MY HALF ❤️
SEHEMU YA 01
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupoahapa.com
Jamani ukisikia watu wanaimba Mungu ndo mtalaamu mtalaamu wa kumetcha ndo maana kanipa wewe wewee ona tunavyo metcha🥰 usifikiri wanatania nikweli Mungu ni fundi bwana tena anajua kufinyanga haswaaa👌🥰🥰
Embu kabla ya yote nitoe salamu kwanza msije kuniona binti nisie na adabu bure wakati mtoto wawatu nimkuzwa haswa😊, haya habari zenu mnaendeleaje na hali? Haya salamu tayari.
Sasa tunaweza kuendelea na story yangu 😊 mimi bwana naitwa Latoya Vicent hili ndo jina langu ni binti wa miaka ishirini na point ,kazi yangu ni muuguzi katika hospital flani hapa jijini, na leo niko hapa kushare story yangu kwanzia mwanzo hadi nilivyo kutana na huyu MY HALF ❤️..
Kijana ambae ananipa jeuri ya kuimba Mungu ndo mtalaamu mtalaamu wa kumetsha 😇😊 aiii jamani mapenzi matamu bwana😋 .
Sasa jamani Ikiwa ni weekend nilikuwa nimekaa zangu nyumbani sina hili wala lile ,mara simu yangu ikaita kuangalia ni Rafiki yake nikapokea chap .
Akanipa habari za mtoko ambao ulikuwa ni wafanyakazi na haikuwa wafanyakazi tu bali ilikuwa ni kila mtu anatoka na mtue ☺️, walai mitoko ya kiofisi ninaipenda sana yaani kuna kuwaga na kavibe flani 😇ee unyama mwingi 😊,so mara zote nilitamani sana mitoko ya aina hii .
Lakini huu wasafari hii naona ukinipita kushushoto😮💨 maana siwezi kwenda nakuonekana yatima wamapenzi😪 au kubaki mpenzi matazamaji kwenye mapenzi ya watu😒.
Na sio kwamba sina mpenzi maana unaweza hisi sina mpenzi ,ndugu yangu mpenzi ninae ila mpenzi wangu anampenzi wake 😮💨na sio mpenzi tu niseme ni mume wa mtu.😪
Na kibaya zaidi ni wote tunafanya nao kazi 🙃,hivi umeelewa ? Nimesema huyo mpenzi wangu na mkewe wote tunafanya kazi pamoja 🥲( msiiniite shetani ni maisha🥲,maana kuna watu wanajua kuaattack ), basi baada ya maongezi mafupi niliagana na rafiki yangu huyo kisha nikajilaza huku nikitafakari maisha yangu.
Unajua bhana sidhani kama kuna mtu anapenda kudate na mume wa mtu ,ila maisha ya mahusiano yanaforce kuingia kwenye hilo janga 😮💨.
Kwa sasa staki kuliongelea sana hili husiano maana nahisi hisira ,penzi gani lisilo na afya yaani lipo lipo tu halina hata muelekeo😏.
Nilitulia na kuendelea kufikilia maisha yangu mara sm ikaita kuangalia mpigaji ni huyu mpenzi mpuuzi mwenye kichwa kama nazi ya lushoto🙄, niliiangalia kwa mda na kupokea .
"Hello "
"Yes Latoya mambo mpenzi"
"Poa nambie "
"Mbona kama hauna furaha kuna tatizo gani my loo"
"No niko sawa mh nambie haraka haraka usije kukutwa na mkeo au leo hayupo"
"Hahahaha kumbe ndio maana umechukia !!, sikia mamy punguza wivu kipenzi mimi niwako na kama kuna lolote ambalo nimefanya hujapenda I'm sorry mamy but please malkia wangu usikae na hasira "
"Umemaliza kuongea au ndo unaanza maana nataka kupumzika "
"Okay naona leo una mood mbaya ,vp kama tikitoka tukaenda mahali walai urefresh mind"
"Na huo mtoko wa wapenda nao utatoka sangap ?"
"Achana nahiyo mitoko imekaa kishamba ,me nitatoka na wewe so jiandae nitakuja kukuchukua sawa sweet "
"Hapana we nenda na mkeo me niko sawa "
"Came on babe mke wangu ni wewe kipenzi changu "
(🙄uongo sasa kaujaza 😏) kweli sikuwa na mood hata ya kuongea nae nikakata sm na kuizima kabisa , nipanda kitandani na kulala tena na kujifunika juu 😮💨.
Yalipita kama masaa mawili nikasikia mlango ukingongwa , nikatulia kwanza ukagongwa tena nikakaa kimya kwa mara ya tatu ukagongwa .
Nilichukia na kuamka kwa hasira nikafungua na kukutana na sura ya mpenzi ,sikuongea nikaachia mlango na kurudi kitandani na kujilaza kuangalia ukutani , taratibu akafunga mlango mwenyewe na kuweka mifuko aliyokuja nayo pembeni.
Kisha akapanda kitandani na kuanza kunibembeleza🙄,nikisema mapenzi ni nyoko nitaonekana nina matusi au mdomo mchafu ,lakini ukweli mapenzi ni nyoko😒.
Yaani pamoja na kujua kuwa maneno aliyokuwa akinambia ni uongo wala hakuna hata moja litakalo simama ila bado moyo ulifurahi na kuona napendwa , nikakunjua moyo na kuruhusu ashinde shenzi mimi😏🙄
Haya bwana baada ya kulainishwa na maneno matamu mjinga mie nikaliwa bila mboga 😪, baada ya zoezi hilo nilitulia juu ya kifua chake huku mwamba akishusha nondo zake za uongo😒.
Sikuwa najibu kitu zaidi ya kutulia , mara mwenye mali akapiga mwanaume kuona ni mke wake aliinuka haraka na kusahau kama nilikuwa nimejilaza kifuani mwake.
Nikarushwa nusu nimwage ubongo kwa kujipigisha kichwa ukutani, ajabu hakujali ndo kwaanza aliniweka kidole mdomoni mwake akiniambia shiiiii🤫.🥺
Nifanye nini mie zaidi ya kufunga domo langu 😐 basi akaongea pale alivyo maliza tu akainuka huku akisema ," sasa mpenzi naondoka nyumbani mama Vee asije kukasirika ikawa msala"
Bila kujali kuwa nimejipigiza kichwa akaingia bafuni na kujimwagia maji chap alivyo maliza akavaa na kuchukua wallet yake akatoa noti kumi za elfu kumi na kuweka kitandani.
Akasema "sasa tutaongea baadae ,na kumbuka usinipigie wala kutuma sms nitakucheki mwenyewe"
Aliongea na kuondoka😔 ,nilibaki nimeganda huku nikiwa bado nasikilizia maumivu ya kichwa, nisiwe muongo niumia sana .
Na nilijiona mbaya nisie na thamani hata kidogo, kweli mimi nimefikia hatu hii nakaa kwenye mahusiano ya aina hii ? Kwani ninekosa nini haswa hadi kujipa maumivu makali hivi?"
Niliwaza na kuinuka nikasimama kwenye kioo na kujiangalia , bila kujipendelea jamani mimi ni mzuri kwanzia sura rangi hadi shep .
Lakini pamoja na.uzuri wangu huu mpenzi yanani kaanga mwisho na nimeenda kujitupa kwenye shimo refu la kufisha eti kisa staki kuwa single 😔,poor me😪.
ITAENDELEA
MY HALF ❤️
SEHEMU YA 02
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupoahapa.com
SONGA NAYO.................
Kichovu nilifuta machozi na kuingua bafuni nikafungulia maji ya juu na kismama chini yakawa yananishukia tu, mawazo yalinipeleka mbali sana 😮💨.
Nikawa nakumbuka kila husiano nililowahi kupitia , moyo ulihisi huzuni isiyo ya kawaida machozi nayo yalinishuka nikachuchumaa huku nikilia kwa kwikwi 😫.
Nilihisi kujichukia na kujiona mwanamke asie na thamani hata kidogo, basi kinyonge niliinuka na kuoga nilivyo maliza nikatoka na kukaa mbele ya kioo 🥺.
Nilikaa kwa mda mrefu bila kufanya kitu chochote zaidi ya kujiangalia tu, mwisho niliinuka na kupanda kitandani kwaajili ya kulala bila hata kupata chakula cha usiku.
Siku iliisha vibaya sana ,kesho yake asubuhi niliamshwa na sm ya mama aliekuwa akinitaka niwahi kwenda kanisani.
Nilimjibu sawa na aamka ila ukweli hata wazo la kwenda kanisani sikuwa nalo na sio leo tu yaani mimi toka nimeanza kudate na huyu mwanaume wa mtu.
Nikama roho yangu imekufa, sina kiu ya kusali au kufanya lolote linalo husiana na Mungu coz mda wote najiona mkosefu nisie faa kusimama mbele za Mungu.
Ni mwaka wa tatu sasa sijui lolote kuhusu kanisani wala mambo ya Mungu , na jambo la kutoshiriki ibada au kujihusisha na Mungu linaweza kuwa kawaida hasa kws kizazi hiki.
Ila kwangu naweza kusema ni maisha magumu na mabaya saana , we imagine huendi kanisani it okay unaweza sema uko bize but hata ile ya kusema leo nisali au ombe kitu flani huna hiyo nguvu.
Coz masaa yote unajiona hufai ,(hii hali inatesa na kunyong'onyesha roho sana 😪) .
Basi bwana niliendelea kulala hadi ilipofika saa tano kasoro nikaamka na kuandaa chai nakunywa, baada ya kunywa chai nikawa nataka kutoa nguo za kufua .
Mara mume wa mtu akapiga sm niliiangalia tu bila hata kupokea akapiga tena na tena bado sikupokea, mwisho akatuma meseji akiuliza shida nini mbona sipokei sm zake.
Sikujibu nikaacha na toa nguo , sasa akili yangu ilivyo vurugwa niliishia kutoa nguo na kujipa kazi nyingine hiyo nayo nikaacha ,ikawa mwendo wa shika hichi acha 😢.
Hadi inafika saa tisa hakuna hata kazi niliomaliza , nikajionea usiku vyote nikaviacha na kupanda kitandani hapo nimefunga mapazia na milango yote.
Kiufupi sikutaka kelele ya mziki wala mwanga wa nje ,zaidi nilijiskia kuka kimyaa 😔😔.
Mda ulisogea ilipofika saa kumi nikasikia geti likifunguliwa ,moja kwa moja nikajua ni huyo kiumbe wa mtu ,maana nyumba ninayokaa tuko wapangaji wawili tu .
Na mwenzangu hayupo so huyo anaefungua geti ni huyo mwanaume , na kweli kwani baada ya kuingia tu nilisikia sauti yake akiongea na watu .
Haraka nikasogea dirishani na kuchungulia nikaona amekuja na vijana watatu huku kukiwa na gari dogo ile pick-up ,niliwaza ameleta nini cha kubebea kwenye gari 🤔.
Niliamua kuacha kujiuliza na kutoka nje ,alivyo niona tu akaja kunihug kwa mapenzi mazito na kunitambulisha kwa wale vijana aliokuja nao huku akinimwagia sifa kede kede 🙄.
Sikuwa na la kuongea zaidi ya kuachia tabasamu fake , akawa anavimba mwenyewe ,ukimuangalia kama mtu mwenye mapenzi kweli wakati ushubwada tu😒.
Basi vitu vialianza kushushwa pale yangu yakawa macho tu😶,wakashusha vyote na kulipwa hela yao kisha wakaondoka ndo bwana yule akaanza .
"Aam mrembo wangu kipenzi nimeona nikuletee vitu kidogo hivi walau vikusaidie kwenye shughuli zako za hapa na pale , siunajua mwanaume wako sitaki kuona ukiteseka☺️"
"Una maanisha hapa nateseka eeh?"
"Yeah coz swala la wewe kuhangaika kufua nguo na mikono ni mateso, mtoto mzuri kama wewe hutakiwi kutesa mikono yako kufikinya minguo .
Unapaswa uweke kwenye mashine ifue wewe kazi yako kukunja tu kwanza hata hiyo kukunja naona bado inakutesa so inabidi nikuletee mdada awe anafanya kila kitu.
Wewe utakuwa ukitoka kazin unapumzika zako na siku nikija kazi yako inakuwa moja tu kunipa raha baasi "
"Oooh"
"Yeah, aaaa! Ukiachana na washing machine, nimeona nikubadilishie tv na muonekano wote wa sebleni, pamoja na chumbani coz najua hizo ndo sehemu unazopenda zaidi.
So furniture zitafika mda si mrefu hivi na yale masifuria uliyosema umeyapenda nitaenda nikuchukulie kesho , sawa mamito "
"Okay asante "
"Ondoa shaka nipo kwaajili yako and nenda kajiandae leo tuaenda kulala hotel ili nyumba ifanyiwe usafi na kupangwa vitu vizuri "
"Hapana siko sawa so siwezi kutoka "
"Naelewa kwamba hauko sawa na ndio maana niko hapa kukufanya uwe sawa , so usihofu wala kuweka kizingiti we niachie mimi nitakwenda kurudisha tabasamu lako kwa sekunde chache."
Sikuwa na neno lingine kupinga ,nikaingia ndani na kujiandaa kisha tukatoka na kwenda hotelin kama alivyo sema ,kufika huko akawa anapambana kuonesha upendo na kunijali ili niweze kufurahi.
Lakini moyo uligoma nikawa naigiza tu😪, basi mda ulienda siku ikaisha kesho yake asubuhi na mapema akaniamsha tukajiandaa kisha akanipatia hela na kuondoka.
Eeh aliondoka bila mimi😌 maana hatuwezi kuongozana hadi kazn akihofia watu wanaweza kuongea yakamfikia mkewe ikaja kuwa shida🥲.
Unajua pamoja na Oscar kunionesha kujali na kusimamia kila kitu kwenye maisha yangu kama mwanaume bado hainipi furaha.
Coz natamani kupendwa kweli ,kuheshimiwa na kipewa kipaumbele bila kuwa na hofu yoyote ,lakini hii anafanya vitu ila bado nawekwa nyuma ya mlango inaniumiza mnoo😪.
Najua naweza kuwa nashangaza coz kama sina furaha why naendelea kuwa nae ,ukweli ni kwamba sina nguvu ya kumuacha coz nampenda kuliko neno lenyewe.
Na kila leo natamani mtu aje anaiambie kwamba hajaoa hayo ni mawazo yako ila bado hajaoa so nijisikie kuwa niko mwenyewe na nitabaki kuwa mimi tu😔😔.
Lakini ni ndoto na haifichiki kwamba mimi ni chaguo la pili aka mchepuko, dah inauma sana kuwa namtu ambae unajua wazi huwezi kuwa nae milele, bali mnasogezana tu ikifika mda kila mtu atapita njia yake😔😞.
Haya mchepuko mie baada ya bwana kuondoka na mimi nikafuata nyuma ,kufika ofisin kila mmoja akaingia kwenye majukumu yake huku tukipishana kama hatujuani 😩.
Jioni nikajikusanya zangu na kutembea mdogo mdogo kwenda kutafuta usafiri, sasa nikiwa natembea mdogo mdogo kuelekea geti la kutokea likaja gari na kusimama pembeni yangu.
Nilishtuka maana nilikuwa natembea huku nikiwa kwenye dimbwi la mawazo , basi yule mwenye gari akashusha kioo nikaona ni mkaka tu ambae kwa haraka haraka hajazidi miaka 30 .
Kaka yule alinisalimia na kunambia niingie kwenye gari,weee akili zangu ni ndogo lakini haziwezi kuniruhusu kuingia kwenye gari la mtu nisie mjua .
Nilimshukuru na kukataa ,akawa ananibembeleza pale lakini nikakata , kelele za magari yaliyokuwa nyuma yake zilimfanya akaondoka .
Mimi nae mdogo mdogo nikagoka na kuchukua bajaji, ajabu nimefika nyumbani hata nusu saa haijapita namuona Oscar huyu hapa .
Jicho lilikuwa limemuiva hatari me nikamuuliza " vip mbona uko hivyo kuna tatizo ?"
"Yeah tatizo lipo ,ulikuwa unaongea nini na Aman?"
"Aman ndo nani tena "
"Unajifanya humjui wakati mlitufanya wote tusimame kwenye folen kusubiri mmlalize kuongea "😠
Alivyo sema hivyo nilikumbuka anaongelea nini ,kumbe yule kaka alietaka kunipa lift ndo anaitwa Aman 😐.
Nilitabasamu na kumwambia "Oh yule kijana me simjui na hakukuwa na kitu cha serious kiasi hicho"
"Hakukuwa na kitu cha serious ndo mkasimama nusu saa nzima , Latoya unaniona me mjinga eeh? "
😅😅akii huu wivu unaenda pabaya sasa, jamani nisangap nimesimama nusu saa hiyo kuniomba nipande kwenye gari lake ndo tutumie nusu saa kweli?.
Nilijikut nacheka na kumwambia "aaaah Oscar umeanza ,nimesimama nusu saa sangap wakati hata dakika 10 hazijafika"
"Na kwanini usimame dakika kumi tena na mwanaume, kwani hujui kama una mwanaume??"
"Okay sorry "
"Alikuwa anakwambia nini?"
"Jamani alikuwa anataka kunipa lift basi"
"Hilo tu ndo limefanya mmesimama mda wote huo,na ni mara ngap nimekwambia uwe unarequest na kupandia ndani au unataka kusema haukuwa na hela ya kutosha ?"
"Oscar! Embu relax basi maana unataka kufanya hii inshu iwe kubwa , me nimekwambia alitaka kunipa lift basi sasa tunaendelea kuongea nini"
"Huwezi kuniambia nitulie wakati sijalizishwa na majibu yako ,eti ametaka kukupa lift ina maana amekuona wewe tu kwanini asinge wapa wengine?"
"Dah haya bwana" niliongea na kutaka kuingia chumbani akanizuia na kunambia .
"Usinambie unataka kunisaliti!!😥, Latoya please usifanye hivyo sitaweza kuvumilia kuona ukiwa na mwanaume mwingine.
So please naomba usinisaliti kama kuna lolote nimeenda kinyume nambie ila usiruhusu hisia zako kwenda kwa mtu mwingine "
Ni ajabu msaliti kuogopa kusalitiwa 😆, yaani yeye anamke wake ila hataki mimi niwe na mume wangu😆 make kwanza ncheke😅.
ITAENDELEA
MY HALF ❤️
SEHEMU YA 03
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupoahapa.com
SONGA NAYO..................
Nilitabasamu na kumwambia " Okay nimekuelewa "
"Kweli babe ?"
"Yeah "
"Asante na nina ahidi kukupenda daima "
"Asante kwa hilo ,nafikili mda umeenda ungeenda nyumbani " nilivyo sema hivyo aliniachia na kuangalia saa huku akisema.
"Yeah uko sahihi acha niondoke "
(Ona ulivyo na haraka ya kuondoka ile hali umetoka kunambia unanipenda ,huo upendo wako ukoje 🤨) niliwaza huku nikimuangalia kwa uso wenye tabasamu.
Bila kupoteza mda aliniaga na kuondoka haraka, mtoto wawatu mie nikakaa chini na kuanza kuwaza mawazo yasio isha 😔.
Mda ulienda ilipofika saa moja nikaingia jikoni na kupika chakula ,nilivyo maliza nikaweka mezani na kula huku nikichezea sm ,mara ujumbe ukaingia .
Kuangalia namba ilikuwa ngeni ,nikafungua na kusoma ujumbe ule ulikuwa unasema " hello, David hapa sorry kuna mtu anataka namba yako maweza kumpatia?"
Niliisoma sms hiyo mara mbili mbili nikaona nimpigie , sm ikaita akapokea " Hello ."
"Yes D mambo "
"Poa Latoya habari ya kushinda"
"Nzuri kuna ujumbe nimaona umenitumia sijauelewa ,nani anataka namba yangu?"
"Aaam Kuna mshijaki nahisi ni mdogo wake boss kama sio mwanae ndo ametaka namba yako"
"Mdogo wake boss au mwanae yupi huyo?"
"Aisee sijui ila me nimetafutwa nikaombwa namba yako nikaona sio poa kutoa bila ruhusa yako"
"Mdogo wake boss , sikia usimpe "
"Okay poa basi usiku mwema " niliitikia sawa na kukata sim huku nikiwa najiulia huyu mdogo wake boss yupi na kwanini atake namba yangu ?.🤔
Au ndo huyo Aman ,lakini hapana hawezi kuwa yeye lakini huyu mtu ni nani na kwanini atafute namba yangu je kuna shida yoyote 🤔.
Ila hapana kungekuwa na shida ningetafutwa na boss mwenyewe, niliwaza sana mwisho niaachana nayo na kula chakula .
Baada ya kula nikaingia zangu kulala ,kesho yake asubuhi na mapema niliamka na kujiandaa tayari kwenda kazin .
Kama kawaida nilifika na kuingia kwenye majukumu yangu ya siku, na ilipofika mda wa kula nikawa nimekaa zangu huku nikiwa bize kula .
Akawa amekuja rafiki yangu Zulfa alivyo fika tu akanambia "mmmh mrembo wetu imekaa kwa kujiachia huna shida mtoto wawatu"
"Wewe tena ,enhe ambie maana umepotea "
"Kupotea wapi yaani siku mbili tu umeona kama mwaka "
"We uhujui kukaa mbali na mtu unaempend siku moja tu ni nyingi kama mwaka "
"Laaaa!! Dada umeanza kuiga maneno ya wanaume 😆, embu tuachane na hili jana boss kanipigia usiku anataka namba yako "
"Boss gani Mr Ranjit au 😳?"
"Huyo huyo kwani tuna boss mwingine zaidi yake "
"Okay alikuwa anataka nini ?"
"Namba yako tu na ilionekana ilikuwa muhimu sana sasa sijui huko nini kiliendelea baada ya wewe kupigiwa "
"Me sijapigiwa sim na mtu yoyote kwanza nashangaa kwanini namba yangu ilikuwa I inatafutwa kama almasi iliyopotea"
"Kuna mwingine kakwambia eeh?"
"Yeah David alinipigia kunambi hivyo hivyo "
"Basi ndo hivyo bwana " nilibaki nawaza kwani kuna nini hadi boss atafute namba yangu kwa haraka hivyo🤔, sikupata jibu nikaamua kula kisha tukarudi kwenye majukumu yetu.
Ila mda mwiingi nilikuwa naangalia sim yangu kama nimetafutwa na namba ngeni lakini hadi inafika jioni sikuona sm wa sms ya mtu, nikaamua kulipotezea ,kama wanashida na mimi watanitafuta kwa mda wao😒.
Basi bwana nilifika nyumbani nikaingia jikoni kuandaa chakula maana Zulfa na Esta walikuwa wanakuja kulala kwangu leo , so lazima niandae msosi wa kutosha .
Haya nikafanya yangu pale hadi saa tatu nikawa nimemaliza kila kitu nikaingia chumbani chap na kuoga baada ya kuoga tu nikasikia geti linagongwa .
Nikachukua kanga na kutoka nje nikafungua walikuwa ni hawa vichaa wangu ,nikawakaribisha pale na kurudi chumbani kuvaa .
Nilivyo maliza nikarudi tukapata chakula kwanza na baada ya chakula Esta akaanzisha maongezi " Latoya hongera naona kila seheku kuna mabadiliko "
Aliongea huku akiangaza macho yake huku na huko ,nilitabasamu na kumjibu " Asante mwenye pesa yake kaamua kubadilisha muonekano"
"Naona ila shoga angu umemkamata huyu baba vibaya sana ,yaani anakuhudumia kama mke halali hadi raha"
"Kweli anajitahidi kufanya majukumu yake vyema,lakini naona nikienda kukatisha hii safari mapema coz siwezi tena "
"Khee tena, kwani amekufanya nini?"
"Hajanifanya kitu lakini nimechoka wala sioni maana ya haya yote "
"Una maanisha nini kusema huoni maana ya haya yote wakati mtu anakujali na kukuhudumia vizuri "
"Esta najua anahudumia lakini me siko nae kwasababu ya huduma zake ninachotaka mimi ni upendo na kupewa thamani kama mwanamke wake lakini yote hayo siyapati"
"We una matatizo unataka thamani gani tofauti na hii , na unafikili anafanya hivi kwasababu gani kama sio kukupenda ?"
"Esta sidhani kama unaelewa ninacho maanisha "
"Nakuelewa vizuri na sijui shida yako nini , dada huku nje watu tunalia kupata hata wa kutupa laki moja tu,wewe uko hapa inalipiwa kodi.
Tena sio ya chumba kimoja nyumba nzima bado bill zote na chakula anatoa yeye kaenda mbali zawadi unapewa kila leo ona saizi kabadilisha karibu kila kitu cha ndani.
Halafu bado unalia lia kwani we unataka hiyo ndoa uipeleke wapi kwa mfano ? Unakosa mjurusi jibu hapana unakosa mahitaji yako ya msingi ?hapana .
Haya ni hiyo heshima maana utasema ndo unaitaka , labda ni kuulize we unataka heshima uipeleke wapi kwani hapa unatembea uchi.
Au wewe na walio olewa mnavuta pumzi tofauti huenda labda yakawako imepunguzwa kidogo .
Wewe umepata mtu mnaeelewana nae tulia hayo mambo ya ndoa achana nayo ,na labda nikwambie tu ndoa si ya kila mtu wengine tumeumbwa tuwege michepuko tu'"
Alivyosema hivyo mimi na Zulfa wote tukajikuta tunamwambia( "Wee ukome umeumbwa kuwa mchepuko mwenyewe")
"Haya kataeni ,ila ndo iko hivyo sio kila mtu aliandikiwa ndoa na nikwambie tu hiyo ndoa unayiitaka unaweza kupewa leo ila ukapondwa mwisho utaona bora haya maisha."
Nilishusha pumzi na kumwambia " Sikia ndugu yangu me siko tayar kuendelea kuwa mchepuko ,nataka mwanaume wangu mwenyewe mume wa maisha yangu "
"Kakojoe ulale dada maana naona una usingizi, eti mwanaume wa peke yako unaongeza kiungo eti wa maisha yako .
Labda umuumbe mwenyewe ila kinyume chake huwezi kumpata miaka buku"
"No sina maana kuwa nitakuwa mimi tu najua ni ngumu mimi ninachotaka awe halali yangu ikitokea katoka nje basi ni yeye ila ni wangu"
"Oooh endelea kuoga iko siku utajibiwa"
Zulfa alikohoa kidogo kuweka koo sawa na kusema " Esta sidhani kama inamuelewa vizuri Latoya ila yuko sahihi ,mume wa mtu hawezi kuwa wako .
Zaidi atakutumiaa wee mwisho atarudi kwa mke wake na kukuacha na majeraha so kama anaona hana amani muache aondoke kwenye hayo mahusiano "
"Anaondokajee bhana, kwamba huyo wake atakuwa mkamilifu ama ?"
"Hatuzungimzii ukamulifu hapa inabidi uelewe "
"Zuu nakuelewa vizuri ila siungi mkono hata moja ,Latoya unajua rafiki yangu dhambi ni kutoka na mume wa mtu asie na hela ,hiyo ndio dhambi kubwa.
Maana unatoka nae ili iweje sasa!, lakini akiwa na hela kama hivi aaah dhambi yake ni ndogo sana tena yenye faida kabisa "
"Wewe usitupotoshe ,hakuna dhambi yenye faida, dhambi ni dhambi tu"
"Eeh haya ,mtu unadhambi nyingi kwanini usiachane na hizo zingine ubaki na hii moja tu ,na Mungu mwenyewe anaona maisha yalivyo "
Niliamua kuwakatisha na kubadilisha mada ,tukawa tunapiga story huku tukiangalia movie na mda wa kulala ulipofika kila mmoja aliinuka nakutafuta kitanda kilipo.
ITAENDELEA
MY HALF ❤️
SEHEMU YA 4& 5
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupoahapa.com
SONGA NAYO..............
Tulilala na asubuhi na mapema wote tuliamka na kujiandaa kwenda kazin, ambapo mimi na Zulfa tunafanya kazi sehemu moja ila Esta yeye alikuwa anafanya kazi sehemu ngingine .
So mimi na Zuu wangu tulifika na kuanza kazi kama kawaida na ilipofika jioni mwenzangu akaondoka nikabaki mimi maana nilikuwa na zamu ya usiku.
Sasa bwana ilifika saa tano kuelekea akawa ameletwa mgonjwa yuko hoi bin taabani, tukampokea haraka na kuanza kumtafuta doctor aliekuwa zamu .
Haikuchukua mda akaja na bila kupoteza mda akamuona mgonjwa , sasa kukawa na shida kwenye masuala ya Bima yake na akawa anahitaji private room.
Jambo ambalo lilikuwa ngumu kwenye kupatiwa huduma kwa wakati, nilimuangalia yule baba (mgonjwa) namna alivyo kuwa na hali mbaya .
Nikaangalia na watu walio mleta walivyo kuwa wakihaha nikaona acha nijitoe, nikamfuata doctor na kuongea nae ili apewe huduma kwanza hayo mengine wataangalia hata hivyo ni usiku.
Niseme tu doctor alikuwepo alikuwa na roho mbaya kiufupi hanaga mda na watu ,so hata ushauri wangu aliukaa kata kata na kutaka kuondoka .
Nikaona huyu analeta masiala na maisha ya watu, kwanza yuko zamu na alikuwa hayupo hapa amekuja kwa kupigiwa sm halafu kafika kisa kuna changamoto kidogo anataka kuondoka tena.
Aisee nilivalia njuga kama aliekuwa anaumwa na baba angu mzazi, tukapandishiana sauti na doctor vya kutosha ila mwisho akafanya kazi yake.
Nikaacha na hilo na kupambania chumba ,na penyewe haikuwa rahisi maana chumba kilicho kuwepo kilikuwa tayari kimesha fanyiwa booking.
Lakini kwa uwezo wa Mungu nikafanikisha vyote ,kichwa kikabaki kuuma nikiwaza itakuwaje iwapo kitu chochote kikienda tofauti coz nimeenda nje ya mipaka ya kazi .
Ila nikajipa moyo kuwa hakuna kitakacho tokea ,basi usiku ulipita kesho yake asubuhi kabla sijaona nikaonana na mgonjwa kisha nikaomba kuongea na ndugu anae muuguza kumwambia kama itatokea tofauti yoyote anipigie.
Aliitikia sawa nikaaga na kuondoka zangu, kwa uchovu wa pilika pilika za usiku nilifika nyumbani na kulala kama pono,nikaja kuamka saa nane mchana.🥱
Kichovu nilijivuta na kushuka kitandani ,kwa hatua za taratibu nikaelekea jikoni ili nikaandae chakula maana sio kwa njaa ile .
Ajabu nilishtuka nakaribia jikon nasikia movement za mtu akiwa jikoni ,mmmmh nikasimama kwanza hapo moyo unakaribia kuuacha mwili kwa hofu🥲.
Taratibu nikarudi chumbani na kufunga mlango vizuri kisha nikachukua sm na kumpigia Oscar, nilishtuka kusikia sim inaitia chumbani kwangu .
Tena kwenye dressing table, aaah kwani huyu mtu kafika hapa sangap🤔ina maana nililala usingizi mzito kiasi cha kuto sikia mtu akiingia ndani🤔🤔.
Niliwaza na mda huo huo Oscar akagonga nimfungulie mlango,nikafungua akaingia bila hata salamu akaenda moja kwa moja ilipo sm na kuichukua .
Nikamuuliza "umefika hapa sangap na kwanini uko hapa mda huu ?"
"Maswali yako yanaashilia hujapenda mimi kuwa hapa"
"Hapana nataka kujua tu coz sikusikia ukiingia "
"Nina nusu saa toka nimefika hapa"
"Oooh sawa ,mh mbona hauko kazn ?"
"Embu acha kuniuliza maswali na unijibu kwanini ulifanya ujinga jana usiku ?"
"Ujinga gani ?"
"Wewe usinifanye mtoto ,kitu gani ulikifanya kazini usiku?"
"Oooh kumbe hilo ,aaam nikama ulivyo sikia "
"Kama nilivyo sikia ,hivi unajua madhara ya ulicho fanya na matokeo yake ?"
"Naelewa Oscar lakin...........!"
"Wait leo umeniita jina langu Latoya leo umeniita kwa jina langu ? Nambie nani ameingia kwenye maisha yako na kukufanya uache majina mazuri yote uliyokiwa ukiniita na kuniita kwa jina langu"
"Jamani kwani kuna ubaya gani mimi kukuita kwa jina lako mbona tukiwa kazin nakuitia hivyo why upanick sasaiv"
"Usema kazini na hiyo ikogo hivyo but mara zote tunapokuwa nyumbani huwa huniiti kwa jina langu why leo "
SEHEMU YA 05
(Aisee🤦♀️)
"Sikia mpenzi wangu nimechoka sana hivyo samahani kama nimekukwaza but inabidi uzoee "
"Nizoee nini na kwanini nizoee? Umepata mtu mwingine ndo maana unajihisi hatia kuniita hivyo?"
"Oscar please bhna mbona unakuwa kama mtoto, jina ni lako sasa nimekosea wapi kukuita hivyo "
"Oooh umerudia tena kuniita " nilitaka kutoka chumbani maana naona kama ananiletea mambo ya kitoto, lakini hakuruhusu nitoke .
Alinizuia na kuniuliza huku akiwa ameweka uso mkavu "nisiku kadhaa zimepita nilikuona umesimama na Aman nikasemehe ,bado juzi nimesikia boss alikuwa akikutafuta bila sababu yoyote ya kikazi.
Leo unaniita kwa jina langu kitu ambacho hujawahi kufanya toka tumeanza mahusiano, unaweza kunambia nini kinaendelea ?"
Nilishusha pumzi ndefu na kumwambia " sioni kama kukuita jina lako ni kosa la kukufanya ureact namna hii ila nikwambie tu sina mwanaume mwingine zaidi yako..
Wala sina mpango wa kuwa nae na hilo unalijua so please naomba haya mambo tuyaache "
"Tuyaache simple like that eeh ,hivi unataka kusahau kama kabla ya kuwa nurse ulipita kwenye mikono yangu, na baada ya kuhitimu ni mimi niliekupa kazi hii kazi .
Na sijui kama umefikilia kuwa ninaweza kukuondoa kazin na hautakuwa na chakufanya sijui kama umewaza "
"Unataka kusema nini ?"
"Unaelewa vizuri sasa endelea kufanya ujinga wako familia yako itasaidiwa na serikali "
Aliongea na kuchukua sm yake na kuondoka , nilibaki nimesimama kama nimepigwa short, unajua nilimuelewa ni nini alikuwa akimaanisha.
Na katika sehemu alizonigusa ni kutaja familia yangu, nilirudi nyuma na kukaa kitandani kama mzigo .
Picha ya maisha ya nyumbani kwetu ilinijia kichwani nikajikuta nikitokwa na machozi 😭, unajua nyumbani kwetu maisha ni magumu sana tena saana .
Na mimi ndio tegemeo pakee katika familia yangu, na ukiachana na kuwa tegemeo baba yangu ni mgonjwa na matibabu yote anaghalamikia Oscar.
Ni ukweli usio pingika kuwa nilishindwa kuendelea na shule kisa Ada Oscar akalibeba na kunilipia Ada na kila kitu kinacho nihusu .
Hakuishia hapo akawajengea wazazi wangu nyumba na kutoa mtaji wa biashara kwaajili ya kuendesha mambo madogo mdogo ya nyumbani.
Niliwaza sana kiasi cha kukosa hamu ya kula nikabaki nimejilaza nisielewe nifanye nini , lakini ukweli sina amani tena na haya mahusiano, yaani nahisi moyo wangu umechoka .
Na sio kwamba si mpendi no napenda sana lakini kinacho niumiza nikwamba sio wangu wala hawezi kuwa wangu zaidi tunavuta mda tu😔.
Mda ulienda jioni ikafika akarudi tena kwa mara nyingine na kufika anaingia chumbani, nilikuwa nimejilaza hivyo alivyo ingia na kukuta nimelala .
Aliweka wallet na simu yake mezani na kukaa pembeni yangu akaniita " Latoya !"
Bila kuitika niliinua uso wangu na kumuangalia , macho yangu yalikuwa yamevimba kwa kulia huku kwi kwi ya kilio ikiwa kali.
Taratibu alinyosha mkono wake na kunifuta machozi huku uso wake ukionesha huzuni sana😥 , akanambia .
"I'm sorry sikuwa nakusudu la kukuumiza ni wivu tu so nisamehe mke wangu "
"Hapana uko sahihi sitakiwi kuongea lolote mbele yako lakini Oscar naumia hivi umeshawahi kufikilia najisikiaje kuona ukiwa na mwanamke mwingine tena ukimpa kipaumbele kuliko mimi"
"Naelewa Latoya lakini unajua ni kiasi gani nakupenda "
"Unaelewa kwamba upendo peke yake hautoshi kusimamisha mahusiano au ndoa ? Na upendo ulio nao kwangu si ule ninaohitaji Oscar.
Wewe upo kwa mda tu na huo mda ukiisha utaniacha na kwenda kwa mkeo ,je mimi nitabaki na nani?"
"No mimi niwako Latoya na nitaendelea kuwa wako "
"Acha kunidanganya basi ninaona na kuelewa pia so kama unaweza please niache "
Nilivyo sema hivyo alitabasamu na kuniachia mkono ,akainuka na kupiga hatua kadhaa Kisha akanigeukia na kuniuliza .
ITAENDELEA
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote