MEI (CHAGUO LA MOYO WANGU)

book cover og

Utangulizi

Mei ni binti wa kishua nikimaanisha wazazi wake wana uwezo wa hali ya juu. Licha ya wazazi wake kuwa matajiri ila haimfanyi yeye kuchagua kazi gani ya kufanya anachojali yeye ni maslahi kwa kile anachokifanya. Mei alijiajiri biashara ya kuuza karanga zilizochanganywa na dawa za nguvu za kiume na kwa siri sana anafanya biashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya. Wateja wake asilimia 99% ni wanaume. Hali hiyo inamshangaza kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Mr Park. Mr park mala zote anazopita eneo hilo anashangazwa na umati wa wanaume wenzie wakiwa wamepanga foleni kwaajili ya kununua karanga. Siku moja na yeye anajitoa muhanga. Anapanga foleni pia ya kununua karanga za Mei. Baada ya kula zile karanga hali yake inakuwa mbaya sana uume wake unasimama muda wote mpaka anashindwa kuendelea na kikao ofisini. Baada ya kufanyiwa uchunguzi na daktari wake anaambiwa chanzo ni karanga. Anaapia kumkamata Mei na kumpa adhabu stahika ila Ajabu baada ya kuludi kwao muda mchache wanapokea ugeni, Ni binti muuza karanga Mei na wazazi wake. Wazazi wao wanapendekeza watoto wao wawe wana ndoa ili kuhudumisha urafiki wao.......Sheria ya mji huo wazazi ndiyo wenye mamlaka ya kuamua ndoa kwa mkwe wamtakaye na sio mtoto. Mei na Mr park wanafunga ndoa japo hawapendani kabisa......Mei anaendelea na mapenzi ya siri kwa mpenzi wake wa zamani Dan. Mwisho wa siku anamuelewa Mr Park maana yupo vizuri sana kimuonekano hadi kitandani pia. Rasmi wanaamua kuishi maisha ya mke na mume na penzi lao zinazidi kuwa zito kila iitwapo leo. Hali hiyo inamuuma Dan mpenzi wa zamani wa Mie. Anapia lazima amludishe Mei kwenye Himaya ya Moyo wake maana yeye ndo CHAGUO LA MOYO WAKE. Mr Park nae hayupo tayari kumuacha Mei kivyovyote vile. Hapo sasa ndiyo vita ya mapenzi inaibuka mpaka damu za watu zinamwagika........HII SIO YA KUKOSA...........

SIMULIZI : MEI (CHAGUO LA MOYO WANGU)
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 01

MWANZO.
Katika Jiji la Chengdu Nchini China, ambapo gharama ya maisha inapanda kwa kasi kila kukicha, watu wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na maisha. Miongoni mwa watu hao ni binti mdogo Mei, mwenye ndoto ya kuwa mfanyabiashara maarufu. Anajulikana sana kwa kuuza karanga za mayai tamu, bidhaa yake ina ladha isiyoweza kupingwa. Pamoja na kuuza bidhaa hiyo, anajihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya pamoja na virutubisho vya nguvu za kiume kwa siri.

Wateja wake wengi ni wanaume, na kati yao alikutana na mteja mpya, Mr. Park, mwenye shauku ya kujua bidhaa za Mei zina nini kiasi cha Wanaume kukaa kwenye foleni.

Mei anaachia tabasamu baada ya kumuona Mr. Park mteja mpya kabisa. Muonekano wake mzuri ulitosha kumuambia mwanaume huyu atakuwa ni Playboy.
Anaamua kumpatia karanga zilizo changanya na virutubisho vya dawa za nguvu za kiume.

Wakati Mr. Park alipokula karanga hizo, hakuwa na habari kama alikuwa anajichanganya na virutubisho vya dawa za nguvu za kiume, na siku hiyo ilikuwa muhimu sana kwake. Alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yake, lakini alijikuta akishikwa na hamu iliyopitliza kufanya sex, pamoja na kuletewa Malaya wa kutuliza hisia zake lakini bado uume wake uliendelea kusimama, maumivu yalimzidia kiasi kwamba alishindwa kuhudhuria kikao cha Waandishi wa habari.

Daktari wake aligundua ukweli mbaya—karanga alizokula zilikuwa na virutubisho vya kuongeza nguvu za kiume. Mr. Park alihisi makasiriko kupita kiasi, uwezo wa kumkamata Mei bila kushirikisha Polisi alikuwa nao.
Alichukua vijana wake wapatao 20 wakaelekea eneo analopatikana Mei.

Anastaajabu baada ya kumkosa Mei, alipojaribu kuuliza kwa Wafanyabiashara wengine waliokuwa hapa walidai hawajui sehemu alipoenda.

Akiwa hajui ni hatua ipi achukue ujumbe uliingia kwenye simu yake

🌾Njoo nyumbani haraka, familia ya Dr. Henry wapo njiani kujumuika pamoja nasi kwa ajili ya chakula cha usiku🌾 Ujumbe ulisomeka kutoka kwa Mama yake

Anaamua kusitisha ratiba zake kisha akaelekea nyumbani.

"Siku ya leo umahitaji kupendeza kuliko siku zote.....sitaki uniaabishe" Fei (,Mama yake Park) aliongea huku akifikiria ni aina gani ya nguo Kijana wake anapaswa kuvaa.

Akili ya Mr. Park haikuwa mahali hapa, aliwaza ni kwa namna gani atamkamata Mei.

Wakiwa wamekaa sebuleni familia ya Dr. Henry iliwadia.
Fei alimshika mkono Kijana wake kisha wakaelekea nje kuwakaribisha.

Moyo wa Mr. Park ulishtuka baada ya kumuona Mei akiwa katika muonekano mpya.
Pamoja na kumuangalia kwa mshangao lakini Mei hakutoa ushirikiano, aliendelea kukaza sura yake.

Siku zote ni mtu asiyependa kucheka, si mwepesi wa kuachia tabasamu lake hovyo na mbaya zaidi si muongeaji anapokuwa katika muonekano huu.

Fei aliwakaribisha ndani wageni wake, meza ilikuwa imepambwa kwa vyakula vizuri pamoja na vinywaji vya kuvutia.

Mei hakuvutiwa na aina ya vyakula vilivyokuwa mezani, si mtu wa kupenda kula sana.
Mama yake aliligundua hili, alimkonyeza ajitahidi kula hata kama havutiwi na aina ya chakula kilichopo mezani.

Ushikaji wake wa kijiko ulimwakaza Mr. Park na hata akahisi huyu Binti kazoea kupima madawa ya kulevya na si bure

"Kwanini usitumie kijiko cha asili, kula kwa mkono!" Mr. Park aliongea kwa sauti kubwa baada ya kushibdwa kuvumilia

Watu wote walimgeukia, hakuwa tayari kujieleza aliondoka mezani akiwa mwenye hasira kali hasa akikumbuka namna uume wake ulivyomtesa sababu ya karanga za Mei.

Simu ya Mei iliita, yeye pia alielekea nje kuzungumza. Aliusikiliza upande wa pili bila kuongea chochote. Baada ya kuelewa alikata simu.
Ile ana geuka aende ndani alikutana uso kwa uso na Mr. Park.......

ITAENDELEA.......

SIMULIZI : MEI (CHAGUO LA MOYO WANGU)
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 02

ENDELEA......
"Sababu ya karanga zako uume wangu ulisimama karibu siku nzima nikiwa na maumivu makali kupita kiasi, shukuru kuzaliwa katika familia ya Dr. Henry tofauti na hapo ungelipa kwa maisha yako" Mr. Park aliongea

Mei aliachia tabasamu ndani ya moyo wake baada ya kusikia uume wa Mr. Park ulisimama karibu siku nzima.
Alijipa matumaini kuwa dawa zake zinafanya kazi kama alivyo tarajia.

Hakuwa na muda wa kujieleza alitaka kwenda ndani lakini Mr. Park alimtuliza kwa kumshika mkono kwa nguvu

"Wakati unanipatia karanga zako ulikuwa unaongea sana, sielewi kwanini umekuwa bubu kwa sasa sasa au ni kwa sababu umembatana na wazazi wako!" Mr. Park aliuliza

Mei alijitoa kwenye mkono wa Mr. Park, hakuongea chochote alielekea ndani. Hakutaka kumkwaza Mama yake, alikula chakula ilihali hakuwa akifurahia.

"Binti yako ni Mrembo hakika kuna haja ya sisi kuzungumza kuhusu harusi yao" Fei alipendekeza

"Na ndio sababu niko hapa, sikuja kufurahia chakula chako tu, Kijana wako kawa na muonekano wa kipekee, sifa zake nzuri katika midomo ya watu zinanipa hamasa ya kuona anafaa kuwa Mume wa Binti yangu" Dr. Henry aliongea

Wazazi wote wa pande mbili walionekana kuridhia, linapokuja swala la ndoa katika Jiji la Chengdu Watoto huwa hawapatiwi nafasi ya kueleza hisia zao.

Mei aliendelea kutafuna ilihali ndani ya moyo wake akiwa mwenye hasira kupita kiasi. Alipenda maisha ya uhuru na si kummilikiwa na Mwanaume tena asiyempenda.

Mr. Park alirudi ndani pia baada ya Mama yake kumtumia ujumbe kuwa wageni wanataka kuondoka.

"Siku yangu haikuwa nzuri sana siku ya leo na hata Daktari alikuja kunifanyia vipimo. Naomba mnisamehe kwa kuwaacha mezani pekee yenu" Mr. Park aliongea

"Nilikasirika hakika kuona Mwanaume mwenzangu kaniachia meza wenye wanawake tupu, lakini kwa kuwa muda si mrefu utamuoa Binti yangu sina haja ya kukasirika" Dr. Henry aliongea huku akiacheka

Mr. Park alishtuka ndani ya moyo wake kusikia atamuoa Mei. Alionesha tabasamu la uongo mbele ya Wageni. Alipo hakikisha wameondoka alimfuata Mama yake apinge kuhusu harusi.

"Baba yako angekuwa hai angelipitisha hili pia, familia ya Dr. Henry wanajiweza kifedha ikitokea una changamoto huko mbeleni itakuwa rahisi kusaidika. Naomba usisahau kama Dr. Henry ana pendezwa na matendo yako" Fei aliongea kisha akaondoka

Mr. Park alibakia kusimama tu.

Upande wa Mei akiwa chumbani kwake aliangulia kilio bila kutoa sauti, tayari ndani ya moyo wake alikuwa na mtu anayempenda zaidi. Japo Mwanaume huyo hakuwa na maisha lakini moyo wake ulimuelewa kupita kiasi.

Baada ya kuhakikisha wazazi wake wamelala alitoroka akaenda kuonana na Dan

"Nimesikia wazazi wako wamependekeza ndoa kwa ajili yako..." Dan aliongea huku akilazimisha tabasamu la uongo

"Naomba unisamehe.... siwezi kwenda kinyume na wazazi wangu lakini always utabakia kuwa kipenzi cha moyo wangu. Ndoa yangu na huyo Mwanaume itakuwa pambo tu" Mei aliongea

"Ni rahisi kusema hivi lakini kadri utakavyozidi kumuona kwenye macho yako kila siku nina uhakika utasahau kuhusu Mimi" Dan aliongea

"Si rahisi kwangu kufanya hivyo...." Mei aliongea kisha akambusu mpenzi wake, hawakuishia hapo walijikuta wakifanya mapenzi

Kulivyo pambazuka Mr. Park alielekea ofisini akiwa mwenye hasira kupita kiasi kila akikumbuka anatakiwa kumuoa Mei siku za karibuni.

Kila alichofanya kilikuwa ni kigumu kwake.....
"Nitaenda nje kutuliza akili yangu, kuhusu yule aliyeniuzia karanga zenye virutubisho za nguvu za kiume achana naye nimeshampata" Mr. Park alimuambia Secretary wake

Hakutaka kuongozana na mtu, alitembelea barabarani akitamani kama angekuwa viatu na si binadamu mwenye maji na damu.

Akiwa katika kufikiria, alishtuka baada ya kupokonywa simu yake na Kibaka asiyejulikana ametokea wapi.

Bahati nzuri Dan alikuwa anapita maeneo haya, uwezo wake ulikuwa ni mkubwa sana. Kufumba na kufumbua alimkamata mwizi.

Mr. Park alifurahishwa na uwezo wake, badala ya kuchukua simu alitega mgongo akaendelea na safari yake

"Ume...u...umeniachia simu" Dan aliuliza akiwa haamini

"Kuanzia leo wewe ni bodyguard wangu nifuate..." Mr. Park aliongea

Dan hakuamini masikio yake kama kapata kazi, anamfahamu Mr. Park kupitia kazi zake.
Na hata amewahi kutamani kama angezaliwa kama mtoto wa Fei ili aitwe tu Mr. Park.

Kwa pamoja walirudi ofisini, Dan alipatiwa suti kali tayari kwa kuanza kazi.

Alimtumia ujumbe Mei kwa siri kuwa amepata kazi.

Mei akiwa ana fanya mazoezi ya kutembelea viatu vya harusi aliachia tabasamu kuona kipenzi cha moyo wake kimepata kazi.
Alijikuta akipata nguvu ya kutembea na viatu bila kuanguka.

Mama yake aliachia tabasamu baada ya kuona Binti yake ameelewa haraka.

Hatimaye siku ya harusi ilipangwa, bahati mbaya Mr. Park alipata dharula.

"Hatuwezi kusitisha harusi.....hata bila Park lazima harusi ifanyike" Fei aliongea

Dr. Henry na mkewe walionekana kuridhia.

Mamia ya watu walialikwa kwenye Ukumbi wa Skylines. Watu wengi walikuwa na shauku ya kuwaona Maharusi.
Wakati Mei akiingia ukumbini akiwa kabeba picha ya Mumewe mtarajiwa.
Mr. Park na Dan walipanda ndege kuelekea Tanzania.

Mei alivalishwa pete na Fei kwa niaba ya kijana wake.
Picha za kumbukumbu zilichukuliwa kisha Pastor akamtangaza rasmi kama Mrs. Park.

Kwa mara ya kwanza kabisa alilala kwenye kitanda cha Mr. Park. Hakuweza kupata usingizi kila alipofikiria kupoteza uhuru wa kufanya biashara zake haramu alizozizoea.......

ITAENDELEA.....

SIMULIZI : MEI (CHAGUO LA MOYO WANGU)
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 03

ENDELEA...
Wiki mbili zilikata bila Mr. Park kurejea, Fei alielewa Kijana wake anafanya makusudi kukaa Tanzania muda mrefu akikwepa kuonana na mkewe.

Aliamua kujirekodi video akitapika damu kisha akamtumia Kijana wake.
Baada ya Mr. Park kuipata video ya Mama yake akitapika damu alifunga safari kurudi Jijini Chengdu.

Upande wa Mei akiwa ana furahia ndege waliokuwa kwenye bustani ya Fei, alishtushwa na ujio wa Wafanyakazi.

"Kesho Mr. Park atakuwa hapa hivyo kuanzia sasa unatakiwa kukaa ndani....tutahakikisha muonekano wa ngozi yako unakuwa mzuri zaidi ya hapa" Mfanyakazi aliongea

Mei hakuwa na la kusema katika hili, aliingizwa bafuni kisha kazi ya kumuogesha kila sehemu ilianza.

Fei alikuja kukagua mambo yanavyoenda, aliachia tabasamu baada kuona mkwe wake ana umbo zuri kupita maelezo.
Alifurahia ndani ya moyo wake kuona Kijana wake atafaidi maisha yake yote.

Siku iliyofuatia ikiwa ni mida ya jioni, Mr. Park alimtumia ujumbe Mama yake kuwa yupo tayari ndani ya Jiji la Chengdu.

Fei aliachia tabasamu, alienda kuhakikisha kama Mei yupo kwenye muonekano mzuri.
Akiwa ana msubiria Mumewe, alipatiwa chai yenye karafuu ili kuongeza joto ukeni.

Upande wa Mr. Park akiwa na Dan anawasili nyumbani kwao.
Anashangaa kuona picha ya Mei ikiwa ukutani amevalia shela.
Hakuamini kama ndoa iliwezekana hata bila uwepo wake.

Dan ndio kushtuka kuiona picha ya kipenzi cha moyo wake. Hakuamini kama boss wake ndio Mume wa Mei.
Alijilaumu kwanini hata hakuuliza, pengine asingekubali kuwa Bodyguard wa huyu Mwanaume.

Mr. Park alielekea chumbani kwake akiwa mwenye hasira ndani ya moyo wake, anashtuka baada ya kumkuta Mei akiwa kakaa pozi la kusubiliwa kuliwa.
Hakujua anaanzia wapi kumuongelesha, aslimia kubwa ya maungo yake yalikuwa wazi.

Sehemu zake zilianza kufurukuta hasa akikiangalia kifua cha Mei. Taratibu alimsogelea asijue ni kitu gani anapaswa kuongea

"Ni....ni...ni...saidie kulegeza tai" Mr. Park aliongea

Mei akiwa amesoma vitabu saba vinavyo elezea namna ya kujali Mume alisimama huku akitembea kwa mwendo wa kunyata, alimsaidia kutoa Mume wake tai pamoja na shati.

Moyo wake ulipasuka baada ya kuona mwili wa Mwanaume huyu ulivyojengeka kana kwamba ana nyanyua vyuma. Aligeukia pembeni haraka huku akikikumbuka kifua cha Dan kisichokuwa na mambo mengi kama hiki.

Mr. Park akiwa mwenye uchu wa kutuliza maumbile yake alimshika Mei kiunoni.

"Nj....ni... nipo period" Mei aliongopa.

Mr. Park akiwa anahema kwa kasi alielewa, aliingia bafuni akaoga.
Baada ya kumaliza alivaa vizuri, alitaka kujitoa out pekee yake. Lakini baada ya kukumbuka namna Mama yake alivyomtumia video akiwa anatapika damu hakutaka kumkwaza. Alimuambia Mei ajiandae pia,

Dan akiwa sebuleni alibakia kumkodolea macho Mei akiwa na Mr. Park.........

ITAENDELEA.......

SIMULIZI : MEI (CHAGUO LA MOYO WANGU)
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 04

ENDELEA........
Mei pia alibakia kumtazama Dan, Mr. Park hakuwa akifahamu kama wawili hawa wana fahamiana.

Alimpokonya mkewe mkoba akampatia Dan.
Ni jukumu lake kubeba mkoba lakini kwa kuwa Mwanamke huyu hakuwa chaguo lake hakuona sababu ya kujipendekeza.

Alimrushia pia Dan briefcase yake....Mei hakupendezwa na hiki kitendo aliamua kuvibeba vitu vyote yeye.

Kwa pamoja waliingia kwenye gari, Dan alikaa seat ya mbele kisha wao wakakaa seat ya nyuma.

Walipita sehemu ambayo barabara ilijulikana kama snake road kutokana na namna ilivyojengwa.

Mr. Park na Mei walijikuta wakilaliana mara kwa mara sababu ya gari kulazimika kwenda kama nyoka.

Kwa bahati mbaya midomo yao iligusana....hakuna aliyekuwa tayari kushiriki busu na mwenzie walijitoa haraka.

Wanafika katika hotel ya Shangri La.... Ulinzi wa sehemu hii ulikuwa umeimarishwa zaidi.
Dan alitaka kubakia nje lakini Mr. Park alimkaribisha pia.

"Kwa kuwa wewe ndio Mwanamke mahali hapa tuchagulie chakula" Mr. Park alimuambia mkewe

Mei aliagiza chakula, muda wote macho yake yalikuwa kwa Dan. Mr. Park hakulitambua hili kwa sababu alikuwa busy kuchat na mmoja wa Wahudumu wa kike anayepatikana hapa.

"Nipeni kama dakika 40 nitakuwa hapa....kuna emergency imetokea nahitaji kutatua. Please usinifuate" Mr. Park alimuambia Dan baada ya kuona ana simama pia.

Moja kwa moja alielekea ghorofa ya juu zaidi, hakupoteza muda. Alifanya mapenzi na Mhudumu aliyekuwa akimuelewa linapokuja swala la ngono.

Huku nyuma, Mei alihitaji kwenda chooni. Isingekuwa rahisi kwa Dan kumuacha mke wa Boss kwenda pekee yake. Alimfuata kwa nyuma pia....baada tu ya kuingia chooni, Mei alifunga mlango kisha akamparamia Dan. Walianza kubadilishana mate, hawakuishia hapo Mei alishika ukuta wakavunja amri ya sita.

Mr. Park anakuwa wa kwanza kurudi kwenye kiti, ana shangaa kumkosa Dan na mkewe. Ile anataka kuwa fuatilia, aliwashuhudia wakishuka kwenye ngazi.

Baada ya Mei kukaa kwenye kiti aligundua....Mr. Park katoka kulala na Mwanamke.
Alifurahi ndani ya moyo wake kuona Mwanaume huyu kamaliza haja zake kwa Mwanamke mwingine.

Baada ya outing kuisha waliondoka, safari hii Mr. Park na mkewe walikaa mbele.
Uendeshaji wake wa gari ulikuwa wa fujo sana hasa akifikiria usiku wa leo anaenda kulala na Mwanamke aliye chaguliwa na Mama yake.

Mei aliingilia kati kwa kushika usukani, alianza kuendesha mwenyewe kwa mwendo alioona unafaa.

Walivyoingia chumbani kila mmoja alionekana kuwa na uhitaji wa kutumia bafu, kwa kuwa Mr. Park alikuwa na haraka alitangulia yeye kwanza. Baada ya kumaliza Mei alielekea bafuni pia, anaachia tabasamu baada ya kumuona Mumewe amelala tayari.

Kama kawaida yake alihakikisha anakuwa katika muonekano mzuri hata kama anaenda kulala. Wakati anafanya mbwembwe zote, Mr. Park alikuwa ana mtazama.

Japo hakuwa akimpenda huyu Mwanamke lakini alivutiwa na umbo lake.
Mei anapanda kitandani akiwa mwenye amani ndani ya moyo wake hasa akifikiria kuwa Mr. Park amelala.

Ghafla alishangaa mkono unatua kwenye nyonyo zake.
Alijitetea kuwa yupo period bado lakini Mr. Park alipenyeza kidole kwenye nguo yake ya ndani kujihakikishia.

Anaachia tabasamu baada ya kugundua mkewe ni muongo.
Pamoja na kwamba Mei hakuwa na hisia na huyu Mwanaume lakini baada ya kushikwa kila sehemu alitulia na hata akawa tayari kwa lolote.

Hakutaka kuonekana mzembe alionesha ufundi wake pia kama anavyokuwa kwa Dan.

Mr. Park ana kurupuka usingizini kukiwa kumepambazuka, anashtushwa na ulalaji wa Mei. Alimsogelea tararibu akaanza kumkagua kucha zake, zilikuwa zinavutia, lakini kwa namna zilivyo ndefu aligundua zinatumika kupimia madawa ya kulevya, alichukua nailcuter akaanza kukata, kwa jinsi Mei anavyopenda kucha zake alirikurupuka usingizini.......

ITAENDELEA......

SIMULIZI : MEI (CHAGUO LA MOYO WANGU)
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 05

"Weee Mwanaume nani kakupa kibali cha kushughulika na kucha zangu..." Mei aliuliza huku akiangua kilio

Kilio chake kilimfikia Dan aliyekuwa nje akifuta gari la boss. Bila kufikiria mara mbili alikimbia mpaka mlangoni kwa Mr. Park akiwa kakunja ngumi tayari kwa kufanya maangamizi.

Anajikuta ana tabasamu baada ya kusikia Mei analia sababu ya kucha yake moja kukatwa.

Fei (Mama yake Park) alifika mlangoni pia kujua nini kinaendelea, anaachia tabasamu baada ya kuona mkwe wake ana kichaa kikali.

"Nafurahi kuona wameanza kucheza michezo ya kitoto...." Fei alimuambia Dan kisha akamtaka waondoke

Mr. Park alijikuta akitamani kukata kucha zote lakini Mei alikuwa mbishi, walifukuzana huku na kule.
Mei alikuwa hatanii, safari hii alishika mto akaanza kumpiga nao.

"Ni kucha moja tu vipi kama ningekata yote...." Mr. Park aliuliza akiwa mwenye tabasamu usoni.

"Hilo tabasamu unanionesha Mimi!" Mei aliuliza kwa mshangao kwa sababu hawakuwa wamefikia hatua ya kuoneshana matabasamu.

Mr. Park alijishtukia pia kwa kuachia tabasamu lake kwa muuzaji wa dawa kulevya.
Aliingia bafuni akaanza kuoga, wakati anajipaka povu kichwani alikumbuka kiuno cha mkewe.

Japo hakuwa na hisia naye lake alijikuta akimtamani. Ile anatoka bafuni alikutana na Mei akiwa ana subiria kuingia bafuni, alimpisha.... hakutaka kuvaa badala yake aliendelea kumsubiria.

Mei anashtuka baada ya kumkuta Mumewe akiwa na taulo bado. Hakujua ni kitu gani anapaswa kusema....kwa mara nyingine walijikuta wakifanya mapenzi tena.

Dan anafika mlangoni kwa mara nyingine amkumbushe boss wake kuhusu kuchelewa kazini, anapoa baada ya kukutana na sauti ya Mei akionekana kufurahia dozi anayopatiwa.

Moyo wake ulimuuma kupita kiasi, hakutaka kuendelea kuwa msikilizaji

Mr. Park anaelekea kwenye gari akijihisi mwepesi, kama kawaida yake alimsalimia Dan kwa tabasamu pana. Kwa pamoja waliingia kwenye gari.....

Huku nyuma, Mei alijifunika gubigubi huku akikumbuka kila hatua aliyokuwa anafanyiwa na Mr. Park mpaka akaridhika.

"Naogopa nitamsahau Dan kwa haraka kama nitaendelea kukutana na Mr. Park, ingawa simpendi lakini anajua kuniridhisha,....." Mei alijisemea ndani ya moyo wake huku akikumbuka namna alivyokuwa anauza madawa ya kulevya na karanga zenye virutubisho vya kuongeza nguvu za kiume. Aliyatamani haya maisha ya kufukuzana na Polisi bahati mbaya alizaliwa katika familia inayojiweza.

Upande wa Dan baada ya kupata wasaa wa pekee yake, alifikiria ni kwa namna gani ataweza kumrudisha Mei mkononi mwake.

Njia aliyopata ilikuwa ni moja tu, kujiunga na kikosi hatari cha Uuzaji madawa kulevya kilichokuwa Jijini Chengdu. Kupoteza maisha ilikuwa ni kugusa kwa sababu muda wote kikosi hicho hufukuzana n Polisi.

Aliona ni bora kufa akiwa ana pambana kwa ajili ya Mei na si kukaa tu akishuhudia Mr. Park akimfaidi.

Wazo la kuacha kazi kama Bodyguard wa Mr. Park lilimuijia. Taratibu alipiga hatua kuelekea ofisini kwa boss wake akiwa na sababu mkononi ya kumuachisha kazi......

ENDELEA......


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote