LEAH (JASON'S MAID)

book cover og

Utangulizi

Ni simulizi inayomuhusu kijana Jason Hudson ,

Jason ni kijana wa miaka 28 na ni dactari wa magonjwa ya wanawake kwa miaka mingi Jason alikuwa akiishi nchini canada huko alikutana na msichana mmoja aliyeitwa Asmina ambae alikuwa ni mnenguaji katika club moja maarufu nchini canada

Jason alimpenda sana Asmina hakujali watu walimuongelea vipi aliamua kumbadirisha na kuishi nae

Aliamua kukata mawasiliano na familia yake kwa miaka 9

Badala yake Asmina alimsaliti na mwanaume wa kikanada
Jason aliamua kurudi nchini Tanzania na kufanya kazi kwenye hospital ya baba yake iliyoitwa st Joseph

Jason alitaka kuishi maisha ya kujitegekea mama yake bi lulu aliamua kumtafutia msaidizi wa kazi

Kila mfanyakazi aliyeenda kufanya kazi nyumbani kwa Jason hakufikisha hata mwezi aliondoka

Ndipo bi lulu aliamua kwenda kumchukua Leah kijijini

Leah hakuwa muoga Wala hakuwa mnyonge hakuishi na Jason kwa kumuogopa hata kidogo alifanya kila anachoona ni sawa

Jason alipambana sana kumfukuza Leah lakini alishindwa mwisho wa siku alijikuta anaanza kuvutiwa na Leah

Lakini aliogopa huenda yakamtokea kama yaliyomtokea kwa Asmina
Wakati Jason anaukataza moyo wake kumpenda Leah kumbe Leah nae alikuwa ameanza kumpenda Jason

Jason alivumilia lakini mwisho aliamua kuweka wazi hisia zake kwa Leah na rasmi walikuwa wapenzi na sio mfanyakazi na boss wake

LEAH (JASON'S MAID)

SEHEMU :1 &2

" Habari za asubuhi madam lulu "

alisalimia bibi zubeda ambae ni mfanyakazi wa jumba la Mr Hudson

" Salama nikusaidie Nini bi zubeda mbona asubuhi asubuhi chumbani kwangu ?"

Aliuliza bi lulu ambae ni mke wa Mr Hudson

" Samahani sana madam kama nimekuamsha mapema ila ni jambo muhimu sana "

" Ni jambo Gani Hilo ?"

Bi lulu alikaa vizuri pale kitandani kumsikiliza bi zubeda

" Mr Hudson ampiga sana simu anasema haupokei amepiga simu ya nyumbani na kuacha maagizo anasema mtoto wenu kipenzi Jason anarudi Leo mnatakiwa kwenda kumpokea pamoja uwanja wa ndege "

" Wow siamini zubeda siamini Mimi jamani au naota kweli mwanangu kipenzi Jason anarudi hii ni kama ndoto kwa miaka Saba baada ya kumaliza masomo yake ameng'ang'ania kukaa huku ughaibini nimefurahi sana sijui nijielezee vipi hii furaha yangu "

bi lulu aliongea huku machozi ya furaha yalimtoka

" Ni kweli kabisa madam Wala huoti kinavhotakiwa ni kumshukuru mungu na kumuomba agile salama asipate misuko suko ya aina yoyote "

alisema bi zubeda

" Ni kweli namuombea sana afike salama , zubeda unaweza kwenda Mimi ngoja nijandae nataka kufika uwanja wa ndege mapema kabisa sitaki kuchelewa hata kwa dakika Moja "

bi lulu aliongea huku akitabasamu kwa furaha " Sawa madam "

bi zubeda nae pia alikuwa na furaha sana kwa ujio wa Jason kwani ni yeye aliyemlea Jason tangia akiwa mdogo kabisa Katika familia ya bwana Hudson na bibi lulu walibarikiwa kuwa na familia nzuri na uwezo mkubwa sana wa kifefha walimiliki mashule , mahospitali na makampuni mbalimbali pia na mungu hakuwaacha kinyonge aliwabariki watoto wawili wakiume walimpa Jina la Jason na wakike wakampa Jina la jasmine

" Bi zubeda umemwambia jasmine kuwa kaka yake Jason anarudi ?"

Bi lulu alimuuliza bi zubeda

" Hapana madam sikumwambia chochote "

" Vizuri muache hivyo hivyo hii itakuwa ni surprise yake , Mimi natoka zubeda unanionaje nimependeza ?"

Bi lulu aligeuka kumuonyesha bi zubeda nguo ilivyomkaa

" Umependeza sana madam hakuna nguo inayokuchukiza "

bi zubeda alimsifia bi lulu

" Mmmmh siku zote unanisifia hakuna siku uliyowahi kunitoa kasoro "

alisema bi lulu huku anajiangalia

" Umesahau kuwa ulikuwa mwanamitindo mashuhuri Kila unachokichagua ni kizuri na kinakupendeza "

" Sawa Asante kwa kunisifia "

bi lulu alitabasamu Kisha akaondoka Lulu na zubeda wamekuwa marafiki kwa miaka mingi sana Kwa Upande wa kampuni iitwayo Mineson inayomilikiwa na Mr Hudson

alionekana Mr Hudson akiwa kwenye kikao na baadhi ya wafanyakazi wake

" Hii project nimeipitia na ninakubali Iko vizuri , Kila kitu kipo tayari nataka utendaji kazi tu "

Mr Hudson alisimama baada ya kusema hayo maneno akaondoka

" Mmmh kazi mwingine bila kupumzika "

alisema mfanyakazi mmoja

" Kitu kizuri ni kwamba Mr Hudson ametoa uhuru ambae Hataki kushiriki kwenye hii kazi anaweza kujitoa ,kwahiyo kama umechoka unaweza kutupisha wengine tukafanya kazi "

alisema mfanyakazi mwingine

" Nimetamia tu jamani kuna ambae Hataki marupurupu "

Mr Hudson alipanda kwenye gari yake na kuelekea uwanja wa ndege njia alimpigia mkewe bi lulu

" Hallo mume wangu nipo njiani naelekea uwanja wa ndege"

" Nilitaka kujua uko wapi kwa Sasa basi tutakutana huko na Mimi pia nipo njia "

Mr Hudson alikata simu Baada ya kama dakika 30 Mr Hudson alikuwa amefika uwanja wa ndege na alimkuta mkewe bi lulu ameshawasili

" Ninafuraha sana Leo mume wangu sijui hata nijielezee vipi "

bi lulu alianza kulia

" Basi acha kulia hata Mimi ninafuraha sana kijana wetu kurudi nyumbani "

Mr Hudson alimkumbatia bi lulu

" Wacha weee Yani mmekuja kunipokea Mimi lakini mnakumbatiana nyie wenyewe basi kama ndo hivyo narudi zangu Canada "

bi lulu na Mr Hudson walishtuliwa na sauti ikitokea nyuma yao wote waligeuka kwa Kasi kuangalia ni nani

" Jason .."

wote walijikuta wametaja kwa pamoja Jina la mtoto kipenzi Jason

" Yeah ndo mimi "

Jason alifungua mikono yake na wazazi wake walienda kumkumbatia

" Hatimaye , hatimaye nimemshika mwanangu Tena kwenye mikono yangu nilidhani nimekupoteza "

bi lulu alilia kwa furaha

" Maneno Gani hayo mke wangu mtoto amerudi tunatakiwa kufurahia na kusherekea na sio kulia "

alisema Mr Hudson huku anamfuta machozi mke wake bi lulu

" Kweli mama nipo hapa na waahidi sitokuja kuwaacha Tena "

" Really ? Unamaanisha unachokisema "

aliuliza bi lulu

" Ndiyo mama namaanisha "

Dereva wa Mr Hudson alichukua mabegi ya Jason na kuyaweka kwenye gari Kisha safari ilianza ya kwenda kwenye jumba la Mr Hudson Kwenye gari njia nzima waliongea na kucheka kwa furaha

" Jasmine wangu mbona hakuja kunipokea inamaana yeye hakunimiss au hakufurahia ujio wangu ?"

Aliuliza Jason

" No ,sio hivyo Jason unajua mdogo wako anavyokupenda sana endepo tungemwambia unakuja Leo nakuhakikishia angelala uwanja wa ndege tunataka kumfanyia surprise"

alisema Mr Hudson

" Ni kweli kipenzi hata bi zubeda anafuraha sana si unamkumbuka ?"

aliuliza bi lulu

" Yeah namkumbuka sana shangazi zubeda nimemmiss sana jamani "

Safari Yao iliishia kwenye jumba la Mr Hudson walishuka kwenye gari walikaribishwa na wafanyakazi kama kumi na zaidi waliosimama kwa mstari wakiwa na tabasamu wengi wao walimsifia tu Jason hawakuwahi kumuona wa mwisho alikuwa ni bi zubeda

" Shangazi nimekumiss jamani shangazi yangu "

Jason alikimbia na kwenda kumkumbatia bi zubeda

" Hata Mimi nimekukumbuka sana umezidi kuwa mbaba ukiondoka hapa ukiwa na miaka 18 tu ona Leo unarudi mbaba kabisa wa miaka 28"

bi zubeda alilia kwa furaha

" Usilie shangazi nimerudi Sasa na sitoondoka Tena na kuwaacha vipenzi vyangu "

Wafanyakazi waliingiza ndani mabegi ya Jason nankuyapeleka kwenye chumba cha Jason

" Jason muache shangazi wewe nenda ukaoge upumzike "

alisema bi lulu

" Sawa mama shangazi tutaongea badae "

Jason aliondoka na kwenda chumbani kwake alioga akala na Kisha alipumzika alikuja kuamka usiku wa saa 5
watu wakiwa wameenda kulala alienda kunywa maji alifungua fridge akatoa chupa ya maji alikaa na kuanza kunywa taratibu alishtuliwa na kelele za mdogo wake jasmine

"Mr Hudson ,bi lulu na wafanyakazi wengine walitoka vyumbani mwao wakaenda upande ambao kelele zilitokea huko

" Kuna Nini ?"

Aliuliza Mr Hudson, Jason hakuongea alinyoosha kidole chini wote walishangaa kumuona jasmine amezimia

" Kimempata Nini ?"

Aliuliza bi lulu huku anamkagua jasmine

" Itakuwa ni mshtuko alipiga kelele baada tu ya kuniona kwani hamkumwambia ujio wangu ?"

Jason alimuuliza mama yake

" Oo maskini nilisahau kumwambia alirudi nyumbani akiwa mechelewa sana nikaona nimwambie tu kesho "

alisema bi lulu

" Tumpeleke hospital "

alisema Mr Hudson

" Hapana Wala msisimnuke Bure ataamka Sasa hivi haziwezi kupita dakika Tano "

Jason aliangalia mishipa ya damu ya jasmine na upumuaji wake Jason alisomea udactari wa binadamu huko nchini Canada

" Sawa basi ngoja tukamlaze kwenye kiti "

Mr Hudson alisaidiana na Jason kumbeba jasmine mana alikuwa ni kibonge

Na kweli baada ya dakika Tano jasmine alizinduka na kukuta watu wamekaa pembeni yake

" Mom , daddy nimeona mzimu wa kaka Jason"

jasmine alianza kulia
LEAH (JASON'S MAID)

SEHEMU :3

Mr Hudson alisaidiana na Jason kumbeba jasmine mana alikuwa ni kibonge

Na kweli baada ya dakika Tano jasmine alizinduka na kukuta watu wamekaa pembeni yake

" Mom , daddy nimeona mzimu wa kaka Jason"

jasmine alianza kulia

" Basi nyamaza usilie "

bi lulu alimbembeleza jasmine huku anacheka

" Mom unanicheka unaona Mimi muongo sitanii nimeona mzimu wa kaka Jason "

jasmine aliangea kwa kudeka

" Umeuona kweli ?"

Aliuliza bi lulu

" Yeah sitanii "

" Huo mzimu upo hivi "

Mr Hudson alimvuta Jason aliyekuwa amejificha nyuma ya pazia

" Aaaaaaaaa"

jasmine alipiga kelele

"Sasa kelele za Nini Tena au hukupenda Mimi kuwa hapa ?"

Aliuliza Jason huku anamsogelea jasmine Jasmine alisimama kwa Kasi akaenda kujificha nyuma ya bi zubeda

" Huenda na nyie wote ni mizimu "

jasmine aliwanyooshea vidole baba yake na mama yake Watu wote walianza kucheka

" Jasmine mdogo wangu inabidi tukakupime hicho kichwa chako kama ni kizima "

Jason alizanza kucheka mpaka akakaa chini

" Eti shangazi ni kweli yule ni kaka Jason ? Hii haiwezekani kaka Jason kwa mdomo wake alikataa kabisaa kurudi Tanzania kwa miaka Tisa yote kwasababu ya mpenzi wake sijui ndo Asmina "

aliongea jasmine bila kumeza mate na kwa sauti kubwa Kila mtu alimsikia vizuri sana

Kicheko cha Jason kiliisha baada ya kusikia maneno ya jasmine alisimama na kuelekea chumbani kwake akiwa hasira sana

" Wewe jasmine uwe unachagua maneno ya kuongea umeona Sasa kaka yako amekasirika "

alisema bi lulu

" Mom kwani nasema uongo na sio kweli? kaka jason alitutelekeza sisi familia yake kwasababu ya mwanamke"

" Jasmine taratibu atasikia "

bi zubeda alimzuia jasmine asiongee kwa sauti kubwa

" Kwani nasema uongo msinizuie acheni asikie Sasa Nina miaka 20 kwa miaka Tisa nimenyanganywa upendo wa kaka yangu na mwanamke wa hovyo "
" Hata sisi tunaumia sana jasmine sio wewe peke yako lakini kwa Sasa kaka amerudi naomba usiwe hivyo hatujui amepitia mangapi akiwa huko "

Alisema Mr Hudsonjasmine

Jasmine aliondoka na kwenda chumbani kwake hakutaka kumsikiliza Tena mtu mwingine
Bi lulu alianza kulia

" Nyie wengine mnaweza kwenda kulala "

Mr Hudson aliwaambia wafanyakazi waondoke Mr Hudson alianza kumbembeleza mkewe

" Mke wangu usilie najua zile ni hasira tu lakini Kila kitu kitakuwa sawa "

Chumbani kwa Jason , Jason alikuwa analia pia alikumbuka miaka kadhaa iliyopita mambo yote yaliyotokea baada ya yeye kukutana na Asmina mnenguaji wa club moja maarufu nchini canada

" Baba msinitafute Mimi ni mtu mzima Sasa naweza kufanya chochote ninachokitaka sitaki kupelekeshwa kama shida ni hizo pesa hata Mimi naweza kutafuta na kingine nataka kuoa huku Canada nitakuwa na familia yangu huku "

ni maneno aliyoyasema Jason kumwambia baba yake Mr Hudson miaka tisa iliyopita kupitia simu yale maneno yalizidi kumuumiza Jason Kila akiyakumbuka alijikuta analia sana

Asubuhi mapema sana jasmine alieamka na kuandaa kifungua kinywa alienda kumgongea Jason

" Kaka Jason fungua mlango au bado umelala ?"

Jasmine aligonga mlango wa chumba cha Jason kwa nguvu muda huo huo mlango ulifunguliwa Macho ya Jason yalionekana kuwa mekundu na yamevimba sana

" Ingia.. "

alisema Jason Kisha alienda kukaa kwenye kochi lililopo chumbani kwake

" Kaka Jason nisamehe Jana nilikuwa na hasira sana sikutakiwa kusema maneno kama Yale natumai utanisamehe"

alisema jasmine huku ameshika masikio yake Jason alitabasamu

" Hukufanya kosa lolote ulisema ukweli mtupu nilikuwa mbinafsi sana na Sasa nipo hapa Sina chochote nimeyachezea maisha yangu Mimi mwenyewe ndomana nataka kufanya Kila niwezavyo kulipia Kila kitu nilichowafanyia "

aliongea Jason huku USO wake ukiwa na huzuni kubwa

" Usijali kaka Jason kwasababu tupo pamoja Tena Kila kitu kinawezekana hakuna kitakacho kuja kwenye njia yetu Tena "

" Asante sana kibonge wangu jasmine "

Jason alivuta shavu la jasmine

" Apo tu ndo unapoanzaga kunikera Sasa Mimi kuwa mnene kidogo tu tayari umepata pa kunichokoza "

jasmine alinuna

" Basi sikuchokozi Tena mdogo wangu sawa ee na nimekuletea zawadi nyingi sana "

" Kweli nataka kuziona "

Jason na jasmine walienda kufungua mabegi ya Jason , Jason alimnunulia mdogo wake jasmine zawadi nyingi sana na sio jasmine tu hakusahau kumnunulia zawadi mama yao bi lulu , baba Yao Mr Hudson pamoja na bi zubeda

" Baba nataka kuanza kazi sitaki kukaa tu nyumbani "

alisema Jason

" Ni uamuzi wako popote utakapo taka kufanya kazi ni ruksa baba yako ana makampuni ,mahoteli , shule na hospital ni wewe uchague unataka kwenda wapi "

alisema Mr Hudson

" Aaah Mimi ningependelea kwenda kufanya kazi kwenye hospital ya st Joseph kama itawezekana "

" Kwanini isiwezekane siku yoyote utakayotaka kwenda wewe Niambie tu "

alisema Mr Hudson

" Asante sana baba "

Jason alifurahi sana na baada ya week Moja tu kupita alianza kazi kwenye hospital ya baba yake iitwayo st Joseph


LEAH (JASON'S MAID)

SEHEMU :4

week Moja tu kupita jason alianza kazi kwenye hospital ya baba yake iitwayo st Joseph

Tukiachana na nyumbani kwa Mr Hudson katika Kijiji cha mtakuja anaonekana Binti akilinda mpunga alikuwa amesimama juu ya kibanda na mkononi alikuwa ameshika manati

" Leah ...Leah "

aliita bi Tunu

" Abee mama "

Leah aliitika na kushuka kwenye kile kibanda

" Njoo ule haraka tufungashe vitu vyetu turudi nyumbani usiku ndo huo unataka kuingia "

" Sawa mama ila mama Leo tumechelewa sana kula Hadi tumbo linaniuma "

alilalamika Leah

" Pole mwanangu jikaze maisha yenyewe yako wapi na unajua kabisa hali yetu ilivyo tumechukua mkopo na mazao hayakuzaa vizuri shamba la bondeni inabidi tujibane tuweka akiba "

" Enheee afu mama nimeota mamdogo zubeda amekuja kutusalimia na mazawadi tele "

alisema leah kuku anakula

" Mmmh huna lolote umemkumbuka tu " alisema bi Tunu

" Kweli mama sikudanganyi haki ya mungu Tena "

" Haya kula Sasa usiongee Sana "

" Subiri kwanzanikumalizie basi mama "

" Enhee endelea "

alisema bi Tunu huku anaendelea kula

" Alivyokuja Sasa mamdogo zubeda na mazawadi kutoka mjini akasema anataka kuondoka na Mimi kuna Kazi natakiwa kwenda kufanya huko mjini .."

Leah aliweka kituo akamuangalia mama yake usoni

" Sitaki tena kusikia hizo habari zako najua tu hio sio ndoto Wala Nini bado unatamaa ya kutaka kwenda mjini kwasababu shoga yako Tatu yupo mjini "

alifoka bi Tunu

" Mama Mimi nimeshaachaga kutaka kwenda mjini ninachokifanya hapa ni kukuhadithia ndoto yangu kama hutaki kuamini basi "

Leah alisusa akanawa mkono

" Ndo umesusa ? Ukisusa sisi twala na utalala na njaa na kwambia "

bi Tunu aliendelea kula ule ugali na mchicha mpaka ukaisha Walikusanya vitu vyao wakarudi nyumbani walimkuta Mzee Jacob ambae ni baba wa Leah anapasua Kuni

" Shkamoo baba "

alisalimia Leah

" Marahaba , mbona umenuna hivyo Leo umechoka sana ?"

Mzee Jacob alimuuliza Leah

" Hana lolote achana nae "

alijibu bi Tunu

" Kama mtoto amechoka sana kesho apumzike tutaenda Mimi na wewe "

" Umeona unavyomdekeza mwanao kitu kidogo tayari unayakuza mambo , kanuna tu Kwa yake akiamka kesho atakuwa sawa "

Leah Jacob ni Binti wa miaka 20 muongeaji sana ,katika Kijiji Chao hakuna anaemchukia wanakijiji wote wanampenda sana ni rafiki wa Kila mtu hakubagua rika , kitu kinachomuumiza Leah ni kutokubahatika kumaliza elimu yake ya sekondari kutokana na matatizo ya kifamilia Kesho yake asubuhi kama alivyosema bi Tunu ,Leah aliamka akiwa na tabasamu usoni alisahau Kila kitu kilichotokea Jana

" Shkamoo mama , shkamoo baba "

" Marahaba naona umeamka mapema sana Leo "

alisema bi Tunu

" Nimeamka kuandaa uji wa kumbeba shamba na kufagia uwanja "

," Umeona si nilikwambia atakuwa sawa "

bi Tunu alimwambia mumewe Mzee Jacob

" Mara zote yupo hivyo anahuzuni moyoni lakini usoni anatuonyesha tabasamu , unakumbuka siku aliyofukuzwa shule kwa kukosa ada alitabasamu lakini najua alihuzunika sana natamani ningekuwa na uwezo ningempa Binti yangu Kila kitu "

alisema Mzee Jacob kwa huzuni

" Usihuzunike mume wangu huenda na sisi siku yetu ikafika ya kupata tunachokitaka na matatizo yetu yote yakayeyuka kama barafu kwenye jua Kali "

" Ni kweli hatujui kesho yetu tunapaswa kuwa na subira "

Bi Tunu , Mzee Jacob na Binti Yao Leah waliongozana kwenda shambani

Nyumbani kwa Mr Hudson Jason aliamka mapema sana na kujiandaa Kisha alielekea hospital ambapo ndo eneo lake la kazi na alikuwa kitengo cha magonjwa ya kina mama

" Jamini naomuonea huruma mwanagu Jason Kila siku anaondoka asubuhi sana na kurudi ni usiku sana mpaka naona ameanza kukonda "

alisema bi lulu

" Ni majukumu yake na anafanya kazi vizuri tangia awe msimamizi wa pale hospital Imekuwa kama amekuja na bahati njema maendeleo ya hospital ni mazuri sana "

alisema Mr Hudson huku anakunywa kahawa yake

" Maendeleo ya hospital ni mazuri lakini mtoto wetu naona kama anateseka "

alilalamika bi lulu

" Nitaongea nae baadhi ya majukumu ayaache "

alisema Mr Hudson Kisha akondoka

" Bora iwe hivyo mwanangu anakuosa hata muda wa kukaa na mama yake jamani "

alisema bi lulu

" Samahani doctor Jason kuna mgonjwa anakuulizia "

alisema nesi mmoja

" Mwambie anisubiri nje ya ofisi yangu nakuja Sasa hivi "

Jason alimalizia kumfanyia vipimo mgonjwa aliyekuwa ametoka kumfanyia operation

" Naki mfanyie mgonjwa uangalizi mzuri namuacha mikononi mwako baada ya dripu kuisha utaichomoa sindano "

" Sawa doctor nitafanya kama ulivyoagiza "

alijibu dada mmoja aliyejulikana kwa Jina la Naki na ni nesi katika hospital ya st JosephJason alienda ofisini kwake alimkuta mama mmoja akimsubiri

" Karibu mama "

" Asante sana , sijui unaikumbuka mwanangu ?"

Aliuliza yule mama

" Ndiyo nakumbuka sana tu wewe si ni mama yake na levina alikuwa ni mgonjwa wetu "

alijibu Jason huku anatabasamu

" Hujakosea hata kidogo , nimekuja kukushukuru na hiki kidogo nilichobarikiwa nashkuru sana levina wangu anaendelea vizuri sikutegemea kama atapona nilikataa tamaa kabisa tulizunguka mahospitali mengi na majibu hayakuwa mazuri "

aliongea yule mama

" Usijali mama hii ni kazi yangu na nashkuru sana kwa zawadi "

Jason amekuwa ni mtu wa kupokea zawadi za shukurani nyingi sana tangia aanze kazi hapo hospital

" Yani Hadi raha doctor Jason ni handsome ,anatoka kwenye familia inayojiweza , ana roho nzuri "

alisema nesi Naki huku ameshika shavu anamuangalia Jason anavyowapitia wagonjwa wake kuwajulia maendeleo Yao

" Umeona eee ila anachonikera ni kuwa Hana muda na mtu muda wote yeye ni kazi ,kazi na yeye "

alisema nesi mwingine aliyeitwa Catherine

"Awe na muda na sisi tuna kipi cha ajabu ? Kwa ninavyosikia doctor Jason amesomewa nchini Canada kwahiyo ni wazi huenda anampenzi wa kizungu uko atahangaika na sisi weusi "

alisema nesi mwingine aliyeitwa Amber

" Kweli shoga angu apo umesema kweli , ngoja tuendelee na majukumu yetu "

Naki alienda kupeleka baadhi ya mafaili ofisi kwa doctor Jeremiah

Siku hiyo Jason aliondoka hospital mapema sana

" Leo naona umewahi kurudi umeshampa mtu mwingine majukumu yako mengine ?' aliuliza bi lulu "

Hapana mama nitapumgiza baadhi majukumu yangu mwezi ujao ila Kwa Leo kuna kitu anataka kukwambia wewe na baba "

alisema Jason

" Sawa kipenzi muda simmrefu baba yako atakuwa hapa "

Jason alienda chumbani kwake baada ya kuoga na kupumzika kidogo alienda sebleni na muda huo Mr Hudson alikuwa ameshwasiri

" Nimeambiwa unataka kuongea na sisi ni jambo Gani Hilo unataka kutwambia ?"

Aliuliza Mr Hudson

" Ni jambo muhimu sana na natumai hamtonikatalia wazo langu "

Jason alienda kuketi pembeni ya baba yake


LEAH (JASON'S MAID)

SEHEMU :5

Jason alienda chumbani kwake baada ya kuoga na kupumzika kidogo alienda sebleni na muda huo Mr Hudson alikuwa ameshwasiri


" Nimeambiwa unataka kuongea na sisi ni jambo Gani Hilo unataka kutwambia ?"

Aliuliza Mr Hudson

" Ni jambo muhimu sana na natumai hamtonikatalia wazo langu "

Jason alienda kuketi pembeni ya baba yake

" Mmmh tunakusikiliza "

alisema bi lulu

"Nimenunua nyumba karibu na hospital nataka kuhamia hupo "

alisema Jason

" Ni wazo zuri lakini mpaka tukapaone kwanza na tukirizishwa napo ndipo utahamia huko "

alisema Mr Hudson

" Asante sana baba "

Jason aliondoka na kwenda chumbani kwake

" Mume wangu unamuachaje mtoto akaishi mwenyewe unajua kabisa akiwa mbali na nyumbani na huo ubusy wake huenda hata asile tutakuja kumpoteza mtoto"

alilalamika ni lulu

" Tatizo ni Hilo tu ?"

Aliuliza Mr Hudson

" Ndiyo mume wangu wewe huoni kama ni tatizo ?"

" Basi hesabia Hilo limeisha "

" Kivipi nieleweshe basi mume wangu "

" Bi zubeda alisema kuna mtoto wa dada yake anataka sana kuja mjini kwahiyo unaonaje tukimwambia akamchukue na tutamlipa vizuri Bora awe ni mtu wa karibu Dunia imeharibika sana "

alisema Mr Hudson

" Enheee nilisahau kabisa ngoja Tena nikamwambie Sasa ivi kama ikiwezekana hata kesho aende akamchukue "

alisema bi lulu

" Kwani hatuwezi kumtumia tu nauli akaja mwenyewe unajua kabisa hapa akiondoka bi zubeda hakuna kinachoendelea yeye ndo Kama kiongozi wa wafanyakazi wetu hapa "

alisema Mr Hudson

" Hapana bhana ngoja aende akamfuate itakuwa sio vyema mtoto wa watu atumwe tu kama mzigo inabidi zubeda aende hata na zawadi kidogo kwa dada yake "

alisema bi lulu

" Sawa Hilo pia ni wazo zuri "

Mr Hudson alikubaliana na wazo la mke wake

" Ngoja basi nikaongee nae "

bi lulu alinyanyuka na kumfuata bi zubeda

" Zubeda Nina maongezi na wewe kidogo muachie hiyo kazi Zay atamalizia "

" Subiri kidogo nakuja Sasa ivi , Zay malizia kutengeneza hiyo juice na uiweke kwenye fridge "

" Sawa bi zubeda "

Bi zubeda alitoka nje na kwenda kukaa kiti cha pembeni ya bi lulu

"Zubeda Nimekuita hapa ninashida kidogo ?"

Alisema bi lulu

" Shida Gani hiyo Niambie tu usiwe na wasiwasi naoan kama unaogopa kuniiambia "

" Naogopa kwasababu nahisi kama unaweza kukataa Ombi langu "

" Hapana siwezi kukataa kama lipo kwenye uwezo wangu basi nitakusaidia "

" Mmmh Leo Jason ametwambia anataka kuhama hapa nyumbani na kuhamia kwenye nyumba yake ambapo ni karibu na hospital "

bi lulu aliweka kituo

" Ni jambo zuru kwani wewe umelipokeaje ?"

Bi zubeda alimuuliza bi lulu

" Ni jambo zuri hata Mimi nimefurahi sana kuona mtoto wangu anataka kujitegemea yeye mwenyewe lakini shida inakuja kwa upande wa afya nadhani unamjua alivyo akitoka ni asubuhi sana na kurudi ni usiku sijui kama anapata hata huo muda wa kula nataka apate Msaidizi wa kazi atakae mpikia na kumfanyie kazi ndogo ndogo "

alisema bi lulu

" Anha kwa hiyo shida ni mfanyakazi basi Hilo limeisha kuna msichana mmoja anaitwa furaha mkimpata huyo ankuwa anafanya kazi zote na jioni anarudi kwao "

bi zubeda alimpendekeza furaha

" Kwani yule mtoto wa dada yako hawezi kuja kufanya hiyo kazi ?"

Aliuliza bi lulu

" wazazi wake hawatakimkabisa Binti Yao akanyage hapa mjini kwahiyo haitawezekana "

" Oo jamani nilitamani sana angekuwa ni yeye sifa zake unazonipa angewezana kabisa na Jason , Jason anahitaji mtu mvumilivu sana "

alisema bi lulu

" Ni kweli na ndomana nimempendekeza furaha mnauhakika ataiweza hii kazi "

" Sawa basi fanya mpango tumapate tutamlipa vizuri "

Bi lulu na mumewe Mr Hudson walienda kukagua nyumba ya Jason na waliridhika na Yao siku chache baadae Jason alihamia kwenye nyumba yake na furaha alianza kazi

" Furaha ...furaha inamaana hunisikii au "

alifoka Jason

" Abeee nakusikia kaka nakuja "

furaha alienda haraka sana mahali alipokuwepo Jason

" Umeona ulichokifanya ?"

Jason alimuuliza furaha

" Nimefanya Nini kaka ?"

Furaha alimuuliza Jason

" Yani nakuuliza swali badala ujibu na wewe unaniuliza swali , unataka kuniunguzia nyumba yangu ona masufulia yalivyo ungua wewe uko busy unangalia tamthilia "

Jason alimuonyesha furaha mboga ilivyoungua mpaka sufuria Imekuwa jeusi kama mkaa "

Nisamehe sana kaka Jason haitokuja itokee Tena"

furaha aliomba msamaha lakini Jason hakumsikiliza

" Huu ni mshahara wako wa siku ulizofanyankazi hapa kwanzia kesho sitaki kukuona nyumbani kwangu "

Jason alimaliza kuongea akaondoka Hazikupita siku nyingi bi lulu alimtafutia Jason msaidizi wa kazi mwingine na yeye pia mambo yalikuwa yaleyale

" Wewe mboni mbona unaakili za kuku si nimeshakukataza mashati yangu meupe kufua na nguo nyingine za rangi kwanini umezifua pamoja ?yunajua kama hizi nguo zinamaana kubwa Sana kwangu "

Jason aliongea kwa kufoka

" Nisamehe kaka Jason sitorudia tana "

mboni aliomba msamaha

" Hakuna haja ya kuomba msamaha Leo ndo mara Yao ya mwisho kukanyaga hapa na huu ndo mshahara wako "

" Jason mbona unanivunja moyo baba kwa week Moja umeshafukuza wasaidizi wawili utaweza kuishi na nani wewe mtoto "

bi lulu alilalamika

" Mama unajua kabisa mwanao nilivyo sitaki mambo ya uzembe uzembe kama mtu kaja kwaajiki yankazi afanye kazi kwa usahihi na sio kufanya makosa tu Kila siku "

" Tutakutafutua msaidizi mwingine "

alisema bi lulu

" Hapana mama Mimi Wala sitaki tena kuwa na mfanyakazi kazi zote nitazimudu Mimi mwenyewe "

alisema Jason

" Nitaongea na baba yako tutajua Nini cha kufanya lakini hatuwezi tukakuacha ufanye kazi zote mwenyewe "

" Sawa mama "

Jason aliitikia tu lakini moyoni hakutamani kupata usumbufu mwingine yeye aliona kuwa na mafanyakazi ni Bora afanye kazi zote mwenyewe

Bi lulu na Mr Hudson waliongea vizuri kuhusu suala la Jason kupata mfanya kazi waliamua kumbembeleza bi zubeda akamchukue mtoto wa dada yake mana mara zote alikuwa aki!sifuankuwa ni mchapakazi , mcheshi na anaheshima

"Bi zubeda nakuomba sana Sana sisi ni kama ndugu ongea na dada yako Ili akubali mtoto wake akubali kuja kufanya kazi huku nitamlipa vizuri "

bi lulu aliongea kwa kubembeleza

" Mmh sawa nitajaribu lakini itabidi niende nikaongee nao ana kwa ana la sivyo watakataa kirahisi Sana hawatafikiria mara mbili "

alisema bi zubeda

" Asante sana zubeda kesho ni safari nitakuandalia Kila kitu Mimi mwenyewe "

bi lulu alimkumbatia bi zubeda kwa furaha Kisha alienda kumpa Mr Hudson habari njema

" Amesemaje ?"

Mr Hudson alimuuliza mkewe bi zubeda

"Amekubali kwenda kuongea na dada yake nahisi Kila kitu kitakuwa sawa "

" Wow vizuri sana Sasa Hofu yangu imepungua Nina uhakika hawataweza kukataa ofa yetu "

alisema Mr Hudson


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote