RAFIKI YANGU ALIVYOOLEWA NA MCHUMBA ANGU 💔
BFF ili neno Mara nyingi watu wamezoea kulitumia kaka best friend forever, lakini Mimi ngoja niwaaambie tu msiliamini ili neno limekaa kinafiki sana 😭 .
Paula mimi nikisalitiwa na RAFIKI yangu ambaye tulikuwa tunavaliana mpaka Nguo za Ndani, Zuri RAFIKI yangu nilimpenda kuliko chochote, ni msichana ambaye nilimpa kipaumbele ambacho hakuwa anastahili.
Siku ya ndoa yangu ilibadilka na Kuwa siku ya ndoa ya RAFIKI yangu 💔😭 ushawai kutelekezwa saloon wewe ? ? Ushawai kuvuliwa pete ya uchumna mbele ya RAFIKI zako ?
Anyway nisimalize uondo tukitane Ndani Ndani uku…..
RAFIKI YANGU ALIVYOOLEWA NA MCHUMBA ANGU
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 01
ANZA NAYO……
Paula, ndio Jina langu Jina ambalo nilipatiwa na wazazi wangu ikiwa ni Jina nililorithi kutoka kwa Bibi yangu mzaa baba, Mimi Bwana nilichukua kila kitu kutoka kwa Bibi yangu, kuongea sana , weupe shape na kila kitu, wazazi wakaona Kuwa haitoshi wakaamua kunipatia Jina la Bibi yangu.
KWa kifupi Mimi na Bibi yangu ni watu ambao tunapendana sana, kuna muda uwa nataka kukaa na Bibi yangu tu, kuna Namna ni Kama ndugu zangu walianza kunionea wivu hivi maana daaah sio kwa upendo ambao nilikuwa naupokea kutoka kwa Bibi yangu.
Katika harakari za maisha ya hapa na pale Paula Mimi niliweza kupata mchumba jamani, mkaka fulani hivi, mzuri sana, Yaani naweza kusema Kuwa ni ndoto ya kila mwanamke kwa muonekano wake ulivyokuwa ukivutia.
Jaden ndio Jina la mwanaume wangu, mwanaume ambaye aliniingiza mzima kabisa kwenye ulimwengu wa mapenzi, Sijui Kama mnanielewa lakini jaden alinifanya nione Kuwa love is a beautiful thing.
Sio kwamba uko nyuma sikuwai Kuwa na mahusiano lahasha, mahusiano nilikuwa nayo lakini nilikuwa nikipigwa tukio baada ya tukio.
Tuachane sasa kwanza na jaden njooni uku kwenye masuala ya bff 😍🔥 uwiiiih uku ndio hot kabisa, Mungu alinikutanisha na huyu msichana Mrembo, mzuri kabisa Kama jina lake kwani alikuwa akiitwa ZURI.
Mimi na zuri ni watu ambao tumekutana tukiwa kidato cha Tano kwenye Shule ya wasichana tupu, ZURI alikuwa ni roommate wangu, lakini pia tulikuwa tukisoma kasımı ambayo yanaenda na hii ndio ilizidi kutuweka Karibu zaidi.
Sio hivyo tuna jamani, Mimi na ZURI tuliaminiana sana ilifikia kipindi ata tukaanza Kuvaliana Nguo za Ndani Sijui mnaelewa 😂🙌 Yaani Mimi kuchukua Pichu ya ZURI na kuivaa nilikuwa sioni shida ata kidogo.
Shule nzima ilitufahamu kutokana na jinsi ambavyo tulikuwa tunapendana Sanaa, kuna muda nikaanza kuona Kuwa ni Kama tuna za kufanana hivi na kwasababu hiyo tukaamua kujiita twins.
Ushoga kati yangu na ZURI Ulikomaa na kuota mizizi kabisa. Na hapo tukaamua kuwakutabisha wazazi wetu na hii ndio ilizidi Kuchangamsha urafiki wetu na wazazi walikuwa akifurahi sana kutokana na jinsi ambavyo tunapendana.
Mungu Mwema Mimi na ZURI tuliweza kumaliza kidato cha sita lakini pia tulifauru vizuri sana na hapo tukaamua kwenda chuo kimoja lakini pia tulisoma kozi moja ili tu tusiwe mbali mbali.
*****
Anyway maelezo yasiwe Mengi sana jamani, kuna uondo mkubwa. Sana nataka Kuwasimulia so, weka popcorn zako Karibu, weka kinywaji chako Karibu halafu nisikilize kwa makini nikuoneshe ni kivipi Rafiki yangu aliolewa na mchumba wangu ikiwa yeye pia alikuwa na mchumba Ake.
Ilikuwa ni siku ya jumamosi, of course ndio siku nzuri kabisa kwaajili ya ndoa za kikristu.
Niliamka zangu asubuhi na mapema nikiwa a kimuhemuhe na ndoa ambayo ilikuwa unatalajiwa kufungwa Saa 6 mchana kwenye kanisa la mtakatifu THERESIA.
“Paula“
Ilikuwa ni Sauti ya Rafiki yangu zuri, Sauti iliyojaa uchovu wa hali ya juu kutokana na kukesha kwenye single part ambayo ilifanyika pale Nyumbani kwetu.
“Endelea tu kuniitilia na Sauti yako hivyo halafu uone ninavyokuacha, Zuri amka Tuwai saloon kipenzi”
Nilizungumza na Kuanzia kumtikisa zuri ili aweze Kuanzia an twende saloon kwa pamoja kwani zuri ndio alikuwa maid of honour.
Basi zuri aliamka chap na Haraka akaoga na safari ya kwenda saloon ikaanza.
“Woiiiiiih, mtume mtumeeeeh toba toba toba “
Alizungumza zuri na kunifanyia niogope sana na wakati huo tulikuwa Ndani ya Gari.
“Nini na wewe jamani Mbona tunastuana Kama hivyo “
Nilimfokea maana amenistua sana kwakweli.
“Uwezi amini, nimeacha Gauni yangu na Wigi kule Nyumbani kwangu, Yaani huu Mfuko una Viatu tu “
Alizungumza zuri uku akionesha Kuwa na wasiwasi sana.
“Ila wewe, Sijui lini Italy wa unafanya shughuli Zako kwa mpangilio, anyway hakijaharibika kitu, Nafikili ukachukue then tuonane saloon au unaonaje ??”
“Ni Sawa Tena ni chap tu wacha niwai”
Basi Zuri akashuka kwenye Gari na kuondoka uku na Mimi nikiendelea na safari yangu ya kwenda saloon.
Muda wote nilikuwa Nilizungumza na jaden wangu kupitia video call na yeye kWa upande wake alikuwa kwenye maandalizi ya tukio let’s muhimu kabisa.
Majila ya Saa 5 na nusu kwa upande wangu nilikuwa tayali kwenye kila kitu, lakini pia kwa upande wa Zuri hakuwa amerudi tangu alivyosema Kuwa anaenda kufuata Nguo.
Nilijaribu kimpigia lakini hakuwa akipokea kabisa, nilijikuta nikipata wasiwasi wa Hali ya juu, kiukweli sikutaka kabisa rafiki yangu akose kwenye siku yangu ya muhimu kama hii.
Naweza nikasema siku hii ilikuwa ni siku ya mazing zong, baada ya kumpigia simu zuri kwa muda mrefu na kumkosa, nikaamua kumpigia babe wangu yaani Jaden kwani muda wa ndoa ulikuwa umshakaribia ajabu jaden pia hakuwa akipatikana kabisa na hii ilizidi kunipatia wasiwas.
Kwakweli sikuweza ata kukaa chini kwa wakati huo, nilibaki nikizunguka uku na uku kama nimerukwa na akili vile, wasiwasi wangu ulikuwa ni nini iitokea kama Jaden atokuja kwenye siku yetu ya muhimu kama hiyo.
Nikiwa nimechanganyikiwa sana gafla mchumba wa rafiki yangu zuri aliwasili katika eneo ilo.
"eeeh afadhali shemeji yangu umekuja walahi nachanganyikiwa mwenzio "
Nilizungumza kwa jazba sana na sauti ya kupaniki maana mambo yalikuwa yanavulugana tu.
"Kuna kitu nataka uone "
Alizungumza shemeji yangu lakini pia alionekana kutokuwa sawa na alinipa wasiwasi zaidi.
"Kuna nini shemeji mbona unanishtua sana jamani "
"Unatakiwa kuona hii kabla ujaingia kwenye matatizo "
Hapo nilijikuta nikipata wasiwasi zaidi na haraka Mimi na shemeji yangu tukasogea pembeni kisha akanipatia simu yake.
"Ni nini hii ??"
Nilimuuliza shemeji yangu baada ya kuona picha ya zuri na Jaden na walikuwa wamependeza sana na mikononi mwao walionesha karatasi.
"Kusoma ujui ata picha uoni shemeji yangu, tumesalitiwa shemeji yangu, naweza nikasema kuwa Jaden na zuri wametuweza safari hii na wamejua kutufedhehesha "
"Shemeji unanichanganya jamani nini kinaendelea kwani ??"
"Jaden na zuri wamefunga ndoa ya mahakamani hii Leo, namaanisha Sasa hivi yani"
Nyie nilihisi kuzimia zimia walahi, yaani hizi habari zimejua kustua moyo wangu na kama ningekuwa na presha basi tungeongea mengine.
Sijui ata machozi yalinitililika muda gani lakini nilijikuta nikilowesha uso wangu na kuharibu make up yangu yote.
Muda huo huo simu yangu iliita na Jaden ndio mtu pekee aliyekuwa akinipigia haraka nikapokea na kwa hasira nikamuuliza.
"Kwanini ilikuwa upatikani ??"
"Ooooh babe, I am so sorry, simu yangu ilizima chaji lakini pia hakukuwa na umeme kabisa, lakini pia nipo kanisani uko wapi naona muda umefika "
Alizungumza Jaden kana kwamba hakukuwa na kitu kinachoendelea.
"Nakuja "
Nilijibu na kukata simu.
"Usiniambie unaenda kufunga ndoa na Jaden ??"
Shemeji yangu aliniuliza kwa mshtuko maana aliamini kuwa nitakataa kuolewa.
Kwa muda huo nilikuwa niisikiliza moyo wangu tu na akili yangu, nilijiweka sawa kisha safari ya kwenda kanisani ikaanza.
Mungu alisaidia sana na tuliweza kufika kanisani lakini pia familia yangu na ya Jaden ili wasili kanisani, kiukweli kila mtu alikuwa na furaha sana isipokuwa mchuna wa rafiki yangu zuri lakini pia na mimi sikuwa a amani ata kidogo.
"Paula, uko tayali kuolewa na Jaden, awe kama mume na rafiki wa maisha yako ? Mtakayependana kwenye shida na raha, uzima na magonjwa ??"
Lilikuwa ni swali kutoka kwa padri ikiwa ni sehemu ya kukamilisha ibada ya ndoa.
Kwa wakati huo moyo wangu ulikuwa na maumivu makali sana, na wakati huo huo zuri waliwasili kanisani, kitendo cha kumuona zuri nikajikuta nikilopoka.
"Siko tayali"
Kila mtu aka.......
ITAENDELEA......
RAFIKI YANGU ALIVYOOLEWA NA MCHUMBA ANGU 💔
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 02
SONGA NAYO….
Majibu yangu yaliwashtua sana watu especially familia yangu na. Familia ya jaden, jaden pia alishtuka sana Sijui ata Kwanini alishtuka ikiwa yeye ni msaliti mkubwa.
“Babe uko Sawa ??”
Jaden aliniuliza kwa sauti ya wasiwasi sana.
“Yaaah niko Sawa hii ni kwaajili yetu sote “
Nilijibu uku nikianza kushuka ngapi za mbele ya kanisa.
“Paula uko Sawa kipenzi ?? “
Rafiki yangu zuri aliniuliza baada ya kusogea pale mbele, Yaani zuri ni Kama panya tu anayeng’ata na kupuliza Yaani hana huruma ata kidogo.
Kila mtu alikuwa na maswali Mengi sana juu yangu lakini baba yangu hakuwapa nafasi ya kuniuliza kwani baba yangu alinisogelea haraka sana na kunitoa katika Eneo ilo.
Familia yangu na famili ya jaden ilitufutaa nyuma nyuma kwani wengi walitaka kujua ni kitu gani kinaendelea.
Tuliweza kufika Nyumbani na kwa muda huo niliitaji Kuwa Mwenyewe, muda huo niliitaji kukaa kwa utulivu wa hali ya juu maana kichwa change akikuwa Sawa kabisa.
“Baba Naomba nikapumzike chumbani kwangu “
Kabla baba yangu hajajibu, jaden pia alikuwa amewasili na kwa hasira akazungumza.
“Ukapumzike halafu Mimi unaniachaje ? Eeeh Paula ni nini umeniachia hiki ? Ni nini umenifanyia umeamuakunidhalilisha mbele ya familia yangu na kila mtu si ndio “
“Naitaji kupumzika kwanza akili yangu ikikaa Sawa tutazungumza, kwa sasa Naomba radhi kwa haya yote yaliyojitokeza, najua nimemkosea kila mtu lakini haya mambo yapo nje ya uwezo wangu kwa sasa “
Nilizungumza kwa utulivu wa hali ya juu.
“Paula kipenzi hii siku ulikuwa ukiisubili sanna Kwanini Unajifanyia hivi pacha wangu eeeh ??”
Alizungumza Zuri utazani ni mtu ambaye Anajali sana.
Nilimuangalia zuri kWa muda kisha akili yangu ikaniambia Ebu mtolee huyu snichi uvivu maana ananizoea tu.
“Zuri unafikili Mimi nilikuwa nikiisubili hii siku Kama ambavyo ulikuwa ukiisubili wewe. ??”
Muda huo huo mchumba wa zuri alinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu sana na kwa uchungu akazungumza.
“Msemo wa adui atoki mbali uwa unamaana kubwa sana kwakweli, Paula yupo kwenye hali hii kwaajili yenu ninyi Wawili halafu muda huu mnajifanya Kama amjui kitu gani kinaendelea”
“Ebu kwanza muachie mke wangu na uache kuongea upuuzi, tupo hapa kwaajili ya kutengeneza na sio kubomoa”
Alizungumza jaden na kumsukuma mkaka wa watu.
Mama mzazi wa jaden alinisogelea na kunishika mkono kwa nguvu sana na kuniuliza.
“Ilipanga kutuzalilisha si ndio ??”
“Sijapanga kumzalilisha mtu lakini siwezi kufunga ndoa na mume wa Rafiki yangu, jaden na zuri ni mume na mke na wamefunga ndoa asubuhi ya Leo pale kwenye Mahakama ya kati niambieni nawezaje Kuwa mke wa pili ??”
Kwanza kila mtu aalishtuka sana, zuri aliogopa sana na kujikuta akiitaji kukimbia maana ha kujua Kuwa Mimi Najua kila kitu.
Mama mzazi wa jaden alimsogelea Kijana wake na kumuuliza.
“Kuna ukweli gani juu ya haya Maneno ??”
“Momy I can explain “
Kitendo cha jaden kusema tu I can explain ilikuwa ni majibu tosha, kWa upande wangu sikuwa Sawa nikisogelea kochi na kukaa chini.
“Nisingeweza kumuacha Zuri mama ikiwa amebeba Mtoto wangu “
Alizungumza jaden.
Woiiiiij 🥹🥹 huu usaliti ni wa hali ya juu Yaani hawa watu walijufanya shemeji shemeji kumbe wanazima na taa kabisa💔😭 najuta Mimi kumuamini rafiki najuta kwa kila kitu Walahi.
“Nafikili tunaitaji kubaki Kama familia tu “
Alizungumza mama yangu na Kuwafanya watu kutawanyika, kwa upande wa Zuri aliondoka akiwa na Aibu ya hali ya juu, baba yangu alinishika mkono na kunipeleka chumbani kwangu na kuniacha nipumzike.
Kiukweli Sawa Mimi Sawa nilikuwa nikiumia sana lakini wazazi wangu walikuwa wakiumia zaidi yangu, kila mtu alishindwa kulala kwaajili yang, Mimi nilibaki nikijililia tu maana nilijipa matumaini makubwa sana juu ya jaden, Yaani watu waliokuja kunisaliti ni watu wangu wa Karibu.
Familia yangu ilishindww kulala, Bibi yangu ndio kabisa muda wote alikaa pembeni yangu kuhakikisha Kuwa nakuwa Sawa.
*******
Nilishindwa kulala kabisa jamani, usingizi uligoma na hatimaye siku ikashika nafasi, muda huo wa asubuhi, familia ya kina jaden iliweza kuwasili na waliomba mazungumzo na sisi.
“Kwani wanataka nini hawa watu baada ya kila kitu wanapata nguvu ya kuja hapa kweli jamani “
Bibi yangu alianza kulalamika baada yakusikiaa Kuwa familia ya jaden imekuja.
“Bibi wao pia wamekosewa na Mtoto wao, hatujui wamekuja kufanya nini lakini wanahaki ya kusikilizwa”
“We nawe Yaani tangu imempata huyu jaden wako umekuwa na tabia za malaika wa amani mi unanikela ujue “
Ila Bibi yangu ni mtu Mwenye Maneno sana jamani 😂🙌 Bibi umeenda lakini weeeh Mdomo kama Katoto Ka elfu Mbili 😁.
“Ila Bibi Bwana mi sitaki kucheka ujue “
“Kwenda zako haya inuka nikakuogeshe haraka ukaonane na wakwe zako “
“Na Kwanini uniogeshe we mzee ata hivyo sijisikii kuoga “
“Utajua Mwenyewe, najua kabisa Kuwa wewe upendagi kuoga tangu utoto wako “
Ila Bibi jamani.
Kiukweli sikuwa najisikia kufanya chochote kile, nilivuta kijora changu na Kuweka mwilini kisha nikatoka nje na kwenda kuonana na wazazi wa jaden.
Nilifika na kwenda kukaa Karibu na mama yangu na kumuegemea kwani nikihisi Kuchoka sana..
“Unaendeleaje Binti yangu ??”
Mama wa jaden aliniuliza.
“Niko Sawa mama “
“Utakuwa Sawa Binti yangu, iki kipindi kwako kitapita na it akiwa Sawa kabisa Sawa. ??”
“Sawa mama “
Basi tulikaa kimya kwa muda kisha baba wa jaden akazungumza.
“Aaaah tumekuja kuomba radhi kutokana na kila kitu ambacho kilitokea siku ya Jana, kiukweli jaden ametuzalilisha Jana, ukiachana na kudhalilisha ameiumiza familia lakini pia amemuumiza sana Paula wetu hapa, sikuwai kufikili Jambo Kama ili kutokea Tunaomba mtusamehe sana “
Basi mazungumzo yaliendelea pale na naweza kusema Kuwa wazazi wa jaden ni watu wenye Busara sana na ni watu ambao wnaajielewa sana.
Maongezi yakiwa yanaendelea gafla jaden aliingia na aliinekana Kuwa amelewa sana, haraka baba yake akamuwai na kumuuliza kWa hasira.
“Ümefata nini hapa ??”
“Nimemfata mke wangu, namtaka Paula wangu, najua nimemkosea lakini kamtaka yeye”
Baba yangu aalichukia sana na kwa haraka akamsogelea jaden na pasi na kufikilia akamtuliza na Ngumi moja matata.
Wote tuka…..
ITAENDELEA….
RAFIKI YANGU ALIVYOOLEWA NA MCHUMBA ANGU 💔
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 03
SONGA NAYO….
Wote tulishtuka sana Aswah mimi jamani, sikuwai kumuona baba yangu akiwa na hasira kiasi iki sikuwai kumuona baba yangu Akinyanyua mkono wake kumpiga mtu yeyote Yule ata Mimi jamani si hakuwai kunipiga.
Baba yangu amekuaa ni mtu wa kuzungumza na mtu kwa utulivu snaa, Mara nyingi baba yangu amekuwa akitumia Maneno katika kuweka mambo Sawa lakini Leo hii alinyajnyua mkono wake na kumpiga jaden.
Vulugu lilikuaa kubwa sana kwakweli maana baba alikuwa na. Hasira sana kwakweli, wazazi wa jaden waliangaika na Mtoto wao na mwisho walimchukua na kuondoka nae.
*******
Week Mbili zilipita uku nikiwa sijawaasha ata simu yangu jamani, Yaani niliamua Kujipa likizo na kila kitu na kwa wakati huo niliweza Kuwa Sawa, niliweza kuchagua maisha ya kujipenda Mwenyewe na kuishi maisha yangu.
Siku hiyo ilikuwa ni siku Mpya sana kwenye maisha yangu yangu nilipopata matatizo ya usaliti, niliamka asubuhi na mapema nikaoga na kuweka kila kitu Sawa kisha nikatoka nje.
Moja kWa moja nikaingia jikoni na kujiandalia kifungua kinywa changi ninachokipenda walahi siku hiyo nilikuwa na tabasamu pana sana kuliko siku zote.
“Umeokota Pochi la Mzungu ndotoni au ??”
Bibi yangu cha Maneno aliniuliza.
“Umeanza bi Paula haya ulitaka niamke na mood gani Leo eeeh “
“Eeeh huyu sasa ndio Paula ninayemjua mimi, Yaani huyu ndio Paula ambaye nilikuwa namsubili muda wote Yaani mdomo mrefu Kama chuchunge “
“Kwanza bi Paula nilikuwa nakusubilia sana tu uje unisaidie Kuchagua Nguo, leo naenda kwenye Bachela patty ya chido si unajua kesho ni Harusi yake, nataka nipendeze sana. “
Bibi yangu aliniangalia kwa muda kisha akaniuliza.
“Una uhakika unataka kwenda uko ??”
“Na Kwanini nisiende bibi ? chido amekuwa na Mimi kwenye kila kitu changu siwezi kumuacha”
“Namaanisha Kuwa utakuwa Sawa kwenda uko? Maana nina uhakika Kuwa Zuri na jaden wars Kuwa uko”
“Nitakuwa Sawa kabisa Bibi yangu usijali kwa sasa naitaji kuishi maisha yangu, sasa hivi nataka kuishia maisha ambayo Mimi nayaona kuwa ni Bora kwangu, sitawaruhusu walioniumiza kuja kuniumiza Tena lakini sitaruhusu wao kuharibu Furaha yangu ata Mara moja “
Nyie nini yangu alifurahi sana mpaka akajikuta akitokwa na macho ya Furaha.
Majila ya Saa 2 usiku, nilijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye bachelor party 🥳 Walahi nilipendeza sana sana, nilipendeza kuliko kawaida naweza kusema Kuwa nilikuwa Paula Mpya na sio Yule wa Zamani.
“Bi Paula how do I look ??”
Nilimuuliza Bibi yangu uku nikijizungusha uku na uku kwa kujilingisha.
“Yaani unaonekana kama enzi zangu za ujana Yaani daaaah umependeza sana kujuso”
“Eeeehh ndio tumefikia kwenye kijuso jamani ??”
“Kwendaga uko unachelewa fanya haraka haraka uwende “
Basi nikatoka chap na kwenda kuwaaga wazazi wangu na ndugu zangu ambao walikuwa wakiangalia movie kwa wakati huo.
“Khaaaah hapo sister umeua Walahi Yaani umependeza sana “
Alizungumza Mdogo wangu, nilibaki nikitabasamu tu.
“Nikupeleke ??”
Mamma aliniuliza.
“Hapana mama nitakuwa Sawa kabisa msijali, zaidi nilikuwa Naomba funguo ya Gari hii Mpya “
“Hahahaha nilijua tu Kama utataka kutumia hiyo Gari haya jamani mpatieni funguo Binti Malingo “
Alizungumza baba yangu na kila mtu akacheka.
Hatimaye niliweza kufika kwenye Sherehe, nyie watu walipendeza sana sana sana, na kila mtu aliku na Furaha sana, Rafiki zangu waliponiona haraka wakanikimbilia.
“Walahi tulikumisi sana kipenzi “
“Aaaaah Kama ni kukutafuta kwenye simu ingekuwa ni alamu Walahi Mimi ningekamatwa “
“Ila pole sana kipenzi utakuwa sawa. “
“You’re so strong my girl”
Walahi kila mtu alikuwa na Ana niambie Mimi kuna muda ilifika nikawa sijui nimsikilize Nani nimuache Nani Walahi.
Basi patty iliendelea na kila mtu alikuwa na Furaha, baada ya muda niliweza kumuona zuri na jaden Yaani ndio kwanza walikuwa wanafika kiliwaangalia na kujikuta nikilalamika kimoyomoyo.
“Waone walivyo Kama mawakala wa mashetani vile 😎 chefu mie”
Baada ya muda walifika nilipo na kWa Kuwa zuri hakuwa mtu kwenye aibu alinisogelea na kunikumbatia kwa nyuma na kunisikisi kwenye shavu haraka nikajukuta nikilopoka.
“Naona kampeni ya yuda Unaendelea”
Jaden aliniangalia sana na kwa hasira akazungumza.
“Huu uswahili ndio siutaki kabisa, unasalimiwa unaanza kuleta mambo meusi “
Niliwaangalia kwa muda kisha nikainuka na kutaka kuondoka kwenye meza hiyo lakini garaja jaden akanidaka mkono na kwa sauti ya hali ya juu akanifokea.
“Naomba Pete yangu ya uchumba sio mali yako Tena “
Kwanza nika….
ITAENDELEA….
RAFIKI YANGU ALIVYOOLEWA NA MCHUMBA ANGU 💔
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 04
SONGA NAYO….
Kwanza nikageuka na kuangalia uku na uku Walahi ilikuwa ni Aibu ya hali ya juu maana kila mtu alikuwa akiangalia eneo ilo, kuna Namna niliona ni Kama Nimekuja kuongeza matatizo tu Bora ningebaki Nyumbani kwetu.
Muda huo huo Chido alisogea kwenye eneo ilo na kuuliza..
“Jaden unaona iki unachokifanya ni Sawa ? “
“Kudai haki yangu au ? Ata hivyo ni kitendo cha kuvua tu hiyo Pete na kunigawia”
Muda huo ndio niligundua Kuwa bado Mkononi mwangu nilikuwa nimevaa Pete ya uchumba Ali’yi ibik a jaden, kwa uchungu wa hali ya huu Niliivua na kumkabizi.
“Naomba muondoke kwenye sherehe yangu “
Chido alimwambia jaden na Mwanamke wake Yaani zuri.
“Noooh chido waache hii ni siku yako muhimu Ana Nafikili wanaitajika hapa “
Muda huo huo alisogea Mwenyekiti wa kikundi chetu cha amani na upendo kwa utulivu akazungumza.
“Nafikili jaden na zuri taarifa ya kutolewa kwenye kikundi mliipokea mapema kabisa, sasa niwaulize hapa mmekuja kama Nani ? Kwa akili ya haraka haraka kwanza mnafikili Kuwa mnastahili Kuwa hapa, hiki ni kikundi cha amani na upendo lakini nyie mlichofanya ni kuondoa amani na upendo kwa mtu mmoja na amuoneshi kujitia ningeomba mwende kWa sasa hakuitajiki hapa “
“Ata hivyo hatuna haja ya Kuwa hapa ila mtajutia sana kutupoteza watu kama sisi kwenye maisha yenu.
Basi jaden na mwanamke wake wakatondoka na kuniacha sherehe ikiendelea.
“Uko Sawa. ?”
“Niko Sawa “
Walahi me napendwa jamani, kwa wakati huo kila mtu alikuwa na wasiwasi na Mimi, kila mtu aliniwazia Mimi na walihakikisha Kuwa nakuwa Sawa.
“Paula hizi pombe zinatosha sasa”
Chido alijiambia baada ya kuona Kuwa nakunywa sana na wakati huo nilikuwa nimelewa sana, nilikuwa nikicheza mpaka matangazo 😂🙌 Yaani daaah Walahi nilikuwa ni kituko lakini watu wangu wa Karibu waliweza kunielewa hali yangu.
*******
Asubuhi na mapema nilikuwa Kuamka nikiwa kwenye Chumba ambacho sikuwa nikikifahamu kabisa, lakini pia nilikuwa Nina maumivu makali sana ya kichwa, Sijui ata nisemeje lakini sikuwa Sawa.
Katika angaza angaza na uku na uku, niliweza kumuona mwanaume mtannashati kabisa akiwa amesimama kwenye kioo akijitazama, kwa wasiwasi nikamuuliza.
“Wewe ni Nani na hapa Nimefikaje ?!”
“Oooj umeamka Nafikili kwa sasa utakuwa hauko Sawa wacha update ata supu si ndio ??”
Walahi nilijikaza na kusogelea mbele yake ili kwenda kumuona ata sura yake uku akiwa amenipatia mgongo.
“Wewe ni Nani na unataka nini kwangu ??”
“Nashukuru Mungu umewai kuamka maana nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana juu yako, by the way naotwa TINO ni Rafiki yako Mpya “
“Hapa ni wapi na nimefikaje ? Simu yangu iko wapi ??”
“Kama nilivyokuambia Kuwa naitwa TINO ni Rafiki yako Mpya tulikutana Jana barabarani ulikuwa umelewa sana, lakini pia ulikuwa umepaki gari yako sehemu ambayo sio salama, ulikuwa ukilia sana ni wazi Kuwa kuna mambo hayako Sawa kwa upande wako Mimi Kama binadamu mwenzio nikakuchukua na kukuleta Nyumbani kwangu kwani ni salama zaidi kuliko pale barabarani nilikokukuta “
Daaaah nilishusha pumzi Ndefu sana na kumuangalia mkaka Yule kwa Mara nyingine Walahi amejua kunisaidia maana usiku sikuwa Sawa kabisa na sikumbuki niliondokaje pale kwenye sherehe.
“Na gari yangu iko wapi ??”
“İpo nje hapo, kWa Kuwa sisi tulikuwa Wawili Mimi niliamua kuendesha Gari”
“Asante sana kaka Angu, yaaani pasi na uwepo wako Sijui ni kitu gani kingenikuta mimi”
“Yaaah umefanya Jambo la hatari sana, ungezulika wewe lakini pia na kila Ulicho Kuwa nacho kingeibiwa binadamu hatuna wema kwa sasa “
Nilibaki kimya tu maana ni kweli nilikuwa nimekosea sana sana niliweza kuweka maisha yangu hatarini kwaajili ya watu wapumbagu tu.
“Unaweza ukaenda kuoga then upate kifungua kinywa ndio ulejee nyumbani kwako me natoka kidogo”
Nilimuangalia kwa muda kisha nikamuuliza.
“Naweza nikapata mawasiliano yako ??”
Mkaka huyo alishika wallet yake na kutoka business card yake na Kunipatia kisha akaniuliza.
“Jina lako Nani ??”
“Paula “
“Ooooh Walahi wakina Paula ni wazuri sana “
“Asante”
Basi niliingia bafuni na kuoga na kWa upande wa TINO alishika njia na kwenda kwenye shughuli zake za kila siku.
Kiukweli nilihudumiwa vizuri sana na baada ya hapo niliaga na kuondoka zangu.
Nilifika Nyumbani na kila mtu alikuwa na wasiwasi sana juu yangu.
“We Mbona upokei simu jamani “
Mama yangu aliniuliza uku akinisogelea Karibu zaidi.
“Ahaha Yaani acha nilitelekeza simu kwenye Pochi na nisiwe muongo Jana nililewa sana”
“Aaah umetutisha sana ujue. “
“Poleni sana Nimekuja mübadili Nguo niwai kwenda Kanisani mie “
“Sawa “
********
Basi siku ziliendelea kusonga na kwa upande wangu ndio nilizidi Kuwa Sawa zaidi mawazo juu ya jaden yalinitoka kabisa na nilianza kuyaishi maisha yangu.
Lakini pia kWa wakati huo, Mimi na TINO tulikuwa ni watu wa Karibu sana, TINO alikuwa mtu Mwema sana kwangu, alihakikisha Kuwa nakuwa na Furaha wakati wote, kuna muda nilitamani ata kuingia kwenye mahusiano lakini kila nikikumbuka tukio nililopigwa nikawa najiambia utakufa vibaya mbwa wewe 😂🙌.
Ikiwa ni siku ya weekend Mimi na TINO tulifunga safari na kwenda sehemu Fulani hivi nzuri sana Naa tulikuwa kwaajili ya kuoga Lea lakini pia kupata Chakula cha mchana.
“Aaaah we kweli ni bata maji 😂”
Alizungumza TINO baada ya kuniona naogelea sana.
Tukiwa bize tunaogelea gafla niliweza kumuona Zuri, nilibaki mdomo wazi baada ya kumuona TINO akitoka Ndani ya maji na kumkimbilia Zuri na kwa Furaha sana wakaumbatiana nika…….
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote