Follow Channel

PACHA ALIYE LAANIWA

book cover og

Utangulizi

"Wewe ni mkosi na laana inayotembea. Hustahili kuishi kabisa. Nakuchukia sana Livia natamani ufe hata muda huu". Ni maneno yaliyotoka kinywani mwa mama yake mzazi aliyembeba tumboni kwake miezi tisa na alijifungua watoto mapacha ambaye ni Livia na Luna. Haijulikani kwanini mama yake anamchukia kupita kiasi licha ya yeye kumpenda sana mama yake. Hajui kwanini mama yake anamuita mkosi na mwenye laana kubwa, anafika mbali anataka livia afe. Bahati mbaya luna anakufa kwa kansa ila mama yao anaamini laana ya Livia ndiyo imemuuwa Luna. Kifo cha Luna kinamuuma sana mama yake maana kwenye akili yake alijihesabia ana mtoto mmoja tu ambaye ni Luna. Baada ya kifo cha Luna mama yao anaapia kumuuwa na Livia maana endapo ataendelea kuwa hai ataendelea kuleta mikosi kutokana na laana aliyo nayo. Hajali kuwa ndiye mtoto wake wa pekee aliyebaki nae anachotaka yeye Livia afe. Katika mateso na miangaiko anayopitia Livia anasaidiwa na kijana Allen lakini hali inakuwa mbaya tena baada ya mama Allen kugundua Livia ana mkosi na endapo ataendelea kuwa karibu na familia yake basi wataingia matatizoni na hata kumpoteza mwanae wa pekee Allen. Mama Allen anamuondoa Livia nyumbani kwake kwa siri hataki mwanae ajue........hii story nzuri sana na inafundisha pia......USIKUBALI IKUPITE

SIMULIZI : PACHA ALIYE LAANIWA
MTUNZI: NURU HALISI
SEHEMU 01

MWANZO.......
"najua Mama hanipendi...najua Mama hapendezwi na uwepo wangu, nitaondoka nyumbani nitaenda kuishi sehemu yoyote ile haijalishi nitafananishwa na mbwa au la lakini sitakaa nijitokeze mbele ya Mama" nilimuambia Luna (pacha wangu).

"sijakuita hapa kuzungumza habari za Mama wala Baba, nimekuita hapa tupate chakula cha pamoja....maisha ni mafupi sana Livia" Luna aliniambia huku akinifuta usoni.

"ndiyo maisha ni mafupi lakini Mimi na wewe tutaishi miaka mingi kuliko watu wote hapa..." nilimuambia Luna.
Luna alitabasamu tu hakunjibu chochote.

Baada ya kupata chakula Luna alinitembeza sehemu mbalimbali, pacha wangu ni bahili sana juu ya pesa zake lakini siku ya leo alininunulia vitu vingi mpaka ni kashangaa.

"pesa hutafutwa lakini mtu akishaondoka katika uso wa dunia ni ngumu kupatikana....hivyo furahia vitu vyote nilivyo kupatia leo" Luna alizungumza.

Maneno ya Luna niliyaacha yapite, furaha niliyokuwa nayo juu vitu alivyoninunulia ilikuwa kubwa sana.

"hupaswi kuishi na makasiriko, najua Mama anakupenda angekuwa hakupendi angekuua ukiwa mdogo" Luna aliniambia.

"muda wowote mvua inaweza kunyesha twende nyumbani..." nilimuambia Luna baada ya kuona anazungumza maneno mengi.
tuliondoka tukaelekea nyumbani....baada ya kufika tu Mama alizungumza maneno ya kuumiza.

"Luna nilishakukataza kuambatana na Livia hakuna kitu unapata zaidi kuchukua laana zake tu..." Mama alizungumza
Luna hakujibu chochote alipitiliza chumbani kwake.

nilienda chumbani kwangu pia kauli ya Mama iliniumiza sana, furaha niliyokuwa nayo juu ya zawadi ilipotea.
nilianza kucheza gemu kwenye simu baada ya kuchoka niliamua kulala.
nililala usingizi mzito kuliko siku zote, kama si Mama kuja kunigongea huenda ningelala mpaka mchana.

"amka ukamuamshe Luna Mimi na muamsha lakini haamki..." Mama aliniambia akionekana kuwa mwenye hofu kubwa.

niliamka ni kaenda chumbani kwa Luna nilimuamsha lakini Luna hakuamka, kitu kilichonishtua ni ubaridi uliokuwa umetawala mwili wa pacha yangu.

"tumpeleke hospital..." nilimuambia Mama
Mama alikubaliana na Mimi tulianza harakati za kumnyanyua Luna, nilijikuta ni kiogopa zaidi kwa sababu mwili wa Luna ulikuwa umekakamaa sana.siyo kukakamaa tu hata pumzi zake zilikuwa hazitoki

"umemfanyaje Luna kwanini mwili wake umekakamaa" Mama aliniuliza kwa sauti ya uoga hivi.
sikujua nimjibu kitu gani kwa wakati huo
Mama alianza kunihoji kwa sauti ya ukali ikiambatana na kilio.Baba alikuja alitukuta katika hali ya kutoelewana

"mume wangu Luna haamki...haamki kabisa..." Mama alizungumza kwa majonzi
Mimi pia nilijua kitu gani kinaendelea....nililia sana machozi ya uchungu kwa sababu ni siku ya jana tu nilikuwa na Luna.

Baba alimpigia simu dreva wake, aliwapigia pia ndugu zake aliwapa habari juu ya msiba
Mama alizidi kunitaka nimuamshe Luna, sikuwa ni kimjali kwa sababu nilikuwa katika maumivu makubwa.

Ndugu zake Baba walifika hivyo Luna alipelekwa mochwari
ndugu wa Mama walifika pia walisaidia kuandaa mazingira ya msiba, nilijifungia chumbani kwa Luna japo Mama alinitaka nitoke kwenye chumba cha binti yake lakini sikufanya hivyo.

nilianza kukagua vitu vya Luna akili yangu iliniambia kuna kitu hakipo sawa
nilikutana na vidonge vingi sana vikiwa vimetupwa tu uvunguni mwa kitanda sikujua vile vidonge vilikuwa na maana gani
nilishika diary ya Luna nilianza kuikagua...nilikutana na maneno ya kuumiza sana.

Pacha wangu Mimi alikuwa akisumbuliwa na Cancer haikuwa Cancer ya muda mfupi...ni wazi kabisa ugonjwa wake ulikuwa ni wa muda mrefu pengine ndio sababu Mama alimjali sana Luna
nililia kwa uchungu mkubwa....Mama aliendelea kunitaka nitoke chumbani kwa Luna
nilitoka nikiwa mwenye hasira.

"kwanini hukuwahi kuniambia kama Luna ni mgonjwa...." nilimuuliza Mama

"kama ningekuambia ugonjwa wa Luna huenda angekufa mapema....na kuchukia sana Livia siku ya jana hukupaswa kuambatana na mwanangu, angalia sasa umemuua...." Mama alizungumza kwa uchungu.

nilijikuta ni kimhurumia kwa sababu maneno yake yalitoka kabisa ndani ya moyo hakuwa akiigiza.

Mamkubwa alinishauri niondoke, aliniambia nijitahidi kukaa mbali na Mama mpaka msiba utakapoisha.

nilizingatia ushauri wa Mama mkubwa...kwa kipindi chote cha msiba nilijitahidi kukaa mbali na Mama.

Mama yangu hakuweza hata kumpumzisha Luna kwa sababu alikuwa ni mtu wa kuzimia zimia.

Baada Ya Mwezi Kupita
Maisha yaliendelea kama kawaida, hali ya Mama haikuwa nzuri kusema...biashara za Baba ziliyumba sana kiasi kwamba kila mara yeye na Mama hawakuisha kugombana.

"naomba upunguze matumizi ya pesa, mke wangu kwa sasa umeshakuwa mtu mzima mambo ya saluni waachie watoto wadogo..."

"kila mwanamke anayepita mbele yako humuachi salama...kwanini usipunguze kwanza umalaya wako ndio useme na Mimi, Livia amekuwa akitumia pesa vibaya kwanini yeye humsemi...hakika nimechoka kukaa hapa" nilimsikia Mama akilalamika.

"Mama yangu ni mgonjwa nitafurahi endapo utaenda kumuuguza...Livia pia ataambatana na wewe nahitaji kurekebisha sehemu niliyokosea sitachukua muda mrefu" Baba alizungumza

"nitaenda lakini siwezi kuambatana na Livia".

"ni mtoto wako pia acha kuzungumza maneno ya ajabu....narudia kusema utaondoka na Livia".

"sawa nitaondoka naye..." Mama alijibu kwa haraka.

mazungumzo yao yaliishia pale, ndipo Baba alishtuka baada ya kuniona lakini Mama hakujali aliniambia nijiandae tunaondoka mida ya mchana, nilienda kujiandaa, Baba alitupeleka mpaka stendi kisha akarudi.

"tunaenda Mah..." Mama alizungumza.

"Baba kasema tunaenda kwa Bibi...".

"twende Mah kwanza Mimi na wewe tunahitaji kumaliza tofauti zetu, najua sijawa Mama bora kwako..." Mama alizungumza kwa upole sana
nilifuata Mama alivyosema tulipanda Meli tayari kwa kuelekea Mah.

pamoja na kwamba Mama alikuwa akizungumza na Mimi kwa upendo, moyo wangu haukuwa na amani kabisa.... pengine ni kwa sababu sikuwahi kupanda Meli kubwa kama hii....hakika sikupata majibu.........ITAENDELEA.......

SIMULIZI : PACHA ALIYE LAANIWA
MTUNZI: NURU HALISI
SEHEMU 02

ENDELEA......
Giza lilianza kuingia taratibu, bado safari ilikuwa ndefu.

"tutatumia siku tatu kufika Mah, najua hii safari imekuwa ngumu ni samehe kwa hilo tungeweza kupanda ndege lakini akili yangu haipo sawa nahitaji kutazama maji kama hivi" Mama alizungumza.

"ni mara yangu ya kwanza kupanda Meli hakika nimefurahi sana" nilimuambia Mama.

"nahitaji kukaa sehemu nzuri kwa ajili ya kupata chakula, hii Meli ni ya kipekee watu wenye kipato cha chini hawawezi kumudu....twende mwanangu tukale" Mama alizungumza.

niliambatana na Mama, Meli hii ilinishangaza ilikuwa na hotel pamoja na sehemu ya kukaa kupiga story...tulipata chakula baada ya hapo tulitafuta sehemu nzuri tukakaa.

Mama alinisimulia mambo mengi yaliyomhusu yeye mwisho aliniambia kitu cha kushangaza
"nilikaa na Baba yako mwaka mzima bila kushika ujauzito, ndugu zake walianza kuzungumza sikutaka nimpoteze Baba yako....nilienda kwa mganga kupata usaidizi kwa sababu hospitalini sikupata msaada.....nilifanikiwa kupata ujauzito kupitia mganga wa kienyeji" Mama alizungumza kisha akatulia kidogo na mimi nilikuwa makini kumsikiliza.

"pamoja na kupata ujauzito sikuacha kwenda kwa yule Mganga.....siku moja nilienda nikiwa nimekunywa pombe nilikuwa na mawazo sana, nilimfuma Baba yako akiwa na rafiki yangu hivyo nilijikuta ni kinywa pombe bila kudhamiria... yule Mganga alikasirika sana baada ya kujua nimekunywa pombe alidai nimemharibia kazi yake, alinipatia laana juu ya watoto waliokuwa tumboni kwangu...na yakumbuka maneno yake vizuri alisema mtoto mmoja atazaliwa na laana itakayo muua mwenzake.....ataisababishia familia yake umasikini na kila mwanaume atakaye kuwa naye atakufa....." Mama alizungumza.

Sikujua ni zungumze kitu gani kwa sababu alikuwa akinisema Mimi, mara nyingi amekuwa akinilaumu kuwa nina laana.

"umemuua Luna, biashara za Baba yako zimeanza kuyumba hakika naumia sana Livia....nimejaribu kukutolea hiyo laana lakini imeshindikana kwa sababu mtu aliye kulaani alikufa ile siku niliyoenda nikiwa nimelewa.....natamani ufe pia" Mama alizungumza akiwa kanikazia macho.

Kuna vijana wawili walikuja sehemu tuliyokuwa tumekaa, niliwakumbuka vizuri ni vijana ambao tulipanda nao Meli toka Mini.....ghafla tu mmoja wao alinifunga mdomo kwa mkono wake.

"mtupeni baharini sasa hivi...sipo tayari kuishi na mtoto ambaye ni tishio kwa familia yangu" nilimsikia Mama akizungumza eti wanitupe baharini
nilihisi nimechomwa na kitu mgongoni mfano wa sindano.

"haitapita nusu saa atakufa hii sindano imewekwa sumu" mmoja wa vijana wale alizungumza.

Mama alinitega mgongo hakutaka hata kunitazama.huwezi amini nilitupwa baharini mfano wa jiwe.
kwa mshtuko niliokuwa nimeupata sikuweza hata kupiga kelele..nilifumba macho yangu tayari kwa kufa, sikuwa ni kijua kuogelea hivyo nilikunywa maji bila kutaka
sikumbuki nini kilitokea lakini nilikuja kushtuka nikiwa nimelala katika chumba kidogo
nilijaribu kukumbuka nimefikaje hapa lakini sikuweza.

"bora umeamka.... Allen amekuwa akinifokea sana kisa amenilipa vipesa vyake vya mawazo, naenda zangu kaa hapa hapa atakukuta...wiki nzima umelala kitandani nimepoteza muda wangu kukuhudumia wewe...mahusiano yangu yameingia doa nipo na hasira" binti aliyeonekana kuwa nurse alizungumza kisha akaondoka.

Sikuweza hata kumuuliza chochote, kichwa changu kilizidi kuuma kwa sababu nilikuwa na kilazimisha kukumbuka vitu bila mafanikio....nilishuka kitandani ni kafungua mlango sikujua hata naenda wapi.

"umeamka ..." nilisikia sauti ya kiume
niligeuka mkono wangu wa kushoto ndipo nilifanikiwa kumuona kijana mmoja
sikuwa ni kimfahamu....kichwa changu kilianza kuuma kwa sababu nilitaka kiniambie huyu kijana ni nani.

"unaitwa nani..." kijana huyu aliniuliza.

"naitwa Livia...."

"kwenu ni wapi...."

swali lake lilikuwa gumu sikuwa ni kijua chochote kuhusu kwetu.

"matarajio yangu yalikuwa sahihi sumu niliyoitoa mwilini mwako ilikuwa kali sana, kwa kuwa jina lako unalikumbuka basi itakuwa rahisi kurejesha kumbukumbu zako zote....Mimi ni Daktari naitwa Allen, nimekuokota pembezoni mwa bahari ya Mah.... pengine bado kifo hakija kuhitaji ndio maana umenusurika kufa....." Allen alizungumza.

Maneno yake yalinishangaza sana
"nitakupeleka kwetu....Mama yangu ni mtu mwenye kisirani kwa kuwa huna sehemu ya kwenda itabidi uvumilie kisirani chake, kitu kingine usizungumze kwa mtu yoyote kuwa umepoteza kumbukumbu huenda wakakutumia vibaya" Allen alizungumza.

kwa kuwa sikuwa na sehemu ya kwenda niliondoka na Allen mpaka kwao
nyumba yao ilikuwa nzuri sana pengine ni kwa sababu Allen alikuwa na kazi nzuri
tuliingia mpaka sebuleni, kuna mwanamke alikuwa akifanya usafi baada ya kutuona aliacha.

"kazi za humu ndani zinachosha, sitaki kujua huyo ni house girl au ombaomba naomba anisaidie kwanza kuosha vyombo kule jikoni baada ya hapo ndio tutazungumza" yule mwanamke alizungumza.

"nitaenda kuosha vyombo Mpenzi wangu yupo na matatizo mengi anahitaji kupumzika" Allen alizungumza.

nilijikuta ni kimtazama kwa macho makubwa kwa sababu hatukuwa na uhusiano.

"na yule uliyenionesha kwenye simu ni nani....mwanangu umezidi umalaya mara nyingi na kuambia tafuta mke haunisikii, una sikia binti mwanangu Mimi ni Malaya ana badilisha sana wanawake hivyo usisikilize maneno yake kama amekuleta hapa kula na kunywa sawa, lakini kama kakuambia juu ya ndoa ana kudanganya...." Mama yake Allen alizungumza kisha akaendelea na kazi yake.

Allen alinichukua mpaka chumbani kwake.... kitandani kulikuwa na chupi za kike
Allen aliona aibu alizifunika funika huku akijitetea
"mara nyingi nawasaidia mabinti ila shida zao zikiisha wanaondoka hivi mpaka nguo zao za ndani wananiachia" Allen alizungumza
nilitabasamu tu kwa sababu alionekana kuongopa.

"utakaa hapa mpaka pale kumbukumbu zako zitakaporejea....mara nyingi sishindi nyumbani kazi yangu inanibana sana naweza maliza wiki nzima sipo hapa hivyo naomba uvumilie....kama nilivyokuambia Mama yangu ni mtu mwenye kisirani sana lakini akikupenda ni mtu mzuri... na kuahidi utapona na utarejea kwenu"
kabla sijamjibu Allen chochote, Mama yake aliniita.

"binti mgeni njoo unisaidie kukata mboga huku jikoni achana na huyo Malaya"
Allen aliniambia ni pumzike, sikutaka kumkera Mama yake nilienda kumsaidia........ITAENDELEA........

SIMULIZI : PACHA ALIYELAANIWA
MTUNZI : NURU HALISI
SEHEMU 03

ENDELEA....
Nilianza kumsaidia kukata mboga
"at least wewe unajua hata kukata mboga kuna binti huwa anakuja hapa hajui chochote zaidi ya kunitazama" Mama yake Allen alizungumza.

"si kila mtu amekua kwenye mazingira ya kufanya kazi..." nilimuambia Mama yake Allen.

"siwezi kukubali hata siku moja Allen aoe mwanamke asiyejua kazi, sasa hivi nipo kimya kwa sababu bado Allen anatapa tapa ila litakapokuja swala la kuoa nitaongea sana...."

"Mimi siyo Mpenzi wa Allen kanisaidia tu kwa kuwa sina sehemu ya kwenda nitafanya kazi zote za hapa" nilimuambia Mama yake Allen.

"hata Mimi nilijua tu wewe si Mpenzi wake Allen, kwa kuwa umesema kwa mdomo wako basi utakaa hapa kwa amani Mimi sina shida kabisa....tena nitakupatia chumba chako sitaki ulale kule kwa Allen si muamini kabisa..." Mama yake Allen alizungumza.

huo ndio ulikuwa mwanzo wa mahusiano mazuri kati yangu na Mama ya Allen, alinipenda sana kwa sababu nilikuwa muongeaji na kuhusu swala la kazi za ndani kwangu haikuwa tatizo nilifanya kazi zote bila kinyongo....kitu kingine Mama yake Allen alikuwa ni mtu mzima hivyo alihitaji kupumzika.

"jiandae baadae tutaenda kununua vitu vya ndani..." Mama yake Allen aliniambia
niliingia bafuni kuoga, muda ulivyofika tuliondoka.
tuliingia sokoni tulinunua mahitaji muhimu ya ndani tuliviweka vitu ndani ya gari kisha tukaanza kuzunguka tena.

"nunua chochote unachotaka nitalipia....mie napenda urembo sana japo nimezeeka lakini vitu kama hereni sijui make-up huwa havinipiti...." Mama yake Allen alizungumza
sikuvunga nilichagua make-up pia kwa sababu nilikuwa napenda urembo.

wakati tunatoka tuliona watu wamerundikana kwenye kibanda kidogo hivi, tulisogea tuone kitu gani kinaendelea.

"kuna mwanamke hapa ni Msoma nyota lipia pesa akuambie vitu vinavyo kuhusu" binti mmoja aliniambia huku machozi yakimlenga lenga bila shaka alitoka kuambiwa mambo yake.

"huwa napenda vitu kama hivi acha nilipie pesa ni kasikilize..nikitoka na wewe utaenda pia...." Mama yake Allen alizungumza kisha akaingia ndani ya kile kibanda.

Nikiwa na msubiria nje nilisikia watu wakimsifia Msoma nyota kwa kazi zake za uhakika
Mama yake Allen alitoka baada ya dakika 20 ndipo na Mimi niliingia.

"wewe ni yai bovu, kuku aliyekutaga alipaswa akuangamize kabla ya kutotolewa..." Msoma nyota alizungumza baada ya kushika mkono wangu.nilitaka kuzungumza lakini alinizuia.

"wewe ni mjane hujaandikiwa kuishi na mume, kila mwanaume atakaye kupenda atakufa, familia ya huyo mwanaume itaangamia.... mwisho familia yako itapoteza kila kitu itaishi kwa ugumu kama mbwa koko waishivyo....." Msoma nyota alizungumza kisha akanisogelea.

"laana uliyonayo mwilini mwako ndio ilimuua pacha wako.....laana yako ni nyeusi haiwezi kung'aa hata kama ikioshwa kwa maji ya dhahabu..... siwezi kukusaidia katika hili, ondoka" Msoma nyota alizungumza.

"sielewi una zungumza kitu gani, Mimi hapa nimepoteza kumbukumbu zangu je, unaweza kunisaidia niweze kukumbuka...."

"nimesema siwezi kukusaidia chochote fanya kuondoka....tena usije kuzungumza haya maneno niliyokueleza kwa mtu yoyote kwa sababu watakuua....." Msoma nyota alizungumza kwa ukali.
niliondoka nikiwa sielewi vitu gani kanieleza.

"yule si tapeli kaniambia kila kitu nilichowahi kukutana nacho....kakueleza kitu gani" Mama yake Allen aliniuliza.

"Mimi kanidanganya, kaniambia nina watoto watatu wakati sina mtoto hata mmoja" nilimdanganya Mama yake Allen

"achana naye....funga mlango tuondoke nishaanza kupata njaa"

nilifunga mlango wa gari kisha Mama yake Allen aliondoa gari,
maneno ya yule Msoma nyota yalinikaa sana kichwani kiasi kwamba sikuwa ni kiyaelewa maneno ya Mama Allen.

Tulifika nyumbani, nilimuomba Mama yake Allen ni pumzike
aliniruhusu hivyo nilipanda kitandani, nikiwa kitandani nilianza kusika sauti
ya mwanamke ikinifokea kuwa Mimi ni mkosi hivyo ni kae mbali na Luna
kichwa kilianza kuniuma sana
mlango wangu uligongwa kwa maumivu niliyokuwa na yapata sikuweza hata kuamka
sikumbuki nini kilitokea lakini nilikuja kushtuka nikiwa hospital, Allen alikuwa kasimama alionekana kutafakari mambo mengi.

"Allen nini kimenipata...." nilimuuliza Allen.

"sijui pia, ni kuulize kitu gani kimekutokea maana Mama alinipigia simu kuwa umezimia... "

"kuna sauti ilikuwa inanifokea...sijui ni sauti ya nani imeniumiza kichwa sana pengine ndio sababu nilipoteza fahamu"

"Livia, na kuhakikishia utakumbuka kila kitu.....wiki hii nitakuwa free hivyo nitautumia huo muda kukusaidia ukumbuke kila kitu...."

"nitakulipa fidia pindi nitakapopona..."

"ni mapema sana Livia, haipendezi kuanza kuweka ahadi...." Allen alizungumza
simu yake ilianza kuita alipokea.

"namtuma dreva tax aje kukuchukua....kuwa na amani tutaonana baada ya nusu saa hivi, okay I love you too" Allen alizungumza kisha akakata simu.

"utapumzika kama masaa manne hivi...Mama kasema atakuja kukuchukua, nafikiri tutaonana jioni kuna mtu muhimu nahitaji kuonana naye..." Allen aliniambia
nilimkubalizia kisha akaondoka...dakika mbili hazikupita alirudi tena.

"hebu niambie kuna haja ya kupita saluni...vipi hili shati ni badilishe au liko sawa.." Allen aliniuliza ni wazi kabisa alikuwa anaenda kuonana na Mpenzi wake.

"upo sawa hauna haja ya kupita saluni..."

"ahsante na samahani kwa usumbufu" Allen alizungumza kisha akaondoka,
nilikaa hospital kwa masaa manne, Mama yake Allen alikuja kunichukua alinipa pole kwa kilichonitokea.

"Mama leo una furaha sana, niambie kuna nini" nilimuuliza Mama yake Allen.

"siku zote Allen amekuwa akiniletea wanawake wa ajabu, siku ya leo kaniletea mwanamke mwenye heshima zake....tena si Mwanamke wa kuletwa tu ni Mchumba wake na pete walisha valishana, kama Mama hiki kitu kimenivutia sana".

"ni jambo la heri nimefurahi pia...." nilimuambia Mama yake Allen
kwa pamoja tuliondoka baada ya utararibu kufanyika.

Tulifika nyumbani kulikuwa kuna nukia vizuri ilikuwa ni harufu ya chakula
"oh umerudi.." Mdada aliyekuwa amekaa sebuleni alizungumza.

"ndiyo Tina, huyu anaitwa Livia, Livia huyu anaitwa Tina ni Mchumba wa Allen" Mama Allen alifanya utambulisho, kwa pamoja tulisalimiana.

Muda wa chakula ulifika tulipata chakula kwa pamoja kama familia
kwa haraka niligundua Allen na Tina wanapendana sana na wapo serious na uhusiano wao.
wakati na kula kuna sauti iliniijia kichwani, ilikuwa ni sauti ile ile niliyosikia ikiniambia Mimi ni mkosi ni kae mbali na Luna
kwa wakati huu ilinishtumu kuwa nimemuua Luna....siyo hivyo tu kuna taswira ya Mwanamke iliniijia akiwa amekaa na Mimi kwenye Meli
kichwa changu kilianza kuuma sana, niliondoka sebuleni ni kaelekea chumbani kwangu
Allen alinifuata, alinipatia dawa za kutuliza maumivu.

"kuna sindano nilikuchoma mwezi mmoja uliopita nahisi imeanza kufanya kazi, kwa sasa kila kitakacho kuwa kina kuijia kichwani jitahidi kukiandika kwenye diary naamini itakuwa msaada mzuri kwako.... sikuweza kumficha Mama juu ya hali yako ila Tina hafahamu, tofauti na Mama sitaki mtu mwingine afahamu hali yako huenda wakakutumia vibaya.....pumzika kwanza" Allen alizungumza.

Nilimshukuru kwa ukarimu wake, baada ya Allen kuondoka nilipanda kitandani ni kalala.

Maisha yaliendelea kama kawaida, mwanzoni Tina alikuwa ni mtu wa kupenda kuzungumza na Mimi lakini kadri siku zilivyozidi kwenda alipunguza mazoea na Mimi,
sikumjali sana nilihisi huenda akawa mjamzito hata Mama yake Allen alifikiria hivyo
jioni moja Allen aliniletea nakala iliyokuwa na tangazo la kazi kabla hata sijaisoma Tina alikuja chumbani kwangu,

"nipatie hiyo nakala uliyopewa na Allen" Tina alizungumza akiwa kasimama.
Nilifanya kama alivyotaka cha ajabu aliichana kisha akanitazama kwa macho makubwa

"naomba upunguze mazoea na Allen kuanzia sasa, kila muda Allen amekuwa ni mtu wa kukuzungumza wewe hii hali inanikera sana hata kama unaishi hapa kwa msaada haimaanishi sasa kila muda watu wakuhurumie nadhani tumeelewana" Tina alizungumza kwa ukali.

Sikuweza kumjibu chochote, alinitazama kwa muda kisha akaondoka huku akiachia sonyo kubwa......ITAENDELEA.......

SIMULIZI : PACHA ALIYE LAANIWA 04
MTUNZI: NURU HALISI
SEHEMU 04

ENDELEA......
Siku iliyofuatia niliwahi sana kuamka kwa sababu sikuwa na usingizi
nilifanya kazi zote kama kawaida yangu... nilienda jikoni kuandaa chai ndipo Tina alikuja.

"umefanya kazi zote pekee yako wengine tutafanya kazi gani sasa....punguza kujipendekeza kwa Mama Allen hakuna kitu kitabadilika" Tina alizungumza,
nilikaa kimya kwa sababu sikuwa na jibu la kumpa.

"ukimaliza kuandaa chai njoo uniite nitakuwa barazani ni kisoma kitabu" Tina alizungumza kisha akaondoka.

nilifahamu fika anahitaji ugomvi na Mimi kwa kuwa sikuwa na sehemu ya kwenda sikuhitaji kabisa kujibizana naye.

Niliweka chai mezani kisha ni kaenda kuwa karibisha wote, hata Tina pia aliyekuwa barazani akisoma kitabu nilienda kumkaribisha
tulikusanyika wote mezani.

"nakala niliyokupatia jana uliifanyia kazi" Allen aliniuliza.

"ni muda wa chai mtazungumza baadae" Tina alimkatisha Allen

ukimya ulipita tuliendelea kunywa chai

"Ahsante kwa chai..." Mama Allen alizungumza kisha akaondoka hakuwa muongeaji sana siku hiyo.
Baada ya kumaliza kunywa chai niliondoka pia, nilimuacha Tina na Allen
sikujisikia kukaa ndani akili yangu ilikuwa ikiwaza mambo mengi sana hivyo niliamua kuzunguka zunguka mjini.

Nikiwa na tembea nilisikia mtu akiniita kwa jina langu niligeuka, nilikutana na Mwanamke sikuwa ni kimfahamu hata kidogo

"Livia....." yule Mwanamke aliniita kwa mshangao
"una ni fahamu Mimi" nilimuuliza
"una mkumbuka yule Mwanamke aliyekuwa ana waletea mboga za majani nyumbani kwenu" aliniuliza
nilitikisa kichwa kuashiria sikumbuki

"mara nyingi Mama yako alikuwa hataki unisalimie hivyo si rahisi kunikumbuka, nilisikia ulimtoroka Mama yako mkiwa safarini.....sijui ni kitu gani kilikupata lakini ni busara kama utarudi Maana wazazi wako wana kutafuta sana hasa baba yako..." Mwanamke ni siye mfahamu alizungumza.

"muda ukifika nitarudi kwa sasa nipo na tafuta maisha" nilimuambia huyu Mmama japo nilikuwa sielewi kitu gani ana zungumza lakini sikutaka afahamu kama Mimi sina kumbukumbu.
Tuliagana baada ya kumaliza mazungumzo....nilipata kujua kwetu ni Mini na wazazi wangu wapo hai hiki kitu kilinifurahisha
kuna sehemu nilipita niliona tangazo la kazi, ningeweza kuomba kazi ya kufanya usafi kwenye ofisi lakini sikuwa na vigezo
nilitembea sana mtaani baada ya kuchoka nilirudi nyumbani.
baada tu ya kuingia sebuleni nilikutana na kelele.

Allen na Tina walikuwa wakibishana, nilisikiliza kwa umakini ndipo niligundua tatizo ni Mimi.

"kama Livia hawezi kuondoka hapa basi Mimi nitaondoka....umekuwa ni mtu wa kufikiria maisha ya Livia, umeniita hapa kwa ajili ya harusi lakini mwezi umeisha sioni chochote...."

"Tina unanikosea mbali na kuwa Mpenzi wako Mimi ni Daktari ni wajibu wangu kujali afya za watu, hebu nipe mwezi mmoja nimsaidie Livia akishapona Mimi na wewe tutaendelea na ratiba yetu, mara ngapi na kuambia sina hisia na Livia kwanini hutaki kunielewa"

"niambie kitu kinachomsumbua Livia kama kweli unaniamini..."

"na kuamini lakini kazi yangu inanifunga siwezi kutoa siri za wagonjwa...."

"unanitania ngoja niondoke labda utafanya maamuzi" nilimsikia Tina akizungumza
sikuwa tayari kuona mahusiano ya watu yana vunjika kisa Mimi....niliamua kuingia chumbani kwao bila hodi

"Allen, ni haki ya Tina kuwa na wivu juu yako....nimekaa hapa kwa muda mrefu bila kuchangia hata mia, ni wakati wa Mimi kuondoka kuhusu hali yangu usijali na amini kila kitu kitakuwa sawa... naomba usinikatalie katika hili" nilimuambia Allen.

"afya yako ni muhimu kuliko hata huu ugomvi, naomba uende chumbani kwako Mimi na Tina tutamalizana " Allen alizungumza.
sikutaka kuzungumza tena niliondoka nikiwa najua nini napaswa kufanya.

nilienda chumbani kwangu nilimkuta Mama yake Allen akikunja nguo zangu
"nilikuambia napenda kusikia hadithi za yule Msoma nyota.... nilienda kumtembelea baada ya kupata chai" Mama yake Allen alizungumza
nilimsikiliza sikujua anataka kuzungumza kitu gani.

"naomba urudi nyumbani kwenu, yule Msoma nyota kaniambia kwenu ni Mini naamini ukifika kule watu watakutambua na watakupeleka kwenu, sitaki familia yangu iingie matatizoni kwa sababu yako.... naomba unisamehe kwa sababu na kufukuza bila kufikiria hali uliyonayo, pole kwa hali unayopitia naamini siku moja utapata ufumbuzi wa tatizo lako" Mama yake Allen alizungumza bila kunitazama machoni.

"sikumbuki chochote pengine kumbukumbu zangu zikirudi nitaelewa nini una zungumza, nilikuwa na mpango pia wa kuondoka hivyo naomba usijisikie vibaya katika hili". nilimuambia Mama yake Allen
tuliongea mengi sana, baada ya kuelewana alinisindikiza kimya kimya...nililala hotelin kwa sababu nisingeweza kupata Meli kwa wakati huo
usiku mzima niliyatafakari maneno ya Mama Allen.

sikumbuki hata nililala saa ngapi lakini nilikuja kushtuka kukiwa kumekucha
nilisogea mpaka kivukoni ambako Meli inayoelekea Mini ilikuwa inapatikana
nilikata tiketi kisha ni kakaa kusubiri Meli ifike

"una fanya nini hapa" sauti ya Allen ilinishtua
niligeuka kwa haraka kweli alikuwa ni Allen
Allen alinilaumu sana kwa kuondoka bila kumuambia chochote.

"sijakumbuka chochote lakini naamini ni kirudi Mini nitakumbuka naomba usijali kuhusu hili"

"sielewi na shida gani katika moyo wangu naomba usiondoke Livia...." Allen alizungumza.

"siku moja nitarudi kuwa salimia hivyo naomba uwe na amani...."
tuliongea mengi na Allen mwisho alikubali niondoke.
Meli ilifika, Allen aliniaga kwa maumivu makubwa, niliingia kwenye Meli baada ya kuonesha tiketi
safari ilianza, watu walikuwa bize na mambo yao
sikuwa na simu hivyo nilijikuta ni kichoka kukaa tu.

ghafla nilisikia mlio wa risasi...watu wote tulitulia, mlio wa risasi ulijirudia tena
"Meli imetekwa na Maharamia" tangazo lilisikika
hofu iliniingia, watu walianza kujirusha kwenye maji ovyo
nikiwa sijui ni fanyeje kichwa kilianza kuuma, nilijikuta ni kikumbuka matukio mengi sana
hakika nilikumbuka vitu vingi sana...kwa ufupi kumbukumbu zangu zilirejea sikuwa ni kijua kuogelea lakini nilijirusha kwenye maji sikuwa ni kitamani kuishi nilihitaji kufa
nilihitaji kwenda kumueleza Luna kuwa mwanamke aliyenileta duniani alinitendea unyama wa hali ya juu....

sikumbuki ilikuaje lakini nilikuja kushtuka nikiwa kwenye chumba chenye mandhari mazuri.
Niligeuza macho yangu huku na kule ndipo nilifanikiwa kumuona Allen.

"ungeniacha ni kafa kwanini umekuwa na kiherehere cha kuniokoa kila wakati..." nilimuuliza Allen kwa ukali.

"acha kuzungumza maneno mengi ishukuru bahari kwa kukuacha hai kwa mara nyingine..."
ukimya ulipita kama dakika mbili hivi.

"nahitaji kwenda Mini..... naomba unisaidie nifike Mini lakini si kwa kupanda Meli...." nilimuambia Allen baada ya akili yangu kukaa sawa

"utasafiri na wanajeshi wa Mah siku ya kesho, ningesema upande ndege lakini huna passport.....nitakusindikiza pia sitakuacha uende pekee yako...." Allen alizungumza
ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu aliingia Tina akiwa kakunja sura yake
kwa pamoja tulibaki kumtazama.........Hii story ni nzuri sana alafu ndefu pia.........
SIMULIZI : PACHA ALIYE LAANIWA
MTUNZI: NURU HALISI
SEHEMU 05

ENDELEA.......
"Allen hapa ndio kazini...." Tina aliuliza kwa ukali.

"kuna tatizo lilitokea nitakuelezea baadae".

"tatizo? tatizo mkiwa katika chumba kizuri kama hiki tena Livia amekaa kwa kujiachia namna hiyo....nyie wawili ni wasaliti mmekuwa mkinichoma kisu kila ni kiwatega mgongo... Allen siwezi kuvumilia huu usaliti kwa kuwa umeamua kumchagua Livia badala yangu naomba uendelee naye Mimi nitarudi kwetu" Tina alizungumza kwa uchungu.

Sikujua ni zungumze kitu gani kwa sababu hakuna baya lolote lililokuwa likiendelea kati yangu na Allen.

Allen alimshika mkono Tina akamtoa nje sijui walienda kuzungumza vitu gani lakini Allen alirudi pekee yake

"Tina ana wivu sana naomba usiya zingatie maneno yote aliyo ya zungumza....siku ya kesho Tina atakusindikiza Mimi nitaendelea na ratiba zangu naomba ujisikie amani, jioni atakuja hapa mtalala wote..." Allen alizungumza
sikuona shida kabisa nilichokuwa na hitaji Mimi ni kurudi nyumbani na si kitu kingine
Allen aliondoka.....mida ya jioni Tina alirudi alikuwa kachangamka sana, aliniomba msamaha kwa kunifikiria vibaya
tuliongea mambo mengi sana, Tina alinisimulia jinsi walivyokutana na Allen
ilikuwa ni hadithi nzuri sana
usiku ulivowadia tulilala.... na kulipo pambazuka Mimi na Tina tulijiandaa.

"tutapanda gari la kawaida, tutakutana na Wanajeshi kwa mbele kidogo" Tina alizungumza
nilimkubalizia lakini moyo wangu ulianza kuwa na hofu kubwa sana.... nilijitahidi kuipuuza hofu niliyokuwa nayo lakini haikusaidia, nilianza mpaka kutetemeka

"nilisahau kukununulia koti mida ya asubuhi huwa kuna baridi kali sana lakini usijali tumekaribia kuwafikia Wanajeshi ..." Tina alizungumza.

nilimkubalizia kwa kichwa....katikati ya safari dreva alisimamisha gari alidai kuna tatizo limejitokeza hivyo alitutaka wote tushuke
kwa pamoja tulishuka, dreva alianza kukagua kagua tairi za gari huku akituongelesha

kuna vijana wawili wakiwa na pikipiki walitukaribia
walianza kuzungumza na dreva wetu, lakini ghafla wale vijana waliokuwa kwenye pikipiki walinikamata
"mfungeni sehemu ambayo hakuna mtu ataweza kumuona hili pori ni kubwa sana hakikisheni haonekani.....msimpige wala kumfanyia ubaya wowote, nahitaji afe taratibu bila maumivu yoyote" Tina alizungumza.

sikuweza kuamini kabisa...kwa jinsi tulivyo zungumza usiku wa jana kwa upendo Tina asingeweza kunitendea hivi.

"kwanini unanifanyia hivi Tina...."

"Mimi siyo mpuuzi kama mnavyo fikiria, siwezi kukuacha uendelee kuwa doa kwenye mahusiano yangu....utakufa kifo cha taratibu nitamuambia Allen ulifanikiwa kuondoka na Wanajeshi hivyo usihofu kuhusu hilo" Tina alizungumza kisha akaingia kwenye gari.

Wale vijana walinichukua walinipeleka mbali kidogo na tulipokuwa, walinifunga kwenye mti mkubwa kisha wakauziba mdomo wangu kwa kitambaa.
Hawa kuzungumza chochote waliondoka wakaniacha nikiwa katika maumivu makubwa
sikuweza kupiga kelele wala kujinasua katika duara la kifo alilonisukumizia Tina.

Kulipambazuka hatimaye giza liliingia....mvua ilianza kunyesha, mwanzo nilikuwa naogopa muungurumo wa radi lakini kadri mvua ilivyozidi kunyesha niliacha kuogopa
niliyakumbuka maneno ya Mama kuwa Mimi ni mkosi sipaswi kuishi.
Nilijicheka mwenyewe niliona kufa ni haki yangu hivyo nilikaa kwa kutulia ni kisubiria kifo.

Asubuhi kulikucha nikiwa mwenye kuchoka sana...njaa ilinitesa kiasi kwamba nilijuta kwanini nimezaliwa.
Nikiwa mwenye kukata tamaa nilisikia sauti ya Mwanamke ikiimba....nilitazama vizuri alikuwa ni yule Msoma nyota.
Msoma nyota alinitazama pia huku akizidi kuimba.

mwisho alinisogelea.
" sijaja hapa kukusaidia wewe nimekuja kulisaidia jiji la Mah kama ukifia katika ardhi yetu basi kuna matatizo makubwa yatajitokeza wewe ni mkosi hupaswi kufia hapa..." Msoma nyota alizungumza kisha akanifungua kamba
kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka nilidondoka kama mzigo.

"sina nguvu za kukubeba acha kunitia hasara" Msoma nyota alizungumza.
Nilijikuta ni kiona giza zaidi, sikumbuki hata kitu gani kilitokea lakini nilikuja kushtuka nikiwa nyumbani kwa Msoma nyota.

"amka hapo kitandani....kula hiki chakula jua litakapozama nitakusafirisha urudi Mini..."

nilikuwa na njaa sana nilikula kwa fujo mpaka Msoma nyota akawa ananitazama
wakati na kula nilijikuta ni kiyakumbuka maneno ya Tina, niliumia sana kwa namna alivyo ni tendea unyama.

Jioni ilifika Msoma nyota alinipeleka mpaka ufukweni mwa bahari ya Mah....kulikuwa na boat moja kubwa

"nimeshalipia kila kitu naomba urudi nyumbani kwenu....kamwe usije kutamani kuwa kwenye mahusiano kwa sababu hujaandikiwa kuwa na mume...kitu kingine jitahidi kutafuta pesa ili ukae mbali na familia yako kwa sababu utawa sababishia matatizo endapo utaendelea kuwa karibu yao"

"ni kweli Mimi ni mkosefu kiasi hicho....unataka kusema laana yangu haiwezi kuondolewa...." nilimuuliza Msoma nyota kwa sababu maneno yake yalikuwa yakiumiza.

"kama ni hivyo basi Mama yako asinge chukua maamuzi ya kukuua.....sina uhakika kama hatma hubadilika.... naomba uwe na maisha mema" yule Msoma nyota alizungumza kisha akaondoka.

Nilimshukuru kwa msaada wake, niliingia kwenye boat nikiwa mwenye mawazo sana
pembeni yangu kulikuwa na Kijana mmoja sikuweza kuiona sura yake vizuri kwa sababu kofia ilikuwa imemfunika
safari ilianza, upepo ulikuwa mkali kidogo watu wote waliokuwa wamelala waliamka
Kijana aliyekuwa karibu yangu aliamka pia, nilishtuka sana baada kumuona sura yake alikuwa ni Allen......
ITAENDELEA........STORY TAMU SANA HII.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote