, yaani ikija upande wa pesa huyu mzee yuko vizuri.

Lakini pia mzee Mengi amebarikiwa mke mazuri sana, mke mtaratibu na mtulivu, katika uzazi wao, wazee hawa waalibarikiwa mabinti watatu ambapo binti yao wa kwanza alijulikana kama NEEMA, binti yao wa pili Alijulikana kama MANKA na binti yao wa mwisho ni DIJAH.

Neema na Manka ni wasichana ambao tayali wameshaanza maisha yao, yaani wameshaolewa na wanamakazi yao, ila wamejiwekea ratiba ya kukutana nyumbani kwao kila mwisho wa mwezi.

Dijah ndio binti wa mwisho wa mzee Mangi, lakini naweza kusema kuwa Dijah ni binti kivuluge sana, ukimuuliza mzee Mangi ni mtoto gani amemsumbua basi lazima atamtaja Dijah

Dijah ni binti ambaye alikuwa akipewa pesa ya ada apeleke shuleni ujue hiyo pesa haifiki na kama ikifika Basi inafika ikiwa pungufu.

Dijah ni binti wa miaka 26, amehitimu elimu yake ya chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 24, na aliweza kuajiliwa kwenye moja ya ofisi maalufu sana hapa dar es salaam tena kwa kupitia connection ya baba yake.

Tuachane na utambulisho na tuendelee sasa, Dijah ndiye msichana ambaye aliota ndoto na kujikuta akipiga kelele na kuwaamsha wenzie.

Wasichana hao baada ya kushuka sebuleni na kuungana na familia yao, walikuta kuwa kuna mambo tofauti sana, kulikuwa na vyakula vya kutosha, lakini pia wazazi wao walionekana kuwa na furaha ya hali ya juu.

Kama kawaida, mcharuko wa familia, yaani Dijah baada ya salamu akamsogelea baba yake karibu na kumuuliza.

"Kuna nini? Au mnagawa mali ??"

Ila Dijah daaah, kama ako na akili zingine basi atatoboa kwenye maisha yake lakini kama ni hizi hizi aandike ameumia.

Mzee Mengi alimuangalia last born wake kisha akatabasamu na kumwambia.

"Sogelea meza ya chakula na upate chakula na uachane na mawazo yako ya njaa "

Dijah hakuonekana kuridhika na majibu ya baba yake hivyo akapaza sauti na kuuliza.

"Nini kinaendelea umu ndani jamani, kwanza ni asuhuhi lakini naona kila mtu ana hekaheka za kutosha, sawa najua ni siku yangu ya kuzaliwa lakini hii mood sio ya birthday kabisa "

"Kuna wageni wa muhimu sana tunawatalajia siku ya leo " alijibu Mke halali wa mzee Mengi, lakini pia mama mzazi wa mabinti hao ambao ni warembo sana.

"Mmmh wageni gafla hivi ni wageni wa aina gani ambao wanakuja pasi na sisi kupewa taarifa ??" Neema aliuliza.

"Acheni maneno mengi, kunyweni chai hapo na muangalie mazingira uko nje na jikoni, kama amuwezi nyie wenye makazi yenu mnaweza kuondoka " alijibu mzee Mengi na kuelekea chumbani kwake.

Mabinti hao walicheka na kubaki wakiangaliaana tu uku wasijue ni nini kinaendelea aswa aswa maana ni kama wazazi wao walikuwa wanawaficha jambo.

Majila ya saa 8 mchana, magari mawili ya kifahari, yaliwasili nyumbani kwa mzee Mengi, Mzee Mengi na mkewe walionekana kufurahi sana, waliwakaribisha wageni wao wakiwa na tabasamu pana usoni mwao.

Upande wa pili wanaonekana mabinti hao watatu wakiwa juu ya ghorofa wakiwaangalia wazazi wao wanavyokaribisha wageni.

Manka aliangalia kwa muda kisha akazungumza.

"Mmh hizi sura ngeni kabisa au wenzangu mmeshawai kuziona ??"

"Labda tumuulize Dijah, mama mwenye makazi yake, na vile ataki kuolewa eeeh hii nyumba utajionea mengi binti " alijibu Neema na wote wakamgeukia dijah.

"Mnaniangalia hivyo kama nini? Ata hivyo siwajui pia, halafu hayo mambo ya mimi kuolewa yamefata nini, unajua bhana maisha ni kuchagua, yaani mimi na umri huu nikakae na kuanza kukua mke wa mtu? Aah tuheshimiane my zangu mimi kutoka kwenye hii nyumba mpaka nifikishe miaka 35, kwanza subulini naondoka kwenda wapi 😆 yaani umu ndani labda Mzee Mengi na mke wake watoke ila sio mimi "

Yaani Dijah ni mtu ambaye unamuongelesha mambo madogo tu ila mjibu ambao anakupa unaweza ukajaza karatasi tatu, tena usiombe umkuta akiwa amechukia.

Kwa namna moja au nyingine, naweza kusema mabinti hao wamefunzwa vizuri aswah, baada ya kelele zao zote, walishuka ngazi na kwenda sebuleni kwaajili ya kukaribisha wageni lakini pia kuwasalimia.

Upande wa pili, wafanyakazi wa nyumba waliandaa chakula na kutenga mezani.

Dijah baada ya kusalimia, kwa mwendo wa polepole alimsogelea baba yake na kumuuliza kwa sauti ya chini sana.

"Kwani hawa wakina nani baba maana sio kwa kuwachekea uko, wanawekeza kwenye biashara zako au ??"

Mzee mangi alijichekesha kisha akajibu.

"Unaweza kwenda chumbani nitakuita"

Basi dijah akiwa na dada zake wakaongozana na kwenda chumbani kwao, walibaki wakijiuliza uliza maswali ambayo hayakuwa na majibu kwa upande wao.

Baada ya muda, Neema na Manka wakatoka chumbani na kwenda sebuleni ambapo baba yao alikuwa amewaita.

Baada ya kama nusu saa hivi, manka alitoka sebuleni na kumfata Dijah chumbani na hapo alimkuta Dijah akiwa zake live uko mjini tiktok akipiga story na fans wake kwani alikuwa na kijiji chake uko tiktok.

"Baba anakuita "
Manka alimwambia Dijah.

"Aaah huyo mzee nae jamani, me ndio kwanza nimeingia live saa hizi, kwani kuna haraka sana mpaka nije saa hizi?"

"Acha ujinga wewe, inuka haraka "

Basi vuta nikuvue zikaanza pale mwisho Manka alishinda na kwa pamoja wakatelemkia sebuleni.

Dijah alibaki akishanga tu kwani kitendo cha yeye kufika sebuleni ni kama kilimfurahisha kila mtu maana watu wote walimgeukia na kubaki wakitabasamu tu.

Baada ya dijah kutulia, mzee Mengi alisafisha koo lake kwa kunywa maji kisha akaanza kuzungumza.

"Aaaah Mr Tony, huyu ndiye Dijah binti yangu wa mwisho kabisa "

"Oooh waoooh watoto wanakuwa haraka sana, nakumbuka huyu mara ya mwisho namuona alikuwa sijui darasa la 5 yaani hadi sura imenipotea ningekutana nae barabarani ningempita "

alijibu Mr Tony ambaye kwa kumuangalia unaona kabisa kuwa umri umeenda, yaani Mr Tony na mzee Mengi wanalingana.

"Ata yeye najua hakukumbuki " alijibu Mzee Mengi.

"Ni kweli "

Mke wa mzee Mengi aliinuka kwenye sehemu ambayo alikuwa amekaa na kumsogelea dijah kisha akaanza kuzungumza.

"Dijah binti yangu, siku zote mema ndio kitu ambacho sisi binadamu tunaitaji, tumekuwa tukifunga na kusali mema yatutembelee, na leo hii mema yamatutembelea, Mr Tony na familia yake kama unavyowaona wako hapa kwaajili yako wewe"

Dijah alitoa macho na kuweka umakini mkubwa sana ili kuelewa maneno ambayo alikuwa akiambiwa.

"Mr Tony hapa ana kijana wake ambaye anaitaji kuoa, na amekubali familia yake imchagulie mke, na jicho la Mr Tony limekuona wewe Dihaj wetu"

Dija aka.....

ITAENDELEA

KIND LOVE ❤️ (Mapenzi na ahadi)
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 02

www.tupohapa.com

SONGA NAYO.......

Dijah akainuka kwa jazba, lakini kabla ajazungumza kitu baba yake akadakia na kuzungumza.

"I told you Mr Tony, binti yangu atafurahi sana sana, tazama jinsi ambavyo yuko existed, nafikili jambo limeenda kama lilivyopangwa"

Ukiachana na dijah Kuwa mcharuko na msumbufu kwenye familia yake, lakini pia Dijah ni msichana ambaye anatunza heshima ya familia yake kwa namna fulani hivi.

Dijah kwa sura ya aibu na tabasamu la mgongo wa chupa, alimsogelea Mr Tony na kumpa mkono uku akipiga goti ikiwa kama ni ishara ya kumshukuru na kuonesha kupokea ombi lao.

Wanawake kama ujuavyo tena, mke wa Mr Tony na mama mzazi wa dijah waliinuka na kuanza kushangilia uku wakipiga vigelegele.

Baada ya kila kitu familia ya Mr Tony iliaga na kuondoka na hapo Dijah akaamsha mashetani yake.

"Kwahiyo hii familia mmeamua kunifukuza nyumbaninkwa stahili hii ??"

Neema na Manka waliangua vicheko vya maana kisha mama yao akazungumza.

"Na nyie acheni utoto mnachocheka kitu gani badala ya kumuelekeza mdogo wenu, Dijah mama, hakuna mtu anayekufukuza nyumbani kipenzi changu lakini utakaa nyumbani mpaka lini ??"

"Kama ishu ni kukaa nyumbani basi nitaama, nitaenda kupanga mbali na hapa na nitakuja kusalimia kama awa wengine "

"Dijah binti yangu jiandae kuwa mke na mama bora kama mama ako " alizungumza Mzee mengi na kuachia tabasamu mwanana kabisa.

"Halafu baba wewe ndio umepanga hivi vitu si ndio? Me sitaki kuolewa, muda bado me bado mdogo sana baba angu niangalie kwa jicho la pili " Dija aliendelea kulalamika.

"Mdogo wich ??" Neema aliamua kuuliza na kuachia kicheko.

Dijah akimuangalia neema kwa hasira sana maana aliona kama anamkejeri hivi kisha akamwambia.

"We nawewe kaa kimya uko, mkubwa mzima hovyo "

Kwanza kabisa naomba niseme kuwa katika watu ambao ni dakika mbili mbele ni neema na Dijah, yaani hawa ni watu ambao dakika mbili wanacheka, dakika mbili wanagombana.

Neno la mkubwa mzima hovyo lilimkela sana Neema ambaye aliishia kumuangalia tu Dijah mwisho akapanda ngazi na kuelekea chumbani akiwa na hasira ya kutosha.

"Ni maneno gani umemwambia dada ako??" Mama Dijah aliuliza kwa hasira.

"Amezidi" alijibu dijah na kisha kutoka nje.

Mara nyingi Dijaha anapokuwa na hasira uwa anatoka nje na kwenda kukaa kwenye bembea zilizopo kwenye bustani kubwa sana ambayo ilikuwamo ndani ya fensi yao.

Upande wa neema aliingia chumbani na kuanza kupaki mavazi yake akitaka kurudi nyumbani kwake.

"Usiniambie kuwa unaondoka muda huu na tumekubaliana kuwa tutaondoka kesho?" Manka alimuuliza Neema pale tu alipoingia chumbani.

"Aaah nafikili ni muda wa mimi kufocus na maisha ya ndoa yangu, haiwezekani kila nikija kwenye hii nyumba lazima nipewe maneno machafu na huyu sisimizi mmoja ambaye ata kiganjani ajai"

"Neema bhana, yaani wewe ndio mkubwa kati yetu ujue, unapaswa kumzoea Dijah ata hivyo si unajua akili ya Dijah jamani "

"Manka wacha nikatulize akili yangu nyumbani kwangu"

Neema alinyanyua pochi yake na kutoka nje akutaka kabisa kusikia wala kuelewa maneno ya Manka, kwa haraka akaenda kuwaaga wazazi wake na kuondoka.

Kwa upande wa Dijah alivalia headphones masikioni na kuweka wimbo wake wa huzuni ambao mara nyingi amekuwa akiusikiliza pale tu anapokuwa hana amani.

Majila ya usiku, Dijah bado akionekana kutokuwa sawa, aliingia chumbani kwake na kujitupia kitandani na kuendelea kusikiliza wimbo wake.

Dijah aliwa bize na mziki, Manka aliingia chumbani na kukaa pembeni yake na kuomba azungumze nae.

"Unajisikiaje??" Manka alimuuliza Dijah.

"Like am drowning " alijibu Dijah na kujikuta akianza kulia.

Ila jamani, Dijah ni kwamba atakj kuolewa tu au tabia za last born zinamsumbua, maana sio kwa stahili hii.

Manka kama dada mwema alitimia muda wake kumtuliza Dijah kisha akaanza mazungumzo.

"Kwanza kabisa naomba ujue kuwa maneno uliyomwambia dada Neema si mazuri ata kidogo, mimi yamenikela lakini pia yamemuumiza sana Neema na kumfanya aondoke akiwa hayuko sawa kabisa "

Dijah alishtuka sana na kuka vizuri maana likiwa ameegema mgongo wake na kwa sauti ya mshangao akauliza.

"Ameondoka!!"

"Yaaah ameondoka, ameondoka akiwa na maumivu makubwa, ameondoka akiwa hana amani ata kidogo, maneno yako machafu ya hasira yamemnyima amani"

Dijah alijikuta akiumia sana, kwa haraka akachukua simu yake na kumpigia dada ake lakini simu haikupokelewa.

******

Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya kazikazi, yaani siku ambayo kila mwajiliwa atawajibika kwenda kazini.

Ikiwa ni asuhuhi ya saa mbili asubuhi, dijah alijiandaa kwaajili ya kwenda kazini lakini kabla hajatoka akaamua kumpigia simu neema lakini bado neema akupokea simu.

DIJAH akafunga safari na kwenda kazini kwa Neema baada ya kuona Kuwa Neema Apokei simu zake.

“Umekuja kufanya nini??”

Neema alimuuliza DIJAH baada ya kumuona DIJAH ofisini kwake.

“Nimekuja kuzungumza na wewe dada’’

Alijibu Dijah kWa sauti ya upole na yenye utulivu wa hali ya juu Ndani yake.

“DIJAH huu ni muda wa kazi lakini pia na wewe ni muda wako wa kwenda kazini”

“Najua lakini siwezi kuchukua muda wako mwingi, Nimekuja kukuomba radhi juu ya kitu kilichotokea siku ile, Nisamehe sana dada Angu, Nisamehe Neema wangu’’

Neema Aligeuka na kumuangalia Mdogo wake kisha akatabasamu na Kimjibu.

“Unachelewa kazini ujue, me niko Sawa na Nimekusamehe kipenzi chaangu’’

Mtu na Mdogo wake wakakumbatiana pale kisha Dijah akaaga na kwenda kazini.

******

Siku zilikimbia hatimaye mwezi mmoja ulikatika tangu DIJAH apate mchumba ambaye ajawai kumuona.

Ikiwa ni siku ya weekend, familia ya dijah ilimchukua Binti Yao na kumpeleka kwenye familia ya mr Tony kwaajili ya kwenda kukutana na mwenza wake kWa Mara ya kwanza.

Walifika pale na kila mtu alikuwa Na furaha sana isipokuwa Dijah ambaye hakuwa akitaka kuolewa kabisa, Yaani dijah ni Anajiona yeye Kuwa ni Mdogo sana.

“Mishy, mpeleke Dijah chumbani kWa mwenza wake wakaongee kidogo “

Alizungumza Mr Tony na mishy ambaye ni Binti wa mwisho wa familia hiyo akafanya Kama alivyoambiwa.

Mishy alimfikisha Dijah kwenye chumba hüsına kisha akaondoka.

Ndani ya chumba iko, anaonekana mkaka akiwa amesimama na alikuwa akiangalia dirishani na kumfanya Dijah aone mgongo tu.

Wawili hao walisalimiana pasi na kuonana kisha mkaka huyo aliyejukikana Kama ZION akauliza.

“Kwanini umekubali kuolewa na mtu ambaye umefahamu ??”

Dijah akasogea mbele kidogo kisha akajibu.

“Walionichagulia ni wazazi wangu na ndio watu Baki hivyo siwezi kuwakatalia, na ni wazi Kuwa mzazi awezi kumpeleka Mtoto wake motoni “

Mkaka huyo akatabasamu na kuonesha Kuwa amevutiwa sana na majibu ya DIJAH kWa furaha Akageka nyuma ili aweze kumuona msichana huyo ambaye alionekana Kuwa na Busara sana.

Baada ya Zion Kugeuka, kWa pamoja Wakashtuka.

“Wewe ??”


JE AWA WATU NI WANAJUANA AU LAAAH? TUKUTANE SEHEMU IJAYO….

KIND LOVE 🧡 ❤️(Mapenzi na ahadi)
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 03

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……..

Dijah na Zion walibaki wakishangaana tu mwisho Zion akamuuliza Dijah.

“Kwahiyo unataka kuolewa na Mimi??”

Dijah akamuangalia Zion kWa muda Tena kWa yale macho ya dharau ya hali ya juu kisha akajibu.

“Ningejua kama ni wewe Wala nisingekubali”

“Ata hivyo hatujachelewa maana ata Mimi ningejua kama ni wewe Wala nisingekubali”

“Lione sura lake baya, sasa
Sikia hapa Tunatoka nje kwa pamoja na kwenda kukataa mbele ya wazazi Sawa??”

Alizungumza Dijah uku machoni mwake akionekana Kuwa na wasiwasi wa hali ya juu.

“Sawa”


KWa pamoja wakatoka nje na kwenda sebuleni ambapo wazazi walikuwa wakiwasubilia kWa hamu sana.

“Mmeshazungumza na kujuana si ndio??”

Mr Tony aliwauliza.

“Ndio baba”

Basi wazazi wakaangaliana kisha mr Tony akauliza.

“Kila mtu si amekubaliana na hili na tunaweza kuendelea na process zingine??”


Dijah na Zion wakaangaliana kisha kwa pamoja Wakajibu.

“Ndio”

😂🙌 Ila hawa watu Sijui Kama ni wazima si wakikubaliana Kuwa wanaenda kukataa haya mahusiano Yao sasa imekuwaje wote wamekubali Tena kwa pamoja.

Wazazi walifurahi sana wakabaki wakipongezana, mwisho Dijah na Zion wakarudi chumbani kila mtu akiwa na hasira sana na mwenzie.

“Sasa Kwanini umesema ndio??”

Dijah alimuuliza Zion baada ya kufika chumbani.

“Ulitaka niseme nini ikiwa wewe pia umekubali? Halafu Dijah nahisi hii yote ni mipango yako Walahi Tena”

“Weeeh unawazimu nini, kwani nilikuambia useme ndio au? Zion you’re my ex okay, na sikuwai Kuwa na ndoto ya kurudiana na wewe”

“Kaa kimya Dijah kimya naitaji kufikilia me siwezi kuoa mwanamke Kichaa Kama wewe”

“Kichaa wewe na ukoo wako Sawa? Zion wewe ni mwanaume ongea na familia yako waambie Kuwa ujanipenda Sawa, kWa upande wangu muda wa kuolewa bado sana, lakini ata ukija kufika sitakuja kuolewa na wewe kunguni mmoja wa kiume”

Okay my zangu iko hivi, Dijah na Zion ni watu ambao walishawai Kuwa na mahusiano uko nyuma kipindi Wanasoma na mahusiano Yao haya kwenda Sawa hivyo Wakaachana, tutajua uku mbele ni Kwanini hawa watu waliachana.

“Dijah huu Mdomo wako utakuponza ni Nani Unamuita kunguni? Walahi nakuchukia sana wewe Binti, I hate you okay”

“Aliyekuambia Kuwa nakupenda Nani na bichwa lako Kama Tunda za ubuyu”

Wawili hao walibaki wakizozana tu hakukuwa na maelewano ata kidogo.

Majila ya jioni Dijah na familia yake walifunga safari na kurudi Nyumbani kwao.

“Aaaah Binti yangu umebahatika jamani, Yaani Yule Kijana anasifika vizuri sana”

Alizungumza mama Dijah, muda huo walikuwa kwenye gari wakirejea Nyumbani kwao.

“Aaaah mama jamani, aaaaah me sitaki uniambie masuala hayo, ata hivyo mnanionea mimi bado ni Mdogo sana “

Wazazi wa Dijah wakaangaliana na kucheka sana kisha mama Dijah akazungumza.

“Una miaka 26 sasa wewe sio Mtoto Tena, Dijah Mwanangu, Mimi mwenzio niliolewa na baba yako nikiwa na miaka 17 tu na nilichaguliwa na wazazi, Tena bora wewe umeweza kukuutana na mwanaume wako kabla ya kila kitu lakini Mimi nilikuja kumuona siku ya harusi”

Hapo Dijah ni Kama Ka story kalianza kumnogea kwa shauki akauliza.

“Yaani ulikubali kuolewa na mtu ambaye ujamuona ata sura yake??”

“Ndio, aaaah sisi kwetu Tuna ile kuchezwa baada ya Binti kuvunja ungo, sasa Mimi nilivunja ungo nikiwa shuleni, na nilipomaliza tu Nikachezwa na siku hiyo hiyo nikaolewa”

“Aaaaah me ningekataa, ulimuaminije labda kaushadamu au Mchuna ngozi “

“We Mtoto wewe Ebu funga Mdomo wako, unaongelea kuhusu baba yako ujue’’

“Aaaah hapa tunaongelea miaka hiyo si ndio baba??”

Ila Dijah daaaah akili yake ni mwendo kasi.

Utani wa hapa na pale uliendelea kwa Wanafamilia hao na mwisho wakafika Nyumbani kwao.

KWa upande wa dijah alipitiliza moja kWa moja mpaka chumbani kwake Wala hakutaka kukaa sebuleni Kama ambavyo wazazi wake walifanya, Dijah alifika na kusimama mbele ya Kioo na kujiangalia kisha akazungumza.

“Hivi ni kweli Kuwa siwezi kumuepuka Zion? Au nitoloke tu’’

Dijah aliendelea kujiiliza maswali ambayo haya Kuwa na majibu sahihi kwa upande wake.

*********

Upande wa pili, anaonekana Zioni akiwa chumbani kwake na alikuwa Akizunguka uku na uku na akikuna kichwa chake.

Baada ya muda, Zion akachukua simu yake na kupiga, zioni akasalimiana na mtu ambaye alimpigia kisha akazungumza.

“Naomba Namba ya dijah’’

Zion akakaa kimya kidogo akisikiliza majibu ya upande wa pili kisha akaendelea.

“Kaka we nitumie Namba kwanza halafu nitakuelezea kila kitu kWa sasa Namba ya dijah ni muhimu sana’’

Zion akamaliza kuzngumza na simu kisha akashusha Pumzi Ndefu sana na kujitupia kitandani.

********

Siku iliyofuata ikiwa ni Majila ya jioni, anaonekana zion akiwa amesimama nje ya ofisi ya kina Dijah, Zion alionekana kuangalia uku na uku lakini muda mwingi aliangalia Saa aliyokuwa amevaa mkononi ni wazi Kuwa alikuwa akihesabu muda.

Baada ya muda, wanaonekana wafanyakazi wakitoka nje kwani ulikuwa ni muda wa kuondoka.

“Dijah”

Zion alimuita dijah baada ya kumuona akiwa akaondoka kupitia upande mwingine.

“Nilikuwa nakusubili wewe’’

Alizungumza Zion baada ya kumfikia Dijah.

“Unaonekana una Ishu ya muhimu sana mpaka wewe kufika hapa’’

Alizungumza dijah uku akimkazia macho Zion.

“Ni muhimu sana Tena sana Dijah, Jana nimekupigia simu yako mfululizo ukupokea ata simu moja”

“Uwa sipokeagi Namba ngeni at least ungejitambulisha kWa sms”

KWa upande wa Zion alionekana Kuwa serious sana lakini kwa dijah ni Kama alikuwa akimkomoa tu mkaka wa watu.

“Tunaweza kutafuta sehemu iliyotulia na tukakaa tukazungumza?

Zion alimuuliza Dijah.

“Nafikili kwenye gari yako itatosha sana yasiwe maongezi marefu kwani Nina haraka sana’’

“Hakuna shida”

KWa pamoja Zion na dijah wakapanda kwenye Gari na mazungumzo yakaanza baada ya Zion kumuuliza Dijah.

“Dijah Unafikili uko tayali Kuwa na maisha na Mimi? Yaani Namaanisha uko tayali mimi Kuwa mwenzangu wako??”

“Siko tayali”

Alijibu dijah akiwa mkavu kabisa, Ila hawa watu Sijui walikosana kitu gani mpaka wanachukiana kiasi hiki.

“Vizuri, sasa Leo niko serious sana, nataka ili Jambo tufanye kwa ushirikiano wa hali ya juu”

Alizungumza Zion uku akionekana Kuwa na mipango Fulani ya kusitisha ndoa kati Yao, ndoa ambayo wazazi wameivalia kibwaya pasi na kujua Kuwa watoto wao ni watu ambao walishawai Kuwa na mahusiano uko nyuma.

“Leo nitakaa na wazazi wangu na kuwaeleza Kuwa siitaji Kuwa na wewe, lakini pia nitawaeleza Kuwa Nina mahusiano na mtu mwingine na ikiwezekana waniozeshe na mtu ninayemuitaji”

Alizungumza Zion uku akionekana Kuwa serious na kitu ambacho anakizingumza.

KWa upande wa Dijah alikuwa kimya kabisa lakini Alizungumza na nafsi yake.

“Lakini Kwanini niiache nafasi ya Kuwa na mtu nimpendae? What if Zion ndiye mwanaume ambaye Mungu ameniandalia? “

Dijah akiendelea kubishaanaa na nafsi yake uku asijue ni kitu gani cha kufanya.

“Dijah unanisikiliza au ??”

Zion aliuliza baada ya kuona Kuwa dijah amekaa kimya.

“Nakusikia na Mimi pia nitafanya hivyo “

Alijibu dijah kisha akataka kushuka kwenye gari lakini Zion akamdaka mkono wake na kumuuliza.

“Gari yako umepaki wapi?? “

Dijah a akatabasami na kujibu.

“Tangu lini umeniona Mimi naendesha gari? “

Zion akamuangalia dijah kwa muda kisha akacheka sana na kusema.

“Usiniambie Kuwa bado unaogopa kuendesha gari “

“Na sitakuja kuendesha”

“Ouk I can drop you off maana Sina mizunguko Mingine “

“Sawa”

Kwa Pamoja wawili hao wakaanza safari ya kwenda Nyumbani kwa kina dijah.

Zion alimshusha dijah getini kwako kisha akaondoka.

“You still the same Zion so caring”

Alizungumza Dijah na kujikuta akitabasamu.

Moja kwa Moja dijah akaingia Ndani kwao ambapo Alikutana na hekaheka Kama zote.

“Mbona umechelewa sana Leo??”

Mama dijah alimuuliza Binti yake.

KWa bashasha na furaha Daija akajikuta akilopoka.

“Nilikuwa na Zion mama “

Jibu ilo lilimfurahisha kila mtu na waliamini Kuwa watoto wao wako tayali kWa kila kitu.

“Anyway, kajiandae wakwe zako wanakuja kutoa mahali usiku wa Leo”

Dijah aka…….

NAKUJA MY ZANGU……..

KIND LOVE 🧡 ❤️(Mapenzi na ahadi )
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 04
www.tupohapa.com

SONGA NAYO……..

Dijah akashtuka sana mwisho akauliza.

“Kwani wazazi wangu mnaniozesha au mnaniuza jamani? Mbona mambo yamekuwa haraka haraka sana ??”

“Weeeh Mtoto Mdomo mrefu Sijui kitu gani, hivi Unafikili wazazi wako tunaweza kukuuza wewe? Dijah nimeshazungumza na wewe mwanangu kila kitu punguza wasiwasi na upokee maisha yako mapya mama, wako wenzio uko umri unakimbia na awaoni dalili ya kuolewa”

“Sawa”

Alijibu dijah kisha akakimbilia chumbani kwake.

Dijah alifika chumbani kwake na kuanza kuruka ruka kWa furaha sana, dijah alionekana Kuwa na furaha ambayo aielezeki.

Ila dijah ananichanganya sana jamani au nyie wasomaji mnamuelewa 😂🙌 maana mpaka sasa niko njia panda Sijui anataka kuolewa au ataki.

Muda huo huo dada wa dijah ambaye alijulikana Kama manka akatoka kwenye kabati la nguo za dijah na kuzungumza.

“Nilipanga kuku surprise lakini wewe ndio umenisurprise sasa, hivi dijah ni wewe ndio unashangilia hii ndoa au kuna kitu kingine??”

Kwa upande wa dijah alibaki akiwa ameshikilia kifua chake na kupima Mapigo ya moyo maana dada yake alimshtua sana mwisho dijah akazungumza.

“Utakuja kuniua dada yangu hivi unajua umenishtua sana”

“Pole”

“Asante”

Alijibu dijah kisha akakaa kitandani na kWa sauti ya furaha Akajibu.

“Sijui Kwanini lakini Nina amani sana na ili linaloendelea sasa, Nina imani na kila kitu kuna muda naona Kama nachelewa hivi “

Alizungumza dijah na kumfanya dada yake Kuwa makini kumsikiliza.

“Dada uwezi amini Kuwa mwanaume ambaye naenda kuanza nae maisha ni Zion”

Manka alishtuka sana na kusema.

“Chinekeneeeeeeeh 😳 wewe, unasema kweli??”

“Yaaaah, ni yeye, am so happy dada ingawa Zion yeye ataki kabisa lakini pia awezi kukatalia wazazi wake”

“Jamani, hivi Kwanini amuoni Kuwa umoja wenu ni umepangwa na Mungu jamani “

Alizungumza manka akiwa na furaha sana kwaajili ya Mdogo wake.

Ila hapa kati kati nahisi kuna kitu ambacho atufahamu wacha tuone.

Baada ya Kama masaa mawili hivi, familia ya Mr Tony iliweza Kuwasili Nyumbani kWa kina dijah, aiseeeh watu wako serious sana na hii ndoa Mjue, watu wako serious kuliko huo u serious wenyewe Yaani mambo ni shwwaaaaaah 😂, lakini pia na Pesa ipo Bwana, maana kuna wenzangu na Mimi hapa wametolewaga barua tu Basi wakaenda kuishi na my zao na awajui hizo mahali zinapelekwa lini. Halafu kuna ma fellow wenzangu wa sogea tukae 😂🙌 Mungu atupe nguvu kwakweli.

Basi taratibu zote zilifuatwa lakini Zion alionekana Kutokuwa Na furaha ata kidogo, muda wote Zion alifosi tabasamu tu lakini hakuwa na furaha ata kidogo.

Taratibu zote zilikamilika, watu wakiwa bize na story za hapa na pale, baba mzazi wa zioni akamshika mkono Dijah na kutoka nae nje.

“Binti yangu “
Baba Zion alimuita dijah baada ya kutoka nje.

“Abeeeh baba “

“Kwanza Nikushukuru sana kWa kila kitu, nikushukuru kwa Kukubaali kuwa mke wa Kijana wangu ambaye uku wao kumjua”

Dijaha akatabasamu na kuendelea kumsikiliza.

Baada ya Kama robo Saa hivi dijah alionekana Kuwa ni mtu kwenye huzuni sana lakini pia alimkumbatia baba Mzazi wa Zion akiwa analia sana, Yaani dijah ndio alikuwa akilia na baba Zion alikuwa akimbembeleza.

Baada ya muda wawili hao wakarudi Ndani na kuungana na watu wengine.

Dijah kabla ajajichanganya na watu wengine, Zion akamuwai na kutoka nae nje.

“Ulikuwa unaongea nini na baba yangu ??”

Zion alimuuliza dijah uku akiwa na hasira sana.

“Ni baba yangu mkwe sio baba yako Sawa “

Alijibu dijah kWa kujiamini sana.

Majibu ya dijah yalım Changan ya sana Zion ambaye alibaki akiwa ameshika kiuno na kisha akamuuliza dijah.

“Unamaanisha nini kusema hivyo? Dijah tunatakiwa kumaliza plan yetu, lazima Tuwaambie wazazi kuwa hatuko tayali kufunga ndoa”

Dijah akamuangalia Zion kisha akajibu.

“Utawaambia kwa niaba yaako lakini kwa upande wangu, am ready to be your wife, niko tayali Kuwa Mrs Zion ata any cost”

Alijibu dijah uku akimlingia zioni ambaye alihisi kuchanganyikiwa.

“Dijah unaongea kuhusu nini? Acha Basi ujue niko serious sana”

“Ukiniangalia unaniona Kama bibi yako na tupo kwenye utani si ndio?, Zion sitanii niko tayali, bu the way nitakuwa Chizi kuachana handsome man like you “

Zion alihisi Kama anaota hivi akabaki akijichapa vibao vya mashavu.

“Maandalizi mema future husband”

Alizungumza dijah kisha akaingia Ndani na kwenda kuungana na watu wengine.

*******

Week nzima iliisha uku Zion akijitaidi kumkatisha tamaa dijah lakini dijah alionekana kuitaka sana hiyo ndoa.

Hatimaye mwezi mmoja Ulipita na ndoa kati ya dijah na zioni ilipita na wakawa nje na mume, kWa upande wa Zion hakuwa na furaha ata kidogo, lakini kWa upande wa dijah alikuwa ni mwanamke Mwenye furaha sana.

Ila dijah anazidi kutuchanganya ata sisi watu wa pembeni sasa maana daaah imekuwa gafla sana yeye kukubali kuolewa na Zion, lakini pia ni kitu gani dijah Alizungumza na baba Zion mpaka akawa analia? Anyway, tutakuwa mbele ya safari.

“Zion kifungua kinywa kiko tayali”

Alizungumza dijah akiwa amesimama pembeni ya meza ya chakula, lakini pia kWa upande wa Zion alikuwa amevalia mavazi yake ya kazini na yuko tayali kuondoka.

Zion alimuangalia dijah kisha akajibu.

“Ukinywa wewe hiyo chai utatosha sana “

“Nakunywaje peke wake peke yangu na nimeandaa kwaajili yako na yangu?? “

Zion akarudi nyuma na kumsogelea zaidi dijah kisha akamwambia.

“Si Ulitaka ndoa? Ndoa ndio hii sasa, pambana nayo Ila isinizoee “

“Hus B jamani 🥰 Nimekuandalia chai kWa mahaba mazito sana mwenzio “

Ila dijah anajua jumkela mtu 😂🙌, Yaani mwenzie ako na hasira Kama yote halafu yeye anamletea matani tu.

“Usinizoee dijah “

“Zion siwezi kumzoea lakini Mume wangu namzoea kupitiliza”

“Hivi wewe unajua auna akili vizuri “

Alizungumza Zion lakini mwisho akajikuta Akicheka na mwisho akakaa chini na Kupata kifungua kinywa akiwa na dijah wake.

Walimaliza kupata kifungua kinywa kisha dijah akazungumza.

“Aaah jioni uje kule Nyumbani maana nitaenda kumuona baba anataka nikampikie ndizi”

“Ooooh Kama auna kazi nyingine naweza kukupitisha chap pale jiandae “

Alijibu Zion ambaye mwanzo alijifanya Kuwa ni mtu mwenye haraka sana.

Ila hawa wawili 😂🙌 aliyewaloga Nafikili alishakufa, Yaani dakika Mbili wako vitani dakika Mbili wannaelewana haya ngoja tuone.

Basi dija akajiandaa chap na kwa pamoja wakaondoka.

*******

Baada ya muda, Ndani ya chumba kimoja kizuri sana, anaonekana mr tony Yaani baba mzazi wa Zion, akiwa amelala lakini pia akiwa na mipira ya kupumulia puani mwake.

Ndani ya chumba iko pia, alionekana Mrs Tony na Dijah, wawili hawa walionekana kuzunguka uku na uku mwisho Dijah akazungumza.

“Mama Nafikili tungempeleka tu hospital akapate uangalizi mzuri, haya mambo ya dokta wa kuja na kuondoka sio Sawa kabisa “

Muda huo huo mr Tony anageuka na kuzungumza kwa sauti ya shida sana.

“Dijah usijali Binti yangu niko Sawa”
Kwakuwa mgonjwa amesema Basi hakukuwa na made nyingine, Sina akatoka nje na kumpigia simu Zion Na kwa wasiwasi akazungumza.

“Naomba uje Nyumbani haraka sana hali yababa inanipa wasiwasi sana”

Kisha dijaha akakata simu.

Baada ya nusu Saa Zion aliwasili Nyumbani kwao na Moja kWa moja akataka kwenda chumbani kWa baba yake lakini akakutana na dijah akitoka nje uku analia sana.

“Dijah nini shida??”

Dijah hakuwa aya na nguvu haraka akamkumbatia mume wake na kwa sauti ya uchungu akazungumza.

“Umemchelewa baba mume wangu “

OOOOOH JAMANI REST IN PEACE MR TONY.

NAKUJA NIKO MSIBANI JAMANI.

KIND LOVE 🧡 ❤️
(Mapenzi na ahadi)

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 05

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……..

Kwakweli ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa familia ya mr Tony, imagine kiongozi wa familia anapoteza maisha kipindi ambacho bado familia Inanuitaji sana.

Niwakumbushe Kuwa ndoa ya Zion na dijah ndio kwanza ilikuwa na week moja tu, Yaani wametimiza week moja tu na baba mkwe anafariki.

Taarifa za kifo cha mr Tony zilisambaa uku na uku na ukizingatia alikuwa ni mtu mzito Basi watu wengi sana waliwakimbilia.

Kwa upande wa Dijah ndio alikuwa msimamizi wa kila kitu, dijah aliamua kujikaza kWa niaba ya familia nzima, Yaani naweza kusema Kuwa dijah alikuwa zaidi ya mwanaume maana alijua kusimama imara kwa kila mtu.

Dijah alihakikisha Kuwa mume wake anakuwa Sawa lakini pia na wanafamilia wengine akiwemo mke halali wa mr Tony, Ila huyu mama viatu vyake ni vizito sana imagine kuondokewa na mume ambaye umemzoea sana.

Ila kuna kitu ni Kama akiko sawa, kwanza ni ndoa ya Zion na dijah kumpelekwa haraka haraka then baada ya week tu mzee anakata moto, anyway nisije nikaonekana Nakuza mambo bure.

Hatimaye taratibu za maziishi zilikamilika na Mr tonya kapumzishwa kwenye Nyumba yake ya Milele.

Baadhi ya marafiki na jamaa wa hapa na pale walianza kutawanyika na wanafamilia tu ndio walibaki.

Nje ya Nyumba hiyo, anaonekana dijah akiwa na wazazi wake ambao walikuwa Wanajiandaa na kuondoka.

“Dijah mwanangu, Walahi hizi siku Tatu zote za msiba umejua kunishangaza last born wangu “

Alizungumza mama dijah uku akichezea mashavu ya Binti yake.

“Kwanini mama ??

Dijah aliuliza.

“Imefanya kazi kubwa sana, umenionesha mama yako Kuwa sikukulea vibaya, dijah umenionesha mama yako kuwa wewe ni mwanamke ambaye unaweza ukabeba na kulinda familia Kiukweli Mungu akusimamie Binti yangu mrembo “

“Mungu yupo pamoja na Mimi mama “

Alijibu dijah lakini alionekana Kuwa ni Mwenye huzuni sana..

Baada ya muda wazazi wa dijah wakaondoka na dijah akarudi Ndani na kukutana na kikao cha familia na yeye akajiunga.

“Sasa Kama ambavyo nilisema hapo awali, Zion itakupasa kurudi hapa na kukaa na mama yako lakini pia na Mdogo wako huyu ambaye anaendelea na masomo si vyema Kuwaacha wenyewe kwenye Jumba kubwa Kama ili “

Alizungumza mmoja wa wanaume ambaye alionekana Kuwa ndio mkubwa wa familia kati ya watu wote waliokaa.

Basi Zion akakubali pale lakini pia na dijah hakuwa na pingamizi.

*******

Majila ya usiku dijah na Zion wakiwa chumbani, Zion alionekana Kuwa na mawazo sana, Zion hakuwa Sawa ata kidogo, Mara nyingi alitililisha machozi machoni pake”

“Mume wangu “

Dijah alimuita zion kwa utulivu wa hali ya juu sana.

Zion akuitika zaidi akageuka tu na kumuangalia dijah.

“Jamani unalia”

Dijah alishtuka sana mwisho akamsogelea mume wake na kumkumbatia kwa nguvu sana.

“Utakuwa Sawa kipenzi changu, lakini usilie Kama hivi unanivunja nguvu Mimi mke wako”

“Dijah Sijui Kama unaweza kunielewa, Kiukweli siko Sawa, Sawa Nina mama, Sawa Nina ndugu lakini am not fine at all, moyo wangu unahisi Kama nimebaki Mwenyewe kwenye hii dunia, kuna muda nahisi labda baba yangu ndio mtu Pekee ambaye nilibaki nae “

“Aaaah usiseme hivyo Utakuwa Sawa mpenzi Sawa? Mimi niko hapa, mama yuko hapa, dada zako na ata Mdogo wako Mishy, hivi Kama wewe unakuwa hivi mama atakuwa kwenye hali gani ? Jikaze mume wangu Utakuwa Sawa”

Nyieeeeh muda mwingine Kumbe ni raha sana Kuwa na mwenza wako ujue, imagine Leo hii Zion angekuwa na hali gani kama dijah asingekuwepo.

Dijah na Zion wakaakumbatiana kWa nguvu sana kama sio wao ambao walikuwa awataki kuoana..

Wakiwa wameendelea kumkumbatiana gafla simu ya Zion ikaita na Jina lilitokea “MY LIFE PARTNER” eeeeh hii nayo Kali, life partner si ni huyu amekimbatiana nae jamani sasa huyu anayepiga simu ni Nani ?

Zion akamuachia dijah na haraka akapokea simu na saut ya kike ikasikika.

“Toka nje mpenzi “

Dijah alibaki akishangaa tu, Zion akanyanyuka chap akachukua Tshirt yake na kuvaa dijah akamuuliza.

“Ni Laila huyo ??”

Zion akabaki akimuangalia tu Daija na pasi na kujibu kitu akatoka nje.

Dijah akasogea kitandani na kukaa tu.

Kwa upande wa Zion alitoka nje na kukutana na msichana AMBAYE ni mrembo lakini mavazi yake uwiiiiih 🥹🙌 imagine ameenda na mavazi ya club kwenye Nyumba ambayo Imetoka kumalizana na msiba.

Zion KWa furaha akamkumbatia msichana huyo, Kiukweli Zion alikuwa na maumivu sana hivyo akajikuta akilia tu.

“Pole sana mpenzi wangu “

Alizungumza msichana huyo ambaye alikuwa na sauti ya jaiva na sio ya kumtoa nyoka Pangoni.

“Kwanini ukutokea kwenye msiba. ??”

Zion alimuuliza msichana huyo.

Laila alimuangalia Zion kWa macho ya mahaba snaa mwisho akajibu.

“Nilikuwa nikiumwa sana uwezi amını nilikazwa na Leo ndio nimetoka hospital ila nikaona nije kukuona mpenzi wangu “

“Ooooh pole sana Unaendeleaje lakini ??”

“Nashukuru Mungu Unaendeleaje na wewe ? Nimekumisi sana babe tunaweza kutoka ??”

Laila alimuuliza Zion.

“Aaaah hapana si unajua ndio kwanza tumezika Jana tu, ata hivyo siko sawa na nimefurahi sana kukuona hapa mpenzi wangu “

“Huyo mke wako kibibi yupo ??

Laila aliuliza uku akimaanisha Kuwa dijah ndio kibibi.

Muda huo huo sauti ya dijah ikasikika ikijibu.

“Am here umenimisi sio “

Laila akamgeukia Zion kisha akazungumza.

“Eeeh haya muwe na usiku Mwema”

Zion akamshika Laila mkono akimzuia Kisha akamgeukia dijah na kumuuliza.

“ Hivi uoni Kuwa tuna mazungumzo ?”

“Nilikuja kuangalia usalama wa mume wangu uku nje sizani Kama nimefanya kosa “

Alijibu Dijah uku akiwa na tabasamu panda sana usoni mwake.

“Kwani una shida gani dijah ? Upendi kabisa kuniona nikiwa na furaha si ndio ??”

Zion alimuuliza dijah.

“Ouk endeleeni na mazungumzo yenu me niko Ndani”

Alijibu dijah kisha akaondoka na kumuacha Zion akiwa na Laila ambaye ndiye mwanamke Anampenda sana.

*******

Miezi miwili ilipita tangu kutokea kifo cha Mr Tony.

Maisha ya Zion na dijah ni drama tupu, ni watu ambao wallionesha kupendana sana mbele ya macho ya watu lakini ukija kwenye ukweli, ndoa Yao ilikuwa ni ndoa Jina, Zion ajawai ata kushiriki tendo la ndoa na Dijah, Yaani wanalala kaka na dada, na Zion alikuwa akilala kitandani na dijah alikuwa akilala kwenye kochi.

Ikiwa Ni Majila ya mchana, kila mtu akiwa kwenye Mishe Zake za utafutaji, anaonekana Mrs Tony yaani mama wa Zion akiangaika Iuku na uku, Alifungua droo zote na alionekana kuchanganyikiwa Sawa.

Muda huo huo akatokea Dijah akiwa na file mkononi mwake kisha akauliza.

“Unatafuta hizi ??”

Mama huyo alionekana kupata furaha gafla kisha akamsogelea dijah na kuchukua file kWa kumpokonya na pasi na kuzuungumza kitu chochote kile akaampushi dijah na kuondoka.

Dijah alibaki akitabasamu tu na kutikisa kichwa chake kWa ishara ya kusikitika kisha akasema.

“All the best mama mkwe “

Majila ya jioni dijah akiwa jikoni anaandaa chakula cha jioni, gafla mishy akaja, aaaah my zangu huyu mishy ni Mtoto wa mwisho wa mr Tony na huu Binti ni anasoma yuko chuo.
Mishy akamuuliza dijah

“Hivi wifi ni kweli ujafua nguo zangu ? “

Dijah akamgeukia WiFi yake yake na kumuuliza.

“Nilivyokuwa Sipo ni Nani alikuwa akikufulia Binti ??”

Hapa sasa Bwana ni ma last born ndio wamekutana 😂🙌 Sijui Kama ata watawezana maana yoooooh 🤣.

KWa hasira mishy akanyanyua mkono wake na kumchapa dijah kibao cha Shavu, kabla dijah ajajibu mashambulizi Zion akatokea na kukuta situation ile, zion Wala akuuliza ni kitu gani kimetokea zaidi akanyanyua mkono wake na kumtandika kibao dijah.

JE ITAKUWAJE ? TUKUTANE KWENYE WEBSITE .


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote