Sikuwahi kufikiria kwamba siku moja ningevaa vazi la harusi lililotengenezwa kwa ajili ya dada yangu. Sikuwahi kufikiria kwamba nitashika mkono wa mwanaume aliyekuwa wa kwake — na kupewa jina la mke wa mtu ambaye moyo wake haukuwa wangu.
Jina langu ni Raven Du Pont, na nimeishi maisha yangu nikitazama kwa ukimya jinsi upendo, fursa, na heshima vinavyomiminika kwa dada yangu, Hannah. Nilijifunza kutabasamu hata pale moyo wangu ulipokuwa ukivunjika. Nilijifunza kusimamia harusi yao bila kuonyesha maumivu yangu ya ndani.
Lakini siku ile Hannah alipotoroka, aliniachia mzigo mzito — kumrithi mwanaume ambaye moyo wangu ulimpenda kimya kimya kwa miaka mingi.
Ares Windsor — mtanashati, tajiri, mwenye nguvu… lakini pia ni mwanamume ambaye hakuwahi kuniona kwa jicho la mapenzi. Sasa, mimi ndiye mke wake. Si kwa sababu alinichagua, bali kwa sababu hakuwa na chaguo jingine.
Katika ndoa ya hila, sheria, na majeraha ya zamani, nimejifunza kuwa kimya siyo tena kinga. Nimeamua kupigania nafasi yangu. Sitaishi tena katika kivuli cha Hannah.
Nitaonyesha kuwa mimi ni zaidi ya mbadala. Mimi ni chaguo sahihi — hata kama ilibidi dunia nzima isijue hilo.
Na labda… labda, kwa wakati, hata Ares atagundua hilo pia.
SURA YA 1
RAVEN
Siwezi kuamini huyu mshenzi. Sierra alivamia ofisini kwangu kwa hasira huku akizungumza kwa sauti kali. Nikaweka penseli yangu mezani na kuachana na gauni la jioni nililokuwa nalichora — mawazo yangu yakirudi kwenye dunia ya kweli.
Baada ya wiki kadhaa za kukwama kifikra, leo asubuhi niliamka na maono mapya kabisa. Nilijua hasa nitachora nini kwa ajili ya cpllection yangu mpya mitindo. Lakini sasa, marafiki wa kweli wanapokuja, unalazimika kuwasikiliza kwanza.
"Asubuhi njema mpenzi," nilimwambia Sierra nikijaribu kuficha tabasamu. Yeye ni mtu pekee anayeniweza hivi. Nilijua anachotaka kusema kitakuwa na drama ya hali ya juu.
"Xavier Kingston ameiba wazo langu na kulifanya lake. Amechukua mradi nilioufanyia kazi kwa miezi mingi — kwa kutumia mawazo yangu!"
Nilirudi kwenye kiti changu huku nikimtazama rafiki yangu huyu mwenye nywele za kahawia zilizochangamka, zilizochafuka kwa hasira ya ghafla. Sierra huwa mtanashati kila siku, lakini leo amepasuka. Huyu Xavier amemgusa pabaya leo.
"Si wewe ndiye ulimharibia mkutano wake wa mwisho?" nilimuuliza. "Ulitoboa matairi ya gari lake ili achelewe kwenye kikao, ukijua mteja hachukulii uchelewaji kirahisi?"
Alitabasamu kwa ukatili, macho yake ya kijani yaking’aa kwa furaha ya kumbukumbu hiyo.
"Kama si hivyo, kampuni yake ingeweza kupata ule mkataba wa hoteli. Ilikuwa dili la mamilioni ya dola. Kwa kweli, nilivunjika moyo kuona ilikuwa rahisi hivyo kumchezea. Kwa kawaida huwa ana akili zaidi."
Nilitingisha kichwa nikimsikiliza kwa makini. Asingeondoka mpaka apate nafasi ya kulalamikia adui wake mkubwa, Xavier Kingston. Kampuni yake, King Enterprises, imekuwa mpinzani wa Windsor Real Estate tangu zamani — lakini urafiki huu wao umeenda mbali zaidi.
"Basi ungetarajia atajibu mapigo," nilimwambia.
Alinichoma macho kwa hasira ya kuchekesha, lakini alijua nipo sahihi.
"Nataka kulipiza kisasi," alisema kwa hasira. "Mpumbavu huyo! Siwezi kumvumilia tena. Raven, lazima unisaidie."
Nikachukua penseli yangu na kuitikisa. "Hapana. Usinitumbukize humo." Siko tayari kugombana na bilionea kichaa kama Xavier Kingston. Sierra ndiye mwanamke pekee anayemchezea bila kuumia — na sidhani kama anajua kuwa anakubaliwa tu kwa sababu anamvutia.
Simu yangu ilianza kuita. Nikaifikia bila kufikiria sana, kisha nikagandia jina lililoonekana: Ares.
Moyo wangu uliuma, nikatazama simu ikilia.
“Raven?” Sierra aliniita, sauti yake ikibeba wasiwasi.
Nilimtazama na kujilazimisha kutabasamu. “Ni kaka yako,” nilimwambia, kisha nikapokea simu.
“Halo, Ares,” nilisema kwa utulivu, nikijaribu kuficha mparaganyiko wa hisia moyoni mwangu.
Alicheka kidogo, na sauti yake iliniletea msisimko wa ghafla. “Raven, nashangaa umepokea simu. Hivi karibuni imekuwa vigumu kukupata. Hata unanizidi shughuli.”
Nikainama nyuma kwenye kiti na kutabasamu. Imekuwa muda tangu nimsikie akisema jina langu kwa namna hiyo. “Kuna nini?” nilimuuliza, nikijua lolote atakalosema litaniumiza. Ares ni ushaishi mbaya kwangu — siri chafu nisiyoweza kuiacha.
"Unataka kuja dukani na mimi? Nahitaji kununua zawadi ya siku ya kuzaliwa ya Hannah, na nani wa kunisaidia kama si wewe?"
Nilipaswa kusema hapana. Sitaki kabisa kusindikiza mwanaume ninayempenda kununua zawadi kwa dada yangu. Lakini pia, bora nimuone akifurahia juu yake kuliko nisiwe naye kabisa.
"Sawa," nilimjibu, nikiwa najilaumu tayari.
Sierra alinikazia macho baada ya simu. "Alitaka nini?" aliuliza kwa hasira. “Anataka zawadi ya Hannah,” nilimjibu kwa tabasamu la kukata tamaa.
Sierra alikaza taya zake na kugeuka. “Usiende,” alisema kwa sauti ya chini. “Rave, tafadhali usiende. Ares anaweza kufikiria mwenyewe zawadi. Kwa nini bado anakugeuza msaada wa mahusiano yao?"
"Ni sawa," nilimwambia, ingawa nilikuwa sina uhakika. Imepita miaka mingi, lakini bado siwezi kumkataa chochote.
"Hapana," Sierra alisema. “Nakupenda kama ninavyompenda kaka yangu, lakini huu uhusiano wenu unakuumiza. Unatakiwa kujifunza kujiweka mbali naye. Kila unavyomuona, moyo wako unavunjika tena."
Nilitikisa kichwa. “Sisi ni marafiki tu, Sierra. Tangu zamani.”
Alikunja mikono yake kifuani na kunikazia macho. “Ujilinganishe utakavyo, Rave, lakini huwezi kunidanganya.”
Nilitazama pembeni. Sierra ndiye pekee anayejua kilichotokea zamani — na ingawa nimekuwa nikikanusha, ukweli ni kuwa bado nampenda Ares Windsor, kama zamani.
Endelea….
SURA YA 2
RAVEN
Moyo wangu uliruka kwa furaha nilipomuona Ares amesimama mbele ya jengo la ofisi yangu, akiwa amesimama kando ya gari lake. Alionekana mtulivu na mwenye mvuto ule ule ambao huwa haueleweki, lakini unanifanya nipotee kila mara.
Nilisimama kwa sekunde chache kumtazama. Nywele zake nyeusi zilikuwa zimepangika vizuri, taya yake iliyochongwa kwa umbo kamili, na yale macho yake ya kijani yaliyofanana kabisa na ya dada yake Sierra. Haki ya Mungu, anazidi kuwa mtanashati kadri miaka inavyosonga mbele — na kila ninavyomuona tena, ndivyo anavyokuwa mbali zaidi na mimi.
Ares aliponiangalia, alinyanyua kichwa chake kidogo na kutabasamu, uso wake ukibadilika kwa upole wa kushangaza.
“mammbo!” nilimwambia huku ananifungulia mlango wa gari lake. Alitabasamu zaidi nilipotabasamu, na kwa mara nyingine, nilijua nitajuta uamuzi wa kutoka naye leo — lakini niliamua kufurahia kila sekunde.
“Tunaenda wapi?” nilimuuliza alipokaa kando yangu, mikono yake ikiwa kwenye usukani.
Aliegemea kwenye kichwa cha kiti na kunitazama kwa upande, sauti yake ikiwa ya manung’uniko yaliyobeba hisia nzito. “Raven,” alisema kwa upole wa ajabu. Nilijikuta nikimgeukia, moyo wangu ukipiga kwa kasi. “Kwa nini siku hizi huonekani?”
Sauti yake ilibeba masikitiko, kana kwamba alinikosa kweli. Moto niliokuwa nikijaribu kuuzima mioyoni mwangu ulianza kuwaka tena.
“Nimekuwa tu bize,” nilijibu kwa sauti ya chini isiyo na uthibitisho. “Nina mikataba mingi ya uanamitindo na bado najaribu kukuza chapa yangu ya mavazi. Wakati mwingine hata muda wa kula au kulala haupo.”
Alinyoosha shingo na kutazama mbele, uso wake ukiwa na mashaka na wasiwasi, lakini alitikisa kichwa kwa uelewa. “Usijichoshe sana, Rave. Jitunze. Unahitaji maisha ya kijamii pia. Uliwaona wazazi wako lini mara ya mwisho?”
Nilitabasamu kwa kujilazimisha na kukunja mikono. Kwa miaka ya karibuni, mahusiano yangu na wazazi wangu yamekuwa ya mbali. Dunia yao inamzunguka Hannah tu. Mimi ni kivuli. “Sierra alikuwa ofisini kwangu leo,” nilimjibu kwa kupotezea. “Bado nina marafiki, unajua.”
Alinitazama kwa jicho lile lile analotumia kunielewa, kana kwamba anaweza kunisoma kupitia uongo wangu — lakini hakusema kitu.
“Unataka kununua zawadi gani mwaka huu?” nilimuuliza kwa sauti ya kirafiki. Alinitazama tena kwa tabasamu. “Vipi kuhusu vito? Labda cheni au pete?”
“Ningependelea cheni yenye mvuto wa kipekee.”
Alinichungulia kwa mshangao kana kwamba hakujua ninachomaanisha, nikalazimika kucheka. Alicheka naye, tabasamu lake likinifanya nihisi joto moyoni. “Sijakusikia ukicheka kwa muda mrefu, Raven. Nilikumisi.”
Tabasamu langu lilitoweka polepole. Maneno yake yalikuwa kama sindano. Yeye huniona tu kama rafiki wa zamani — na sasa, shemeji mtarajiwa. Lakini anaposema amenimisi, ni vigumu kujifanya kuwa sihisi chochote.
Alipaki gari kwenye moja ya maduka ya kifahari ya familia yao na akakimbia kunifungulia mlango. Alinipa mkono wake, nami nilishuka nikimtazama.
Ghafla mwanga mkali uling’aa upande wetu. Nikageuka na kumwona mpiga picha maarufu ambaye amekuwa akinifatilia siku za karibuni. Nilijiandaa kumkabili, lakini tayari alikuwa anakimbia.
Ares akaweka mkono wake chini ya mgongo wangu na kunisogeza. “Nilipaswa kujua kuwa kukuleta sehemu za wazi kungetuletea matatizo. Samahani, Raven. Nitashughulikia picha hiyo.”
“Ni sawa,” nilimwambia. “Nimeshazoea. Huwezi kuacha kuishi kwa sababu ya kamera. Hapo awali nilikuwa naogopa sana. Sasa ni kero tu ya kazi yangu.”
Alikuwa kimya tulipoingia dukani. “Labda nikutafutie walinzi wa kukulinda,” alisema kwa sauti ya hasira iliyofichika.
“Hapana,” nilikataa. “Sitaki mtu ndani ya nafasi yangu binafsi muda wote. Bado sihisi tishio.”
Tuliingia kwenye moja ya maduka ya vito anavyovipenda Hannah. Meneja wa duka, mwanaume mwenye mvi zilizoonekana kupendeza, alitukaribia kwa haraka na heshima. Alinitazama kwa njia niliyozoea kutoka kwa wanaume — ile macho ya picha zangu za ndani ya mavazi.
Ares alikasirika. Alinivuta mbali na yule mwanaume. “Alikutazama vibaya. Huu ni upuuzi.”
Nikacheka kimya kimya. “Ares, mimi si msichana yule wa zamani. Sasa mimi ni mmoja wa wanamitindo wanaolipwa zaidi duniani. Wengi wananifahamu. Usistuke.”
Alinitazama kwa mshangao lakini hakusema zaidi. Tulitembea mpaka kwenye sehemu ya mikufu ya shingoni. Nikamwonyesha cheni ya almasi aina ya choker.
“Vipi kuhusu hii?”
Alimwita Andy aje aitupatie. Ares akainyoosha nyuma ya shingo yangu, akinipunguzia nywele kwa upole. Mikono yake iliponigusa kwenye ngozi, nilihisi mwili wote ukitetemeka — lakini sidhani kama aligundua.
"Jaribu kuivaa," aliniambia.
Nikatikisa kichwa. “Hii ni kwa ajili ya Hannah. Najua atapenda.” Alitikisa kichwa na kunivalisha cheni hiyo. “Ukipenda, nitakunulia wewe. Tutaangalia nyingine kwa ajili ya Hannah.”
Macho yangu yakapanuka. “Ni kubwa sana.” Nilishika cheni nyuma ya shingo. “Lakini asante. Atapenda sana. Hii ndiyo zawadi bora kwake.”
Ares akaitoa polepole, macho yake yakinitazama kwa upole ambao sikutaka kuukubali.
“Rave,” aliniita kwa sauti ya chini. “Tuko sawa? Sijui kwanini siku hizi hunipigii, hatonani tena.”
Nikamsogelea na kutabasamu. “Tuko sawa, Ares. Nimekuwa bize tu.” Alinitazama kwa macho yanayoelewa uongo. Lakini aliniacha niendelee. Na moyoni, nilijua — jinsi alivyonitazama, bado hajui kuwa moyo wangu ulikwishampenda kwa miaka mingi. Na najua, sikuwahi kuacha.
SURA YA 3
RAVEN
"Siwezi kuwaweka familia ya Astor karibu sana na kaka zake Ares," mama alisema. "Lazima tuwaalike, familia yao inalingana na ya kina Windsor… lakini hatuwezi kuwaweka karibu nao. Kwa ninavyokumbuka, Adrian Astor hampendi kabisa kaka yake Ares, Lexington."
Nikainua kichwa kutoka kwenye karatasi zangu. “Adrian hampendi Lex?” nilimuuliza kwa mshangao. “Mbona sikujua hilo?”
Mama alitikisa kichwa kwa haraka. “Ndivyo nilivyosikia. Inasemekana Adrian hakubaliani na tabia ya utani kupita kiasi ya Lexington.”
Nikatazama chini nikitabasamu kimya kimya. Lex anapenda kuchokoza — na sina shaka alimtania Leia, dada wa Adrian. Naam, naweza kuelewa ni kwa nini Adrian hachukulii hilo kwa urahisi.
“Sawa basi, tutaweka meza zao mbali,” nikasema.
Mama alitikisa kichwa, akihamisha majina ya meza kwenye mfano wa ukumbi wa harusi aliouagiza kutengenezwa. “Kila kitu lazima kiwe kamilifu,” alisema kwa sauti ya chini. “Hannah amengoja siku hii kwa muda mrefu.”
Nilibana meno ili nisiangalie juu. “Yeye mwenyewe ndiye aliyoiahirisha harusi mara tatu, Mama. Haonekani kuwa na haraka sana.”
Mama aliniangalia kwa haraka, hasira ikijitokeza machoni mwake. “Hiyo ni kwa sababu kazi yake ni ngumu, Raven. Huwezi kuelewa maisha ya kuwa muigizaji. Wewe kazi yako ni kusimama tu na kuonekana mrembo — lakini Hannah? Anateseka kwenye seti zisizo na starehe, mbali na familia kwa wiki nzima. Unafikiri alitaka kuahirisha harusi? Hana hiari. Huwezi kuelewa, lakini ikiwa huna la kusema jema, ni bora unyamaze.”
Nilimeza mate nikijizuia kujibu. Anajua jinsi kazi ya uanamitindo inavyoweza kuwa ngumu — wiki chache zilizopita nilipata hypothermia kwa sababu nililazimika kupiga picha kwenye barafu. Lakini nadhani kwake, siwezi kamwe kufikia kile Hannah amekuwa.
Nilishika faili la orodha ya watoaji huduma kwa mikono inayotetemeka. “Kwa nini bado ninajirudisha hapa?” nilijiuliza kimoyomoyo. “Kwa nini ninarudi kusaidia kupanga harusi ya dada yangu na mtu niliyempenda kwa miaka mingi?”
Mama akaniangalia tena, sauti yake sasa ikibeba ukali uliofichwa na majuto. “Samahani, Raven. Harusi hii imenitia mkazo sana, na nimekuwa nikikutoa hasira zangu. Nakuomba msamaha, binti yangu. Unaelewa, sivyo? Harusi hii ni
muhimu kwa familia zote mbili. Mkataba huu wa biashara umekuwa ukisubiri kwa miaka. Harusi ikiisha, tutasaini nyaraka na kuwakabidhi kampuni kwa Ares na Hannah. Familia ya Windsor hawataki kuendelea mbele mpaka ndoa ifanyike — na baba yako na mimi tunahitaji msaada wao kifedha.”
Nilikunja kichwa na kusema polepole, “Naelewa, Mama.”
Mama alitabasamu kwa upole. “Wewe ni msichana mzuri sana, Raven. Hannah na mimi ni watu wenye bahati kukupata.”
Nilitabasamu kimya kimya, nikitafuta faraja kwenye maneno hayo machache mazuri aliyoyasema. Nilijua Hannah hatajihusisha kabisa na maandalizi ya harusi, na ingawa inauma kuhusika katika kitu kinachoumiza moyo wangu, angalau nimespendi muda na mama. Ni nadra kwa sisi kuwa karibu.
“Siwezi kuamini binti yangu mrembo atakuwa mke wa mtu muda si mrefu,” Mama alisema kwa upole, akitazama mfano wa bustani ya mizabibu ambako harusi itafanyika.
Kisiki kikali cha huzuni kilinikaba koo. Sikuwa na haki ya kumwonea wivu dada yangu. Lakini ndani yangu kulikuwa na maumivu. Sikutarajia mengi kutoka kwa mama, ila nilitamani upendo wa kawaida — hata wa kiasi tu.
“Gauni lake limefikia hatua gani?” Mama aliuliza kwa wasiwasi. “Umeweza kufanya mabadiliko aliyotaka?”
Nilitikisa kichwa. “Ndiyo. Kila mara anapobadilisha tarehe, hubadilisha kila kitu, hata gauni — kwa hiyo nashughulikia upya kila mara. Lakini nimeshaikamilisha.”
Mama alikaa kimya kwa sekunde kadhaa, kisha akasema kwa upole, “Ni jambo zuri kwamba alikuomba umtengenezee gauni lake. Hiyo ni njia nzuri ya kukujumuisha. Nilifikiri angechagua brand maarufu, lakini hii itakusaidia kupata umaarufu zaidi. Ukumbuke, Hannah ni mtu wa ushawishi mkubwa.”
Nilimeza mate na kusema kwa sauti ya chini, “Nimeshinda tuzo kadhaa za mitindo, Mama. Chapa yangu ina orodha ya wateja wanaosubiri kwa miaka miwili. Na orodha hiyo imeongezeka tangu Alanna Sinclair alivyoolewa akiwa amevaa gauni kutoka kwangu.”
Mama alinitazama kwa tabasamu la kujifanya — tabasamu lile la ‘sawa’ ambalo linaniuma zaidi. “Bila shaka,” alijibu kwa haraka.
Kisha akainua kadi ya mialiko. “Hakikisha hizi zinafika mikononi mwa wageni siku tatu kabla ya harusi. Harusi hii ni ya siri. Paparazzi wakifika, itaharibu kila kitu.”
Nilisimama taratibu na kusema, “Nitashughulikia kesho.”
Mama alinitazama kwa mshangao. “Hutakaa chakula cha usiku?” “Hapana. Nipo na shughuli mapema kesho.”
Mama alitikisa kichwa. “Vizuri. Usiendelee kunenepa sana — hutapendeza kwenye gauni lako la maid of honor.”
Niligeuka na kutoka, moyo wangu ukiwa kama umefinywa. Kila mara ninapoondoka nyumbani, najihisi kuwa mtu mbaya — mtu asiye na furaha kwa sababu ya mafanikio ya dada yake. Na kisha ninajichukia kwa sababu ya hilo.
Lakini mawazo mabaya haya yananitesa sana siku hizi.
Vipi kama Ares angekuwa wangu?
Vipi kama sikumleta Hannah kwenye sherehe ile ya Sierra?
Vipi kama nisingekubali kupanga harusi hii?
Vipi kama ningemwambia Ares ukweli?
Najua, hayo ni mawazo ya mtu aliyejaa wivu. Lakini kwa kila kurudi nyumbani, ninajiona kuwa mtu asiyeweza kujizuia — ninakuwa kivuli cha kile nilichotamani kuwa.
Endeleaa..
SURA YA 4
ARES
Nilikaza mkono wangu kwenye simu, nikavuta pumzi ndefu nikiwa nimekasirika. “Hannah, uliahidi tutakwenda wote. Hii ni mara ya tatu mwezi huu unaniambia dakika za mwisho kwamba huwezi kuja. Hata kunipa taarifa mapema umeshindwa?”
Simu ikasikika ikigugumia, kisha sauti ya Hannah ikaja, dhaifu na ya kujitetea. “Samahani, Ares. Nilitaka sana kuwa hapo leo. Unajua ningependa kumwona Raven na kuwa na wewe, lakini siwezi kuondoka. Kuna vipande vya filamu vinatakiwa kurudiwa, na hali haiendi vizuri.”
“Ni sababu zile zile kila wakati, Hannah. Ninajitahidi kukuunga mkono kadri niwezavyo, lakini unazidi kunifanya nione haya mahusiano haya ni ya upande mmoja.”
“Najua,” alisema kwa sauti ya huzuni. “Nitakufidia.”
“Ndio maana? Hutaki watu waone tupo pamoja?” Nilivuta pumzi kwa hasira. “Hannah, tunafunga ndoa baada ya mwezi mmoja. Tulikubaliana kuwa tukishaoana, tutatangaza uhusiano wetu hadharani. Sasa leo tu hauwezi kujitokeza?”
“Ares, siyo hivyo. Sikutaka kuwa mbali, ila najua nitakuwa likizo kwa ajili ya harusi, na nataka kazi yangu iendelee vizuri. Sitaki mimi niwe sababu ya ucheleweshaji.”
Nilinyamaza, nikitazama dari la ofisi yangu. “Naelewa,” nilisema kwa sauti ya kushindwa. Hata kama namwelewa, najihisi kuchoka. Nilifikiri mimi ndiye mwenye bahati kati ya kaka zangu. Dion haongei hata na mchumba wake. Wengine bado hawajachaguliwa wake. Mimi ndiye niliyempata yule niliyempenda hata kabla ya ndoa.
Lakini siku hizi, nahisi kama nipo peke yangu kwenye uhusiano huu. Mambo yanahisi kama masharti, siyo upendo.
“Hannah hatakuja, siyo?”
Niligeuka na kumkuta mdogo wangu, Lex, amesimama mlangoni. Uso wake haukuwa na hisia nyingi, lakini macho yake yalionesha kuchoshwa. Nilihisi kutetea Hannah, lakini sikuwa na nguvu.
“Hatakuja.”
“Inamaanisha utabaki peke yako tena kwenye hafla ya leo?” Lex aliuliza. “Unajua wanawake wanavyokuwa kwenye matukio kama haya — utazidi kusumbuliwa usiku mzima.”
Nilitikisa kichwa. “Sawa tu. Wewe una safari ya asubuhi, si ndiyo?” Nilijaribu kuhamisha mazungumzo. Pia, Lex huwa hapendi tasnia ya burudani. Yeye ni mkuu wa idara ya magari katika biashara za Windsor.
“Kama kawaida, Raven atakuwepo. Yeye ndiye nyota wa onyesho leo. Hajawahi kuonekana mzuri hivi. Laiti ningekuwa na muda ningeenda.”
Nikakaza misuli. Tangu lini aliona Raven ni mzuri hivyo? Si alikuwa kama dada yetu mdogo? Je, amebadilika machoni mwake?
“Umejuaje atakuwepo?”
Alinionesha simu yake. “Nimeongea naye leo.”
Moyo wangu uliganda. Mimi najaribu kumtafuta kila mara, hapokei. Lakini kwa Lex amempigia simu?
“msalimie Raven,” alisema Lex akitabasamu.
Nilikunja uso, nikiapa sitamsalimia. Hisia za wivu zilinishika — na si kwa sababu ni kaka yangu, bali kwa sababu siwezi kuvumilia mtu mwingine kumtazama Raven kwa namna ile.
Nilielekea kwenye tukio nikiwa na hali ya kiroho iliyochafuka. Sina uhakika nini hasa kilichonikera zaidi — kutoonekana kwa Hannah, au mawazo yangu kuhusu Raven.
Nilipoingia kwenye ukumbi wa tukio, macho yangu yalitua moja kwa moja kwenye jukwaa. Raven alikuwa anatembea, akivaa gauni linaloambatana na kila mvuto wa uumbaji. Gauni hilo lilikuwa na umbo linalofichua kila sehemu ya mwili wake wa kipekee.
Nilimwangalia bila kupepesa macho. Sijawahi kuona uzuri kama huu. Mwanamke huyu ambaye alikuwa rafiki wa dada yangu — na karibu nami tangu zamani — sasa anaonekana kama malkia. Ni ajabu. Hannah pia ni mrembo, lakini Raven... yeye ni moto wa roho.
Nilikumbuka vizuri, miaka ile nyuma, wakati bibi yangu alipendekeza ndoa ya kufanikisha muungano wa familia. Wakati huo, waliompendekeza kuwa mke wangu hakuwa Hannah. Alikuwa Raven.
Sasa namtazama akirudi jukwaani, na moyo wangu unatetemeka. Ndio kwanza naanza kuhisi — labda tulifanya makosa.
SURA YA 5
ARES
“Ongeza uandishi wa habari juu ya hili,” niliagiza, nikitazama picha na makala zinazomhusu Raven na chapa yake ya mitindo. Sikujua hadi jana kwamba baadhi ya mavazi kwenye jukwaa yalikuwa kutoka kwenye chapa yake. Kwa
maoni niliyoyaona, watu wamepokea mkusanyiko wake vizuri — na anastahili zaidi ya anachopata.
Naamini katika kutumia ushawishi wangu vizuri. Kama ninamiliki majarida kadhaa ya mitindo na burudani, kwa nini nisiyatumie kumsaidia rafiki yangu?
Ninatumaini kampuni yake itaendelea kukua hadi atakapolazimika kuacha kazi ya uanamitindo kwa sababu ya muda.
Sikupenda kuona jinsi anavyotazamwa na wanaume kama kitu — hawamwoni kama mtu halisi, mwenye akili, ndoto, au moyo. Wanamwona kama picha. Kama hisia. Kama tamaa tu. Ndio maana natamani aachane na kamera, na aendelee kama mbunifu mzuri wa mavazi aliyekuwa akijenga jina lake hatua kwa hatua.
Dom, katibu wangu, akaingia ofisini na kusema, “Bradford Manson alipiga simu. Alitaka kujua kuhusu ule muswada aliyoleta. Kwa mujibu wa maoni yako, tulikuwa karibu kuidhinisha fedha kwa ajili ya mradi wake. Niiendeleze?”
Nikakaza meno, nikamkodolea macho. “Hapana,” nilimwambia kwa sauti iliyojaa hasira. Akili yangu ilirudi kwa tukio la jana, pale nilipomsikia mtu huyo akimdhalilisha Raven mbele yangu — akimtolea ofa ya ‘tarehe moja’ kwa hela nyingi kuliko anazopata kwa mwaka.
“Hatutaendelea naye. Nataka kila mtu ajue: yeyote atakayefanya kazi na Bradford Manson hatatambuliwa tena na Windsor Media. Na wala hatutafadhili chochote kinachohusiana naye. Tuweke wazi.”
Dom alitazama kwa mshangao. “Unajua hii ni kama kihama kweli, sivyo? Jina lake halitasikika tena.”
Nilitabasamu kwa uchungu. “Ameshavuka mstari. Na wala sijutii. Raven hastahili hilo.”
Dom alitikisa kichwa na kuondoka kwa haraka, tayari kuanzisha mashambulizi ya kisiasa ya kifedha.
Lakini kabla hajaondoka kabisa, nikasema kwa sauti: “Ngoja. Kuna meneja wa duka la vito… Andy. Yule aliyekuwa kwenye duka la Hannah analopendelea. Nataka aondolewe. Leo.”
Dom alijisemea kwa wasiwasi, “Eeh, hilo lipo upande wa mali isiyohamishika — upande wa Sierra. Najua hutakiwi kuingilia…”
Nilimtazama kwa macho ya msumeno. “Mwambie Sierra — Andy alimkazia macho Raven kana kwamba ni bidhaa. Kama kweli anajali rafiki yake, hatahitaji sababu nyingine ya kumuondoa.”
Dom aliondoka akiwa na hasira iliyokolea kwenye sura yake — Raven si tu rafiki yangu, bali ni mpendwa kwa wote.
Nilikaa kwa dakika kadhaa kimya, nikitazama dirishani. Mawazo yangu yakirudi kwa tukio lile la jana — la Raven, akiwa kwenye jukwaa, akiwa na furaha ya kweli machoni mwake kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Aling’aa.
Niligusa simu yangu, nikakaza uso. Kisha nikapiga simu kwa mtu ambaye sipendi hata jina lake — Silas Sinclair.
“Ares Windsor,” nilisema mara tu alipopokea.
“Ninajua. Kuna caller ID siku hizi.” Sauti yake ilikuwa na dhihaka ya kawaida. Nampenda Raven — lakini Silas? Hapana.
“Nahitaji walinzi wawili wa kipekee zaidi. Lakini kuna masharti.” “Nasikia.”
“Lazima wawe wasiri. Wasimjulishe Raven kwamba wanamlinda. Sitaki hata ahisi. Lengo ni kumzuia asifikwe na watu kama Bradford — kabla hata hajajua kuna tishio.”
Silas alicheka. Kicheko kile nilichokichukia miaka yote. “Ni nani huyu anayehitaji ulinzi wa aina hiyo? Mchumba wako?”
Nilinyamaza kwa sekunde kabla sijajibu kwa sauti ya ndani kabisa: “Raven Du Pont.”
Kimya kilitanda kwa sekunde chache. “Ungefanya yote hayo… kwa ajili yake?” aliuliza.
“Ndio,” nilijibu.
“Utalipia,” alisema kwa upole wa kishetani.
“Kwa kiasi gani?” niliuliza.
“Sio pesa. Nataka favour moja — kuitumia wakati wowote, huwezi kukataa.”
Nilikaza taya. Ninamchukia Silas, lakini hakuna mwingine mwenye uwezo wake.
“Ndio,” nilikubali. “Muda wowote — mradi haivunji maadili yangu.”
“Done,” alisema. “Na kwa kwataarifa yako, Raven tayari alikuwa analindwa na watu wangu kwa miaka mingi — bure. Wewe umelipa gharama kubwa kwa kitu ambacho nilikuwa nafanya bure. Jiulize, Ares… kwa nini?”
Akanikatia simu. Na nikaachwa nikiwa na hasira, mchanganyiko wa maswali, na hisia za kushindwa.
SURA YA 6
ARES
Nina wasiwasi ninapopaki mbele ya jumba la familia ya Du Pont. Nilipaswa kuwa na furaha kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Hannah leo usiku, lakini mambo kati yetu hayajawa sawa kwa muda, na inazidi kuwa ngumu kwangu kupuuzia hali hiyo.
Tukiwa na wiki chache tu kabla ya harusi yetu, kila tatizo tulilowahi kuwa nalo linaonekana kuzidi kuwa kubwa. Labda ni baridi ya mwisho kabla ya ndoa, lakini nahisi ni zaidi ya hilo. Sehemu ya nafsi yangu inajiuliza kama sababu pekee ya sisi kuanza kutoka kimapenzi ni kwa sababu tulijua kuwa hatimaye tungekuwa pamoja, kupitia ile ndoa iliyopangwa na familia.
Isipokuwa... je, kweli tungekuwa? Mwanamke ambaye wazazi wangu walitaka nioe alikuwa Raven. Kama singefanya… kama usiku ule usingetokea, je, ningekuwa naoa Raven sasa?
Napitisha mkono kwenye nywele zangu na kuvuta pumzi kwa shida. Sasa hiyo haijalishi tena. Hatuwezi kurudi nyuma kwenye wakati uliopita, na kama ni hofu au la, nitalazimika kumuoa Hannah kama nataka kubaki na kazi yangu na urithi wangu.
Ninajituliza nikitoka ndani ya gari, nikihisi kama niko nje ya mwili wangu. Hivi karibuni, sijisikii kama mimi mwenyewe, na siwezi kuelewa ni kwa nini. Hii si tu kuhusu harusi. Ni zaidi ya hapo.
“Ares!”
Ninainua macho na kumwona baba yake Hannah akiwa amesimama mlangoni,
akitabasamu kwa upana. Ni muda umepita tangu nimuone mara ya mwisho, na sina shaka kuwa ana chupa nzuri ya scotch anayotaka kushirikiana nami. Kuhusu baba mkwe wangu wa baadaye — bila shaka, nimepata zawadi ya maisha. Ni mtu mwema kwa dhati, na haraka aligeuka kuwa kama baba wa pili kwangu. Anafanya pengo la baba yangu mwenyewe kuwa jepesi kidogo kubeba. Maumivu ya kuwapoteza wazazi ghafla hayaishi, lakini hupungua kadri muda unavyopita.
“Arthur.” Namkumbatia na kupeana naye mikono kabla hajaniingiza ndani, huku vicheko vikisikika tunapokwenda hadi kwenye patio ya nyuma.
“Kazi imekuwaje, mwanangu? Sijakuona sana. Unalala hapa usiku wa leo?” Ninatikisa kichwa. “Kazi imekuwa nyingi, lakini nimeachia nafasi ya wikendi.”
Hannah anainua macho anaponiona nikimkaribia, nikiwa na zawadi ya siku yake ya kuzaliwa mkononi. Kwa bahati nzuri, leo ni usiku wa familia tu na marafiki wake wa karibu. Matukio makubwa huleta msongo mkubwa kwetu
wote, na hivi karibuni, yameongeza presha kubwa sana katika uhusiano wetu. Usiku wa leo ndio tulichohitaji hasa.
Ninamkumbatia na kumnong’oneza kwa karibu kabla sijampiga busu la haraka shavuni.
“Hey, Han,” ninasema kwa sauti ya chini, kisha namkabidhi zawadi yake. “Ares,” anasema huku akitabasamu. “Siwezi kusubiri kuona ni nini kilichomo!”
Marafiki zake wanamzunguka anapofungua boksi, wote wakiwa na msisimko uleule. Wote ni waigizaji pia, kwa hiyo huwa siwezi kujua kama furaha yao ni ya kweli au maigizo tu.
“Ni nzuri sana,” anasema. “Unaweza kunisaidia kuivaa?”
Nikatabasamu na kuchukua mkufu huo, kisha namfungia nyuma ya shingo.
“Unapendeza sana ukiuvaa,” ninasema kwa sauti ya chini, ingawa akili yangu inapiga picha ya Raven alivyouinua mkufu huo shingoni mwake.
Hannah ananiangalia machoni na kutabasamu. “Nilikuwa nashangaa kwa nini kulikuwa na picha za paparazzi zikionyesha wewe na Raven pamoja. Kusema kweli, kuonekana pamoja katika duka la vito kulizua tetesi nyingi zisizoeleweka. Kumbe ni kwa ajili ya zawadi hii.”
Ninatikisa kichwa kimya. Tangu Raven awe maarufu, ameacha kutoka mara kwa mara, na naelewa kwa nini. Vyombo vya habari hupagawa kabisa kila wanapomuona hadharani. Siku hizi, humuona tu Windsor Estate au akiwa na Hannah. Umaarufu haujambadilisha kama ulivyombadilisha Hannah — badala yake, umemfanya kuwa mtu wa kujificha zaidi.
Marafiki wa Hannah wote walimzunguka wakati alipokuwa akijionyesha na mkufu wake mpya, nami nikavuta pumzi ndefu niliporudi hatua moja nyuma. Si jambo la kawaida kwa Hannah kupata usiku wa mapumziko akiwa na watu wake wa karibu, kwa hiyo nilikuwa na furaha kumpa nafasi.
Ninayo usiku mzima kuwa naye, mwishowe.
Nikajichotea kinywaji na kuelekea kwenye bembea ya kona — wala sikushangaa hata kidogo nilipomkuta Raven ameketi pale, macho yake yakiwa yamegandia tablet yake. Bila shaka alikuwa anachora miundo mipya ya chapa yake ya mitindo, nami nikatabasamu kimya.
Niliketi kando yake, nikaanza kuisukuma bembea ile polepole. Alinigeukia, macho yake yakikutana na yangu.
“Ares,” alisema. Kuna namna ya kipekee anavyosema jina langu — huwa tofauti. Ni kama mraibu wa kitu usichoweza kuelezea.
“Kwa nini umekaa hapa peke yako, Cupcake?”
Alicheka — sauti laini, safi, ya kupumzika katikati ya kelele bandia za vicheko vilivyotuzunguka.
“Utaendelea kuniita hivyo maisha yetu yote?” aliuliza.
Nilinod nod. “Bado nakumbuka ile keychain ya cupcake, t-shirt, na pini uliyokuwa nayo kwenye begi lako. Ulikuwa na mapenzi makubwa na cupcakes.”
Alinikazia macho kwa mchezo, lakini bila hasira.
“Nilikuwa na miaka kumi na nne! Nilikuwa kwenye kipindi cha maisha. Nafikiri nashukuru hatukukutana wakati nikiwa kwenye phase ya emo — hiyo ingekuwa balaa la mwaka.”
Nilitabasamu nikatazama sketch ya gauni la jioni aliyokuwa anachora. Daima hunishangaza ni kwa kiasi gani Raven ana kipaji kikubwa.
“Hujanijibu swali langu,” nilimkumbusha. “Kwa nini umekaa hapa peke yako? Hupaswi kuwa unasherehekea na dada yako?”
Alifunga tablet na kunitazama.
“Nilijaribu,” alisema kwa sauti iliyovunjika, kisha akalazimisha tabasamu usoni.
Naam, huenda alijaribu kweli. Raven daima hujaribu. Sikuwahi kuelewa kikamilifu, lakini wazazi wake wamekuwa wakimpa Hannah nafasi ya kipekee kila mara — wakimuweka katikati ya kila kitu. Tulikutana kwa mara ya kwanza baada ya wazazi wake kufuta likizo yao ili wamsindikize Hannah kwenye usaili, hivyo Raven akaenda likizo na Sierra badala yake.
Hannah pia anafanya hivyo. Anamchukulia dada yake kama kitu kilichopo tu. Na naamini anajua.
Raven ndiye amepanga kila undani wa harusi yetu. Hata leo, amekuja hapa kwa sababu anajua Hannah angesikitika asingeonekana — lakini Hannah hajafanya jitihada yoyote kuhakikisha Raven anahusishwa.
“Pole Cupcake. Inaonekana tupo boti moja usiku wa leo.”
Alitikisa kichwa.
“Yeye huwa anawaona marafiki zake mara chache sana. Si rahisi kwake kama ilivyo kwetu. Ninalielewa.”
Raven huwa anafanya hivi — anatafuta sababu ya kumlinda Hannah. Anafanya hivyo kila wakati. Je, hata anatambua hilo?
“Nionyeshe unachochora.”
Alitikisa kichwa na kuegemea kwangu, mkono wake ukigusa wangu kwa upole, upepo mkali ukitukumbatia.
“Nafikiria kutumia rangi mbalimbali za ‘nude’ zenye mapambo mazito. Mtindo wa kushikamana na mwili, lakini wa heshima.”
Aliendelea kubadilisha kurasa, nami nikajawa na hisia za fahari. “Wewe ni wa kipekee. Unajua hilo, siyo?”
Aliniangalia kwa mshangao. Napenda jinsi mashavu yake hujaa aibu kila ninapomsifia. Yeye ni mtu maarufu, anapendwa na mamilioni — lakini bado
hujawa na haya ninapomwangalia tu.
Raven ni wa ajabu kweli. Na najivunia kumwita rafiki.
“Hey, nina kitu kwa ajili yako. Najua bado mapema na siku yako ya kuzaliwa ni mwezi ujao, lakini nadhani utafurahi kuwa nayo sasa.”
Nikamkabidhi mfuko mdogo wa karatasi niliobeba, na akautazama kwa mshangao. Nikamtazama kwa makini alipofungua boksi ndani yake, moyo wangu ukigonga kama kengele ya wasiwasi. Ni lini mara ya mwisho nilihisi hofu kwa zawadi rahisi tu?
Raven akapumua kwa mshangao.
“Ares! Hii tablet bado haijatoka sokoni! Nilikuwa nimeiweka oda mapema — haitatoka hadi miezi sita ijayo. Umewezaje—”
Aligeuza kifaa hicho na kutabasamu zaidi alipoona cupcake ya enamel upande wa nyuma.
“Wow. Wewe… umewezaje?! Hawa hawatengenezi za aina hii!”
Naam. Hii ilikuwa zawadi ya thamani — hata kama ilimaanisha kuvumilia mzaha wote kutoka kwa Lexington, nilipomlazimisha amuombe Aria Callahan msaada. Kama ningemjua Aria binafsi, nisingemhusisha Lex. Lakini niliamini angefanya hivyo kupitia uhusiano wake na familia ya Grant, hasa kwa kuwa Amara na Leia ni marafiki wa karibu wa Lex.
“Najua mtu anayemjua mtu anayemjua mtu mwingine,” nilimjibu kwa mafumbo. Hakuna njia nitampa Lex ushindi wa zawadi hii. Hakustahili tabasamu hilo kutoka kwake. Mimi ndiye niliyestahili.
“Naiipenda!” alifurahi. “Siwezi kuamini umefanya hivi kwa ajili yangu. Wewe huwezi kabisa kuchagua zawadi!”
Nilitikisa kichwa.
“Hapana, siwezi. Zako huwa nachagua kila mwaka.”
Alikunja uso.
“Siyo Dom alikuwa anazichagua?”
“Dom?” niliuliza kwa hasira ya dhihaka. “Yule mshenzi alikuwa anajivunia zawadi zote nilizokutafutia?”
Alicheka na akaweka mkono wake juu ya mkono wangu, akabonyeza kwa upole.
“Hapana. Nilikuwa nafikiria tu bila msingi. Ares, naipenda hii zawadi. Kwa kweli. Ni zawadi yangu ninayoipenda zaidi kuliko zote. Siwezi kusubiri kuchora miundo yangu mipya kwa kutumia hii.”
Nikatabasamu alipoanza kubadili mipangilio ya tablet hiyo.
“Huwa hupumziki kweli, Raven? Wewe ni mfanyakazi kuliko mimi — na hilo si rahisi kusema. Si afya.”
Alishusha pumzi.
“Niko sawa. Kazi hunituliza. Ndivyo napenda.”
Nikamtazama kwa muda.
“Unakimbia nini hasa?”
Raven akakakamaa. Akatabasamu, lakini macho yake yakaonyesha maumivu aliyojifunza kuyaficha.
“Hey, anaonekana kufurahia ule mkufu. Sikuwa nimekwambia?” alijibu kwa haraka.
Nikacheka, nikasukuma bembea kwa mguu wangu.
Njia yake ya kubadili mada kila anapoulizwa swali asilotaka kulijibu haitanichosha kamwe.
“Naam, ulifanya chaguo zuri. Asante.”
Nikamtazama tena. Yeye ni mrembo kupita kiasi. Si ajabu ana umaarufu mkubwa. Hannah ni mrembo pia, lakini Raven... Raven ni kama kitu kutoka kwenye picha ambayo haijachakaa.
“Unahitaji kupumzika hata kidogo, Raven. Hebu nikupeleke pwani kesho asubuhi. Je, bado unapenda kutazama jua linapochomoza?”
Alitazama mapajani mwake.
“Unalala hapa leo?”
Nikatikisa kichwa.
“Naam. Nilijua nitakunywa, kwa hiyo niliona ni bora kubaki.”
Aligeuka upande mwingine, sura yake ya pembeni ikiwa maridadi kama mchoro wa kale. Siwezi kuelewa ni kwa nini bado hajawa na mtu maishani mwake.
“Nadhani nitarudi kwenye chumba changu leo. Hivyo mmoja wa marafiki wa Hannah atatumia chumba changu hapa.”
Nikatikisa kichwa kimya, nikiwa na huzuni.
Nilitaka kupendekeza tukutane siku nyingine, lakini Hannah akaniita. “Ares!” Hannah akarudia, akinyosha mkono wake.
Nikavuta pumzi, nikasimama, nikamtazama Raven kwa mara ya mwisho. Lakini tayari alikuwa amejificha nyuma ya tablet yake mpya.
Kadri tunavyokaribia harusi, ndivyo Raven anavyozidi kunikwepa. Sielewi kwa nini, lakini najua tu — nachukia hisia hii.
Endeleaa…
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote