MY POOR BILLIONEA HUSBAND 1
MTUNZI SMILE SHINE
Tamina ni binti ambae alizaliwa kwenye matabaka yeye na ndugu zake wawili. Mama yao Bi zawadi aliwazaa kila mtoto na baba yake.
Tamina baba yake alikuwa na asili ya kichina , Sasha na Maria baba zao walikuwa waswahili lakini kila mmoja alikuwa na baba yake.
Ni zawadi aliwaleta watoto wake kwa shida bila msaada wowote kutoka kwa baba zao lakini alikuwa mwanamke mpambanaji sana akimiliki duka kubwa la nguo na vipodozi pia alikuwa na saloon ya wanawake.
Tamina alikuwa ni binti mwenye bahati sana mara nyingi alipokuwa akiongozana na ndugu zake alikuwa akitongozwa sana na wanaume hasa wale wenye kipato cha juu, wenye magari pia wenye muonekano mzuri . Pia katika utafutaji wake alikuwa mtu ambae anapata sana pesa hii hali ilimfanya dada yake Maria amuonee wivu sana. Kuna wakati alichukua vitu vya Tamina bora ruhusa Tamina alipoongea neno lake lilikuwa ni moja.
" Acha roho mbaya nyota yako ya jaa unejaaliwa kupata acha na sisi tutembelee nyota. Kuna muda Tamina alikuwa alinunua nguo ilamkaa vizuri Maria nae alienda kutafuta nguo kama ya Tamina.
Tamina hakuwa anapendezwa na tabia za dada yake lakini kwakuwa ni dada aliamua kupotezea na kumchukulia kawaida.
Pamoja na Tamina kufuatwa na wanaume wengi hakuwa akiwashobokea sababu alikuwa na mwanaume wake ambae wakipendana sana na alikuwa akimsaidia kwenye mambo yake mengi mpaka kumpa mtaji wa kuuza ice cream .
Kwenye mahusiano yao hakuna aliefahamu maana Tamim alitaka iwe siri kwasababu alikuwa na sababu zake binafsi.
Hata jimmy alipotaka afike nyumbani kwao Tamina alimzuia na kumwambia muda ukifika ataenda kumtambulisha.
Siku moja Tamina alikuwa kwenye kibanda chake akiuza ice cream mara ilifika gari moja ya kifahari na kusimama mbele ya kibanda chake.
Alishuka kaka mmoja mtanashati akaelekea kwenye kibanda cha Tamina, wakati huo Tamina alikuwa akimkaribisha kwa tabasamu mwanana.
" Karibu mpenzi wangu Jimmy.
" Asante baby.
Walikumbatiana na kujuliana hali baada ya hapo Tamina alimkaribisha kwenye kiti.
" Niambie mpenzi wangu.
" Sina cha kusema zaidi ya neno I miss you and I love you.
" Asante mpenzi nilikukumbuka pia na nina kupenda pia .
Jimmy alisogea nyuma kidogo kisha akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali akatoa kiboksi kidogo kisha akajifungua , ndani ya kile kiboksi kulikuwa na pete nzuri sana.
Tamina alishangaa huku akiwa kaweka viganja vyake mdomoni.
Jimmy alishuka ile pete vizuri kisha akamuangalia Tamina usoni alafu akasema.
" Tamina upo tayari kuwa na mimi milele? ni kiwa namaanisha uwe mke wangu?
" Ndio baby nipo tayari.
Bila kuchelewa Jimmy aliushika mkono wa kushoto wa Tamina kisha taratibu akaingiza pete kwenye kidole cha Tamina.
Tamina alishindwa kujizuia machozi yalimtoka kwa furaha. Jimmy alimkumbatia kwa upendo mkubwa huku akimwambia kuwa anampenda.
Wakiwa bado wamekumbatiana mara alitokea Maria na kuwakuta wamekumbatiana , Maria alisimama kidogo na kuwaangalia kwa muda, jimmy alipomuona alivunja kumbatio . Maria akaitwa jina la mdogo wake na kufanya Tamina ageuke kumuangalia
" Tamina....
" Mmmm karibu.
" Nilikuwa nimekupitia twende nyumbani. Huu ni muda wako wa kuondoka
" Sawa. Lakini ungenipigua kwanza simu kama unavyofanya siku zote. Alisema Tamina kama kwamba hakupendezwa na Maria kumkuta akiwa na Jimmy tena mbaya zaidi kwenye hali aliyoyakuta.
" Ndio imeshatolewa nimekufuma.
Maria aliongea huku akimuangalia sana Jimmy, alishindwa kuvumilia akauliza.
" Tamina huyu ndio shemeji yangu?
Tamina hakuwa na namna ilimbidi atoe utambulisho.
" Ndio anaitwa Jimmy. Jimmy huyu ni dada yangu anaitwa Maria.
" Sio jina geni mara nyingi huwa unamtaja. Nashukuru kukufahamu shemeji Maria.
Walipeana mikono na kuendelea kuongea.
" Inabidi Tamina anilete nyumbani kuwafahamu na ndugu wengine maana hatua tuliyofikia niya uchumba.
" Uchumba? Kwahiyo mmechumbiana?
" Ndio nimemvalisha pete .
Tamina alitamani kumzuia Jimmy wasiendelee kuongea lakini hakuweza na wakati huo kwa kiasi flani Maria alikunja uso ni kama hakupendezwa na kile alichoambiwa na Jimmy.
" Inamaana umemchumbia bila sisi kujua?
" Sio mbaya maana tunaweza kurudia zoezi.
" Hayo ni makubaliano yangu na mpenzi wangu nyie ni watu wa kupewa taarifa tu. Alisema Tamina na kumfanya Maria amkate jicho badae anajichekesha kinafki na kusema.
" Hongereni sana.
Tamina akikatisha maongezi yao kwa kusema.
" Acha nifunge tuondoke , Jimmy unaweza kwenda kupumzika tutaongea badae kwenye simu.
" Tamina mpenzi usijali sijachoka ki hivyo nitawapelekea nyumbani.
" Hapana tutachukua usafiri.
" Kwanini mchukue usafiri wakati gari ipo? Nitawapeleka.
" Kama gari ya shemeji ipo kwanini tukabanane kwenye daladala . Alisema Maria.
Tamina alikubali akafunga duka lake la ice cream wakaenda kupanda kwenye gari .
Tamina alikaa mbele na Jimmy, Maria alikuwa kakaa nyuma anachati na simu yake.
Safari iliendelea mpaka nyumba ya tatu kabla ya kufika kwao Jimmy akasema.
" Baby mtashukua hapa au?
Kabla Tamina hajajibu Maria akadakia.
" Kwanini hapa shem nyumbani ni hapo mbele tafadhali tufikishe nyumbani.
Jimmy alimuangalia Tamim ili kupata ruhusa maana siku zote Tamina hakutaka Jimmy amfikishe nyumbani alishuka huko nyuma kabla ya kukaribia nyumbani kwao.
Siku hiyo Tamina alikubali awafikishe nyumbani kwao.
Walifika mpaka mbele ya nyumba yao jimmy akasimamisha gari Tamina na Maria wakashuka na kuagana nao.
Tamina akashituka baada ya kumuona Sasha na mama yao akiwa wamesimama wanawaangalia.
Tamina aliingiwa na uoga.
" Maria , mama na Sasha mbona wapo hapa kuna nini?
Maria alitabasamu kisha akasema.
" Niliwatumia msg nikawaambia watoke kumuona handsome boy wako....
" Umefanya nini Maria ndio maana mimi sikuwa nata mjue kuhusu Jimmy leo imekuwa bahati mbaya kuonana nae umekosa Subra ukawaambia.
" Sasa ulikuwa unafichua nini? Laiti ningekuwa mimi siku ileile ya kwanza aliyonotongiza ningemleta mpaka sebleni.
" Sijapenda.
Walienda mpaka aliposimama Sasha na mama yao wakasalimiana.
" Hongera mdogo wangu ila punguza kufanya siri bila Maria tusingejua kuwa una mwanaume na pia amekubaliana pete ya uchumba.
Tamina alibaki katoka macho huku akijiuliza hizo taarifa zote wamepewa saa ngapi?
MY POOR BILLIONEA HUSBAND 2
MTUNZI SMILE SHINE
Mama yake Tamina alikuwa akimuangalia Tamina ili asijue chochote kutoka kwa Tamina.
" Ni kweli mama ila nilikuwa natafuta muda wa kukwambia na kuja kumtambulisha.
" Acha kufanya mambo kienyeji wewe una wazazi alafu imeruhusu vipi kuvalishwa pete kabla ya dada zako?
Tamina alimuangalia mama yake bila kujibu
" Mwambie huyo mwenzio kila familia zina taratibu zake alitakiwa kufika nyumbani kabla ya kukuvalisha hiyo pete.
" Nisamehe mama .
Tamina aliingia ndani na kuwaacha bado wakiwa wamesimama nje.
Siku zilienda mara kwa mara Maria akawa anaenda kumpitia Tamina pindi anapotoka kwenye mihangaiko yake pia walikuwa wakikutana na Jimmy wakawa wanatoka pamoja kwenda kupata chakula cha usiku na sehemu mbali mbali.
Kuna muda Tamina na Jimmy walikuwa wakionyesha na upendo kama kujuliana hata kupishana kile kitendo kilikuwa kinamuumiza Maria alikuwa anatamani nafasi ya Tamina iwe yake .
Taratibu akaanza kujenga ukaribu na Jimmy wakawa wanawasiliana , Maria alimpigia simu waende kula chakula cha mchana. Hata alipokuwa na shida ndogo ndogo Jimmy alimsaidia .
Mwisho wa siku jimmy aliingia kwenye mitego ya Maria , Siku moja Maria alimuomba jimmy waende club, jimmy hakukata walifika huko walicheza na kunywa hatimae mwisho wa siku wakajikuta wamelala kitanda kimoja na hapa ndipo mambo yalianza kuharibika, Maria na Jimmy wakawa na uhusiano wa siri lakini mwisho wa siku Maria alishindwa kuficha hisia zake kwa Jimmy watu waliona na kumpa taarifa Tamina.
Siku moja Tamina akiwa kazini kwake alipokea simu kutoka kwa mtu ambae anamfahamu.
" Tamina hivi una habari kuwa jana usiku dada yako Maria alikuwa na Jimmy club na hawakuonekana kama mtu na shemeji yake bali ni mtu na mpenzi wake.
Tamina aliposikia hivyo alishituka na mapigo ya moyo wake walienda mbia , kwa upande mwingine aliamini sababu anamjua sana ndugu yake hasa Maria amekuwa na kesi nyingi ya kutembea na mabwana wa mashoga zake. Na hakuwa na rafiki mtaani .
" Sawa Dina asante kwa taarifa. Tamina alijibu kisha akakata simu .
Siku hiyo alikosa furaha , alikuwa mtu mwenye mawazo sana. Ilipofika jioni alimpigi simu ongea Jimmy wanaongea vizuri pia kuna pesa kidogo jimmy alimtumia kwaajili ya matumizi yake madogo.
Majira ya saa mbili usiku Maria alikuwa anajiandaa alivaa nguo vizuri kwaajili ya kutoka akiwa anataka kutoka Tamina alisimama mbele ya mlango akauliza
" Unaenda wapi saizi?
" Khaaaa Kwani kila safari natakiwa kukuaga?
" Nilitaka kujua.
" Hebu nipishe.
Maria alimsukuma kisha akapiga na kuondoka.
Tamina alihisi kitu akachukua viatu akatoka nje na kuanza kumfuatilia, alimuona anapanda pikipiki nae hakuchelewa alichukua pikipiki na kumwambia dereva.
" Naomba zifuate ile pikipiki , tafadhali usije ukaipoteza.
" Sawa.
Tamina aliwafuatilia mpaka walifika sehemu pikipiki aliyoipandaa Maria ilisimama Maria akashuka.
"Kaka naomba usimame hapa. Tamina alimwambia dereva wa pikipiki aliyokuwa amepanda.
Maria alilipa nauli kisha akasogea karibu na gari lililokuwa lime simama pembeni ya barabara alipoangalia kwa makini alimuona Jimmy akishuka kwenye gari akamkumbatia Maria na kuanza kukiss.
Tamina aliwaangalia huku akiwa kakunja uso
"Samahani kaka naomba unisogeze mpaka pale kwenye lile gari.
" Pale waliposimama wale wapenda nao wawili?
" Ndio.
boda boda aliwasha pikipiki wakasogea mpaka waliposimama.
Jimmy alipomuona Tamina anashuka kwenye pikipiki alishituka akamuachia Maria na kumsukuma nyuma.
" Vipi mbona unataka kuniangusha. Alisema Maria.
" Tamina inamaana ulikuwa unafuatilia?
"Nyamaza sina muda wa kuongea na wewe. Jimmy unanifanyia nini hiki kwani hujui kuwa Maria ni dada yangu?
" Tamina baby....
" Acha unafiki nani baby wako ungejuwa thamani yangu usinge fanya huu uchafu Jimmy.
" Punguza hasira nisikilize.
Tamina alishindwa kudhibiti hasira zake alinyanyua mkono na kumpiga kibao cha shavu.
" Siwezi kukusikiliza shetani wewe alafu na wewe Maria hiki unachokifanya sio sawa sisi ni ndugu.
" Bwana wewe hebu niache yani wewe uko na mwanaume mzuri lakini unambania acha tunaojua kuhendo wanaume tuwasaidie.
Jimmy mpenzi achana na huyu mshamba asiejitambua twende zetu
Maria alimshika mkono na kumvuta Jimmy wakapanga kwenye gari na kumuacha Tamina akilia kwa uchungu hakuamini kama Jimmy anaweza kumfanyia usaliti mkubwa vile tena na dada yake.
Kumbe wakati haya yote yatatokea kulikuwa kuna kaka mmoja alikuwa amekaa kwenye gari akawa anawaangalia . Kitendo cha Tamina kulia kilimuumiza sana alitamani kushuka na kwenda kumbembeleza lakini hakuwa na nafasi nzuri ya kufanya hivyo.
Tamina alienda kupanda pikipiki na kurudi nyumbani kwao huku akiwa bado analia.
Yule kaka wa kwenye gari alimwambia dereva wake.
" Sam hebu ifuate hiyo pikipiki. Alisema Arshan na sam akaanza kuendesha gari kuifuata ile pikipiki.
Tamina alishuka kwenye pikipiki na kuingia ndani kwao , dereva toyo aligeuza pikipiki akawa anaondoka , alipokaribia lilipo gari Arshan alishuka na kumsimamisha
" Mambo vipi.
" Safi
"Samahani huyu dada uliemshusha hapo ndio kwao?
Dereva toyo alimuangalia Arshan kisha akauliza
" Kwani vipi, kuna usalama?
" Usalama upo kwa asilimia mia moja . Alijibu Arshan huku akitoa pesa na kumpatia.
Dereva toyo alipokea na kujibu maswali yote aliyoulizwa.
" Huyu dada namfahamu anaitwa Tamim hapo ndio kwao na kule tulikotoka alikuwa kamfumania dada yake alie zaliwa nae tumbo moja akiwa na mwanaume wake. Yani hii dunia acha tu . Ila Maria kiboko kuranda na wanaume wa rafiki zake kumemkinahi sasa anatamba na mwanaume wa mdogo wake.
" Asante sana kwa maelezo yako.
Arshan alipanda kwenye gari yake akaondoka huku akilini kwake akipanga kuendelea kumfuatilia Tamina shombe shombe wa kichina.
MY POOR BILLIONEA HUSBAND 3
MTUNZI SMILE SHINE
Tamina aliingia ndani kwao alimpita Sasha na mama yake kwa kasi akaelekea chumbani.
" Huyu ana shida gani?
Mama yake alimuuliza Sasha, Sasha alipandisha mabega ishala kama kwamba hana anachojua.
" Analia ujue?
" Ndio analia , sijui ndio kashagombana na huyo mwanaume wake.
" Hebu kamuangalie.
Sasha alinyanyuka alipokuwa kakaa akaelekea kwenye mlango wa chumba cha Tamina alishuka kitasa ili afungue mlango haujufunguka Tamina alikuwa kafunga kwa ndani.
Sasha aligonga huku akiita jina la Tamina.
" Tamina fungua mlango.
" Dada Sasha niache nahitaji kukaa mwenyewe.
" Acha kuziweka roho juu sema kimekupata nini?
" Nenda dada nahitaji muda wa kukaa mwenyewe.
Sasha alirudi sebleni .
" Vipi ?
" Kafunga mpango anataka kukaa mwenyewe.
" Naona wadudu wa kichina wamepanda achana nae akiwa sawa atasema.
Tamina aliendelea kulia kwa uchungu huku akimpasni Maria kwa kumkatisha ndoto zake na kumnyang'anya furaha yake.
Kesho yake kulikucha Maria na Tamina walipishana kama hawajuani na Maria hakuonyesha kujali kabisa .
Jimmy alipiga simu kuomba msamaha lakini Tamina hakujibu bado alihitaji muda.
Aliendelea kuchunguza akabaini bado Jimmy yupo na Maria.
Tamina aliendelea kwenda kazini huku kila siku Arshan akiwa anamfuatilia kwa kificho bila Tamina kujua kama anafuatiliwa.
Siku jioni Tamina akiwa anafunga biashara yake gari ya Jimmy ilisimama mbele ya kibanda chake mara alishuka jimmy akiwa na Maria . Tamina alipowaona moyo wake ulishituka , alisimama akawa anawaangalia jinsi walivyokuwa wakimuangalia.
Hatimae walifika karibu yake Maria akishika mkono wa Jimmy.
Tamina aliwaangalia usoni kisha akasema
" Ni wasaidie nini?
Maria alimuangalia jimmy usoni kisha akasema .
" Baby hebu mwambie.
Jimmy alikaa kimnya kwa muda kisha akavuta pumzi na kushusha kwa nguvu.
" Tamina nimekuja kukwambia uhusiano wangu mimi na wewe umefika mwisho sasa nipo na.....
Kabla jimmy hajamaliza kuongea Tamina alirusha kibao kikamfikia jimmy usoni.
Maria alimsukuma Tamina mpaka Tamina akaanguka chini.
" Wewe kwanini unampiga shemeji yako huna adabu eee..
Maria alitaka kwenda kumpiga lakini jimmy akamzuia.
" Achana nae . Tamina ukweli ni kwamba Maria ni bora kuliko wewe acha niwe shemeji yako na wewe nakuombea upate mwanaume mwema wakienda na nae.
" Wewe shetani kumbuka kuwa niliacha na wanaume wa maana na wenye nia nzuri na mimi pia walikuwepo bora kuliko wewe lakini niliacha na nao kwasababu ya kukupa thamani wewe....
" Ooooh kumbe una bahati basi msahau utapata mwingine.
" Maria nadhani tumemaliza tuondoke.
Alisema Jimmy .
wakati wanaondoka Tamina alimvamia Jimmy akamsaidia mgongoni na kuikana shingo yake.
Kwakuwa Tamina hakuwa na nguvu Jimmy alimuangusha chini na kuanza kumshambulia . Wakati huo huo Arshan alikuwa amefika akaona lile tukio la kushambuliwa kwa Tamina.
Arshan alitahamaki akafungua mlango kwaajili ya kwenda kumsaidia lakini aliishia kushusha mguu mmoja kisha akasita, alimgeukia sam kisha akasema.
" Fanya haraka nenda kamsaidie .
Sam alishuka haraka akakimbia alipofika walipo alimsukuma Jimmy na kumnyanyua Tamina.
" Vipi mbona unanisukuma?
" Ulitaka nifanye nini, kwanini unampiga mwanamke tena hadharani?
" Wewe yana kuhusu nini , kwani nani kwake?
" Haya kuhusu. Kama una hamu ya kugombana njoo ugomvane na mimi mwanaume mwenzio.
Jimmy alimsogelea sam kwaajili ya kugombana kabla hajafunga ngumi tayari ngumi ya Sam ilitua usoni kwa Jimmy mpaka jimmy akainama.
Sam alivua koti lake akatupa chini kisha akiweka tayari kupambana na Jimmy .
Maria alivyoona vile alimsihi jimmy waondoke.
" Mpenzi achana nao hao twende zetu.
Waliondoka wakaenda kupanda kwenye gari huku Sam akiwa anawaangalia .
" Vipi upo sawa? Sam alimuuliza Tamina.
" Nipo sawa asante.
"Unaelekea wapi?
" Naenda nyumbani.
" Ok ngoja nikutafutie usafiri.
" Usijali.
" Acha nisimamie kila kitu .
Ilipita pikipiki Sam alisimamisha na kulipa nauli. Tamina alipanda kwenye pikipiki na kushukuru.
" Asante.
" Karibu.
Pikipiki iliondoka na Sam akarudi kwenye gari.
" Kila kitu kipo sawa.
" Yule mwanaume mshenzi sana hakutakiwa kuishia kumpiga ngumi moja ungemtandika haswa .
" Akirudia wakati mwingine atajuta.
Tmina alifika nyumbani kwao huku akiwa kavimba jicho.
" Tmina mbona hivyo? Mama yake alimuuliza Tamina hakujibu alienda kukaa kwenye kochi huku akiwa kashikilia mbavu zake.
" Una nini binti yangu.
" Maria mama.
" Maria kafanya nini? Sasha na mama yake wakiuliza pamoja.
" Maria na Jimmy wamekuja kunifanyia fujo.
" Jimmy huyu mpenzi wako?
" Ndio Maria alipofahamiana na Jimmy walianzisha uhusiano wa siri nilipogundua Maria akaamua kuweka wazi na kujiletea chuki za chinichini.
" Huu ni ushetani gani anafanya huyo Maria? hajui kama wewe ni mdogo wake , ndugu yake wa damu.
" Maria kazidi sasa amemaliza mabwana wa mashoga zake sasa kahamia kwa mchumba wa ndugu yake.
Sasha alimchukua Tamina akampeleka chumbani huku mama yao akiwa jikoni aliandaa maji kwaajili ya kumkanda sehemu alizotumia .
" Huyu mshenzi atarudi hawezi kumfanyia mwenzie ukatili wa aina hii .
Baada ya siku mbili kupita Maria alirudi nyumbani kwao.
" Shikamoo mama.
" Umetoka wapi?
" Kwa rafiki yangu.
" Kwa rafiki yako siku mbili bila kutoa taarifa.
" Mama mimi sio mtoto ni mtu mzima ni vizuri mkaniacha na maisha yangu .
" Ni kweli umekuwa mpaka roho yako imekuwa kubwa mpaka hautosheki inamchukua mchumba wa ndugu yako.
" Mimi sijamchukua mwanaume wake mwenyewe inaleta Shobo na mimi nikamuelewa sasa kosa langu liko wapi? Alafu Tamina anaroho mbaya tu yeye mwenzetu ana bahati anapata wanaume wa maana sasa kumuachia huyu mmoja yeye akajiweka kwingine kuna tatizo gani.
" Hivi kumbe wewe kichaa unatembelea nyota ya mwenzio. Alisema Sasha.
" Wewe ongea tu hapo na usijiongeze utaishia kuwapata walala hoi.
Mama Tamina alichukua sturi akamrudia bahati Maria aliwahi kukwepa .
" Mshenzi wewe na kama utaendelea na hiyo tabia sikutaki hapa nyumbani kwangu.
" Hata hivyo nitaondoka.
Maria aliingia ndani baada ya dakika chache alitoka na begi lake la nguo.
" Jamani kwaherini .
"Unaenda wapi na mabegi?
"Naenda kuishi kwa Jimmy.
" Wewe mtoto jipe thamani ya maisha yako usijirahisishe hivyo huyo mwanaume huna unasaba nae.
Maria hakusikia maneno ya mama yake alivuta begi lake akaondoka.
" Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Maria ulimwengu utakufunza.
Maria hakujali maneno ya mama yake alifungua mlango na kubamiza kwa nguvu.
MY POOR BILLIONEA HUSBAND 4
MTUNZI SMILE SHINE
Maria hakujali maneno ya mama yake alitoka na begi lake akaenda kupanda kwenye gari ya Jimmy wakaondoka.
" Afadhali niondoke maana hizi kero za humu ndani zingenikondesha nisingekuwa kwa amani.
" Nilijua huwezi kukaa na simba mwenye hasira kali ndio maana nikasema tukaishi wote mpenzi wangu. Kwangu utaenda kupata kula kitu kumbuka nina kazi nzuri na mshahara wangu mnono.
" Najua hilo mpenzi ndio maana Tamina limemuuma sana hili nimemnyang'anya tonge lake.
Baada ya Tamina kuachana na Jimmy alikuwa Bize na biashara zake hakutaka kuanzisha mahusiano mengine japo kuwa wanaume wengi walimfuata kwa nia njema tu lakini hawakufanikiwa bado alikuwa na jeraha moyoni kwake na hakuwa na imani na kiumbe anaeitwa mwanaume hasa alipofikia upande wa mama yake amewataka na hawaishi na baba na yeye kaka kusalitiwa vibaya . Aliamua kuyaweka kando mapenzi.
Siku zilisogea ,Siku moja Arshan alitamani kumuona Tamina kwa karibu akambidi aende kununua ice cream akamkuta Tamina anaongea na mwenzake wakawa nawaongea.
" Unafikiri Asma mimi siwezi kuwa na uhusiano na mwanaume anaejiweza kipato "
" Lakini Hemedi anakupenda na ana mapenzi ya dhati kwako.
" Nimesema sitaki labda nipate mwanaume asiye kuwa na kitu maana huyo atakuwa wa pekee yangu. Si unajua wanawake wa siku hizi hawawataki wanaume wasio kuwa na kitu.
Asma aliona kama utani aliishia kucheka.
" Hebu muhudumie mteja.
Tmina alimuhudumia Arshan baada ya hapo Arshan aliondoka akiwa na jambo lake kichwani.
Baada ya miezi sita kupita Tamina aliamua kuacha kufanya kazi kwenye kibanda cha ice cream alifungua biashara ya mgahawa wa kuuza supu na chapati. Wateja wengi walijaa mgahawani kwake .
Siku moja akiwa anatoka kukusanya hela kwa wateja wake alimkuta kaka mmoja akiwa kasimama mlangoni kwake . Huyo kaka alikuwa kavaa nguo zilizokuwa zimechafuka na mkono wa kulia alikuwa kashika mfuko uliokuwa na chupa za maji.
" Vipi kaka mbona umesimama hapa, karibu ndani uhudumiwe.
Tamina alimkaribisha bila kujali muonekano wake.
" Nilikuwa nina shida na supu lakini hela niliyokuwa nayo haitoshi. Aliongea yule kaka huku alimuonyesha sarafu ya shilingi 500.
Tamina aliachia tabasamu kisha akasema.
" Ingia nitakupatia supu.
Yule kaka aliweka mfuko wake pembeni ya mlango kisha akaingia na kwenda kukaa kwenye meza ya pembeni akisubiri huduma.
Baada ya muda Tamina alienda akiwa na trei iliyokuwa na bakuli la supu pamoja na chapati mbili. Alimletea na kumkaribisha.
" Karibu.
Yule kaka alimuangalia .
" Kula, karibu ule
" Lakini sina hela ya kulipia hivi vyote.
Tamina aliachia tabasamu na yule kaka alikuwa akimuangalia tu usoni .
" Usijali wewe kula. Alisema Tamina kisha akaondoka kwenda kuhudumia wateja wengine waliokuwa wakimuita. Japokuwa alikuwa na wasaidizi lakini watu wengi walipenda huduma yake.
yule kaka aliendelea kunywa lile supu mpaka alipomaliza alisimama na kumfuata Tamina.
" Asante dada nimeshiba .
" Karibu.
" Mmmm naomba ipokee hii hela kesho nikipata hela nyingine nitakuja kulipa deni lililobaki.
" Usijali mimi nimekupa tu.
" Lakini hii ni biashara.
" Najua lakini chapati mbili na bakuli moja ya supu haiwezi kusababisha biashara yangu ikafa au ikayumba. Huyo hela yako weka mfukoni unakunywa hata maji.
" Asante sana dada . Mungu akiongezea pale ilipofunguliwa na aongoze vyema biashara yako.
" Amiiin
Yule kaka alionekana kushukuru sana kisha akaondoka . Tamina akimsindikiza kwa macho huku akijisemea.
" Masikini hawa watu ndio wanaofaa kusaidiwa huenda ndio baraka zenyewe hizi maana amekimbilia na kumuombea dua njema.
Mara kwa mara yule kaka alikuwa akitembelea kwenye mgahawa wa Tamina pia kuna muda alikuwa akimuungisha na hata kumsaidia kazi ya kuchota maji. Walipiga stori , yule kaka alionekana ni mtu mwenye akili sana maana alikuwa akimpa Tamina mbinu za kibiashara kuna muda alimshauri kuweka freza kwaajili ya vinywaji na vitu vingine . Tamina alifuata ushauri wa yule kaka na mambo yake yakawa yanaenda vizuri sana.
Kwa hali hiyo Tamina alitokea kumzomea sana na kutamani kumfahamu zaidi maana siku zote hata jina lake alikuwa halijui alikuwa akamuita kaka .
Siku moja baada ya kumaliza kati yule kijana alikuwa amekaa akiwaangalia wanavyo weka mazingira safi.
Tamina alimaliza akaenda kukaa pembeni yake.
" Unajua siku zote huwa nakuitana kaka silijui jina lako leo ningependa kulifahamu jina lako na kama ikiwezekana nafahamu historia yako kwa ufupi
" Ahaaaaaa mimi naitwa Arshan kwenye huu mji ni mvamizi nipo hapa kwaajili ya kutafuta maisha.
" Kwahiyo huna ndugu kwenye huu mji?
" Wapo ila kila mtu na maisha yake si unajua haya maisha.
" Ooooh pole.
" Kawaida.
" Kwahiyo unaishi wapi?
" Ghetto na washikaji. Ila muda sio mrefu naweza kupata sehemu yangu ya kuishi.
" Ni jambo zuri maana huko kwenye mchanganyiko wa watu kila mtu huwa na tabia yake inaweza kukuletea madhara badae.
" Nimeliona hili ndio maana nimeona nijitoe mapema sana.
Siku hiyo walipiga story mpaka usiku ukaingia .
" Arshan acha niwahi nyumbani Mungu akipenda tutaonana kesho .
" Sawa.
Tamina alichukua pochi yake na kufunga mlango.
Wakiwa wamesimama nje Arshan alimuaga.
" Tamina uwe na usiku mwema na ufike nyumbani salama.
Tamina aliachia tabasamu
" Na wewe pia ars....
" Arshan.
" Jina lako gumu kutamka.
" Ipo siku utakizoea na kila mara utazamaji kulitaja mdomoni kwako.
Tamina alimuangalia
" Aaah ni utani.
Mara dereva wa pikipiki alifika Tamina akapanda, Arshan akampigia mkono. Pikipiki iliondoka ilipofika mbele kidogo Tamina aligeuka nyuma kumuangalia alimuona bado kasimama akiwaangalia wanavyoondoka. Arshan alinyanyua mkono na kumpungia tena.
MY POOR BILLIONEA HUSBAND 5
MTUNZI SMILE SHINE
Siku moja ilikuwa siku ya jumapili Tamina alikuwa haingii kazini ilikuwa ni siku yake ya mapumziko hivyo alitulia nyumbani kufanya kazi zake au kutembelea ndugu jamaa na marafiki.
Jumapili huyo Arshan na Tamina walikubaliana kwenda matembezi .
Walitembelea maeneo ya beach walikaa sehemu wakanywa juice na upepo mwanana wa pwani ukiwauliza huku wakiongea na kupeana moyo kuhusu maisha.
Wakiwa katikati ya maongezi Tamina alizubaa na kuangalia sehemu moja kwa moja. Arshan alimgusa mkononi na kumuuliza
" Vipi Tamina kuna nini?
Tamina hakujibu aliendelea kuangalia huku akionekana kuumia moyoni. Arshan aligeuka kuangalia kule alikuwa anaangalia Tamina ndipo akamuona Maria na Jimmy wakiwa wanacheza kwenye maji mara wabebane mgongoni na kucheza michezo kama wapendanao wanavyofanya
" Tamina .....
" Arshan naomba tuondoke hapa.
" Sawa.
Walinyanyuka na kuondoka lile eneo wakaenda kukaa sehemu nyingine lakini Tamina hakuonekana kuwa sawa, alifungua mkoba wake akatoa pete na kuiangalia. Ilikuwa ni ile pete aliyokuwa kavalishwa na Jimmy.
" Kwanini unahifadhi pete nzuri kwenye mkoba badala ya kuivaa kidole ni kwako?
Aliuliza Arshan akijua wazo ile pete ni pete ya uchumba.
" Kweli ni pete nzuri sana lakini haina thamani kwangu taifa ya kujiongezea machungu kila ninapokuona. shika nenda kauze kwa sonara utapata hela .
Arshan akiupokea ile pete akaiangalia ilionekana niya gharama.
" Inaonekana imetengenezwa kwa madini ya dhahabu na gramu zake ni nyingi kwanini unanipa?
" Nimesema kauze haina maana kwangu.
" Unaonekana ina kukumbusha machungu.
" Ni zaidi ya machungu.
Alisema Tamina kisha akanyanyuka kimnya pia Arshan hakuongea alitulia huku akiwa anaangalia ile pete.
Badae alimuangalia Tamina usoni akaona machozi yakishuka mashabiki kwake
" Tamina kwanini unalia?
" Acha nitoe machozi huenda ikawa nafuu kwangu.
Nilimuacha kila aliyetaka kuwa na mimi nikampa kipaombele nikijua yeye ndio wangu wa maisha, mwanaume sahihi kwangu lakini alinigeuka alinilipa machungu mazito mno , ambayo sikuweza kuyavunilia alimchukua dada yangu wa damu badala yangu yani wamenivunja nguvu ya kupenda sitamani tena kupenda ....
" Hapana usiseme hivyo Tamina kuna watu wanakupenda sana na wanaijua thamani yako . Hata mimi nakupenda sana Tamina natamani unipe nafasi ya kuwa na wewe nikuonyeshe kuwa mapenzi ya kweli yapo .
Tamina akijifuta machozi kisha alimuangalia Arshan jinsi alivyokuwa akiongea kwa hisia yani alikuwa akimaanisha kile alichokuwa anakiongea.
Tamina aliendelea kumkagua Arshan jinsi alivyokuwa na ndevu zisizokuwa na mpangilio hata uvaaji wake ulikuwa bado wa kishamba na maisha ndio kwanza anajitafuta na kazi yake ni kubeba mizigo na kuokota Makopo.
" Tamina najua sifai kuwa mwanaume wako kutokana na muonekano wangu lakini nina kitu ndani yangu inawezekana mimi ndio nikawa furaha yako na kukufanya usahau kila kitu.
Maneno ya Arshan hayakumuingia akilini Tamina .
" Arshan acha niende nikapumzike.
Alisema Tamina huku akinyanyuka na kuondoka akamuacha Arshan akiwa bado kakaa anamuangalia anavyoobdika.
Baada ya Tamina kupotea Arshan alimpigia simu Sam na kumuelekeza sehemu alipo aende akamchukue.
Baada ya dakika kadhaa sam alifika akamchukua .
" Tunaelekea wapi boss?
" Nipeleke nyumbani.
Safari ya kuelekea nyumbani kwa Arshan kwenye jumba la kifahari ilianza .
" Nipe habari zilizojiri siku ya leo. Alisema Arshan huku akionekana kama mtu aliechoka
" Mama yako alikuja kukuangalia kama kawaida yake alianza kuongea kuwa nyumba ipo rafu unatakiwa kupata mwanamke wa kukutunza na kutunza nyumba.
" Oooh achana na hizo habari zinazidi kunichosha.
" Vipi kuhusu Tamina?
" Nimemueleza kuhusu kumuhitaji lakini naona kama ananidharau kutokana na muonekano wangu.
" Kwanini usimfuate ukiwa na uhalisia wako?
" Hapana nitahakikisha Tamina ananikubali hivi nilivyo. Siwezi kukata tamaa kirahisi.
Zilipita siku Arshan akawa hajaonekana mgahawani kwa Tamina. Hiyo hali ilimfanya Tamina ajisikie vibaya. Alihisi Arshan amekasirika baada ya kuona kuwa kamdharau .
Mara kwa mara Tamina alipokuwa ametoka akirudi aliwauliza wahudumu wake.
" Arshan amefika?
" Hapana.
" Ooooh sijui kapatwa na nini ?
" Huenda anaumwa .
" Ningejua anapoishi ningeenda kumuangalia.
" Kwani hajawahi kukwambia anaishi wapi?
" Sijawahi kuona kama kuna umuhimu lakini sasa nahisi kuna umuhimu wa kujua.
Kitendo cha Arshan cha kutokuonekana kulimpa huzuni Tamina alihisi kama kuna kitu kapungukiwa kwani Arshan alikuwa kama mtu anaepa faraja na kumpa ushauri mzuri wa kimaisha hususani biashara yake. Alikumbuka kicheko cha Arshan pamoja na maneno yake ya kichokozi pia alikumbuka maneno ya mwisho walioongea kabla hawajaachana siku ile ya mwisho.
" Arshan inawezekana kweli wewe ndio ukawa faraja yangu? Mbona nakosa furaha baada ya kupoteza na kutokukuona kwa siku chache ? Kwangu imekuwa kama mtihani.
Siku hiyo hiyo ilipofika jioni Arshan alifika mgahawani akiwa kabeba mfuko.
" Habari. Arshan alimsalimia Zena msaidizi wa Tamina.
Zena hakuitika salamu alianza kuita
" Tamina, Tamina......
" Wewe nini unaita kama unanidai?
" Njoo Arshan kaja.
Tamina aliposikia jina la Arshan alitoka haraka kwenda kumuangalia, alipomuona tabasamu kilichanua usoni kwake.
"Karibu Arshan .
" Asante
"ulikuwa wapi siku zote?
" Nilikuwepo sema mambo yalikuwa mengi si unajua ridhiki imekuwa ya shida lazima tukimbizane na kufanya kazi , kumbuka mimi ni mwanaume hapo mbele natakiwa kuwa na familia itakayonitegemea kama kichwa cha familia
Tamina aliachia tabasamu kisha akasema
" Uliniweka kwenye wakati mgumu wewe, kila wakati nilikuwa nachungulia kukuangalia Arshan kama utatokea.
" Pole
"Hebu njoo huku .
Tamina alimshika mkono wakaenda kukaa kwenye kiti.
" Vipi upo sawa?
" Ndio.
" Ulikuwa wapi?
" Nilikuwepo hapa mjini si unajua mambo ya mishemishe.
" Mmmmm sio vizuri nikajua labda una umwa au umerudi kijijini kwenu.
" Nipo sawa na nipo kwenye hili hili jiji, shika huu mzigo wako.
Tamina alipokea mfuko akachungulia ndani akaona ma apple mawili na kijora.
" Japo ni kitu kidogo naomba upokee.
" Asante. Alafu hiki sio kidogo ni kikubwa sana kwangu. Asante sana.
" Asante kwa kushukuru. Hivi umekula
" Nilikula....
" Basi subiri nikuletee chochote ule. Alisema Tamina huku akinyanyuka kwenda kuchukua chakula na Arshan akiwa anatabasamu na kujipa moyo.
" Mwendo utakuwa ni huu huu Tamina lazima aingie kwenye mfumo wangu mama Arshan jiandae kupokea mkwe miezi michache hapo mbele.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote