LORAH (A slay Queen)

book cover og

Utangulizi

LORAH (A slay Queen)

LORAH (A slay queen) 🧚🏻‍♀️

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 01


ANZA NAYO.......

Lorah ni binti mwenye umri wa miaka 28, ni mzuri kwa umbo na sura pia, ukimuangalia ata ukiwa mwanamke lazima urudie kumuangalia tena na tena uku ukijiuliza kichwani mwako kwamba ameumbwa au ameshushwa.

Binti Lorah ni binti ambaye amebarikiwa sana aswa kwa muonekano wa nje na lakini pia amebarikiwa bahati ya hali ya juu, yaani kwa kifupi nyota yake inang'aa kuliko kawaida.

Lorah ni binti ambaye alibarikiwa sana, ukiachana na kuzaliwa kwenye familia ya kimasikini ambayo ata kupata Unga robo ilikuwa shida, lakini Mungu aliamua kumuinua Lorah kutoka chini na kuwa mtu ambaye anapesa na matamanio ya kila mtu.

Muonekano wa Lorah umeweza kuwa chachu kubwa sana ya mafanikio yake, sio kwamba alitumia mwili wake katika kutajilika hapana, Lorah alibahatika kufanya kazi na wasanii kadhaa kama video queen, lakini pia na makampuni tofauti tofauti kwaajili ya ngozi yake nzuri na ata watu wa shape walimtumia Lorah katika kujibland.

Binti Lorah bhana, alifundwa akafundika katika maisha yake, baada ya Lorah kuwa mtu maarufu na kupata kazi kila kona, aliamua kutumia pesa zake katika kuendeleza elimu yake na hiyo ikamuongezea Thamani kwa kila mtu au makampuni ambayo alikuwa akufanya nayo kazi.

Nikisema kuwa Lorah ni mwanamke mwenye Bahati muwe mnanielewa jamani, Lorah akabahatika kupata mume ambaye alikuwa na pesa nyingi sana.

Mume wa Lorah alijulikana kama Donovan lakini watu wengi walimkatisha kwa kumuita Don, Don ni mkaka ambaye anajielewa sana, ukiachana na na kuwa na pesa nyingi bado amekuwa mtu mwenye kuthamini kila mtu.

Ukiachana na Lorah kuwa maarufu sana, lakini Don hakuwa maarufu ata kidogo mara nyingi aliishi kwenye kivuli cha mtu mwingine kwa kujificha sana na hakutaka kuonekana kabisa kwa watu kuwa yeye ni mtu mwenye pesa, sababu hii ikapelekea Don kuwa mbali kabisa na mitandao ya kijamii.


SONGA NAYO.....

Haya sasa baada ya kupata historia fupi ya Lorah uko, juu naomba niwaambie kuwa Lorah mwenyewe nimefika na nipo hapa kukugawia story yangu ambayo kwa namna moja au nyingine itakufundisha pakubwa sana.

Lorah mimi nimezaliwa kwenye familia ambayo ata kipata Unga wa uji ni shida, yaani ni mtihani over matatizo, katika familia yetu tumezaliwa watoto watatu tu na mimi ndio wa kwanza.

Baada ya kuangaika sana na maisha, mpaka nikafikia hatua ya kuishia elimu ya kidato cha pili, niliamua kuingia mtaani na kufanya kazi yoyote ile ambayo iliniingizia pesa.

Kwa wakati huo sikujali kiasi cha pesa ambacho nililipwa, kitu cha muhimu kwa wakati huo ilikuwa ni Mimi kupata pesa ambayo ingenisaidia mimi na familia yangu.

Katika kuangaika uku na uku mimi na ndugu zangu, Mungu aliamua kunichagua na kuniinua kutoka chini na kuja juu.

Muonekano wangu mzuri ulinifanya kukubarika sana na watu, kila kona nilijikuta nikipendwa na kujulikana, nikaanza kupiga pesa kama sina akili nzuri, ukiingia uko Instagram ndio kabisa nimekichafua hatari, followers wa kutosha.

Ukirudi upande wa tiktok ndio uniambii kabisa yaaani mambo ni yente yente.

Katika baraka ambazo Mungu alinijaalia, ndoa pia ilikuwa ni moja kati ya baraka ambazo Mungu alinibariki.

Mume wangu alikuwa ni mwanaume mtulivu sana walahi, alikuwa ni mwanaume ambaye pesa ipo lakini hana majigambo ata kidogo, kitu ambacho kilipelekea mimi nayeye kupishana kidogo.

Kwa upande wangu naweza kuunga mkono msemo wa masikini akipata matako ulia mbwata.

LORAH mimi baada ya kupata pesa nilibadilika kila kitu, nilikuwa na weusi wangu mzuri kabisa wa melanin lakini nikaamua kujikoboa na kuwa mweupe peeeh, na kwakuwa nilitumia vitu original nilipendeza mno.

Familia yangu niliinunulia nyumba na kuwaamisha kule kwenye mazingira ya kimasikini na kuwafanya kuishi maisha mazuri.

********

Ikiwa ni miezi sita baada ya ndoa yangu, niliamka asubuhi na mapema na kujiandaa, nikapigilia mavazi yangu ambayo yaliacha sehemu kubwa ya mwili wangu wazi.

Kwa wakati huo sikujali kabisa kuhusu mavazi, nilichojali ni kwamba watu wananitazama na kunipa attention kubwa.

Nilimaliza kuvaa na kujipulizia marashi pale kisha nikashika njia na kutoka nje ambapo sebuleni niliweza kukutana na mume wangu ambaye alikuwa bize na laptop yake akiendelea na shughuli za kujenga Taifa.

"Unaenda wapi asubuhi yote hii??" Don ambaye ni mume wangu aliniuliza.

Niligeuka na kumuangalia kisha nikajibu.

"Oooh kumbe sikukuaga ?, anyway naenda kwenye kampuni ya.......kwaajili ya tangazo jipya la Lotion, nafikili nitarudi jioni "

Mume wangu aliinuka alipokuwa amekaa na kunisogelea karibu kisha kwa sauti ya chini na yenye kumaanisha akaniuliza.

"Ukuona kama kuna umuhimu wa kuniambia mapema ??"

"Si ndio nimekuambia hapa lakini kwani shida iko wapi ??" Nilijibu tena kwa kufoka.

"Lorah, mimi ni mume wako sawa umu ndani tunaishi mimi na wewe kwahiyo ninachofanya mimi lazima wewe ujue, na unachofanya wewe lazima mimi nijue ".

"Ukoloni sasa" nilijibu kwa sauti ya chini lakini mume wangu aliweza kusikia.

" kwa wewe unaona ni ukoloni lakini huo ndio utaratibu mzuri, umekuwa mtu wa kujifanyia mambo yako pasi na kunishirikisha, yaani unafanya mambo utakavyo tu nakuangalia tu "

"Don unanichelewesha, kwanza huu sio muda wa wewe kunifokea, ni muda wa wewe kunipa baraka kedekede ili dili langu likatiki uko "

"Sawa amna shida, me baraka zangu uko nazo muda wote but ili vazi lako sijalipenda kabisa "

"Umeanza I have to go "

Nilijibu na kwa mwendo wa haraka nikaondoka zangu.

Kwa upande wa mume wangu alibaki akiniangalia tu, kwa wakati huo naweza kusema kuwa umaarufu uliniadaa tu, muda wote niliwaza watu wa nje na sikujali kuhusu Mimi na familia yangu.

Ila mimi jamani, kazi yenyewe niliambiwa ni saa 7 mchana lakini saa 1 asuhuhi nimetoka nyumbani kwangu.

Safari yangu ilikuja kuishia kwa shoga yangu ambaye alikuwa na pesa sana na alikuwa akiishi maisha yake ya ubachela tu.

Kuna wakati nilikuwa nikiyatamani sana maisha ya shoga angu sema ndio hivyo na mimi nilikimbilia ndoa mapema sana.

Kwa shoga angu huyo nilipafanya kama kwangu jamani, niliingia muda wowote na kutoka muda wowote ule.

"Mmmh mke wa mtu asubuhi na kivazi iko safari ya wapi ??" Rafiki yangu aliniuliza baada ya kunikaribisha.

"Aaah mke wa mtu hiyo kwiyo, mke wa tu mwamba nina muhuri usoni au ??" Nilimuuliza na kuangua kicheko cha kishangingi.

"Aaaah mbona kama unakataa hivi eeh, sio muhuri lakini Pete ya ndoa si hiyo kidoleni"

"We nawe nitokee hapa, aaah leo ndio siku ile ya lile dili langu, so nimejiandaa kwaajili ya kwenda uko ila nimekuja kutulia hapa niweke mambo sawa then baadae naenda"

"Eeh utabaki mwenyewe me naingia kazini leo "

alijibu shoga angu na kunifanya nibaki mdomo wazi kwani sikutalajia kuwa nitabaki mwenyewe pale nyumbani kwake.

Majila ya saa 7 niliwasili kwenye kampuni husika na kusaini mikataba pale kisha nami nikaanza kazi chapu.

Kwa wakati huo pesa kwangu ilikuwa ni kitu cha kawaida sana, naingia mikataba mikubwa mikubwa na watu wakubwa bhana hivyo nilikuwa najiamulia tu.

Ila sasa naweza kusema kuwa akili yangu ni kama finyu hivi, nilipata pesa za kutosha lakini niliishia kwenye kujipendezesha na kuzichezea tu.

Ingawa niliolewa lakini kusafiri na kwenda kwenye nchi za jilani ilikuwa kawaida sana, niliweka starehe mbele kuliko kitu chochote kile.

Majila ya usiku nikiwa na mume wangu kitandani, Don alianza kunishika uku na uku ili tuweze kushiriki tendo lakini nilisogea pembeni kwa kuonesha kukataa.

“Shida nini mama ??"

Don aliniuliza kwa sauti ya chini lakini yenye mshangao.

"Aaah, niko siku za hatari mpenzi kwani Kinga ipo ??" Nilimuuliza.

Don aliinuka kwa jazba sana kisha akaniuliza.

"Kwanini tutumie Kinga ? Lorah usiniambie kuwa bado utaki kuwa mama, mimi na wewe ni mke na mume, tuna kila kitu cha kutufanya tuwe na familia, familia ambayo haitapata shida na itakuwa bora zaidi wasiwasi wako ni nini ??"

"Unawaza familia tu wala uwazi kuhusu mwili wangu, unataka nizeeke au ? Muda bado kwakweli, Don hii kila siku narudia siko tayali kuwa mama please "

nilijibu kwa dharau na kuinuka na kwenda kwenye chumba cha wageni kulala.

ITAENDELEA......

LORAH (A slay queen) 🧚🏻‍♀️

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 02

ANZA NAYO.......

Nililala kwenye chumba cha wageni nikiwa sina wasiwasi ata kidogo, kwanza sikuwaza wala kufikilia kwamba nilikuwa nakosea.

Kwa wakati huo nilijali sana muonekano wangu kuliko kitu kingine, suala la mimi kuzaa lilikuwa gumu sana na yote ni kwasababu nilitaka tu kuendelea kuwa Kigoli na niliamini kuwa nikizaa nitazeeka na kupoteza mvuto.

Asubuhi na mapema niliamka zangu na kuingia live, na kuanza kuongea na watu wangu, nyie me napemdwa bhana, yaani ni asubuhi lakini nimeingia live watu kama wote kila mtu ananiangalia mimi.

Nikiwa bize na live yangu, mume wangu alikuja na kukaa pembeni yangu, hapo nilichukua simu na kugeuzia upande wake ili mashabiki wamuone lakini aliinuka chapu na kutoka nje.

"Lorah naitaji tuongee " alizungumza mume wangu akiwa amesimama nje ya mlango.

"Ouk baby I am coming "

nilijibu kwa sauti ya mahaba kabisa, baada ya kumjibu niligeukia simu yangu na kusema.

"Hellow bebes, nawapenda sana ila mume kanipenda zaidi ananiitaji kwa wakati huu so, nitawaona baadae vipenzi vyangu love you ".

Nilimaliza live yangu nikiwa na hasira sana maana Don ndio ameniharibia, kwa upande wangu mimi ni mwanamke ambaye, mbele za watu niliigiza kuwa responsible sana, lakini ukijakurudi kwenye ukweli nilikuwa mwanamke wa hivyo sana.

"Ni nini asubuhi yote hii ??" Nilimuuliza Don kwa hasira sana baada ya kutoka nje.

"Lorah usianze please, ndio kwanza ni asubuhi sawa, sijakuita kwaajili ya kugombana so please over please naomba usitake kuharibu siku yangu mapema"

"Haya niambie umeniitia nini ? "

"Naitaji kutoka saa hizi kuna project naitaji kwenda kufanya, naomba uniandalie kifungua kinywa haraka while mimi nikiwa najiandaa"

"Sijakuelewa" nilimwambia.

"Nimesema hivi, Lorah mke wangu, niandalie kifungua kinywa naitaji kunywa chai ndio niondoke "

"Don, you can't be serious, yaani niingie jikoni saa hizi ??"

"Lorah nachelewa please, naomba niandalie kifungua kinywa, unajua kabisa mimi sio mtu wa kula nje uko sijui migahawa na nini, na sioni sababu ya mimi kula nje ikiwa My darling wife yuko hapa na anaweza kuniandalia kifungua kinywa"

"Nafikili juzi ukuwa umenielewa, nilikuambia kabisa, utafute mdada wa kazi ambaye atakuwa anafanya hizi kazi, mimi siwezi kuingia jikoni nikachoma mwili wangu, na kuharibu kucha zangu "

"Lorah, lorah "

"Bwana weeh lorah jina langu, tafuta mdada wa kazi nitakuwa namlipa lakini mambo ya kunifanyisha mikazi no way siwezi kufanya "

Nilijibu na kurudi chumbani kwetu ambapo tulikuwa tunalala mimi na mume wangu.

Nilishika simu yangu na kumpigia simu shoga angu na kuanza kumpa umbea, naweza kusema kuwa, nilikuwa mwanamke mjinga sana, yaani kila kitu kilichokuwa kikitokea ndani ya familia yangu nilikuwa nikimuadithia shoga angu.

Don aliingia chumbani na kujiandaa akiwa na hasira sana akaondoka zake, kwa upande wangu niliona ni kawaida kabisa na ndio alinipa nafasi ya mimi kuendelea na mishe zangu.

******

Siku ziliendelea kwenda uku maisha yangu na mume wangu yakiwa ni ya kugombana tu, machoni mwa watu tulionekana ni watu wenye Amani sana lakini ukija ndani ni moto wa kuotea mbali.

Ikiwa ni siku ya jumamosi, nikiwa zangu nyumbani, bize kabisa na simu yangu, wifi yangu aliwasili akiwa na msichana ambaye ukimuangalia tu unajua kuwa ametoka kwenye mazingira duni.

"Karibuni "

niliwakaribisha kwa bashasha la hali ya juu.

Ila mimi jamani, nilikuwa mzuri sana kwenye kufich

Nilipiga story na wifi yangu pale, lakini kwakuwa aliitaji kula, niliamua kudanganya kuwa jiko letu limepigwa shoti hivyo nikaagiza chakula kutoka nje.

"Kaka naona anachelewa kurudi "

alizungumza wifi yangu ambaye alikuwa amekaa kwa muda mrefu akimsubili kaka ake.

"Yah nafikili kutakuwa na jam njiani au kazi zimembana sana uko alikoenda " nilijibu kama mke kweli.

"Anyway, huyu ni mdada wenu wa kazi maana kaka alisema kuwa mnaitaji mdada so nimemleta, huyu anaitwa Belle nimemtoa uki kujijijini kwa kina mama " alizungumza wifi yangu.

"Oooh Asante sana, Belle karibu sana nyumbani, jisikie huru kipenzi sawa mama "

nilijibu kwa kumchangamkia sana.

Kwa wakati huo nilifurahi sana niliona sasa ni muda wa mimi na mume wangu kuinjoy maisha pasi na kuwa na mawazo ya kazi za hapa na pale.

Majila ya saa 3 usiku mume wangu alirudi na kwa shangwe nilimpokea.

Mume wangu ni mtu ambaye anapenda sana Amani, hivyo furaha yangu ilimfanya afurahi zaidi.

Kwa siku hiyo nilimpa mume wangu style zote na ukizingatia sikuwa kwenye siku za hatari hivyo sikuwa na mawazo ata kidogo.

"Nimefurahi sana kwa kuniletea dada wa kazi " nilimwambia mume wangu baada ya kumaliza mechi yetu.

"Ahaha cha uvivu, nilijua kuwa utafurahi na furaha yako ndio furaha yangu enjoy babe"

"Ahaahah sa mbona kuniita cha uvivu jamani ??"

"Kwani uongo, bhana mke wangu wewe, kazi za kuingiza pesa ndio unafanya kwa moyo wote, ila hizi za nyumbani "

"Aaah kweli babe wangu unanijua kiundani mpaka unanifanya naona aibu 😁"

Siku hiyo walahi mimi na my wangu tulipiga story tukiwa na furaha sana kuliko siku zote.

*****

Asubuhi na mapema niliamka na kukuta kila kitu kimefanyika, mume wangu alikuwa zake sebuleni akiendelea na kazi zake za ofisini na dada wa kazi aliendelea na majukumu yake.

Nilisogelea meza ya chakula kwaajili ya kupata kifungua kinywa.

"Belle "

nilimuita dada wa kazi kwa sauti ya juu sana ambayo ilimshtua sana mume wangu.

"Abeeeh dada "

alijibu dada wa kazi na kuja chapu.

"Naitaji sosage na sio mayai naomba kaniandalie haraka "

"Sawa dada "

alijibu mdada wa watu kwa upole sana.

"Na ufanye haraka "

Nikiwa naendelea kusubili sosage zangu, simu yangu iliita na niliweza kupokea taarifa ya kuwa baba yangu ni mgonjwa sana na anaitaji kupelekwa hospital.


Don ni mtu ambaye anajali sana, baada ya kupokea taarifa ya ugonjwa wa baba angu, aliacha kazi zake na sote tukajiandaa kwaajili ya kwenda nyumbani ili kumuwaisha baba hospital.

Tukiwa njiani, niliweza kupigiwa simu ya kazi na ilikuwa ni dili kubwa sana ya pesa hivyo sikuona sababu ya kwenda nyumbani na kuacha pesa ndefu inipite.

"Don nafikili wewe uwende nyumbani then utaniambia nini kinaendelea, siwezi kuacha ili dili kwakweli "

"Lorah are you serious 😳, yaani unaacha kwenda kumsaidia baba ako kwaajili ya pesa ??"

"Aaah usifananishe pesa na vitu vya ajabu, nafikili ungeita huba na uwende me naitaji kutumia ili gari"

Maneno yangu yalimuacha don wangu mdomo wazi kwakweli, yaani sikuonesha kujali wala kuogopa, zaidi nilimshusha kwenye gari na kisha nikaenda kwenye kishe zangu mie.

Ebu niambieni lorah mimi nimekosea au laah.

ITAENDELEA.....
LORAH (A slay queen) 🧚🏻‍♀️

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 03
ANZA NAYO.......

Kwa upande wangu nilifika eneo la kazi, na ilikuwa ni kazi ya kushoot video, na pesa ilikuwa ndefu sana, ukiachana na pesa msanii alikuwa ni maarufu sana na muda mwingi nimekuwa nikiwazia sana kuhusu kufanya nae kazi na Mungu aliweza kujibu maombi yangu.

Kwa upande wa mume wangu, aliita usafiri wa huba na kwenda nyumbani kwetu, kwakweli hali ya baba yangu ilikuwa mbaya sana, wadogo zangu na mama walikuwa wakilia tu kutokana na wasiwasi mkubwa ambao walikuwa nao.

"Lorah yuko wapi ??"

Mama alimuuliza Don baada ya kumuona amefika nyumbani peke yake.

"Aaaah, aaah "

Don alijikuta akipata kigugumizi kabisa na kushindwa kujibu swali la mama ambapo mama akaamua kuuliza tena.

"Lorah yuko wapi mbona umekuja mwenyewe ??"

"Lorah hayuko sawa kiafya, week nzima hii anaumwa yupo tu kitandani anaendelea na dozi "

mume wangu aliamua tu kudanganya ikiwa kama ni sahemu ya kunitetea.

Kwa pamoja Don na famili yangu walimchukua baba na kumuwaishah hospital.

Walifika hospital na kupokelewa na baba akaanza kupatiwa matibabu, kwa jinsi ambavyo Don alikuwa akiangaika uku na uku kwaajili ya baba yangu unaweza ukasema kuwa yeye ndiye mtoto wao halali.

Kwa upande wangu kazi ya kushoot ilikuwa nzito sana, hii wanaweza kuelewa wale watu ambao, wanafanga yazi ya video queen au video king.

Kwakuwa kazi ilikuwa ndefu sana, tulifanya mpaka usiku lakini pia hatukuweza kumaliza, mume wangu alikuwa akinipigia simu mfululizo lakini sikupokea ata moja niliofia kuwa atanifokea Sana, lakini kwa upande mwingine niliona kama ni usumbufu na kuamua kuzima simu kabisa.

Kwa siku hiyo niliweza kulala nje ya nyumba yangu pasi na kutoa taarifa, niseme kuwa nilipata mwanaume na nusu, mume wangu alisimama vizuri sana na familia yangu na kuweka mazingira vizuri ili wasijue kama mimi nilienda kwenye mishe zangu.

Don hakuishia hapo tu, baada ya kuona kuwa anipati kwenye simu alienda kwa rafiki yangu na kuniulizia lakini pia akakuta patupu kwani pia sikuwa nimemwambia rafiki yangu mahali nilipo.

******

Hatimaye siku nyingine ilishika nafasi na kuwapa wapambanaji nafasi ya kupambana, kwa upande wangu niliingia tena kwenye kazi ya kushoot, walahi kazi Bado ilikuwa ndefu lakini nashukuru Mungu majila ya saa 10 jioni tuliweza kumaliza.

"Tajiri, ubarikiwe sana, mzigo nimepata naomba niwaache sasa " nilimwambia boss wangu pale tu aliponilipa.

"Oooh sawa Lorah Asante pia kwa Muda wako, Asante kwa kila kitu nafikili tutaendelea na kufanya kazi zaidi na zaidi "

"Tajiri hauna baya " nikaanza kumpamba pale.

Baada ya kila kitu nilipanda gari na kuanza safari ya kurudi nyumbani, nikiwa njiani niliwasha simu, kitendo cha kuwasha tu simu yangu iliita na mpigaji alikuwa ni Don.

"Eeeh huyu nae jamani khaaah " niling'aka kwa hasira.

Niliiangalia simu ile kwa muda kisha nikapokea.

"Yes Baby "

"Lorah uko wapi ??" Don aliniuliza.

"Niko njiani narudi nyumbani, uko wapi ??"

"Unaenda nyumbani sio ?, Lorah sina muda wa kugombana na wewe saa hizi, fanya hivi, hakikisha unavaa mavazi ya heshima na uje nyumbani kwenu sasa hivi "

"Kwamba sivaagi mavazi ya heshima au ? Don unashida gani wewe ? Muda wote unanionaga mimi kuwa na makosa tu, ata hivyo mavazi yangu yanashida gani ? Nitavaa ninavyojisikia, as long as nipo comfortable "

nilifoka na kukata simu.

Don aliamua kupiga tena lakini sikupokea kabisa, akapiga na kupiga lakini zote nilibaki nikiziangalia tu.

Niliona Don ananisumbua tu, nikashika simu na kumpigia shoga angu ili tu nisiweze kuongea na Don, lakini pia kila Don atakapopiga aambiwe naongea na mtu mwingine.

Ila shoga angu ni kama alikuwa askisubili mimi nimpigie hivi, kitendo cha mimi kumpigia simu akapokea muda huo huo yaani.

"Mmmmh shost shost , mbona umepokea chapu ujataka ata kasimu kaite kidogo "

niliongea nikiwa na bashasha la hali ya juu, shoga angu akaachia kicheko kisha akajibu.

"Eeh mtu mkubwa wewe ujue, yaani nilivyoona simu yako tu kamoyo kakafanya paaah boss kubwa anapiga simu, nilichofanya ni kupokea tu"

Walahi rafiki yangu huyu sawa ako na pesa lakini anapenda sana kunipaisha mimi aswa aswaah likija jambo la pesa.

Na kwa upande wangu kwakweli, nilikuwa nikipenda sana sifa na kwa namna moja au nyingine shoga angu alijua kuniteka kwa njia ya kunipasha joto juani 😂🙌🏿.

"Anyway kipenzi, kama Tajiri ndio kwanza nimefika nyumbani naitaji kupumzika, nikiamka tutaongea mambo ya vocation niko na pesa chafu dyadyaaa 💃" nilizungumza kwa kujishauwa sana.

Nilikata simu na kupiga honi, baada ya dakika chache nilifunguliwa geti, na kuingia ndani.

Kiukweli nilikuwa na uchovu wa kutosha kutokana na kazi ambayo nimefanya uko nilikitoka, akili ikawa inaniambia nilale lakini moyo unaniambia nenda nyumbani kwenu kama ambavyo mume wako amekuita.

Baada ya kuwaza na kuwazua kwa muda mfupi niliamua tu kujiandaa kwajili ya kwenda nyumbani kwetu.

Ila mimi napenda sana kuudhi watu jamani, yaani mume wangu ameniambia nivae vazi la heshima, lakini mimi nikaenda kuvaa vazi ambalo kwa wakaka wa mjini lazima wakiniona waseme kuwa wanakula kwa macho.

Nilivaa vazi ambalo, naweza nikasema ni nusu utupu, ngoja niwaambie vazi langu likoje, juu nilivaa, top ambavyo ilionesha kitovu, na sio kitovu tu kwani sehemu ya mgongo pia ilikuwa wazi.

Ukija chini nilivaa sket fupi ya kubana, lakini pia ikawa na mpasuo mrefu sana, sikuishia hapo nikabadili na wigi kabisa na kujipaka ka make up pambe.

"Don umeoa mdada wa mjini so lazima nishine baby"

nilizungumza kwa sauti uku nikijishaua kwenye kioo.

Nilitoka nje na kwenda kuonana na Belle, kabla sijaondoka.

"Belle, natoka nitarudi baadae na kaka, nakuomba ufue nguo chafu za chumbani kwangu zote, nisije nikakuta nguo chafu nikija kurudi "

Nilizungumza na sikuwa na sababu ya kusubili jibu tajiri ndio nishaongea, nilishika njia na kuondoka zangu.

Safari ya kwenda nyumbani kwetu ilianza, muda wote huo Don hakuacha kupiga simu lakini pia kunitumia jumbe, jumbe zake zilisisitiza sana kuhusu mimi kuvaa vizuri lakini Mimi ndio kwanza nilikuwa naona kama nachelewa hivi kwenda kumkela mtoto wa mama mkwe.

MUNGU mkubwa, nikafanikiwa kifika nyumbani, jambo zuri ni kwamba niliweza kumkuta mume wangu nje akizunguka uku na uku, lakini pia kulikuwa na watu kadhaa wakizunguka nao, na siku hiyo geti kubwa la nyumbani kwetu lilikuwa wazi.

Baada ya mimi kupaki gari, Don alikuja chapu na kuangalia ni mavazi ya aina gani nimevaa.

"Uwezi kunisikiliza ata kidogo si ndio ??"

Don aliniuliza baada ya kuona nimevaa mavazi ambayo hakutaka kabisa nivae.

"Aah we nawe, kwanza kuna nini mbona geti wazi kama hivyo, watu wanaingia ingia kuna nini ??"

"Lorah uwezi kushuka kwenye gari ukiwa na mavazi kama hayo "

"Nitokee hapa nakuuliza unijibu "

Nilijikuta nikimfokea Don kwa sauti ya juu sana na kuwashtua watu wa pembeni, lakini pia nilifungua mlango na kushuka nikiwa na nguo zangu za hovyo nikaongoza njia kuingia ndani.

Baada ya kuvuka geti niliweza kukutana na makundi makundi ya akina mama na akina baba, walahi sijawai kuona aibu lakini siku hiyo niliona aibu.

Kila mtu aliniangalia kwa jicho lake na kwa namna moja au nyingine niliamini kuwa walinisema vibaya.

Mmoja lati ya wamama akainuka na kuja kunistili kwa tenge kisha akaniambia

"pole sana binti "

Neno pole lilinishtua sana nikamuangalia yule mama mara mbili mbili, kabla sijamuuliza swali lolote, Don alikuja na kunishika vizuri kabisa na kuniingiza ndani.

Niliingia sebuleni na kukuta familia yangu ikiwa imekaa kiuzuni sana, mama angu alikuwa ameiva uso anapumua juu juu, aliponiona tu akapaza sauti yake na kusema.

"Lorah baba hayupo tena jamani' Mume wangu mie"

Nilishtuka sana na kujikuta nikianza kutetemeka kwa wasiwasi, katika maisha yangu yote sikuwai kufiwa na mtu wangu wa karibu hivyo, nilijikuta nikiumia sana.

Kwa sauti ya kilio na majonzi, nikapiga ukunga kwa kuitilia jina la baba yangu mwisho nikamsogelea mama angu na kumkumbatia.

ITAENDELEA


LORAH (A slay queen) 🧚🏻‍♀️

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 04

www.tupohapa.com

SONGA NAYO…………

Nililia sana siku hiyo, ila mama yangu na ndugu zangu ndio walilia zaidi, baada ya kulia na kutulia, nilitoka nje na kuanza kumtafuta mume wangu yaani Don na nilipomuona tu nikamwambia.

"Naomba tuongee "

Don aliachana na wanaume wenzie na kuja kunisikiliza.

"Hivi Don ulishindwa kuniambia kuwa nimepoteza baba ? Ulipanga nidhalilike kwenye msiba wa baba yangu si ndio ??"

"Lorah, usianze mama sawa ? Ulitaka nikuambie ili upate ajali barabarani kwaajili ya kupaniki au ?"

"Aliyekuwambia nani kwamba nitapaniki ? Kufa kupo na kila mtu atakufa Don sawa ? Ata wewe unaweza ukafa, kiukweli sijapenda, yaani nimezalilika sana leo, nimekuja kwenye msiba wa baba yangu nikiwa mtupu kabisa"

"Na hiyo ndio maana halisi ya asiyesikia la mkuu uvunjika guu, nilikuambia vaa mvazi ya heshima ukaamua kunipuuzia me kosa langu ni nini hapo ??"

"Nitokee hapa "

Niliamua tu kuondoka na kumuacha Don akiwa ananishangaa tu, moja kwa moja nikaenda kwenye gari yangu na kukaa kwa muda.

Nilitumia muda huo kuposti na kuwajuza watu kuwa nimepata msiba, kwakuwa nilikuwa mtu maarufu sana kwa wakati huo niliweza kupata muitikio wa hali ya juu.

Mpaka giza linaingia, watu walijaa sana kwenye msiba huo, sio watu tu wa mchezo mchezo ni watu wa Zito yaani mpaka msanii mkubwa kabisa ambaye nimetoka kushut nae alikuja.

Ila umaarufu raha sana, watu walijua kunikimbilia jamani, ukiachana na kunikimbilia, nilipokea kila aina ya michango, yaani simu yangu ilipokea miamala tu.

******

Hatimaye siku nyingine ilishika nafasi na ndio ilikuwa ni siku ya mazishi ya baba yangu, sawa mimi niliumia sana lakini naomba nikili kuwa kuna muda nilikuwa nikilia kwa kuigiza.

Kuna muda nilikuwa naona kama Yale macamera ayanichukui vizuri hivi, hivyo nilijikuta nikifanya kila aina ya drama ili tu nionekane na watu wanionee huruma.

Don ni mwanaume na nusu jamani, alijua kusimama na mimi, alihakikisha kuwa kila kona anakuwa na Mimi, Don hakuweza kuruhusu wanaume wengine wanisaidie pale ninapolia ikiwa yeye yupo.

Mungu alisaidia na tukaweza kumpumzisha baba angu kwenye nyumba ya milele, kama ilivyo kawaida kwenye misiba, baada ya mazishi lazima familia na ndugu wake vikao kidogo na kuweka mambo sawa.

Kwa upande wangu akili ilikuwa inawaza kwenda nyumbani kwangu, naweza nikasema kuwa maisha ya ustar niliyatumia vibaya sana, yaani ustaa niliuchukulia kwa namna nyingine kabisa.

Marafiki na majilani walitawanyika na nyumba nzima tukabaki sisi wahusika na ndugu wengine.

Kwakuwa Don alitakiwa kuwasili kazini siku iliyofuata, hivyo hakuweza kabisa kusibili, kwa utulivu wa hali ya juu akamsogelea mama na kuanza kumuaga.

"Aaah mama, nafikili tutaonana kesho jioni, saa hizi nalejea nyumbani kwangu then kesho nitakuja jioni"

"Mwanangu, we nenda ukapumzike baba, Mungu akubariki sana sana, yaani mkwe nimepata kwakweli, kapumzike baba, na uwe na majukumu mema "

alijibu mama yangu kwa unyenyekevu wa hali ya juu.

Baada ya Don kumuaga kila mtu alinishika mkono na kwa pamoja tukatoka nje.

"Mbona kama nimekuona unaaga watu unaenda wapi ??"

Nilimuuza Don.

"Naenda nyumbani si tulishaongea jamani mke wangu "

alijibu Don uku akishika shika mashavu yangu ambayo yalijazia kiasi.

"Yaani unaondoka halafu mimi unaniacha hapa ?, ata hivyo kila kitu kimeisha nisubili nichukue pochi tuondoke "


Ila mimi ni kama sio mfiwa hivi, yaani sina sifa ya kuwa mtoto wa marehemu Ata kidogo, imagine naitaji kuondoka na mume wangu kisa tu yeye anaondoka.

"Acha kuigiza kama mtoto mdogo lorah sawa ?, me siondoki hapa kwakuwa napenda, naondoka kwaajili ya majukumu yangu tu, lakini pia kesho jioni baada ya kazi nitarudi "

Nilifanya kila aina ya ubishi lakini sikufua dafu zaidi nilibakizwa pale pale nikiwa nimechukia Sana.

Ndugu wote wakiwa sebuleni, mimi nilikuwa zangu chumbani nikipeluzi tu mtandani, wadogo zangu wakiwa wanaendelea na kuomboleza msiba wa baba, kwangu ilikuwa tofauti kabisa kana kwamba nilikuwa nimeshasahau kila kitu.

Nikiwa zangu bize naperuzi uku na uku, gafla akaingia mdogo wangu anayenifatia na kuniuliza.

"Dada tunaweza kuongea ??"

Niliimuangalia kwa muda kisha nikajibu.

"Acha kunizeesha niite lorah inatosha, kwani mpaka kila mtu ajue kuwa mimi ni dada ako "

"Oooh samahani lorah tunaweza tukaongea ??"

"Zungumza nakusikiliza"

"Hivi kwanini ukutaka kuja kumuona baba alipokuwa akiumwa ??"

Ila mimi jamani, dharau ya pesa, umaarufu na uzuri vilijua kunibeba jamani, niljikuta nikipata hasira na kuinuka pale kitandani na kuanza kumtimua mdogo wangu aweze kutoka nje.

"Toka nje "

"Lorah usisahau kuwa chumba hiki ni chumba changu, yaani ni chumba ambacho nalala mimi na mdogo wangu "

"Nitolee mdomo wako hapa, yaani kidomo juu juu Kama Bata vile, eti usisahau kuwa hiki chumba ni ngungu, sawa chumba chako, vipi kuhusu nyumba ? Bila mimi kuwanunulia hii nyumba ungekuwa unasema kuwa unachumba wewe ??"

"Lorah wewe sio dada angu ambaye nimekuzoea umebadilika mno, unajua baba kabla hali yake haijawa mbaya aliniambia nini ?"

"Sina haja ya kujua, we kunguni mdogo toka nje "

Mdogo wangu jamani ni jeuri hatari, akiamua jambo lake lazima litimie hivyo aligoma kabisa kutoka nje.

Nilijikuta nikipata hasira sana, kuna muda nilitamani ata kumuwasha mabao Lakini nilishindwa kabisa kutokana na watu kuwa wengi.

Kwakuwa yeye aligoma kutoka, niliamua mimi kutoka tu, nilinyanyua simu yangu na kutoka nje.

******

Siku nne zilipita nikiwa nyumbani kwetu, ndugu na jamaa wankaribu waliondoka na kutuacha wenyewe pale nyumbani.

"Nafikili me kesho nitaondoka kwangu sasa "

nilizungumza nikiwa nimekaa mimi na wadogo zangu lakini pia na mama.

Mama aliniangalia Kisha kwa sauti ua upole akaniambia.

"Nafikili unatakiwa kumaliza Ata week moja hapa nyumbani, lorah siko sawa ata kidogo, kuna muda nahisi kama na mimi sitaishi sana "

"Aaah mama nawe jamani " alidakia mdogo wangu, Shine.

"Nasema ukweli, Lorah mama endelea kukaa na sisi kwanza, na kama Don anakuzuia basi mama yako nipo tayali kuzungumza nae"

Niliamua kukubali kishingo upande tu maana mama nae aking'ang'ania kitu basi aachi.

Majila ya usiku, nilitoka nje ya nyumba na kwenda kuonana na rafiki yangu ambaye nilimuita kwaajili ya mazungumzo mfupi.

"Lorah umenitisha sana usiku huu shida nini ??"

"Hakuna kitu kikubwa Wala nini, Yaani najikuta niko bored nataka niende kwangu lakini bi mkubwa Ana kaza sana aiseeeh “


Kwanza Rafiki yangu aliniangalia sana kisha Akatabasamu na kusikitika muda huo huo kisha akamuuliza.

“Sasa hivi unanyonyesha ?”

Nikacheka na kujibu.

“Kuzaa tu sitaki unaongelea habari za kunyonyesha, unajua nini Mimi ata Don tu sijawai kumruhusu aacheze na kifua changu ziwa lisije likaanza kubembea bure “

Rafiki Alishangaa sana na kunitumbulia macho kisha akaniuliza.

“Hii ndoa ulikazimishwa au uliitaka Mwenyewe ?”

“Nimeitaka Mwenyewe, lakini uzuri wa Don ndio ulinichannganya, lakini pia nilifikili Don Anapesa sana lakini Nimekuja kugundua Kuwa nampita Don kipato “

“Sawa umempita kipato lakini kumchukua Kuwa Don hajawai kukuruhusu ununue ata kibiriti kWa Pesa yako, dön amehakikisha Kuwa kila kitu chako muhimu unapata kWa wakati, tazama alivyosimama na wewe kwenye msiba wa baba yako “

“Mmmmh shoga yangu Mbona Leo unazungumza Kama Malaika wa amani, hii vibe yako sijaizoea “

Nilizungumza na Kuangua kicheko.

“Lorah, Mimi na wewe ni marafiki wa kubwa sana, ni marafiki ambao tumejuana ukubwani lakini pia tunapendana sana, mimi nawewe sote tupo kwaajili ya kujenga na sio kubomoa, unajua Jana usiku Don alikuja Nyumbani kwangu “

Weeeeeh nilishtuka na kWa jazba nikamuuliza.

“Alikuja kufanya nini ??”

“Aaah relax dada amekuja kuzungumza na Mimi akitaka kuweka mambo Sawa na wewe, lorah, Don anakupenda sana, Yaani katika wanaume wanaokupenda ukiachana na baba yako Don anafuatia, Don amenisimulia kila kitu, ingawa kila kitu Nakijua nikafanya Kuwa Sijui, hivi lorah hivyo vituko vyako unavyomfanyia Don kumbe ni kweli ? Me ulivyokuwa unanisimulia nilijua ni utani tu, lakini nimeamini baada ya Don kunisimulia vyote ambavyo unaniambia, lorah unakosea sana Rafiki yangu, makosa unayoyafanya sio madogo jirekebishe “

Nilimuangalia Rafiki yangu kwa hasira mwisho nikamwambia.

“Nilizani Nina Rafiki kumbe manafiki mmoja tu”

Nikashuka kwenye gari ya Rafiki yangu Koku kWa hasira sana na kuingia Ndani kwetu na kumuacha koku akinishangaa tu.

Walahi nilijikuta nikipata hasira sana, niliingia Ndani nikachukua pochi yangu na kuondoka pasi na kuaga.

Nilifika Nyumbani kwangu na kumkuta mume wangu Don akiwa na amekaa mezani na Belle na ni Kama walikuwa wakisoma kWa pamoja.

“Ooooh babe “


Don aliniita baada ya kuniona na kwa furaha akanyanyuka na kutaka kunikumbatia lakini aliponifikia tu, nikamchapa kibao kimoja Matata sana.

Dok aka……..

SWALI KWAKO MSOMAJI, UNAWEZA KUMCHAPA KIBAO MUME WAKO ?? WELA MAONI YAKO….
LORAH (A slay Queen) 🧚‍♀️🧚

SEHEMU YA: 05

MTUNZI: PATRICIA DAMAS

www.tupohapa.com

SONGA NAYO……

Wooiiiiiiih Yaani Mimi nilimpiga mume wangu kibao Tena mbele ya mfanyakazi wetu wa Ndani, Dön aliniangalia uku akiwa amshikilia shavu lake, na kwa sauti ya utulivu akaniuliza.

“Hii ni nini ??”

Nilimuangalia kwanza kWa hasira sana kisha nikamgeukia Belle na kumfokea.

“Na wewe unasubili nini hapa toka ukooo “

“Belle endelea na kazi yako nakuja “
Don akanishika mkono kwa nguvu sana na kunivuta mpaka chumbani, tulipofika tu akaniuliza.

“Ni nini umefanya ? Kwanza Kwanini umanipiga??”

“Na ukitaka nitakupiga Tena Don Sawa, hivi wewe Una akili gani wewe eeeh , Yaani mwanaume mzima unatoka hapa unaenda kutoa Siri za Ndani kWa watu wengine we una akili au Chizi ? Koku ameniambia kila kitu “

Ila Mimi daaaah Pesa zinaniadaa sana , Yaani kwakuwa kafanya mume wangu ndio naona Kuwa amekosea wakati Mimi kila
Siku natoa Siri za Ndani na kwenda kumsimulia huyo koku na sio kwamba namsimulia kWa kutaka Masada hapana namsimulia ili kumuonesha Kuwa Mimi ndio kinara kwenye familia.

“Are you serious right now??”

Don aliniuliza akiwaamini kabisa.

“Usiniulize maswali ya kipuuzi, kulikuwa na haja gani ya wewe kwenda kumsimulia koku mambo yetu, unataka Mimi nionekanaje ??”


“Loran serious umenyanyua mkono wako na kunipiga Mimi ??”

“Na nitakupiga Tena Kama hautapata akili, hivi kwanza Don uoni aibu, umu Ndani Nani Ana Pesa zaidi yangu? Uoni aibu kupitwa Kipato na mwanamke ??”


Ila hizi Pesa jamani zilikuwa zikiniendesha vibaya sana Walahi, 🥹 Yaani Pesa zinanifanya nishidwe kuona ni kiasi gani napendwa na huyu mikaka, Yaani hapa Angekuwa kaka mwingine Saa hizi ningepigwa kipigo ambacho ningeshindwa ata kutembea.

Don aliniangalia kisha akaniuliza.

“Kwahiyo nimefanya kosa mimi kwenda kutafuta furaha ya ndoa yetu ??”

“Acha kupiga soga Bwana, ukitaka Kuwa na furaha umu Ndani, kwanza kabisa hakikisha Kuwa unanipita Kipato na sio Mimi nikupite, hakikisha Kuwa unipigii Kelele za kupata Mtoto Sijui kitu gani, eeeh nilitaka kusahau, Kuanzia sasa kila mtu atalala chumba chake, Sina hisia zozote zile juu yako lakin pia nimechoka kusikia ili jasho lako la kimasikini”

My zangu kiburi changu kiliongezeka baada ya kaka msanii, Yaani msanii mkubwa ambaye nimetoka kufanya nae kazi kuniambia Kuwa ananipenda sana lakini pia anaitaji Kuwa na Mimi, Yaani kwa njia yoyote ile mimi ni wake.

Don aliishia kuniangalia, kWa uchovu na maumivu ya hali ya juu akasogea kitandani na kutaka kukaa nikamfokea.

“Utaenda kulala kwenye kile chumba cha wegeni, cha chini, Kuanzia sasa iki chumba ni changu “

“Lorah wewe ni Chizi au ??”

“Hapa Chizi ni wewe ambaye usikii, nimesema sitaki kulala na wewe Sawa “

Don aliniangalia kisha aakatabasamu na kuniambia.

“Ukinipigia Kelele Tena au kunigusa nakuhakikishia Kuwa Mimi na wewe tunagawana majengo ya serikali”

Eeeeh hapo kwanza niliogopa maana Don Alizungumza akiwa serious sana ni Kama alikuwa akimaanisha anachokiongea.

“Haya baki wewe ufurahi na roho yako “

Nilizungumza na kutaka kutoka nje lakini Don akaniambia.

“Ukitoka nje ya huo mlango, utataja Majila yangu matatu ya utotoni”

Eeeeh huyu nae nini sasa Mbona Kama ananitisha sasa.

Nilichukia sana, nikarudi nyuma nikachukua mto na Shuka na kujifanya Kuwa nalala chini, Don aliishia kuniangalia tu mwisho akageukia upande wa pili na kuanza kuutafuta usingizi.

Nyieeeh kulala chini ninkipaji, Yaani nusu Saa tu niliona Kuwa kila kitu kinaniuma mwilini, kWa mwendo wa pole pole na kunyata, nikasogea kitandani nikapanda na kulala.

****

Asubuhi na mapema niliamka na sikumkuta mume wangu kitandani, kwakweli sikujali ata kidogo zaidi nikaingia live na kuanza kuwaonesha watu morning routine yangu uku nikiwadanganya sana.

“So guys, nimeshamalizana na usafi wa chumbani, nikawa Cheka baadae naenda kumuandalia mume wangu kifungua kinywa na nguo zake za kazini byeee. “

Niliwaaga fans wangu na kuondoka nje.

Nilitoka na kumkuta belle akiweka kifungua kinywa mezani.

“Kaka yuko wapi ??”

Nilimuuliza belle maana sikupma dalili ya Don Kuwepo pale Ndani.

“Aaah kaka ameondoka asubuhi sana ilikuwa ni Saa 12 kasoro “

“Sawa”

Nikarudi zangu chumbani na kujiandaa kwani kuna sehemu nilikuwa nataka kwenda.

Nilijiandaa na kutaka kutoka, nilipofika nje ndio nilichoka kabisa, Picha linaanza nikakuta gari moja tu, Tena ni gari ambayo ni mbovu.

My zangu iko hivi, Mimi na mume wangu tuna magari mawili, gari moja ni la mume wangu ambalo nilimkuta nalo, lakini pia gari ya pili ni ya kwangu ambayo pia mume wangu alinikuta nayo.

Sasa Bwana gari yangu Mimi ni kimeo, Tena sio kimeo cha kawaida Yaani hii gari uwiiiiih ni huzuni, cha kwanza inakula sana mafuta lakini pia inapata moto kWa muda mfupi tu na kuzima yenyewe.

Kwakuwa mume wangu ni mtu ambaye anajali sana akaamua kuniachia gari yake na yeye alikuwa akienda kazini kWa huba, cha ajabu siku hii ya Leo ameondoka na gari yake imagine na Mimi Nina safari yangu ya muhimu sana.

Walahi nilichukia sana Tena sana, nikachukua simu yangu na kumpigia Don lakini pia hakupokea ata simu yangu moja, nilijitaidi kumtumia kila aina ya ujumbe lakini pia hakujibu ata sms moja.

Kwakuwa safari yangu ilikuwa ni muhimu sana, nikaamua tu kubolt gari na kuondoka zangu.

Majila ya usiku Don alirudi na kunikuta Mimi pia nikiwa nimesharudi kwenye majukumu yangu na nilikuwa sebuleni nikiangalia movie.

“Belle umeshindaje ??”

Don alimuuliza Mdada wa kazi.

“Salama kaka shikamoo “

“Marahaba”

Don akajibu na kwenda zake chumbani.

“Inamaana ajaniona au?”

Nilijiuliza kimoyomoyo, mwisho nikanyanyuka na kwenda kumfuta uko uko chumbani maana hii ni dharau sasa.

“Inamaana ukuniona pale sebuleni ??”


Nilimuuliza mume wangu baada ya kufika chumbani.

“Lorah nimechoka snaa Tena sana, kichwa changu akiko saaa so siitaji Kelele “

“Kwahiyo Mimi nakupigia Kelele ??”

Don Wala hakunijibu kitu zaidi akabadili mavazi yake na kutaka kwenda kuoga lakini nilimsimamisha na kumuuliza.

“Kwahiyo umenipokonya gari yako ??”

Don aliniangalia kisha akajibu.

“Lorah wewe ni Tajiri sana, una Pesa zaidi yangu, unaingiza Pesa Ndefu sana, kiufupi ile gari sio hadhi yako kabisa, so boss lady Sijui Don dada, fanya hivi, nunua gari ya hadhi yako “

Nilimuangalia Don kWa kumpandisha na kumshusha kisha nikatoka nje kWa hasira sana.

Sawa mimi Nina Pesa lakini sasa Pesa zangu azikai ata kidogo 😂🙌, Yaani Pesa yangu Mimi ni Mawigi ya bei, nguo za bei, mapochi, vipodozi, Sijui, viatu, macheni ya dhahabu Basi, na muda huo nilikuwa Nina Pesa lakini ilikuwa ni ya vacation Dubai ambayo nilipanga kwenda na Yule shoga yangu koku.

Nilikuwa na hasira sana mwisho nikafhukua simu yanngu na kumpigia koku, ambaye kWa ya kwanza akachelewa kupokea simu yangu.

“Shoga yangu ulikuwa mbali na simu au ??”

Nilimuuliza koku baada ya yeye kupokea simu yangu.

“Yaaah nilikuwa na kazi kidogo, nambie babe “
Ila koku sio mtu wa kuweka mambo moyoni ata kidogo, ata kama nilimkwaza lakini Wala ajanikasilikia.

Tuliongea kiasi kisha tukaagana.

******

Siku Tatu zilipita uku Mimi na Don tukiishi Kama maadui hivi, Yaani Mimi na Don tuliishi chumba kimoja lakini ata salamı atupeani.

Siku moja ikiwa ni Majila ya asubuhi sana, son aliamka najiandaa na wakati Anavaa akazungumza.

“Nasafiri kikazi naenda Arusha, nitakuwa uko kwa week moja tu then nitarudi, Lorah najua hatuko Sawa lakini Kaa ukijua Kuwa nakupenda sana Tena sana, nilirudi tutazungumza kiundani zaidi”


“Sawa”

Nilimjibu kWa kiufupi kabisa kisha nikaendelea kuchezea simu yangu.

Dön akamaliza kujiandaa kisha akanikumbatia na kuondoka.

Majila ya mchana, niliweza kupokea ugeni ambao ni kaka msanii, Yaani Yule msanii ambaye nimeingia nae kwenye mahusiano, siku hiyo nikaingia jikoni na kumpikia kaka msanii utazani yeye ndio mume wangu.

Nilimpikia kisha akala na tukabaki tukiangalia movie.

“Belle “

Nilimuita dada wa kazi.

“Unachoka kujifungia Ndani ? “

Nilimuuliza belle.

“Sina pa kwenda dada “

“Sawa Leo kuna mnada kule Mtaa wa chini, so Pesa hii hapa utanınca vitu ambavyo vimeisha umu Ndani lakini pia na vitu vyako Kama nguo na chochote unachotaka.

Siku hii nilikuwa Mpole sana ata Belle alinishangaa sana, mwisho belle akachukua Pesa na kuondoka.

Aaaah Kiukweli muda huo nilikuwa niko hot sana na niliitaji sana penzi la kaka msanii hivyo nilimtoa belle Kijanja, sikujali Kuwa ni sebuleni nilichojali Kuwa ni Nyumba nzima yuko wenyewe.

Nilimsogelea kaka msanii na pasi na upoteza muda tukaangukia kwenye kiss zito sana.

Kaka msanii ni Kama alikuwa na uchu sana hivi, alinigeuza chap na kunifanya niwe chini na yeye juu, pole pole akaanza kucheza na mwili wangu na hapo ndi akazidi kunichanganya.

Maandalizi yalikamilika na mwisho tukaingia mchezoni, aaah Walahi nilikuwa Niliinjoy sana, si unajua kufanya kitu na mtu umpendae ?.

Tukiwa Tunaendelea na mambo yetu gafla mlango ukafunguliwa na Don akaingia Ndani, Yaani Mume wangu aliingia Ndani……

JE NINI KITATOKEA ? ILI KUPATA KUJUA NINI KILITOKEA BONYEZA HII LİNK www.tupohapa.com
LORAH (A slay Queen) 🧚‍♀️🧚


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote