PILOT NIACHIE NIMEKOMA JAMANI
MTUNZI:BABY SMILE
EP 1.
Mwenzenu yamenikuta leo, mimi ni mhudumu wa ndege, hii kazi niliipambania mno, ili tu nimkwepe mama angu aliekuwa anataka kuniozesha, kisa anaona siolewi kila siku yeye anachangia watu, anataka na yeye afanye shughuri na hana mtoto mwingine zaidi yangu, nikaona niache biashara yangu ya mitumba nitafute ajira niliyosomea ili nisiwe na onana nae mara kwa mara, nilipata kazi na hii ilikuwa ruti yangu ya kwanza, lakini haikuchukua muda tukarudi tena, ni kama wiki tatu tu, nikaona ni bora nichukue room nisiende kwanza nyumbani, kwa kuwa hapa tutakuwa na siku tatu tu, ya nne tunaondoka, nitaenda nyumbani awam nyingine, nilichukua chumba kwa siri sana nisionekane, lakini wakati nimechukua naingia, namuona pia Pilot wangu nae anaingia chumba jirani na changu, akanishangaa, lakini hakuuliza, baada ya muda kuna mhudum akasema naitwa na yule pilot nikashangaa naitwa🤔....
Nilitii nikaenda akaomba nimsaidie kwenda kununua kitu dukani yeye hayuko sawa, hawezi kutoka, nilitamani kulia, angejua mwenzie nimejificha angenihurumia tu, alinipa pesa ety nikamnunulie nguo, hana nguo za ziada alizonazo ni chafu, na hana ratiba ya kwenda kwake, nilitamani ata anipe tu nimfulie ila sikuwa na jeuri ya kuongea kabisa, nilitoka, mpaka maduka ya kiume uku najificha uso wangu, nilipewa card ya benk sijui alijiamini nini uyu mwamba kunipa card yake aisee, nilitoa pesa aliyonambia...
Nikaingia kuchagua nguo, nilikuwa mtaalam wa fashion, coz nilishafanya biashara ya nguo hivyo kwenye kuchagua nguo mimi ni moto wa kuotea mbali, nilichagua pamba haswaa, nikageuza na Bolt mpaka hotel, nimefika moja kwa moja mpaka chumba cha Pilot Amir
Nikampatia card yake na nguo, apo nishampiga ganji, nguo anazochukulia 80, mimi nimechukuria elf 45, kwa hio kwenye kila nguo nimepiga pesa yakutosha tu, na nguo nimechukua OG, alifurahi nimechagua rangi nzuri mno, akasema atakuwa ananiagiza mimi kwenye nguo yeye hawezi huwa anateseka sana kuchagua nguo, ndio maana ananunua mashati meupe tu...
Nilicheka nakumwambia asijari ngoja nimpishe ajaribishie then atanambia kama kuna tatizo lolote, tukaelewana, nikawa natoka nyie nyie nafungua tu hivi mlango, nakutana na timu, kuna mbibi na walinzi, na kucheki nyuma mama angu nyie nilihisi kupaa, nikachanganyikiwa, nikataka kufunga mlango nikimbie kujificha, ila nilikuwa nimeshacherewa, walinzi walinishika nikarudishwa ndani na kumkuta Pilot T, ametoa shart yuko kifua wazi, yeye mwenyewe kwanza akashtuka...
" Bibi nini hiki tena, muda huo na mimi namwambia mama mbona umekuja huku? " Kwa hio Alice hapa ndio kazini ee? Mama sio hivyo hujanielewa twende nikakueleweshe, Bibi ake Pilot akazuia hapa tutaelewana hapa hapa hakuna cha kwenda kuelewana pembeni, kwa sababu tumewakuteni pamoja, " Bibi hujaelewa muache aende mtoto wa watu, " Amir naona umenisahau, sasa ni hivi mama wa bint si yuko hapa ee?..
Kupata mwendelezo bonyeza link hii hapa juu au chini ukasome yote hadi mwisho kwa buku tu...
Itaendelea...💥
PILOT NIACHIE NIMEKOMA JAMANI
MTUNZI:BABY SMILE
EP 2.
Bibi unataka kufanya nini? Nyie kumbe Pilot nae alikuwa na mtihani kama wangu, na aliogopa kurudi kwake kwa sababu tu ya kelele za kuoa, sasa Bibi yake akataka kutuozesha apo apo, mama nae akaunga mkono, tukaanza kujitetea mimi mkristo mwenzangu mwislam lakini haikusaidia mama angu yuko kusema mwanamke hana dini, nilianza kulia naomba watuelewe, lakini haikusaidia, Pilot Amir akamuomba bibi yake sana, lakini bibi akatishia kujiua ikabidi, Amir anibembeleze tu nikubari, nyie nyie nilisrimishwa kama utani, na ndoa ikapita siku hio hio, wakapanga kufanya sherehe baada ya sisi kurudi hio safari yetu ya kikazi, apo nikama mwezi mmoja tu...
Tuliachwa kwenye room wenyewe kila mtu anastress yake watu atujuani vizuri yani, mmh nilimuomba nikalale kwenye chumba changu akasema, ata usijisumbue nina uhakika utarudishwa tu, wewe lala tu umu umu apo nje hapawezi kosa walinzi wa bibi, na hata iko chumba chako wahudumu watakuwa washakiuza kwa mteja mwingine, kwa sababu wameshuhudia umeozeshwa kwangu wanauhakika hutokitumia, na kama utaleta shida kama walivyowaleta kutuozesha watakushitakia, namjua bibi yangu vizuri, awezi ondoka bila kuacha maelekezo kwa watu wake, na hawa wafanyakazi..
Nilichoka aisee, Amir aliniambia nilale kitandani yeye atalala kwenye kochi, nilimtizama nikimcheki ni mtoto wa kishua sio kama mimi nishazoea shida, nikamwambia wewe lala kitandani mimi nitalala kwenye kochi, kwanza mimi mfupi naenea hapo, wewe ni mrefu apo utaumia, aligoma tukarumbana mpaka nikaamua kunyamaza na kutumia vitendo, kwa sababu alikuwa hajakaa kwenye kochi nikawahi kwenye kochi, nayeye akawa amenishtukia kuwa naenda kwenye sofa, akakimbia kuniwahi, bahati mbaya tukagongana, akawa amenishika pabaya bila kujua,alitoa mkono haraka kama kapigwa shot tukajikuta tunaoneana aibu tu...
Akawa anashindwa ata kunitizama, na mimi ndio kabisa ikabidi nimuache alale anapopataka make tukiendelea hivi yanaweza kutokea mengine zaidi, lakini wakati naondoka kumbe kakalia nguo yangu nikajikuta nimedodokea tena kwa Amir, tena nimekaria sehemu hatali na inaonekana kabisa imevimba, inapumua mno...
Kupata mwendelezo bonyeza link hii hapa juu ukasome yote hadi mwisho...
Itaendelea...💥
PILOT NIACHIE NIMEKOMA JAMANI
MTUNZI:BABY SMILE
EP 3.
Nilishtuka nikainuka lakini nguo bado ilikuwa imekaliwa, ilibidi aitoe, uku anaona aibu, nikakimbia kwanza kuoga, nikaja kulala, nguo zangu kwenye kile chumba zililetwa usiku huo huo mizigo yote nikaletewa, Amir aliipokea mimi nilikuwa nishalala, kesho yake , nikapelekwa kwa Amir nyie nyie kuna watu wanaishi afu kuna kina sisi sasa tunasindikiza tu...
Mama nae akaleta kabisa na mizigo yangu kutoka nyumbani yaani ni kama alikuwa amenichoka jamani😭, nilichukia, nikapewa muda wa kuongea nae pembeni nilimlalamikia mno, alijitetea nakusema alifanya hivyo kwa sababu ameshafatilia kijana hana tatizo ni sehemu salama hajui yeye atakufa lini sina ndugu anatamani kuniacha sehemu salama, nilimshangaa kwa nini anaongelea kufa anaijua kesho yake?...
Vipi kama nitatangulia mimi hivi mama angu anashida gani jamani 🙌, alikuwa na maelezo ya ajabu ajabu tu, ata sikumuelewa, aliondoka jioni yake na kuniaga kabisa make naenda kazini, nilimpa na pesa ya matumizi akadai bado anapesa nikamwambia tu, atunze hizo zinaweza kutusaidia ata siku nyingine,alipokea nilijikuta nasikia tu maumivu wakati mama angu anaondoka nikaanza kulia, Bibi yake Amir alikuwa na huruma jamani, alianza kunibembeleza mpaka nikapitiwa usingizi...
Nimekuja kuamka naitwa nikale, nafika vyakula walivyopika mimi kwa kazi yangu, sitakiwi kutumia inaweza kupelekea nikaongezeka uzito, na sitakiwi kunenepa, wala kuongezeka uzito kuna kiwango cha uzito sitakuwi kuvusha...
Ilibidi niandaliwe matunda tu, Bibi alianza kusema hio kazi itabidi nitafute nyingine, nilitabasamu tu, chumba cha Amir nikikubwa sana na anasofa ambalo anaweza lifanya kitanda niyeye tu...
Leo tulilala bila shida, tofauti na jana, Amir aliteseka ameamka shingo inauma, kulikucha tukaamka kujiandaa kwenda kazini, lakini tukaombwa kuomba ruhusa ili mimi nianze kufundishwa dini, lakini pia tupate mapumziko mazuri kwa ajiri ya ndoa, Amir alikubari, tukaondoka apo akuna alieongea hii ndoa inakuwaje yaani tunaishije, tulikuwa kimya tumefika kazini kila mtu bize na kitengo chake kama vile hatujuani...
Kazini kila mtu aliishi chumba chake na maisha yake, japo matumizi Amir alikuwa anatoa, kila siku alikuwa ananitumia pesa ya matumizi,na kunijulia hali, ila kulala kila mtu kivyake, siku moja mkurugenzi kaja akasema kapokea ujumbe kutoka kwa bibi, wote tukashtuka afu apo ni mbele ya wafanyakazi wote wa kampuni...
Kupata mwendelezo bonyeza link hii hapa juu au chini ukasome yote hadi mwisho...
Itaendelea....💥
PILOT NIACHIE NIMEKOMA JAMANI
MTUNZI:BABY SMILE
EP 4.
Tulitizamana tukiwa na hofu, hatukutaka tujulikane,zawadi yangu itawafikieni na tutatuma wawakilishi kwa sasa muendelee na kazi mwezi ujao nitawapa likizo ya miezi miwili,mkafurahie ndoa yenu, tulishukuru Mungu hajafafanua vizuri kwa hio bado watu hawajajua kama ni mimi ila kwa Amir ashajulikana ameoa, na washahisi kaoa hapa hapa, watu wakawa bize kupekenyua lakini kujua ilikuwa ngumu, make na sisi tuliongeza umakini, huwezi tukuta pamoja...
Ni tunamalizana kwenye simu, kimbembe wiki iliyofuata mkurugenzi akagawa chumba changu na kuniweka room moja na Amir, apo tulichoka itakuwaje bahati nzuri, tulitakiwa siku hio hio kusafiri ila bajet ya kulala huko tuendako ni ya room moja, hatukuwa na ujanja tulijua kabisa hii ni kazi ya bibi na sio mtu mwingine, siku io tulivyofika na kukuta hali ilivyo, ilibidi Amir aniulize kama niko sawa kulala nae room moja, niliona ni mtihani ata sijamzoea yani🫣, nikamuomba kama hatojali anichukulie room mimi, alikubari akasema nisijali ndio maana kaniuliza...
Alilipia room nyingine, leo kachoka sana akaomba nimsaidie kuweka mambo yake sawa, ata kuagiza tu chakula alikuwa kachoka mno, ilibidi niagize nimuandalie nguo zake vizuri akiamka ni kuvaa tu, chakula kililetwa cha watu wawili, kwa maelekezo ya mkurugenzi, apo najificha kama bangi wenzangu wasijue,nilijitahidi kuficha mno, tulikula nikatoka kwenda kulala kwangu, asubuhi tumeamka, tukajuliana hali, kama kawaida nikatumiwa pesa ya matumizi, na ata hayo matumizi kwanza sikuwa nayo, kila kitu kilikuwepo, nilijikuta nakuwa na pesa za ziada za kutisha, sikutaka kuchezea make hali ya nyumbani kwetu naijua vizuri mno...
Nilijiandaa tukaondoka, Amir alinishukuru sana nimemsaidia mno angekuwa mwenyewe kuna vitu asingeweza kufanya ingebidi amlipe mtu au aachane navyo, nilimjibu tu ni wajibu wangu kwa sasa kama mke kuhakikisha kila kitu kiko sawa, nilimuona wakati tunachart kwa mbali kasoma sms akatabasamu, kisha akanijibu, na emoj ya kumbato, niliirudisha pia...
Tulikuwa na furaha mno, kuchart kwenye simu, kuna muda tulichart ata masaa matatu, ila kuongea kila mtu alikuwa anakwepa sana, na hata tukikutana tulikuwa hatuna story sana kama inavyokuwa kwenye sms, maisha yalienderea mpaka zikawa zimebaki kama wiki moja tu na siku 2 siku ya sherehe ya ndoa ifike...
Kupata mwendelezo bonyeza link hii hapa juu au chini ukasome yote hadi mwisho...
Itaendelea....💥
PILOT NIACHIE NIMEKOMA JAMANI
MTUNZI:BABY SMILE
EP 5.
Siku zilikuwa zinakimbia jamani, yani zilitufanya tukawa na pressure mno, Amir alinambia Bibi yuko huku kwa ajili ya mavazi yetu ya harusi, tunapaswa kwenda kuonana nae, tulikubaliana mida ipi tuondoke, tuliondoka kila mtu kivyake, tukakutania mbele, bibi alifurahi mno kutuona, akanambia napaswa kubadili mavazi yangu ya kazi na hata ya nyumbani, nilikubari...
Tukaanza kutafuta nguo, nilikuwa na mwili wa nguo hivyo kwangu haikuwa na shida kabisa, mwenzangu pia alipata zilikuwa nzuri na za gharama mno,nguo ya pili pia nilipata, kila kitu kiliwekwa sawa bibi akaondoka navyo, tukabaki wenyewe sasa, Amir alionekana ni kama kuna jambo anawaza sana, nilimuuliza kwa sms tukiwa njiani, uko sawa? Naona ni kama unamawazo...
Alinitizama kwanza kabla ya kujibu sms,ndio akajibu uko vzr sana kumsoma mtu, Alice mimi siko sawa, kuna mambo natafakari sana, naomba usiniulize kwa sasa ila lazima nitakwambia usijari,lakini sijakipenda kile kiatu chako mlichochagua, unaonaje turudi nikuchagulie kingine? Nilishangaa make kiatu mimi nilikielewa mno, kilikuwa kizuri sio poa...
Ilibidi tu nikubali, make mwanaume ndo hajakipenda, tulirudi wenyewe, kumbe bibi alikuwa hajaondoka, akatudaka, ikabidi tuseme ukweli, bibi akafurahi akasema tuchague ila hiki harudishi, yeye kakipenda hiki, tulianza upya kutafuta kiatu, mpaka akapata anachokitaka, kilikuwa kizuri pia, tulilipia, akaulizwa kingine kipi hajakipenda, ikabidi tucheke tu...
Alisema sasa apo kila kitu kiko sawa, ila gauni la pili, kama hajalielewa ivi, Bibi alicheka nakusema bwana harusi kachangamka huyu, dah tulianza kutafuta tena gauni jingine, yani ilikuwa mtihani sio kidogo, badae tulienda kupata chakula, Amir nikama alimtumia ujumbe bibi, na mimi akaniaga kwa sms kuna kitu anaenda kuchukua atanipitia nikae na bibi, sikuwa na shida nilimruhusu, aliondoka, bibi akaanza kunidadisi, kama tuko sawa, nilikubali hakuna tatizo lolote...
Bibi alianza kunishauri, kazi yangu ni ngumu sana upande wa ndoa, hata kama ninafanya kazi na mme wangu, lakini sio salama kwa ndoa, " sikuzuii kufanya kazi mke mwenzangu ila nakupa tu kama ushauri, ujiandae mapema kazi yako haitaki mjamzito, wala mnene, na kg pia zinazingatiwa na age badae inaweza kuwa tatizo, umeshawaza itakuwaje? Niliwaza nikaona hii kitu anayosema hakosei iko sawa kabisa, nilimshukuru bibi nakumwambia nina jipanga, nikishakuwa tayari nitaacha kazi ili nifungue biashara, bibi alifurahi na kuahidi atanisaport nisisite kumjulisha nikisha kuwa tayari...
Usijali Bibi, kwa sasa siwezi kukatisha mkataba, itakuwa ni gharama sana, nitasubiri tu mkataba uishe muda huo najipanga, niliweka mkataba wa mwaka na nusu bado mwaka mmoja tu mkataba utaisha, nitafungua biashara, Bibi alifurahi na kunishukuru, akawa ananipa mawaidha na kunipa mbinu za maana kabisa...
Muda ulikuwa unazidi kwenda Amir harudi yalipita masaaa 4 sasa adi giza lilianza kuingia, ikabidi tumpigie, akawa hapatikani kabisa,tulianza kupata hofu, mpaka saa 2 na nusu usiku hajafika, Bibi alianza kupata wasiwasi, hata mimi uoga ulianza kunishika, wakati tunahangaika tunampataje,, simu yangu ikaita kucheki ni Amir, nikapokea ajasema kashafika kazini aliona kacherewa na simu imezima akajua nitakuwa nimesharudi, aisee nilikasilika sikujibu chochote nilikata tu simu, nikampa taarifa bibi, bibi hakufurahi, alimpigia mjukuu wake simu pale pale nakumgombeza, usiku huu anamuacha mwanamke, katikati ya mji, hana ata aibu, kwa hil anarudije vipi kuhusu yeye...
Amir aliomba msamaha, akaja kunichukua, tukaanza kwanza kumpeleka bibi hotel, ndo tukaanza kurudi kazini, njiani sikuwa sawa, bado nilikuwa na hasira na mashaka na Amir, alinitumia sms, lakini hata kuifungua tu sikufungua, ikabidi atumie mdomo, nisamehe Alice najua nimekukwaza lakini sikupanga kuchelewa, naomba usinune basi, nahitaji muda wako leo, ukiwa kwenye hali hii nitawezaje kuwa na wewe?, kuna mambo nahitaji tuyaweke sawa sasa kama wanandoa...
Sikujibu chochote, nilianza kuhisi hatari tu, Amir alivyoita sijibu aliamua kunikumbatia ili kuchukua utulivu, nisifikirie mambo mengine, nirudishe akiri kwake, niliigiza tu niko sawa niuchovu tu, Amir alijitoa kwenye kumbato, akanitizama nakugundua kabisa, kuna kitu hakiko sawa,alitulia tufike, akaomba nimfate chumbani kwake, nikamwambia leo nimechoka sana, kama anajambo, tuliongee tu kwa simu, alijibu, haliongeleki kwa simu ndio maana kaniita chumbani kwake...
Nilikubari kishingo upande tukaingia, alinitizama sana nakuniuliza, "Alice unaweza kunisamehe mke wangu?
Nilimtizama, afu nikashusha macho nikamwambia, mimi sina hasira nae, " Alice huwezi nidanganya nakujua vizuri, niambie basi nifanye nini ili unisamehe, siwezi kulala na amani kama utaendelea kuninunia...
Nilitaka kuandaa kitu cha special kwetu, hivyo nilihitaji muda, toka tumeoana, tunaishi tu kama mtu na dada ake, nahitaji tupande stage sasa, nilishtuka yani kivipi? Alitabasamu, nakusema, kwanza naomba unipe ruhusa nitoke kwa siku 4 tu, ila hii usimwambie Bibi, lakini pia leo nakuhutaji kama mme...
Kupata mwendelezo bonyeza link hii hapa juu au chini ukasome yote hadi mwisho kwa buku tu....
Itaendelea....💥
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote