PENZI LA CEO NA AMORA

book cover og

Utangulizi

PENZI LA CEO NA AMORA

AMORA Binti aliyeishi maisha magumu sana , anakutana na Kijana frank ambaye ni CEO wa kampuni kubwa sana hapa mjini, mwanzo wao unakuwa mbaya sana lakini mwisho wao ndio what matters.

Frank Kijana ambaye hakuwai kupata mapenzi kwa mama yake mzazi m, anakuja kuchanganyikiwa na huba zito kabisa kutoka kwa Mtoto wa buza ambaye ni AMORA.

Mapenzi Yao yanakumbwa na kila aina ya madhoruba ambayo kwa Namba moja au nyingine yaliwakatisha tamaa.

JE AMORA NA FRANK WATAFIKIA LENGO ? TUKUTANE NDANI NDANI UKO

PENZI LA CEO NA AMORA
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 01
www.tupohapa.com

ANZA NAYO......

Hivi ushawai kukutana na Boss mwenye kisilani wewe ? Yaani boss jambo si jambo tayali hasira zimempanda, kitu si kitu tayali anakutafutia sababu, yaani ni mtu fulani hivi ambaye muda wote anatamani watu wasilosee ata kidogo.

Anyway naitwa AMORA binti wa pekee wa mama muuza vitumbua na mkaa kwenye mtaa wetu, yaani ukija mtaani kwetu mimi na mama yangu ni watu maarufu sana, sababu ya kwanza ya mimi na mama yangu kuw amaarufu ni kwamba tumeishia hapo kwa muda mrefu sana, nikisema muda mrefu muwe mnanielewa.

Mama yangu alizaliwa kwenye mtaa huo huo na nyumba hiyo hiyo, lakini pia akakulia hapo hapo, akasoma akiwa kwenye nyumba hiyo hiyo, cha kuchekesha zaidi na mimba yangu pia alipata akiwa umo umo ndani 🙌🏻😅 not funny lakini inachekesha.

Mama yangu alikuwa na mahusiano na mpangaji wao na ndio akapata mimba yangu, mpangaji alivyoona kuwa ameshaharibu akichofanya ni kukimbia tu na ndio sababu pia ya mimi kuzaliwa umo umo na kulelewa umo umo.

Kitu ambacho nashukuru mpaka sasa ni kwamba bado nina babu na bibi yangu ambao ni kidogo umri umeenda lakini awajazeeka, yaani ni watu ambao wanaendelea na kazi zao za hapa na pale.

Ingawa maisha yetu yalikuwa ya kubangaiza sana, lakini mama yangu na bibi na babu yangu, walihakikisha kuwa nasoma na kufika level za juu kabisa na waliamini kuwa mimi ndio naweza nikawa ufunguo katika mafanikio ya familia nzimaa.

Kwa namna moja au nyingine, niseme kuwa sikuwaangusha kabisa, juhudi zao juu ya elimu yangu nilishika vizuri sana, nilihakikisha kuwa nasoma sana.

Katika moja na mbili, niliweza kufika juu zaidi na nikapata master's yangu nzuri kabisa ya biashara.

Picha linaanza kwenye kupata kazi bwana, hii niliielewa baada ya kumaliza na masomo na kuingia mtaani kwaajili ya kutafuta kazi.

Nyieeeeh 😅🙌🏻 nilikuwa nazurula na ma file yangu kila ofisini na ilikuwa kawaida sana kwa mimi kutoka patupu, kuna muda nilikuwa naona kama naotaji connectio tu na sio vyeti 😩.

"Ila mama nimeshachoka kuzurula na hizi karatasi kila kona, yaani me ata sielewi hawa waajili ni kitu gani wanataka iliwa CV yangu inakila sifa ya kufanya mimi niajiliwe "

Nilizungumza kwa kulalamika na muda huo ndio kwanza ilikuwa asubuhi na nilikuaa nikimsaidia mama kichoma vitumbua vyake na yeye alikuwa kipanga mkaa kwenye mifuko na makopo"

"Utapata tu binti yangu ni vile tu muda wako bado mama "

Alijibu mama yangu.

Muda huo huo akaja msichana fulani hivi ambaye mimi nilisoma nae chuo kimoja na yeye aliishia level ya degree tu hakuendelea kama mimi.

"Weeeh cheupe weeeeh unazidi kuwaka dada "

Nilianza kumtania maana alikuwa ni mweupe sana.

"Ujaacha mambo yako da kijumbe, sema nimekumisi sana"

"We si umenisusa kisa nimepauka shonga angu"

Nilijibu kwa utani lakini ukiangalia ni kweli bwana yani nimepauka kuliko kawaida.

"Naomba vitumbua kumi shoga angu, yaani tangu rafiki yangu ammonia vitumbua vyenu uko kazini ni kila siku ananiambia nimpelekee"

Alizungumza cheupe uku akionekana kuwa na haraka sana.

"Weeeh basi ulete na wateja wengine dada"

Nilimwambia.

Nilimfungia vitumbua vyake kisha akaondoka.

Eeeeeeh nimekumbuka kumbe sikuwaambia naishi Wapi ? 😅🙌🏻 naishi buzz kwa mpalange kwenye zile nyumba za kizamani kabisa, nyumba ambazo nimechoka na kuchakaa nyumba azina mbele wala nyuma.

Kuhusu uswahili tu niko vizuri, mimba yangu yenyewe imepatikana kwa nahati mnaya halafu nikazaliwa kwa makusudi.

Majila ya saa 4 nikajianda zangu na kuingia tena mjini uko kwaaji ya kutafuta kazi, walahi nilijua kuzunguka kila ofisi, nilikuwa nikizunguka kama kichaa lakini hakuna mafanikio yoyote yale.

Sasa nikiwa nimeshachoka sana, jua kama lote limeniishia mwilini, nilifika kwenye jengo fulani hivi kubwa sana, kwanza kabisa nikajiambia..

"Hii ni ofisini ya mwisho kabisa nikikosa narudi zangu nyumani "

Nilizungumza nikiwa nimesimama kwenye ngazi ambazo nilikuwa napiga mahesabu nawezaje kupanda na zilivyokuwa nyingi

Nikiwa nimesimama sina ili wala lile, gafla nikasukumwa kwa nguvu sana na hii ikapelekea mimi kuanguka kama mzigo vile.

"Eeeh we nawe uoni au??"

Nilifoka kwa sauti sana pasi nankuangalia ni nani alinisukuma.

Muda huo huo nikamuona mkaka fulani hivi, ambaye kwa umri alionekana kuwa hajapishana mbali na mimi, alikuwa ni mkaka fulani hivi hot sana, ananukia kuliko kawaida, mkaka huyo alikuwa amevaa suti Moja kali sana.

Mkaka huyo ndio alinisukuma, japo nilianguka, aliniangalia tu na akusema kitu akaanz kupanaa ngazi, kwa hasira nikamuuliza.

"Kwahiyo wewe ujui kusema samahani ??"

Mkaka huyi akuniitikia wala akugeuka zaidi alikaza mwendo.

"Kumbe unijui wewe, me chini kuliko huo uchizi wenyewe"

Nilizungumza na kuanza kunkumbilia, haraka nikimfikia na kusimama mbele yake.

"Wewe chotara, kwahiyo ukuona kuwa umeniumiza ??"

Nilimuuliza.

Mkaka huyo alinuangalia mwisho akaingiza mkono wake mfukoni na kutoka na wallet pasi na kupoteza muda akachomoa not za elfu 10 kadhaa na kunipiga nazo usoni.

"Utajitibia, kama utakuwa haujapona utakuja kuchukua zingine"

Walahi huyu kaka anadharau ya hali ya juu, a kwa wakati huo sikuona dharau yule niliona zile hela tu, niliinama chini na kuanza kukota zilizoanguka.

"Nisukume tena basi "

Nilijikuta nikilopoka😅🙌🏻.

Niliokota pesa ile nainuka tu nilijikuta nikiwa mwenyewe, yule kaka hakuwepo kabisa, nilimuangalia uku na uku na mwisho nikagundua kuwa pembeni yangu ni kuna lift hivyo ametumia lift kupanda juu.

Kwanza nilitoka nje na kwenda kusome kibao cha maelezo ya kwenda uko juu, yaani ili ni jengo kubwa sana hivyo mimi nilikuwa nikiitaji kwenda kwenye kampuni ya YOUNG AND RICH ni kampuni ambayo imebase sana na vijana ba ilijihusisha na bishara.

Niliangalia vizuri pale na kuona kuwa ni floor ya 15, hataka nimarudi kwenye lift na kwenda sehemu husika.

Kufika na kufika kwanza upande wa mapokezi nikakutana na yule mdada cheupe ambaye ananunuaga vitumbua kwetu..

"Weeeh cheupe usiniambie unafanya kazi hapa "

Nilizungumza kwa kumchangamkia sana.

"Yaaaah hivi kumbe sikukuambia, anyway unafanya nini hap"

Cheupe aliniuliza

"Aaah shoga angu weeh natafuta kazi, nimezunguka weeh hapo nje nimeona tangazo la nafasi za kazi nikasema ngoja nijaribu bahati yangu "

"Ooooh tena umewai dada, boss ameingia muda sio mrefu maana alitoka mara moja"

Basi cheupe akazungumza na secretary wao, na secretary akanisaidia kumuuliza boss wao kama naweza nikaenda kwenye ofisi yao.

"Lakinu kwanini aende kwa boss si lazima aanzie kaa HR??"

SECRETARY alimuuliza cheupe.

"HR hayupo nawe boss alisema kuwa waombaji ajila wote wanafikia kwake leo "

Hapo cheupe akaninong'oneza.

"Kuwa makini na boss "

Basi mguu mosi mguu pili mimi na secretary tukaanza safari ya kwenda kwa boss, hatimaye tulifika na ile kuingia tu yaani ni uso kwa uso na mkaka ambaye alinitupia pesa usoni baada ya kumfokea kwenye ngazi.

HAPA KAZI NAPATA KWELI JAMANI ? AU NDIO NITEMBEZE TU MIGUU YANGU ?
PENZI LA CEO NA AMORA
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 02
www.tupohapa.com

ANZA NAYO......

Mkaka huyo aliniangalia kWa muda kisha akazungumza.

“Niwasaidie nini ?”

Hapo secretary aliniangalia Mimi na kuna Namna niliona Kuwa huyu dada ni Kama Ana wasiwasi na hayuko comfortable.

Kwa upande wangu bado moyo wangu ulikuwa kwenye taaruki hivyo nilishindwa kujibu na wote tukajikuta tukiangaliana tu Kama tumepotea chumba.

“Tokeni nje “

Mkaka huyo alifoka.

Woiiiiiih nilishtuka maana sio kWa kufoka kiasi kile utazani kuna kitu tumemkosea.

“Boss huyu ndio msichana ambaye amekuja kuomba kazi “

Secretary wa watu mwaya alijikaza na kuzungumza.

“Huyu ndio anaomba kazi na wewe unataka nini hapa ??”

Yooooooh huyu kaka ni nzima kweli jamani 😂 sasa mtu si amenisindikiza Mimi ambaye sipajui.

Mdada wa watu aliniangalia kisha kWa utaratibu akatoka.

“”Umekuja kuomba kazi au kuongeza Pesa ??”

Mkaka huyo aliniuliza.

Nilimuangalia kisha nikajibu.

“Sorry about that, ni mistake yangu, ata hivyo Pesa zako hizi hapa “

Nilijibu kWa upole lakini kWa sauti Fulani hivi ya kuburi.

“Keep it, eeeh unataka kazi gani drama queen “


Alijibu uku akiachia tabasamu kWa mbali.

Nikaona huyu ni Kama ananiongelesha Sana hivi, kWa utaratibu nikatoa file langu lenye CV na kumkabizi.

“Sina haja ya kuangalia, utaanza kazi kesho, hakikisha ofisini kunakuwa safi kabisa, hakikisha Kuwa jikoni panakuwa vizuri, nenda kWa secretary pale atakuelekeza majukumu yako “

Hapo kwanza niliduwaa maana ni Kama nilikuwa simuelewi hivi, yaani anaongelea mambo ya jikoni Mara kufanya usafi, Yaani mtu Nina masters nzuri kabisa naanza kuambiwa kuhusu Sijui usafi ndio nini sasa..

“Sir ungepitia CV zangu “


Niliamua kumsisitiza.

“Fanya hivi, shika hizi cv zako halafu pita njia uliyokuja nayo na uende ukazeekee nyumbaani”

Eeeeh huyu kaka jamani, mkaka mzuri lakini KISILANI sasa.

“Lakini….”

Nilitaka kujitetea Tena lakini nikashindwa kwani alinizuia.

“Toka ofisini kwangu, utachagua kuchukua kazi niliyokupa au kuondoka, Nina shughuli nyingi sina muda wa kupiga Kelele na ma jobless “


Eeeeh hii ya Leo kisanga, kila sehemu uwa naenda kuomba kazi Ila hapa Niliyakanyaga, Yaani boss anakisilani utazani katoka kupokea taraka ukweni.

Kwakuwa Mimi Mwenyewe ni Kiongozi wa machizi, nilichukua file langu kwa hasira na kumwambia.

“Baki na ofisini yako “

Niliondoka nikiwa na hasira sana nilisahau ata Kuwaaga watu ambao walinipokea kwa Furaha sana.


Hatimaye nilifika Nyumbani lakini nilikuwa Nina hasira sana, Sawa uwa nazunguka sana kwaajili ya kutafuta kazi lakini sikuwai kukutana na ofisi ya kipuuzi kama hiyo.

“Kulikoni ??”

Babu yangu aliniuliza baada ya kuona Kuwa nimevimba sana kWa hasira Kana kwamba nilikuwa nataka kupasuka.

“Unajua kuna watu wengine ni Kama hawana akili hivi, Au Basi tufanye Kuwa akili Wanazo ila wamejawa na roho mbaya, sasa Mimi kosa langu ni nini ? Kwanza yeye ndio alinisukuma, halafu ata hivyo, hajapitia taarifa zangu halafu anataka niwe mfanya usafi, anawazimu “

Nilijibu kwa hasira uku nikizunguka uku na uku, babu yangu hakuweza kunielewa maana nilikuwa naelezea kama mlevi hivi 😂😂🙌.

Muda huo huo bibi yangu akaiingia, na kuzuungumza.

“Eeeeh naona Kisukari kimepanda mama kunywa maji “

Alizungumza bibi yangu uku akinipatia kikombe cha maji.

“Mjinga sana Yule “

Nilizungumza na kuchukua kikombe cha maji.

İle napeleka tu mdomoni ili nipate kunywa ni uso kWa uso na Mende haraka nikatupa kikombe chini na kuanza kulalamika.

“Kwahiyo mmepanga kuniua si ndio ? Yaani bibi unanipa maji yana mende kweli ?”

“Yaani unipite hapo nje pasi na kunisalimia halafu Mimi nikupe maji unywe ??”

Hapo nilijikuta tu nikutabasamu Yaani bibi yangu nae akili zake ni Mbili Walahi, Yaani kısa kutokumsalimia tu ndio ananipatia maji yenye mende.

Nilituliza hasira zangu na kuanza kuwasimulia kila kitu ambacho kilitokea na hapo babu akazungumza.

“Shukuru ata huyo amekupatia hiyo kazi, umezunguka sehemu ngapi pasi na kupata kazi yoyote ile ? Kila mtu amekupa majibu ya kukukatisha tamaa lakini huyo amekupa ata hiyo kazi na unakataa ? Amora najua Kuwa akili yako ni fupi lakini lazima ujue kujiongeza, Nafikili ungeanza na kazi hiyo hiyo then uendelee kutafuta nyingine, lakini pia Nafikili huyo huyo kuna siku anaweza aka kupatia kazi ni vile tu Leo mmeanza vibaya”

“Babu yako yuko sahihi…”

Alizungumza bibi yangu

Basi niliwasikiliza na niliwaelewa sana, baada ya muda nikafunga safari na kwenda kwa kina Cheupe Yaani kwa kina Yule Mdada ambaye anafanya kazi kwa boss Mwenye kisukari chake mjini”

Nilifika na kufanya nae mazungumzo kadhaa tu mwisho nikaomba Namba ya boss na kuondoka zangu, Sawa Namba nilipata shida inakuja kwenye kumpigia 😂🙌 Yaani nilijikuta namuogopa sana mkaka huyo, Yaani ndio kwanza tumeonana Mara moja lakini weeeh ni hatari na nusu.

Kiukweli nilishindwa kumpigia simu na hatimaye siku iliisha naa siku nyingine ilishika nafasi.

Asubuhi na mapema niliamka, nikasaidia kazi Mbili Tatu za pale Nyumbani kisha nikashika njia na kwenda kazini.

Mungu Mwema jamani, nilifika na nilikutana na wafanyakazi kadhaa na moja kwa moja nikazungumza na secretary ili aniambie majukumu yangu.

Majila Kama ya Saa 3 hivi, ndio nilimaliza kazi zangu zote pale ofisini, Yaani kazi ambazo nilielekezwa wa na secretary, ikumbukwe Kuwa wakati wote huo nilikuwa najifanyisha kazi lakini boss sikuwa nimemwambia kuwa kazi yake nimeipokea.

“Amora boss anakuita ofisini kwake “

Alizungumza secretary, muda huo Mimi nilikuwa nimejisimamisha tu kwenye chumba cha jikoni.

Sikupoteza muda baada ya dakika Mbili Tatu niliwasili kwenye chumba cha ofisi ya boss..

“Unatikisa kibiriti uku unajua kabisa Kuwa kimejaa”

Alizungumza boss baada ya Mimi kuingia ofisini kwake.

“Za asubuhi boss “

Nilimsalimia.

“Una miaka mingapi Binti ??”

Aliniuliza.

“Huyu nae miaka yangu ya nini sasa “

Nilijiuliza kimoyo moyo, nilikaa kimya kWa muda kisha nikajibu.

“26 boss”

“Ooooh sasa hizi za asubuhi sijjui za Saa hizi achana nazo, inakupasa uwe unaniamkia uku unatambaa “

Eeeh hii ya Leo Kali sasa, Yaani nimsalimie mtu uku natambaa ? Hao wazazi tu na walezi wangu siwasalimiii Kama ambavyo yeye anataka, kWa sauti ya mshangao wa hali ya juu nikamuuliza.


“Nikiwa Natambaa ??”

“Ndio “

Nilitamani kumpa jibu lake moja matata, lakini nilijikuta tu na kukubali.

“Sawa boss “

“Unaitwa Nani ??”

Baada tu ya kukubali nikaulizwa swali lingine.

“Naitwa Amora “

İli swali Nilijibu pasi na kuleta utata.

“Amora, nimefurahishwa na kazi zako, ofisi inang’aa sana nimependa, keep going, aaah MKATABA wako upo kaa sharifa utaupitia na kusaini kazi njema”

Basi nilimaliza mazungumzo na boss kisha nikageuka kwaajili ya kuondoka Ila nafungua tu mlango, kwanza nikakutana uso kwa uso na Msichana mrembo sana, alikuwa Mdada Fulani hivi, White nini, nywele ya bei Kali.

“So Mimi napiga simu upokei kumbe uko bize unabebika na huyu nguruwe pori”

Alilallamika msichaana huyu baada ya kuingia.

Walahi Mikosi ni mikosi tu, Yaani ata mtu umjui Hamjawai kukutana tayali anakuita nguruwe pori nyie 😂🙌 nika…….

ITAENDELEA…





PENZI LA CEO NA AMORA
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 03
www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

🤍🤎🤍🤎🤍🤎🤍🤎

Nilibaki nikiwa nimetoa tu macho , boss aliniangalia kisha akanifokea.

“Unanidai ??”

“Mmmmh “

Niliishia kuguna maana sikuwa nimeelewa anamaanisha nini.

“Toka nje wewe “
Eeeh hapo ndio nilifokewa kwa sauti ya juu kabisa na katika harakati za kutoka nje haraka haraka, nikajikuta nikianguka chini Kama Mzigo.

Walahi mtu mzima kuanguka ni aibu sana, kitu cha kushukuru ni kwamba nilionwa na watu Wawili tu, Yaani boss na huyo mgeni wake mpuuzi.

“Mbona unachechemea ??”

Aliniuliza mfanyakazi mwenzangu wa kiume, ambaye tangu Nimeonana nae amekuwa ni mkaka mkalimu sana.

“Aaaah nimeumia kidogo kwenye Goti “

Nilijibu.

“Ungepumzika sehemu moja”

Alizungumza mkaka huyo kisha akanishika mkono ili kunisaidia kwenda kukaa kwenye benchi lililokuwepo Karibu na meza ya mapokezi.

“Kulikoni wenzetu Mbona kushikana ??”

Cheupe aliuliza maana tulimkuta hapo kwa secretary.

Aaah kwakuwa Cheupe nimemzoea nikacheka kisha nikajibu.

“Nimeanguka hapo kwa boss, Yaani daaaah nimeumia sio Mchezo”

Hapo Cheupe na mkaka ambaye alinishika waliangaliana na kisha wakagonganisha mikono Yao na kucheka kishambenga.

Walahi hii ilinishangaza sana, Yaani hii ofisi ina kila aina ya kuoja, sasa Mimi kuanguka tu ndio wao wacheke kwa staili hiyo, nilitamani kuzungumza kitu lakini nilitulia ukizingatia ni siku yangu ya kwanza kazini.

Muda huo huo simu ya secretary iliita, haraka akapokea, baada ya muda akakata na kuzungumza.

“Unaitwa kWa boss uko “

Mkaka ambaye alinishika akauliza.

“Hapa ni Nani anaitwa sasa??”

“Amora”

Hapo ndipo mkaka huyo akagundua Jina langu na kwa shauku akazungumza.

“Unique name, ndio maana mzuri Kama Jina lako “

Kila mtu akacheka kisha Cheupe akazungumza.


“Wewe Tena usione kitu mbele yako mbwa wewe “

Eeeh hii ofisini nimeshaichoka, Niliinuka na kwenda nilikokuwa nimeitwa.

“Abeeeh boss “

Niliitika baada ya kufika.

“Amora sio ??”

Msichana ambaye alikuwa na boss aliniuliza.

“Ni Mimi madam”

“Ouk, kwanza umeniita vizuri sana madaaaam waooooh, Ila hapo kwenye madam ongezea Ruby, Yaani madam ruby, nimekuita ili unijue na unitambue kiundani zaidi”

Nilitulia Kama Maji ya kwenye mtungi hili nikisikiliza kitu ambacho nilikuwa nambiwa.

“Ruby please hii ni ofisini ujue “

Boss alimwambia ruby.

“Frank, relax babe aaaah”

Hapo na Mimi ndio nikajua Kuwa boss wetu anaitwa frank, imagine nimeanza na kazi kabisa na Jina la boss sikuwa nalijua 😂🙌.

“Naitwa Ruby na sio tu Ruby, mimi ni mwanamke wa boss wako hapa, Mimi ndio usingizi wake, utamu wake na kila kitu, kabla ujakaa na wenzio kuanza kukupa Maneno ya umbea Naomba Nikujuze Mimi Mwenyewe Kuwa, kaa mbali na mwanaume wangu, maana nyie mabinti wa low class uwa amuachi kitu kikipita mbele yenu “

Eeeh ya Leo Kali Walahi, nilibaki Kuwa msikilizaji tu na baada ya hapo nikawaaga na kutoka nje.

Muda kwakweli ulikuwa umesogea hivyo niliingia jikoni na Kuanza kuandaa chakula cha mchana kwani ni moja kati ya majukumu yangu.

Nikiwa jikoni napika gafla akaingia mkaka Yule ambaye ni Mcheshi sana.

“Amora”

“Nambie “

“Unatupikia nini Leo ? Maana daaah nilishachokaga kwenda kula nje Pesa zilikuwa zinaisha tu “


“Ratina ni ndizi nyama”

“Waooooh “
Story ziliendelea pale mwisho akazungumza.

“Naitwa Shabani maana naona ata uniulizi Jina langu au wameshakutajia ??”

“Nalijua “

Nilimjibu tu ingawa sikuwa nikilifahamu.

Kabla mkaka huyo ajajibu boss akaingia jikoni.

Walahi hapo nilimuona Shabani akitetemeka sana, nilimuangalia na kubaki nikishangaa tu.

“Hii ni ofisi yako Mpya ??”

Boss frank alimuuliza Shabani.

“Hapana boss, aaaah, aaah, nilifuata maji ya kunywa, aaah kikombe cha chai au Basi, sitaki Tena “

Wenge la Shabani lilinifanya nicheke tu maana daaah sio kwa kujiongelesha mfululizo.

“Potea hapa”

Shabani alitoka mbio pasi na kugeuka nyuma na msala ukaamia kwangu.

“Alikuwa anafanya nini uku ??”

Boss aliniuliza..

“Amefika muda sio Mrefu hivyo ata Mimi si fahamu amekuja Kufanya nini “

Nilijibu kwa utulivu uku nikiendelea na mapishi.

“Unaishi wapi Amora ??”

Boss aliniuliza ya na kwa sauti ya utulivu mpaka nikashangaa.

“Buza “

Nyie Nilijibu kWa sauti ya chini sana, sauti ambayo ata Mimi wenye we niliisikia kwakuwa Mimi ndio nilizungumza 😂🙌 imagine unamwambia mtu Kuwa Unaishi kWa mpalangee weeeh 😎😁.

“Wapi ??”

Boss aliniuliza kwani hakuwa amenisikia.

“Buza “

“Ooooooh, Mbona mbali sana, lakini ndio utafutaji huo “

Alijibu na kuondoka.

Tangu Nimemjua huyu kaka Leo ni siku ya pili lakini naweza kusema Kuwa kWa sasa ndio amezungumza na Mimi kwa utulivu maana yeye Mara nyingi uwa Anafoka tu kama huyo mwanamke wake.

Majila ya kuondoka Nyumbani, nilitoka nje na kubaki nikimtegea Cheupe ili aweze kunipa lift kwani alikuwa amekuwa na gari kwa siku hiyo.

“Wewe Mbona bado upo hapa ??”

Cheupe aliniuliza baada ya kunikuta nje ikiwa niliwaaga muda Mrefu sana.

“Eeeh nilikuwa nakusuubili shoga yangu unipe lift maana Pesa niliyokuwa nayo haitoshi chochote kile, Yaani ata daladala moja sipandi”

“Eeeeh pole me kuna sehemu naenda sote ni watu wazima naenda kwa babe wangu “

Nilibaki nikimtumbulia macho tu, nilitamani kumuomba ata buku tu ili kuweza kufika Nyumbani lakini sikuweza. Kabisa nilijikuta nikiona aibu .

Kila mtu allipanda kwenye gari na kuondoka zake, kWa upande wangu nilibaki nikiendelea kushangaa, muda huo huo Shabani akatoka nje.

“Nikiendelea kuona aibu nitalala hapa “

Nilijiambia kimoyomoyo kisha nikamsogelea Shabani na kumuelezea shida yangu.

“Ooooh hakuna shida Mtoto mzuri me nitakupa lift mpaka kwenye kile Kituo cha mbele ili upate urahisi wa kuondoka”

“Utakuwa umenisaidia sana “

Pasi na kupoteza muda nikaingia Ndani ya gari, lakini kabla hatujaondoka boss akatokea na kuzungumza kwa hasira.

“Wewe shuka uko “

Jamani huyu Kijana Sijui linataka nini Walahi, boss ni boss Bwana nilishuka kwenye gari na Shabani akaambiwa aondoke.

“Kuna kazi nyingine au ??”

Nilimuuliza boss, boss wangu Bwana hakujibu kitu zaidi aka……..

NAKUJA MY ZANGU HUYU BOSS ANAJUA KUNIVULUGA


PENZI LA CEO NA AMORA
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 04
www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

🤎🤍🤎🤍🤎🤍🤎🤍

Boss akanishika mkono na kuniongoza kuelekea kwenye gari yake.

“Unanipeleka wapi ??”

Nilimuuliza nikiwa na wasiwasi sana maana boss Mwenyewe huyu ata aeleweki dakika Mbili mbele.


“Kukuchuna ngozi”

Alijibu boss Tena alionekana Kuwa serious sana na jibu lake.

Nilimuangalia kWa muda uku kasi ya kutetemeka ikiongezeka, tulifika kwenye gari yake akaniachia na kufungua mlango na kuniambia.

“Panda “

Weeeeh mtu ameshaniaambia anataka kunichuna ngozi naanzaeje kupanda 🙌😂 tuheshimiane, niko lazi nitembee Kuanzia uku Morocco mpaka Buza.

Kitendo cha kuachiwa tu nilinyoosha miguu yangu nikitaka kukimbia lakini nilidaka Kama kumbikumbi aliyekosa mabawa, mwanaume ni mwanaume chap nikaingizwa kwenye gari.

“Lakini kosa langu nini Aswa, Kama utaki Mimi kufanya kazi kwenye ofisini yako ni sawa tu nitaacha”

Nilizungumza uku nikitamani kulia, boss aliniangalia kisha akacheka sana na kuzungumza.

“Nitakupeleka mpaka Nyumbani, naitaji kukufahamu kiasi “

Mmmh huyu sasa Naye ananichanganya, anataka kufahamu nini sasa.

“Kwetu ni mbali”
Nilijiuongelesha tu.

Safari ikaanza na kuna Namna Mimi na boss tukaanza kupiga story, na pia niliona Kuwa boss uwa na panda Mbili, pande ya kwanza ni utulivu na ya pili ni hiyo ya ukali aswa ikija kwenye suala la kazi.

Hatimaye tulifika Nyumbani, Walahi Jumba letu ni Chakavu sana mpaka kuna Namna nilianza kuona aibu bora nisingemfikisha Nyumbani.

“Asante sana Mungu akubariki “

Nilimwambia boss.

“Usijali”

Nilishika mlango nakutaka kushuka lakini boss akanishika mkono na kunipatia elfu kumi.

“Itakusaidia kWa nauli kesho “

Weeeeeeh majilani 😂🙌 Kama ni process za kuchunwa ngozi ndio zinaanzaga hivyo Basi huyu mkaka atanipata Walahi, Yaani Mimi na Pesa ni shwaaah, Mimi na Pesa ni Kama watoto na pipi Muda wowote Natekwa.

Walahi kwenye Pesa uwa sioni aibu haraka nikapokea na kumshukuru na kushuka, kabla hajaondoka nikazungumza.

“Ufike salama Tajiri Angu “

Muda huo mama yangu alikuwa amesimama tu akiniangalia uku akiwa amenishikia kiuno, gari ya boss wangu ilivyoondoka tu nikashtuka nikipigwa na ndala ya mgongoni.

“Hiiiiiih mama jamani “

Nililallamika maana ndala iliniuma Bwana.

“Mama kitu gani, umepata kazi Jana tu Leo unaturudia na magari Makubwa si ndio ? Unaweza kuniambia Yule ni Nani ? Amora utakuja uchinjwe wewe paka Mweusi wewe “

Iko hivi jamani, nilishawai kupotea kipindi nasoma sekondary, mambo ya lifti yaliniponza hivyo mama yangu mpaka Leo Ana wasiwasi sana juu yangu na ukizingatia Mimi ndiye Mtoto wake wa Pekee kama ambavyo yeye alivyo kwa wazazi wake.

“Mama Yule ni boss wangu lakini “

Nilijibu lakini mama hakunielewa aliendelea kufoka na kulalamika.

Majila ya usiku tukiwa Tunapata chakula nikaanza.

“Nani alichukua Pesa yangu kwenye mkoba wangu ? “

Niliuliza maana nilikuwa na zile Pesa ambazo alinipatia boss frank siku ya kwanza kabisa ambayo alinisukuma.

Kila mtu alikataa Kuwa hajachuka na hii ilinichanganya sana.

********

Siku ziliendelea kwenda na hatimaye niliweza kutimiza miezi miwili kazini na niseme Kuwa naipenda snaa kazi yangu, Walahi nainjoy sana mambo ya jikoni.

Ukiachana na jikoni, kWa wakati huo boss alikuwa ni Rafiki yangu mkubwa sana, Sawa alikuwa ni mtu mkali mkali lakini kuna muda nilikuwa nikipiga nae sana story.

Ikiwa ni siku ya weekend, nikiwa nimetulia tu mtaani sina ili Wala lil, niliweza kupokea simu kutoka kwa boss wangu.

“Uko free Amora tunaweza tukatoka ??”

Boss aliniuliza pale tu nilipopokea simu yangu hakukuwa ata na salamu ni shwaaaah.

“Leo au ??”

“Yaaah usiku Kama inawezekana”

“Aaaahh eeeh usiku sio kweli huyu mama yangu anaweza akanitoa masikio “

Nilijibu.

Mama yangu ni ananilinda kuliko kitu chochote, Mara nyingi amekuwa akisema Kuwa ataki nipotee Kama ambavyo yeye alipotea , ilifikia hatua mama pale Nyumbani akawa ataki mpangaji wa kiume ambaye ajaoa.

“Basi sasa hivi Kama inawezekana”

Boss aliniambia.

Kwakuwa ilikuwa ni mchana, nilikubali na sikupoteza muda chapu nikaenda kujiandaa, mama yangu nilimpa uongo wa hapa na pale na kwakuwa ni mchana akakubali.

KWa Mara ya kwanza Amora Mimi nikaingia kwenye hotel moja kubwa sana, Walahi ushamba Mzigo, nilikuwa nikishangaa kuliko kawaida.

Tulifika na kuagiza chakula, Walahi chakula kulikuwa kuzuri sana nyama Kama zote.

“Mimi sina Furaha Ata kidogo Amora “

Alizungumza boss Wangu nami nikamuuliza.

“Kwanini boss??”

“Niite frank Bwana aaah au unataka kila mtu ajue Kuwa wewe ni mfanyakazi wangu au ? “

“Sawa frank”

“Siitaji kumuoa Ruby, Ila mama yangu ndio anampenda sana ruby “

Alizungumza boss frank, kwa muda huo alikuwa ameshaanza kulewa maana alikuwa akinywa sana pombe Tena zile Kali Kali.

“Ruby na mama yangu ni zaidi ya mashetani, Amora Shukuru Mungu umepata familia inayokujali sana, Mimi mama yangu alinitelekeza, alinitesa sana halafu Leo hii anataka kuniendesha “

Alizungumza boss frank na kuanza kulia, Ila Mimi jamani Sijui ndio machozi ya Karibu au ni kitu gani maana nilijikuta nikianza kulia na Mimi badala ya kumtuliza mkaka wa watu.

Tulilia kwa muda na kila mtu aliamini Kuwa tulilewa lakini ukweli ni kwamba Mimi uwa sinywi pombe Yaani kabisa na ata siku hiyo siku sikuwa nimekunywa Ila nililia kutokana frank alivyokuwa alkilia.

Baada ya muda wahudumu walikuja na kutuongoza kwenye chumba cha hotel, nilishangaa sana baada ya kukuta Picha za frank kwenye chumba icho, yaani chumba cha hotel inakuwaje kuna Kuwa na Picha za frank.

KWa upande wa frank ndio alikuwa ajitambui kabisa kwani alishazima na kuzima kutoka na kulewa sana.

Muda ulizidi kusogea na hatimaye Saa 6 usiku ilinikuta kwenye chumba iko nikisubili frank aweze kuamka, kWa wakati huo mama Yangu alikuwa alinipigia sana simu, nilimtumia tu ujumbe Kuwa niko Sawa kisha nikazima simu yangu.

********

KWa upande wa frank Bwana pombe zilikuja kumuisha Saa 11 alfajil, kWa wakati huo Mimi ndio kwanza nilikuwa nakoloma kwenye kochi.
Hatimaye kulipambazuka na niliamka, ile kufungua macho tu uso kwa uso na frank ambaye alikuwa ameniinamia kabisa akiniangalia.

“Aaaaaaah “
Nilipiga ukunga maana ilikuwa gafla sana na aliniinamia sana.

“Ndio nini sasa ??”

Nilimuuliza na sauti yangu ya usingizi.

“Mwanangu unakoloma Kama trekta “

Alizungumza frank na kunifanya nione aibu maana daaah kuhusu kukoloma ni nakoloma sana mpaka mama uwa analalamika sana.

“Achana na habari za kukoloma frank ni Saa ngapi ??”

“Saa nne “

Weeeeh macho yalinitoka jamani, Yaani nimelala nje ya Nyumbani na bado nimelala mpaka Saa 4.

“Oooooh Leo mama yangu ananifanya Kuwa kitoweo “

Nilizungumza kwa uwoga sana.

“İla unanichanganya sana Amora, Yaani wewe ni mtu mzima, hausomi, Unafanya kazi lakini Kwanini mama yako anakulinda kiasi iko ? “

Frank aliniuliza maana alikuwa naona mapicha Picha tu.

Hapo nilijikuta nikiaanza kumuelezea frank kila kitu kuhusu maisha yangu a familia yangu, jinsi ambavyo wanaangaika kwaajili yangu na kila kitu.

“Am sorry Amora, nisamehe kwa kila kitu, Naomba niwe mkweli, sababu ya Mimi kutokupitia CV zako ni dharau, niliamini Kuwa hakuna chochote cha ziada kutoka kwako, sikujua Kuwa wewe ni msomi kiasi iko “

“Ni Sawa “
Nilijibu uku machozi yakinitoka, nyie mama yangu kaangaika kunisomesha halafu Leo hii mtu ananidharau daaah.


Frank alinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu kabisa, hapo nilitulia kwenye kifua chake na kusikilizia mapigo yake ya moyo yanavyoenda kasi.

Baada ya muda tulijiandaa kisha Mimi na frank tukaongozana kwenda Nyumbani.

“Frank sikia usifike mpaka Nyumbani “

Nilimwambia frank tukiwa njiani na tulikuwa tunakaribia kufika Nyumbani.

“Ni makosa yangu”

KWa pamoja Mimi na frank tulifika Nyumbani na kwa Mara ya kwanza frank akashuka kwenye gari yake kwani Mara nyingi uwa ananishusha na kuondoka.

“Karibuni sana “

Mama yangu alitukaribisha kwa utulivu wa hali ya juu na ili lilinishtua sana.

“Aaaah babu, bibi na mama hapa, Naomba nitangulize samahani kwa kila kitu, aaaah Jana Mimi na secretary wangu hapa, tulijikuta Kuwa kazi nyingi sana ingawa sio siku ya kazi, nikamuomba tuendelee kufanya kazi na nitamlipa kwa bonus “

Hapo kwanza jicho lilinitoka, huyu kaka anazidi kunitafutia matatizo, Nyumbani wanajua Kuwa Mimi ni mtu wa usafi tu na mapishi halafu yeye anasema Kuwa Mimi ni secretary wake binafsiii 😂🙏 ili bomu analopika mlipuko wake sio wa kitoto.

Hatimaye maongezi yaliisha na Frank akaondoka zake.

Kitendo cha frank kupotea tu kwanza nilipigwa bao moja zito sana mgongoni nika…..

HUYU MAMA YANGU ATANIUA WALAHI….


PENZI LA CEO NA AMORA
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 05
www.tupohapa.com

SONGA NAYO…..

🤎🤍🤎🤍🤎🤍🤎🤍

Walahi nilipigwa jamani, yani kosa langu ni kulala nje ya Nyumbani hakuna kitu kingine.

Majila ya Saa 11 jioni, Mimi na shoga yangu tulijinyanyua wenye we miguu mosi miguu pili tukaenda barabarani kwaajili ya kula miguu ya kuku, Bwana siku hiyo nilikuwa na Pesa Mzigo ulitema kutoka kwa boss frank.

Nikiwa bize nakula miguu yakuku, nilishtuka sana baada ya kusikia sauti nzito ya kiume ikiniuliza.

“Unaninunulia mingapi ??”

Hakuwa mwingine Bali ni frank, mkiniuliza kafikaje fikaje Walahi sina majibu maana ata Mimi sikumuona wakati anakuja.

“Wewe Tena Kama mzimu “

Nilimwambia.

Hapo alinishika mkono na kunisogeza pembeni kisha akazungumza.

“Nimekuletea mavazi ya kuvaa kesho kazini “

“Mmmmh “

Niliguna uku nikimuangalia usoni, eeeh Mbona gafla tumeanza kununuliana nguo.

“Unamaanisha nini nguo za kuvaa kesho “

“Kuanzia sasa wewe ni personal secretary wangu, tutatumia ofisi moja na kazi inaanza kesho. I want you to look different, naitaji uwe na muonekano wa elimu yako Sawa”

“Frank Unanitania “

Nilishindwa kuamini kabisa, Yaani gafla tu anabadili historia ya maisha yangu.

KWa Furaha ambayo nilikuwa nayo, nilishindwa kabisa kuvumilia kwa nguvu nikamkumbatia na kuzungumza.

“Asante sana frank wangu nakupenda “

Eeeeeh nyieeeeh 😂🙌 Mbona Kama Binti yenu nimelopoka hivi, Naomba niwaibie Siri, Walahi nampenda sana huyu mkaka ni vile Mimi na yeye ni level Mbili tofauti, lakini pia kitu ambacho nashindwa ni kumtongoza, Ila Walahi nampenda Sijui nafanyaje, sijali kuwa anamchumba wake au laaah.

Hivi ushawai kufikia hatua ya kumpenda mtu mpaka akikufokea unaona Kama anakuimbia ? Basi huyu ni Mimi, Yaani kipindi cha mwanzo wakati ananifokea nilikuwa naona Kama ananibembeleza hivi 😁.

“Nakupenda secretary wangu “
Alijibu frank lakini hakuwa ameelewa maana halisi ya nakupenda yangu.

Alinikabizi mizigo yangu kisha akakata na kuondoka.

“Weeeh Yule ndio shemeji au ??”

Rafiki yangu aliniuliza.

“Ahaha we nawe, Rafiki yangu Yule nilisoma nae”

“Mmmh ndio Mikumbato yote ile ? Au uniambie tu jamani kwani hata mimi hauniamini ??”

“Acha ujinga wako wewe “

******

Hatimaye siku nyingine ikashika nafasi jamani, niliamka asubuhi na mapema na. Kujiandaa, nyieeeeh niliwaka hatari, Sijui frank Namba ya viatu vyangu alijulia wapi lakini kiatu alichoniletea ni size yangu kabisa, ukirudi kwenye mavazi ndio kabisa, ukirudi kwenye wigi weeeeeeh ndio usiseme Mtoto wa kishua huyu hapa.

“How do I look mama “”?

Nilimuuliza mama yangu ambaye kwa wakati huo alikuwa anachoma zake Vitumbua.

“Ujapendeza “

Mama alinitania.

Kwakuwa nilikuwa naenda kuanza kazi Mpya familia yangu ilinipatia baraka na kisha nikaondoka.

Picha linaanza kwanza siku hiyo nili request , yaani Sikupanda daladala nilikodi Bajaji ambayo ilinifikisha mpaka ofisini.

Siku hiyo naweza kusema Kuwa mimi ndio mtu wa mwisho kufika ofisini, Ile nafikaa Kwanza nikakutana na kikao cha kuniteta pale kwa secretary ambapo Cheupe pia alikuwepo.

“Ndio hivyo mwaya katimuliwa me wakati NAKUJA uku nimemuacha kwao anachoma vitumbua kama kawaida yake “

Alizungumza Cheupe, Ila nyie huyu dada ni muongo Walahi 😂 Mimi na yeye tumeonana wapi lakini.

“Kazidi nae aaah akwendege uko. Kwanza alikuwa ananinyima amani ule ukaribu wake na Shabani wangu “


Eeeh kWa siku hii sasa ndio nilijua Kuwa secretary ni demu wa Shabani, mkaka ambaye nimemzoea sana hapa ofisini.

Muda huo huo nikaamua kujitokeza na cut walk wangu moja matata, kiatu changu kirefu hakikuacha kupiga Kelele maana kilichongoka sana.

Kila mtu hakuamini baada ya kuniona maana nilipendeza sana .

“Habari zenu “

Niliwasalimia kisha nikapita ZAngu sikuwa na haja ya kusubili majibu Yao.

Moja kwa moja nikaenda ofisini kWa boss.

“Talaaaaaah “

Nilimshtua boss uku nikijizungusha aweze kuniona nilivyopendeza.

Frank alibaki akinishangaa tu, Kila kitu Amenunua yeye lakini aamini jinsi nilivyopendeza.


“Waooooh “

Siku hiyo Bwana boss akaitisha kikao na kuwatambukisha watu Kuwa Mimi ni secretary wake tu.

“So Kuanzia sasa kabla ujawasiliana na Mimi hakikisha Kuwa umewasiliana na madam Amora “

Weeeeeh nimeanzakuitwa madam uku.

*******

Siku ziliendeea kwenda uku nikifanya kazi ofisi moja kabisa na frank, Yaani huyu kaka ni Kila siku anazidi kunivutia kwenye macho yangu, Zoezi la kumwambia Kuwa nampenda lilikuwa gumu sana.

Ikiwa ni siku ya jumatano na ni siku ya kazini, nilijifungia chumbani kwangu na ilikuwa nu asubuhi, nilishika simu yangu na kumpigia frank.

“Amora kuna shinda gani mama Mbona Ujafika ofisini ??”

Frank aliniuliza baada ya kupokea simu yangu.

“Siko Sawa boss wangu siko Sawa frank “

Nilizungumza kWa kulia kabisa mwisho nikakata simu.

My zangu sikuwa na shida yoyote ile, hii ni michezo yangu tu nikitaka kumuweka frank kwenye njia zangu, Walahi siwezi kumkosa huyu kaka.

Muda huo huo simu yangu ikaita na frank ndio alikuwa anapiga.

“Uko Nyumbani au ??”

Frank aliniuliza.

“Ndio “

“NAKUJA “

Jibu la frank lilinipa Raha sana, nilikata simu na kuweka Picha yake kisha nikaikisi uku nikijichekeesha.

“We Amora Kama uwendi kazini toka uje uoshe vyombo”

Alizungumza Mama yangu, kwakweli zoezi la kuosha vyombo sio kweli kabisa je frank akinikuta naosha vyombo si msala huu.

“Najianda mama tuna kikao na ofisi nyingine hivyo boss atanipitia “

Nilimdanganya mama yangu.

Baada ya hapo nilijiandaa na kubaki nikimsubili boss wangu.

Baada ya Kama Lisa limoja hivi frank alifika na alionesha Kuwa na wasiwasi sana.

“Mama bye “

Niliaga na kukimbilia kwenye gari, sikutaka frank ashuke maana mambo yangeweza kuharibika.

“Kuna shida gani umenitisha sana “

Frank aliniuliza na alionesha Kuwa na wasiwasi sana.

kWa sauti ya kulia nikazungumza.

“Naomba ondoa gari, nipeleke sehemu iliyotulia sana, sehemu ambayo naweza nikatulia”


Frank wangu hanaga mbambamba Bwana, safari yangu na frank iliishia kwenye chumba cha hotel ambayo tulilala siku ile ambayo alilewa sana.

“Hapa ni Sawa ??”

Frank aliniuliza.

“Yaaah”

“Shida nini jamani Yaani unaniweka roho juu”

“Nimeachwa “

Nilijibu uku nikiangalia chini “

“Nini wewe ??”

Frank aliniuliza kwa mshangao Kana kwamba hakuwa ametalajia jibu Kama ilo.

“Najua uwezi kunielewa kwakuwa wewe na Ruby mnapendana sana, nilikuwa na mwanaume ambaye alitoa kwetu barua ya uchumba, alionesha kila dalili ya kunioa lakini Jana ameoa “

Nilimdanganya mkaka wa watu mwaya 😂.

Hapo frank sasa akanielewa na kunionea huruma sana,kwakuwa alikuwa amekaa Karibu yangu, akanivuta na kunikumbatia.

Nilijiliza kWa muda kisha nikazungumza Tena.

“Mama yangu Sijui atalipokeaje ili “

“Kila kitu kitakuwa Sawa Amora Sawa mama ??”

Weeeeh nimeanza kuitwa mama sasa, lakini Mbona aoneshi kama na Mimi Ananipenda au ndio Nipo kwaajili ya kujizalilisha.

*******

Siku ziliendelea kwenda na hatimaye nikatimiza miezi miwili nikiwa Kama secretary kwenye ofisini ya boss frank.

Tukiwa ofisini, Frank aliinuka kwenye kitu chake na kuja kwenye meza yangu kisha akaniuliza.

“Umeshafikilia Kuwa na mahusiano mapya ??”

Swali lake lilinistua sana, kWa wakati huo nikishaona Kuwa kumpata frank sio kazi rahisi, Yaani nilishauambia moyo wangu Kuwa. Frank awezi Kuwa wako.

Nikimuangalia frank kisha nikamuuliza.

“Kwanini umeniuliza hivyo ??”

Frank alitabasamu kisha akanisogelea sikioni na kuning’oneza.

“Nataka kuuteka moyo wako “

Weeeeh nyie huyu ataniua na presha Mtoto wa mwanaume mwenzie.

Nilibaki nikimlegezea macho tu, Ila mapenzi ni uchizi Yaani anazungumza Mimi mawazo yalishaenda mbali kabisa, boss frank aliniangalia na kuniuliza.

“Uko tayali ??”

Weeeh naanzaje kukataa ? Bora mniite maharage ya Mbeya lakini sio kumkataa huyu mkaka.

“I love u frank “

Nilizungumza KWa sauti ya chini sana yenye kumaanisha.

Pasi na kupoteza muda, frank alinisogelea Karibu zaidi na tukaanza kukiss pasi na kujali Kuwa hapo ni ofisini.

Zoezi lilikuwa ni rasmi kabisa jamani, Mimi ndio nilikuwa naona ni kama tayali tupo chumbani hivi 😂🙌 Ila khaaaahh na Mimi nimezidi sasa.

Kiss likiwa limenoga gafla mlango ukafunguliwa Na Ruby akaingia.

🥹🥹 EEEEH NINI KITATOKEA TUKUTANE SEHEMU IJAYO….


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote