PENZINI NA SHEMEJI (sababu ni dada yangu )
Maisha ni fumbo kubwa sana , maisha ni kitu ambacho akielezeki kwa upande wangu.
Niite piya au Mrs jafeth, 😂🙌 nacheka kalma mazuri, huyu jafeth ni mume halali kabisa wa dada yangu lakini nilimbadilisha na akawa mume wangu wa ndoa na nilimzaliwa watoto mfululizo, najua unajiuliza Kwanini na niliwezaje lakini wacha nikuambie Kuwa.
UKIKIVAA KIATU CHANGU HAUTEMBE….
🤍🤎🤍🤎🤎🤍🤎🤍🤍🤍🤍🤍🤍
PENZINI NA SHEMEJI (Sababu ni dada yangu)
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 01
www.tupohapa.com
ANZA NAYO.......
Muombe Mungu akujaalie ndugu wanaojali na kujua umuhimu wa kuwa na ndugu lakini pia utu, Dunia yetu sasa hivi imebadilika sana, rafiki anachukua nafasi ya ndugu, halafu ndugu anachukua nafasi ya rafiki yaani mambo ni kinyume nyume tu hakuna kitu kinaenda sawa.
Niite PIYANA lakini wengi wamezoea kuniita PIYA hivyo na wewe niita Piya itapendeza zaidi.
Piya mimi nimezaliwa kwenye familia masikini sana, familia ambayo kupata unga wa uji tu ilikuwa ni kazi.
Achana na hivyo sasa, tulikuwa tuliishi mbeya ndani ndani kabisa baridi Kama lote hakukuwa ata na nguo nzuri za kutustili na baridi ilo.
Kwenye familia yetu tumezaliwa watoto watatu tu, ambapo mimi ni wapili na wa kwanza no dada yangu ambaye alijulikana kama Tusa lakini wa mwisho ni mdogo wetu wa kiume aliyejulikana kama Mwaisa.
Mwaisa alizaliwa na afya afifu sana, muda mwingi aliumwa, muda mwingi alikuwa akilia na hii ilichangia sana kwenye kudoloza ukuaji wake.
Katika tafuta tafuta za uku na kulez dada yetu tusa aliweza kupata kazi mjini, yaani alipata kazi za ndani na hii ilikuwa nafuu sana kwetu, tulikaa tukiamini kuwa dada yetu atakuwa chanzo cha kuvunja umasikini kwenye familia yetu.
Mambo yalibadilika pale tu tuli alipoingia mjini, hatukuweza kupata mawasiliano yale, lakini pia hatukuwa ata na namba ya simu wa boss wake na hii ndio ilibaribu kila kitu.
Maisha yalizidi kusa magumu sana, wazazi wetu walipata wasiwasi sana kila mtu aliamini kuwa uwenda dada tusa amepoteza maisha maana atukujua taarufa yoyote ile kuhusu yeye.
"Mama, Baba mnaweza mkaniamini tu, nipeni baraka zenu niende nikafanye kazi mjini"
Ilikuwa ni majila ya usiku sana na nilikuwa nikizungumza na wazazi wangu, kwa wakati huo tusa mimi nilikuwa nimepata kazi ya kazi za ndani na jilani yetu ndio alinitafutia.
Kwakweli moyo wa wazazi wangu ulikuw mgumu Sana , kila mtu alikuwa na wasiwasi sana ukizingatia dada yangu Tusa alienda mjini na hakufanikiwa kurudi kabisa.
"Tutaendelea na kilimo Piya hakuna sehemu unaenda, tumempoteza dada yako na hatujui kama yuko hai au laah na wewe tena unataka ukapotelee uko mjini"
"Lakini baba......"
Nilijaribu kujielezea lakini baba akanikatiza na kusema.
"Ni miaka minne sasa hatuna taarifa za dada yako, mimi kama baba yako nasema hivi hakina sehemu utaenda na hapa hakuna kikao kingine kile mtu akalale "
Hapo baba yangu akainuka na kuondoka.
Hali ngumu ya maisha ya pale nyumbani ilikuwa ikinitesa sana, hali ya mdogo wangu mwaisa ndio kabisa ilinifanya nikosea Amani na kujikuta nikitamani sana kwenda kufanya kazi mjini nankubadilisha maisha ya nyumbani kwetu.
Asubuhi na mapema, nilitoka nyumbani kwetu kww kutoloka na safari ya kwenda mjini ikaanza, muda huo nilikuwa nina namba ya boss wangu tu ambaye niliambiwa kuaa atanipokea.
Tangu kuzaliwa kwangu sijawai kumiliki simu jamani.
Mungu mwema, kwa msaada wa raia wema nilifanikiwa kufika mjini, walahi ili jiji la dar es salaam limejengeka sana tena sana, yaani ni majumba makubwa makubwa tu lakini pia na mataa ya kutosha.
Nilifika stendi na mwenyeji wangu aliweza kunipokea kwani nilikuwa nikiwasiliana nae kwa namba ya abiria mwenzangu.
Mwenyeji wangu alikuwa mkaka fulani hiviz mzuri sana, mweusi, ameenda hewani, kifua kimechanika vizuri, kwa muonekano tu alionesha kuwa ni mtu na pesa zake, yaani ni mtu ambaye pesa ipo bila pingamizi.
"Hope ujapata shida njiani )
Alizungumza mwenyeji wangu tukiwa kwenye gari yake.
"Mimi ? Aaah mimi naitwa Piya sio hopu "
Nilijibu.
Kwanza mkaka huyo alitabasamu kisha akazungumza tena.
"Ooooh kumbe ni Piya basi sawa, una umri gani wewe ??"
Aliniuliza.
"Miaka 23 kama sio 24 au tufanye 25 tu maana mimi na dada yangu mama alisema kuwa tumepishana miaka mitatu tu hivyo ata sijui sasa hivi yeye anamiaka mingapi"
Walahi majibu yangu yalikuwa yakimchekesha sana mkaka wa watu ambaye alishindwa kabiss kubana kicheko chake na kujikuta akicheka kwa sauti.
"Umesema unaitwa piya si ndio ??"
"Eeeh unauliza sana jina langu wakati jina lako sijalijua unaitwa nani na wewe ??"
Nilimuuliza mwenzangu maana kakazana kuulizia jina langu tu halafu ata jina lake alitaji maana yake nini.
"Naitwa jafeth lakini ningependa Uniite kaka, mimi ndio boss wako wa kiume na mke wangu ni boss wako wa kike "
Hapo sasa ndio nikagundua kuwa huyo mkaka ni boss wangu maana muda wote nilihisi kuwa yeye ni mtu ambaye alitumwa kunifuata tu.
Mwendo ulikuwa mrefu sana na foleni za dar nikajikuta nikilala usingizi kabisa kwenye gari ya watu na nilikoloma utazani nipo mbeya 😅.
Hatimaye tulifika nyumbani kwa boss, walahi alijaaliwa nyumba nzuri saana, ilikuwa ni nyumba nzuri na yenye uzio wa kisasa geti imara kabisa.
"Karibu sana piya "
Alinikaribisha boss wangu huyo na kwa pamoja tukaingia ndani.
"Babe, honey "
Mwanaume huyo alianza kuita mimi nilibaki nikishangaa uzuri wa nyumba yao.
Muda huo huo akatoka mwanamke fulanj hivi, akikuwa mweupe sana na kwa bashasha mwanamke mke huyo akamkumbatia boss wangu..
"Nimekumisi sana mume wangu "
Alizungumza mwanamke huyo na kummwagia mwanaume wake makiss ya kutosha.
"Sauti yake inafanana ba ya dada tusa "
Nilizungumza kimoyomoyo tu.
Bwana bwana, katika kumuangalia vizuri nikagundua kuwa ni dada tusa , kwa furaha nikataka kumkumbatia lakini alinipa ishara ya nitulie na nikae kimya kwa haraka nikachukua kidole changu na kuweka mdomoni, ila mimi akili zangu nazijua mwenyewe walahi.
Baada ya muda nilikaribishwa vizuri sana na dada yangu ndio alinipeleka kwenye chumba changu.
"Da Tusa tumekutafuta sana "
Nilimwambia baada ya kuingia chumbani.
Kwanza da tusa alinigeukia kwa hasira sana na kuniuliza.
"Tusa ni nani ??"
Nilitabasamu na kumwambia.
"Sawa sasa hivi umekuwa mweupe lakini haimaanishi kuwa wewe sio tusa, me nakujia vizuri sana "
Hapo kwanza nilijikuta nikichezea kibao kimoja matata, wenyewe tunaitaga kibao cha mwanaukome 🥹 yaani dada yangu leo hii ananipiga kibao kwakuwa tu nimemuita jina lake.
"Ukitaka kazi ikushinde umu ndani refusha huo mdomo wako ndio utajua mbivu na mbichi, ukitaka kujua kuwa mjini sio nyumbani kwa kila mtu endelea kunijua jua mpuuzi wewe "
Hapo alisukuma kichwa changu na kwa hasira akatoka nje, nilibaki nikishangaa tu, lakini muda huo huoa akarudi na kuzungumza.
"Bafuni ni umo, hakikisha unatoa jasho zote mwilini na huo utoko wako wa harufu mbaya unaonuka dohoho na uje kuungana nasi kwenye chakula"
Eeeeeh 😩 hii ya leo kali, yaani let hii mimi nanika dohoho kweli ?. .
"Au sio da tusa ni watu tu wamefanana ??"
Nilijiuliza kimoyo moyo.
"Lakini ni yeye, sauti na sura ni ile ile, aoichobadilika ni rangi tu na kunenepa, lakini kwanini anikatae ??"
Nilibaki nikijiuliza maswali ambayo hayakuwa na majibu.
Kasheshe bwana likaanzia bafuni, picha linaanza, hakukuwa na ndoo ya kuogea wala lile Kopo la kushika, walahi ni choo cha kusasa sana ambacho kwa upande wangu sikuwai kukiona wala kukitumia.
"Jamani, hii ni nini sasa ??"
Nilijiuliza uku nikipapasa ile tank ya maji ya kuflashia, katika fusa gusa si ndio nikabonyeza bwana na maji ya kuflash yakatoka 😅 unafikili nilifanya nini ? Hapo hakuna kingine ni hatua moja mbele, dakika yangu moja tu tayali nilikuwa sebuleni.
"Piya kuna shida gani ??"
Boss wangu wa kiume aliniuliza baada ya kuona kuwa nimepaniki sana.
"Kuna mafuliko chumbani kwangu "
😅😅 ila mimi jamani khaaah nimezidi sasa, yaani maji ya kuflash yanakuwaje mafuliko.
"Ahahaha utani wa aina gani huo, haya mafuliko yanakujaje chumbani kwako au Bomba limeharibika ??"
Aliniuliza kwa utulivu mno lakini pia alionesha kunicheka.
"Twende ukaone "
Nilijibu uku nikimshika mkono na kwa haraka mimi na yeye tukaingia chumbani kwangu, na moja kwa moja tukaenda chooni.
"Hapa, yalikuwa yanafulumia '
Nilizungumza uku nikimuonesha kwenye choo ambacho kilikuwa ni cha kukaa.
Aaah boss wangu hana baya bwana, alinicheka kwa muda mwisho akatumia muda wake kunielezea kila kitu.
"Asante sana "
Nilimshukuru.
"Most welcome "
Baada ya muda sote tulikutana kwenye meza ya chakula, wenzangu walitumia uma kwenye kula chakula lakini mimi nilitumia tu mkono wangu maana ata kijiko kilinishinda.
Muda wote tukiwa mezani nilikua nilimtazama sana boss wangu wa kike, nilikuwa najitaidi kuhakikisha kuwa ni dada yangu au laaah, kila nilivyozidi kumuangalia ndio nilizidi kupata majibu kuwa ni yeye na si mtu mwingine.
"Kwanini unaniangalia hivyo ??"
Dada tusa aliniuliza.
"Aaah, mmmmh "
Nilishindwa kujibu nikabaki nikijiuma uma tu.
Baada ya kumaliza kupata chakula, boss wangu alitumia muda wake kutoa utambulisho ili kuweza kujuana kiundani.
"Aaah Piya, huyu ni mke wangu anaitwa Linda, ni boss wako wa kike, lakini ningependa umuite wifi kwasababu mimi ndio kaka yako sawa ??"
Boss jafeth alionekana kuwa mkaka fulani hivi, mtulivu na amcheshi sana.
Kuna namna akili ilikuwa inaniambia nilopoke kuwa huyu ni tusa na sio Linda, yaani dada yangu kufika tu mjini kabadilisha rangi ya ngozi yake lakini pia na jina 😅😅.
*******
Hatimaye nilitimiza week moja nikiwa kama house girl kwe ye nyumba ya dada yangu, na kipindi chote icho nilikuwa nikimuita wifi Kama ambavyo boss jafeth aliniambia.
Kwa upande wa dada yangu bwana hakuwana muda na mimi ata kidogo, alihakikisha kuwa mimi na yeye hatupati nafasi ya kuzungumza chochote kile.
"Kaka, nilikuwa naomba simu yako nitapate kuwapigia simu nyumbani "
Nilimuomba bos
"Ooooh hivi kumbe hauna simu ? Ngoja tuone nakusaidiaje kuanzia kesho "
"Sawa "
Haraka nikaingia chumbani na kuchukua namba za baba yangu na kuzipeleka kwa boss jafeth.
Baada ya muda niliingia chumbani kwangu nikiwa na simu ya boss wangu.
"Baba shikamoo "
Nilisalimia baadanya simu kupokelewa.
Nilikaa kimya kisogo kisha nikaendelea.
"Mnisamehe sana wazazi wangu, lakini niko salama kabisa, hali ya maisha ya nyumbani haikuniruhusu kabisa kuendelea kukaa hapo, nawaaidi kuwa nitaangaika na kuhakikisha tunabadilisha maisha yetu "
Nilianza kujielezea sasa maana baba yangu alikuwa akigomba saba.
"Lakini baba, dada tusa yuko hai, na ni mtu mwenye pesa sana kwa sasa, ndio boss wangu hapa nilipofikia lakini amenikana kuwa ani......."
Kabla sijamaliza nilishtuka baada yakupigwa bao moja matata sana mgongoni.
Nika.......
Je ni nani amenipiga ? Tukutane sehemu ijayo....
PENZINI NA SHEMEJI (Sababu ni dada yangu)
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 02
www.tupohapa.com
ANZA NAYO.......
Hakuwa mwingine Bwana zaidi ya dada yangu ambaye alikuwa amekunja sana sura yake utazani anataka kuweka kwenye mfuko 😃.
Muda huo huo akanipokonya simu na kukata kabisa na hapo hapo akablock namba ya baba kwenye simu ya mume wake.
"Mwanzo mwisho leo kutumia simu ya mume wangu kuwapigia simu hivi vibwengo vyako sawa ? Subilia mshahara wako utanunua simu na sip kusumbua watu, muone kwanza sura yake kama katuni za masudi kipanya "
Kaaaah kama ni chuki basi hii ni viwango vingine sasa, yaani kosa langu ni nini jamani, ebu mniambie na dada zenu waliofanikiwa wapo hivi hivi au ??🥹
"Hivi tusa ni kweli unijui mimi ??"
Nilimuuliza kwa sauti yenye maumivu sana ndani yake..
"Nafikili kazi imekushinda "
Alizungumza hivyo na kwa haraka akatoka nje na muda huo huo nikasikia boss wangu wa kiume akiita jina langu.
Haraka nikakimbilia sebuleni.
"Kwanini utaki kazi ? Nyumbani umepata matatizo au ??"
Boss wangu mwaya aliniukiza maswali mfululizo, nilibaki nikimuangalia tu dada yangu ambaye yeye ndio alitunga uongo shidi yangu.
Nilikosa majibu sahihi nilijikuta nikiangua kilio tu maana daaah, imagine huyu mtu anayenifanyia visa ni dada yangu kabisa, tunashare mpaka ukucha.
"Piya hayuko sawa, ata hivyo ni mazingira mapya tu, nafikili tumpatie muda na atakuwa sawa "
Boss jafeth alimwambia mke wake ambaye alikuwa akutaka mimi niondilolewe.
"Mume wangu huyu msichana sio mzima tutakuja kupata matatizo "
"Tuliza wasiwasi mke wangu, piya atakuwa sawa "
Aaaah Mungu mwema bwana mawazo ya boss shemeji yakatiki na sikuweza kutolewa ndani umo.
*******
Hatimaye siku nyingine ikashika nafasi jamani, niliendelea na shughuli zangu kama kawaida, kuna muda nilijikuta nikianza kumchukua dada yangu, walahi tusa amebadilika sana, sio tusa yule ambaye nilikuw anikicheza nae udako tukiwa kijijini.
Majila ya jioni, shemeji aliweza kurudi kutoka kazini, lakini pia dada tusa alirudi kutoka kwenye biashara zake kwani alikuwa na duka kubwa tu la nguo hapa mjini.
"This is for you piya "
Shemeji ambaye ni boss jafeth alinikabizi box la simu ndogo, kabla sijajibu kitu dada tusa akadakia.
"Ni nini hii ? Mmeanza kununuliana zawadi si ndio ? Tena mbele yangu mnapeana kabisa "
Jafeth alimuangalia mke wake kisha akamjibu.
"Linda hii ni simu tu, na nakumbuka jana usiku nilikuambia kuwa nitamnunulia Piya simu kwaajili ya mawasiliano anapikuwa hapa nyumbani, lakini pia apate kuwasiliana na wazazi wake "
"Waoooh waoooh kwa sasa ni Linda eeeh sio tena babe wala honey, nilijua tu haya yatatokea "
Haki ya Mungu walahi, ningekuwa na mamlaka walahi ningemtwika ngumi huyu tusa mpaka akili imkae sawa, yaani yeye muda wote anawazia drama, drama juu ya drama kweli jamani, haya ni maisha ya aina gani 🥺💔.
"Nkmechoka Linda "
Alijibu boss jafeth na kwa hasira akainuka na kwenda chumbani kwake.
"Umefurahi sasa au ? Hivi pita umesharithi uchawi wa baba na mama si ndio ??"
Aaaah afadhali kwanza amekubali kuwa yeye ndio tusa maana nilikuwa njia panda muda wote.
"Kwahiyo wewe ni tusa ??"
Nilimuuliza.
"Yaah ila sio tusa yule wa kujijini, kwa sasa naitwa Linda, huyo tusa alishazikwa kwenye vumbi la kijijini mbeya, Piya nakuonya, nakuonya nikiwa nimeshika titi langu la kushoto, nikuone ata siku moja umenyanyua huo mdomo wako na kumwambia mume wangu kuwa mimi na wewe ni ndugu nitakutoa uhai "
Eeeeh kama ni pepo ili la tusa limeingia mpaka kwenye damu walahi.
Siku hiyo bwana nyumba ilijua kuchafuka walah, hakikuwa na amani ata kidogo..
Siku iliyofuata nilimuomba kaka mlinzi anisaidie kuset simu yangu, kuniwekea laini ambayo shemeji hafeth alinisajilia na kila kitu.
Bwana bwana ikawa kama kichaa kapewa lungu hivi. Baada ya kila kitu kutimia, niliingia chumbani kwangu na kumpigia simu baba.
Hapa nilibahatika kuzungumza hadi na mama yangu ambaye alifuraha sana kusikia kuwa binti yake wa kwanza yuko hao na yuko sehemu salama.
"Mateso ambayo Tusa ananipatia utazani anifahamu, mama, tusa hatuiraji tena, maisha ya mjini yamemuharibu sana dada yangu "
Nilipata muwa wa kuwasimulia wazazi wangu kila kitu mwisho mama akasema.
"Piya binti yangu ishi maisha yako tu, upo na baraka zeti zote, kwa sasa tunakutegemea sana, kwa sasa wewe ndio ufunguo wa familia hiina kuhusu Tusa lolote limkute, natema mate chini atokuja kuona furaha kwenye maisha yake "
Mama alitoa kila aina ya laana kwaajili ya dada tusa.
"Mama mwaisa ni maneno gani hayo kwa mtoto jamani "
Baba yangu ambaye ni mpole sana, alimtuliza mama uku akimpa moyo kuwa kila kitu kitakuwa sawa.
Baada ya kumaliza kuzungumza na wazazi wangu, jioni ilikuwa tayali imeshaingia, haraka nikaingia jikoni kwaajili ya kuandaa chakula.
Nikiwa bize sina ili wala lile dada tusa akaingia jikoni na kuzungumza.
"Nikupe kiasi gani wewe na familia yako muondoke kwenye maisha yangu ??"
Nika......
JE NI KITU GANI KIMETOKEA MPAKA NAULIZWA HIVI ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO....
PENZINI NA SHEMEJI (Sababu ni dada yangu)
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 03
www.tupohapa.com
ANZA NAYO.......
Nikageuka na kumuangalia kwa dharau sana kisha kwa kujiamini nikazungumza.
"Hatuitaji chochote kile kitoka kwako tusa, oooh samahani Linda, Linda kipenzi hakuna kitu tunaitaji kutoka kwako, kuanzia leo mimi ni piya kijakazi wako na wewe ni Linda boss wangu imekaaje hiyo ??"
"Vizuri sana, umefanya vizuri mno, masikini wa kutupwa weee "
Daaaah imagine, huo umasikini ndio umemkuza mpaka hapa alipofikia halafu leo hii anakuja kuninyooshea mdomo kama alizaliwa kwenye maisha mazuri vile.
"Babe "
Ilikuwa ni sauti ya shemeji jafeth akimuita mke wake, yaani watu wa mjini bwana ni kuitana tu majina mazuri.
Kuna namna niliona kuwa ndoa ya Dada tusa aina amani ata kidogo, kuna muda walikuwa akigombana kwa sauti sana na mara nyjngi dada yangu ndio alionekana kuwa juu kuliko shemeji.
Ikiwa ni siku ya jumamosi, familia nzima ilikuwa ni siku ya kuwa nyumbani, lakini shemeji jafeth akipata dharula na kuondoka.
Baada ya shemeji kuondoka, alikuja msichana mmoja hivi alikuwa mrembo sana na alikuwa mweupe kama dada tusa msichana huyo alikuwa ni rafiki wa sasa tusa.
"Aaah shoga yangu umejua kuniweka walahi, yaani nilimuwa najua kuwa hautaweza kuja "
Alizungumza da tusa uku akimkumbatia rafiki yake.
Ikumbukwe kuwa uku mjini kila mtu anamjua da tusa kwa jina la Linda na sio tusa kama ambayo kijijini tunamjua.
Muda huo niliingia jikoni na kuanda juice kisha nikaipeleka mezani kwaajili ya mgeni.
"Karibu sana "
"Asante "
Alijibu msichana huyo ambaye aliganda akinitazama sana mwisho akauliza.
"Linda huyu ni mdogo wako au ??"
Hapo Dada yangu akishtuka sana, akaaangalia uku na uku kisha kwa kujichekesha akazungumza.
"Mdogo wangu ? Why? How ? No way "
Walahi kwa upande wangu nilikuw anikizisikia hizo why, how, no way lakini sikuw ata najua anaongea kuhusu nini , yaani sasa hivi dada yangu anaongea kingereza kweli ametuacha mbali walahi 😅🙌🏻.
"Noooh nimeuliza tu maana kuna namna naona kama mnafanana hivi, kwa kifupi naweza kusema kuwa mnatofautiana rangi tu na mwili kiasi maana wewe ni unanenepeana tu "
Hapo da tusa aliniangalia na kwa hasira akaniuliza.
"Unasubuli nini hapa ??"
Aaah sikua na cha ziada haraka nikarudi jikoni na kuwaacha waendelee na maongezi yao.
"Aaah shoga yangu we acha tu, me mwenyewe siku ambayo huyu binti amefika nikushtuka sana nilipomuona, lakini sisi hatunuani ata kidogo, mwenzangu anatokea mbeya Na mimi niko zangu uko kwa wahaya"
Daaaah yaani da tusa amebadili mpaka mkoa wake 🙌🏻😅 ila huyu mbwa atakuja kuzalilika vibaya huyu me nipo tu namtazama.
Story ziliendelea pale na mimi nikaendelea na shughuli zangu.
*******
Hatimaye na mimi nikamaliza nusu mwaka nikiwa mjini jamani, kidogo nilianza kupendeza, nilianz kuoga vizuri na kutumia vimanukato, vinguo nguo kidogo vya mtumba walahi niliona utofauti.
Kwa nyumbani kwetu nilijitaidi sana kuwatumia pesa, kila nilipokuwa nikipomea mshahara nilihakikisha kuwa nyumbani anaapat nusu yake, ingawa haikuwa kubwa lakin pesa hizo zilikuwa zikiwasaidia sana.
Kila simu nilikuwa nikipokea maombi mazito sana kutoka kwa wazazi wangu.
Kwa upande wa dada yangu ndio alikuwa bize na maish ya mjini tu.
Dada yangu na shemeji ni watu ambao wanaugomvi mkubwa sana, ugomvi wao ulikuwa ni juu ya kuwa na mtoto.
Kwa upande wa shemeji alikuwa akiitaji sana mtoto, lakini dada hakutaka ata kusikia.
"Jafeth, muda wa mimi kuwa mama ni bado saba kwakweli, naitaji ku maintain uzuri wangu, natamani kuwa mrembo kila iitwapo leo, sitaki kupoteza shape yangu nzuri kwaaji ya kuzaa "
Hata ndio yalikuwa majibu ya dada yangu kwa shemeji kila walipokuwa wakizungumzia suala la wao kuwa na mtoto.
Naweza kusema Kuwa shemeji yangu ni mtu Mtulivu sana, na mnyenyekevu, Sijui maisha Yao ya uko nyuma, lakini kwa maisha haya ambayo nayaona Walahi dada yangu ajielewi.
Siku moja nikiwa chumbani kwangu na na ilikuwa majila Ya Saa 4 usiku, shemeji Jafeth alikuja chumbani kwangu na kuniuliza.
“Dada yako alikuambia Kuwa atachelewa ??”
“Hapana kaka sijazungumza na dada Leo “
Hapo shemeji yangu alishusha pumzi nzito sana kisha akakaa pembeni yangu na kwa sauti ya utulivu akazungumza .
“Ndoa zinamambo Mengi sana, lakini hii ya kwangu Inaitaji moyo sana “
“Pole “
Niliishia kumpa pole tu maana sikutaka kuingilia maisha ya watu Mie.
“Unaweza kunisaidia kitu Piya ??”
Shemeji aliniuliza.
“Kitu gani ??”
Nilimuuliza.
“Niambie tu kwanza unaweza kunisaidia ? Hii kitu tutanufaika Mimi na wewe Tena kwa haraka sana “
“Mmmmh, ni kitu gani iko ??”
“Unizalie “
Mmmmh 😳😳 woiiiiih Mbona gafla jamani……
HUYU SHEMEJI YANGU ANAMAANISHA AU NI MITEGO TU YEYE NA MKE WAKE WAMENIWEKEA ??
PENZINI NA SHEMEJI (Sababu ni dada yangu)
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 04
www.tupohapa.com
ANZA NAYO.......
Nilimuangalia shemeji yangu kwa muda weeeh kisha nikazungumza.
“Inawezekanaje ? Wewe ni boss wangu na Nimekuja uku kwaajili ya kufanya kazi tu “
Niwakumbushe watu wangu Kuwa muda wote huo, boss jafeth hakuwa anajua Kuwa Mimi na mkewe ni mtu na dada yake, lakini pia mkewe Jina lake halisi ni tusa na sio Linda Kama ambavyo yeye anafahamu.
“Najua nakuchanganya lakini huo ndio ukweli wangu kwa sasa, piya, Nimekuwa nikitafuta mwanamke wa kuzaa nae kwa muda Mrefu sana, nimekuwa nikiangaika uku na uku lakini sijaona aina ya mwanamke ambaye namtaka, naitaji mwanamke Mtulivu na anayejali Sanaa na sifa hizo nimeziona kwako”
Kuna Namna moyo wangu uliniambia mwambie Kuwa wewe ni shemeji yake, lakini niliamua kunyamaza tu kwani dada hakutaka kabisa watu wajue Kuwa Mimi ni Mdogo wake.
“Sizani Kama naweza, hayo ni maamuzii makubwa sana, lakini pia wewe ni mume wa mtu, Kama ni kuhusu kupata Mtoto zungumza na dada Linda tu “
“Piya, hii kitu itakuwa Siri yetu, itakuwa ni maisha yangu tu Mimi na wewe, nitakutoa hapa na kukupeleka sehemu nzuri na salama niamini Mimi “
“Siwezi “
Shemeji yangu aliinuka kisha akazungumza.
“Nakupa muda ufikilie na ukipata majibu usisite kuniambia”
Eeeh nilibaki nikipumua tu maana khaaah mambo makubwa haya..
Siku ziliendele la kwenda na nilianza kumkwepa shemeji sikutaka kabisa Mazoea nae, Sawa mwanza nilikuwa nikimuheshimu, lakini safari hii niliongeza heshima 😂 Yaani nilianza kumuamkia nikiwa nimepiga goti Sijui mnaelewa 😂😂🙌.
Siku moja nikiwa nimejipumzisha tu naangalia tv, niliweza kupokea simu kutoka kwa mama na alikuwa akilia sana.
“Piya, zungumza na tusa, mwambie tusa Kuwa kwa sasa tunamuitaji sana, Mwambie Kuwa kwa sasa yeye ndio Mkombozi wa maisha ya Mwaisa, mwaisa ako na hali mbaya sana”
Hapo wasiwasi ilinipata na kwa woga nikauliza.
“Mwaisa anasumbuliwa na nini Tena mama??”
“Mwaisa anaitaji upasuaji wa haraka sana, kwa sasa hivi tupo hospital ya Mbeya mjini, Mwaisa anapumulia Mipira Mtoto wangu anateseka sana”
“Upasuaji wa nini mama ??”
“Mwaisa amekutwa na uvimbe kwenye ubongo na damu imevilia
“
Woiiiiih 😭🙌 hii ni nini jamani, maisha yenyewe ndio haya ya kuunga unga halafu matatizo ndio Kama haya kweli jamani 😭.
Majila ya jioni, nilimsubili da tusa aweze kurudi Kazini, na kwa upole wa hali ya juu nikamfata.
“Haya ni nini unanijia hivyo na sura yako ya jioni ??”
Tusa aliniuliza.
Na kweli nilikuwa na sura ya jioni maana daaah, siku hiyo nililia sana, nilikuwa namuwazia sana Mdogo wangu Mwaisa.
“Tunaweza kuzungumza ??”
Nilimuuliza.
“Sina cha kuzungumza na wewe, hivi Piya Kwanini mnafosi udugu wangu wewe na hiyo familia yako?”
“Kwasababu wewe ni ndugu yetu, kwasababu wewe ni familia yetu 🥺 tusa sijui tumekukisea nini lakini Kama kuna chochote kile tumekukosea niko mbele yako kuomba msamaha “
“Niondolee uchuro hapa, Yaani natamani ungekuwa unaelewa ni kiasi gani nakuchukia, natamani wewe na hao ndugu zako mngeelewa ni kiasi gani nawachukia na sitaki ata kuwasikia”
Eeeeeh huyu jamani, Yaani hapa sijaanza ata kumuelezea shida tayali ananipatia majibu Kama haya kweli jamani 🥺 hapa nitapata msaada mmmh.
“Tusa Mwaisa maisha yake yapo hatarini”
Hapo tusa aliniangalia kisha Akatabasamu na kusema.
“Huyo sasa nae afe khaaah, yangu amezaliwa ni kuumwa na kuumwa, muda wote watu wamekuwa wa kumuangalia tu, mtu gani hakui “
“Usiseme hivyo tusa, Mwaisa anatuitaji sana “
“Akafie mbele uko “
Muda huo huo simu ya dada tusa ikaita na Rafiki yake ndio alikuwa akimpigia haraka akapokea na Kiwelu loudspeaker.
“Tajiri Mbona ufiki wenzio tutazalilika uku “
Ilisikika sauti ya Rafiki wa dada kwenye simu.
“Ndio kwanza nimefika home, ngoja nioge chap nije “
“Tushaanza kunywa na kila hapa lakini hatuna ata mia kwani hautachelewa ??”
“Kuna sehemu napitia, anyway wacha nikuwekee laki 3 muanze nayo si itatosha ??”
“Huna baya Tajiri”
Alizungumza Rafiki wa dada.
Daaaah kweli kuzaa sio kupata, Yaani wazazi Nyumbani wanashindia uji halafu yeye anawapa watu Pesa zote hizi kwaajili ya starehe 😭💔.
Dada yangu aliniacha hapo na akaingia chumbani kwake, kwa muda huo mama alikuwa akiitaji Pesa ya chakula, haraka nikaingia chumbani na kuchukua akiba yangu na pasi na kupoteza muda nikakimbilia kwa Wakala.
Majila ya Saa 3 shemeji alirudi na kunikuta Mimi tu, tulisalimiana pale kisha akaingia chumbani kwake kwaajili ya Kwenda kuoga.
Baada ya muda akatoka nje na kuja kuungana Nani kwenye meza ya chakula, nilikuwa nikila uku nikimtazama shemeji, mwisho nilijitosa na kumuota..
“Kaka jafeth “
“Niambie “
Jafeth aliitika pasi na kunitazama .
“Nilikuwa naitaji Msaada wako, sina mtu wa kunisaidia zaidi yako “
Hapo nilijimwaga Bwana, Nikita shida zangu zote uku nikilia michozi gadagada.
“Utanitukia Namba ya mama au account ya malipo ya hospital ili nifanye malipo “
Nyie sikuamini macho yangu, Yaani amekubali haraka haraka pasi na kuniuliza maswali yoyote.
Nikapiga goti na kumshukuru.
“Mungu akubariki sana, Sijui bila wewe Leo hii ningekuwa mgeni wa Nani Mimi “
“Usijali “
Hapo shemeji aliniinua na kunikumbatia kwa nguvu sana na akazungumza..
“Ukiwa na shida yoyote ile niambie”
*******
Asubuhi na mapema siku iliyofuata, malipo kwaajili ya upasuaji wa Mdogo wangu Mwaisa yalilipwa full kabisa na Mlipaji ni shemeji yangu na nusu Yaani jafeth.
Wazazi wangu wali Shukuru sana sana, niliwaambia Kuwa mkwe Yao ndio Amelipa, lakini pia nikawajuza Kuwa dada amekataa kata kata kunisaidia.
Majila ya usiku Kama Saa 3 hivi nikiwa chumbani, niliweza kupokea simu na safari hii baba ndio alikuwa anazungumza.
“Aaah Mwambie shemeji yako Kuwa tunashukuru sana sana, kwaajili yake Leo hii Mwaisa ameweza kufanyiwa upasuaji ambao ulikamilika Saa 8 mchana, ingawaje wakati huu nasikitika kusema Kuwa Mwaisa hatukonae tena.
NIKA…….
ITAENDELEA
PENZINI NA SHEMEJI (Sababu ni dada yangu)
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 05
www.tupohapa.com
ANZA NAYO.......
Daaaah Yaani baba Ames za vizuri kabisa halafu ameliyat kuharibu uku mwishoni, Yaani anasemaje Kuwa upasuaji ulikami halafu tu mara mtu kafa ndio nini jamani 😭.
Nilijikuta nikilia sana, nilikuwa kwa sauti ya huu ambayo ilimshtua dada yangu ambaye hakupoteza muda akaja yeye akiwa na shemeji.
“Kelele zote hizo za nini usiku huu ??”
Kama kawaida dada akaanzaa kunifokea.
KWa upande wa shemeji ilikuwa tufauti, alinisogelea na kuniuliza.
“Kuna shida yoyote ??”
“Mwaisa, Mwaisa wangu jamani “
Hapo kila mtu alielewa Kuwa Mwaisa amefariki.
Shemeji alinikumbatia na Kuanza kunituliza lakini dada alibaki akiniangalia Kama anaangalia shombo ya samaki.
“Msiba uko uko kabisa halafu unalia Kama uko hapa, save hayo Machizi yako ukalilie Nyumbani kwenu “
Alizungumza dada yangu Mwenyewe, Yaani dada ambaye ata huyo Mwaisa aliyefariki na. Yeye ni Mdogo wake kabisa.
Shemeji kWa hasira akamsogelea mke wake na kumwambia.
“Huyu sio Linda wangu Mimi, Linda umekuwa na roho ya kinyama sana, Mbona ikiwa hivi umepatwa na nini ??”
“Eeeh baba huruma, sikia Naomba Niwaache tu sina huu muda “
Dada alitoka nje na kuniacha nikiwa na shemeji, nyieeeh nilijikuta nikipata hasira sana, chuki ya hali ya huu ilijijenga shida ya dada yangu pasi na kufikilia Mara Mbili nikazungumza.
“Niko tayali kukuzalia kaka jafeth “
“Piya, relax mama Sawa, Najua kuwa hauko Sawa, Najua Kuwa Unapitia kipindi kigumu sana”
“Nilichoongea Namaanisha, niko tayali Kuwa mama wa Mtoto wako na na ukiitaji mimi niwe mke Basi pia niko tayali”
Shemeji alifurahi sana ana kWa haraka akanikisi Mdomoni.
KWa msaada wa shemeji nilipaki kila kilichokuwa changu, alinipatia kiasi cha Pesa ambayo ingenisaidia kwenye safari yangu lakini pia kwenye shughuli nzima ya Mazishi.
********
Hatimaye ni mwezi mmoja sasa umeisha yangu nimzike Mwaisa wangu, ni Kijana ambaye nilizoea sana kucheza nae, na kufanya nae kila kitu Kama Mdogo wangu, Sawa alikuwa tofauti na watoto wengine lakini alikuwa ni zaidi ya upendo kwangu.
KWa safari hii Bwana wazazi wangu walinipa kila aina ya baraka kwaajili ya kwenda mjini ki tafuta maisha, lakini pia niliwaambia Kuwa sitaenda Tena kufanya kazi kwa da tusa kwani nimepata kazi sehemu nyingine.
Safari yangu ya kurudi dar es salam ikaanza, safari hii nilikuwa nikiwasiliana na shemeji na sikuwa nikimuita Kama kama ambavyo nilizoea tulishaanza kuitaba mpenzi, Mara babe na wakati mwingine mume.
Niliweza kufika dar es salama na jafeth Kama kawaida akaja kunipokea, safari hii Mimi na yeye tuliishia kwenye hotel Fulani hivi ya kawaida hapa mjini.
“Nilikuwa nikikusubili sana mpenzi “
Alizungumza shemeji jafeth.
Ouk my zangu Kuanzia sasa huyu ni wa kwetu Sawa jamani 😂🙌 hakuna cha shemeji au kaka, not Mwendo wa mume na babe tu.
“Mimi pia mume wangu kipenzi, nilikuwa naona nachelewa kuja kulala kwenye kifua chako “
Nilizungumza kwa mahaba lakini sasa rafudhi yangu ya kinyakyusa ndio iliniangusha 😂🙌 anyway kikubwa tupo penzini, penzi Tunalo na tunatamba nalo.
“KWa hiyo nikuogeshe ??”
Jafeth aliniuliza.
“Yaaah babe mi siwezu kuoga Mwenyewe na wewe ukiwa umekaa hapo”
Nilijibu kwa kudeka.
Iko hivi, sio kwamba nimeingia kwenye mapenzi na shemeji kwakuwa nampenda hapana, hii ni plan yangu kuhakikisha Kuwa da tusa anaumia lakini pia nilitaka kumuona tusa anakosa Furaha maisha yake yote.
“Nitakufanya uwe mchungu kwenye maisha ya da tusa “
Nilizungumza kimoyo moyo.
Basi Mimi na my wangu tukaingia bafuni na kwenda kuoga, hatukuishai kuoga Bwana, tukapeana kimoja cha wima kisha tukarudi chumbani na kuendelea na mtililiko wa Mechi zingine 😂🙌 kila mtu Acheze mechi zake kudadeki.
Rasmi sasa Mimi na shemeji jafeth tukaingia kwenye mapenzi.
Baada ya muda niliweza kupangishiwa Nyumba nzima.
Utaratibu ulikuwa ni kwamba, hakuna kulala kwangu, Yaani anashinda kwangu lakini kulala ni kwa mkewe.
Walahi nilianza kupendeza sana, nilianza kubwa mavazi ya kısasa, Kunukia ndio usiseme.
KWa upande wa Nyumbani Bwana, nilihakikisha Kuwa wanaapata maitaji Yao muhimu yote na nashukuru Kuwa niliweza kusema tabasamu kwenye Nyuso za watu wangu wa Karibu Yaani wazazi wangu.
Miezi kadhaa ilikatika uku Mimi na shemeji jafeth tukiangaika kupata Mtoto, Mimi nilikuwa ni mtu wa kupima Mimba kila iitwapo Leo lakini ola ola.
Siku hiyo nikiwa zangu jikoni namuandalia my wangu chakula, niliweza kujisikia vibaya sana na pasi na kutalajia nikajikuta nikianza kutapika hovyo hovyo.
My wangu akanichukua na kuniwaisha hospital.
“Hongereni sana jamani, Piya wewe ni mjamzito “
Nyieeeeeeh Ebu sikilizeni kwanza, niwekeeeni kuna nazi hapa nimkunie my wangu, jafeth wangu ameweza halafu ameweza Tena, Yaani Kama ni mchezo wa kumuumiza da tusa ndio Kwanza umeanza.
Majila ya jioni, baada ya kutoka hospital, jafeth alijiandaa na kutoka kuondoka kwa sauti ya kudeka nikazungumza.
“KWa hiyo utaniacha mama wa Mtoto wako nilale Mwenyewe Leo ??”
Jafeth aliniangalia kisha akajibu.
“Lazima nirudi Nyumbani, sitaki Linda agundue Kuwa Nina Nyumba ndogo”
Hapo niliangalia tumbo langu na kuanza kupapasa na kuzungumza.
“Daddy ataki kulala na sisi “
Ila wa mama jamaani. 😂🙌.
Walahi jafeth alishindwa kutoboa na kwa Mara ya kwanza akalala nje ya Nyumba yake, Yaani Akalala na Mimi usiku kucha.
TUSA JIPANGE MAMA PIYA NIPO NA SIRAHA ZOTE HAKUNA SEHEMU UTATOBOA 😂😂.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote