Mali Safi Ya Msela

book cover og

Utangulizi

MALI SAFI YA MSELA
By Miss Hamida
UTANGULIZI.

Baada ya Mama kufariki Baba ana amua kuoa mwanamke mwingine mwenye watoto wanne! Ambao Watatu wa kike na mmoja wa kiume. Mwanzoni wanaonyesha mapenzi kwangu ila mambo yanabadilika tu baada ya baba kufariki.

Na hapo ndipo nikaanza kupitia mateso toka kwao, kasoro tu kwa kaka yangu wa kambo anaeitwa Meshack. Lakini hali inakuja kuwa tofauti baada ya kukutana na Puttin.

Huyu ni kijana mhuni tena msela wa mtaa anae endesha bajaji. Mwanzoni anaonyesha nia ya kutaka kuwa kwenye mahusiano na dada zangu wa kambo ila wanaishia kumkataa sababu eti ni maskini.

Lakini kwangu inakua tofauti. Namkubali Puttin na kuwa nae kwenye mahusiano bila kujua ni kijana wa Tajiri, tena tajiri huyo ni Boss wa Meshack ambae alikua akitafuta mke kwaajili ya kijana wake.

Dada zangu wanapogundua ukweli, wivu unawakaba, wanafanya kila njia ili wampate Puttin tena, na mbaya zaidi Kaka yangu wa kambo Meshack anajikuta akianza kunipenda kimapenzi.

Ivyo ndugu hawa wa kambo wanashirikiana kunitenganisha na mhuni wangu Puttin! Je watafanikiwa??

SEHEMU YA : 1

Ni miaka 12 imepita sasa toka alipofariki mama yangu. Aliugua ghafla tu tena ugonjwa wa ajabu ambao ulipelekea kifo chake.

Kiukweli niliumia mno maana alikua mtu wangu karibu kushinda baba ambae mara nyingi alikua safarini kikazi.

Baada ya kumzika mama, baba hakuchukua mda mrefu alioa mwanamke mwingine. Mwanamke ambae tayari alikua na watoto wanne.

Ambapo kati ya hao watoto wanne, mmoja ni wa kiume anaeitwa Meshack, na hao watoto waliobakia ni wakike ambao ni Tamara, Lulu na Lydia.

Mwanzoni sikuona shida sababu mama yangu wa kambo pamoja na ndugu zangu wapya walinipenda sana. Tuliishi kwa amani japokua maisha yetu hayakua mazuri.

Ila ghafla tu mambo yalibadilika, na hii ni baada ya baba kufariki akiwa safarini. Toka hapo maisha yakaanza kuwa magumu kwangu. Ule upendo wote alio nionyesha Mama ulibadilika na kuwa chuki na kisirani.

Ukija kwa ndugu zangu napo ndo ivyo ivyo kasoro kwa Meshack tu ambae alikua karibu yangu kushinda mtu yoyote yule.

Ikabidi nivumilie mateso japo kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Hawakuona kabisa umuhimu wangu kiasi kwamba wakawa wananitambulisha kwa watu kama mfanyakazi wao wa ndani.

Kuona vile nikakaza moyo na kuendelea na maisha. Siku sio nyingi Meshack alianza kufanya biashara yake ya kuuza madafu. Kusema kweli kipato chake hakikutosha kabisa kutulisha wote.

Ikabidi na mimi nitafute kazi kwaajili ya kumsapoti. Sikua nimesoma kwaiyo niliishia kufanya vibarua vya mtaani. Sikuchagua kibarua kabisa maana mpaka vyoo nilizibua hadi kazi za ujenzi nilifanya.

Cha ajabu Tamara, Lulu na Lydia hawakua wakifanya chochote kile. Kazi yao kubwa ilikua kujipodoa na kukaa ndani.

Alafu mbaya zaidi Mama aliwadekeza sana, aliwaita malaika sababu ni wazuri kweli kweli hasa kwa rangi zao na shepu zao za namba nane.

Basi siku moja nilikua nimetoka zangu kwenye kibarua cha kufua nguo. Nakumbuka nilifua kweli kweli mpaka nikahisi vidole vinakatika.

Alafu matokeo yake yule Mama akanipa elfu 10! Aisee nilijikuta nagombana nae vibaya mno ila hata haikusaidia chochote maana hakuniongezea hela.

Basi nilipofika tu nyumbani nikaenda jikoni moja kwa moja nilipo hifadhi chakula changu. Kabla sijaondoka kwenda kwenye vibarua vyangu huwa napika kabisa chakula cha mchana, kisha namtengea kila mtu chakula chake kwenye sahani.

Changu huwa nakifichaga kabatini. Sasa nilipo angalia sehemu nilipo kificha nilikuta sahani nyeupee pee. Walikula chote hawakuniachia hata punje.

Daah, nilichukia kwakweli sababu toka asubui sikua nimeweka chochote tumboni. Nilitoka jikoni haraka na kwenda sebuleni walipokua wamekaa.

“Nani kala chakula changu?” Niliuliza kwa hasira

“Sisi tumekula!” Alisema Mama kwa kujiamini sababu alijua siwezi kumfanya kitu

“Kwanini jamani na wakati mimi sijala toka asubui??”

“Kwaiyo? Kama hatukushiba je? Siku hizi unabania sana kipimo cha chakula ndo maana hatushibi”

“Nabania sababu hakuna chakula kingi kilichobakia!”

“Aaah tumekula bhana!”

“mimi nitakula nini?” Machozi yalianza kunilenga lenga

“jiongeze! We si unafanya kazi? Kanunue chakula ule au kama vipi msubirie Meshack aje mle wote”

Nilijihisi vibaya mno, nilitoka pale sebuleni nikatoka nje kwa hasira na kwenda kukaa nyuma ya nyumba.

Huko ndani wenzangu hata hawakujali, walinicheka na kunisema, walipochoka waliendeleza stori zao zisizokua na maana.

Basi Jioni Meshack aliporudi nilimuomba nikala nae. Hakua mchoyo kabisa na sijui roho yake nzuri alirithi toka kwa nani maana ndugu zake hawakua kama yeye kabisa.

“Kula, mbona unani tegea?” Aliniuliza wakati tunakula

“Chakula kidogo sana na sidhani kama tutashiba”

“Mimi nilikula mihogo mchana, wewe ndo hujala kabisa toka asubui kwaiyo kula”

“Na wewe je?”

“Tunu, si nimekuambia hapa nimekula mihogo mchana?”

“aya basi nakula” nilinyanyua kijiko na kuanza kufakamia chakula. Ila ukweli ni kwamba Meshack hakua hata kala mihogo, alinidanganya tu ili nisijihisi vibaya kula chakula chake.

Basi, siku iliyofuata kama kawaida niliamka asubui na kuanza kufanya kazi. Kwanza lazima nifue nguo za watu wote kule ndani, kuanzia Mama, Tamara, Lulu pamoja na Lydia! Ni Meshack peke yake ndo alikua akijifulia nguo zake.

Baada ya kufua, nikapika chai na chakula cha mchana. Nilipomaliza hapo Meshack akawa amesha amka, aliniaga na kuondoka zake kwenda kwenye shughuli zake.

Nikamalizia kufanya usafi wa kufagia uwanja ndipo na mimi nikaenda kujiandaa ili niende kwenye vibarua nyangu.

Ile natoka tu nje nikamkuta Mama amekaa kwenye kigoda. Sikujua hata aliamka saa ngapi.

“Shikamoo Mama” nilimsalimia

“Hakuna kitafunwa ndani!”

“aah, sina hela mama”

“Kwaiyo unategemea ndugu zako watakunywaje chai? Unataka wanywe chai kavu?”

“mbona mimi nimekunywa kavu?? Alafu uzuri chakula cha mchana kipo tayari kwaiyo watakunywa na chai”

“Wee, chai ni chai na chakula cha mchana ni chakula cha mchana! nipe hela huko”

“Mama sina hela”

“usinitanie mimi” alinyanyuka alipokua amekaa akanikamata kwa nguvu na kuanza kunisachi. Aliingiza mikono hadi kwenye sketi yangu na kutoa noti ya elfu mbili.

“Hii ni nini??”

“hela ya emergency mama, sina nyingine zaidi ya hiyo” niliongea kwa unyonge

“Tunu wewe una roho mbaya sana wewe! Yani vibarua kidogo ndo unajiona tajiri je ungekua unafanya kazi serikalini? Si ungetushindisha njaa humu ndani?? Embu toka hapa usiniangalie kwa huruma mimi sijakuzaa” alinisodoa kwa kidole chake kisha akaingia ndani.

Nilihuzunika mno, nijiweka sawa kisha nikaanza safari ya kuelekea kibaruani kwangu. Nikiwa njiani nilikutana na Remmy.

Huyu alikua ni mpenzi wa Lydia. Na Penzi lao ndo kwanza lilikua jipyaa tena zito. Sasa Remmy aliponiona akasimamisha gari na kuniita.

“Tunuu!”

Nilipo ona ni yeye ambae alikua akiniita, sikuona ajabu. Nilivuka barabarani na kwenda upande wa pili kumsikiliza.

“vipi Tunu! Asubui asubui namna hii?”

“kuna mahali nimeitiwa kazi ndo ninaenda”

“Alafu sio mara ya kwanza kukuona ukipita hii barabara, vipi Lydia na yeye ameshakwenda kazini?”

“Kazini? Mbona hafanyi kazi?” Niliongea bila kujua kuwa, Lydia alikua amemdanganya Remmy mambo mengi kweli. Na swala la yeye kufanya kazi ni mojawapo ya uongo alio mdanganya.

Je nini kitaendelea?
Nakuja………


SEHEMU YA : 02

“Hafanyi kazi? Kivipi? Mbona amesema anafanya kazi kwenye supermarket?” Remmy alikua na mshangao

“Hakuna! Hafanyi kazi mbona, ni mimi na kaka Meshack ndo tunaofanya kazi” niliongea vile kwa nia nzuri na wala sikua na wazo kwamba namharibia Lydia

“Anhaaa! Asante kwa taarifa” aliingiza mkono mfukoni akatoa noti ya elfu 10 na kunipa.

“Ya nini hii shem?”

“Tumia kama nauli”

“Hapana, mimi sihitaji”

“Chukua tu Tunu! Sina nia mbaya”

“asante” nili ipokea nikaiweka mfukoni kisha nikaagana nae na kuendelea na safari yangu.

Kumbe huku nyuma Remmy alimpigia simu Lydia asubui ile ile. Akamuambia yale yote niliyo mueleza na mbaya zaidi Remmy akavunja mahusiano yake na Lydia.

Basi nawaambia Lydia akawa kakasirika hatari. Akaanza kulia mpaka Dada zake na Mama wakamsikia.

“Wewe unalia nini?” waliingia chumbani kwake na kumuuliza

“si huyu Tunu! Unajua kamuambia nini Remmy? Binti mshenzi sana huyu! Kaharibu mambo yangu yote”

“Unaongea sana pasipo kutueleza Tunu kakufanya nini??” Tamara alimuuliza

“Remmy kanipigia hapa mda sio mrefu, kaniambia kaambiwa na Tunu kuwa sifanyi kabisa!”

“Enhee??”

“Remmy kachukia hatari, amesema hapendi wanawake waongo na wanawake ambao hawajishuhulishi! Kwaiyo ameniacha!” Lydia akazidi kulia

“nini? Embu subiri kwanza, Remmy huyu huyu anae kuhongaga pesa? Ambazo ndo tunanunulia viwalo?” Mama alikua kama kachanganyikiwa

“Ndio mama”

“Weeeee! msichana anaroho mbaya huyu! Mwanaharamu mkubwa! Unajua nini malaika wangu? Subiri arudi tutamkomesha! Mbona ataomba pooh!”

“Ndio Lydia ata usiwaze! Kichapo tutakacho mpa leo ataomba mpaka maji” alidakia Lulu na wote wakawa wamepanga kunipiga.

Upande wangu sikua najua chochote, siku hiyo nilikua kwenye kibarua cha kufua nguo za watoto, na zilikua nyingi mno! Ila uzuri walinipa elfu 20! Niliridhika, nikashukuru na kuondoka.

Nilitembea haraka haraka kurudi nyumbani. Nilipofika nikawakuta wamekaa kibarazani wote wanne wakinisubiria.

Niliwasilimia ila hawakuitikia badala yake nilishangaa wakinizunguka na kuniweka katikati.

“Enheee, cha umbea! Mdomo wako hauna breki wewe??” Alisema Mama

“Mbona sielewi?” Ni kweli sikua naelewa chochote

“Umemuambia nini Remmy wewe? Kuwa sifanyi kazi? Nikaonekana muongo mpaka akaniacha” Lydia alizungumza kwa hasira na kabla hata sijamjibu akanivamia na kuanza kunipiga.

Nae Tamara na Lulu wakamsaidia. Asiee walinipiga sana siku hiyo sitakaa nisahau. Baada ya hapo mwili mzima ukawa unaniuma na nilikua nina ngeu mpaka usoni.

Ukija kwenye mikono sasa ndo usiseme, nahisi kati ya Mama au Lulu kuna mmoja wapo alitumia meno yake kuning’ata maana sio poa.

Basi Meshack aliporudi alinikuta nimeiva kwa kichapo. Moja kwa moja alijua ni akina nani walio nifanyia vile.

“Ningekuwepo hakuna mtu ambae angesubutu kukugusa”

“Ndo imeshatokea” nilikua na huzuni

“Umeumia sana?”

“Sio sana ila mwili una uma, sidhani kama nitaweza kwenda kwenye vibarua, nitabaki nyumbani kujiuguza”

“daaah! Tunu ata sijui niseme nini, ila sielewi kwanini mama anakufanyia uovu wa namna hii!”

“Mbona ilo lipo wazi? Kwakua mimi sio mtoto wake”

“Ila mwanzoni hakua ivyo, tulikua tukiishi kwa amani kweli”

“napo ni kwakua baba yangu alikua yupo hai, kwa sasa hakuna kitu kinacho mtishia”

“Usiseme ivo, sipendi unavyo lia na kuwa na huzuni kila wakati! Ngoja kwanza nikupe habari nzuri”

“habari gani izo?” Nilikaa vizuri kumsikiliza

“Enhee basi leo nimekutana na Tajiri, ninapo sema Tajiri namaanisha ni Tajiri kweli kweli! Na anapenda madafu mno! Kaniambia niwe nampelekea madafu kumi kila siku ya alhamisi nyumbani kwake, na namba zangu za simu kachukua”

“Weee!” Nilishangaa

“Ndio, kwaiyo siku ya alhamisi itakwenda kuwa nzuri sana! Na sitakua napata shida kuyauza kila wakati”

“Hongera kaka, unajua ni mafanikio hayo”

“Kweli kabisa Tunu”

“Umeshamuambia Mama?”

“Hapana! Sijamuambia bado! Sitaki ajue”

“Hakuna shida”

Tulipiga stori mbili tatu kisha kila mtu akaenda chumbani kwake kupumzika. Kutokana na ngeu nilizokua nazo sikuweza kwenda kwenye vibarua vyangu kabisa. Nilishinda nyumbani nikijiuguza mpaka siku nitakayo pona.

Sasa siku moja nikiwa nimekaa kibarazani mchana nikipunga upepo, lilikuja gari moja ivii chakavu na kusimama mbele ya nyumba yetu.

Alishuka kijana mmoja mtanashati akiwa na mbaba mmoja ivii wa makamu. Nilipowaona nilijua tu walikua ni mtu na mwanae.

Wale wageni walikuja kwa lengo la kuzungumza na mama, ivyo tuliwatengea benchi pale nje maana hatukuweza kuwaingiza ndani.

Na mimi sikua mbali, nilikaa karibu kabisa ili niweze kusikia ni kipi kilichokua kimewaleta pale nyumbani.

“Naitwa Steve, na huyu ni Baba yangu Mzee Robert” alijitambulisha yule kijana

“Na mimi naitwa Monica, na hawa ni mabinti zangu, Tamara, Lulu na Lydia” Mama alitambulisha wote akaniacha mimi, na hata sikujali.

“Vizuri, una watoto wazuri sana” alisifia Mzee Robert

“Ndio! Ni malaika zangu!… enheee Mzee Robert ni lipi lengo la ujio wako”

“Anhaa, Monica, ila ningependa kukuita Mama Tamara! Kijana wangu ametokea kumpenda moja kati ya mabinti zako, aliponieleza, mimi nikaona nije kutoa taarifa, ikiwezekana tuanze taratibu za ndoa”

“Anhaa, kwaiyo kampenda binti yangu? Yupi huyo?” Aliuliza Mama, kisha Steve akamnyooshea Tamara kidole

“Huyo hapo, nampenda huyo!” Alisema Steve, Cha ajabu Mama hakujubu kwanza, alisimama na kusogea hadi walipokua wameegesha gari lao.

Alilitazama lile gari kwa makini kisha akaanza kulikagua.

“Kigari gani hiki? Tena Plate Namba A, wenzenu wapo E, nyie mpo A! Kigari kimekongoroka namna hii, hakina hata bampa! Side mirror sasa, zimepinda kama maisha yenu yalivyo” alisema Mama bila aibu na kuwafanya Steve na Baba yake wajihisi vibaya.

Baada ya kulikagua gari la watu Mama alirudi kukaa kisha akamtazama Steve kuanzia juu mpaka chini na kusema

“bila shaka hata ilo shati umeazima, alafu kijana mdogo kama wewe unanuka kikwapa kikali na kiharufu flanii ivii cha kibeberu, kwa namna hiyo unadhani utaweza kumhudumia Tamara kweli?? Kwanza umemuona alivyo? Embu Tamara simama kwanza wakuone vizuri”

Tamara kwa madaha alisimama na kuzitingisha nyama nyama zake mbele ya Steve na baba yake.

Je nini kitaendelea?
Nakuja……….


SEHEMU YA : 03

“mmemuona sasa? Huyo ndo Tamara! Haendani kabisa na wewe, kama unamtaka binti yangu tafuta kwanza pesa! Tena sio pesa za mawazo??? Pesa za kumwagika kisha ndo uje hapa”

“mama Tamara unatudhalilisha sasa! Tumekuja kwa nia nzuri ya kuunganisha familia zetu na sio kututolea maneno ya shombo” Mzee Robert alikua kachafukwa vibaya mno

“kwaiyo msiambiwe ukweli? Tatizo lenu hamtaki kusikia ukweli maana unauma! Ila jua tu, siku zote vitu vizuri huwa vina gharama! lakini hata msijali, ninae binti ambae atamfaa kijana wako, nae ni mnuka mkojo mwenzie” Mama alinigeukia kisha akanambia

“Tunu njoo wakuone”

Kiukweli sikutaka kwenda sababu alinidhalilisha vibaya mno ila kama ningegoma basi ingekua ni balaa lingine.

Ivyo nilisogea mpaka walipokua wamekaa nikasimama pembeni huku nikitazama chini kwa aibu.

“enheeee, huyu sasa ndo mchafu mwenzenu! anakufaa Steve, kama utakubali kumchukua nipo tayari uondoke nae hata sasa ivi” Mama bila aibu alizungumza huku binti zake wakinicheka

“Hakuna haja, hizi dharau zinatosha sasa” Mzee Robert alisimama kwa hasira huku Steve akimfuata nyuma na kuelekea kwenye gari lao.

“Nendeni bhana nyie kajamba nani na kigari chenu cha miaka 90 ambacho kikipulizwa na upepo kinazimia” Mama aliwarushia maneno mpaka pale walipo ondoka kabisa maeneo ya nyumbani kwetu.

Basi akapongezana pale na binti zake kisha haoo wakarudi zao ndani. Haikua mara ya kwanza kwa wao kuwafukuza vijana waliokuja pale kwa nia ya dhati ya kutaka kuwaoa kisa tu hawakua na hela.

Kuna mmoja alimwagiwa maji ya ukoko wa ugali, mwingine alimwagiwa maji ya mapovu ya nguo chafu. Yani ni basi tu ili wawadhalilishe.

Upande wangu niliumia sana kwa kile mama alicho nifanyia cha kuniita mchafu mbele ya wageni.

Niliona waziwazi kua alishanichoka na kama ingetokea nafasi ya mimi kuolewa basi angeniozesha kwa kasi ya 5G.

Basi bhana ilipofika Alhamisi Meshack alikwenda kwa yule baba ambae alimuomba awe anampelekea madafu kumi nyumbani kwake.

Alipofika huko alishangaa kuona bonge moja la mjumba, sio nyumba tu kulikua na magari ya kutosha kama vile showroom na wafanyakazi hawakua chini ya 15.

“Karibu” alikaribishwa ndani na baiskeli yake ya madafu.

“Asante” alitabasamu akaingia ndani japo kwa uoga na aibu.

Huko ndani alipewa kiti akakaa kisha baada ya dakika mbili akatoka yule Baba aliemuita pale. Jina lake Ni Engineer Simon, Ni moja kati wa maengineer wakubwa wa serikali na wanao aminika sana.

Meshack alipomuona alisimama haraka na kujiweka sawa

“Mzee shikamoo”

“aaah marahaba kijana! Naona umefika kwa wakati”

“Ndio Mzee”

“Anhaa basi fanya mpango bhana nipate dafu angalau moyo utulie”

“hakuna shida Mzee” Meshack alisogelea baiskeli yake kisha akaanza kumchongea madafu huku wakipiga stori za mipira.

Ni dakika chache tu Meshack alizokuwa pale ila tayari walishazoeana na Mzee Simon utadhani walijuana mda mrefu.

“Hii tamu sana! Madafu yako yapo on point! Haya sasa wachongee wafanyakazi wangu bhana wapate ku-enjoy”

“Sawa sawa mzee” Meshack akaendelea kuwachongea wafanyakazi wake wote. Kwaiyo badala ya madafu kumi kama alivyoambiwa, akajikuta anachonga madafu 20 na yakaisha yote.

Kisha mwishoni Mzee Simon akamlipa hela yake na sio icho tu, alimpa na mapocho pocho ya kila aina sababu alidai siku hiyo walikua wakisafisha friji lao.

Meshack alifurai mno, alibeba vifurushi alivyopewa na kurudi navyo nyumbani. Nilipomuona karudi mapema nilimshangaa. Nilimfuata na kumpokea.

“Kaka umerudi mapema kweli”

“Ndio! Nimeuza kila kitu kwa yule Tajiri, na kanipa na mapocho pocho juu! Kuna kuku, samaki, soseji pamoja na nyama ya mbuzi huko kwenye mfuko”

“Kweli?” Nilichungulia na kukuta vitu vyote alivyo vitaja vilikua mule ndani

“Nina furaha sana Tunu, nimeuza madafu 20 na mzigo wangu wote umeisha! Kesho inabidi nikafuate mwingine”

Nilifurai mno kusikia vile, tukajikuta tunashangilia hadi Mama aliekua ndani akatoka nje na kuvuruga furaha yetu.

“Nini kinacho shangiliwa hapa” alinisogelea akanikwapua ile mifuko na kuanza kukagua

“Ni vile siku yangu imeenda vizuri” alijibu Meshack huku akitabasamu

“Na itakua imeenda vizuri sana mpaka umenunua nyama?? Meshack hela umetoa wapi? Usikute umeiba huko ukaniletea matatizo mimi?”

“Ina maana humuamini mwanao kiasi icho??” Ikabidi Meshack aanze kumuelezea Mama kila kitu kuanzia Alipokutana na Mzee Simon mpaka alivyo kwenda nyumbani kwake.

“Kumbe? Mbona hukunambia mapema! Hizi nyama nitapika mwenyewe, leo tutakula ugali na nyama ya kuku”

Mama aliposema vile nikajua kabisa sitaambulia kipande chochote cha nyama ikiwa yeye atapika. Ila tofauti na nilivyo tegemea akanipa kipande cha shingo.

Sikulalamika sababu ilikua afadhali kuliko angeninyima kabisa. Nyama zilizokua zimebaki alikula zote na binti zake hata aliezileta hakuzifaidi vya kutosha.

Basi kila siku alhamisi Meshack akawa anakwenda kwenye jumba ya yule Mzee. Na wakifika huko walikua wakipiga stori nyingi tu na Mzee Simon alimlipa hela nzuri kweli.

Sasa siku moja Meshack akiwa anamchongea madafu, Mzee Simon akaanza kumhadithia habari za kijana wake.

“ivi unajua nina kijana wangu bhana? Yupo Canada sasa ivi” alisema Mzee Simon

“Ooh hongera Mzee”

“Sina mtoto mwingine zaidi yake, ila ananiumiza kichwa sana”

“kwanini Mzee”

“hataki kurudi nyumbani kabisa! Toka amalize chuo amekua akifanya kazi huko hata nyumbani kapasahau”

“ongea nae vizuri, wewe ni baba yake lazima atakubali kurudi”

“Nimeshaongea nae, hata mke wangu ameongea nae mara nyingi tu ila ni mgumu kuelewa! Nataka siku akirudi nimtafutie mke, aoe mwanamke wa huku na atulie”

“Labda pengine hiyo ndo sababu hataki kurudi”

“Sijamueleza mpango wangu wa kumuozesha mwanamke wa huku, nataka siku ambayo atarudi ndipo nimueleze”

“ni mtoto wako sidhani kama ukimueleza atakataa sababu unalojaribu kumfanyia ni jambo zuri” Meshack alitabasamu

“unajua Meshack una busara sana ndo maana naipenda kampani yako! Haya twende ndani tukapate chakula maana tayari Mama amesha kitenga mezani”

Meshack alishindwa kukataa, aliongozana na Mzee Simon wakaingia ndani kupata chakula. Kitu alicho kigundua ni kwamba ile familia ilikua na upendo sana kiasi kwamba hawakua wakiwadharau watu wenye kipato cha chini kama yeye.

Je nini kitaendelea?
Nakuja……..


SEHEMU YA : 04

Ule ushauri ambao Meshack alimpa Mzee Simon aliufuata. Jioni Mzee Simon alimpigia kijana wake kwa njia ya whatsapp na kuzungumza nae

“umegoma kabisa kurudi nyumbani?” Alilalamika Mzee Simon

“baba kwani kuna ulazima wa kurudi sasa ivi?” Sauti nzito ya kiume ilisikika upande wa pili

“Ndio, tangu uende kusoma huko hujawai kurudi kabisa hata kipindi cha likizo, je unajua ni kiasi gani mama yako amekua akiteseka sababu yako?”

“najua, ila tu kuna mambo yangu nataka kuyaweka sawa ndipo nije!”

“Lini sasa maana nataka kuanza harakati za kukutafutia mke wa huku”

“oooh! Ndo maana una ng’ang’ania sana nirudi? Hakuna shida mzee, we nitafutie mke mzuri wa kuoa!”

Mzee Simon aliposikia vile hakuamini alicho kisikia, alidhani pengine akimwambia mwanae anaweza kupinga kama walivyo vijana wengine.

“Umekubali mimi kukutafutia mke?”

“Ndio Baba! Ila nataka mke mzuri mwenye upendo na adabu, icho tu wala hata sitaki mambo mengi”

“Daah! Colfrey kijana wangu hakuna siku uliyonifuraisha kama leo, na kuhusu mke wako hata usijali, nitahakikisha unapata binti mzuri wa kukufaa”

“thanks Baba”

“Haya acha nikuache upumzike, uwe na siku njema”

“Sawa Babaa”

Simu ilikatwa kisha baada ya pale Mzee Simon akaenda kumueleza Mkewe zile habari nzuri.

“Kwaiyo kakubali kurudi! Jamani” mkewe alifurai

“na pia kakubali tumtafutie mke mzuri”

“Kweli? Sasa tutapata wapi binti wa kumfaa mtoto wetu? Mbona hapo ni mtihani maana hakuna binti yoyote ninae mjua ambae atamfaa Colfrey”

“Hili jambo halihitaji haraka sana, tutapata tu mabinti wazuri! Au unaonaje kuhusu ilo?”

“Sawa mume wangu tusitumie nguvu kubwa tusije tukaharibu maisha ya mtoto wetu kwa kumtafutia mwanamke wa ajabu”

“ni kweli na amesema anataka mwenye upendo na adabu”

“kwa miaka ya sasa ni ngumu kuwapata mabinti wa namna hiyo maana wengi wao wanayaweka mbele maslahi yao ya pesa”

“Na hapo ndipo ninazidi kupata stress, sitaki binti ambae atampendea pesa mwanangu”

“Hahaaha unaongea utadhani umesahau jinsi gani kijana wako alivyo handsome!” Alisema mkewe

“Kweli kabisa, tunawakati mgumu sana kuchagua”

“Ni kweli ila tutafanikiwa tu” Alitabasamu

Mzee Simon alikua na shauku sana za kumuambia Meshack zile habari, akaona kama siku ya alhamisi inachelewa kufika.

Na hata ilipofika aliona kama Meshack alichelewa kufika. Ivyo akatoka mpaka nje ya geti lake kumsubiria.

Meshack alipowasili alishangaa kumuona Tajiri yake akiwa nje ya geti na sio kawaida yake. Akapata mashaka labda kuna kitu kibaya alikifanya ndo ikawa sababu ya yeye kusubiriwa kwa hamu namna ile.

“bora umekuja, njoo nikupashe habari” Mzee Simon alimvuta Meshack mkono na kuingia nae ndani

“Kuna nini?”

“Ni kuhusu Colfrey”

“Colfrey? Ndo nani?” Meshack alishangaa anatajiwa jina la mtu ambae hakua akimfahamu

“kijana wangu, jina lake ni Colfrey”

“Anhaaa” Meshack akashusha pumzi ndefu sababu alikua amejawa na uwoga apo mwanzo

“Amekubali kurudi nyumbani na kubwa zaidi amekubali nimtafutie mke”

“kweli? Hongera Mzee wangu! Kijana wako ni mtiifu kuliko nilivyo tarajia”

“hata mimi mwenyewe sikutarajia nahisi Canada imempa busara na utiifu zaidi. Ila shida ni kwamba hatujui jinsi wa kumpata binti mzuri kwaajili ya Colfrey”

“Mhhh! mna marafiki wengi wenye mabinti wazuri, nina uhakika hamtakosa atake mfaa”

“sisi tunataka binti wa tofauti, binti ambae ana adabu na anaejua nini maana ya ndoa. Hawa mabinti waliolelewa na kukulia kwenye maisha mazuri ni ngumu sana kudumu kwenye ndoa, nahisi unaelewa ninacho maanisha”

“ndio mzee nakuelewa vizuri sana”

“Ila naimani mambo yataenda vizuri tu, haya nichongee madafu ninywe mimi, leo nina furaha mno”

Meshack bila kuchelewa akaianza kazi yake, dakika 10 sio nyingi akawa ameshamaliza madafu yote aliyokuwa nayo.

Kisha baada ya hapo Mzee Simon akamlipa hela yake na akampa na mapocho pocho mengine. Tena mda huu alimpa mapocho pocho mengi kushinda mara ya kwanza sababu tu, alikua na furaha.

Basi Meshack hakukataa, alibeba kila kitu na kuja navyo nyumbani. Kama kawaida nilipomuona nikampokea huku natabasamu.

“na leo amekutunuku tena?” Nilimuuliza

“Ndio, alikua na furaha sana leo”

“Imekuaje kwani?”

“yani si unakumbuka nilikuambia kuhusu kijana wake?” Meshack alikaa kwenye kigoda na mimi nikakaa pembeni yake

“Ndio, ulinambia wiki iliyopita”

“Enheee basi kijana wake amekubali kurudi nyumbani na amekubali kutafutiwa mke na baba yake”

“Ni vijana wachache wanaokubali ilo swala” nilishangaa

“Hata mimi sikutegemea kabisa, kutafutiwa mke sio jambo rahisi hata kidogo”

“Kwaiyo wameshampata mke mwenyewe? Ama bado?” Niliuliza kwa shauku

“Bado, ndo wanaumiza kichwa kumpata binti mzuri! Unajua Tunu ilibaki kidogo nimwambie Mzee Simon kuhusu wewe”

“Kwanini sasa?” Nilitoa macho

“Unafaa kuolewa pale! Una adabu na upendo pia, kubwa kuliko ni mrembo. Ingependeza zaidi kama ungeishi maisha mazuri ya kule na ukatoka kwenye maisha ya shida unayo yaishi hapa” Meshack aliongea kwa huzuni

“mmh hapana! Hata sihitaji kuolewa huko, ila asante kwa kunifikiria” nilikataa

“Sasa kwanini unakataa? Nikiongea na Mzee Simon hawezi kukutaaa tena ndoa itafungwa haraka iwezekanavyo”

“kaka Meshack mimi sitaki kuombewa ndoa, nataka pindi nitakapo kubali kuolewa iwe imetoka moyoni na sio vinginevyo. Mwanaume nitakae mchagua mimi atakua kafanikiwa kuzitikisa kuta zote za moyo wangu”

“Umeongea pointi Tunu”

Nilitabasamu kusikia Meshack amekubaliana na mawazo yangu. Kumbe wakati tukizungumza yale Lydia alikua kasimama pembeni akitusikiliza.

Zile habari akazibeba kama zilivyo na kwenda kumueleza Mama yake na dada zake waliokuwa wamekaa chumbani.

“Mama! Mama! Mama! Nimesikia habari nzito huko nje!” Alisema Lydia kwa pupa

“Habari gani bhana wewe, watu tumeshajichokea zetu” alijibu Mama kiuvivu

“huko nje Kaka Meshack alikua anamuambia Tunu kuhusu habari za Tajiri yake, kuwa eti anatafuta mke kwaajili ya kijana wake! Chaajabu Kaka Meshack anataka Tunu ndo aolewe na mtoto wa Tajiri yake, ina ingia kichwani kweli?”

Waliposikia vile wakawa kama wamepigwa na shoti. Ni wazi hawakupenda kile walicho kisikia hasa Mama ambae alikunja hadi sura.

Je ni nini Kitaendelea?
Nakuja……….


SEHEMU YA : 05

“una hakika na ulicho kisikia Lydia?” Mama aliuliza

“Ndio mama nimesikia kwa masikio yangu mawili Kaka Meshack akimuambia ivyo Tunu”

“Enhee Tunu akajibu nini?” Lulu akadakia

“amekataa”

“Na bora angekataa au unadhani ningeruhusu aolewe kwenye familia ya kitajiri ilihali hapa nyumbani nina mabinti zangu walimbwende? Sasa niwaambie tu mabinti zangu, hii nafasi ni yenu”

“Hatujakuelewa Mama” Tamara alisema

“nataka huyo kijana wa Boss wake na Meshack aoe mmoja kati yenu. Na tukifanikiwa tu basi maisha yetu yanakwenda kuwa mazuri zaidi! Au nyie hamtaki ivo? Mnataka Tunu ndo aka enjoy utajiri? Na kumbukeni Tunu akifanikiwa tu basi hatutaishi kwa amani huku ndani”

“Hatutaki iwe ivyo Mama” walijibu kwa pamoja

“Sasa basi fanyeni juu chini ili mfanikishe”

“sasa Mama tutafanikishaje?” Aliuliza Lydia

“Mbona ni rahisi tu? Embu sogeeni karibu niwa ng’ate sikio”

Wote walisimama wakamsogelea mama yao na kusikiliza kwa makini kile walichokuwa wanaambiwa. Mpango wa Mama ulikua mzuri kwani walianza kucheka na kugonga baada ya kumaliza kung’atwa sikio.

“Mama wewe ni balaa, leo ndo nimeamini kwakweli” alisema Lydia huku akicheka

“mama yetu ndo sterling sasa! Na usijali mama tutahakikisha ilo linatimia” Tamara alitilia msisitizo kisha wote wakaendelea kucheka.

Basi, ilifika siku nyingine ya alhamisi! Mimi mapema nilienda kwenye vibarua vyangu nikamuacha Meshack anayafunga madafu yake vizuri kwenye baiskeli ili awahi nyumbani kwa Mzee Simon.

Kabla hajaondoka alishangaa kuona dada zake na wao wakiwa wamejiandaa, tena wamerembeka na kuvaa nguo za heshima juu.

“Kwani kuna mtoko ambao mimi sina taarifa nao?” Alitania Meshack sababu walipendeza vibaya mno

“Hatuna sehemu hata ya maana tunayo enda. Tumeona tukusindikize kwa tajiri yako leo, angalau na sisi tupate elimu kidogo ya namna gani unavyo uza madafu” alijibu Tamara huku akitabasamu.

Meshack aliwashangaa sababu hawakuwai kufanya vile kabla. Na mbaya zaidi hawakuwai kuipenda biashara yake sasa kwanini ghafla tu watake elimu? Alijua kuna jambo tu sio bure

“Ila siwezi kwenda na nyie”

“Kwanini kaka?” Lulu alikunja uso”

“Lile ni eneo langu la kazi, siwezi kwenda na ndugu zangu tena ukizingatia ni nyumbani kwa watu” Meshack alijaribu kuwaelewesha ila hawaku msikia

“Sisi tunataka kwenda alafu mbona kama unatubania,? Kwani ni vibaya kwenda kumsalimia Tajiri yako na kumshukuru kwa mambo mazuri anayo tufanyia sisi?” Tamara alizidi kutilia uzito

“Aya basi twendeni wote” Meshack hakutaka mambo mengi, aligeuza baiskeli yake na kuikokota kuelekea nyumbani kwa Mzee Simon huku dada zake wakimfuata nyuma.

Walipokuwa wamefika macho yakaanza kuwatoka akina Tamara. Lile lilikua ni jumba kubwa la kitajiri na magari ya kutosha hapo nje, wakajawa na tamaa zaidi ya kuishi maisha ya kifahari ya mule ndani.

Muda huo Mzee Simon alikua amekaa na mkewe kibarazani wakisoma magazeti ya asubui. Mara geti likafunguliwa akaingia Meshack akiwa kaambatana na mabinti wa tatu.

“Wale ni akina nani?” Mke wa Mzee Simon aliuliza

“Mhhh! Subiri kidogo pengine Meshack atatupa jibu la maswali yetu”

Na kweli wakamsubiria Meshack kwani aliwafuata hadi pale walipokuwa wamekaa na kusema

“Sidhani kama mtakua mmependezwa na hili, ila dada zangu wameona ni heri waambatane na mimi siku ya leo” Meshack aliongea kwa mashaka.

“Meshack! Kumbe una dada wazuri namna hii?? Hata hukuwai kuniambia” Alisifia Mzee Simon huku mkewe akimsapoti

“Ni wazuri kweli kweli na nguo zao za heshima”

“Ndio dada zangu ni warembo, huyu wa kwanza ni Tamara, wa pili ni Lulu na watatu ni Lydia” Meshack akawatambulisha pale kisha na wao wakatoa salamu zao kwa adabu.

Mpaka pale Mzee Simon na Mkewe wakawa wametokea kuwapenda Tamara, Lulu pamoja na Lydia. Wakatamani sana kama mtoto wao Colfrey angeoa mmoja kati yao.

Ivyo baada ya kupata madafu, Mzee Simon akamuita Meshack pembeni.

“Meshack madafu ya leo yamekua matamu sana” alimsifia

“Kweli Mzee? Nimechagua mazuri kwaajili yako”

“Unajua kwanini madafu yakazidi kuwa matamu? Ni kwasababu ya ujio wa dada zako!”

“Ohh Mzee, ni vile walisisitiza sana na mimi sikuweza kuwakatalia”

“Ilo halina shida kabisa maana umetatua fumbo ambalo tulikua tunajaribu kulitatua kwa haraka sana”

“Fumbo gani Mzee?” Meshack akauliza akiwa haelewi chochote

“Fumbo la mke wa Colfrey, natamani kama kijana wangu angeoa moja ya dada zako”

Meshack alishtuka nusu ya kuzimia, hakutarajia kama lile lingetokea, na pale pale akajua ni kwanini dada zake waling’ang’ania kuongozana nae siku hiyo.

“Mbona mapema ivo? Hata hamjuzijua tabia zao Mzee”

“Meshack, kama wewe una busara na adabu kiasi hiki ni wazi hata dada zako wapo ivo ivo”

“Mzee alafu sisi na nyie ni matabaka mawili tofauti, sisi ni maskini wa kutupwa ambao tunategemea hela ya madafu na vibarua ili tupate kuishi”

“Unadhani sisi tunajali matabaka? Tungekua tunajali matabaka basi huku ndani usingeweza kuingia hata kwa bahati mbaya, wala tusinge kuchukulia kama mwanafamilia! Meshack kwetu sisi upendo ni kitu cha kwanza ndio maana tumeweza kuishi na wafanyakazi wetu kwa kipindi kirefu! Mpaka hapo umepata jibu la swali lako?”

“Ndio mzee” alitazama chini

“Haya na mimi nipe jibu langu, je utakubali dada zako waolewe kwenye familia yangu?”

“Ndio Mzee” Meshack alikubali ila moyoni alitamani sana kama mimi ningeipata ile nafasi pale ila sasa alishindwa kumuambia Mzee Simon habari zangu sababu nilikataa kuombewa ndoa

“Vizuri! Hiyo ni habari nzuri, nitamtumia Colfrey picha za dada zako! Atachagua ni yupi alie mpendeza zaidi kisha pindi atakapo rejea tuanze taratibu za ndoa, au unaonaje kuhusu ilo?”

“Hakuna shida Mzee” Meshack hakuchangamka kabisa, alikua mwenye huzuni kwa zile habari.

Basi baada ya kumalizana na Mzee Simon, aliwachukua dada zake kwaajili ya kurudi nyumbani. Wakiwa njiani aliwageukia na kuwaambia

“najua mlisikia maongezi yangu na Tunu alhamisi iliyo pita”

“Maongezi gani?” Walijifanya hawajui

“kwamba Mtoto wa Tajiri yangu anatafutiwa mke! Mliposikia vile mkaingiwa na Tamaa, mkaona mje na mimi ili kusudi muonekane na Tajiri”

“Hahahah ndio, we huoni kama mpango wetu umefanikiwa? Tajiri na mkewe wametupenda na wanataka mmoja baina yetu aolewe pale” Lulu alimjibu

“Alafu kaka wewe sijui una roho ya aina gani? Kweli uliona Tunu ndo anafaa kuolewa hapa na sio sisi ndugu zako wa damu? Unamchagua mtu baki kabisa!” Lydia aliongea kwa uchungu

“Kwasababu nyie focus yenu ni pesa tu na sio kingine! Hamna adabu wala busara, mnakesha nyumbani mkijipamba na kutafuta wanaume wenye pesa! Hamjui kabisa kitu kinacho itwa nidhamu! Mngekua mnajua icho kitu basi mngekuwa kama Tunu”

“We bhana we embu tupishe sisi! Iyo busara na upendo imemfikisha wapi huyo Tunu? Si yupo huko anafua nguo za watu zenye mavi ili tupate kula! Tena unabidi uwe na shukrani kabisa maana kwa siku sijazo sisi ndo tukakuwa tunaihudumia hii familia na sio wewe na madafu yako ama Tunu na vibarua vyake! umenisoma hapo? Aya twendeni” Tamara aliwashika wenzake mkono kisha wakaondoka na kumuacha Meshack akiwa anawasindikiza kwa macho.

Upande wangu baada ya siku ndefu kwenye vibarua vyangu nikawa nimerudi nyumbani usiku. Nikakuta wanafuraha kupita maelezo yani hadi walikua wamefungulia na mziki.

Sikutaka hata kuwauliza chochote, niliwapita na kwenda kuzungumza na Meshack, na ndipo aliponieleza kila kilicho tokea siku hiyo.

“Huwezi jua kaka labda hii ni bahati yao” nilimwambia

“Lakini nilitaka iwe bahati yako, uolewe kwenye familia nzuri ili upate kuishi kama malikia, ama wewe Tunu hutamani maisha hayo?” Alilalamika

“Natamani sana, ila mimi sipendi kuombewa ndoa nishakuambia kuhusu ilo! Nataka mwanaume wangu awe amenipenda kutoka rohoni alafu pili unajua kabisa Mama asingeweza kukubali niolewe pale! We huoni waliposikia tu mazungumzo yetu wakaamua kujipeleka wao ili waonekane”

“Daah umezungumza ukweli Tunu”

“Kwaiyo hata usijali kaka yangu, waache waolewe, wakati wangu mzuri ukifika nami nitaolewa! Tena najua hakuna atakae ingilia ilo swala”

“Mpaka raha yani Tunu, huwa sichokagi kuongea na wewe! Natamani dada zangu wangeiga vitu vichache toka kwako”

“au labda umesahau Mungu hakupi vyote?”

“na kweli, uzuri wote ule na kichwani hakuna kitu” aliposema vile nikajikuta nacheka vibaya mno hadi nikasahau purukushani zangu za siku nzima.

Tukirudi kwa Mzee Simon na Mkewe walikwisha zituma picha za Akina Tamara kwa Colfrey. Na Colfrey alipoziona picha zao akampigia baba yake haraka iwezekanavyo.

“Nilijua tu ukiziona picha utapagawa!” Alisema Mzee Simon huku akicheka

“Ni wazuri, Mungu kweli kajua kuwaumba! Umewatolea wapi baba?”

“Aaah unamkumbuka Meshack?”

“Meshack….. Meshack……. Meshack muuza madafu??”

“Huyo huyo, sasa hawa mabinti ndio dada zake”

“Basi Mungu kawabariki kwa uzuri! Sasa hapa napata wakati mgumu wa kumchagua yupi”

“Chagua yoyote kijana wangu, ukirudi tu mwezi ujao tuanze taratibu za ndoa”

“Mmh! Ingekua vizuri zaidi kama ningezijua tabia zao” alisema Colfrey

“Niamini mimi baba yako! Tumewaona leo ila kwa dakika chache tuliokua nao tumegundua kuwa ni mabinti wenye adabu sana, huwezi amini hadi wamemsaidia mama yako kupika jikoni”

“Kweli kabisa mwanangu, nimewapenda kweli” alisema Mama mtu

“Ok basi nitachagua, ila sitawaambia ni yupi nilie mchagua! Pindi nitakapo rudi ndipo nitaweka chaguo langu hadharani, ila kwa sasa mvumilie na kuendelea kusubiria”

“Hakuna shida Mwanangu! Take your time”

“Sawa Baba acha niende tutazungumza zaidi kesho! Msalimie pia mama apo pembeni”

“sawa kijana wangu”

Simu ilikatwa na mazungumzo yao yakawa yameishia hapo. Je unadhani ni nani atakae chaguliwa na Colfrey??

Nakuja……….


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote