MY JEALOUS BILLIONAIRE HUSBAND

book cover og

Utangulizi

Husqer baltazar
MY JEALOUS BILLIONAIRE HUSBAND
Ep 1.

Naitwa neema thobias, nikiwa nimemaliza mafunzo yangu ya urembo na ususi, nilipata bahati ya kuajiliwa kwenye kampuni ya lasta nje ya nchi,nilikidhi vigezo nikapelekwa marekani, kupata elimu zaidi ya ngozi ya kichwa na uso, ndipo nikafanye nao kazi...

Nilipata mafunzo yangu kwa miaka miwili, nikawa nimeiva haswaaa,nilipelekwa kwenye kampuni ya lasta na mecup jamani kampuni ilikuwa kubwa sio mchezo,ilikuwa inaitwa BEROYA HAIR&MECUP COMPONY ilikuwa ikijihusisha na urembo wote wa uso na kichwa ndani yake kulikuwa na dawa za nywere, nk...

Siku ya kwanza naingia kazini, niliingizwa kwanza kwenye interv na ilikuwa interv ya online, Mungu hamtupi mjawake nilifaulu, mimi ni aina flani ya kidada kipole, nina mwili mzuri sana sijipendelei ila ndio uhalisia, langi yangu ni chocolate glas skin..

Navutia hasa nikiwa natembea na ule upole wangu, sijui kutembea halaka hata kama nitahalakishwa huwa siwezi, nilipass nikapewa mkataba na nyumba ya kuishi mpaka pale nitakapoamua kujitegemea...

Napenda sana kumtanguliza Mungu kwa kila kitu, niliandaa sadaka ya shukrani kwa kufaulu mtihani nilimtumia mama angu apeleke kwa wahitaji tanzania,kisha nikalala, sehemu niliyopewa ilikuwa ni mchanganyiko room moja watu wawili...

Nilipagwa na dada mmoja wakichina,anaitwa chichi, nililala kulikucha tukaendelea na majukumu, nilijitahidi kuchapa kazi ili nisijekuhalibj kibarua,kwa siku nilikuwa nalipwa dola 200..

Watu walianza kunipenda, lakini wakunuchukia hawakukosekana, nikiwa na miezi mitatu kazini wasimamizi wa kuu walipita, mmiliki wa kampuni alikuwa ni kijana mdogo sio mkubwa sana, alikuwa na miaka 39 tu...

Lakini utajili aliokuwa anamiliki mo akasome, alipita kukagua kila sehemu siku nzima iliisha akipita kila idala, alifika idara yangu, alisimama kwa muda kunitizama kisha akamikabidhi note book mpya...

Itaendelea...๐Ÿ”ฅ


Husqer baltazar
MY JEALOUS BILLIONAIRE HUSBAND
Ep 2.

Nilipokea nakumtizama, nisikie maelekezo,alismile kisha akasema uko smart nimependa, angekuwa mwingine angeshaniuliza badala yakusubili maelekezo, naomba uambatane na mimi, na ujaze taarifa zote, kila kitengo tutakachopita make sure husahau chochote, tutafanya hivyi kwa wiki mbili, na nitakulipa kwa hii kazi dola 300 kwa siku, hii ni nje na mshahara wako, nilitafakari kazi ninayopewa nikubwa mno, ndio maana nalipwa pesa nyingi kuliko mshahara, kuzunguka wiki nzima na kunote kila jambo, sio kazi ndogo, nilitafakali kama dakika 5...

Kisha nikajibu sawa nikasain, kisha nikaanza kazi pale pale kwenye kitengo changu,boss alipenda nilivyokuwa shap na smart na kazi yangu, kuna wadada na kiongozi wangu mmoja hakupenda alivuta mdomo huyo๐Ÿ™Œ,ata sikujali nimetumwa na watanzania kusaka pesa, izo kerere za chura sio shida zangu...

CEO alikuwa mkaka haswaaa, yani ni wale wanoume ukiwa nao kila mtu atatamani kukuibia,ukimilikiwa na mwanaume wa aina hii kama huna moyo wa chuma, kimbia mapema ata usijalibu kwa sababu, presure, haitakucha, steress,machozi yani atageuka kitunguh maji kila dk...

Ata kama yeye hawataki ila kile kihofu, acheni tu, kwa hali niliyoiona pale kazini niliapa sitaki mwanaume mzuli,ila hawa wenye sura ya mama tuwaachie wakurya na wachaga, CEO alikuwa ananijali mpaka watu wakahisi kuna kitu sio kawaida lakini sio kweli, nilimuheshimu na yeye aliniheshimu hakukuwa na uhusiano wowote kati yetu...

Nilimaliza kazi yangu ya wiki zote, nikakabidhi, alikagua kisha akanipongeza kwa kazi nzuli, mwandiko wangu ni mzuli, na nimepangilia taarifa zangu vizuli sana, alipenda, mwenzenu darasani sikuwa vizuli ila kwenye isha, kutia maelezo namaliza kalatasi vibaya mno..

Najua kupangilia taarifa, hii kitu nilizaliwa nayo, na nimwepesi wakujua lugha sana, najua lugha zaidi ya tano, tena sio kwa kuzipapasa nj ninazijua kindaki ndaki...

Basi niliongezewa pesa akaomba niwe sectary wake wa ziada, kwa sasa secretary wake yuko nje na mji kwa miezi sita ndio atalejea, alianza kunipa ofa, nikaomba muda nifikilie kwa kina, asante sana mkurungezi kwa ofa yako, nimeipenda sana, lakini nahitaji muda nitafakali kwa kina, ninaweza kukubali kazi, kwa sababu ya tamaa ya cheo na mshahara, lakini nikashindwa kuitendea haki...

Kazi nzuli ni ile mtu anaifanya akiwa anaipenda, na anaifanya kwa ufasaha, natakiwa nijitafakali je naweza kutimiza majukumu hayo vyema, na kama napenda,kama siwezi ni bola nibaki hapa kufanya kitu ninachokiweza kuliko kuja kuhalibu sifa yangu na utendaji wangu wa kazi kwa tamaa ya kitu kikubwa...

Nahitaji kujua zaidi kazi za sectary kwa undani, kisha nifanye maamuzi kama yako ndani ya uwezo wangu, nitafanya kazi ila kama nitaona kuna uwezekano wakukuangusha CEO, utanisamee sitopokea ofa yako...

Mkurungezi alipenda nilivyojibu, kweli hajakosea kukuchagua, nikashangaa na kuuliza nani hajakosea kunichagua? No nimekosea, sijakosea kukuchagua, unajua nini unafanya nimekuelewa hivyi nakupa siki tatu utanipa majibu...

Asante kwa kunielewa mkurungezi,naomba nikuache nikaendelee na majukumu, alinitizama sana mpaka nikajishtukia kulikoni, ila nikapuuza...

Itaendelea...๐Ÿ”ฅ


Husqer baltazar
MY JEALOUS BILLIONAIRE HUSBAND
Ep 3.

Niliaga nakisha nikaondoka, nafika chumbani kwangu, namkuta kiongozi wangu wa kitengo ananisubili kwa hasila sana, nilifika na kumsalimia alikuwa anaitwa madam Celine, ni mzungu na alionekana kumpenda sana mkurungezi, alijionesha wazi wazi ila CEO, alikuwa akimpuuza na nikama, aliamua kunichagua mimi makusudi tu ili kumkatisha tamaa madam celine...

Nilijua kabisa ananichukia kwasababu ya kukubali kuandamana na mr CEO, niliingia nakumsalimia lakini hakuitiakia, nakuona we neema, usiniletee giza lako kwenye anga zangu, nitakupoteza hunijui, unapata wapi ujasili wa kutembea na mchumba wa mtu...

Samahani madam Celine, mimi nilikuwa kikazi tu wala sina shida nae, nyamaza kama kweli huna shida nae kwa nini ulikubali kufanya kazi isiyokuhusu,lakini madami ni kunote tu taarifa," nyamaza ety kunote taarifa ni kazi yako? Wewe ni secretary wake ama ni kihelehele kinakusumbua unataka kuiba mabwana za watu,njaa itakuponza binti, nakupa onyo kaaa mbari na mchumba wangu...

Alimaliza kuongea kisha akaondoka, niliingia kuoga nikiwa na mawazo sana, mwisho nikamwambia Mungu wangu anioneshe njia nakunilinda na kila baya na jema asimame na mimi, kila hatua ninayopiga, niliomba kwa muda mlefu kisha nikatoka, nilimkuta chichi kapika chakula, alinikalibisha nilikaa nikala...

Neema unaonekana hauko sawa, usinambie hayo maneno ndo yamekusononesha kiasi hicho, acha kujipa hatia huna kosa, na kama ni mkurungezi kukutaka hilo, sio tatizo kwasababu ni nyota kama yeye hapendwi, asifikiri ni kwa kila mtu..

Mkurungezi anahaki yakuchagua adate na nani, hilo ni swala la moyo, lakini chichi rafiki yangu mimi si date na mkurungezi, wala hakanitongoza kabisa mimi nashangaa haya yote yanatokea wapi jamani...

Neema mdogo wangu, nyota njema huonekana asubuhi, usionw unapigwa vita , ukajua ni makosa tu sometime ni zahabu inpashwa kwenye moto ili iwe dhahabu, niliamua kunyamaza, sikutaka kuchosha ufahamu wangu...

Usiku tukiwa tumelala simu iliita kucheki no ngeni,nikapokea kisha, haloo neema unaendeleaje? Nimekupigia kukutakia usiku mwema, aliongea hivyo kisha akakata bila kusikia jibu langu..

Itaendelea..๐Ÿ”ฅ


Husqer baltazar
MY JEALOUS BILLIONAIRE HUSBAND
Ep 4.

Nilitafakali sauti lakini sikuitambua, badae ikaja kama ya mkurungezi nikaona ya nini kujichosha,atajitambulisha mwenyewe, niliamua kulala, kulikucha, nikaingia kazini jamani hii siku nilijua kufanyishwa kazi, mpaka inafika jioni, mwili wote unauma..

Siki ilipita kesho yake pia niyale yale ila bahati nzuli kuna kaka alinionea huruma, akaanza kunisaidia, waliongea sana na kumandama kijana wa watu likini jonh hakuniacha, alikuwa mchesi sana, alinisaidia sana tukajikita tumekuwa malafiki wakubwa...

Zilipita siku nne jonh akiwa na mimi bega kwa bega ila siku ya 5, hakuonekana, na hata kwenye simu sikumpata kabisa, niliulizia kila mtu akasema hajui roomate wake akasema kabadilishiwa kituo cha kazi kapelekwa kampuni nyingine...

Nilishangaa kwa nini hata hakuniaga, niliamua kupotezea, maisha yaendelee, nikapata mwingine alikuwa anaitwa jack, huyu alikuwa ananitaka, alikuwa ananizuia kufanya kazi anafanya yeye, alikuwa ni meneja wetu...

Nayeye baada ya wiki mbili akapotea bila kuaga, niliendelea na kazi zangu, kila nikipata kampani, wakiume wanaondoka bila kuaga ila wa kike hapana, siku moja alikuja mdogo wake na mkurugenzi, jamani ni mzuri kams wakuchora, CEO cha mtoto, alinivutia nikabaki nashangaa huu ujinga nimeanza lini mimi...

Nilijipiga kichwa nikatulia, yule kaka alisogea mpaka kwangu, kwa hasira aliniongelesha kama vile ni adui yangu, tena adui wa muda mlefu, alianza na jicho la chuki na hasila ndio akashushia na neno, we binti unahitaji kazi kweli kwa huu mwenendo wako?...

Nilibaki nashangaa nimekosea nini tena, nilitaka kuuliza ila akawa, amenipuuza nskuondoka, nilibaki nashangaa ata kumcrush kote kuliyeyuka, nilibaki na waza mno, badae nikaamua kupuuza, ili akili itulie niendelee na kazi...

Siku iliyofuata niliwahi kazini, nikiwa kazini,nilihisi uwepo wa mtu mwingine, nikachunguz sikuoa nikapuuza,baadae nilikuja niksongezewa kazi, nilifanya kazi, mpaka saa 5 usiku..

Kisha nikarudi kulala, nikiwa chumbani saa 5 na nusu, niliona tena ile no ngeni, niliipuuza, ikatuma ujumbe wa simj,mimi ni mr Mathew, nilishtuka mkurungezi ? Nikiwa natafakali simu ikaita tena nikapokea, alinijulia hali, kisha akaniuliza kuhusu kazi, nilimwambia bado nachunguza, akasema neema samahani, lakini kuna jambo naomba kukuomba, na sitamani unikatalie, nakusihi mnoo, nisikilize kwa makini na unijibu sasa hivi siwezi kungoja zaidi....

Itaendelea...๐Ÿ”ฅ


Husqer Baltazar
MY JEALOUS BILLIONAIRE HUSBAND
Ep 5.

Ninauhitaji mkubwa wa secretary, lakini pia, ni kwa lengo la kukulinda, hapo ulipo kwa sasa sio salama, najua unajiuliza kwa nini wewe, yes kuna sababu ya kuwa wewe kwanza naomba unielewe ukubali kuwa secretary kisha mengine utatambua...

Niliwaza nikiamgalia na heka heka njnazopitia nikaona acha nikubali, alishukuru kisha akakata nakusema kesho atakuja kunichukua, kisha nisaini mkataba nakuondoka...

Kweli kesho yake alikuja, nikasoma mkataba nakusain nilimuaga chichi kwa hudhuni kwani nimtu mwema sana, nilifika nikakuta mkurugenzi yuko na mdogo wake, kwa jinsi ninavyomuogopa nilitamani kujificha, ila sikiwa na jinsi ilibidi tu nijikaze, mdogo mtu aliniwahi mizigo yangu, akanisaidia kuingiza kwenye gari, nilishangaa sana mmmh huyu! Ama sie yeye...

Ilibidi nikae nae siti moja,tukiwa kwenye gari,nilipitiwa usingizi, nakuja kishtuka niko kwenye mapaja ya mr martin, tena kanilaza vizuli, nakunifunika koti lake,kabla hawajajua kama nimeamka nikafuma maongezi yao...

Bro hujui tu inavyouma, yani mtu nampenda then anakuwa na ukalibu na mwanaume kiasi hicho, nimechukia basi tu hakajui, huku umenisaidia ndio kumleta karibu na mimi, lakini siwezi kuvumilia zaidi nahitaji ajue kabisa kama tuko kwenye mahusiano...

Max mdogo wangu, usiwe na papala ongea na neema vizuli, kwanza onyesha upendo wako kwa vitendo sio ukali, na kuwahamisha wanaume anaokuwa nao karibu sio tiba, tiba ni wewe kuweka hisia zako wazi, akuelewe, kisha itafuata hio hatua ya wivu, akishakuwa wako utamwambia kinachokunyima amani...

Kwa sasa hupaswi kumlaumu kwasababu hajuinchochote, dah bro hujui tu nateseka sana, mpaka nimefunga safali kuja huku, ujue moyo umeshindwa kuvumilia,sijui kwa nini nimependa, mateso ya moyo wangu ni makari naogopa hatima yangu, na vipi kama atanikataa, sijui kama nitaweza kuhimili hayo maumivu...

Max najuanulivyozaifu katika mapenzi, naomba ujiandae kwa yote acha kuwaza ujinga nitajitahidi nikusaidie katika hili lakini nakushauli acha wivu kupitiliza utamkosa...

Kaka najitajidi nashindwa mimi namtaka awe wakwangu peke yangu sio wa uma, sitaki mwilinwake ushikwe na mwanaume yoyote zaidi yangu hilo tu kaka ndio tatizo, na siwezi kuzoea katika hili..

Mh nilishangaa, inamana naongelewa neema mimi! Kumbe apa kumnembelezwa kuwa secretary ni kwasababu ya huyu chawivu mmmh, nikajua ata mr CEO, kanipenda kumbe nmdogo wake, acha inyeshe nione panapovuja...

Nilijikausha tu, muda huo, tukawa tumefika,kwenye kampuni kibwa sana kuliko ata ile niliyotoka,sikiwa naona kwa mud huo il a nlnilovyoamshwa niliiona,mr chawivu aka max, alisema vipi umechoka sana? Kama bado unauchovu unaweza kupumzika kwa leo...

Nilimtizama mr CEO, ili kuhakikisha jawabu, ghafra max akanuna nakuondoka, neema mzoee huyo ndo atakuwa boss wako, ni CEO wa hapa, unahitaji kumzoea hapendi secretary wake, uwe na urafiki ama mazoea na watu wengine, lakini pia anapenda umsikilize yeye zaidi na umuamini...

Nilishangaa lakini mkurungezi uliniomba niwe secretary wako kulikoni tena,ndio neema ndio hivyo lakini kwa sasa namkabidhi mdogo wangu ili nikajiendeleze, nimekuomba wewe uwe sectary kwa sababu naamini ukinisaidia katika hili, kampuni itakuwa salama, wewe nimuelewa kwa aina ya tabia za mdogo wangu natumainj utazishika halaka na kuepuka kumkwaza ili mfanye kazi, ukishamkwaza hawezi kufanya kazi...

Nilichoka mwilina roho, ikabidi tu nikubali, niliamua kuingia kwanza kuomba msamaa kwa boss wangu max,nilimkuta ofc niliyoelekezwa ata sikugonga niliingia tu, na ndo maelekezo niliyopewa na mkurungenzi...

Niliingia nakukuta analia machozi kabisa, nina huruma mwenzenu nilikaonea huruma, nikasogea nikaanza kumnembeleza, yeye alijua ni kaka ake nilivyomgusa tu, akashtuka nakufuta machozi halaka...

Neema umefuata nini humu? Samahani boss nisamee, sikujua nani napaswa kufanya nae kazi, yani neema kutokujua ndo unipuuze mimi kila mala, unajua unachonifanyia lakini,unatambua alionge kwa huzuni mno...

Nilisogea nikamkumbatia ili amalize hasira zake, lakini nilivyomkumbatia tu,alinivaa mpaka ukutani, alinibananisha, akajivutua juice yake, kwa muda mlefu, mpaka nikahisi sasa huyu anataka anikaushe mate...

Itaendelea...๐Ÿ”ฅ


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote