PISI KALI YA CHUGA

book cover og

Utangulizi

PISI KALI YA CHUGA 1
HUSQER BALTAZAR
Sijui nicheke au nilie, yaan na uchuga girl wangu wote, kujifanya kote mgumu hatimae nimekutana na kijana wa kitanga akanifanya nikawa mrs romantic, siamini mimi ambae sikuwa najali kabisa kuhusu wanaume, na kupigana na ugomvi ulikuwa ni sehemu wa maisha yangu, magauni na madera yalikuwa kama dhambi kubwa kwangu, leo hii mimi navaa maabaya na sendo badala ya allstar na supra, nimeacha kuvaa mabuti navaa viatu vya juu juu, yaan mtu yoyote Yule ambae anamfahamu Samira hawezi kudhani kama naweza kubadilika na kuwa mwanamke ambae naweza kuwa ndoto ya mwanaume anaetaka kuoa, ila mume wangu sabry amenibadilisha kwa kiwango kikubwa mpaka mimi mwenyewe sijiamini, ingawa ka uhuni hakawezi kuisha moja kwa moja…

Basi bana ngoja niwasimulie, kipindi hicho nilikuwa nimemaliza kidato cha nne, nilikuwa nasoma shule ya secondary ya ngarenaro, mwaka ambao nilimaliza kulikuwa na matukio mengi sana, yaan tulisumbua sana walimu wakati ule, na mimi ndio nilikuwa kiongozi wa ukorofi na ubabe, yaan tukitaka kwenda nyumban hakuna wa kutuzuia, sio mwalimu wala mlinzi, labda kama hajipendi, kama ni kusimamishwa shule nimeshasimamishwa sana, siongei kama sifa ila ubabe na ujeuri wangu ukanizalia divison zero kwenye mitihani yangu ya kidato cha nne…

Sasa siku hio nilikuwa nimeamka asubuh, na jana yake ilikuwa nimepokea matokeo yangu ambapo wazaz wangu walinisema sana, kwamba pesa zao za nauli na za kula shule bora hata wangewekeza kwenyue kilimo huenda wangekuwa matajiri kuliko kunisomesha mimi, yaan hata sikulala, ila kama mnavyojua sisi wadudu hatulii lii kizembe, hivyo nikawa najiambia tu maneno ya kanga hayo, kanga ikichanika hayana thamani, ila hapo naongea mwenyewe maana mzee wangu ni zaidi ya gaidi, alishanilaza ndani mara mbili, hivyo siwezag kumchezea uhuni wangu ni mtaani ila sio nyumbani kwa wazee wangu, maana nitapigwa niuwawe…

Sasa nimeamka asubuh naenda zangu kununua mihogo nile, nikapishana na wanaume watano, walikuwa wageni pale mtaani, kuna mmoja akasema “ aiseee huyu demu ni mkali sana yaan, ila tatizo lake anajikuta mdudu sana, mwingine akadakia “ mwanamke wa namna hii hata akinikalia uchi au akinishika m*oo haisimami…

Nilimind sio mchezo, ila nikajiambia ngoja niende nirudi atanijua mimi ni nani, basi nikanunua mihogo wakati narudi nikaenda moja kwa moja kwa Yule mwanaume ambae alisema hata nikishika mtambo wake hausimami, nikaushika sasa…
Hakuna alietegemea, na Yule mwanaume alitoa macho na hapo hapo akasimamisha, wenzake wakaanza kumcheka, kisha nikamuambia “ sio kila manzi unaemuona unatakiwa kumletea maneno ya kanga mzee, mbona nimeishika imesimama, so kuwa na adabu, kisha huyo nikaondoka zake…

Yule mwanaume wakati ule ule alisimama na kuondoka akiwa na aibu za kutosha, mimi hata sikujali, na wala sikumfuatiliza kabisa, hapo kijiweni wenzake ni wanacheka balaa hawana mbavu, nikajua yameisha kumbe mwamba ameniweka kiporo bila kujua mimi ni chizi kiasi gani…

Basi siku zikapita nikawa nimeshasahau kabisa kama nilishawahi kufanya ujinga , maana nafanyaga matukio alafu hata siyazingatii naendelea na mambo yangu, siku moja pale mtaani kuna msela alikuwa anaoa, tukaalikwa kwenye harusi kama wacheza shoo, na kama mnavyojua miondoko ya kichuga ni mwendo wa mamong’oo mpaka majogoo, na nyimbo zetu ni zile zile…

Sasa pale ukumbini kukawekwa nyimbo moja inaitwa jogoo kichaa, mwaka huu ndio ilikuwa imetoka, yaan kila club ya arusha ilikuwa inapiga hio nyimbo, na kama una shughuli yako, ukiweka hio nyimbo ya jogoo kichaa unaonekana mjanja kweli, kama hamuikumbuki ngoja niwaimbie kidogo … “mii ndo jogoo kichaa aisee mii ndo jogoo kichaa, kanga ndembe ndembe na suruali za kitambaa, naruka kimende mende kibata na kutambaa …….”
Basi tumecheza wee ukafika muda wa kula, nilikuwa nimepania hio minyama hatari nikaenda nikachukua zangu nyama choma, na ndizi za kutosha, na nilikuwa nashushiaga na viroba, sasa kabla sijaanza kula nikamuona mwanaume mmoja kachukua zake chips na mishkaki pale amekaa anakula, nikamsogelea kisha nikamuambia “ bila shaka wewe ni mwanaume wa dar..

Kumbe ndio Yule mwanaume ambae siku ile nilimshika nanii yake, nimeshasahau maskini..
“ kwani nikiwa mwanaume wa dar kuna shida gani? Akaniuliza…
“ yaan mwanaume mzima unakula chips na vimishkaki kazi utaiweza kweli wewe, yaani mwanaume kama wewe akioa mke wake, nina uhakika kila siku atakuwa anapigiwa na wahuni, kaza kijana, nikasema huku nampiga piga bega kisha nikaondoka zangu…

Walikuwa wenzake pembeni, yaan walimcheka sana, mmoja kati ya wanaume waliokuwa karibu nae akasema “ huyu demu anashida na wewe, au anakutaka nini?, mpe shoo aamiini wewe ni kidume aache dharau..
Si akaropoka tena akajua simsikii na wakati nilikuwa nyuma yake, akasema “ huyu demu hata kama ikisimama nikiingiza inalala, kwanza mwanamke kama huyu si sawa na mwanuame mwenzako, hata nguvu ya kumkiss unakosa, unajikuta akikukiss badala ya kupata msisimko unapata hasira…

Yale maneno yakaingia kichwani kwangu, nikawa najiambia kuwa “ huyu mpuuzi hanijui huyu, ngoja tuone kama nikimkiss hatosisimka au anaongea tu, sijui nilikuwa najiamini maskini mimi, kumbe najisogeza mwenyewe kwenye mdomo wa mamba bila kujua…

Basi nikala zangu pale pole pole, nikawa namuomba mungu asiondoke mpaka nimalize kula, kweli nikamaliza kula nikaenda kutafuta ndizi mbivu ili nisinuke mdomo, na sikupiga viroba maana sikutaka kunuka mdomo na wakati nilikuwa nina zoezi pevu, na kujiamin kote huko sijawahi hata kumbusu mtu, na sijui hata watu wanabusiana vipi, yaani kiufupi hata mapenzi sijawahi kufanya ila ninavyojiamin sasa unaweza kudhani mtu kumbe marehemu…

Basi wakati huo alikuwa anatoka na marafiki zake wanaondoka zao, walikuwa wameshafika kwenye lango kuu la kutokea nje, nikamuona nikamfata nikamvuta kisha nikampiga busu moja matata kabisa, akabaki kaduwaa, akawa kama anataka lile busu liendelee ila wenzake walikuwa wengi hivyo kuna namba aliona aibu, maana mpaka alinishika kiuno akawa anataka kuendeleza mapambano ila hayo mambo ya kuendeleza mapambano hayakuwa mambo yangu hivyo nikamuachia kisha nikamuambia “ mbona kama nimekusisimua, hadi nanii yako naona kabisa imesimama, ila wanaume sijui kwanini mnapenda sana kuropoka, hizo sio sifa za wanaume bana, unakuwa kama pisi kali maana nilisikia unasema hata nikikubusu usisimki, bro achana na mademu wa chuga wengi wao hawana akili acha kuropoka ropoka, kisha nikaondoka zangu hapo nimevaa maviatu makubwa kuliko umri wangu, sharti kubwa kama dera alafu nadunda tu najifanya sijali lolote lile…

Yule mwanaume akabaki amejishikilia mdomo wake huku akiwa ananiangalia, hapo wenzake wanacheka balaa, na namna ambavyo walikuwa wanacheka nilikuwa najiona mwamba balaa, kumbe dawa yangu ipo jikoni inachemka na sijui nitainywa lini,….
ITAENDELEA…


PISI KALI YA CHUGA 2
HUSQER BALTAZAR
Basi nikaenda zangu nyumban na maisha yangu yakawa yanaendelea kawaida, na huwa nina kawaida ya kutozingatia mambo, hivyo mambo yote ambayo nilikuwa nayafanya sikuwa hata nakumbuka maana nilikuwa na matukio mengi sana, na huo muda wa kuyakumbuka ndio sikuwa nao kabisa…

Siku moja tukakodiw tena kwenda kucheza kwenye sherehe, maana tulikuwa wacheza shoo maatrufu mkoani arusha, nilikuwa mweupe, nilikuwa na umbo flani hivi matata, ila nilikuwa navaa kihuni sana kiasi kwamba hata lile umbo langu maridadi na uzuri wangu haukuwa unaonekana kabisa, na kwanza kubana bana pua, na kuongea kama demu ndio mambo nisiokuwa nayafagiliaga kabisa yaan, ni mwendo wa ugumu mwanzo mwisho…

Basi tumeenda tumecheza shoo tumemaliza nikashangaa kuna kijana ameniita, nilipomuangalia nilikuwa kama namjua flani hivi, ila sikuwa nakumbuka hata nimemuona wapi, maana huwa nakutana na wanaume wengi kwenye matukio mengi tofauti tofauti…

“ unaitwa nani? Akaniuliza Yule kijana nikajua huyu mpuuzi anataka kunitongoza…
“ naitwa jiwe, au unaweza kuniita mwamba, kuna kingine unataka dingi lai, nikamjibu…
“ mbona wewe ni mwanamke mrembo sana kwanini unaongea kihuni na unaishi maisha ya kihuni hivyo, embu nambie siku mwanaume akija kukuoa utazaa watoto wa aina gani? Akawa anaongea Yule kijana na alikuwa anaongea kistaarabu sana, mpaka nikawa nashangaa…

“ heee kama utanizalisha wewe fresh tu, ila mimi mambo ya kuzaa kwanza siwazi hata kidogo, alafu kama hauna mambo ya maana ya kunambia naomba niyeyuke mara moja, nikasema…
“ nina maongezi mengi na wewe naomba muda wako, akaendelea kusema ..
“ unataka kunena na mimi au unataka kunihubiria, bro unakipaji kikubwa sana cha kukemea mapepo, nenda katafute kanisa uhubirie achana na mimi, na niliropoka tu kuwa unataka nizae na mwanaume mwenyewe unaonekana mla chips zege, sio kila demu wa kusemeshwa, utakuja kuchomwa bisi bisi za mbavu uone watu wa baya, nikasema kisha huyo nikasepa zngu, ila Yule mwanaume alikuwa ananiangalia tu huku anatabasamu, nilikuwa namshangaa ila nikawa namuona kama mwenda wazimu …

Basi maisha ya kitaa ni magumu kinoma, nikaamua kutafuta kazi, ila maswala ya kufanya kazi za ndani sikuwa naweza, yaan zile kazi za kike nilikuwa naona kama kujishusha brand hivyo nikaona nikawe zangu kondakta wa tengeru, hapo wazaz wangu walikuw wanajua nafanya kazi ila hawakuwa wanajua nafanya kazi gani, nikaona kama kukaa nyumbani ni kujidhalilisha nikamuambia bimdashi kuwa nataka nikapangishe, akaenda kumfikishia mzee, na kama mnavyojua hizi familia zetu, hawakuwa wanataka nikapange kwa kuwa mimi ni mtoto wa kike..

Sio siri niliwamind kinyama, maana nilikuwa najiona kama najiweza kwa kila kitu, nilikuwa naona kama kukaa nyumbani mwamba kama mimi sio poa, ni udada na nilikuwa najikuta mdudu balaa, sasa siku moja niko mihangaikoni, nikampandisha baba yangu kwenye kidala bila kujua bana, sasa watu wamejaa na mdingi alikuwa amekaa siti ya nyuma, na sio mimi ambae nilikuwa napakia abiria, sasa wakati wa kudai nauli ndio nakutana na mzee, alinikata jicho ila hakusema lolote, sio siri nilipomuona niliogopa kinyama, akaenda anapoenda akajua tu mahesabu jioni…

Kweli usiku nafika nyumban namkuta mzee ameshafika na amekaa ukumbini na mama kana kwamba walikuwa wananisubiri nifike…
“ samira embu eleza leo mbele ya kila mtu huwa unakosa nini nyumbani mpaka unaamua kufanya kazi unayoifanya, kwa sababu wewe ni bint wa kiislamu unavaa unavyuovaa tumeongea sana, tumepiga sana imeshindikana ukaona haitoshi unaenda kufanya kazi ya ukonda ili uoneshe watu kuwa wazaz wako wameshindwa kukule kama mtoto wa kike na wamekufanya dume si ndio , kweli mwanangu kati ya kazi zote ukaona kabisa kazi inayokufaa zaidi ni ukondakta kweli mwanangu, akasema baba yangu kwa ukali..

Namjua huyu mzee, yaan ukaksi huwa nawafanyia watu wengine ila sio baba yangu, maana nitapigwa mpaka nisahau jinsia yangu, basi baada ya kuniuliza nikakaa kimya, maana sikuwa nimejipanga kwa majibu yoyote yale, mama yangu akaniangalia sana, kisha akasimama na kuingia zake chumbani nikajua hapa tayari nimeshayabananga, ila nikawa najiambia jamani kazi si kazi, kwani cha msingi si nina ingiza hela, iwe ukondakta au iwe kazi nyingine yoyote ile kwani kuna shida gani, nikawa najiambia…

Baba yangu nae akaniangalia kisha akasimama na kuingia chumban kwake, nikaona hawajanisema sana huenda mambo yameshaisha, ila wakati ambapo naamka asubuh nikashangaa mama yangu ameshnipangia nguo kwenye begi, hakuw amepanga kabisa nguo zangu ambazo nilizoea kuvaa, sijui ni lini nilinunuliwa maabaya na magauni na mitandio, kisha akanikabidhi na kusema “ wewe ni binti wa kiislamu ni marufuku kuvaa ujinga wako, na ole wako uwe unatoka hapa nyumban na nguo tunazozitaka alafu ukifika huko unapoenda uje uvae mavazi yako ya kihuni, na kuanzia leo ni marufuku kutoka nje bila sababu za msingi, kama ni dukani nitaenda mimi, unatakiwa uanze kuishi kama mwanamke, na sio kuishi kihuni kama unavyoishi utasema hauna wazazi…

Nilishangaa kwanini wanasema vile, na ukweli ni kwamba nilikasirika, ila kwakuwa sikuwa natakiwa kutoka nje ilikuwa nafuu, maana angalau sitaonekana nimekaa kimanzi manzi mimi…

Basi siku moja baba yangu alikuja na kunambia ameshanipatia kazi ya kufanya, nikawa namsikiliza kwa makini kutaka kujua natakiwa kufanya kazi gani…
“ nimeongea na shangazi yako Yule wa sakina amesema kazini kwao kuna nafasi za kazi na ameshakutafutia, hivyo utaanza kwenda kazini ila na mavazi ambayo wanayataka wao ila sio mavzi yangu ya kihuni, sasa baba hata hakuniambia ni kazi gani hio, na akanambia kuwa nitakuwa nakaa kazini huko huko kuna nyumba za wafanya kazi, hivyo nitakuwa narudi nyumban mwisho wa mwezi tu maana baba alikuwa anahisi labda mtaa ndio ulikuwa unaniharibu…

Basi nikaanza safari ya kwenda kwa shangazi yangu, yaan huyu shangazi yangu ni wale waislamu walioshika dini sana, hivyo nikaanza kufundishwa ibada na ni lazima sio ombi, na kuvaa stara ni lazima na mavazi ya kihuni kama nayapenda sana basi niyavalie chumbani kwangu nikiwa nataka kulala na sio mbele yake…

Basi nilikaa kwake sikumbili kesho yake akanambia kuwa tunaenda kazini, hapo maskini ya mungu sijui naenda kufanya kazi gani, kweli nikafika kwenye shule moja ilikuwa ni hizi shule binafsi, nikaambiwa kazi yangu ni kufanya usafi na shangazi yangu alikuwa mpishi pale…

Nilitamani kukataa kufanya hio kazi ila sikutaka kubishana na mtu nikakubali nila kishingo upande, nikawa najiambia kuwa nitakuwa navuruga kazi mpaka nihakikishe nafukuzwa, bora hata ningeenda kufanya kazi za ujenzi kuliko kufanya kazi za kinyonge kiasi kile, alafu mshahara ni laki na nusu, na wakati nikienda site kujenga Napata zangu elfu kumi na tano kwa siku, na ukondakta nilikuwa naondoka hadi na elfu kumi na mbili mpaka kumi na saba kwa siku…

Basi nikaanza kazi, nikasafisha siku hio madarasa, maana tulienda mapema sana, na baada ya hapo ndio nikaenda ofisini, kulikuwa na ofisi ya meneja wa shule, ile naingia tu kusafisha nikakutana na kijana, ni kama nilikuwa namfahamu, ila sikumfatiliza, ila nilipomuona nilimsalimia maana niliambiwa ni mtoto wa mwenye shule, maana mwenye shule huwa ni baba na mama yake alikuwa ameshafariki, ila kulikuwa na mama wa kambo, ambae walikuwa na wasiwasi kuwa anataka mali, ndio maana Yule kijana akawa anasimamia kila kitu..
Yule kijana aliponiona akatabasamu kisha akasema “ pisi kali ya chuga hatimae tumekutana tena, aliposema hivyo ndio nikaanza kuvuta kumbukumbu, kumbe ndio Yule mwanaume ambae nilimshika mashane yake na kuna siku nilimbusu hadharani, kwa mara ya kwanza nilijisikia aibu sana…
“ kumbe mashallah wewe ni bint wa kiislam na majuba unaweza kuvaa bana, ila uwe unapaka hata viwanja na vipoda basi uonekane kama mwanamke, maana umekaa kigumu kama unataka kupigana na ukuta…
“ kama unaniona nimekaa kigumu nifukuze kazi, huwa siwezi kukaa sehemu na wanaume wa laini kama wewe…
Aisee Yule kijana alisimama kisha akanisogelea na kunishika kiuno tukawa tunaangalia na kusema “ sasa upo kwenye milki yangu, usifikiri utanidhalilisha kama ulivyofanya hapo nyuma mimi kuanzia leo ndio nitaamua uishi vipi, kisha akachukua simu yake na kupiga sehemu huku akiwa amenishika, na kusema “ mansoor nimemuona mfanya kazi mpya, naomb huyu mumtoe kwenye majukum mengine atakuwa ananiangalia mimi na bibi yang u tu, na baada ya hapo akakata simu..
Na huyo mansoor alikuwa ndio kiongozi wa wafanyakazi wengine wote tofauti na waalimu, mara tukasikia sauti nyuma yetu inasema “ bora hata mjukuu wangu umeshapata mke, sasa muache kushikana shikana hivyo mfanye muoane, maana siunajua dini yetu haipendi zinaa, nilipigeuka kumtazama ni nani ambae alikuwa anaongea hivyo nikakutana na sura ya bibi wa kama miaka 80 akiwa anatabasamu kana kwamba dua zake zilikuwa zimeshapokelewa….
ITAENDELEA…


PISI KALI YA CHUGA 3
HUSQER BALTAZAR
“Njoo njoo njoo mjukuu wangu, huyu sudeys ni mkorofi sana njoo nikufundishe mambo ya kwetu, akawa anasema Yule bibi, ingawa nilikuwa natakiwa kufanya usafi ila nikaona nimfate tu, maana kukaa na huyu nyang’au sikuwa naweza maana nilijua lazima atafute sababu ya kunikera tu, na sikuwa nataka kuharibu siku yangu…

“ embu nambie mmekutana wapi na mjukuu wangu na je hakuwa anakuletea tabia zake za hovyo hovyo, maana mpaka ameamua kuja na wewe kazini ina maanisha amekukubali sana, maana kila siku namuambia aniletee mke mwenzangu nimuone hataki, ila leo nimewafuma, embu nambie mmekutana wapi?...
Nikaona sasa hichi kizaa zaa, bibi anaamin mambo ambayo hata hayapo, sasa anataka nimjibu nini huyu bibi, nikaanza kuchekecha ubongo, nikajua kabisa huyo mjukuu wake ni lazima atakuwa ananichukia sana, nikaona sasa niharibu nijifanye kama tuna mahusiano kweli, akiwa na hasira nikawa najiambia kuwa lazima atanifukuza kazi, maana hanipendi hivyo akisikia hizo habari lazima akasirike…

“ yaan bibi ni ztory ndefu sana, yaan huyu mjukuu wako tumekutana kita, kitaa kule ngarenaro ambapo alikuja kwa washkaji zake, akaniona nakatiza akanifata na kunisimamisha, ila siunajua sisi mademu sikugeuka, akaja akasimama mbele yangu akanambia anataka kunioa, nikashangaa katumwa nini, yaan anataka kunioa na hata hanijui, je kama mimi ni jini ataniweza kweli, nikagoma, maana mimi mwenyewe kama unavyoniona bado pisi ya kwenda na umri wangu bado upo upo tu, hivyo nikaanza maringo yangu, nikaanza kusema…

Yule bibi akatabasamu kisha akasema “ jamani kweli mungu mkubwa, nilikuwa napendaga sana watu wanaoongea kama wewe, jamani mjukuu wangu kapata bahati sana, maana wanasemaga wadada wa huku arusha hawawezag kusaliti mwanaume, shida yao ni ubabe tu, asante mungu, na naomba usije ukamsaliti mjukuu wangu, na kuhusu huo ubabe mimi ndio nitakuwa kungwi wako wakati mkitaka kuoana, nitahakikisha unakuwa mke bora sana kwa mjukuu wangu, maana mapenzi yamemuendesha sana, angalau sasa amepata mtu sahihi…

Nikawa namshangaa huyu bibi anaota ndoto za wapi hizo, yaan nilijua kuongea kwangu kihuni lamba kutamkwanza kumbe ndio namburudisha, nikaona sasa hichi kizaa zaa, ukisikia zile taarifa za kuanza kukubalika ukweni kabla mwanaume hajakupenda na wewe haujampenda ndio hizi, yaani mimi nije kuolewa na mwanaume mla chips, labda sio mimi, nikawa nawaza, utasema najua hata hao wanaume wala chips wanachangamoto gani na wakati hata kulala na mwanaume sijawahi…

Basi tukakaa na bibi mpaka saa saba, mara akaja mwana mama alikuwa amevaa juba ila yupo kama shangingi flani hivi, akaja na chakula chake akampa bibi, bibi akamuangalia kisha akasema “ ni mara ngapi nilishakuambia kuwa sitaki uniletee chakula chako kazini, na wala sitaki kukuona karibu yangu wala na mjukuu wangu hata mara moja, au umetuwekea sumu unataka tufe…
Yule mama akacheka kisha akapiga picha kile chakula nan a akachukua video fupi kisha kuna sehemu kama akawa anaituma kisha akawa anarecord na voice akawa anasema “ nipo hapa shuleni mume wangu kipenzi nimekuja kula na mama na kijana wetu, naomba na wewe ule si unajua wewe ndio nguzo yetu babaa, kazi njema mume wangu, kisha akatuma na baada ya hapo akamuangalia Yule bibi na kusema “ wewe mwenyewe unajua sina huo muda wa kuhangaika na mama mkwe kama wewe, ni kwamba mume wangu anataka nihakikishe umekula, ila kama hautaki kula chakula ambacho nimekipika siwezi kukulazimisha hata kidogo, kisha akabeba mahotpot yake akawa anaondoka zake…

Sijui ni kwanini nilijisikia vibaya sana Yule mwana mama alivyokuwa anaongea, nikasimama na kusem “ kama ulipika kwa ajili ya mama mkwe wako basi utakiacha hapa, na kama hicho chakula kina sumu tutawapa hata mbwa wale mamlai, ila hauondoki nacvho, usiwe unajifanya mnafki kiazi, kumuonesha mdingi kuwa unapenda familia yake kumbe wewe ni snichi asie kuwa na akili, nikasema kwa sauti ya kujiamini..

Yule mama alirudi na kuweka mahotpot yake mezani kisha akanifata na kusema “ unasema nini wewe bint unajua mimi ni nani…

Sikuwa hata na mja wa kubishana nae, nikaenda kufungua yale mahotpot nikakutana na kuku na ndizi za kukaanga na kachumbari, nikaanza kula, bibi akawa ananizuia akawa anasema “ usile anaweza kukuwekea sumu huyu shetani mjukuu wangu…

“ usijali bibi kama nikifa wewe utaenda kutoa ushahidi ila hakuna chakula ambacho kinaondoka hapa, nikasema huku nikiwa naendelea kula…
“ wewe kinyago nani kakupa ruhusa ya kula chakula changu, akafoka Yule mwanamke…
ITAENDELEA…

PISI KALI YUA CHUGA 4
HUSQER BALTAZAR
“ ulimletea mkwe wako, na anaonekana hakitaki nimeona nimsaidie kula mamaa, ila wewe mwanamke unajua kupika sio siri, nikawa nasema huku nakula, yule mama akaja akawa anataka kuniweka kibao, aisee nilimshika mkono nikaukunja na kumuambia “ mamaa usione wembamba wa reli treni inapita hapa, ukitaka kuingia kwenye historia za dunia kwa kupasuliwa na kabinti kadogo kama mimi jichanganye, mimi sio wala chips, yaan hapa unaponiona kinachonifanya nionekane mwanamke ni jinsia tu, ila nikisema nakupasua hautajua kama umepigwa na jiwe au mtu, maana ngumi yangu tofali, kibao mbao, potea mimi nile zangu, nikasema kwa kujiamin, na sijui kujiamini kote huko nilikuwa nakutoa wapi maskini, ila hata kama ni wewe ungemuacha mbibi wa watu anyanyaswe na mwanamke ambae hana mbele wala nyuma, na wakati wote huo bibi alikuwa amekaa kimya…

Yule mwanamke akaniangalia kisha akasema “ dawa yako ipo jikoni, lazima nikufundishe adabu, kisha akawa anaaondoka, bibi akanambia “ kwanini umemjibisha hivyo huyu mwanamke ni mzigua ni mchawi balaa…
“ uchawi haupatanagi na bangi bibi, ajichanganye aone namna ambavyo naenda kuwapasua yeye na huyo mganga wake, nikasema , bibi akataka niache kile chakula tukale chakula cha shule au tukapike chakula chetu…

“ mimi mwenyewe siwez kula, mbona huyu mwanamke hajui kupika, yaan kuku kamuosha mpaka amekuwa kama mate, nilikuwa nataka kumtia tu hasira hawez kukudharau na wakati wewe ndio umesababisha mpaka akamjua huyo mwanaume ambae anasema ni mumewe na anajivunia nae…

“ umenifurahisha sana, na moyo wangu haujawah kukosea kabisa, maana niliamin kuanzia nakuona kuwa unafaa kwa ajili ya mjukuu wangu, akasema bibi kisha tukamuita mbwa na kumpa kile chakula, kisha tukazunguka nyuma ya ile sehemu tuliokuwa tunakaa kulikuwa na nyumba, ilikuwa ina kila kitu ndani, ni kama room mbili na sebule, bibi akanambia kuwa wakati majukum yakizidi mjukuu wake analalaga hapo….

Basi tukaingia ndani na kuanza kupika, yaani mimi na kupika ni maadui, maana wadudu hatupikagi bana, nilikuwa najua kuchemsha chai, kuchemsha maji ya kuoga na uji, ila hata ukisema nikupikie ugali utalia, nikaona nisijivunge nikamuambia kabisa bibi kuwa mimi sijui kupika ili asije kuniachia jikoni nikaja nikamuonesha maajabu ya wanawasiraeli dakika za kuhesabu…

“ usijali mjukuu wangu nitakufundisha, basi akaenda kwenye jokofu na kutoa samaki, akaanza kunielekeza namna ya kumuandaa tukawa tunamuandaa wote, kisha yeye akaenda akamkaanga, na baada ya hapo akawa anatakata kata kachumbari, akanambia nikorogee uji, basi nikawa nakoroga pale, akaja akasonga ugali, akapakua chakula akaweka kwenye hotpot akataka nimpelekee mjukuu wake sudeys kisha nile nae ili tuzidi kuzoeana…

Huyu bibi sijui alikuwa anawaza nini, yaani mimi nizoeane na sudeys labda niwe nimezimia, nikawa najiambia, ila kwakuwa Yule bibi alinionesha mapenzi makubwa sana, sikutaka kupingana nae, nikaenda mpaka kwenye ofisi ya sudeys na kugonga mlango, akaniruhusu niingie, aliponiona nimeingia akatabasamu kisha akasema “ nilikuwa nasikia njaa sana, hatimae nimepikiwa na pisi kali ya chuga, unajikuta jike dume akati wewe ni mchumba tu, haya mrembo njoo nitengee chakula boss wako tena kwa adabu…

Nikamuangalia kwa sekunde kadhaa kisha nikamuambia “ hivi unajikutaje, yaani mimi nikae nakutengea chakula mtu kama wewe labda maiti yangu ndio ifanye hio kazi, na kama nisingekuwa namuheshimu bibi yako hata hiki chakula nisingekuletea…

Nikashangaa Yule mwanuame amesimama kisha akaenda kufunga mlango na funguo, alafu funguo sijui akaiweka wapi, na kusema “ sasa hapa ndani tumebaki mimi na wewe, ukiongeza neno lingine la ajabu, njitahakikisha mikono yako ndio inatumika kunilisha, na nikimaliza kula nitakula tena, haya kwa ustaarabu na unyenyekevu wa hali ya juu nitengee chakula mrembo…
Nikaona sasa hichi kizaa zaaa …
ITAENDELEA


PISI KALI YA CHUGA 5
HUSQER BALTAZAR
“ mimi sio mke wako, siwez kufanya majukum ambayo hayanihusu, na ukweli ni kwamba haunivutii hata kidogo, hivyo chukua chakula chako ule na ufungue mlango niondoke kabla sijaanzisha kichaa changu, maana nahisi umenisahau…

Akaniangalia kisha akacheka, “ haya embu endelea kupandisha kichaa chako maana napendaga sana watu wenye vichaa mimi, haya unaanza kupandisha saa ngapi hicho kichaa….

Nikaanza kumsogelea kibabe, nikawa najua kuwa anaweza kuwa Yule ambae nilishamletea ubabe siku kadhaa nyuma, wakati namsogelea nilikuwa nasema “ haya utafungua au haufungui mlango…
Hapo sudeys yupo kimya ananiangalia huku anatabasamu ila hata hakuwa anajisumbua kusogea nyuma, nilipomfikia nikawa nawaza nimuweke hata teke la kwa nini, ili akiwa anaugulia maumivu mimi niwe naondoka zangu, ila ile nimemkaribia akanishika kiuno na kunambia “ najua unachokiwaza kisha akaanza kunipiga busu moja matata, nilikuwa namuonaga kama mwanaume ambae nammudu hivi ila alikuwa na nguvu sijawah kudhani, aliponishika nikawa hata sitetereki, akanikiss pale hata nguvu za kujisogeza sikuwa nazo kabisa yaan, akanibusu mpaka hamu yake ikaisha kisha akasema “ sikujua kama una lips tamu kiasi hichi, yaan mpaka najikuta kama natamani niendelee kuzinyony*…

Nilimkata jicho hilo, akatabasamu kisha akasema “ hata ukinuna bado unaendelea kuwa mzuri sana mamaa, haya endelea kununa…
Yaan sijui ule ubabe wangu ulipotelea wapi, na sijui hata yale maneno yangu ya majigambo na ubabe yalizama kwenye meli gani, maana nilipoa kama nimemwagiwa maji ya barid, na mbaya zaidi lile busu ambalo alikuwa amenibusu kuna namna lilikuwa limenisumbua sana, yaan nikajikuta nashika lips zangu bila kujitambua, nikashangaa anacheka na kusema “ do not say that I am the best kisser, ohhhh my God mpaka umeshika lips zako, maana kuwa nimekusisimua na kukuachia alama, ila usijali nikikuoa nitakuwa nakupa hayo mabusu kila siku na hautakaa ujute kupata mume kama mimi, hta kama nakula chips ila kazi naiweza hautojuta…

Nikajua ameshaanza kunitambia kutokana na namna ambavyo nilishawah kumuambia huko nyuma , nikawa kimya tu maana sikutaka afanye jambo lingine la ajabu, akafungua hotpot kisha akasema “ sijui hata nina haraka za nini na wakati mke wangu yupo, mke wangu kipenzi utaendelea kusimama hapo hata kama mume wakonasikia njaa na wakat unajua natakiwa kula…

“ wewe mwanaume mbona una akili za kiwaki sana aiseee tangu lini nikawa mkeo, embu jiheshimu basi, ni kwamba tu sitaki kuanzisha vagi hapa maana bibi yako ni mtu mzuri na hapa ni shule wanafunzi wasije wakashangaa tu, ila laa sivypo ningepasua pasua hivyo vimiwani vyako na vioo vya ufo si yako vingegeuka chenga, ila nimekaa kimya unaanza kunipanda kichwani, mimi sikuanyi bro ni basi tu najifunza kuwa mstaarabu tu hapa, nikasema na hapo kuna vihasira nilikuwa navyo maana kuanzia Napata akili kiumbe pekee ambacho kilikuwa kinaweza kunambia acha kufanya kitu flani na nikaacha ni wazaz wangu tu, ila hawa raia wengine nilikuwa siwaogopi hata kidogo, hata kama nikikutana na mtu anamvi kwenye nywele zote mpaka nywele za chini, ila sikuwa naogopa kabisa yaan, alafu huyu nyang’au amenituliza anataka nipoe kirahisi hivyo haiwezekani aiseee…

Alipoona naanza kumletea mdomo akaniangalia kisha akaja nyuma yangu na bila kutegemea akapitisha mikono yangu kwenye kifua changu, na kuanza kunichezea tuchuchu twangu, lilikuwa ni jambo la ghafla ambalo hata mimi sikuwa nalitegemea kabisa, nikajikuta napatwa na msisimko wa ajabu sana, alafu yeye akawa nyuma yangu ananinong’oneza na kusema “ maneno ambayo umetoka kuniambia muda mfupi uliopita yamenisisimua sana, mpaka nikajikuta sitamani kula ila nataka kula, hivyo nimeona bora nibadilishe msosi….

Ingawa mwili wangu na akili yangu vilikuwa vinatoa ushirikiano tofauti ila sikutaka kuliwa kizembe vile yaan, nilikuwa naona bora kama nikuliwa niliwe na mwanaume ambae nitampenda na sio mtu ambae anapambana sana kuhakikisha kuwa anafanya anachotaka juu yangu kibabe…

Nikaanza kujitoa kwake, yaan hata hakunipa muda akaanza kupitisha ulimi wake kwenye shingo na maskio yangu, yaan mpaka nikajikuta nimelegea , liponiona nimelegea akaanza kucheka, kisha akasema “ nilijua wewe una hisia za kiume hivyo hauwezi kusisimka, kumbe hadi kulegea unaweza, najua ningeongeza hapo ungeanza kutoa na miguno ya mahaba bila kutaka, maana unaonekana….
ITAENDELEA….


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote