ONE NIGHT WITH MY BOSS

book cover og

Utangulizi

ONE NIGHT WITH MY BOSS.
Ni simulizi inayomuhusu sherry binti machachali kutoka uswahilini, sherry anafanya kazi kwenye mgahawa na duka la pizza point. Siku moja anachelewa kwenda kazini akiwa barabarani anafanyia pikipiki na kuahidi atalipa kiasi chochote anafika kazini anatakiwa bei ya juu anagoma kulipa anaongea maneno mengi kisha anaingia zake kazini.
Jioni akiwa anatoka kazini anakutana na mtu wa pikipiki anamkamata kwa nguvu na kutaka wanakutana kwa njia yoyote, sherri anakimbilia kwa kijana mmoja mtanashati na kujifanya mpenzi wake lakini yule kaka anamkataa dereva toyo anambeba begani ili aondoke nae Derick anaamua kumsaidia lakini bado sherry anamlaumu kwa kuchelewa kumsaidia.

Kesho yake kazini kwao wanatetewa boss mtoto wa mmiliki wa mgahawa ambae ni Derick. Sherry anatokea kuniongelea vibaya Derick anamsikia anaanza kumdai pesa yake aliyomlipia na kumpa kazi nyingi kabla hajamaliza kulipa deni anafahamisha kuanguka simu ya boss kwenye maji deni linaongezeka marumbano yakazuka kati yao.
Baada ya siku kwenda Derick anamchukia na kwenda nae sehemu kwaajili ya kumtlrusha roho mwanamke aliemuacha wanakubaliana akifanya hiyo kazi deni linakuwa limeisha .
Sherry anafanya kazi inaenda vizuri baada ya hapo wanaipongeza kwa kunywa pombe.pombe zinasaidia wanapeleka na chumbani na kujikuta wamelala pamoja. Sherry valilia kwa uchungu kwa kupoteza usichana wake alioutumia kwa muda mrefu wakati huo Derick anashangaa inakuwaje binti machachali kama sherry bado anakuwa na bikra yake? Baada ya tukio sherry anakuwa hataki mazoea na Derick ndio amekufa kaoza kwa sherry na yupo tayari kwa chochote ilimradi awe wake wa maisha kwani aliamini bikra ya sherry ilikuwa ni zawadi kubwa kwake.

ONE NIGHT WITH MY BOSS 1

MTUNZI SMILE SHINE

Ilikuwa ni majira ya saa moja asubuhi Sherry ndio kwanza alikuwa kakanyagua shuka huku usingizi mnono ulimpitia na ndoto nzuri iliyomfanya Aachie tabasamu . Kwa mbali alisikia simu yake ya mkononi ikiita, alipuuzia ikapita mpaka ikakata lakini mtu aliyepigwa hakukoma aliendelea kupiga mpaka ikawa kero kwa sherry ikabidi aamke akachukua simu akaangalia aliekuwa anapiga.
" Aaaaah sheyla mbona msumbufu hivi kukatisha usingizi wangu.
Alilalamika kisha akapokea ile simu.
" Hallow.
" Sherry inamaana bado ulikuwa umelala unafikiri ile kazi ni kazi ya baba yako.
" Lakini mbona bado mapema .
" Hivi umeangalia saa, unajua saizi ni saa ngapi?
Sherry alitoa simu sikioni na kuangalia saa.
" MUNGU wangu saa mbili kasoro, sheyla acha nijiandae tutakutana kazini.

Sherry alikata simu akakimbilia bafuni kuoga .
Kama unavyojua nyumba za familia kubwa ulichelewa kuamka inakutana na foleni.
" Jamani ulikuwepo huko bafuni fanya haraka wengi vibarua vyetu vinaninginia huko .
Aliendelea kupiga maswali huku akisubiri mtu atoke, alimaliza kuswaki yule mtu alikuwa bado hajatoka. Sherry aliamua kusogea mlangoni na kuugonga huku akisisitiza huyo mtu atoke . Mara mlango ulifunguliwa akatoka baba yake mzee Nyange akiwa kakunja sura.
" Ooohooooo kumbe ni wewe baba naomba unisamehe mzee wangu nilijua ni hao ndugu zangu wengine.
" Pumbavu na hiyo tabia ya kupiga mlango mpaka unakaribia kubomoka ukome.
Alisema Mzee Nyange kwa ukali kisha akaondoka na sherry akaingia bafuni kuoga.
Akijimwagia maji haraka na kutoka .
" Wewe sherry umeoga umejimwagia? Aliuliza mama yake
" Nimeondoka jasho nitaoga vizuri nikirudi.


Baada ya kuvaa haraka alitoka akaenda uasimama kando ya barabara akisubiri usafiri , aliangalia saa yake ya mkononi kila wakati.
" Jamani haya magari yana nini leo au mpaka nifukuzwe kazi ndio hawa walimwengu wafurahie.
Alisimama zaidi ya kama dakika tano bila usafiri kutokea akaamua kutembea kwa miguu .
" Hii ni kazi bure siwezi kuwahi sijui kwanini nilichelewa kuamka . Sherry alilalamika huku akitembea kati kati ya barabara magari na pikipiki yalimpigia honi.
" Acha kelele.
" Acha ujinga wewe pisha njiani, au umechoka ugali? Alisema dereva mmoja wa bodaboda na mwingine akadakia
" Ni stress za mapenzi zinamsumbua.
" Itakuwa kaachwa vibaya sasa anataka kufa.

Sherry hakujari maneno ya hao watu alisogea pembeni akaendelea kutembea alifika sehemu akakuta pikipiki imesimama akadandia bila kuongea chochote na muhusika.
" Wewe dada vipi?
" Kwanza habari za asubuhi.
" Salama.
" Naomba unisaidie kaka kuna sehemu muhimu nawahi nitakupa hela yoyote utakayotaka.
Yule kaka kusikia hela yoyote akakubali
" Sawa unaenda wapi?
" Pizza point.

Yule kaka Safari ya kuelekea pizza point ilianza . Ndani ya dakika 15 wakawa wamefika sherry alishuka haraka na kutaka kuingia kwenye duka la pizza pamoja na mgahawa aliokuwa anafanyia kazi.
" Wewe dada unaondoka je bila kunipa hela yangu?
" Oooh samahani ulisema sh ngapi vile?
" Ni elfu kumi.
" Hiyo elfu kumi ya nchi hii au nchi jirani?
"Unataka kunilipa ya kenya?
" Acha ujinga hapa huwa nakuja na elfu moja tu kwakuwa nilikwambia nitakupa hela utakayotajwa sio unifanyie utapeli wa aina hiyo nitakuongezea elfu moja iwe elfu mbili basi.
" Wewe acha kujitoa ufahamu nataka hela yangu. Alisema yule dereva huku akiwa anashuka kwenye pikipiki.
" Unashika kwenye pikipiki unataka kunifanyia nini?
" Nataka hela yangu.
Dereva alitaka kumnyang'anya pochi
" Weeee usije ukajaribu nitakujazia watu na hela yako hautapata itakuwa imelipa kwako. Hunijui wewe...

Kwakuwa wanavutana alifika mzee Malco mmiliki wa ule mgahawa.
" Nyie nini kinaendelea hapa mbele ya biashara yangu?
" Boss huyu kijana simuelewi amekuja kunifanyia fujo kazini kwangu.
" Sio kweli mzee nina mdai hela ya usafiri hataki kunipa.
" Unadai shilingi ngapi?
" Elfu kumi.
" Kijana umemtoa wapi mpaka umdai hela yote hiyo.
Mzee Malco alihoji maana ilikuwa ni pesa nyingi kwa usafiri wa palepale mjini.
" Umeona boss huyu kaka ni tapeli kwanza hanidai alikuwa ananisumbua mimi simtaki sasa anakuja kunisumbua hapa.
" Kijana naomba uondoke hapa kabla sijawaambia walinzi waje wakutoe.
" Lakini mzee .....
" Nimesema toka hapa.
Alisema mzee Malco huku akiingia ndani ya mgahawa.
" Nilikwambia ukileta ubishi hutapata hata hiyo hela yako iliyostahili kupata.
" Usinione umeshinda nitakukamata na pesa yangu utatoa .
" Kama sitatoa sasa basi sitatoa tena
Sherry aliondoka akaingia ndani kwenda kuendelea na kazi.

Sherry alienda kwenye chumba cha kubadilisha nguo akabadili nguo alipomaliza alienda kuendelea na kazi .
" Niambie Anitha.
" Safi.
" Mbona leo boss amekuja kuna nini kinaendelea hapa?
" Nasikia kuna kijana wake anakuja kutoka masomoni na ndio atakuwa msimamizi wa huu mgahawa.
Sherry alicheka
" Una cheka nini?
" Mambo mengine yanafurahisha sana yani watu wanaenda kusoma nchi za nje alafu baada ya hapo wanakuja kusimamia migahawa na maduka ya pizza
" Sasa ulitaka afanye kazi gani?
" Ninavyojua wasomi huwa wanafanya kazi zinazoeleweka kama vile bank, na dokta, urubani sasa huyu wa mr Malco amevunja rekodi anakuja kusimamia mgahawa labda huko alienda kusomea kuoka mikate na kutengeneza pizza pamoja na supu ya mboga mboga. Aliongea sherry huku akicheka
" Anitha alimuangalia akaanguka kicheko.
" Unajua wewe una madharau sana , lakini unatakiwa kuwa makini huyo anayekuja ni kijana na sio mzee kama mr Malco ambae umemzoea kama babu yako.


ONE NIGHT WITH MY BOSS 2

MTUNZI SMILE SHINE


" Hata hiyo kijana naweza kumfanya Babu yangu tu si unajua mimi huwa sina nidhamu ya uoga , siogopi mtu.
Sherry aliongea kwa kujiamini alafu akaenda kuendelea na kazi zake.
Mara sheyla alifika.
" Wewe nimepata habari kuwa ulikuwa unagombana na mtu huko nje kulikoni?
" Achana nae ni mpuuzi mmoja anasema kutoka nyumbani mpaka kunileta hapa nauli ni 10000 anafikiri tunaokota hela.
" Hahahaha sasa ikawaje?
" Nadhani unanijua vizuri huwa sitapeliwi nimempa elfu mbili kataa ikawa ndio basi tena katia msaada atalipwa na MUNGU.
" Wewe kiboko. Hivi umesikia ujio wa boss mpya?
" Hivi mbona mnahaha na huyo boss mpya, na aje tu atatukuta.
" Nasikia ni bonge la handsome boy.
" Jamani wenye vitanda mtawajua tu ndio maana hakuachi kuniongelea sababu handsome . Mwenzenu mimi hihsngaikagi na hayo mambo sasa kazi kwenu.
Baada ya maongezi kila mmoja alipita njia yake wakaendelea na kazi.

Ilifika jioni muda wa kutoka kazini ulikuwa umewadia. Wafanyakazi wote waliondoka na sherry alikuwa wamwisho kutoka. Alitoka nje ya jengo akasimama pembeni ya barabara huku akiwa akajinyoosha.
Pale alipokuwa amesimama upande wa pili kulikuwa kuna kaka kasimama pembeni ya gari lakini alikuwa bize na simu yake. Sherry alimuangalia na kujisemea.
" Jamani MUNGU fundi, anajua kuumba .
Aliishia kusifia tu lakini hakutilia maanani sana kuhusu huyo kijana ambae alionekana anamvito kwasababu huwa anaamini kitu chenye mvuto badae huwa kina madhara .

Akiwa bado kasimama mara pikipiki ilifunga breki mbele yake, sherry alishituka na kumuangalia dereva wa pikipiki ambae alikuwa kavalia helmeti kichwani.
" Ni nini maana ya wewe kuja kusimamisha hilo pikipiki lako mbele yangu? Kwanza ulikuwa unataka kuniuwa , unataka kuniteka au unataka kunifanya nini? Sherry aliongea kwa ukali . Yule kaka hakujibu alivua helmeti kisha akamuangalia.
" Ni wewe tena? Aliuliza sherry baada ya kuiona sura ya yule boda boda wa asubuhi.
" Ulifikiri naweza kusamehe pesa yangu kizembe hivyo? Unajua leo kutwa nzima sijafanya kazi nilikuwa nazungukia haya maeneo kwaajili yako ...
" Hayo ni yako wewe wewe , mimi nikikutumia uzunguke hapa? Umefanya kazi hujafanya hizo sio shida zangu tena fanya uende .
" Hapa siondoki mpaka unipe shilingi elfu 20 au niondoke na wewe.
" Unasemaje wewe kichaa?
" Sina muda wa kurudia kama vile natangaza matangazo ya kupotea kwa mtu ,utapanda ua nikupandishe? Yule dereva boda boda alimuuliza na sherry alifyonza na kugeukia pembeni.
" Una wazimu nini nipande wapi?
Yule dereva boda akawa anashuka kwenye pikipiki.
" Mmmmh hili jamaa halitanii nitakuja kupandishwa kwa nguvu.
Sherry alikimbia akavuka upande wa pili wa barabara na kwenda kusimama pembeni ya yule kaka, yule kaka alimuangalia sherry akamsalimia huku akitabasamu.
" Habari.
" Salama.
Aliitikia yule kijana alafu akaendelea na mambo yake. Sherry aliendelea kujisogeza karibu na yule kaka huku akimuangalia yule dereva toyo

Yule dereva wa toyo alimuangalia alipoona kasimama aliamua kumfuata.
" Mungu wangu yule mjinga anakuja sasa nitafanya nini? Sherry alijiuliza huku akiwa anafikiria afanyeje. Alifikiria kukimbia lakini haikuwezekana alikuwa kavalia sketi fupi tena ilikuwa imembana. Alipoona dereva toyo anakaribia kuwafikia alijisogeza zaidi kwa yule kaka na kuushika mkono wake.
" Ghaaaaa unafanya nini hivi ungesababisha simu yangu iangukie chini unape......
" Shiiiii ! Samahani naomba unisaidie .....
Kabla hajamaliza kuongea yule dereva alikuwa kafika na kumsalimia yule kaka.
" Habari kaka
" Salama.
" Hivi bado unanifuatilia mpaka muda huu kwasababu ya pesa ndogo tu, hebu nipishe kwanza niongee na mpenzi wangu. Alisema sherry na kusababisha yule kaka amuangalie huku akiwa akunje uso.
" Wewe , mimi na wewe......
" Jamani mpenzi najua ulishanikataza kukopa kopa watu wasio waelewa ila hii ni mara ya mwisho na ilitokea kama dharula tu na nimemuahidi kumlipa.
" Kaka huyu mwanamke wako ni tapeli asubuhi nimembeba na pikipiki yangu lakini hataki kunilipa hela yangu na hela yenyewe sio hata kubwa kama vipi mlipie.
" Mbona mnanichanganya , yani sina ninachowaelewa. Naomba mnipishe kadaianeni huko.
" Basi kaka hiyo imeisha kama wewe mwenyewe umemchoka mwanamke wako basi acha niende nikamalizane nae mbele ya safari.
" Itakuwa vizuri. Alijibu yule kaka

Yule dereva alimshika mkono akawa anamvutia.
" Niache unanipeleka wapi, alafu na wewe kaka huna hata huruma , hujui thamani ya mwanamke hujui huyu mjinga anaenda kunifanya nini huko na nakwambia kama baya kitanikuta basi utalaanika wewe na kizazi chako na kama nikifa basi mzimu wangu utakuganda kila uendako.

Walivutana pale dereva toyo alipoona anazidi kumsumbua alimnyanyua na kumuweka begani.
Safari hii sherry aliomba msaada huku akilia. Watu walipohoji kuna nini yule dereva toyo alijibu.
" Ni mke wangu ana matatizo ya mwezi mchanga hivyo kipindi hiki huwa ananisumbua sana .
" Jamani muongo huyu ananidai elfu moja
" Hakuna aliemuamini sherry ,watu waliamini kweli ana matatizo.

Badae yule kaka akakumbuka kama aliona nembo pizza point kwenye shati la sherry.
" Ni mfanyakazi wa pizza point?
Yule kijana alivuka barabara na kwenda mgambo ya pili akawakuta bado wanasumbua na kupandisha na kwenye pikipiki.
" Hey hivi ulisema unamdai shilingi ngapi?
" Alfu kumi tu.
Alijibu dereva toyo huku akicheka .
Yule kijana alitoa Wallet akatoa noti ya shilingi elfu kumi akamlipa.
" Pesa yako hii hapa achana na huyo.
" Hicho ndicho nilichokuwa nakitaka. Alafu wewe kuanzia leo ukiona hii pikipiki barabarani kaa mbali nayo .
" Mmmmh pikipiki lenyewe baya kwanza bovu .
" Baba ako analo. Alijibu dereva toyo alafu akaondoka zake akamuacha sherry na yule kijana.
" Ila wewe kaka una roho ngumu sana ulitaka niadhilike ndio unipe msaada , sasa wewe pale ulichokuwa unakataa ni nini kwani ungekubali kuigiza kuwa mimi ni mpenzi wako ungepungukiwa na nini ?
Yule kijana hakuwa na muda wa kumsikiliza aliamua kuondoka lakini sherry hakukoma kuongea alimsindikiza kwa maneno mpaka alipovuka barabara na kupanda kwenye gari yake na kuondoka.

Kesho yake asubuhi wafanyakazi walifika wakawa wanaendelea na kazi wakati huo sherry alikuwa upande wa mgahawa anafanya usafi.
Akiwa anafuata futa meza alifika Damas mfanyakazi mwenzie alipita kwa kila mfanyakazi na kumwambia kuwa wote wanaitwa na mr Malco.
" Jamani hivi vikao vya mapema yote kuna heri au kuna ambae ameingiza shoti? Sherry aliuliza.
" Twendeni tutaenda kujulia hukohuko.


ONE NIGHT WITH MY BOSS 3

MTUNZI SMILE SHINE

Wafanya kazi wote walikutana sehemu moja wakasimama kwa utulivu ili kujua nini kinaendelea .
Baada ya sekunde chache alifika mzee Malco na yule kijana aliemlipia hela sherry, sherry alipomuona alishituka.
" Huyu barobaro anaweza kufanya kazi hapa au ndio anakuja kutoonyesha hizo Cheni zake kama minyororo ya mbwa na herein masikioni kama binti.
Sherry alijisemea huku akimuangalia.

" Habari zenu vijana! Alisalimia mzee Malco.
" Salama shikamoo.
" Marahaba, ninewaiteni hapa ili kumtambulisha kijana wangu anaitwa Derick na atakuwa boss wenu hapa majukumu yangu yote namuachia yeye msimamo mtamsapoti na kufanya nae kazi pamoja kama mlivyokuwa mkifanya na mimi.
" Sawa boss.
" Derick hii ndio timu ya wafanyakazi wetu hapa , kwa uzoefu wao mtafanya kazi pamoja .
" Sawa baba.
" Yangu yalikuwa ni hayo sasa mnaweza kwenda kuendelea na kazi.

Wafanyakazi wote walitawanyika wakaenda kuendelea na kazi na Derick aliongozana na baba yake walienda ofisini kwaajili ya kwenda kukabidhiana ofisi.
Sherry aliendelea kufanya kazi huku akiongea na wenzake.
" Jamani huyu Sharo anaweza kufanya kazi hapa au ndio tumeletewa kaka moyo.
" Usimzungumzie mtu hivyo sababu hujui ni mtu wa aina gani tumpe muda kwanza.
" Mimi nawaambieni huyu mtu tulielezwa ni mtata.....
Kabla hajamaliza kuongea alisikia sauti ikisema
" Wewe unaongea sana hebu njoo. Sherry aligeuka kuangalia alimuona Derick. Aliwaangalia wenzie akiwa anajua amesikia alichokuwa anaongea , alirudi kumuangalia Derick alafu akauliza
" Unaongea na mimi?
" Ndio wewe nifuate.
Sherry aliacha kazi aliyokuwa anafanya akamfuata Derick ofisini kwake.
" Ofisi yangu inaonekana haijafanyiwa usafi pia inatakiwa kubadilishwa baadhi ya vitu ningependa hiyo kazi ufanye wewe.
" Boss lakini hii sio kazi yangu mimi kazi yangu ni kule mgahawani .
" Unabishana na boss?
" Hapana nilikuwa najaribu kukuelekeza tu.
" Sitaki kuelekezwa fuata maagizo yangu anza kufanya usafi.
" Sawa.
Sherry alitaka kutoka Derick akamuuliza .
" Unaenda wapi?
" Kwani humu ndani kuna vifaa vya kufanyia usafi?
" Unaniuliza au unaniambia?
" Naenda kuchukua vifaa.
Alijibu sherry kisha akafungua mlango akatoka.
" Nilijua tu huyu kijana ni mpuuzi tu na kazi imeshaanza na ameamua kuanza na mimi. Sherry alilalamika huku akienda kuchukua vifaa vya usafi.

Baada ya muda alirudi akaanza kufanya usafi huku Derick akiwa kakaa huku akiwa Bize na simu yake anacheza game la magari.
" Hivi unaitwa nani vile?
" Sherry.
"Mmmh ! Sherry hivi unajua una deni na mimi?
" Wewe kaka deni gani na ndio kwanza tunaonana?
" Kumbe una matatizo ya kusahau kiasi hicho? Hukimbilia kama jana nilikuamulia kwenye ugomvi wako?
" Oooh sawa nimekumbuka.
" Nakudai ile hela niliyomlipa bodaboda unaonaje kama utailipia au nikukate kwenye mshahara wako mwisho wa mwezi?

Sherry alisimama akawa anamuangalia huku akiwa kashika kiuno.
" Kwani hayo ndio yalikuwa makubaliano yetu?
Derick alisimama akamsogekea karibu na kuutoa mkono wa sherry kwenye kiuno chake.
" Unanishika kiuno kwani tunasutana hapa alafu naomba ukumbuke mimi nilisimama hapa sio yule ulikutana nae jana huyu aliyesimama hapa ni boss wako unatakiwa kuwa na heshima .
Sherry alikuwa mpole na kuomba msamaha.
" Nisamehe boss.
" Namna hiyo, endelea na kazi.

Sherry aliendelea na kazi huku akiwa kakasirika .
" Watu wengine sijui wakije hawafai hata kukutana nao kwa bahati mbaya yani hela yenyewe ndogo bado anataka kuikata kwenye mshahara , mwajuma anadai hela yake ya kijora , mama zuu anataka mchango wa harusi ya mwanae bado nae akate hiyo hela yake.
Derick alisikia alivyokuwa analalamika alinyanyuka na kumnyatia kwa nyuma.
" Unasemaje?
Sherry alishituka akageuka kwa nguvu na kuugonga mkono wa Derick, simu aliyokuwa kashika mkononi ulidondokea kwenye ndoo ya maji . Wote kwa pamoja waliangalia kwa mshituko kisha wakiangaliana usoni.

ONE NIGHT WITH MY BOSS 4

MTUNZI SMILE SHINE

Derick na Sherry Waliendelea kuangalia na huku Derick akimuangalia kwa hasira, sherry alimuangalia kwa uwoga
" Umeona kilichotokea?
" Sasa mimi na husika vipi hapo au unataka tu kunisingizia?
" Bila wewe yasingetokea haya.
" Bila wewe kuja hapa simu yako isingedumbukia kwenye maji ungeniacha niendelee na kazi uliyonipa lakini sijui wewe umefuata nini hapa.
Sherry aliwaza kutoa simu kwenye maji kumbe na Derick aliwaza hivyo hivyo wote waliinama kwa pamoja wakajikuta wanagombana vichwa. Sherry alishika pale alipogongana na kusema kwa sauti ya chini.
" Nimeongea na kichwa cha mtu au nazi?
Derick aliinama akatoa simu yake kwenye maji aliiangalia alafu akamuangalia sherry usoni.
" Umesemaje?
" Sitaongea chochote.
Derick alimuangalia alafu akasema
" Simu yangu imeingia maji inabidi ukaitengeneze au ukanunue simu mpya kama hii.
" Kheeeee nawezaje kununua simu kama hiyo wakati mimi mwenyewe natumia hii vunja chama yangu.
" Utajua mwenyewe shika hii simu nataka irudi hapa ikiwa nzima au mpya.
Derick alichukua mkono wa sherry na kumpatia ile simu.
Derick hakuwa na wasiwasi na simu yake kwasababu alijua simu yake haina shida kubwa na alifanya vile kucheza na akili ya sherry .

Sherry alishindwa kumalizia hata huo usafi akichukua vitendea kazi vyake akatoka ofisini kwa Derick akiwa hayupo sawa aliweka vifaa vya usafi akatoka nje na kuiweka ile simu Juani ili ikauke .
" Huyu mtu kwanza tu kunikomoa kwani kosa langu mimi ni kunilipia ile hela , sasa hii simu ya bei ghari naenda kuitengeneza kwa shilingi ngapi.....
Sherry aliendelea kulalamika mara rafiki yake sheyla alimfuata.
" Wewe vipi mbona unaongea mwenyewe?
" Sheyla mwenzio nimepatikana huyu boss wenu nao kapania kuniachisha kazi anataka mimi nirudi mtaani kuuza vitumbua vya mama Nurdin (mama yake).
" Kwani imekuwaje?
Sherry akimsikiliza kila kilichotokea na kumuonyesha ile simu.
" Mmmmh shoga yangu pole hapa unauza ile nyumba yenu ya urithi wa babu yenu kwenye ule mgao wako ndio unanunua hii simu na haitakiwi hata na hela ya kununulia kijora cha ukumbusho.
" Acha kukuza mambo bwana hapa naenda pale kwa mbwana fundi simu anarekebisha mara moja.
" Ubishi nao imebarikiwa haya kajaribu bahati yako. Lakini hapo Juani itoe hiyo simu sio nguo useme itakula kama maji yapo kwa ndani.
Alisema sheyla alafu akaondoka na kumuacha sherry akiwa haelewi afanye nini
" Yani kila unachofanya sicho hawa watu mbona watanifanya niwe chizi mwaka huu.

Sherry alitoka kazini alienda moja kwa moja ofisini kwa mbwana.
" Mbwana nimeleta simu yangu hii hebu iangalie.
Mbwana alipopokea akiangalia alafu akacheka.
" Sherry huu mtambo umepata wapi?
" Fanya kazi yako maneno mengi ya nini?
" Haifahamiki na wewe kabisa, umeifanya nini?
" Imeingia kwenye maji.
" Mmmh hii simu siwezi kuitengeneza sjmhika simu yako uondoke.
" Kumbe ufundi wako ni wakuchovyachovya?
" Hizo simu zina mafundi wake sio sisi wa huku vichochoroni maana hicho kioo chake kinauzwa laki tano.....
" Unasemaje wewe?
" Kama ulivyosikia na pita huko mtaani ukiwa umeshika kama vile umeshika chapati za mama Nurdin utaona kitakachokuwa.
Taratibu sherry aliingiza simu kwenye mkoba wake na kuanza safari ya kurudi kwao.

Kesho yake asubuhi Derick alipofika tu alienda kuonana na sherry.
" Hallow miss sherry.
Sherry alimuangalia bila kujibu
" Vipi simu yangu imewaka au imenunua nyingine?
" Unajua kabisa siwezi kumudu utengenezaji wala kununua .
" Sasa itakuwaje?
" Maamuzi unayo wewe ila naomba usiguse mshahara wangu mwezi huu nina mambo mengi sana.
Derick akimuangalia kisha akatabasamu.
" Nitajua jinsi ya kulipia hilinipatue simu yangu.
Sherry alienda kuchukua simu yake akampatia, Derick alichukua akaenda ofisini kwake. Sherry alimuangalia alivyokuwa anaondoka alafu akasema
" Asante MUNGU umekubali maombi yangu.

Siku zilienda kazi zinaendelea kama kawaida . Siku moja Derick alifika dukani akamkuta sheyla anafanya usafi.
" Sheyla yule shoga yako mwenye maneno mengi yuko wapi?
" Nani?
" Yule rafiki yako anaongea sana...
" Sherry
"Hiyohiyo
" Yupo mgahawani anahudumiwa wateja.
Derick alienda haraka mgahawani akamkuta sherry anahudumiwa wateja huko akiongea nao kwa uchangamfu kama kawaida yake.
" Sherry.... Derick aliita na sherri aligeuka kumuangalia
" Kumekucha sijui huyu Sharo anataka nini tena. Alijisemea sherry huku akienda aliposimama Derick.
" Abeee boss.
Derick alimshika mkono wakasogea pembeni.
" Ulipokuwa leo ulivaa nguo gani?
" Hilo ni swali gani ?
" Jibu swali.
" Niliva gauni....
" Hebu kavae kama ulivyokuwa alafu uje hapa.
" Lakini najisikia wateja
" Achana na huyo kazi watambue wenzio waendelee na kazi.
Sherry alirudisha trei jikoni kisha akaenda chumba cha kubadilisha nguo akavaa nguo zake za kawaida alafu akamfuata Derick pale alipomuacha. Derick alimuangalia kuanzia juu mpaka chini alafu akamwambia
" Nifuate.
Wakiongozana mpaka kwenye gari la Derick, Derick walifungua mlango wa gari .
" Panda
" Tunaenda wapi?
Derick hakujibu alienda kupanda kwenye gari akawasha na kuanza kuendesha.
" Boss mbona sikuelewi unanipeleka wapi?
" Hivi unakumbuka kuwa unatakiwa kunilipa ile hela yangu pia simu yangu hukuweza kuitengeneza?
" Kwahiyo ndio inakuwaje sasa na vinaingilianaje na hii safari?
Sherry aliuliza huku akiwa anaonekana mwenye hofu. Derick alimuangalia alivyokuwa anahaha alafu akaachia tabasamu
" Tulia wewe upo na boss wako na huu ni muda wa kazi .
" Kazi nje ya jengo la ofisi?
Derick hakumjibu alikata kona wakaingia kwenye saloon moja, alipak gari yake kisha akashuka na kwenda kumfungulia mlango.
" Shuka.
Sherry alishuka .
" Ingia hapo ndani nenda watengeneze hizo nywele zako hakikisha unakuwa kwenye muonekano wa tofauti kidogo kama ni wigi basi wakupe lile la bei ghari gharama zote nitakupa .
Sherry aligsnda akawa anamuangalia.
" Usimame kama sanamu ingia hapo ndani haraka.
" Alafu baada ya hapo ?
" Nitakwambia nini cha kufanya.
" Hela iko wapi?
" Ingia kitambulisho kuwa ni girl friend wa Derick utapokelewa na kupewa huduma.

ONE NIGHT WITH MY BOSS 5

MTUNZI SMILE SHINE

Sherry alimuangalia kwa mshangao maana hilo eno lilimshangaza.
" Unasemaje?
" Unataka nirudie kusema au?
" Imeanza lini mimi kuwa girl friend wako.
" Hapo ndipo unapochosha .
Wakiwa wanakimbizana alitoka dada mmoja anawafuata huku akiwa na tabasamu .
" Habari Derick
" Safi.
" Mbona mmesimama hapa?
" Aaah Zuwena huyu ndio mtu wangu niliekwambia fanya mambo tena fanya haraka.
" Sawa karibu dada.
Sherry alikuwa bado anashangaa shangaa Zuwena alimshika mkono wakaingia saloon.

Baada ya muda sherry alikuwa kashatengeneza nywele akapendeza.
Derick alipomuona aliachia tabasamu.
" Umependeza .
" Ni kweli nimependekeza lakini unanichanganya.
" Usichsnganyikiwe mrembo kuna kazi nataka unisaidie ukiisha hii basi tutakuwa tumemaliza na kwenye lile deni letu.
" Unamaanisha simu na ile elfu kumi?
" Ndio.
" Na haitakuwa unanisumbua na kunipa kazi ambazo sio zangu.
" Panda kwenye gari twende tukamalize zoezi letu. Aliongea Derick huku akiwa anafungua mlango wa gari na sherry akapanda wakaendelea na mizunguko yao.
Walinunua nguo na viatu vipya sherry akavaa na zile nguo zake akaweka kwenye mfuko.
Baada ya hapo waliondoka wakaenda kwenye hotel moja wakaenda kukaa kwenye meza moja na kuagiza vinywaji.
Sherry bado alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini yupo pale.
" Sasa tunafanya nini hapa?
" Hili swali umeniuliza mara nyingi sana na lina nikera mno. Sikiliza sherry tupo hapa kwaajili ya kazi moja tu tunatakiwa kuigiza kama vile wapenzi....
" Ina maana gani kufanya hivyo?
" Kuna mtu nataka kumrusha roho amenikataa akajua siwezi kuishi bila yeye sasa nataka kumuonyesha kuwa nina mpenzi mrembo zaidi yake.
Sherry alimuangalia dericz alafu akaangua kicheko alicheka kwa sauti mpaka kila mtu aliyekuwepo pale aligeuka kumuangalia.
Derick aliona aibu kila mtu alipokuwa anawaangalia.
" Shiiiiii sherry acha basi kila mtu anatuangalia .
Sherry aligeuka kuangalia akakuta watu wanamuangalia ikabidi atulie.
" Samahani boss unajua umenifurahisha alsana sikujua kama na wewe unapitia kwenye mambo kama haya yani bora niendelee kubaki mwenyewe mapenzi niwaache nyie.
" Inamaana huna mpenzi?
" Sijawahi kuwa nae na wala sitaki kuwa nae kwa sasa .
Derick aliona ajabu akauliza .
" Una miaka mingapi?
" Miaka 25 sasa.
" Siamini kwa jinsi ulivyo imeshatolewa siku nyingi sana.
" Sikulazimishi kuamini ukweli najua mimi.

Wakiwa katikati ya maongezi sherry alishangaa akasogea karibu yake na kuushika mkono wake na kumbusu Derick alikuwa amebadilika ghafla na kuwa romantic. Sherry alipopiga jicho pembeni aliona wasichana watatu wameingia huku wote wakiwa wanawaangalia ila mmoja ndio alikuwa akiwaangalia kwa jicho lisilo la kawaida akajua huyo ndio muhusika.
Derick aliongea kwa sauti ya chini.
" Unatakiwa kunipa ushirikiano ili tumalizane na deni letu.
Sherry aliposikia hivyo alianza kujichetua huku akitabasamu na kujionyesha kuwa yupo na mtu ambae wapo kwenye mahaba mazito kile kitendo kilimfanya yule msichana ashindwe kuvumilia alionekana kuteseka sana mwishowe aliwaacha wenzie na kuwafuata wakina Derick mezani kwao.
" Derick naomba tuongee.
Derick alimuangalia sherry alafu akamuuliza.
" Mpenzi ubaniruhusu niende nikamsikilize?
Sherry alimuangalia yule msichana kuanzia juu mpaka chini alafu akasema
" Sawa ila naomba usikawie mpenzi.
" Sawa baby. Alijibu Derick huku akisindikizwa na busu la shavu baada ya hapo alinyanyuka wakasogea pembeni na yule msichana.
" Niambie .
" Kwahiyo umekuja hapa kunionyesha kuwa upo kwenye penzi jipya?
Derick aliachia tabasamu kisha akasema
" Ukibisha ukasema sitaweza kupata mwanamke mrembo sasa nilitaka kukuonyesha kuwa utabiri wako haukuwa na maana nimepata mtoto bomba kama unavyomuona na ananipenda mpaka naumwa.
" Derick unamaana tumeachana kweli?
" Wewe ndio uliniacha ukaenda kwa yule mbeba vyuma wako.
" Ilikuwa bahati mbaya naomba tirudushe penzi letu najua bado tunapendana.
" Hapana kila wakati nimekuwa nikusanehe lakini sasa hii imefika mwisho acha niseme its over.
Alijibu Derick kwa jeuri kisha akarudi kwa sherry wakaendelea kuongea huku wakipiga story na kucheka.
Yule msichana aliamua kuondoka kabisa kwenye lile eneo huku wenzake wakimfuata nyuma huku wakicheka , Derick aliwaangalia na kuwapongeza kumbe ulikuwa ni mpango. Derick alipanga nao na kuwalipa ili walete pake hotelini ili kumrusha roho kwani Derick ilikuwa inaniuma sana kuachwa na mwanamke tena kwa madharau na maneno ya kejeri.
Derick alikuwa na furaha sana.
" Hatimae nimeshinda na moyo wangu una amani sasa.
" Sawa umefurahi na mimi deni langu limeisha na chuki zako juu yangu ziishe kuanzia sasa.
" Hivi unajua wewe mwenyewe ndio chanzo cha mimi kukuandama?
" Nimefanyaje?
" Mara nyingi Ulikuwa ukiniongelea vibaya bila kujua mimi ni mtu wa aina gani.
" Oooh samahani ile siku ya kwanza kukutana na wewe ilinifanya nilifikiri vibaya.
" Basi leo tumemaliza utata wetu tunatakiwa tufurahi zaidi.
" Sawa.
" Sasa hayo majuice weka pembeni hapa tunatakiwa kunywa wine, whisky.
" Hivyo ni vilevi sijawahi kutumia.
" Utakunywa kidogo....
" Hapana.
" Sikiliza basi nimalize kuongea. Kunywa utajisikia mchanga mfu yani fresh.
" Kweli.
" Ndio utakunywa kidogo tu ili uchangamke.
Sherry alikubali.
Derick aliagiza chupa ya wine wakawa wanakunywa huku story zikiendelea, sherry alinogewa na wine akajikuta anaendelea kunywa akajikuta analewa mapema . Derick bar alikuwa kashasnza kulewa baada ya muda kwenda aliamua kuchukua chumba akamchukua sherry wakaenda kwenye chumba cha hoteli. Alimlaza sherry kitandani nae akajitupia pembeni yake akawa anamuangalia.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote