PENZI LA KULAZIMISHA (Mafia Na Wakili)

book cover og

Utangulizi

Penzi la kulazimishwa

Ni simulizi inayomuingizia binti Carina ambae alikuwa kasomea maswala ya sheria pia alitoka kwenye familia ya hali ya kawaida baba yao alipambana na kufanya kazi hata za kudhalilika ilimladi akidhi mahitaji ya familia yake.
Carina anagundua hili anajisikia vibaya sana kuona baba yake anafanyishwa kazi ambazo hakuwahi kutegemea kuanzia siku hiyo ana kuahidi baba yake kuja kuniheshimisha anausaka kazi kwa udi na uvumba na bahati inaangukia upande wake anapata kazi mkoani huko anaenda kufanya kazi kwa bidii kubwa sana mpaka kupelekea kupendwa sana na mkubwa wake wa kazi.

Siku moja kuna watu walienda ofisini kwao kutaka wakili wa kumsimamia kijana tajiri, wengi waliamini kuwa ni mafia (Tigger) mr Patrick anauliza mawakili nani yupo tayari kusimamia kesi ya Tigger?
Mawakili wote walinyamaza lakini ghafla ilisikika sauti ya carina akikubali .
Carina anakutana na Tigger lakini Tigger anaonyesha kumdharau na kumuita mchumba. Kitendo hicho kina mkera sana Carina.
Carina anapambana mpaka anashinda kesi na hapo ndipo ulikuwa mwanzo wa Tigger kumkubali na kumpenda sana Carina akimuweka karibu kama rafiki huku akimpa zawadi kedekede mwisho wa siku anamtambua anampenda.
Carina anamcheka sana na kudai hajui hata kutongoza wakati huo Tigger anajiona yupo romantic. Kitendo cha kucheka kina muudhi hapo ndipo Tigger anaamua kulazimisha penzi yani lazima utanipenda na kama haujawahi kunipenda utajifunza tu siwezi kuteseka sababu ya mapenzi.
Je unataka kujua nini kinaendelea ndani ya hii simulizi yetu ya penzi la kulazimishwa? Basi ungana nami upate burudani mwanzo ,mwisho.

PENZI LA KULAZIMISHA
(MAFIA NA WAKILI) 1
MTUNZI SMILE SHINE

Carina ni binti wa miaka 25 , ni binti aliebarikiwa kuwa na akili sana anatoka katika familia ya watoto 5 yeye akiwa mtoto wa pili. Bwana na bibi Abdu ndio wazazi wake wa kumzaa.
Familia yao ilikuwa ni familia ya kawaida sana lakini wazazi wao walijitahidi sana kuwapambania kwenye swala la elimu . Licha ya wazazi kupambana lakini watoto wawili ndio walifanikiwa kushikamana na elimu.
Dada yao mkubwa Safina aliishia kidato cha pili akaishia kubeba mimba na sasa yupo kwa mume, carina amefanikiwa kuhitimu chuo cha sheria, Ibrahim yeye alikuwa mtoro shuleni kutokana na jitihada za wazazi alijitahidi sana akaishia darasa la saba na sasa hayupo nyumbani inasemekana alizamia huko africa kusini, zamda ni mama nitilie na Halfan yupo kidato cha tano.

Kutokana na maisha yao kuwa chini baba yao alifanya kazi yoyote kuhakikisha kuwa Halfani anasoma na kuhitimu masomo yake ,watu walimzarau sana baba yao kutokana na kuwa na kipato kidogo na maisha yao kuwa ya kubangaiza
" Siku moja carina alikuwa anatoka kwenye mihangaiko yake akapita sehemu akamuona baba yake akiwa anafanyishwa kazi ya kubeba mizigo kwenye nyumba ya muhindi mmoja na kutumwa kama mtoto mdogo tena huku akifokewa. Carina aliumizwa sana na ile hali ya baba yake kutumikishwa alitaka kuondoka ili baba yake asimuone maana alihisi huenda akimuona atajisikia vibaya. Lakini kwa bahati mbaya akiwa anaondoka baba yake aliangalia sehemu alipo na kufanya waangaliane, baba yake alionyesha kushituka lakini carina aligeuza macho yake haraka akaondoka akarudi nyumbani huku moyo wake ukiwa unasononeka kwa kile alichokiona hakujua kama baba yake anatumikiahwa vile kila siku aliaga anaenda kazini akajua anafanya kazi ya maana kumbe ilikuwa ni tofauti na ahavyofikiria.
" Weeee Mungu wangu nitoe nguvu kwenye hili mbona maumivu yake kama nashindwa kuvumilia. MUNGU wangu mfanyie wepesi baba yangu mpe rizki maana anayopitia kwa ule umri hastahili . MUNGU nisaidie nipate kazi niikomboe familia yangu.
Carina aliomba MUNGU amfanyie wepesi kwenye kutafuta kazi ili asaidie familia yake. Siku hiyo alishinda akiwa hana furaha .

Jioni akiwa amekaa nje anapanga na kupangua , akiwaza na kuwazua mara baba yake alirudi kutoka kibaruani kwake.
" Shikamoo baba.
" Marahaba.
" Baba tunaweza kuongea? Carina alimuomba baba yake,
Baba yake alisogea alipokuwa amekaa na kukaa pembeni yake.
" Baba ile ndio kazi unayofanya?
Carina aliuliza na baba yake akatulia kwa sekunde kadhaa kisha akajibu.
" Carina binti yangu sina kazi ya maana ninayofanya ,ninafanya kazi kama zile kwaajili yenu wangu.....
" Lakini ile ni kazi ya kudhalilisha haifai ufanye ile kazi baba.
" Nikiacha mtaishi je ? Unajua hakuna mwenye kipato kikubwa kati yenu, Halfani bado yupo shule ananitegemea, wewe bado haujabahatika kupata kazi unanitegemea mimi unafikiri nilikaa hapa ndani maisha yataendaje?

Carina alionekana kuhuzunika sana .
" Mwanangu usihuzunike pia naomba usiwaambie wenzio kuwa umenikuta nafanya kazi kama ile, sitaki mtu yoyote ajue.

Machozi yalimtoka alijifuta kisha akasema.
" Usijali baba yangu ipo siku nitakuheshimisha.
Baba yake carina alitoa tabasamu na kusema
" Asante mwanangu. Kwa wakati huu mimi kunyanyuka na kusema niwe na kipato kikubwa ni ngumu sana ila naamini utaniheshimisha binti yangu.

Kesho yake carina aliamka mapema sana akiwa na bahasha ya vyeti vyake alizunguka kwenye kampuni nyingi za wanasheria kwaajili ya kuomba kazi lakini kwa siku hiyo ilikuwa ngumu sana kupata ila kwenye kampuni moja aliambiwa aache namba za simu na kuambiwa azatafutwa.
Carina alirudi nyumbani akiwa kachoka sana lakini bado hakukata tamaa kwani alipokuwa anakumbuka jinsi baba yake alivyokuwa akidhalilika alipata machungu hakupata nguvu ya kuendelea kutafuta kazi.

Baada ya wiki moja kupita carina alipigiwa simu na mtu ambae hakufahamu.
" Hallow , habari yako carina.
" Salama.
" Unaongea na mwanasheria mwafongo sijui unanikumbuka?
" Ndio nakukumbuka.
" Leo unaweza kufika ofisini kwangu?
" Bila shaka nitafika. Muda na saa utakayotaka.
" Basi njoo sasa kuna jambo muhimu sana tunatakiwa kuongea bila kuchelewa wala kupoteza muda.
" Sawa.
Baada ya kukata simu carina akijiandaa haraka na kuelekea ofisini kwa mwanasheria mwafongo.
" Afadhali umefika mapema, karibu ukae.
Carina valivutavkiti akakaa na kusikiliza wito.
" Carina nikiangalia cv zako ziko vizuri sana sasa nimeongea na rafiki yangu Patrick ni mwanasheria mkubwa sana pia ana kampuni kubwa anakuhitaji kwenye kampuni yake.
Hatuna alivyosikia hivyo alifurahi sana .
" Ina maana nimepata kazi?
" Ndio na kama upo tayari basi kesho unatakiwa kuondoka uelekee Arusha.
" Sawa nipo tayari , mimi nitaenda popote ilimradi nipate kazi tu.
" Basi ngoja tuwasiliane .

Mwalongo alipiga simu na muda uleule Patrick alipokea simu wakaongea na carina makubaliano ilikuwa kesho yake carina apande gari kuelekea Arusha .
Carina aliondoka ofisini kwa Mwafongo na kwenda kufanya maandalizi ya safari maana pale alipo hakuwa hata na nauli ya kumfikisha Arusha . Alienda kwa watu wake wa karibu na kukopa huku akiahidi kulipa baada ya kupokea mshahara wake wa kwanza.

Carina alifika Arusha na kuanza kazi mara moja na mshahara wake wa kwanza hakuweza kufanyia kitu alilipa madeni na kiasi kidogo alituma nyumbani kwao.

Baada ya mwezi mmoja kupita carina alikabidhiwa kusimamia kesi ya mteja . Kwa mara ya kwanza Carina alisimama mahakamani kumtetea mteja na mambo yanaenda vizuri wakashindwa kesi. Pongezi zilikuwa nyingi kutoka kwa boss na wafanyakazi wengine.
Kutoka na kujiamini kwake Carina alifanya kazi nzuri sana na kuzidi kuipa jina kampuni yao na kufanya watu wengi kwenda kutafuta wanasheria kwaajili ya kusimamia kesi zao.

Siku moja wafanya kazi wote wakiwa kwenye majukumu Patrick alitoka ofisini kwake akiwa kaongozana na wanaume wawili.
" Jamani naomba tusikilizane kuna kesi ipo hapa mezani. Ni kesi ya mauwaji mshitakiwa ni Jofrey mosses almaarufu Tigger.
Wafanyakazi wote waligeuka kuangaliana maana huyo mtu aliyetajwa ni mtuhumiwa sugu mafia hatari. Hakuna aliejibu kama anaweza kusimamia hiyo kesi.
" Advocate Patrick hili swala unatakiwa kusimamia wewe hapa sijaona wa kusimamia kesi ya Tigger. Alisema mwanaume mmoja .
" Nina kesi nyingi hii itakuwa nzito kwangu ila kuna vijana wangu hawaamini sana.
" Mbona wapo kimya hakuna anaejibu?
Mara wakasikia
" Mimi nitasimamia hiyo kesi. Ilikuwa ni sauti kutoka kwa carina.

PENZI LA KULAZIMISHA (MAFIA NA WAKILI)2
MTUNZI SMILE SHINE

Kila mtu aligeuka kumuangalia Carina kwa mshangao lakini advocate Patrick aliachia tabasamu sababu alitaka carina asimamie hiyo kesi kutokana na kujituma kwake na kujituma kwenye kazi yake.
" Advocate huyu binti ataweza kweli? Aliuliza Erick mtu wa karibu sana na Tigger.
" Msijali huyu binti mbali na elimu yake ya sheria pia ana kipaji kizuri sana kwenye kusimamia kesi acha tumpe nafasi asimamie hili.
Erick alimuangalia sana carina ambae alionyesha kujiamini mno kisha akamgeukia mwenzie ambae alionyesha kuwa na wasiwasi.
Patrick aliona wasiwasi wao alimshika bega Erick alafu akasema
" Erick niamini mimi hilo swala litaenda vizuri anaposema Carina ni sawa nimesimama mimi .
" Sawa lakini asije akatuangusha si unajua Tigger?
" Nimesema ondoeni hofu nitashirikiana na carina na kila kitu kinaenda sawa.
" Kama Tigger atafanikiwa kutoka basi atapata milioni mbili kama shukurani.
Patrick alitabasamu kisha akasema
" Andaeni hiyo hela.

Wale watu walilidhika wakaondoka.
Huko nyuma gumzo liliibuka ofisini.
" Carina hivi unamfahamu huyo kutuhumiwa mwenyewe?
" Simfahamu
" Mmmh
" Ndio maana umekubali kirahisi kama ungekuwa unamfahamu usingekubali.
" Kwanini. Kwani ana shida gani?
" Huyo mtu ukimuona yupo tofauti na matendo yake. Kwanza fikiria hilo jina lake Tigger.
" Mbona hamalizi kunielezea mnaishia katikati nipeni maelezo ya kutosha.
" Hapana tusikukatushe tamaa nenda kakutane na mteja wako mr tigger muyajenge .
Carina aliona kama wanamtisha akuwapuuzia akaendelea na mambo yake.

Kesho yake majira ya saa tano asubuhi carina alienda magereza kuonana na Tigger.
Carina alikutana na wahusika na kujitambulisha kama wakili mpya wa Tigger baada ya hapo alipelekwa kwenye chumba maalumu kwaajili ya kukutana na Tigger.

Baada ya dakika chache Tigger alifika na kukaa kwenye kiti huku akimuangalia carina kwa makini. Wakati huo carina nae alikuwa akimuangalia kwani hakuamini kama huyo Tigger anaeongelewa kwa matukio makubwa ndio yule aliyekaa mbele yake.

Tigger alikuwa ni kijana mwenye umri kati ya miaka 35 na usoni alionekana ni mtu mstaarabu sana na sura yake ilikuwa ya kuvutia , alikuwa mkimnya sio mtu wa maneno mengi.
Baada ya kuangaliana kwa muda Carina aliamua kumsalimia na kujitambulisha.
" Habari , naitwa carina Abdu ni mwanasheria wako mpya. Aliongea Carina huku akimpa mkono Tigger lakini Tigger hakuangaika kutoa mkono wake alimuangalia tu.
Carina alirudisha mkono wake na kuendelea kuongea.
" Naomba unipe ushirikiano.
" Unataka ushirikiano gani?
" Unaweza kuniambia siku ya tukio ilikuwaje mpaka kukamatwa kwako?
Tigger bado alimuangalia tu bila kujibu swali aliloulizwa.
" Ongea ukweli wote maana ukweli wako ndio utakuwa mwanzo mzuri wa mimi kujua wapi nianzie.

Safari hii Tigger alitoa kicheko kidogo huku akipapasa kichwa chake alafu akasema.
" Kweli hawa watu wamenichoka yani safari hii wameamua kunileta mchumba . Wewe unaweza kweli kusimamia kesi yangu?
Carina hakupenda kauli ya Tigger .
" Kumbuka mimi ni mwanasheria nipo hapa kwaajili ya kukusaidia kuhusu hiyo kesi yako.
" Mmmmh wameshindwa mawakili wakubwa wanaume wenye ndevu zao wewe mchumba utaweza nini au unataka niozee gerezani kwa kosa ambalo bila kijinga?
Carina alishikwa na hasira kutokana na zarau anazoonyeshwa na Tigger .
" Huyu mpuuzi ananichukulia poa hajui kuwa naweza kuisimamia kesi yake na akawa huru sasa ngoja nimuonyeshe kuwa mimi naweza .
" Unafikiria nini ? Tigger waliuliza baada ya kuona carina yupo mbali kimawazo.
" Nahitaji kusikia neno kutoka kwako.
" Sina cha kusema ni bora uende ukampikie bwana ako na sio kupoteza muda hapa.
Alisema Tigger kisha akasimama na kuondoka huku Carina akiwa anamsindikiza kwa macho.
" Hivi kitu lenye dharau hivi tutaweza na kweli? Acha niondoke kwanza ila nitarudi tena.

Carina alikusanya vitu vyake akaondoka na kurudi ofisini. Alienda moja kwa moja ofisini kwa advocate Patrick.
" Vipi Carina umefanikiwa kuongea nae?
" Nimeona nae lakini sijafanikiwa kuongea nae kitu cha maana.
" Kwanini?
" Yule mtu ni jeuri sana ana dharau sana anahisi siwezi kusimamia kesi yake kutokana na jinsia yangu pamoja na muonekano wangu. Nadhani hii kesi ungesimamia wewe.
" Mmmh Tigger hana ujanja hakuna wa kusimamia kesi yake wewe ndio utakuwa wakili wake.
" Lakini hanipi ushirikiano wowote.
" Usijali kuhusu hilo kila kitu kitakuwa sawa na utafanya kazi yako.

PENZI LA KULAZIMISHA
(MAFIA NA WAKILI)3
MTUNZI SMILE SHINE

Aliongea Patrick akiwa anaamini kuwa Tigger hatakuwa na msaada sehemu yoyote ila carina pekee ndio atafanya hiyo kazi.
" Kwahiyo kesho niende tena kuonana nae?
" Carina nenda kajuandae na hiyo kesi ya mauaji kesho tutajua cha kufanya
" Sawa.
Carina alikubali na kutoka ofisini kwa Patrick.

Wakati anaelekea nyumbani aliongozana na wakili Catheline ambae pia ni rafiki yake na mikutano yake .
" Vipi umefanikiwa kuonana na uteja wako?
" Ndio nimeona nae.
" Kila kitu kipo sawa?
" Sijafanikiwa kuongea nae chochote anaonekana ni mtata sana.
" Ni mtata sio kidogo, inasemekana ni mafia lakini watu wengine wanasema ni mtu safi sana anatetea wanyonge na kusaidia wasiojiweza.
" Kwahiyo ukisema hivyo tunamuweka kwenye fungu gani? Kwenye kundi la umafia au mtu safi?
" Hata sielewi maana sifa zote anazo yeye.
" Mmmh huu ni mtihani lazima nipatie majibu.
" Sio mtihani mdogo lakini nakuombea kipenzi uweze kushinda maana dau lililotangazwa sio la kitoto.
" Unawaza dau wakati mimi nawaza huyo kesi itaenda je na mtu mwenyewe ndio huyo haeleweki ananiita mchumba.
Catheline alimuangalia carina na kuanza kucheka.
"Kwahiyo unanicheka badala ya kunitia moyo.
" Sicheki kwa mabaya ila inafurahisha ila nakuamini hili litapita.

Kesho yake majira ya saa nne asubuhi Patrick na carina walienda kuonana na Jofrey, Patrick alianza kuonana nae kwaajili ya kuongea nae carina akabaki nje.
" Tigger unajua jinsi kesi yako ilivyo ngumu na watu wengi wanakimbia sasa kwani i usimpe nafasi wakili carina asimamie kesi yako.
" Advocate Patrick hivi kweli yule msichana anaweza kusimamia kesi yangu na mimi nikawa huru au mnataka mimi niozee jela kwa kosa ambalo sikufanya? Ni kweli mimi najuklikana kama mafia, mkorofi, mbabe lakini sijamuuwa Lameck.
" Sawa sasa mpe nafasi carina ni uhakika utakuwa huru.
" Advocate una uhakika na unachoongea?
" Uhakika hajawahi kuniangusha kazi nyingi anafanya vizuri carina yupo makini sana kwenye kazi yake.

Jofrey alifunga macho na kushusha pumzi ndefu kisha akasema.
" Sawa nimekubali ila kama atafanya Madudu nitajua cha kufanya hata nikiwa ndani nitawafikia tu.
Patrick alimuangalia alafu akasema.
" Naenda kumuita naomba umpe ushirikiano.
Jofrey aliitikia kwa kichwa akimaanisha sawa. Patrick alinyanyuka akatoka nje na kuelekea alipokuwa carina.
" Carina
" Abeee
" Nimeshaongea nae sasa unaweza kwenda kuendelea na kazi yako.
" Sawa .
Carina alinyanyuka na kuelekea kwenye chumba alichokuwepo Jofrey.
" Habari.
" Salama. Aliitikia Jofrey huku akiwa serious na kumuangalia kwa jicho kali ili kumtisha lakini carina hakuogopa aliendelea na kazi yake.
" Mr tigger unaweza kuniambia siku ya tukio ilikuwaje?
" Mimi na Lameck tulikuwa na tofauti zetu siku ya tukio nilienda nyumbani kwake kwaajili ya kumfanya kidogo ili awe na adabu . Tukiwa sebleni kwake tunabishana mimi nilishika bastola kumtishia nae alishika ya kwake nakutaka kufyatua risasi , nilipoona kuwa anataka kuniuwa nilichukua chupa iliyokuwa karibu yangu na kumrushia ile chupa ilimpiga kwenye paji la uso aliachia ile bastola lakini ajabu niliona risasi ikitua kifuani kwake na damu nyingi zilivuja . Nilipofika nyuma kuangalia ile risasi imetokea wapi ila ilipigwa kutokea dirishani ilinibidi nijifiche sababu sikujua kama muuwaji kama yupo au ameondoka .
Baada ya muda nilinyata nikaenda dirisha la pili nikamuona mtu anaondoka huyo mtu sikuweza kumtambua sababu akinipa mgongo pia alikuwa kavalia mavazi Meusi, koti refu na kofia.

Wakati huo carina alikuwa anaandika maelezo alipomaliza kuandika alimuangalia na kuuliza.
"Baada ya hapo ilikuwaje?
" Ilinibidi niondoke wakati nipo getini nikakutana na polisi wakanibeba.
" Lameck alikuwa na maadui wengine mbali na wewe?
" Kumbuka mimi sikuwa adui yake.
" Ok samahani, unawafahamu watu wengine ambao walikuwa na uadui na Lameck?
" Wapo wengi sana na wengine wapo ndani kama mimi.
" Sawa, asante kwa ushirikiano wako nitakuja wakati mwingine endapo kutahitaji kujua kitu kutoka kwako.

Siku zilienda carina alimtembelea Tigger na kuongea nae mawili matatu kuhusu kesi yao.
Ilifika muda wa kesi kwenda kusikilizwa mahakamani carina aliisimamia vizuri sana kesi ya Jofrey( Tigger ) hatimae walishinda na Jofrey alikutwa hana hatia na kuachiwa huru.
Ndugu na jamaa wa Jofrey walifurahi sana tigger kuwa huru pia carina alipongezwa sana na wenzake kwa kazi nzuri aliyofanya hasa Patrick alifurahi zaidi kwani kampuni yake ilizidi kupanda chati na kusifika kuwa na wanasheria wazuri.
" Hongera sana carina umefanya kazi nzuri mno.
" Asante advocate.

Baada ya kupongezana watu wote walitoka nje ya mahakama . Tigger alikuwa anaenda kupanda gari lakini alikumbuka kuwa hajaongea na wakili wake.
Kwa mbali alimuona carina akiwa kaongozana na Patrick aliwafuata.
"Mr Patrick
" Ndio tigger.
" Kilichotokea leo ni kama miujiza.
" Nilikwambia carina ni tegemeo langu kubwa sana na sheria imelala kwenye hicho kichwa.
" Nimeamini , unaweza kunipa muda niongee na wakili wangu msomi?
" Sawa, carina na kusubiri kwenye gari.
" Sawa.
Patrick aliondoka akawa acha wakiwa wamesimama. Tigger alimuangalia kama vile haamini kama carina ndio kafanya yote yale mpaka sasa yupo huru.
" Nilishitushwa sana na muonekano wako lakini kumbe wewe ni balaa.
Carina alitabasamu.
" Sasa mchumba unaweza kufika kwenye sherehe ambayo nitaandaa kwaajili ya kufurahia ushindi wetu?
" Niite carina tafadhali.
" Mimi najisikia vizuri nilikuta mchumba.
" Nimeshasema sitaki.
" Sawa carina. Vipi utakuja?
" Kama nitapata muda nitafika na nisipopata basi nitakutakua sherehe njema.
" Basi na mimi nitaifanya mpaka siku itakayofuata nafasi.
" Sawa acha niwahi kwenye majukumu mengine.
Carina aliondoka tigger akiwa anamuangalia huku akiwa anapapaswa kichwa chake kwa mkono wake wa kulia.

PENZI LA KULAZIMISHA
MAFIA NA MWANASHERIA 4
MTUNZI SMILE SHINE

Tigger akiondoka huku akiwa mwenye uso wa tabasamu akaenda kupanda kwenye gari safari ya kwenda kwenye makazi yake ikaanza. Wakiwa kwenye gari akaanza kuongelea carina na jinsi alivyokuwa akimchukulia.
" Sikutegemea kama yule msichana mdogo angeweza kusimamia kesi yangu na ikaisha kirahisi hivi na sasa tigger nipo huru.
" Hata sisi hatukutegemei ila Patrick alituaminisha kuwa itawezekana wewe kutoka kama akisimamia carina. Alisema Erick
" Inatakiwa mumpatie kiasi cha pesa nilichoahidi kama zawadi , kesho mapema sana apelekewe alafu weekend hii nataka nifanye sherehe kwaajili ya kufurahia ushindi ningependa carina apewe mualiko.
" Mbona mapema sana kufanya hivyo ?
" Unamuogopa nani Erick, kipi kinakutisha kwenye huu mgongo wa aridhi, unawaohopa wale paka mwitu?
" Basi Sawa tutafanya hivyo
" Swala la mualiko lifanyike kesho.
" Sawa mapema sana .

Carina alifika ofisini wenzake walimpongeza na kumshangilia sana kuliko siku zote alizokuwa akishinda kesi.
" Mbona hii ni ajabu jamani leo imekuwa kama sherehe.
" Hata hivyo tutafanya sherehe ya kujipongeza sababu tangia umeingia kwenye hii kampuni umekuwa ukifanya vizuri na umezidi kututangaza.
Alisema Patrick na carina alibaki kutabasamu.
Baada ya muda wafanyakazi wa mgahawa wa Freedom walifika na vyakula na kuanza kuwasambazia wafanyakazi wote hiyo ilikuwa ofa ya Patrick.
" Hajawahi kuniangusha mawakili wangu basi leo tujipongeze kidogo kwa ushujaa wetu na utendaji kazi wetu.

Jioni carina akiwa ndani kwake ametulia huku alipitia mambo yake kwenye laptop yake mlango uligongwa.
" Atakuwa nani muda huu? Alijiuliza kisha akatulia kidogo kusikiliza kama mlango unagongwa tena, baada ya muda mlango uligongwa tena carina alinyanyuka na kwenda kufungua.
" Catheline kumbe ni wewe sijui nilifikiri ni mtu gani mpaka nikajiuliza huyu ni nani muda huu.
" Pole .
" Karibu ndani.
" Asante.
Catheline aliingia ndani .
" Chai, kahawa , juice? Carina aliuliza.
" Kahawa kama inayotumia wewe.
Kwakuwa carina alikuwa anakunywa kahawa alienda kuchukua kikombe akamuona kahawa na kumpatia Catheline.
" Asante. Catheline alipokea na kunywa kidogo kisha akaweka kikombe mezani.
" Shoga yangu hongera.
" Sasa mtanipasua kichwa kwa hizo hongera.
" Wewe zipokee tu maana haikuwa kazi rahisi kumtetea yule mafia mpaka kushinda kesi maana safari hii hakuna aliyeweza kuamini kama angeweza kutoka alikuwa ananichukulia jela.
" Sasa kama mtu hajafanya kosa na vithibitishe vipo sasa kwanini asipate haki yake?
" Kumbe huna unalijua wewe ,hivi unajua Tigger alimuuwa Lameck kwasababu ya kugombania mwanamke .?
Carina alishituka
" Unasemaje cath?
" Ndio hivyo na kila mtu anajua hilo na inavyosemekana mdogo wake Lameck anaeitwa Bosco amepanga kulipiza kisasi hakubali haki ya ndugu yake ipoteze maana tigger alitakiwa kuwa ndani.
" Hayo ni mapya sina ninachojua kikubwa nimefanya kazi yangu nimefanikiwa basi.
" Ndio maana nakupa hongera shoga umekua kunipambania Tigger na umejua kumziba mdomo maana alikudharau sasa heshima imesimama wanawake tunaweza.

Upande wa Tigger alikuwa sehemu na watu wake wakifurahia na kunywa huku nyama choma zilikuwa kwa fujo.
" Mimi ndio tigger kuleni, kunyweni mpaka muoge ikiwezekana niende kwenu mkiwa mnatambaa.
Erickson rafiki na mtu wake wa karibu kwenye hizo kazi zao alimsogelea karibu na kumwambia kwa sauti ya chini.
" Kumbuka wewe unafurahia na kuna wengine wanamachungu ya wewe kushinda kesi hivyo basi kuwa makini inawezekana unawindwa na leo ikageuka kuwa siku mbaya sana kwako.
Tigger alimuangalia Erick alafu akacheka .
" Erick unakuwa kama hunifahamu bwana Bosco ni mtoto mdogo sana kwangu hawezi kulipiza kisasi cha kumuuwa kaka yake.
" Sawa ila nilikuwa nakupa tahadhari tu.
" Tuachane na hayo kesho nenda ofisini kwa advocate Patrick nenda kaonane na yule mchumba aliyesimamia kesi yangu mpatie hizo milioni 5 kama shukran zangu pia hawa kadi za mualiko kwa kila mfanyakazi wa pale nataka tufurahi nao pamoja.
" Sawa nitafanya hivyo.
Baada ya kukubaliana Tigger alienda kujichanganya na wetu wake wakawa wanacheza mziki.

Kesho yake majira ya saa sita carina alikuwa anatoka mahakamani alipofika ofisini alipata taarifa kuwa anatakiwa ofisini kwa Patrick. Alienda ofisini kwake akaweka vitu vyake vizuri kisha akaenda Ofisini kwa Patrick.
"Habari za muda huu.
Alisalimia carina.
" Salama .
" Carina hapa kuna ugeni wako. Carina aliwaangalia wale watu sura hazikuwa ngeni aliwatambua kuwa ni watu wa Tigger.
Patrick akaendelea kusema
" Wamekuja na mzigo wako kutoka kwa Tigger.
Erick alimkabidhi bahasha carina alipokea na kushukuru.
" Asante.
Baada ya kukabidhiwa bahasha yake alitoka kwenda kuendelea na kazi zake.
Alijikuta anatamani kufungua ili angalieni kilichomo ndani .
" Hizi pesa sitakiwi kukaa nazo mimi inabidi mitume nyumbani kwaajili ya mtaji wa kufungua biashara sasa mateso kwa familia yangu yanaenda kuisha baba yangu hawezi kutumikishwa tena na Halfan atasoma bila shida yoyote. Lazima nipambane kuniheshimisha familia yangu.
Akiwa kwenye mawazo mara Catheline alifika mezani kwake.
" Unawaza nini mpaka unataka kulia?
" Hakuna . Alijibu carina huku akijifanya kupanga karatasi kwenye faili.
" Naona bahasha imeona ni kibanda kutoka kwa Tigger?
" Ndio.
" Ni kiasi gani?
Maswali ya Catheline yalikuwa yanachosha carina alimuangalia usoni alafu akasema.
" Unajua nimetoka mahakamani nimeongea sana huko na sasa unaniuliza maswali ambayo jibu lake sijui kwa maana bado sijajifungua hiyo bahasha.
Baada ya muda kidogo Patrick alitoka ofisini kwake akiwa kaongozana na wakina Erick, aliwasindikiza mpaka nje baada ya sekunde kadhaa alirudi ofisini na kuanza kugawa kadi za mualiko.
" Hiki ni nini ?
Wafanyakazi waliuliza lakini Patrick hakujibu aliendelea kugawa kila mmoja ajisimee mwenyewe.
" Kadi ya mualiko wa sherehe ya tigger zimealikwa wafanyakazi wote wa hapa.
Aliongea Catheline kwa sauti ya chini akimwambia carina.
Carina alisoma kadi yake alipomaliza akiweka vizuri.
" Sasa kitandani na sherehe itakuwa kesho kutwa Ijumaa muda kuanzia saa moja jioni.
Alisema Patrick kisha akaingia ofisini kwake.
" Kwani kulikuwa na haja gani kutualika wote kwenye sherehe yake mimi sioni haja ya kwenda huko.
" Carina unajua ndio uliefanikisha awe huru so unatakiwa kuwepo.
" Kwahiyo kama nina mambo yangu niache au?
" Acha kuweka vizuizi kwa siku moja tu sio mbaya.
Catheline alimshawishi carina wahudhurie mpaka carina akakubali.

Siku ya Ijumaa ilifika wafanyakazi walitoka kazini mapema kwaajili ya kufanya maandalizi ya party.
Watu walikuwa na hekaheka wakitangulia jinsi ya kuvaa wapendeze lakini carina hakuwa na habari alichukuliwa ni jambo dogo party ya kujipongeza tu.
Carina akiwa ndani kwake anajiandaa mara Catheline alienda kumpitia.
" Carina unafanya nini mpaka sasa haujavaa?
" Nilikuwa na chagua nguo ya kuvaa.
" Lakini ulikuwa na muda wa kutosha.
" Lakini nilikuwa nina mambo mengi ya kufanya.
" Basi fanya haraka muda umeenda na tunakwenda ni mbali kidogo.

Carina aliendelea kujiandaa huku Catheline akiwa anaangalia saa maana muda ulikuwa unaenda ilikuwa ni saa mbili kasoro.
Carina alimaliza kuvaa wakawa wanajiandaa kutoka mara wakasikia honi ya gari.
" Hiyo gari ni wapi tena? Aliuliza Catheline huku akiwa anachungulia nje.
" Huyo gari mbona kama imesimama nje au ukiongea na dereva taxi aje kutuchukua?
" Hapana.
" Sasa atakuwa nani?
" Catheline acha maswali toka nifunge mlango wangu.
Walitoka wakafunga mlango mara waliona mtu anawafuata pale mlangoni.
" Habari warembo.
"Salama.
" Naitwa Jay nipo hapa kwaajili ya kuwachukua na kuwapeleka kwenye party.
Carina na Catheline waliangaliana kwa mshangao.
" Kwani ulimuita? Caroline alimuuliza carina
" Hapana nilijua wewe ndio ulimwambia aje.
" Hapana.
Catheline alimuangalia huyo Jay kisha akamwambia
" Lakini sisi hatujakuita uje utuchukue.
" Maigizo kutoka kwa Tigger.
Carina na Catheline waliangaliana tena kwa mshangao.
" Warembo tusipotezeuda twendeni.
Catheline na carina waliongozana na Jay mpaka kwenye gari wakakaa nyuma .
Jay aliwasha gari safari ya kwenda kwenye ukumbi wa party ikaanza.
Carina alimnongoneza Catheline.
" Hivi itakuwa ni kweli katumwa na tigger au zinachezewa michezo?
"Itakuwa ni kweli katumwa.
" Tigger amepajuaje nyumbani kwangu?
" Nilikwambia yeye sio mtu mdogo akitaka kufuatilia nyendo zako atakuja kuliko unavyojua mwenyewe.
" Mmmmh. Carina aliguna kisha akatulia.

Baada ya mwendo wa dakika 20 walifika kwenye sherehe
[4/28, 1:35 PM] Fatma Mohamed: Walikuta wenzao wameshafika na party ilikuwa sio ya kitoto walihudhuria watu wengi wenye pesa zao. Walikaribishwa na kwenda kukaa kwenye meza iliyokuwa imeandaliwa vinywaji vya kila aina hapo ni wewe kujihudumia .
Carina alikuwa anashangaa.
" Kumbe mambo ni tofauti na nilivyokuwa nafikiria.
" Kwani ulikuwa unafikiriaje?
" Nilijua ni jambo dogo lakini ni sherehe kubwa.
" Huyu ni Tigger mtu mwenye pesa zake hakuna jambo kubwa kwake.
" Inaonekana unamfahamu vizuri?
" Hahahaha sio kihivyo ila mara nyingi huwa nakutana nae kwenye maeneo flani si unajua ujana.
" Unamaana gani kusema hivyo?
" Utakuwa umefikia mengine sio hivyo kabisa huwa nakutana nae club na sehemu nyingi za starehe pia aliwahi kutoka na shost yangu mmoja .

Wakiwa wanaendelea kuzungumzia Tigger mara alifika kwenye meza yao alivuta kiti na kukaa.
" Habari zenu mawakili warembo
" Salama
" Karibuni sana kwenye party ya kusherehekea uhuru wa Tigger.
" Asante na hongera. Alijibu Catheline.
" Wakili wangu msomi miss Carina nimefurahi kukuona .
" Pia mimi nimefurahi kukuona ukiwa na furaha na ukiwa tofauti na kipindi kile nimekutana na wewe.
" Kipindi kile sikuwa huru sasa huyu unaemuona hapa ndio Tigger mwenyewe .
Aliongea Tigger huku akiwa anatabasamu.
" Basi furahia uhuru wako kwa amani.
" Bila shaka leo tutafurahia pamoja wakili wangu.
" Hapana nitakuwa hapa ukiwa unafurahia.
" Kwanini hapa wakati mahakamani tulikuwa pamoja?
" Ilikuwa ni sehemu ya kazi yangu
" Basi sasa fanya kwaajili ya mteja wako.
Carina alinyamaza wanaangaliana na Catheline ambae hakutoa neno kwenye maongezi yao zaidi ya kuwaangalia.
" Au unasemaje mchumba ?
Tigger aliuliza na kumfanya Carina akunje uso wake kama kwamba hakufurahishwa na hili neno mchumba.
" Sorry miss carina haikuwa nia yangu kukukera nimejikuta naongea tu. Karibuni na ufurahie.
Alisema Tigger kisha akanyanyuka na kuondoka, Carina na Catheline walimsindikiza kwa macho.
" Huyu mtu sio muelewa kabisa.
" Itakuwa akielewa ndio maana inamuona sio muelewa.
" Unaongea nini na wewe?
" Tigger hakupenda , fuata nyuki ule asali.
" Kama utamu wa asali ni kuwa na Tigger basi acha nikwambie tu sukari.
" Wenzako wanalilia hiyo nafasi.
" Ni wao pamoja na wewe ila kwangu hapana.

Sherehe ikiendelea watu walikula, wakanywa na kufurahia lakini mara kwa mara tigger alikuwa akimfuata Carina na hata alipokuwa mbali nae jicho lake lilikuwa kwa Carina.
Kuna muda Tigger alikuwa anaongea na wageni wake hivyo hakumakini sana kumuangalia Carina, baada ya kupata nafasi alitupia macho kwenye meza waliyokuwa wamekaa hakuona mtu alianza kukatisha katikati ya watu akimtafuta hatimae alimpata akiwa anacheza mziki na kijana mmoja.
Tigger hakupendezwa na alichokiona alisogea mpaka pale walipokuwa wanacheza akamshika bega yule kijana akamuangalia juu mpaka chini kisha akamshika mkono na kumvutia pembeni.
" Wewe ni nani na una wadhifa gani au unapesa kiasi gani mpaka ucheze na yule mrembo?
" Kwani kuna tatizo kaka?
" Kumbe sio tatizo mtu kucheza na mwanamke ninaempenda?
" Sikujua kama ni mwanamke wako.
" Leo ni siku ya sherehe yangu sitaki kumpiga mtu wala kufanya chochote cha kunipa sifa mbaya hasa akiwepo mrembo wangu nakupa onyo la kwanza na la mwisho kaa mbali na yule mwanamke.

PENZI LA KULAZIMISHA
( MAFIA NA WAKILI) 5
MTUNZI SMILE SHINE

Baada ya muda kidogo Patrick alitoka ofisini kwake akiwa kaongozana na wakina Erick, aliwasindikiza mpaka nje baada ya sekunde kadhaa alirudi ofisini na kuanza kugawa kadi za mualiko.
" Hiki ni nini ?
Wafanyakazi waliuliza lakini Patrick hakujibu aliendelea kugawa kila mmoja ajisimee mwenyewe.
" Kadi ya mualiko wa sherehe ya tigger zimealikwa wafanyakazi wote wa hapa.
Aliongea Catheline kwa sauti ya chini akimwambia carina.
Carina alisoma kadi yake alipomaliza akiweka vizuri.
" Sasa kitandani na sherehe itakuwa kesho kutwa Ijumaa muda kuanzia saa moja jioni.
Alisema Patrick kisha akaingia ofisini kwake.
" Kwani kulikuwa na haja gani kutualika wote kwenye sherehe yake mimi sioni haja ya kwenda huko.
" Carina unajua ndio uliefanikisha awe huru so unatakiwa kuwepo.
" Kwahiyo kama nina mambo yangu niache au?
" Acha kuweka vizuizi kwa siku moja tu sio mbaya.
Catheline alimshawishi carina wahudhurie mpaka carina akakubali.

Siku ya Ijumaa ilifika wafanyakazi walitoka kazini mapema kwaajili ya kufanya maandalizi ya party.
Watu walikuwa na hekaheka wakitangulia jinsi ya kuvaa wapendeze lakini carina hakuwa na habari alichukuliwa ni jambo dogo party ya kujipongeza tu.
Carina akiwa ndani kwake anajiandaa mara Catheline alienda kumpitia.
" Carina unafanya nini mpaka sasa haujavaa?
" Nilikuwa na chagua nguo ya kuvaa.
" Lakini ulikuwa na muda wa kutosha.
" Lakini nilikuwa nina mambo mengi ya kufanya.
" Basi fanya haraka muda umeenda na tunakwenda ni mbali kidogo.

Carina aliendelea kujiandaa huku Catheline akiwa anaangalia saa maana muda ulikuwa unaenda ilikuwa ni saa mbili kasoro.
Carina alimaliza kuvaa wakawa wanajiandaa kutoka mara wakasikia honi ya gari.
" Hiyo gari ni wapi tena? Aliuliza Catheline huku akiwa anachungulia nje.
" Huyo gari mbona kama imesimama nje au ukiongea na dereva taxi aje kutuchukua?
" Hapana.
" Sasa atakuwa nani?
" Catheline acha maswali toka nifunge mlango wangu.
Walitoka wakafunga mlango mara waliona mtu anawafuata pale mlangoni.
" Habari warembo.
"Salama.
" Naitwa Jay nipo hapa kwaajili ya kuwachukua na kuwapeleka kwenye party.
Carina na Catheline waliangaliana kwa mshangao.
" Kwani ulimuita? Caroline alimuuliza carina
" Hapana nilijua wewe ndio ulimwambia aje.
" Hapana.
Catheline alimuangalia huyo Jay kisha akamwambia
" Lakini sisi hatujakuita uje utuchukue.
" Maigizo kutoka kwa Tigger.
Carina na Catheline waliangaliana tena kwa mshangao.
" Warembo tusipotezeuda twendeni.

Catheline na carina waliongozana na Jay mpaka kwenye gari wakakaa nyuma .
Jay aliwasha gari safari ya kwenda kwenye ukumbi wa party ikaanza.
Carina alimnongoneza Catheline.
" Hivi itakuwa ni kweli katumwa na tigger au zinachezewa michezo?
"Itakuwa ni kweli katumwa.
" Tigger amepajuaje nyumbani kwangu?
" Nilikwambia yeye sio mtu mdogo akitaka kufuatilia nyendo zako atakuja kuliko unavyojua mwenyewe.
" Mmmmh. Carina aliguna kisha akatulia.

Baada ya mwendo wa dakika 20 walifika kwenye sherehe
Walikuta wenzao wameshafika na party ilikuwa sio ya kitoto walihudhuria watu wengi wenye pesa zao. Walikaribishwa na kwenda kukaa kwenye meza iliyokuwa imeandaliwa vinywaji vya kila aina hapo ni wewe kujihudumia .
Carina alikuwa anashangaa.
" Kumbe mambo ni tofauti na nilivyokuwa nafikiria.
" Kwani ulikuwa unafikiriaje?
" Nilijua ni jambo dogo lakini ni sherehe kubwa.
" Huyu ni Tigger mtu mwenye pesa zake hakuna jambo kubwa kwake.
" Inaonekana unamfahamu vizuri?
" Hahahaha sio kihivyo ila mara nyingi huwa nakutana nae kwenye maeneo flani si unajua ujana.
" Unamaana gani kusema hivyo?
" Utakuwa umefikia mengine sio hivyo kabisa huwa nakutana nae club na sehemu nyingi za starehe pia aliwahi kutoka na shost yangu mmoja .

Wakiwa wanaendelea kuzungumzia Tigger mara alifika kwenye meza yao alivuta kiti na kukaa.
" Habari zenu mawakili warembo
" Salama
" Karibuni sana kwenye party ya kusherehekea uhuru wa Tigger.
" Asante na hongera. Alijibu Catheline.
" Wakili wangu msomi miss Carina nimefurahi kukuona .
" Pia mimi nimefurahi kukuona ukiwa na furaha na ukiwa tofauti na kipindi kile nimekutana na wewe.
" Kipindi kile sikuwa huru sasa huyu unaemuona hapa ndio Tigger mwenyewe .
Aliongea Tigger huku akiwa anatabasamu.
" Basi furahia uhuru wako kwa amani.
" Bila shaka leo tutafurahia pamoja wakili wangu.
" Hapana nitakuwa hapa ukiwa unafurahia.
" Kwanini hapa wakati mahakamani tulikuwa pamoja?
" Ilikuwa ni sehemu ya kazi yangu
" Basi sasa fanya kwaajili ya mteja wako.
Carina alinyamaza wanaangaliana na Catheline ambae hakutoa neno kwenye maongezi yao zaidi ya kuwaangalia.
" Au unasemaje mchumba ?
Tigger aliuliza na kumfanya Carina akunje uso wake kama kwamba hakufurahishwa na hili neno mchumba.
" Sorry miss carina haikuwa nia yangu kukukera nimejikuta naongea tu. Karibuni na ufurahie.
Alisema Tigger kisha akanyanyuka na kuondoka, Carina na Catheline walimsindikiza kwa macho.
" Huyu mtu sio muelewa kabisa.
" Itakuwa akielewa ndio maana inamuona sio muelewa.
" Unaongea nini na wewe?
" Tigger hakupenda , fuata nyuki ule asali.
" Kama utamu wa asali ni kuwa na Tigger basi acha nikwambie tu sukari.
" Wenzako wanalilia hiyo nafasi.
" Ni wao pamoja na wewe ila kwangu hapana.

Sherehe ikiendelea watu walikula, wakanywa na kufurahia lakini mara kwa mara tigger alikuwa akimfuata Carina na hata alipokuwa mbali nae jicho lake lilikuwa kwa Carina.
Kuna muda Tigger alikuwa anaongea na wageni wake hivyo hakumakini sana kumuangalia Carina, baada ya kupata nafasi alitupia macho kwenye meza waliyokuwa wamekaa hakuona mtu alianza kukatisha katikati ya watu akimtafuta hatimae alimpata akiwa anacheza mziki na kijana mmoja.
Tigger hakupendezwa na alichokiona alisogea mpaka pale walipokuwa wanacheza akamshika bega yule kijana akamuangalia juu mpaka chini kisha akamshika mkono na kumvutia pembeni.
" Wewe ni nani na una wadhifa gani au unapesa kiasi gani mpaka ucheze na yule mrembo?
" Kwani kuna tatizo kaka?
" Kumbe sio tatizo mtu kucheza na mwanamke ninaempenda?
" Sikujua kama ni mwanamke wako.
" Leo ni siku ya sherehe yangu sitaki kumpiga mtu wala kufanya chochote cha kunipa sifa mbaya hasa akiwepo mrembo wangu nakupa onyo la kwanza na la mwisho kaa mbali na yule mwanamke.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote