LIBBY (Call Me Mama )

book cover og

Utangulizi

Baada ya kupoteza wazazi wangu wote nikabaki nikilelewa na bibi yangu kijijini morogoro, pande za tuliani uku, Sawa maisha ya Mimi na bibi yangu yalikuwa magumu sana lakini bibi yangu alihakikisha Kuwa kila kitu kinaenda Sawa kwenye maisha yangu, bibi yangu alihakikisha Kuwa napata maitaji yangu madogo madogo.

Kipindi kigumu kikajongea kwenye maisha yangu baada ya bibi yangu pia kufariki, Walahi mambo yakawa ni kuchanganyana tu baada ya Mimi kuchukuliwa na shangazi yangu na kwend nae mjini dar es salaam.

Walahi familia ya shangazi ilinifanya nione Kuwa dunia ni changu sana.

Achana na familia ya shangazi sasa kuna huyu mkaka ambaye nilimpenda siku ya kwanza kabisa nilipomuona.

Picha linaanza ni kwamba Mimi nimempenda huyu mkaka halafu huyu kaka moyo wake wote uko kwa jojo Mtoto wa kwanza wa shangazi, je nitampata kweli huyu kaka au ndio vita itazuka ? Twende Ndani Ndani tukajue mbivu na mbichi…..

LIBBY (call me mama )

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 01

www.tupohapa.com

ANZA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Call me libby, Jina halali kabisa nililoptatiwa na wazazi wangu siku ya kuzaliwa kwangu.

Kiukweli Mimi wazazi wangu nawajulia kwenye Picha tu lakini sijawai kuwaona kabisa, nakumbuka Bibi yangu mzaa mama aliniambia Kuwa wazazi wangu walifariki kwa ajali kipindi ambacho nikiwa mi Mdogo Sanaa.

Mimi Malezi yangu yote nimekuwa Nilimjua bibi tu na nimekulia uku kijijini kwetu TULIANI, kWa watu ambao ampajui Tuliani ipo morogoro, uku Bwana ni full mchele full wali, Yaani uku ukija kipindi cha mavuno ni unakula ubwabwa mpaka Mwenyewe unasema Basi.

Nilipofikisha umri wa miaka 23, bibi yangu aliweza kuuguaa sana na kufariki.

Ndugu na jamaaa waliweza kutukimbilia na kuweza kumpumzisha bibi yangu, baada ya maziko na kila kitu, shangazi yangu ambaye ni dada wa baba yangu, aliamua kunichukua na kunipeleka mjini ambapo alikuwa akiishia yeye na familia yake.

Shangazi yangu Bwana Alibarikiwa watoto watatu ambapo mkubwa alikuwa na miaka 24 na alikuwa ni msichana Kama Mimi na wadogo ni walikuwa ni wa kiume ambapo umri wao ulikuwa ni kwenye 20 na 17.

KWa Mara ya kwanza tangu nianze kujitambua nikaingia mjini jamani, aaah watu wa mjini Walahi walikuwa wakifaidi sana jamani, Yaani muonekano tu wa jiji unashawishi mtu kuendelea kuishi.

KWa shangazi yangu Bwana watu wote ni wasomi vingereza kama vyote halafu kuna Mimi hapa kudadeki 😂🙌 ukinichanya kidogo nakutuliza na kiruguru Wala sitaki Utani.

KWa shangazi yangu Bwana Mimi ndio nikawa Kama ndio mfanyakazi za Ndani hivi, watoto wake Walahi ni wavivu sana, Mara nyingi ungewakuta na simu zao.

Baba Yao pia alikuwa akiwadekeza San watoto zake na kuwapenda Jambo ambalo lilikuwa lininiumiza sana moyo Mimi ambaye sikuwai kulelewa na baba.

Siku moja nikiwa chumbani na Jojo, Mtoto wa kwnza wa shangazi yangu na ilikuwa ni Majila ya usiku, nilisogea Karibu yake na kuanza kuangalia alichokua akiangalia kwenye simu yake kwani alikuwa akiangalia na kucheka sana hivyo nikajikuta nikivutiwa sana na kutamani kutaka kujua.

“Eeeh wewe jamani ni nini si ulale
Sehemu yako”

Jojo alinifokea.

“Oooh samahani, nilikuwa naitaji kuangalia kidogo nioshe oshe macho na Mimi “

Nilimjibu kWa utulivu.

“Angalia kwenye simu yako tusichoshane “

Daaah hapo nilinyanyua mkono wangu na kuangalia simu yangu ambayo ni kibatani na bado niliishikisha na lababendi ili tu betri lisipate kutikisika.

“Toka nyuma yangu Bwana “

Jojo akanifokea kwa Mara nyingine utazani alikuwa akimfokea Mtoto Mdogo vile.

Kwa unyonge wa hali ya juu nikasogea nakurudi kwenye sehemu yangu ya kulala.

“Kesho Nitamuomba shangazi na Mimi aninunulie simu Kama hiyo “

Nilizungumza Kimoyo moyo.

*******

Asubuhi Kama kawaida niliamka na kuanza kufanya usafi wa Nyumba kwani nilishazoea na najua majukumu yangu.

“Shikamoo shangazi “

Nilimsalimia shangazi yangu ambaye alikuwa Ametoka chumbani kwake na alikuwa yuko tayali kwaajili ya kwenda kazini.

“Marahaba”

Alijibu shangazi na Kunikabizi mkoba wake .

Hii ni hali ya kawaida sana, Mara nyingi shangazi uwa ananikabizi Mkoba wake ili niweze kuupeleke kwenye gari yake.

Basi niliuchukua mkoba wa shangazi na kutoka nje ili kwenda kumuwekea kwenye gari yake, nilifika na kuweka lakini nikasimama hapo hapo kwani nilikuwa niliitaji kuzungumza na shangazi.

“Unalinda gari au ??”

Shangazi aliniuliza baada ya kutoka nje na kukuta nikiwa nimesimama pembeni ya gari yake.

“Hapana shangazi, kuna kitu nataka kukuomba ndio maana nimesimama hapa nikikusubili “


Nilijibu uku nikijichekesha chekesha.

“Aaah nilikuwa Naomba uninunulie simu Kama ya dada jojo”

Nilimwambia shangazi.


“What? Ahaahha unatania eti ? We unajua bei ya I phone 15 wewe ? Au Unafikili ni Kama iko kisimu chako cha buku Jero ? Ata hivyo siwezi kukununulia simu kama ile msichana”

Alijibu shangazi kisha akapanda kwenye gari yake na kuondoka.

“Sasa simu ya kupangusa ni ya kumnyika mtu jamani”

Nilizungumza kWa sauti uku nikisindikiza gari ya shangazi kwa macho.

Nikiwa nimeendelea kumshangaa shangazi Anavyoondoka, gafla mume wa shangazi akaja na kwakuwa alikuwa nyuma yangu, alinishtua kWa kutekenya kiuno changu na hapo alinishtua sana kwakweli.

“Oooh mjomba shikamoo “

Nilimsalimia mjomba uku nikisogea mbali kidogo na yeye maana alinisogelea sana.

“Unafanya nini hapa nje. ??”

Mjomba aliniuliza.

“Nilikuwa namuaga shangazi tu”

“Haya rudi Ndani, hakikisha ndugu zako Wanakunywa chai kWa wakati, lakini pia hakikisha Kuwa mchana unawapikia mapema Aswaaah jojo uwa awezi kuvumilia njaa “

“Kwani kujipikia awezi au ??”

Eeeh Nilijiuliza tu kimoyomoyo Wala sikuweza kutoa sauti.

“Umenielewa ??”

“Ndio mjomba “

Basi mjomba nae akapanda kwenye gari yake na akaondoka.

Mchana Kama kawaida nikaandaa chakula na kWa pamoja tukala, wenzangu Mara nyingi wallikuwa na simu zao na Mimi macho yangu yalikuwa bize kwenye TV nikiangalia tu vipindi mbali mbali.

Majila ya jioni, ikiwa ni muda wa kumwagilia Maua , nilivuta mpira wa maji na kuupeleka nje kwaajili ya kumwagilia maua, nikiwa bize namwagilia maua, gafla ilikuja gari moja nzuri sana, ata Sijui Inaitawaje lakini we jua Kuwa ni nzuri 😂🙌.

Aaaah Kama tulivyo wa Tanzania hakuna kitu kinatupita, niligeuka na kuliangalia vizuri gari la watu ambalo pia lilisimmaa Karibu yangu na muda huo huo Kioo cha mbele kikashushwa na nikakutana uso kWa uso na mkaka ambaye uzuri wake unaweza kusema Kuwa ni mwanamke, Yaani usoni alikuwa Ni mzuri sana, na kilichofanya apendeze zaidi ni macho yake ya paka.

“Mambo”

Mkaka huyo alinisalimia kwa sauti yake nzito sana ambayo ilinivutia sana, na kubaki nikimshangaa pasi na kujibu salamu yake.

Muda huo huo jojo akatoka nje akiwa na simu yake na kWa Furaha akamsalimia mkaka huyo.

“Hi Luke “

Hapo ndio nikajua Kuwa huyo mkaka anaitwa Luke.

Basi mkaka huyo akashuka kwenye gari na kWa bashashaa ya hali ya juu wakakumbatiana na Jojo.

“Unajua sikuamini ulivyoniambia Kuwa upo Tanzania “

Alizungumza jojo kisha kWa pamoja yeye na mkaka huyo Wakapanda kwenye gari na kusogea kwenye Nyumba ya jilani ambayo ilikuwa nzuri sana kuliko hii ya shangazi, ilikuwa ni Nyumba kubwa ya ghorofa katika mtaa huo .

“Nikiolewa na mkaka Kama huyu nitapata watoto wazuri sana”

Nikaanza kujiongelesha Mwenyewe mambo ambayo haya Kuwa na maana kabisa 😂🙌 Yaani kumuona mtu Mara moja tu tayali nimeanza Kuwaza kuwa mke wake 😂 naitaji maombi kwakweli.

Majila ya usiku ikiwa ni muda wa Kulala, muda huo nilijilazimisha kupata usingizi lakini uligoma kabisa, muda wote akili yangu ilimuwaza Luke na kujikuta nikijichekea Mwenyewe.

“Umepatwa na ugonjwa wa chekelea au ??”

Jojo aliniuliza.

Kitendo cha jojo tu kuniuliza nikajikuta nikilopoka.

“Hivi Luke ni mchumba ako ??”

Jojo aka……

IJE JOJO ATANIPA JIBU GANI TUKUTANE SEHEMU YA 2…

LIBBY (call me mama )

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 02

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Jojo akanigeukia akiwa amechukia sana mpaka nikamuogopa nikabaki nikimkodolea macho tu nikisubili kibao changu cha shavu maana ni ameshazoea kunipiga vibao pale ninapomchukiza na Jambo.

Lakini gafla Muda huo huo jojo akaangua kicheko cha hali ya juu na kunijibu.

“Yaani Mimi ndio nitoke na na Luke ? 😂🙌 unaleta utani wewe si ndio ? Sasa Yule si Kama mwanamke mwenzangu tu jamani, mtu Unakuwaje na mahusiano na mtu amekuzidi uzuri “

Hapo nikamuuliza Tena.

“Kwahiyo ata umpendi ??”

“Nampenda Kama Rafiki yangu tu, ata hivyo ni mtu Mwenye dharau sana”

“La…..”

Nilitaka nikuuliza swali lingine lakini jojo akanizuia na kusema.

“Sitaki Tena maswali “

Eeeeh nikaamua tu kutuliza komwe langu nikalala.

Ikiwa ni siku ya weekend, nikiwa jikoni naandaa chakula, uku familia nzima ikiwa sebuleni inaangalia movie, hakukuwa na na mmoja Aliyesema aje kunisaidia, gafla nikasikia sauti ya shangazi.

“Libby, Libby niletee hiyo juice ya chungwa “

“Sawa shangazi “

Nilijibu nikiwa nimechukia sana, Yaani wao wanajua tu kutuma awajui mtu yuko na kazi nyingi za kufanya kazi ni kumtuma utazani wao awawezi kufanya.

Basi nilichukua juice na kwenda nayo sebuleni.

“Eeeh mama nimekumbuka”

Jojo alimwambia mama yake.

“Nini Tena princess “

“Sitaki kulala Tena na Libby, I need my privacy Walahi, na ukiachana na hivyo uwa nakosa usingizi maana Libby anakoloma sana “

Shangazi akanigeukia kisha akazungumza.

“Lakini hakuna chumba kingine ambacho anaweza akakaa, kile cha wageni mnajua kabisa bibi yenu akija ataki kabisa kukuta mtu Yaani ni chumba chake peke yake”

Hapo hapo mjomba akadakia.

“Nafikili chumba cha store ni kikubwa sana, ni kupanda vitu vizuri tu, kesho nitaingia mjini kumnunulia godoro “

Daaaah napelekwa store mwenzenu 🥹.

Shangazi nae akazungumza.

“Yaaah ni kweli “

Kisha shangazi akanigeukia na kuniambia.

“Ukimaliza kupika ukasafishe store ile, hakikisha unapanga vitu vizuri ili upate sehemu ya kuweka godoro “

“Sawa “

Nilijibu na kurudi zangu jikoni uku machozi yakinitililika na sikutaka wajue kaama nilikuwa nalia.

Baada ya kumaliza kupika nikatenga chakula mezani na kwa pamoja tukakaa mezani , kila mtu akapakua chakula chake na nilipotaka tu kupakua shangazi akaniuliza.

“Umemaliza kazi zako zote ??”

“Ndio shangazi bado kumwagilia maua jioni lakini pia na kufanya usafi kule store “

“Sio store ile ni chumba chako Binti uwe na shukurani, kWa bibi yako Mlikuwa mnalalia vilago, ukiamka asubuhi mwili wote unauma, kaendelee na kazi zako kwanza, Kuanzia sasa uwezi kukaa na sisi meza moja “

Daaaaah Ila nyie hawa watu kwani nimewakosea nini Mimi jamani, kWa unyonge sana uku tumbo la njaa likiniunguruma, Niliinuka na kwenda kuendelea na usafi kwenye store.

Aaah store ilikuwa na vumbi Kama lote, Ndani ya dakika 2 tu nilianza kupiga chafya mfululizo lakini pia na mafua nikapata.

Majila ya jioni kama kawaida nikarudi zangu kwenye kumwagilia maua na muda huo huo Luke akaja nikabaki nikimshangaa tu.

“Unanifananisha au ??”

Luke aliniuliza baada ya kuona Kuwa namuangalia sana.

“Aaaah, aaaah, mmmmh”

Aaah kigugumizi Sijui nilitoa wapi mie 😂🙌 Yaani nilishindwa ata kuzungumza.

“Hivi wewe ni bubu au ? Jana nimekusalimia umebaki unanitolea macho tu, Leo Tena hivyo hivyo, au usikii vizuri Binti ??”

“Hapana Luke “

Nilijibu Tena kwa kutaka Jina lake.

“Na Jina langu unalijua pia “

“Nililisikia jana wakati unaongea na dada jojo tu “

“Ooooh kumbe wewe ndio mfanyakazi wao Mpya ??”

Luke aliniuliza.

“Hapana “

Nilikataa lakini muda huo huo jojo akatoka nje akiwa kwenye mavazi ya mazoezi Kama ambavyo Luke amevaa, jojo akadakia maongezi.

“Unakataa nini sasa ? Utaki crush wako ajue Kama wewe ni kijakaazi ??”

Daaaaah me najua hawa watu ni ndugu zangu kumbe wao wananiona Mimi Kama KIJAKAZI wao tu, Walahi moyo uliniuma sana.

“Crush ? Unataka kumaanisha nini ??”

Luke akauliza kwa mshangao mkubwa sana.

“Umemdatisha KIJAKAZI wa mama jojo, usiku kucha alikuwa akikuongelea, na kuniuliza Kama Mimi na wewe tuna mahusiano”

Luke alinigeukia na kuniangalia snaa kisha akazungumza.

“Ahahaa, khaaaaah hii nayo Kali Binti tafuta wa hadhi yako, halafu usinizoee”

Kheeeeeeh Walahi Nina damu ya kunguni Walahi Mbona kila kona wananikataa ? Yaani sipendwi ata kidogo.

*******

Siku ziliendelea kwenda uku manyanyaso yakizidi kuongezeka Ndani kWa shangazi, hakuna mtu ambaye alinipenda Wala kuniheshimu.

KWa upande wa mjomba Chuki yake ni kwakuwa tu nimekataa kumpa mwili wangu hivyo ni hasira zake zinamfanya anitese.

KWa upande wangu, moyo wangu ulizidi kumuwazia Luke na kuamini Kuwa kuna siku nitampata na atakuwa wangu.

Ikiwa ni siku ya kumbukizi ya harusi ya shangazi, shangazi na mume wake walikuwa wakisherehekea miaka 14 ya ndoa Yao, siku hiyo kulikuwa na ndugu na jamaa wengi sana, na siku hii ndio niligundua Kuwa shangazi na mume wake Wana connection kubwa snaa na watu wenye Pesa zao.

Nikiwa naendelea kuwahudumia vinywaji wageni waalikwa, gafla akaingia Luke akiwa na baba yake, weeeeeeeeeh what a shegeeeeeeeeh Naomba niseme Kuwa like father like son, Walahi Luke amefanana sana na baba yake Yaani amefanana kila kitu hadi Yale macho ya paka.

Nilijikuta nikiganda na Kuwaangalia tu.

Baada ya muda nikawakaribisha na kuwapa vinywaji.

“Unaitwa Naani Binti ??”

Baba mzazi wa Luke aliniuliza baada ya kuwahudumia vinywaji.

“Naitwa Libby “
Nilijibu uku nikitabasamu.

“Jina zuri sana “

Majila ya Saa 6 usiku sherehe yote iliisha na watu wakatawanyika isipokuwa Luke na baba yake ambao ni majilani wa Karibu.

“Jilani na Mimi nataka Mdada jamani, ningepata Kama huyu ningefurahi sana, lakini pia nataka wa kuja na kuondoka tu maana ni usafi wa ijumaa jumamosi na jumapili tu”

Shangazi akanigeukia kisha akajibu.

“Kama ni siku hizii tu Libby atakuwa Ana kufanyia maana siku hizoo hapa Nyumbani uwa anapumzika tu afanyi chochote “
Kheeeeeh Ila shangazi ni Muongo jamani.

NAKUJA MY ZANGU…
LIBBY (call me mama )

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 03

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Nilitamani kusema Jambo lakini shangazi alikuwa akiniangalia sana hivyo nikabaki nikijichekesha tu kisha baba Luke akazungumza.

“Daaaah jilani umenisaidia sana sana kwakweli, tangu nimefika hapa Nimeona juhudi za huyu msichana “

Aaaah at least ata kuna mtu ananisifia Walahi.

Baada ya mazungumzo Luke na baba yake wakaaga na kuondoka, baada ya wao tu kuondoka, jojo akaanza mambo yake.

“Mama unamruhusuje huyu aendee kule jamani ? Hizi kazi za hapa atakuwa Akifanya Nani ??”

“Hivi jojo Unafikili me mama yako sina akili eti ? Najua nini nafanya, kazi za hapa atakuwa akifanya usiku tu, na nafanya hivyo ili awe analipwa uko na atupatie Pesa zetu na kumlisha kila siku na kumpa hifadhi kwenye Nyumba yetu “

Eeeeh hii Nyumba kila siku Wana njia Mpya ya kunifanya niumie.

“Libby , hakikisha Kuwa Nyumba Ina Kuwa safi hii sasa hivi, maana ni chafu sana, uko nje kuna makopo Sijui tishu hakikisha unamaliza ndio unaenda kulala”

Eeeh Tena jamani, Yaani siku nzima maandalizi nimefanya peke yangu, kujudumia wageni na kila kitu, lakini pia Saa hizi natakiwa kufanya usafi kweli jamani, aaah Mungu atulindie tu wazazi wetu wasituache kwenye mazingira mabaya Kama haya 😭”

Kila mtu akaingia kulala na Mimi nikaanza kufanya usafi, nilitoka hadi nje kabisa kwaajili ya kuokota makopo Kama ambavyo iliambiwa na shangazi, Sawa nilikuwa nikiogopa sana lakini sikuwa na chaguo.

“Libby “

Nilishtuka sana baada ya kusikia mtu Akiita Jina langu kWa usiku huo tena ni usiku, haraka nikageuka uku Nikijiami kWa kunyoosha Fagio ambalo nilikuwa nimelishika mkononi.


“Aaaaah “

Nilishusha pumzi Ndefu baada ya kukutana uso kWa uso na baba mzazi wa Luke.

“Umenishtua sana “
Nilimwambia uku nikishikilia upande wenye moyo.

“Unafanya nini usiku huu Tena peke yako ??”

Baba huyo aliniuliza.

“Aaah naweka mazingira tu Sawa then naenda kulala”

“Unajua nilikuwa pale juu nimeshtuka sana kuona mtu anazunguka zunguka hapa na sikujua Kama ni wewe, ni hatari kWa wakati huu wewe Kuwa nje Ebu ingia Ndani hii kazi utafanya ata kesho “

Daaaah kuna Namna nilitamani ata kumwambia Kuwa ni amri niliyopewa na shangazi lakini nilishindwa kabisa nikabaki nikimtolea macho tu.

“Ni wazi Kuwa unaipenda kazi yako, haya endelea kufanya nitakuwa hapa na wewe mpaka Umalize “

Aaaah hapo alinipa nguvu kabisa nikaendelea kufanya kazi yangu nikiwa sina wasiwasi, huyu mbaba jamani ni Mcheshi sana, sitaki kumuita mzee kwakuwa ni hajazeeka ata kidogo, ana mwili wake mzuri kabisa, body imeenda shule, muonekano ni 10 over ten 🔥 kiufupi huyu baba yuko hot kama Kijana wake.

“Haya ukapumzike sasa Binti mrembo “

Aaah nyieeeh kuna mtu ata ananiita mrembo ikiwa wengine wote wananiona Kama pimbi vile.

*******

Siku iliyofuata Tena nikaamua asubuhi na mapema kwaajili ya Kuwaandalia watu kifungua kimya then nikarudi Tena kulala maana nilikuwa Nina usingizi sana.

******

Hatimaye siku ya kuanza kazi Nyumbani kWa kina Luke iliwadia jamani, niliendelea asubuhi sana kutokana na maelezo niliyopewa na shangazi.

Baba mzazi wa Luke alinionesha kona zote za Nyumba na sehemu ambazo natakiwa kushughulika nazo.

“Aaah ikiandaa chai utakuja kuniita Nipo chumbani “

Baba Luke aliniambia.

“Sawa boss “

Nilijibu uku nikikunja goti langu kidogo.

“Hahaha Libby Bwana Niite Papaa na sio boss “

“Sawa papaa”

“Waooooh that’s good, kazi njema “

Mbaba huyo akaaondoka na Mimi nikaingia kwenye majukumu yangu.

“Hivi ulishundwa kukataa hii kazi ??”
Luke aliniuliza baada ya kujnikuta sebuleni nikiendelea na usafi.

Nilimuangalia kWa muda Walahi huyu kaka achoshi kwenye kumtazama kwanza nashukuru Kuwa nimepata kazi Nyumbani kwao itakuwa rahisi kWa sisi kujenga ukaribu.

“Hivi masikio yako yanachelewaga kupokea taarifa au ni nini ?? Yaani mtu anakuongelesha unabaki unamshangaa tu “

Luke alilalamika.

“Za asubuhi Luke “

Nilimsalimia uku Nikijaribu ata kubana sauti yangu labda anaweza akadata kWa kiasi Fulani.

“Sina shida na salamu yako, kitu ambacho nataka uwende askılını mwako kWa sasa ni wewe kukaa mbali na Mimi, Yaani umu Ndani tuishi kama hatuonani, usiniongeleshe Wala kunisalimia”

Gafla nikalopoka.

“Labda Kama nitakuwa bubu kweli Kama ambavyo unazania”

“Unasemaje wewe “

Niliona huyu atanichelewesha tu maana Nina kazi nyingi sana, natakiwa nimalize hapa halafu nikaendelea na kazi za Nyumbani Yaani hakuna kupumzika ni Kama mashine hivi.

Nilinyanyua ndoo yangu ya maji na kuondoka na kumuacha akiendelea Kuchongoa mdomo wake.

“Idiot “

Alizungumza Luke kisha akaondoa kwenye mazoezi.

*******

Week Mbili zilipita tangu nianze kazi kWa kina Luke na niseme Kuwa huyu mzee ni baba na nusu, kwanza ni mtu ambaye anajali sana, ukiachana na hivyo ni baba ambaye anahakikisha Kuwa Kijana wake anaishi vizuri kabisa na anajua majukumu yake.

Tukiwa kwenye meza ya chakula Mimi na baba Luke, nilijikuta tu nikilopoka.

“Samahani papa, lakini Naomba kujua mama Luke yuko wapi mpaka unaishi wewe na Luke tu??”

“Ooooh aaah yuko marekani ameolewa uko, na Anamaisha yake sasa “

“Ooooh samahani kwa kuuliza na pole pia”

“Pole ya nini Tena jamani ??”

“Ya Kuishi tofauti na mwenza wako, bibi yangu aliniambia Kuwa watoto uteseka sana wazazi wanapotengana “

“Aaah usijali ni changamoto tu, Mimi na mama Luke ni miaka 9 sasa tangu tumeachana na lakini pia ni watu wenye amani sana, tunawasiliana vizuri na ukizingatia yuko na Binti yetu wa mwisho uko “

“Ooooh kumbe Luke Ana ndugu yake ??”

“Yaaah anaitwa Lucy”

Muda huo simu ya baba Luke ikaita na kwa Furaha akazungumza.

“Ooooh umemtaha tu na yeye ananipigiw ni mama Luke “

Basi akapokea wakazungumza kWa muda kisha akanitambulisha kWa mama Luke.

“Luke akusumbui kweli ??”

Mama huyo aliniuliza.

“Hapana anisumbui mama “

Siku hiyo Tulizungumza na muda wangu wa kuondoka ulipofika nikaenda kumuaga mbaba Luke.

“Oooh nilisahau Nina zawadi zako Binti yangu mpendwa “

Alizungumza baba Luke, kisha akanyanyuka kwenye kitanda chake na kusogelea kabati lake kisha akatoa mfuko mkubwa Kiasi na Kunikabizi.

“Ni nini hii papaa ??”
Nilimuuliza uku nikiushangaa mfuko huo.

“Ni mavazi tu kidogo nilikununulia Jana, samahani kama nitakuwa Nimekosea lakini hizii siku ambazo uko hapa nimegundua Kuwa umarudia sana nguo lakini pia asılı kwenye hali nzuri “

Nyieeeeh ukisikia destiny helper ndio huyu sasa, Yaani ni siku chache tu lakini anazidi Kuwa Mwema pasi na kujali Kuwa Mimi sio sehemu ya familia yake.

KWa Furaha sana nilijikuta nikilia lakini pia nikamkumbatia kWa nguvu sana.

“Asante sana, Asante Mungu akubariki sana, Mungu akuongezee pale ulikotoa papaa”

Baba Luke akanikumbatia kwa nguvu sana na kunituliza kwani nilikuwa Nikilia kWa uchungu sana.

Baada ya hapo nikachukua zawadi zangu ile natoka tu uso kWa uso na Luke ambaye alikuwa Amesimama sebuleni lakini macho yake yote yalikuwa kwenye chumba cha mlango wa baba yake.

“Umetkka kufanya nini kwenye chumba cha baba yangu ?? Na iki ni nini ??”

Luke aliniuliza uku akinipokonya mfuko ambao nilikuwa nimeushika mkononi.

“Nilienda tu kumuaga boss, na hizo ni zawadi ambazo amenipatia “

Luke kWa hasira akabinua mfuko ule na kumwaga nguo zangu chini.

“Kusanya uchafu wako na upote hapa “

Luke akanifokea kisha akaondoka.

Basi nikakutana nguo zangu na kurudi Nyumbani ambapo nikakutana na Kisangani kingine kutoka kwa shangazi yangu.

JE NI KISANGA GANİ TUKIMBIE KWENYE LINK WATU WANGU.
LIBBY (call me mama )

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 04

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Picha linaanza ile kuingia tu ni uso kWa uso na shangazi yangu unaweza ukasema Kuwa alikuwa akinisubilia mimi tu.

“Shikamoo shangazi “

Nilimsalimia shangazi uku nikikumbatia mfumo wangu wa nguo vizuri maana Weeeh.

“Hiyo ni nini ??”

Shangazi akaniuliza kWa jazba sana uku akinipokonya mfuko ule ambao nilikuwa nimeushika, na kWa haraka akamwaga nguo zote chini.

Haraka haraka Jojo akainuka alipokuwa amekaa na kuja kuangalia kwa ukaribu.

“Hizi nguo umetoa wapi ??”

Shangazi aliniuliza uku akinitolea macho utazani nimerudi na kitu cha ajabu Nyumbani.

Kabla sijajibu chochote kile Jojo akazungumza akiwa na furaha sana.

“Uwiiiiiih hii Gauni nzuri jamani, utanifaa sana Tena navaa kesho kwenye party”

Shangazi akamgeukia Binti yake na kumwambia.

“Ebu rudisha hapa unajua hizo nguo Zimetoka wapi au ??”

Kisha shangazi akanigeukia Mimi na kuniuliza KWa Mara nyingine .

“Nikuulize umekuwa bubu au ? Hizi nguo umetoa wapi wewe Mtoto ??”

“Ni baba Luke ndio amenipatia, sifahamu Kama ni Mpya au ni za zamani “

Shangazi akaniangalia kisha akaniuliza.

“Ulishindwa kukataa au ? We Mtoto utakuja utolewe kafara wewe Sijui unanielewa, umeenda kule kwaajili ya kufanya kazi na sio kupokea misaada unanisikia ??”

Hapo shangazi akavuta masikio yangu kWa nguvu sana na kunifanya nihisi maumivu makali sana na ukizungatia nilikuwa nimevaa zile heleni za ring ambazo ni Mia 5 tu.

“Kusanya uchafu wako na upotee hapa”

Nikaokota nguo zangu zote na kwenda chumbani kwangu, Yaani Mimi amani naipata nikiwa nyumbaani KWa kina Luke tu, Tena naipata nikiwa na baba Luke Peke yake maana huyu Luke ni kisanga kingine.


Yaani Luke ni Kijana ambaye amejawa na dharau ya hali ya juu, uwa ananifokea mimi utazani anazungumza na Mtoto Mdogo kumbe ni mtu mzima kabisa kama yeye.

******

Siku iliyofuata haikuwa ni siku ya kwenda kwa kina Luke hivyo nilikuwa bize nikifanya shughuli zangu za Nyumbani.

Nikiwa bize na kazi za jikoni, nilishtuka sana baada ya kuhisi Kuwa kuna mtu amepapasa kiuno changu haraka nikageuka na kukutana uso kWa uso na Freddy ambaye ni Mtoto wa kiume wa shangazi huyu ana miaka 20 nimempita miaka 3.

“Ni nini jamani ??”

Nilijikuta nikimfokea.

“Nini kuhusu nini na wewe ? Eeeh Mtoto kiuno kama cha nyigu Walahi aaaah “

Alizungumza Mtoto wa shangazi uku akiniangalia kWa macho yake ya tamaa sana.

“Hivi libby una mchumba kweli wewe ??”

Freddy aliniuliza.

“Sina shida na wachumba”

Nilimjibu kWa dharau kisha nikaendelea na kazi zangu.

“Nina Uhakika wazungu wamejaa “

Alizungumza Freddy lakini sikuwa nimemuelewa hivyo nikaendelea tu na shughuli yangu niliyokuwa nikiifanya.

Freddy ni kisha ambaye adabu ni imepita kulia ikatokea Kushoto, kiufupi watoto wa shangazi ni zaidi ya hasara Yaani na hii yote ni kutokana na malezi ambayo wao Kama wazazi wamewapatia watoto wao.

“Aaah unaweza kuja chumbani kwangu usiku wa Leo ??”


Freddy aliniuliza kwa utulivu wa hali ya juu sana hali ambayo ilinishangaza sana maana umu Ndani hawajuagi kuzungumza na Mimi kwa utaratibu ata kidogo.

Niliendelea kufanya kazi zangu pasi na kumjibu na muda huo huo sauti ya baba yake ikasikika hivyo haraka akatoka nje.


Ikiwa ni siku ya weekend, siku hiyo ilikuwa ni zamu ya kufanya kazi kwa kina Luke, nilifanya usafi wa Nyumba nzima kisha nikaenda chumbani kWa Luke kumuuliza kuhusu chakula kwani baba yake hakuwepo kwa wakati huo.

“Luke utapendelea kula nini ??”


Nilimuuliza Luke ambaye alikuwa akiniangalia kWa dharau sana.

“Sitakula “

Alijibu Luke kisha akarudishaa macho yake kwenye simu.


“Luke, Sijui Kwanini unanichukia lakini nakuomba sana usiifanye kazi yangu Kuwa ngumu, asubuhi nimekuandalia chakula umekimwaga pasi na Kuwa na sababu ya msingi muda huo baba yako amekisifia sana iko chakula, Saa hizi unasema utaki kula uko Sawa kweli wewe “

Hapo Luke kWa hasira akanyanyuka na kunisogelea Karibu kabisa na kWa kung’ata meno yake akazungumza.


“Kaa mbali na Mimi wewe mnuka jasho, Kaa mbali na Mimi wewe masikini wa kutupwa uliyelaaniwa, libby, najua Kama unanipenda sana na Unanitaka Leo kesho sasa kwa taarifa fupi kabisa Kaa ukijua Kuwa nakuchukia sana na sitakuja kukupenda na, Ukipata nafasi ya kuondoka kwenye Nyumba hii Naomba uondoke maana unanipa kichefu chefu “

Luke alimaliza kunifokea kisha akanitemea mate usoni na kutoka nje, hapa ndio niliamini kweli Mimi sipendwi na Kama ni mikosi Basi hii ni imezidi 🥹.

Kwakuwa Nilimaliza kila kitu, nilifungasha kila kitu na kwenda kukaa nyuma ya Nyumba Nikimsubili baba Luke..

Nilikaa Sana kule nyuma uku muda ukiyoyoma tu, hatimaye masaa mawili yakapita pasi na baba Luke kurudi, lakini muda huo huo Luke akaja na kuanza kuniuliza kwa kunifokea.

“Umu Ndani Leo Hatuli au ??”

Walahi huyu Kijana Kama sio kichaa Basi kichaa ndio kinamuanza, yaani ni yeye ndio amekataa kabisa kuniambia ni chakula gani anataka kila lakini muda huo huo anakuja kuulizia chakula.

Nilimuangalia mwisho nikanyanyuka na kwenda Ndani ambapo pia akanifuata.

“Naongea na wewe libby umu Ndani hatuli au ? Asubuhi me Sijala, Saa hizi mchana naona jiko limenuna kabisa shida nini ??”

“Luke kwani uko na shida ya akili au shida ya kusahau ??”

Nilijikuta Nilimuuliza kWa hasira sana.

“Ni Mimi ndio unaongelesha hivyo au ??”

Luke aliniuliza uku akinisogelea Kana kwamba anataka kuniipiga .

“Ni wewe ndio kwani Naongea na Nani hapa, Nimekuwa Mtulivu na mkimya sana tangu Nimekufahamu lakini sio sasa Sawa ? Luke Mimi pia ni binadamu kama wewe na Ninaitaji amani, sijawai kukukosea, sijawai kwenda kinyume na matakwa yako lakini umekuwa ukitafuta kila njia ili uweze kugombana na Mimi , umekuwa ukitafuta kila njia ili uniambie Maneno ya karaha na kuniumiza na vyote nimepokea sio sasa, Kama Pesa na maisha mazuri ni yako achana na maisha yangu Broh “

Nyieeeh nilijikaza sana kuzungumza hivi mbele ya kule ambaye alionekana kuchukia sana.

“Akija baba ako Mwambie nimeacha kazi shetani wa mguu mmoja wewe “


Nyieeeej 😩🙌 Leo nimeweza halafu nimeweza Tena, Luke hakuamini kabisa kama ni Mimi ndio namwambia Maneno kama hayo, alibaki akiniangalia tu, nilichukua mfuko wangu ambao nilienda nao na kurudi Nyumbani.

Walahi kWa wakati huo nilikuwa Nina hasira sana, nilifika kWa shangazi na kumkuta akiwa amekaa na watoto zake Wanaangalia movie wakiwa na furaha sana, nikiwaangalia mwisho nikawapita kama siwaoni.

“Weeeh paka wa kirugulu “

Shangazi aliniita, yaani kwenye hii Nyumba kila siku napata Jina jipya.

“Mbona umerudi Saa hizi au umeshalipwa ??”


Shangazi aliniuliza baada ya Mimi kusimama.

“Nimeacha kazi “


Nilijibu kWa hasira sana mpaka Shangazi na familia yake wakanyanyuka kWa pamoja.

“Ni Mimi ndio unanijibu Kama mie mwenzako ??”


Shangazi aliniuliza uku akinisogelea Karibu zaidi.

Kwa hasira Shangazi akanyanyua mkono wake na kutaka kuniachapa kibao lakini nikawai na kudaka mkono wake Shangazi aka…..

NAKUJA MY ZANGU ILA MNIOMBEE 🥹🥹
LIBBY (call me mama )

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SEHEMU YA: 05

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍

Kitendo cha Mimi kudaka mkono wa shangazi kilimshtua kila mtu, Yaani hakuna mtu alitegemea Kuwa kuna siku nitakuja kujitetea Kama hivyo.

Kiukweli nilisshachoshwa na manyanyaso ya umu Ndani hivyo niliona ni muda wa mimi kujisimamia, kiufupi Mimi ni msichana Mtulivu sana lakini pia ni mikorofi pale mambo yanaponifika shingoni, kijijini kwetu wananijua kabisa Mimi ni ngumi jiwe Yaani sitaki mambo Mengi.

“Wewe ndio unanidaka mimi ??”

Shangazi aliniuliza uku akiangalia mkono wake Mara Mbili Mbili, kWa Kuwa niliwa na hasira sana nikajibu.

“Ata kama ningetakiwa kuukata Basi ningekata, nimechoshwa na manyanyaso ya kipigo kila hiitwapo Leo, nimechoka Kuwa mtumwa kwenye maisha ya kila mtu, hivi ata nikikuuliza ni kosa gani nimewai kukukosea ni nini utaniambia ? Ni jibu gani sahihi ambalo utanipatia”

Jojo akaniangalia kWa muda mwisho akataka kunivamia mwilini lakini nilimuwai na kumsukuma kWa nguvu sana na kumfanya aanguke chini Kama Mzigo.

Aaaah hapo Bwana Nilimfanya kila mtu kukasilika, shangazi alinivuta kwa nguvu sana na akanichania nguo yangu ya juu na kunifanya niwe mtupu mbele ya watoto wake wa kiume.

“Mama, muache Bwana”

Mtoto wa mwisho wa kiume wa shangazi ambaye alijulikana kama Niko akajaribu kumtuliza mama yake ambaye alikuwa na hasira sana kWa wakati huo.

“Niko kaa kimya huyu kima anatakiwa kujifunza adabu “

Nyieeeeh nilipigwa siku hiyo, Sawa napigwagwa lakini iki kipigo cha Leo ni kaama cha mbwa mwizi, Yaani nilipigwa na kuzalilika nimshukuru niko ambaye alipopata nafasi tu akanivuta na Kunikimbiza kwenye chumba cha store ambacho nilikuwa nikilala.

“Usitoke nje mpaka watulie “

Alizungumza niko na kuniambia nifunge mlango kWa Ndani.

Hakuna siku nimelia kama hii Walahi, Yaani Kama ni maumivu Basi yalikuwa Makubwa sana moyoni kwangu, nilikuwa na maumivu ya kila aina yaani kuna muda mpaka nikawa nahisi naweza nikachizika.

Nilibaki store Nikijililia tu, Majila ya Saa 2 usiku mjomba alirudi kutoka kwenye mizunguko yake na kupewa taarifa ya ugomvi ambao ulitokea uku nikionekana Kuwa Mimi ndio mkorofi.

“Mke wangu huyu Mtoto wa kaka yako Kiukweli utanisamehe lakini sitaki kumuona umu Ndani , na Ninaposema hivi Namaanisha sasa hivi aondoke “

Mjomba Alizungumza kWa hasira sana lakini Niko kwa upole akazungumza.

“Lakini Saa hizi ni usiku sana, Nafikili mngemuacha then asubuhi ataondoka “

“Tena wewe Kaa kimya Sawa ? Niko Kaa kimya kabla Sijakumaliza, baba yako yuko sahihi libby anaondoka sasa hivi “

Aaah Basi mwaya mkuku mkuku nikaja kutolewa kule chumbani, nikakusanyiwa kila kilichokuwa changu na kufukuzwa mpaka nje kabisa.

Kitu ambacho nilikuwa sikielewi ni niko kunitetea, Yaani niko alihakikisha Kuwa anasimama upande wangu, niko hakuwai Kuwa Mwema kwangu Ila kWa Leo Walahi Mungu ambariki.

Basi mwaya nikafukuzwa nje na mfuko wangu mkubwa kabisa wa shangazi kaja.

“Nafikili ni bora Kama nitarudi kijijini tu “

Nilizungumza Mwenyewe.

Nikavaa moyo wa ujasili kisha huyo nikashika njia mpaka Nyumbani kWa kina Luke.

“Baba Luke Amerudi ??”

Nilimuuliza mlinzi wa getini ambaye uwa anakuwepo pale Majila ya usiku tu Ana asubuhi anaondoka.

“Yaaah yupo Ndani “

Alijibu mlinzi uku akinishangaa sana na lile fuko langu lakini pia kWa jinsi ambavyo nilikuwa nimevimba, Yaani alama kila kona.

Moja kwa mona nikaingia Ndani ambapo sebuleni nikakutana na Luke ambaye alikuwa Ana Angalia movie kwenye tv lakini akili yake yote ilikuwa kwenye simu yake, 😂🙌 hii watu wa dasilamu ndio Wanaelewa, Yaani wanawasha Tv halafu Wanakuwa bize na simu zao.

“Umekuja kufanya nini muda huu ??”


Luke aliniuliza na kunyanyuka pale alipokuwa amekaa.

“Sijaja kwaajili yako Nimekuja kuzungumza na huyu mzee anayekuweka mjini “

“Unasemaje wewe ? Hivi we Binti unanichukuliaje ??”

Kabla Luke ajanifanya chochote sauti ya baba yake ikasikika ikiuliza.

“Hizi kelel za nini ??”

Luke aligeuka na kumuangalia baba yake kwa hasira sana kisha akaondoka chumbani kwake.

“Libby nini shida ??”

Baba Luke aliniuliza baada ya kuona Kuwa Nimevimba lakini pia Nipo na shangazi kaja langu.

“Shikamoo “

Nikamsalimia.

“Libby Ebu njoo ukae chini maana ni Kama hauko Sawa hivi “

“Niko Sawa, aaaah Nimekuja kuchukua Pesa yangu nataka kurudi kijijini kwetu tu “

“Pesa ? Mbona nilipigwa simu na hao unaoishi nao Wakaniambia nitume nikatuma muda mrefu sana tangu Saa 10 jioni “

Woiiiiiiiih hii familia jamani Sijui inataka Niishi maisha gani mimi kWa wakati huo sikuwa ata na nauli ya kwenda kwetu na nilikuwa Nikitegema hiyo hela sasa me Nafikaje kijijini kwetu.

“Naomba unisaidie kitu baba “

Nilimwambia baba luke.

“Nakusikiliza”

“Aaaah Kwa sasa Nimefukuzwa hapa nilipokuwa nikikaa hivyo nilikuwa naitaji kwenda kijijini kwetu, kitu ambacho Naomba kutoka kwako ni nauli tu ya kunisaidia kufika Nyumbani”

“Ebu libby polepole kwanza, kWa haraka haraka nakumbuka Kuwa uliwai kuniambia Kuwa hii ndio familia uliyobaki nayo, nakumbuka uliniambia Kuwa hauna wazazi na bibi yako uliyekuwa unaishi nae amefariki sasa unataka ukaishi na Nani uko ??”

“Bora kule Nina majilani ambao nimewazoea lakini pia wananipenda sana, Naomba unisaidie nauli”

“Hakuna shida Ila kWa sasa Naomba ulale utaondoka asubuhi “


Ni kweli muda ulikuwa umeenda sana hivyo, moja kWa moja nikapelekwa kwenye chumba cha wageni.

********

Asubuhi na mapema nikaamka na kufanya usafi wa Nyumba nzima kisha nikajiandaa na kubaki nikimsubilia baba Luke apate kuamka na anipe nauli.

Majila ya Saa 2 baba Luke akaamka na kuniita chumbani kwake.

“Libby, Jana nimetumia usiku wangu kufikilia sana Nimeona uwe mfanyakazi wangu Rasmi, Yaani nikuajili moja kWa moja lakini pia nitakuongezea mshahara unaonaje ??”

“Mmmmh sio kwamba italeta shida na shangazi ??”

“Shangazi yako aniletee shida Mimi ? 😅 Libby sio shangazi yako Wala Mjomba ako anayeweza kunipandishia sauti labda Kama watataka kuishi maisha magumu “

Aaah kwakuwa baba Luke alinihakikishiia usalama niliamua kubaki.

*******

Ndani ya mwezi mmoja tu jamani niliona mabadiliko, nyie nilipendeza sana, kiufupi nilinona sana Yaani nilipata muonekano wa tofauti sana.

KWa upande wa Luke na Mimi kugombana ni kila siku Kama mtu na mke mwenzie.

Ikiwa ni Majila ya Saa 5 usiku nikiwa chumbani kwangu, niliweza kusikia mlango wangu ukigongwa haraka nikaenda kufungua na kukutana uso kWa uso na baba Luke, uwiiiih nilitamani ata kukimbia kutoka na mavazi yangu niliyokuwa nimevaa.

“Oooh baba Karibu “

Nilimkaribisha uku nikiona aibu sana haraka nikawai kanga na kujifunga vizuri.

“Mbona usiku baba kuna shida ??”

Nilimuuliza.

“Kubwa sana “

Alijibu baba Luke na kunifanya nipate wasiwasi.

“Nini shida baba “

“Aaaah relax Libby Sawa, Kaa chini “
Basi sote tukakaa na kWa utulivu baba Luke akaniambia.

“Aaaahh kWa sasa naitaji kuoa, naitaji Nyumba iwe na mama ili ipendeze zaidi na ikiwezekana Kuwe na watoto wengine Yaani Luke apate wadogo zake “

“Oooooh wazo zuri sana baba, nakuunga mkono”

“Mwanamke huyo nataka uwe wewe Libby”

“Mmmh 😳😳 “

Nilishtuka na kubaki nikiwa nimetoa macho.

“Nimerizika na wewe kwenye kila kitu, nimependezwa na tabia yako lakini pia na uelewa mkubwa ambao uko nao, ukiachana na hivyo moyo wangu unakupenda na kukuitaji sana”

Alizungumza baba Luke uku akishika mikono yangu yote miwili na kuipapasa.

EBU NIAMBIENI NIFANYEJE JAMANI MBONA NACHANGANYIKIWA SANA.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote