Follow Channel

PENZI LA MKATABA

book cover og

Utangulizi

Penzi la mkataba ni story inayo muhusu binti Naomi ambae alijikuta akiingia kwenye Penzi la mkataba na hii ni baada ya kuumizwa vibaya na mapenzi Je uamzi aliochukua Naomi ni sahihi ? Na nini kinaendelea basi ungana nami katika story hii tamu na yenye kusisimua 😌

SONGA NAYO.................

PENZI LA MKATABA
SEHEMU YA 01
MTUNZI :RITHA STORIES

https://www.tupoahapa.com

Kabla sijaendelea na story yangu naombeni Dj anipigie ule wimbo wa mapenzi kulanina ,bila kukatisha wala kuweka chikichiki ikiisha hiyo malizia na mahaba ya king Kiba walau nijifariji maana yalonikuta nimakubwa mno😫.

Kwa maumivu niliyonayo nashindwa hata pakuanzia ,maana moyo wangu una Uma mnoo 😫mapenzi mapenzi kwanini lakini 😣.

Nilikupenda ila unaniumiza namna hii kama si wewe uliekuwa unanifanya nijione mkosefu kwato kukujua mapenzi why😫, jamani naumia mwenzenu mapenzi yamenifanya kitu hakuna 😫.

Acha niwape story kilichonikita mtoto wa mwenzenu , mimi bwana nilikuwa na mpenzi wangu wa toka kitambo .

Huyu mkaka tulikutana miaka mitatu iliyopita , tena nakambuka siku niliyokutana nae ilikuwa ni kwenye kituo cha mwendo kasi kimara .

Tulibadilishana namba na kuanza kuongea baada ya wiki kadhaa tukaingia penzini, mwanzo wa mapenzi yetu mwanaume alikuwa ananipenda na kunijali mno.

Yaani kuna mda nilikuwa nikikaa hivi namshukuru Mungu kwaajili ya huyu kijana, maana kwa namna alivyokuwa akinionesha upendo ilikuwa ni zaidi ya mapenzi😔.

Hata ahadi zake alizokuwa akinipa alihakikisha anazitimiza kwa wakati ,na kunipatia mda wa kutosha.

Lakini mambo yalikuja kubadilika baada ya kusafiri kikazi ambapo alikaa kama miezi mitatu na wiki kadhaa, nakumbuka wiki ya pili tu baada ya kwenda alianza kutopokea sm zangu kwa wakati .

Na nikilalamika jibu ni (nilikuwa bize na kazi) nilivumilia nikiamini kweli yuko bz na kazi , na kuwa nikisubiri walau akitoka kazin au zile siku za weekend ndo tuongee .

Lakin hata huo mda wa dakika kadhaa niliukosa, maombi yangu yakabaki kusubiri arudi maana huko kumeshakuwa basi tena , na hata kulalamika kila mda nilikuacha kwasababu kila nilipotoa lalamiko nilionekana sijali anachofanya.😔

Mda wa kukaa kule uliisha akarudi walau kidogo penzi likarudi, nami ilikunogesha penzi nikahakikisha nakuwa karibu nae sana ili niweze kurudisha bond iliyokuwa inapotea.

Katika kukaa karibu nae nikajipa majukumu ya kufanya kila kitu kinachohusu nyumbani kwake, yaani kupika ,kufua , kufanya usafi ,pamoja na kufanya manunuzi yote .

Unaweza kuuliza kwamba nilipata wapi mda wa kufanya hayo yote huku nikiwa nyumbani, tena nikiwa naenda kazin kila siku za wiki.

Ilikuwa hivi ,nilipanga ratiba yangu kuwa kabla sijafika ofisini kwangu ilikuwa lazima nipite nyumbani kwake niandae chai ,nikimaliza hapo namfungia maana alikuwa anadai anaenda kunywa kazin.

Jioni pia nilikuwa kabla ya kurudi nyumban napita tena kwake napika na kuacha nimeosha vyombo vizuri kisha huyoo narudi nyumbani, akirudi kutoka kazn anaweza kunipigia au asipige hadi nitakapo mtafuta na sikiona shida .

Weekend ilikuwa siku ya usafi wa nyumba na nguo yaani nafua nakunja,au kupasi nikimaliza napika chakula cha jioni kabla ya kuondoka lazima atahitaji umuache kihisia yuko sawa ndo uondoke.

La sivyo mda unaofika ndo unamridhisha kwanza ndo unaanza kufanya Kazi, hayo ndo majukumu niliyojipatia kwa mda wa miaka mwili na nusu .

Na niseme ukweli sikuwahi kuona kama nakosea au nini yaani mda wote niliona kuwa niko sawa ,na niliona nijambo la kawaida sana japo rafiki yangu alikuwa akinisema sana ila sikuwahi kumsikiliza kwanza nilimuona kama mkata kamba kwenye mahusiano yangu.

Maana hakuwahi kusimama na mimi kwenye jambo la mahusiano yangu na Ibra, lakin kilichokuja kunipata baada ya yote hayo kilinifanya nikamuelewa kwann alikuwa hayuko upande wangu .

Nakumbuka siku moja nikiamka nikajiandaa zangu vizuri na kumuaga bibi yangu maana ndo ninaishi nae , kisha nikaenda kwa mpenzi wangu.

Nilifika nikakuta hayupo sikujiuliza sana kwasababu huwa ni mtu wa mazoezi so nikajua kaenda Gym kipiga zoezi so mtoto wakike nikaingia kazin.

Nikaosha vyombo na kuandaa chai pamoja na vitafunwa kisha , nikaingia chumbani nikiwa na lengo la kubadilisha mashuka maana kila ijuma moss ilikuwa lazima nibadilishe mashuka .

Sasa nikashangaa yamebadilishwa na yale yaliyotolewa yakiwa kwenye tenga , nilisimama na kubaki nikijiuliza Ibra leo amekuwaje hadi amebadilisha shuka.

Maana namjua katika vitu ambavyo hapendi ni kubadilisha mashuka, na hata akibadilisha huwezi kukuta ameweka kwenye tenga utayakuta chini .

Sasa leo baada ya miaka miwili kabadilisha mwenyewe bila hata kuambiwa na kaweka sehemu inayotakiwa, hii ajabu ,basi nikachukua tenga na kutoka nalo nje .

Nikaweka maji kwenye beseni na kuanza kuchambua zinazofaa kulowekwa ili niloweke , katika chugua chagua bwana sangap nikite chupi ya kike tena ikiwa juu kabisa na imevaliwa .

Moyo ulinilipuka nikabaki nimeishikilia , niliiangalia kwa mda na kuiweka pembeni nikaendelea kupekua mara nakutana na bra nayo imevaliwa.

Mikono ilinitetemeka kama mtu aliezeeka sana , taratibu nikashika mashuka na kuyanusa , machozi yaliishuka kama matone ya mvua .

Shuka zilikuwa zinanuka shombo zao 😫 nguvu ziliniisha nikakaa chini , mapigo ya moyo yalikuwa kasi kuliko kawaida nilikuwa kama naona kile walichokuwa wakifanya .

Nikiwa nimekaa chini huku machozi yakinitoka nilisikia gate likifunguliwa, niliinuka haraka na kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma .

Macho yangu yalitua kwenye gari lililokuwa likiingia , mara kwenye gari hilo akashuka Ibra na mdada wakiwa wamevaa nguo za mazoezi.

Walishikana mikono na kuingia ndani, Ibra alishtuka baada ya kuniona , yule mdada akauliza .

"Babe una msichana wa kazi ?"

Ibra akijichekesha na kujibu" yes honey ni msichana wangu ila huwa anakuja na kuondoka"

"Oooh ,nilikuwa nimeshtuka , wewe sijui unaitwa nani niandalie chai haraka maana nahisi njaa sana " aliongea na kunipita akaingia chumbani.

Nilibaki nimesimama huku nikimuangalia Ibra kwa hasira sana , alijishika kiuno na kukuna kichwa kisha akataka kukaa ila akaacha na kunifuata nilipo simama, na kusema.

"Tricia naomba nenda nyumbani tutaongea baadae "

"Hahahaha una vituko sana niondoke tutaongea baadae , hivi naonekana kama mjinga kwako si ndio?" Niliongea kwa ukali uliochanganyikana na hasira .

Ibra alinishika na kunitoa nje haraka ,na kunambia .

"Hey nimekwambia uje tongee badae na sio uazishe vurugu lako hapa"

"Ibra umenisaliti mbele ya macho yangu halafu unaniambia niende halafu nirudi hivi unawazimu wewe , maana haikingii akilini nikufumanie halafu ulivyo huna haya unaniambia ujinga .

Kwanu nimekosa nini hadi kustahili haya , nimekupenda na kukuheshimu miaka yote .

Nimekiwa kwako kama kama mke ,ila leo hii unanitambulisha kwa Malaya wako kama kijakazi wako kweli Ibra haya ndo malipo yangu?"

"Oya sikia sitaki drama zako, kama unaweza kurudi freshi hutaki tambaa, kwanza sikutaki mwanamke gani huna mbele wa nyuma "

"Leo Ibra leo mimi Tricia sina mbele na nyuma kwako, mwanamke ambae nime kuvumilia katika hali zote, nimekuwa nikipika na kufanya kila kitu kwaajili yako halafu unaniambia sina mbele wala nyuma kweli Ibra?"

"Bwanaee ondoka ulinivumilia kwani nilikuomba ,au nani alikwambia nahitaji house girl wa kufanya kila kitu changu si shobo zako .

Na ukiondoka hapa usirudi muone minywele yake , mwanamke hujipendi upo upo tu eti najiweka nature umekuwa msitu embu ondoka bwani unanijazia nzi"

Aliongea na kuongoka akiniacha nikiwa namuangalia nisiamini yale maneno kama ameyatamka yeye , mlinzi alibaki akiniangalia kwa huruma mno ila hakuwa na chakufanya.

Kwa hasira nikasema hapana huwezi kunichezea namna hii , nilimfuata haraka na kutaka kuingia ndani ili nikalishe kwa huyo kijuba wake ila nilidakwa hata kabla sijaufikia mlango.

Haraka akanikokota hapo napiga makelele ajabu ,na sijui bidada aliamua kuuchuna au maana hakutoka hata nje .

Basi Ibra baada ya kunikokota alinitoa hadi nje ya geti na kufika anani sukuma kama furushi la mchanga na kunambia " nimekwambia ondoka kwa upole ila naona unataka utoke ukiwa unachechemea "

Niliinuka na kumuangalia kwa hasira na kumuuliza "hivi ulikuwa na maana gani kunipotezea mda wangu na kunilisha vumbi kila siku "

"Wewe embu ondoa fuvu lako haraka nisije kugombana mke wangu kwanza ukitoka hapa hakikisha unafuta namba zangu na sio zangu tu hata za rafiki zangu sawa "

Aliongea na kurudi ndani huku akiniacha nikiwa nimepigwa butwaa, machozi yalishuka mashavuni mwangu huku mdomo ukiwa mzito hata kuongea.

Kwa maumivu ya hali ya juu niligeuka na kurudi nyumbani, njia nzima nilikuwa nalia kama nimefiwa 😔

Maumivu yalikuwa makali mno, kila nilivyofikilia na kukumbuka moment zetu nilijikuta nikizidi kuumia .

Nilifika nyumban na kuangukia mapajani mwa bibi 😫, bibi alishtuka na kuuliza shida nini nilimueleza huku nikilia kwa uchungu mno.

Bibi aliniinua mapajani mwake na kuniambia................

ITAENDELEA



PENZI LA MKATABA
SEHEMU YA 02
MTUNZI RITHA STORIES

https://www.tupoahapa.com

SONGA NAYO.....................

"Tatizo nini mjukuu wangu mbona uko hivi" bibi aliongea kwa huzini sana lakini sikumjibu zaidi nikaendelea kulia, na mda huo huo akaja rafiki yangu na kunikuta bado niko katika hali ya kilio.

Alishtuka na kuuliza " bibi kuna shida gani mbona Naomi analia hivi!?"

"Mimi sijui lolote maana kafika akiwa hivi hivi na hajaongea kitu" Ratifa alikaa chini taratibu na kunishika kichwani kwa upole sana akaniuliza .

"Naomi rafiki yangu nini shida mamy 🥺" sauti ya upole ya Ratifa ilinifanya nikajisikia vibaya zaidi haraka nikajitoa kwa bibi huku nikifuta machozi na kusema.

"Ratifa ! Ibra kanisaliti yaani nimemfumania na mwanamke nyumbani kwake cha ajabu hajali ndo kwaanza kanifukuza kwake"

Nilivyo sema hivyo Ratifa alizungusha macho🙄na kupiga mikono kama vile anafuta vumbi na kusema.

"Nilijua tu huu ndo utakuwa mwisho wenu ,lakini nilikwambia ila wewe ukajifanya kajol eeh dada unajua kupenda wewe haya ona sasa"

"Lakini Ratifa ulitaka nifanye nini wakati nilimpenda "

"Kwa hiyo kama ulimpenda ndo ufanye upuuzi kiasi kile ,haya ona sasa upendo wako ulivyo kuumiza "

Ratifa baada ya kusema hivyo bibi akamuuliza" kuna nini mbona kama siwaelewi" bila kuongeza neno wala kupindisha Ratifa alimueleza bibi kila kitu kuhusu mahusiano yangu na Ibra .

Aise bila kutegemea nilishtukia napigwa na mwichi wa kutwangia vitunguu swaumu 😬😢 haraka niliinuka na kusogea pembeni huku nikiwa nimeshika kichwa.

Bibi ambae ndio aliniponda na mwichi aliamka huku akifoka " mtoto mpumbavu sana wewe ina maana mda wote nimekaa nakubembeleza nikijua unalia cha maana kumbe ujinga tu.

Hivi nimekulea vibaya au umetingishwa ubongo ukubwani , yaani unawezaje kuvua utu wako na kufanya majukumu ya mke ile hali huyo mpuuzi wako hajulikani hata na balozi "

Nilibaki kimya huku nikisugua sehemu niliyo pigwa maana nundu tayar ilisha toka 🥺, basi kama ujuavyo wazee wakisha Pata la kuongea ni siku nzima .

Siku hii nilisemwa hadi nikoan eeeh inatosha ,jioni nikachukua pochi yangu na kwenda kwa Ratifa , kufika huko akanikaribisha vizuri tu.
Dakika mbili nyingi na yeye akaanza kunisema , nilichukia nikaamka na kutaka kuondoka akanizuia " hiyo ndio shida yako hutakagi kuambiwa ukweli mpuuzi wewe"

"Sikuka hapa kuambiwa ukweli nimekuja kupata faraja ila naona umekalia kunisema badala ya kunipa moyo"

"Nikupe moyo ili uupeleke wapi nilivyo kuwa nakwambia hakufai uliniona mjinga leo umepigwa tukio ndo unaona unahitaji faraja"

"Kwa hiyo kama ulikuwa unaniambia ndo kukufanye uniseme kila mda ,nimeshajua nimekosea sawa yaishe basi aaa!"

"Yaishe wakati limoyo ndo kwaanza linavuja damu, naa ilikuwaje ukaondoka bila kumponda hata na jiwe ?"
"Huelewi tu Ratifa sikuwa hata na nguvu zaidi nilikuwa kama nimepigwa shot, unajua nilimuamini sana Ibra na nilijua tunafika malengo lakini nimeachwa njiani ."

"Ndo ukome hata hivyo shukuru umeachwa salama maana wenzako huko wanaacha na mimba kama si ukimwi "

Alivyo ongea hivyo nilishtuka na kukaa , kaa yangu ilimshtua Ratifa akaniuliza " usiniambie una mimba !!"

Nilimuangalia usoni kwa macho yaliyojaa hofu na kusema " ni wiki ya pili sasa sijaona siku zangu "

"Yeeelewi mtume 🙆‍♀️, Naomi umeisha ndugu yangu wiki ya pili ee Mungu saidia hili jinga lako na umepima kweli?"

"Sijapima ila nilitaka baada ya chakula cha mchana twende tukapime "

"Mkapime na nanii?"

" Na Ibra "

"Kwa hiyo mmeenda?" Sikumjibu nikaa kimya ,aliniangalia kwa sekunde kadhaa Kisha akasimama na kuingia chumbani na kutoka akiwa amebadilisha nguo na kusema.

"Embu amka hapo twende hospital "

"Hospital kufanya nini ?"

"Kununua maparachichi au hujaya miss embu amkaaa bwana lione kama jinga "

Bila kuongeza neno niliamka tukatoka nje nikavaa viatu nakuongoza mbele ,mara nikasikia "wewe ndo nini sasa?" Niligeuka namuuliza .

"We nae nini tena "

"Ndo umetoka nyumbani hivi au umebadilishiwa njiani " aliongea huku macho yake yakiwa miguuni mwangu ,kujiangalia hivi mamaaa nimevaa viatu tofauti.

Nilimuangalia Ratifa wote tukaangua kicheko kwa pamoja , nikabadilisha viatu na safari ya kwenda hospital ikaanza .

Kufika huko nikapima magonjwa yote ya zinaa pamoja na mimba , majibu yalitoka nikaingia chumba cha dactari huku moyo ukidundua miguuni🥺 roho muombaji nae akawa kando yangu.
Nikawa nasikia kuomba tu 😅 uzinzi tunaupenda ila linapokuja swala la matokeo yake moyo unakaa juu juu 🥲 na mda huo huo unamkumbuka Mungu😐.

Basi bwana niliingi na kukuta doctor amekaa kunisubiri ,na baada kukaa aliniagalia jicho ambalo lilifanya nikaona hapa baaaasi nimeukwaaaa😩😫😫.

ITAENDELEA



PENZI LA MKATABA
SEHEMU YA 03
MTUNZI RITHA STORIES

https://www.tupoahapa.com

SONGA NAYO..........

Haya baada ya kukaa doctor aliiangalia kwenye computer yake kwa sekunde kadhaa Kisha akainua uso na kushusha pumzi ndefu kisha akasema.

"Naomi "

"Yes doctor "

"Aaam ,hivi ulivyo kuwa mdogo ulitamani ukiwa mkubwa uje kuwa nani?" Dactari aliuliza huku akiwa ameweka uso wa tabasamu , nilishusha pumzi kwa mbali huku nikijifanya kuto kuwa na hofu na kujibu.

"Nilitamani kuwa ntu mkubwa sana "

"Na umeshafikia lengo lako ama bado "

"Bado "

"Okay ila siunaamini kwamba unaweza kufika bila kujali hali ya kiafya au mambo mengine "

Nilitabasamu na kusema " yeah naamini " dactari aliniangalia tena kwa sekunde kadhaa ,mtoto wakike nikakaza roho na kujifanya sina hofu.

Nikaona dactari anatabasamu na kurudisha macho yake kwenye computer yake na kuniuliza " umeolewa ?"

"Hapana "

"Una watoto"

"Hapana "

"Mpenzi au mchumba je "

"Sina " nilivyo jibu hivyo aliinua uso na kuaniangalia kisha akarudisha macho kwenye computer na kuwa kimya kama sekunde 10 kisha akasema tena.

"Aaam sasa Naomi majibu ya vipimo yametoka na baadhi vinaonekana kuwa sawa but vingine vina shida kidogo "
"Ndio " nilijibu akarudi kuniangalia usoni kwa kunikazia na kusema.

"Hauna mimba , hauna UTI hauna gono wala maambukizi yoyote kwenye uke wako but .......!" Alivyo fika kwenye but akakaa kimya ,jamani nilikuwa nahisi kufa kwa presha .

Ila kama kawaida nilijikaza na kuweka tabasamu la uongo na kweli ,basi akasema .

"But kingine cha mwisho kidogo kilitaka kuleta mkanganyiko ila nimeangalia vizuri uko sawa ,hauna ukimwi"

Neno hauna ukimwi lilienda kuushusha moyo wangu kama vile mtu aliekunywa maji ya baridi baada ya kutoka kwenye jua kali😌.
Nilijifanya kuinama chini kama najikuna mguu nikatabasamu 😊 na kuinuka nikiwa nimeweka uso kawaida kabisa , basi dactari baada ya kusema hivyo alinipongeza kwa kupat majibu mazuri.

Nikapokea pongezi yake na kumuuliza " naweza kwenda tafadhali!!"

"Yeah ila samahanai naweza kupata namba yako ?" Bila hata kukwepesha nikamwambia " hapana asante sana na uwe na siku njema "

Alijibu sawa nikainuka na kuondoka ,moja kwa moja nikaenda alipo Ratifa nikampa majibu akaangalia na kusema .

"Umeponyoka kwenye mdomo wa mamba mbwa wewe na siku nyingine urudie sawa "

"Bwanaee embu niache nipumue kwanza maana hapa nilipo naona kama pumzi imebana"

"Na bado mbona utabanwa sana tu"

"Kwa hiyo unanitabilia mabaya sio "

"Eeeh twende maana naona unatafuta njia ya kuhamisha hasira zako"

Tuliondoka na baada ya mda tukafika nyumbani akapika tukala ,ilipofika jioni nikajikusanya na kurudi nyumbani.

Kama mjuavyo heartbreak haipatani na usiku kabisa 🥲 yaani ukiachwa ikafika usiku maumivu huwa yanaongezeka kwa kasi unakuwa kama umeachwa na dunia nzima 😔😔.

Moyo uliuma nikabaki nalia kwa uchungu , mda ulienda usingizi nao ukawa mbali na mimi kama masiala tarehe ikabadilika nikiwa bado sijalala .

Kila mda nikawa naangalia picha zangu na jambazi langu hili,nikawa natamani anitafute basi tuzungumze yaishe tu 😫 lakini hakujisumbua hata kidogo.

Basi bwana usiku uliisha kwa maumivu sana ,kesho yake sikuwa na mood ya kufanya kazi yoyote nikashinda nimejifungia ndani.

Na ilipofika jioni nikaona acha nikaupoze moyo huenda nitakuwa sawa , kweli nikajiandaa na kwenda sehemu flani hivi kali nikaagiza pombe Kali ambayo sijawahi hata kuitumia nikaipiga .

Fundo la kwanza lilikuwa kali ila haikunifanya niache ndo kwaanza nikashika chupa na kumimina yote tumboni na kuja kuiachia ikiwa tayari haina kitu .

Nikaagiza zingine na kuendelea kunywa kwa pupa sana huku mawazo yakiwa full, sasa bwana wakati nikiwa zangu bize kufakamia mipombe kulikuwa kuna kijana pembeni ananipimia tu.

Mimi bila kujali nilikunywa hadi ikafika mda sijitambui hata kidogo na kubaki nikiropoka mineno kama chizi ,na sikujua ni kitu gani kiliendelea zaidi nilikuja kuamka na kujikuta nimelala kitandani.

Kichovu niliinuka huku nikipiga miayo , taratibu nikageuza shingo yangu kuangalia
Maeneo niliyopo moyo ukashtuka kuona siko nyumbani. 😳

Tayari wameshani shenyenta😫😫.

ITAENDELEA



PENZI LA MKATABA
SEHEMU YA 04& 05
MTUNZI RITHA STORIES

https://www.tupoahapa.com

SONGA NAYO..............

Nilitoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango , moyo nao ulikuwa mbio nusu kuuacha mwili 😬.

Nikiwa bado natoa macho kama mhuni aliekamatwa na bangi mlango ukafunguliwa akaingia mwanaume akiwa anaongea na sm, 😢 mapigo ya moyo yaliongeza kasi nikawa nahisi kufa kwa mshtuko ulio ambatana na hofu kubwa .

Mara yule kaka akatoa sm sikioni na kusogea karibu ,hapo jasho linanitoka kama nimekaa pembezoni mwa tanuri🥵, basi baada ya kunifikia akanisalimia.

"Hello binti mzuri !"

Aliongea nikaa kimya huku nikijaribu kurudisha mafaili nyuma huenda nikakumbuka nimefikaje hapa 😮‍💨,lakini sikukumbuka kitu zaidi ya kuishia kupata maumivu makali ya kichwa 😪😪.

Kaka yule baada ya kuona nimekaa kimya alirudi nyuma akakaa na kusema ,"usihofu uko salama "

Baada ya kusema nilimuangalia usoni huku nikipeleka mkono kunako ikulu kukagua usalama , taratibu nikatoa bila uoga nikanusa huku nikiwa bado namuangalia 🤓 kitu ambacho kilimfanya akaangua kicheko kama katekenywa 🙄.

Mapigo yalipunguza kasi nikashusha pumzi ndefu na hii ni baada ya kuona niko salama kabisa ☺️ ,na nguvu ya kuongea ikaja nikamuuliza .

" Nimefikaje hapa na we ni nani?"

Nilivyo muuliza hivyo alicheka na kisema ," baada ya kuona pussy wako yuko salama umepata nguvu ya kuongea 😃 halafu nimependa unusaji wako ni wa viwango vya juu😆."

"Asante ,ila naomba uniambie nimefikaje hapa"
"Ooooh kuhusu hilo ,aaam nilikuchukua kwenye mikono ya wahuni walio taka kujisavia mautamu "

Nilimuangalia usoni kwa kumkazia macho maana nikama alikuwa anatania kwanza hata ongea yake imekaa kimasiala sana .

Sikutaka kuendelea kukaa nikainuka na kushuka kitandani ,nikawa naangalia pochi yangu ,akanambia " unacho angalia hakipo "

Alivyo sema hivyo nilimgeukia na kumuuliza " una maanisha nini !?"

" Namaanisha vitu vyako vilichukuliwa so hapo ulipo hauna kitu zaidi ya hiyo Pussy yako"

"We kaka sikia ,acha matani yako na uwe serious maana naona unaleta matani kama vile tunafahamiana "

Nilivyo sema hivyo aliinuka pale alipokaa na kunisogelea huku akiniangalia usoni, kwa hofu nilirudi nyuma akawa ananifata huku anasema.

"Unatak niwe serious si ndio ,mmh! Hivi unajua nimeacha mangapi yote kuhakikisha uko salama ?, nakuuliza wewe unajua nimeacha mangap "

Aliongea akiwa serious sana ,nikashuka na kumwambia " samahani sana lakini naomba uniambie vitu vyangu viko wapi"

"Vitu vyako ndo vya thamani sana kuliko utu wako? Au unajua hapa ilipo ni wapi na umefikaje na mimi je unanifahamu? "

Aliongea nikabaki kimya bila kuongea neno, akarudi nyuma na kusema " wasichana wasiku hizi sijui mmerogwa na nani?.

Mtu unahatarisha maisha yako kwa ujinga halafu hujali wala nini, kama ulikuwa unataka kujiuza ungeenda kwenye madanguro huko sio kuwenda sehemu hatari vile mfyuu"

Aliongea na kutaka kuondoka nikamwambia " hey subiri, uko sahihi kuwa na hasira ila hauko sahihi kuongea na mimi hivi hata kama nimekosea , kilicho nipeleka pale hukijui so usinifananishe na hao malaya"

"Oooh! Kwa hiyo ulikuwa na nia njema kabisa si ndio haya nambie umepata nini katika hilo lililo kupeleka pale , hivi unajua nisije kuja ungekuwa na hali gani kwa sasa au unaropokwa tu kwasababu uko sawa ?"

"Kaka asante kwa msaada wako na naweza kuondoka tafadhali!!?"

"Kuondoka namna hii !?" Jamani sijui ni hasira za kuachwa au ni kisirani sijui ila nilikuwa na naona kama vile anataka kuniletea usiku .

Bila kuongea nikampita na kutaka kuondoka akanishika mkono na kunambia " so dharau ndo malipo ya wema wangu si ndio ?" Aliongea akionesha kukasirika .

Niliutoa mkono wangu kwake na kumuuliza " kaka nimesema asante kwa msaada wako ila sijaelewa unataka nini kutoka kwangu maana kama kushukuru nimeshukuru "

"Unafikili nahitaji nini kutoka kwako ??🤨"

"Nikuulize wewe maana kunisaidia kidogo tu unataka kushukuriwa kama vile umeikomboa dunia🙄"

"Wow ,ningejua kama unatabia chafu hivi nisinge poteza mda wangu kufanya upuuzi "

"Asante ,na kama unahitaji kulipwa nambie maana najua hili jiji halinaga cha bure so sema nikupe nini kwa wema ulio ufanya ?"

Niliongea nikionesha kuvurugwa, kaka yule aliniangalia na kusema ...........


SEHEMU YA 05

"Natamani ningekuwa vile unafikilia ila sina huo ujinga " aliongea na kuondoka kwa kubamiza mlango .

Sikutaka hata kubaki asije kurudi bure ,haraka nikatoka kwa mwendo mkali ngoma ikaja nimefika nje ya chumba nashindwa kuelewa nipite wapi ili kutoka nje 🥲.

Nilisimama huku nikiangalia huku na huko mara akaja muhudumu na kuniuliza ,""Samahani wewe ndo umo kwenye chumba hiki ""

Kuulizwa hivyo niliogopa nikajiuliza nitaambiwa nilipe chumba nini ? Mama yangu naomba isiwe hivyo maana hapa sina hata mia 🥺.

Kama nilivyo waza akasema natakiwa kulipa , niliganda kama nimepigwa na shot😶 ,moyoni nikajisema leo nitaibika vibaya mno 😔 sijui nani kanituma kunywa pombe 😫.

Kwanza ngoja ni hotel gani au lodge gani ambayo utapewa /kulala bila kulipa 🤔 hawa wananiona wakuja sasa ngoja 😏.

Bila kuchelewa nilianza kumpa muhudumu maswali huku nikiwa na ujasiri wa hali ya juu 😊 ,mabishano yakiibuka kati yetu ikabidi aitwe kiongozi .

Kakaja kamdada kakopoa kinyama , kwanza tembea yake tu nikama alikuwa hakanyagi chini 😒, nikia nimesimama huku sijavaa viatu kalifika na kusema.

" dada unatakiwa kulipa bill sasaiv maana mda wako umeisha "

Kabla ya kumjibu nilimuangalia vizuri na kumuuliza " kama sijakosea hakuna utaratibu wa mtu kuingia chumbani bila kufanya malipo so nashangaa mnataka malipo gani.

Au kuna kitu mpenzi wangu alitumia labda hakijalipiwa ? Kama kipo semeni ila sio chumba "

Nilivyo sema hivyo ,bidada ambae alikuwa ndo meneja pale akawaka na kukazania kuwa sijalipa , na mimi sikutaka kuzalilishwa niling'ang'a kuwa chumba kililipiwa toka jana .

Ngoma ikaja baada ya kuulizwa kuwa kama kweli jina lililo andikwa kwenye kitabu cha malipo ni nani , nikawa haraka haraka na kumwambia sijui maana alielipia ni mpenzi wangu na sio mimi.

Bidada yule akasema ni uongo na kutaka kuita police ,nami kusikia police jicho lilinitoka nikajisemea hapa sitoboi 😦.

Basi bidada kuona nimepoa akatabasamu na kusema " unataka kujifanya wa mjini wakati wa kuja ,haya unalipia au niite police ukafundishwe adabu "

Mdomo ulikuwa mzito kuongea ,nikaishia kumeza fundo la mate huku mapigo ya moyo yakienda mbio 😪, alivyoona niko kimya akauliza tena .

Nikataka kumjibu ila kabla sijaongea nikasikia sauti ya kiume nyuma yetu ikiuliza nini kinaendelea ,, sauti ile ilifanya wote tukageuka nyuma .
Nikashusha pumzi baada ya kuona ni yule kaka alie nisaidia , ajabu wale wadada walivyo muona tu wote walipoa na kuwa wapole..

Kaka yule alipiga hatua hadi tulipo na kuuliza " nimeuliza nini kinaendelea hapa!?"

Bidada meneja akajibu " aam Nathan huyu dada hajalipia room na amegoma kulipia "

"Hajalipia! Imekuwaje mtu analala bila kulipia ,,? Huo ndio utaratibu mnaoenda nao sasaiv kwamba mtu analipia baada ya kutumia chumba ?"

"Hapana Nathan ila sijaelewa imekuwaje maana nimekuta chumba kimepikwa tik kuwa kimechukuliwa ila sijaona hela yake wala haijaandikwa kuwa imechukuliwa na nani"
Alivyo sema hivyo kaka yule ambae anitwa kwa jina la Nathan alinigeukia na kuwaambia " inaoneka hamko makini ,anyway tutamalizana baadae kuhusu ni mgeni wangu "

Kusikia neno ni mgeni wangu sura ziliwashuka mmoja wao akaniomba msamaha ila bidada mejena hakuongea kitu ndo kwanza akaondoka kwa hasira.

Basi baada wote kuondoka nikabaki na Nathan, hapo natafuta neno la kuongea maana najua kweli nimekosea kuongea nae vile .

Nikiwa sijaongea kitu alinitupia mfuko aliokuwa ameshika na kuondoka , aisee nilikuwa nataka kushuka niombe samahani ila kwa kitendo cha kunitupia mfuko ule nilichukia sana .😡😠
Yaani kisa kunidia ndo anataka kunifanyia upuuzi kiasi hiki 😠 hapana , niliinama kuchukua ule mfuko hapo akilini nilitaka nimtwange nalo la kichwa mshenzi huyu.😐

Nilichukua na kujikuta nikigaili kufanya kile nilicho taka kufanya na kubaki nikimuangalia namna alivyo kuwa akiondoka kwa hasira .

Unajua kwanini nimebaki nimesimama tu , mfuko alio leta ulikuwa na viatu ndani yake na mimi mda huo nilikuwa peku ,kwa maana hiyo viatu vile ameniletea mimi🥺.

Nisiwe muongo niliulaumu mdomo wangu uso kuwa na subra wala adabu 🤦‍♀️, nikaona ngoja nimfuate nikaombe msamaha maana niwazi nimekosea.

Basi nilivaa viatu na kutoka haraka kumfuata nyuma .

Endelea.............


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote