MY POSSESSIVE CEO

book cover og

Utangulizi

SIKUTEGEMEA KAMA NINGEBEBA MIMBA.

basi mwenzenu niliajiriwa kwenye kampun flan hivi..
Nikafanya kazi kwa siku kadhaa pale bila kumjua ceo wa hio kampun, siku ya siku nikapamiana na kijana mzuri huyo ananukia kama jini..
Aliponigusa tu ghafla mapigo yake ya moyo yakaaanza kwenda kasi, nikajua labda anaumwa kumbe ndio hisia zake zilikuwa zimepanda mno juu yangu...

Nikafanya harakat za kumpeleka hospital bila kujua ndio ceo kwenye kampun ninayo fanya kazi...
Ceo ambae watu walidhan labda anamatatizo ya nguvu kwa sababu hakuwah kuonekana na mwanamke kumbe hakuwa amekutana na mwanamke wake...

Siku ya siku nikaitwa ofisin ndio nakutana na huyo kijana, aliponiona tu ni kama akili yake ilihama na kunifata kisha akaniingilia akiwa kama kachanganyikiwa na baada ya hapo akaniomba msamaha sana na kuniahidi kuwa atawajibuka kwa kila kitu..
Kumbe aliniachia mimba ya mapacha..


Niliacha kazi nikihisi amenidhalilisha kumbe nimemuachia maradhi ya moyo boss wangu, na mimi kaniacha na mimba..

Unajua ni kipi kilichotokea, basi usikose simulizi hii ya kusisimua ya the possesive ceo

MY POSSESSIVE CEO
HUSQER BALTAZAR

EP 1.

Marcus Kwa nini huniekewi mjukuu wangu, nilini utaoa unataka nife ndo uoe sina mjukuu mwingine zaidi Yako, hizi kampuni huwezi kuziedesha bila mke..

Bibi usijali nitalifanyia kazi, soon utapata mpinzani wako, nipe muda kidogo niweke sawa kazi zangu, kampuni ya mahari hapa Tanzania naona inasua sua nataka nisimamishe Kisha akili ikishatulia nitaoa..

Marcus mjukuu wangu timiza hio ahadi Yako nakupa miezi 8, ikiisha bado hujaniletea mkwe wa hii familia ni bola nirudi Canada nikasubili kifo changu kuliko kukaa nawewe hapa ukaniua na pressure...

Bibi maneno Gani tena hayo, nimeshakuelewa nitajitahidi acha niwahi kazini nikakague Nina miaka miwili Sasa nimemkabidi Max kampuni hivyo Leo, napaswa kuwahi..

Marcus aliondoka lakini akiwa ni mwenye mawazo sana, alifika kwenye gari akamkuta rafiki yake kipenzi watoka utotoni William akimsubili, aliingia kwenye gari dereva akatoa gari..

Vipi mwanangu mbona unaonekana kukosa furaha, na leo ni siku muhimu sana kwako tatizo nini?..

Dah Wil rafiki angu bibi anasumbua, analazimisha nioe, Sasa bro kwani kinachokuzuia kuoa ni nini unajua unamuda Sasa sikuoni na dem yeyote uko sawa kweli?..

Wili acha kuwaza ujinga, Kwa muda mrefu niliokaa single, Sasa hivi, naona kabisa mbavu yangu ilitumika kupika supu..

Sina hisia na Kila ninae muona, hivyo ubavu wangu nafikili haupo hapa duniani, wazungu hawanisisimui ata kidogo ata wafanye nini, sijawai hisi chochote juu Yao, Hawa waafrica ata kabla hawajaingia kwenye mchujo wangu Huwa wanafeli, hawafai, nilivyokuwa Canada niliamua kutafuta muafrica Kwa njia ya mtandao aisee hawa wadada wa Africa, wafundishwe kutafuta pesa zao na umuhimu wa upendo hawa hawapendi mtu ni pesa..

Yani uko kwenye stage ya urafiki tayari Kodi yake imeisha, mala camera ya simu yake Yani ni matatizo kibao hata wiki hammalizi sio mmoja sio wawili bro ni zaidi ya kumi wao kwenye mapenzi wanawaza kuhudumiwa tu matatizo Yao, sitaweza kuishi na mtu wa aina hio kamwe inamaana huyo hajanipenda kapenda vitu vyangu..

Duh bro kweli hili nitatizo na Kwa waafrica ni tatizo zaidi, lakini itakulazimu uoe bro mimi mwenyewe nyumbani kumewaka na Mwajuma ananiumiza kichwa haeleweki ni kama ulivyosema, nafkiri hata Mimi Natakiwa kufanya chagua jingine...

Umeona mwanangu awa wanawake sio ogopa mwanamke anatokwa damu Kwa siku 2,3,4,5 na hafi bro sio, Mimi nitamuolea bibi sio Mimi, nakuapia kabisa hisia zangu hazipo hata mwanamke aniguse sishtuki..

Marcus sasa hilo ni tatizo huenda unashida ya kiafya bro, mwanaume kamili huwezi ukaguswa na mwanamke yuko utupu utoke salama, Wil i rafiki yangu unamawazo mafupi sana, Mimi sina tatizo lolote ila tu ubavu wangu kwenye hii Dunia haupo na nyeti zangu ziliubwa Kwa ajili ya mtu mmoja tu naijua nafasi yangu ndio maana acha kuniwazia ujinga..

Boss naweza tia neno( dereva aliuliza kwa uoga kwasababu Marcus ni mkali huwa hacheki ovyo mtu pekee anaecheka nae ni Wili na bibi yake basi wengine wote ni mwendo wa amri)..

Wili aliamua kumruhusu lakini Marcus alikuwa kimya tu, dereva akasema boss hujapata mtu mwenye udhaifu wako lakini lazima utampata ata Mimi niliwahi kuwa kama wewe na sikuwa mgonjwa ila uwe makini ukishazama nakuapia hutoboi boss yaani unaweza changanyikiwa kabisa huu muda ambao hujampata nakushauli uanze kupiga dua kumuombea huko aliko awe na akili nzuli na akija awe ametulia na mwerevu, usisubili aje aanze kukuliza..

Marcus alimtizama dereva wake Kisha akajibu, kaka Mark hilo kwangu halitokaa litokee kamwe katika hii Dunia, nakuapia mbele ya William, endapo nitapenda nikawa zoba hivyo unavyosema, nitakukabidhi nyumba, gari na biashara ya ml 100, walifunga mazungumzo Kwa kuwekeana huo mkataba mgumu...

Upande mwingine huku, Mimi Gemima yatima nisie na wazazi, nimelelewa kituo Cha yatima Kwa Sasa najitegemea nimeajiliwa katika kampuni ya (*MARHARABU MOTORS COMPONY* ) siishi mwenyewe naishi na yatima mwenzangu, Chaupole Veneranda, nilikuwa njiani nawahi kazini kwani Leo Kuna ujio wa C.E.O wa kampuni yetu, binafsi simjui namsikia tu nina miezi nane toka niajiliwe, nilifika kazini nikakuta watu wako HEI HEI roho juuu juu..

Niliwasalimia nakuwauliza vipi nimecherewa? Walisema hapana, James alijibu,nikatulia huku napanga ofc yangu vizuli,Tina alikuja huyu ni mfanyakazi mwenzangu,
G tuliza hizo bia zako huyu boss hapendi kelele wala uchafu, nimkali hivyo kuwa makini, nilishukuru Kwa kunipa picha ya huyo C.E.O...

Itaendelea..🔥

MY POSSESSIVE CEO
HUSQER BALTAZAR

EP 2.

Nilipanga vitu vyangu na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, CEO Marcus alifika akiwa na mwenzake William, waliingia muda huyo mimi nilikuwa zangu nimeenda kunywa kahawa kwanza, yaani nina shida na njaa ya asubuhi hasa saa mbili nisipokunywa kahawa ama chai sitoboi, yaani nitaumwa tumbo mpaka nikome sikujua kama CEO kashafika…

Nilimaliza nikaludi, nakutana na ukimya mkubwa, sikujali nikaamua namimi nikae kimya, huwa naishi kulinganya na mazingira niliendelea na kazi, zangu, nilipata tu taarifa za chini chini CEO leo yuko na wawekezaji na ma Hr wakampuni, sisi zamu yetu ni kesho..

Nikajiambia bola sijui ingekuwaje, make nilitoka ilivyofika mchana kulikuwa na kaubaridi fulani hivi muda wa kula nikatoka kwenda kupiga kwanza kahawa ndo nile huwa nakuja na chakula changu kabisa, chakula cha kampuni sijawai kukielewa..

Nikiwa namwendo wangu speed 150 za miguu , nikagongana na kaka mmoja hivi dah mzuri huyo chotara limepanda hewani ila nikiwanamshangaa, ikapita pikipiki Iko les nilikoswakoswa kugongwa isingekuwa huyo kaka kunivutia kwake, nilimshukuru huku nagomba yani viumbe wengine, sijui wakoje yaani hapa leo historia yangu ingekuwa fupi jamani dah, yaani ni alizaliwa akatengeneza kahawa akafa..

Yule kaka alicheka nilivyokuwa naongea, japo sio kwa kutoa sauti ni just smile tu, na kaharifu kake sasa duu nikaona apa hii harufu nataka, nikaamua kumuuliza, samahani kaka inanukia vizuli unaweza kunipa code ya ulichopulizia bila kusahau bei plz🙏, nikaweka na mikono mbele..

Alinijibu ni carmina perfume, inauzwa ml 5, heee kaka acha tu usiendelee, kumbe unaweza kutana na mtu ananukia utajili wako tena ambao ni ndoto yako 🤔, wee kaka uliwezaje uwiii eeee mimi siwezi nitakufa napresure yaani nitoe ml 5 napenda kunukia vizuri ila apo kwenye ml Tano hapana yaani apo ni nanunua kiwanja na msingi wa nyumba mpaka madisha..

Huyu kaka ata hakujibu chochote nilimuaga kuondoka, ila nikateleza tena ikabidi anidaake ila nikama alikuwa na tatizo nilikuwa jilani kabisa na mapigo yake ya moyo ni yalikuwa speed kama mtu anataka kukata roho, Sasa ni inakataa kutoka nikaogopa nikajua Kisha nikamwambia kaka kimbia hospital haraka unaumwa sana, nimesikia moyo wako unavutana na Israel wahi usijekufa na uzuri wako yaani nilikuwa naongea Kwa kumaanisha kabisa niko serious kabisa namsihi…

Itaendelea..🔥
MY POSSESSIVE CEO*


HUSQER BALTAZAR

EP 3.

Mimi napambana kumsihi yeye kaganda kunishangaa Mimi, nikajua kabisa apa Israel anataka kufanya yake, nikaanza kuomba, shindwa shetani, Mungu muangalie mtoto wako Israel anamuwinda, muokoe Leo usimchukue mbona Israel ananionea sana Mimi, Kila mtu anaenijali anamchukua amewachukua mama na baba hatosheki tu uyu kaka kunisaidia tu kashaanza kuivuta roho yake Mungu sikubaki nakwambia Mungu wangu Leo na Mimi unisikilize sio tu Kila siku unaemsikiliza Israel, Yani nilikuwa serious mpaka machozi yananitoka...

Watu walianza kujaa wanashangaa, ikabidi yule kaka anitoa hapo haraka lakini sikukoma nikamwambia twende hospital, akaamua kunisikiliza huenda Kuna jambo kweli nimeona, tukapanda tax namuwahisha mgonjwa hospital...

Kufika hospital Niko waru waru speed kubwa, wakampokea nakuanza kumfanyia vipimo Mimi ni ninaomba hatari, walicheka wanacheka wengine wananihurumia mpaka wanalia, vipimo vikatoka hata tatizo lolote hata malalia hana...

Ikabidi watuchukue maelezo nilichokisikia, kwanza wakaanza kucheka nakumtuzama huyo kaka , nayeye akahisi kitu akaona aibu, akaomba radhi Kwa usumbufu wangu Kisha akanishika mkono kunitoa hospital, lakini alivyonishika akawa kama kashtuka, akaniachia haraka..

Nakuniambia niwahi anirudushe alikonitoa, kaacha kazi nyingi sana tulipanda tax ndo nikakumbuka kazini huko dah nikaanza kulia, akaniambia unashida Gani we binti? Wewe kaka hujui tu apa nawaza Kwa ajili ya kukuokoa Israel akuache naweza kupoteza kazi na Leo kazini Kuna CEO nasikia ni kauzu, hacheki n awowote ata mtu akicheka tu kazini Hana kazi na hapo ni kucheka tu Mimi Sasa nimeondoka lunch mpaka muda huu sijui itakuwaje we Mungu nisaidie Mimi wafunge ufahamu maboss wote na wafanyakazi wasiniwazie ata kidogo, nisikukuzwe kazi wahisi tu nilikuwepo, nilianza maombi yangu dereva mbavu hana...

Tulifika tulipokutania nikashuka nikampa dereva nauli, nakukimbia kuwahi kazini hata sikuaga, huyo mpaka ofcn, nilifika nikawa napita Kwa kujificha mpaka ofcn kwangu, niliwakuta wenzangu wakaniuliza nilikuwa wapi, nikawaambia Leo naharisha sana..

Walinipa pole nakuniambia niombe ruhusa, ngoja nisikilizie likizidi nitaenda tukiwa pale ghafra nikashangaa watu wote kimya, nikaamua kuchunguza nini tatizo kucheki naona mtu anaishilizia sikumuona vizuli afu harufu ni kama naijui ila nikajipiga kichwa Gemima huyo mtu sio wa humu, umu hakuna wakununua perfume ya million 5, nikwasababu ulikuwa nae kakushika perfume imebaki kwako..

Mr. CEO Marcus aliingia ofcn kwake akiwa anahisi joto ilihali hata joto hakuna kuna baridi, alivuta mkoti wake akaanza kuregeza na tai kabisa, wakati huo rafiki yake William alikuwa ofcn, alimuuliza Marcus ulikuwa wapi ujue tuna kazi kubwa sana..

Wili rafiki yangu, yaliyonikuta sitamani ata kuelezea, na sielewi ni kama kuna tatizo, ilibidi Mr. Marcus amsimulie mkasa mzima rafiki ake, Will alihamaki na kucheka sana, bro uyo demu akili zimo kweli ha ha ha lakini subili umesimama moyo wangu ulishtuka na kitu ilisimama inamaana amekuvutia..

Wili rafiki angu acha kunichanganya ilihali nimeshachanganyikiwa tayari,hii hali haaijawai kujitokeza Kwa miakaa Sasa hata Mimi sielewi nahitaji kukaa mbali sana na huyo mwanamke nikama anashort, alielezea Marcus huku akihisi msisimko usio wa kawaida mwilini mwake Kila akikumbuka, hasa alivyonishika mwili unasisimka kwa hisia kalli..

Itaendelea..🔥

MY POSSESSIVE CEO*

HUSQER BALTAZAR

EP 4.

Alikimbia kunawa, lakini haikusaidia kitu, alijikuta kazi haziendi ni kuniwaza tu, Mimi mwenzie ata habari sikuwa nayo, Mr william alimuonea huruma mwenzake, Marc rafiki yangu, nahisi tayali umeipata ubavu wako hujawai kuteseka hivi tuka nikujue hata Kwa Viviani, hukuwa na hisia kiasi hiki...

Wili ebu acha mambo yakijinga, mi sijampenda nikwakuwa nina muda tu na haya mambo huenda ndio maana, nilishakwambia moyo wakumpenda kiumbe wa kuishi nae sina,"Marco rafiki yangu, hujajielewa tu bado lakini niamini Mimi bro umeshazama mzima mzima, na ninauhakika ni swala la muda tu, utamtafuta uyo binti kama mvua ya mafuriko, nikwamba hutaki kukubaliana naukweli kuwa umepata kiboko wa hisia zako niamini bro..

Wili naomba tuachane na haya mambo tufanye kazi, " Mimi sina tatizo bro wewe ndo hata kama nitanyamaza hunauwezo wakufanya kazi, nikushauri tu uende ukamtafute, kabla hujampoteza uanze kunisumbua" ...

Bro tupige kazi, unavyonifikilia nitofauti kabisa, waliendelea kupitia kazi na taarifa muhimu za kampuni, lakini Mr Marcus akili yote ilikuwa inarudi kwangu tu alishindwa kufanya kazi akabaki kakaa tu, Will aliamua kumtizama tu Kwa sababu alishatambua tatizo lake..

Mr. Marcus aliamua kuondoka alifika nyumbani kwanza akatulize akili, Will alibaki kupiga kazi, muda huo Mimi nilikuwa bze na kazi sikutaka nilaze kazi..

Ata Mr. CEO anaondoka Mimi sikuwa na habari kabisa, akili yangu yote ilikuwa kwenye kazi, Marcus alifika nyumbani akaingia moja Kwa moja chumbani kwake, hata bibi yake alipomsemesha hakusikia, wala kutambua kama alikuwepo sebulen..

Bibi Marcus alipata hofu, akaamua kumpigia William kwanza kujua kama Kuna tatizo Kwa mjukuu wake, haloo bibi shikamoo, marhaba we mwanaume, uyu mwenzio anashida gani usinifiche kaka hapa simuelewi, " usijali mchumba uyo hana tatizo kubwa atakuwa sawa mwache tu alale kwanza, wewe usinitanie naomba ufunguke hakuna jambo dogo hapa..

Unamjua Marcus sio mtu wakuteteleshwa na jambo kiulahisi kiasi kwamba, ananipita Mimi sebulen namuita haitiki naomba unipe maelezo kamili kabla sijabadilika, naona nyie wanaume mnataka kuniua mapema kabisa, Kuoa hamtaki ivi mnataka nini nyie au mnapakuana Mimi sijui?..

Heee bibi sisi kweli niwakufanya hivyo! Hapana bibi, huyo Kuna mwanamke anapita pita kichwani sasa yeye hataki kuamini kama kampenda , anamuwaza ila hataki kukubali kama kampenda ni hivyo tu bibi, kashindwa kufanya kazi akaona aje kwanza kupumzika..

Kiriiririiiiii, Sasa jambo la heri kama hilo nilakunificha sasa fanya hivi mme wangu, nipe no za huyo binti ata ikiwezekana niunganishe nae tumsaidie mwenzako, " bibi Mimi sijui ata no hajachukua wamekutana tu leo alitoka kula mimi nilibaki ofcn..

We nae sasa nakupa hio kazi unisaidie kuipata, " sawa bibi nimekuelewa" bibi alikata simu huku akiwa na tabasamu la kipekee kabisa, aliamua kumuandalia chakula mjukuu wake mwenyewe , mfanyakazi akimsihi asifanye hivyo lakini alikataa nakuanza kupika, bibi alikuwa fundi wa jiko atari...

Alimaliza akaandaa nakuamua kumpelekea mjukuu wake yeye mwenyewe, aligonga mpaka akatumia sauti kubwa sana, ndio CEO Marcus kushtuka akaenda kufungua, haaa bibi ungeacha tu ningeshuka kuja kula..

Hapana mjukuu wangu, nimekuletea juice hii ikusaidie kutuliza akili na hiki chakula nitakulisha mwenyewe, leo umenifurahisha sana, bibi nimekufurahisha na nini mbona sijui, bibi alikuwa na furaha kiasi kwamba alimuambukiza furaha CEO Marcus...

Hujui tu kiasi gani nilikuwa na mashaka juu yako, nilijua haisimami kabisa, nilikuwa nahofu uzao wangu ndio basi tena yani leo umenifurahisha sana, Marcus alivuta picha akajua tu Wili kamsaliti..

Bibi usinambie uyo bwana ako ndo kakujaza maneno ya uongo, wewe usimuite mme wangu muongo yule ni bonge la mwanaume hana sifa za kike nimemtisha, akaamua kusema ukweli, ehee ebu niambie kwanza huyo mke mwenzangu unamleta lini? Na vipi unaweza kunipa no zake..

Bibi jamani kumbe kunimbembeleza kote nachakula kizuli na juice unalako jambo? Bibi nakumbuka sana enzi za Babu ndo tabia Yako ukiwa na jambo lako unambembeleza na mbwembwe kibao nakumbuka ilikuwa ikifika mwisho wa mwezi tarehe zikikaribia tu inakuwa na mahaba ya kihindi ukishapewa tu kamshahala, uyo nakujua bibi hii tabia naichukia sana sitaki mwanamke wangu eti awe na upendo wa mwisho wa mwezi, aisee nitamuacha mchana kweupe sitasikiliza mtu kabisa..

Mjukuu wangu husahau tu jamani, sikuwa hivyo ilivyokuwa unawaza wewe, ebu usinipotezee pont nipe no, bibi Mimi no sina sikutarajia kama nitakuja kukutana nae tena, yaani wewe sijui ni mwanaume gani, Yani unachanganyikiwa mpaka hosptal unapelekwa unashindwa kujiongeza, kuonesha uanaume wako..

Yani we ni mwanaume suruali tu, ata hio mashine yako, huenda haifanyi kazi vizuli, ndio maaana unamuogopa mwanamke, dume Zima ataujasili wakuchukua no Kwa binti unakosa sasa kumtia wewe kweli utaweza au ata kuomba tu mechi huwezi..

Itaendelea..🔥



MY POSSESSIVE CEO*
HUSQER BALTAZAR

EP 5.

Bibi nimekuelewa, sitaki ugomvi na wewe, kichwa changu hakiko sawa nawewe umeamua kuja kukimaliza kabisa dah!..

Ndo maana sitaki kuoa yaani wewe tu nachoka, nikiongeza mwingine huku ndani kutakalika kweli? Mtu muda wote ni kuongea na kusikilizwa, aya bibi umesomeka sasa nikija kukunyoshea mtu umu ndani mwako, nisisikie kelele tena tafadhali..

Ukitaka kelele ziishe wewe niletee mke mwenzangu tu, utaona kama nitakupigia kelele ata kidogo, sawa bibi nitamleta basi naomba nilishe nilale kichwa kinaniuma, bibi alimlisha mjukuu wake huku wanapiga story zingine kama sio wao waliokuwa wanazozana..

Kuingilia ugomvi wa Hawa watu ni kujichanganya tu, upande wangu, tayari nilikuwa nyumbani nimechoka kweli nilipika Kwa sababu ilikuwa zamu yangu, wakati tunakula nilianza kumsimulia kisa cha Leo , kilichonitokea..

Nilimshukuru Mungu Kwa kusikiliza maombi yangu, sikutafutwa kazini na hakuna aliejua sikuwa eneo la kampuni, niliamua kulala mapema Ili niwahi kazini kwasababu kesho CEO anakisa na sisi..

Upande wa Marco alijikuta ananiwaza kupita kiasi, alikosa raha kabisa, alibaini kweli kashakamatika anapaswa kuwa makini sana Ili asiumie zaidi aliamua atanikwepa Ili kuepuka kujirudia akilini mwake nakutengeneza udhaifu zaidi..

Ama aoe mke wa mkataba haraka, Ili kukata ukaribu na Mimi japo hajui ninaishi wapi na hata kazini kwangu hapajui bila kujua Mimi ni mfanya kazi wake, hakutaka kuwa na udhaifu hasa udhaifu wa mke..

Alilala kwa tabu sana alijikuta ananivutia hisia sana, kulikucha mapema niliwahi kujiandaa mwenzenu Nina kauzuli kaumbo, na rangi black beuty ya kung’aa , rangi fulani hivi adimu, mfupi kiasi, Nina titi la size ya kati sio dogo Wala kubwa na limesimama haswaa, in short namba 8 inajichora vizuli mno sura sio sana ila umbo aaah ni hatali napenda kuvaa nguo ndefu na zakuficha umbo langu..

Ila Leo niliamua kujiachia , nilivaa kigauni fulani chakushepu kifupi Cha gotini, nywere nikibana tu zilikuwa ndefu na safi,nilijipangilia vyema na kasplay kangu kakupima nilitengeneza mchanganyo fulani hivi wa harufu ya matunda na maua eee nilikuwa nanukia Hadi Raha harufu tamu afu imepoa sio Ile ya kukera..

Nilitoka nakwenda kazini, upande wa Marco aliamka akajiandaa japo Kwa mbinde, Will alijua Hali ya mwenzake hivyo aliwahi kuja kumpa saport, afadhali umekuja Will sijielewi kabisa sijui nifanye nini..

Marcus tatizo lako ndo Hilo bro, hujui kupenda kabisa wakati mwingine Huwa naona ni bola ukawa single tu hapa hata aujamjua, umeshachanganyikiwa kiasi hiki nashauli Leo baada ya kikao na wafanyakazi wako..

Tumtafute huyo binti, tukimpata uondoke kwanza urudi Canada nimchunguze, Kama nisalama basi ukubali kumuoa kama sio salama uugulie huko huko utapona halaka, kuliko hapa unamuona hutoweza kuchomoka Kwa Hali Yako bro huwezi, umeshazama bila kutafakali..

Wili sio Mimi nilie amua ni moyo bro, Mimi pia sitaki Niko tayali Kwa wazo lako, kama umeafikiana na wazo langu naomba utulize akili, tukamalizane nakikao ukamtafute bila shaka yale maeneo kutakuwa Kuna mtu anaemjua lazima..

Sawa bro twende nimeshajiandaa, walitoka na kuja kazini, walifika na kukuta wafanyakazi wote tuko chumba Cha mkutano, waliingia nilikuwa bze naandika kitu nakuja kupiga jicho hivi kusalimia, nikahamaki..

Nikapata ata kiwewe chakusalimia, sio Mimi tu, hata yeye alipata kamshangao ila will alikuwa karibu na alimsaidia sana kutokujulikana, Kwa mshangao wake, nilikaa nikiwa na hofu nawaza inamaana huyu ndo CEO? Kwa hiyo Jana🤔, maombi yangu nilikuwa naomba kwasauti jamani Leo Mimi nimekwisha ama yeye nimwakilishi tu huyo mwingine ndo CEO…

Nilijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe, meneja Max, alitutambulisha CEO Marcus na msaidizi wake William , aisee nilichoka, na jamaaa alikuwa kavu kavu ata kunitizama hakuna, kikao kiliisha na tukawa tunatoka wakati natoka niliitwa jina laangu na Mr William akiomba nipeleke kahawa mbili ofce ya CEO..

Niliogopa nikamua kufanya haraka haraka nikaandaa, kimbembe sijui hao ninaowapelekea , wanatumia aina Gani ya kahawa, nikaona nisiumize kichwa ninawapelekea ninyotumia Mimi..

Nilipeleka wakanikaribisha William alitoka kama anaongea na simu, niliweka kahawa zote mezani nikamkatibisha CEO karibu kahawa,alikuwa kama kazubaa fulani hivi nikaamua kuondoka, wakati natoka hivi jamaa anaspeed sijawai ona kabla sijaufikia mlango akawa kafika, akaufunga kabisa…

Itaendelea…🔥


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote