SAILAH (Binti boss)
SEHEMU YA: 01
Katikati ya jumba la kifahari, jumba ambalo kwa mtu kama mimi wa low life lazima niogopa nikiingia yaani nikiingia lazima nihisi kama nachafua hivi.
Anaonekana binti mrembo sana, akiwa kwenye chumba chake, chumba kilichopangwa na kikapangika, muandaaji pia wa chumba alikuwa vizuri sana kwenye upangiliaji wa chumba.
Achana na chumba turudi kwa huyu binti sailah nyie, alikuwa mwembamba, sio sana, kishape cha uchokozi na weusi wake wa kung'aa, nywele zake nyingi kabisa Natural yaani hakuweka dawa, uzuri wake ulimfanya kila alipopita kumjadili, shida ya saila ni kulinga.
Yaaah umenielewa, sailah ni binti anayejisikia sana, ni binti ambaye anajipa kipaumbele sana na kuwazarau wengine, na hii imetokana na mama yake na baba yake kumdekeza kwani ndio binti yao pekee kabisa ambaye wamebarikiwa.
Sailah amekuwa akifanyiwa kila kitu na
wafanyakazi ambao Baba yake aliwaajili, yaani
yeye sio wa kuosha vyombo, kupika wala kufua, kazi ya sailah ni kuchezea simu kwenda chuo kwani alikuwa mwaka wa pili na kula tu.
Wadada wa kazi wa kina sailah wamekuwa wakimuogopa sana kwania amekuwa akiwafokea kwa namna moja au nyingine tena pasi na sababu maalumu.
Niite saddy, kijana wa kimasikini kabisa ambaye nimepoteza wazazi wangu wote wawili na waliniachia mdogo wangu wa kike ambaye ako na miaka 13 kwa sasa.
Sara ndio mdogo yangu, ndo furaha yangu na ndo kila kitu kwangu.
Saddy ni kijana handsome kwa namna yake, maana watu wengi wamekuwa wakinisifia, ukiachana na kusifiwa saddy mimi nimefanana sana na mama yangu.
Mrefu kiasi, sio mweusi wala mweupe niko katikati , ukirudi kwa hawa was waswahili wenzangu utasikia ni maji ya kunde �sijui ndo rangi gani hiyo maana sijawai ata kuisoma.
Tangu wazazi wafariki maisha yamekuwa magumu mno kisukosuko ya uku na uku, kuna muda uwa nakata tamaa kabisa ya maisha, lakini nikimkumbuka mdogo wangu Sara, uwa
nainama chini nakaza kamba za viatu na kuendeleza safari ya utafutaji.
"Huyu binti anakela sasa kwani ajanisikia nikipiga honi au ??" Nililalamika, muda huo nilikuwa nyumbani kwa kina sailah nilimfata kwaajili ya kumpeleka chuoni, kwani mimi ndoo dereva wake na ndio kwanza nilikuwa na siku ya pili.
Nilisubili kama nusu saa ndipo sailah akatoka nje, alikuwa akitembea kwa madaha na mikucha yake kama jini.
Nilibaki nikimuangalia tu, sio kwamba namchukia sailah hapana, ila ni binti ambaye ametokea kunikela sana siku ya kwanza ambayo nilianza kazi.
Muda huo sailah alikuwa mbele na mdada mmoja wa kazi alikuwa nyuma akiwa amebebelea pochi ya sailah, yaani hadi pochi ya madaftari anabebewa na mfanyakazi.
"Unapiga honi, as if kuna kiziwi umu ndani kwani uliambiwa sijasikia ??" Sailah akaanza kunifokea baada ya kuingia garini.
"Nisamehe " nilimuomba tu msamaha maana kwa muda huo kitu muhimu ni kazi yangu.
"Sasa hivi utakuwa unanipigia simu na sio kupiga honi uwa sipendi kelele "
"Hakuna shida sailah" nilijibu.
"Well, kuna kitu akiko sawa, mama yangu jana nimekusikia unamuita madam, so na mimi pia ni madam, usiniita sailah"
"Unasema ??" Nilimuuliza."
"Umenisikia saddy, tuwai nimeshachelewa".
Niliishia kusikitika tu, nikawasha gari na safari ikaishia kwenye chuo kikuu cha dar es Salaam yaani UDSM.
Nilimshusha na kuanza kurudisha gari nyuma ili niweze kuondoka.
"Unaenda wapi ??" Sailah aliniuliza.
"Naenda wapi unamaanisha nini yaani ? " na mimi nilimuuliza.
"Nafikili baba ajakuambia, kitu mimi dereva akinileta chuo uwa ananisubili mpaka nitoke anirudishe nyumbani ndo aendelee na mishe zake "
"Kwahiyo saddy mimi, nikae hapa kama pambo nakusubili wewe sio ? Ata madereva wa school bus awafanyi ujinga huo, sailah, oooh sorry madam, kabla ya saa mbili nitakuaa hapa " nilijibu na kuondoa gari.
Yaani kama hakuwai kukutana na watu vichaa basi mimi ni wa kwanza maana aiwezekank kitoto kidogo kama iki kitake kuniendesha akili yangu, yaani anaanzaje kunisumbua.
Nilipitiliza mpaka shuleni kwa kina Sara, na walikuwa wamesharuhusiwa nilimchukua na kurudi nae nyumbani.
Sara akiwa anaendelea kufua nguo zake, nami nilikuwa nikipika chakula cha mchana na usiku moja kwa moja hii yote ni kubana matumizi ya gesi isije ikawai kuisha �.
"Kaka natamani kumuona huyo mtoto wa jilani unayemuendesha " alizungumza Sara baada ya kuja jikoni.
"Kwanini ??" Nilimuuliza.
"Kuna rafiki yangu anasema kuwa aliwai kumuona simu moja amesema kuwa ni mrembo mno "
"Ni mrembo wa sura tu na sio tabia " nilijikuta nikijibu kwa hasira.
"Mmmh mshaanza kugombana sio bure maana wewe kaka angu uwezagi kuficha hasira zako " kiukweli Sara ananijua mno.
"Anakela sana yule msichana, san" nilijibu.
Basi tulibadilisha mada na kuendelea kupiga story nyingine,tu maana sikutaka tuendelee kumuongelea sailah.
**
Majila ya saa 12 kama na nusu hivi, niliwasha gari na safari ikaanza kwenda chuoni kwaajili ya kumfata sailah, ingawa
darasani wanatoka saa mbili usiku, niliitaji kuwai saa ili kupishana na foleni.
Nilifika chuoni kwao kwa wakati, na saa mbili ilifika, sailah akutokea kwenye gari, nilimtafuta kwa njia ya simu lakini akupokea, nilimuulizia chuoni na kila mtu alisema ajui.
Yaani kama lisaa lizima nilitumia kumtafuta mtu mzima, yaani unaweza kusema natafuta mtoto mdogo kumbe ni jitu Zima kabisa.
Baada ya kuona kuwa sina dalili ya kumpata niliamua kumpigia simu baba yake na kumpa taarifa.
"Naomba rudisha hiyo gari nyumbani kijana naona kabisa kazi imekushinda, binti yangu amekaa sana akikusubili mpaka nimemfata mwenyewe"
Eeeeeeh � mbona nilifika kwa wakati tu, kazi ndo kwa siku ya pili na naambiwa nirudishe gari.
SAILAH (Binti boss)
SEHEMU YA: 02
Kwa mawazo makubwa sana na wasiwasi, nikaanza kurudi kwenda kwa boss wangu maana kazi hiyo ndo nilikuwa nikiitegemea kwaajili ya kumlisha mdogo wangu na mambo mengine.
Nimekaa muda mrefu pasi na kuwa na kazi, leo nimepata inataka kuniponyoka kirahisi kama hivi, nitakuwa mgeni wa nani Mimi eeeh �.
Nilifika nyumbani kwa boss wangu na kumkuta akiwa amekaa sebuleni akinisubili kwa hasira sana.
"Shikamoo...." nilimsalimia ingawa kwa woga sana.
"Naomba funguo ya gari yangu, na uniambie nikulipe kiasi gani kwa siku mbili ulizofanya " daaah boss akujibu ata salamu yangu.
"Kwanza kabisa niombe radhi kwa kilichotokea boss wangu, lakini nafikili ni kutokuelewana, maana nilifika kwa wakati kabisa � na nili "
"Kimya wewe" boss aliinuka kwa hasira na kunifokea.
Nilitulia na kumuangalia kwa jicho langu la huruma kabisa na huzuni ili aweze kuniangalia kwa jicho la pili, lakini hasira yake ilionekana kuwa ya kiwango cha juu sana.
"Kabla ujaanza kazi unakumbuka nilikuambia kuwa visingizio na maelezo mengi siitaji si ndio ? Na nilikuambia sitaki princess wangu awe anapata shida au sio wewe ??"
"Ni mimi boss "
"Naomba funguo
zangu "
Daaah nilibaki kuwa mpole sana, kwakuwa funguo nilizishika mkononi nilichofanya Ni kumkabizi kwa heshima ya hali ya juu kabisa.
"Nashukuru kwa nafasi ambayo ulinipatia, na Mungu akubariki " nilimwambia.
Sikuwa na la ziada nilichofanya ni kugeuka na kuanza kuondoka, sawa nina shida, lakini kumbembeleza mtu ambaye anaonekana wa hovyo uwa siwezi kabisa.
"Nikupe kiasi gani kwa hiyo pesa yako ??" Aliniuliza.
Niligeuka nyuma kwa hasira mno maana ata machozi yalikuwa yameanza kunitoka, sio kwamba nimekosa kazi hapana, ni dharau ambayo yule baba amenionesha na mke wake alikuwa akiniangalia kama Takataka tu �.
"Hizo siku mbili si kitu kwangu, fanya kama nilifanya msaada" nilijibu na kuondoka zangu.
Nilifika nyumbani nikiwa nimechoka sana aiseeeh yaani hasira ambayo nilikuwa nayo juu ya binti sailah ilikuwa haipimiki, maana uongo wake ndo umesababisha yote haya.
****
Asubuhi na mapema niliamka na kufanya shughuli zangu, sikutaka mdogo wangu Sara ajue kuwa nimekosa kazi hivyo nilifanya kila juhudi kumfanya asielewe.
"Ukitoka shule, leo utapanda daladala sitaweza kuja kukufata boss amenituma mbali sana "nilimdanganya.
Nakumbuka siku ya kwanza nilipopata gari, nilienda kumfata shuleni kwao na kumuaidi kuwa nitakuwa nikimfata kila siku.
"Usijali kaka, nitawai kurudi uwe na kazi njema"
Labda niseme sara alikuwa ni binti muelewa sana, nahisi ni hali ya maisha ambayo tumekuwa nayo hapo nyuma, maisha yamemfanya Sara wangu kuwa mature kabla ua umri wake.
Baada ya Sara kuondoka, nilijiandaa na kuingia mtaani kutafuta Ata kibarua ili niweze kufanya na kupata ata pesa ya kula jioni na mdogo wangu.
Mungu uwa amtupi mja wake, nilifanikiwa kupata kazi ya kubeba zege, nilifurahi Sana utazani nimepata kazi ya ofisini.
Siku hiyo nilijua kupigika bhana, jua kali na nini lakini ndo nabeba zege kwenye ndo na kupandisha kwenye maghorofa ya watu.
Majila ua jioni boss alifika pale tukalipwa pesa zetu, nilifurahi kuwa nimepata pesa ya kwenda kula nyumbani na Sara wangu.
Nilipitia sokoni na kununua chakula, maana sokoni ndo bidhaa kidogo ndo bei rahisi, nilifika na kumkuta Sara akiwa amejilaza kwenye kochi ni wazi kuwa njaa ilikuwa ikimiwangua.
Sikuwa na haja ya kumuamsha nilichofanya ni kuingia jikoni na kwenda kumpikia, ingawa ata mimi sikuwa nimekula siku nzima lakini yeye nilihisi kuwa ndo njaa imemkaba zaidi si unajua mambo ya masomo.
Nilimaliza kupika, nikatenga na kumuamsha, mwaya aweze kula. "Oooh kaka shikamoo " alinisalimia.
"Marahaba, pole, nimekuweka na njaa "
"Ahahah, nilikuona leo kwenye lile ghorofa unabeba zege " alizungumza Sara.
Nilistuka sana, yaani amenionaje ? Kwani si nilimpa pesa ya kupanda daladala sasa pale amenionaje ??.
"Oooh kumbe, yaah nilikuaa namsaidia mshikaji wangu maana tulikuwa tunataka kwenda mahali sasa angebeba mwenyewe tungechelewa "
Baada ya uongo wa hapa na pale, tukaanza kula wenyewe, tukawa tunacheka na kufurahi, mwaya maisha yangu na mdogo wangu ni mazuri tukiwa tunacheka tu lakini ukirudi kwenye uhalisia ni
machungu mno �.
Majila ya usiku niliingia chumbani kwangu kwaajili ya kulala, nilikaa tu kitandani niliwaza kesho pia nitafanyaje, ingawa chakula nimenunua cha kututosha siku mbili au tatu, lakini mawazo yalikuwa mengi.
Nikiwa nawaza sana ujumbe uliingia kwenye simu yangu niliwai na kuangalia.
"Unajisikiaje baada ya kukosa kazi ??" Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa sailah, ila huyu binti ana roho mbaya jamani � kwahiyo yeye anafurahia anguko langu.
Niliiangalia tu nikatoa sauti kwenye simu yangu na kulala zangu.
Zilipita siku mbili maisha yalikuwa magumu sana kwenye upatikanaji wa pesa, siku hiyo, kuna rafiki yangu aliniita kuwa kuna kazi ya kusafisha bustani, hivyo nimpitie kwao twende wote.
Sasa ili kufika anapoishi mshkaji wangu lazima nikatize mbele ya uwanja wa kina sailah, nilipita na kwa bahati mbaya nikakutana na sailah.
Nilimuangalia sana, mwenyewe alikuwa bize akiongea na simu uku anavuta vuta maua nilijua kabisa huyu anaongea na muchumba �.
Nilimpita kama simjui, haraka akakata simu na kuniwai.
"Kwahiyo wewe sms zangu auzioni au ??' Aliniuliza baada ya kusimama mbele yangu.
"Toka mbeole yangu " nilimfokea.
"Ahaha najua inakuuma eeh � mimi ndo binti boss nikimwambia baba yangu fanya ili anafanya, ulikosea sana kujifanya mjuaji "
"Haya binti boss toka mbele yangu nataka kwenda, ila kaa ukijia kuwa una uzuri wa sura na unaubaya wa nafsi" nilimpa dongo lake na kumsukuma.....
Mtume si akaanguka kama mzigo...�.
KITANILAMBA MWENZENU.................................. �
SAILAH (Binti boss)
SEHEMU YA: 03
Sikuona haja ya kusimama maana yeye ndo alianza kunichokoza nilichofanya ni kuondoka zangu.
Nilifika kwa mshikaji wangu na kumkuta akiwa ananisubili mimi tu. Tulishika njia pamoja na kuondoka.
Majila ya usiku nikiwa nyumbani napata chakula na Sara, yaani mdogo wangu, simu yangu iliita na nilipoangalia ilikuwa ni baba sailah niliogopa Sana nikajua kabisa ni janga la mchana la kumsukuma binti yake.
Niliiangalia kwa muda sana mpaka ikakata, ikaita tena na tena sikupokea mwisho alinitumia ujumbe na kusema kuwa anaitaji kuonana na mimi.
Nilifikilia sana mwisho nilimbipu maana sikuwa na salio alipopokea tu nikazungumza nae na akaniomba nifike nyumbani kwake usiku huo.
"Liwalo na liwe naenda nikajue mbivu na mbichi " nilizungumza kimoyomoyo.
Niliinuka na kumuaga Sara, nikaanza safari, hakukuwa mbali sana hivyo ilikuwa ni mwendo kama wa dakika 10 hivi nikawasili nyumbani hapo.
"Shikamooni " niliwasalimia baada ya kuingia ndani na kumkuta mzee huyo akiwa na mke wake.
"Marahaba karibu sana kijana" walijibu kwa pamoja na walikuwa wamechangamka sana aiseeh nilishangaa.
Muda mfupi alikuja dada wa kazi na kuniletea kinywaji pale na biscuit, ni jambo la ajabu mnajua, kuna muda nilikuwa nahisi kama wanataka kuniua hivi �.
Ila mimi sijui nina nini, kuna muda nilikuwa natamani niwaambie anzeni kuonja ninyi na mimi ndo ninywe maana sio kwa kunikalimu kiasi kile.
"Aaah mtoto wangu, umeshapata kazi ??" Mzee huyo aliniuliza yaani tena ananiita mtoto wake
kweli jamani au wanataka kunitoa mzukule mimi � maana ata utajiri wao sina amani nao.
"Hapana " nilijibu kwa ufupi tu sikutaka kujieleza.
"Aaah imekuwa vizuri, kwani nina ofa ya kazi kwaajili yako " alizungumza mzee huyo nilibaki nikimuangalia tu.
"Aaah najua mikwaluzano ya hapa na pale ikitokea lakini sisi ni binadamu, na baada ya kufikilia sana nimeona nikurudishe kwenye kazi yako kijana wangu "
Ebu subilini kwanza, huyu mzee na familia yake wananichukuliaje
? Yaani wananifanya kama mdoli hivi, wananiachisha kazi na kunirudisha muda wanaotaka.
Baada ya yote kiukweli nina shida na kazi hivyo basi sina muda wa kupoteza zaidi ya kupokea kazi hiyo ili kuendelea na majukumu yangu.
"Asante sana, na nitafanya kazi ka juhudi sana " nilijibu.
"Sawa, shika funguo zako na utawasiliana na sailah atakupatia taarifa zake za chuo, mtaendelea kazi zenu "
Nilipokea maelezo pale mwisho niliaga na kuondoka, nilifika nyumbani, na kumpigia simu sailah ili aweze kuniambia muda wake wa kwenda chuoni.
"Aaah hatimaye umepata kazi yako haya sema Asante sailah maana bila mimi usingepata hiyo kazi " alizungumza sailah baada ya mimi kumpigia na kumuuliza kuhusu muda wa yeye kwenda chuo.
"Sawa Asante sailah, naweza nikajua muda wa wewe kwenda chuoni kwako sasa "
"Weeh unajua jeuri yako ndo inakuponza, mtu uko na maisha ya shida magumu, mpaka mafuta ya mwili yanakushinda halafu unaniletea jeuri " ila sailah ako na dharau Sana.
Nilikata simu, maana naaniletea mambo yake meusi, me mwenyewe akili yangu inawaka moto muda wote, muda wote nina hasira halafu ananiletea ujinga hapa.
Muda huo huo akapiga na kuanza kunifokea pale tu nilipopokea.
"Unakata simu sio ? Weeh kijana una nini wewe eeh ? Kama kazi utaki si useme au ?"
"Nimekuuliza muda wa wewe kukupeleka chuoni unaanza kuleta mambo meusi, sailah labda unijui vizuri, me mwehu kuliko wewe, mie ni kichaa kuliko wewe sawa, umasikini sijui shida zangu aziwezi kunifanya nikusujudie mtoto mdogo kama wewe " nilimfokea kwakweli maana alinichosha.
"Ouk, naenda saa sita mchana " alijibu, na kukata simu.
Nilichukua simu na kumtumia tena ujumbe, kwa kumuuliza muda wa kwenda chuo kwa mara ya pili na akanijibu kwa sms kuwa ni saa 6 mchana.
****
Siku iliyofuata, nikifanya mishe zangu muda wote, na kazi zote, baada ya kila kitu, saa 5 nilianza kujiandaa lakini muda huo huo simu yangu iliita na ilikuwa ni simu ya boss.
"Kijana, mbona jana ukusema kama utaki kazi ??" Alianza kuniuliza pasi na salamu.
"Sijaelewa sir, sitaki kazi kivipi na mimi niko najiandaa nikamfate sailah"
"Ukamfate wapi ? Yaani chuoni ni saa 3 asubuhi saa 5 hii ndo unaniambia kuwa unajiandaa eeh "
Kwanza nilikaa kimya kwa muda na kisha nikauliza kwa mshangao.
"Anaingia saa 3 asubuhi? Mbona mimi ameniambiaa saa 6 mchana lakini "
"Naomba uje jioni tuongee" nikasema hii familia sasa inanipanda kichwani aswaah huyu sailah na baba yake, maana mama sio muongeaji kabisa.
Majila ya jioni nilijiandaa na kufika nyumbani kwa mzee huyo, yaani ni kama alikuwa akinisubili mimi, nilipoingia tu akakaa chini na kuanza kuniuliza kwa hasira.
"Boss ni mimi au ni wewe ??"
Sikuweza kumjibu nilimuangalia tu maana kwa mtu mwenye heshima zake uwezi kumuuliza mtu maswali kama hayo kwa mimi niliona ni ya kijinga tu.
Niliingia kwenye meseji ambazo nilichati na sailah na kumpatia Baba yake, aliangalia kwa muda mwisho nikaona akiwa mpole sasa, kidogo akashusha kifua chake.
"Sailah, sailah, weeh sailah " mzee huyo aliita kwa hasira sana.
Muda huo huyo sailah alishuka kutoka chumbani kwake ambapo ni ghorofani aiseeh mavazi ambayo alikuwa amevaa kwa mtu kama mimi siwezi ruhusu Sara avae mbele yangu.
"Yes, daddy " aliitika sailah kwa kudeka kabisa.
"Saddy ulimwambia kuwa chuoni unaingia saa ngapi ??'baba yake alimuuliza kwa hasira.
"Saa 3 baba na nilijaribu kumpigia simu asubuhi lakini akupokea kabisa "
Baba yule aliinuka na kumpatia zile sms sailah, na kumwambia. "Hii ni saa 3 au sita sailah ??"
Sailah alinigeukia mimi akaniangalia, kwa jicho fulani hivi la kusema nitakukomesha kisha akamgeuki baba yake.
"Oooh nahisi ni typing error baba na sikuwa nimeangalia, samahani sana, baba na saddy nisamehe kaka angu " alizungumza sailah unaweza sema ni mtu kweli lakini ni kapuuzi tu.
"Kwa nini princess wangu anaomba msamaha ??" Ilikuwa ni sauti ya mama sailah ambaye aliuliza uku akiingia ndani kwani alikuwa nje kwenye mate matembezi yake.
Sailah alimkimbilia mama yake na kumkumbatia.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote