Follow Channel

MY HOUSE GIRL SASHA

book cover og

Utangulizi

MY HOUSE GIRL SASHA
EP01
MTUNZI; BABY SMILE

(Location; South Korea, Seoul)
"Naitwa Sasha ni mfanyakazi wa ndani wa CEO Wang, ameondoka bila kunywa chai sababu ya upuuzi wangu, niko hapa kurekebisha makosa yangu. Naomba usogee pembeni nipite" Sasha aliongea akijitahidi kuweka sura ya tabasamu

"CEO Wang yupo kwenye kikao siwezi kukuruhusu....na hata hivyo nyumba yake haiwezi kuajiri mfanyakazi mwenye muonekano wa kupoa kama wako....sina uhakika kama chakula unachopika huwa kinaiva" Mlinzi aliongea huku akikisukuma kikapu na rungu lake. Hakuwa akimtambua huyu Binti kwa sababu ni Mfanyakazi mpya

Sasha alivunga kama anaondoka hivi, baada ya kuona Mlinzi kazubaa alichoma mbio. Pamoja na kuitwa arudi lakini hakusikia.
Alihitaji kuonana na CEO Wang....hakuwa akijua conference room (chumba cha mkutano au kikao) kilipo.
Hivyo alikimbia huku na kule.

Bahati ilikuwa kwake, alifanikiwa kukiona chumba cha kikao. Alisukuma mlango akaingia.....watu wote walimgeukia.

CEO Wang alijikuta akikasirika kupita kiasi, kama angemfukuza Sasha kwa aibu basi angeona kama kubwa la katili kwa Wajumbe wa bodi.

Alimpa ishara Secretary wake amtoe kwa utararibu.

Sasha alikaa ofisini kwa CEO Wang akawa ana msubiria. Muda wote alisali chapati zake pamoja na supu aliyoandaa viweze kukubalika.

Baada ya kama dakika kumi hivi CEO Wang aliingia akiwa kakunja sura yake.

"Kitu gani kimekuleta hapa na huo muonekano wako?... usiniambie siku ya leo umeandaa breakfast nzuri kuliko zote" Wang aliongea huku akitoa hotpot kwenye kikapu

Mapigo ya moyo wa Sasha yalikuwa yanasikika puuh! puuh! puuh!

"Secretary Kimmmmmm!" Wang alipaza sauti

Secretary wake aliingia akiwa na shauku ya kujua nini kaitiwa.

"Vunja hii chapati....endapo utaweza nitakupa pete ya dhahabu!" Wang aliongea

Secretary Kim alichukua chapati aivunje lakini hakuweza

"Kalete nyundo..." CEO Wang alitoa amri

Nyundo ililetwa ndipo chapati iliwezwa kusambaratishwa.

"Huyo ndio Mfanyakazi wa ndani aliyeletwa na Bibi yangu....!" CEO Wang aliongea akitaka kuhurumiwa

Secretary Kim hakutaka kuhukumu kwanza alichukua mnofu wa nyama akatia mdomoni.
Aliitema nyama kwenye beba taka akiwa kakunja sura yake.

"Hii ni kokoto na siyo nyama..... CEO Wang nina wasiwasi na afya yako, nina uhakika umepungua kilo kabisa" Aliongea

Sasha kuona kaharibu mambo alipiga magoti chini akaomba kuhurumiwa.

"Nenda nyumbani, kamwe usije kukanyaga hapa ofisini bila ruhusa yangu" CEO Wang aliongea

Sasha alibeba kapu lake akaondoka, alipofika nyumbani alifikiria afanye kitu gani ili kumfurahisha CEO Wang

Alichukua karatasi akaanza kuchora picha ya bata na vifaranga wake.
Alikaa sebuleni akamsubiria lakini hakutokea.
Anaamua kwenda chumbani kwake kulala.

CEO Wang anarejea nyumbani akiwa amelewa kupita kiasi. Chumba cha Sasha hakikuwa kimezimwa taa, aliamini hicho ndicho chumba chake.
Aliingia kisha akajitupa kitandani, wote wawili walikuwa hawajui kulala hivyo walijikuta wakilaliana,

Sasha si mtu wa kuvaa nguo anapokuwa amelala.

CEO Wang anashtuka usingizini, makalio ya Sasha yakiwa karibu kabisa na mdomo wake. Kama atafungua tu mdomo kuongea basi kuna hatari ya kuyagusa

Itaendelea πŸ’₯


MY HOUSE GIRL SASHA
EP02
MTUNZI; BABY SMILE

Sasha naye alishtuka baada ya kusikia jogoo anawika.

"Mamaaaaaaaaa!" Alipiga kelele

Walijikuta wakitazamana, kwa kifupi ilikuwa ni aibu kwa pande zote mbili.
CEO Wang aliondoka kwa kukimbia alijilaani ndani ya moyo wake kwanini siku jana alikunywa pombe kupita kiasi. Kuna namna alihisi heshima yake imeshuka hasa kulala kitanda kimoja na Mfanyakazi wa ndani anayemchukulia poa kupita kiasi.

Akiwa anajiandaa kwenda kazini mlango wake uligongwa

"CEO Wang karibu chai....." Sauti ya Sasha ilisikika

"Ahsante, nakuja.." Alijibu

Sasha aliendelea na majukumu yake baada ya kujibiwa.
Aliukumbuka mchoro wake aliochora, aliufuata chumbani kwake akauweka mezani pia.

Baada ya CEO Wang kufika mezani alikagua vitafunwa pamoja na chai kwa macho.
Kwa mara ya kwanza kabisa alikula....kidogo leo Sasha amejitahidi.

"Nini hiki...." Alijiuliza huku akifunua karatasi iliyokuwa karibu na chupa ya chai

Mchoro wa Bata na vifaranga vyake ulimvutia sana.... alijikuta akiachia tabasamu.

Muda wa kwenda kazini ulifika aliondoka, Sasha alikimbilia mezani aone kama chai yake imeguswa. Aliachia tabasamu pana hasa baada ya kuona Wang amekula.
Alianza kuitafuta karatasi yake ya mchoro pia.
Aliinama huku na kule akihisi pengine imedondoka. Alibinua makochi, akasukuma kabati pamoja na friji....kwa kifupi ilikuwa ni vurugu sebuleni.

Alipiga kelele za furaha baada ya kugundua mchoro wake umechukuliwa na CEO Wang.

Upande mwingine CEO Wang akiwa anakagua bustani kubwa ya matunda ya apple iliyokuwa ndani ya Kampuni lake, alimsimulia Secretary Kim kuhusu kujikuta amelala chumbani kwa Sasha

"Una uhakika huna hisia naye!" Secretary Kim aliuliza

Swali hili lilimtia hasira CEO Wang, hakutaka kufikiria mara mbili.... alimpiga teke akaangukia kwenye bustani.

Secretary Kim alijilaumu kwanini amezungumza upuuzi.

Upande wa Sasha baada ya kumaliza kazi zote aliingia bafuni kuoga.
Baada ya hapo alikaa kwenye TV akawa ana mfuatilia Amber Rose mwanamitindo wa Marekani.
Alijikuta akitamani kujipamba pia.... chumbani kwake kulikuwa na vipodozi hakujua hata ni vya nani, huenda ni vya Mfanyakazi aliyepita.
Alikaa kwenye kioo chake akaanza kujiremba, alipiga kelele kutokana na muonekano wake mpya.

Alinawa uso akarudia tena na tena lakini bado alijiogopa mwenyewe.
Kabla hajafuta mapambo yote simu yake iliita.

"Andaa chakula cha mchana kwa ajili ya mjukuu wangu....kesho nitakuwa hapo" Bibi yake Wang aliongea kisha akakata simu

Sasha aliingia jikoni akaanza kuandaa chakula haraka haraka. Siku zote huwa hazingatii ladha anachojali yeye ni chakula kuiva tu na si vinginevyo.

Baada ya kumaliza alitia kwenye kapu, njiani alionekana kama kituko. Hakuwa akikumbuka kuhusu mapambo aliyoweka usoni....

Mlinzi wa getini alimruhusu akaingia, aliamini binti huyu atakuwa mwenda wazimu.

CEO Wang akiwa anapitia ripoti ya Secretary Kim alishtushwa na muonekano wa Sasha

"Hello CEO Wang, nimekuletea chakula cha mchana" Sasha aliongea

CEO Wang alinyoosha mkono akafunua alijikuta akipiga kelele baada ya kukutana na samaki akiwa ana muangalia

"Ni....ni.. samehe sikujua kama hupendi kichwa cha samaki" Sasha alijitetea.

CEO Wang akiwa mwenye hasira kali alimshika mkono akampeleka bafuni

"Naomba uoshe huo uso wako, unaniabisha Mimi pamoja na Bibi..."

Sasha alianza kunawa uso wake, lakini alishtukia zipu ya gauni yake inafunguliwa

"Oga mwili wote..... kuanzia sasa utakuwa na muonekano mwingine" CEO Wang aliongea, alipoona Sasha bado kazubaa amvulisha gauni lake kibabe

Itaendelea πŸ’₯
MY HOUSE GIRL SASHA πŸ˜‹
EP 03
MTUNZI; BABY SMILE

"Unataka kunifanya nini...." Sasha alipanic baada ya kuona ubabe umekuwa mwingi

"Nachotaka ni wewe kuoga... nitaleta Mtu akusaidie kupendeza," CEO Wang aliongea kisha akaondoka alijitahidi kuizuia akili yake isikumbuke kuhusu uchi wa Sasha

Secretary Kim anafika haraka baada ya kuitwa

"Huyo mtu huko bafuni anatakiwa kupendeza....ni aibu kwangu na kwa Bibi kuishi na mtu mwenye muonekano kama huyo!...niletee mtu atakaye mpendezesha akiwa huko huko bafuni" Mr. Wang aliongea

Secretary Kim alitaka kupinga lakini baada ya kukumbuka teke alilopigwa asubuhi alikausha.

Dakika 10 hazikupita, aliingia mdada mmoja anayesifika kuwa na huduma nzuri kuhusu swala zima la mrembo. Alimpendezesha Sasha huku akimhurumia.

"Kwanini unaniangalia kwa macho ya huruma...." Sasha aliuliza

"Pole, kwa kupoteza usichana wako bafuni....huyu mbwa ni mtu wa Wanawake lakini alitakiwa kukuhurumia."

"Hapana, nimejimwagia chakula bahati mbaya na ndio ma..." Kabla Sasha hajamaliza kuzungumza alikatishwa

"Uwe na amani Mimi ni mtu wa kutunza siri za watu hasa za CEO Wang...."

Sasha hakukuwa na namna, alipendeza sana....mtoa huduma alilipwa chake kisha akasepa.

Macho ya CEO Wang yalitua usoni kwa Sasha, alikuwa kapendeza sana

"Unaweza kuondoka!..." Aliongea

Sasha alibeba kapu lake kisha akaondoka, hakuna hata mmoja aliyemtambua.

Alipofika nyumbani alikaa kwenye kioo akawa anajitazama, kazi zote zilisimama.
Pamoja na mvua kuanza kunyesha hakushtuka kabisa. Ilikuwa ni mvua ya upepo hivyo nguo zote za CEO Wang zilizokuwa kwenye kamba zilipeperushwa hovyo.

Baada ya mvua kukatika ndipo alikumbuka kuhusu nguo za CEO, alitoka nje akiwa mwenye hofu.

Nguo zote zilikuwa chini isipokuwa boksa moja tu ilinasa juu kabisa ya mti mrefu kuliko yote.

"Hili ni jaribu...." Sasha alijisemea kisha akaanza kupanda kwenye mti, ilikuwa ni heri boksa ikutwe kwenye kamba lakini si juu ya mti.

Watu wote waliokuwa barabarani walimshuhudia yeye akiwa juu kabisa ya mti.

Taarifa zinamfikia CEO Wang kuwa nyumbani kwao kuna mtu anafanya jaribio la kujiua.

CEO Wang alipanic hasa alipokumbuka namna alivyomvua gauni kibabe aoge.
Alihisi mtu huyu kajisikia kudhalilika na ndio maana anataka kujiua.

Aliondoka haraka sana, Sasha anaachia tabasamu baada ya kuishika boksa.
Alianza kushuka taratibu, CEO Wang anafika akiwa ana tiririkwa jasho jembamba.

Alijikuta akikodoa macho baada ya kumkuta Sasha akishuka kwenye mti akiwa kashika boksa yake.

"Wakati mvua inanyesha nilikuwa napika ndani, nilisahau kama nimeanika nguo.... naomba unisamehe! boksa yako ilinasa kwenye mti bahati mbaya" Sasha alijitetea

"Kwahiyo ulipanda mpaka kwenye kilele cha juu kabisa kutoa hiyo boksa?...." CEO Wang aliuliza

"Ndiyo...." Sasha alijibu kwa kujiamini akihisi ni ushujaa

"Nifuate...." CEO Wang aliongea kisha akaelekea chumbani kwake akiwa mwenye hasira kupita kiasi

"Niiingie chumbani pia?" Sasha aliuliza.... hadithi za huyu mtu kufanya ngono na wasichana tofauti tofauti alizisikia kwa Dada aliyekuwa ana mremba. Alijikuta akiogopa kuingia.

Hasira ya CEO Wang ilikuwa juu sana, alimvuta akamsukumia kitandani.

"Tafadhali usinibake..." Sasha alikurupuka

"Chukua hilo godoro ukalifue...." CEO Wang alitoa adhabu kwa ujinga aliofanya

Itaendelea πŸ’₯

MY HOUSE GIRL SASHA
EP04
MTUNZI; BABY SMILE

Sasha alikodoa macho kwa kazi aliyopatiwa. Ni mara yake ya kwanza kusikia godoro linafuliwa.
Hakutaka kuuliza maswali mengi alilitoa godoro nje.

Alilimwagia maji akaanza kulisugua na brashi.
Baada ya dakika 40 kupita alimaliza kazi yake.
Ile anaingia ndani aliona aibu baada ya kumfuma CEO Wang akipika

"Ulisema nguo zililowa kwa sababu ulikuwa unapika!....nimetafuta chakula bila mafanikio na ndio maana nimeamua kupika mwenyewe!.... nikimaliza hapa nitahitaji kupumzika chumbani kwangu, hakikisha godoro liwe limekauka" CEO Wang aliongea

Sasha aligundua makosa yake, alipiga magoti chini akaomba msamaha kwa kitendo cha kupanda kwenye mti.

CEO Wang alimgeukia, macho yao yalikutana.
Sasha alijikuta akibabaika huku na kule

"Ni kitu gani ulimshawishi Bibi yangu mpaka akaona unafaa kuwa Mfanyakazi wa hii nyumba?" CEO Wang aliuliza

Sasha alikosa jibu la kutoa, alitazama chini.

CEO Wang aliendelea kupika mpaka alipomaliza.
Kilikuwa ni chakula kingi sana, isingekuwa rahisi kukimaliza pekee yake. Alimwalika Sasha mezani, kilikuwa ni chakula kitamu sana Sasha alishindwa kujizuia....alijikuta akila kama anafukuzwa hivi.

Kwa mara ya kwanza tangu afike hapa alipiga story na CEO Wang

"Ni kweli unaweza kunywa chupa kumi za pombe kali na usilewe?" CEO Wang aliuliza

"Siyo kumi tu....huu mdomo unaweza kunywa pombe kali zaidi ya 50 na nisilewe" Sasha alijinadi.

Baada ya kumaliza kula, CEO Wang aliagiza pombe kali kreti mbili.
Walianza kunywa kwa kushindana, ulikuwa ni mdomo tu. Sasha hakuweza hata kumaliza chupa mbili alizima.

CEO Wang alikunywa chupa saba ndipo akalewa. Alijikuta akimfananisha Sasha na yule mrembo wa kwenye katuni ya Cinderella. Taratibu alisogeza mdomo wake akambusu kwenye paji la uso. Hakuishia hapo alianza kuzishika lips zake.

Tamaa ilimuingia, alianza kupunguza nguo zake moja baada ya nyingine. Alimsogeza karibu Sasha akaanza kumvua taratibu.
Muonekano wa umbo la Binti huyu lilimchanganya zaidi..,bila kufikiria mara mbili mbili alimtanua miguu yake, mmoja ulikaa magharibi na mmoja ukakaa mashariki

Itaendelea πŸ’₯

MY HOUSE GIRL SASHA
EP 05
MTUNZI; BABY SMILE

CEO Wang alijikuta akimfaidi Sasha.....
Sasha akiwa bado na wenge la pombe alijikuta akitoa ushirikiano kwa kitendo alichokuwa anafanyiwa.

Walijikuta wakilala fo fo fo baada ya kumaliza shughuli zote.

Kulivyo pambazuka asubuhi, CEO Wang anashtuka usingizini baada ya simu yake kuita.
Macho yake yalimtoka baada ya kujiona yupo mtupu.

Sasha ndio kushtuka pia, aliziba mdomo wake baada ya kugundua nini kimetenda.
Honi ya gari iliwashtua zaidi, Sasha alivaa nguo zake haraka haraka.... alichungulia kupitia dirisha, aliogopa zaidi baada ya kumuona Bibi. Alitengeneza sura ya tabasamu akaenda kufungua mlango

Bibi aliachia tabasamu baada ya kumuona.
"Sikuwa na uhakika kama ningekukuta, vurugu za Wang nazifahamu....nafarijika kukuona"

"Nitoke hapa niende wapi, sijui kupika vizuri wala kutumia baadhi ya vifaa vya umeme. Hakuna familia inaweza kuniajiri" Sasha aliongea

"Lile godoro kule nje usiniambie Wang alikojoa kitandani" Bibi aliongea

"Hapana, nilijisikia tu kulifua kwa sababu lilikuwa limechafuka,"

"Kwahiyo huwa analala bila kuoga mpaka godoro lichafuke!....au ni uchafu upi unaosemea!" Bibi aliuliza

Kabla Sasha hajajibu CEO Wang alifika akiwa kapendeza tayari. Alimkumbatia Bibi yake kwa sababu imepita miezi miwili sasa bila kuonana

"Nimechelewa kazini, nikirudi tutazungumza...." Wang aliongea kisha akambusu Bibi yake, macho yake na ya Sasha yalikutana, mioyo yao ilishtuka hasa wakikumbuka uzinifu waliofanya usiku baada ya kulewa

Sasha aliingia chumbani kwake, alijitazama kwenye kioo akajikuta akiona aibu.

"Fanya haraka umpelekee chai Wang naelewa ameondoka bila kula" Bibi alimkumbusha baada ya kuona hatoki chumbani kwake

Sasha alivaa haraka haraka, ile anataka kubeba kapu Bibi alimzuia

"Sitaki kuamini huwa unaenda ofisini kwa Wang ukiwa umevaa hivyo..."

"Nimevaa kwa kujisitiri Bibi tatizo liko wapi" Sasha aliongea

"Hapa South Korea tunajali kupendeza na si kujisitiri, usisahau hata kuku huwa wamejisitiri. Kampuni la simu za Samsung Electronics linaongoza kwa kufanya vizuri kuliko Kampuni nyingine za simu. Ni aibu kwenda umevaa hivyo" Bibi aliongea kisha akaingia jukumu la kumpendezesha....kuna kitu alikiona kifuani kwake akajikuta akishangaa

"Hii ni kama love bites?" Bibi aliongea

"Nahisi niling'atwa na mdudu" Sasha aliongea huku moyoni mwake akiwa na hofu, hakutarajia kama CEO Wang anaweza kunogewa namna hiyo kiasi cha kumuwekea alama

Baada ya kupendeza alipanda kwenye gari la familia, Dreva wa Bibi alipatiwa jukumu la kuhakikisha anamfikisha ofisini na kumrudisha.

Baada ya CEO Wang kumaliza kikao aliingia ofisini kwake, macho yake na ya Sasha yalikutana. Kuna namna yalikumbuka uzinzi wao

"CEO Wang, karibu chai" Sasha aliongea kwa kupepesa macho

Wang alifunua hot pot, aliachia tabasamu baada kuona sambusa zilizo tengenezwa na Bibi yake.

Alishika chupa ya chai akanusa, harufu nzuri aliyokutana nayo ilimfanya atabasamu.

Sasha alimsaidia kuweka mambo sawa kisha akamkaribisha, isingekuwa rahisi kwake kufurahia maisha ya ulaji huku mtu mwingine ana mtazama.

"Kaa ule pia...." Alimkaribisha Sasha

Sasha alijitia kuvunga ilihali anataka, alishika kipande cha sambusa akamuwekea mdomoni.

"Sambusa tamu...." Sasha aliongea huku akichukua nyingine, breakfast ya Wang iligeuka kuwa ya yote.

Secretary Kim aliingia akiwa kabeba files mkononi.
Alishangaa kuona CEO kawa mwema namna hii kwa Mfanyakazi wake wa ndani.

"Miss Oh yupo njiani anakuja, saa nane kamili mchana nitaenda kumpokea" Secretary Kim aliongea

"Miss Oh anarudi South Korea!" Wang aliuliza asiamini kabisa

Sasha alijikuta akitulia, siyo mara yake ya kwanza kulisikia hili jina....ni kama amewahi kufanya kazi kwenye nyumba ya mtu anayeitwa Miss Oh lakini hawakuishia vizuri.

"Muambie Bibi nimefurahia chai yake..." Wang aliongea huku akimpatia Sasha kikapu

Sasha alichukua kikapu kisha akaondoka, bahati nzuri au mbaya alisahau simu yake.
Isingekuwa rahisi kwake kuendelea na safari bila kuwa na mawasiliano.

Ile anataka kurudi ofisini achukue simu yake alishangaa baada ya CEO Wang kumletea

"A.. ahsante..." Sasha aliongea

"Kuhusu jana naomba unisamehe ilikuwa ni pombe tu.....tafa.." Kabla Wang hajamalizia maneno yake Sasha aliondoka baada ya kuona mtu huyu ana zungumza upuuzi

CEO Wang hakukubali kushindwa alimfuata akamtangizia kwa mbele

"Una maanisha nini kuondoka kabla sijamaliza kuongea..."

"Ni vizuri kama ungekausha tu....umenifanya nijisikie hatia ndani ya moyo. Sikuwahi kufikiria kama ipo siku nitakuja kugawa K yangu nikiwa katika akili mbovu" Sasha aliongea akiwa kamkazia macho Wang

Hakuona sababu ya kukaa hapa aliondoka akiwa mwenye hasira, bahati mbaya alijikwaa kwenye jiwe. Kama si Wang kuwahi kumdaka huenda angeumiza kichwa chake kwa kujigonga kwenye jiwe

Wang alishindwa kuhimili uzito wa Sasha, kwa pamoja walianguka.... ilikuwa ni faida kwa watazamaji.

Kilichomshtua zaidi Sasha ni pale alipohisi nyeti ya CEO Wang imemgusa sehemu mbaya. Bila kujali alisaidika alimsukuma kwa nguvu akaanguka kule

Itaendelea πŸ’₯


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote