MWIZI WA MOYO WANGU
By Miss Hamida
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Siku mbili kabla ya harusi yao Nayce anamuacha Rolland na kwenda Zanzibar kwaajili ya mwanaume mwingine.
Rolland anapo gundua, anapata maumivu makali na kuamua kumuoa Nirvana kwa nguvu ambae ni mdogo wa Nayce, ili kuficha aibu.
Ndipo Nayce anajua kuwa mwanaume alie mfuata Zanzibar alikua anaoa mwanamke mwingine. Akajutia sana kumuacha Rolland.
Anarudi na kukuta tayari Rolland kashaoa tena kamuoa mdogo wake. Hataki kukubali, anatumia nguvu zake zote kumrudisha Rolland kwake.
Mwanzoni anafanikiwa lakini kadri siku zinavyo zidi kwenda ndivyo Jinsi ambavyo Rolland anampenda Nirvana zaidi.
We unadhani Nayce atafanya nini???!
SEHEMU YA : 1
Ni jioni moja tulivu sana, familia ya Wakili Dickson ilikua inapata chakula cha jioni kwa furaha mno sababu zilibaki siku mbili tu ili kijana wao apate kufunga ndoa.
Stori za hapa pale zilikua zikiendelea huku matabasamu yakitawala usoni mwao. Mara ghafla simu ya Rolland ikaingia ujumbe mfupi.
Hakutaka kuusoma maana haikua adabu kwa mtu kushika simu wakati wa kupata chakula. Lakini jinsi alivyo zidi kupotezea ndivyo meseji zilivyo zidi kuingia kama mvua.
Aliweka kijiko pembeni, akachukua simu yake na kusoma zile jumbe. Jumbe za kwanza zilitoka kwa mchumba wake Nayce, na jumbe za pili zilitoka kwa Nirvana ambae ni mdogo wa Nayce.
Rolland alianza kwanza kwa kusoma ujumbe toka kwa Nayce, na ujumbe wenyewe ulisomeka hivii :-
“Najua unanipenda na mimi nakupenda pia! Ila kuna mtu nampenda zaidi! Huyo ndie aliefanikiwa kuushikilia moyo wangu kisawasawa! I am sorry Rolland siwezi kufunga ndoa na wewe”
Rolland alipomaliza kuusoma ule ujumbe akahisi kupagawa. Jasho lilimtoka kama mvua huku akianza kupanick.
Akahisi labda amekosea kusoma. Akaufungua kwa mara nyingine na kuusoma tena! Alipojihakikishia kua hajakosea kusoma, akapagawa zaidi!
Akasimama haraka huku familia nzima ikimshangaa
“Rolland kuna nini?” Mama yake alikua wa kwanza kumuuliza
“Nakuja sasa ivi!”
“Unaenda wapi?”
Hakujibu, alikimbilia mezani, akachukua funguo za gari na kutoka spidi spidi kuwahi nyumbani kwa Nayce.
Huku nyuma familia yake ikabakia kuwa kwenye mshangao na taharuki.
“Kuna nini??”
“Ukiniuliza mimi nitamuuliza nani?” Wakili Dickson ambae ni Baba wa Rolland alijibu
“Robson wewe si rafiki wa Rolland, utakua unajua nini kinaendelea” Mama Rolland akamgeukia rafiki wa mwanae
“No! Sijui chochote! Nimeona akisoma ujumbe kwenye simu yake na ghafla tu akabadilika”
“Na ametoka mbio mbio kweli sasa sijui itakuaje”
“Yule ni mtu mzima sasa! Muacheni, sisi tuendelee kula! Akirudi atatuambia ni kipi kinacho endelea”
Wote Wakamsikiliza wakili Dickson kisha wakarudi mezani kuendelea kula chakula, na mara hii walikua kimya sana hata stori hazikuendelea tena.
Upande wa Rolland alikua tayari kashafika nyumbani kwa Nayce. Alipoingia tu alikutana na Nirvana mlangoni
“Yupo wapi Nayce??”
“Ameondoka” Nirvana alijibu kwa uoga maana Rolland alikua serious vibaya mno
“Whaat? Kaondoka kaenda wapi? Kuna nini kinacho endelea”
“Ameenda Zanzibar! Ameenda kukutana na Johnson!”
“Johnson ni nani? Mbona sikuelewi Nirvana”
“Dada anampenda Johnson! Alikua na mahusiano nae kipindi alipokua chuo! Kipindi icho wewe ulikua Masomoni Canada ivyo hukuweza kumuona. Lakini kwa bahati mbaya Johnson alipata nafasi ya kwenda kusoma nchi za nje! Tangu aondoke hajawi kumtafuta dada tena. Sasa leo kampigia simu na kumuambia tayari amerudi Tanzania na yupo Zanzibar. Na dada kusikia vile akawa kama amechanganyikiwa sababu anampenda sana! Ivi ninavyo ongea na wewe amemfuata huko alipo”
Rolland akahisi kuzimia, alidhani yeye ni mwanaume wa pekee aliekua anapendwa na Nayce kumbe Nayce alikua na mapenzi makubwa na mtu mwingine.
“Samahani sana Shem, dada pia amenambia nikupe hii” Nirvana alimkabidhi pete yake, Rolland akawa haamini anacho kiona
“Kwaiyo Nayce alikua na mwanaume mwingine?? Sasa kwanini hakunambia kama hanipendi?? Anakuja kuniacha siku mbili kabla ya harusi?? Tena kwa njia ya sms???” Aliongea kwa uchungu kiasi cha Nirvana kumuonea huruma.
“Am sorry shem, mimi mwenyewe sikutegemea kama hili lingetokea”
Rolland alinyamaza kwa dakika kadhaa, alifikiria jambo kisha mwishoni akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Nayce mara nyingi na haikua ikipatikana.
“Hapatikani”
“Amezima simu yake, hata mimi nime mpigia hapatikani”
“Okay! Twende”
“Wapi?” Nirvana alitoa macho
“Kama dada yako ameondoka unategemea nitamuoa nani mwingine zaidi yako? Wewe ndo utakua mbadala wa dada yako”
Nirvana aliposikia vile akadhani ni utani.
“Shem najua unaumia lakini sidhani kama ni mahali sahihi kwa kuleta utani?”
“Umeona kama nachekesha hapa?? Tuondoke” alimkamata Nirvana mkono kwa nguvu na Nirvana nae akawa hayupo tayari ivyo akaanza kuleta vurugu.
“Niachie Rolland! Niachie mkono wangu” 😭
Aliomba lakini hata hakusikiwa. Rolland alipoona anamsumbua zaidi alimpiga taksi bega na kuondoka nae juu juu kama mwenge 🤣.
Safari yao iliishia nyumbani kwa akina Rolland. Apo Nirvana alikua ameshalia mno mpaka amechoka. Machozi yake mda huo Rolland hakuyathamini sababu na yeye pia aliumizwa.
“Shukaa”
Kwa huzuni Nirvana alishuka toka kwenye gari, Rolland akamkamata na kuanza kumvuta kuelekea ndani. Aligeuka mnyama kabisa na kuvaa roho ambayo hakua nayo.
Nakuja…….
SEHEMU YA : 2
Wakili Dickson na familia yake walikua wameshamaliza kula chakula, wakawa wamekaa sebeleni wakitazama Tv, mara ghafla mlango ukafunguliwa akaingia Rolland akiwa anamkokota Nirvana.
Wakashtuka na kusimama kwa mshangao
“Kuna nini kinaendelea” aliuliza Mama Rolland
Rolland hakujibu badala yake alimsukuma Nirvana alie enda kudondokea kwenye miguu ya Mama yake.
“Nirvana mwanangu kuna nini” Mama Rolland alimuonea huruma, aliinama na kumuokota pale chini.
“Rolland ni adabu gani hiii?? Kwanini unamtesa binti wa watu??” Wakili Dickson alikua mkali
“Ana stahili! Baba unajua ni kitu gani dada yake alicho nifanya??? Amevunja ndoa yetu siku mbili kabla ya harusi! Je ni haki iyo??” Rolland aliongea kwa jazba mpaka mishipa ikawa inajichora kichwani mwake
“Nini?? Unasemaje??” Wote wakashangaa
“Mnashangaa sio?? Eti kisa anampenda mtu mwingine! Akasahau yote yale niliyowai mfanyia!”
“Mungu wangu weee! Tutaweka wapi sura zetu! Binti ana roho mbaya huyoo” Mama Rolland akamuachilia Nirvana na kumsukuma pembeni. Ile huruma aliyokua nayo moyoni mwake ikayeyuka kabisa.
“Aibu gani hizi!” Wakili Dickson aliishiwa nguvu na kurudi kukaa kwenye kochi lake.
“Bro, umempigia simu?? Labda amekurupuka tu hajafanya maamuzi sahihi” Robson alijaribu kutetea
“Amekurupuka??? No! Amejifikiria akaona mimi sifai akamchagua mwanaume mwingine, tena kamfata huko huko Zanzibar! Na pete ya uchumba kaniachia”
“Daaah! Usipaniki ngoja nimpigie” Robson alitoa simu yake mfukoni akitaka kumpigia Nayce lakini Rolland akamzuia
“Hata usijisumbue! Hapatikani”
Mpaka pale Robson hakujua afanye nini tena.
“Sasa itakuaje? Tutaambia nini watu? Eeeh? Si aibu hii?? Habari zote zitasambaa kesho kwenye magazeti! Shoga zangu watanicheka maana niliwatambia sana kuwa nina mwali msomi” Mama Rolland alilalamika mno
“Usijali mamaa! Ndoa ipo pale pale! Kama dada mtu ameshindwa kutekeleza majukumu yake basi mdogo mtu atamsaidia”
“Unasema nini mwanangu”
“Ikiwa mpaka kesho kutwa Nayce hatorejea basi nitamuoa Nirvana badala yake”
“Unaongea nini wewe??? Dickson unamsikia mwanao??” Mama Rolland alimgeukia mumewe
“Nimemsikia vizuri! Na mimi nayakubali maamuzi yake! Hapa hakuna namna zaidi ya yeye kumuona huyu binti! Sipo tayari kuona jina langu linaharibika, iwapo skendo mbaya kama hii ikitokea basi sitapata nafasi kwenye siasa” Wakili Dickson alikubaliana na mwanae
Basi ikabidi familia nzima ikubaliane kuwa kama Nayce hatarejea, Rolland atamuoa Nirvana.
“Mimi sikubali, tafadhali msinifanyie ivii” Nirvana aliongea kwa uchungu
“Hizi ni dhambi za dada yako unapaswa kulipia” Mama Rolland alizungumza kwa dharau.
Maskini Nirvana hakuchoka kuomba, alienda kwa Rolland, akapiga magoti na kuishika miguu yake.
“Wewe ni shemeji yangu! Ni kama kaka yangu! Sijawai kukufanyia baya lolote lile sasa kwanini unitese namna hii! Nina maisha yangu nayopaswa kuishi, please nihurumie… sipo tayari kuolewa na wewe! Tutafute njia nyingine lakini tafadhalii sitaki kuolewa”
Nirvana aliomba kwa uchungu lakini hakuna alie msikiliza. Watu wote walikua na hasira juu yake na dada yake kasoro Robson pekee aliekua ana mhurumia.
Rolland alipoona Nirvana analia lia sana akamburuza na kwenda kumfungia chumba cha wageni. Akatoa onyo kuwa hakuna atakae ingia kule mpaka yeye ama wazazi wake waseme.
Baada ya pale alitoka kwaajili ya kwenda kulewa. Kichwa chake hakikua vizuri na alihisi pombe ingeweza kumtuliza.
Robson alipoona rafiki yake hayupo sawa aliamua kumfuata ili akazungumze nae. Walienda kwenye bar moja ya pombe ambayo ilikua karibu na nyumbani kwao.
“Bro!”
“Robson niache sipo vizuri”
“Najua ndo maana nahitaji tuongee kiume”
“Nakusikiliza” Rolland alimimina whisky kidogo kwenye glass na kuipeleka kinywani
“Hujafanya fair kabisa! Unamuonea Nirvana! Kosa lake ni lipi hapa”
“Mbona kama una mtetea sana?”
“Simtetei, naongea ukweli ambao nyie hamtaki kuuona”
“Sasa vipi kuhusu mimi nilie achwa siku mbili kabla ya harusi?? Niko kwenye maumivu sababu mwanamke nilie kua nampenda kwa dhati ana mpenda mwanaume mwingine”
“Inauma naelewa ilo”
“Unajua kabisa mimi na Nayce ni wapi tulipotoka! Nilikua nampenda toka tupo watoto, tumesoma wote mpaka sekondari! Unadhani nilipokua Canada nilikosa wanawake??? Kule kuna pisi kali za kizungu but no nilijichunga sababu yake! Niliporudi Tanzania kitu cha kwanza nilimueleza jinsi ninavyo jihisi juu yake, sasa kwanini asinge nikatalia?? Angenambia ana mpenzi wake huko nchi za nje anae msubiri mimi nisinge msumbua” Rolland alilalamika sana sababu pombe zilianza kumpanda kichwani
“Hayo yote najua hakuna haja ya kunieleza tena! Lakini please…”
“Stop bhana Robson acha kuniharibia mood! Maaumuzi niliyofanya na familia yangu yapo pale pale hakuna kitakacho haribika”
“Okay”
Robson alinyamaza kimya sababu hakuna chochote ambacho angeweza kuongea kingesaidia kubadili mawazo ya Rolland hata kidogo.
Basi alfajiri na mapema wakati Nirvana akikesha kulia huku upande wa pili Nayce ali wasili Zanzibar, uso wake haukujawa huzuni hata kidogo, muda wote alitabasamu sababu alikwenda kuungana na mwanaume wa maisha yake.
Alichomfanyia Rolland hakikumuuma wala hakikumfanya ajihisi vibaya. Alipofika Zanzibar cha kwanza alisajili laini mpyaa! hakutaka kabisa usumbufu toka Rolland wala mdogo wake.
Baada ya pale alimpigia Johnson simu
“Hey ndo nimefika” alizidisha tabasamu
“Ooh sorry Nayce sitafika kukupokea but nime mtuma dereva atakupeleka kwenye hoteli ambayo nimefikia! Tutaonana jioni, so ukifika hotelini pumzika na u relax”
“Hakuna shida Johnson”
Nayce aliendelea kusubiri na mwishoni dereva alifika. Alimpeleka hadi kwenye hoteli kubwa ya kifahari.
Huko chumba chake kilikua kimeshaandaliwa. Alipewa funguo kisha akaenda kwanza kumpuzika sababu usiku mzima hakua amelala kwenye meli.
Alipo amka tayari jua lilikua limeshachanganya! Alipiga simu kwa wahudumu, akaletewa supu nzito ya kuchangamsha tumbo.
Alipomaliza kula alienda akaoga, akabadili mavazi na kwenda kutembea tembea ufukweni. Alishinda huko mpaka pale giza lilipo ingia ndipo alirudi chumbani kwake.
Akiwa anakaribia kuufikia mlango wa chumba alichokua anakaa alifanikiwa kumuona Johnson wake akiwa anamsubiria.
Nayce alifurai mno, ni kama miaka mitano ilipita toka alipomuona mara ya mwisho. Haraka alimkimbilia na kwenda kumkumbatia.
“Johnson! Nimeku miss sana”
“Oooh mimi pia”
“Daaah! Sijui hata niseme nini!” Machozi yalimlenga lenga Nayce.
“Najua unavyo jiskia, mimi pia nilikukumbuka sana” Johnson alimtoa Nayce kifuani mwake asijue mwenzake hakua ametosheka na kumbato.
“Nina mengi sana ya kuongea na wewe! Sijui nianzie wapi”
“Mimi pia ila kwanza naomba nikapumzike! Leo nimekua na siku ndefu na bado kuna mambo sijayaweka sawa”
“Kwaiyo hatuta spend usiku pamoja??”
“No! Ila kesho tutaongea mengi sana! Ikifika saa na nusu please nitapenda uje kule ufukweni! And please naomba uvae upendeze”
“Kuna nini?”
“Ni suprise na nina imani utafurai”
Nayce aliposikia vile akatabasamu akajua kwa namna moja ama nyingine ile suprise ilikua ikimuhusu yeye.
“Sawa nitakuja”
“Ok! Ngoja niende! Uwe na usiku mwema”
“Kwako pia”
Waliagana kisha Nayce akaingia chumbani kwake. Alipoingia tu akaenda kufungua sanduku lake la nguo.
Akachagua gauni moja zuri sana lenye mpasuo pajani. Akaona lingefaa sana sababu lilikua linampendeza mno pindi anapo livaa.
Akaandaa na viatu vizuri na kuviweka pembeni. Kila kitu kilipokamilika akalala kwaajili ya mtoko wake na Johnson siku iliyo fuata.
Nakuja………..
SEHEMU YA : 3
Kweli Mungu akajalia pakakucha salama, Nayce akamka mapema na kuanza maandalizi ikiwemo kujipodoa na kuvaa.
Ilipotimu saa nne na nusu juu ya alama akawa tayari. Akasimama mbele ya kioo na kuona namna ambavyo aliumbwa akaumbika.
Aliporidhika na maandalizi yake akatoka nje ya chumba chake na kuelekea ufukweni alipo hitajika kufika.
Akiwa ana karibia aliona pakiwa pamepambwa mnoo na palivutia sana. Na kila alipozidi kusogea ndivyo aliona pia kuna kundi la watu mbali mbali.
Alipokaribia zaidi akakutana na bango kubwa lililokua na picha ya Johnson akiwa na mwanamke wa kizungu! Tena wameshikana kimahaba sana.
Akashindwa kujua ni kipi kilicho kuwa kinaendelea. Sio kwamba hakuelewa?? Hapana, alielewa vizuri tu kuwa Johson alikwenda kuoa mwanamke wa kizungu pale ufukweni ndo maana palipambwa vile, tena lile bango lilijitosheleza kwa kutoa ujumbe wa harusi.
Hakutaka kuamini, miguu ilikua mizito kiasi kwamba alibaki akiwa amesimama pale pale kwa mda mrefu mno.
Mawazo yalimjaa kichwani, alikuja kushtuka aliposikia vigele gele toka kwa watu waliokua pale. Alipo geuka alimuona Johnson ndani ya suti akiongozana na mke wake mtarajiwa ambae ndo yule ambae picha yake ilikua kwenye bango.
Machozi yakaanza kumtoka Nayce! Johnson alijua kumuumiza mno tena ukizingatia hadi aliacha harusi yake iliyokua inafungwa siku hiyo hiyo kwaajili yake.
Taratibu aligeuka nyuma na kurudi chumbani kwake. Hata ile nguvu ya kuendelea kubaki pale hakua nayo.
Tukirudi nyumbani kwa akina Rolland palikua pamefana sana utadhani bibi harusi hakua amekimbia.
Wakati hayo yote yakiwa yanaendelea upande wa ndani Nirvana alikua akivalishwa nguo na kupodelewa. Kila wakati alikua akilia na kumfanya mpaka make-up apate wakati mgumu zaidi.
“Utalia mpaka saa ngapi?? Tafadhali acha kulia”
Woiii kwani Nirvana alikua anaelewa sasa? Ndo kwanza alizidisha mvua ya kilio. Aliumia mno sababu hakua tayari kuolewa na Rolland.
Moyoni alimlaumu sana dada yake maana pasipo yeye hayo yote yasinge mkuta. Aliendelea kulia, alipochoka machozi yakawa hayatoki tena.
Nao walio kua wanamuandaa wakawa wameshamaliza. Walimsifia sababu Nirvana ni mrembo mnoo kushinda hata Nayce. Na hivi anaka mwili kadogo dogo ndo akazidi kupendeza akawa kama mdoli.
Baada ya pale walitoka nje na kumuacha kule chumbani peke yake. Alikaa kwa dakika 20 tu na ndipo alifuatwa na wafanyakazi kwaajili ya kutolewa nje.
Kwakua Bibi harusi alietegemewa kuolewa na Rolland alikimbia, basi Wakili Dickson aliona hakuna haja ya kwenda tena kufunga ndoa kanisani ikiwa ile ndoa haikua takatatifu.
Badala yake alitaka ifungwe kimahakama tena pale pale nyumbani. Na pindi itakapo malizika kufungwa watu wale chakula na kwenda majumbani kwao! Hapakua na haja ya kwenda ukumbini sababu hapakua na umuhimu wa kusheherekea.
Basi Nirvana akatolewa nje na wageni waalikwa wakampokea kwa makofi. Rolland hakutaka kumtazama hata kidogo! Kwa alicho fanyiwa na Nayce alijikuta hadi anamchukia mdogo wake.
Nirvana alipomfikia Rolland alisimama pembeni yake na ndoa ikaanza kufungwa. Walianza kwa kiapo, ndipo zoezi la kubadilisha pete likafuatia. Kisha wakamalizia kwa kusaini cheti cha ndoa na mpaka hapo Nirvana akawa mke halali wa Rolland.
Baada ya ndoa kufungwa tu wageni wakaanza kuseviwa chakula. Mpaka wageni waalikwa wakashangaa na kujiuliza kwanini mambo yalikua yakipelekwa haraka namna ile.
Hamuwezi amini hata mziki haukupigwa! Mambo yalikua kimya kimya na ilipofika saa kumi na mbili jioni kila kitu kilimalizika na watu wakaondoka kwenda makwao😔.
Upande wa Nayce sasa majuto yakamuanza. Akajutia mno uamuzi wake wa kuvunja uchumba na kukimbia ndoa yake.
“Johnson umeniponza mimi! Ona sasa umeharibu maisha yangu” alilia sana lakini haikusaidia chochote kwani kama kuharibu tayari alikwisha haribu.
Akiwa kule chumbani alisikia mlango ukigongwa. Alipokwenda kufungua alikutana uso kwa uso na Johnson akiwa na furaha
“Vipi mbona umevimba ivo!! Unalia nini?”
Nayce alikasirishwa na swali la Johnson
“Nalia nini??? Wewe hujui kinacho niliza?”
“Ningejua Nayce nisinge kuuliza! Mimi sijakuona kule ufukweni nikaona nije kukuangalia”
“Wewe ni mtu mbaya sana Johnson! Umeniita huku ili unionyeshe kua umepata mwanamke mwingine, vipi kuhusu mimi?? Eeeh?”
“What?” Johnson mwenyewe alishangaa
“Unacho kishangaa ni nini??”
“Mimi nimekuita huku kwaajili ya harusi yangu! Na nimekufanyia suprise nikiamini utafurai”
“Sijaja huku kwaajili ya harusi! Bado nakupenda Johnson na hio ndo sababu yangu ya kuja huku, ama umesahau ahadi yetu!”
“Oooh Nayce! Iyo ilikua zamani, alafu pia niliona picha zako mtandaoni ukivalishwa pete na mwanaume mwingine! Nikajua tayari umeendelea na maisha yako nami nikaendelea na maisha yangu”
“Una tegemea mimi ningefanya nini kama tangu ulipoenda kusoma hukunitafuta? nilikubali kuwa nae yule ila sikua na namna, mimi moyo wangu upo kwako! Nakupenda Johnson” Nayce alimsogelea akitaka kumshika ila Johnson hakutaka ilo
“Am sorry Nayce mimi siwezi kuwa na wewe! Nampenda mwanamke mwingine na ndio huyo nilie muoa! Rudi kwa mchumba wako”
“Siwezi kurudi! Nimesha vunja uhusiano wetu nikidhani nikija huku tutaendelea na penzi letu”
“Mpaka hapo sina cha kukusaidia! Ila tu nisamee kwakua hatukuelewana”
“Unadhani huo msamaha wako utanisaidia kitu gani?? Nimesha chelewa sasa unataka nifanye nini?”
Johnson hakutaka kuendelea kubishana na Nayce. Aliondoka zake na kumuacha peke yake.
Basi Nayce alitoa kilio kikali mno. Akamkumbuka Rolland mara mia!
“Nimefanya nini mimi!! Tamaa zangu zimeniponza! Sijui Rolland atanisamee??? Eeeh Mungu wangu”
Nayce akachukua simu yake na kuirudishia ile laini aliyoitoa mwanzo. Alipowasha tu simu, meseji zikaanza kumiminika kama mvua.
Nyingi zilitoka kwa Rolland, Nirvana pamoja na rafiki zake wengine. Alitaka kumpigia Rolland moyo wake ukasita. Akaona apige namba za Nirvana nae hakua akipatikana.
“Ngoja nimpigie Robson” alitafuta namba za Robson na kuzipiga. Dakika zile zile simu ikapokelewa.
“Robson!”
“Nayce! Upo wapi??”
“Nipo Zanzibar”
“Oooh kumbe ulienda Zanzibar kwa mwanaume wako!” Robson alimpa maneno makali
“Usiseme ivo! Najua nimekosea ila please nahitaji msaada wako”
“Upi? Mimi sina cha kukushauri after vyote ulivyo mfanyia Rolland”
“Najua ila please nahitaji kuongea na Rolland, naomba unisaidie ili nipate mda wa kuzungumza nae”
“Hayupo! Kaenda honeymoon”
“Honeymoon??” Akatoa macho kweli kweli.
Nakuja……….
SEHEMU YA : 4
“Ndio honeymoon”
“Honeymoon kivipi?”
“Nayce watu wakifunga harusi si wanaenda honeymoon? Ama hujui?”
“Ina maana Rolland ameoa?”
Moyo ulimchoma sana Nayce, maumivu yakamjaa akahisi hadi kupasuka.
“Ndio”
“Kamuoa nani?? Imekuaje ameoa? Mbona kanifanyia ivoo?? Ni kosa gani kubwa nililo tenda mpaka akanifanyia ivo” Nayce aliongea kana kwamba hakua na kosa lolote lile alilofanya
“Unajua unachekesha sana?? Kwaiyo ulitaka labda Rolland afanye nini?? Aaibike kuwa mke wake mtarajiwa kamkimbia siku mbili kabla ya harusi?? Come on Nayce acha kua mbinafsi kiasi icho”
“Please nisaidie niongee nae Robson please”
“Subiri arudi honeymoon kama vipi mpigie simu”
“Najua hawezi pokea simu zangu, na mimi sitaki kumpigia nataka kuongea nae uso kwa uso! Nisaidie tafadhali”
“Ok! Akirudi honeymoon nitakuambia” Robson hakutaka mambo mengi, alikata simu yake na kuiziima kabisa.
Upande wa Nirvana alikua huko South Africa kwenye honeymoon yake na Rolland. Hakua na furaha hata kidogo maana yeye na Rolland walikua kama maadui.
Walikaa chumba kimoja ila kila mtu alilala upande wake. Nirvana alilala kitandani na Rolland alilala kwenye kochi.
Palipokucha Rolland alitoka mapema kwenda kulewa kisha alirudi zake jioni na kwenda kulala moja kwa moja. Hakua na mda kabisa na Nirvana. Hakujali kama alikula ama alishinda njaa.
Sio icho tu, hawakusemeshana kabisa! Walikua kama mabubu na mbaya zaidi walipishana bila hata ya salamu.
Hali ilikua vile kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya sita! Ilipofika siku ya saba ambayo ilikua ni siku ya mwisho ya honeymoon yao, Rolland aliamua kumsemesha Nirvana.
“Sioni kama kuna haja ya kuendelea kunyamaziana!” Aliongea vile akitegemea Nirvana angemjibu ila hakumjibu.
“Kama hakuna ulazima wa kuongea sioni kama kuna haja ya kuongeleshana lakini kama kuna ulazima tutaongeleshana”
Bado Nirvana hakufungua mdomo wake! Rolland akachukia, akatoka na kwenda alipokua anaendaga kunywa pombe. Aliporudi usiku alikuta tayari Nirvana alisha paki nguo zao zote kwenye sanduku.
“Asante!” Alishukuru na wala hata Nirvana hakuitikia asante yake.
Basi siku iliyofuata walianza safari ya kurudi Tanzania. Kwenye ndege walikaa siti tofauti na hii nikwa sababu Rolland hakuona kama kuna ulazima wa kukaa na Nirvana ikiwa hataki kuongea nae.
Kweli Nirvana alipanga kuweka mgomo wa kutoongea nae hadi pale Rolland atakapo muomba msamaha kwa kosa la kumlazimisha kuolewa nae na kumfungia chumbani bila chakula.
Wakiwa ndani ya ndege Rolland alikua akigeuka nyuma kila baada ya dakika 10 ili kuhakikisha kama Nirvana alikua sawa. Alipochoka alijilaza kwenye siti na kupitiwa na usingizi.
Alipokuja kushtuka nayo ndege ilikua ikitua kwenye ardhi ya Tanzania. Baada ya pale walishuka toka kwenye ndege, wakakaguliwa mabegi yao na kuruhusiwa kuondoka.
Upande wa Nje dereva aliwasubiri kwaajili ya kuwapeleka nyumbani.
“Pole kwa safari Mr Rolland!” Alisema Dereva huku akipokea mizigo yao
“Asante!”
“Vipi tunaelekea wapi!”
“Twende nyumbani kwangu”
“Hakuna shida”
Dereva aliwapeleka hadi alipokua akiishi Rolland. Walipofika getini wakashangaa kumkuta Nayce pale.
Nirvana kumuona dada yake alifurai mno, alifungua mlango wa gari haraka na kwenda kumkumbatia lakini ajabu ni kwamba dada yake alimpokea na kofi zito
“Huna haya wewe! Kuondoka kidogo tu tayari ulishakimbilia kwa shemeji yako! Umeona nikiolewa mimi nitafaidi sana!” Nayce alikua na hasira vibaya mno, taarifa za Nirvana kuolewa na Rolland alizipata baada ya kurudi toka Zanzibar
“Dada mimi sikupanga iwe ivi” machozi yakaanza kumshuka Nirvana! Laiti angejua masimango na mateso aliyo yapitia asinge mpiga kibao namna ile
“Eti hukupanga iwe ivii??? Nyooo! Kumbe nilivyokua nae ulikua una mtamani sio?? Mtoto mdogo una roho nyeusi sana wewe”
“Dada jamani usiseme ivo! Please sijafanya kwa kupenda” Nirvana alijaribu kujitetea ila Nayce hakutaka kumsikiliza kabisa! Wakawa wanaendelea kulumbana pale getini huku Rolland akiwatazama.
Alipoona Nayce anazidi kumtolea maneno machafu Nirvana ndipo akashuka toka kwenye gari.
“Baby…! Babyyy” Nayce akaanza kutoa machozi pale pale alipomuona Rolland.
“Nirvana nenda ndani!”
Nirvana akakubali, akafungua geti na kuingia ndani! Akawapisha waweze kuzungumza.
“Umekuja kufanya nini hapa Nayce???”
“nimekuja kukuona! Nahitaji kuongea na wewe! Please nisamehe! Nisamehe sanaaaa”
“Hahhah! Unajua ni kiasi gani umeniumiza??? Unajua ni namna gani umenitia kwenye matatizo?? Mambo yangu yamevurugika kwaajili yako!”
“Najua! Ila nakupenda Rolland! Ni tamaa tu! Ni tamaa” Nayce akapiga hadi magoti
“Toka nyumbani kwangu”
“No! Siondoki”
“Tokaaa” Rolland alimsukuma Nayce pembeni kisha akaingia ndani na kufunga geti kwa ndani.
Moyo wake uliuma kwa kumfanyia Nayce kile kitendo. Bado alikua ana mpenda mno na hakua na mpango wa kumsahau leo wala kesho.
Aliendelea kusimama pale nje mpaka pale Nayce alipoondoka ndipo nae akaingia ndani. Alimkuta Nirvana amekaa kwenye kochi akiwa analia.
Kwa namna fulani akajikuta ana mhurumia ila hakutaka kuonyesha kama ana muonea huruma. Mwanzoni alipanga kua mpole kwa Nirvana ila baada ya kumuona Nayce akaamua kuendelea na roho yake ngumu.
“Umeona sasa? Ichi ndo ulichokua unakitaka? Sindo umetaka dada yangu anichukie sio!” Nirvana alipomuona alianza kulalamika
“Sasa ivi ndo umepata nguvu ya kuongea?! Na mimi nikiamua sitakujibu vile vile” Rolland ali ikunja sura yake
“Sitakusamehe kwa hili Rolland! Nakuchukia sana”
Rolland akamsogelea Nirvana karibu zaidi na kumuangalia machoni
“Sijali kama unanichukia sababu mimi sikupendi vilevile! Piganeni, uaneni hilo ni juu yenu! Na kama umemaliza kulia lia nenda chumbani kalale! Sitaki kelele” Rolland alifoka na kumfanya Nirvana aogope, akazidi kumchukia Rolland zaidi!
“Utalala chumba cha pili! Ondoka mbele yangu”
Basi Nirvana akatoka mbio mbio na kwenda kujifungia kwenye chumba cha wageni ambako alitakiwa kulala huko!
Nakuja………
SEHEMU YA : 5
“Eeeh Mungu nisaidie! Ona Dada yangu anani chukia wakati sio makosa yangu! Unajua kabisa ni namna gani sikua tayari kwa hii ndoa! Sikuwai kumtamani kabisa Rolland hapo kabla! Naomba dada angu apunguze hasira”
Aliomba Nirvana huku akisogelea kitanda taratibu. Kile chumba kilikua kimeshapangiliwa mda mrefu kweli, na kabatini kulikua na nguo zake zote.
Wakati walipokua honeymoon Rolland alituma watu nyumbani kwa Nayce, wakachukua kila kitu cha Nirvana na kuhamishia nyumbani kwake.
“Kila kitu changu kipo huku! Nitaweza kweli kuchomoka katika hii ndoa?? Eeeh Mungu” akaanza kulia tena, alilia hadi usingizi ulipo mpitia.
Aliposhtuka ilikua ni saa moja asubui, aliamka akaoga na kujiandaa ili awahi chuoni. Ile anafungua mlango wa kutoka nje akakutana uso kwa uso na Rolland aliekua anarejea toka gym.
“Unaenda wapi?”
“Chuo”
“Kwa ruhusa ya nani? Ama ukijisikia tu unatoka”
“Nina kama wiki mbili sijafika chuo, vipindi vinanipita na mitihani inakaribia! Please naomba niende chuo”
“Ningeruhusu uende iwapo ungeomba ruhusa alafu kingine huoni kama nyumba yangu ni chafu?? Au unadhani unakaa bure tu huku ndani??”
“Lakini…”
“Nyumba yangu isafishwee! Nitaongea na Robson aombe ruhusa yako chuoni”
“Nitasafisha nyumba nikirudi ila please niruhusu niende”
“Sogea”
“Rolland” Nirvana aliweka macho ya huruma ila Rolland hakumuelewa! Ndo kwanza alimsukuma pembeni na kuingia ndani.
Ikabidi Nirvana aanze kufanya usafi kwenye ule mjumba. Alifuta vioo, alideki, alifuta kila mahali na mwishoni alimalizia kwa kufagia nje.
Alipomaliza nae Rolland alikua ameshajindaa kwaajili ya kwenda kazini.
“Nimesha maliza usafi naweza kwenda chuo sasa”
“kuna nguo kwenye washing machine hazijafuliwa bado! Nyingine za kupiga pasi”
“Rolland unanikomoa ama vipi?? Kumbuka kusoma ni haki yangu! Nitese vyovyote vile lakini usini nyime mimi kwenda chuo” Nirvana aliongea kwa hisia sana ila haikufanya Rolland abadili mawazo yake.
Alishuhudia Rolland akiwasha gari lake na kuondoka. Maskini akaanza kulia tena! Huku dada anamchukia huku chuo kakatazwa kwenda unadhani angefanya nini kama sio kulia???
Basi majira ya jioni wakati Rolland akimalizia malizia kazi zake alipata ugeni wa Nayce ofisini kwake.
“Unaingia tu kwenye ofisi za watu unavyo jisikia??” Rolland alichukia
“Mbona mwanzo nilikua naingia bila shida”
“Huo ulikua ni mwanzo! Enzi za uchumba wetu! Sahivi huna cheo chochote na kama utahitaji kuniona utaomba appointment kama wengine”
“Rolland acha utani bhana ivi hujani miss??? Mbona mimi nimekumiss sana?? Nashindwa mpaka kulala”
“Stop!”
Nayce hakuacha, anajua namna ya kumlegeza Rolland ndo akawa anatumia njia iyo. Akazidi kumsogelea hadi alipo mfikia. Akakaa juu ya mapaja yake huku mikono yake akiizungusha shingoni mwa Rolland
“Nakupenda baby! Nisamee tafadhali! Ni tamaa tu na nimejifunza kutokana na makosa yangu! Kweli utafanya hasira ziharibu penzi letu?? Eeeh???”
“Nimeoa sasa! Mimi ni mume wa mtu”
“Come on Rolland unadhani sijui kua ulimuoa Nirvana kwa hasira? Huna mapenzi nae hata kidogo!, wewe unanipenda mimi tena mimi pekee, macho yako yanathibitisha kila kitu! Bado unanipenda tena kama kichaa, please turudishe penzi letu, nakuahidi nitakua muaminifu na hata ukitaka ndoa sasa ivi nipo tayari”
Yale maneno yalimuingia Rolland kwa kiasi chake lakini bado hakutaka kukubali kirahisi. Alitabasamu kidogo kisha akamtoa Nayce mapajani mwake.
“Next time ukiingia ofisini kwangu kama chooni nitakuita walinzi! Na sidhani kama utapata hata iyo nafasi ya kuingia tena humu ndani”
“Hakuna shida, ila naomba ufikirie kwa makini ombi langu, unanipenda Rolland je upo tayari kunipoteza kwaajili ya ndoa ambayo haina maana?”
“Nayce toka nje”
“Natoka! Pia nataka ujue simu yangu ipo hewani, nasubiri sana kwa hamu unipigie”
Nayce alichukua pochi yake akatoka nje. Alijiamini vya kutosha kuwa alikua na uwezo wa kumrudisha Rolland kwenye mikono yake tena kwa sababu anapendwa.
Huku nyuma Rolland alifungua droo ya chini akatoa chupa ya pombe iliyo bakia nusu. Hakuona haja ya kutumia glass, yeye ali ipeleka mdomoni vile vile akainywa kama maji.
Mawazo yalimjaa mno kichwani, alijiuliza je ampe Nayce nafasi nyingine?? Vipi akimuumiza tena?? Na itakuaje kuhusu mkewe??
Aliendelea kugigida ile pombe hadi ikaisha yote. Akatazama saa yake ya mkononi ilisoma saa kumi na mbili na nusu.
Muda ulienda na alipaswa kufunga kazi. Alifunika laptop yake, akachukua koti lake na kuondoka kurudi nyumbani.
Alipofika tu nyumbani akakimbilia kwenye kabati lake la pombe. Bado alitaka kuendelea kujidunga pombe ili kupunguza stress.
Alichukua glass na chupa ya whisky, akajimiminia na kuendelea kunywa taratibu akiwa amekaa kwenye kochi.
Nirvana alikua kasimama pembeni akimtazama. Hakujali sana kuhusu unywaji wake wa pombe, yeye alicho jali ni kwenda chuo tu.
Taratibu alimsogelea na kusimama kando yake kwa uoga
“Kama usafi leo nimefanya wa kutosha! Nimeshafua na kupasi nguo zako, naomba kesho niende chuo”
“Siko vizuri Nirvana toka mbele yangu”
“Kwaiyo nisubiri mpaka uwe vizuri ndo unipe ruhusa! Mbona unani tesa namna iyo kwa kosa ambalo si langu”
“Toka Nirvana” Rolland hakutaka kelele za Nirvana ila Nirvana hakuelewa
“Naomba niende chuo kesho! No! Sio naomba, ni nataka kwenda chuo kesho”
Rolland akazidi kupandisha hasira sababu sauti ya Nirvana akiwa analalamika ni sawa na sauti ya mbu masikioni mwake.
Alitaka utulivu na Nirvana hakumpa nafasi ya kutulia. Alizidi kupandwa na hasira hadi akapasua glass yake ya whisky miguuni mwa Nirvana.
Hakufanya vile kwa kutegemea, ila alianza kujutia baada ya kuona damu zikimtoka Nirvana miguuni.
“Umeumia???” Alipanick, akamsogelea na kumtazama miguuni. Hakuishia hapo, alimshika kiuno na kumsogeza pembeni.
Nirvana akawa hoi kwa kushikwa kiuno. Yale mambo yalikua mageni kwake ukizingatia bado alikua msichana. Badala ya kuendelea kulia alibaki akimtazama Rolland.
“Unaumia sana?”
“Hapana!”
“Subiri”
Rolland alienda kuchukua kiboksi cha huduma ya kwanza na kuanza kufuta jeraha la Nirvana. Akajikuta ana mjali mno mpaka ile chuki moyoni mwake ikaisha.
“Am sorry! Najua unapitia mengi sababu ya hasira zangu” aliacha kufuta Jeraha na kumtazama Nirvana
“Mimi sijawai kukukosea kwa namna yoyote ile! Lakini unani adhibu na kunifanyia unyama ambao sipaswi kufanyiwa”
“Haitajirudia tena! Nataka tuishi kwa amani kama tulivyo kua tukiishi mwanzo! Sitakugombeza wala kukukaripia, just peaceful life (Maisha ya amani)”
“Kuishi kwa amani una maanisha utaniruhusu niende chuo?”
“Yeah utaenda chuo”
“Asante sana Shem” Nirvana aliachia tabasamu la furaha mpaka Rolland mwenyewe akadata maana nikazuri kweli kweli.
Nakuja………
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote