Follow Channel

LISSA TABASAMU LA BOSS

book cover og

Utangulizi

LISSA TABASAMU LA BOSS 1
MTUNZI SMILE SHINE

" Jamani leo ndio siku yangu ya kwanza kwenda kuripoti kazini na bado mnataka nichelewe.
Aliongea binti Lisa huku akiendelea kupekua kila kona ya chumba ambacho kulikuwa na mabinti wengine wawili waliokuwa wamelala kitandani.
Lisa alisogea kitandani na kuanza kuwaamsha wenzie huku akiwatingisha
" Rehema, Amina hebu amka ni uniambie pochi yangu iko wapi?
" Aaah acha kutusumbua bwana kwani pochi yake huwa tuna share? Si kila mtu huwa anatumia pochi yake. Alijibu Rehema huku akivuta shuka akajifunika vizuri na kuendelea kulala.
" Nyumba hii mna makusudi sana sijui ndio wivu wenu ama vipi? Mnajua kabisa leo ndio siku yangu ya kwanza kuanza kazi lakini unanifanyia kusudi kunifichia pochi yangu.

Lisa aliendelea kulalamika huku akitafuta pochi yake, mara alifika mama wa makamo alisimama mlangoni huku akiwa kafunga kitenge kifuani .
" Lisa kwanini unapiga kelele mapema yote hii hujui kama watu bado wamelala?
" Mama pochi yangu niliweka hapa lakini sioni....
Najua ni makusudi ya hawa wanao wananionea wivu , wanataka niendelee kuuza mitumba kutwa kupasuka mpaka koo linakauka.
" Basi hizo kelele zinazopigwa hapa ndani ni mfano wa kelele zinazopigwa huko kwenye mitumba yako naomba upunguze watu bado wamelala.
" Sasa vipi kuhusu pochi yangu?
" Tafuta taratibu.
" Nisaidie basi mama muda umeenda.

Mama yake aliangaza macho pale chumbani kisha akasema.
" Sijui kwanini unakuwa msahaulifu pochi yako hiyo apo juu ya tenga la nguo zenu chafu.
Lisa aliangalia juu ya tenga wanaliweka nguo chafu kisha akashuka kiuno chake na kutingisha kichwa.
" Ooooh jamani kutafuta kiti kisichoongea ni kazi sana.
Lisa alienda kuchukua pochi yake na kuiweka begani.
" Mama naomba dua na baraka zako leo ndio siku yangu ya kwanza kwenda kuanza kazi.
" Kila siku dua zangu zipo na wewe mwanangu.
" Asante mama.
Lisa hakutosheka na dua za mama yake alienda kuwaamsha ndugu zake wamuombee dua.
" Amina, Rehema naombeni dua zenu.
" Wewe mbona msumbufu lakini unataka kuombewa dua mara ngapi hebu tuache bwana.
" Acheni roho mbaya kupata kwangu ndio na nyie mmepata jamani.
" Haya kila la kheri.
" Asante.

Lisa anaondoka nyumbani kwao akaelekea kazini kuanza kazi yake mpya.
Alifika kwenye jengo kubwa la ofisi ya Future line Ltd. Na hiyo ndio kampuni mpya akiyoenda kuanza kazi.

Aliingia ndani ya jengo akaelekea mapokezi.
" Habari za asubuhi dada judith.
" Salama Lisa , karibu.
" Asante.
" Bila shaka unataka kuonyeshwa ofisi yako ya kazi.
" Ndio dada.
" Ok , sasa nenda kwenye lift itapanda mpaka ghorofa ya tatu hapo utakutana na John atakueleza sehemu yako ya kufanyia kazi.
" Sawa asante .
Lisa alienda kupanda lift na kuelekea ghorofa ya tatu , alipofika alikutana na mr John .
John alimpokea vizuri na kumuelekeza ofisi yake mpya.
Lisa avutiwa na ofisi yake mpya ilikuwa nzuri pake pale alitoa simu yake na kuanza kupiga picha ndani ya ofisi mpya.
Kumbe wakati anafanya hivyo kulikuwa na mwanaume anapita alipomuona akasimama nje ya mlango wa kioo ambao ulionyesha ndani akawa anamuangalia. Hakuwa mwingine bali alikuwa mr David Ceo wa kampuni ya future.
David alikuwa ni kijana mtanashati , anaejituma kwenye kazi zake ,alikuwa makini, hakupenda kupoteza muda kwenye mambo ya kijinga , alichukukia mfanyakazi mzembe kufukuza kazi ilikuwa ni jambo dogo sana kwake.

David aliendelea kusimama huku akiwa kaweka mikono yake kwenye mifuko ya suruali , alimuangalia Lisa kwa makini kwa kile alichokifanya .
Baada ya Lisa kumaliza kupiga picha mara mlango ulifunguliwa na david akaingia.
Lisa alishangaa mtu yule kuingia bila kuwa na nidhamu lakini hakuulizia chochote zaidi ya kumkaribisha kwa tabasamu.
" Karibu.
David hakuitika alimuangalia .
" Naweza kukusaidia chochote tafadhali?
" Unaweza kuniambia tangia umeingia hapa ofisini umefanya kazi gani ?
Hili swali lilimfanya Lisa ahisi kuwa aliyopo mbele yake ni boss wake.
" Sijafanya chochote ndio kwanza nimeingia ofisini muda huu.
" Unapata wapi ujasiri wa kupiga picha ikiwa haujui mezani kwako kuna nini cha kufanya?
Lisa aliangalia mezani aliona makaratasi na ma faili mawili.
" Samahani boss.
" Sipendi hili kujitokeza tena upo hapa kwaajili ya kufanya kazi na sio kwaajili ya kutangaza biashara au kujionyesha kuwa na wewe una miliki ofisi.

Baada ya David kuongea hivyo aliondoka kuelekea ofisini kwake na Lisa alikaa kwenye kiti chake na kuanza kukagua faili na yake makaratasi.
Alianza kufanya kazi alivyotakiwa kufanya baada ya kumaliza alitakiwa kupeleka ofisi kwa David.
David aliagiza ile kazi na kukuta ipo sawa .
" Kazi nzuri miss......
" Lisa.
" Nadhani ukisoma vizuri mkataba wetu
" Ndio.
" Basi kama utafanya vizuri zaidi nitakupatia mshahara wako wote na sio nusu tena.
" Sawa boss nitahakikisha na fanya kazi kwa bidii na vizuri.
" Ok hebu chukua hizi karatasi uzibane pamoja
Lisa alisogea karibu na David alichukua karatasi akatoweka pamoja alipokuwa anataka kubana alijikuta karatasi zote zimeanguka miguuni kwa David na nyingine zilikuwa mapajani kwa David.
David alimkata jicho ambalo lilimpa wasiwasi Lisa.
" Samahani.

Lisa akiinama na kuokota zile karatasi haraka.
" Kwanini unakuwa mzembe hivyo , unajua hizi karatasi niza muhimu kiasi gani? David alifika na kumfanya Lisa atetemeke.
" Inatetemeka nini fanya haraka. David aliendelea kuongea kwa ukali.
Lisa alitikisa ya haraka na kubana wakati anataka kuweka mezani akashangaa David nae anasogea pia David alikuwa anamuangalia usoni.
Kuja kushituka Lusa anagundua kumbe zile karatasi alikuwa kabana pamoja na tai ya boss.

LISSA TABASAMU LA BOSS 2
MTUNZI SMILE SHINE

Lisa alishituka sana alipogundua kuwa kabana tai ya boss na karatasi muhimu za kazi, alimuangalia David usoni akakuta David anamuangalia huku akiwa kakunja uso.
" Samahani boss, ni bahati mbaya.
Lisa aliomba msamaha lakini David alizidi kumuangalia usoni huku akiwa kakunja uso wake.
Lisa alisogeza mikono yake ili kutoa ile tai mara mlango ulifunguliwa na secretary.

Secretary alipowaona alionyesha kama mshangao kuwakuta wakiwa wamekaribiana, alishindwa kusema kilichompeleka akawa anawaangalia.
" Acha Lisa unaweza ukaenda, na wewe ulikuwa unasemaje?
" Samahani boss nilikuja kukwambia kuwa baada ya nusu saa utakuwa na kikao na wawekezaji.
" Una nitania si ndio?
" Hapa a boss.
" Si nilikwambia taarifa ya kikao unipe saa moja kabla.
" Ndio
" Sasa kwanini ukaniambia muda huu?
" Haukuwa umefika kazini boss.
" Hauna email yangu, hauna namba ya simu zangu?
" Samahani boss.
" Nachukia neno samahani, Hili kisijirudie tena.
" Sawa.
Secretary alitoka ofisini , David akawa anatoa tai yake iliyokuwa imebanwa na karatasi.

Lisa alirudi nyumbani akawakuta mama na ndugu zake wamekaa kibarazani nae akaungana nao. Alimsalimia mama yake kisha wakaanza kujuliana hali
" Vipi habari za kazi?
" Salama lakini balaa.
" Umeshavurunda huko?
"Yani huyo boss ni balaa yani hacheki na yoyote uso wa mbuzi kila muda sheria kama zote ukali ndio usiseme yani leo tu nimeshafokewa mara kibao yani mpaka kuna muda nikawa nimekumbuka biashara yangu ya mitumba kupiga kelele kuita wateja.
" πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Ukute ulikuwa unaongea ovyo kama mpiga debe.
" Wala sio hivyo kwanza nimepiga picha nikiwa kazini akanikuta. Pili nimebana karatasi na tai yake.....
Lisa alivyosema hivyo wote waliangua kicheko.
" Kuwa makini na kazi yako mwanangu kosa dogo litafanya uharibu kazi yako.
" Sawa mama acha nikapumzike nimechoka sana.
Lisa alinyanyuka akaingia ndani.

Kesho yake Lisa alifika kazini mapema sana , akiwa parking ya nje alipata wazo asogee kwenye moja ya gari ajiangalie kwenye kioo ili ajiweke sawa.
Alisogea kwenye moja ya gari zilizokuwa zimepark mwanzo alijiangalia kwenye kioo akagundua make up yake haijakaa sawa na anatakiwa kupendeza.
Alitoa make up akaanza kujipaka huku alijiangalia kwenye kioo cha gari
" Natakiwa kuwa smart bwana.
Alichukua lipstik yake akapaka mdomoni wakati anaisambaza vizuri kwenye midomo yake alishangaa kuona kiiooo cha gari kunashusha anakutana uso kwa uso na David.
" Mungu wangu leo tena nafanya kosa kwa mara nyingine tena bado mapema sana .
Alijisemea Lisa.
" samahani boss sikujua kama ni gari yako.
Alisema Lisa alafu akaondoka haraka bila hata kugeuka nyuma.

Mambo ya Lisa yalimfanya David zaidi kumfuatilia Lisa kwenye utendaji wake wa kazi.
Na kwa upande wa Lisa aliongeza juhudi na umakini akawa anafanya kazi zake vizuri mpaka ikafikia hatua David akawa anavutiwa sana na utendaji wake kazi..
Kuna baadhi ya kazi walifanya pamoja.
Siku moja Lisa na David walikuwa wanatoka kwenye mambo yao ya kazi walifika sehemu wakashuka kwenye gari na kwenda kupata chakula . Wakati wanarudi kwenye gari Lisa aliona matunda mchanganyiko yalikuwa yanauzwa akatamani na hakuwa na hela.
" Samahani boss una hela ya chenchi hapo?
" Ya nini?
" Matunda yale pale nahisi wanauza mia tano mimi nina hela kubwa hapa nahofia hawatakuwa na chenchi.
David alijipapasa hakuwa na hela ndogo alitoa Wallet na kutoa elfu 10.
"" Shika hii.
" Mbona kubwa.
" Wewe shika kanunue unachotaka.
Lisa alienda kununua matunda kisha akarudi na kumpa chenchi.
" Asante boss chenchi hii hapa.
" Kaa nayo.
" Yote?
David hakujibu.
" Naomba unishikie.
David alishika konteina ya matunda Lisa akaweka hela kwenye pochi yake , alipomaliza alichukua matunda yake wakaondoka.

Siku moja Lisa aliingia ofisini kwa David, siku hiyo David alimpokea kwa bashasha na tabasamu kubwa . Lisa alishangaa sana ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona tabasamu kutoka kwa boss wake .
" Duuu kumbe akitabasamu anakuwa mzuri hivi.
Alisema Lisa huku akiwa bado kamkodolea macho.
" Karibu Lisa.
" Asante.
" You look smart, but It hope you're smarter inside.
Aliongea David huku akiendelea kutabasamu na kumuangalia Lisa kwa makini wakati huo Lisa alikuwa anashangaa tu.

LISSA TABASAMU LA BOSS 3
MTUNZI SMILE SHINE

Lisa alikuwa bado kaduwaa akimshangaa David
" Kaa Lisa.
Lisa alivuta kiti akakaa.
" Nimeleta hili file, nimeshamaliza kazi.
" Good.
David alichukua
Lile file alikagua baada ya kumaliza kukagua alifunika na kumuangalia Lisa usoni.
" Lisa tunaweza kupata kahawa pamoja.
" Hapana boss nina........
" Kwanini hapana? Hapa mimi ndio boss, kampuni yangu, kazi zangu na wewe mfanyakazi wangu sasa wasiwasi ni Wanini kama kila kitu ni cha bwana heri?
Lisa alitoa tabasamu la mbali. David alipiga simu na kuagiza kahawa mbili pamoja na biscut za tangawizi.

Baada ya dakika chache kahawa ilipelekwa wakaanza kunywa , David alikuwa kachangamka sana aliongea sana siku hiyo
" Vipi unaionaje kahawa?
" Nzuri.
" Mbona kama unakunywa kahawa kwa uwoga unaniogopa?
" Hapana.
" Basi changamka mrembo pindi unapokuwa na mtu kama mimi.
Linda alikuwa anakunywa kahawa akajikuta anapaliwa na kuanza kukohowa.
David aliweka kikombe cha kahawa juu ya meza na kumfuata alipokaa.
Alimpiga mgongoni huku akimpa pole, alitoa kitambaa na kumfuta.
Linda bado aliendelea kukohowa. David alienda kuchukua grass ya maji na kumpatia anywe kidogo.
Lisa alikunywa na kuacha kukohowa. David alimuangalia usoni jinsi alivyokuwa mwekundu na macho yakitoka machozi, David akajikuta anapata hisia flani alisogea karibu na kutaka kumbusu midomo ya Lisa.
Kabla hajafika Lisa alisogea hatia moja nyuma. Wakati huo mapigo yake ya moyo yalidunda kwa kasi, jasho wembamba lilianza kumtoka, mikono yake ilitetemeka.
Wakati huo David alikuwa akimuangalia sana usoni.
Taratibu David alipiga hatua akamsogelea na kuishika shingo ya Lisa kwa nyuma taratibu alisogeza uso wake , Lisa alipoona wanaenda kukutanisha midomo yao alifunga macho.
David aliifikia midomo ya Lisa a na kuanza kunyonya taratibu.
Lisa alitulia na kukiacha David aendelee na alichokianzisha.
David alimaliza akamuachia na kumuangalia usoni, Lisa aliona aibu na kuinamisha macho yake tena.
" Lisa...
David aliita kwa sauti ya upole na kufanya Lisa anyanyue macho kumuangalia.
Waliangaliana kwa sekunde kadhaa David alionyesha nia ya kutaka kurudia kitendo cha mwanzo Lisa alijitoa mikononi kwa David na kutoka ofisini kwa David akaelekea ofisini kwake.
Alifika ofisini kwake alikaa kwenye kiti chake na kushika midomo yake.
" Ni nini kimetokea? Lisa umefanya nini na boss wako?
Lisa alijiuliza maswali kisha akaachia tabasamu ikiwa na maana kwamba alifurahishwa au kile alichofanya David kilimsisimua.
Lisa akiwa bado anafikiria mara mlango wa chumbani kwake ulifunguliwa.
Lisa alishituka kumuona David kaingia,Lisa alisimama akawa anamuangalia.
David alisogea karibu na meza anayofanyia kazi Lisa , akavuta kiti akakaa na kukunja nne .
" Mbona umesimama?
Aliuliza David na kufanya Lisa akae.
" Vipi kazi zinaenda je?
" Zinaenda vizuri.
Alijibu Lisa huku akiwa na wasiwasi na hakuweza kumuangalia David usoni kutokana na kuwa na aibu ya kile kilichotokea ofisini kwake.
" Hivi umetolewa au una mchumba?
Hilo swali kilimshitua Lisa akawa anamuangalia bila kujibu.

David aliendelea kumuangalia kwa sekunde baada ya hapo akasema.
" Basi kuwa makini kwenye kazi zako maana umakini huwa unaanzia kwenye kazi na badae kuwa mama bora kwenye familia yako na wala usifikirie kila tabasamu ni nafasi ya mapenzi.

Lisa alihisi kauli hiyo kama sindano moyoni kwake na wala hakueleza David alikuwa anamaanisha nini kumwambia vile.
David alikuwa akimuangalia jinsi alivyokuwa kaduwaa baada ya hapo alinyanyuka akatoka na kufunga mlango.

Lisa alijitupa juu ya kiti chake na kuvuta penzi ndefu.
" Huyu mtu ana maana gani au anafikiria mimi ni mwanamke rahisi baada ya kutulia pale alipokuwa ananibusu.
Lisa alifikiria sana badae akasema
" Potelea kote nipo hapa kwaajili ya kazi tu.

Usiku Lisa alikuwa kasimama mbele ya kioo cha dressing table chumbani kwao akawa anajiangalia kwenye kioo huku akifikiria sana boss wake.
" Hivi kwanini nafikiria hilo jambo kwa siku mzima, kwanini hatoki akilini?
Rehema alifika ghafla na kusikia alivyokuwa anaongea.
" Ni nani huyo asietoka akilini mwako?
Lisa aligeuka kumuangalia
" Umefika hapa saa ngapi?
" Tangia ulipoanza kuongea mwenyewe.
" Aaah potezea maongezi yangu hayana maana.
" Mara hii Umepata mpenzi huko kazini?
" Siku fuata mapenzi nimefurahi kazi sijui unanielewa?
Alisema Lisa kisha akaenda kupanda kitandani akajifunika shuka na kulala.

Kesho yake Lisa alienda kazini akaendelea na kazi zake kama kawaida lakini kila alipokutana na boss wake aliona aibu. Moyo wake haukuweza kusahau kilichotokea kwa mbali alikuwa akihisi kuwa ameanza kumpenda boss wake.

Siku moja Lisa alikuwa kakosea kidogo kufanya kazi yake, David alipiga simu na kumtaka afike ofisini kwake haraka sana.
Lisa alienda ofisini kwa David kusikiliza alichoitiwa ,alimkuta David anapekua faili baada ya kumaliza alifunika akamuangalia Lisa usoni.
"Hii kazi umefanya wewe?
" Ndio boss.
David alisukuma kwa nguvu lile file likaanguka chini. Lisa akiinama akaokota na kuishika mkononi kwake.
" Hiki ni nini umefanya? Hebu angalia ulichofanya humo ndani.
Lisa alifungua faile akaangalia na kugundua lile kosa dogo alilokuwa kafanya.
" Samahani boss imetokea bahati mbaya haitakuja kujirudia.

David alikuwa na hasira lakini sauti ya Lisa ni kama ilimtuliza flani akajikuta anapunguza hasira.
" Kuwa makini Lisa, kuwa makini na kazi yako na uepuke usumbufu wa kijinga. Ukifanya vizuri kazi zako nitakupa heshima lakini kuvurunda sitasita kukuchukulia hatua.
" Nisamehe.
" Ok nenda karekebishe hiyo kazi haraka sana nalihitaji hilo file hapa baada ya dakika 30.
" Sawa.
Linda alichukua file na kuondoka haraka pale ofisini .

LISSA TABASAMU LA BOSS 4
MTUNZI SMILE SHINE

Kuna wakati David alikuwa mkali sana kwa wafanyakazi wake na wengine walifukuzwa kazi kwasababu ya makosa ambayo yalikuwa madogo Madogo. hali hiyo ilimfanya Lisa awe muoga,makini alimuogopa sana David pia alikuwa analinda kibarua chake kisije kikaota nyasi.

Siku moja asubuhi Lisa alikuwa anaenda ofisini kwa David , alikutana na Anna secretary wa boss. Walisimama na secretary nje ofisini kwa boss wakawa wanaongea.
" Vipi Lisa nasikia ilinusurika kufukuzwa kazi?
" Nani kakupa hizo habari?
" Kila mtu anajua hivyo.
" Sio kweli lilikuwa ni onyo tu kila kitu kipo sawa.
" Kuwa makini huyu kiumbe huwa haeleweki hata kidogo maisha yake hayana tofauti na kinyonga huwa anabadilika mara kwa mara ni ngumu kumuelewa.
" Ni kweli. Kwani Boss yupo ofisini kwake?
" Nadhani bado hajafika maana huu sio muda wake wa kuingia kazini. Alijibu secretary.
" Unaweza kunipeleka hili file?
" Lisa nina mambo mengi natakiwa kufanya kabla boss hajafika naomba unisaidie kupeleka tafadhali.
" Sawa.
Lisa alikubali a
akasogelea mlango wa ofisi ya David akafungua na kuingia huku secretary akiwa anaendelea na kazi zake nyingine.

Lisa alisogea karibu na meza ya David akaweka file alipopiga jicho pembeni akaona picha ambayo ilikuwa imechanwa na kugawanywa vipande viwili kipande kimoja kilikuwa cha picha ya David na kipande kingine kilikuwa cha mwanamke mrembo aliekuwa na tabasamu mwanana lililomfanya avutie zaidi na kupendeza.
" ni mrembo sasa sijui ni nani wake boss?
Lisa akiwa bado anaangalia vile vipande vya picha na kujiuliza maswali mara akashituka kuona mtu kaweka grass ya mvinyo mezani .
Lisa alishituka sana na kugeuka kumuangalia.
Lisa akajikuta ameuliza swali bila kutegemea
" Kumbe ulikuwepo?
" Ndio nilikuwa chumba cha kupumzika leo nilifika mapema sana.
Alijibu David huku akiangalia vipande vya picha vilivyokuwa mkononi kwa Lisa.
Lisa alipoona anaangalia alirudisha mezani haraka.
" Samahani...... Nilileta faili.
Alisema Lisa huku akitaka kuondoka .
David alinyoosha mkono na kushika kiuno cha Lisa.
Lisa alisimama na kugeuka kumuangalia.
" Lisa hivi unajua tofauti kati ya kosa na hatari?
" Hapana boss
David alitoa mkono wake na kugeukia alafu akasema.
" Makosa inaweza kugharimu kazi na hatari inaweza kugharimu ❀️ moyo.

Lisa alikuwa anashangaa maana bado alikuwa hajaelewa David anamaanisha nini kusema hayo maneno.
" Unamaanisha nini boss?
" Kumbe wewe bado mtoto? Basi nenda ila ipo siku utajua tu.
Lisa alipiga hatua kuelekea mlangoni ili atoke ofisini , lakini kabla hajafungua mlango David alimuita.
' Lisa.....
" Abeee. Aliitikia Lisa na kugeuka kumuangalia.
" Nimependa muonekano wako wa leo. Nilitaka ujue hivyo.
Alisema David huku akiwa anatoa tabasamu la kulazimisha.
Baada ya kumwambia hivyo Lisa alitoka ofisini na kwenda ofisini kwake.

Mambo ya David kutokueleweka anataka nini kwa Lisa yalikuwa yakuimchanganya Lisa.
Siku moja alikuwa amekaa na rafiki yake wakawa wanaongea.
" Vanessa hivi mtu ambae anampenda mtu huwa anaonyesha dalili gani?
Vanessa alimuangalia Lisa alafu akaanza kucheka.
" Umependwa au umependa?
" Hapana nataka kujua tu.
" Kama huniambiii sababu ya kutaka kujua siwezi kukwambia lolote.
" Unajua boss wangu haeleweki kuna wakati nahisi kabisa ananitaka lakini kuna muda haionyeshi kabisa hizo dalili anakuwa Bize na mambo yake yani kama vile hanioni.
" Usiniambie na wewe umeanza kumpenda
" Sikuwa na wazo hilo lakini kuna baadhi ya mambo anafanya yananisisimua na kunifanya nianze kumpenda lakini msimamo wake kwangu haueleweki.
" Lisa wewe ni rafiki yangu nakujua vizuri sana na maswala ya mapenzi nayaelewa japokuwa sio kwa kina.
Lisa kwa jinsi unavyosema nakushauri usimchukulie serious huyo boss wako huenda akawa na tamaa zake tu ndio maana anafanya hivyo , unaweza ukafuata hisia zako badae ukaja kuumia na kujutia maamuzi yako.



LISSA TABASAMU LA BOSS 5.
MTUNZI SMILE SHINE

Lisa alikubaliana na ushauri wa rafiki yake baada ya hapo aliondoka kila mmoja akarudi kwao.
Usiku Lisa alipokuwa kajilaza kitandani kwake akitafuta usingizi alianza kufikiria maneno ya David.
" Alikuwa ana maana gani kuniambia kosa linaweza kugharimu kazi lakini hatari inaweza kugharimu moyo. Hili neno linanichanganya sana sijui alikuwa anamaanisha nini yani maneno yake yamekuwa ya mafumbo sana.

Siku zilizidi kwenda Lisa aliendelea na kazi alikuwa anamkwepa sana boss wake maana alikuwa akimuona akili yake ilikuwa inahama .
siku moja Lisa na wenzake wanaofanya kazi kwenye idara yao walikuwa kwenye chumba cha mkutano wakijadili kitu mara David aliingia na kwenda kukaa kwenye kiti chake kisha baada ya hapo akaanza kuzungumzia maswa la miradi mpya unaotaka kuanzishwa kwenye kampuni yao.
Wakati David anaongea mara nyingi jicho lake lilikuwa kwa Lisa , Lisa akiinamisha kichwa chake chini kuepuka kuangaliana nae, kuna muda alinyanyua kichwa wanakutana macho na kutazamana kwa sekunde kisha Lisa aliangalia pembeni.

Baada ya mkutano kuisha kila mtu alinyanyuka na kuondoka , Lisa wakati anakusanya vitu vyake aondoke David alimwambia.
" Lisa unaweza kubaki hapa kwa muda kidogo?
" Sawa boss .
Wafanyakazi walitoka wote wakabakia Lisa na David.
David alinyanyuka kwenye kiti na kumsogelea Lisa huku mkononi akiwa kashika bahasha.
" Naona sasa umekomaa kwenye kazi , unafanya kazi zako vizuri sana kwenye ile mpango uliopita ulinifurahisha mno, shika
Hii ni kama shukurani yangu kwako.
Alisema David huku alimkabidhi bahasha .
" Lakini haina haja ya kufanya hivi ni wajibu wangu kufanya kazi kwa makini......
" Mmmmmh sitapendezwa kama hautapokea hii zawadi ninayokupatia

Lisa aliamua kupokea ile zawadi akafungua pake pale wakiwa wamesimama wote. Alikuta kuna Cheni iliyotengenezwa kwa madini ya dhahabu tena ilikuwa na kito cha jina lake Lisa pia kulikuwa na saa ya mkononi ya bei ghari
Lisa alishangaa
" Boss hivi vitu ni vya gharama sana , sidhani kama inafaa kuwa yangu.

David alimuangalia Lisa huku akitabasamu alafu akasema.
" Ni yako nataka uvae hii saa zingatia kuivaa kila wakati kwaajili ya kuangalia muda sahihi wa kufanya mambo yako. Pia ukiwa inaivaa kuna hali fulani nitakuwa naisikia moyoni kwangu na pia kuna mtu namthami zaidi ya vile anavyofikiria.

Kwa kiasi flani David alionekana kuongea kwa hisia , Lisa alikuwa kaduwaa hakujua aseme nini.
Alishukuru kwa sauti ya chini na kutaka kuondoka lakini David alimzuia tena
" Lisa
" Abeee boss
" Ukihitaji kitu chochote unaweza kuniambia hata kama ni nje na kazi.
Lisa bado alikuwa kaduwaa na David alikuwa kamkazia macho usoni.
Lisa alitabasamu kwa uwoga kisha akaondoka.
Lakini moyoni alikuwa na hisia sana na David na zilizidi kukuwa siku hadi siku
Kwa upande wa David nae ilionekana nae alikuwa na hisia lakini alikuwa akijizuia labda alifanya hivyo sababu Lisa ni mfanyakazi wake au kulikuwa na sababu tofauti na hiyo.

Usiku Lisa alikaa kitandani akawa anaangalia zawadi zake huku akitabasamu lakini ghafla ile kauli ya David ilijirudia kichwani kwake
" Hatari inaweza kugharimu moyo.
" Hapa naanza kupata picha huenda David anaogopa kuniambia kuwa anampenda lakini inawezekana ameshawahi kupitia magumu kwenye maswala ya mapenzi , acha nimuachie afanye anachofanya ipo siku moja atatambua anataka nini.

Siku moja baada ya muda wa kazi kuisha Lisa hakuondoka alibaki ofisini kwake na kufanya kazi zake , alifanya kazi huku giza likiwa linaanza kuingia.
" Natakiwa kuwasha taa ili nimalize hii kazi siwezi kuondoka bila kumaliza.
Lisa alinyanyuka kwaajili ya kwenda kuwasha taa lakini kabla hajapiga hatua taa uliwashwa aliewasha al hakuwa mwingine alikuwa ni David amesimama huku akiwa kashika grass ya mvinyo mkononi kwake pia alionekana amelewa.
" Boss kumbe bado upo?
David hakujibu alimsogelea aliweka grass ya mvinyo mezani alafu akasema
" Lisa nimekuwa nikikuona kujituma kwenye kazi ,hii imenivitia sana alafu kuna hili lingine nimekuwa nikijiuliza sana ......
Aliongea David huku akishika nywele za Lisa alizokuwa kabana na nyingine zilikuwa zimeanguka pembeni ya uso kisha akaendelea kusema.
" Najaribu kujizuia sababu mimi ni boss kwako huenda nitajaribu kila kitu lakini kila ninapokuona moyo wangu unapata sababu mpya ya kupambana na hisia . Lisa sijui kama ni kosa au hatari umekuwa zaidi ya mfanyakazi kwangu.
Lisa alihisi dunia imesimama kwa sekunde , moyo wake ulianza kudinda kwa kasi akawa anamuangalia moja kwa moja.
" Boss kwanini iwe hivyo kwangu?
Swali la Lisa lilimfanya David ashituke kama vile mtu aliekuwa usingizini na alikuwa akiota ndoto.
" Vipi boss naongea na wewe.
" Aaaaah Lisa usichukuliwe makini hiki nilichokiongea .
Alisema David kisha akaondoka ofisini kwa Lisa na kumuacha Lisa njia panda asielewe David anataka nini.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote