Follow Channel

​​MNADA WA BIKIRA

book cover og

Utangulizi

Kosa moja nililolifanya nikiwa nimelewa… lilizua madhara makubwa kuliko nilivyowahi kufikiria.
Sijawahi kuwa kwenye mahusiano tangu nizaliwe. Sijawahi kumbusu mwanaume, wala kushika mkono wa mtu nikiwa na hisia zozote. Nilikuwa bikira — kwa mwili na kwa moyo.
Sasa niambie, ni kitu gani kingeweza kunisukuma kushiriki mnada wa kuuza bikira yangu?
Na sio mnada wa kufikirika kwenye sinema au kwenye mtandao wa giza. La hasha.
Huu ulikuwa mnada halisi, wa watu halisi, kwenye ulimwengu huu huu wa kawaida.
Na kilichonisikitisha zaidi — ni kwamba watu waliokuwa tayari kulipia hilo walikuwa wengi kuliko nilivyotarajia.
Swali kubwa likabaki: Ni nani anayenunua bikira?
Na kwa nini alinichagua mimi?
SONGA NAYO….

MNADA WA BIKIRA
SURA YA 1

ANDREW
Wakati mkutano wa mji wa Misty Cove, Florida, unamalizika, ninawapungia mkono wafuasi wangu kisha kuelekea kwenye gari langu lililo nje. Ni wakati wa kuruka kuelekea mkutano mwingine kule New York.
Hivyo ndivyo maisha yangu yalivyo—kurukaruka kutoka mkutano mmoja hadi mwingine. Hicho ndicho kinachoniweka kazini, kinachoniletea mabilioni ya pesa mfukoni.
Kabla dereva wangu hajaondoka kutoka kwenye jengo, mlango unafunguliwa. Mama yangu, akiwa amevalia suti yake ya kijivu yenye sura ya kiofisi, anaingia na kuketi kando yangu kwenye siti ya nyuma.
“Si dhani kama ni wazo zuri kuondoka sasa,” anasema kwa sauti yenye ukali wa heshima. “Uchaguzi ni wiki mbili tu kutoka sasa. Unapaswa kutumia muda mwingi zaidi ukichangamana na wananchi.”
Ninapumua kwa nguvu na kupitisha mkono kwenye nywele zangu zenye mawimbi. “Mama, nina mkutano muhimu sana wa wanahisa kule New York. Siwezi kuukosa.”
“Je, huoni kwamba kuwatumikia watu wa mji wako ni muhimu zaidi kuliko kuwaridhisha wanahisa wako?” Macho yake ya buluu—yanayofanana kabisa na yangu—yanang’aa kwa kutoridhika. Sijawahi kukutana na mtu aliyekuwa mwaminifu kwa mji wake kama yeye.
Baada ya kuhitimu chuo kikuu, alikataa kazi Ikulu ya Marekani, ambako alifanya mazoezi ya mawasiliano kwa kipindi cha kiangazi. Hakuweza kabisa kujizuia kurudi nyumbani.
Nina uhakika moja ya sababu zilizomfanya anisukume kugombea umeya ni ili anishikilie karibu naye. Tangu baba yangu alipofariki kwa mshtuko wa moyo mwaka jana, amekuwa kivuli cha yule aliyekuwa zamani. Lakini nilipokubali kugombea umeya, niliona mwanga ukirudi machoni pake.
“Tuondoke, Sam,” namwambia dereva, kisha namgeukia mama yangu tena huku nikiwa na tabasamu dogo mdomoni. “Usijali. Nitarudi baada ya siku chache. Kuna mambo mengi ya kufanya kabla sijachaguliwa kuwa meya.”
Sina shaka hata kidogo kuwa mimi ndiye nitakayeshinda katika uchaguzi huu.
Kwa kuwa nimeweza kuanzisha nafasi nyingi za ajira hapa mjini, haikuwa vigumu kupata wafuasi. Lakini kusema kweli, sijui kama kuwa meya wa Misty Cove, au mji mwingine wowote, ni jambo linalonivutia sana. Sijui kama niko tayari kabisa kurudi kuishi mjini hapa milele. Niliondoka nilipoenda chuo kikuu na nilirudi tu wakati baba alipofariki, ili kumsaidia mama kupitia huzuni yake ya kupoteza mwenzi wake.
“Kuna jambo lingine nilitaka kuzungumza nawe,” mama anasema huku akirudisha nyuma kwa ustadi nywele zake zilizochanganyika na mvi. “Unahitaji kubadilisha baadhi ya mambo katika mtindo wako wa maisha, Andrew.”
“Sielewi unamaanisha nini,” nasema huku nikinyoosha miguu yangu na kuinamisha kichwa nyuma, nikijaribu kuondoa maumivu ya kichwa yaliyosababishwa na ukosefu wa usingizi wa muda mrefu. Ingawa nimekuwa nikiishi Misty Cove kwa mwaka mzima sasa, mara kwa mara huwa nasafiri kote duniani, na makazi yangu ya pili yako New York ambako kampuni yangu ina makao yake makuu.
“Usijifanye kama hujui ninachozungumzia.” Midomo yake sasa imekunjamana. “Unakimbiza saana sketi. Hilo lazima likome. Ni wakati wako wa kukua sasa.”
Natikisa kichwa kwa kuchanganyikiwa. “Mama, nina miaka ishirini na minane. Mimi ni mtu mzima. Na kile ninachokifanya katika maisha yangu binafsi hakiwezi kuathiri uwezo wangu wa kuwa meya bora zaidi kuwahi kutokea katika mji huu.”
“Usiwe mwepesi wa kuamini mambo, mwanangu.” Anavuta pumzi kwa nguvu. “Ukishakuwa meya, huna tena maisha binafsi.”
Ninatazama nje ya dirisha gari linapopita kwa kasi karibu na duka la icecream nililokuwa napenda sana nilipokuwa mtoto. Kisha namshika mama mkono na kuushika kwa upole. “Naahidi kuwa makini sana.”
“Umakini haujawahi kuwa silaha yako kuu.” Anauvuta mkono wake kutoka kwangu na kuchanua nywele zangu kama alivyokuwa akifanya nikiwa mtoto. Wakati mwingine huonekana kusahau kuwa mimi sasa ni mwanamume mzima. “Wakati umefika wa wewe kutulia. Acha kufuata sketi fupi ovyo ovyo na ujitafutie msichana mwema. Wapo wengi hapa mjini. Unapaswa kuanza kufikiria kuhusu ndoa na watoto.”
“Mimi si mtu wa kuoa,” nasema kwa sauti thabiti. “Na ningefurahi kama tusingerejea kwenye mjadala huu tena.”
“Upuuzi mtupu, Andrew. Siku moja utampata msichana atakayebadilisha mawazo yako hayo.”
“Nashuku sana hilo,” nasema huku nikinyanyua chupa ya maji na kujimiminia glasi. “Unataka?”
Anatikisa kichwa. “Kuna jambo moja tu ninahitaji kutoka kwako,” anasema kwa msisitizo huku uso wake ukionekana kuwa mzito zaidi. “Jiweke sawa. Na hakikisha siri zako chafu hazifiki magazetini.” Anapumua kwa nguvu kisha anageuza uso wake kutazama nje ya dirisha. “Na kama jambo lolote litakutokea, hakikisha unanijulisha mara moja ili niweze kulituliza kabla jina lako halijachafuliwa.”
Hakuna kati yetu aliyesema neno lolote hadi tulipofika kwenye ndege iliyokuwa ikinisubiri kunipeleka New York. Midomo ya mama yangu bado ilikuwa imekunjamana kwa kutoridhika alipoanza kunibusu kwa kwaheri na kunitazama nikitoweka ndani ya ndege.
Mara tu ninapoketi vizuri kwenye kiti changu, ninatoa nyaraka fulani ambazo msaidizi wangu binafsi alinitumia kwa ajili ya sahihi. Juu ya nyaraka hizo kuna nembo ya Declan Group yenye rangi nyeusi na dhahabu—kampuni ya mabilioni inayotengeneza vito vya kifahari, ambayo niliijenga kuanzia mwanzo.
Kabla sijasaini hata ukurasa wa kwanza, simu yangu inapiga. Ni Lincoln George, rafiki yangu wa karibu tangu chuo kikuu.
“Umerudi New York tayari?” anauliza.
“Niko njiani muda huu,” nasema huku nikitazama dirishani ndege ikianza kupaa kuelekea angani. “Uchaguzi unakaribia kumalizika, na kwa hali ilivyo, naweza kushinda.”
Lincoln anacheka. “Kuna kitu chochote ambacho hujawahi kushinda kweli?”
Najiunga na kicheko chake, kisha nanyamaza. “Kabla sijawa meya, nahitaji kufurahia maisha. Nikifika New York, nina mikutano kadhaa niliyopangiwa. Lakini baada ya hapo, nataka kujiachia kidogo. Imetosha sasa.”
“Ninajua mahali sahihi pa kukupeleka,” Lincoln anasema kwa uhakika. Yeye ni mmiliki wa vilabu kadhaa vya kifahari kwa wanaume wanaotafuta burudani. Kila ninapohitaji mwanamke, yeye hunipatia bora zaidi jijini. Mimi hukubali tu bora kabisa.
“Vizuri. Nahitaji kufanya jambo lisilo la kiungwana kabisa kabla sijaanza kuwa mtu wa kuwajibika.”

SONGA NAYO….

MNADA WA BIKIRA
SURA YA 2

HAILEY
Leo ni siku yangu ya kuzaliwa—nimefikisha miaka ishirini na tano—lakini sisherehekei. Sijawahi kusherehekea. Nani angetaka kusherehekea siku ya kuzaliwa inayomkumbusha siku mbaya zaidi maishani mwake?
Ukweli ni kwamba, nilikuwa sihitajiki tangu mwanzo. Siku mama yangu alipojifungua, aliondoka hospitalini na hakurudi tena. Aliniacha nikiwa kwenye kitanda kidogo cha hospitali, peke yangu. Simfahamu, na sikuwahi kujisumbua kumtafuta. Mwanamke anayeweza kumfanyia mtoto wake hivyo si mtu ninayetaka kukutana naye.
Ninaingia kwenye nyumba yangu na kumkuta rafiki yangu kipenzi, Mariel Nichols, akiwa amelala ovyo kwenye kochi. Chupa kadhaa za pombe zimesimama mstari mmoja kwenye meza ya kahawa mbele yake.
“Ulikuwa wapi, Hailey? Nimekuwa nikikusubiri kwa saa mbili,” ananiuliza.
“Niliahidi kumfanyia Bi. Marga manunuzi,” najibu. Tumbo langu tayari linaanza kujikunyata kwa wasiwasi kwa sababu najua sababu ya kuwepo kwake. Nimekuwa nikijaribu kumuepuka mchana mzima.
“Wewe ni binti wa kufikirika mzuri sana,” anasema huku akijisukuma kutoka kwenye kochi. “Heri ya siku ya kuzaliwa, mpenzi.” Ananibusu mashavuni kisha ananikumbatia kwa nguvu.
Baada ya kumkumbatia kidogo, najitoa. “Mariel, unajua kabisa hayo ni maneno yaliyopigwa marufuku. Nilidhani tulikubaliana.” Ninatupa mkoba wangu juu ya kochi na kuketi pembeni yake.
“Lakini leo ni siku yako ya kuzaliwa ya ishirini na tano, bwege wewe. Nina haki ya kuvunja sheria. Bado najisikia na hatia kwa kutokukusisitiza kusherehekea ile ya ishirini na moja.” Anaketi karibu nami. “Nilitaka kukupa mshangao.”
“Unajua sipendi mshangao.” Ninakazia macho chupa za pombe. “Na pia sijawahi kunywa... pombe.”
“Hailey jamani. Ni mara ngapi mtu anafikisha miaka ishirini na tano? Tafadhali, sherehekea leo kwa ajili yangu. Hutalazimika kufanya hivyo tena.” Anavuta bega. “Hadi utakapofikisha thelathini. Hapo nitavunja sheria tena.”
“Huwezi kuamini.” Natikisa kichwa huku nikicheka. “Sawa basi, umepanga nini kwa usiku wa leo?”
“Hiki hapa ndicho,” anasema Mariel huku akiinua chupa ya rum na kuifungua. “Unakumbuka ile kozi ya kutengeneza vinywaji niliyochukua mwaka jana?”
“Niwezaje kusahau? Kila mara ulipotoka darasani ulikuwa umelewa kiasi,” nasema huku nikitupa kichwa nyuma na kucheka kwa sauti.
“Basi sasa nitaweka ujuzi wangu kazini. Kwa kuwa sina tena masomo, natafuta kazi kama mhudumu wa vinywaji vya mchanganyiko (cocktail). Tayari nimeomba kazi kwenye baa ya kisasa inayoitwa Little Black Dress. Umeshawahi kuisikia? Ni maarufu sana. Naamini ipo angalau moja katika kila jiji kubwa.”
Nilipepesa macho mara kadhaa kwa mshangao. “Umehitimu shahada ya ukarimu wa wageni halafu unataka kufanya kazi ya kuhudumia vinywaji?”
Mariel anatupa nywele zake nyeusi zilizonyooka nyuma ya bega lake na kunitazama kupitia upenyo wa paji lake la uso. “Ni kitu gani bora zaidi kuliko kuzungukwa na ‘watanashati’ kila usiku?”
“Unamaanisha kweli, siyo?” Napumua kwa kina. “Nilidhani tulikubaliana kufanya kazi kwenye kampuni za kupanga harusi hadi tuanzishe kampuni yetu wenyewe.”
Tulikutana chuo kikuu wakati tukisomea shahada ya ukarimu. Kwa kuwa wote tuna mapenzi ya kipekee kwa harusi, tuliamua kwamba baada ya kuhitimu, tungeanzisha biashara ya kupanga harusi.
“Usijali, kipenzi. Naweza kufanya yote mawili. Mchana nitakuwa mpangaji wa harusi na usiku mhudumu wa vinywaji. Si ni bomba hiyo?”
“Sawa,” nasema huku nikiahirisha mada hiyo hadi siku nyingine. “Lakini sidhani kama niko tayari kuonja vinywaji vyako.” Mara ya kwanza na ya mwisho kunywa pombe ilikuwa kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Mariel alipofikisha miaka ishirini na miwili, miaka miwili iliyopita. Sitasahau jinsi nilivyoamka asubuhi iliyofuata nikihisi kama vile roho yangu ilikuwa inaitazama miili miwili.
“Hailey, kwa nini huwa kama una aleji na raha? Kwa nini usijiachie hata mara moja na kufanya jambo lisilo na hesabu?”
Ninavuta bega na kuvua ndala zangu za ngozi. “Mmoja wetu lazima awe mwajibikaji.”
“Lakini si usiku wa leo, mrembo. Usiku wa leo tutaleweka wote!”
Mariel anaendelea kunishawishi mpaka mwishowe najikuta nikikubali kusherehekea. Labda kuzamisha huzuni yangu kwenye vinywaji ni kitu ninachohitaji.
Vinywaji vyake vinachukua muda kuzoeleka, lakini cha kushangaza, najikuta nikivipenda haraka. Vinywaji vyenye nazi vinanivutia zaidi. Sijui hasa ni glasi ngapi nimepokea kutoka kwake huku tukiangalia sinema ya ajabu ya rangi nyeusi na nyeupe. Nachojua ni kwamba baada ya saa mbili, siwezi hata kusimama vizuri. Na ninacheka kwa nguvu kuliko nilivyowahi kujiruhusu kufanya.
“Hii hapa choco colada yako ya mwisho.” Mariel ananipatia glasi.
“Hapana kabisa.” Nakumbatia tumbo langu. “Siwezi tena. Unaweka rum nyingi mno. Tumbo langu linawaka moto.” Saauti yangu inayochanganyika na ulevi inanifanya nicheke.
“Sawa basi.” Anapandisha mikono juu hewani. “Kazi yangu hapa imeisha. Nimejivunia sana kukuona ukitoka kwenye mipaka yako ya kawaida. Inapendeza kufanya jambo la kichaa mara moja moja.”
“Unajua nini kingekuwa kichaa zaidi?” Nauliza huku nikicheka kiasi kwamba tumbo linakunjamana. “Kama ningepoteza ubikira wangu usiku wa leo. Labda twende nje tukamtafute mtu wa usiku mmoja.” Nampungia kidole. “Nakuchora tu. Usianze kupata mawazo yoyote.”
“Afadhali unachora kweli.” Mariel anatikisa kichwa chake kama mtu aliye slow-motion. “Umeshikilia hilo kwa muda mrefu sana. Kama utaamua kuliachia, basi iwe kwa mtu anayelistahili. Kwa muda wote huu, thamani yake lazima imepanda.”
Wote tunazidiwa na kicheko hadi machozi yanatujaa mashavuni.
“Unajua kitu?” Mariel anafuta jicho lake kwa nyuma ya kiganja. “Niliwahi kusoma makala kuhusu mwanamke mmoja aliyouza ubikira wake mtandaoni. Mwanaume alimnunua kwa dola milioni mbili. Si kichaa hicho?”
“Unafanya utani.” Najigeuza kwake kwa kasi hadi kichwa changu kinaanza kuzunguka. “Ni nani anayefanya kitu kama hicho? Na ni nani ananunua ubikira wa mtu?”
“Watu hufanya mambo ya ajabu kila siku.” Anavuta bega. “Lakini kiukweli, sioni shida yoyote. Wanaume wengi ambao wasichana hupoteza nao ubikira hawastahili hata kidogo. Kama mimi ningekuwa bado bikira, huenda ningefikiria hilo.”
“Basi labda nami niuze wangu.” Natania, lakini inachukua muda kabla sijagundua kwamba Mariel hacheki.
“Labda unapaswa kufanya hivyo,” anasema kwa sauti ambayo kwa ghafla inaonekana kuwa makini zaidi. “Unaweza kuuweka kwenye Bidders. Huko watu huweka vitu vya ajabu kuviuza mnadani. Na unazo zile picha zako za kusisimua tulizopiga kwenye likizo ya spring break kule Boca Raton. Unaweza kuzitumia kutangaza hilo ua lako lisiloguswa.”
“Mariel, wewe ni kichaa zaidi ya nilivyodhani.” Bila kufikiria, nachukua ile choco colada aliyokuwa amenipa awali na kunywa kwa mfululizo. Latha yake inaingia kinywani mwangu kama rafiki wa zamani.
Mariel, ambaye sasa anaonekana kuwa kwenye mawazo mazito, hasemi chochote hadi glasi yangu inapokuwa karibu kuisha na mimi nikiwa siwezi hata kufikiria sawa sawa.
Anaporudia tena mada kuhusu mimi kuuza ubikira wangu, namsindikiza tu kwa utani—au labda sichezi. Sina uhakika kwa sababu akili yangu ya kawaida inaonekana kuondoka chumbani.
“Ah basi, tufanye tu!” Nachangamka huku nikicheka. “Lakini sidhani kama kuna mtu atakayenunua.”

SONGA NAYO….


MNADA WA BIKIRA
SURA YA 3

HAILEY
Kosa kubwa, nadhani huku nikikohoa na kujitupa juu ya choo, mwili wangu ukitetemeka wakati matapishi yanaporomoka kutoka mdomoni mwangu. Harufu yake ni mbaya mno, ladha yake ni chungu, chachu, na ya kuchukiza inavyojipaka kwenye ulimi wangu na kunifanya macho yaanze kutoa machozi.
Niko karibu kuinuka wakati wimbi jingine la kero hilo linajaa kooni na kutoka kwa kasi kupitia mdomo na hata puani.
Nilipaswa kutomsikiliza Mariel. Nilikuwa nawaza nini?
Baada ya muda unaohisi kama milele, hatimaye napata afueni. Nikiwa nimehema kwa nguvu, nasuuza mdomo wangu na kujimwagia maji usoni.
Ninaponyoosha mkono kufikia taulo la zamani kwenye ndoano ya ukutani, mlango unagongwa. Natazama macho yangu mekundu kwenye kioo kwa mshangao.
Ni nani anakuja kuniangalia saa 1:00 asubuhi ya Jumamosi?
Bi. Marga huwa haamki kabla ya saa tano, wakati ninapoenda kumwandalia kifungua kinywa—kazi ambayo nimekuwa nikifanya kila Jumamosi asubuhi.
Bi. Marga ana miaka sabini na tano, mwili wake ukisumbuliwa na baridi ya kudumu na tatizo la macho la katarakti. Nilipoamia kwenye jengo hili la vyumba miaka mitatu iliyopita, aliniambia jinsi mumewe alivyofariki miezi michache tu baada ya kuoana. Alimuacha akiwa mjamzito na peke yake. Cha kusikitisha zaidi, binti yake, Rosie, ambaye alikuwa polisi, alifariki akiwa kazini miaka mitano iliyopita.
Nilichukia wazo la yeye kuishi maisha ya upweke. Nilianza kumtembelea kila nilipopata muda hadi tukazoeana kiasi kwamba sasa ni vigumu kuamini hatuna uhusiano wa damu kabisa.
Mkono wangu uko kwenye paji la uso wangu linalouma kichwa ninapojikongoja kuelekea mlangoni.
“Nani huyo?” Hakuna tundu la kuchungulia mtu upande wa pili wa mlango.
“Ni mimi, Mariel. Fungua mlango.”
“Kwa nini hukutumia funguo yako?” Namuuliza ninapomfungulia mlango. Sikumtarajia kuja mapema hivi. “Na kwa nini uko hapa saa hizi?”
Nilidhani bado angekuwa amelala akiuguza hangover, lakini kwa mtu aliyekunywa vinywaji vingi kuliko mimi, anaonekana yuko makini kabisa. Nywele zake za kawaida zenye mng’ao, nyeusi kama kunguru, sasa zimevurugika juu ya macho yake ya mviringo, na sauti yake ina mshiko wa ulevi bado, lakini macho yake yako macho kabisa.
“Niliisahau hapa jana usiku.” Anaufunga mlango nyuma yake. “Umeangalia tangazo lako kwenye Bidders? Mnada unaisha ndani ya dakika tano.”
“Tangazo gani?” Najiandaa kuelekea bafuni. Tumbo langu linaanza kujigeuza tena. Mariel ananifuata hadi ndani. “Ingiza kwa hatari yako mwenyewe,” namwambia nikimwonya kuhusu harufu kali inayotanda hewani.
“Ee Mungu wangu.” Anakunjamana uso kwa chuki. “Inaonekana mtu aliharibu pombe yangu yote.”
“Nyamaza.” Ninasafisha choo. “Sikupaswa kukusikiliza. Pombe ni shetani.”
“Lakini utashukuru kwamba ulinisikiliza kuhusu jambo lingine.”
“Unazungumzia nini sasa?” Nachukua mswaki wangu.
“Unahitaji kuona hii.” Ananichukulia mswaki mkononi na kunipatia simu yake. Kupitia macho yangu yenye ukungu, natizama kwenye skrini.
“Napaswa kuwa naangalia nini hapa?” Inachukua sekunde kadhaa kwa ubongo wangu kuelewa kile macho yangu yanaona. Lakini mara tu ninapolielewa, nafungwa na ngumi ya mshangao moja kwa moja tumboni. Ninajikokota nyuma kwa hofu hadi miguu yangu inagonga bafu. Ninaketi kwenye ukingo wa bafu.
“Ee Mungu wangu.” Ninamshika koo kwa mshtuko.
Mariel anaketi karibu nami. “Hilo ndilo nililosema pia nilipoiona.”
Ninamtupia macho ya kushangaa kupindukia. “Tafadhali niambie kwamba nipo ndotoni. Hili haliwezi kuwa halisi.”
“Kichekesho kabisa, sivyo? Usee! Nilikwambia ubikira wako una thamani—dola laki mbili na hamsini elfu, kwa mujibu wa hilo tangazo. Hongera, malkia.” Anafukuza nywele machoni mwake.
“Kwani nilikuwa kichaa gani kumpa ubikira wangu Dannie, yule jamaa wa maktaba? Ningeweka pesa kichwani hivi sasa.”
Ninamrudishia Mariel simu kwa nguvu na kuporomoka tena mbele ya choo. Natapika hadi hakuna kilichobaki ndani yangu.
Kisha namgeukia Mariel, ambaye bado ana tabasamu la kuridhika usoni.
“Hili halichekeshi. Hili ni janga kamili.”
“Sikubaliani na wewe.” Anatazama skrini. “Lo! Mtu mwingine ameweka dau. Sasa upo kwenye dola 300,000.”
Sijathubutu hata kuichukua simu na kujionea mwenyewe. Mwili wangu mzima na akili yangu vinaonekana kuwa na ganzi.
“Hii ni habari nzuri, Hailey. Ya ajabu, lakini nzuri.”
“Hapana. Hapana!” Naanza kuzunguka ndani ya bafu dogo, mkono wangu ukiivuta nywele zangu kwa wasiwasi. “Hii ni makosa. Nilidhani ilikuwa mzaha. Siwezi kuamini kwamba kweli—”
“Ulifanya. Na sasa ua lako linaenda kutatua baadhi ya matatizo yako ya kifedha,” anasema kwa mzaha.
Ninamrukia na kumtikisa kwa mabega. “Unaweza kuacha mzaha kwa dakika moja? Hili ni la kichaa kabisa. Hata sijui kama ninaweza kufuta tangazo la mnada.”
“Basi huna chaguo, mrembo,” anasema kwa tabasamu la kijasusi. “Lazima ukabidhi bidhaa kwa aliyeshinda kwa dau kubwa.”

SONGA NAYO…


MNADA WA BIKIRA
SURA YA 4

HALIEY
Ni saa sita usiku, siku mbili tangu mnada umalizike. Chumba kimejaa giza na ninatazama skrini ya laptop yangu yenye mwangaza wa buluu hafifu, tumbo langu bado limebanwa kwa wasiwasi.
Nimejaribu kila njia kufuta muamala huu, lakini hakuna kilichofanya kazi. Hata nilimwandikia mnunuzi aliyeweka dau kubwa zaidi, anayejulikana kwa jina la mtandaoni Mr. Declan. Nilijikusanya kwa ujasiri na kumtumia barua pepe usiku uliopita, na sasa natazama majibu yake.
"Haitatokea."
Wako kwa heshima,
Mr. Declan
Nilisoma majibu yake mara ya kwanza saa moja iliyopita, lakini bado sijapona na mshituko. Ni mtu wa aina gani anayenunua ubikira wa mtu? Lakini kwa upande mwingine, lazima na yeye alidhani mimi ni kichaa alipokutana na tangazo lile.
Ninapiga laptop yangu na kuifunga kwa nguvu, kisha ninachimba chini ya mto kutafuta simu. Ni usiku sana, lakini nahitaji kuongea na mtu. Kwa kuwa ni Mariel pekee anayejua, nampigia.
“Siwezi kuamini hukunitisha kuacha kufanya hivyo,” nasema mara tu anapopokea simu. Nimekasirika naye kwa kuniambia hadithi ile ya mwanamke aliyouza ubikira wake—na zaidi kwa kuniacha nikaitekeleza.
“Pole, Hailey,” anasema kwa sauti ya kuogopa. “Sikufikiria vizuri usiku ule. Na pia sikuwahi kufikiria kuna mtu angeweka dau.”
Watu watatu walikuwa wameweka dau kwenye tangazo hilo.
“Naam, nami pia.” Naisukuma laptop upande wa pili wa kitanda changu na kujilaza, magoti yakiwa yamekunjwa kifuani. “Samahani. Sio kosa lako. Singepaswa kunywa mpaka nikajisahau. Lilikuwa jambo la kipumbavu.”
“Usijilaumu, mpenzi. Na samahani kama nilionekana kama malaya siku ile. Sitakuzuia kama utaamua kuvunja muamala.”
“Asante. Lakini siwezi. Yule Mr. Declan alijibu. Maneno mawili tu. Haitatokea.”
“Basi tu hivyo?”
“Ndiyo.” Tumbo langu linavurugika kwa wasiwasi. “Sijui hata nifanye nini sasa.”
Mariel haneni kitu, lakini nasikia akiendeleza kutafuna kwa upole. Yeye huwa na chewing gum kila mara, lakini hata usiku wa manane? “Samahani mpenzi, lakini kama huwezi kujitoa kwenye hili, labda... unajua... ungetafuta faida zaidi kutokana nalo.” Anashusha sauti. “Hela hiyo inaweza kukusaidia sana. Ungeweza kulipa madeni ya chuo. Na kama hutaki, unaweza kunipa ilipe madeni yangu.”
“Nikilala na mtu huyu, hiyo haitanifanya kuwa kahaba?” Ninafumba macho yangu kwa uchungu. Akili yangu inarudi nyuma hadi shule ya sekondari, ambapo mmoja wa wale wasichana wabaya aliwahi kuniambia kwamba Hailey ni jina ambalo kahaba angejichagulia. Maneno yale yalinikata moyo kwa sababu nilikuwa tayari nachukia jina langu—kitu pekee alichoniachia mama yangu mzazi.
“Wewe si kahaba. Wewe ni msafi mno kwa hilo. Angalia tu kama tukio la usiku mmoja lenye faida kubwa. Watu wanafanya hivyo kila mara na wageni.”
“Wewe ni kichaa kabisa.” Najikuta nikicheka licha ya kila kitu.
“Najua. Na natamani ningeweza kukutoa kwenye sakata hili, lakini sijui jinsi.”
“Tazama, heri niendelee kulala. Kuna mengi ya kuwaza.”
“Nijulishe utakachoamua. Nipo hapa kwa ajili yako, hata kama utaamua kukimbilia nchi nyingine na ‘mzigo’ wako salama.”
“‘Mzigo’? Sawa, niache kabla hujaongea jingine la kichaa.”
Baada ya kukata simu, nachukua risiti ya dukani juu ya droo yangu ya pembeni ya kitanda na kalamu. Kisha naandika orodha ya mambo ambayo ningeyafanya kwa pesa hiyo:
1. Kumlipia Bi. Marga upasuaji wa macho
2. Kulipa madeni ya chuo kikuu
3. Mtaji wa kuanzia biashara
Ninapofika namba ya tatu kwenye orodha, paniki inanipanda ghafla—kwa sababu natahadharika kwamba hata simjui huyu mtu anayeitwa Mr. Declan kwa sura.
Kabla sijajizuia, nachukua tena laptop yangu na kuifungua ili kumjibu ujumbe wake.
“Nahitaji kuona picha yako.”

SONGA NAYO….


MNADA WA BIKIRA
SURA YA 5

HAILEY
“Unawaza nini, mpenzi?” Bi. Marga anauliza ninapomletea supu ya kabichi niliyompikia.
Natikisa kichwa na kutabasamu. “Sio kitu kikubwa. Natumaini utaifurahia supu hii.”
Anainua kijiko. “Unajua huwa naifurahia kila mara.”
“Kuna jambo lingine unataka nikufanyie kabla sijaondoka?”
Ni saa kumi na mbili jioni na nimepoteza karibu siku nzima nyumbani kwake—kusafisha, kufua, na kumletea kampani. Kila ninapomtembelea, huniambia hadithi kuhusu binti yake. Hadithi ambazo amenieleza zaidi ya mara mia.
“Umenifanyia vya kutosha, Rosie,” anasema bila hata kuinua macho.
Huwa anafanya hivyo mara nyingine, kuniita kwa jina la binti yake. Wakati mwingine huwa na wasiwasi kwamba anaweza kuwa na dalili za Alzheimer’s. Lakini kwa kuwa hali hiyo hutokea mara moja au mbili tu kwa mwezi, labda ni matamshi ya bahati mbaya tu.
Sijawahi kumsahihisha. Jambo la mwisho ninahitaji ni yeye kuanza kujihangaisha. Ikiwa itaendelea mara kwa mara, nitamwambia.
“Nitakuona kesho.” Naweka tena kifuniko juu ya sufuria.
“Utanisindikiza kanisani kesho?”
Nakohoa kwa aibu. “Sidhani kama nitaweza. Pole. Nina fomu nyingi za kazi za kujaza.”
Ni uongo—na najisikia vibaya mno. Lakini siwezi kwenda naye kanisani, si katika hali hii ambapo ninatafakari kufanya jambo ambalo Mungu anaweza asilikubali.
Ninapombusu Bi. Marga shavuni, siwezi kujizuia kujiuliza—angefikiria nini kuhusu wazo langu la kuuza bikira Yangu?
Je, bado ninafikiria, au tayari nimeshafanya uamuzi?
“Labda siku nyingine,” Bi. Marga ananiambia kwa tabasamu. “Hakikisha umefunga milango yako.”
Wiki tatu zilizopita, mtu alivunja nyumba kwenye jengo letu. Tangu siku hiyo, amekuwa akinisisitizia kila mara kuwa makini.
“Usijali, nitahakikisha hilo.” Nainua mkoba wangu begani na kutoka nyumbani kwake.
Dakika mbili baadaye, ninaketi kwenye meza yangu ndogo ya chakula, nikiwa na kikombe cha hot chocolate mbele yangu, nikitazama karatasi ambayo inathibitisha kwamba hakuna mwanaume aliyewahi kulala nami.
Ukweli kwamba nilikwenda kwa daktari kupata uthibitisho huo unanitia hofu. Hii ina maana kwamba labda ninaenda kweli kufanya jambo hili.
Mwanzoni nilikasirika kwamba Mr. Declan aliomba uthibitisho kwamba mimi ni bikira kweli. Lakini baada ya kuwaza kwa kina, naweza kumwelewa. Analipa pesa nyingi sana. Bila shaka, anataka kujua kama nasema ukweli. Ni kitu gani kingemzuia mwanamke yeyote kudai kuwa ni bikira?
Bado nikiwa natizama karatasi hiyo, naimalizia hot chocolate yangu na kumpigia Mariel.
“Imekwisha,” nasema, tumbo langu likijikunja kwa mshtuko.
“Kimekwisha nini? Tayari umelala naye?”
Natikisa kichwa. “Hapana, kichaa wewe. Nimekwenda kwa daktari jana na kupata uthibitisho alioutaka yule jamaa.”
Kimya. Kisha sauti ya Mariel inakuwa ya umakini. “Uko makini kabisa kufanya hili, siyo?”
“Sijui. Labda. Najihisi kama vile... ndiyo. Ulikuwa sahihi, ni pesa nyingi sana.” Ingawa najisikia najichukia kwa sasa, kuna hisia kuwa nitaweza kujuta sana kutoenda mbele na mpango huu. Ningeweza kutumia pesa hizo kufanya mambo mengi mazuri—labda hata kuchangia sehemu ya pesa kwa kituo cha watoto yatima nilichokulia, ambacho bado husaidia mara moja au mbili kila mwezi.
“Najua nilikushawishi kwa namna fulani, lakini sasa najisikia na hatia kidogo.”
“Haikuwa wewe uliyeweka tangazo kwenye Bidders, Mariel. Ingawa nilikuwa mlevi, mimi ndiye niliyekifanya. Mimi ni mtu mzima na nitachukua majukumu ya matendo yangu.”
“Naam... nafikiri kinachosaidia ni kwamba jamaa ni bilionea mwenye mvuto.” 😏
“Lakini vipi kama amenitumia picha ya bandia?”
“Basi atakuwa mjinga kutuma picha ya mtu maarufu,” anajibu Mariel.
Mr. Declan si mtu wa kawaida. Mara tu nilipomwonyesha Mariel picha yake, alimtambua mara moja kama mwanzilishi wa kampuni ya vito vya thamani—Declan Jewelry Group. Ilinitisha sana kufikiria kwamba mtu mwenye utajiri na mvuto kama huo angependa kulala nami. Nilitazama picha yake kwa saa kadhaa, nikiwa siwezi kuondoa macho yangu kutoka kwenye yale macho ya buluu yenye kuvutia, midomo mipana, na pua yenye umbo kamili la kifalme.
“Uko sahihi,” nasema. “Angekuwa mjinga kweli kufanya hivyo.”
“Na kwa kweli ni jambo jema kwamba sasa tunajua ni nani hasa. Kama atakufanyia jambo lolote baya, tutamshtaki mara kumi ya zile dola elfu mia tatu. Na mimi binafsi nitaharibu jina lake kila kona,” Mariel anasema kwa msisitizo, kisha anapumzika kidogo. “Umeshampatia majibu ya daktari?”
“Karibu leo, lakini nilikosa ujasiri. Nafikiri inabidi nimtumie, sivyo?” Nachokonoa kona ya kucha yangu kwa wasiwasi.
“Mpenzi, kama itakusaidia kupunguza hofu, naweza kwenda nawe kwenye mkutano wenu wa kwanza, kuhakikisha tu kwamba ni yeye kweli na si mtu wa ajabu.”
“Unamaanisha nini unaposema utaenda nami?”
“Unaweza kumwomba akutane nawe kwa chakula cha jioni au kitu kama hicho, na mimi nitahifadhi meza kwenye mgahawa huo huo.”
“Mariel, huyo ni bilionea. Vipi kama anakuchukua kwenye mgahawa ambapo glasi ya divai inagharimu zaidi ya mshahara wa wiki ya mtu wa kawaida?”
“Basi mimi nitaagiza maji. Au nitajipa ujasiri na kuagiza glasi ya divai. Unaweza kunilipa ukishapata fedha zako.” Anacheka.
“Ungeenda kweli nami?”
“Mimi pia nina sehemu ya lawama kwenye haya yote. Kwa hiyo, ndiyo.”
“Na vipi kama anataka tukutane hotelini?” Tumbo langu linajigeuza kwa mawazo ya kwamba anaweza kutaka kulala nami mara tu baada ya kukutana. “Unajua nini, sitaki kukuingiza kwenye matatizo yoyote. Usijali kunihusu. Mimi ni msichana mkubwa sasa. Naweza kujitunza.”
“Sawa. Lakini hakikisha simu yako imejaa chaji ili niweze kukufikia. Na nipigie mara moja kama kuna kitu kinakwenda tofauti.”
“Naahidi.”
Ee Mungu. Nimeshafanya uamuzi.

SONGA NAYO….


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote