MR. ARROGANT 💎🔥 1
MTUNZI: SMILE SHINE
Ilikuwa majira ya saa kumi jioni msichana mrembo (Jasmine) aliye kuwa amevalia gauni lake zuri la rangi ya gold na kikoti cheupe alikuwa anatembea kando ya barabara huku akibinyeza simu yake ni wazi alikuwa akichati na mtu.
Ghafla lilopita gari na kumwagiwa maji ya mvua yaliyokuwa yametuama kwenye dimbwi.
Jasmine alishituka akasimana na kuanza kutoa maneno.
" Hivi nyie wenye magari mna nini lakini ? Anajiona nimemaliza kila kitu kwenye hii dunia ... Aliongea maneno mengi sana lakini ile gari haikusimama.
" Huyu mtu jeuri sana na hawa watu nawapenda mno ipo siku tutaonana tu .
Wakati Jasmine anasema hivyo kumbe alikuwa ameshika namba za ile gari.
Baada ya wiki mbili kupita akiwa kwenye mizunguko yake alipita sehemu akalikuta ile gari imesimama mbele ya super market moja.
Alisoma namba na kuhakikisha ndio ile gari iliyomwagika maji.
Alitabasamu kidogo kisha akasema.
Dawa ya jeuri ni jeuri sasa ngoja nilipize. Aliangalia kila upande akaona watu wapo Bize na mambo yao.
Aliangalia chini akaokota kipande cha chupa alafu akasogea karibu na gari na kuanza kukwambia rangi ya gari huku akiandika.
" Acha ulimbukeni hata sisi tunayo magari ila tuna nidhamu .
Alipomaliza kuandika akasimama na kusoma kwa sauti alafu akasema.
" Pumbavu ujumbe utamfikia.
ile anageuka anakutana na kijana mtanashati ambae alikuwa akimuangalia huku akiwa kakunja uso wake mpaka matuta yakajichora usoni kwake.
kijana huyo hakuwa mwingine ni Leon Maxwell tajiri mwenye sura ya kuvutia na jeuri isiyoelezeka. Alijulikana mjini kama Mr. Arrogant mtu asiyejali hisia za wengine, mwenye dharau na anayeamini kila mtu yuko chini yake.
Leo alimsogelea karibu
" Kwanini umeharibu gari yangu?
" Sijaharibu nilikuwa najaribu kufikisha ujumbe.
" Ujumbe gani wa kipuuzi?
" Upuuzi uliuanza wewe juzi, kwani ilinimwagia maji machafu na ukaisha kuchungulia , ukiniangalia kama takataka kisha ukaendelea na safari yako.
" Unajua hii gari yangu ina thamani gani?
Jasmine alitabasamu kwa jeuri, mikono yake ikiwa kifuani kwake.
“Sijui, na sitaki kujua Lakini najua kitu kimoja thamani ya gari lako haiwezi kulipa heshima unayopaswa kuwapa binadamu wengine. Ndio maana niliandika ili nikufundishe nidhamu kila ukisoma hapo utakuwa unakumbuka unatakiwa kuwa na heshima pamoja na utu.
Watu waliokuwa karibu na supermarket wakawa wamesimama, wakifuatilia mrumbano yao kama sinema ya bure.
Leon alicheka kwa dharau, akamuangalia Jasmine juu,chini kisha akasema kwa sauti ya kudharau:
“Kwa mara ya kwanza nimekutana na mwanamke mwenye ulimi mrefu kuliko akili yake.
Umejiingiza kwenye matatizo makubwa bila kujua.
Jasmine akamkaribia kwa hatua moja zaidi, macho yake yakimwangalia bila woga.
“Na wewe kwa mara ya kwanza umekutana na mwanamke ambaye hakubali kuonewa hata kidogo. Umenimwagia maji, sasa nimekulipiza. Ni rahisi tu, haki sawa.
Leon hakupenda aliona kama anadhalilishwa. Kwa mara ya kwanza alihisi kuvunjiwa heshima Hakuna aliyewahi kumsimamia kwa ujasiri namna ile, tena mbele za watu.
Aliinama karibu na sikio la Jasmine, akasema kwa sauti ya chini lakini kwa ukali:
“Umeamua kucheza na moto, na moto wangu unachoma vibaya. Nitaona utavumiliaje.
Jasmine akasogea nyuma hatua mbili, lakini tabasamu lake halikupotea usoni mwake
“Nami nataka kuona moto wako unachoma kiasi gani, Mr. Arrogant.
Walitazamana kwa sekunde chache, kukawa kimya .
Leon akapanda gari lake, akawasha gari na kuondoka huku vumbi kidogo likitimka
Jasmine alibaki akitabasamu, akipiga makofi kwa kujipongeza.
“Leo nimekutana na jeuri mwenzangu. Huu mchezo utakua tamu sana.”
Hapo ndipo mchezo wa jeuri dhidi ya jeuri ulipoanza rasm.
MR. ARROGANT 💎🔥 2
MTUNZI: SMILE SHINE
Siku zilisogea Jasmine akiwa kwenye duka la shangazi yake wakiwa wanaongea.
" Shangazi sasa inakuwaje kuhusu kupata kazi bado haujaongea na huyo rafiki yako.
" Amesema mpaka mwezi wa sita ndio kutakuwa na nafasi za kazi .
" Kwahiyo nitakaa miezi yote hii bila kazi. Sasa nini maana ya elimu yangu nimesoma kwa bidii changamoto kwenye ajira , daaaah inakatisha tamaa sana.
"Haifai kukata tamaa kabla haujafanikiwa.
Jasmine aliondoka na kwenda kupanga nguo mpya ambazo zilikuwa zimeingia muda sio mrefu na wateja walianza kuja kununua mali mpya maana shangazi yake aliwapigia simu wateja wake.
Muda uleule, akiwa anapanga mizigo ya dukani, ghafla gari jeupe likasimama mbele ya duka, mlango ukafunguliwa na mtu akashuka taratibu.
Hakuwa mwingine, bali ni Leon Maxwell. Aliekuwa amevalia Suruali yake nyeusi iliyokaa fit, shati la kifahari lililofunguliwa kifua, na miwani ya nyeusi iliyositiri macho yake makali. Alitembea kwa kujiamini, kila hatua ikionekana kama inatetemesha dunia.
Jasmine alishika kiuno, akamwangalia moja kwa moja.
Leon alienda kukutana na Nadia shangazi yake Jasmine.
" Habari.
" Salama Leon karibu.
" Nimeshakaribia nataka kuona mali mpya.
" Kuna binti yangu yupo huko unaweza kwenda kuangalia.
Leon alianza kuangalia nguo kabla hajamuona Jasmine .
Alivyozidi kusogea ndio wakitaja uso kwa uso. Leon alivua miwani yake na kumuangalia .
" Wewe kivuruge tumekusanya tena leo?
“Leo umekuja kununua nini? Au umekuja kuomba msamaha?” aliuliza kwa dhihaka.
Leon akatoa macho yake makali yakimkodolea.
“Msamaha? Mimi? Kukuomba msamaha wewe?” alicheka kidogo, sauti kwa dharau alafu akaendelea kusema
“Hapana, nimekuja kukuonya. Mara ya pili ukigusana na gari yangu au mali yangu, utajuta kuishi kukifahamu.
Jasmine alicheka kwa sauti, wateja waliokuwa dukani wakageuka.
“Jeuri zako hazinitishi Nimeshakuambia mimi sio wa kuonewa. Sasa ukitaka vita, vita tutapigana. Nani ashindwe ni hadithi ya baadaye.”
Kwa mara ya kwanza, Leon alibaki kimya sekunde mbili, akimtazama tu. Ndani yake moyo ulianza kushtuka kulikuwa na kitu cha ajabu kwa msichana huyu. Ujasiri wake, namna anavyoongea bila woga .
Baada ya Nadia kuona kuna kitu hakipo sawa alisogea karibu.
" Jasmine kuna shida gani na mteja wangu?
Kabla Jasmine hajajibu Leon alijibu.
" Usijali dada Nadia mimi na Jasmine tunakutana na tupo kibiashara nenda kaendelee na wateja wengine.
" Sawa.
Nadia aliondoka akawa acha .
Jasmine alimuangalia usoni na kuachia tabasamu .
Leon nae alitabasamu kwa jeuri, akamsogelea karibu kabisa.
“Basi Jasmine kuanzia leo mimi na wewe utakuwa na mchezo wa paka na panya. Tuone nani atashindwa.
Jasmine naye hakurudi nyuma.
“Naona unaona kuwa wewe ni paka. Mimi si panya, mimi ni simba.”
Kuna wateja wawili walikuwa walishindwa kujizuia, wakaanza kucheka kimnya kimnya
“Hawa watu wawili wakioana lazima nyumba iwake moto.
Leon a akaondoka taratibu huku tabasamu la kijanja likibaki usoni mwake aliendelea kuchagua nguo huku Jasmine akabaki akitetemeka kwa hasira, lakini ndani ya moyo wake kulikuwa na kitu kipya mapigo yake ya moyo yalikuwa yanadunda haraka mno.
Alijisemea kimoyomoyo:
“Huyu Mr. Arrogant atanitesa lakini sitakubali hata kidogo.
Leon alichagua nguo anazitaja alipomaliza alipitia alipokuwa anapanga nguo Jasmine akasimama na kusema.
" Jasmine binti mwenye jina tamu lisiloendana na matendo yake. Nadhani tuna safari ndefu na huu ni mwanzo .
" Sawa mr arrogant. Safari ndefu niya kwenda mbinguni bila shaka tutaenda pamoja huku tukiwa tumeshikana mikono.
Leon alitoa tabasamu dogo kisha akaenda kulipia nguo zake na kuondoka.
MR. ARROGANT 💎🔥 3
Mtunzi: Smile Shine
Wiki moja badae Jasmine alikuwa anajiandaa kutoka mara Rafiki yake mkubwa, Sasha, alifika nyumbani kwao akiwa na furaha kubwa.
“Jas! Leo nimekuja na habari nzuri.
" Habari gani?
"Hii ni nafasi yako. Kuna kampuni kubwa imetoa tangazo la kazi. Wanaajiri receptionists, secretaries na hata personal assistants. Jaribu bahati yako shoga yangu. Sasha alimkabidhi tangazo lililochapwa.
Jasmine alilisoma kwa makini, moyo wake ukijaa matumaini.
“Kampuni ya Maxwell Empire…” alisoma kwa sauti ya chini.
“Hiyo ni kampuni kubwa sana. Ila watakubali kweli mtu kama mimi?”
Sasha akamshika mkono.
“Hakuna lisilowezekana. Wewe ni mrembo, una akili, na una ujasiri. Hebu jaribu. Hii inaweza kubadilisha maisha yako.
" Asante rafiki yangu kwa kunitia moyo .
Ilipofika Usiku Jasmine aliandaa CV yake vizuri, akakaa akiiombea nafasi hiyo kwa moyo wa dhati.
" MUNGU wangu naomba wakati huu ufike wakati ule uliopanga mimi nifanikiwe. Kesho niende kupata kazi kwenye hii kampuni kubwa.
Siku ya interview ilipofika, Jasmine aliamka mapema, akaivaa sketi ndefu nyeusi na blouse nyeupe iliyompendeza sana. Alionekana kama mwanamke wa ofisini.
Alikaa kwenye foleni kusubiri interview kuanza.
Interview ilianza baada ya dakika chache, na jambo la kushangaza ni kwamba Jasmine hakuulizwa maswali mengi wala magumu. maofisa walivutiwa na kujiamini kwake, na baada ya dakika chache walipeana macho kana kwamba tayari walikuwa wameamua.
Mmoja alimuangalia usoni alafu akasema
“Tutawasiliana na wewe ndani ya siku tatu.
" Sawa , asanteni sana , muwe na kazi njema.
Ndani ya siku mbili tu alipigiwa simu kutoka kwenye kampuni ya aliyofanya interview
“Hongera Jasmine! Umechaguliwa kujiunga na kampuni yetu kama secretary mpya!”
Jasmine alipiga kelele za furaha, akamkumbatia Sasha ambaye alikuwa karibu.
“Hii ni ndoto yangu imetimia. Hatimaye nimepata kazi kwenye kampuni kubwa!”
" Hongera sana rafiki yangu .
" Niliomba sana jamani.
" Hata mimi nilikuwa nina matumaini kuwa utapata kazi. Jasmine na Sasha waliendelea kufurahia bila kujua ilikuwa jaribio kubwa la moyo wake.
Kesho yake jasmealiamka mapema sana na kuanza kufanya maandalizi, siku hiyo alivalia nguo yake mpya ambayo alichukua dukani kwa shangazi yake , nywele zake alizitengeneza vizuri na kuwa kwenye muonekana mzuri.
Jasmine alifika kazini akiwa na furaha, akitembelea jengo kubwa la kifahari la Maxwell Empire. Alivutiwa na ujenzi wa kisasa, magari ya kifahari kwenye parking, na wafanyakazi waliovaa suti safi.
Alipofika mapokezi, receptionist aliangalia orodha na kumwambia:
“Karibu, Jasmine. Utakuwa secretary wa boss.”
Jasmine akatabasamu.
“Boss gani?” aliuliza.
Receptionist akamjibu na kusema:
“Mheshimiwa Leon Maxwell.”
Jasmine alibaki ameduwaa.
“What?!” alishusha pumzi, moyo wake ukianza kudunda kwa kasi.
“Yaani… yule… yule mwenye jeuri ndio boss wa hii kampuni?!”
Hapo macho yake yakajaa mshangao na hasira kwa wakati mmoja.
Mara mlango wa ofisi kubwa ulifunguliwa. Leon Maxwell mwenye suti nyeusi iliyompendeza sana akatokea, akitembea kwa kujiamini. Macho yake makali yakatua moja kwa moja kwa Jasmine.
Tabasamu la dharau likajaa usoni mwake.
“Karibu Jasmine. Sikujua mbinu zako tungefanya kazi haraka sana, sasa umekuja moja kwa moja kwenye himaya yangu. Huu mchezo sasa ndio unaanza rasmi.
Jasmine akavuta pumzi ndefu, akainua kichwa kwa ujasiri.
“Hata kama wewe ndio boss, Leon, kumbuka kitu kimoja Mimi siogopi. Na usitegemee nitainama mbele yako....
Kabla hajamaliza kuongea leon alimkatisha.
" Wewe ni secretary wangu sasa , njoo ofisini kwangu haraka.
Leon alitangulia kuelekea ofisini kwake na Jasmine alibaki akiwa kasimama huku akiangalia baadhi ya wafanyakazi usoni.
" Huu ni ujinga Jasmine mimi sijawahi kuogopa kitu naenda. Alijisemea kimnya kimnya kisha akapiga hatua kuelekea ofisini kwa boss Leon ambae yeye alimpa jina la mr arrogant.
MR ARROGANT 💎 🔥 4
MTUNZI SMILE SHINE
Jasmine alipoingia ofisini kwa Leon, macho yake yote yaliangaza ukutani kuangalia mapambo ya kifahari, viti vya safi vya ngozi , hadi harufu ya manukato ya kiume yaliyotawala mume ndani.
Kwa sekunde chache alikuwa ameshajua huyo mtu sio wa mchezo na kinachompa jeuri ni utajiri wake.
kweli huyu jamaa alikuwa tajiri tofauti na alivyoonekana barabarani.
Leon, akiwa amekaa kwenye kiti chake kikubwa cha ngozi, alimkodolea macho huku akitabasamu kwa dharau.
“Karibu ofisini kwangu, Jasmine. Najua hujawahi kufika kwenye ofisi ya aina hii. Hapa siyo barabarani, hapa kuna nidhamu. Na kama secretary wangu, utajifunza nidhamu na kufanya kile ninachotaka mimi.
Jasmine akapumua kwa nguvu, kisha akasimama mbele yake kwa ujasiri.
“Usijisumbue, sitaki upoteze muda wako kunifundisha. Mimi najua kufanya kazi. Nikuambie kitu, Mr. Arrogant… nitaifanya kazi yangu vizuri zaidi ya vile unavyotarajia, na sitakupa nafasi ya kunidharau hata kidogo maana hapa tupo kwaajili ya kutegemeana wewe unataka nikufanyie kazi ili mambo yako yaende kama ulivyotaka na mimi nitafanya ilinilipwe kukamilisha mambo yangu.
Leon, akiwa amekaa kwenye kiti chake kikubwa cha ngozi, alimkodolea macho huku akitabasamu kwa dharau.
“Karibu ofisini kwangu, Jasmine. Najua hujawahi kufika kwenye ofisi ya aina hii. Hapa siyo barabarani, hapa kuna nidhamu. Na kama secretary wangu, utajifunza nidhamu na kufanya kile ninachotaka mimi.
Leon akacheka kwa dharau, alinyanyuka kisha akasogea karibu zaidi na aliposimama Jasmine
" Unaongea sana kwasababu mdomo mali yako lakini usisahau mimi ni boss hapa.
" Kumbuka nina uwezo wa kuacha kazi.
" Kama unaweza fanya.
" Unafikiri nashindwa?
" Kama una milioni 50 basi nikupe alafu uondoke.
" Milioni 50 ya kwenda wapi? Kwa kazi gani uliyo fanya.
" Ukisoma vizuri ile mkataba uliosaini?
Jasmine alitulia kwanza akakumbuka hakusoma vizuri ule mkataba alikurupuka kusaini.
Leon akiendelea kutabasamu huku akimzunguka.
" Hiyo pesa huna ,Kwa sasa, nakupa kazi rahisi nenda ofisi ya chini chukua mafaili ya mikataba mia moja, uyapange kwa majina na tarehe kabla saa saba kazi iwe imekamilika.
Jasmine akashtuka.
“Mikataba mia moja? Leo leo?”
“Ndiyo. Ama uanze sasa hivi, ama uandike barua ya kujiuzulu kabla siku yako ya kwanza haijaisha .Leon alijibanza nyuma kwenye kiti chake, macho yake yakimwangalia Jasmine kwa majivuno.
Kwa sekunde chache, Jasmine alihisi hasira zinapanda mwilini mwake ilitetemeka, lakini hakutaka kuonyesha udhaifu.
Alikuna nywele zake taratibu, kisha akasema kwa sauti ya utulivu:
“Sawa boss. Tutaona .
Akatoka ofisini kwa hatua kubwa, huku Leon akimtazama akiondoka.
Kwa mara nyingine, alihisi kuwa na amani kufanikiwa kucheza na akili ya Jasmine japokuwa Mwanamke huyu hakumwogopa, hakujipendekeza, na hakutetemeka mbele yake kama wengine.
“Jas…mine,” Leon alirudia jina hilo kwa sauti ya chini, macho yake yaking’aa kana kwamba ameona changamoto mpya.
“Huyu secretary mpya anaweza kunichosha lakini pia inanivutia kwa njia ambayo sijawahi kuhisi.
Wakati huo, Jasmine alishuka haraka kwenye ofisi ya chini. Faili zilikuwa nyingi kweli kweli, lakini alikaa mezani na kuanza kazi kwa bidii.
Sasha alimtumia messege kuuliza “Mambo yakoje kazi mpya?” Jasmine akajibu:
“Nipo vitani, lakini usijali. Nitaibuka mshindi.
" Kwanini unasema hivyo?
" Sasha kunitumia msg ni kama kunipotezea muda , tulia kwanza nikija nitakwambia kila kitu.
Alimaliza kutuma messege kisha akaweka simu pembeni na kuendelea kufanya kazi.
Saa zikapita, na muda wa saa sita na nusu ulipofika, Jasmine akabeba mafaili yote yaliyopangwa kwa mpangilio sahihi, akayapeleka ofisini kwa Leon.
Alipoyapiga mezani kwa kishindo , Leon akainua macho, akashangaa.
“You did it?” aliuliza kwa mshangao.
Jasmine akatabasamu kwa ushindi.
“Ndiyo, boss. Sio kila mtu anakimbia matatizo. Wengine tunayakabili. Hiyo ndio tofauti yetu.
Kwa mara ya kwanza, Leon hakujua aseme kitu gani. Alihisi kama vile amedhalilishwa.
Akasogeza kiti chake nyuma, akamuangalia Jasmine juu mpaka chini, kisha akasema kwa sauti ya chini lakini yenye nguvu:
“Hii michezo haitakuwa rahisi kwako, Jasmine. Nakuhakikishia, nitakufanya ukimbie mwenyewe.
Jasmine naye akainua kichwa na kumuangalia usoni bila kukwepesha macho
“Na mimi nakuhakikishia, Mr. Arrogant… mimi siyo wa kukimbia. Hata mbele ya moto wako, nitabaki imara.
Kimya kikatawala ofisini, macho yao mawili yakakutana kwa jeuri, chuki, lakini ndani yake kulikuwa na cheche mpya.
" Hebu toka ofisini kwangu.
" Sawa mr arrogant.
" Am your boss.
" Oooh kumbe ... Sawa boss.
Alijibu Jasmine kisha akageuka akawa anaondoka alipofika mlangoni alifungua mlango kisha akageuka kumuangalia wakati huo Leon bado alikuwa anamuangalia. Jasmine aliachia tabasamu kisha akatoka na kufunga mlango.
Siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwa Jasmine hakupata muda wa kutulia kila mara aliitwa ofisini kwa leon tena hata bila sababu maalumu.
Jioni alirudi nyumbani kwao akafukia sebleni alivua viatu vyake virefu na kutupa huko .
" Watu wengine wa roho za kinyama kweli yani sijui alikuwa anafikiria nini kunizungusha na hivi viatu virefu ona vilivyonichubua.
Jasmine waliongea mwenyewe huku akiangalia miguu yake . Mara Sasha aliingia.
" Vipi shost kazi imeendaje?
" Mmmh kwanza nikuulize unamfahamu boss wa ile kampuni?
" Hapana .
" Tangazo la kazi ulipata wapi?
" Nilipewa na yule binamu yangu Jerry alijua bado natafuta kazi nikaona sio vibaya kukupa wewe rafiki yangu maana umehangaika sana kupata kazi.
" Ni kweli nikehangaika lakini nilipoingia nipa moto.
" Vipi yani sijakuelewa.
" Boss wa ile kampuni ni kichaa , ni yule niliekwambia nimegombana nae.
" Eeeee....
" Wewe endelea kuitikia hapo lakini mwenzio nipo kwenye kikaango na sijui natokaje.
" Kaka ni ngumu kwako kwanini usiache kazi.
" Mwenzio alijua hilo mapema akajua kucheza na akili yangu kanisainisha mkataba kuwa nilitaka kuacha kazi natakiwa kulipa milion50.
" Tobaaaaa. Alisema Sasha huku akiweka mikono kichwani.
" Kwahiyo huku sina mkataba ila saini tu.
" Nilipotoa juu juu kuna vipengele sikusema vizuri.
" Pole rafiki yangu.
" Muda wa kunipa pole bado haijafika nitakufanyia vituko mpaka ataimba poo. Mbona atanifukuza kazi mwenyewe.
MR ARROGANT 💎🔥 5
MTUNZI SMILE SHINE
Kesho yake mapema sana Jasmine aliwahi kazini baada ya dakika tano kufika na Leon alifika ambapo haikuwa kawaida yake kufika mapema.
" Afadhali umewahi kufika kabla yangu maana ungenikuta ningejua fahamu moja matata sana.
Jasmine hakujibu zaidi ya kumuangalia .
“Jasmine, leta kahawa yangu ofisini tena ufanye haraka.
" Sawa boss.
Jasmine alienda kuchukua kahawa na kupeleka ofisini kwa Leon kisha akaweka mezani na kutaka kuondoka.
" Unaenda wapi kaka sijaonja vipi kama ikiwa mbaya?
Jasmine alisimama,
Leon alinyanyua kikombe akaangalia kisha akainua uso kumuangalia Jasmine “Nimekosea kukwambia nilitaka cappuccino siyo black coffee. Rudisha hii, leta nyingine.
" Huu ni utani wa ngumi . Alisema Jasmine kwa sauti ya chini.
" Unasemaje?
" Kwani umesikia nini? Haamini alichukua ile kahawa alafu akatoka ofisini .
Aliporudi tena alipeleka na cappuccino, Leon alipouona alitingisha kichwa.
“Ah! Hii haina sukari, unadhani nakunywa sumu?”
Jasmine alimkodolea macho.
“Ungetoa maelekezo yaliyokamilika , sasa mimi ningeomba kuwa unataka na sukari boss.
Leon akacheka.
“Naam, unanijibu sasa? Kumbuka wewe ni secretary, mimi ni boss.
“ Uwe Boss au sio boss uhalisia unabaki pale pale mimi sio mtumwa wako. Jasmine alijibu kwa sauti ya kujiamini, kisha akatoka ofisini bila kumuogopa.
" Kakobe alivyokuwa na jeuri yani sijui ni kabila gani huyu msichana.
Baadaye mchana:
Leon alimuita tena ofisini kwake.
“Niletee faili la mkataba wa kampuni ya Eastland haraka.”
Jasmine alifika na faili. Leon akalipokea bila hata kumtazama.
Baada ya dakika mbili, akabonyeza tena intercom.
“Jasmine! Faili hili halina kurasa za 45 na 46. Unajua hii ni kazi unaifanya kizembe sana na mimi huwa sipendi kufanya kazi na watu wa aina hiyo .
Jasmine alirudi ofisini kwa Leon huku amekunja uso. Akafungua faili pale mbele yake, akazitoa kurasa hizo kutoka katikati akasema,
“Ziko hapa boss. Labda macho yako yalikuwa yamechoka au hawaoni vizuri . Ila kwa ushauri wa bure ni bora uwe unakula karoti kwa wingi. Itasaidia kuona vizuri pia kuwa Mjanja kama sungura.
Leon alikodolea macho Jasmine.
“Unaanza kunichokoza eeh?”
“Siwezi chokoza mtu asiyekuwa na maana kwangu. Najua kazi yangu na naifanya vizuri. Kama huwezi kuthamini, huo ni udhaifu wako boss.” Jasmine alijibu kwa sauti thabiti, kisha akatoka.
" Daaaah! Alisema Leon kama kwamba anaanza kushindwa kwenye hili pambano.
Jioni Leon alikaa peke yake nyumbani kwake akiwa kajishika kidevu huku akifikiria Kila mara alipojaribu kumkandamiza Jasmine, binti huyo hakuwahi kuyumba. Hakumlilia, hakumwogopa, wala kuomba msamaha .
“Mbona huyu msichana ni tofauti na wengine?” alijiuliza.
Kila secretary aliyewahi kufanya naye kazi aliishia kuogopa au kuacha kazi. Lakini huyu Jasmine alikuwa moto wa kuotea mbali.
Kwa mbali, moyo wake ulianza kuchora taswira ya Jasmine kwa namna nyingine siyo kama mpinzani, bali kama kitu cha pekee.
Lakini kwa jeuri yake, Leon alijifunga moyo.
“Hapana… sitawahi kuangukia kwa secretary. Mimi ni Leon Maxwell. Mimi ndio mr arrogant kama mwenyewe alivyonipa hilo jina.
Kesho yake asubuhi Jasmine alikuwa ofisini akipanga mafaili ghafla simu ya mezani ikaita.
Aliangalia ile simu kisha akashusha pumzi .
" Uuuuh kumekuja mr arrogant ameshaanza usumbufu wake. Alipokea ile simu na kusikiliza
“Jasmine, njoo ofisini kwangu mara moja.”
Sauti ile nzito, ya kuamuru, haikuhitaji majibu. Ilikuwa ya Leon. Jasmine akirudisha simu kisha akaenda ofisini kwa Leon.
Alisimama mlangoni, Leon alimuangalia kutoka juu mpaka chini kisha akakunja mdomo wake kwa jeuri.
“Chukua hii faili alimrushia bila hata kumuangalia vizuri, "peleka ghorofa ya tatu, kisha rudi haraka kuchukua box hili, ulipeleke ghorofa ya chini. Nataka ukimaliza turudi tena hapa kuna kazi nyingi za kufanya.
Jasmine alibaki akimtazama .
“Unanichezea wewe, aliongea kwa ukali kidogo.
Leon alitabasamu kijeuri.
“Hii ni kazi yako. Au ulifikiri kazi ya secretary ni kupaka lipstick na kutabasamu tu au kuvaa visketi vifupi kama hivyo?
Jasmine walifikiria kwa sekunde chache alitaka kumwambia aende akamtafute mtu wa kumtumikisha. Lakini hakuona haja ya kumjibu hivyo
“Vizuri. Kama hii ndio kazi yangu nitafanya. Lakini usisubiri ukafikiri nitaonekana dhaifu.
Alibeba box kwa ujasiri na kuelekea kwenye lifti. Leon alimsindikiza kwa macho, akibaki kimya. Ndani ya moyo wake, badala ya kufurahia kwamba amemkomesha alijihisi kama kuna kitu cha kipekee kwenye msimamo wa Jasmine.
Leon alichukua simu akampigia mtu.
" Nataka lift zisifanye kazi kwa muda wa nusu saa.
Alifanya yote hayo ili kumkomoa Jasmine.
Saa nzima ilipita Jasmine akibeba mafaili kutoka juu kupeleka chini kwa kutumia ngazi bila kulalamika, jasho likimtoka lakini kila aliporudi ofisini, aliweka tabasamu kubwa tu.
Baada ya kumaliza kazi alisimama mbele ya leon na kusema
“Boss, niingie mission nyingine au kazi imeisha?” alimuuliza akiwa ameegemea mlango, akicheka kwa dharau ndogo.
Leon alibaki kimya sekunde chache, akitabasamu upande mmoja wa mdomo wake.
“Unapenda changamoto, Jasmine. Tuone nani ataweza kushinda hii vita ya jeuri mimi au wewe.
Jasmine valijivuta kivivu mpaka mezani alishika meza na kuinama kidogo.
" Huna lolote Leon kuna kitu nimegundua kipo kwenye moyo wako.
" Kitu gani.
" Unanipenda.
Leon alimkazia macho wakajikuta wanaangaliana moja kwa moja.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote