MY MIKE TYSON

book cover og

Utangulizi

GAIDI ALIEUTEKA MOYO WANGU..
kuna baadhi ya watu wanapitia changamoto ambazo zinakuja kuharibu kabisa maisha yao ya baadae, mwanaume mmoja baada ya kushuhudia usaliti wa mama yake kwa baba yake anajikuta anachukia sana wanawake, na hata alipokuwa mkubwa anaamuwa kuwa busy na utafutaji na kuachana kabisa na maswala ya kukaa karibu na wanawake..
Anafungua hospital na hakuwa anahutaji daktar wa kike, ila anakosekana docta wa upasuaji wa kiume na kuamua kuajiri docta wa kike, akawa hampendi kabisa na ni kama amemuajiri kwa sababu hakuwa na namna ila mwisho wa siku anajikuta anampenda huyo docta wa kike ila anajitahidi kupambana na hisia zake maana hakutaka kuwa na mwanamke ila kama tunavyojua, penzi ni kikohozi kulificha haiwezekani nducho kilichomkuta kijana kauzu unajua nn kiliendelea usikose simulizi hii ya kusisimua ya MY MIKE TYSON (raha ya kuuteka moyo wa gaidi)

MY MIKE TYSON
( Raha ya kumiliki moyo wa gaidi๐Ÿฅฐ )
Husqer Baltazar.
EP 01

Ilikuwa ni hukumu ya kifo kama Mwanaume angebainika kumuingilia mke wake au mtu yoyote kinyume na maumbile ๐Ÿ–๏ธ

Hii sheria ilijulikana hata kwa mtoto aliyeko tumboni, kwa asilimia 99 jamii yetu ilikaa katika mstari mnyoofu like rula hivi ๐Ÿ˜‰

Life stlye la familia yangu lilikuwa bomba sana, ingawa kipato chetu kilikuwa cha chini but tuliishi kwa upendo kiasi kwamba majirani zetu walituonea wivu ๐Ÿ˜„

Sijui ni demon gani ilimvaa Mama, kwani nilivyo fikisha miaka 16 alianza kulalamika kwa kila kitu alichofanya my Dad ๐Ÿ˜ญ

Amani iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya familia yetu ilipotea

"Mwanamke hafurahishwi tu kitandani!....kila nachokuomba imekuwa mtihani ni heri tuachane!" Huu ndio ulikuwa wimbo wa Mama kila siku

Mwanzo alizungumza hivi akiwa amehakikisha nimelala but siku zilivyozidi kwenda hakujali uwepo wangu, alikuwa anamdhalilisha Baba yangu infront of me ๐Ÿ˜ž

Jioni moja Baba yangu aliniletea zawadi ya viatu vipya.....vilikuwa ni vya gharama sana ๐Ÿค—. Hakuishia hapo alimnunulia Mama yangu pochi kali.

Ilikuwa ni furaha ndani ya familia yetu because of Dad. Nilikuwa wa kwanza kufika shuleni ๐Ÿ˜„ si mnajua tena nilitamani kila mtu avione viatu nilivyo nunuliwa na Baba.

"Tangu Mama yako aanze kutembea na yule tajiri maisha yenu yamebadilika....I can see hata viatu ulivyovaa ni jasho la yule jamaa ๐Ÿฅด, mtaa mzima tunajua Baba yako hana uwezo wa kununua vitu hivi" Classmate wangu ambaye pia ni jirani yetu aliongea

Maneno yake yalikuwa magumu sana kwangu nilijikuta ni kimrushia ngumi iliyompelekea adondoke chini ๐Ÿฅต

"Huna haja ya kumpiga....kila mtu ana fahamu kuwa Mama yako anatembea na yule tajiri na verysoon ataolewa pale, seriously namhurumia Baba yako ๐Ÿ˜ž" Kijana mpole kuliko wote darasani aliongea

Nilijikuta ni kikosa nguvu ya kukaa shuleni. Nilirudi nyumbani kwa kukimbia.... nilihitaji kumuuliza Mama yangu kuhusu hizi dirty scandal nilizoambiwa na classmates wangu ๐Ÿ˜ญ

Niliingia ndani bila hodi, nilishtuka sana nilivyomkuta Mama yangu akifanya mapenzi sebuleni kwetu na Mwanaume nisiyemjua ๐Ÿ˜ต

Mwanzo nilihisi Mama yangu anabakwa lakini baada ya kunitaka nitoke ndani avae niligundua si ubakaji tena bali ni makubaliano ๐Ÿฅถ

Hasira zilinipanda ghafla....nilichukua mkuki uliokuwa nyuma ya mlango ni mshambulie Mwanaume aliyejimilikisha vitu vya Baba ๐Ÿ˜ญ

Itaendelea ๐Ÿ’ฅ

_**MY MIKE TYSON*_*
( Raha ya kumiliki moyo wa gaidi๐Ÿฅฐ )
Husqer Baltazar.
EP 02

Cha ajabu my Mama aligeuka kuwa ngao, I don't know kama naeleweka but alikuwa tayari kufa yeye na si huyu Mwanaume ๐Ÿ˜ญ

Ni kama alikuwa ananiambia Mike kill me ila siyo yeye ๐Ÿ˜ญ

Nilitupa mkuki kisha ni kaondoka kwa hasira sikuwa na direction wapi niende but suddenly wazo la kwenda kazini kwa Baba liliniijia ๐Ÿ˜“

Yes! nilitaka kumuambia ujinga wa Mama.... Baba yangu Mimi ni carpenter, kazi yake hii ndogo ndio imenifanya ni vae viatu vikali

"Mike huu ni muda wa shule don't tell me umefukuzwa kisa hicho kipara ๐Ÿ˜€" Baba yangu aliongea huku akiachia tabasamu, hajawahi kuwa serious kwangu

Nguvu za kuzungumza ujinga wa Mama ulikata....sikuwa tayari kumuumiza moyo wake ๐Ÿ’”

"Nipo hapa kukusaidia.... mwalimu wa kiswahili hayupo hivyo nitatumia muda wake kukusogezea hizo mbao ๐Ÿ˜‰" Niliongea

Baba yangu alitaka kugoma lakini kwa namna nilivyokuwa stubborn aliniacha.
Ilikuwa ni raha sana kwangu kufanya kazi pamoja na my Dad โค๏ธ

Baada ya kufunga kazi tulirudi nyumbani.... Mama yangu alikuwa amepika chakula kizuri sana.
Gharama yake ilikuwa ni kubwa, ni wazi kabisa Baba yangu alitamani kuuliza but alipotezea

Japo nilikuwa na njaa lakini sikuwa tayari kula chakula cha Mama....ndani ya moyo wangu kulikuwa na hasira kali ๐Ÿ˜ก

Niliingia chumbani kwangu ni kajifungia....nilisikia tu Mama akimtupia lawama Baba yangu kuwa nimekuwa jeuri sababu yake.

Ugomvi mkubwa uliibuka kati yao hata chakula hakikulika

"Naijua sababu iliyokufanya ubadilike hivi....fanya chochote unachoona ni sahihi but Mimi hapa sitakuuliza, ahsante kwa chakula" Nilimsikia Baba yangu akiongea

"Ndiyo, nimetembea na yule tajiri hapa sebuleni kwako Mike ni shahidi na nitaendelea kutembea naye kwa sababu ananitimizia mahitaji yangu " Nilimsikia Mama yangu akiongea

Sikuweza kulala, nilifika sebuleni kuamua ugomvi wao.....niliogopa sana baada ya kumfuma Baba akiwa kashika mkuki

Akili yangu ilinituma anataka kumuua Mama cha ajabu aliuchoma kwenye kochi

"Najua Mimi si hadhi yako lakini nakupenda..... nitajitahidi kukutimizia mahitaji yako hata kama itamaanisha kuniua ๐Ÿ˜ญ" Baba alizungumza kisha akaenda chumbani

Mama yangu alinisogelea kisha akanishika bega

"Jifanye kipofu pale unapoona vitu vibaya.....pia kuwa kiziwi pale unaposikia migogoro ya watu wazima, fanya hivyo utaishi miaka mingi" Mama yangu aliongea kisha akarudi mezani kula

Sijui nililala saa ngapi lakini nilishtuliwa na kelele za king'ora cha gari la Polisi.
Kichwa changu kilikuwa kizito kama nimebeba dunia nzima ๐Ÿฅต

Guys ๐Ÿ˜ญ.....sijui wanawake ni viumbe gani lakini Mama yangu alitamka zaidi ya mara sita mbele ya Polisi kuwa Baba yangu Mimi amemlawiti mbele yangu ๐Ÿ˜ต

"Mike, waambie Polisi kitu alichonitendea Baba yako usiku mzima ๐Ÿ˜ญ" Mama aliongea huku akitokwa machozi

Majirani walijaa uwanjani kwetu kusikia what's happening

Itaendelea ๐Ÿ’ฅ

_**MY MIKE TYSON*_*
( Raha ya kumiliki moyo wa gaidi๐Ÿฅฐ )
Husqer Baltazar.
EP 03

Mimi, Baba pamoja na Mama tuliwekwa kwenye gari la Polisi.
Ni kama nilikuwa nimepatwa na mshtuko hivi kwani sikuweza kuongea chochote ๐Ÿ˜ท

Mama yangu alizidi kulalamika maumivu mpaka tulipofika kituo cha Polisi.

Kila kitu kilienda haraka na hata ni kajiuliza nani yupo nyuma ya Mama ๐Ÿฅบ

Vipimo vya Daktari vilidhibitisha kuwa Mama kaingiliwa ๐Ÿ˜ญ

Hakukuwa na haja ya kumkalisha Baba mahabusu.....kauli ya Hakimu ilikuwa ni kunyongwa mara moja kabla jua halijazama

"Mike.....hata kama utafanya nini kamwe huwezi kumridhisha Mwanamke. Nimefanya vitu vingi sana kwa ajili ya Mama yako siwezi kuvizungumza mbele yako kwa sababu ni aibu....ni muda wa Mimi kupumzika am sorry kwa kukuacha ๐Ÿ˜ญ" Baba yangu aliniambia

Kila nilipotaka kupaza sauti it's not him sauti hauikutoka. Ni kama kuna kitu kiliziba mdomo wangu ๐Ÿ˜“

Nililia kilio kisichoelezeka..... infront of me my Dad โค๏ธ alinyongwa, watu wasiojua nini kinaendelea waliirushia mawe maiti yake.

Sikumbuki nini kilitokea lakini nilikuja kushtuka nikiwa chumbani nimelala

"Baba yako alikuwa ni mshenzi sana....acha afe tu, acha afe.... kuanzia sasa nitakupa kila kitu" Mama yangu aliongea

Nilijikuta ni kimkaba koo lake, nilitaka afe pia kama alivyokufa Baba ๐Ÿ˜ก

Mama alipambana mpaka akafanikiwa kujiokoa mikononi mwangu ๐Ÿฅต

"Nilitaka ni kuchukue ukaishi kwenye ghorofa lakini kwa kitendo cha kutaka kuniua kisa yule mshenzi ni unforgivable ๐Ÿ–๏ธ.... mtoto wa nyoka ni nyoka ๐Ÿ˜ก....jipambanie mwenyewe, maiti ya Baba yako iko sebuleni utazika mwenyewe na majirani" Mama alinifokea akataka kuondoka

Nilimshika mkono wake kwa nguvu zote ๐Ÿ˜ก

Itaendelea ๐Ÿ’ฅ

_**MY MIKE TYSON*_*
( Raha ya kumiliki moyo wa gaidi๐Ÿฅฐ )
Husqer Baltazar.
EP 04

"Nitamzika my Dad โค๏ธ bila msaada wako....kama Baba yangu hakuweza kuridhisha moyo wako hakuna Mwanaume kwenye ulimwengu huu ataweza kukufurahisha.....Mzimu wa my dad utakuwinda maisha yako yote....nakuchukia kwa kumdhalilisha Baba yangu....." Niliongea nikiwa na hasira kupita kiasi ๐Ÿ˜ก, sikuelewa kama makucha yangu yalikuwa yanatoboa mkono wa Mama kiasi kwamba damu zilichurizika

"Darling kama unataka tuishi kwa amani muue huyu Mtoto kama ukimuacha he will come for us ๐Ÿ–๏ธ" Yule Mwanaume niliyewahi kumfuma na Mama wakifanya mapenzi aliongea

"Si....si...wezi kumuua mwanangu ๐Ÿ˜ต" Mama aliongea akionekana kuchanganyikiwa

"Kama uliweza kuua Baba yake kwa kuzungumza uongo huna haja ya kusita.... huyu ni mtoto wa Tyson na si wako๐Ÿฅด" Mwanaume huyu aliongea

Nilikuwa nimechoka kuishi, nilijikokota ni kaelekea sebuleni ilikokuwa maiti ya Baba yangu. Sikutaka kusika namna wanavyopanga mikakati yao juu yangu ๐Ÿ’”

My Dad alikuwa ametulia as if ataamka baadae, nilijilaza taratibu kwenye kifua chake
Maneno yake ya mwisho yalijirudia kichwani kwangu ๐Ÿ˜ญ

I don't know Mama na bwana wake walitoka nje saa ngapi....nilisikia harufu ya vitu vikiiungua ๐Ÿ”ฅ

Sikutaka ku escape, kama Mama aliyenizaa anaona sistahili kuishi sikuona sababu ya ku struggle ๐Ÿ˜ญ dying here ilikuwa the best option kwangu.

Nilifumba macho ni kasubiria kifo kinichukue.....sikumbuki hata nini kilitokea

Nilikuja kushtuka nikiwa hospitali....sijui ni nani alinileta hapa lakini kwa kuwa intention yangu ilikuwa ni kufa nilianza kutafuta kitu kikali like panga au kisu nijimalize ๐Ÿ’”

Nikiwa katika kutafuta silaha mlango ulifunguliwa, nilishtuka baada ya kumuona Mwanaume aliyekuwa anapenda kuja kazini kwa Baba

Alinisogelea akanishika mikono....kwa haraka tu alikuwa amechanganyikiwa hivi though aliforce kuwa sawa ๐Ÿฅต

"Mike..... Mama yako ni shetani, kama si Mimi kujitokeza haraka basi ungefia kwenye moto. Tyson kafariki kwa sababu ya upendo aliokuwa nao kwa Mama yako ๐Ÿ˜ญ..... naomba uishi, kamwe usije kufikiria kujiua kwa sababu Mimi hapa nitakuwa bega kwa bega na wewe...." Simeon aliongea

"Uncle natamani kufa....siamini kama Mama anaweza kutufanyia hivi" Niliongea ๐Ÿ˜ญ

"Mwanamke? sijawahi na sitawahi kuweka imani yangu kwa mwanamke.... viumbe hawa ni makatili, nitakufundisha kutafuta pesa bila kujali ni njia halali au haramu....all I want ni Mama yako kujutia kwanini alikuacha ufe kwenye moto mkali kisa mapenzi ๐Ÿฅถ kwa ajili ya Tyson nitafanya chochote" Uncle Simeon aliongea huku akijipiga piga kifua chake ๐Ÿ˜ก

Nilijikuta nikilia kwa namna rafiki wa Baba alivyokuwa anateseka sababu ya matendo ya Mama.

Nilimshika mkono kwa sababu niliona anaumiza kifua chake

"Ndiyo, Wanawake wote ni mashetani..... sitakuwa na huruma na hawa viumbe maisha yangu yote ๐Ÿ˜•" Niliongea

Itaendelea ๐Ÿ’ฅ

_**MY MIKE TYSON*_*
( Raha ya kumiliki moyo wa gaidi๐Ÿฅฐ )
Husqer Baltazar.
EP 05

Baada Ya Miaka Miwili Kupita;
Sikuwa ni kikumbuka kuhusu shule tena.... shughuli nilizokuwa nafanya nilikuwa nazielewa mwenyewe na Uncle Simeon ๐Ÿ˜

All I want ilikuwa ni kujikusanyia pesa na si kingine. Siku moja nikiwa na Uncle Simeon kwenye mission ngumu ya usafirishaji dawa za kulevya tulikumbana na Polisi ๐Ÿฅถ

Tulikuwa na machaguo mawili tu kukamatwa au kuwaua Polisi. Japo silaha zetu hazikuwa nzito sana ukilinganisha na zao lakini tulipambana kiume ๐Ÿ˜ซ

"Tyson (Baba) atatuona wajinga kufa wote hapa.... hebu fanya kuondoka bila Mimi, ni heri Mimi nife lakini si wewe. Believe me kama utafanikiwa kufikisha huu mzigo mahali unakotakiwa utalipwa pesa nyingi sana. Hutaishi kuwaza pesa kama ilivyokuwa kwa Baba yako.... pindi utakapo tajirika achana na hizi mission, naomba uwe mtu mwema, kufukuzana na Polisi ๐Ÿ‘ฎ siyo kitu cha kufurahisha" Uncle Simeon aliongea kisha akanisukuma ni kadondokea upande wa pili

Alianza kukabiliana na Polisi bila Mimi ๐Ÿ˜ญ....nilitaka kurudi upande wake lakini baada ya kukumbuka namna Baba yangu alivyo kufa niliendelea na safari yangu

Ndani ya moyo wangu nilikuwa na maumivu ๐Ÿ’” makubwa ya kutengana na Uncle Simeon lakini nilipiga hatua mbele bila kujali ataishi au kufa. Mzigo niliokuwa nao ulikuwa na thamani kubwa kuliko Wanawake wote duniani ๐Ÿ˜

Niliachia tabasamu baada ya kuiona Meli.... nilitoa ishara ya vidole โœŒ๏ธ kama nilivyo fundishwa na Uncle Simeon, Mwanamke aliyevalia nguo nyeusi alinirudishia ishara hii๐Ÿคž

Nilirusha begi lenye mzigo kisha na wao walinirushia begi lenye pesa....
Sikuwa na shaka ya kulikagua begi, kutokana na maelezo ya Uncle Simeon watu hawa ni waaminifu kuliko viumbe wote duniani ๐Ÿ˜

Wanaliheshimu jasho la Mtu....I wish Mama yangu angekuwa kama hawa watu ๐Ÿ˜“.....

Tabasamu lilizidi kuongezeka usoni mwangu baada ya kumuona Uncle Simeon ๐Ÿ˜Š....bega lake lilimeza risasi lakini furaha ya thamani ya kitu kilichokuwa ndani ya begi ilitufanya tulale ufukweni mwa bahari ๐Ÿ˜€

"Pesa zote hizo ni za kwako.....kila kitu kilikuwa ni kwa ajili yako, hakikisha dunia hii inakaa kiganjani kwako kuanzia sasa ๐Ÿคจ Mwanamke ni kiumbe asiyeridhika, kamwe usije kujituma kwa ajili yake ๐Ÿ˜‰" Uncle Simeon alinikumbusha

Itaendelea ๐Ÿ’ฅ


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote