Follow Channel

MY TAQUILA

book cover og

Utangulizi

MY TAQUILA 1
Penzi la nurse na mwanajeshi
HUSQER BALTAZAR
Naitwa agness ni nurse karibu na kambi ya jeshi ya makutupora jijini Dodoma, ila hii hospital ninayofanya kazi haipo kambini nan i hospital binafsi sio hospital ya jeshi..

Siku moja nikiwa kazini, siku hio nilikuwa nina zamu ya usiku, nikiwa natibia wagonjwa, mara akaingia mwanaume ambae alikuwa anachechemea na mwili wake ulikuwa unavuja damu maeneo ya pemben na bega, alikuwa kajazia, ukimuangalia kwa haraka haraka unaweza dhani ni wale wanaoshiriki mashindano ya ndondi, au ngumi, nilimfata kwenye mlango wa kuingilia kisha nikamuomba nimsaidie kuingia ndani..

Kweli nikampeleka mpaka kwenye chumba kimoja cha wagonjwa kisha nikaanza kumpatia huduma ya kwanza, alikuwa ananiangalia sana, kisha akaniuliza “ unaitwa nani?..

“ nadhani afya yako ni muhimu zaidi kuliko jina langu, ukikaa sawa tutaongea, nikajibu, akatabasamu kisha akasema sawa…

Basi nikawa namtibu pale na wakati wote alikuwa kimya ananiangalia, nimemaliza nikamchoma sindano ya usingizi, maana niliamini kama akiamka huenda maumivu yakapungua, maana alikuwa na maumivu makali sana, ila hakuwa ananionesha, nikajua anavumilia tu kwakuwa yeye ni mwanaume…

Amekuja kuamka asubuh, na wakati huo zamu yangu ilikuwa imeshaisha na alikuwa anatakiwa kuingia muuguzi mwingine, nikashangaa naitwa na mkurugenzi wa hospital na kuniambia kuwa kuna kazi ya muda na ataongeza pesa kwangu hivyo kama sitajali basi nimuhudumie mgonjwa flani mpaka atakapo kaa sawa…

Nikaomba hata nikajimwagie maji kwanza na kupata chakula cha asubuhi ndio nije kuzungumza nae, maana nilikuwa nahisi uchovu wa hali ya juu, na Yule boss wangu hakubisha kabisa…

Nikaingia pale pale hospital nikaoga kisha nikapata chai na kwenda kumsikiliza nashangaa napelekwa kwenye chumba cha Yule mgonjwa ambae nilimpokea jana yake usiku, alikuwa na hali mbaya maana misuli ilianza kukaza, hivyo akawa anasikia maumivu ya ajabu, ila aliponiona akatabasamu kisha akasema “ karibu sana my Taquila..

Hakuna ambae alielewa kuhusu hio my tequila maana mimi naitwa agness na Yule boss wangu alikuwa ni mwanaume, tukajua labda maumivu yanamchanganya hivyo tukampuuza kama wauguzi tu, basi nikaambiwa kuanzia siku hio kazi yangu itakuwa ni moja tu, ambayo ni kumuhudumia huyo mwanaume…

Sikukataa, maana nilihisi kama majukumu yangu yanaweza kuanza kupungua, maana kuhudumia mtu mmoja ni rahisi kuliko kufanya kazi kwa watu wote ambao wanaingia na kutoka pale hospital..
Kwakuwa nilikuwa zamu ya usiku, nilikuwa nimechoka sana, nikaomba nikapumzike, Yule mwanaume alijua kabisa kuwa nimechoka, akaniangalia kisha akasema “ njoo ulale hapa…

Alikuwa anamaanisha kuwa nikalale kwenye kitanda chake, nikashangaa huyu mwanaume vipi, yaan mimi muuguzi nikalale kwenye kitanda cha wagonjwa, akasimama na drip yake mkononi akaanza kunigfata, kisha akasema kwa sauti ya ukali na kusema “utalala au nikufanye ulale…
Sikutaka hata kumjibu nikataka kuondoka, sijui hata alinigusa wapi nikashangaa napitiwa na usingizi, akanikokota kwa tabu kisha akanilaza kitandani, nimekuja kuamka kulikuwa kama jioni, na pembeni yangu kulikuwa na meza ile ya wagonjwa ilikuwa ina mahotpot na chupa ya sharubati ya azam…

“ umeamka? Akauliza kana kwamba anataka kunipiga maana aliuza kwa sauti ya amri sana..
Sikumjibu hata nikaanza kuamka na kumtaka alale na kumuambia sisi wauguzi haturuhusiwi kulala kwenye kitanda cha mgonjwa, akaniangalia akasema “ kama unaona kulala kwenye kitanda changu acha kazi, ila hakikishA unaacha kazi siku nitakayoondoka hapa, sipendi kupangiwa na mwanamke mimi………….
NAKUJA


MY TAQUILA 2
HUSQER BALTAZAR

“chakula hicho hapo, utakula mwenyewe au nifanye namna ule? Akauliza..
Sikutaka kubishana nae hata, maana mara ya kwanza ilikuwa ni kulala nikawa najivuta vuta, nikashangaa nalazwa, hivyo sikutaka tena nilishwe, nikakaa nikaanza kula, maana pia nilikuwa nasikia njaa balaa..

Ilikuwa ni ndizi nyama, na sijui hata alijuaje kama napendaga ndizi, nikala pale na wakati wote alikuwa ananiangalia tu, ila kama mnavyojua wanawake tulivyo, sikula sana, nikashangaa ananiambia kuwa “ kama ndio unakula kidogo hivyo nikianza kufanya ile shughuli na wewe utaweza kuhimili kasi yangu wewe, embu kula mtoto wetu akae kwenye tumbo lenye mafuta asije akafa kwenye baridi kwa sababu ya kukaa kwenye mwili wenye mifupa mitupu..
“ mimi nimeshiba, nikajibu, hakutaka kubishana na mimi, akaja kitandani, alipofika mimi nikasimama, maana sikutaka kukaa nae….

Kuna muda sasa nikawa nataka kumchoma sindano ya maumivu, nikamuambia nataka kukuchoma sindano naomba uamke, maana alikuwa ana sindano za masaa..
Akatabasamu kisha akasema njoo mrembo..
Sikutaka hata kubishana nae, nikaenda kumchoma sindano, ila wakati nataka kuondoka nikashangaa kanivuta nikamuangukia kifuani, alafu akanikumbatia kwa nguvu na kusema “ unaitwa nani tequila wangu…

“ wewe una shida gani na mimi, mimi siitwi tequila, kwanini unaniita hilo jina kila ukiniona…
“ najua hauitwi tequila, ila mimi ni mlevi na sina uhakika kama unapenda wanaume walevi na kinywaji ninachokipenda zaidi ni Taquila mamaa ndio maana nakuita hivyo maana nakupenda…

Niliposikia maneno yake nilitoa macho kama fundi saa, anawezaje kunipenda mtu kama mimi, maana kwanza hakunivutia hata kidogo, na kiukweli nilikuwa namuona kama mwizi vile au jambazi, hivyo sikuwa nataka kabisa mazoea nae…

Akawa ananisumbua na kila nikimuangalia ananikonyeza, na kila nikimsogelea kumpaka dawa ananivuta kisha ananibusu na kuniambia kuwa “ nakupenda sana my tequila…

Mpaka wakati huo sikuwa najua hata ni mtu gani na anafanya kazi gani, maana sikutaka hata kumuuliza, iola nikawa nashangaa namna ambavyo boss na watu wa kubwa wa kwenye hio hospital namna ambavyo wanamnyenyekea sana, ila cha kushangaza, nikawa nashangaa kama kila nikiwa narudi nyumban kama kuna mtu ananifuatilia, maana ukiwa unafuatiliwa na mtu ni lazima uhisi, ila sikuwah kumjua huyo anaenifuatilia ni nani na kwanini anafanya hivyo…

Kuna siku kabisa nikahisi mtu nyuma yangu nilipogeuka nikashangaa naona kivuli nikapotelea kwenye kona ya nyumba ambayo ilikuwa karibu na hapo nilipokuwa. Sio siri nilitoka mbio sio mchezo, nikajua labda nafuatiliwa na vibaka, au wezi, na nikawa nikiingia ndani nafunga mlango na nasogeza mpaka ndoo mlangoni maana mara kwa mara nilikuwa nahisi kama kuna mtu anataka kunidhuru tu, kumbe ni mwamba aliweka watu wake ambao walikuwa wanatakiwa kuhakikisha nafika nyumbani salama, na mpaka muda huo sikuwa namjua hata anaitwa nani, na sikuwa na huo muda wa kumuuliza jina, maana nilimchukulia kama mgonjwa na kitu kinachonihusu kwake ni kumpa matibabu, ila maisha yake hayanihusu hata kidogo…….

Nikaanza kumfanyia makusudi sasa, maana sikuwa nataka kabisa mazoea nae, kwanza simjui na sikuwa nataka kabisa kujua chochote kile anachokisema, na kikubwa zaidi nilikuwa na mwanaume wangu, sikuwa naweza kumuacha kwa sababu yake kabisa…

Nikaanza kumzidishia dozi, hasa hasa za usingizi, maana sikuwa nataka anisumbue akawa analala mpaka basi, yaan hata dawa nikawa namchoma usingizini, maana dawa zake nyingi ni sindano..

Sasa nilimchoma siku ya kwanza, siku ya pili akashtuka, ile na nataka kumchoma tu akanishika mkono kisha akanipa sindano nyingine na kusema “ hio ulioweka nina uhakika umeweka dawa gram 1000 na mimi natumia 500, sasa kwakuwa unataka kuniua chukua hii ina gram 2000, yaan ukinichoma nakufa kabisa…

Alikuwa anaongea akiwa amekaza sura, nikaona hapa nimeshakutwa, nikabadilisha sindano na kusema “ sio hivyo umenielewa vibaya, nikashangaa anatabasamu kisha akasema “ una makusudi lakin hauwezi kuniua mimi bana, maana ninauhakika lazima utanipenda taratibu…

Sikumjibu, nikamchoma sindano zake, na akawa anatakiwa kuruhusiwa siku hio, sikuwa najua kama ni mwanajeshi, ingawa hio hospital kuanzia amekuja naona ona wanajeshi wanazagaa zagaa nikajua wana mambo yao tu, hivyo sikuwa nataka kufatiliza jambo lolote lile…

Basi kuna wakati nilikuwa nataka kumuandaa aondoke, wakati nataka kuingia nikassikia sauti kama inatoa amri, ila sikusikia alikuwa anasema nini, kisha nikasikia mwingine anasema “ sawa kamanda tutafanya kama unavyotaka…..

Mara nikasikia anasema “ mpishe wife nataka kuongea nae, kisha nikashangaa mwanaume wa miraba minne anatoka akiwa amevalia magwanda ya jeshi, kisha akanambia “shemu ingia ndani mwamba anakusubiri..

Nikatoa macho huyo, maana nilikuwa nadhani mara ya kwanza alikuwa anasema kama utani, ila mpaka wenzake wananiita shemu nikaona kama mambo yameanza kuwa serious sasa, nikaingia ndani nikawa kimya ila yeye akawa ananiangalia tu, nikafanya ya kufanya, kisha nikaenda kumuondolea drip maana alikuwa nayo bado mkononi kisha akanambia “ naondoka wife ila nitakuja kurudi kwa ajili yako nikimaliza mambo yako, hakikisha hakuna fala yoyote yule ambae atakusogelea maana nitaua mtu, kisha akanisogelea na kunibusu kwenye lips zangu kisha akasema “ chunga na hio nanii yangu My tequila, kisha akaondoka zake…
NAKUJA…………

MY TAQUILA 3
Penzi la nurse na mwanajeshi
HUSQER BALTAZAR
Basi kuanzia ameondoka sikuwahi kumuona wala kujua jambo lolote lile linalomuhusu akili yangu ikawa inaniambia kuwa hatutakaa tuje kuonana tena, na wale wanajeshi sikuwah kuona tena maeneo ya hospital…

Maisha yangu yakawa yanaendelea kama kawaida, na wakati huo nilikuwa na mahusiano na kijana mmoja, alikuwa ni mwanaume wa kanisani sana, na akili zangu nikawa naamini kuwa ni mtu wa mungu sana kumbe alikuwa ananiigizia…

Mwanaume wangu alikuwa anaitwa frank, siku moja frank akanitoa kwaajili ya kupata chakula cha usiku, ile tumefika hio sehemu nikashangaa namuona anapiga magoti, nikashangaa namuona dada yangu na marafiki zangu wengine wakazin, na ndugu wa frank, kisha mwamba akapiga magoti kisha akasema “ Agness will you marry me…

Kwakuwa ni mwanaume ambae nilikuwa nampenda, na alikuwa anaheshimu sana maamuzi yangu, maana hata nilipomuambia kuwa hawez kunigusa mpaka ndoa akakubali, na kuniambia kuwa nijitunze mpaka atakaponioa, na tulikuwa tunashiriki wote kwenye ibada za kila mara kanisani, mpaka nikaona mwanaume ndio huyu sasa….
Basi baada ya kuvalishwa pete ya uchumba frank akaenda kutoa posa nyumbani kwetu na baada ya miezi mitatu ndio nikawa natakiwa kufunga ndoa na frank, kila wakati nilikuwa najiona mwenye bahati sana kukutana na frank, na nilikuwa namuona kama mwanaume ambae amekamilika sana kwangu…

Basi siku zikaenda na hatimae siku yangu ya ndoa ikafika, ilikuwa ni siku bora sana kwenye maisha yangu, nilipambwa hapo wakati wote nilikuwa nawasiliana na mwanaume wangu, ananimabia nay eye yupo anajiandaa kwa ajili ya ndoa yetu, basi kila mtu ambae alikuwa na bashasha mno, mpaka nilikuwa natamani sana dakika ziende hatimae ndoa ipite na niwe halali ya frank wangu kipenzi, kumbe siku zote kwenye maisha mipango ya mungu ni mikubwa kuliko mipango ya kibinaadamu…

Tumefika kanisani hapo tunamsubiri frank, masaa yanaenda, akawa hapokei simu na ndugu zake walikuwa wameshafika ila hakuna hata mmoja ambae alikuwa anajua alikuwa wapi wakati huo, nikapata wasiwasi nikihisi labda amepatwa na matatizo, muda wa ndoa ulikuwa ni saa saba mchana, ila mpaka inafika saa kumi bwana harusi hajafika, nikasikia padre anasema kwamba harusi iahirishwe mpaka wakati ambao tutakuwa tumejipanga, ila kabla hajaondoka tukasikia sauti nyuma ya ukumbi na hatukuwa tunajua ni nani, sote tukageuka kuangalia ni nani ambae alikuwa anazungumza, nilipogeuza machpo nashangaa nakutana na Yule mwanajeshi…

Nikashangaa wanajeshi wanaharakisha kubadilisha Jina na badala ya frank wakaandika William , nikawa nimetoa macho, nikashangaa Yule mjeda amenifata kisha akanikumbatia na kusema “ nilikuwa nashangaa ety mke wangu anataka kuolewa na mtu mwingine,mumeo nimekuja huyo mpuuzi bora kakimbia hivyo ole wako ukatae, nikashangaa naona bunduki, ikabidi nikubali, hapo alikuwa na magwanda ya jeshi, yaan ni kama alikuwa ametoka kwenye harakat zake akasikia naolewa akaona asipoteze muda…

Nikakubali na kumtaka mchungaji afungishe ndoa, baba yangu akapinga akasema kuwa anamtambua frank, maana alikuwa ni kijana mwema sana, na ndugu wa frank nao wakasimama, nikashangaa William anatoa picha akampa baba yangu, kumbe willium alikuwa anaonekana kunipenda sana ila alikuwa ana mwanamke wake, ambae ndio alikuwa anamalizia shida zake za kimwili…

Sasa kumbe kabla hajaja kwenye ndoa akapitia kwanza kwa huyo mwanamke ili wamalizane kabla ya ndoa kisha ndio aje kwangu, ila Yule mwanamke ni kama alikuwa anampenda sana, hivyo akamuwekea kilevi, hivyo mpaka wakati huo alikuwa amelala…
NAKUJA……


MY TAQUILA 4
HUSQER BALTAZAR

Nilihisi kuchanganyikiwa, yaan inawezekana vipi mwanaume wangu akalale na mwanamke mwingine kwenye ndoa yetu, inawezekana vipi akalale na mwanamke mwingine….

Nilikubali kuolewa na willium ila sio kwamba nilikuwa nampenda sana, ila sikutaka familia yangu pamoja na mimi mwenyewe kubeba ile aibu , hivyo nikakubali nikaolewa, baada ya kufungishwa ndoa, willium akanibusu kwenye paji la uso, kisha akanambia naenda kumalizia majukum wife kisha nitarudi ili twende fungate, kisha akaondoka zake………….

Baada ya ndoa kupita willium akawa anaondoka ndipo tunamshangaa frank anakuja na wakatin huo nilikuwa tayari nimeshafunga ndoa kitambo tu, akaja akanimbatia, willium akamkata jicho kisha akasem “ huna mke wewe nenda kwa kimada wako, na ukimsumbua mke wangu ndio utajua umekutana na jini au binaadamu mwenye mapembe, kisha wala hakuongeza neno akaondoka zake…….

Frank akaanza kuniomba msamaha, ila hata sikuwa nataka kumuelewa, yaan kumbe kipindi chjote anajifanya ananitunzia kumbe kuna mwanamke analala nae kila siku, alafu leo anajifanya anataka kunioa, hapana kwa kweli, siwezi kuwa na mwanaume ambae ni muongo na sio muaminifu, akili yangu ndio ilikuwa inaongea lugha hio, ndugu wa frank wakamchukua ndugu yao, maana hata akikazana na mimi kkiasi gani tayari mimi ni mke wa mtu, amechelewa chelewa mwenyewe na hatimae amekuta mwana sio wake…

Kwa kuwa sikuwa najua willium anaishi wapi, hivyo nikarudi kuishi kwa wazaz wangu, na kuanzia nimeaanza kukaa kwetu sijawah kuona willium amenipigia wala kunitumia sms, kwanza nilikjuwa nahisi kama hana namba yangu ya simu na wala hapajui kwetu, ila sikujali, maana kwanza sikuwa nampenda hata kidogo na nilikuwa namuogopa sana maana alikuwa ni mtu wa amri amri tu yaan….

Basi baada ya mwezi, nikawa natoka nyumban naenda kazin, maana nilikuwa likizo na likizo yangu ndio ilikuwa imeisha, hapo frank ameshanisumbua vya kutosha ety anasema amewekeza muda wake mwingi ili awe na mimi, na hakuna mwanaume asiechepuka, ila alikuwa ana malengo ya mbali na mimi hivyo akawa anaomba sana nimsamehe, sikutaka kumsikiliza maana sikutegemea kama nitapitia maumivu ya usaliti mapema yote hio, yaan naanza kupitia usaliti kabla hata sijaingia kwenye ndoa….
Ingawa sikuwa namtaka ila alikuwa ananisumbua sana, akawa ananikumbusha mambo m,bali mbali ambayo tumeshawah kufanya pamoja, hata kama kuna mambo mengi kiasi gani ambayo tumeshawah kufanya pamoja ila hakuwa na haki ya kunisaliti, hivyo sikutaka kuusikiliza msamaha wake, maana nimejitunza sana, na sikuwa nimejitunza kwa sababu ya mtu ambae anaivunja thamani yangu kwa kuwa na mwanamke mwingine, hivyo hata hizo kumbukumbu ambazo tumeshawah kuzitengeneza pamoja sikuwa nataka kuzisikia kabisa yaan…

Sasa siku hio natoka, nikawa natafuta bajaji ya kunipeleka kazini, ila nikiwa nimesimama mara nikasikia honi nyuma yangu nikasema nigeuke, nashangaa nakutana na gari nyeusi, ilikuwa ni range rover, nikapuuza, maana sina ndugu wala jamaa anaemiliki gari, hivyo nikahisi kama hio honi imepigwa tu…

Honi ikapigwa tena, nikageuka, safari hii nilipogeuka nikashangaa namuona willium akiwa anananiangalia kwan tabasamu kisha akasema “ hautakuja kumkumbatia mumeo, maana amekumiss sana…

Sijui kwanini sikutaka hata kumuona, maana kama ni kunioa amenioa kwa sababu nilikuwa na hasira na nilikuwa naogopa aibu ya kuachwa siku ya harusi, ila sio kwa sababu nilikuwa nampenda sana…
“ naomba niende kazini, sidhani kama nakuhitaji, nikajibu kwa sauti ya kujiamini, nikashangaa ananibeba taksi bega na kusema “ ndio nimerudi sasa mke wangu tunatakiwa tukaanze kula fungate yetu, kisha akaniingiza kwenye gari…
“ natakiwa kwenda kutoa taarifa na kuandika barua ya kwanini sijafika kazini mpaka wakati huu, naomba uniache maana sitamani kuharibu kibali changu, nikaanza kulalamika…
Akachukua simu yake kisha akaanza kutafuta namba kwa sekunde kadhaa kisha akaona namba moja na kuipiga na baada ya sekunde kadhaa simu ikapokelewa, alikuwa ni mkurugenzi wa hospital akamuambia kuwa “ nipo na mke wangu ndio nataka tukaanze kula fungate yetu, nimeona nikupe taarifa maana hatofika kazini…
“ ni nani huyo? Upande wa pili ukauliza..
“ my Taquila , akajibu willium nikashangaa kwanini ajibu my tequila ni kwamba hajui jina langu, ikabidi nidakie na kusema “ ni mimi agness boss, basi akatutakia fungate njema kisha akakata simu…
Willium akaniangalia kisha akasema “ natumaini hauna mashaka tena , kisha akawasha gari na tukaanza kwenda sehemu ambayo sikuwa naifahamu hapo natetemeka balaa…
NAKUJA………..


MY TAQUILA 5
Penzi la mwanajeshi na nurse
HUSQER BALTAZAR
“ unanipeleka wapi lakini wewe, mbona mambo yako ni ya kibabe babe sana, naomba nikatoe taarifa kwa wazaz wangu wajue kuwa nipo na wewe, maana siwez kwenda sehemu ambapo hakuna ndugu wala jamaa yangu yoyote Yule mwenye taarifa, na kingine mimi sikukupenda kabisa, nilikubali kuolewa na wewe kwa sababu ya kuficha aibu ya kuachwa siku ya ndoa yangu, ila sikukukubali kwa sababu ya mapenzi, hivyo naomba uniache niendelee na maisha yangu………..

Hapo naongea mtu yupo kimya kana kwamba anisikii ninachoongea, nikawa naendelea kulalamika, nashangaa naambiwa “ shuka kwenye gari, akili yangu ikawa inanituma nimekuja kuachwa porini, ila nakuja kuangalia nje, nashangaa tupo kwetu, nikajikuta natabasamu…
“ usicheke sana maana unatakiwa unambie nikupe dakika ngapi za kwenda kuaga wazaz wako, maana nina hamu na wewe ajabu, siwez kulala mbali na wewe kwa siku ya leo, akasema willium …

Sikutaka kumjibu, nikashuka kwa bashasha kubwa mno, maana niliamin nikishafika nyumbani mambo yote yatakaa sawa tu, naweza nikapata hata namna ya kumtoroka willium nikaendelea na maisha yangu, maana ukweli ni kuwa sikuwa nataka hata kumuona….

Sasa willium akaingia kwa heshima kubwa sana, akawasalimia na wazaz wangu, akawa amekaa zake anachezea simu, hapo ananisubiri niage kisha niondoke nae, nikawa najivuta vuta, mara nifanye hivi mara vile ilimradi tu aondoke, maana sikuwa nataka kuondoka nae…
Akasimama kisha akasema “ samahani baba na mama, huyu ni mke wangu kisheria, naona kama hana mpango wa kwenda kuishi na mume wake hivyo naomba niseme tu kuwa muda wangu wa kumsubiri aendelee kunipotezea muda umeisha, kwa heshima na ridhaa yenu naomba niondoke na mke wangu…

“ mwanangu hajakupenda anaogopa kuondoka na wewe, akajibu mama yangu akijua ananinusuru…
Willium akatabasamu lile tabasamu la kiroho mbaya kisha akasema “ hata mimi sikuwa nimempenda ni yeye mwenyewe ndio alisababisha mpaka leo niwe hapa, na nihangaike nae, sasa basi hata nay eye atanioenda taratibu, na mimi sio jambazi wala mtu mbaya hivyo nitamlinda, my tequila toka twende nyumbani kwetu…

Nilikuwa natetemeka mpaka utumbo, maana sikujua naenda wapi na sikujua anaenda kunifanyia nini, sikuwa nataka kutoka nikiamin wazaz wangu watanisaidia, akajua kabisa kuwa sitaki kuondoka nae, nikashangaa nafatwa jikoni kisha nikabebwa taksi bega na willium akasema “ samahani wazee nimemteka mke wangu hivyo sina kosa, kisha akaanza kuondoka na mimi, hapo mama yangu analia, na baba yangu amekaa kimya anaangalia, akaniingiza kwenye gari kisha siji akanigusa wapi nikashangaa napitiwa na usingizi wakati huo huo, na baada ya kuona amefanikiwa kunifanya nilale akalock milango na kurudi kwa wazazi wangu…

Aliona kabisa hali za wazaz wangu haziko sawa, na hakutaka kuwauwa wazaz wangu na pressure, akamfata mama kisha akapiga magoti na kusema “ huenda kazi zangu zimenifanya nisiwe mtu wa kawaida, ila mama naomba unipe ruhusa ya kuondoka na binti yako nakuahidi kuwa sitakaa nimuuzime, na nitahakikisha anakuwa mwanamke mwenye furaha zaidi, mimi sio katili, ila nina mpenda binti yenu na sikuwa najua kama alikuwa anataka kuolewa na Yule mpuuzi, nisingeruhusu hilo litokee, na ningehakikisha mnanipenda kama mkwe wenu, ila kwa bahati mbaya tukakutana sehemu ambayo haikuwa sahihi kukutana, mahari nitaleta maana najua nimeoa kibabe na mnahaki ya kula mahari ya binti yenu, ila naomba mnipe Baraka zenu tu wazaz wangu, maana mtanisamehe hata msipotaka siwezi kumuacha mtoto wenu hata kwa bahati mbaya…
Vuta picha mwanaume anawaambia hivyo wakwe zake..
ITAENDELEA


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote