My wangu hivi ulishawahi kumpenda mtu kiasi cha mtu huyo kuwa pain killer wako ? Yaani wewe ukiwa na maumivu au ghasia zozote mtu huyu akiwa karibu na wewe tu baasi moyo unapona.🥰
Maumivu yote yana sambalatishwa na kuwa mpyaaa🥰,ushawahi kweli? Kama hujawahi basi kaa vizuri na Mungu wako muelezane vizuri maana huenda kuna mahali una kwama.
Haya vuta kiti kaa usikilize /some story yangu uone nilivyo kutana na PAIN KILLER WANGU 🥰, .
SONGA NAYO........
PAIN KILLER 💘
SEHEMU YA 01
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
My wangu hivi ulishawahi kumpenda mtu kiasi cha mtu huyo kuwa pain killer wako ? Yaani wewe ukiwa na maumivu au ghasia zozote mtu huyu akiwa karibu na wewe tu baasi moyo unapona.🥰
Maumivu yote yana sambalatishwa na kuwa mpyaaa🥰,ushawahi kweli? Kama hujawahi basi kaa vizuri na Mungu wako muelezane vizuri maana huenda kuna mahali una kwama.
Haya vuta kiti kaa usikilize /some story yangu uone nilivyo kutana na PAIN KILLER WANGU 🥰, .
SONGA NAYO........
Jamani niite Jemima hilo ndio jina nililopewa na wazazi wangu , nina miaka isiyo pungua 25, kikabila mimi ni mmakonde😊 so unaweza kuniita konde girl 🥰.
Kwa elimu nimesoma japo sio saana ila nina vyeti vyangu ambavyo nikienda ofisi yoyote ile napokelewa kwa tabasamu nono ,sema tu mambo ya sasa kupata kazi imekuwa kamzozo 😮💨.
Kusoma unasoma ila kazi hamna wanapata wenye connection zao 🥲, sasa baada ya kukosa kazi bwana niliamua kujitafuta kivingine.
Ambapo nimeajiliwa kwenye hotel moja hivi kama waitress, ila nje ya hiyo ninafanya biashara ya mashuka, nguo hata vyombo pia.
Na huwa nauza kwa order kwasababu sina ofisi , na kiasi chake namshukuru Mungu maana walau inanipush katika mambo mengi.
Eeh kula nakula kwa pesa yangu ,navaa kwa pesa yangu nalipa kodi kwa pesa yangu hata mama angu anapata chochote kitu kwa hicho hicho kibiashara.
Na mimi ni mtu wa mitandao sana ,hivyo kila leo natafuta kuangalia nini kimekuja juu kwa wakati huu then natafuta machimbo kisha naanza kutangaza biashara.
Jambo hili limenipa mafanikio mengi ikiwemo na kunikutanisha na watu wengi sana ambao wanafanyika baraka kila iitwapo leo🥰.
Na katika watu hao bwana kuna mwanadada anaitwa Juliet huyu dada ni mtu na nusu, na naweza kusema yeye ni mtu wa thamani sana kati ya wote nilio kutana nao .
Maana amekuwa si mteja tu bali rafiki, dada na hata mwalimu au mshauri , kiufupi ni mtu muhimu sana kwangu 🥰.
Sasa dada yangu huyu siku hii ya leo alikuwa na sherehe ya kumbukizi ya miaka miwili ya ndoa yake , hivyo kama mtu wake wa karibu nilijiandaa vyema ili niweze kufika.
Basi nilioga nikavaa nguo ambayo ilinitoa sana kisha nikapaka make up na nilivyoona niko sawa nikabolt kisha safari ya kuelekea kawe ambako ndiko alikuwa akiishi Juliet.
Na huewezi amini pamoja na kuwa karibu sana na Juliet sijawahi kabisa kufika kwake ,kwanu mara nyingi nimekuwa nikienda kumuona kazn kwake.
Wakati mwingine alikuja kwangu au tulikutana sehemu kama restaurant beach basi , so siku hii ilikuwa ni siku ya kwanza kabisa kufika kwake .
Safari ya kutoka nyumbani kwangu hadi ilichukua mda maana mimi nilikuwa natokea kigamboni , so nilijikutana nachelewa kufika japo sio sana.
Basi bwana baada ya kufika nililipia usafiri kisha nikaingia ndani ,ambapo nilikuta watu tayari wamshafika wote na sherehe ilkiwa imeanza .
Juelit aliniona wakati na ingia so akatoka na kuja kunipokea , " wow kama kawaida yako mrembo wa kimakonde ndani ya fashion 😍, aisee umependeza sana kipenzi " Aliongea Juliet huku akiwa amenikumbatia.
"Asante mamy ,umependeza pia "
"Sijakufikia bhna yaani umetuzidi wote hapa ona make up ilivyo kukaa hadi raha"
"Hahaha basi dada usinipe bichwa "
"Ona haka nakusifia unaona kama nakupa kichwa ?,anyway twende ukamuone shemeji yako"
Alivyo sema hivyo nilitabasamu maana nilikuwa natamani sana kumuona mume wake, kwasababu sikuwahi kumuona hata kwenye picha.
Najua itakufikilisha kuwa inakuwaje niwe karibu sana na Juliet na nisimfahamu mume wake. 🤔
Iko hivi Juliet ni mtu flan hivi asiependa kumuonesha mume wake , na kama nilivyo sema nimejuana na Juliet kwenye mitandao ambapo nilikuwa katika mihangaiko yangu ya kutafuta ugari.
So mara nyingi nimekuwa nikimsikia mume wake kwenye story tu ,na kwakua hakutaka kumuonesha onesha kwa watu so nikabaki kumsikia tu.
Ila ukweli nilitamani sana kumuona maana story alizokuwa akinipa kuhusu mume wake ni moto 🔥, na uongo dhambi kwenye maombi yangu nilikuwa mimi.
Nilikuwa namwambia Mungu nipe mume kama wa Juliet maana sio kwa sifa zile 🥰, basi bwana alinishika mkono tukaingia ndani maana pale nje hakuwepo.
Haya kufika ndani akamuita kwa jina flani tanu tamu🥰🥰, sauti ya kidume ikasikika ikiitika kutokea chumba jirani na sebleni.
Sauti ya mwanaume huyo ilipenya kwenye moyo wangu na kuhisi kitu flani hivi🤔, sekunde kadhaa akatoka na kuja tulipo aloooh nilijikuta natoa macho nisiamini kama naona au naota.
Mapigo ya moyo yalienda mbio kuliko kawaida, mdomo ukawa mzito kama umebebeshwa jiwe.
Si mimi nilieshtuka hata mwanaume yule alishtuka , Juliet kuona mumewe kafika alisimama na kusema .
"Babe huyu ndo Mima niliekuwa namuongelea kila siku, na Mima huyu ndo mfalme wa moyo wangu, mwanaume alienichagua kati ya mamillioni ya watu.
Akaniona nafaa na kuniweka ndani kwa mapenzi mazito "
Niliachia tabasamu na kusema " Ooh nimefurahi sana kumuona , hongereni sana kwa kumbukizi hii "
Mumewe Juliet nae alitabasamu na kunijibu " Asante nimefurahi kukuona pia"
Hakukuwa na laziada hivyo tukatoka nje na kwenda kukaa waliko wengine, sasa wakati naelekea kwenye meza ili nikae nikakutana uso kwa uso na mkaka ambae ni rafiki wa mume wa Juliet.
Nae alivyo niona tu alishtuka na geuka kumuangalia mume wa Juliet (Benson ) kwa mshangao sana , bila wasi wasi nilitabasamu na kuomba nipite maana alisimama mbele yangu.
Akiwa bado katika hali ya mshangao akanipisha nikapita na kwenda kukaa ,kisha sherehe ikaendelea na ilipokwisha nikaaga na kuondoka.
Je Unafikili kuna nini hadi Benson yaani mume wa Juliet kushtushwa na uwepo wa Jemima, je kuna story nyuma ya pazia ?
Ungana nami katika sehemu ya pili ya kisa hiki..........ITAENDELEA
PAIN KILLER 💘
SEHEMU YA 02
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO.............
Niliingia kwenye gari na kukaa huku nikiwa kama sielewi nilichoona ni kweli au nimeanza kuona mawenge , jamani Benson huyu huyu ndo mume wa Juliet 🤔
Ah hii nimaajabu sana , niliwaza na kubaki nikijionengelesha mwenyewe kama mjinga, mbaba wawatu alibaki kunishangaa tu( naona aliona tayari binti akashapigwa kipapai)
Asijue nashangazwa na mambo ya ulimwengu ila hii ni baabu kubwa walai,yaani Benson huyu huyu aaah nyie acheni niseme wanaume wote ni mbwa 😒
Ila sio wote maana baba yangu hawezi kuwa mbwa 🥲, basi bwana nilifika nyumbani bado kichwa kikiwa na maswali mengi , kwakua nilikuwa nimechoka moja kwa moja nilipitiliza chumbani.
Ona eti nilipitiliza moja kwa moja chumbani wakati ninakaa chumba kimoja ambacho kiko kama store ,maana humo humo kuna jiko, sebule na chumba.🥲
Basi bwana nilifika zangu na kupanda kitandani huku nikijiambia Jemima lala hilo uliloniona huenda ikawa ndoto maana ni makubwa .
Haya nikafunga macho ili nilale mie mara simu yangu ikaita nikanyosha mkono na kuvuta pochi yangu kisha nikaitoa sm na kuangalia anaepiga .
Nilijikuta nikibaki kuiangalia sm bila kupokea na hii ni baada ya kuona anaepiga , sm iliita sana sikupokea mwisho nikaona kama inanipigia kelele nikaizima na kuitupilia mbali.
Niliamua kuweka mwazo yote pembeni na kulala zangu, kesho yake asubuhi niliamka mapema sana maana nilikuwa natakiwa kuingia kazin .
Bila kupoteza mda niliingia bafuni nikaoga vizuri kisha nikavaa na kuweka nywele zangu vizuri nilivyo maliza nikaenda kupanda daladala na safari ya kuenda kazn ikaanza.
Dakika 40 zilitosha kunifikisha kituo husika, nikashuka mwenyewe na kutembea mdogo mdogo hadi kazn kwangu .
Kufika nikasalimiana na wenzangu vizuri kisha nikaingia chumba cha kubadilisha nguo nikavaa sale za kazi na kuanza kazi, mda ulienda ilipofika saa nne kasoro mwenzangu akaja kunambia naitwa.
Niliuliza naitwa na nani akasema hajui basi bila kuchelewa nikaenda hadi aliponielekeza nashangaa kumkuta Benson akiwa ndo ananiita.
Nilitabasamu kama vile hakuna kitu na kumuuliza " Karibu sana Mr Benson, je nikusaidie nini?"
Kwa sauti ya upole Benson akasema " Jemima tunaweza kuongea tafadhali?"
"Kuongea ??, bila shaka unaona kuwa niko kazn so kama maongezi yako yanahusiana na kazi haina shida ongea ila kama sio please rudi ulikotoka"
"Sio ya kazi ila tafadhali nipe nafasi japo kidogo tu "
"Naona kiswahili kimekuwa kigumu eeh !? Nimesema kama maongezi yanahusu kazi ongea kama sio geuza kwato zako na urudi ulikotoka "
"Jemima !!"
"Yes "
"Please nipe nafasi japo kidogo"
"Hahahaha, kumbe unakuwaga mpole hivi!? Okay tuseme nimekupa dakika moja mh ongea unachotaka kuongea "
"Aaam nilitaka kuongea kuhusu tukio la jana "
"Yes tukio la jana mh endelea " alishusha pumzi na kuvuta kiti akakaa na kusema.
"Nilikuwa naomba ibaki kuwa siri "
"Mmh siri ,ukiniangalia usoni unahisi nina kifua cha kukaa na siri ya mtu?"
" Najua unaweza "
"Umekosea tena umekosea pakubwa ,kaka mambo yangu mwenyewe yananishinda kukaa nayo niende nikakae na ya mtu ili iweje kwanza nitaanzia wapi kuweza?.
We sikia jambo lolote linalopita mbele yangu haliwezi kuwa nyuma ya rafiki zangu kiufupi sina siri mbele ya mkeo .
Na nikuulize wewe ni mtu au shetani ulie kazini kuingiza watu jehanamu, maana nimejaribu kukutafakari lakini sikupatii picha .
Mwanaume mmoja eeh unawanawake wawili na wote unawaita wake zako? Na sio kuwaita tu umefuata taratibu husika .
Na sio ajabu ila kunachofanya jambo hili kuonekana ajabu ni kuwa wewe ni mkristo huna ruhusa ya kuoa mwanamke zaidi ya mmoja .
Haya niambie umemuoa Juliet kwa ndoa na bado umeenda kuwa na Naomi masiki dada wawatu miaka mitano anakusubiri wewe umuoe ila umeishia kumvalisha Pete nampa matumaini hewa
Unajua nini toka mbele yangu maana nahisi nitakuua niende jera kwa mambo yasonihusu"
"Natamani kuongea sana ila siwezi maana huu sio wakati sahihi na pia hii sio sehemu nzuri ya kuongea hata hivyo uko kazn so naomba tu usiongee chochote kwa Naomi na Juliet "
Aliongea na kuinuka akaacha elfu kumi na kusema niya juice aliyo tumia inayo baki nichukue.
Bila kuongea neno nilichukua ile pesa na kubaki nikimuangalia hadi anaondoka eneo lile.
Ngoja niwape story maana najua hamuelewi nini kinaendelea haswa.
Iko hivi Benson ni mchumba wa Naomi ambae ni best friend wangu toka chuo , na mahusiano yao yana mwaka wa tano sasa ,ambapo ndani ya hiyo miaka mitano wamefanikiwa kutambulisha na kwa wazazi.
Kijana akatoa posa na kumvika binti Pete, sasa nimekuja kushtuka baada ya jana kutambulishwa na Juliet kuwa ni mume wake tena wa ndoa.
Nisiulizwe kuwa inakuwaje usindwe kufahamu mapema ikiwa Juliet amekuwa mtu wa karibu kwako.
Jamani kama nilivyo sema mwazo kuwa mimi na Juliet tumefahamiana mtandaoni, na mda wote nilio mfahamu Juliet hakuwahi hata siku moja kunionesha picha ya mume wake wala hajawahi kumpost kwenye mtandao wowote ule .
Huku sababu yake kubwa ni kuwa hataki kuweka ndoa yake au mume wake kwenye mitandao au machoni mwa watu ,(tuseme ametaka ibaki private)
Haya sasa kumbe mwanaume anaesema ni mumewe ni mchumba wa best friend wangu ,sasa hapa sijui inakuwaje maana naona kama nataka kuchanganyikiwa .
Na nitafanya nini maana Benson amenities nikae kimya , jambo ambalo ni gumu kwangu maana wote ni marafiki zangu je nitaakaje kimya yaani naanzaje kukaa kimya .🤔
Na nikisema pia niongee nitanzaje na nini kitafutaa baada ya mimi kuongea🤔,woii nachoka mwili na roho ila hii ngoja nitulie kwanza .
ITAENDELEA
PAIN KILLER 💘
SEHEMU YA 03
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO...........
Niliamua kurudi kuendelea na kazi zangu, ilipofika jioni nikarudi nyumbani na kukaa chini nikaanza kufikilia inshu ya Benson, niliwaza cha kufanya nikaona hapa natakiwa kutumia akili.
Taratibu nilizungusha macho nikaangalia chumba changu na kufikilia majukumu niliyo nayo nikaona ngoja hii itaenda kunipunguzia baadhi ya mambo.
Haraka nikainuka na kuingia bafuni nikaoga vizuri kisha nikatoka na kwenda kwa Naomi, kufika pale nikagonga mlango.
Haikuchukua mda nikafunguliwa " hello my beautiful girl " niliongea mara tu Naomi alivyo fungua, kwa furaha alicheka na kusema.
" Wewe tena bi shosti uso penda kukaa kwako ,kutwa kiguu na njia 😒"
"Aaaah mara hii! Haya funga mlango wako nirudishe mbao zangu kwangu usinichefue😏"
"We nae utani kidogo unawaka kaone ka jinga "
"Utani gani huo, mi nimetoka mbali huko nakuja nikuone unajifanya unajua kuongea embu nipishe niingie kwanza na njaa"
"Wewe na kula inabidi tukutafutie dawa utakuwa una spirit ya mchwa so bure"
" Achana na mimi unataka nifanye nini wakati maisha yenyewe ndo haya haya "
"Shauri yako utaja kufumuka uwe kama mwafulani 😃, na ulivyo kafupi utakuwa kama kibanda cha m pesa "
"Hata nikiwa kama mtungi wa gesi fresh tu kikubwa mbinguni tutapewa miili mipya baasi wasi wasi sina😇"
"Jichanganye "
"Embu acha maneno mengi na unipe chakula mie"
"Eeeeh usinichoshe bwana kama mikono huna kaa hapo usubiri kitajipakua chenyewe"
Alivyo sema hivyo niliinuka na kuingia jikoni nikapakua na kurudi seblen(mwenzangu maisha alikuwa nayo hivyo alipanga nyumba nzima , mimi sasa huzuni tupu🙁)
Sema kila mmoja anishi kwa uwezo wake so sina shida kikubwa nikwangu na nalala kwa amani baasi🥰.
Haya bwana baada ya kurudi kukaa nikaanza kula huku Naomi akinipa umbea kidogo, nilikuwa mtu wa kuitikia huku nikimuangalia usoni .
Moyoni nilimuonea huruma sana maana anavyo mpenda Benson hakuna mfano, sasa saizi aje kusikia jamaa ameoa sijui atalia kilio cha aina gani.😥
Swala la kuitikia huku nikimuangalia lilimpa ishara kuwa kuna kitu ,akakatisha story na kuniuliza " Mimah kuna nini mbona kama hauko sawa?"
"Mimi ! No niko sawa "
"Umeanza kunificha vitu si ndio maana nakuona kabisa hauko sawa "
"Niko sawa bwana ,sema nini kazin wazingua sana " (niliamua kumdanganya.)
" Wamefanya nini tena ?"
"Aah ni upuuzi tu, sema leo kuna vurugu limetokea mambo yalikuwa moto balaa"
"Ewaa hayo ndo mambo sasa mh tena nondo"
"Kwa umbea tu hujambo 😁, okay kuna mkaka kafumaniwa na mpenzi wake , bidada yule anewaka kama mbogo cha ajabu sasa picha likageuka na kujikuta kumbe yeye ndo mchepuko."
"Weeee! Nyie wanaume hawa, sasa ikawaje na imekuwaje mfumania akajikuta yeye ndo mchepuko?"
"Imekuwaje nini wakati jamaa alimdanganya yuko mwenyewe kumbe kashaoa kitambo"
"Aisee "
"Ndo hivyo kwa hiyo limezuka bonge la ungomvi watu tukabaki tunakodoa macho tu, ila wanaume ndo maana sitakagi kumpa moyo kiumbe kinachoitwa mwanaume maana ni sekunde tu unasambalatiswa vibaya mno."😮💨
"Hamna bhna wasi wasi wako tu wala hawako vile unavyo fikilia sema ni akili yako ndo umeshaiaminisha hivyo ila mapenzi ni matamu"
"Nimatamu wakati yakiwa moto ila jua likishaanza kuwaka ndo unayaona vizuri, na ni kuulize hivi hili linge kutokea wewe ungefanyaje ?"
"Nimesha kwambiaga usinitolee mifano kwenye mambo mabovu namna hiyo, kwanza kwangu haiwezi kutokea kamwe"
"Haiwezi kutokea 🧐 ?"
"Yeah haiwezi "
"Kwanini ?"
"Kwasababu na muamini mwanume wangu, Benson hawezi kunisaliti hata siku moja .
Amenichagua mimi na atadumu na mimi siku zote , na nikuulize atanisaliti kwa lipi haswa eeh nione mtoto nilivyo umbika msiri ya malaika😊.
Sura imetubu shape ndo usiseme ,sijasema kwenye sita kwa sita jinsi ninavyo mpeleka puta mtoto wa kingoni mie Aah ☺️😇"
"Mmmm!"
"Yeah hawezi ,yaani mimi kucheatiwa na Benson sahau my friend tena sahau"
"Punguza sauti na ubakize maneno ya kesho mpenzi "
"Kwanini nipunguze my friend nina muanini mwanaume wangu asilimia mia "
"Nakukumbusha bakiza maneno ta kesho"
"Aaah bwana eee we kama umekutana na majambazi wakaukata kata moyo wako ni wewe ile mimi no kama ni safari bado kwa Benson wangu ndo mwisho his my soulmate. "
"Naomi wanaume sio wakuwa proud nao hivyo hawa viumbe ni moto wa kuotea mbali"
"Hiyo ni yako mpenzi sio kwangu, hivi nikuulize kwa unavyo niona mimi Naomi toto la kingoni niliefundwa nikafundika eeh mtoto nikapikwa nikaiva haswa naweza kuachwa?
No sikitu ambacho hakiwezekani yaani hapa Ben hatoki na sio kutoka tu hakohoi, na sijamroga akuuu mwenyewe kajaa kwenye dunia yangu"
"Mmh kwa hiyo unafikili wanaume wote wanao cheat wapenzi wao wanakuwa sio mafundi?"
"Asilimia tisin na pia unajua unaweza kuwa fundi ila ukawa kama makande yasio na chumvi eeh ? "
"Oooh"
"Sio oooh, ndo iko hivyo ,yaani unakuta mtu hana radha hata kidogo kapooza kama mfu tena hasa nyie wenye rangi nyeupe hamna radha wala joto yaani mmepooza kama meziweka kwenye jokofu😏.
Ila njoo kwetu sasa aaah weusi tuna dunia yetu, nikwambie tu Mimah mimi nikimshika bwana wako wallah hutobi yaani unasahaulika ndani ya sekunde.
So my dear sahau kuhusu mimi kusalitiwa upo 😇"
"Kwa hiyo unataka kusema mimi sina radha "
"Aah hiyo iko wazi my dear mwanamke mweupe unaanzaje kuwa mtamu ? Mh hakuna kitu kama hicho nyie ni wazuri wa sura tu ila huko hamna kitu🤧"
Aisee😄 nilitamani kucheka ila maneno yake linichoma nikabaki namuangalia tu, mimi eeh sina aise😃😃 haya bhna .
"Vp imekuuma eeh pole bwana ukweli huwa unakuwaga mchungu maana ni dawa"
"Hapana kwanini iniume 🥲 ila hongera kwa kumpata mwenza wa maisha yako"
"Asante babe girl 😇"
Niliamua kutoka moyoni kuwa sita ongea kitu ,maana so kwa shombo hivi , na sishangai Naomi ni rafiki yangu sana ila dada huyu ananyodo vibaya mno.
Sema hazioneshagi kwangu maana anakijua kichwa changu vizuri ila leo naona ameamua anifurahishe 😁, ila kanivuruga yaani kanivuruga haswa eti mimi sio aaah hili limaniuma sana .
Kwa hiyo mimi kuachwa ni kitu ambacho nastahili kisa tu sina utamu ila yeye hawezi kuachwa ,😆😅 acha dunia imfunze kwamba mwanaume ni kiumbe ambae hajawahi kueleweka.
Na maisha buku sitafungua mdomo wangu ,kama nakosea fresh ila kumwambia no hata nikabwe sisemi.
Halafu nione siku akijua atajisikiaje mpuuzi huyu, kazi kujiona cake kumbe biscuit ya mia 😏.
Niliamua kubadilisha mada ila akawa hataki anataka tuzungumzie uzuri wa wanawake weusi na wenye mishape tu🤧, sikutaka kumkata mood yake nikampa bega.
Akaongea wee kujisifia kwa wingi ,akahamia na kunambia jinsi Benson anavyo mpenda na mchana wa leo amemwambia ajiandae wiki ijayo waende vacation.
Neno langu moja tu hongera dear,, akasema .
"Usijibu hongera tu, jirahidi kutumia vitu ambavyo vitakupa joto na mnato na ikiwezekana uanze kujifunza utundu ili usije kuwachwa tena.
Au mwenzangu huchoki kuanzisha mahusiano mapya kila siku maana toka hadi sasa tukipiga mahesabu ya watu waliopita kwako ni team ya mpira wa miguu.
Huku mimi niko na Ben wangu na soon tunaenda kuwa Mr and mrs,, so shost amka utatumika mwisho hako karadha uliko pewa kaishe kabisa ubaki makapi "
(Aisee 🤨) nilichukia nikahisi hasira ikaaa hapa kwenye koo , kwa hasira niliinuka kumwambia.
ITAENDELEA
PAIN KILLER 💘
SEHEMU YA 04& 05
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO..........
"Asante kwa chakula na kwaheri"
"Kheee sasa mbona unaondoka ?"
"Nilipita kukusamilia tu " nilipeleka sahani jikoni nikarudi na kuchukua sm yangu bila hata neno nikaondoka.
Unajua nilikuwa na hasira kali vibaya mno, na uongo dhambi kama ningekuwa na tabia chafu walai ningemuonesha kuwa wanaume sio wa watu wa kuwakingia kifua hivyo.😏
Na msifikilie eti nasakarika kwa sababu ni kweli hapana hakunaga upuuzi kama huo, japo ndio najua nimekuwa na historia mbaya kuhusu mapenzi🥺.
Lakini haina maana kuwa naachwa kwasababu sina radha ni basi tu sijapata bahati ya kupata mapenzi ya kweli😭, ila najua ipo siku nitampata .
Sijui ni lini wapi au mwaka gani ila naamini nitampata wala hatajali nimetoka na watu wangap wala historia , zaidi atanipenda na kunijali☺️
Basi nilirudi nyumbani na kufika nalala, kesho yake kama kawaida nikaingia kazn jioni nikarudi zangu nyumbani.
Cha kushangaza nilifika nyumbani na kumkuta Benson akiwa amekaa nje, nilimuangalia na kumpita bila hata kumsalimia.
Alijiongeza akanifuata nyuma nikafungua mlango na kumgeukia nikamuuliza" unaenda wapi?"
"Nimekuja nataka tuongee"
Nilitaka kumtoa balu ila nikaona nipunguze kupanick kwa mambo yasonihusu ,hivyo nikamruhusu akaingia ndani na kukaa.
Kwa upole nikampa maji na kukaa tayar kumsikiliza "mh unaweza kuongea"
"Asante, am nimekuja na ombi lilelile la jana nakuomba jambo hili liwe siri kati yetu."
"Sitaki kuuliza maswali mengi ila nikuulize walau moja tu, unapotaka jambo hili liwe siri unategemea nini au una mpango gani "
"Kuhusu mpango hilo halikuhusu ninachotaka ni wewe kukaa kimya , na ikiwezekana ukae mbali nao wote "
"Unawazimu unataka nikae nao mbali unajua tumetoka wapi? Sikia kama umekuja hapa na ubabe wako unaweza kuondoka wala usinipangie cha kufanya.
Eti ukae nao mbali yaani nivunje urafiki wangu kisa upumbavu wako ?"
"Okay tuliza hasira na unisikilize, najua unashida na pesa sema nikupe shingap ili ufanye vile ninavyo taka"
Huyu kenge , hivi ananionaje mimi🤨, nilichukia nakutamani kumtukana ila nikaona ngoja , hivi niko serious kuacha hela kwa kitu ambacho hata nisipo sema mimi kitafuchuka.
Eeh kwani kuna kitu kinachokaa gizani milelel? Jibu ni hamna siri lazima itakuja kufichuka tu na ikifichuka nini kitafuata lazima mmoja ataumia.
Na hapa wakuumia zaidi ni nani Naomi ,bidada anaejifanya oh siwezi kuachwa mara nyonyonyo🤧.
Sasa ngoja nijipatie ujira wa kuwa shemeji hayo mengine watajua wenyewe,na kama watajua nilijua hili mapema nikachukua na hela sawa sa nifanyaje .
Nikatae hela na nina shida kibao no huu utakuwa ni upuuzi uliopitiliza , acha nichukue pesa nifanye mambo yangu hayo mengine yatajijua .😊
Nilivyo waza hivyo nikamwambia Ben, " inaonekana wote ni muhimu sana kwako ndo maana uko tayari kutoa pesa ilimradi tu ibaki siri"
"Unajua ni kiasi gani nampenda Naomi lakini pia nampenda Mke wangu Juliet "
"Oooh hongera, sasa mimi hata usipe pesa nyingi nipe million moja tu"
Nilivyo sema hivyo Ben alitabasamu kwa dharau na kusema " mara zote nimekuwa nikikuona wa maana sana ila umenifanya nione kuwa nilikuwa nakosea.
Coz mtu mwenye kuthamini utu hawezi kuchukua hela na kumficha rafiki jambo zito namna hii "
"Kijana kama umegeuka mhubiri inuka ukahubirie familia yako, eti wa ulikuwa unaniona wa maana sijui sina utu ,huo utu we ndo unao?.
Au unataka nifanye nini kiseme halafu kitafuta nini?we nipe pesa yaache yatakuja kujulikana mbele ya safari"
Baada ya kusema hivyo Ben alitoka nje na kwenda kwenye gari kisha akafika na kunitupia hela kadharau, na kusema .
"Hakikisha unafunga mdomo wako"
Aliongea na kuondoka huku akiacha amebamiza mlango, aisee hawa watu wananiona mimi kama makalio yao .
Yaani wa ajifanya wao ndo wao ,sasa ngoja niwaoneshe kuwa dharau ni nini, yaani pesa nimechukua na siri nitaitoa halafu tuone shenzi😏
SEHEMU YA 05
Niliinuka nikafunga mlango na kupanda kitandani na kuanza kupanga mambo yangu, hapo kodi ilikuwa imeisha nikawaza kulipa nikaona hapana bora nitafute chumba kingine.
Kweli kesho yake niliamka na kumtafuta dalali nikamwambia anitafutie sehemu nyingine , ambapo ilinichukua siku tatu chumba kikapatikana.
Nikaenda kukianagalia nivyo ridhika nikalipia na kuhamia ,na unajua kwanini nimeamua kuhama nilipo kuwa nakaa ?
Kwasababu najua ninachoenda kufanya kitaenda kuleta kamzozo so sitaki mtu yoyoye kuja kulia nyumbani kwangu😏.
Basi baada ya kuhama nikapanga siku nikaonana na Juliet, aisee kukutana nae tu hivi hakuna story inayoongeleka zaidi ya kumsifia mumewe .
Nilibaki nimeshika shavu namuangalia tu namna anavyo tiririka, yaani kwa namna alivyo kuwa akimuelezea utafikili huyo mwanaume ni Malaika 😅
Moyoni nikasema ungejua huyo unae msifia sijui mwaminifu sijui anajua mapenzi sijui vile ni chovya chovya ungekaa chini ulie😏.
Kwa maneno yale nikajiambia Jemima dear umeshapewa hela yako umetatua shida yako haya mambo embu yaache.
Usije kuvunja furaha za watu, kwanza hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja 😒,japo najua kukaa kimya na kuendelea kuongea nao ni unafki na najua ikija kujulikana huu urafiki hautaendelea .
Ila naomba ni kae kimya ,hizi sifa zao zitakuja kuisha wakijua ukweli.😁
Basi bwana niliamua kukaa kimya ,nikabaki napambani mambo yangu siku zikaenda ila kila nilipokaa nilikumbuka maneno ya Naomi nilijisikia vibaya .😪
Nilitamani na mimi ningepata mahusiano ya kueleweka lakini kila mara nimekuwa nikipata mabomu tu😩.
Moyo umechoka imani kuhusu mapenzi imekufa nipo nipo tu kama msukule alie potea njia 😥😩, au usikute nikweli sina maajabu ndo maana naachwa🥱.
Niliwaza na kuumia mno ,nikaamua embu ngoja nijipe nafasi nijitoe out huenda nikabahatika kupata mapenzi ya kweli.
Hivyo nikaanza kujitoa karibu kila weekend lakini nikawa kama sionekani😩, nilijisikia vibaya nikamwambia nikamueleza mama , akanambia mwanangu wewe ni mzuri.
Usilazimishe kutafuta mahusiano kisa ukuwa single kwa mda mrefu, we tulia fanya mambo yako omba Mungu na wakati ukifika utampata Adam wako.
Maneno ya mama yalirudisha tumaini nikaona kweli sina haja ya kuwa na presha na mapenzi yatakuja yenyewe kwa mda wake. 😊
Basi mtoto wa kike nikajiweka bz na biashara yangu huku nikiendelea na kazi yangu ya waitress🥰.
Miezi miwili ilipita bhana siku hiyo nikawa zangu off, na mara nyingi nikiwa nyumbani huwa napenda kutumia mda mwingi kufanya usafi wa ndani.
Kisha ikifika jioni natoka zangu, basi miliamka mapema nikafanya usafi mchana nikapika vizuri, na ilipo karibia jioni nikaandaa nguo na pesa kwaajili ya kwenda kujipoil☺️.
Lakini mood yangu ilikuja kuisha baada ya kupigiwa sm na kuambiwa nahitajika kazn kwani alietakiwa kuingia jioni amepata dharura hivyo inabidi nishike nafasi yake😮💨.
Nilichukia na kulaani vibaya mnoo bila kujua kuwa ilikuwa ndio ticket ya kwenda kuonana na My pain killer 🥰, ilikuwaje embu tukutane sehemu inayo☺️.
(Kilio cha mapenzi kwiisha habari 😇)
ITAENDELEA
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote