Follow Channel

MOYO WA JENERALI JAX

book cover og

Utangulizi

MOYO WA JENERALI JAX
EP 01
MTUNZI;HUSQER BALTAZAR

"Docta Mei, docta Mei fungua mlango tuna kufa huku" Sauti hii ilipenya masikioni mwa binti mrembo mwenye taaluma yake ya Udaktari

Mwanzo alihisi yupo ndotoni hivyo alijifunika gubi gubi.
Sauti ilizidi kusikika, alifumbua jicho moja kusikilizia....

"Aiseee tangu nije hapa sipati hata usingizi....." Sia alilalamika huku akitoka kitandani.

Hakutaka kufungua mlango alichungulia dirishani.

"Leo kuna shida gani tena!...." Sia aliuliza kwa ukali kidogo

"Sijui mbuzi tuliyekula ana nini, Wanajeshi wote wako wana lalamika tumbo....pekee yangu tu nimenusurika" Mwanajeshi mmoja aliongea

"Kwahiyo mie nifanyaje....sipo zamu nendeni hospitali, " Sia aliongea kisha akafunga dirisha....kichwa chake kilikuwa kimevurugika.

Alishika simu yake aone kama boyfriend wake kamsamehe kwa kosa alilofanya lakini hakukuwa na majibu😭.

Kwa hasira alivaa Sweta kisha akaongoza na Mwanajeshi aliyemuijia akatoe msaada.

Alijishika kiunoni baada ya kukuta Wanajeshi wote wamekunja sura zao.

"Tangu Jenerali asafiri basi mnafanya kufuru ya kula mbuzi wenye dege dege!" Sia aliongea, huku akiichukua mnofu mmoja wa nyama ya mbuzi.
Aliunusa puani kisha akatafuna, mbuzi hakuwa na tatizo

Alichukua chupa moja ya bia iliyokuwa chini.
"Wajinga nyie kwanini mna kunywa bia zilizo expire...." Mei aliongea huku akiwaonesha chupa moja

Alipiga simu hospitali, huduma ya haraka ilifanyika. Kwa jinsi alivyokuwa na stress za mapenzi alijikuta akiwachoma sindano kwa uchungu wote

"Mei leo una nini!...." Mwanajeshi mmoja alishindwa kuvumilia

"Stress za mapenzi zinauma kuliko hata matumbo yenu!" Mei aliongea

Pamoja na kisirani chake lakini Wanajeshi hawa walikuwa wanamkubali sana.

"I wish boyfriend wangu angekuwa kama hawa Wahuni..." Mei alijisemea kisha akaondoka baada ya kumalizana nao.

Ile anajitupa tu kitandani sauti ilisikika

"Docta Mei....Docta Mei kuna emergency!"

Mei aliziba masikio yake, japo ni kazi yake lakini imekuwa usumbufu sasa. Hapa Kambini kuna Madaktari wengi tu haelewi kwanini wanamganda yeye tu.

"Mbwa hawa utadhani Mimi ni Nabii" Mei alijisemea kisha akafungua mlango kwa hasira

"Jenerali Jax karudi, fanya haraka yupo na jeraha kwenye mguu wake!" Mwanajeshi mwenye cheo cha Kopro aliingia

"Jeraha tu la mguu ndio unanibwekea hivyo...mwambie avumilie nitamhudumia saa 12 asubuhi siyo sasa" Mei aliongea kisha akafunga mlango kwa kuubamiza

"Huyu ana wazimu, mara hii tu amekisahau kichaa cha Jenerali Jax... okay mjumbe hafagi acha nirudishe majibu" Mwanajeshi aliyeagizwa alijisemea kisha akaondoka

Jax akiwa anapuliza sigara yake kubwa mfano wa karoti, alikodoa macho kwa majibu aliyopatiwa.

"Ni kama ananiambia nimfuate....nitamfuata" Jax aliongea kisha akatoka kitandani kwake

"Weee kafiri, shetani wewe huwezi kuniacha usiku wa manane. Wallah najinyonga humu ndani!....kosa dogo kama lile ndio uniache! haiwezekani" Jax anakutana na haya malalamiko baada ya kufika mlangoni kwa Mei

Aliachia tabasamu huku akiendelea kuvuta sigara yake.

"We kahaba unayevuta sigara mlangoni kwangu naomba usepe!" Mei aliachia tusi baada ya kunusa harufu ya sigara

Itaendelea 💥



MOYO WA JENERALI JAX
Ep02
MTUNZI;HUSQER BALTAZAR

Kipisi cha sigara kilimdondoka Jenerali Jax kwa tusi alilopatiwa.
Siku zote hufurahia kuwaita wenzake majina mabaya, lakini kwake imekuwa chungu kinoma.

Alimpa ishara kopro atoe taarifa kuhusu uwepo wake

"Docta Mei, Jenerali Jax yupo mlangoni kwako fungua mlango"

Mei alishtuka baada ya kusikia Jax yupo mlangoni kwake. Kuna namna huwa anamuogopa hasa akiwa karibu yake.
Yaani anaweza fanya ujeuri wote Jax akiwa mbali lakini wakiwa pua na mdomo huwa anatumikishwa kama punda.

"Hello, umerudi lini...." Mei aliuliza, pua yake ilikuwa nzito sababu ya kulia. Macho yalimuuka sababu tu ya kuachwa

Jax alimuangalia kwa kumkadiria kisha akaingia ndani bila kukaribishwa.
Anashtuka baada ya kuona mkojo kwenye ndoa.

"Daktari mzima unakojoa kwenye ndoo! vipi kama ningenawa bahati mbaya!"

"Weee Mwanaume! umekuja kutibiwa jeraha lako au kuangalia ndoo zina nini!" Mei alifoka, moyo wake ulikuwa unamuuma sana.... hakutarajia kama boyfriend wake anaweza kumuacha kisa tabia yake ya kukojoa kwenye ndoo

"Sijui ni kitu gani kilitokea lakini nilishtukia tu mguu wangu unavuja damu nashindwa kuelewa chanzo ni nini" Jax aliongea

Mei alichukua sindano akaanza kuuchoma choma mguu wa Jax mfano wa chips inavyoliwa

"Nini nini hicho unafanya!" Jax aliuliza baada ya kuona kama ana komolewa hivi

"Naangalia rangi ya damu....kuna sehemu inatoka nyeusi sana na pengine ya kawaida. Hii itakuwa ni sumu kali.... naomba ukaze moyo wako kwa sababu utasikia maumivu makali sana" Mei aliongea

"Tumia ganzi, mwili wangu wote unauma sitaki kusikia maumivu ya aina yoyote ile" Jax aliongea

"Ungeenda hospitali, kwa kuwa umenifuata nyumbani acha ni kusaidie....tena sumu imeanza kupanda zaidi ukiendelea kubishana na Mimi nitakukata mguu" Mei aliongea

"Hamna shida.....!" Jax aliongea

Mei alivaa gloves mikononi mwake kisha akaachua wembe na mikasi midogo.
Jax alijikuta akiogopa kwa jinsi Mei alivyo shika mkasi kwa mkwara.

"Subiri kwanza!... naomba usahau hicho kitu kinacho sumbua akili yako tofauti na hapo nitaenda hospitali kupatiwa huduma"

"Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge, umeniharibia starehe yangu ya usingizi....acha tu niitoe hii sumu..." Mei aliongea kisha akaanza kufanya kazi yake

Kila alipokuwa ana mshona nyuzi Jax alimkumbuka boyfriend wake Daktari.
Alijikuta akivuta nyuzi kwa nguvu zote

"Wee mbwa mbona ni kama unanikomoa!" Jax aliongea akiwa kamshika mkono kwa nguvu zote

"Niachie bado kidogo tu...." Mei aliongea

Jax alilegeza kamba, Mei alishona chapu chapu.

"Hakikisha huu mguu haugusi maji....unaweza kuondoka" Mei aliongea

Jax anaamua kumkomoa kwa kuipiga teke ndoo ya mkojo.
Mei aliporomosha matusi lakini haikusaidia kitu.

Vile alikuwa na hasira alianza kulia akihisi Wanaume wote wana mdharau.

Usingizi unampatia muda ukiwa umeenda, anakuja kushtuliwa na simu.

"Mama yangu, natakiwa kutoa ripoti ya wiki nzima" Mei alijisemea huku akisukuma mlango

Alisikia kuchanganyikiwa baada ya kugundua usiku wa jana Jenerali Jax alimfungia kwa nje

"Mbwa huyu ana nini na Mimi, vipi kama joka lingenivamia humu ndani!" Mei alilalamika huku akitupa viatu na mkoba wake kwa njia

Kwa jinsi alivyokuwa mwembamba alijipenyeza dirishani. Hakuona sababu ya kuvaa viatu, alianza kukimbia.

Jenerali Jax akiwa anaongea na simu alimshuhudia, alijikuta akicheka kwa jinsi alivyokuwa kuwa kama kichaa

Itaendelea 💥



MOYO WA JENERALI JAX
EP03
MTUNZI;HUSQER BALTAZAR

Mei anaingia kwenye chumba cha kikao akiwa hajanawa hata uso.
Aliomba msamaha kwa kuchelewa kisha akaanza kutoa ripoti ya wiki nzima.

"Alaas! siamini kama hili jambo nimelimaliza" Mei alijisemea ndani ya moyo wake

Aliingia mtandaoni aone kinacho endelea.
Machozi yalimdondoka baada ya kumshuhudia boyfriend wake akimvika pete Mwanamke mwingine.
Kwa hasira aliifuta namba ya boyfriend wake, huku akiumia mno,

"Nyoka huyu, hakutakuwa na second chance tena katika dunia yangu nina uhakika atapigwa na kitu kizito muda si mrefu. Bwege huyo sitamsamehe hata kidogo" Mei alijifariji akihisi bwana wake atamrudia tena, hakujua kama kuna watu wanajua kuachwa

Wakati anaelekea ofisini alikutana na Jenerali Jax.
"Hello...." Aliongea kwa ufupi akitaka kuendelea na safari yake lakini alizuiliwa

"Sijapata usingizi usiku mzima, mguu ulikuwa unavuta sana natamani hata hizi nyuzi zitolewe" Jax aliongea

"Kama una ndoto za kukatwa mguu toa hizo nyuzi,..." Mei aliongea

"Kwa haraka tu upo kwenye maumivu makali.... mapenzi ndivyo yalivyo jifunze kukubali matokeo mbwa wewe, nitakustahi kwa hili kosa lakini usirudie kutoa huduma mbovu kama hii kisa mapenzi" Jax aliongea kisha akaondoka

Kwa namna alivyokuwa anatembea isingekuwa rahisi kujua kama ana jeraha katika mguu wake.
Anaachia tabasamu baada ya kumuona Sia, huyu binti ni Mwanajeshi pia.
Ukaribu wao umewafanya waingie kwenye mahusiano serious kabisa.

Sia alimpiga teke kwenye mguu aone kama kapona

"Ouch umeniumiza.....nesi aliyenishona ni mbwa" Jax alilalamika

"Nitakupa kimoja usiku wa leo," Sia aliongea kisha akaendelea na safari yake

Upande wa Mei akiwa ofisini kwake alishika kioo akaitazama sura yake

"Mimi huyu ni wa kuachwa kisa na kojoa kwenye ndoo. Huyu Mbwa kajua kunidhalilisha. Ni Wanawake wangapi wanakojoa kwenye ndoo na kupuu juu!... kwaninj mie anifanyie hivi" Mei aliongea pekee yake, ndipo alikumbuka kama mkojo uliomwagwa jana na Jenerali Jax hakuufuta🙆.

Alifunga ofisi yake kisha akaondoka kwa kukimbia.
Jenerali Jax ana mshuhudia kwa mara nyingine tena

"Ndiyo tupo Jeshini lakini huyu panya amezidi.... muda wote ni mchaka mchaka tu" Jax aliongea pekee yake
Hakuwa na kazi ya kufanya, alijikuta akiingiwa na shauku ya kujua ni kitu kina mharakisha Mei namna hiyo.

Baada ya Mei kuingia ndani alianza kudeki kwa fujo.
Vitu vyote alivyowahi kupatiwa na boyfriend wake alianza kuvirusha nje

Jax aliendelea kukodoa macho, ile Mei anatoka nje na mafuta ya taa alishangaa kumuona.

Alitest mitambo kwa kumpiga teke kwenye mguu wake.

"Ouch!....vipi wewe" Jax alilalamika

Mei hakuongea chochote, alimkunjia suruali kwa lengo la kuangalia jeraha.

"Nilisema kidonda kisiguse maji, vipi unataka kukatwa mguu au unataka ni bebeshwe lawama kwa kushindwa kukuhudumia vizuri!" Mei alifoka

Alimuingiza Jax chumbani kwake kisha akachukua dawa akaanza kumfanyia usafi.
Muda wote Jax alikuwa ana muangalia,
Mara paah macho yao yalikutana, Mei alishtuka utadhani katazamana na shetani mwenyewe

Itaendelea 💥



MOYO WA JENERALI JAX
EP 04
MTUNZI;HUSQER BALTAZAR

"Kwanini unaniangalia!" Mei hakukawia kuuliza

"Nadhani wewe pia umeniangalia..." Jax aliongea

Mei alifanya majukumu yake fasta fasta kisha akamtaka asepe
"Ahsante kwa huduma yako nzuri, huo mdori hapo nje nitauchukua sifurahii ukiutupa"

"Usipende kuomba omba madukani zinauzwa kwa bei chee tu" Mei aliongea kisha akafunga mlango hakuwa akitaka mazoea

"Mbwa huyu kwanini alikuwa ananiangalia namna hiyo!...." Mei alijiuliza
Simu yake iliita baada ya kugundua mpigaji ni Daktari mwenzie alijua kimenuka. Mara nyingi akipigiwa simu na huyu Daktari huwa ni swala la kusaidiana kufanya upasuaji na si kingine.

Alitikisa mlango wake kama mara tatu hivi ndipo aligundua umefungwa kwa nje.
Aliachia sonyo kubwa yakifuatiwa na matusi. Kama Jenerali Jax angesikia namna anavyo tukanwa huenda presha ingepanda akafa.

Mei alijipenyeza kama ngamia kwenye tundu la sindano.
Hakutaka kutembea, alikimbia mpaka alipofika chumba cha operation.
Alivaa gloves chapu huku macho yake yakimuangalia mgonjwa aliyekuwa katika hali ya kukata tamaa

"Kama umevurugwa naomba usinisaidie kwa chochote nakujua..." Daktari T alisisitiza

"Huu si muda wa kunichota mambo yangu acha tuokoe huyu mtu...." Mei aliongea akijua ni wapi ataanzia

Kwa pamoja walifanya upasuaji kwa kushirikiana,

Wakati Mei anatoka kwenye chumba cha upasuaji alikutana na Jax akiwa na Sia (demu wake) kwa namna walivyokuwa wanatembea kwa kunyata aligundua hawa wawili wana mahusiano

"Hello..." Aliwasalimia akitaka kuendelea na safari yake.
Jax alimrudisha kwa kumvuta koti lake

"Fanya kuniangalia mguu wangu"

Mei alitaka kugoma kwa sababu ameshamfanyia check-up dakika chache zilizopita lakini kwa ajili ya Sia alikubali kufanya hivyo.

Ile anataka kumkunjia suruali, Sia alimuwahi, huyu demu ana wivu kupita kiasi.

"Unaweza kumuangalia bila kumshika mguu wake...." Sia aliongea

Mei aliachia tabasamu kimtindo, alimkagua Jax kwa kutumia macho kisha akamtazama.

"Unaendelea vizuri, kama utajitahidi kukiweka kidonda mbali na maji kesho kutwa utakuwa bomba kabisa" Mei aliongea kisha akampiga teke kimtindo, hakukaa sehemu hii aliondoka

"Mbona ni kama kakuzoea kupita kiasi, anawezaje kukupiga teke kama mna date vile!" Sia alilalamika

"Punguza wivu mbwa wewe!...." Jax aliongea huku akimsindikiza kwa macho Daktari Mei, kama Sia angemfuma basi ingekuwa ni shida nyingine

Ikiwa ni majira ya saa saba usiku, Mei anarejea nyumbani kwake akiwa amechoka kupita kiasi.
Hakuona hata sababu ya kuoga....ile anataka kuzima taa alale alisikia mtu akigonga hodi

"Sitoi huduma yoyote ile tafadhali sana nenda hospitali...." Mei alilalamika

Mlango uliendelea kugongwa, alienda kufungua akiwa kakunja sura yake. Anashangaa baada ya kumuona Jenerali Jax

"Kitu gani kimekuleta hapa...."

"Nimekuja tupige stori..." Jax aliongea huku akipitiliza ndani

Mei alifunga mlango huku akitikisa kichwa chake.

"Ni story zipi hizo unataka kuongea na Mimi?....za kidini,vita siasa au mpira!" Mei aliongea kwa jazba

"Nimekuja tuzungumze kuhusu mapenzi..... natamani kusikia ni vitu gani Wanawake wanapenda kufanyiwa. Demu wangu ana wivu sana naomba kujua shida ni nini" Jax aliongea

"Huna marafiki wa kuwauliza hizi mambo!.... Mwanaume wewe huna hata bando ufatilie mtandaoni!"

"Unaonekana una akili kuliko marafiki zangu pamoja na Google" Jax aliongea huku akitoa sigara yenye ukubwa wa karoti

Mei aliipiga teke ikaanguka kule
"Punguza kumfikisha kileleni demu wako wivu utamuisha...."

"Vipi boyfriend wako amewahi kukufikisha kileleni mara ngapi!" Jax aliuliza swali lililomfanya Mei akodoe macho

Itaendelea 💥



MOYO WA JENERALI JAX
EP05
MTUNZI;HUSQER BALTAZAR

"Bhana eeh stori gani hizi hebu sepa bhana" Mei aliongea

"Kwani ni vibaya kuuliza kitu kama hicho....!"

"Saa saba za usiku unakuja kwenye chumba cha mtu kuuliza kuhusu vilele mbona na kuheshimu sana bwana Jenerali" Mei aliongea

Jax alitaka kutoa sigara nyingine tena baada ya kuona Mei kama kapanic hivi.

"Kwanini unapenda sigara..." Mei alifoka kisha akamkwapua.
Safari hii Jax alimuwahi akamshika mikono yote.

"Unaonekana hujawahi kufikishwa kileleni na ndio sababu wewe ni mtu wa hasira kupita kiasi...." Jax aliongea akiwa kamkazia macho

"Emu niachie halafu uondoke nataka kulala nimechoka kesho na ratiba ngumu...." Mei aliongea

Jax aliachia tabasamu kwa namna Mei alivyo vurugika.
Alimsogeza karibu akamkumbatia

"Huwezi kuendelea kuwa na hasira namna hii kisa mahusiano, nilikuja hapa kukufariji.... tafadhali sana naomba usinifikirie vibaya. Na wala usinichukulie punguani kwa swali nililokuuliza"

Mei aliangua kilio, tangu atemwe hakuwa amelia vizuri. Pamoja na kwamba Daktari T ni rafiki yake lakini hajapata nafasi ya kueleza machungu yake.

Japo Jax hajawahi kukutana na hii hali lakini anaamini sex ni njia pekee ya kufuta maumivu katika moyo wa mtu.
Alijikuta akimshika shika Mei, yaani pamoja na kwamba ana mpenzi wake katika kambi hili lakini aliingiwa na tamaa ya kumfikisha binti huyu kileleni. Alihitaji kumfutia kumbukumbu mbaya za boyfriend wake.

Ubongo wa Mei uliusikia mpapaso wa Jax. Tararibu machungu ya maumivu yalipungua, badala ya kulia alianza kutoa ushirikiano pia wa kumshika shika.

Walijikuta wakifanya mapenzi, siku ya leo ilikuwa sikukuu kwa Mei kwa sababu alikishuhudia kilele namna kinavyo kuwa.

Jenerali Jax alinogewa pia kulala kwa Mei usiku mzima, kama ujuavyo siku zote nguo mpya huziba nafasi ya nguo kuukuu.

Mei anakuja kushtuka asubuhi akiwa kalalia kifua cha Jax.
Walijikuta wakipeana cha asubuhi kisha kila mtu akashika hamsini zake.

Walianza kama utani kuwa wanapeana kama msaada. Lakini kadri siku zilivyoenda walijikuta wakibadilishana namba za simu.

Asubuhi moja Mei akiwa ametulia ofisini kwake alijikuta akiiangalia picha ya Jax.
Alikuwa na kazi ya kuikuza, alianza kuikagua kuanzia pua, macho, masikio na mdomo.

Daktari T anashindwa kuelewa ni kitu gani kimemuweka Mei bize mpaka ashindwe kumsikia.

Tobaaaaa wee! anashtuka baada ya kuikuta picha ya Jax.
Alimkwapua simu akihitaji kujihakikishia zaidi kitu anachokiona, walijikuta wakikimbizana kuzunguka hospitali. Bahati mbaya Daktari T aligongana na Sia (demu wa Jax).
Simu ilitaka kwenda chini Sia alikuwa mwema kwa kumsaidia kuidaka, anashangaa baada ya kuiona sura ya Jax

"Hii ni simu yako...." Sia alimuuliza Mei aliyekuwa nyuma ya Daktari T

Itaendelea 💥


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote