Follow Channel

MADAM JOY NA MIMBA YA CEO MWANAFUNZI

book cover og

Utangulizi

MADAM JOY NA MIMBA YA CEO MWANAFUNZI
MTUNZI: BABY SMILE
EP 1.

Nilikwambia jamani, hukutaka kunisikia, ogopa sana mwanaume aliyeokoka, wana roho ngumu sana,kama kaweza kuachana na dhambi, wewe ni nani asikuache!🤔...

Madam Roz alikuwa akiniambia, mwenzenu,nimeachika kwa peter mlokole, kosa tu la kubandika kucha miguuni😃, mlokole wa watu akaona akaaaa hanitaki tena, naumia mwenzenu uyu ndo alikuwa mwanaume pekee aluekubali kuwa na mimi bila kumpa tamu, alikubali kusubili hadi ndoa, leo kaniacha nitapata wapi tena😭, na haka ka mwili kangu kakitoto kila mwanaume wamaana ananichukulia mtoto, vijana ambao hawajui ata kama watakuja kuoa ndo wananiona mimi saizi yao😭...

Naitwa madam joyce, ni madam wa shule ya msingi, nina mwaka mmoja sasa toka niajiliwe shule binafsi, kama mwalimu wa darasa la kwanza,shule ilikuwa kubwa sana, mpaka advance pia walikuwa hapa, ilikuwa ni ya kutwa na bweni...

Baada ya kuona, madam Roz, hanipi tumaini lolote wala mbinu, nikaamua kutoka, nikatulize maumivu mahali,nilifika nnje kidogo na shule na kwangu nilipanga jilani kabisa na shule ili kuepuka gharama, kulikuwa kuna msitu lakini sio ile ya kutisha sana, nilijibanza mahali peke yangu, nikaanza kulia na kutafakali...

Nikiwa nalia na kuwaza, ghafra alipita kaka mmoja, mzuli kama jini na nillishtuka nikahisi ni jini, nikasimama nakutaka kukimbia,akanidaka mkono na kuniita madam J, nilikuwa na hofu mno, akasema "samahani madam, unaonekana hauko sawa, nilikuwa pale toka umefika unaweza kusgare na mimi maumivu yako? Kama huwezi pia sio mbaya, lakini siwezi kuluhusu ulie mbele yangu...

Nilimtizama nijagundua kavaa sare ya kushindia ya shuleni kwangu, na ni sare ya wanafunzi wa advance, lakini nikasita nakuhisi sio, kwa sababu huyu alikuwa mkubwa japo sio sana, lakini alionekana kunizidi hata mimi umri, na alikuwa msafi sana, na kavaa kwa heshima mno..

Niliamua kujibu tu, niko sawa nimdudu tu aliniingia machoni, na wewe kwa nini uko nje ya shule, ilihali hamruhusiwi kuwa nje?, unatafuta matatizo ee?
Ajabu hata hakuwa anaogopa akanitizama kavu kavu machoni, ikabidi mimi ndo nishushe macho uku naumia yani mwanafunzi ananionea kisa mimi mdogo mdogo😭...

Nikajikuta machozi yanapita, ajabu yuke kaka akasogea nakunikumbatia huku ananifuta machozi, lakini sauti yake ilikuwa tofauti, sikumfatilia sana nikaamua kujikaza asinichukulie dhaifu, naomba uniachie kuwa na mipaka, aliludi nyuma kisha akatabasamu na kusema " naitwa Jeon William, niko 4m 6 PGM...

"Nakujua kwa sababu wewe ni mtu muhimu sana kwangu, nimekuja huku kwa sababu yako, nilikuona shule asubuhi haukuwa sawa, na najua usipokuwa sawa huwa unakuja huku, ndio maana nikaja, kifupi tu nakupenda madamu, sitaki kuendekea kusubili,muda wangu hapa shuleni sasa ni mdogo, kaa mbali na wanaume wote, kwasababu mmeo nipo hapa, wewe ni wa kwangu liweke hilo akilini....
Kupata full bonyez link hio hapo juu ukasome yote hadi mwisho kwa buku tu...
Itaendelea…💥


MADAM JOY NA MIMBA YA CEO MWANAFUNZI
MTUNZI: BABY SMILE
EP 2.

Nilishangaaa ivi uyu mwanafunzi 🙄, anajisikia anavyoongea jamani🤔, nilinyanyua mkono nikataka kumuwasha kofi, akalidaka nakutabasamu, "J nakupenda mke wangu mzuri, lakini siwezi kukuacha unipige bila kosa, relax najua saivi hujanielewa ila niamini tu, soon utakuja kunielewa, na kama unatatizo linahitaji msaada usisite kuniambia, na kichwani kwako usinichukulie kama mwanafunzi itakusaidia sana kunielewa...

Aliniachia nakupiga hatua kidogo, akaludi tena na kunipiga busu la kushtukiza, nikiwa kwenye mshtuko akaanza kukausha maji yangu, yani alikuwa na ulimi mtamu nyie🫣, nilikuwa sipendi hii kitu, nakuona ni kinyaa nilikuwa nakataa sikuwahi kuluhusu mtu aingize ulimi wake kwangu, ila leo nimeshangaa tu kitu, aisee sikutegemea kana hii kitu kumbe ni tamu hivi...

Nilijikuta natoa ushilikiano mkubwa, kijana alijua kunilegeza, mpaka anakuja kuniachia hata nguvu za kusimama mwenyewe tena sina, alioneka hata yeye hali sio shwali, macho yake yalikuwa yamekegea vibaya mno, alinikumbatia kwa muda kisha akaniketisha chini,akaomba aniludishe kwangu, muda huo tayali ilikuwa ni kigiza kama saa mbili kasoro hivi, nikashtuka anipeleke kwangu🙄, nikaongea kwa aibu, nitaenda mwenyewe, nilivyojibu ivo ata hakunisikiliza....

Alinibeba kwa nguvu mgongoni, nikaanza kusumbua, akanishusha na kuludia zoezi tena, nilikuwa nashindwa hata kuongea, hakunipa kabisa nafasi, alivyoona niko vibaya sana akaniachia nakunibeba mgongoni...

Nilipata hofu, nikiwa mgongoni, nikamsemesha karibu nasikio, naogopa usinifikishe nyumbani wewe ni mwanafunzi, aliganda kwa muda kisha akaendelea na safari,mpaka kwangu, tumefika, nikatoa fungua bahati nzuli nyumba niliyopanga mwenzangu alikuwa kasafili tuko wawili tu nyumba nzima...

Tuliingia ndani halaka, sikuwa nimepika na nilipanga kulala njaa, kwasababu ya maumivu niliyokuwa nayo hata hamu ya chakula sikuwa nayo, Jeon alitoka bila kuniaga, nilijikaza nikaingia kuoga make hali yangu haikuwa sawa hata kidogo...

Nimemaliza kuoga nikawa naludi kufunga geti ili nilale, nakutana na jeon, alinitizama kama mtu anausongo na msosi wake pendwa, afu uko mbele yake, nilijitizane kitauli kilikuwa kifupi mno, nililudi chumbani mbio kubadilisha,nikatoka nikiwa nimevaa, Jeon alikuja na chips kuku, akaniomba nile ndo aondoke...

Ivi Jean unatambua kama wewe ni mwanafunzi, na unatakiwa kuwa wapi saivi? Hujui kama unatengeneza tatizo kwangu na kwako?..

" Joy huo muda unaoongea ungeutumia kula, ili mmeo niwahi kujisomea, ungekuwa umefanya jambo la maana sana, hapa nilipo umeshanivuluga J, nakupigia mahesabu vibaya mno, kama utaendelea kunifanya niwe hapa zaidi nakuhakikishia nitakukula...

" Unacheki hali yangu ilivyo? Alitoa nyoka wake kunionesha, nyie nilifunika macho halaka nisione, Jeon ujue sio tabia nzuri hio, naomba uludishe basi nitakula sasa hivi, " aya kula niondoke usipokula nitatoa na nitaingiza sehemu husika sasa chagua mwenyewe...

We kusikia hivyi nilikula kama kichaa kafumania chakula jalalani, nilipitiliza hata ulaji wangu wa kawaida muda huo Jeon aliingia jikoni kumbe alienda kupika kaludi na ugari, akala na kuku wake uyo akaniwekea kadi ya benk mezani na no ya sili, na pesa cash laki...

" J mke wangu, hio kadi yako utatumua kwenye mahitaji yako, na hii pesa naomba kesho ukasoke hizo nywele, kasuke nywele nzuri, sio hizo twende kilioni kila siku, kama pesa itapekea chukya kwenye kadi, na sitaki ukatae kama utakataa nitalala hapa, na usiposuka pia, nitakuja hapa kukusuka mwenyewe, na ukinifanya nije ujue kabisa nitakukula...

Alivyomaliza kuongea, ajaondoka sikutaka kuongea kabisa niliogopa na hivi niko peke yangu mmh, yasije kunikuta makubwa...
Kupata mwendelezo bonyeza hii link apo juu itakupeleka moja kwa moja kwenye hadithi full ukasome kwa buku tu...

Itaendelea....💥


MADAM JOY NA MIMBA YA CEO MWANAFUNZI
MTUNZI: BABY SMILE
EP 3.

Alivyotoka tu mimi mbio kufunga funga milango, kesho yake ilikuwa jumamosi, niliamua kufanya fanya usafi nyumbani, nilivyomaliza nikatoka kwenda kuosha nywele ndo nikakumbuka yaliyonitokea jana, ila sasa kimbembe sehemu kubwa nikawa nakumbuka tu mambo ya kijinga...

Nilienda kuosha nywele, lakini sikusuka, nilifunga zangu mchicha, uyo nikaenda kuhemea chakula na mahitaji ya nyumbani kwangu, sikuisahau laki, ila kadi sikubeba kabisa, nilijua tu, huyu mwanafunzi hana pesa, amedunduliza za kuomba omba na kudanganya kwa wazazi ndo kaamua anipe mimi...

Nilienda duka ninalochukulia vitu nakuta nimeshalipiwa tena zaidi ya ninavyochukua, niliuliza nani kanilipia, nijahisi huenda mlokole wangu kaludisha moyo nyuma, lakini hakuwa akinihudumia hii vipi🤔,niliwa nahoji mwenye duka akanionesha oicha ya Jeon, dah nikachoka na hofu juu vipi wakijua ni mwanafunzi, niliomba nikahemee kwanza vitu nitapitia hivyi vingine make vilikuwa vingi mno, mcheke kg 50 ilihali mimi sijawahi kuhemea zaidi ya kg 15...

Sukai mfuko, maharage, ngano, mafuta dumu zima, yani vitu vilikuwa ni vingi, nikaambiwa adi mbebaji ameshalipwa nilichoka,nilienda kuhemea vitu vyangu vidogo dogo, huku nawaza mno, pesa niliyopanga kuchukuliw chakula nikamtumia bibi yangu, alifurahi mno...

Nililudi nikachukua mizigo na uyo dereva alielipwa kunibebea, akanikabizi na jagi la kuchemshia maji na jiko kubwa la oven, linalotumia umeme na gas, nilichoka uyu kijana kachukua pesa ya ada ama🤔...

Tulifika nyumbani nakuta tena kuna watu getini, wako na kitanda kimoja kizuli yani mmmh, na godoro inch 10 ya spring, nao wananipa maelekezo ety, wameagizwa na Jeon, nikaona sasa huu msala Jeon hawezi toa vitu vyote hivi, huenda ni mtego, kuna mtu jatuona jana au mzazi wake, sasa wananitega, nikavikataa na kusema simjui, wakanionesha picha bado nikakataa...

Wakampigia nakunipa simu, kupokea hivi sauti ni yake kabisa,J mke wangu, acha usumbufu wafungulie waingize vitu ndani, jioni nitachomoka nije kukusaidia kufunga kitanda, najua nikija saivi hutokuwa na amani ama nije? Kusikia nije nikajibu halakahalaka hamna, waingize tu na kitanda usijali ninaweza kufunga...

Hakujibu chochote alikata tu simu, muda huo natetemeka vibaya mno, nikawafungulia mlango, waliingiza kila kitu, wale wa kitanda walikuja pia na feni,tv inch 60, bufa kubwa, sikuwa na king'amuzi kiliwekwa,wakiwa wanamalizia malizia, umbea ukawa umeshafika kwa madam rozi, saa 12 jioni huyu hapa, wale wa king'amuzi ndo walikuwa wamemaliza tu kuhakikisha kama king'amuzi wamekufunga sawa, na kifulushi nimelipiwa cha mwaka mzima...

Roz kafika anashangaa ndani kwangu kumebadilika mno, yani kunavutia nilikuwa na tv inch 24, imetolewa sasa nina mtv tena hinsence smart tv, uku bufa linadunda sio pw,kwa mshahara wangu ivi vitu vyote ni uongo labda kama nimekopa lakini ata mkopo mmmh ni pesa ndefu mno kukopeshwa itanighalimu miaka kkuna hadi frij la milion moja na nusu yani gharama za hivi vitu vilivyoingia leo kwa haraka haraka Tu si chini ya ml 6 ...

Roz alianza " shoga ebu nipe chimbo umepata wapi hili danga? Inaonekana mlokole alikuwa anakuzibia ridhiki, siamini wewe huyo🤔, umetoa wapi nisanye basi shogaangu na mie,nilibaki namshangaa tu kwanza mwenzake apo, nipo kwenye mshtuko wa hatali, nawaza uyu mwanafunzi kulikoni, mbona sielewi...

Niliamua kuchekecha halaka huyu mbea asijue kitu, nikamjibu, Rozi sasa hivi hasila zangu nimehamishia kufanya maendeleo, nimekopa, shuleni pesa, nataka pia kufungua biashara, nitakuwa nalejesha kila mwezi kwa kukatwa kwenye mshahara mpaka deni langu litakapo isha,nilijibu lakini ndani naogopa...

Joy ivi huogopi🤔, utaishije yani umeenda kukopa ununye vitu vya gharama ndani, umesahau kama kuna kuka na kuna kodi? Shoga umeyakanyaga, kumbe kweli wewe bado unautoto sana, badala ungefungua hata biashara, 🙌 naomba usije kuomba hifadhi kwangu wala kunikopa, nakupa kabisa angalizo...

Sikujibu chochote, ajabu akaanza nipeko basi mchele shoga angu nikasukumie siku, siunajua tena hizi taree ni ngumu, mshahara tumeshamalizs runasubili hio wiki ijayo nigawie wakusukumia izi siku basi...
Kupata mwendelezo full bonyeza hii link hapa juu ya hadithi, ukasome yote hadi mwisho kwa buku tu....

Itaendelea....💥


MADAM JOY NA MIMBA YA CEO MWANAFUNZI
MTUNZI: BABY SMILE
EP 4.

Nilimtizama nikaona kabisa, unafiki mkubwa niliamua kumtoa kwangu kwanza ninayangu yamejaa kichwani natakiwa kutafakari, nilimchotea kg 2 tu, bahati nzuli aliona mcheke tu, sukari na mafuta vilikuwa chumbani, hata kitanda hakukiona aliona frig, tv, jiko, meza ya kioo, sofa pia vipenzi sikuwaambia ila adi sofa tena zile za bei mbaya...

Nilimpa huo mcheke, " jamani joy ndo kidogo hivi shoga niongeze basi, hee jamani ivi uyu mtu mbamuelewa kweli haaa, Roz kumbuka mwenzio sina mshahara,na hata nikikwama ushasema huwezi nisaidia, apa natakiwa nijibane ili nisijekulala njaa, labda nikukopeshe tuandikushane kabisa, ili ukiisha niijie, nijaona kavuta mdomo nakusema " heee yani kunipa tu mchere mpaka tuandikushane, makubwa asante huu utanitosha,muda huo huo akapigiwa simu na bwana ake, pale pale akaondoka, nikashukuru Mungu, nikabaki kuwaza uyu mwanafunzi katoa wapi hizi pesa jamani,nilibaki nazunguka zunguka sebreni kwa mawazo mno...

Au kaiba jamani dah, natakiwa kuwa makini sana, niliwaza mpaka kichwa kikaanza kuniuma, saa mbili ilifika mimi ndo naingia kupika, nimeivisha mboga, nasikia geti linagingwa, kwenda kufungua, ni Jeon, jamani nilianza kuchungulia kama kuna mtu kamuona, kisha nikafunga geti kwa hofu mno...

Nililudi ndani, nikakuta mtu yuko zake bize chumbani kafungua kitanda anataka kufunga kipya, kwanza nikatizama kama kaona kabati zangu, nilizoanika chumbani, nikakimbia kuzitoa, akanitizama huku anatabasamu, "huna haja yakutoa, nishaziona na kuzinakili kichwani kabisa, njoo basi unishikie apa tufunge kitanda mke wangu...

Jean unajua unanizoea vibaya, hivi huoni aibu kuniita mke wako?, ujue wewe ni mwanafunzi jamani, utaniletea shida kuwa muelewa basi dah,niliongea huku nataka ata kulia, " J acha utoto naomba uje unishikie tufunge muda sio lafiki, kumbuka natakiwa kuludi shule, nikakaze kwa ajili yenu wewe na watoto wetu...

Dah nilichoka ivi ananielewa kweli uyu kiumbe🤔, " J ama unataka nitumie njia mbadara kukuelewesha eee? Aliuliza huku anaweka spana yake chini aliyokuja nayo, wee nikaona huyu huenda sio timamu faster nikakamata upande wa kitanda afunge...

Alinitizama huku anatabasamu, akafunga tukaweka chaga, na godoro, " mke wangu naomba unipikie ugari nina njaa mno, mimi sio mke wako, niliongea huku natoka chumbani asije nikabia uko, mtu mwenyewe mlefu vile na ule mwili akhaaaa...

Nilienda jikoni nijasonga huo ugari, nikamtengea mimi nilikaanda ndizi nikala na nyama, tukiwa tunakula geti likagingwa, ajainuka kwenda kufungua, wewe Jeon ebu acha mambo ya kijinga, unajua ni nani ukute umeonwa tumekuja kukamatwa...

" Punguza presure basi mke wangu, ao ni watu wangu nimewagiza vitu walete,wamenitumie ujumbe wako getini soma uhakiki, kweli nikaona, ila mashaka nikaomba twende wote tu,akakubali tukatoka wote mpaka getini,kufika nikafungua ila mikono yote imejaa unyevu, nikaona watu wako na cret za soda, maji, juice na maziwa, wakaingiza ndani, wakatoba na aliewaagiza, baada ya dk 3 akaludi...

Akamimina maziwa mgando, akaendelea kunywa, mimi nikachukua soda,kimya kimya,tulivyomaliza tu kula, nikatoa vyombo, nikamkuta mtu sebren akuna naingia chumbani, nasikia tu maji bafuni, nikatoka haraka nisije nikaona vitu vya ajabu...

Nilifika sebleni, nikaanza kupanga soda na vitu vya kwenye frig, nimemaliza nikaon niwashe tu mziki, nikawasha, kidogo jeon akatoka kapaka roshen yangu, sikutaka hata kuuliza, nikakimbilia chumbani, nikafunga kabisa mlango nioge, nilioga nikavaa..

Nikaja kuchungulia kama kaondoka, nakuta mtu yupi kajaaa sebre, niliona ndo muda wakumuhoji, Jeon naomba tuongee, " ok ongea haina shida...

Ivi hizi pesa umetoa wapu ilihali wewe ni mwanafunzi, na kwa nini umeamua kuninunulia mimi, yani sikuelewi unajua unakosea sana?
" Joy naelewa ninachokifanya, kuhusu nimetoa wapi na nimwanafunzi, usisahau mimi ni mwanaume, sitegemei elimu pekee kwenye utafurahi wangu, natafuta uku nasoma, kuhusu kwa nini kwako, kwasababu wewe ni mke wangu, ni kitu muhimu kwangu, na niwajibu wangu kukutunza, siwezi kuwa na amani kulala kwenye kitanda ukichogharamikia kwa pesa zako, au kupewa, siwezi kulala nyumba ambayo inalipiwa kodi na mtu mwingine tofauti na mimi...

"Wewe ni wajibu wangu, hivyo natimiza majukumu yangu, hata kodi nimeshalipia na nimesahau kukupa mjataba , akatoa kwenye koti lake, kweli kodi imelipwa ya mwaka mzima, " kuhusu kukuletea matatizo hilo halitotokea,na endapi litatokea,siwezi kushindwa kulitatua...

Jeon ujue unanichanganya, yani mimi ni jukumu lako kivipi,na mimi na wewe how, yani nitajibu nini ety natembea na mwanafunzi kweli wewe unaona imekaa sawa? Wazazi wako wakijua si nitakuwa kituko mimi tena nitaambiwa nabemenda wanafunzi...

Jeon alicheka, " ha ha ha ha ha joy ebu acha kunichekesha, miaka 21 unambemenda nani? Nakuzidi miaka 7, acha wenge, unachotakiwa saivi, nikunijali tu mmeo, ayo mambo mengine niachie mimi"...

Jeon mimi na wewe hatujakubaliana, umejuaje kama nakupenda? na kama niko na mtu mwingine mbona unajiamini sana?..

Kwa sababu najua moyo wako ni wangu, na hio habari ya mtu mwingine, nafkili usiutafute upande wangu wa pili, najya hauna mtu, sasa jichanganye, uludiane nae ama ujiingize pengine utauona upande wangu wa pili ulivyo...

Aliongea kwa hasira, akaniambia njoo ufunge mlango niondoke, naona nikiendelea kuwa hapa utahalibu siku yangu...

Alivyoanza kutoka nijamuwahi kwa mveke kumuzuia, tukatazamana, alinikazia macho ikabidi nishushe tu yakwangu, nikamwambia huondoki adi tufikie muafaka, huwezi kunipeleka peleka tu kama gari bovu, " J naona una unachokitaka leo si ndio? Jeon aliongea hivyo uku anavua koti lake, nakuludi ndani...
Kupata mwendelezo wote adi mwisho bonyeza hii link apo juu ukasome yote adi mwisho...

Itaendelea...💥


MADAM JOY NA MIMBA YA CEO MWANAFUNZI
MTUNZI: BABY SMILE
EP 5.

Niliogopa huyu mbona anavua tena, hee uwiii🙆, Jeon basi baba nenda tu sitaki tena kukuuliza chochote we nenda tu, " J usinipime haswa ukiona nimebadilika, kwa leo nakausha, ila ukiludia nitakufundisha namna nzuri ya kuongea na mimi, nini uulize na nini usiulize, nini ujibu na kipi usijibu, alivyomaliza akabeba mkoti wake mkononi, huyo akasepa nyie mmmh naonewa jamani sijui ni huu udogo wangu 😭, nilifunga milango na mageti nikaingia kulala...

Upande wa jeon alifika getini akaingia bila shida mlinzi anapewa pesa kiasi kwamba, anamchukulia jeon kama boss wake,muda wowote akitaka kutoka hakuna wakumzuia, alifika bwenini kwake akiwa na hasira kisa tu nimeongelea mwanaume mwingine, alikuwa anaumia akaamua kwenda darasani, hasira zote akazihamishia kwenye kitabu, alipiga kipindi mpaka saa 9 usiku...

Ndo akaingia kulala lakini akili yake haikumluhusu ikaanza kumkumbusha muonekano wangu, alijitahidi kujizuia lakini wapi, amekuja kupitiwa usingizi saa 11 asubuhi, akaona kuepusha amsha amsha akalale juu ya dari, au kwa mlinzi, akaamka na kuelekea kwa mlinzi kulala...

Upande wangu niliamka nikiwa nimechoka nikaanza kujiandaa niende kanisani, nilioga nikapika nakachai ili nikitoka tu nifikie kunywa,nimefika kanisani mida ya saa mbili ivi asubuhi, kila mtu ananitolea macho, nikajiuliza au kuna tatizo?...

Kuna mama mmoja akanisogelea na kunishika mkono, nikamsalimia, akaitikia kisha akanambia" mwanangu kwa nini usingebaki tu nyumbani, huoni kama umekuja kujiumiza mwenyewe?...

Nikashangaa kujiumiza? Kivipi mama, kwani hujui kama leo peter anafunga ndoa na madam Esta?...

Nyie nyie nilichoka mwili na roho, huyu Esta aliekuwa akijitia dada ushauli wa mahusiano yangu🤔,nilijikuta nasikia maumivu makali kuliko hata maumivu ya kidonda, sijakaa sawa gari ya bwana harusi ikaingia nyie nyie...

Dk 20, gari la bi harusi, nilijuta kuja kanisani, tena kibaya zaidi nilihama kanisa kisa peter, huu ujinga nilioufanya matokeo yake ndo haya😭, nilijikaza nisilie lakini nilishindwa, ilibidi yule mama anitoe pale, alinipeleka mpaka kwangu, alinipa ushauli kibao, nilionesha kuelewa lakini sio kweli,maumivu niliyokuwa nayapata hayaelezeki, bora angeoa mtu mwingine, lakini Esta niliemuheshimu kama dada angu,jilani yangu, akanidanganya kasafili kumbe kaenda kujiandaa na ndoa...

Hii kwangu ilikuwa zaidi ya maumivu, yule mama aliomba nimpigie simu mtu wangu wa karibu yeyote atoke awezi kuniacha peke yangu, lakini kila nikiwaza mtu wa karibu, naona kama nimetukanwa, sitaki tena kuwa na mtu wa karibu, mtu ambae atageuka adui kwenye maisha yangu sihitaji tena, nitaishi kivyangu vyangu, nilijiwazia hivyo moyoni, wakati huo yule mama, abahangaika kunitoa kwenye mawazo yangu kwa kuniita, lakini haikusaidia mpaka akanitingisha ndo nikashtuka...

Akaludia tena, nikamjibu mama angu, kuwa na amani siwezi kufanya chochote kibaya kisa maamuzi ya moyo wa mtu, ndio nimeumia lakini sio sababu ya mimi kujizuru haitosaidia chochote zaidi ya aibu na hasara kwa familia yangu...

Yule mama alinikumbatia na kuahidi jioni ataludi, nisiwaze huenda nimeepushwa na balaa zito, alisema ataludi na chakula,nilikubali, alivyotoka tu,nikaingia zangu kulala huku nalia vizuli,nililia mpaka nikapitiwa usingizi, nakuja kushtuka nakuta mtu pembeni yangu kalala, nilishtuka mpaka nikamuamusha, alikuwa ni jeon...

Aliamka akanitizama sana kisha ajauliza, "J unampenda sana huyo jamaa kuliko mimi?
Nilishangaa inamaana huyu kajua kwa nini niko hivi? Na kwanza ameingiaje ndani🤔,niliganda tu kumtizama huku nawaza yakwangu, alinikumbatia kwanguvu na kuniambia " J mke wangu, naumia mno unavyomfikiria mwanaume mwingine, naomba ujikaze na umsahau, huyo sio sahihi kwako...

"Niko hapa mmeo, nitakuwa bora kuliko yeyote kwako, sitokutia machozi, alinimbembeleza adi nikajisikia vizuli,alipika nakuleta chakula tule, nilijilazimisha, vikawa vinaninyiga tu, Jeon alionekana kuchukia na kuumia sana mpaka mishipa yaje ikawa inajichola kwenye ngozi...

Niliogopa nikaamua kumtafutia sababu, Jeon usijali saivi niko sawa, unatakiwa ukajiandae siunajua kesho ni jumatatu, usije kukosa vindi na uko darasa la mwisho ujue,alinitizama nakunijibu, " nimeomba ruhusa ya wiki moja, sio tu peke yangu nimekuombea pia wewe ya siku 10, na ruhusa zote zimekubarika, nilitumbua macho Jeon ujue uache utani...

Wewe ni mke wangu, kuna vitu ndio tunaweza kutaniana lakini sio hili, na kingine kesho tutasafili mimi na wewe kwenda nje kidogo, tutaludi kumamosi ili jumatatu niludi kwenye vipindi, Jeon asante, lakini hakukuwa na haja ya yote haya, sio sahihi kwako kuacha vipindi ujue, " J niamini hakuna kitakachohalibika, ninaweza na sitofeli naomba ule ukaoge...

Nilijikaza ivo ivo, nikaingia kuoga na nguo zangu nilivyoingia bafuni sikurock mlango, kimbembe nimeanza kuoga wakati najimwagia maji nakuja kufumbua macho hivi,naona mende na mimi na mende ni hatuelewani kabisa bola nione mdudu mwingine sio mende namuogopa mno,nilipiga kelele mpaka jeon akaja, sasa balaa na ule uoga sina hata taulo nimeshajisahau napiga tu kelele, mwenzangu kkuniona tu hali yake taabani, akashindwa ata aanze na nini...
Kupata mwendelezo bonyeza hii link hapo juu ukasome full kwa buku tu...

Itaendelea...💥


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote